Nini maana ya huu mstari?“Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika”

Nini maana ya huu mstari?“Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika”

SWALI: Nini maana ya huu mstari?

1Wakorintho 13:8 “Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”…Nini maana ya ukiwapo unabii utabatilika?


JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu karama iliyo kuu kuliko zote ni upendo..(1Wakorintho 12:31)..Hii Ndio karama yenye nguvu kuliko karama nyingine zote (hakuna kitu chenye nguvu kuliko upendo)…Na karama hii ni tofauti na zile karama 9 ambazo mtu anakuwa na kipawa cha kipekee kutoka kwa Mungu, ambacho kinamtofautisha yeye na wengine katika kanisa…Karama ya Upendo ni karama ambayo Mungu anampa kila mtu pindi tu anapojiweka tayari kutaka kuwa na huo upendo.

Upendo unapokuwepo mahali hata unabii unakuwa hauna nguvu..Kwamfano Adamu na Hawa walipoasi tayari walikuwa wameshajitenga na uwepo wa Mungu milele, wao (pamoja na sisi wote maana wote tumetoka kwa Adamu)..kitendo tu cha kula lile tunda, basi mwanadamu alitoka katika nafasi ya kuwa mwana wa Mungu (kuishi milele) na kubakia kuwa tu kiumbe cha Mwenyezi Mungu tu!…. Muunganiko wa Mungu na mwanadamu ulikatikia pale Edeni kutokana na Adamu na Hawa kula lile tunda.

Lakini kutokana na Upendo Mungu aliotupendea alighairi mpango huo wa kumtenga mwanadamu milele na kumrudishia tena uzima wa Milele..

Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.

Umeona hapo?

Upendo umeutangua ule unabii wa sisi kutengwa na Mungu milele, ndio maana biblia inasema hapo juu “ukiwapo unabii utabatilika”..Upendo umebadilisha mawazo ya Mungu juu yetu moja moja…Tulikuwa tumetabiriwa kupotea milele, sasa kinyume chake kwasababu ya Upendo wake kwetu tumepokea Uzima wa Milele kupitia Yesu Kristo mwanawe.

Ndio maana Biblia inazidi kutuambia hata mambo yajayo (yaani Unabii) hayawezi kututenga sisi na upendo wa Mungu ulio katika Kristo, hata malaika, hata mbingu haziwezi kututenga sisi na Upendo wa Kristo kwetu..Tumependwa tumependwa! Hakuna kinachoweza kubadilisha hilo..

Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.

34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.

35 NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?………. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,

39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”

Hivyo ni muhimu kulipata hili pendo la Kristo, ambalo linaweza kutangua hata unabii, upendo huo tukiupata tunaweza na sisi tukawapenda ndugu zetu hata kama wametufanyia mabaya kiasi gani, hata kama tulikuwa tumewatabiria kuwalipiza kisasi, upendo huo unayafuta hayo na kuwapenda ndugu pasipo masharti.

Vilevile unabii pia unatabia ya kuisha muda wake pale unapotimia, unao ukomo wake, lakini Upendo unaotoka kwa Mungu hauna mwisho, na sio Unabii tu peke yake wenye ukomo bali hata lugha, na maarifa yoyote ya kimbinguni au ya kiduniani vina ukomo haviwezi kuushinda upendo. Upendo una nguvu kuliko kitu kingine chote..Ndio maana amri iliyo kuu na kubwa kuliko zote ni UPENDO!

Biblia inasema katika..

1Wakorintho 13: 1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;

10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika”.

Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5

Bwana aliposema kuwa yeye ni “Mungu wa miungu” alikuwa na maana gani?..je! yeye ni Mungu wa sanamu?

SAYUNI ni nini?

Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments