SWALI: Maana ya Mithali 27:18 Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake; Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.
JIBU: Mstari huo una vipengele viwili cha kwanza ni Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake
Na cha pili ni naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.
Tukianzana na hicho cha kwanza. Tufahamu kuwa Mungu ameiandika injili yake sio tu kwenye kitabu chake, bali pia kwenye vitu vya asili, ndio maana Yesu alitumia mifano mingi ya namna hiyo, kuzungumza nao habari zake mwenyewe. Kuanzia wakulima, mimea, wanyama, wafanya biashara, wafalme n.k.
Sasa hapa anasema yeye atunzaye mtini atakula matunda yake. Kumbe kula matunda ni “kutunza”. Usipotunza huwezi pata chochote. Ili uone kazi yako, utaiwekea mbolea, utaipalilia, utaipiga dawa n.k. Na mwisho utakuwa mvumilivu aidha miaka mitatu/ minne ukisubiri mazao.
Halidhalika rohoni. Sisi kama watoto wa Mungu (tuliookolewa), kila mmoja wetu anao “mtini” moyoni mwake, na huo si mwingine zaidi ya Yesu Kristo. Wengi wasichojua ni kwamba Kristo huanza kama kichanga, kisha huwa kijana mdogo, baadaye huwa mtu mzima, na mwisho huanza kutenda kazi zake. Kama tu alivyokuwa hapa duniani alivyoishi na Mariamu na Yusufu, hakuanza kufanya chochote pindi anazaliwa.
Hivyo usipomlea ipasavyo hutafaidi matunda yake vema. Ndio mfano wa mpanzi ambao Yesu mwenyewe aliutoa, akasema zile mbegu ziliporushwa nyingine zikaishia njiani, nyingine kwenye miamba, nyingine kwenye miiba, na nyingine kwenye udongo mzuri, moja ikazaa thelathini, nyingine sitini, nyingine mia. Akatoa ufafanuzi wake, kwamba zile zilizofanikiwa kuzaa, ni kwamba zilichangiwa na KUVUMILIA (Luka 8:15). Sasa kuvumilia nini? Kuvumilia hatua zote tatu za mwanzo, yaani dhiki kwa ajili ya Kristo, kujiepusha na anasa, udanganyifu wa mali, na uvivu wa kulitendea kazi Neno.
Ukuaji wa kiroho tafsiri yake ni ‘Kristo kukua ndani yako’. Ukiona upo ndani ya wokovu kwa miaka mingi, halafu huoni matunda yoyote ya wokovu wako, katika ufalme wa Mungu, tatizo linakuwa hapo, hukuwa na nafasi ya kuutunza mtini wako.
Ukiokoka, ni lazima bidii ya kusoma Neno iwe ndani yako kila siku, usiwe mvivu wa maombi, vilevile epuka maisha ya kidunia, na ubize uliopitiliza, ambao unakufanya hata nafasi ya Mungu wako unakosa. Ukizingatia hayo, baada ya kipindi Fulani utaona Kristo anavyojengeka nafsini mwako , na kukutumia.
Lakini pia sehemu ya pili inasema naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa,. Ni hekima ya kawaida, ukiwa mfanyakazi mwema kwa bwana wako, hawezi kukuchikia kinyume chake atakupa heshima yako, lakini pia na watu wengine wote wa nyumbani kwake watafanya hivyo.
Si zaidi Mungu?
Heshima hasaa kwa Mungu wako, sio kumwambia “Shikamoo” au kuomba kwa sauti ya unyenyekevu, au kuinamisha kichwa uwapo ibadani. Heshima yake hasaa ni pale unapomtumikia, unapotii agizo lake la kuwaeleza wengine habari za injili, na pale naposimama katika nafasi yako kwenye mwili wa Kristo.
Tutafute kuheshimiwa na Bwana kwa kuwashuhudia wengine injili.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Biblia imemaanisha nini kusema Nyoka atakula mavumbi?(Opens in a new browser tab)
(Opens in a new browser tab)Je ile habari ya mtini kunyauka inajichanganya?(Opens in a new browser tab)
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.(Opens in a new browser tab)
Jibu: Turejee…
Isaya 13:10 “Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze
“Matangamano” ni “Mkusanyiko wa nyota” unaoonekana na kutengeneza umbile Fulani. Wanajimu baadhi wameyataja matangamano hayo kwa maumbile ya wanyama mbali mbali, kwamfano lipo kundi moja wamelitaja kuwa na umbile kama la N’ge, lingine kama Dubu, lingine kama Simba, lingine mapacha n.k
Kwamfano kundi la nyota lenye umbile kama la Ng’e jinsi linavyoonekana mbinguni kwa macho ya damu na nyama ni kama linavyoonekana kwenye picha hapo juu.. Lakini kwa jinsi lilivyounganishwa na wanajibu mpaka kuleta umbo kama la Ng’e ni kama inavyoonekana hapa chini..
Na makundi haya ya nyota, sasa yanatumika kwa unajibu (ambayo ni elimu ya shetani asilimia mia) kwaajili ya utambuzi wa majira na nyakati za watu, Elimu hii kwa jina lingine inaitwa FALAKI, Fungua hapa kwa maelezo Zaidi >>>Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).
Elimu hii wanajimu wanaitumia kutabiri mambo yajayo juu ya mtu, ndio hapo mtu anaenda kusomewa nyota yake na kufanyiwa utabiri, jambo ambalo kiuhalisia ni elimu ya giza, mtu yule anakuwa haambiwi mambo yajayo bali anapangiwa mambo yajayo na ibilisi, akidhani ndio katabiriwa.
Sasa Elimu hizi za Falaki pamoja na ibada zote za jua na mwezi na sayari, Bwana Mungu kazilaani, na siku za mwisho Jua, na mwezi vitatiwa giza, na Nyota zote za mbinguni zitaanguka na Matangamano yote yatazima.. kuonyesha kuwa mambo hayo yaliyotukuka kwa wanadamu si kitu mbele za Mungu, na Bwana atawaadhibu waovu pamoja na ulimwengu, ndivyo maandiko yasemavyo.
Isaya 13:9 “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali”.
Kuhusiana na unabii wa kufutwa kwa Mwezi, nyota na sayari zote siku za mwisho pitia maandiko haya Yoeli 3:15, Marko 13:24, Mathayo 24:29, na Ufunuo 6:12.
Kwahiyo ndugu usiende kusoma gazeti kwa lengo la kutafuta utabiri wa nyota, ni machukizo kwa Bwana, usiende kwa waganga ili wakakusafishie nyota, kinyume chake ndio unaenda kuharibu maisha yako, badala yake mfuate Bwana YESU naye atayasafisha maisha yako.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?
Mungu anaweza kuahidi, lakini kama hujui kanuni za kusubiria ahadi za Mungu unaweza usipokee lolote. Kila mmoja wetu amestahili kupokea lolote analo mwomba Mungu endapo ameomba sawasawa na mapenzi yake (yaani sio kwa matumizi mabaya). Yawezekana wewe umeomba Bwana akupe kazi, akupe mke/mume bora, akuponye ugonjwa wako, aikuze karama yako n.k.
Sasa mahitaji kama hayo na mengine yoyote. Mungu alisema kwenye Neno lake, atatupatia (1Yohana 5:14). Na hivyo inakuwa kwake ni ahadi ambayo lazima aitimize. Kwahiyo wewe unachopaswa kufanya ni kusubiri tu. Kuzingojea hizo ahadi za Mungu kwasababu ni lazima zije. Jifunze tu kungojea.
Maombolezo 3:25 Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. 26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu
Sasa unazingojea katika mazingira gani?. Hapo ndipo unapopaswa ujue.
Embu tuangalie kwa mtu mmoja ambaye aliahidiwa jambo na Mungu. Na hivyo alikuwa katika mazingira gani, mpaka akalipokea. Mtu mwenyewe si mwingine zaidi ya Simeoni.
Tusome.
Luka 2:25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, NAYE NI MTU MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, AKIITARAJIA FARAJA YA ISRAELI; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;
30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,
31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;
Wengi wetu tukimtafakari Simeoni, tunatengeneza picha ya mtu Fulani, mzee aliyekuwa anamngoja Mungu tangu ujana wake hadi uzee atimiziwe ahadi yake. Lakini biblia haituelezi katika picha hiyo, inatueleza alikuwa ni “mtu mwenye haki mcha Mungu”. Na tazamio lake lilikuwa ni kuona mkombozi anakuja duniani, Mungu akasikia kiu yake, ndipo akamwambia utamwona.
Ni jambo gani unapaswa ujue?
Kungojea ahadi za Mungu sio tu kusema ‘Bwana naomba hiki au kile’. Hapana, ni pamoja na kutembea katika haki na kumcha Mungu. Simoni alikuwa hivyo, hakuwa mtu anayetarajia jibu lake, huku anaendelea na udunia kama wengine, huku anaendelea na anasa kama wanadamu wengine, huku anaendelea na uzinzi kama wapagani.
Alidumu muda wote, kuyalea maono aliyoonyeshwa na Mungu, katika hofu ya Kristo. Ndipo wakati ulipofika akaona alichokuwa akikitarajia.
Palilia maono yako uliyomwomba Mungu akutimizie/ au aliyokuonyesha, kwa kutembea ndani ya Kristo. Mche Mungu, kuwa mtu wa rohoni uliyejazwa Roho kama Simoni, tembea katika usafi wa Kristo, kataa udunia, na maisha ya kipagani, kuwa mwombaji.
Ni hakika hilo ulilomwomba Bwana utaliona tu, baada ya wakati Fulani, haijalishi ni gumu/zito kiasi gani, au limepitiliza muda kiasi gani. Utalipokea tu, katika ubora ambao hukuutegemea.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Mithali 20:13 “Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula”.
Usingizi unaozidi unachelewesha utekelezaji wa majukumu ya muhimu. Kwamfano Mwanafunzi anayelala kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa shule, vilevile mfanyakazi alalaye kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa kazini, mfanya biashara anayelala kupita kiasi ni lazima atachelewa kuanza biashara yake.
Upo usemi usemao “biashara ni asubuhi” maana yake kwa mtu anayefanya biashara labda ya kuuza duka, asubuhi ndio wakati wa kufungua bishara maana watu wengi wanawahi kutafuta bidhaa asubuhi Zaidi ya mchana, hivyo alalapo sana hatapata zile faida za asubuhi, na hivyo yupo hatarini kufilisika.
Atapanga kweli kuwahi kuamka mapema kesho, lakini ifikapo asubuhi kitanda kinakuwa na nguvu kuliko maamuzi yake, atajiongezea muda wa kulala, na mwisho wa siku atashtukia kumeshapambazuka na jua linawaka..na hayo ni matokeo ya kusema “bado kulala kidogo”.
Mithali 6: 9 “Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?
10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!
11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.
Sasa biblia ni kitabu kilichojaa hekima ya kumwongoza mtu hata katika maisha ya kawaida Zaidi ya yale ya rohoni…. ni kitabu kilichojaa mafunzo mengi mema yahusuyo kanuni za kimaisha na kitabu cha Mithali kimejaa mafunzo hayo.
Hivyo biblia inatufundisha wakristo tuwe na kiasi katika kulala, kwani usingizi unaozidi una matokeo mabaya.. Si kila changamoto inasababishwa na “wachawi”….. nyingine zinatokana na tabia zetu wenyewe.., na hivyo biblia inatufundisha jinsi ya kuepukana nazo, kwamba ni kubadili tu mienendo.
Maana yake ni kwamba, tukitaka kuepukana na “umasikini” kanuni sio tu “kufunga na kuomba” bali pia ni KUTOUPENDA USINGIZI!. Ukifunga na kuomba na huku unaendekeza usingizi kupita kiasi hakuna matokeo yoyote utakayoyaona.
Maana yake kama ni mfanyakazi basi usiwe mtu wa kupenda kulala mno..Ni kweli hatuwezi kuacha kulala kabisa, lakini kusizidi mipaka, kwani usingizi uliozidi ni zao la ibilisi.
Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”
Lakini pia kiroho hatupaswi kulala kabisa, kwani usingizi wa kiroho matokeo yake ni mabaya kuliko ule wa kimwili.. Matendo yote ya giza mtu ayafanyayo ni matokeo ya usingizi wa kiroho..
Mtu anayefanya uzinzi, uasherati, anayelewa pombe, anayeiba, anayetukana, anayesengenya…huyo macho yake yamefumba kwa usingizi mzito.
Je na wewe umo miongoni mwa waliolala kiroho? Basi huu si wakati wa kuendelea kulala, bali wa kuamka na kuyaacha matendo ya giza.
Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba SAA YA KUAMKA KATIKA USINGIZI imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
12 USIKU UMEENDELEA SANA, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.
13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu”
Waefeso 5:14 “ Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”.
Bwana atubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
Masomo maalumu kwa wahubiri.
Isaya 29:16 “NINYI MNAPINDUA MAMBO; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?”
Kama Mtumishi/Mhubiri jihadhari na MAPINDUZI yasiyo na msingi!.
USIIPINDUE INJILI YA KRISTO KWASABABU YA TAMAA YA FEDHA.
Unapoanza kuwadanganya watu wa wenye nia ya kumtafuta Mungu, ili tu upate fedha kutoka kwao!.. unapoanza kuwatumainisha watu wa Mungu mambo ya uongo ili tu uwatoe fedha!.. Hiyo ni ishara mbaya na hatari kubwa sana kwako!. Bwana ataenda kukupindua nawe pia!.
Tito 1:11 “Hao WANAPINDUA watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu”.
Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kufanya biashara katika nyumba ya Mungu (ambayo ni wewe mwili wako sawasawa na 1Wakorintho 3:16) kwa kuanza kufanya uasherati na uzinzi na ukahaba fahamu kuwa Bwana naye atakupindua (Soma 1Wakoritho 6:19).
Ukilipindua Neno la Mungu kwa kuiharibu nyumba yake (kama jengo) kwa kuanza kufanya biashara ndani yake na kufanya yasiyofaa Bwana YESU atazipindua meza zako (soma Mathayo 21:12)
Ukilipindua Neno la Mungu juu ya utakatifu wa mwilini na rohoni (sawasawa na 1Wathesalonike 5:23) na kuanza kufundisha/ kuhubiri kuwa Mungu haangalii mwili bali anaangalia roho tu peke yake ni kupindua maandiko ambako matokeo yake ni Mungu kuyapindua maneno yako na wewe kwa ujumla.
Mithali 22: 12 “Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali HUYAPINDUA MANENO YA MTU HAINI”
Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kuhubiri kuwa YESU KRISTO bado sana arudi, au kwamba hakuna mwisho wa dunia, huko ni kupindua mambo ambako matokeo yake ni mabaya kama ya Fileto na Himenayo.
2Timotheo 2:17 “na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,
18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata KUIPINDUA imani ya watu kadha wa kadha”.
Kama Mhubiri Ni heri KUPINDUA ulimwengu kwa mambo ya kweli ya INJILI kama walivyofanya Mitume wa kanisa la kwanza kuliko kuigeuza/kuipindua injili kwa faida zetu wenyewe.
Matendo 17:6 “na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa WALIOUPINDUA ULIMWENGU WAMEFIKA huku nako”
Siku ya Mapinduzi makuu inakuja, ambapo Bwana ataipindua dunia yote kama alivyoipindua miji ya Sodoma na Gomora (soma Kumbukumbu 29:23) na kipindi cha gharika ya Nuhu (Soma Ayubu 12:15).
Ezekieli 21:27 “NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa”
Hegai 2:22 “nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake”.
Usipindue Mambo yaliyonyooka, bali pindua yale yaliyopotoka.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
SWALI: Nini tafsiri ya Mithali 27:22
Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.
JIBU: Kama tunavyojua mtwangio na kinu ni vyombo vinavyotumika kuponda-ponda nafaka ngumu kuwa unga, au wakati mwingine mimea migumu kuwa milaini. Mfano wa kisamvu ambacho ili kiweze kulika, majani yake huwezi yapika hivyo hivyo huna budi kuyatwanga twanga kidogo, yalainike ndipo upike ule.
Na vivyo hivyo, nafaka kama mahindi, au ngano, ili viweze kulika zamani vilikuwa vinatwangwa kwenye vinu ,tofauti na sasa vinasagwa na mashine.
Sasa katika mithali hiyo, Mungu anatoa, asili ya mtu mpumbavu, kwamba hata akitwangwa, mfano wa ngano kinuni, huo upumbavu hauwezi kumtoka. Yaani njia gani ya lazima itumike bado hawezi kuacha upumbavu.
Sasa ni vizuri kufahamu, mpumbavu ni nani?
Mpumbavu kibiblia sio mtu Fulani mjinga tu hapana, bali ni Neno pana, linalolenga kuanzia
mtu anayesema hakuna Mungu (zaburi 14:1)
Mtu mgomvi (Mithali 9:13),
Mtenda maovu (Mithali 10:23)
Anayejiona njia yake ni sawa machoni pake (Mithali 12:15)
Mwenye kiburi (Mithali 14:3)
Mwenye dharau (Mithali 15:5)
Yaani kwa kifupi mpumbavu ni mtu ambaye hana Mungu ndani yake. Kwasababu dhambi ndani ya mtu ndio chanzo cha Upumbavu wote.
Sasa mtu kama huyu, hakuna kitu kinachoweza kuutoa upumbavu huo ndani yake, waweza kusema elimu, lakini ni watu wangapi wameelimika, lakini walevi, watukanaji, mashoga. Hata atwangwe vipi kinuni hawezi lainika, ikiwa hajui ni kipi sahihi kinachoweza kutoa upumbavu huo.
Kumfunga mwizi, hakumfanyi wizi au tamaa ya kuiba itoke ndani yake, mara ngapi unasikia mwizi katoka jela, karudia wizi wake, au ni kiongozi ambaye anaaminiwa awe kielelezo cha kupambana na ufisadi, lakini yeye ndio anakamatwa katika ufisadi, au teja ametolewa hospitalini karudia, tena madawa la kulevya. Ndio maana jamii ijapojaribu kudhibiti vitendo viovu, bado haviishi, bali hubadilika tu maumbile. Kwasababu mpumbavu hata atwangwe kinuni, hawezi geuka, hakuna nidhamu inayoweza mbadilisha. Huwezi acha mwenendo wake mbovu kwa semina za kijamii, au kuwekewa sheria
Je! Ni kipi kinachoweza kumgeuza?
Ni Yesu Kristo tu. Yeye ndiye aliyetiwa mafuta, na Mungu kuwaokoa watu wa Mungu na kuwafungua. Amwaminiye na kudhamiria moyoni mwake kumfuata, basi atageuzwa moja kwa moja na kuwa mtu mwingine, huo ni uhakika.
Alisema.
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.
Ni ahadi yake kuwa Ukimwamini jambo la kwanza ni kukusamehe dhambi zako, kwasababu ndio jambo lililomfanya aende msalabani kwa ajili yako miaka elfu mbili iliyopita,. Unakuwa huhesabiwi dhambi tena, unahesabiwa haki bure kwa neema yake. Lakini sambamba na hilo anakupa UWEZO wa kuwa kama yeye kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu atakayemwachia ndani yako, pindi tu unapoamini.
Na baada ya hapo utashangaa tu unavyoanza kubadilika moyoni mwako.
Zingatia tu toba ya kweli, pamoja na ubatizo sahihi (kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la Yesu Kristo). Na kumtii yeye.
Upumbavu utakutoka.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Fahamu Maana ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.
Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?
SWALI: Nini maana ya Mithali 26:2
Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
JIBU: Mungu anafananisha laana isiyo na sababu na ndege wanaotanga-tanga angani.
Kama tunavyojua ndege hawa aina ya shomoro na mbayuwayu, kila siku tunawaona wanaruka angani, kila siku tunawaona wapo hari-hari, wanaonekana kama wapo buzy, lakini katika kazi zao zote, na juhudi zao zote, na mikakati yao yote, kamwe huwezi ona yanaleta madhara yoyote kwa mwanadamu. Hata kama utawaharibia viota vyao, hata kama watakauwa na hasira na wewe, huwezi ona wanamshambulia mwanadamu, kwasababu uwezo huo hawana. Huwezi wafikiria na kila wanapokuona wanakimbia. Wewe mwenyewe ukiwaona huwezi kuwaogopa, tofauti na ukimwona nyoka, utajidhatiti asikuume. Lakini ndege huvai ‘chapeo’ kichwani kujilinda naye asikuume, kwasababu hana madhara.
Ndivyo Mungu anavyotufundisha, laana zisizo na sababu, haziwezi kukupata ni kama ndege tu angani, zitapita, na kuendelea na shughuli zake, kamwe haziwezi kukupata ikiwa wewe ni mtakatifu, Hii ni kutufundisha kuwa hatupaswi kuwa waoga wa maneno ya watu (laana) ambayo hayana sababu.
Ukiona laana imekupata basi ujue kulikuwa na sababu nyuma yake, (lakini sio tu maneno matupu mtu anayoyatoa), mfano wa laana hizi ni ile ya Elisha aliyowalaani wale vijana 42, walioraruliwa na dubu. Kwasababu walimdhihaki. (2Wafalme 2:22-25)
Lakini mfano wa laana zisizo na sababu, ni ile Goliathi aliyomlaani Daudi kwa miungu yake, ambayo ilikuwa ni kazi bure..
1Samweli 17:42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri. 43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake
Ni mfano mwingine ni ile Balaamu mchawi alivyojaribu kuwalaani Israeli ikashindakana, kwasababu huwezi laani vilivyobarikiwa. (Hesabu 23)
Hata leo, ikiwa wewe umeokoka, hupaswi kuogopa, maneno yoyote iwe ya waganga au wanadamu. Kwasababu wewe tayari ni mbarikiwa. Ni ajabu sana kuona mkristo, analia na kutetemeka, eti! Mchawi kamwambia mwaka huu hautaisha atakuwa watoto wake wote watakuwa wamekufa!!. Mzee wa mila kamwambia atapata ajali kwasababu hakutambika kijijini mwaka huu.
Mwingine anawaza, mzazi kamwambia hatafanikiwa kwasababu kaamua kuokoka. Haa! Unaogopa nini hapo?. Hizo ni laana zisizo na sababu. Ishi kwa amani zione tu kama ndege wa angani ambao hukai kuwafikiria kama watakushambulia siku moja.
Ukiokolewa na Kristo umebarikiwa, wewe sio wa kunenewa maneno ovyo ovyo tu, na yakatokea. Wewe ni uzao wa kifalme usiotetemeshwa, ngome imara isiyoangushwa. Mwamba mgumu usiogharikishwa. Yatambue mamlaka na nguvu ulizopewa ndani ya Kristo. Usiogope!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Elewa maana ya Mithali 26:2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,
Maana yake nini, Mwe na hofu wala msitende dhambi? (Zaburi 4:4)
Katika Ayubu 41, tuona Mungu akieleza kwa urefu sifa ya mnyama mamba.
Ametumia taswira ya mamba huyu tunayemwona, kumwelezea mamba wake wa rohoni, ambaye hasaa Ayubu alionyeshwa habari zake kwa urefu kupitia sura hii.
Na ndio maana kuna sifa nyingine ukizisoma hapo, huwezi kuziona kwa mamba huyu tuliye naye sasa, lakini Mungu hupenda kutumia mifano halisi walau tupate taswira wa kile alichokimaanisha. Ndio maana akaweka sifa chache kwenye mambo wetu huyu ili tumwelewe.
Sasa katika sura hii, Mungu anaanza kwa kumwonyesha Ayubu jinsi anavyomtofautisha sana mnyama mamba na viumbe vingi mbalimbali vilivyopo duniani, kuanzia vya kwenye maji kama vile samaki, mpaka vile vile vya angani kama vile ndege, hadi wanyama wa kufugwa kama ng’ombe na wale wa mwituni kama vile simba.. Hawa wote hakuna aliyelinganishwa naye.
Mungu anamwonyesha ukali mwingi alionao, nguvu alizonazo, ugumu ulio katika ngozi yake, kiasi cha mkuki wowote kushindwa kupenya kwenye ngozi yake, zaidi sana ujasiri alioumbiwa. Kwa ufupi kulingana na habari hii hakuna mnyama aliyeweza kulinganishwa na huyu duniani kote.
Sasa embu soma hizi sifa, na mwishoni utamjua mamba huyo ni nani, na uzao wake ni upi. (Zingatia maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa)
Ayubu 41
1 Je! Waweza wewe KUMVUA MAMBA KWA NDOANA? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba? 2 Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu?
3 JE! ATAKUSIHI SANA? Au, atakuambia maneno ya upole? 4 Je! Atafanya agano pamoja nawe, UMTWAE KUWA MTUMISHI WAKO milele?
5 Je! UTAMCHEZEA kama ndege? Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako? 6 Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara? WATAMGAWANYA kati ya wafanyao biashara?
7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa? 8 Mwekee mkono wako; Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.
9 Tazama, kumtamani ni bure; Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama? 10 HAPANA ALIYE MKALI HATA AKATHUBUTU KUMWAMSHA; Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi? 11 Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.
12 Sitanyamaa kusema habari za via vyake, Wala nguvu zake kuu, wala umbo lake zuri. 13 Ni nani AWEZAYE KUMBAMBUA MAGAMBA YAKE? NI NANI ATAKAYEPENYA DIRII YAKE MARADUFU? 14 Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake? Meno yake yatisha kandokando yake.
15 Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake, Yamefungamana pamoja kama kwa kufungwa kwa muhuri. 16 Jinsi yalivyoshikamana Hata upepo hauwezi kupita kati. 17 Yamefungamana pamoja; Yameshikamana, hata hayawezekani kutengwa.
18 Kwa kuchemua kwake mwanga humemetuka, Na macho yake yanafanana na makope ya alfajiri. 19 MIENGE IWAKAYO HUTOKA KINYWANI MWAKE, NA MACHECHE YA MOTO HURUKA NJE. 20 MOSHI HUTOKA KATIKA MIANZI YA PUA YAKE, Kama nyungu ikitokota, na manyasi yawakayo.
21 Pumzi zake huwasha makaa, Na miali ya moto hutoka kinywani mwake. 22 Katika shingo yake hukaa nguvu, Na utisho hucheza mbele yake. 23 Manofu ya nyama yake hushikamana; Yanakazana juu yake; hayawezi kuondolewa.
24 MOYO WAKE UNA IMARA KAMA JIWE; Naam, imara kama jiwe la chini la kusagia. 25 Anapojiinua, mashujaa huogopa; Kwa sababu ya woga wao huvunjwa moyo. 26 Mtu AKIMPIGA KWA UPANGA, HAUMWINGII; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.
27 Yeye huona chuma kuwa kama nyasi, Na shaba kama mti uliooza. 28 Mshale hauwezi kumkimbiza; Na mawe ya teo kwake hugeuka kuwa kama makapi. 29 Marungu huhesabiwa kama mabua; Naye hucheka mshindo wa mkuki ukitupwa.
30 Pande zake za chini ni kama vigae vikali; Hutandika malazi kama kuweka chombo cha kupuria nafaka juu ya matope. 31 Yeye huchemsha kilindi mfano wa nyungu; Hufanya bahari kuwa kama mafuta.
32 Hufanya mapito yake kung’aa nyuma yake Hata mtu angedhani kilindi kina mvi. 33 JUU YA NCHI HAPANA ALIYEFANANA NAYE, ALIYEUMBWA PASIPO OGA. 34 Yeye hutazama kila kitu kilicho juu; Ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.
Mamba huyu si mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO.!
Hakuna ufalme, au mwanadamu, au mamlaka iliyoweza au inayoweza kuutetemesha ufalme wa Kristo, zaidi dunia nzima humuhofu. Yeye sio samaki, yeye ni zaidi ya mamba.
Lakini pia anao uzao wake tofauti na uzao wa viumbe vingine. Na watoto wake watafanana na yeye, ndio wale waliomwamini. Ndio maana ukimpokea Kristo kwa kuzaliwa mara ya pili, unakuwa mtu mwingine kabisa duniani, kwasababu asili yake inakaa ndani yako.
Ndugu, utaishi kinyonge hapa duniani, mapepo yatakusumbua, dunia itakusumbua kwasababu wewe ni dhaifu, na utaendelea kuwa dhaifu tu kama visamaki vingine vinavyovuliwa-vuliwa tu ovyo na ndoano. Lakini ukimpokea Kristo maishani mwako. Wewe ni mtu mwingine.Rohoni unaogopeka mno.
Embu leo tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, mwambie Yesu naufungua moyo wangu, ingia ndani yangu, na hakika ataingia, na kukusamehe dhambi zako zote, kama hakikisho la uzima wa milele . Atakufanya kiumbe kipya, hakikisha tu unamaanisha kusema kimatendo kuanzia leo YESU ni wangu, mimi ni wake. Hilo tu, kisha nenda ukabatizwe ikiwa hukubatizwa. Baada ya hapo asili yako itabadilishwa. Uwe mamba, umiliki na kutawala sio samaki.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Neno “Via” linamaanisha nini katika biblia?
KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?
Waefeso 2:10
MAANA TU KAZI YAKE, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu tujifunze maneno ya uzima.
Mimi na wewe kama vile maandiko yanavyosema hapo, ni “kazi ya Mungu”..Hivyo ni lazima kujua kama ni kazi ya Mungu basi ni lazima pia tumekusudiwa kutimiza jukumu fulani hapa duniani.
Kwamfano unapoona gari, unasema lile ni kazi ya mtu sio mbuzi.. Na kama ni kazi yake, basi kuna wajibu fulani nyuma yake ambao liliumbiwa lifanye. Na wajibu wenyewe ni kumsafirisha mtu au vitu kwa haraka na wepesi.
unapoona nyumba, tunasema ni kazi ya mtu, imejengwa kuwa makao ya kupumzika, haijajengwa tu, bila kusudi lolote duniani.
hata unapoona kiota, ile ni kazi ya ndege kakijenga sio kiwe tu pale kama takataka, bali aishi ndani yake.
