Yohana 12:28-30
“28 Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja SAUTI kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.
29 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba KUMEKUWA NGURUMO; wengine walisema, Malaika amesema naye.
30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, BALI KWA AJILI YENU.”
Katika habari hii tunasoma kuwa kuna SAUTI ilitoka mbinguni ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya umati uliokuwa unamsikiliza BWANA, lakini cha kuogopesha haikuwafikia walengwa kama SAUTI bali ilikuja kama NGURUMO. Ndugu Kumbuka biblia ni sauti ya Mungu katika maandishi, kabla haijaandikwa ilizungumzwa na Roho wa Mungu mwenyewe ndipo baadaye yale maneno yakaja kuandikwa kwa ajili yetu katika karatasi.
Hivyo biblia kwetu sisi inakaa kama ngurumo na inahitaji Roho wa Mungu kuisikia sauti nyuma ya hiyo ngurumo vinginevyo hatutaelewa chochote kilichomo humo.
Na hichi kitabu kinajishuhudia chenyewe kuwa ni kitabu kilichofungwa soma (Danieli 12:4 & Ufunuo 10:4 utaona jambo hilo). Hivyo inahitajika Roho wa Mungu mwenyewe kukifungua, sisemi kuwa hutaelewa hadithi zilizoandikwa humo hapana, unaweza ukaelewa habari zote, lakini hautapata ufahamu wa kuelewa ufunuo wa yaliyoandikwa kule hata uwe ni msomi wa theolojia kiasi gani. Kama hakuna msaada wa Roho wa Mungu kitakachosomwa huko ni ngurumo tu! Na sio sauti ya Mungu.
Mahali Fulani Bwana Yesu alitoa mfano wa mpanzi kwa makutano, na alipomaliza akaondoka bila kuwafafanulia chochote. Wale makutano kwa kuwa hawakuwa na kiu ya kutaka kujua zaidi walikisia pengine ni hadithi tu inayohusu habari Fulani ya mkulima isiyokuwa na ulinganifu wowote na mahitaji yaliyowapeleka pale, na kwasababu wao kilichowapeleka pale ni miujiza tu, wakapuuzia zile habari za ule mfano wakidhani wameelewa na kuondoka zao wakiwa wameponywa kwa furaha. Na Bwana naye akawaacha hivyo hivyo mpaka wanafunzi wake kwa unyenyekevu mwingi walipoamua kumfuata na kuomba wafafanuliwe maana ya ule mfano..Ndipo Bwana Yesu akawaambia;
Mathayo 13:10-16 “10 Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?11 Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
12 Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
13 Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, KUSIKIA MTASIKIA, WALA HAMTAELEWA, KUTAZAMA MTATAZAMA, WALA HAMTAONA.
15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
16 Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.”
Na tukiendelea kusoma ndipo tunaona Bwana Yesu akiwafumbua macho wanafunzi wake tu na kuuelewa ule mfano wa mpanzi.
Na vivyo hivyo kila mahali alipokuwa akifundisha makutano alimalizia na kusema “MWENYE MASIKIO NA ASIKIE”. Ikiwa na maana kuwa linahitajika sikio lingine la ziada kusikia kile ambacho Mungu anazungumza, vinginevyo itakuwa kwako kama ngurumo badala ya sauti.
Ukiona unasoma biblia wewe unayejiita mkristo halafu maisha yako ni yale yale, hapo umesikia ngurumo bado hujaisikia sauti ya Mungu. Tafuta kuisikia sauti ya Mungu.
Ukiona unahubiriwa injili halafu haubadiliki, Sikio lako limefumbwa ili unaposikia usielewe. Tafuta mapema kusikia sauti ya Mungu kabla nyakati za hatari hazijakufikia.
Jenga tabia ya kuchunguza maandiko kama mitume, wao hawakuridhika na ufahamu waliokuwa nao kuhusu Maneno ya Mungu, na ndio maana unaona walikuwa wanamfuata Yesu faraghani na kumuuliza, na ndipo wanafafanuliwa, sasa kama mitume waliochaguliwa na Mungu walifanya hivyo. Inatupasaje sisi??.
Unaweza ukawa umepitia biblia yote mwanzo hadi mwisho, lakini bado hujamsikia Mungu, bali ngurumo tu kwasababu maisha yako yanaonyesha. Unaweza ukawa umesoma biblia yote lakini bado msengenyaji, bado mwasherati. Hapo kusoma umesoma lakini hujaelewa. Laiti ungesikia SAUTI YA MUNGU usingebakia hivyo hivyo.
Kwahiyo ndugu unaposoma Neno la Mungu usilichukulie tu juu juu, fahamu kuna sauti nyuma yake inayosema na wewe. Muombe Mungu akupe ufahamu wa kuisikia, Na hiyo ndiyo itakayokupa sababu ya wewe kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
Fungua moyo wako sasa, utafute kujifunza habari za Mungu, na sio kusoma tu kama kitabu cha hadithi, Na Mungu atakusaidia kuisikia sauti ya NENO lake inayosema nawe katika maisha yako na sio NGURUMO.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Ukiwa mgonjwa, labda unaumwa TB, ukapewa dozi na Daktari ukaambiwa utumie hizo kwa muda wa miezi 6 bila kuruka siku hata moja!! Je! Utaacha baada ya mwezi mmoja kwasababu masharti ni magumu au kwasababu umepata unafuu??. Ni dhahiri kuwa hutaacha kwasababu unajua madhara yake, kwamba ukiacha hata kama unajihisi kama umepona, yatakuwa ni makubwa zaidi na badala ya kupona utajikuta utaleta ugonjwa sugu zaidi hivyo hali yako ya mwisho inakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Ndio hapo utajua Daktari anayo sababu muhimu kwanini utumie dozi hiyo kwa miezi 6.
Vivyo hivyo na wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji wanafahamu kuwa wasipofuata maagizo wanayopewa huko, kuna mawili aidha isilete matokeo yoyote au ilete madhara makubwa zaidi.
Kadhalika na Bwana wetu YESU KRISTO kama TABIBU wetu mkuu wa roho zetu atupendaye alitoa TIBA(damu yake) ya kuponya dhambi zetu. Na hii tiba iliambatana na MAAGIZO kuwa ni lazima yafuatwe, Na yasipofuatwa kisahihi au kuvunjwa kuna hatari ya matokeo kuwa hasi. Mungu huwa anatembea katika kanuni zake tu.
Bwana Yesu alisema maneno haya katika
Marko 16:15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. AAMINIYE na KUBATIZWA ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.”
Unaona hapo tiba ya dhambi imekuja na maagizo, : Hatua ya kwanza ni kuamini; Ambayo hii inakuja pale mtu anapoiamini injili na kutubu na kukusudia kabisa kuacha dhambi kwa moyo wake wote,. Sasa baada ya mtu huyu kukusudia kufanya hivyo hapo ni sawa na amekutana na daktari akamweleza ugonjwa wake, na akaamini kwamba huyo daktari anao uwezo wa kumponya.
Hatua ya PILI inayofuata, ni KUBATIZWA: Haya ni maagizo Bwana Yesu aliyatoa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, ni sawa na daktari amekupa dawa na kukuambia Katie kwenye maji na kuogea kwa muda wa wiki mbili kisha huo ugonjwa wa ngozi unaokusumbua utaisha. Lakini ukivunja maagizo, na kwenda kujinyunyuzia badala ya kuiogea je! Ugonjwa utatoka?. Ni wazi kuwa ugonjwa utabaki.
Vivyo hivyo katika ubatizo, Neno “Ubatizo” maana yake ni “kuzamishwa”, kwahiyo baada ya kuamini hatua inayofuata ni kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, kiashirio kuwa damu ya Yesu Kristo imefuta dhambi zako zote, Bwana Yesu alipokufa pale msalabani damu na maji vilitoka ubavuni mwake kuashiria kuwa hivi vitu viwili vinaenda pamoja. Na ndio maana siku ile ya Pentekoste baada ya watu kuiamini injili ya Petro ndipo walipomuuliza;
Matendo 2:37-38 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, TUBUNI, MKABATIZWE kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
Umeona hapo maagizo yametolewa ili tuwe na uhakika kuwa dhambi zetu zimeondolewa ni lazima Tutubu kwanza kisha tubatizwe(Kwa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU) na dhambi zetu zitakuwa zimeondolewa.
Lakini kinachohuzunisha ni kwamba pale unaposikia mtu anapoambiwa juu ya umuhimu wa ubatizo sahihi na kuanza kutoa udhuru, na kusema hilo halijalishi, ni imani yako tu, iwe maji mengi au kidogo haijalishi!!! .. Ndugu inajalisha sana, Hivi daktari anapokuambia kaogee dawa hii mara tatu kwa siku, utamwambia hiyo haijalishi mimi nitainyunyuzia mwilini, ni imani yangu tu?? Kuna uhakika wa kupona kweli hapo?
Mgonjwa kweli aliyetayari kupona hatafikiria mara mbili mbili juu ya suala hilo hata aambiwe afanye hivyo mara kumi kwa siku atatii kwasababu yeye shida yake tu awe na uhakika wa kupona.
Maagizo mepesi kama haya yakitushinda tutaweza maagizo gani tena?.
Ubatizo sahihi ndugu ni muhimu katika safari yako ya ukristo, ikiwa kweli umemaanisha kwenda mbinguni utatii maagizo yote uliyopewa na mkombozi wa roho yako, ukisoma biblia yote hakuna mahali popote mtu alibatizwa kwa kunyunyiziwa, wote walizamishwa tena wakabatizwa kwa jina la YESU na sio kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu kama wengi wao wafanyavyo kimakosa soma (Matendo 2:38. Mdo 8:16, Mdo 10:48, Mdo 19:5 utathibitisha jambo hilo), Unapaswa ufahamu jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu Bwana alilolizungumzia katika Mathayo 28:19 Ni lipi? Utakuja kugundua kuwa ni jina moja hilo na ndilo mitume walilitumia kubatizia, nalo ni JINA LA YESU.
Ukizidi kujifunza maandiko utaona pia hakuna ubatizo wa vichanga, kwasababua mtoto mchanga hajatubu bado, hafahamu jema wala baya, hivyo hawezi kubatizwa, watoto wachanga wanawekewa mikono tu kama Baraka juu ya maisha yao yamwishie Mungu basi na sio kubatizwa. Mambo ya wokovu yanahitaji uamuzi binafsi na sio kufanyiwa kwa niaba ya mtu mwingine. Pale wakishafikia umri wa kujua jema na baya ndipo kwa uamuzi wao wenyewe wanamwendea Yesu na kuoshwa dhambi zao kwa kubatizwa, Hivyo ndugu kama ulibatizwa utotoni unapaswa ukabatizwe tena, ili kuufanya wito wako na uteule wako imara.
Na pia ubatizo hauhitaji shule yoyote ya kupitia kama baadhi ya dini zinavyofanya, pale unapoamini tu na kukusudia kuishi maisha mapya katika Kristo haraka sana nenda kabatizwe, Filipo alipokutana na yule towashi mara tu alipoamini akabatizwa saa ile ile.
Matendo 8: 35-38 “Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?
37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]
38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.”
Hivyo kama ulishaamini na haujabatizwa, au ulibatizwa utotoni, au haujabatizwa kwa ubatizo sahihi kwa jina la YESU, ni vizuri ukafanya hivyo sasa kwa uhakika wa safari yako ya wokovu.
Na Hatua ya TATU na ya mwisho baada ya kubatizwa ni Roho Mtakatifu. Biblia inasema Roho Mtakatifu ni MUHURI wa Mungu(Waefeso 4:30, Waefeso 1:13, 2wakoritho 1:22), Unapopokea Roho Mtakatifu unakuwa umekamilishwa mpaka siku ya ukombozi wako.
Matendo 19:1-5
“1 Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;
2 akawauliza, Je! MLIPOKEA ROHO MTAKATIFU MLIPOAMINI? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.
4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
5 Waliposikia haya WAKABATIZWA kwa JINA LA BWANA YESU.
6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, ROHO MTAKATIFU akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.”
Hivyo hatua hizi TATU ni muhimu sana kwa mkristo aliyemaanisha kuokolewa, kwa kufanya hivyo atakuwa “ameufanya wito wake na uteule wake imara 2 petro 1:10”.
Kama haujabatizwa ipasavyo tafuta mahali wanapobatiza ubatizo sahihi, au wasiliana na mimi, uwe ni wa kuzamishwa mwili wako wote na kwa jina la YESU.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
NINI MAANA YA “TAMAA YAKO ITAKUWA KWA MUMEO”?
JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?
Hii neema tuliyonayo watu wa mataifa, haikuanzia kwetu, bali ilitoka kwa wengine lakini kwa huruma za Mungu walipokonywa wao tukapewa sisi. Israeli kama Taifa teule la Mungu walikuwa wameshafikia kilele cha kula matunda ya taabu yao kwa kuja kwake mkombozi ambaye ni Mesiya wao waliyemngojea kwa miaka mingi, ambaye angewaokoa na dhambi zao na maadui zao, lakini mambo hayakuwa kama yalivyo kwasababu badala ya wao kufaidi lile TUNDA, wakanyang’anywa na kupewa wengine ambao ndio sisi mataifa.
Hivyo mkombozi wa nafsi zao alipokuja Mungu aliwapiga upofu, wasiweze kumuamini kwasababu maalumu ili sisi (mataifa:mimi na wewe) tuweze kumwamini na kushiriki kipawa hicho cha neema.
Biblia inasema hivi juu ya Taifa la Israeli.
Warumi 11: 10 “Macho yao yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote.11 Basi nasema, Je! Wamejikwaa hata waanguke kabisa? Hasha! Lakini KWA KOSA LAO WOKOVU UMEWAFIKILIA MATAIFA, ili wao wenyewe watiwe wivu.12 Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! SI ZAIDI SANA UTIMILIFU WAO?”.
Hii ni dhahiri tukiliangalia taifa la Israeli tangu kipindi kile Bwana Yesu alipokuja, mpaka sasa wayahudi wamekuwa wakiupinga ukristo, hawataki kumwamini Bwana Yesu kama ndiye Masia wao aliyetabiriwa, wanasema Yule ni mtu tu wa kawaida, Taifa zima haliamini habari za Yesu ni masalia tu (yaani watu wachache sana) waliopewa neema ndio wanaoamini lakini sio taifa, sio kwasababu ni waovu sana, hapana bali ni kwasababu Mungu mwenyewe kawapiga upofu makusudi wasilione hilo, kwa ajili yetu sisi mataifa, kwasababu mfano wangeamini sisi mataifa tusingekuwa na nafasi yoyote katika ufalme wa mbinguni. Kwasababu Mungu huwa hashughuliki na mataifa mawili kwa wakati mmoja. Alipotembea na Israeli, watu wa mataifa aliwaweka kando, vivyo hivyo na sisi.
Lakini hilo halitadumu milele, Mungu analipenda na analionea wivu taifa lake Israeli siku zote, ambalo hilo lingestahili kuwa la kwanza kupokea Baraka za mwokozi kwasababu hiyo basi utafika wakati Bwana atalirudia taifa lake tena, na watu wa mataifa waliobakia walioikataa neema watapigwa upofu wa mauti na kuondolewa. Ni kipindi cha hatari na kimeshaanza taratibu taratibu.
Ndugu tukishakifikia huo wakati hata uiweje watu hawataweza kuipokea injili tena, maana ili kuiamini inahitajika neema kutoka kwa Mungu mwenyewe, kwasababu biblia inasema
Yohana 6:44 “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho”.
Hivyo hiyo nguvu ya kuvutwa kwa Mungu haitakuwepo tena kwa mataifa, kitu kitakachobakia kwa watu wa mataifa ni NGUVU YA UPOTEVU inayotoka kwa Mungu soma..
2Wathesalonike 2: 10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 KWA HIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu”.
Watabakia katika dini zao na madhehebu yao wakidhani kuwa ndio wanamwabudu Mungu, kama wale mafarisayo na masadukayo walivyokuwa wakati ule neema ya Kristo ilipotolewa kwao, badala ya kumpokea kinyume chake walimsulibisha, ndivyo itakavyokuwa kwa watu wanaokataa KUIAMINI KWELI sasa hivi. Sasa kama wayahudi ambao walikuwa ni watu wa Mungu yaliwakuta mambo kama hayo Na sisi je! Tutawezaje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii??(Waebrania 2:3).
Biblia imetufananisha sisi watu wa mataifa kama mizeituni mwitu, na Israeli kama mzeituni halisi, kwamba wao walikatwa ili sisi tupandikizwe tulio mzeituni mwitu na tuzae matunda halisi ya mzeituni. Kama Mtume Paulo alivyoandika katika.:
Warumi 11:15-24 “15 Maana ikiwa kutupwa kwao{ISRAELI} kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?16 Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika.
17 Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe MZEITUNI MWITU ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,
18 usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe.
19 Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi.
20 Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.
21 KWA MAANA IKIWA MUNGU HAKUYAACHIA MATAWI YA ASILI, WALA HATAKUACHIA WEWE .
22 Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.
