Title Devis

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Karibu tuongeze maarifa katika Neno la Mungu,

Tukisoma kwenye biblia kitabu cha warumi 4 tunaona mtume Paulo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kwa matendo yake bali kwa Imani, lakini tukisoma tena katika kitabu cha Yakobo 2, Yakobo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki kwa Imani tu, bali pia na kwa matendo. Tunaona sentensi hizi mbili zinaonekana kama kupingana, Lakini je! Biblia kweli inajipinga au ni sisi uelewa wetu ndio unaojipinga??..tuichambue mistari hii miwili kwa undani kidogo..

1) Warumi 4:1-6

“1 Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili?
2 KWA MAANA IKIWA IBRAHIMU ALIHESABIWA HAKI KWA AJILI YA MATENDO YAKE, ANALO LA KUJISIFIA, LAKINI SI MBELE ZA MUNGU.

3 Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.

4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.

5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

6 Kama vile Daudi anenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,.

Ni dhahiri kuwa hapa mtume Paulo alipokuwa anazungumzia MATENDO, alikuwa analenga matendo yatokanayo na sheria  ya kwamba hakuna mwanadamu yoyote anaweza akasimama mbele za Mungu kwa matendo yake kuwa ni mema au amestahili kumkaribia Mungu.

Kwa mfano mtu kusema nimestahili kwenda mbinguni kwa matendo yangu mazuri, mimi sio mwasherati, sio mwizi, sio mtukanaji, sio mlevi, sio mwongo, sio mwuuaji n.k. kwa kusimamia vigezo kama hivyo hakuonekana hata mmoja aliyeweza kumpendeza Mungu isipokuwa mmoja tu naye ni BWANA wetu YESU KRISTO! wengine wote kama biblia inavyotaja kuanzia Adamu mpaka mwanadamu wa mwisho atakayekuja duniani Mungu alishawaona wote tangu mwanzo kuwa wamepungukiwa na utukufu wake,

Warumi 3:23″ kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; “

 na ukisoma pia Zaburi 14:2-3 inasema

 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.” 

Hivyo hii inadhihirisha kabisa hakuna hata mmoja atapata kibali mbele za Mungu kwa matendo yake mazuri.

 Lakini swali ni je! kama sio kwa matendo, basi mtu atapata kibali mbele za Mungu kwa njia gani tena??..

Ukiendelea kusoma mbele tunasoma mtume Paulo anasema ni kwa njia moja tu tunaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu nayo ni njia ya kumwamini BWANA YESU KRISTO tu!. Ndio njia pekee inayotupa sisi kupata kibali mbele za Mungu, kwa namna hiyo basi tunayo haki ya kuwa na uzima wa milele, kwenda mbinguni, kubarikiwa kwasababu tumemwamini mwana wa Mungu YESU KRISTO na sio kwa matendo mema tuyatendayo.

Kumbuka zipo dini nyingi zenye watu ambao wanatenda matendo mema lakini je! wanao uzima wa milele ndani yao? utakuta ni wema kweli wanatoa zaka, wanasaidia maskini, sio waasherati, sio  walevi n.k. lakini bado Mungu hawatambui hao. Lakini sababu ni moja tu, hawajamwamini mwana wa Mungu ili aziondoe dhambi zao.

Kwahiyo tunaona hapo jambo kuu Mungu analolitazama ni wewe kumwamini mwana wa Mungu, na ukishamwamini (yaani kumpa maisha yako) ndipo ROHO wake MTAKATIFU anakutakasa na kukufanya uishi maisha matakatifu ya kumpendeza.

2). Lakini tukirudi kusoma kitabu cha Yakobo 2:21-26 

“21 JE! BABA YETU IBRAHIMU HAKUHESABIWA KUWA ANA HAKI KWA MATENDO, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?

22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.

23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.

24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.

25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?

26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Katika kifungu kile cha kwanza ukiangalia kwa undani utaona kuwa mtume Paulo alikuwa anazungumzia juu ya MATENDO YATOKANAYO NA SHERIA. Lakini hapa Yakobo hazungumzii habari ya matendo yatokanayo na sheria bali ni MATENDO YATOKANAYO NA IMANI.. hivyo ni vitu viwili tofauti. 

MFANO WA MATENDO YATOKANAYO NA IMANI:  

Kwamfano: Mtu amepimwa na daktari na kuambiwa kuwa anaugonjwa wa kisukari, na hatakiwi kula vyakula vyenye asili ya sukari na wanga. lakini mtu yule akilishikilia lile Neno kwenye biblia Mathayo 8:17 linalosema ” ….Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu. ”

Na kuliamini na kuamua kuchukua hatua na kusema mimi ni mzima na sio mgonjwa kwasababu yeye alishayatwaa madhaifu yetu, na kusimama na kutembea kama mtu mzima asiyeumwa na kula vyakula vyote hata vya sukari na wanga ingawa daktari alimkataza, akiamini kuwa amepona kwa NENO lile atapokea uponyaji wake. sasa  kitendo cha yeye kuchukua hatua ya kuishi kama mtu mzima ambaye haumwi japo ni mgonjwa na kula vile vyakula alivyoambiwa asile hicho ndicho kinachoitwa MATENDO YA IMANI Yakobo aliyoyazungumzia..

Unaona hapo haki ya huyo mtu kuponywa haikutokana na matendo ya sheria (yaani utakatifu, kutokuwa mwasherati, au mlevi au mwizi n.k.). bali ni matendo yaliyotakana na kumwamini YESU KRISTO katika NENO lake ndio yaliyomponya. Na ndio jambo hilo hilo lililomtokea Ibrahimu pale alipomwamini Mungu na kumtoa mwanae kuwa dhabihu, kwahiyo kile kitendo cha yeye kumtoa mwanawe hayo ndiyo MATENDO yanayozungumziwa na Yakobo YA IMANI kwasababu hiyo basi ikampelekea yeye kupata haki mbele za Mungu.

Unaona hapo haikuwa sababu ya yeye kutokuwa mwongo, au mlevi, au muuaji n.k. ndio kulimpa haki yeye ya kubarikiwa hapana bali ni kumwamini Mungu na kuiweka ile imani katika matendo. Kwasababu kama ingekuwa kwa usafi wake Mtume Paulo asingesema Ibrahimu hana la kujisifu mbele za Mungu.

Vivyo hivyo kwa mambo mengine yote kwamfano haki ya kuzungumza na Mungu, haki ya kuponywa magonjwa,  haki ya kubarikiwa, haki  ya kwenda mbinguni, haki ya karama za rohoni, haki ya kuwa mrithi, n.k. havitokani na MATENDO YA SHERIA bali MATENDO YA IMANI. Kwa sisi kumwamini YESU KRISTO katika Neno lake ndipo tunapopata vyote.

Kwahiyo matendo yote mema ya sheria yanakuja baada ya kuwa ndani ya Kristo na hayo ndiyo yanayokupa uhakika kama upo ndani ya Kristo, ni kweli huwezi ukawa ni mkristo halafu bado ni mlevi, mwasherati, mwongo, mwizi n.k.. lakini jua katika hayo mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kama tukitaka tuhesabiwe katika hayo hakuna mtu atakayesimama mbele za Mungu.

Kumbuka Ibilisi anawinda IMANI yetu kwa Bwana pale tunapoiweka katika matendo na sio kingine, tunasamehewa dhambi kwa imani, tunaponywa kwa imani, maombi yetu yanajibiwa kwa imani, kila jambo tunapokea kwa Mungu kwa IMANI IPATIKANAYO KATIKA NENO LAKE.

Lakini shetani anaenda kinyume kukufanya udhani utasamehewa dhambi kwasababu unashika amri kumi, au  kwa kufunga na kuomba sana ndio utapata haki ya kuponywa, n.k. Bwana amesema Waebrania 10:38 ” Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. “

Wagalatia 2:16 ” hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki. “

Waefeso 2:8-9 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;  wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. “

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA

KUNA TOFAUTI GANI KATI YA SALA NA DUA?


Rudi Nyumbani

Print this post

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA.

Kumbukumbu 22:5″ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.

Kumbukumbu 22:5" Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako".

Na bado Isitoshe  BWANA anawapelekea watu wake kuwaonya lakini bado wanadhihaki na kuziba masikio yako wasisikie

Warumi 1:18-28″ Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.

 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.

 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.

Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;…….Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo,………………

Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;

 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.

