Filipo ni nani na je! Kuna Filipo wangapi katika biblia?

Katika biblia wapo watu wanne Wanatajwa Kwa jina la Filipo.

1) Filipo mtume

Huyu ndiye anayetambulika sana, ambaye alikuwa ni mmoja wa mitume wa Yesu Kristo

Yohana 1:43-44

[43]Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate.

[44]Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro.

Soma pia (Marko 13:18)

2) Filipo mwinjilisti

Huyu ni moja ya wale watu saba (mashemasi), waliochaguliwa na mitume wasimamie shughuli za kanisa. Habari yake tunaisoma Katika..

Matendo ya Mitume 6:2-5

[2]Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani.

[3]Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;

[4]na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.

[5]Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;

Huyu ndiye alikwenda kumbatiza yule towashi mkushi, na baadaye Kunyakuliwa na kupelekwa sehemu nyingine kwa ajili ya injili (Matendo 8).

Lakini pia anaonekana kuja kuishi Kaisaria ambapo alikuwa na mabinti wake wanne waliokuwa wanatabiri (Matendo 21: 8-9)

3) Filipo mfalme (Iturea)

Huyu alikuwa mtoto wa Herode Mkuu.

Luka 3:1

[1]Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Uyahudi, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,

Kulingana na historia Huyu hakuonekana na sifa za chuki au ukatili bali mtenda haki, ndiye Aliyekuja kujenga mji wa Kaisari-Filipi, ulioitwa kwa jina lake (Mathayo 16:13).

4) Filipo mume wa Herodia

Alikuwa mtoto mwingine wa herode mkuu, wengine humchanganya na Filipo mfalme wa Iturea. Herode mkuu alikuwa na watoto.wawili walioitwa Filipo. Huyu hakuwa mfalme kama ndugu zake, ndiye aliyekuwa mume wa Hedoria, Ambaye alimwacha na kwenda kuolewa na kaka yake Herode, kitendo ambacho kilikemewa Na Yohana mbatizaji? Ikampelekewa yeye kufungwa na baadaye kukatwa kichwa. (Marko 6:17-19).

Nini tunaweza kumulika katika Filipo hawa wote.

Ijapokuwa walifanana majina Lakini tabia zao zilikuwa tofauti, Filipo wawili Wa kwanza walikuwa wakristo, lakini wawili wa mwisho hawakuwa wakristo.

Kuonyesha kuwa majina sio yanayowageuza watu. Bali Ni mwitikio wa injili. Ni vema kuwa na majina mazuri, Lakini ikiwa hakuna mwitikio wa kweli haiwezekani kubadilika hata tupewe majina mazuri namna gani.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii.>>>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

BWANA, SISI TUNATAKA KUMWONA YESU.

Je! ile habari ya Herode kutaka kumwua Yohana mbatizaji inajichanganya?(Mathayo 14:5 na Marko 6:20).

Ni sahihi kusema sikuitiwa kuhubiri ubatizo kama Paulo alivyosema (1Wakorintho 1:17)?.

Print this post