23 Na hao pia, wasipokaa katika kutokuamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena.
24 Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, SI ZAIDI SANA WALE WALIO WA ASILI KUWEZA KUPANDIKIZWA KATIKA MZEITUNI WAO WENYEWE?.
Unaona hapo kuna wakati utafika ambao Mungu ameuamuru kwa watu wake Israeli, KUPANDIKIZWA TENA na sio siku nyingi. Na ukishafika huo wakati Israeli wote watafumbuliwa macho na kumpokea Bwana Yesu na kufahamu kuwa walifanya makosa kumsulibisha masihi wao, watamlilia na kumuombolezea biblia inasema hivyo (Soma Zekaria 12:9-14). Na neema hii itakaporudi Israeli itakuwa imebakia miaka 7 tu mpaka dunia iishe.
Kumbuka wakati huo Bwana atakuwa ameshamaliza kushughulika na watu wa mataifa, na shughuli hiyo itaishia na UNYAKUO wa kanisa, baada ya hapo ni giza kuu kwa mataifa yote na kufunuliwa kwa mpinga-kristo akitenda kazi katikakati ya wale waliobaki wasiokwenda kwenye unyakuo.
Ukiendelea mstari wa 25-27 utaona mtume Paulo anaendelea na kusema..
“25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UWASILI.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.”
Kwa miaka 2000 sasa, Mungu amekuwa akilia katika mioyo ya watu wa mataifa, akiwaambia “waje wanywe maji ya uzima bure”. Neema imekuwa kubwa kiasi kwamba Mungu analithibitisha Neno lake kwa ishara na miujiza ya kupita kiasi, wengine anawavuta kwa njia ya ndoto, wengine kwa maono, wengine kwa wahubiri, n.k. ili tu waingie katika karamu ya Mungu aliyowaandalia watu wake wa mataifa. Wapo ambao wameitii injili na kuiamini na kuifuata lakini cha kuhuzunisha ni kwamba wapo ambao wanaitupilia mbali NEEMA hii, na kumbuka kukatwa kwa mataifa kumeshaanza, kama tu vile kupandikizwa kwa Taifa la Israeli kunavyoanza.
Hauoni mataifa mengi hususani ya magharibi ambayo hapo kwanza yaliitwa ya kikristo na kutuletea sisi injili sasa hivi yamegeuka kuwa ni mataifa yanayo mpinga Kristo?. Hizo ni dalili za kukatwa, Na ukiangalia injili inamalizikia na Afrika(chini ya jangwa la Sahara) kwasababu ndio waliokuwa wa mwisho kupelekewa injili, na ndio inamalizikia hivyo, Irejee ilikotoka Israeli. Embu fikiri ni wakati gani huu tunaoishi??. Israeli inarudiwa na maandalizi ya kujenga Hekalu la Tatu huko Yerusalemu yameshakamilika. Miaka 70 sasa imeshapita tangu Israeli kupata uhuru wake baada ya kukaa zaidi ya miaka 2500 bila taifa. Leo hii mataifa yote macho yao yanaelekea Israeli ni nini kinachojiandaa kutokea?.
Ndugu Unyakuo ni muda wowote tokea sasa, tumeambiwa “KWA MTINI JIFUNZENI(ambalo ni Taifa la Israeli)”..Hivyo jitahidi kuingia katika huo mlango wa NEEMA sasa kabla haujafungwa, Biblia inasema
Luka 13: 23-24 “Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.”
Tujitahidi ndugu.
Unapohubiriwa injili na kuipinga ndani ya moyo wako..ni dalili za awali kuwa neema inaondoka kwako.
Maombi yangu ni ufungue moyo wako sasa, Kristo ayabadilishe maisha yako.
2Wakoritho 6:1-2“ Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;TAZAMA, WAKATI ULIOKUBALIKA NDIYO SASA; TAZAMA SIKU YA WOKOVU NI SASA)”.
Ubarikiwe sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.
NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.
NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!
Kila mnyama tunayemwona, kwa namna moja au nyingine yupo mwanadamu au jamii au taifa linalobeba tabia zinazofanana na huyo mnyama, Kwamfano Bwana Yesu kumwita Herode “Mbweha” hakuwa anamtukana, bali alikuwa anaelezea jinsi tabia yake inavyofanana na ya mbweha. Mbweha ni mnyama anayekaribia kufanana na mbwa, isipokuwa huyu anararau wanyama wadogo wadogo na pia tabia yake nyingine inayofanana na mbwa ni kuzaliana na mbweha mwingine yeyote bila mpangilio maalumu, hivyo tabia hizi zilionekana kwa Herode, Kwanza alikuwa muuaji: alimuua Yohana Mbatizaji nabii wa Mungu, na bado akaongeza kuoa mke wa ndugu yake, tabia zisizo na tofauti na mbweha.
Kadhalika kitabu cha Danieli kinaeleza juu ya zile Falme 4 zitakakuja kutawala mpaka mwisho wa Dunia, nazo pia zilifananishwa na tabia za wanyama, kwa mfano Babeli ilifananishwa na Simba, Umedi & Uajemi ilifananishwa na dubu, vivyo hivyo na Uyunani ulifananishwa na Chui.(Danieli 7)n.k.
Shetani naye alifananishwa na joka, kwasababu ya tabia aliyokuwa nayo nyoka ya kumdanganya mwanadamu kumuasi Mungu kwa kula tunda. Kama tu anavyoendelea kufanya sasa hivi kuudanganya ulimwengu watu wamwasi Mungu, waishie kwenda katika ziwa la moto.
Vivyo hivyo na BWANA wetu YESU KRISTO alifananishwa na mnyama fulani na huyu si mwingine zaidi ya MWANA-KONDOO.
KWANINI MWANA-KONDOO?
Tabia ya kwanza ya kondoo ni mnyenyekevu na mpole, na ni mnyama ambaye hawezi kujiongoza mwenyewe siku zote anategemea mchungaji wake kumuongoza tofauti na mbuzi, Mbuzi yeye anao uwezo wa kujichunga mwenyewe.
Na ndio maana tunaona sehemu zote Bwana Yesu aliitwa “mwanakondoo”, Yohana alimwona kama mwanakondoo achukuaye dhambi za ulimwengu, si ajabu hata kuzaliwa kwake kulikuwa ni kwenye hori la ng’ombe. YESU Alipoishi duniani alikuwa ni mpole na mnyenyekevu sana, kiasi kwamba japo alikuwa ni Mtakatifu lakini alikaa katikati ya watoza ushuru na makahaba, japo alikuwa ni mfalme lakini aliwaosha miguu wanafunzi wake. Biblia inamshuhudia alikuwa anawakemea waovu lakini moyoni mwake alijaa huruma. Yeye mwenyewe alishuhudia na kusema..
Mathayo 11: 28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa MIMI NI MPOLE NA MNYENYEKEVU WA MOYO; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”.
Ni mtu ambaye aliwaponya maadui zake waliokuja kumuua kwa mapanga na marungu, Alilia kwa dua nyingi na machozi kwa ajili ya ndugu zake(mimi na wewe).
Na kama vile kondoo wanaponyolewa manyoya yao kwa ajili ya sufu au wanapopelekwa machinjoni wanakaa kimya tofauti na mbuzi, ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu, alitukanwa hakurudisha, alipigwa makofi hakurudisha, alitemewa mate, hakurudisha, japo alisikia maumivu kama mwanadamu mwingine yeyote lakini aliishia na kusema BABA WASAMEHE. Hii ilitoka ndani ya moyo wake kabisa na sio kinafiki.
Nabii Isaya alimwona miaka mingi sana kabla ya kuja kwake akaeleza habari zake..
Isaya 53:3-8 “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; MTU WA HUZUNI NYINGI, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
4 HAKIKA AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU, AMEJITWIKA HUZUNI ZETU; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
7 Alionewa, lakini ALINYENYEKEA, Wala hakufunua kinywa chake; Kama MWANA-KONDOO APELEKWAYE MACHINJONI, Na kama vile kondoo ANYAMAZAVYO Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, HAKUFUNUA KINYWA CHAKE.
8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.”
Zekaria 9: 9 “Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; NI MNYENYEKEVU, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.” Haleluya, Bwana Yesu alikuwa ni wa kipekee sana.
Vivyo hivyo Roho Mtakatifu alifananishwa na HUWA (yaani NJIWA)..Kutokana na tabia za njiwa huwa ni MPOLE. Na njiwa siku zote anatua sehemu zenye utulivu na amani..hawezi kutua sehemu nyingine yoyote kama Kunguru. Wanaofuga njiwa wanaelewa itakuchukua muda mrefu sana mpaka akuzoee kiasi cha kufikia hatua ya kutua kwenye mikono yako au mabegani mwako, Njiwa anayo desturi ya kuhakiki jambo Fulani kwa muda mrefu mpaka alizoee, inahitaji upole wa hali ya juu. Na inajulikana mahali palipo na makelele njiwa huwa hakai atahama hata kama anahudumiwa vizuri kiasi gani.
Na hapa tunaona ROHO mfano wa HUWA akitua juu ya Bwana Yesu Kristo kiashirio kuwa ni mahali sahihi penye utulivu wa kutua. Roho aliridhishwa na upole na unyenyekevu wa Bwana YESU kama mwanakondoo.
Marko 1: 9 “Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani.
10 Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake;
11 na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.”
Vivyo hivyo na watoto wa Mungu wote wanafananishwa na wana-kondoo, na hao ndio ROHO WA MUNGU anaowashukia juu yao. Wanapaswa wawe wapole, wanyenyekevu, wanapotukanwa hawarudishi, wanapoudhiwa hawawaudhi wengine, hawasengenyi, wanawaombea wanaowaudhi, wanawapenda maadui zao na kuwasamehe kama Bwana alivyokuwa. Na zaidi ya yote hawajiongozi wenyewe kama mbuzi, wanamtegemea Mungu(Mchungaji mkuu YESU) kwa kila kitu, hawachukui maamuzi yoyote pasipo yeye, wanadumu katika NENO tu, hawaabudu miungu mingine, wanachofikiria ni utakatifu tu, wapo tayari hata kutoa uhai wao kwa ajili ya ndugu zao wengine kama yeye alivyoutoa uhai wake kwa ajili yetu. Watu kama hawa Roho wa Mungu anashuka juu yao na kuwafanya waendelea kuzaa matunda yote ya Roho.(wagalatia 5:22).
Lakini wasio wa Mungu wanafananishwa na mbuzi, wao huwa wanajiongoza wenyewe na kujiamulia mambo yao, hawana haja na mchungaji (yaani Bwana YESU), hawa hawawezi kuwa wanyenyekevu au wapole kwasababu wanajiona kuwa wanafahamu kila kitu.
Je! Wewe ni kondoo au mbuzi?. Kumbuka Roho wa Mungu hawezi kukaa juu ya mbuzi. Japo leo hii wanajificha katika kanisa la Mungu lakini utafika wakati wa kutengwa..KONDOO upande wa kuume, na MBUZI upande wa kushoto. Je! Utakuwa upande upi siku ile??
Mathayo 25: 32-46 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 ATAWAWEKA KONDOO MKONO WAKE WA KUUME, NA MBUZI MKONO WAKE WA KUSHOTO.
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Shalom.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
KAENI NDANI YANGU NAMI NDANI YENU.
KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA
NENO “MASHEHE” TUNALIONA LIKITAJWA KATIKA BIBLIA(AGANO LA KALE); HAWA MASHEHE NI WAKINA NANI?
JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?
Tunaposoma biblia tunajifunza mambo mengi sana, yahusuyo tabia za Mungu, na moja ya tabia ya kipekee sana ya Mungu ni “kutokumlazimisha mtu kufanya jambo Fulani”. Kuna kipindi nilitamani na nilimuomba sana Roho Mtakatifu anivae na kuniendesha pasipo mimi mwenyewe kujitambua kama vile mtu aliyepagawa na mapepo.
Kwasababu watu wenye roho za mashetani huwa wanaendeshwa mpaka wanakuwa hajitambui tena mfano vichaa. Niliendelea kuomba hivyo mpaka siku Bwana aliponipa ufahamu na kugundua kuwa Mungu hatendi kazi kwa namna hiyo japo anao uwezo huo, lakini hamvai mtu na kumfanya mateka kama vile pepo linavyofanya.
Roho Mtakatifu ni msaidizi na mshauri na pia ni mpole, kamwe hamlazimishi mtu kuchukua uamuzi Fulani, Na ndio maana mtu anapoamua kuwa mwovu, haendi kumlazimisha aokoke, yeye anachofanya ni kumshawishi na kumshauri na kumpa kila sababu ya kuacha dhambi, lakini akikataa anamwacha aendelee kufanya anachokitaka lakini akikubali anaendelea naye.
Na vivyo hivyo katika kuifanya kazi ya Mungu, wengi wanangojea waone maono kama mtume Paulo alivyoona, au watokewe na malaika, au washukiwe na uweza wa ajabu walazimishwe kama Yona, au wasikie sauti kutoka mbinguni ikiwaambia nenda, au watabiriwe n.k.
Napenda kukwambia ndugu ukitegemea njia hiyo mwisho wa siku utaishia kuvunjika moyo pale utakapoona hakuna jambo lolote lililotokea kwa kipindi ulichokuwa unasubiria na muda umeshakwenda. Njia kama hizo Mungu akizitumia ni kwa neema zake tu! Kwa kuonyesha uweza wake. Lakini sio njia aliyoikusudia kutumia kuwatuma watu wake katika kazi yake. Tunamtumikia Mungu kwa imani na sio kwa kuona, na Mungu anataka mtu afanye kwa moyo wake mwenyewe na sio kwa kulazimishwa.
Tunaweza tukajifunza mifano ya watu watatu katika biblia ambao wanaweza kutusaidia katika kujua njia sahihi ya kumtumikia Mungu.
Daudi alikuwa ni mfalme wa Israeli, aliyepitia taabu nyingi katika maisha yake lakini Bwana alipomstarehesha, na kumpa ufalme na vitu vyote, alifikia wakati akaanza kumtafakari Mungu wake, dhamiri yake ikaanza kumchoma..akasema mimi Daudi naishi katika jumba la kifalme wakati Mungu wangu anakaa kwenye hema liliochakaa tena kwenye giza katika kijiji Fulani huko Shilo??. (Kwasababu wakati huo sanduku la Agano la Mungu lilikuwa linakaa Shilo). Ndio Daudi akaazimu moyoni mwake kumjengea Mungu nyumba nzuri ya kukaa kwa hiari yake mwenyewe.. Na alipofikiria hivyo tu biblia inasema..
1 Samweli 7: 1 “Ikawa, mfalme alipokuwa akikaa katika nyumba yake, hapo Bwana alipomstarehesha, asiudhiwe na adui zake waliomzunguka pande zote,2 mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika nyumba ya mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia.
3 Nathani akamwambia mfalme, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; maana Bwana yu pamoja nawe.
4 Ikawa usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia Nathani kusema,
5 Enenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake?
6 Kwa maana mimi sikukaa ndani ya nyumba, tangu siku ile niliyowatoa wana wa Israeli katika Misri, hata leo, lakini nimekaa katika hema na maskani.
7 Mahali mwote nilimokwenda na wana wa Israeli wote, JE! NIMESEMA NENO LOLOTE NA MTU YEYOTE WA WAAMUZI WA ISRAELI?, niliyemwagiza kuwalisha watu wangu Israeli, NIKISEMA, MBONA HAMKUNIJENGEA NYUMBA YA MIEREZI?.
8 Basi, sasa, mwambie mtumishi wangu, Daudi, maneno haya, Bwana wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli;
9 nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani.”
Ukizidi kusoma mbele utaona Daudi kwa kufanya hivyo aliahidiwa kuwa kiti chake cha enzi na ufalme utathibitika milele, Na ndio maana Mungu aliuchagua uzao wa Daudi kupitia yeye Kristo atokee huko, na mji wake Yerusalemu kuwa makao makuu ya MASIHI duniani.. Na Daudi ndiye aliyeupendeza moyo wa Mungu kuliko watu wote.
Sasa je! DAUDI ALINGOJEA MAONO YAMJIE ILI AMJENGEE MUNGU NYUMBA??.. Hapana aliona kila sababu ya kwanini asifanye vile kwa Mungu angali anao huo uwezo?. Na ndipo Mungu akampa thawabu kuu kwa maamuzi ya busara aliyoyafanya.
Mfano mwingine tunamwona Nehemia, aliyekuwa mnyweshaji wa Mfalme wa Uajemi..Lakini siku moja ndugu zake walitoka Yerusalemu, na kumpasha habari kuwa nyumba ya Mungu, na Ukuta wa Mji umebomolewa. Habari zile zilimuhuzunisha sana hata akaamua afunge na kuomboleza na kulia kwa siku nyingi kwa ajili ya mji wake, na kumuomba Mungu dua na msamaha kwa Israeli, kumbuka Nehemia hakuwa nabii, alikuwa ni mtu tu! wa kawaida, mfanyaji wa kazi za ndani za mfalme wa mataifa.
