Title September 2019

MAFUMBO YA MUNGU.

Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tuyatakari maandiko pamoja, lakini kabla hatujaendelea mbele zaidi naomba ulitafakari fumbo hili fupi kwa muda kidogo, ukipata au ukikosa jibu endelea kusoma habari hii, nitakupa majibu mbeleni… Fumbo lenyewe ni hili “Daudi ananyoa hata mara mia kwa wiki lakini kidevu chake bado kina ndevu nyingi, Je! Unaweza kunielezea ni kwanini? ”….Tafakari kisha utanipa jibu baadaye.

Lengo la kusema hivi ni kuwa kitabu kinachoitwa biblia ni kitabu kilichobeba mafumbo mengi sana, ambayo wakati mwingine majibu yake yanaweza yakawa ni marahisi kama tu tukimruhusu yeye aliyeyatunga kutufunulia, lakini pale tunapokosa kupata majibu sahihi, hatutaki kukiri kuwa hatufahamu, matokeo yake tunaishia kuona labda biblia ilikosewa au pengine tunaishia kutoa tafsiri zisizo sahihi ili tu tuonekane tunafahamu kile kilichoandikwa, hakuna asiyejua biblia imejaa mafumbo mengi sana, lakini miongoni mwa hayo ni suala la uungu wa kiMungu, kama vile biblia inavyosema Mungu ni MMOJA tu, lakini inakuwaje Yesu naye anaonekana kuwa ni Mungu, Roho Mtakatifu naye ni Mungu kama Mungu ni mmoja…

Sasa tunapokosa majibu ya maswali kama haya huwa tunaishi kusema Mungu ni mmoja ila kagawanyika katika nafsi tatu zinazojitegemea..Majibu tunayoyatoa ni marahisi sana, lakini hatujui kuwa tunazua maswali mengi, hata kwa wale ambao hawamjui Mungu wa wakristo, ndio linawafanya waende mbali zaidi ya ukristo wanapopata majibu kama hayo ambayo hayaoenekani kwenye biblia..Lakini hiyo yote ni kwasababu tumeukwepa uongozo wa Roho Mtakatifu kutufundisha ni jinsi gani Kristo ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu Yule Yule asiyekuwa na mshirika mwingine pembeni.

Kipengele kingine ambacho nacho kimezua utata mwingi, tunakipata katika mstari huu:

Mathayo 16:13 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?

14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.

15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?

16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.

17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”.

Mstari huu, unatafsiriwa na wengi hususani kanisa Katoliki kuwa mwamba huo unaozungumziwa kuwa Bwana Yesu atalijengea kanisa lake ni Petro, hivyo inaamika tangu zamani kuwa sisi sote tumejengwa juu ya Petro, na yeye ndiye PAPA wa kwanza, na kanisa la Kwanza ndio kanisa Katoliki.. Lakini kiuhalisia hapo Kristo hamzungumzii Petro bali anazungumzia juu ya UFUNUO ambao Petro alifunuliwa na Baba yake wa mbinguni wa kumjua YESU KRISTO ni nani, ambao wengi sana walishindwa kuuju, huo ndio mwamba ambao kanisa linajengwa juu yake?….Kwamba kwa ufunuo huo ndio atakalolijengea kanisa lake na malango ya kuzimu hayatalishinda…

Hivyo pale alikuwa hazungumziwi Petro na Petro hakuwa Papa, yeye alioa ma-papa huwa hawaowi, Yeye hakusujudia sanamu mahali popote wala kumwomba Mariamu dua mahali popote, lakini Mapapa wanafanya hivyo….vile vile Petro alimkana Bwana, lakini kanisa haliwezi kumkana Bwana, vilevile injili kwetu kwa mataifa ililetwa na mtume Paulo kuliko hata Mtume Petro , hivyo ambaye angestahili zaidi kuwa mjenzi wa kanisa basi angekuwa ni Paulo na sio Petro…Hivyo tunapaswa tumwombe Roho Mtakatifu atusaidie sana katika kuyachambua maandiko..

1Wakorintho 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata MAFUMBO YA MUNGU.

11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.”

Kadhalika leo hii tukikosa shabaha ya ufunuo wa Roho kumhusu Yesu Kristo katika katika maisha yetu, hatutaweza kusimama wala kumshinda shetani, Tunapomwona Yesu Kristo kwa kiganja chake, mtoa rizki tu, wa kubariki tu, wa kutusaidia kutatua matatizo yetu ya kimwili tu!…Na hatumfahamu kama mwana wa Mungu aliyetumwa kutuokoa, na kututakasa na dhambi zetu, kisha atupe uzima wa milele.. hatutakaa kamwe tumshinde shetani. Tutakuwa matajiri wa mali, lakini maskini wa roho.

Sasa tukirudi kwenye fumbo letu juu, linalouliza “Daudi ananyoa hata mara mia kwa wiki lakini kidevu chake bado kina ndevu nyingi, Je! Unaweza kuelezea ni kwanini”?..Jibu ni kuwa Daudi ni KINYOZI, huwa ananyoa vichwa vya watu wengi kila siku, hivyo basi hilo halihusiani na kidevu chake…je! ulifikiri hivyo? Au ulifikiri kwamba Kidevu cha Daudi ndicho kinachonyolewa mara mia kwa wiki?..Kama ulifikiri kuwa ni kidevu cha Daudi ndicho kinachonyolewa mara mia kwa wiki, na ukatafuta na ukajitafutia sababu za nywele hizo kuota kwa kasi kiasi hicho basi fahamu kuwa ulikosea… Na biblia sehemu nyingi ndio ipo kwa mafumbo kama hayo hayo…Unasoma hivi, na kufikiri hicho unachokisoma ndio tafsiri yenyewe kumbe, umekosea pakubwa, tafsiri yake ni nyingine tofauti na hiyo uliyokuwa unaifikiria wewe, na Yesu Kristo kumwelewa haihitaji kumhakiki kwa andiko peke yake bali kwa Roho Mtakatifu, kwasababu maandiko pasipo Roho yanapotosha.

2 Wakorintho 3: 6 “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, BALI WA ROHO; KWA MAANA ANDIKO HUUA, BALI ROHO HUHUISHA”.

Bwana atusaidie sote tuweze kumwelewa yeye kwa utimilifu wote, kama anavyotaka yeye sisi tumwelewe.

Ubarikiwe na Bwana.

Kama hujampa Kristo Maisha yako, mlango upo wazi sasa, lakini hautakuwa wazi hivyo si siku zote, parapanda ya mwisho inakaribia kulia, na Kristo kuchukua watu wake waliokombolewa kwa damu yake, je! Una uhakika umo miongoni mwao?..una uhakika wa kwenda na Bwana atakapokuja?..Uamuzi ni wako.

Maran atha! Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

ANGALIA JINSI USIKIAVYO:

FIMBO YA HARUNI!

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?


Rudi Nyumbani

Print this post

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

Shalom! Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze maandiko, Katika kitabu cha Warumi Mlango wa 7, tunaona biblia imetaja kuwepo kwa vitu viwili, ambapo cha kwanza ni SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI, na cha pili ni SHERIA YA ROHO WA UZIMA Hizi ni sheria kuu mbili zinazofanya kazi ndani ya mtu. Leo tutazitazama hizi sheria ni zipi, na ni jinsi gani zinafanya kazi. Naomba usome taratibu, ukisoma haraka hutaelewa chochote!

Sasa kabla ya kuingia kuzitazama hizi sheria mbili hebu kwanza tujifunze nini maana ya sheria?..

Sheria ni mfumo au utaratibu uliowekwa na jamii Fulani au mtu Fulani ufuatwe bila shuruti, kwamfano jua kuchomoza mashariki na kuzama magharibi hiyo ni sheria iliyowekewa jua, ni lazima litii hiyo sheria pasipo shuruti, kadhalika maji ya mvua kutoka juu kuja chini hiyo ni sheria iliyowekewa, ni lazima yatii, haiwezekani siku moja mvua ikanyesha kutoka chini kwenda juu…kadhalika giza kukimbia mwanga hiyo ni sheria iliyowekewa giza, haiwezekani hata siku moja giza likazidi mwanga kwa nguvu….n.k, Sasa katika maandiko pia zipo sheria hizi mbili zinazotenda kazi katikati ya wanadamu..

1)SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI.

Hii ni sheria ya kwanza inayotenda kazi ndani ya mtu. Sheria hii kama jina lake lilivyo ni sheria ya dhambi na Mauti, yaani maana yake ni kwamba sheria hii inamlazimisha mtu kutenda dhambi hata kama hataki…kama vile jua linavyotii sheria ya kulimulikia jua, hiyo litatii hata kama lingekuwa na uwezo wa kukataa lisingeweza kubatilisha hiyo sheria..Na kadhalika sheria hii ya dhambi ilianza kufanya kazi baada ya anguko pale Edeni.

Adamu na Hawa walipokula tunda sheria hii iliingia kwao na kwa Watoto wao, kwamba ni lazima utende dhambi tu hata kama hutaki, na sheria hii inatenda kazi katika viungo vya mwili….

Ndio maana utaona mtoto mdogo anapozaliwa tayari kitendo cha kuzaliwa tu, hapo hapo anaanza kutenda dhambi, utaona siku kadhaa au miezi kadhaa, anaanza kuwa na hasira zisizokuwa na sababu, kabla hajaelewa jema na anaanza kuwa na kiburi ukimwita anakataa, ukimwambia afanye kitu saa nyingine hafanyi au anasusa vitu na kuwa na chuki na vitu visivyokuwa hata na sababu…. au utaona anaanza kuwa mkatili, anaweza kuona mjusi pale akamrushia hata jiwe na kumwua kikatili, Watoto wengine utaona wana miaka 5 lakini wameshaanza kutamani uasherati.n.k…Hiyo yote hafanyi kwa kupenda! Hapana! Ni sheria ambayo tayari kashazaliwa nayo ambayo inafanya kazi katika mwili wake…Inamlazimisha yeye kufanya dhambi hata kama hapendi au hajui. Hata kama mtu moyoni mwake hapendi hicho anachokifanya atajikuta tu anarudi kukifanya tena na tena…

Mtume Paulo aliitaja sheria hii na kusema katika

Warumi 7:20

“Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

21 Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.

22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,

23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.

24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?”

Na sheria hii mtu anazaliwa nayo na anaendelea nayo mpaka siku ile atakapozaliwa mara ya pili..na kupokea sheria mpya ya pili ambayo tutakuja kuiona mbeleni kidogo. Na kama mtu hatazaliwa mara ya pili basi sheria hii ya dhambi na mauti ataendelea nayo mpaka siku anakufa..Hakuna namna yoyote mtu wa kawaida anaweza kushindana na dhambi!! Hakuna!, Mtu yeyote hawezi kuishinda dhambi kwa nguvu zake, ni lazima atakuwa chini ya utumwa wa sheria ya dhambi…

Na kumbuka sheria hii haiitwi tu sheria ya dhambi peke yake hapana bali inaitwa sheria ya dhambi na mauti! Ikiwa na maana kuwa, ni sheria inayozaa mauti! Ya kimwili na kiroho…Kama Biblia isemavyo “Mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23)”..Na tena “roho itendayo dhambi itakufa (Ezekieli 18:4)”

Sasa mtu anayefanya punyeto, anayefanya uasherati unaojirudia rudia, anayetazama mara kwa mara picha za ngono, anayerudia rudia kutukana, anayerudia rudia kusengenya na kuchukia watu, na anayerudia rudia kuwekea watu vinyongo, na hapendi kufanya hivyo lakini anajikuta anafanya, mtu huyo yupo chini ya HII SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI! na ANAKUWA NI MTUMWA WA DHAMBI..Na mshahara wake ni MAUTI na ZIWA LA MOTO!!..

Lakini ipo sheria ya pili ambayo ilitengenezwa na Mungu mwenyewe kuimaliza nguvu hii sheria ya dhambi na Mauti, na hiyo si nyingine Zaidi ya SHERIA YA ROHO.

2) SHERIA YA ROHO

Sheria hii ilikuja Baada ya Bwana Mungu, kuona hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kushindana na dhambi wala kuishinda dhambi kwa nguvu zake..Kwa kupitia Roho wake Mtakatifu aliileta sheria hii mpya, ambayo ilimpasa Kristo aje kufa msalabani, na kutuachia sisi kipawa cha Roho wake Mtakatifu, Roho huyu Mtakatifu kazi yake ni kuleta sheria ambayo itatufanya sisi KUTIMIZA Sheria za Mungu na amri zake pasipo kusukumwa sukumwa wala pasipo kutumia nguvu nyingi…Yaana mtu tu unajikuta unaichukia dhambi na kuipenda haki!….wakati sheria ya dhambi na mauti ni kinyume chake, yenyewe inakufanya uchukie haki na kupenda dhambi hata kama ndani ya moyo wako huipendi ile dhambi. Lakini sheria hii ya Roho inafanya kazi kinyume chake..

Inamfanya mtu kujikuta tu! Anampendeza Mungu hata kama hajahubiriwa! Inamfanya mtu anajikuta anauchukia uasherati hata kama hajahubiriwa, inamafanya mtu anajikuta anamwogopa na kumheshimu Mungu pengine Zaidi hata ya mchungaji wake..Ndio hapo unamkuta binti anavaa tu nguo za kujisitiri hata kama hajaonyeshwa andiko lolote kwenye biblia. Kwanini? Kwasababu sheria ya mpya ya Roho inafanya kazi ndani yake…na hiyo ndio maana ya kuishi kwa Roho, kuishi kwa Roho sio kuishi kwa kuona maono! Au kwa kunena kwa lugha! Au kwa kutabiri hapana bali ni kuishi katika sheria mpya ya Roho wa uzima haleluya!!

Waefeso 5: 16 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sharia”.

Sasa jambo pekee la kufahamu lisilojulikana na wengi ni kwamba Mtu aipokeaye sheria hii mpya ya Roho wa Uzima ndani ya moyo wake, haimaanishi kwamba ile ya kwanza ya dhambi imeondolewa!! Hapana sheria ile ya dhambi na mauti bado ipo!, isipokuwa imefunikwa na sheria hii mpya! Ikiwa na maana kuwa endapo mtu huyu aliyeipokea sheria hii mpya ya Roho akizembea na kumhuzunisha Roho Mtakatifu hata kuondoka basi huyu mtu anairudia ile sheria ya kwanza ya dhambi na mauti ambayo bado ipo ndani yake! Ndio maana inahitajika umuhimu mkubwa sana wa kushika kile tulichozawadiwa.

Ndio maana utaona mtu alikuwa moto! Hata uasherati alikuwa hafanyi lakini kapoa na kuanza kuwa baridi na kurudia matapishi ya kwanza! Kuna hatari kubwa sana juu ya huyu mtu!!

Kwahiyo sheria hii mpya ya Roho kazi yake sio kuondoa sheria ile ya zamani ya dhambi bali kazi yake ni kuifunika!

Sasa swali linakuja nitaipataje sheria hii mpya ya Roho ndani ya Moyo wangu itakayonisaidia kushinda sheria hii ya dhambi?

Mtume Paulo aliendelea kusema katika…

Warumi 7:24 “Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.…..

Warumi 8 :1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;

4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho”

Umeona hapo? Dawa ya dhambi ni Kristo Yesu, kwanza kumwamini yeye, pili kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi! Wengi hawapokei msamaha wa dhambi kwasababu wanatubu tu kwa midomo na si toba halisi itokayo mioyoni mwao inayoambatana na kuacha vile walivyokuwa wanavifanya…Na cha tatu baada ya Toba, ni ubatizo sahihi, na cha mwisho ni kupokea Roho Mtakatifu…

Na baada ya kupokea Roho Mtakatifu ni kuishi kwa kutomzimisha Roho Mtakatifu(Waefeso 4:30)..hapo dhambi haitakuwa na nguvu juu yako! Hutahitaji mhubiri akuhubirie kuwa ulevi ni dhambi, hutahitaji askofu akuambie kuwa kuishi na mwanamke/mwanamume ambaye hamjaoana ni dhambi! Hutahitaji mtu akuhakikishie katika maandiko kwamba uvaaji mbaya ni dhambi na upakaji uso rangi, hamu ya kuwa mtakatifu na ya kujiepusha na uovu itakuwa inamiminika tu ndani yako…Msukumo wa kutamani uasherati wala wa kufanya punyeto na kutukana hutauona tena. Hilo Ndio agano jipya lililoletwa na Bwana wetu Yesu Kristo kwamba sheria za Mungu tuzimize ndani yetu pasipo kusukumwa sukumwa wala pasipo kuwa watumwa wa sheria..

Yeremia 31:31 “ Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”

Bwana akubariki.


Mada zinazoendana:

JE! “MAJIRA NA SHERIA” MPINGA-KRISTO ATAKAYOKUJA KUBALISHA NI KUPINDUA SIKU YA SABATO NA KUWA JUMAPILI?

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

BIBLIA ITUAMBIA TUSALIMIANE KWA BUSU TAKATIFU. HILI BUSU NDIO LIPI?


 

Rudi Nyumbani:

 

Print this post

DALILI NYINGINE INAYOUTAMBULISHA UZAO WA NYOKA

Shalom mtu wa Mungu, karibu tena tuyatafakari maandiko, leo tutaona dalili nyingine kubwa inayoutambulisha UZAO WA NYOKA..kama biblia inavyosema ulimwenguni kuna watu ambao wanafanya dhambi kwa makusudi huku wakijua kabisa watu wanaofanya hivyo wanastahili hukumu ya mauti lakini wao wanaendelea kufanya hivyo kwasababu ile hali ya kujali au kuchukua tahadhari haipo ndani yao(ukisoma Warumi 1:32 utaona jambo hilo), hao watu sio wachache ni wengi sana..Embu tuitazame hii habari fupi itatukumbusha kitu  kingine cha msingi.

Mathayo 28:1 “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.

2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.

3 Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji.

4 Na kwa kumwogopa, wale walinzi WAKATETEMEKA, WAKAWA KAMA WAFU.

5 Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa”………

11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka.

12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi,

13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. 14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.

15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.”

Sasa kama tukiwatazama hawa askari ambao walikuwa wanalilinda kaburi la Bwana Yesu, pindi tu walipomwona Yule malaika kashuka pale, walitetemeka kwa hofu kubwa wakawa kama wafu, Na unajua mfu tabia yake ikoje?, Mfu huwa hawezi kufanya lolote anakuwa ameganda tu hapo chini, ndivyo ilivyowatokea hawa, ile hofu iliwafanya washindwe hata kukimbia au kufanya kitendo kingine chochote isipokuwa kungojea tu lolote litakalotokea, ni wazi maono yale ya wazi yaliwaingia sana moyoni, walitamani ingekuwa ni ndoto lakini haikuwa hivyo lilikuwa ni jambo la wazi kabisa mbele ya macho yao..

