Mungu aliupenda ulimwengu kwasababu asili yake upendo, Maandiko yanasema yeye ni UPENDO.
1Yohana 4:16 Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
Lakini ifahamike kuwa aliposema ameupenda ulimwengu haimaanishi kuwa amependa kila kitu ulimwenguni, ikiwemo mifumo ya ulimwengu huu, hapana, kazi nyingi za ulimwengu ni mbovu, na hivyo hawezi kuzipenda, tena alizikemea (Yohana 7:7), bali aliwapenda walio-ulimwenguni (yaani sisi wanadamu). Bila kujali jinsia zetu, rangi zetu, jamii zetu, mataifa yetu, waovu, na wema, wote alitupenda sawa.
Ni upendo uliodhihirika katika hali yetu ya kupotea. Mahali ambapo tulikuwa hatuna tumaini lolote, hatuna uzima wowote wa milele ndani yetu, tumeteswa na ibilisi, yeye mwenyewe kwa mapenzi yake akatuhurumia, ndipo akatujia tena ili kutuokoa katika hali ya kifo na mauti tuliyokuwa nayo bure.
Na hivyo hakutupenda kwa mdogo tu, bali aliingia gharama. Na gharama yenyewe ni kumtoa mwanawe wa pekee Yesu Kristo, kuja katika mwili wa kibinadamu ili afe kama fidia ya dhambi zetu, ili sisi tupone kwa kifo chake yeye. Tupokee uzima wa milele.
Maana yake mtu yeyote ambaye ataukubali wokovu huo, ulioletwa kwa kufa na kufufuka kwake, basi uzima wa milele unaingia ndani yake. Ndio maana ya hilo andiko;
Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Lakini ijapokuwa uzima umeletwa kwetu bure kwa gharama kubwa, wapo wengine hawaukubali, wakidhani kuwa wataweza kuushinda huu ulimwengu kwa nguvu zao, au kwa dini zao, au kwa matendo yao wenyewe.
Yohana 3:19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
Je! Umeupokea uzima huu wa milele?. Ikiwa bado basi fungua moyo wako sasa, mwamini Yesu, mpokee kama ‘Bwana’ kwako, umfuate kwa moyo wako wote, uokoke, dunia hii ni ya kitambo tu, vilevile kesho yako huijui kama utakuwa hai au maiti. Ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi fungua hapa kwa msaada wa mwongozo wa sala ya wokovu >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Ulimwengu wa Roho ni nini? Na mtu anawezaje kuwa wa rohoni?
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
Maisha ya wokovu, hayatoshi tu kusema nimeokoka, halafu basi, nitamwabudu Mungu kivyangu. Hapana, Mungu hajaagiza hivyo, na kuna hatari kubwa ya kuenenda kwa namna hiyo, tutaona ni kwanini?
Ni sawa na mwanafunzi anayesema mimi sihitaji shule, nitajisomea tu nyumbani peke yangu, nitapata elimu yote, na maarifa yote kupitia vitabu na tafiti zangu. Ukweli ni kwamba si rahisi akipate anachokitafuta, kwasababu shuleni wapo waalimu atawahitaji wamfundishe vitu asivyovijua, atauliza maswali pale ambapo hajaelewa, wapo wanafunzi wenzake atajadiliana nao, zipo nidhamu atajifunza, ipo hamasa ataipata, tofauti na akiwa peke yake, na mambo mengine kadha wa kadha, .
Vivyo hivyo na maisha ya rohoni. Wokovu ni mtu binafsi, lakini kusimama katika wokovu na kuendelea mbele na kukua kunahitaji kanisa. Mungu aliagiza hivyo akasema, tusiache kukusanyika pamoja.
Waebrania 10:25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia
Akasema pia, heri walio wawili kuliko mmoja, kwasababu katika wingi, kuna kutiana nguvu ya kuendelea mbele.
Mhubiri 4:9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?
12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.
Mkusanyikapo pamoja mtatiana moyo, mtaomba pamoja n.k.
Vilevile Kanisa la kwanza lilikuwa na desturi ya kukusanyika pamoja, kusikiliza fundisho la mitume, kumsifu Mungu na kumega mkate, nyumba-nyumba kwa nyuma pamoja na Kutambuana.
Matendo 2:46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
Lakini pia kusaidiana kimahitaji, Kutiana moyo (Warumi 1:12), Kuonyana (Wagalatia 5:13)
Lakini pia kufaidiana kwa karama za Roho Mtakatifu. Yaana kuruhusu uweza wa Mungu kutenda kazi katikati ya waamini.(Waefeso 4:11, 1Wakorintho 12) Mambo ambayo huwezi kuyapata ukiwa peke yako.
Hivyo huwezi kutenganisha maisha ya wokovu na kanisa. Kila mwamini ni lazima awe na mkusanyiko, kwa uthabiti wa maisha yake ya rohoni. Usiabudu kivyako vyako.
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
WALA TUSIACHE KUKUSANYIKA PAMOJA
FUNDISHA NENO KANISANI NA NYUMBANI.
(Opens in a new browser tab)WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; NAO WATAMWOMBOLEZE
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?(Opens in a new browser tab(Opens in a new browser tab)
Rudi Nyumbani
Neno hilo utalisoma katika ule utabiri wa Yakobo kwa watoto wake, alipokuwa anawabariki, na alipofikia kwa Dani, yeye alimfananisha na Bafe. Swali ni je Huyu bafe ni nani?
Tusome
Mwanzo 49:17 Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali. 18 Wokovu wako nimeungoja, Ee Bwana.
Bafe ni nyoka aina ya kifutu. Hivyo Yakobo alimwona Dani kama nyoka, ambaye ijapokuwa maisha yake ni ya mavumbi, lakini ameng’ata farasi kisigo hatimaye farasi Yule akashindwa kuendelea na hapo hapo mpanda farasi naye akashindwa kuvifikia vita vyake.
Akimaanisha kuwa Dani anaweza dharaulika, lakini ana wokovu mkuu kwa watu wake, pale ambapo wangetarajia mpanda farasi arushiwe mikuki na majeshi ya watu, au avamiwe kijeshi, yeye anauma tu kisigo cha farasi wao, sumu inaingia na nguvu yao inaisha.
Ni kufunua kuwa kila mmoja wetu amepewa karama yake tofauti na mwingine, na kama ikitumika kifasaha huweza kumweka adui chini, sawa tu na zile karama ambazo huonekana zina heshima mbele ya macho ya watu kama vile, utume, uchungaji, uinjilisti n.k.
Kamwe usidharau karama yako, kumbuka sikuzote vile visivyoonekana kwa urahisi ndio huwa vina umuhimu mkubwa. Unaweza usiwe mguu au mkono, lakini ukawa moyo, au figo, vilivyojificha ndani, ambavyo tunajua uthamani wake ulivyo.
Halikadhalika, katika Baraka zile, Yuda aliitwa simba, Isakari aliitwa punda, Dani aliitwa Bafe, Lakini wote waliitwa Israeli. Taifa la Mungu.
Je ! unaitumia vema karama yako, au umeidharau? Na kutamani za wengine?
Kwa msaada wa jinsi ya kuitambua karama yako fungua hapa >>> NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.
UFUNUO: Mlango wa 6(Opens in a new browser tab)
Maana ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake(Opens in a new browser tab)
(Opens in a new browser tab)MIHURI SABA(Opens in a new browser tab)
Katika biblia zipo aina mbalimbali za kumsifu Bwana, lakini kuna kuu saba ambazo zilitambuliwa na wayahudi kwa wakati wote. Hivyo ni vema kuzifahamu ili wigo wako uwe mpana zaidi katika eneo hili la sifa. Kwasababu ndio huduma kuu tuliyonayo duniani kwa Mungu wetu. Kumbuka chakula chetu ni Neno, lakini chakula cha Mungu wetu ni Sifa zetu. Hivyo ni lazima tujue tunamsifuje yeye kiufasaha kwa jinsi apendavyo.
Hizi ni aina saba za sifa.
Hii ni aina ya kumsifu Mungu ambayo, mwimbaji hujidai, hujigamba mbele za Mungu wake kwa kuuhusisha mwili wake, yaweza kuwa kuruka kuruka, au kucheza.
Agizo hilo lipo katika Zaburi 149:3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie.
Ndio lile Daudi na Israeli wote walilolifanya walipokuwa wanalileta sanduku la Bwana Yerusalemu,
2Samweli 6:14 Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
15 Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la Bwana kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta.
16 Ikawa, sanduku la Bwana lilipoingia mji wa Daudi Mikali, binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akiruka-ruka na kucheza mbele za Bwana; akamdharau moyoni mwake.
Hivyo na wewe kama mtu uliyeokolewa na Kristo, kujidai kwa ujasiri wote mbele ya Mungu wako usijizuie, angalizo tu ni kwamba usifanye kidunia, kana kwamba unacheza dansi, huku moyoni mwako hakuna ibada. Hiyo sio sawa, lakini kumwimbia Mungu kwa kucheza hakuna kosa lolote ikiwa ni jambo la kububujika moja kwa moja kutoka moyoni mwako.
Hii ni aina ya kumsifu Mungu kwa kuinua mikono juu, Kama ishara ya kutambua tegemeo lako kwake, kama mtoto mdogo kwa mzazi wako anapomlilia. Na kuonyesha upendo wako wa dhati kwa Mungu wako.
Zaburi 63: 3 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. 4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Kama mtakatifu jizoeze mara nyingi, kunyanyua mikono yako juu wakati unamwabudu Mungu, au wakati mwingine unapoomba. Binafsi, nimeona tofauti kubwa sana, niinuapo mikono yangu, pindi niombapo au nisifupo, najikuta nazama rohoni kwa haraka sana, zaidi ya napoweka mikono yangu chini. Kumbuka ile habari ya Musa, alipoinua mikono juu, Israeli ilishinda, lakini alipoweka mikono chini, Waamaleki walishinda. (Kutoka 17:11) Hivyo jifunze sana, kuiinua mikono yako juu, katika ibada zako.
Hii ni aina ya kumsifu Mungu kwa kumbariki Mungu, lakini kwa kuonyesha heshima kubwa kama mfalme, kujishusha chini, kusujudu au kupiga magoti, kuonyesha yeye ni mkuu sana wa kuogofya zaidi ya wafalme wote na wakuu wote ulimwenguni.
Zaburi 5:7 Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako, Nitaingia nyumbani mwako; Na kusujudu kwa kicho, Nikilielekea hekalu lako takatifu.
Kama mwamini, sifa zako zisiwe za mdomo tu wakati wote, jifunze kupiga magoti, au kusujudu ni ishara ya unyenyekevu wa hali ya juu. Fanya hivyo nyakati za sifa, nyakati za maombi.
Aina ya kusifu moyoni mwako, kwa namna isiyo na maandalizi Fulani maalumu, mfano wa kwaya, ni nyimbo ambazo zitainuka katikati ya mapito yako fulani, wakati mwingine unapopitia kutendewa mema mengi na Mungu, na hapo ghafla tu moyoni mwako unasikia kumsifu Mungu, kumpa utukufu.
Kwamfano Daudi alipokuwa anapitia magumu,au anashindaniwa na Mungu, akimtafakari Mungu, mara anaachilia kinywa chake, Mungu anaanza kububujisha nyimbo mpya ulimini mwake.
Mfano mwingine wa sifa kama hizi, ni pale Mungu alipowavusha wana wa Israeli, bahari ya Shamu, na kuona maadui zao wamefunikwa na habari, ndipo Israeli wote, pamoja na Miriamu na wanawake wakasimama kumwimbia Mungu nyimbo za Furaha (Kutoka 15).
Mfano mwingine ni pale Mariamu alipomtembelea Elizabeti, na kutolewa unabii kuwa atamzaa Masihi, alishangalia na ghafla akafungua kinywa chake kwa wimbo, kumsifu Mungu kwa namna hii, (Luka 1:46-56)
Hivyo kila mkristo, katika majira yote, vipindi vyote, viwe vyepesi, viwe vingine, hana budi kutafakari na kufungua kinywa chake kumsifu Mungu kwa aina hii ya sifa ya Tehillah. Ni muhimu sana, na inampendeza, Mungu, hii haina maandalizi, haina mpangilio maalumu, hutoka moyoni mwako, kwasababu Fulani Mungu alizokuonekania.
Mungu aliwaagiza pia watu wake, wamwimbie si kwa vinywa vyao tu na makofi, lakini pia pamoja na kuchanganya zana mbalimbali za muziki.
Zaburi 150:3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; 5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.
Ni wazi kuwa kuchanganya ala mbalimbali,kama vile gitaa, vinanda, filipi, tarumbeta, ngoma, zeze, marumba, n.k. Katika kumwimbia Mungu, huongeza ladha na hisia njema katika kumsifu, na hivyo hupendeza sana machoni pake. Wapo watu hawaamini katika matumizi ya vyombo. Lakini maandiko yanatuagiza tumsifu Mungu kwa hivyo.
Aina hii ya sifa, ni kwa kupaza sauti yako juu sana kwa Mungu. Hii Huonyesha ujasiri wa Mungu unayemwabudu, na kuutangazia umati na ulimwengu kuwa yupo Mungu mahali hapo anayeabudiwa.
Zaburi 47:1 Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.
Sifa hizi zina nguvu sana, ndio zile ambazo ziliangusha kuta za Yeriko. Wana wa Israeli walipoambiwa wapaze sauti zao kwa Mungu. Zile sauti hayakuwa makelele tu, bali zilikuwa ni sauti za kumtukuza Mungu.(Yoshua 6:20).
Tumwimbiapo Mungu, hatupaswi tuwe kama mabubu, au tuimbe kinyonge, au kwa kutegea-tegea. Mungu anajivunia sana watu wale wanaomwabudu kwa ujasiri, kwa kufumbua vinywa vyao na kupaza sauti zao kwa nguvu kumwadhimisha yeye.
Ni aina ya sifa inayofanana na ile ‘Yadah’,ya kumwinulia Mungu mikono kumwimbia. Isipokuwa hii, ni kumwadhimisha Mungu, kwa matendo ambayo bado hujayaona kwa macho. Kutambua uweza wa Mungu, hata kama huoni matokeo yoyote, na kumshukuru katika hayo. Hata pale ambapo hujisikii. .
Mfano ya sifa hizi, ni labda wewe ni mgonjwa, daktari amekuambia una siku chache za kuishi, ukiangalia umeombewa mara nyingi hakuna matokeo yoyote, lakini unakumbuka Neno la Bwana linalosema ‘kwa kupigwa kwake sisi tumepona’. Unaanza kufurahi, ukimwinulia mikono Mungu na kumshukuru ukisema asante, Bwana kwa kuniponya, huku ukimsifu katika hali yako hiyo hiyo ya udhaifu.
Sifa hizo ni muhimu sana kwetu, na zinaugusa moyo wa Mungu kwa namna ya kipekee, Kwasababu kamwe haziwezi kuwa na unafiki ndani yake.
Hizi zinapaswa ziwepo ndani yetu wakati wote. Unakumbuka ahadi za Mungu ambazo bado huoni zimetimia, unamsifu Mungu sana kwa furaha kana kwamba umekwisha vipata vyote sasa, umetafuta kazi umekosa, unamsifu Mungu kana kwamba umepokea ripoti ya kuajiriwa.
Hizi ndio aina saba za sifa, ambazo ukiziachilia katika maeneo yako yote ya kiibada. Utampendeza Mungu sana. Lakini pia zinapaswa ziwe katika Roho na Kweli, tafsiri yake, ni sharti mtu umsifuye Mungu uwe umeokoka, umeshatambua kazi ya Kristo ya ukombozi kwenye maisha yako ipoje. Tayari wewe ni mfuasi wa Kristo. Ndipo sifa hizo zitakubalika. Vinginevyo haziwezi kumpendeza Mungu hata kama utazifanya zote kwa ufasaha.
Ikiwa bado hujaokoka, na upo tayari kufanya hivyo leo. Basi kwa msaada unaweza fungua hapa kwa msaada wa mwongozo huo wa kumkaribisha Yesu maishani mwako.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Agano la kale lina jumla ya mistari 23,145, na mistari 7957 kwenye agano jipya. Kuleta jumla ya mistari 31,102 kwa biblia nzima.
Ambapo tukileta katika eneo la wastani ni sawa na kusema biblia ina mistari 26 kwa sura.
Washirikishekishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Biblia ina sura na milango mingapi?
Je kumwimbia Mungu kwa kucheza ni sahihi kibiblia?