Tunahitaji uthibitisho gani tena kuwa tunaishi katika siku za mwisho nyakati za hatari kama hizi?? JE! umeokolewa,..umempa KRISTO maisha yako? umeoupokea ujumbe wa wakati huu aliouleta Mungu kupitia mjumbe wake ndugu William Marrion Branham wa kanisa la saba na la mwisho ?.

Kama hujafanya hivyo ndugu ni vema ukamgeukia BWANA kabla mlango haujafungwa…

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group


Mada Nyinginezo:

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

SIRI YA MUNGU.

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani

Print this post

EDENI YA SHETANI:

Pale Edeni Mungu alimweka Adamu na Hawa, Na kwa muda wote waliokuwepo bustanini Biblia inatuambia walikuwa UCHI na hawakujitambua kuwa wako vile, lakini baada ya dhambi kuingia ndipo walipojijua kuwa wapo uchi. Hii ina maana gani?.

Hapo mwanzo Mungu alipowaumba Mungu aliwawekea “UTAJI MTAKATIFU” katika macho yao ambao ungewafanya wasijue dhambi na ule utaji ulikuwa si kingine bali ni ROHO MTAKATIFU. Lakini tunajua walipoasi ule utaji ukaondoka hivyo Mungu akaamua kuwafanyia mavazi ya ngozi ili kuwasitiri.

Lakini Shetani naye tangu ule wakati alianza kutengeneza EDENI yake kidogo kidogo, awarudishe watu katika kuwa UCHI tena na kuwavua mavazi ambayo Mungu aliwavisha.

Takribani Miaka elfu sita sasa tangu Adamu kuumbwa imepita na shetani amekuwa akiimarisha hii edeni yake kwa kuwatia watu “UTAJI WAKE MCHAFU” wa kuwafanya watu waishi na wasijione kuwa wako uchi na wenye dhambi. Hii  ni hatari sana.

Miaka ya zamani kwa kweli mwanamke kutembea amevaa suruali barabarani alikuwa anajulikana kama KAHABA, Lakini sasa hivi zimekuwa ni nguo rasmi kuendea kila mahali mpaka kwenye nyumba za ibada, na sasa imevuka zaidi ya hapo vimini na nguo zinazoonyesha maungo yote wazi ni jambo la kawaida kuliona na  hata haliwashangazi watu tena..Huoni kama ni “UTAJI” wa shetani huo umewavaa watu hata pasipo wao kujua??. na wanaume pia wanaonyesha maumbile yao wakiwa na nguo za ndani tu!. Leo hii wanaume na wanawake wanatembea uchi wa mnyama barabarani pasipo aibu yoyote.

Edeni hii ya shetani inaanzia katika roho. Tunaona kanisa la kwanza lililoanza na Mitume lilikuwa na ule UTAJI wa ROHO MTAKATIFU, Ikiwa na maana kazi zake zote zilitendeka katika uvuvio wa Roho wa Mungu na usafi lakini sasa hivi katika kanisa hili la mwisho tunaloishi  ule utaji wote umeondoka kilichobakia ni utaji wa shetani unaomfanya mtu awe VUGUVUGU na asijijue,

Utakuta mwanamke anaingia kanisani nusu uchi na asijione kuwa yupo uchi, mwanamume ni mzinzi lakini anajiona yeye yupo sawa tu mbele za Mungu, mtu ni mlevi na anajiona yeye ni mkristo aliyesafi, mwanaume anafuga rasta na kujiona hana hatia, utakuta mkristo anaabudu sanamu na asione shida yoyote angali biblia inasema usijifanyie sanamu ya kuchonga usiisujudie wala kuiabudu, mtu kaokoka ni msengenyaji na hata hasikii kuhukumiwa nafsini mwake juu ya hilo analolifanya.n.k.

Ni dhahiri kabisa tunaishi katika kanisa la mwisho linaloitwa, LAODIKIA na ujumbe wetu tuliopewa na BWANA ni huu..

Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, YA KUWA HU BARIDI WALA HU MOTO; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 KWA KUWA WASEMA, MIMI NI TAJIRI, NIMEJITAJIRISHA, WALA SINA HAJA YA KITU; NAWE HUJUI YA KUWA WEWE U MNYONGE, MWENYE MASHAKA, NA MASKINI, NA KIPOFU NA UCHI.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “

Kama unavyoona sisi tunaambiwa  tunajiona kuwa ni matajiri kumbe ni maskini na tu “UCHI”

Ni uthibitisho kabisa kuwa huu ni UTAJI WA SHETANI umelifunika kanisa hili la mwisho. Tunaishi nyakati za hatari tubu. mpokee ROHO MTAKATIFU  huo ndio muhuri wa Mungu utakaotuokoa sisi katika kizazi hichi cha mwisho. kumbuka pasipo Roho Mtakatifu hakuna unyakuo, Umeamua kumfuata Bwana mfuate kweli kweli na kama umeamua kumfuata shetani mfuate kweli kweli usiwe vuguvugu.

Tazama video chini, ujionee mwenyewe ulimwengu tunaoishi ulipofikia na jinsi Edeni hi ya shetani ilipofikia ili ujue tunaishi katika nyakati za hatari watu kutembea uchi barabarani si ajabu tena..Na kama vile shetani alivyoiharibu Edeni ya Mungu vivyo hivyo na ya kwake imeandaliwa kwa ajili ya uharibifu ambao upo karibu kutokea.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU

BWANA YESU ALIMAANISHA NINI PALE ALIPOSEMA “MKONO WAKO UKIKUKOSESHA UKATE?


Rudi Nyumbani

Print this post

MAJI YA UZIMA.

Una kiu? Kunywa MAJI YA UZIMA.Siku zote roho ya mwanadamu imejawa na KIU ya mambo mengi yahusuyo mema, kwa mfano KIU ya kupata FURAHA, kiu ya kuwa na AMANI, kiu ya UZIMA USIOKOMA,kiu ya kuwa na UPENDO kiu ya KUTENDA MEMA, kiu ya kutaka UTAKATIFU,  kiu ya kuwa MNYENYEKEVU na MVUMILIVU, kiu ya KUWA NA RAHA, kiu ya KUWA KARIBU NA MUNGU ..n.k..

Lakini wengi wanatafuta njia za kuzikata kiu hizi kwa njia nyingi tofauti tofauti za kibinadamu. wengine wanatafuta RAHA kwa kufanya anasa, wengine wanatafuta AMANI kwa kunywa pombe, wengine wanatafuta FURAHA kwa kupata mali, wengine wanatafuta UZIMA WA MILELE kwa waganga na wapiga ramli, wengine wanatafuta UPENDO kwa kulaghai, wengine wanatafuta UHURU kwa kuua n.k..

Lakini ni dhahiri kuwa njia zote hizo ni batili, yaani aidha hazikati kabisa au zinakata kiu kwa muda tu! baada ya hapo tatizo linarudi  palepale..Lakini kuna habari njema, ya mmoja tu anayeweza kuikata kiu yako moja kwa moja isikuwepo tena naye si mwingine zaidi ya BWANA YESU. 

Kwa yeye utapata Raha nafsini mwako, furaha isiyokoma, amani, upendo, unyenyekevu, upole, utakatifu, kujua kumcha Mungu, na uzima wa milele n.k..Hivyo nakushauri Mkaribishe moyoni mwako na hakika ataikata KIU yako, usiipuuzie sauti yake ikuitapo . kwa maana maandiko yanasema:

Yohana 7:37-38 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, YESU akasimama, akapaza sauti yake akisema, MTU AKIONA KIU, NA AJE KWANGU ANYWE. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake”. 

Yohana 4:13-14 “Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

SEHEMU ISIYO NA MAJI.

MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?

NI RAHISI KWA NGAMIA KUPENYA KATIKA TUNDU LA SINDANO, JE! NI SINDANO IPI HIYO INAYOZUNGUMZIWA?

JE! MABALASI BWANA ALIYOYATUMIA KUGEUZIA MAJI KUWA DIVAI, YALITUMIKA TU KWA KAZI HIYO?


Rudi Nyumbani

Print this post

ZIFAHAMU NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE SABA.

Tangu kipindi cha Bwana Wetu Yesu Kristo kuondoka duniani mpaka sasa imepita miaka takribani elfu mbili na katika hichi kipindi cha miaka hii elfu mbili kanisa limekuwa likipitia katika vipindi tofauti tofauti saba vinavyoitwa NYAKATI SABA ZA KANISA, kulingana na kitabu cha..

Ufunuo 1:12-20″ Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake.
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

Ufunuo huu alipewa Yohana na Bwana Yesu alipokuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, akionyeshwa jinsi kanisa litakavyokuja kupitia katika siku za mwisho. Leo hii si rahisi sana kuona kitabu cha ufunuo kikiguswa au kuelezewa katika kanisa, na shetani hataki watu wafahamu siri zilizoandikwa katika hiki kitabu maana ndio kinaelezea hatma ya mambo yote ikiwemo na shetani mwenyewe. Kwahiyo ndugu fungua moyo wako ujifunze na Mungu akusaidie unapoenda kusoma ujue ni wakati gani tunaishi na jinsi Bwana Yesu alivyo mlangoni  kurudi kuliko hata unavyoweza kufikiri. Tafadhali pitia taratibu mpaka mwisho ili uelewe.

  • vile vinara saba vinavyozungumziwa ni makanisa saba tofauti tofauti ambayo yamepita tangu wakati wa Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani hadi wakati tunaoishi sasa.
  •  Na zile nyota saba ni malaika saba/wajumbe wa duniani(wanadamu 7 ambao Mungu aliwatia mafuta ) kupeleka ujumbe kwa hayo makanisa saba. Kila mjumbe kwa kanisa lake.

NYAKATI YA KWANZA:

Kanisa: Efeso

Malaika/Mjumbe: MTUME PAULO

kipindi cha kanisa: 53AD -170AD

Tabia ya kanisa: limeacha upendo wake wa kwanza,tangu wakati wa mauaji ya wakristo yaliyoongozwa na Nero mtawala wa Rumi hadi kifo cha mtume Yohana. Na kipindi hiki ndipo matendo ya wanikolai yalianza kuingia katika kanisa (mafundisho ya kipagani). kuanza kujichanga na ukristo. ufunuo 2:1-7

onyo kwa kanisa- litubu lirudi katika upendo wake wa kwanza, lililopoteza.

Thawabu: Yeye ashindaye atapewa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu.


NYAKATI YA PILI;

Kanisa; Smirna

Malaika/Mjumbe;IRENIUS

kipindi cha kanisa: 170AD -312 AD

Tabia ya kanisa; Ni kanisa lilopitia dhiki nyingi kutoka katika utawala mkali wa Diocletian wa Rumi , watakatifu wengi waliuawa katika hichi kipindi kuliko kipindi chochote katika historia ya kanisa.walichinjwa wengi, na wengine kutupwa kwenye matundu ya simba na wanawake kukatwa matiti na kuachwa mbwa walambe damu zao, na ukatili mwingi sana wakristo walitendewa katika hichi kipindi lakini walistahimili dhiki zote hizi soma kitabu cha (Foxe’s book of Martyr- kwenye archives zetu kinaelezea vizuri mauaji ya wakristo). Japo wakristo walikuwa maskini sana  Lakini Kristo aliwafariji kuwa wao ni  Matajiri. ufunuo 2:8-11

Thawabu; Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

NYAKATI YA TATU;

Kanisa ; Pergamo

Malaika/Mjumbe; MARTIN

Kipindi; 312AD -606AD

Tabia ya kanisa; Kanisa laingiliwa na mafundisho ya uongo zaidi, ambayo ndio yale matendo ya wanikolai sasa wakati huu yamegeuka kuwa mafundisho ya kidini. Ukristo ukaoana na upagani ukazaa Kanisa mama mfu Katoliki, katika baraza la Nikea AD 325 siasa na mafundisho ya miungu mitatu,ibada za sanamu na za wafu,sherehe na sikukuu za kipagani, ubatizo wa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, vyeo vya upapa n.k ndipo vilipochipukia. kwa mambo haya basi ikasababisha kanisa kuingia katika kipindi kirefu cha giza (Dark age). Ufunuo 2:12-17

Onyo kwa kanisa: litubu lirudi katika imani iliyoanzishwa na mitume wa Kristo

Thawabu; Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, ila yeye anayelipokea.

NYAKATI YA NNE:

Kanisa; Thiatira

Malaika/Mjumbe;COLUMBA

Kipindi; 606AD -1520AD

Tabia ya kanisa; Japo kanisa lilikuwa na juhudi na bidii katika kumtafuta Mungu, lakini bado lilikuwa na mafundisho ya yule mwanamke kahaba Yezebeli yaani mafundisho ya Kanisa Katoliki.

Onyo; Litubu litoke katika mafundisho ya wanikolai. Ufunuo 2:18-29

Thawabu;Yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.

NYAKATI YA TANO:

Kanisa; Sardi

Malaika/Mjumbe; MARTIN LUTHER

kipindi; 1520AD -1750AD

Tabia; Ni kanisa lililokuwa linarudi katika matengenezo kutoka katika mafundisho ya yule kahaba mkuu kanisa katoliki. lakini lilikuwa bado na Jina lililokufa, wakishikilia baadhi ya mafundisho ya kanisa mama katoliki, huku ndiko chimbuko la walutheri lilipoanzia.Ufunuo 3:1-6

Onyo: litubu, lirejee kwenye mafundisho ya mitume.

Thawabu; Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri Jina lake mbele za baba yangu na mbele ya malaika zake.

NYAKATI YA SITA;

Kanisa;Filadelfia

Malaika/Mjumbe; JOHN WESLEY

Kipindi; 1750AD -1906AD

Tabia; Ni kanisa lililosifiwa kwa matendo yake mema, lilifanikiwa kujua na kuyarekebisha mafundisho ya uongo Kristo alisema ”tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo, tazama nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda”.ufunuo 3:7-13

Thawabu;Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu, huo Yesalemu mpya ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.

NYAKATI YA SABA;

Kanisa; Laodikia

Mjumbe;WILLIAM BRANHAM

Kipindi;1906- Unyakuo

Tabia; Ni kanisa ambalo sio baridi wala moto, bali ni vuguvugu, Kristo anasema ni heri lingekuwa moto au baridi, hii ndiyo hali ya kanisa tunaloishi sasa mimi na wewe, uvuguvugu mbaya umeingia katika kanisa, watu wanajiona kuwa wanamwabudu Mungu katika uzuri wao wa majengo ya kanisa, kwaya na injili ya mafanikio, wakidhani kuwa hivyo yatosha tu kumjua Mungu kumbe hawajui wameshaingia katika udanganyifu wa shetani pasipo wao kujua, watu wanasema kuwa wanampenda Mungu na bado wanapenda mambo ya ulimwengu huu kama fashion za mitindo ya kisasa wanawake kuvalia mavazi ya nusu uchi, michezo, miziki, muvi, ponography, ulevi. anasa,uasherati,na shughuli za ulimwengu huu ambazo zinawasonga wengi hususani kwa kizazi hichi cha ubize, watu wanapata muda wa kufanya kazi sana, lakini muda wa kumtolea Mungu hawana na bado ni wakristo., huu ndio uvuguvugu Kristo anaouzungumzia kwa kanisa letu la Laodikia.Hapa Kristo anasema unajiona kuwa tajiri kumbe ni maskini na mnyonge na uchi na unamashaka na kipofu, jiulize ni hali gani ya kanisa tulilopo sasa.

Na hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hili, na ndio linakaribia kuisha. jiulize umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu akirudi mara ya pili?. Mungu alimtuma mjumbe wake ndugu William Branham kulionya kanisa letu lirudi katika NENO na imani iliyohubiriwa na mitume pamoja na utakatifu.

Onyo; Kristo anasema kanisa liwe na bidii likatubu na kumgeukia Mungu.

Thawabu;Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba yangu katika kiti chake cha enzi. ufunuo 3:14-22

Watu wa Mungu hili ndilo kanisa la mwisho tunaloishi hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hapa, tunaishi katika wakati ambao Kristo yupo mlangoni kulichukua kanisa lake teule, JIULIZE! UMEKWISHA KUJIWEKA TAYARI KUMLAKI BWANA, TAA YAKO INAWAKA??UMEMPOKEA ROHO MTAKATIFU??YEYE ALIYE NA SIKIO, NA ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA.

Mungu akubariki

MARAN ATHA!

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

+255693036618/ +255789001312

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo

VIPINDI VINNE VYA MAISHA VILIVYO VIGUMU MTU KUMKUMBUKA MUUMBA WAKE.

WALE WAZEE ISHIRINI NA WANNE (24), WANA KAZI GANI?

