Category Archive maswali na majibu

Ni dhiki ipi hiyo watu walio kwenye ndoa huipata sawasawa na 1Wakorintho 7:28?

1Wakorintho 7:28  Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.

Awali ya yote katika vifungu hivi, Mungu hashinikizi kwamba watu  wasioe au wasiolewe.  Ndoa ni jambo jema, na lina faida nyingi sana katika maisha na pia katika huduma, kwasababu humsaidia mtu akae mbali na uzinzi na tamaa mbaya, (1Wakorintho 7:2). Pia huondoa upweke (Mwanzo 2:18), wawili wawapo mwili mmoja, ni nguvu zaidi na faraja.

Lakini Mungu anatoa pia uchaguzi, kwa mtu ikiwa anao uwezo wa kujizuia yaani kutawala hisia zake (1Wakorintho 7:9), akaishi hivyo hivyo, bila shida yoyote, ni vema zaidi kihuduma. Kwasababu humfanya asisongwe na mambo mengi ya kindoa.

Kwasababu mtu aliye kwenye ndoa ni wazi kuwa upendo wake utagawanyika kwa sehemu, biblia inasema atatafuta ampendezeje mume/mke wake.

1Wakorintho 7:32  Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

33  bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.

Lakini pia atakutana na dhiki, zinazoambatana na ndoa. Kwamfano kutatua migogoro ya kifamilia,  malezi ya watoto, kuwagharamikia, kuwasomesha,matibabu, kuwafuatilia, kuivisha familia yako, na mambo kama hayo. Ni dhiki ambazo, zinaongezeka, na hivyo hutinga ufanisi wako kwenye utendaji kazi wa injili.  Paulo huiita “shida iliyo” sasa. Yaani Kusalitiana, upendo kupoa, kupishana,  ni vitu ambavyo mara kwa mara hujitokeza katika maisha ya ndoa.

1Wakorintho 7:26  Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo.

27  Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke

Hivyo kihuduma mtu ambaye hajaoa/kuolewa, hujipunguzia dhiki, kuliko yule aliye kwenye ndoa. Hiyo haimaanishi kuwa aliye kwenye ndoa hawezi kutenda kazi vizuri, hapana kazi anaweza itenda hata zaidi ya Yule ambaye hajaoa, isipokuwa tu kwake dhiki na shida zitaongezeka.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MASWALI NA MAJIBU: YAHUSUYO NDOA

NDOA TAKATIFU NI MKE MMOJA/MUME MMOJA.

NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!

Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?

Rudi Nyumbani

Print this post

Je biblia inajichanganya kwa habari ya hukumu ya Mungu (Yohana 12:47 na Yohana 5:22, 27).

Swali: Katika Yohana 5:22 na 27 tunaona biblia inasema kuwa Mungu amempa Mwana (Yaani Bwana Yesu) hukumu yote…. lakini tukiruka mpaka ile sura ya 12:47 tunaona tena Bwana YESU anakanusha kuwa yeye hamhukumu mtu?.. Je biblia inajichanganya hapa?.


Jibu: Awali ya yote ni muhimu kufahamu kuwa Biblia ni kitabu kilichovuviwa na Roho Mtakatifu, hivyo kamwe hakina makosa…kinachoonekana kinajichanganya si Biblia, iliyo Neno la Mungu, bali ni tafakari zetu na pambanuzi zetu.

Sasa turejee mistari hiyo..

Katika Yohana 5:22  “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, BALI AMEMPA MWANA HUKUMU YOTE………….

27  Naye AKAMPA AMRI YA KUFANYA HUKUMU kwa sababu ni Mwana wa Adamu”.

Hapa ni kweli Mwana kapewa mamlaka yote ya kufanya hukumu… Tusome tena ile Yohana 12:47..

Yohana 12:47 “Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, MIMI SIMHUKUMU; MAANA SIKUJA ILI NIUHUKUMU ULIMWENGU, ila niuokoe ulimwengu”.

Tukisoma mistari hiyo kwa juu juu, ni rahisi kuona kuwa maneno hayo yanajichanganya… lakini kiuhalisia hayajichanganyi hata kidogo.. kwani ni suala la kuelewa lugha tu hapo!.

Katika Yohana 5:22, Baba amempa Mwana hukumu yote, maana yake Amri ya kuhukumu amempa yeye.. Maana yake mamlaka yote kapewa (Bwana YESU), kama vile Farao alivyompa Yusufu mamlaka yote ya Misri.

Sasa kama Bwana YESU kapewa mamlaka yote ya kufanya hukumu… ni chaguzi lake yeye ni nani amhukumu na nani asimhukumu, ni wakati gani afanye hukumu na ni wakati gani asihukumu…(kwasababu vyote vipo mikononi mwake).

Sasa kwasababu yote yamewekwa chini ya mapenzi yake, basi mapenzi yake ni “kumtomhukumu mtu yoyote duniani”…sawasawa na maandiko hayo ya Yohana 12:47.. ingawa anayo mamlaka  hayo ya kumhukumu mtu yoyote duniani kwasababu kashapewa na Baba.

Lakini hakutumia huo uwezo, wa kupitisha hukumu duniani kwa wote waliomkataa au wanaomkataa sasa, bali anawavumilia mpaka siku ya mwisho.. Mfano mzuri unaomwonyesha Bwana akiwa ameizuia hukumu yake ni ile habari tunayoisoma katika Luka 9:52-56.

Luka 9:52 “akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.

53  Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu. 54  Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?

55  Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]

56  Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine”.

Huo ni mfano wa hukumu ambayo Bwana angeweza kuito kwa Wasamaria hao, lakini alizuia… utasoma tena jambo kama hilo hilo katika Mathayo 26:51-53.

Mathayo 26:51 “Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.

52  Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga.

53  AMA WADHANI YA KUWA MIMI SIWEZI KUMSIHI BABA YANGU, NAYE ATANILETEA SASA HIVI ZAIDI YA MAJESHI KUMI NA MAWILI YA MALAIKA?”

Kwahiyo ni kweli Bwana YESU amepewa hukumu yote, lakini hatumii uwezo wa hukumu yake yote, kwetu sisi tunaoishi sasa, laiti akifanya hivyo, hakuna mwenye mwili atakayepona.. Lakini anatuvumilia sana kwasababu hataki mtu yoyote apotee (2Petro 3:9).

Ila tukiudharau wingi wa huruma zake hizi, na kupuuzia Neema mpaka siku tunaondoka katika haya maisha au siku amerudi, basi tutahukumiwa na yeye pasipo huruma… Na atatuhukumu kupitia maneno yake hayo hayo.

Hivyo ndugu yangu, YESU sasa ni mwenye huruma na mvumilivu kwetu, lakini siku ile ya hukumu hatakuwa na huruma..kwahiyo si muda wa kudharau wema wake na uvumilivu wake kwetu, bali ni wakati wa kutengeneza maisha kabla ya ile siku ya hukumu..

Warumi 2:4 “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?

5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,

6 atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake”

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

IKIWA MWENYE HAKI AKIOKOKA KWA SHIDA, MWENYE DHAMBI ATAONEKANA WAPI?

UFUNUO: Mlango wa 20

Kuna hukumu za aina ngapi?

Tirano alikuwa nani na darasa lake lilikuwaje? (Matendo 19:9)

Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?

Rudi Nyumbani

Print this post

Je wafu wanafufuliwa au hawafufuliwi kulingana na Ayubu 14:12 na 1Wakorintho 15:51?

Swali: Katika Ayubu 14:12 tunasoma kuwa wafu hawafufuliwi, lakini katika 1Wakorintho 15:51 tunaona tena biblia inasema wafu watafufuliwa, sasa tuchukue ipi tuache ipi?.. au je biblia inajichanganya yenyewe?


Jibu: Biblia kamwe haijichanganyi, wala haijawahi kujichanganya, isipokuwa tafakari zetu ndizo zinachojichanganya au kuchanganyikiwa.

Turejee mistari hiyo na kisha tuone majibu yake kupitia biblia hiyo hiyo..

Ayubu 14:10 “Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?

11 Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika;

12 Ni vivyo MWANADAMU HULALA CHINI, ASIINUKE; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.”

Ni kweli hapa maandiko yanasema kuwa MWANADAMU HULALA CHINI, ASIINUKE TENA… lakini hebu turejee agano jipya katika kitabu kile cha Wakorintho tuangalie biblia inatuambiaje..

1Wakoritho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

52  kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana PARAPANDA ITALIA, NA WAFU WATAFUFULIWA, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.

Na hapa maandiko yanatuambia, parapanda italia na wafu waliolala katika Kristo watafufuliwa. Sasa swali tuchukue lipi tuache lipi?, maneno kama hayo hayo yanarudiwa tena katika 1Wathesalonike 4:16.

Jibu ni Dhahiri kuwa “Wafu watafufuliwa siku ya mwisho”.. sawasawa na Yohana 5:25.

Kwanini maandiko hayo ya 1Wakoritho 15:51 yana nguvu kuliko yale ya Ayubu 14:12, yanayosema kuwa “wafu hawafufuliwi”?… Ni kwasababu Agano jipya ni ukamilifu wa agano la kale.

Manabii waliotangulia walifahamu mambo kwa sehemu, lakini Roho Mtakatifu katika agano jipya, amekamilisha yote na kufunua yote… Na kawaida ni kwamba unapokuja ule ufunuo mkamilifu, bali ule uliokuwa unajilikana kwa sehemu unabatilika ndivyo maandiko yasemavyo..

1Wakorintho 13:9 “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;

10  lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika”.

Manabii wengi wa agano la kale hawakujua mengi kuhusiana na ufufuo, au mbingu mpya na nchi mpya, ingawa walikuwa wanafahamu siku moja watajua mambo yote..hivyo walitoa unabii kwa sehemu waliyopimiwa…lakini mwisho wa nyakati Roho Mtakatifu anakamilisha ufunuo wote sawasawa na hiyo 1Wakorintho 13:9-10.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Wafu watafufuliwa siku ya mwisho, na watahukumiwa.

Yohana 5:28  “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.

29  NAO WATATOKA; WALE WALIOFANYA MEMA KWA UFUFUO WA UZIMA, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.

Na kumbuka hoja hii ya kufufuliwa kwa wafu ndiyo iliyoleta mgawanyiko mkubwa katikatika ya wayahudi hata kuzaliwa makundi (madhehebu) mawili ambayo ni MAFARISAYO NA MASADUKAYO, ambapo Mafarisayo waliamini ufufuo na masadukayo hawakuamini ufufuo kwa kutumia andiko hilo la Ayubu 14:12 pamoja na maandiko mengine machache..

Lakini Bwana YESU alikuja kuondoa huo utata kama tunavyosoma katika Mathayo 22:23-32..

Mathayo 22:23 “Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,

24  wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.

25  Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.

26  Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.

27  Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.

28  Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.

29  Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.

30  Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.

31  Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema

32  Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai”

Kwahiyo wafu watafufuliwa, lakini swala la msingi ni je!.. sisi tutakuwepo upande upi wakati huo wa ufufuo?.. Je tutafufuliwa ili tukavikwe taji na kuurithi uzima wa milele, au kwaajili ya hukumu ya ziwa la Moto?

Kumbuka wote walio nje ya Kristo, ambao hawajampokea Bwana YESU na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake, wametabiriwa kuwa miongoni mwa watakaohukumiwa katika hukumu ya milele. Je umeokoka?..umebatizwa katika ubatizo sahihi?.. umejazwa Roho Mtakatifu?.

Kama bado unangoja nini?… Ni heri ukafanya maamuzi leo ya kubadili maisha yako.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KUZIMU ni mahali pa namna gani, Je! huko wanaishi watu wakifa na kwenda kupata mateso au ni vinginevyo?

UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.

UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.

MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE.

Kuna ufufuo wa aina ngapi?

Rudi Nyumbani

Print this post

NIFANYE NINI NIMSHINDE SHETANI?

1) WOKOVU: 

Hilo ndio jambo la kwanza. Kamwe huwezi kumshinda shetani ikiwa upo nje ya Kristo, Ndicho kilichowakuta wale wana wa Skewa, walipotaka kutoa pepo kwa jina la Yesu. Lakini Yule pepo akawaambia Yesu namjua, na Paulo namfahamu, lakini je ninyi ni akina nani?

Matendo 19:13  Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.

14  Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo.

15  Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? 16  Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.

Wokovu, ni Kristo ndani yako, na kwa huo nguvu za adui zote huyeyuka mara moja. Mtu aliyempokea Yesu, shetani kamwe hamwezi, kwasababu anamwona Kristo ndani yake.

2) MAOMBI: huharibu mipango ya ibilisi.

Unaweza ukawa umeokoka, lakini shetani akapata nguvu za kukusumbua kwa majaribu, kwasababu unashindwa kutumiza baadhi ya wajibu wako kwa mwamini, Yesu alisema..

Mathayo 26:41  Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.

Yesu ijapokuwa alikuwa ni mkamilifu hana dhambi, alijaribiwa na adui, wewe ni nani usikutane na hayo? Usipokuwa mwombaji, uvivu ukakumeza, unaona shida kuomba kila siku, kuhudhuria mikesha ujue tayari upo majaribuni. Hata kama utajiona upo sawa, fahamu tu hapo ulipo kuna eneo Fulani adui anakusumbua, utakuja kugundua pindi utakapoanza kuwa mwombaji. Na ndio maana maisha ya wokovu hayatengwi na maombi. Shetani akimwangalia mwombaji anaona moto umemzunguka mkali, hawezi jiamulia tu kufanya analotaka kwake.

3) KUBALI KUWA MJINGA: Utamweka chini shetani.

Warumi 16:19  Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. 20  Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]

Hapo anasema tuwe wajinga katika mambo mabaya. Ni nafasi kubwa kwa Mungu kumweka shetani chini ya miguu yetu. Kwamfano, unapokuwa hujui kuhusu mitindo mipya ya kidunia, sio mfuatiliaji wa miziki ya kidunia, muvi mpya mpya zilizotoka duniani, yaani kwa ufupi unapitwa na mambo ya kidunia yasiyokuwa na maana kwako, kinyume chake, unakuwa na ujuzi na hekima katika mambo ya rohoni jua hapo umemshinda shetani kwa sehemu kubwa. Hana kitu kwako, kwasababu bidhaa zake, huna mpango nazo, hununui chochote kwake.  Kuipenda dunia ni kuwa adui wa Mungu, na rafiki wa shetani.