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
Rudi Nyumbani
Jibu: Kuna mambo makuu mawili ya kuzingatia katika kulitafakari hili.
1. KWANINI UNACHEZA
2. NACHEZAJE
Tutazame moja baada ya lingine.
1. KWANINI UNACHEZA!
Tafakari umempa mtoto kitu anachokipenda, au mwanamichezo kashinda mchezo wake, au mwanafunzi kapata taarifa za kufaulu mitihani yake, huwa ipo furaha ambayo inaweza kumpelekea kuruka ruka kwa shangwe.
Sasa furaha ya namna hiyo inayompelekea kuruka rukwa kwa shangwe haina nia ya Maonyesho, au majivuno, bali ni mwitikio wa jambo jema linaloendelea au lililotokea.
Na kadhalika tunapofanyiwa jambo na MUNGU (Ambaye kwaasili huwa haishi matukio wala miujiza) zipo hisia zinazoambatana na shangwe, ambapo shangwe hiyo inaweza kuambatana na kuimba kwa kuruka ruka kama ndama!.
Raha ya namna hii inayoambatana na kuruka ruka na kucheza cheza tutaipata Zaidi siku ile tutakapomaliza mwendo, na kutangaziwa na BWANA KWAMBA TUMESHINDA!!, NA HIVYO TUNAUINGIA ULE MJI MTAKATIFU, NA KUKAA HUKO MILELE… Hapo baba, au mama hata kama hupendi kucheza utacheza tu!!.
Malaki 4:2 “Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, NA KUCHEZA-CHEZA KAMA NDAMA WA MAZIZINI”.
Sasa ikiwa kuna ahadi ya sisi kucheza cheza huko mbeleni tutakapomaliza maisha haya na kutangaziwa ushindi.. vipi vipindi vidogo vidogo ambavyo Mungu anatupa ushindi hapa duniani?.. kwamba tulikuwa tunaumwa kiwango cha kufa, sasa Bwana katuponya, ndoa zilikuwa zinayumba sasa Bwana kazisimamisha.
Watoto walikuwa wanasumbua sasa Bwana kawatengeneza, Wokovu ulikuwa huna sasa Bwana kakupa… Kwasababu kama hizo wakati mwingine shangwe inaweza kuzidi mpaka kufikia hatua ya kucheza na kuruka ruka kama ndama huku ukimwimbia Bwana. (Hapo inakuwa ni wewe na Bwana na si wewe na mtu).
Unapozitafakari hizo sababu na nyingine nyingi, hauhitaji au husubiri uambiwe umshangilie Mungu, bali hiyo hali itatoka tu yenyewe ndani yako, na wala haitakuwa na lengo la kutazamwa na watu.
2. UNACHEZAJE
Hili ni jambo la pili la kuzingatia.. UNACHEZAJE!!.. Ukiona unatafuta mtindo/style ya kucheza wakati wa Sifa, hapo kuna jambo la kutafakari!!!.. Sifa zinazozalika kwa kutafakari matendo makuu ya Mungu, hazinaga step, hazinaga kanuni maalumu, na pia zina staha!!..
Huwezi kumshangilia Bwana kwa staili za disko,..huwezi kutikisa makalio kama wafanyavyo wanenguaje wa disko..huwezi kucheza kwaito, na kushikana shikana na mwingine kama watu wa duniani wafanyavyo.. wengine wapo nusu uchi halafu wanasema wanacheza!..hiyo ni hatari sana.
Sifa za namna hiyo sio kutoka katika roho, bali na za NIA ya mwilini,..ambazo lengo lake kuu ni kutazamwa na watu na kusifiwa nao au kuwapendeza..na ndizo ambazo mkristo hapaswi kuzifanya.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba iwe katika kuabudu, au kusifu, au kuruka ruka ni lazima yote yafanyike kwa staha na kwa utukufu wa Mungu.
Wafilipi 4:8 “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je tunaruhusiwa kushirikiana na wasanii wa kidunia katika kumwimbia Mungu?
Jicho kucheza ni ishara ya nini?
NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?
Nini maana ya Shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo Ayubu 20:4
Swali: Ukaufu ni nini na Koga ni nini kama tunavyosoma katika Kumbukumbu 28:22?
Jibu: Turejee.
Kumbukumbu 28:22 “Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa UKAUFU, na kwa KOGA; navyo vitakufukuza hata uangamie”
“Ukaufu” ni ugonjwa wa mazao unaotokana na utandu (fangasi), tazama picha juu. Ugonjwa huu unaposhambulia zao la nafaka basi linapata mabaka mabaka na kisha kunyauka na mwishowe kutozalisha chochote.
Sasa hapo Bwana alikuwa anasema na watu wake Israeli (ambao ni sisi pia) kwamba tutakapomwacha Bwana na kufuata miungu mingine na kuiabudu basi tutakuwa tumefungua milango ya laana juu ya maisha yetu, kwani tutapigwa kwa magonjwa ya mwilini lakini pia mazao ya mashamba yetu yatapiwa kwa magonjwa.. na pia tutapigwa kwa misiba na majanga ya nchi.
Mfano wa magonjwa ya mwilini ni hayo yaliyotajwa hapo (Kifua kikuu, homa na kuwashwa).. na mfano wa magonjwa yatakayoshambulia mimea yetu hata tusipate chakula ni hayo yaliyotajwa hapo (Koga na UKAUFU),
Koga ni utandu mweupe unaoshambulia mimea ambao nao pia ukikamata zao la chakula, basi zao lile linadhoofika na hatimaye kufa. (Tazama picha chini).
Lakini pia mfano wa majanga nchi yatakayotupata ikiwa tutamwacha Bwana ni hayo yaliyotajwa hapo juu (hari ya moto na upanga)..Hari ya moto inayozungumziwa hapo ni vipindi vya ukame na jua kali na upanga unaozungumziwa hapo ni vita (au umwagaji damu).
Na sio kwa mambo hayo tu, bali pia kwa mambo mengine mengi yaliyotajwa hapo katika Kumbukumbu 28 na yasiyotajwa… yote yatatupata ikiwa tutamwacha BWANA MUNGU WETU, na kujitumainisha katika mambo mabaya…
Kumbukumbu 28:58 “Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, Bwana, MUNGU WAKO;
59 ndipo atakapofanya Bwana mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.
60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.
61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa”.
Lakini kinyume chake, ikiwa tutamtii Bwana MUNGU WETU, na kwenda katika njia zake, basi tutafanikiwa sana kufungua milango ya Baraka nyingi, wala hatutapatwa na hayo yote (Saswasawa na Kumbukumbu 28:1-14)
Bwana atusaidie na kutuneemesha.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MAGONJWA YAKUPATAYO MARA KWA MARA.
Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
ATAANGAMIZWA NA KUTENGWA NA WATU WAKE.
Jibu: Turejee..
Isaya 54:16 “Tazama, nimemwumba MHUNZI avukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu”
Mhunzi/ Wahunzi wanaozungumziwa katika biblia ni watu “wanaofua Vyuma, shaba, fedha au dhahabu”. Maana yake wanaviyeyusha vyuma hivyo au madini hayo na kuyaumba kwa maumbile mbalimbali kama silaha na urembo.
Tofauti ya Mhunzi na mfinyanzi, ni kwamba Mfinyanzi yeye anashughulika na udongo, anafanya kazi ya kutengeneza vyombo au zana kupitia udongo, (Soma Isaya 41:25, Isaya 64:8 na Yeremia 18:6) lakini “Mhunzi” yeye anatumia vitu vya metali kama vyuma, fedha, shaba au dhahabu kutengeneza vito au zana za kazi au silaha.
Mistari mingine katika biblia inayotaja Wahunzi (wafua vyuma/dhahabu/shaba au fedha) ni pamoja na 1Samweli 13:19, 2Wafalme 24:16, Isaya 44:12, Isaya 46:6, Yeremia 24:1, Zekaria 1:20, Matendo 19:24, na 2Timotheo 4:14.
Je umempokea BWANA YESU?. Kama bado fahamu kuwa upo katika hatari kubwa yenye mwisho mbaya, ni vyema ukafanya maamuzi leo ya kumpokea YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yako, kabla ya kumaliza muda wako wa kuishi, kwani hakuna nafasi ya pili baada ya kifo.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).
KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?
Mchuuzi ni nani? (Hosea 12:7).
Jibu: Turejee..
Mwanzo 36:15 “Hawa ndio MAJUMBE wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; JUMBE Temani, JUMBE Omari, JUMBE Sefo, JUMBE Kenazi,
16 JUMBE Kora, JUMBE Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio MAJUMBE, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada”.
Jumbe/Majumbe ni “WAKUU WA KOO” (machifu),
Majumbe walikuwa ni watu wenye heshima katika ukoo, na walijulikana sana katika nchi yote… na pia Majukumu yao yalikuwa ni kutatua migogoro ya kifamilia, na migawanyo ya ardhi kwa familia.
Katika biblia majumbe waliokuwa maarufu ni Majumbe wa wana wa Esau, (Hawa ndio waliokuwa Majumbe maarufu na wenye heshima kuliko Majumbe wa kabila nyingine za watu).. Jamii yao iliwapa heshima Majumbe hawa kiasi kwamba wakajulikana mpaka nje ya mipaka.
Kutoka 15:14 “Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika.
15 Ndipo MAJUMBE WA EDOMU wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka”.
Sehemu nyingine katika biblia zilizotaja Majumbe ni pamoja 1Nyakati 1:51-54, Esta 1:3, Esta 9:3
Lakini pamoja na kwamba “Majumbe wa Esau” walikuwa maarufu na waliojulikana sana na wenye heshima, lakini kutoka huko hakutoka “MKUU WA UZIMA (YESU KRISTO), lakini badala yake kutoka katika Ukoo mdogo sana, (wa Majumbe ya Yuda), alitoka Mwokozi wa ulimwengu, Haleluya!!..
Mathayo 2:5 “Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, HU MDOGO KAMWE KATIKA MAJUMBE WA YUDA; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli”.
Je umemwamini Bwana YESU?.. Kama bado fahamu kuwa tunaishi majira ya kurudi kwake, na ule mlango unazidi kuwa mwembamba kila siku na ile njia ya upotevuni inazidi kuwa pana kwa kadiri muda unavyozidi kwenda, hivyo usikawie kusimama katika wokovu, muda umebaki mchache sana.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.
MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.
Swali: Sifa na Lami ni nini kama tunavyosoma katika Kutoka 2:3
Jibu: Turejee..
Kutoka 2:3 “Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka SIFA NA LAMI, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto”
“Sifa” inayozungumziwa hapo sio “Utukufu” bali ni aina ya “Nta” inayopatikana/kuzalishwa na aidha mimea au mafuta. Mfano wa Nta ya mimea ni ile inayotokea katika baadhi ya mashina na miti (Tazama picha chini).
Lakini Nta ya “Sifa” ni ile inayopatikana kutoka katika mabaki ya “Makaa ya mawe” ambayo ni nyepesi kuliko Lami. (Tazama picha chini)
Na “Lami” ni Nta nzito Zaidi inayoganda ambayo kimwonekano ni nyeusi na inapatikana katika hali ya uasili au baada ya kuchujwa kwa mafuta ya petroli kiwandani.
Lami inapatikana katika uasili wake maeneo ya bahari ya chumvi (Sidimu)mpakani mwa nchi ya Israeli na Yordani..
Mwanzo 14:10 “Na bonde la Sidimu lilikuwa limejaa MASHIMO YA LAMI. Nao wafalme wa Sodoma na Gomora wakakimbia, wakaanguka huko, nao waliosalia wakakimbia milimani”
“Lami” kimwonekano ni nzito kuliko “Sifa” na rangi yake ni nyeusi kama tu “Sifa”. (Tazama picha chini).
Biblia inatabiri siku ya mwisho (ya kisasi cha Mungu) juu ya wanadamu wote watendao maasi, dunia itapigwa (kwa kuunguzwa kwa moto) na vijito na ardhi yote itakuwa Lami.
Isaya 34:8 “Maana ni siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.
9 Na vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, NA ARDHI YAKE ITAKUWA LAMI IWAKAYO”.
Sasa kufahamu kwa mapana kwanini Safina ile iliyomficha Musa ilipakwa Sifa pamoja na Lami?.. na ni ufunuo gani uliopo nyuma yake?, fungua hapa >>>>SAFINA NI NINI?
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nini maana ya Mithali 27:21 inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”
NI NINI KINATOKA KINYWANI MWA MTOTO WAKO?