Hivyo akawaza moyoni mwake tu, siwezi kukaa katika hali hii ya raha huku nyumba ya Mungu wetu kule Yerusalemu imekaa katika hali ya kuharibiwa. Kwa kufanya hivyo Mungu akamuhurumia na kumpa kibali cha mfalme kwenda Yerusalemu kukarabati nyumba na ukuta wa mji..
Japo alipitia taabu nyingi sana wakati wa kujenga ukuta, maadui waliwazunguka kila upande, mkono mmoja ulishika silaha na mwingine nyenzo za ujenzi, lakini kwa bidii yeye na wenzake walifanikiwa kumaliza kuujenga ukuta wa mji, mpaka akafikia kusema UNIKUMBUKE MUNGU WANGU, kwa taabu hizi..
Huyu naye pia hakuwahi kuona maono, wala kuota ndoto, au kuzungumza na malaika, au kushukiwa na upako aliona tu nyumba ya Mungu ipo katika hali mbaya inanipasa nifanye kitu!!.. Lakini leo hii tunaona ushujaa wa Nehemia Mungu kampa kumbukumbu lisilofutika leo tunakisoma kitabu chake japo hakuwa nabii wala kuhani wala mwandishi.
Mfano mwingine tunamwona Yule mwanamke mwenye dhambi aliyemwendea Yesu, pamoja na dhambi zake zote alizokuwa nazo aliona kuna mapungufu katika mwili wa Yesu, aliona kuwa miguu ya Yesu ni michafu, ndipo akaona kuna sababu ya kuiosha kwanza, hivyo akatumia machozi yake, badala ya maji, akatumia nywele zake kumfuta badala ya kitambaa, na baada ya kuona imesafishika akampaka mafuta yenye manukato ya thamani nyingi sana (thamani yake kwasasa ni sh. Milioni 6)…Kumbuka huyu hakuona maono aliamua tu mwenyewe kufanya hivyo baada ya kuona mapungufu, lakini baada ya tukio hilo Bwana Yesu aliwaambia..
Luka 7: 44 “Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake.
45 Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu.
46 Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu.
47 Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.
48 Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako.”
Kumbe iliwapasa wajue wao wenyewe kuwa miguu ya Bwana ni michafu na inahitaji kuoshwa, lakini wao walisubiria waambiwe..ndugu nataka nikuambie kama na wewe leo unasubiria Mungu akuambie nenda kafanye kitu fulani angali unafahamu kabisa kuna huo uhitaji,..jua tu hatakuambia …Ni jukumu lako wewe kuchukua hatua.
Ipo mifano mingi ya namna hii katika biblia yupo mwanamke mwingine alifanya kama huyu wa kwanza ukisoma Mathayo 26:13, utaona alimmwagia Bwana mafuta katika nywele zake, japo wengine waliona kama anatapanya pesa lakini Bwana alimwambia kuwa kwa kuwa amefanya vile Popote itakapohubiriwa injili, tendo hilo litatajwa kwa kumbukumbu lake. Huyu naye hakusubiria neema imshukie, au asubirie nabii amtabirie.
Hivyo ndugu, mahali ulipo,au kanisa ulilopo au chochote unachokifanya..je! unaugua kwa ajili ya kazi ya Mungu au unasubiri jambo Fulani Mungu akutendee ndipo uanze kumtumikia Mungu?. Mungu amekubariki katika Mali zako, zitumie hizo kufanya kazi ya Mungu, habari njema ziwafikie wengi kama wakina Martha, sio lazima uwe muhubiri, Nehemia hakuwa muhubiri, lakini alimfanyia Mungu kitu kinachoonekana, unaona choo kichafu kanisani, nyasi zimeota, unangoja uone maono juu ya hilo?.
Unaona kuna umuhimu wa kuwavuta watu kwa Kristo unasubiria kuitwa?? Utaitwa lini na huku umeshakaa katika ukristo kwa miaka mingi?. Lakini mtu atasema mimi sijui wito wangu..ndugu tumeitwa wote kuwa mashuhuda wa Kristo?.
Wewe ni fundi wa nyumba au technician unaona kuna kasoro katika nyumba ya Mungu embu kuwa kama Nehemia usingojee maono yakushukie kwenda kufanya hivyo, usisubirie mtu mwingine aajiriwe kuja kuifanya hiyo kazi angali ipo katika uwezo wa mikono yako.
Umepata nafasi ya kukaa mitandaoni na unaona kabisa kuna uhitaji wa watu kumjua Mungu usisubirie lolote kwasababu kamwe Bwana hatakuambia au kukulazimisha kufanya hicho kitu.. Inahitaji hekima tu kulitambua hilo.
Ni maombi yangu utachukua hatua sasa kwa kila sehemu Bwana alipokuweka kwa ajili ya Kristo. Mungu atakusaidia na kumbukumbuku lako halitaondoshwa milele.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano, maombi/ushauri/ubatizo/ whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.
MAMBO AMBAYO MALAIKA WANATAMANI KUYACHUNGULIA.
JE! MKRISTO ANARUHUSIWA KULA NGURUWE, NA KUVUTA SIGARA NA KUNYWA POMBE?
Ni rahisi KUANGUKA au KUPOA katika Imani kama hautajiwekea utaratibu wa Kujikumbusha matendo yote mema Mungu aliyokutendea nyuma katika maisha yako.
Jambo lililowafanya Wana wa Israeli kule jangwani washindwe kusonga mbele na kukwazwa na mabaya, lilikuwa si lingine zaidi ya KUSAHAU fadhili za Mungu walizotendewa nyuma, kwamfano walipotoka Misri, na kukutana na kikwazo cha bahari, walianza kunung’unika wakasahau siku chache tu nyuma Mungu aliwapigania kwa mkono hodari dhidi ya maadui zao wamisri,
vivyo hivyo mara baada tu ya kufanyiwa muujiza mwingine wa bahari kupasuka walimshangilia Mungu kwa furaha na kumwimbia nyimbo za shangwe lakini baada ya siku tatu mbeleni, manung’uniko yakaanza tena pale walipokosa maji ya kunywa, tatizo lilikuwa ni moja tu! Walisahau wema wa Mungu waliotendewa siku chache nyuma, laiti wangetilia maanani mema yale na kukumbuka fadhili zote zile, wasingeshindwa kustahimili majaribu waliyokutana nayo. Na ndivyo ilivyoendelea kuwa katika safari yao yote, manung’uniko kila walipokutana na changamoto.
Na ndio sababu Mungu aliwakataza Israeli wote wasile WANYAMA WASIO CHEUA, kwa mfano nguruwe au farasi nk. Unajua ni kwa sababu gani??, kwasababu katika roho wanafunua kitu Fulani. Mnyama anayecheua ni mnyama ambaye akila chakula anao uwezo wa kukirudisha tena kinywani mwake na kukitafuna kisha akimeze tena, kwa mfano ng’ombe analo tumbo la akiba, akila baadaye anarudisha na kukitafuna tena.
Hivyo wanyama wa namna hiyo hawakuwa najisi, kwa tabia hiyo tu. Ikifunua katika roho kuwa watu wote wasiokuwa na uwezo wa kuzikumbuka na kuzitafakari fadhili na sheria za Mungu ni NAJISI mbele zake. Watu wote wa Mungu wanapaswa wawe na uwezo wa kucheua, baada ya kusikia au kufanyiwa miujiza, sasa kinachofuata ni kuyarudisha tena katika akili na kuyatafakari hayo kila mara.
Yakobo 1: 22-25 “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.
25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, ASIWE MSIKIAJI MSAHAULIFU, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.”
Kadhalika na kwa wakati tuliopo sasa, ili tusonge mbele au tuweze kusimama katika IMANI na kushinda wakati wa majaribu inatupasa tujiwekee utaratibu wa kutafakari na kujikumbusha kila siku mambo mema ambayo Mungu amewahi kututendea katika maisha yetu ya nyuma, Kwa mfano ulipowahi kupatwa na ugonjwa Fulani ambao ulikutesa sana na Bwana akakuponya, ni vizuri kujikumbushia jambo hilo kila siku, au ulimwomba Mungu jambo Fulani akakupa na kukufanikisha katika mambo yako na ukafahamu kabisa huyo ni Mungu aliyekutendea hivyo, unapaswa kulifikiria hilo kila siku usije ukasahau pale tatizo litakapokuja ili uweze kukabiliana nalo.
Kumbuka tena mahali Mungu alipokushindania ambapo unajua kabisa pasipo yeye usingeweza kufanikiwa, uwe unalitafakari hilo kila siku litakusaidia huko mbeleni ili umsimnung’unikie Mungu..Kuna hatari kubwa sana ya kuanguka kama hautajijingea huo utaratibu wa kukumbuka mambo uliyotendewa..
Sisi wanadamu tuna tabia ya kusahau hivyo ili usisahau ni vizuri uwe unaandika chini kila wema Mungu anaokufanyia kila siku.Kwa kufanya hivyo ndivyo utakavyoweza kudumu katika IMANI siku zote. Na pia unaposoma Neno la Mungu jenga tabia ya kujikumbusha kila wakati ili usisahau mapenzi ya Mungu katika maisha yako.
Wakati mwingine unajikuta unadondoka katika dhambi za usengenyaji, kwasababu unasahau Neno la Mungu, linakuwa halijakaa kwa wingi ndani yako, unajikuta unashindwa kusamehe kwasababu huna tabia ya kutafakari kila siku NENO LA MUNGU, Unajikuta wewe ni mkristo lakini unazungumza maneno ya mizaha, kwasababu mistari inayohusiana na mambo kama hayo imefutika ndani ya moyo wako, huna jambo la kukukumbusha kila wakati.
Ni maombi yangu utaanza kujenga utaratibu kuanzia leo wa kurekodi mambo yote mazuri Mungu anayokutendea ili yawe akiba kwa wakati wa shida au majaribu mbeleni. Na pia utaanza kutafakari NENO la Mungu kila siku. Sulemani kwa hekima ya Roho alituandikia sisi tulio watoto wa Imani na kusema;
Mithali 7:2 “Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako.
2 Uzishike amri zangu ukaishi, NA SHERIA YANGU KAMA MBONI YA JICHO LAKO.
3 ZIFUNGE KATIKA VIDOLE VYAKO; ZIANDIKE JUU YA KIBAO CHA MOYO WAKO.”
Na Daudi alisema;
Zaburi 119: 97 “Sheria yako naipenda mno ajabu, NDIYO KUTAFAKARI KWANGU MCHANA KUTWA.98 Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, KWA MAANA NINAYO SIKU ZOTE.
99 Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo NIZIFIKIRIZO.
100 Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.”
Ubarikiwe na BWANA YESU.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano, maombi/ushauri/ubatizo/ whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “Kandake” (Matendo 8:27)
MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU
Naomba usome ushuhuda huu mfupi utakujenga,
“Mimi na ndugu yangu tumekuwa na desturi ya muda mrefu kukaa pamoja na kushirikishana NENO LA MUNGU mara nyingi ili kuepuka usumbufu wa watu tumekuwa tukiondoka na kwenda mbali na makazi ya watu, sehemu zenye utulivu na kutumia muda mwingi kulitafakari NENO LA MUNGU, pamoja na kutiana moyo katika safari yetu ya Ukristo. Siku moja wakati tunatembea muda wa mchana kama saa 7 huku tunazungumza habari za Mungu na kutafakari ghafla mbele yetu njiani umbali si mrefu sana, tulioana punda watatu wamefungwa NIRA wanafuata njia, wakikokota kigari cha mzigo wa majani na nyuma kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akiwaendesha hao punda, lakini jambo moja lilitushangaza kidogo ni kuona punda 3 wamefungwa nira huku wakikivuta kile kigari wakati mara nyingi inakuwa ni punda wawili tu!.
Hivyo tulipokaribia kuwasogelea ili tuone vizuri, Yule punda aliyekuwa katikakati yao alitoweka wakabaki punda wawili kama kawaida. Wakati tunalishangaa hilo tukio lilitokea wale punda walifika mahali wakakuta na mtaro, uliokuwa mgumu kidogo kuvuka kutokana na ule mzigo waliokuwa wanauvuta, hivyo Yule Bwana wao aliokuwa anawaongoza alipoona wamesimama aliwachapa kwa fimbo yake aliyokuwa nayo, lakini japo ule mzigo ulikuwa ni mkubwa kwa wao kuuvukisha katika ule mtaro mwishoni walifanikiwa kupandisha na kuendelea na safari.
Tulibaki tunajiuliza maswali ni kitu gani tumeona? Ni mazingaumbwe au nini?. Ndipo Mungu akutupa ufahamu saa ile ile ni kwamba Mungu alitufumbua macho tuone jambo linaloendelea katika roho kuhusu sisi,”
Biblia inasema Mathayo 18:20 “ Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”
Tafsiri ya lile ono ni kuwa wale punda wawili wanatuwakilisha sisi wawili mimi na ndugu yangu, Yule punda wa tatu aliyekuwa katikati na kisha baadaye akaja kutoweka alimwakilisha Bwana YESU.
Na ule mzigo wale punda waliokuwa wameubeba ni SHERIA ZAKE, hivyo tunapokuwa wawili au zaidi Mungu anatufunga Nira yake mwenyewe sisi kwa sisi, na yeye akiwa katikati yetu kutusaidia mzigo wake(sheria zake), hivyo sheria zake zinakuwa nyepesi kuzishika.
Bwana Yesu pia alitupeleka kwenye hili andiko Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 JITIENI NIRA YANGU, MJIFUNZE KWANGU; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 KWA MAANA NIRA YANGU NI LAINI, NA MZIGO WANGU NI MWEPESI.”
Bwana alituonyesha kuwa anayo NIRA yake na MZIGO wake kwa watu wake, japo watu wa nje watauona kama ni mzigo mzito lakini Bwana akiwa katikati yetu unakuwa mwepesi kwasababu yeye anatusaidia, anakuwa anafanyika kama punda wa tatu katikati yetu.
> Kuishi maisha ya kuukataa ulimwengu huo ni mzigo wa Kristo aliokutwisha, na ndio maana wengine watakushangaa unawezaje kuishi maisha ya kutokufanya uasherati.
> Kufanya kazi yoyote ya Mungu ni mzigo wa Kristo, lakini yeye anakupa wepesi hususani mnapokuwa wawili au zaidi na ndio maana kila mahali Bwana alikuwa akiwatuma wawili wawili kazini kuhubiri injili.
Hivyo ndugu, kuna umuhimu mkubwa kuwa na mwenzako au wenzako mnaofanana imani, kwasababu mnapokuwa wawili au watatu au zaidi kwa jina lake lile NENO lazima litimie, ATAKUWA KATIKATI YENU. Mnakuwa mmefungwa NIRA na Kristo pamoja, hivyo mtajikuta kiurahisi mnazitimiza sheria za Bwana bila ugumu wowote tofauti na unapokuwa mwenyewe.
Umuhimu wa kuwa na mwenzako au kukusanyika na wenzako ni uwepo wa kipekee unashuka mahali mlipo, vitu kama faraja, kutiana moyo, kulindana, kushirikishana, mafunuo n,k. vinatoka huko kiasi kwamba hata shetani inamuwia ugumu kupata nafasi ya kukujaribu kwasababu yupo ndugu yako pembeni anayekuchunga.
Ndio maana biblia inasema katika
Mhubiri 4:9-12 “Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?
12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.”
Unaona hapo, kuna umuhimu wa kuwa karibu na ndugu anayeenda na wewe imani, Sisi baada ya Bwana kutufundisha hayo, tumekuwa tukikaa pamoja muda mrefu wakati mwingine kuanzia asubuhi mpaka jioni na tumekuwa tukimwona Mungu kwa namna ya kipekee isiyokuwa ya kawaida tofauti na pale mwanzo kila mtu alipokuwa kivyake.
Unawakumbuka wale watu wawili waliokuwa wanatoka Yerusalemu na kuelekea Emau, Njiani wakati wanazungumza habari za kufufuka kwake Yesu, Bwana mwenyewe aliwatokea na kuungana nao pasipo wao kujijua, baadaye kabisa mwishoni ndipo walipofunguliwa macho na kufahamu kuwa Yule alikuwa ni BWANA YESU mwenyewe(Luka 24).
Vivyo hivyo na wewe utakapojumuika na mwenzako au wenzako na kuanza kumzungumzia Bwana Lile Neno lake la ahadi lazima litimie. Na safari yako ya ukristo haitahitaji nguvu nyingi.
Natumai ushuhuda huu utakufanya uchukue uamuzi wa kujumuika na ndugu aliye moja na wewe.
Bwana akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano, maombi/ushauri/ubatizo/ whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
TUSIFUNGWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.
KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?