UFUNUO: Mlango wa 1

DANIELI: Mlango wa 1

Rudi Nyumbani:

Print this post

JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA?

Jibu ni ndio kwasababu biblia inasema pasipo kumwagika damu ya Yesu hakuna ondoleo, ukisoma waebrania 9:22 “Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. ”

Hii ndio njia pekee ambayo Mungu aliichagua tangu awali kwamba, ili tendo lolote la rohoni lifanyike na kufanikiwa ni lazima damu ihusishwe, na ndio maana tunaona katika agano la kale ilikuwa kwamba ili mtu apate kibali mbele za Mungu ni lazima aende na sadaka, ambapo mnyama alisiyekuwa na mawaa anachinjwa ili kufanya upatanisho, na mambo yote yanaliyohusishwa na dhambi yalikuwa yanatakaswa kwa damu, hiyo ilikuwa ni kanuni.

Kwahiyo tunaona damu ina mahusiano makubwa kuwa  kama kiunganishi kati ya ulimwengu wa mwilini na wa rohoni, na ndio maana hata shetani kwa kulijua hilo anapenda kutumia damu ili kufanikisha mambo yake maovu katika ulimwengu huu,

Kwamfano mara nyingi wachawi wanawaambia watu wapeleke damu za mnyama fulani ili kufanikisha mambo yao ya kishirikina pamoja na  haja za hao watu, na ukitazama kwa makini utaona kuwa wanapendelea zaidi damu za wanadamu kuliko za wanyama kwasababu wanajua hizo zina mlango mkubwa zaidi wa kuunganisha mambo ya rohoni na ya mwilini kiurahisi. Na ndio maana hao wanaotoa damu za watu utakuta matokeo yao ya kiroho(kichawi) yanakuwa ni makubwa zaidi kuliko wale wanaotoa za wanyama.

Kuna kitu kikubwa sana ndani ya DAMU ambacho mkristo akikitambua hakuna chochote kitakachomsumbua na hakika ataweza kufanya mambo yote, ataweza kufanya yote ya mwilini na ya rohoni, na kama tunavyojua  hiyo damu ili iwe na nguvu ni lazima iwe ya mwanadamu na sio mnyama, tena inatakiwa ipatikane ya mwanadamu asiyekuwa na hila wala mawaa, hakika ikipatikana hiyo ni zaidi ya tambiko lolote ambalo lilishawahi kufanyika duniani!!!

Kumbuka mambo yote yanatoka rohoni, ni ngumu kushindana na watumishi wa shetani ambao wamepata nguvu nyingi za kumkaribia shetani kwa sadaka zao za damu za watu wasio na hatia,halafu  na wewe unataka kwenda kushindana nao pasipo damu yoyote, hapo ni lazima ushindwe tu! ni lazima ujue mbinu za kumshinda adui yako, mambo ya rohoni yana kanuni zake.

Lakini habari njema ni kwamba hii damu yenye nguvu ipitayo damu zote isiyoharibika ambayo inaweza ikashinda mambo yote ipo na inajulikana, na hii si nyingine zaidi ya DAMU YA YESU ambayo haikuwa na hila wala mawaa yoyote. lakini wengi wanashindwa kuielewa matumizi yake, na ndio maana shetani anaendelea kupata nguvu juu yao, 

Jambo shetani analotaka ni waifahamu tu lakini wasiielewe matumizi yake, kila mtu anaifahamu damu ya mwanakondoo lakini ni wachache wanayoielewa, siku utakapoielewa kisawasawa utamshinda shetani kwa kila nyanja.

ukisoma;

Ufunuo 12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

11 NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANAKONDOO, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. “

Unaona hapo? ni Damu tu ya mwana-kondoo inayoweza kumshinda yule joka ( shetani ) na hakuna kingine chochote. Lakini wengi wanadhani utamshinda kwa  kutamka tu  “nakukemea kwa damu ya Yesu”……akidhani hapo amempata shetani, kumbe hajui hapo hajafanya lolote kama hajaingia ndani ya hilo Agano kwanza. Ni lazima uingie kwanza.

JINSI YA KUINGIA KATIKA HILI AGANO LA DAMU YA YESU.

Kumbuka katika agano la kale kuhani mkuu alipokuwa akienda kila mwaka kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa njia ya damu za wanyama, hakuwa anafanya kwa watu wote wa ulimwengu mzima bali tu kwa wale waliokuwa katika hilo agano yaani wana wa Israeli pekee. Na ndio waliokuwa wanafunikwa dhambi zao na kushiriki baraka zote za rohoni na sio watu  wa ulimwengu mzima.

Vivyo hivyo katika Agano jipya ili maombi yako yasikiwe, ili sadaka zako zikubaliwe, ili dhambi zako zisamehewe, ili uweze kumshinda shetani na magonjwa yake yote na laana ni lazima uingie katika hili Agano jipya la DAMU YA YESU KRISTO. na hauingiii kwa kuzaliwa katika familia ya kikristo, wala hauingii kwa kujiunga na dhehebu fulani, wala hauingii kwa njia nyingine yoyote isipokuwa KWA KUTUBU kwanza, NA KUMWAMINI YESU KRISTO, NA KUBATIZWA KWA JINA LA YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kisha upokee ROHO MTAKATIFU hapo ndipo umezaliwa mara ya pili na umeingia katika hili AGANO HILI KUU.

Sasa kuanzia hapo na kuendelea ile damu inaanza kunena kwa ajili yako mbele za Mungu, shetani hana la kukushinda kwa lolote, wala la kukushitaki, kwasababu damu isiyoharibika tayari ipo kunena kwa ajili yako, hauhitaji kupigana na wachawi, wala waganga, wala kuogopa magonjwa au shida, ipo hiyo damu tayari inafanya kazi kuliko tambiko lolote lililowahi kufanyika tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.

Kumbuka shetani anapotaka kuleta laana juu yako jambo la kwanza analoangalia ni je! upo chini ya damu? shetani hawezi kulaani kilichobarikiwa kama vile Balaamu alivyoshindwa kuwalaani wana wa Israeli.

Kwahiyo ndugu hakuna njia nyingine yoyote katika hii dunia unaweza ukamshinda shetani isipokuwa kwanza kutubu, na kumruhusu Yesu Kristo ayasafishe maisha yako kwa damu yake, uchukua uamuzi wa kubatizwa leo kwa ubatizo ulio sahihi wa kuzamishwa na sio wa kunyunyuziwa na iwe ni  kwa jina la YESU KRISTO kulingana na maandiko ( matendo 2:38.), kisha Bwana atakupa Roho Mtakatifu hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili na kuingia katika lile AGANO KUU LA DAMU YA YESU, kwa uhakika wa maisha yako ya sasa na ya baadae, kumbuka hakuna ubatizo wa watoto wachanga, kama ulifanyiwa hivyo hapo hujabatizwa unapaswa ukabatizwe tena.

Nakukumbusha tena ndugu yangu hauwezi ukamshinda shetani kwa njia nyingine yoyote ile, sio kwa matendo, wala kwa juhudi yako bali kwa damu ya mwana-kondoo pekee. 

Ufunuo 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. “. tubu, kabatizwe na upokee Roho Mtakatifu.

Mungu akubariki!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

MKATAE SHETANI NA MAWAZO YAKE YA KIBINADAMU.

JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?

UBATIZO WA MOTO NI UPI?

JINSI DHAMBI INAVYOMGHARIMU MTU SANA.


Rudi Nyumbani

Print this post

NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?

Kazi kubwa shetani anayoifanya kwa mkristo kila siku ni kutaka kumwangusha katika imani yake hivyo anatumia njia ya majaribu kumwangamiza, majaribu ni vikwazo, na kuna vikwazo vya aina nyingi katika safari ya ukristo ambavyo shetani lazima avilete na sio kila mtu atakutana navyo bali ni mkristo tu aliyeamua kujitoa kikamilifu na kumfuata YESU KRISTO kwa moyo wake wote.

kwahiyo shetani akishajua umechagua njia hiyo ndipo atakapoanza kuamua kukupepeta kwa njia zozote zile; anaweza akaja aidha kwa njia ya magonjwa, shida, mafarakano baina yako na watu wanaokuzunguka ili tu kuikana imani yako, au vikwazo vya nguvu za giza, mabalaa, ajali, mikosi, na vishawishi vya kukufanya utende dhambi zisizo za kukusudia, n.k.. haya yote shetani anayaleta kwa dhumuni tu la kukufanya wewe ulegee katika imani, au umkane Mungu, au uteseke na pengine ufe kabla hata hujamaliza kusudi lako uliloitiwa duniani, kumbuka mambo haya shetani anayalengesha kwa mkristo tu aliyeamua kusimama,

Tunaona Bwana YESU aliwaonya wanafunzi wake akiwaambia “makwazo hayana budi kuja”. Lakini pamoja na hayo alitoa njia ya kuweza kuyadhibiti, na ni kwa njia moja tu nayo ni kwa “KUOMBA”.

Tufuatilie mahali pengine alichowaambia wanafunzi wake:

Mathayo 26:40 ” Akawajia wale wanafunzi wake, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, je! hamkuweza kukesha pamoja nami hata SAA MOJA?.

41Kesheni, MWOMBE, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.

Tunaona hapo Bwana YESU aliwasisitiza wanafunzi wake waombe kwasababu majaribu mazito yalikuwa yanawangojea mbeleni, na ndio maana Bwana angali akiyaona hayo ya kwenda kupata mateso alimwomba Mungu amwepushe na kile kikombe cha majaribu, hivyo kwa kufanya vile japo lile jaribu halikuondolewa lakini alipewa nguvu ya kulishinda na ndio maana malaika walimtokea na kumtia nguvu, lakini kwa wale wengine (wanafunzi wake) ambao nao majaribu mazito yalikuwa yanawangojea walila wakidhani kuwa adui yao(shetani) na yeye alilala?. Lakini tunafahamu kitu gani kilichowatokea dakika chache baadaye, tunaona shetani alipomjaribu Petro alimkana KRISTO pale pale na wengine wote walikimbia na kujitenga na Bwana.

Lakini je! mfano wangekesha na BWANA kuomba wasiingizwe majaribuni, unadhani yale yote yangewatokea? La! Hakika Mungu angewaepushia pengine malaika angewaonya waondoke maeneo yale, au mazingira ya wanafunzi kushikwa na wale askari au mazingira ya Petro kutaka kumkana Bwana yasingekuwepo, na kama wangekaa kuomba na YESU wasiingie majaribuni hata kama wangeingia majaribu Mungu angewapa wepesi wa kushinda kama Bwana alivyopewa ule wepesi wa kushinda.

Na jambo hili hili linajirudia hata sasa hivi, kwa mkristo yoyote aliyesimama, wakati wewe umelala fahamu kuwa adui yako hajalala yupo nje anaandaa majeshi ya kukuangamiza wewe, unadhani kama yalimpata BWANA kwanini yasikupate na wewe?, kama alimwomba BABA amwepushe na majaribu inakupasaje wewe?. Na ndio maana hata tunaona pale alipowafundisha wanafunzi wake kusali aliwaambia hivi ” ..USITUTIE MAJARIBUNI, BALI UTUEPUSHE NA YULE MWOVU..” . Haya maombi ni muhimu sana katika maisha ya kila mkristo.

Na ukiwa kama mkristo ni muhimu kufahamu maeneo ambayo adui anapenda sana kutumia kukushambulia na hapo ndipo unapotakiwa kutilia mkazo katika kuomba Mungu atoweshe majeshi ya mwovu katika eneo hilo, yapo maeneo mengi mfano, mara nyingine shetani anaweza kutumia marafiki zako wa karibu au ndugu zako kudhoofisha imani yako unashindwa aidha kusoma NENO, au kuwa huru na imani yako au kusali, na unaona unaishi katika mazingira ambayo hayaepukiki kuwa na hao watu, hapo sasa unatakiwa umwombe BWANA awalinde ndugu zako dhidi ya yule mwovu asipate nafasi ya kuwatumia kuidhoofisha imani yako.

Au mara nyingine shetani anaweza kutumia wafanyakazi wenzako au maboss wako kukuharibu wewe uiache au uikosee imani yako, pengine hata kuikana, maeneo kama hayo ni vema ukeshe katika kuomba BWANA awafunike wafanyakazi wenzako shetani asiwatumie wao kama vyombo kwa kukujaribu wewe. Kwa kufanya hivyo utajikuta imani yako haisumbuliwi hata kama upo katikati ya watu wasioamini kiasi gani na hata kama ikitokea shetani akiruhusiwa kuwatumia kukujaribu wewe Mungu atakupa nguvu ya kuyashinda kama alivyompa Danieli hutaweza kumkana Mungu hata kama utatupwa katika tundu la simba, utashinda kama Bwana YESU hata kama ni kuwekwa msalabani, lakini ni kwanini ? ni kwasababu ULIMWOMBA BWANA AKUEPUSHE NA MAJARIBU.

Lakini usipokuwa mwombaji ndugu, hutaweza kumshinda shetani utabakia tu kutamka ushindi wa mdomoni lakini mwisho utaishia kuikana imani kama vile tu Petro, Kumbuka nia ya Petro ilikuwa kweli sio kumkana BWANA lakini kwasababu alikuwa hana nguvu ya kushinda majaribu alijikuta ameingia katika matatizo makubwa, na nguvu hii ingepatikana kwa njia ya MAOMBI TU!.

Na ndio maana Bwana alisema tuombe walau hata “SAA MOJA” kwa siku. Ni hatari sana kama wewe ni mkristo hata dakika 10 husali, si ajabu unaona ukristo ni mgumu kuuishi, mitego ya adui chungu nzima imetuzunguka, pasipo maombi tutawezaje kuishinda?. Wachawi hawalali wanakesha kila siku kuloga na kuilaani siku yako kwa BWANA, wewe unatakiwa uamke uibariki siku yako.

Utawezaje kushinda tamaa za uasherati, kama Yusufu kwenye maeneo yako ya kazi, au shule, au makazi unayoishi,? katika kizazi hichi cha uzinzi kama sio mwombaji?..NI WEWE AMBAYE UNASEMA KUWA NI MKRISTO.

Yakobo 4: 1″ Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?.

2Mwatamani wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu KWA KUWA HAMWOMBI.

Hivyo ndugu ni muhimu kutenga walau SAA MOJA kila siku kuomba, kuibariki siku yako, yapo mambo mengi ya kuombea ipo familia yako,ukoo wako, jamaa zako na marafiki zako mwombe Mungu awalinde wasiwe vyombo vya shetani kukuangamiza Katika UKRISTO wako, ombea wakristo wenzako na watumishi wa Mungu shetani asipate nafasi ya kuliharibu kanisa, ombea taifa unaloishi pamoja na viongozi wake ili uishi kwa amani, wasikuingize majaribuni kumbuka usipofanya hivyo wanaweza hata kuibua sheria zilizotungwa kuzimu ushindwe kumwabudu Mungu wako kwa uhuru, ombea kazi yako, vyombo vyako vya usafiri, shule yako, n.k. shetani asivitumie kuharibu imani yako au uhusiano wako na Mungu.,

Wakati mwingine unajikuta muda wote upo buzy hujamaliza hili linazuka lingine, na hali hiyo inaendelea kila siku mpaka inasonga imani yako na uhusiano wako na Mungu, hayo ni majaribu unapaswa UOMBE Mungu ayaepushie mbali hayo majaribu ili shughuli za kidunia zisizoisha ziondoke mbele yako na upate Muda mwingi binafsi na Mungu wako.

Usipofanya hivyo ndugu shetani atakuwa amekushinda utafananishwa na ile mbegu iliyotupwa kwenye miiba, ilipomea shughuli,udanganyifu wa mali na masumbufu ya maisha hayo yakaisonga ikawa haizai(mathayo 13:22). Kwa nyanja zote hizi ukiomba hakika hautashindwa kumaliza saa moja.

Hivyo kwa wewe mkristo ni muhimu sana kumwomba Mungu akuepushe na Majaribu maadamu upo safarini, vikwazo na majaribu Bwana alituonya hatuna budi kukutana navyo na ni kwa MAOMBI tu! tunaweza kudhibiti.

OMBA WALAU SAA MOJA KILA SIKU.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA

FAIDA ZA MAOMBI.

HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?

KWANINI MUNGU HAKUMUUA NYOKA MPAKA AKARUHUSU AJARIBIWE PALE BUSTANI NA EDENI?


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?

Waefeso 1 : 4 ” Kama vile alivyotuchagua katika yeye KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na urathi wa mapenzi yake.”

JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?

