Nakusalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo, Karibu tujifunze habari njema za uzima wa roho zetu.
Neno la Mungu linatuambia..
2 Wafalme 19:30
[30]Na mabaki yaliyookoka ya nyumba ya Yuda yatatia mizizi chini, na kuzaa matunda juu.
Unaelewa maana ya mstari huu? Anazungumzia kustawi kwa nyumba ya Yuda (ambao ndio sisi kanisa)..
Lakini kustawi kwake hakuji hivi hivi, matunda yake kutokea kule juu, anasema kanuni yake ni lazima pia mizizi yake ikite chini.
Haiwezekani mti ukazaa kama hauna mzizi, jiulize je wewe una mizizi imara ya rohoni, ya kukufanya uweze kuzaa matunda yampendezayo Bwana?
Kumbuka kuthamini kwako wokovu, ndivyo hueleza urefu wa mizizi yako yenye nguvu, itakayokuwezesha kustawisha matunda juu.
Jani haliihitaji mizizi yoyote ya maana, kwasababu halina matunda ya kutoa.
Ukiona huwezi kuzama ndani katika wokovu, hauwi siriazi na maisha yako ya rohoni ujue pia hautakuwa na matunda yoyote kwa Mungu wako.
Katika ule mfano wa mpanzi Bwana Yesu alieleza kitu kilichofanya ile mbegu ya nne kustawi mpaka kuzaa matunda..anasema ilizaa kwa kuvumilia.(Luka 8:15)
kuvumilia nini?
Kuvumilia hatua zote 3 za mwanzo. yaani alihakikisha adui haibi mbegu iliyopandwa ndani yake, ni mtu ambaye aliweza kuvumilia dhiki, na majaribu yaliyozuka kinyume na lile neno lililopandwa moyoni mwake, alijiepusha na anasa, na kutoruhusu masumbufu ya ulimwengu huu kumsonga akashindwa kuivisha chochote. Hayo ndio mambo aliyovumilia.
Huyu ni mtu ambaye yupo makini na wokovu alioupokea.
Swali la kujiuliza je tunayo matunda hayo? kumbuka Hayaji kwa kutamani au kusubiri yanakuja kwa urefu wa mizizi yetu yenye uwezo wa kufikia vyanzo vya chini kabisa vyenye virutubisho vyote vya kustawisha matunda.
Ndio maana biblia inasema
Zaburi 1:1-3
[1]Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. [2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. [3]Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
[1]Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
[2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
[3]Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Anza sasa kushughulika na mizizi yako, mpaka ifikie kwa hakika mito hiyo ya maji.
Usipoe kimaombi, kimifungo, kiibada, kiuinjilisti, na kiusomaji Neno.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KWA KUVUMILIA AKAIPATA ILE AHADI.
Rudi Nyumbani
Print this post
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu tujifunze maneno ya uzima.
Katika nyakati hizi za hatari na udanganyifu mwingi, ni vizuri kujichunguza sana, ni Roho ipi umeipokea ndani yako. Kwasababu tabia unazozionyesha ni matokeo ya roho iliyopo nyuma yake, ikiwa wewe ni mpenda dunia basi roho ya dunia ipo ndani yako.
1Wakorintho 2:12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
Vivyo hivyo ukijiona wewe ni mwizi, ujue roho ya wizi ipo nyuma yako.
Lakini maandiko yanasemaje kuhusu Danieli?
Yanasema ROHO BORA ilikuwa ndani yake.
Danieli 6:3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote
Maana yake ni kuwa Roho iliyozidi viwango, ndio iliyokuwa ndani yake.. Unajua mpaka inasema bora, maana yake zipo ambazo hazina ubora, kwa tafsiri nyingine “feki”, zenye mfano wa ile orijino. Ndicho shetani anachokibuni sana, ili awapoteze watu, wadhani wanaye Roho Mtakatifu, kumbe ni bandia.
Sehemu nyingine, inasema “Roho njema kupita kiasi”. Ilikuwa ndani yake..
Danieli 5:12 kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danieli, naye ataionyesha tafsiri.
Umeona sifa ya roho hiyo ni lazima iwe ya ‘kupita kiasi’, sio ya kawaida, vinginevyo ni feki. Sifa za Roho wa Mungu, anapita kiasi. Katika ubora na wema.
Ndio iliyomfanya Danieli awe mkamilifu kama tunavyomsoma kwenye maandiko. Kiasi cha watu kutafuta kosa ndani yake, bila mafanikio.
Danieli 6:4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
Na mtu yeyote anayesema ameokoka, Roho hii naye ni lazima imkalie. Roho iliyo bora, na njema kupita kiasi. Uthibitisho wa kwanza wa Roho uliyempokea ni Roho Mtakatifu, atakusukuma, kuwa Mtakatifu kama jina lake lilivyo.
Lakini iweje tunasema, tumepokea Roho, tunanena kwa lugha usiku kucha, tunatabiri, lakini Ubora wa huyo Roho hauonekani ndani yetu? Cha kushangaza utaona huyo mtu anasema haiwezekani kuishi maisha matakatifu hapa duniani, ndio hapo tunamhubiri Kristo, wakati huo huo, tunaishi kidunia, tunafunga na kuomba wakati huo huo, tunavaa ovyo ovyo, tunaabudu pamoja lakini chini kwa chini tunavisasi na vinyongo. Tunatoa sadaka lakini nyuma kwenye biashara zetu ni za rushwa rushwa.
Je! Hiyo ni Roho bora? Au imechakachuliwa?. Tumepewa ruhusu ya kujipima (1Yohana 4:1). Jihakiki, tangu ulipookoka hadi leo je, kuna mabadiliko yoyote ndani yako? Kama huna ni aidha ulimzimisha alipokuwa anaugua ndani yako ugeuke, au huna kabisa Roho Mtakatifu.
Habari njema ni kuwa Roho bora, ukimwita, huja ndani yako, au huamka tena. Ni wewe kuamini, na kutii kwa moyo wako wote. Kuwa tayari kuacha vyote(vya kidunia), na kumgeukia yeye. Na hatimaye atakuongoza na kukuweka sawa. Lakini sharti kwanza uaminifu kuwa utakatifu unawezekana, lakini pia ulimwengu utaukana.
VIASHIRIA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU KUWEPO NDANI YAKO.
OMBA, TAFUTA NA BISHA.
JE UMEUPOKEA UWEZA WOTE WA UUNGU NDANI YAKO?
Bwana ametupa agizo na wajibu wa kwenda kuihubiri injili ulimwenguni kote, na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wake.(Mathayo 28:19)
Alisema pia mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache. Ikiwa na maana lengo lake ni yeye apate mavuno mengi kutoka kwetu. Lakini huwenda tukaona sisi ni shida, kufanya hivyo.
Hata kama itakuwa kwetu ni shida kuvuta watu, bado Yesu anaona ni rahisi kwetu..Kwani mahali pengine alisema mashamba yameshakuwa meupe tayari kwa mavuno, wapo ambao tayari walishayataabikia, sisi ni kumalizia tu. Hivyo ni rahisi sana.
Lakini ili injili yetu itoe matokeo aliyoyakusudia, yatupaswa tujifunze kanuni zote za kiuinjilisti na kuzitumia, kisha miongoni mwa hizo Bwana azitumie kuleta matokeo yake. Kuliko kutegemea kanuni moja tu Fulani na kupuuzia nyingine.
Ni sawa na mvuvi ambaye anashikilia uvuvi wa ndoano tu, lakini hajui kuna wa nyavu, au wa mkuki au wa kutegea, lakini pia kuna wa majira mbalimbali ya kuvua, kuna ya usiku, au ya mchana.
Na sisi katika utumishi wetu wa kuwavuta watu kwa Yesu, tufahamu pia njia zote.
Sasa kibiblia zipo kanuni kuu (8), zinazovuta watu.
Hii ndio njia kuu na ya kwanza, ambayo ndio inasimama kama uti wa mgongo wa uinjilisti. Kwamba ni sharti kila mmoja wetu atumie kinywa chake, ujuzi wake, elimu yake, ufahamu wake, kumuhubiri Kristo kwa watu kwa namna yoyote. Utashuhudia shuleni, nyumba kwa nyumba, masokoni, barabarani, vijiweni, mitandaoni n.k. Ni agizo la Bwana na linapaswa lifanywe na wote.
Mathayo 5:16
[16]Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Wapo watu si rahisi kugeuka kwa kusikia unawaelezea habari za Yesu, ni rahisi kugeuka wanapomwona yule anayewahubiria mwenendo wake ni tofauti na wa kwao. Na hilo likamchoma moyo na kumfanya amgeukie Kristo moja kwa moja.
Hivyo angaza mwenendo wako, kwa watu, ikiwa hawataamini kwa lile Neno, basi waamini kwa mwenendo wako mzuri.
1Petro 3:1 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu
Ni ile hali ya kujaribu kuchukuliana na mawazo ya wale watu, na wakati mwingine hali zao, kana kwamba ni mmojawao, kisha kutumia fursa hiyo kuwaeleza habari za Yesu. Wengine huvitiwa kwanza na jinsi unavyothamini hali zao, sio kwa jinsi unavyo eleza vema Neno au mwenendo wako. Ni njia ambayo aliitumia Paulo na ikamletea matokeo mengi sana ya waongofu.
1Wakorintho 9:19 Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. 20 Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria. 21 Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria. 22 Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu. 23 Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.
1Wakorintho 9:19 Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.
20 Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.
21 Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
22 Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.
23 Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.
Zingatia kujichanganya sio kushirikana na dhambi zao, hapana, bali kuwepo katikati yao ili kuwaondoa huko, huku wewe mwenyewe ukijilinda nafsi yako usitekwe na dhambi zao.
Unaweza kudhani kila eneo unaweza kuhubiri na kuleta matokeo unayoyatazamia. sio kweli, Mitume walivua samaki usiku kucha lakini hawakupata kitu, baadaye Yesu akawaambia tupeni jarife upande wa kuume mtapata (Yohana 21), sehemu nyingine aliwaambia waende vilindini. Na walipofanya vile walipata samaki wengi. Paulo mwanzoni aliegemea injili yake kwa wayahudi sana, akapitia ukinzani, lakini kumbe Mungu alimkusudia aende kwa mataifa, na alivyotii agizo lile matokeo yakawa makubwa. (Matendo 22:21)
Hivyo ni muhimu kuomba Bwana akupe dira, lakini pia katika kuhubiri kwako utaona eneo Fulani lina matunda mengi, basi ujue hapo ni dira yako. Au njia Fulani ukiitumia wengi huvutiwa kwa Kristo, basi fanya hivyo. Lakini hili ni kuendelea kuomba na kuhubiri Mungu mwenyewe ataielekeza dira yako, kama ni hapo au kwingine, kama ni njia hiyo au njia nyingine, la kuzingatia ni kuwa mwepesi kutambua upepo wa Roho unakufanikisha wapi. Kisha ongeza nguvu nyingi sana hapo, kuliko kule kwingine.
Yapo makundi ambayo, Mungu anajua yakiona tu muujiza au ishara fulani huvutika kirahisi. Na hili pia ni eneo la kumwomba Bwana, ajalie kunyosha mkono wake kuponya maana lina mvuto mkubwa na wa haraka sana.
Kanisa la kwanza liliomba maombi ya namna hiyo.
Matendo 4:29 Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, 30 ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu
Hivyo popote uendapo pia hakikisha unawaombea na watu, shida zao. Kwasababu kwa njia hiyo Roho Mtakatifu hupata nafasi ya kupenyeza mvuto huo, kwao.
Busara ni namna nzuri kunena, hadi kuushawishi moyo wa mtu. Bwana Yesu anataka na sisi tujae busara ndani yetu aliyoifananisha na kama ile ya nyoka.
Mathayo 10:16 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Nyoka alijua akimwendea Hawa kwa ukali, au kulazimisha isingewezekana, lakini alijishusha na kujifanya kama mtu wa mashauri, afichuaye siri, Jambo ambalo ni uongo. Na sisi hatuna budi kujua kunena kwa hekima, ili wale tuwahubirio tuishawishi mioyo yao, mpaka kumgeukia Kristo ambaye ndiye kweli. Tujifunze kueleza uzuri wa Yesu. Lakini pia tusiwe watu wa kauli mbaya kwa tunaowahubiria hata kama watatupinga.
Kuna la watu hatutaweza kulipata kama hatutaingia gharama kubwa kwa ajili yao. Wakati mwingine hata kuhatarisha maisha. Kwasababu mahali walipofungwa na adui, pana ngome nzito. Mfano wa hawa ni wale waliofungwa katika vifungo vikali sana vya kidini.
Kuwang’oa huko ni kujiandaa na dhiki. Cha kuomba hasaa hapa kwa Mungu ni ujasiri kwa kanisa la kwanza lilivyoomba.
Hichi ndio kilele cha juu kabisa cha kiuinjilisti. Ndio wito Yesu aliowaitia mitume wake utakaowafanya wafikie kona zote. Kuwa tayari kufa kwa ajili ya walio dhambini. Ndio maana si wote waliweza kuambatana nao, Bali walibakia tu kuwaadhimisha.
Matendo 5:12 Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani; 13 na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha;
Matendo 5:12 Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;
13 na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha;
Kuna wengine si rahisi kuokoka ki-uinjilisti tu, bali pia kuwaombea. Hii ni njia inayolegeza nira za mwovu mioyoni mwa watu. Injili yako inaweza isiwe na shida lakini mioyo yao ya jiwe ikawa vile, hata uhubirije hawewezi kukuelewa.
Paulo alikuwa ni mtu wa kuwaombea sana watu wake wayahudi waokolewe. Maandiko yanasema ombeaneni ninyi kwa ninyi mpate kuponywa.
Warumi 10:1 Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe. 2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
Warumi 10:1 Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.
2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
Usione shida kuwaombea ndugu zako ambao hawajaokoka, wafanyakazi wenzako, majirani zako, jamii yako n.k. Ni maombi yasiyo na ukomo fanya hivyo kila siku, maombi yako ni silaha kubwa sana ya kiuinjilisti. Lakini usiombe tu na kukaa ukasema namwachia Bwana. Hapana unawaombea na huku unawahubiria.
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba, tukijifunza njia zote hizi, na kuziachilia katika maisha yetu ya kiutumishi ni hakika kuwa lipo kundi litaokoka tu. Lakini kutegemea njia moja peke yake huubana utendaji kazi wa Roho Mtakatifu ndani yetu, . Ukihubiri changanya na hizo nyingine, kisha yeye aamue ni ipi itamvuta mtu kwa wakati huo.
KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI
UFUATILIAJI NI SEHEMU YA HUDUMA MUHIMU KWENYE UINJILISTI
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
2 Petro 1:3
[3]Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
Kuna mambo makuu sana ya kujifunza ndani ya vifungu hivi;
Hapo tunaonyeshwa kuwa Mungu anao Uweza wake. Kama vile tu mwanadamu alivyo na uweza wake usiokuwa sawa na mbwa. Kwamfano mwanadamu anaweza kuunda silaha, ambayo inaweza teketeza mji mzima kwa maarifa yake. Anauwezo wa kuruka angani zaidi ya kiumbe chochote duniani kwa vyombo alivyovibuni, anaweza kuwasiliana na mtu aliye mbali sana hata na kuona uso wake kwa vyombo vya mawasiliana alivyojibunia.Mambo ambayo mnyama hawezi. Huo ni uweza wake wa kibinadamu.
Vivyo hivyo na Mungu wetu, anao uweza wake wa uungu, ambao ametukirimia sisi, Tunapoupokea huo tunakuwa na sifa kama zake.
Ndio hapo anasema…
“Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
Lakini sasa nataka uone hapo uweza huo umeshushwa juu yetu, si katika kila kitu bali katika mambo mawili makuu.
1) La kwanza ni uzima.
2) la pili utauwa.
Yaani mambo yote yanayohusiana na uzima wetu, ametuwezesha yeye mwenyewe. Ndio maana kwa kumwamini Yesu tunapokea msamaha wa dhambi. Tunakuwa tumevuka kutoka mautini kuingia uzimani. Hatuangamii, tunakuwa na uzima wa milele ndani yetu.
Kwasababu Hatuna kifo ndani yetu, tunalala tu, kupumzishwa ili baadaye tuamshwe. Lakini Uzima huu hauwezi kuupokea kwa juhudi zako, au kwa elimu yako, au kwa matendo yako mema, au kwa dini yako nzuri, hapana..Ni zawadi ya Mungu kupitia Kristo Yesu. Pale unapomwamini tu, unapokea msamaha wa dhambi zako, kwa neema, huu ni uweza wake wa ajabu, ambao wanadamu wanausumbukia hawaupati, kwasababu mwanadamu hana matendo mema ya kutosha kuununua uzima. Isipokuwa Yesu tu peke yake alitununulia kwa damu yake.
Yohana 3:36
[36]Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Lakini sio tu Uzima, uweza huo umetukirimia pia na katika Utauwa wote. Utauwa ni utakatifu.
Mtu ambaye hajaokoka hawezi yatoa maisha ya utakatifu ndani yake. Vinginevyo atajitahidi sana kwa kuutumikisha mwili kwa nguvu, na hatimaye atashindwa, au atafanya kinafki kama mafarisayo na waandishi, ambao walikuwa wananena mambo ambayo hawayatendi,.kwasababu uweza huu haukuwa ndani yao.
Utauwa haswaa ni kazi ya Mungu mwenyewe mioyoni mwetu kupitia Roho Mtakatifu. Ni pale mtu anapompokea Kristo kama mwokozi wake, kisha kukubali kumtii, kwa kujikana nafsi yake. Ndio hapo hapo yeye mwenyewe anakuongezea nguvu, ambayo inakufanya uyakimbie yale maisha ya kale ya dhambi. Lakini kumbuka hiyo inakuja kwa kukubali kumtii Yesu, kukubali kuwa kiumbe kipya. Wakristo wengi wanataka Bwana awasaidie lakini hawataki kujikana nafsi zao wasaidiwe na Bwana. Ukimpokea kwa mdomo tu uweza huu hautakuwa na matunda ndani yako. Lakini ukiwa ni wa geuko la kweli, uweza huo ni lazima utende kazi ndani yako.
Utaweza kushinda zile dhambi ambazo ulikuwa huwezi ziacha.
Yohana 1:12
[12]Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
Unaposema Yesu ni BWANA wangu. Ni lazima, ujue unajifanya kuwa mtumwa wake.. sikuzote bwana yoyote humiliki mtumwa, chochote anachoagizwa.huwa ni amri kwake sio ombi. Kumbali kuongozwa na Yesu, acha kabisa wokovu wa mdomoni.
Kama mkristo, kuwa mtakatifu ni lazima sio chaguzi, ndio kitambulisho chako kuwa umepokea uzima wa milele. Kwasababu pasipo huo huwezi kumwona Mungu (Waebrania 12:14).
Hakikisha uweza wote huu umeupokea ndani yako. Usiseme hicho kingine cha utakatifu hakinihusu, vinginevyo utakuwa hujakamilika
Shalom.
Bwana akubariki
INJILI NI UWEZA WA MUNGU, UULETAO WOKOVU.
Je! Utatu mtakatifu upo kibiblia?
bofya, juu, “download” ufungue makala yake usome..
KILINDI CHAPIGIA KELELE KILINDI.
Kati ya lugha tatu ambazo zinaonekana katika uandishi wa biblia Kiaramu (Aramaic), ni mojawapo nyingine zikiwemo Kiebrania na kiyunani.
Sehemu kubwa ya agano la kale imeandikwa katika lugha ya Kiebrania na maeneo machache machache sana yalikuwa na maandishi ya kiaramu, (Ezra 4:8 – 6:18, Danieli 2: 4 – 7:28)
Lakini katika agano jipya sehemu kubwa imeandikwa katika lugha ya kiyunani (kigiriki), na mahali pachache pachache kuna maandishi ya kiaramu.
Hivyo lugha hii haipo kwa sehemu kubwa katika biblia
Je chimbuko la hii lugha ni wapi?.
Ni lugha iliyozungumzwa na watu walioitwa Waaramu, ambao lugha yao ilienea kwenye mataifa mbalimbali ambayo kwasasa ni nchi za Lebanoni, Syria, Yordani, Iraq, na Uturuki, na sehemu nyingine za mashariki ya kati. Ni lugha ambayo ilikuwa na nguvu sana zamani za falme kama Ashuru, na ufalme wa Uajemi.
Enzi za Bwana wetu Yesu Kristo, lugha hii ilizungumzwa pia maeneo ya Israeli hususani katika miji ya Galilaya, ambapo Bwana wetu Yesu Kristo alilelewa. Huku kiyahudi ikiwa ni lugha ya asili, kidini na kisiasa.
Hivyo lugha kuu ya Bwana ilikuwa ni hii kiaramu, japokuwa alizungumza pia kiyahudi.
Baadhi ya maneno ya kiaramu ambayo yananukuliwa moja kwa moja kutamkwa na Bwana Yesu ni haya; (japo yapo na pia mengine)
Marko 5:41 “Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka”.
Marko 7:34 “akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka.
Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
Maneno mengine ni kama “Hosana” (lenye maana ya okoa sasa), Mathayo 21:9
“Aba” (Marko 14:36), lenye maana ya Baba.
Lakini pia swali la kujiuliza ni nini sababu ya Bwana Yesu, kuipenyeza lugha hii katika baadhi ya matukio?
jibu ni kuwa hakuna jambo la muhimu sana katika hiyo lugha, isipokuwa ni maongozo ya Roho Mtakatifu ndani yake kwa wakati huo. Kama tu sehemu nyingine alipoongozwa kutema mate chini atengeneze tope apake mtu machoni ili apone.
Hivyo Bwana Yesu alikuwa ni mtu aliyetega sikio kuisikia sauti ya Roho. Vivyo hivyo na sisi, misukumo mbalimbali yaweza kuja ndani yetu. Wakati mwingine hutaomba kwa akili, utaomba kwa kunena kwa lugha, utaomba kwa nyimbo, utaomba kwa kuugua na kulia, kwa jinsi Roho atakavyokusukuma ndani.
Ni kutuonyesha kuwa Bwana hakuwa na fomula fulani pekee katika kutenda kazi, alitegemea maongozo ya Roho Mtakatifu.
Vivyo hivyo na sisi tunapojawa Roho vema. Atatugusa kwa namna mbalimbali na hivyo tutatimiza makusudio yake vizuri, katika jina lake kuu.
JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?
SEMA KWA LUGHA NYINGINE.
ZIFAHAMU KARAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA UTENDAJI KAZI WAKE.
UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
WhatsApp
Bwana Yesu karibu na kuondoka alizungumza maneno haya;
Yohana 14:1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Yohana 14:1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Kwa mara ya kwanza anawafunuliwa wanafunzi wake, kuhusu mambo yaliyo kwa Baba yake tuliyoandaliwa sisi. Na hapo anasema huko kuna “makao mengi”. Hasemi kuna “kao”kana kwamba ni moja, bali “makao” tena mengi.. Hatujui idadi labda ni mia, au elfu, au milioni, au bilioni. Yesu kusema mengi, amini ni mengi kwelikweli.
Ndio maana kumaliza mambo mema Mungu aliyotuandalia inahitaji umilele.
Sasa kibiblia tumepewa kuyajua makao ya aina tatu tu.
Moja, alituletea tayari, Lakini Mengine mawili yatakuja baadaye.
Kao la kwanza: Lilikuwa ni yeye kutukaribisha ndani yake.
Hilo lilitimia muda mfupi sana, baada ya kuondoka, Tunaona baada ya siku 10, siku ile ya pentekoste, alirudi tena juu yetu kama Roho Mtakatifu. Akaingia ndani yetu, Kwa mara ya kwanza sisi ndio tulipokea mahusiano binafsi ya moja kwa moja na Mungu, tukaingia nyumbani mwake.
Matendo 2:1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Matendo 2:1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Mtu aliye na Roho Mtakatifu, huishi tofauti na mtu ambaye hana Roho. Kwasababu ulimwengu wake ni mwingine kabisa na ule wa kwao, Kao lako ni kuu zaidi ya kao lao la kidunia. Raha na pumziko analolipata, walimwengu hawawezi kulipata. Hekima na upeo ulionao wewe,wale hawana, Hakika kao hili ni zuri sana. Unapojazwa Roho vema, ndio unaona uzuri wa kao hilo maishani mwako.
Kao la pili: Ni kao la roho zetu.
Kumbuka roho hizi zipo ndani ya miili hii ya mavumbi. Lakini Yesu aligundua udhaifu wa miili hii hivyo, alikwenda kutundalia miili ya utukufu itokayo juu, ambayo hiyo tutavishwa, siku ile ya unyakuo itapofika, miili ambayo haijatengenezwa kwa malighafi za duniani, bali zile za kimbinguni. Miili isiyozeeka, isiyougua, isiyo sikia njaa, wala isiyokufa. Haleluya. Ni kao zuri ambalo hakuna hata mmoja wetu anapaswa alikose.
2Wakorintho 5:1 Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. 2 Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; 3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. 4 Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.
2Wakorintho 5:1 Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.
2 Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;
3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.
4 Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.
Kao la Tatu: Ni mazingira mapya ya watakatifu, ndio ile mbingu mpya na nchi mpya.
Na ule mji wa kimbinguni, Yerusalemu mpya ishukayo kutoka juu kwa Baba. Uzuri ulioko huko hauna kifani. Ni mji unawaka na kumeta-meta utufukufu wa Mungu.
Ufunuo 21:15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake. 16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. 17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika. 18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi. 19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; 20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto. 21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu. 22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake. 23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. 24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake. 25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. 26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake. 27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo
Ufunuo 21:15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.
16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.
18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.
19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;
20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.
21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.
23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.
24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.
26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.
27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo
Haya ni matatu tu! Vipi kuhusu hayo mengine ambayo hatujafunuliwa? Ukiyajua hayo, hutauchukulia wokovu kirahisi-rahisi, utafanya bidii uingie ndani ya Kristo. Mfuate Kristo akupe uzima wa milele. Ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi wasiliana nasi kwa mawasiliano unayoyapata mwisho wa makala hii, bure
Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.
Nini maana ya Mithali 19:21Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.
Jiepushe na tamaa ya Mali/kupenda fedha.
TUMAINI NI NINI?
Yubile, wengine huiita yubilei, au yubilii.
Ni mwaka wa hamsini (50), katika kalenda ya miaka ya kiyahudi. Mungu aliwaagiza wana wa Israeli, wahesabu miaka saba, kisha waizidishe mara saba, 7×7=49.
Na ule unaofuata wa 50, uliitwa mwaka wa yubile.
Ni mwaka ambao Mungu aliwaagiza wapumzike kabisa, hawakuruhusiwa kupanda wala kuvuna. Kwa miaka miwili mfululizo(yaani mwaka wa 49 na ule wa 50), kwasababu ule wa 49 ni sabato ya kila mwaka wa 7, ndio maana miaka miwili inatokea hapo. Sasa swali la kujiuliza wangewezaje kuishi miaka yote miwili bila kufanya kazi? Jibu ni kwamba Mungu aliwabariki mara dufu katika mwaka wa 48, hivyo wakafanikiwa kukusanya vingi vya kuwatosha miaka yote hiyo miwili ijayo bila kazi.
Lakini pia ulikuwa ni mwaka wa kusamehe madeni sambamba na hilo ulikuwa mwaka pia wa kuwaachilia huru watumwa.
Walawi 25:8 Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. 9 Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. 10 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. 11 Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa. 12 Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani. 13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. 14 Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua cho chote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; 15 kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe
Walawi 25:8 Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda.
9 Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote.
10 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake.
11 Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.
12 Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani. 13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake.
14 Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua cho chote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe;
15 kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe
Yubile, ilifunua kazi ya msalaba baadaye. Kwani Bwana wetu Yesu ndiye aliyekuja kutimiza kazi hii rohoni.
Kwanza ndani yake tunapokea pumziko kamili la utumwa wa dhambi. Pili tunasamehewa deni zetu (dhambi zetu), Na Tatu tunafanywa huru, katika vifungo vya shetani. Yaani Magonjwa na mapepo.
Huo ndio mwaka wa Bwana uliokubaliwa, ndio Yubile yetu halisi.
lakini pia sisi kama waamini katika mwenendo wetu, tuna mambo ya kujifunza tuipatazampo Yubile?.
Kwanza ni umuhimu wa kupumzika, kuahirisha mambo yetu kupata muda na Mungu. Si tupate tu siku moja kwa wiki kuwa karibu na Mungu. Wakati mwingine Mungu anataka kipindi kirefu. Wewe kama mfanyakazi, au umejiajiri, jiwekee utaratibu baada ya kipindi fulani uwe na likizo ndefu ambayo unaitenga kwa Mungu wako,kuutafuta uso wake, ni muhimu sana.
pili tunajifunza kusamehe watu madeni yao. Si kila tunayemdai lazima atulipe, fikiria juu ya hilo. Yesu alisema achilieni nanyi mtaachiliwa. Hujui ni wapi na wewe sikumoja utakwama, na utatamani.uachiliwe.
na mwisho kuwapa uhuru watumwa wetu ikiwa wewe ni mwajiri, fikiria kuwa mfanyakazi wako anahitaji pumziko refua, mpatie, bila kumpunguzia mshahara wake. Bwana ataona umeitunza yubilee yake pia kimwili. Na sio kufanya kumbukizi ya ndoa, au kuzaliwa, hiyo sio yubilei.
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?
SIKUKUU YA VIBANDA.
JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.
Kitabu cha Matendo ya mitume hakimtaji moja kwa moja mwandishi wake, lakini tunaweza kumtambua, kutokana na utambulisho wake mwanzoni mwa waraka huo, kwamba ni LUKA. Kwasababu waraka huu aliulekeza kwa mtu mmoja aliyeitwa Theofilo, ambaye anamtaja pia alimtumia waraka wa kwanza uliozungumzia habari za Yesu tangu mwanzo hadi siku alipochukuliwa juu, na huu si mwingine zaidi ya waraka wa Luka. Soma Luka. (1:1-3)
Ndio maana inaaminika aliyeandika waraka huu ni Luka.
Matendo 1:1 Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha, 2 hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua; 3 wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
Matendo 1:1 Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha,
2 hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua;
3 wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
Kitabu hichi cha matendo ya mitume, kama jina lake linavyojieleza kinaeleza hasaa jinsi mitume wa Bwana walivyoanza kulitekeleza lile agizo kuu la Yesu alilowaambia wakahubiri injili kwa kila kiumbe. Tangu Yerusalemu, uyahudi, samaria na dunia nzima.
Kinatufundisha jinsi Roho Mtakatifu alivyowaongoza hadi kukamilisha jukumu hilo la injili ulimwenguni mwote kwa mafanikio makubwa.
Na mambo ambayo tunajifunza kwao ni haya:
Umoja: Hawakuwa na nia tofauti tofauti, bali moja ya Kristo, walikubali kudumu katika fundisho la mitume bila shuku yoyote. Walifanya yote kwa ushirikiano kwasababu vitu vyote waligawana kama kila mtu alivyokuwa na hitaji lake.
Matendo 4:32 Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.
Mashauri ya pamoja: Hata mahali ambapo hakukueleweka vema, au kutokea kwa mikanganyiko waliweza kukaa katika Baraza la wazee na mitume, kutafakari kwa pamoja ndipo hekima ya Roho ikaamua yawapasayo kutenda.(Matendo 15: 1-21).Ndio maana hawakuwa na madhehebu.
Furaha ya Roho: Kanisa lilifurahia ibada, na imani ndani ya Kristo. Sio la watu ambao walisukumwa kufanya majukumu yao, bali wote waliona ni raha kumfuata Kristo kwa moyo mweupe.
Matendo 2:46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe
Maombi: Mara nyingi walidumu katika maombi, hekaluni, na manyumbani mwao (Watendo 1:14)
Upendo: Walipendana, Waliweza kuwa na vitu vyote shirika, hawakubaguana, wala kuwa na ubinafsi kiasi kwamba hakukuwa na yoyote aliyekuwa na mahitaji ndani ya kanisa.
Matendo 2:44 Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja
Uvumilivu: Walipitia dhiki, wengine wapigwa mawe, waliburutwa, lakini hawakuitupilia mbali imani, kinyume chake ndio injili walizidi kuihubiri.
Matendo 8:1,4
1 Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume…..4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.Hivyo hayo ni baadhi ya mambo ambayo na sisi tunaweza kujifunza katika kanisa la mwanzo.
Je! Umeokoka?
Kama bado unasubiri nini? Kumbuka hizi ni siku za mwisho. Tubu dhambi zao leo, mwamini Yesu, ukabatizwe akusamehe dhambi zako, Ikiwa utapenda kupata msaada huo wa kumpokea Kristo, basi fungua hapa kwa mwongozo huo >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
Mwandishi wa kitabu cha Mithali ni nani?
Fahamu Mwandishi wa kitabu cha Wafalme
SWALI: Naomba kufahamu maana ya 1Wakorintho 15:24-25 , hususani hapo anaposema ‘hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti’.
1Wakorintho 15:24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
1Wakorintho 15:24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
JIBU: Bwana Yesu alikuja duniani kwa kazi maalumu ya kumkomboa mwanadamu pamoja na kumkamilisha. Na ukombozi huu, aliukamilisha wote siku ile pale msalabani kwa kifo chake. Hivyo tangu wakati ule mwanadamu ambaye atampokea, tayari maadui zake wote wamewekwa chini yake, ikiwemo na mauti yenyewe.
Lakini pia ni muhimu kufahamu, ukamilifu wa ukombozi wetu, sio sasa, kwasababu ijapokuwa tumeokolewa na ndani yetu tuna uzima wa milele, bado tutakufa (ki-mwili), bado tutaugua, bado tutazeeka, bado tutakula kwa taabu, bado tutapitia dhiki na masumbufu, bado tutakutana na uovu kila mahali tuendapo.
Hivyo ‘ukamilifu’ wetu kabisa kabisa bado. Lakini ‘ukombozi’ wetu tayari, tunaokoka tukiwa hapa hapa duniani, tukifa tunakuwa tunaishi. Sasa Ndio maana Yesu alikuja mara ya kwanza kama MWANAKONDOO achukuaye dhambi za ulimwengu, lakini pia atarudi mara ya pili, ambapo safari hii atakuja kama MFALME, Atawalaye kwa mamlaka na nguvu nyingi.
Safari hii atakuja sasa kwa ajili ya huo ukamilifu, kwanza atayahukumu mataifa na falme zao,(Mathayo 25:31-46) vilevile mapepo (Ufunuo 19:20), kisha ataurekebisha huu ulimwengu ulioharibika,(Ufunuo 6:12-17) na kuufanya kuwa zaidi hata ya edeni. Kisha atatawala na watakatifu wake, kwa kipindi cha miaka elfu moja (Ndio ule utawala wa amani wa Kristo wa miaka 1000), Ufunuo 20, hapa hapa duniani, kwa wakati huo dhiki nyingi sana zitaondoka, watu wataishi muda mrefu sana, biblia inasema mtu atakayekufa na miaka mia ataitwa mtoto mchanga,(Isaya 65:20) wanyama hawatakuwa wakali tena, , hakutakuwa na laana ya nchi kutoa miiba, wala kuzaa kwa uchungu. Hichi ni kipindi ambacho dunia itakuwa salama na tulivu sana. Ni wakati wa Raha ambao Yesu amewaandalia watumishi wake.
Lakini wapo baaadhi watakufa (lakini sio sisi tutakaonyakuliwa), kwasababu shetani alikuwa bado hajahukumiwa amefungwa tu, hicho ndio kipindi ambacho Kristo atakwenda kutokomoza mauti ya mwili, hivyo shetani atafunguliwa kwa muda, ajaribu kuwaangusha watakatifu, atashindwa na kutupwa kwenye ziwa la moto pamoja na watu wote waovu (Ufunuo 20:7-10). Hapo ndipo mwisho wa yote, hakuna tena mauti, wala kifo, wala uchungu, wala huzuni,. Yesu atayakamilisha yote, ambapo adui wa mwisho ndio huyo mauti ya mwili.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. 5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. 6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure
Wakati huo ndio Kristo atakuwa ameikamilisha kazi yake yote, na kumrudishia Baba ufalme wote, kama ilivyokuwa kule mwanzo, ili tumwabudu Mungu, sio katika kukombolewa, au kuchungwa, au katika kuongozwa tena, katika ile mbingu mpya na nchi mpya, Huduma ya Kristo itakuwa imeisha.
Yatakuwa makao yetu milele. Mambo ambayo tumeandaliwa huko ndugu, jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia. Unasubiri nini leo usimpe Bwana maisha yako? Kumbuka tunaishi katika nyakati ambazo Kristo amekaribia sana kurudi. Moja ya hizi siku parapanda italia, tutakwenda mbinguni. Tubu dhambi zako, mwamini Yesu, upokee uzima wa milele.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
KWANINI KUWE NA UTAWALA WA MIAKA 1000
SIFA SITA (6), ZINAZOIKAMILISHA ILE SIKU YA BWANA ITISHAYO.
ILI TUONEKANE WAKAMILIFU MBELE ZA MUNGU.