Kuna hatari kubwa sana kuidharau Neema ya Bwana YESU KRISTO, Katika agano la kale, kule jangwani Mungu alipokuwa anazungumza na wana wa Israeli katika mlima SINAI, Utukufu wa Mungu ulikuwa ni mkubwa kiasi kwamba hata watu wenyewe walikataa kuukaribia ule mlima kwa jinsi ulivyokuwa unatisha, kwa hofu na kwa kutetemeka walifikia hatua ya kumwambia Musa azungumze nao lakini sio Mungu. Mlima ule ulitisha sana hata kwa mnyama yoyote aliyeusogelea ilikuwa ni kifo.
Biblia inasema; katika Waebrania 12:18-25
“18 Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,
19 na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine;
20 maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa, Hata mnyama akiugusa huo mlima atapigwa kwa mawe.
21 Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.
22 Bali ninyi mmeufikilia MLIMA SAYUNI, NA MJI WA MUNGU ALIYE HAI, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,
24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, ZAIDI SANA HATUTAOKOKA SISI TUKIJIEPUSHA NA YEYE ATUONYAYE KUTOKA MBINGUNI;”.
Kama biblia inavyosema sisi tulio kwenye AGANO lililo bora la DAMU YA YESU KRISTO, tunaukaribia mlima wa mbinguni(SAYUNI YA MBINGUNI) mbali na wana wa Israeli wao waliukaribia mlima wa duniani(SINAI),.. Ni dhahiri kuwa wale walioukaribia mlima wa mbinguni, ambao maelfu ya malaika wamekusanyika ndio walio karibu zaidi na Mungu kuliko hao wengine.Hivyo hawa wa mbinguni ndio wanapaswa wawe na hofu kubwa zaidi na wawe makini zaidi, kwasababu wapo karibu na Mungu, hivyo kosa moja linaweza likakugharimu mauti ya kiroho.
Na ndio maana biblia inasema
Wafilipi 2:12b-13 “ UTIMIZENI WOKOVU WENU WENYEWE KWA KUOGOPA NA KUTETEMEKA. 13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.”
Hii tunayoiita NEEMA, ni kweli ni NEEMA lakini sio neema kwa wakati wote, Inapochezewa au kutupiliwa mbali inageuka kuwa laana mbaya kuliko zote. Biblia inasema hali ya mtu Yule aliyeidharau hali yake ya mwisho inakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
2Petro 2:20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”
Pale unapojiita mkristo halafu bado unakwenda kwa waganga ili upate kitu Fulani, ukijifariji kwamba utatubu tu siku moja, kwasababu neema bado ipo!! Usidanganyike NEEMA haifanya kazi kwa namna hiyo shetani anataka ufikirie hivyo ili ukumbane na mauti ya kiroho kutoka kwa Mungu mwenyewe.
Unapojiita mkristo halafu bado ni mwasherati, mlevi, mwabudu sanamu, na huku unafahamu kabisa hayo uyafanyayo sio sawa, ukijifariji utatubu, kwasababu tunaishi chini ya NEEMA, biblia inasema ingekuwa heri kwako kama usingeijua ile haki, Ndugu utaangukia hukumu ya kifo cha kiroho,na ukishafikia hiyo hatua, ndio pale injili kwako inageuka kuwa upuuzi tu masikioni mwako au hadithi za kutunga, ROHO MTAKATIFU anakuacha na kuondoka, na ile hali ya kuugua ndani juu dhambi inaondoka kwako, kutenda dhambi kunageuka kuwa ni kitu cha kawaida, hapo hata uhubiriweje injili huwezi kugeuka unasubiria moto wa jehanum.
Shetani ndiyo agenda yake sasa hivi, kuwapofusha watu na hili Neno “tunaishi chini ya neema” na kusema Mungu ataturehemu tu! Hata tuwe watenda dhambi.. Kumbuka Neema ina pande mbili, kwa Yule anayeikubali ndio italeta manufaa chanya kwake, lakini kwa Yule anayeidharau na kuitupilia mbali inageuka kuwa LAANI kubwa mno.
Waebrania 10:26-29 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAIBAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI;
27 BALI KUNA KUITAZAMIA HUKUMU YENYE KUTISHA, NA UKALI WA MOTO ULIO TAYARI KUWALA WAO WAPINGAO.
28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni KITU OVYO, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?”.
Unaona hapo usitende dhambi za makusudi ukidhani neema itaendelea kudumu siku zote maishani mwako, Ndugu huu ni wakati wa kujitazama tena maisha yako ni wapi haujakaa sawa, unalega lega au vuguvugu. Fanya bidii usimame imara angali bado Roho wa NEEMA analia ndani yako uache dhambi, fanya hima usimfanyie jeuri kabla haujachelewa, kwa maana wakati wa wokovu uliokubaliwa ni sasa.
Tubu mgeukie Kristo aliye mkuu wa uzima wako, naye ni mwaminifu atakuosha na kukupa uzima wa milele.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano, maombi/ushauri/ubatizo/ whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.
USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.
Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?
Wakolosai 3:1 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, YATAFUTENI YALIYO JUU KRISTO ALIKO, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
2 YAFIKIRINI YALIYO JUU, SIYO YALIYO KATIKA NCHI.”
Kama wasafiri hapa duniani, kila siku shabaha yetu inapasa iwe ni kufika mbinguni kwa gharama yoyote ile, Biblia imetuambia “tuyatafute” na “kuyatafakari” yaliyo juu, ikiwa na maana kuwa kwa bidii zote na nguvu zetu zote, tutafute kanuni za kutufanya sisi kuingia mbinguni, tumeambiwa tuutafute kama vile tunavyotafuta fedha au kama hazina iliyositirika (Mithali 2:4),
> Mambo ya ulimwengu huu yasiwe kikwazo cha wewe kuikosa mbingu, unapaswa utumie hekima popote ulipo usiwe na kisingizio kwamba kitu fulani kimekusonga usimtafute Mungu, kumbuka wapo katika dunia hii hii matajiri wakubwa kuliko wewe na bado wanayafikiria yaliyo juu, na maisha yao ni kama wasafiri tu hapa duniani, kama mfano wa akina Sulemani katika biblia, japo alikuwa ni tajiri lakini aliyatafakari sana yaliyo juu ,
> Wapo wenye vyeo vikubwa kuliko wewe katika kizazi hiki hiki unachoishi lakini fikra zao na mawazo yao yapo mbinguni, usiku na mchana wanamwomba Bwana ufalme wake uje!, mfano ni kama Danieli alivyokuwa katika biblia,japo alikuwa mwenye cheo kikubwa lakini kutwa mara tatu alikuwa akimwomba Mungu kuhusu hatma yake na watu wake.
> Vivyo hivyo wapo maskini kuliko wewe, hawana chakula wala nguo wala mahitaji yoyote lakini mawazo yao na fikra zao si katika mambo ya ulimwengu huu bali mbinguni, japo wanapitia magumu, wanaishi kama wasafiri tu hapa duniani…Wanaishi kama Lazaro wa kwenye biblia, ingawa alikuwa anakula makombo lakini hakutupa wokovu wake chini.
> Wapo wenye shida nyingi kuliko zako; wagonjwa, walemavu, hawana watoto, mayatima, lakini kwao hayo yote si kitu, mawazo yao na fikra zao zimeelekea juu mbinguni, siku kwa siku wakijihakiki maisha yao wasianguke, wakijiepusha na maovu wasije wakaikosa mbingu.
Na wewe je! UNAYATAFUTA YALIYO JUU! Au FIKRA ZAKO ZIMEELEKEA JUU MBINGUNI? Katika hali yoyote uliyopo?..Kumbuka vya duniani vinapita, hivyo visiwe sababu ya wewe kukusonga na kuikosa mbingu. Anza sasa kutamani kwenda mbinguni.
Tunaishi katika muda wa nyongeza Bwana Yesu anakaribia kurudi.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.
MUNGU ALIKUWA ANAONGEA NA NANI ALIPOSEMA NA “TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU”,(MWANZO 1:26)?
KATIKA BIBLIA KUNA UFUFUO WA AINA NGAPI?
Huu ni wakati wa kuwa makini sana juu ya hatma ya maisha yetu ya rohoni, kwasababu tusipokuwa makini katika nyakati hizi na kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda tunaweza tukajikuta tunaangukia katika vifungo vya shetani pasipo hata kujijua.
Kumbuka shetani sasa hivi anatenda kazi ndani ya KANISA la Mungu, hawezi kutilia mkazo sana kwa watu wa nje walio waovu kwasababu hao ameshawapata siku nyingi..anakutafuta wewe unayejiita mkristo unayejiona umesimama. Na unadhani atakupatia wapi zaidi ya kanisani.? Huko ndiko kiti chake cha enzi alipokiamishia.
Bwana Yesu alizungumza hivi;
Mathayo 13:24-30
24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.
27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?
28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?
29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.
30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Kumbuka magugu na ngano ni vitu vinavyofanana sana, kwa kuviangalia huwezi ukavitofautisha mpaka vitakapokuwa vikubwa na kutoa mazao, Katika mfano huo tunafahamu kuwa aliyepanda hizo mbegu njema ni BWANA YESU na shamba lake ni KANISA. Tunaweza tukaona jinsi kanisa la kwanza lilivyokuwa safi, takatifu lisilojichanganya na mafundisho yoyote ya uongo au mapokeo yeyote ya kibinadamu, ni kanisa lililokuwa halina dosari,
Lakini baada ya shetani kuona hilo alianza kuja na mbinu za kuliharibu, hivyo aliiga njia ile ile ya kupanda mbegu kama vile Bwana alivyofanya. Ndipo akaanza kwanza kwa kupenyeza mafundisho ya uongo katikati ya kanisa la Mungu, kisha ile mbegu ya uongo ilipomea baadaye ikageuka na kuwa dini, na kukaa katikati ya kanisa la Mungu. Kuanzia hapo hizi mbegu mbili zikawa zipo pamoja zikishindana katika kanisani la Kristo.(Magugu na Ngano)
Mungu kwa kulifahamu hilo aliruhusu vyote vimee kwa pamoja mpaka wakati wa mavuno utakapowadia kwasababu kama tulivyoona magugu yakiwa machanga ni ngumu kuyatofautisha na ngano, yanafanana sana kwa tabia zao. Na Mungu aliposema yaache yakue pamoja ni kiashiria kuwa yote yapate mvua kutoka kwa Mungu.(Mathayo 5:45). Ikiwa na maana kuwa Mungu aliyaruhusu yafanikiwe katika njia zao kama vile tu zile mbegu njema zifanikiwavyo mpaka wakati wa mavuno utakapowadia. Yote yananyeshewa mvua, kumbuka hata manabii wa uongo wanatabiri kwa jina la Bwana na inatokea, wanaponya na kutoa pepo kwa jina la Yesu na yanawatii, lakini siku ile Bwana atawaambia siwajui nyinyi mtendao maovu. Kwasababu hawa walinyeshewa mvua moja na ngano halisi lakini ndani yao walikuwa ni magugu.
Hivyo Kanisa katoliki lilianza kujitokeza katika kanisa la Mungu kama GUGU la kwanza, enzi zile za kanisa la kwanza, lilianza na mafundisho tu (MBEGU), baadaye likaota mizizi na kujiundia dini inayofanana na ukristo katika kanisa, likazidi kusambaa katika shamba la Mungu na kusonga zile mbegu halisi za Mungu na ndio maana tunaona hili kanisa lilianza kuharibu mafundisho ya NENO LA MUNGU na kupachika mafundisho ya uongo na kama tunavyofahamu tabia halisi ya gugu ni kuharibu kile kilicho halisi, na ndio maana baadaye tunavyosoma katika historia liliuawa watakatifu wa Mungu zaidi ya milioni 68 waliojaribu kwenda kinyume na mafundisho yake ya uongo.
Na lilipofikia kilele likazaa na magugu mengine mengi yanayofanana ni hilo, yakifanya kazi moja, kuiharibu mbegu halisi ya Mungu. Lakini biblia inasema wakati wa mwisho ambao ndio tuliopo sasa, yale magugu na ngano vitatenganishwa, yale magugu yataanza kwanza kwa kufungwa matita matita kwasababu yapo mengi,
JE! HAYA MATITA MATITA NI NINI?..Haya si mengine zaidi ya MADHEHEBU, na watakaoyafunga ni akina nani? Hawa Si wengine zaidi ya wanaojiita viongozi wa dini lakini ndani ni mitume wa uongo (2Wakoritho 11:13).
Mhubiri yoyote anayekupeleka kwenye dini yake zaidi ya kukupeleka kwa Kristo huyo ni mvunaji anayekufunga katika mojawapo ya tita la magugu. Kiongozi anayekufundisha mafundisho yasiyotokana na utakatifu, anakuambia tu! Mungu ni wa rehema, huku hana habari na mambo ya toba au kuhubiri utakatifu yeye anakazania mambo ya ulimwengu huu tu, ujue huyo ni mvunaji anayetaka kukufunga katika mojawapo ya tita la magugu lililoandaliwa kwa ajili ya kuchomwa moto.
Mhubiri anayekuhubira kutwa kuchwa mafanikio tu! Agusii hata siku moja hatma ya maisha yako ya rohoni, anayekuhubiria Kristo harudi leo wala kesho..mkimbie huyo ni mvunaji wa siku za mwisho kazi yake ni kuwafunga watu wa namna hiyo wasiotaka kujihusisha na mambo ya Mungu bali wajihusishao na mambo ya ulimwengu huu tu.
Ukiona kanisa linakuambia hakuna kuzimu na mateso yake, au halitaki kudumu katika NENO LA MUNGU peke yake,linakuongoza katika ibada za sanamu ambazo Mungu amezipinga vikali, kimbia haraka sana hilo ni TITA la kukusanya watu wa dizaini hiyo wasiotaka kudumu kutenda mapenzi ya Mungu..
2Wathesalonike 2:10 “na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; KWA SABABU HAWAKUKUBALI KUIPENDA ILE KWELI, WAPATE KUKOLEWA.
11 Kwa hiyo Mungu awaletea NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.”
Na Kumbuka kila siku hawa wavunaji(Manabii wa uongo) na haya matita ya magugu yanazidi kuongezeka kuonyesha kuwa huu ni wakati wa mavuno wa siku za mwisho.
LAKINI NGANO HALISI NI IPI
Ukisoma mfano huo kwa makini utaona kuwa NGANO HALISI haijakusanywa katika matita matita mengi kama magugu yalivyofanywa, bali Ngano imekusanywa pamoja mara moja tu na kupelekwa ghalani. Kuonyesha kuwa bibi-arusi wa Kristo hatakuwepo kati ya mojawapo ya hivyo vikundi, Bibi-arusi hana utambulisho wa kimadhehebu. Baada ya kukusanywa maramoja atapelekwa ghalani (mbinguni). Ndugu tunaishi katika wakati wa bibi-arusi wa Kristo kukusanywa kwa ajili ya unyakuo. Na anakusanyikia wapi?.
Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika
Mathayo 24: 23 “Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.
24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.
26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.”
Hii Ikiwa na maana kuwa katika siku za mwisho watatokea mitume na manabii wengi wa uongo, na zitatokea dini nyingi na madhehebu mengi ya uongo, na kila moja likidai kuwa lenyewe lina Kristo, ili tu yapate kuwakufunga watu kwenye matita yao..lakini Bwana alisema yatakapowafuata na kuwaambia hivyo msisadiki?. Na ndipo wanafunzi wake wakamuuliza..kama hatutawasidiki hao basi tukusanyike wapi sasa? Jibu lake lilikuwa ni hili.
Luka 17: 37 “Wakajibu, wakamwuliza, WAPI, BWANA? Akawaambia, ULIPO MZOGA, NDIPO WATAKAPOKUTANIKA TAI.”
Mzoga ni NENO LA MUNGU, na TAI ni BIBI-ARUSI, Hivyo katika siku hizi za mwisho bibi-arusi safi wa Kristo hatakusanyika katika madhehebu na dini bali atakusanyika katika NENO LA MUNGU tu..yeye hatafungwa na dini bali atafungwa, ‘’na nini NENO linasema’’ Hicho tu. Hii ndio ndio nguvu Mungu aliyoiachia sasa hivi kwa bibi-arusi wake, kurudi katika imani ya Mitume, Biblia.
Hivyo ndugu jitathimini je! na wewe umefungwa kama magugu kwenye matita tayari kwa kuchomwa au unakusanywa ghalani mwa Mungu kwa NENO lake?. Kama umefungwa huko toka, sio kwa miguu bali kwa kugeuzwa moyo wako na kuligeukia NENO linachosema na sio mapokeo ya dhehebu. Kwasababu biblia inatuambia
1Petro 1:23 “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; KWA NENO LA MUNGU LENYE UZIMA, lidumulo hata milele.”
Hivyo Umeona hapo? Bibi-arusi amezaliwa kwa mbegu isiyoharibika KWA NENO LA MUNGU tu, na sio kitu kingine.
Ni maombi yangu kuwa utazaliwa mara ya pili kwa NENO LA MUNGU na kumtazama Kristo peke yake aliyekufia msalabani ili ufanyike kuwa ngano na sio gugu.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU