Title August 2020

MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?

Mto Yordani uko nchi gani kwa sasa duniani?


Mto Yordani upo katika eneo la Mashariki ya kati, ni mto ambao unasimama kama mpaka wa mataifa mbalimbali, Ikiwemo Lebanoni, Syria, Israeli, na Yordani.

Ni kama vile ziwa Tanganyika lilivyo simama kama mpaka wa nchi 4, Congo, Burundi, Tanzania, na Zambia ndivyo ilivyo hata na kwa mto Yordani,

Nchi ya Yordani, unayoisikia leo hii pale mashariki ya kati, imechukua jina lake kutoka katika mto huu.

Mto huu chanzo chake ni kwenye chemchemi kadhaa zinazotiririka kutoka katika mlima Hermoni ulio mpakani mwa Lebanoni na Syria.Kisha kutoka hapo unateremsha maji yake mpaka Israeli kwenye bahari ya Galilaya/Tiberia/Genesareti. Na kutoka hapo unaibukia upande wa pili na kuendelea na safari yake moja kwa moja mpaka bahari ya Chumvi.

Tazama picha chini.

Chanzo cha mto Yordani Mashariki ya kati

Mto huu, umekuwa kitovu katika historia ya Israeli kuanzia agano la kale mpaka agano jipya. Yoshua aliusimamisha mto huu na wana wa Israeli wakavuka kuelekea Yeriko.

Vilevile mto huu huu katika agano jipya ndio makutano mengi yalikuwa yanavuka kumwendea Yesu ili waponywe.(Mathayo 19:1-2),  Na ni mto ambao Yesu mwenyewe  alibatiziwa.

Kuonyesha kuwa ili nawe upate wokovu na ushindi dhidi ya maadui zako,na ili uponywe nafsi yako, ni lazima Uvuke Yordani yako ya Rohoni..Ili ukakutane na Yesu ng’ambo ya pili huna budi kuvuka Yordani, Na Unavukaje Yordani? Ni kwa kubatizwa, kama Yesu alivyobatizwa kwenye mto ule.

Hivyo na wewe sharti ukishamwamini Yesu moja kwa moja ukabatizwe, mahali popote penye maji tele kama ishara ya kuwa umeokoka kweli kweli. Na kuwa unakwenda kuwashinda maadui zako.

Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

Wengi wanapuuzia maagizo haya ya msingi, wanadhani kuamini tu inatosha, Ndugu kubatizwa ni tendo lenye maana kubwa sana kwako rohoni, aliyetupa maagizo hayo hakuwa amekosa cha kutuagiza bali alijua umuhimu wake.

Swali Nji wewe umebatizwa ipasavyo? Kama sivyo basi kafanye hivyo.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda masomo yetu yawe yanakufikia njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Israeli ipo bara gani?

Wafilisti ni watu gani.

 

MJUMBE WA AGANO.

Zile mbao mbili za mawe Musa alizoambiwa achonge zilikuwaje?

Mlima sinai upo nchi gani? Na Je unaijua Sinai yako ya rohoni?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Mlima sinai upo nchi gani? Na Je unaijua Sinai yako ya rohoni?

Mlima sinai upo nchi gani? Na Je unaijua Sinai yako rohoni?


Mlima Sinai, au kwa jina lingine unajulikana kama Mlima Horebu, upo katika Rasi ya Sinai, Nchi ya Misri..Tazama katika picha.

sinai

Mlima huu, ni mlima ambao Mungu aliutumia kuwapa wana wa Israeli Torati na zile Amri 10. Ni mlima ambao wana wa Israeli waliutazama kwa muda mrefu kama mlima ambao unamtambulisha Mungu yupoje pale anapotaka kuzungumza na watu wake. Kufuatana na mstari huu;

Kutoka 19:16 “Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka.

17 Musa akawatoa hao watu katika kituo, akawaleta ili waonane na Mungu; wakasimama pande za chini za kile kilima. 18 Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu Bwana alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuu, mlima wote ukatetemeka sana.

19 Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti.

20 Bwana akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu”.

Unaona, wana wa Israeli walijiundia picha kuwa siku zote Mungu akishuka mahali kuzungumza na mtu/watu ni lazima kuwe na moto, na matetemeko, na upepo mkali n.k. .

Eliya naye alidhani vivyo hivyo, wakati mmoja alipokuwa anamkimbia Yezebeli, alienda kwenye mlima huu wa Musa, mlima Sinai (Horebu) kwa ajili ya kukutana na Mungu, Na yeye akidhani kuwa ili Mungu ashuke mahali Fulani ni lazima uwepo moto, na matetemeko ya ardhi. Lakini siku hiyo alipokwenda kwenye mlima huo ndio alijua ukweli wote wa Mungu.

Ni kweli kama ilivyo ada, Mungu alijifunua kwake kama alivyojifunua kwa Musa na Wana wa Israeli kwa radi, mingurumo n.k. Lakini Eliya aligundua mbona bado simwona MUNGU?

1Wafalme 19:8 “Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.

9 Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya?

10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.

11 Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za Bwana. Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za Bwana; lakini Bwana hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwana hakuwamo katika lile tetemeko la nchi;

12 na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.

13 Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya”?

Unaona Eliya alipoisia tu ile sauti ya utulivu na upole. Hapo ndipo alipousikia uwepo wa Mungu ukibubujika ndani yake akajua sasa Mungu ameshuka kuzungumza na mimi.. Hapo ndipo alipofahamu  kuwa Mungu hakai katika milima, hakai katika tufani, hakai katika upepo wa kisulisuli, bali katika utulivu na upole.

Vivyo hivyo na wewe leo hii unahitaji kumwona Mungu, unahitaji kukutana na Mungu katika Sinai, yako..Basi jifunze kujinyenyekeza mbele zake, kaa katika utulivu mkubwa wa Roho, huku ukijifunza kanuni za Mungu katika maandiko, na hakika atajifunua kwako zaidi hata ya alivyojifunua kwa wana wa Israeli. Mungu ni mnyenyekevu na hivyo anajifunua kwa wanyenyekevu kwake, wanaolitii Neno lake.

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Israeli ipo bara gani?

Neno Korbani linamaanisha nini? (Marko 7:11)

SAYUNI ni nini?

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Nitaitofautishaje sauti ya Malaika na ya Roho Mtakatifu?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Neno Korbani linamaanisha nini? (Marko 7:11)

SWALI: Neno “Korbani” linalozungumziwa katika Marko 7:11 lina maana gani?


JIBU: Ili tupate picha nzuri ya Neno hilo embu tusome sehemu zote mbili zinazozungumzia jambo hilo hilo moja.

Mathayo 15 :1-6

1 “Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema, 

2 Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula. 

3 Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? 

4 Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. 

5 Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu, 

6 basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu”.

Marko 7:8-13 

“8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. 

9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. 

10 Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. 

11 Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, NI KORBANI, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; 

12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; 

13 huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.

Kama tunavyosoma hapo, biblia imeshatoa tafsiri ya hilo Neno Korbani mbele  kidogo kuwa linaamanisha WAKFU.

Kitu chochote kilichowekwa wakfu ina maana kuwa hakitumiwi kwa mtumizi mengine yoyote isipokuwa kwa Mungu tu. Sasa katika habari hiyo, utaona Bwana Yesu alikuwa anawelenga sana sana Mafarisayo na waandishi kwa unafki wao kwa kujifanya kuwa wanaishika torati yote, wakati yapo mambo mengine mengi ya torati walikuwa wanayakaidi.

Na ndio hapo Bwana Yesu akawatolea mfano mmojawapo, ambao ulihusu  kuwaheshimu wazazi, kama mojawapo ya amri ambazo Mungu alizitoa zishikwe na watu wote. Na biblia iliposema kuwaheshimu wazazi, ilikuwa sio tu kuwaonyeshea heshima na utiifu, hapana ilikuwa ni zaidi ya hapo ikiwemo kuwahudumia kifedha, hususani wakiwa wazee.

Sasa hawa waandishi walikuwa wanayapindisha hayo maagizo, kwa kuwashurutisha watu, kuepuka majukumu yao ya kuwahudumia wazazi wao, kinyume chake walikuwa wanawaambia hayo wanayoyapata kwa ajili ya wazazi  wanaweza tu kuyafanya kuwa wakfu(Korbani) mbele za Mungu,  na ikawa ni sawa tu na kama wamewahudumia wazazi wao, isiwe dhambi mbele za Mungu.

Hivyo kama mtu alikuwa ametenga fedha yake kiasi kwa ajili ya matumizi ya baba yake au mama yake kule kijijini, basi walihimiziwa walizete Hekaluni kwa ajili ya Mungu kama wakfu..

Na mzazi akimuuliza, mbona huniletei matumizi, basi Yule kijana atasema, fedha hii au nafaka hii  niliyoivuna ni wakfu kwa Mungu.

Hivyo watu wengi wakawa wanawaacha wazazi wao katika hali ya shida na umaskini wa hali ya juu. Jambo ambalo Mungu hakuliagiza.

Ndipo Yesu anawakemea hawa waandishi kwa kuyapindua maagizo ya Mungu, ya kutotimiza majukumu yao ya kuwahudumia wazazi  kwa kanuni zao walizojitungia.

Nini tunajifunza?

Kumbuka biblia haifundishi watu wakimbie majukumu yao ya kifamilia kwa wazazi wao hususani pale wanapokuwa wazee kwa kisingizio kuwa wanamtolea Mungu.. Biblia inasema usipowahudumia watu wa nyumbani kwako, wewe ni kuliko hata mtu asiyeamini(1Timotheo 5:8).. Lakini pia biblia haifundishi kuwa watu waache kumtolea Mungu kwa kisingizio kuwa wanayo majukumu mengi ya kifamilia.

Lazima ujue kila utoaji una sehemu yake, na Baraka zake. Watu wa nyumbani kwako wana sehemu yao, maskini wana sehemu yao, na Mungu pia anayosehemu yake..Usipojua hilo utakuwa nawe pia unatangua torati kwa kufuata mawazo yako mwenyewe uliyojitungia. Kwasababu wapo watu wengi leo hii, wameacha kupeleka fedha zao kanisani, au kwenye huduma za Mungu, wanasema sitoi sadaka yangu, na ukiwauliza ni kwanini?, wanasema mbona hatuoni zikienda kuwahudumia maskini na wajane kama ilivyokuwa katika kanisa la kwanza la mitume…Lakini mtu huyo huyo hajui kuwa watakatifu wa kanisa la kwanza sio kama hawa wa sasahivi, wale walikuwa wapo tayari kuuza mashamba yao na viwanja vyao na kuleta kwa Mungu, hivyo kwa namna ya kawaida nishati ya kutosha ni lazima iwepo nyumbani kwa Mungu hata kuwahudumia mpaka wajane.

Lakini kama wewe unampelekea Mungu shilingi, wakati hiyo fedha hata gharama za umeme kanisani hazijitoshelezi, unapata wapi ujasiri wa kutaka kujua mfuko wa kanisa unatumikaje?? Fikiria tu. Je wewe unaweza kuuza shamba lako kule kijijini, umletee Mungu?

Bwana atusaidie,. 

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Je! Mwanamke anapaswa afunikwe kichwa anapokuwa ibadani?

WANA JUHUDI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA.

MIJI YA MAKIMBILIO.

JE KUVAA PETE NI DHAMBI?

MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.

YOTE NAMTOLEA YESU_Tenzi za Rohoni.

 Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu

Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu. (Blessed assuarance)


Wimbo huu ulindikwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Fanny Crosby, Mwanamke huyu japo aliishi kwa miaka 95 akiwa kipofu,lakini hakuacha kuitumia neema Mungu aliyompa kutangaza injili kwa njia ya Nyimbo zenye muundo wa Tenzi za rohoni na nyinginezo, katika maisha yake alifanikiwa kuandika nyimbo zaidi ya 8000, Na hii nyimbo  “Ndio dhamana Yesu wangu” Ikiwa mojawapo, Nyingine inayojulikana sana mpaka leo ni “Usinipite mwokozi” yeye pia ndio aliyeiandika nyimbo hii alipokuwa amewatembelea wafungwa gerezani(angalia historia yake chini).

Phoebe Knapp

Phoebe Knapp

Sasa Siku moja  alipokuwa amemtembelea rafiki yake nyumbani kwake  aliyeitwa Phoebe Knapp, ambaye alikuwa ni mtunzi wa sauti za nyimbo, wakiwa  nyumbani kwake Phoebe alianza kupiga mdundo wake aliokuwa ameutunga, kisha baada ya muda alimuuliza Fanny, Je unaweza kuniambia mdundo huu ni wa nyimbo gani?

Ndipo Fanny akamwambia “Ndio dhamana Yesu wangu”. Basi hapo ndio pakawa mwanzo wa mdundo na utunzi wa wimbo huo (1873).

Ndio dhamana Yesu wangu.

Ndiyo dhamana, Yesu wangu;
Hunipa furaha za mbingu;
Mrithi wa wokovu wake,
Nimezawa kwa Roho wake.
 
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.
 
Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu;
Aniletea malaika,
Wananilinda, tutaokoka.
 
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.
 
Sina kinyume; nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu;
Usiku kucha kuna nuru;
Mwokozi wangu; ndimi nuru.
 
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.
 
Hali na mali; anitwaa!
Mara namwona anifaa,
Nami nangonja kwa subira;
Akiniita, nije mara.
 
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.

*****

Uimbapo wimbo huu  kumbuka ni kipofu ndiye aliyeuandika, nawe pia unaposema “Ndio dhamana Yesu wangu” Basi awe kweli  wokovu wako. Mpende yeye bila unafki na kumtumikia kwasababu ndiye aliyekufa kwa ajili yako.

Je! Umeokoka? Unajua kuwa Unyakuo upo karibu sana, kwasababu tunaishi katika kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia? Na kwamba hatutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili? Siku hizi zimekwisha, Hivyo kama upo tayari kumpa Yesu maisha yako leo ili wimbo huu uwe na maana kweli kwako. Basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye  namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

USINIPITE MWOKOZI Lyrics

YOTE NAMTOLEA YESU_Tenzi za Rohoni.

BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics

CHA KUTUMAINI SINA lyrics

KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

MPINGA-KRISTO

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

UFUNUO: Mlango wa 1

Rudi Nyumbani:

Print this post

YOTE NAMTOLEA YESU_Tenzi za Rohoni.

Yote namtolea Yesu_tenzi za rohoni|Swahili hymn.


Wimbo huu uliandikwa na ndugu mmoja wa kimarekani aliyeitwa Judson W. Van DeVenter, Ndugu huyu alilelewa katika mazingira ya kikristo, aliokoka akiwa na miaka 17, kuanzia huo wakati wito wa kujitoa kikamilifu ulianza  kuita ndani yake,lakini bado hakufanya uamuzi huo. DeVenter alifanikiwa kusoma  mpaka chuo kikuu na kutunikiwa shahaba ya Sanaa, aliajiriwa kama mwalimu na mwongozaji katika shule za sanaa, hiyo ilimfanya aweze kusafiri sehemu nyingi mbalimbali katika bara la Ulaya kutokana na kazi yake ya sanaa.

Zaidi ya hilo alisomea pia na kufundisha elimu ya muziki, ilimchukua miaka 5 mpaka “Kumtolea yote Yesu”, Na hiyo ilikuwa ni baada ya marafiki zake kumshawishi sana, aingie katika kazi ya kumtumikia Mungu.

Mwaka 1896 Siku moja alipokuwa anafanya huduma ya muziki katika kanisani, hii ndio siku aliyoamua kuyasalimisha maisha yake ya ki-utumishi moja kwa moja kwa Kristo akiwa na miaka 41, aliamua kujitoa moja kwa moja kwa ajili ya kuifanya kazi ya unjilisti, na ndipo hapo huu wimbo “Yote namtolea Yesu” ulipozaliwa ndani ya moyo wake.

YOTE WA YESU.

Yote Namtolea Yesu.
Nampa moyo wote,
Nitampenda siku zote,
Namwandama kila saa.
 
Yote kwa Yesu,
Yote kwa Yesu,
Yote kwako, Ee Mwokozi,
Natoa sasa.
 
Yote namtolea Yesu,
Nainamia pake;
Nimeacha na anasa,
Kwako Yesu nipokee
 
Yote kwa Yesu,
Yote kwa Yesu,
Yote kwako, Ee Mwokozi,
Natoa sasa.
 
 Yote namtolea Yesu,
Nifanye niwe wako;
Nipe Roho yako, Bwana,
Anilinde daima,
 
Yote kwa Yesu,
Yote kwa Yesu,
Yote kwako, Ee Mwokozi,
Natoa sasa.
 
Yote namtolea Yesu,
Nami naona sasa;
Furaha ya ukombozi;
Nasifu jina lake. 
 
Yote kwa Yesu,
Yote kwa Yesu,
Yote kwako, Ee Mwokozi,
Natoa sasa.

*****

Je! Na sisi tunapouimba wimbo huu tunaweza kumtolea Yote Yesu?. Je! mali zetu tunaweza kumpa yeye, nguvu zetu tunaweza kuzielekeza kwake?, akili zetu tunaweza kuzitumia ziitende kazi ya Mungu? Kama sivyo basi wimbo huu tutauimba kinafki.

Bwana atutupe kutambua hayo.

Shalom.

Je! Umeokoka? Ikiwa bado hujaokoka na unahitaji kuokoka leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA


Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo mbalimbali ya Neno la Mungu, kwa njia ya whatsapp yako, basi tutumie ujumbe kwa namba hii :+255 789001312

Mada Nyinginezo:

YESU KWETU NI RAFIKI

NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics

BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics

KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

MAONO YA NABII AMOSI.

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

MAANA YA KRISTO/ JINA KRISTO LINA MAANA GANI?

Neno Kristo, na Masihi ni kitu kimoja, isipokuwa kwa lugha ya Kiebrania linatamkwa kama Masihi, lakini kwa lugha ya kigiriki linatamkwa kama Kristo.

Yohana 1:41 “Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo)”.

Hivyo Neno hili Kristo/Masihi linamaanisha mtiwa mafuta.

Mtiwa mafuta ni mtu yeyote aliyechaguliwa au aliyetengwa na Mungu kuwa wakfu kwa ajili ya kutimiza kusudi lake Fulani..Aidha na kuokoa, au kutawala, au kuchunga.

> Hivyo manabii wote unaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi au Kristo kwa Mungu, kwa lengo la kuitabiria Israeli, na kuwaelekeza maagizo yatokayo kwa Mungu.

1Nyakati 16:22 “Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu”.

> Makuhani wote tunaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi au maKristo wa Bwana wakifanya kazi ya upatanisho wa dhambi za watu na makosa yao.

> Waamuzi wote unaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi wa Bwana waliotiwa mafuta kwa lengo la kuwakomboa wanadamu.Wakina Gideoni, Samsoni, Yeftha wote hao walikuwa ni masihi wa Bwana.

> Vilevile wafalme wote iwe ni wa wale waliotoka Israeli, au hawajatoka Israeli tunaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi wa Bwana kwa ajili ya kuwaongoza watu wake.

1Samweli 24:5 “Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.

6 Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA,neno hili,kuunyosha mkono wangu juu yake,kwa maana yeye ni masihi wa BWANA”.

 

Isaya 45:1 “Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake,ambaye nimemshika mkono wake wa kuume,ili kutiisha mataifa mbele yake,name nitalegeza viuno vya wafalme;ili kufungua milango mbele yake,hata malango hayatafungwa.

2 Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma”;

Lakini hao wote walikuwa ni kivuli cha MASIHI/KRISTO MKUU NA HALISI atakayekuja, ambaye alitiwa mafuta mengi sana yasiyoelezeka kuliko wote, biblia inasema hivyo, na huyo si mwingine zaidi ya YESU.

Waebrania 1:8 “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; KWA HIYO MUNGU, MUNGU WAKO, AMEKUTIA MAFUTA, MAFUTA YA SHANGWE KUPITA WENZIO”.

Na ndio maana haitwi tu Yesu peke yake, bali anaitwa YESU KRISTO.

Yesu Kristo ametiwa mafuta ya mengi sana ya kuwakomboa wanadamu. Yeye anayo mafuta yote ya kikuhani ndani yake, anayo mafuta ya kifalme ndani yake, anayo mafuta ya kinabii ndani yake, anayo mafuta ya kichungaji ndani yake.. Yaani kwa ufupi mafuta yote ya karama za Mungu yapo ndani yake.

Hivyo mtu akimwamini Yesu, basi amepata kila kitu, ikiwemo ukombozi wa roho yake.

Lakini tahadhari ni kuwa biblia imetabiri kuwa siku za mwisho kutatokea makristo wengi wa uongo ili kuwadanganya watu wengi.

Mathayo 24:24 “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele”.

Kumbuka anasema watatokea makristo, hasemi ma-yesu, ikiwa na maana kuwa watakuwa ni watiwa mafuta lakini ni watiwa mafuta ya uongo, watakuwa wanaweza kweli wakawaombea watu kwa jina la Yesu na wakapona lakini injili yao ni injili potofu isiyoweza kumwokoa yeye, wala hao anaowaongoza.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema..

Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Hivyo je! Swali na  wewe umechukuliwa na hili wimbi la makristo wa uongo?

Tunaishi katika wakati mgumu na wa hatari kuliko yote katika historia, hivyo kama maisha yako yapo mbali na Kristo basi ujue upo hatarini sana kupotezwa.

Kwanini usimpe Kristo leo maisha yako ayabadilishe, kisha yeye mwenyewe akupe Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kuijua kweli yote ya kimaandiko, ambaye atakaa ndani yako kukulinda mitego yote ya ibilisi?. Kama leo upo tayari kufanya hivyo, na unasema sitaki tena maisha ya dhambi nataka Yesu aniokoe awe peke yake masihi ndani yangu. Basi fungua link hii kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

UPAKO NI NINI?

KUWA MWAMINIFU KWA MANENO YAKO MWENYEWE,

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

Yakobo alikuwa na watoto wangapi?

REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

KUWA MWAMINIFU KWA MANENO YAKO MWENYEWE,

Kuwa mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe, ni muhimu sana!.


Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe. Karibu tujifunze biblia.

Mwinjilisti mmoja alichukuliwa katika maono mbinguni akakutana na Bwana Yesu, alionyeshwa mambo mengi yatakayotokea baada ya Maisha haya, kwa wema na waovu, lakini Pamoja na hayo kuna mambo mengine aliambiwa ambayo naamini leo tukiyatafakari yatatusaidia.

Na jambo mojawapo aliloambiwa lilikuwa ni kuhusu “uaminifu”…kulingana na maelezo yake, anasema Bwana Yesu alimwambia haya maneno;

Neno langu ni nguvu inayoshikilia vitu vyote. Kwa kiwango ambacho unavyoamini Neno langu ni kweli, ndivyo unavyoweza kufanya vitu vyote. Wale ambao wanaamini kwamba maneno Yangu ni kweli, basi watakuwa pia wakweli kwa maneno yao wenyewe, Ni asili yangu kuwa kweli, na uumbaji huliamini Neno Langu kwa sababu mimi ni mwaminifu na kwake.

Wale ambao ni kama mimi, pia huwa ni wakweli kwa maneno yao wenyewe. Neno lao ni hakika, na ahadi zao ni za kuaminika. ‘ndio’ yao inamaanisha ‘NDIO!’ na ‘hapana’ yao inamaanisha ‘HAPANA!’. Ikiwa maneno yako mwenyewe sio kweli, ni lazima pia utaanza kutilia shaka maneno Yangu, kwa sababu udanganyifu uko moyoni mwako. Ikiwa wewe sio mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe, ni kwa sababu bado hujanijua kabisa mimi ni nani, mimi ni mwaminifu kwa maneno yangu. Ili kuwa na imani, lazima uwe mwaminifu kwa maneno yako. Nimekuita utembee kwa imani kwa sababu mimi ni mwaminifu. Hiyo ni asili yangu”.

**mwisho**

Ndugu moja ya tatizo kubwa linalowakabili wakristo wengi wa sasa, ni kukosa UAMINIFU. Na uaminifu unaanza kwa mtu kukosa uaminifu kwa mambo yake mwenyewe kwanza. Kwamfano mtu baada ya kumpa Yesu Maisha yake, akaahidi kwamba hatasengenya tena, hatatukana, hataiba, hatafanya hichi au kile anaahidi pia atamtumikia Mungu, au atakuwa mtu wa kumtolea Mungu sana n.k..lakini baada ya muda kupita anaanza kwenda kinyume na kile alichokisema au alichokipanga. Ndugu hiyo ni hatari sana.

Maneno hayo ya mwinjilisti huyo aliyoambiwa na Bwana, nayaamini asilimia mia kuwa ni kweli. Hata katika hali ya kawaida kama huwezi kuwa mwaminifu kwa mali yako mwenyewe ni Dhahiri kuwa haiwezekani kuwa mwaminifu kwa mali ya mwingine. Kama kiatu chako mwenyewe hukitunzi wala hukijali utakijali vipi kiatu cha mwingine aliyekuazima ukivae kwa muda tu!. Uaminifu wa mtu unaanza kwa kile alichonacho yeye mwenyewe, ndipo aweze kuwa mwaminifu kwa kitu cha mwingine.

Kadhalika huwezi kuwa mwaminifu kwa Maneno ya Mungu, kama sio mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe.

Katika Luka 16:10 Bwana Yesu alisema maneno haya..

“Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia”.

Hivyo tujifunze kuyashika maneno yetu wenyewe..Ndipo tutakapoona Neno la Mungu likiwa na nguvu juu ya maisha yetu… Ukisema sitaki hichi au kile!, au nataka hichi!..basi kishikilie hicho kweli kweli usiwe na mawazo mawili mawili… Hiyo nguvu ya Maamuzi ndio chanzo cha nguvu zako za kiroho. Hata likitokea jambo mbele yako, na ukanukuu mstari Fulani kwenye biblia kwa Imani, basi jambo lile ulilolitamka kufuatia mstari huo uliounukuu, litatimia kama ulivyolisema kwasababu wewe pia huwa ni mkweli katika maneno yako…Hivyo Mungu atahakikisha na yeye analifanya neno lake kuwa kweli juu yako. Lakini tusipokuwa wakweli kwenye maneno yetu, basi kuna uwezekano pia neno la Mungu lisiwe kweli juu yetu. Tunaweza tukalinukuu sana na tusiona matokeo yoyote.. kwasababu sisi wenyewe sio waaminifu.

Bwana atusaidie, na atubariki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Je! Ni ipi tarehe sahihi Evil-merodaki alimtoa Yekonia gerezani?

 

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

ZABURI 91, NI ZABURI YENYE NGUVU NYINGI.

SABATO TATU NI NINI?

Je! Mtume Paulo alikuwa ni Mrumi, Myahudi au raia wa Tarso?

JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?

NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,

Hakuna mtu anenaye katika Roho,kusema Yesu amelaaniwa

Rudi Nyumbani:

Print this post

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

Kwanini Amelaaniwa aangikwaye msalabani?


Kutundikwa msalaba au kwa jina lingine kutundikwa mtini, ilikuwa ni adhabu iliyotekelezwa kwa watu wenye makosa ya hali ya juu sana.                               

Adhabu hii ilikuwa sio tu ilikuwa inatekelezwa na watu wa mataifa mengine kama wengi wanavyodhani ni Warumi tu, hapana bali pia ilikuwa inatekelezwa na Israeli pia.

Ni adhabu yenye mateso mengi sana, na vilevile ni adhabu ya aibu. Waliokuwa wanatundikwa msabani walikuwa sana sana ni wauaji. Makosa ambayo yalikuwa yanathibitisha kuwa wamelaaniwa na Mungu.

Kumbukumbu 21:22 “Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti;

23 mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako”.

Utasoma sehemu nyingi, katika biblia mifano ya watu waliangikwa msalabani. (Mwanzo 40:18-19, Esta 2:22-23, Esta 7:10)

Jambo hilo hilo tunaliona mpaka katika kipindi cha karibu na agano jipya, katika ule ufalme wa Rumi, wafungwa wote waliokuwa na kesi kubwa za mauaji au wizi, n.k. Adhabu yao ilikuwa ni kuangikwa/kutundikwa msalabani ukiwa hai.

Lakini cha ajabu ni kwamba, adhabu zilizokuwa zinawahusu watu waliolaaniwa, zilimkuta mtu ambaye hakuwahi kutenda dhambi hata moja..Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO

Wagalatia 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, AMELAANIWA KILA MTU AANGIKWAYE JUU YA MTI;

14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani”.

Lakini ni kwanini yamkute hayo yote?

Je ni ilikuwa ni bahati mbaya tu? Au Mungu alishindwa kumzuia? Jibu ni la, ilitokea vile kwa makusudi kabisa, ili ile hati ya mashitaka ya waliolaaniwa ifutwe juu yetu, aliibeba yeye ile hati ya laana, na ndio maana pale ambapo Baraba muuaji alipopaswa auawe, Yesu aliuawa badala yake, pale ambapo wewe mzinzi ungepaswa uhukumiwe milele kwa makosa yako, Yesu aliichukua laana hiyo siku ile msalabani, pale ambapo wewe uliye na dhambi ambazo nyingine ni aibu kuzitaja, Yesu alizichukua, hatia zote kwako.

Lakini hizo haziwezi kufutika juu yako, hivi hivi tu, bali ni  mpaka uende kuzisalimisha msalabani.

Na ndio maana unahitaji kumpokea Yesu maishani mwako, vinginevyo hati ya mashitaka ya dhambi zako zitaendelea kubakia juu yako hadi siku ya mwisho, na utahukumiwa kama mkosaji.

Lakini ikiwa leo upo tayari kumpokea Yesu maishani mwako, basi leo leo atazifuta dhambi zako bure kabisa, haijalishi wewe ni mwenye dhambi kiasi gani.

Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.

Hivyo kama upo tayari leo kumpa Yesu maisha yako, basi uamuzi huo ni wa busara, hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba  >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Tafadhali Share na wengine, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au katika namba hii hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

Nifanye nini ili niwe na uhakika nikifa naenda mbinguni?

MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.

USINIPITE MWOKOZI Lyrics

Rudi Nyumbani:

Print this post

Watoto wa Ibrahimu/Wana wa Ibrahimu walikuwa ni wangapi?

Je! Watoto wa Ibrahimu/Wana wa Ibrahimu walikuwa ni wangapi?


Jumla ya wana wa Ibrahimu walikuwa ni nane (8). Kulingana na Biblia.

Mwana wa kwanza alikuwa ni Ishmaeli, ambaye alizaliwa na kijazi wa mke wake Sara aliyeitwa Hajiri (Mwanzo 16:1-4).

Mwana wa Pili, alikuwa ni Isaka,(Ndiye mwana wa Ahadi) ambaye alizaliwa miaka 14 baada ya Ishmaeli kuzaliwa.

Mwanzo 21:1 “Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema.

2 Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. 3 Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia”.

Sara alipofariki, Ibrahimu akaoa mke mwingine, aliyeitwa Ketura. (Mwanzo 25:1-2)

Huyu Ketura ndiye aliyemzaliwa Ibrahimu wana wengine 6. Kufanya jumla ya watoto wote wa Ibrahimu kuwa 8, Biblia haielezi kuwa alikuwa na wana wengine wa kike.

Lakini katika wana hao wote, ni mmoja tu, aliyekuwa mrithi wa Ibrahimu, naye ni Isaka. Na siri moja ni kuwa wale wana wengine Ibrahimu aliwapa zawadi nyingi, lakini Isaka alipewa vyote, zawadi pamoja na urithi, kwasababu yeye ndiye aliyekuwa mwana wa Ahadi kutoka kwa Mungu.

Mwanzo 25:5 “Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo.

6 Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu”.

Vivyo hivyo na sisi, tunaweza sote tukawa ni watu wa Mungu, tulioumbwa na Mungu, lakini si sote tukawa wana wa ahadi wa Mungu mfano wa Isaka. Wana wa ahadi ni wale waliozaliwa mara ya pili (yaani waliokoka). Na hao ndio Mungu kawaandalia vyote, thawabu pamoja na urithi wa ufalme wa mbinguni.

Ambapo Yesu alikwenda kuwaandalia waliompokea, Na siku atakaporudi, atawagawia urithi huo ambao alikuwa akiwaandalia kwa miaka 2000. Mambo ambayo jicho halijawahi kuoa wala sikio kusikia.

Swali la kujiuliza  Ni je!  na wewe ni mmojawapo wa wana wa Ahadi? Kama hujaokoka na kusimama, bado hujawa mwana wa ahadi, Lakini habari njema ni kuwa nafasi bado ipo lakini haitakuwepo siku zote ya wewe kufanyika hivyo.. Kama upo tayari leo hii kufanyika mtoto wa Mungu, na kuachana na dunia, na kutaka Yesu akuokoe, basi uaumuzi huo ni wa busara kwako, unachopaswa kufanya ni kufungua hapa ili upate maelekezo ya sala ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tazama chini kwa masomo mengine ya rohoni.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp yako mara kwa mara tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

WATOTO WA YESE KATIKA BIBLIA.

Wafilisti ni watu gani.

Israeli ipo bara gani?

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.

NENO NI LILE LILE, LAKINI UJUMBE NI TOFAUTI.

KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

WATOTO WA YESE KATIKA BIBLIA.

Watoto wa Yese katika biblia walikuwa ni wangapi?


Kitabu cha Samweli kinaonyesha Yese alikuwa na wana nane(8), Daudi akiwa ndio mwana wa mwisho kabisa, Lakini kitabu cha Mambo ya Nyakati  wa kwanza kinaonyesha Yese alikuwa na Wana saba (7). Sasa swali linakuja Je! takwimu zipi ni sahihi? Je! biblia inajichanganya yenyewe?

Jibu  ni hapana..

Tusome..

1Samweli 16:10 “Yese akawapitisha WANAWE SABA mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.

11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, AMESALIA MDOGO WAO, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku”.

Soma tena.

1Nyakati  2:13 “na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;

14 na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai;

15 na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;

16 na maumbu yao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.”

Sasa ukiangalia hapo utaota kitabu cha Mambo ya Nyakati hakijatoa idadi Fulani kwamba wana wa Yese kuwa walikuwa ni saba tu, hapana badala yake kimeorodhesha majina, Sasa kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia utagundua kuwa kitabu cha mambo ya Nyakati kiliandikwa miaka ya mbeleni sana ukilinganisha na kitabu cha Samweli. Na kitabu hicho cha Mambo ya Nyakati wa kwanza kilikuwa kimejikita zaidi katika kuelezea uzao wa makabila ya Israeli(Vizazi vya wana wa Israeli).

Hivyo ilikuwa ni kawaida mtu asiyekuwa na uzao hakuweza kuorodheshwa katika orodha hiyo. Kwahiyo ni sahihi kusema Yese alikuwa na wana 9,  lakini mmojawapo alifariki, pengine akiwa bado hajapata uzao, na hivyo mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati akaona hakukuwa na haja ya kumworodhesha pale. Ni kama tu Samweli alivyoacha kuwaorodhesha dada zao wawili. Kama isingekuwa kitabu cha Mambo ya Nyakati kuwaorodhesha ni rahisi kudhani walizaliwa wana wa kiume tu kwao, lakini kulikuwa hakuna haja ya kuwaorodhesha pale, kutokana na muktadha ya maudhui ya pale, kwamba waliokuwa wanahitajika na wana wa kiume, tu.

Ndivyo ilivyokuwa hata kwa mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati, walioorodheshwa na wale wenye uzao tu.

Kwahiyo kwa kuhitimisha ni kuwa Yese alizaa watoto nane (8) wakiume, na wawili (2) wa kike, Lakini mmoja baadaye alikuja kufa, wakabakia wana wa kiume 7 ndio wale walioorodheshwa katika 1Nyakati.

Shalom.

Tafadhali, angalia masomo mengine chini, ujifunze zaidi;

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo mballimbali kwa njia yaWhatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Adamu alikuwa na watoto wangapi?

Nuhu alikuwa na watoto wangapi?

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 8 (Kitabu cha Ezekieli)

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

YAKINI NA BOAZI.

MANENO ALIYOWEZA KUTAMKA YESU TU PEKE YAKE.

Rudi Nyumbani:

Print this post