Vivyo hivyo na sisi ni kazi ya Mungu tuliumbwa kutimiza kusudi fulani. Hivyo ni lazima ujue, na kusudi lenyewe ni KUTENDA MATENDO MEMA.
Sisi ni vyombo mahususi, Mungu alivyovikusudia kudhihirisha matendo mema, ambayo aliyaumba tangu mwanzo yatendwe, hakuna chombo chochote chenye uwezo wa kufanya hivyo isipokuwa mwanadamu.
Waefeso 2:10
MAANA TU KAZI YAKE, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Sasa wewe kama mtu usipojua wajibu wako hapa duniani, utakuwa hatarini kuangamizwa. Ni sawa na TV isiyoonyesha kitu, gari lisilotembea, pasi isiyotoa moto. ni wazi kuwa vitatupwa kama sio kuwekwa kwenye karakana.
Na wewe vivyo hivyo, fahamu kuwepo kwako duniani ni kutenda matendo mema. ndio kusudi lako
Sasa, si matendo mema, ilimradi matendo mema…hapana…yapo matendo mema, lakini yasiwe na nguvu mbele za Mungu, hayo ndio yale ambayo mataifa huyafanya..lakini matendo mema tunayoyazungumzia hapa ni yale yaliyo ndani ya YESU KRISTO. Ndio maana hapo anasema tuliumbwa katika Kristo Yesu, sio katika Adamu, au Ibrahimu, au nabii fulani bali Kristo Yesu..maana yake matendo ya Yesu, (au kwa namna nyingine tabia za Yesu) ambayo hakuna mwingine awezaye kuyatenda isipokuwa mtu huyo amezaliwa mara ya pili.
Hivyo leo tutatazama aina ya matendo hayo mema ambayo wewe kama mwana wa Mungu huna budi kuyadhirisha uwapo duniani.
Upendo wa Kristo, sio kama upendo wa kiulimwengu, ule ambao, unawapenda wakupendao hapana..mbele za Mungu hapo bado hujafanya tendo la upendo, huo ni mwanzo tu.
bali ni ule wa kupenda wanaokuudhi, lakini sio kupenda tu, unafikia hatua ya kuwaombea, na unapofikia kilele chake unaweza hata kuutoa uhai wako kwa ajili yao.
Mathayo 5:43-48
[43]Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
[44]lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
[45]ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
[46]Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
[47]Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
[48]Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Huu unaitwa upendo wa agape. Mimi na wewe lazima tufanye bidii tuudhihirishe. Ndio ulioumbiwa tangu mwanzo uuonyeshe kwa wengine. Epuka mafundisho ya piga adui zako, kumbuka wewe ni kazi ya Mungu, kuonyesha upendo.
Yesu alisema haki yenu isipozidi ya waandishi na mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Mathayo 5:20
[20]Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Mafarisayo walikuwa hawana Roho Mtakatifu, hivyo mambo yote waliyatimiza kwa nguvu lakini haikusaidia kuondoa tamaa za mwili. walikuwa hawazini lakini mioyo yao ilikuwa na tamaa. Lakini Yesu alitoa mizizi ya uzinzi, ndani ya mtu kwa Roho wake mtakatifu anayempa.
Ndio maana kwanini unapaswa ujazwe Roho, lakini pia utembee kwa Roho Mtakatifu ili uweze kuushinda mwili, vinginevyo hutaweza kwa nguvu zao, utafanya kinafiki. Biblia inasema..
Wagalatia 5:16-17
[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
[17]Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Ni lazima ujifunze utii wa Neno la Mungu, kwa kujikana nafsi, na kumfuata Yesu, wakristo wengi hawajikani nafsi, wanakiri wokovu lakini gharama zake hawataki kuingia, wamesilibiwa kweli msalabani lakini hawataki kufa, hawataki kuvunjwa vunjwa miguu yao wafe,. Ukiingia kwa Kristo kubali kufa ili akuhuishe, ndivyo utakavyoweza kuushinda ulimwengu, kubali kusema bye! bye! kwa ulimwengu. Utaona tu jinsi gani utakavyoweza kuishi maisha matakatifu bila shida yoyote. Roho Mtakatifu huwa anapata nguvu ya kumbadilisha mtu pale ambapo anakubali kujikana kweli nafsi. lakini kama hataki, Mungu kidogo, udunia kidogo, utaendelea kuwa vilevile tu kama mafarisayo na waandishi, ambao vikombe vyao havijasafishwa kwa ndani.
Wewe ni kazi ya Mungu umeumbwa uwe mtakatifu kama yeye alivyo mtakatifu. Kubali tu kuongozwa na Roho kwa kujikana nafsi.
1 Petro 1:16
[16]kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Yesu alipokuja duniani, alitambua kuwa vinywa vyetu viliumbwa mahususi, kuwafundisha na kuwaekeza wengine njia iliyo sahihi. Ndio maana mapema tu, alianza kuhubiri na kufundisha katikati ya vijiji na miji, habari za ufalme..Huoni hayo ni matendo mema?
Warumi 10:15
[15]Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Halikadhalika hatuna budi kufahamu agizo la sisi kuhubiri, ndilo tuliloumbiwa na Mungu tangu mwanzo tulifanye..ndio agizo kuu. Jambo ambalo lipo kwa wakristo tu. Ni mpango ambao Mungu amekusudia kuutumia kuzungumza, kuponya, kufungua watu kupitia watu hao hao.
Sasa ikiwa wewe umeokoka halafu, huna habari ya kuwashuhudia wengine Injili, fahamu kuwa wewe, sio kazi ya Mungu, uliyeumbwa katika Kristo Yesu. Bali ni kazi ya mwingine.
Amka sasa, ondoa woga na uvivu wa kuwatangazia wengine Kristo, usiwe chombo kibovu, anza kuwatangazia wengine wokovu, uwezo huo upo ndani yako, kushuhudia hakuhitaji elimu yoyote ya biblia au vifungu elfu vya kwenye maandiko, ni kueleza ushuhuda wa maisha yako matendo makuu Kristo aliyokutendea, ushuhuda huo unatosha kumgeuza mwingine, kabla hujafikiria kutoa vifungu anzia kwanza hapo. Ndicho alichokifanya yule kichaa aliyetolewa pepo, Yesu alimwambia nenda kwenu kawashuhidie watu matendo makuu Mungu aliyokutendea, na kwa kupitia ushuhuda wake taifa zima la Dekapoli likamwamini Kristo, mwanamke msamaria, kusikia tu habari zake zinafichuliwa akaenda kuwaleza watu, samaria yote ikaamini. Hakuna haja ya kuwa na hofu, anza sasa kuwashuhudia ndugu zako.
Wewe ni kazi ya Mungu, umeumbwa ili uhubiri.
Vilevile Matendo ya imani, tuliumbiwa sisi tangu mwanzo tuyadhihirishe, na ndio maana hatumwoni Mungu kwa macho, tofauti na malaika, kwasababu tumetengenezwa kwa namna hii, haiwezekani wewe kumpendeza Mungu pasina imani.
Waebrania 11:6
[6]Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Lakini imani yetu, haina budi kuzidi ile ya watu wa kidunia, ya kwetu huzaliwa na Neno la Mungu, nguvu ya Mungu iliyo katika msalaba wa Yesu.
tukiumwa tunaamini hakika, Yesu alishayachukua magonjwa yetu, huzuni zetu, umaskini, hatuna mashaka kwasababu Yesu alishayamaliza yote. Hatupaswi kuwa na hofu ya maisha, Yesu mwokozi wetu ameshayamaliza.
Kuwa mtu wa imani, liweke Neno la Mungu kwa wingi ndani yako. Mtegemee Kristo, amini kazi zake. Usiishi kwa kuona.
Maombi ni mawasiliano. Sisi kama kazi yake anatazamia, tuwe watu wa kumtegemea kwa asilimia mia, maombi yapo ya aina mbalimbali, sifa ni moja ya maombi, ibada ni aina ya maombi,
Ndio maana Yesu alipokuja duniani, maombi yalikuwa ni sehemu ya maisha yake. Aliomba zaidi ya watu wa kidini, alikesha, akawataka na mitume wake wafanye vile, alisema ombeni nanyi mtapewa, ombeni bila kukoka, dumuni katika sala. (Mathayo 26:41, Wakolosai 4:2)
Wewe ni manukato ya Mungu, Mungu anataka kusikia harufu yako nzuri. Na harufu yenyewe ni Maombi yako.
Ufunuo 5:8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu
Vilevile fahamu maombi ni mahali ambapo unampa Mungu nafasi ya kukukarabati wewe kama chombo chake uweze kuzifanya kazi zake vyema. Vilevile Haiwezekani mwanadamu uliyeumbwa kwa mfano wa Kristo kwa wokovu uepuke maombi. Ukifa kimaombi, ni umekufa kiroho, huwezi kuzitenda kazi za Mungu.
Jambo lingine ambalo Mungu anatazamia alione kwako, ni wewe kudhihirisha umoja wa Roho ndani ya mwili wa Kristo. (Waefeso 4:3)
Yesu alisema .
Yohana 17:11, 21
[11]Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. … [21]Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ILI ULIMWENGU UPATE KUSADIKI YA KWAMBA WEWE NDIWE ULIYENITUMA.
Lengo la kufikia umoja ni ili ulimwengu umwamini Kristo. Mahali ambapo tunashindwa kupaelewa sisi kama kazi ya Mungu ndio hapo, yaani kila mtu anataka awe kivyake, au wazo lake liwe bora, tukidhani ndio tuliombwa tuishi hivyo..
halitawezekana, endapo hutatambua nafasi zetu katika mwili wa Kristo ni ipi, kama Mungu hajakupa uongozi, kwanini ung’ang’anie nafasi hiyo?
kuwa katika utumishi wa chini, hakukufanyi karama yako kudidimia, Mungu alimtoa Daudi mazizini, vivyo hivyo yule aliyemkusudia atamwinua tu popote lakini sio kugombani au kumwonea wivu mwenzako awapo kwenye nafasi fulani, hivyo ili tuufikie umoja wa Roho ni kukubali kujishusha kwa kuongozwa, na kufundishwa, na kuridhika na ulichokirimiwa na Bwana.
Tukizangatia matendo hayo. Basi tutakuwa ni vyombo bora, vinavyostahili kutumika kwa kazi rasmi za Mungu ambazo bado hazijafuniliwa..Zitafunuliwa katika huo ulimwengu ujao, Huko ambako jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.
Jiulize je! Wewe ni chombo kamilifu cha Kristo?
2 Timotheo 2:20-21
[20]Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.
[21]Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, KIMETENGENEZWA KWA KILA KAZI ILIYO NJEMA.
Hayo ndio matendo yetu mema, yatokayo kwa Kristo Yesu, sio ulimwengu. Fanya bidii kuyatoa ndani yako.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Ni kama machungwa katika vyano vya fedha.
“Vya Kaisari mpeni kaisari” ni vipi hivyo tunavyopaswa tumpe?.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu, (Mkuu wa Uzima na Mfalme wa wafalme), YESU KRISTO libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu wetu lililo taa na Mwanga wa njia zetu (Zab. 119:105).
Kiashiria cha Kwanza ni UTAKATIFU:
kwamba Roho Mtakatifu yupo ndani yako (au umebatizwa na Roho Mtakatifu) ni UTAKATIFU, angalia maisha yako, je dhambi imekuwa hafifu kiasi gani, ukijilingalisha na kipindi cha nyuma.. Ukiona kuna nguvu kubwa ndani yako ya kushinda dhambi, basi tambua kuwa si wewe, bali ni uwepo wa nguvu za Roho Mtakatifu ndani yako.
Kiashairia cha Pili ni KARAMA:
Karama maana yake ni ile shauku/msukumo wa kumtumikia Mungu katika eneo Fulani, ambao unakutofautisha na mwingine.. Ukiona una shauku kubwa ya kumtumikia Mungu, na ukiangalia shauku hiyo huioni kwa mwingine aliye karibu na wewe, au ukijaribu kumweleza mwingine ni kama hakuelewi, basi fahamu kuwa hiyo shauku si wewe, bali ni Nguvu/msukumo wa Roho Mtakatifu ndani yako. (ndio maana zinaitwa karama za roho, 1Wakorintho 12:1)
Kiashiria cha Tatu ni KUCHUKIWA/KULAUMIWA BILA SABABU:
Si kila lawama ni ishara mbaya: Ukiona kila unalolifanya la KiMungu linazua lawama, au shida mahali ulipo..basi hiyo pia ni ishara nyingine ya uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako..
1Petro 4:14 “MKILAUMIWA kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia”.
Kiashiria cha Nne: KUPUNGUA KWA HOFU NDANI YAKO.
Ukiona hofu imeisha ndani yako, kiasi kwamba wakati wengine wana wasiwasi kuhusiana na mambo Fulani wewe huna wasiwasi hata kidogo, na unajihisi kabisa kuwa Mungu yupo na wewe, basi fahamu kuwa kuna uwepo wa Nguvu za Roho Mtakatifu ndani yako, na si wewe kwa akili zako (kwasababu kwa akili za kawaida, hakuna mtu mwenye akili timamu asiyetishwa na misukosuko ya maisha).
Kiashiria cha Tano: FURAHA.
Ukiona kuna furaha isiyoelekeza ndani yako kila unapofikiria habari za YESU, na wakati mwingine unatamani kumweleza mwingine, na ukijaribu ni kama haoni kama unavyoona, basi fahamu kuwa si wewe hisia zako, bali ni nguvu za Roho Mtakatifu ndani yako, Wagalatia 5:22.
Kiashiria cha Sita: MFULULIZO WA MAFUNUO.
Ukiona kila unapotembea unamwona YESU katika neno lake, au unauona uweza wa YESU, ambao unakuletea changamko Fulani, na msisimko wa kipekee, ambao huoni kwa mwingine, basi tambua kuwa ni kazi za Roho Mtakatifu hizo ndani yako.. kwani kwa kawaida macho yaliyofumbwa hayawezi kumwona YESU popote wala kuuona uweza wake.
Vile vile ishara hii inaambatana na kupata ufahamu wa maandiko kwa namna ya kipekee sana.
SASA UFANYE NINI UNAPOGUNDUA KUWA ROHO MTAKATIFU YUPO NDANI YAKO?
Kumzimisha Roho Mtakatifu ni kitendo cha kumfanya Roho Mtakatifu aondoke ndani yako na kukaa mbali nawe aidha kwa muda kwa muda au moja kwa moja.. na vitu vinavyomzimisha Roho Mtakatifu ni dhambi za makusudi…kama uzinzi, wizi, ibada za sanamu na kupenda mambo ya kidunia.
Mambo haya mtu akiyafanya Roho Mtakatifu anaondoka ndani yake, na ile nguvu ya kushinda dhambi inaondoka ndani yake, vile vile ile nguvu ya kushinda hofu pia inaondoka ndani yake.
Kumhuzunisha Roho sawasawa na Waefeso 4:30, ni kitendo cha kumfanya Roho Mtakatifu asifurahiwe na wewe, na matokeo ya kumhuzunisha Roho Mtakatifu kwa muda mrefu, ni kuondoka ndani ya mtu.
Mambo yafuatayo yanaweza kuwa sababu ya Roho Mtakatifu kuhuzunika ndani yetu..
1. Tabia ya kukosa Imani…kama vile Bwana YESU alivyohuzunishwa na wanafunzi wake mara kadhaa, pale walipokuwa wanapungukiwa na Imani, mpaka kufikia hatua ya kuwaambia mara kwa mara “Imani yenu iko wapo”
Vile vile na sisi tunapopungukiwa na Imani katika mazingira tukutanayo hiyo Roho Mtakatifu anaugua ndani yetu, hivyo hatuna budi kuwa watu wa Imani daima.
Na Imani chanzo chake ni kusikia Neno la Mungu, (ambayo tafsiri yake ni kusoma na kujifunza biblia). Neno la MUNGU linapokaa kwa wingi ndani yetu pamoja na maombi basi viwango vyetu vya Imani vinakuwa na hivyo tunakuwa katika hali ya kumpendeza Roho Mtakatifu.
2. Tabia ya uvivu wa kiroho.. Ukiwa mlegevu kutenda yakupasayo, Roho Mtakatifu anaugua kwasababu hutumii kile ulichopewa,
Kama viashiria hivyo havipo ndani yako basi huenda Roho MTAKATIFU bado hajaingia ndani yako, au amesogea pembeni, na hiyo si kwasababu wewe ni mbaya, au una kasoro, au wengine ni bora kuliko wewe mbele zake, LA!..bali ni kwasababu bado hujafungua mlango, au ulikuwa hujui jinsi ya kuufungua mlango..kwasababu yeye anatamani aingie ndani yako Zaidi hata ya wewe unavyotamani.
Sasa swali la msingi, unaufunguaje mlango ili aingie ndani yako?
Kanuni ni rahisi sana, isiyogharimu hata theluthi ya senti moja.. na kanuni yenyewe ni kukiri tu makosa yako, kwamba wewe ni mwenye dhambi na hivyo unahitaji msaada wake (kutubu) kwa kumaanisha kabisa kuacha mambo yote mabaya.., na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU, kama bado ulikuwa hujabatizwa, baada ya hapo yeye mwenyewe ataingia ndani yako, na utaona matunda hayo na mengine Zaidi ya hayo..
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”
Kama haujabatizwa na utahitaji msaada huo, basi waweza wasiliana nasi kwa namba zilizoanishwa hapa chini na tutakusaidia juu ya hilo.
Ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
FAHAMU VIASHIRIA VYA MTU ALIYESAMEHEWA DHAMBI ZAKE.
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.