Mambo yote tunayoyaona sasa katika ulimwengu yalikuwa yameshakusudiwa yawepo kabla hata ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, hakuna lolote linalotokea kwa bahati mbaya ambalo Mungu hakulijua, Kuna swali watu wengi wanauliza je! Mungu anafahamu mtu kabla hajazaliwa kwamba atakuja kwenda mbinguni au kuzimu?? Jibu ni ndiyo anafahamu!..

Ni lazima ajue hayo yote ili awe Mungu..na kuna wengine wanauliza kama ni hivyo basi kwanini aumbe wengine angali anajua mwisho wao utakuwa ni kuzimu?? Jibu ni kwamba ewe mwanadamu wewe ni nani umuulize Muumba wako, kwanini chombo hichi unakifanya hivi na kile unakifanya vile? Hatuwezi kushindana na kusudi la Mungu Akili za Mungu hazichunguziki wala njia zake hazitafutikani.

Mtume Paulo alisema katika warumi 9:20 kwamba vipo vyombo Mungu aliviumba vya ghadhabu kwa ajili ya uharibifu tunaona kama vile Farao,Yezebeli,Balaamu,n.k. na vipo vingine aliviumba kwa ajili ya heshima mfano Musa, Ayubu,Ibrahimu n.k.

Hivyo basi tukivitazama hivi vyombo vya heshima Mungu alivyovichagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu na kuvitengenezea njia ya kupitia mpaka vitakapofikia ule utukufu wa Mungu alioukusudia juu yao. Na ndio maana alisema katika..

Warumi 8:28-30” Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, WALE WALIOITWA KWA KUSUDI LAKE.

29. MAANA WALE ALIOWAJUA TANGU ASILI, ALIWACHAGUA TANGU ASILI WAFANANISHWE NA MFANO WA MWANA WAKE, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

30. Na wale aliowachagua tangu asili hao AKAWAITA, na wale aliowaita, hao AKAWAHESABIA HAKI; na wale aliowahesabia haki, hao AKAWATUKUZA.

Unaona hapo kuna hatua za kufuata kwa kile chombo cha heshima kilichoteuliwa na Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili kifikie utukufu wake uliokusudiwa. Sasa Baada ya kuchaguliwa tangu asili zipo hatua TATU za kufuata 1) KUITWA, 2) KUHESABIWA HAKI, 3) KUTUKUZWA. Embu tuzitazame kwa ufupi hizi hatua.

1) KUITWA:

Waliochaguliwa na Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ni lazima waisikie sauti ya Mungu inapolia masikioni mwao.Kumbuka na sio watu wote wataisikia hiyo sauti, bali ni wale tu Mungu aliowachagua tangu asili,. Bwana Yesu aliwaambia makutano hivi wale waliomtilia shaka kwamba yeye hajatumwa na Mungu kuwaokoa wanadamu alisema hivi..

Yohana 6:43″ …Msinung’unike ninyi kwa ninyi. HAKUNA MTU AWEZAYE KUJA KWANGU, ASIPOVUTWA NA BABA ALIYENIPELEKA; nami nitamfufua siku ya mwisho” kwahiyo unaona ni lazima uvutwe kwanza.

Mahali pengine Yesu aliwaambia hao hao mafarisayo alisema..Yohana 10:26″ Lakini ninyi hamsadiki, kwasababu HAMMO miongoni mwa kondoo wangu. KONDOO WANGU WAISIKIA SAUTI YANGU; NAMI NAWAJUA NAO WANIFUATA. NAMI NAWAPA UZIMA WA MILELE; WALA HAWATAPOTEA KAMWE.

Umeona hapo tena walio wa Kristo wataisikia sauti yake tu!, haihitaji kuwa bembeleza sana, kwani ile mbegu ya nuru Mungu alishaiweka ndani yao tangu asili, wakisikia tu, saa hiyo hiyo wanabadilika na kumfuata Kristo katika hali zote.

Jiulize ni kwasababu gani mafarisayo na masadukayo pamoja na dini zao zote walishindwa kumwamini YESU KRISTO jibu ni rahisi kwasababu hawakuwa miongoni mwa kondoo wake aliowachagua tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, lakini tunaona wale watu wasiokuwa na elimu, wavuvi, wakina Petro walimkubali YESU pasipo maswali mengi au shuku shuku nyingi ni kwasababu gani? ni kwasababu walikuwa ni miongoni mwa wale aliowachaguliwa tangu asili.

2) KUHESABIWA HAKI.

Mtu anahesabiwa haki kwa kumwamini YESU KRISTO katika uweza wa Damu yake inayoondoa dhambi, kumbuka wale wote walio wake baada ya kuitikia wito wao wenyewe watataka kuuliza tufanyeje?? Hapo ndipo Bwana atakapowaongoza katika hatua inayofuata ya kuufanya imara WITO wao na UTEULE wao (2Petro 1:10). Hapo ndipo mtu anapoutafuta ubatizo wa MAJI na wa ROHO MTAKATIFU..

Tunaona ile siku ya Pentekoste Petro baada ya kuwashuhudia wale makutano walio kusanyika waliamini ..tusome

 Matendo 2:37-38″ Waliposikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia, TUBUNI, MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote WATAKAOITWA, na Bwana Mungu wetu WAMJIE.”

Kwahiyo unaona hapo? ili uhesabiwe haki lazima ukabatizwe katika ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. kumbuka hakuna ubatizo wa watoto wadogo, wala hakuna ubatizo wa kunyunyuziwa maji, unapaswa UKAZAMISHWE, na ubatizwe kwa JINA LA YESU KRISTO kulingana na maandiko, hata mimi nilinyunyuziwa nilipokuwa mchanga lakini baada ya kufahamu ubatizo sahihi kulingana na maandiko ilinipasa nikarudie tena. Kisha baada ya hilo una AHADI YA ROHO MTAKATIFU, na ni vizuri kujua kuwa ahadi hii si kwa ajili ya kila mtu(hata kafiri) bali ni kwa wale watakaoitwa na Bwana wamjie. Naamini nawewe ni mmoja wapo wa walioitwa.

3) KUTUKUZWA.

Baada ya kupokea Roho Mtakatifu ambao ndio muhuri wa Mungu (Efeso 4:30). Kitu kilichotiwa muhuri maana yake ni kimehakikiwa na kuonekana kimekamilika. Hivyo mtu anapopokea Roho Mtakatifu anakuwa ametiwa muhuri na Mungu mpaka ile siku ya ukombozi. Kumbuka Kupokea Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni zaidi ya kunena kwa lugha, kunena kwa lugha ni karama sio watu wote wanaweza wakanena, ni kama vile sio watu wote wanaweza wakawa manabii, au wainjilisti, vivyo hivyo mtu anaweza akapokea Roho Mtakatifu na asinene kwa lugha, bali karama nyingine ikajidhihirisha, na pia wapo ambao wananena kwa lugha na hawajapokea Roho Mtakatifu. Kwahiyo kipimo cha kwamba umepokea Roho Mtakatifu sio karama uliyonayo bali ni maisha matakatifu unayoishi baada ya kumpokea Roho.

Hivyo baada ya kukamilishwa kwa kubatizwa na Roho Mtakatifu tunasubiria siku ya ukombozi wetu( yaani siku ya kutukuzwa) kwenda mbinguni, siku tutakapovaa miili ya utukufu na kuwa kama BWANA YESU KRISTO alivyo sasa.

Kwahiyo ndugu tathimini maisha yako, je! unavyoishi leo hii ni miongoni mwa wale kondoo wake aliowachagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu? au vile vyombo vya ghadhabu vilivyowekwa kwa ajili ya uharibifu??..

Kumbuka kuna makundi mawili tu, ni aidha kondoo au mbuzi, umeitikia wito au hujaitikia wito, umechaguliwa au haujachaguliwa, ni wa mbinguni au ni wa kuzimu? jibu lipo moyoni mwako. Je! upo katika hizo hatua? kwamaana biblia inasema wale wote wasio na Roho wa Kristo hao sio wake (warumi 8:9).

2 Timotheo 2:19 ” Lakini msingi wa Mungu ulioimara umesimama, wenye MUHURI HII, BWANA ANAWAJUA WALIO WAKE. NA TENA, KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AACHE UOVU.

20 Basi katika nyumba nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.

21 Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima kilichosafishwa, kimfaacho BWANA, KIMETENGENEZWA KWA KILA KAZI ILIYO NJEMA.

AMEN!

Maombi yangu ndugu ni uchague kufanyika chombo cha heshima. Muda umeenda kuliko unavyodhani Bwana yupo mlangoni kurudi.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/Ushauri/Ubatizo/ Whatsapp. Tupigie namba hizi: +255693036618


Mada Nyinginezo:

JE! WEWE NI MBEGU HALISI?

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

ILI TUONEKANE WAKAMILIFU MBELE ZA MUNGU.

MSTARI HUU UNAMAANA GANI? ″WALAKINI HAUTAPOTEA HATA UNYWELE MMOJA WA VICHWA VYENU? (LUKA21:18).


Rudi Nyumbani

Print this post

GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.

Kuna gharama kubwa sana katika kuupata ufalme wa mbinguni kama Bwana Yesu alivyotangulia kusema kwenye Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. ” Hii ikiwa na maana kuwa ufalme wa mbinguni ni kitu kinachogombaniwa kwa nguvu na watakaokipata ni wachache. Na kumbuka NGUVU zinazozungumziwa hapo sio nguvu za kimwilini, Tukisoma..

Mathayo 13:44-46 “

44 Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda AKAUZA ALIVYO NAVYO VYOTE, akalinunua shamba lile.

45 Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri;

46 naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda AKAUZA ALIVYO NAVYO VYOTE, akainunua. “

gharama ya ufalme wa mbinguni..Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri;  46 naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda AKAUZA ALIVYO NAVYO VYOTE, akainunua. "

Bwana Yesu alifananisha ufalme wa mbinguni na maisha yetu tunayoishi kila siku, kama tukisoma hiyo mifano hapo juu tunaona kuna mfanya biashara aliyekuwa anatafuta lulu nzuri ya thamani kubwa, na alipoiona akaipenda sana, pengine hakuwa na fedha za kutosha, kuinunua kutokana na gharama ya LULU hiyo ilivyokuwa na thamani kubwa, lakini kwasababu ni mfanya biashara, alitafakari sana, kwamba japo inauzwa kwa thamani nyingi, lakini akiipata ataweza kuiuza mahali pengine kwa gharama kubwa zaidi, Hivyo atarudisha fedha aliyoinunulia pamoja na faida nyingi juu yake.

Kwasababu hiyo basi ilimpasa aende kuuza kila kitu alichokuwa nacho pengine hata nyumba yake, na miradi yake yote, ilimradi tu afikie kiwango kile cha pesa akainunue lulu ile yenye thamani kubwa.

Labda pengine alivyodhamiria kufanya hivyo, alionekana mwendawazimu mbele za watu kuuza mali alizozitaabikia kwa muda mrefu, lakini kwasababu ni mfanya biashara alifahamu ni kitu gani anafanya.

Vivyo hivyo na yule mwingine aliyeona hazina iliyositirika katika shamba na kwenda kuuza vyote alivyonavyo hakuwa mwendawazimu, pengine aliiona ALMASI imejichimbia katika kiwanja cha jirani yake, hivyo ili aweze kuipata ni sharti kile kiwanja kiwe chake, ili awe na ruksa ya kuifukua,

Sasa kwa ujanja, akaenda kumshawishi mwenye kiwanja amuuzie hata kwa bei mara 10 ya bei halisi ya kiwanja kile ili aweze kukipata kwa haraka na bila ya usumbufu , kwa kuwa mtu huyo anajua ni kitu gani anachokifanya, akaamua akauze kila kitu alichokuwa nacho, pengine mifugo yake, au majumba yake, au magari yake, na kama fedha isingetosha angeweza hata kwenda kukopa ili atimize lengo lake la kupata kiwanja kile.

Lakini kwa namna ya kawaida watu wangemuona kama amelogwa, au amerukwa na akili, kugharimikia kitu kisichokuwa na faida, lakini yeye hakuona tu kiwanja, bali aliuona UTAJIRI mkubwa zaidi ya kile kiwanja.

Mifano hiyo hiyo inatufundisha sisi kama wanadamu, HATUTAWEZA KUUPATA UFALME WA MBINGUNI, KAMA BADO HATUJAJUA THAMANI YAKE. Kumbuka yule mfanyabiasha hakuona tu lulu bali aliona thamani kubwa iliyopo ndani ya lulu, ndiyo ikamgharimu kuuza kila kitu, vivyo hivyo na yule aliyenunua shamba, hakuona tu shamba, bali aliona thamani ya kitu kilichokuwa kimejificha ndani ya lile shamba na ndipo gharama za kukipata hicho kitu zinajitokeza.

Na katika ufalme wa mbinguni, usiuone tu ufalme wa mbinguni halafu basi, bali tazama thamani na utajiri ulioko ndani ya huo ufalme, ukishalifahamu hilo au kupata ufunuo huo utakuwa na nguvu za kuchukuliana na gharama zozote utakazokumbana nazo kwa furaha zote.

Tukirudi kwa kijana mmoja aliyeitwa Musa, tunaona alizaliwa katika makasri ya kifalme ya FARAO, aliyekuwa msomi, na mtawala mwenye cheo, pamoja na mali nyingi, lakini ilifika wakati neema za Mungu ilifunguliwa machoni pake,na kuuona uzuri ulio katika ufalme wa mbinguni, hivyo kwa furaha yote aliamua kuuza kila kitu alichokuwa nacho ili aupate ,alidharau elimu yake ya kipagani, alidharau cheo chake kama mfalme mrithi, alidharau anasa na fahari alizokuwa anazipata katika jumba la kifalme, ili tu aupate ufalme usioharibika wa mbinguni..

Mtume Paulo aliandika katika.Wabrania 11:24 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;

25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;

26 AKIHESABU YA KUWA KUSHUTUMIWA KWAKE KRISTO NI UTAJIRI MKUU KULIKO HAZINA ZA MISRI; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.

27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana. “

Tunaona hapo Musa alihesabu kushutumiwa kwake Kristo ni Utajiri mkuu kuliko hazina zote za Misri, ilimpasa AUZE baadhi ya mambo, ili aweze KUUNUNUA ufalme wa mbinguni, aliuona utajiri mkubwa huko mbeleni kuliko hazina zote za Misri, Ilimpasa auze umaarufu wake, ilimpasa auze anasa zake, ilimpasa auze ujana wake, ilimpasa auze kiburi chake, ilimpasa auze fashion zake, ilimpasa auze majigambo yake na ujuzi wake, ilimpasa auze dhuluma yake, ili aweze kufikia viwango vya kuununua ule UFALME WA MBINGUNI.

Vivyo hivyo na mtume Paulo mwenyewe aliingia gharama hizo hizo..ukisoma Wafilipi 3:7-8 inasema..

” Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama “MAVI” ili nipate Kristo; “

Paulo ambaye alikuwa ni msomi mwenye cheo na kiburi alihesabu mambo yote kuwa kama mavi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, kumbuka kilichomfanya achukue uamuzi huo sio tu kwasababu ni neno “ufalme wa mbinguni” , hapana bali ni UTAJIRI aliouna angeupata katika huo ufalme.Na kwa kufunuliwa na Roho Paulo alifika wakati na kusema

 Warumi 8:18-19

18 Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama UTUKUFU ULE UTAKAOFUNULIWA KWETU.

19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.

Hivyo ndugu fungua macho yako uone thamani na utajiri mkubwa ulio katika huo ufalme, ndipo utakapoona sababu ya kuacha kila kitu kisichompendeza Mungu kwa furaha zote na kumwandamia Mungu kwa hali zote,. Kumbuka thawabu za UFALME WA MBINGUNI, zitakazokuja huko ni mambo mazuri ambayo biblia inasema katika..1Wakoritho 2:9 “lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,)

Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. “, pia usisahau, kutakuwa na wafalme na wenye mamlaka kubwa, pamoja na makuhani wa Mungu hawa watakaa pamoja na Kristo na kuhudumu pamoja naye, na huko watakuwepo pia watu wa kawaida tu, thawabu zitatofautiana sana, na ni milele, ikiwa na maana kuwa kama wewe ni mdogo kule utabaki hivyo hivyo milele, na kama wewe ni mfalme kule utadumu mfalme milele, na Bwana wetu YESU KRISTO akiwa kama MFALME WA WAFALME.  

Jina la BWANA YESU LIBARIKIWE.

Kuna wakati mitume walimuuliza Bwana..

Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?

28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. “

Hivyo wale watakaoketi karibu na Bwana ni wale tu, walioona thamani na kuingia gharama za kuununua ufalme wa mbinguni, je! ufalme huu unathamani gani kwako? , wewe mwanamke hauwezi ukaacha fashion na kuvaa hivyo vimini na suruali, kwasababu hauoni faida yoyote ya kuacha kufanya hivyo, mwanamume hauwezi kuacha pombe na sigara kwasababu kwako ni sawasawa ni biashara isiyo na faida, hauwezi kuacha uasherati, wizi kwasababu faida ya ile LULU(UFALME WA MBINGUNI) haijafunuliwa machoni pako. Laiti ungeifahamu thamani ya LULU usingefanya hivyo.

Lakini kumbuka wana wa Mungu, sio wajinga kuwaona wanauza mambo ya ulimwengu huu sasa ivi ili wanunue mambo ya ulimwengu unaokuja, ni kwasababu wanaona mbele, na kujipenda na wanapenda maisha ndio maana wanatafuta maisha ya milele yanayodumu, na wanapenda furaha zaidi hata ya wewe unayejiona unajistarehesha katika anasa za ulimwengu huu.

Kanisa tunaloishi ndilo la mwisho linalojulikana kama LAODIKIA kulingana na Kalenda ya Mungu, na ujumbe wetu tuliopewa umeandikwa katika kitabu cha Ufunuo 3:14 unasomeka hivi..

“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, UNUNUE KWANGU DHAHABU ILIYOSAFISHWA KWA MOTO, UPATE KUWA TAJIRI, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.”

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “

Bwana ametupa shauri tukanunue dhahabu kwake tupate kuwa matajiri, kumbuka ili KUNUNUA lazima TUUZE yote maovu tulionayo ili tuweze kukidhi viwango vya kuupata ufalme wa mbinguni. Maombi yangu ni Bwana akupe neema ya kuona THAMANI YA UFALME WA MBINGUNI kwasababu UFALME WA MBINGUNI unapatikana kwa nguvu, na wenye nguvu ndio wanaouteka.

Print this post

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.

Kama tunavyofahamu wakati wa usiku kabla hatujalala, huwa ni lazima tufunge milango yetu yote, kwa makufuli na makomeo, na hii sio kwasababu tunapenda kujifungia tu hapana! bali ni kujiweka katika hali ya usalama dhidi ya WEZI usiku, Kwasababu hatujui ni wakati gani wataingia na kuleta madhara. Hii ni desturi kwa kila mtu,hakuna mtu asiyefahamu kuwa anapaswa kufunga milango yake wakati wa usiku.

Lakini pamoja na hayo kufunga mlango tu na kwenda kulala haitoshi, kwasababu mwizi anajua kabisa akienda atakutana na changamoto ya milango kufungwa hivyo atakuwa amekwisha jipanga kwa njia mbadala ili kuhakikisha kuwa zoezi lake la kuiba linafanikiwa kikamilifu, hivyo ni dhahiri kuwa atakuwa na vifaa husika vya kuvunjia nyumba.

Kwahiyo ili mwenye nyumba aweze kunusuru mali zake au roho yake sio tu KUBANA MILANGO yake bali anapaswa pia AKESHE, Kwasababu mwizi hawezi kuharibu kama mwenye nyumba yupo macho. Hivyo dawa pekee ya kudhibiti wizi usiku ni kubana milango pamoja na KUKESHA.

Ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Bwana Yesu Kristo,akifananisha kuja kwake na kama ujio wa mwizi wakati wa usiku alisema …

Mathayo 24:40-44″ Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;

41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.

42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.

43 Lakini fahamuni neno hili; KAMA MWENYE NYUMBA ANGALIIJUA ILE ZAMU MWIVI ATAKAYOKUJA, ANGALIKESHA, wala asingaliiacha nyumba yake KUVUNJWA. 

44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa damu yuaja.

43 Lakini fahamuni neno hili; KAMA MWENYE NYUMBA ANGALIIJUA ILE ZAMU MWIVI ATAKAYOKUJA, ANGALIKESHA, wala asingaliiacha nyumba yake KUVUNJWA.

Tukisoma pia katika 

Marko 13:32 Bwana Yesu alisema maneno haya: Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.

33 Angalieni, KESHENI, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.

34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.

35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, KWAMBA NI JIONI, AU KWAMBA NI USIKU WA MANANE,au AWIKAPO JIMBI, au ASUBUHI;

36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.

37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, KESHENI.”

Kumbuka hapo Bwana Yesu hakusema “fungeni milango” bali alisema “kesheni” kwasababu inajulikana ni wajibu wa kila mtu kufunga milango yake, na kufunga milango ina maana kujiona umeokoka lakini maisha yako hayaendani na ukristo,umebatizwa na unaenda kanisani lakini umelala katika roho(vuguvugu), nje milango imefungwa lakini ndani umelala kwasababu hiyo basi mwizi atakapokuja hautajua lolote.

Mkristo aliyeridhika na dhehebu lake au mapokeo yake lakini hazingatii mambo ya muhimu yanayohusiana na wokovu wake na maisha yake ya umilele ni sawa na mtu aliyejifungia na kulala usingizi.

Dunia sasa hivi ipo katika GIZA NENE SANA ikiashiria kwamba huu ni wakati wa USIKU na ndio wakati uliokaribia wa BWANA kurudi tena, kuongezeka kwa maovu ulimwenguni kama vile anasa,ulevi,uasherati uliokithiri hususani katika ulimwengu huu wa sasa wa utandawazi,mauaji,uchawi,rushwa,dhuluma, kupenda ulimwengu zaidi ya Mungu,n.k. vinawafanya watu wazidi KULALA usingizi wa mauti, na jinsi giza linavyozidi kuongezeka ndivyo wakristo nao wanavyozidi kushawishika kulala.

Sasa katikati ya kilele hichi cha maovu hapo ndipo Kristo atakaporudi, alisema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu watu walikuwa wakila na kunywa(ikiashiria kufanya anasa),walikuwa wakipanda na kujenga, hata siku ile ikawajilia kama ghafla, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.

1Thesalonike 5:1 Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.

8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. “

Bwana Yesu pia alisema..

Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.) “.

MAANA YA KUKESHA NI NINI?

Kukesha kunakozungumziwa ni KUKESHA KATIKA ROHO, kutokulala katika roho, kudumu katika utakatifu,huku matunda ya roho yakijidhihirisha upole,kiasi,upendo,uvumilivu,n.k pamoja na kuishi maisha ya kama mtu anayemngojea Bwana wake, kama msafiri duniani, asiyefanana na watu wa ulimwengu huu waliousingizini, huku macho yake yakitazama mambo ya mbinguni yanayokuja,

Utajisikiaje siku hiyo utakapoona wenzako wamekwenda kwenye unyakuo na wewe umebaki? ni uchungu usioneneka, mara nyingine Mungu anawaotesha watu ndoto kwamba unyakuo umepita na wenyewe wamebaki, hapo ni Mungu anajaribu kuwakumbusha watu kwamba maisha yao hayajakidhi vigezo vya kwenda mbinguni.Huu ni wakati wa kuamka usingizini biblia inasema..katika Waefeso 5:14 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.”

Amka ndugu utoke katika usingizi wa wafu wa ulimwengu huu, uasherati ni usingizi,kiburi cha uzima ni usingizi,ulevi,sigara,anasa,fashion,ushirikina,usengenyaji,rushwa,ulawiti,utoaji mimba,wizi,utukanaji vyote hivi ni usingizi wa kiroho, na kumbuka siku Kristo atakapokuja kulichukua kanisa lake hawa hawatajua lolote badala yake watabaki hapa wakingojea ile SIKU KUU YA BWANA inayowaka kama tanuru ndivyo biblia inavyosema,

2 Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana ITAKUJA KAMA MWIVI; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo,IMEWAPASA NINYI KUWA WATU WA TABIA GANI KATIKA MWENENDO WENU MTAKATIFU NA UTAUWA,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? “.

Kwa kuwa sisi sote hatujui ni saa gani Bwana atakayokuja , ni wajibu wa kila mtu aliye mkristo kukesha kwa kuishi maisha ya uangalifu katika giza hili nene lililopo dunian sasa.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/Ushauri/Ubatizo/ Whatsapp. Tupigie namba hizi: +255693036618


Mada Nyinginezo:

JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE

LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.

UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

BWANA ALIPOSEMA KUWA YEYE NI “MUNGU WA MIUNGU” ALIKUWA NA MAANA GANI?..JE! YEYE NI MUNGU WA SANAMU?


Rudi Nyumbani

Print this post