4) WEKA NENO LA MUNGU NDANI: Utamfukuza shetani.

Kuweka Neno sio, kukariri vifungu vingi vya biblia, hapana, bali ni kufahamu “ukweli” (ufunuo)  wa kila Neno unaloliweka moyoni mwako. Pale jangwani, Yesu alipokutana na shetani, alimjaribu kwa Neno hilo hilo,lakini Yesu akamwambia kweli yote ipoje.

Mathayo 4:6  akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 7  Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Ni muhimu ukalifahamu Neno la Mungu katika kweli yake, na hiyo huchangiwa na kufundishwa kwa ufasaha Neno la Mungu na waalimu, kwasababu Roho Mtakatifu atasema na wewe kupitia wao. Lakini pia kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya moja kwa moja kukufundisha. Vinginevyo adui atakudanganya sana, hususani kupitia manabii wa uongo, kwasababu hulijui Neno vema.

 5) LITII NENO: Utaweza yastamili majaribu yake yote.

Kulifahamu Neno, na kuijua kweli, ni jambo muhimu lakini bado shetani anaweza pata mianya ya kukunasa endapo hutaweza kulitii Neno. Penda utakatifu, penda kutendea kazi kile unachofundishwa. Yesu alisema, wapo watu wasikiao tu, lakini wapo wasikiao na kuyatendea kazi. Wote hujaribiwa kwa pepo, mafuriko na mvua za shetani. Sasa Yule aliyejijenga  juu ya fundisho tu, na sio kutendea kazi fundisho, ndio huyo anayechukuliwa na mafuriko.

Mathayo 7:26  Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Mateso mengine huwapata watu kwasababu ya dhambi. Kuishi maisha matakatifu, humnyima adui mlango wa kukushambulia kwa namna yoyote. Liishi Neno.

6) HUBIRI NENO: Utamwangusha adui kutoka juu.

Watu wengi hudharau ushuhudiaji. Tunapokuwa na moyo mmoja wa kuitenda kazi ya Mungu, adui hawezi kukaa juu ya anga hili, kutupinga. Tunalisoma wapi hilo? Utakumbuka wakati ule Bwana alipowatuma wanafunzi  wake wawili wawili kuhubiri, waliporudi kwa furaha, huku wakimwambia Bwana  hata mapepo yanawatii. Yesu akawaambia nalimwona shetani akianguka kutoka juu kama umeme. Kuonyesha kuwa kitendo cha wao kuhubiri adui alikuwa anaporomoka kwa kasi sana.

Mathayo 10:17  Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18  Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.

Hivyo ukizingatia mambo  hayo sita (6), Utakuwa sio tu umemdhibiti adui kila Nyanja, bali pia umemteka. Ni wajibu wako mimi na wewe kuboresha mahali ambapo hapako sawa, ili kwa pamoja tukaujenge ufalme wa Mungu na kuziangusha kazi za shetani.

Yakobo 4:7  Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ZIFAHAMU KAZI KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.

USIWE ADUI WA BWANA

Rudi Nyumbani

Print this post

Mungu anaketi katikati ya sifa?

Swali: Kwa namna gani Mungu anaketi katikati ya sifa?


Jibu: Biblia haisemi “Bwana Mungu anaketi katikati ya sifa”…bali inasema “Mungu anaketi juu ya sifa za Israeli”.

Zaburi 22:3 “Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.

4 Baba zetu walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe ukawaokoa”

Ili tuelewe vizuri ni kwa namna gani Mungu anaketi juu ya sifa za watu wake, kwanza tusome andiko lifuatalo…

Mathayo 6:10 “Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni”.

Kwa mantiki ya andiko hilo, tunona kuwa kumbe mbinguni mapenzi ya Mungu yanaendelea kufanyika, na hivyo duniani pia yanapaswa yafanyike kama yanavyofanyika huko juu…

Sasa moja ya mapenzi ya Mungu yanayofanyika mbinguni ni SIFA, ambazo MALAIKA watakatifu WANAMPA MUNGU usiku na mchana.

Na ndio maana maandiko yanasema katika 1Samweli 4:4, 2Samweli 6:2, Zaburi 80:1, Zaburi 99:1, na Isaya 37:16 kuwa Mungu ANAKETI JUU YA MAKERUBI… Na kazi ya Makerubi si nyingine Zaidi ya KUMSIFU MUNGU, na KUMPA UTUKUFU usiku na mchana, soma Ezekieli 10:18 na Ezekieli 11:22.

Na ni wapi katika biblia panapoonyesha kuwa kiti cha Enzi cha Mungu kipo juu ya makerubi, na si chini??…soma Ezekieli 1:26 na Ezekieli 10:20.

Kwahiyo kama mbinguni wanavyompa Mungu utukufu, na kwamba Mungu anaketi juu ya yao wampao sifa, hali kadhalika na duniani, Mungu anaketi juu ya sifa za watu wake! Sawasawa na hilo andiko la Zaburi 22:3.

Zaburi 22:3 “Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli”.

Hivyo tunapompa Mungu sifa, basi tunakamilisha Enzi yake katikati yetu, na hivyo Mungu anashuka. Na ibada ni lazima iwe na sifa,..Sifa ni kiungo cha muhimu sana katika kuuvuta uwepo wa Mungu, na hatumsifu tu Mungu kwasababu katuambia tumsifu….Lakini tunamsifu kwasababu AMESTAHILI!!.

Kitendo cha kumtoa mwanae kwaajili yetu sisi ambao tulikuwa hatustahili, ni Dhahiri kuwa ANASTAHILI SIFA ZETU, kitendo cha kuendelea kutupa uzima na ulinzi kila siku, hakika AMESTAHILI.

Bwana atusaidie kila siku tuone sababu za kumsifu yeye.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

ANGALIA USIJE UKANG’OA NGANO KATIKATI YA MAGUGU.

KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?

NAYE ALIKUWA HANA BUDI KUPITA KATIKATI YA SAMARIA.

Sifa ni nini?

Rudi Nyumbani

Print this post

Bwana YESU alibatizwa na umri gani?

Jibu: Umri kamili ambao Bwana YESU alikuwa nao wakati anabatizwa na Yohana katika mto Yordani, ni miaka thelathini (30).

Tunalithibitisha hilo katika Luka 3:21-23..

Luka 3:21 “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;

22  Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.

23  Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, ALIKUWA AMEPATA UMRI WAKE KAMA MIAKA THELATHINI”

Sasa kwanini Bwana Yesu abatizwe ukubwani na si utotoni?…Jibu rahisi ni kwamba alikuwa anatupa kielelezo, kwamba mwamini anapaswa abatizwe wakati ambao yeye mwenyewe kajitambua na kuona sababu zote za kubatizwa kwa hiari yake mwenyewe na si kwa kuamuliwa.

Kwa uthibitisho huo basi ni wazi kuwa “ubatizo wa utotoni” si sahihi.. Huenda waliosimamia ubatizo huo walikuwa na nia njema, lakini bado Neno la Mungu litabaki kuwa lile lile, kuwa ubatizo wa utotoni sio sahihi kimaandiko, hivyo hatuna budi kuweka mitazamo yetu pembeni, na mawazo yetu, na mapokeo yetu, na kulisimamisha Neno la Mungu.

Hakuna mahali popote katika maandiko, watoto walibatizwa, au watu walibatizwa kwa maji machache… Zaidi sana maandiko yanatuonyesha watu walisafiri kwenda mpaka Ainoni alipokuwa akibatiza Yohana, kwasababu kule kulikuwa na MAJI TELE.

Yohana 3:23 “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na MAJI TELE; na watu wakamwendea, wakabatizwa”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yohana mbatizaji alibatizwa na nani?

Yeremia alikuwa na umri gani alipoitwa?

Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?

Je ni kweli miaka yetu ya kuishi ni 80 tu (kulingana na Zaburi 90:10).

MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.

Rudi Nyumbani

Print this post

Ndugu Yule anayezungumziwa kwenye 2Wakorintho 8:18 ni nani?

SWALI: Kwenye 2Wakorintho 8:18, Mtume Paulo anamtaja ndugu ambaye jina lake hajaliweka wazi. Ni kwanini afanye hivi tofauti na alivyozoea kufanya katika nyaraka zake nyingine, kuwataja aliowatuma?

 2Wakorintho 8:18 Na pamoja naye tukamtuma ndugu yule ambaye sifa zake katika Injili zimeenea makanisani mwote.19  Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nasi katika jambo la neema hii, tunayoitumikia, ili Bwana atukuzwe, ukadhihirike utayari wetu.


JIBU: Katika waraka huu, tunaona Paulo akiwaandikia kanisa la Korintho, suala la changizo kwa ajili ya watakatifu maskini waliokuwa Yerusalemu. Hivyo akawatuma pia na watatu ili kulifanikisha jambo hilo. Wa kwanza ni Tito, Ukisoma mstari wa 16-17, katika sura hiyo hiyo ya 8, anatajwa, wa pili ndio huyu ambaye sifa zake za injili zilivuma kwenye makanisa, na watatu ni ndugu mwingine ambaye pia hajatajwa jina, isipokuwa Paulo alimwita kama ‘ndugu yetu’ ambaye tunamsoma kwenye mstari wa 22

2Wakorintho 8:22  Nasi pamoja nao tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona mara nyingi katika mambo mengi kuwa ana bidii, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini kuu alilo nalo kwenu.

Watu hawa watatu ndio waliotumwa kwa ajili ya huduma hiyo ya changizo kwa wakorintho. Lakini swali huulizwa huyu ndugu wa pili ni nani hasaa?

Wengine husema ni Luka, wengine Barnaba, wengine Apolo, wengine Marko, Aristako. Kutokana na kwamba wengi wa hawa walisifika kwa usambazi injili, lakini pia walikuwa na Paulo mara nyingi kwenye huduma.

Lakini Hayo ni makisio tu, anaweza akawa miongoni mwa hawa, lakini pia asilimia kubwa anaonekana sio kabisa miongoni mwao, waliowahi kutajwa na Paulo.

Jambo la muhimu  ambalo, linalengwa hapo, kufichwa kwa jina lake. Sio kwamba Mungu anataka tumchunguze ni nani? Hapana Lakini alipenda kutuonyesha kwamba SIFA, hujitambulisha zaidi kuliko jina.

Ukichunguza hapo, utaona Paulo anasema sifa zake zimeenea kwenye “makanisa yote”. Ikiwa na maana kuanzia huko Akaya mpaka Makedonia. Alijulikana kuwa mhubiri mwenye juhudi na mwenye kuthamini injili. Na si hivyo tu, walimchagua mwenyewe kusafiri pamoja na Paulo. Hivyo Paulo kuandika waraka huo, kwa kueleza sifa zake, aliona hilo latosha tu, kumtambulisha bila hata ya jina. Kwasababu hakuna mwingine zaidi yake. Yaani kwa namna nyingine Paulo anasema, “Mpaka hapo mmeshamtambua ni nani”.

Sikuzote wanaotambulishwa kwa majina huwa ni watu wasiojulikana, au wasio na sifa za kutosha kwenye jamii husika.

Ndivyo ilivyokuwa pia kwa Yule mtu wa tatu ambaye Paulo alimwita kama “NDUGU YETU”. Kulikuwa hakuna haja ya kumtambulisha kwa jina kwasababu walikuwa wanamwona wakati wote akiwa na akina Paulo katika ziara zake na huduma. Hivyo kumtafaja tu ndugu yetu ilitosha, alijua kila mmoja alielewa ni nani aliyekuwa anazungumziwa, kwasababu mitume hawakuwa na ndugu mwingine zaidi ya huyo, aliyekuwa karibu nao.

Hata leo, Bwana anapenda sisi tutambuliwe kwa SIFA zetu, zaidi ya MAJINA yetu. Kiasi kwamba kazi itakayoonekana kwa ajili ya Kristo, itutambulishe sisi, sio sisi tuyatambulishe majina yetu katikati ya watu.

Utaona baadhi ya wahubiri wanachokifanya, ni kutumia nguvu kubwa kutangaza majina yao, na sura zao, ili wajulikane, lakini kazi zao hazitambuliki. Hilo sio lengo la mhubiri, au Mtumishi wa Mungu. Bwana wetu Yesu Kristo alipokuwa duniani, haikuwa na muda wa kujitangaza, wakati mwingine hakutaka mambo yake yadhihirishwe kiwepesi, mpaka atakapomaliza kazi yake, Na sisi pia tupende aina hii ya utumishi.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Epafrodito ni nani kwenye biblia?

Epafra ni nani katika biblia? (Wakolosai 1:7)

Je ni sawa kuukubali udhaifu kama mtume Paulo alivyojisifia kwa huo? (2Wakorintho 12:9-10)

Rudi Nyumbani

Print this post

Tafsiri ya Wakolosai 2:18 Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu,

SWALI: Nini maana ya vifungu tunavyovisoma katika Wakolosai 2:18,

 ‘Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;


JIBU: Tukianzia mistari ya juu anasema..

16  Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

17  mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. 18 Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;

Katika vifungu hivyo, Mtume Paulo anaanza kwa kuwaambia ‘mtu asiwanyang’anye thawabu yenu’. Akiwafananisha na wana-michezo ambao wanashiriki katika mashindano Fulani, ambao hujitahidi kwa kila namna kujizuia, na kujichunga ili wafanye vema katika mashindano hayo wachukue tuzo.

Sasa Paulo, anatoa angalizo, akirejea mfano wa washindani hao, yawezekana mwingine akamfanyia hila mwenzake, ili asiwe na ufanisi, kwenye michezo hiyo akashindwa kushiriki vema na kuchukua tuzo, kwamfano anaweza kumpa kinywaji Fulani ambacho kitadhoofisha uchezaji wake, au atamdanganya afanya zoezi Fulani,  ambalo anajua kabisa halina manufaa kwake, kwamfano labda mchezaji ni mwana-riadha, utaona Yule mwingine anamwambia akanyanyue vyuma vizito atakuwa mwepesi kukimbia. Kumbe kukimbia hakuhusiani na misuli mikubwa bali pumzi.

Vivyo hivyo Paulo aliona kuwa kuna waalimu wa uongo, viongozi wa uongo,watakaozuka, kuwadanganya watu waiache njia sahihi, ya kukubaliwa na Mungu. Na ndio hapo anataja  mambo matatu ambayo watakuwa nayo;

Jambo la kwanza,

Watachukua thawabu yao kwa kunyenyekea kwa mapenzi yao wenyewe tu,

Kunyenyekea sio kubaya, ni tunda la Roho Mtakatifu ndani ya mtu, na wakristo wote, tunasukumwa katika unyenyekevu. Lakini angalia hapo anasema kunyenyekea KWA MAPENZI YAKE MWENYEWE. Maana yake, ni kuwa hanyenyekei kwa mapenzi ya Mungu, bali yake. Na hiyo ni mbaya, kwasababu watu wa kidini leo hii ndio kanuni yao, hubuni njia zao za kumwabudu Mungu, na hiyo huwavutia watu wengi, waone kama ni Mungu kweli anaabudiwa, kwa unyenyekevu na heshima, nao wanaingia kwenye mkondo huo. Wanasahau kuwa ibada lazima ifanyike kwanza katika Roho na Kweli.

Mambo kama kusujudia, kuvaa mavazi Fulani meupe, kutawadha mwili, kuvua viatu katika nyumba za ibada, kuomba kwa sauti ya kuvuta sana, ya upole, huku umeinamisha kichwa chini, unaibusu biblia. Hudhanikuwa kuwa ndio hicho Mungu anakitaka,  Lakini ndani, kinywa chake kina matusi, akitoka hapo anakwenda kuishi maisha kishirikina, na ulevi.  Huo ni udanganyifu mkubwa sana.

Ndicho Paulo alichokiona kwa kanisa la Kolosai, kulitokea watu wanawaambia usile kambale ni chukizo kwa Mungu, shika siku  ya sabato, inatosha.. Yote hayo yakifanyika kimwili. Lakini wasifundishe kwamba unyenyekevu wa ki-Mungu hutoka rohoni, ukisukumwa na neema katika  Roho Mtakatifu, Ambapo mtu kupaswa kukubali wokovu kwanza, na kutii kwa kumfuata Kristo anayeweza kumfanya mtu kiumbe kipya, na sio jambo la kufanya kimwili tu, akidhani atampendeza Mungu.

Jambo la pili

 wanaweza kuwanyang’anya thawabu yao kwa mafundisho ya kuabudu malaika.

Tangu zamani, kulikuwa na watu waliowaweka malaika katika nafasi ya Mungu. Na kuvuka ile mipaka ya kutuhudumia tu sisi  (Waebrania 1:14). Hivyo ikiwa mtu alikuwa na karama Fulani ya maono, ambapo mengine huletwa kwa mikono ya malaika, tunaliona hilo mara nyingi tangu Musa, na wana wa Israeli jangwani, pamoja na mitume mpaka Yohana kule Patmo. Mungu aliwatumia malaika kwa sehemu kubwa kutufikishia sisi jumbe zake, kwasababu waliwekwa kutuhudumia sisi.

Lakini dini na imani zikazuka kuanzia hapo, kwa baadhi ya watu wakaanza kuwafanyia ibada, jambo ambalo ni chukizo kwa Bwana. Hata leo utaona zipo sala za malaika na watakatifu kuwataka wawaombee. Au wawasaidie vitani. Ikiwa wewe ni mtoto wa Mungu umeokoka, kuwa makini na ibada hizo, taabu yako kwa Mungu yaweza kuwa bure, kwasababu unamudhi Mungu. Ibada za namna hiyo hazina tofauti na ibada za majini. Usiabudu mwanadamu, wala kiumbe chochote kilicho mbinguni wala duniani.

Jambo la tatu

Na mwisho anasema wakijivuna bure kwa akili zao za mwili.

Kujivuna, maana yake kusifia vitu vya mwilini mfano vipaji vyao, wengine ujuzi wa kuongea vizuri, na kupangalia maneno, werevu, elimu za falsafa, mambo ambayo Paulo aliyaona, yakiwavuta wengi, na kuacha njia kamilifu ya Kristo iliyo katika neema, upendo,  Imani na nguvu za Mungu. (2Wakorintho 11:18-20).

Injili inabadilishwa inakuwa vichekesho, na kanuni za ki-ujasiriamali,

Hata leo mimi na wewe ni kuwa makini, bidii yako katika Kristo isichukuliwe na udini, bali Neno, isichukuliwe na maono na karama, na ibada za malaika bali Mungu, isichukuliwe na falsafa za kibinadamu, na mwonekano, bali, Roho Mtakatifu na kweli, katika neema.

mtu asichukue taji lako

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 2)

Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

Rudi Nyumbani

Print this post

Malimbuko ya Akaya maana yake nini? (1Wakorintho 16:15).

Swali: Haya malimbuko ya Akaya tunayoyasoma katika 1Wakorintho 16:15 yalikuwaje?

Jibu: Turejee..

1Wakorintho 16:15 “Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa STEFANA kwamba ni MALIMBUKO YA AKAYA, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu)”.

“Akaya” inayotajwa hapo si mtu, bali ni eneo/mji uliopo maeneno ya Ugiriki kwa sasa. Mji huu umetajwa pia katika Matendo 18:12, Matendo 19:21, 2Wakorintho 1:1, 1Wathesalonike 1:7-8 na Yuda 1:6.

Mji huu wa Akaya, ulikuwa ni moja ya miji ambayo Mtume Paulo alipita kuhubiri injili ya BWANA YESU. Na mmoja wa watu wa kwanza kabisa kumpokea Bwana YESU na kuokoka katika Mji huo ni huyu mtu aliyeitwa STEFANA pamoja na nyumba yake yote.

Hawa ndio walikuwa watu wa kwanza kabisa kuipokea injili katika mji huo, na baadaye wakaongezeka wengine wengi. Hiyo ndio maana ya Malimbuko iliyotajwa hapo… Sio malimbuko ya mazao ile inayotajwa katika Kutoka 22:29, bali inayomaanisha “wa kwanza kupokea injili”.. kwamaana maana tu ya malimbuko ni “kuzaliwa kwa kwanza”, hivyo hawa watu walikuwa ni wa kwanza kuzaliwa katika injili katika mji huo wa Akaya.

Lakini sifa nyingine ya kipekee aliyokuwa nayo huyu Stefana pamoja na nyumba yake yote ni roho ya UKARIMU, ambayo waliionyesha sana kwa Paulo na watumishi wengine waliokwenda kuhubiri injili katika miji hiyo, walikuwa tayari kutoa vya kwao ili kuwatunza watumishi wa Mungu.

Na kwa tabia hiyo, ndiyo Mtume Paulo kwa kuongozwa na roho anawaagiza watu wa Korintho pamoja na sisi kwa ujumla tuige tabia kama hiyo na pia tuwatii sana watu wanaojitoa kwaajili ya kuishika mkono kazi ya Mungu, na pia tuwe tayari kushirikiana nao..

1Wakorintho 16:14 “Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.

15  Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni MALIMBUKO YA AKAYA, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu);

16  WATIINI WATU KAMA HAWA, NA KILA MTU AFANYAYE KAZI PAMOJA NAO, NA KUJITAABISHA.

17  Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu”

Bwana atubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

SADAKA YA MALIMBUKO.

INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?

Yerusalemu ni nini?

HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.

IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.

Rudi Nyumbani

Print this post

Ijapokuwa amekufa, angali akinena(Waebrania 11:4)

SWALI: Maandiko yanaposema Habili ijapokuwa amekufa angali akinena, je! Ananenaje, wakati yeye ni marehemu. Je! Hiyo inamaana wazee wetu wa zamani wanaweza kunena na sisi?

Waebrani 11:4  Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena


JIBU: Kibiblia ni kweli kabisa watakatifu waliokufa kale hunena nasi. Lakini kunena kwao ni tofauti na huku kunakodhaniwa, kwamba mzimu unakutokea kwenye ndoto, au unasikia sauti ya petro makaburini ikizungumza na wewe,  Hapana, ukiona hivyo ujue huzungumzi na huyo mtu, bali ni pepo.

Sasa watakatifu waliokufa wanazungumzaje na sisi?

Ni kwa ushuhuda waliouacha. Maisha yao na maagizo yao, ndio huzungumza nasi, sikuzote, kana kwamba tupo nao sasa, kwa mafundisho yao yaliyopo  mpaka sasa kana kwamba tunawaona wenyewe kumbe wamekufa.

Ndio maana ile habari ya Yule tajiri wa Lazaro, tunaambiwa alipofika kule kuzimu akaomba mtu atolewe kwa wafu awahubirie injili, akakataliwa, kuonyesha kuwa hakuna mtu aliyekufa mwenye uwezo wa  kuja tena kuzungumza na sisi, nafasi hiyo haipo kwao. Lakini waliambiwa WANAO MUSA NA MANABII, WAWASIKILIZE.

Luka 16:29  Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

Maana yake ni kuwa sio kwamba Musa kweli alikuwepo duniani, au manabii wa kale kama Isaya walikuwa duniani kwa wakati huo, anaambiwa hayo maneno. Lakini shuhuda zao na mahubiri yao, huwawakilisha wao. Tunaweza kusema “ijapokuwa wamekufa wangali wakinena”

Ndivyo ilivyo kwa Habili, ijapokuwa aliuliwa na ndugu yake, lakini IMANI yake inasema nasi mpaka leo. Mitume wa Kristo ijapokuwa hawapo duniani lakini sauti zao tunazisikia hadi sasa.

Lakini pia kuna mahali pengine biblia inasema damu ya Yesu hunena mema kuliko ya Habili (Waebrania 12:24). Kufahamu kwa kina damu ya mtakatifu  hunenaje? Pitia somo hili. >>> DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

KUOTA MTU AMEKUFA/NDUGU AMEKUFA.

ALIPOKUWA ANGALI MBALI, BABA YAKE ALIMWONA.

Rudi Nyumbani

Print this post