Waliona walichokiona, walisikia walichokisia, kulikuwa hakuna namna yoyote ungewashawishi kuwa Bwana Yesu hajafufuka kwa tukio lile, lakini kwa kuwa walipenda pesa kama Yuda, wakajiamulia tu kuudanganya uma kwamba hakuna kitu kama hicho, japo  ukweli wote ulikuwa ndani yao..Hiyo ni mbaya sana. Ndugu Uzao wa Nyoka sikuzote huwa na tabii hii, hata kama ukizungumza na Mungu uso kwa uso, hata kama ukaona uweza wake wote na ukuu wake wote ni rahisi kuchukuliwa na jambo dogo sana, na hata kukana alichokiona dakika chache tu hapo nyuma.

Walichokiona askari hawa hakina tofauti na alichokiona Sauli wakati anaelekea Dameski kuwaua watakatifu, tofauti yao ni kwamba Sauli alitubu na kugeuka kwa mono yale, kuonesha kuwa yeye ni uzao wa Mungu, lakini hawa wengine walikwenda kusambaza uzushi pamoja na kwamba wameona maono makubwa kama yale… kuonesha kuwa wao sio uzao wa Mungu, ni uzao mwingine wa nyoka.

Wapo watu wengi leo Mungu kajidhihirisha kwao kwa namna nyingi sana, wengine Mungu kasema nao kwenye ndoto wazi wazi, wengine wametokewa na malaika, wengine wameonyeshwa maono mengi,wengine wameuona mkono wa Mungu waziwazi katika mambo yao, wengine wameepushwa na hatari nyingi na kusema kabisa hakika huyu ni Mungu wala hakuna pingamizi, wengine hata walimwomba Mungu awafanikishe katika vitu vyao akawafanikisha sawasawa na walivyomwomba kwa wakati waliomwomba, wakatetemeka na kusema kweli Mungu yupo… wakaogopa kweli kweli wakalia, wakazimia, wakawa kama wafu wakasema Mungu wangu kuanzia leo nitakutumikia, wengine wakasema ukinipa nafasi ya pili basi mimi nitakutumikia milele, mimi sitatenda dhambi tena kuanzia leo, lakini cha kushangaza akitoka hapo siku chache baadaye, au miezi michache mbeleni, pengine kakutana tu na vitu vidogo vidogo visivyokuwa na maana vya ulimwengu huu vinavyopita, utamwona karudi nyuma kwa kasi kubwa kana kwamba  hajawahi kukutana na Mungu hapo nyuma hata siku moja…

Tena anaweza akawa ndio wa kwanza kuzungumza maneno ya mzaha kuhusu kazi ya Mungu au watumishi wake, lakini ndani ya moyo wake anajua kabisa Mungu alishawahi kumtembelea na kumwambia atubu. Watu kama hao wapo wengi sana inawezekana mmojawapo ni wewe unayesoma habari hii… Fanya utafiti uangalie utaona wale ambao hawajawahi kuuona uweza wa Mungu mwingi wale ambao Mungu anajihirisha kwao mara chache sana hao ndio wanaodumu na wanaomtumikia Mungu kwa moyo thabiti kuliko hawa wengine….na ndio maana Bwana Yesu alimwambia Tomaso heri wale ambao wameamini bila kuona..kwasababu alijua ugumu wa hawa wengine..

Ndugu unaendelea bado kumtumikia shetani na umesahau Mungu aliyokutendea hapo nyuma..Usidhani yataendelea kujirudia rudia hivyo kila siku, wakati utafika Roho wa Mungu ataondoka moja kwa moja ndani yako, utakachokuwa unangojea ni adhabu kubwa kuliko hata ile ya watu wa Sodoma na Gomora, Bwana Yesu ndio alisema  hivyo kama wale wangeona Ishara na maajabu Mungu anayowatendea watu leo hii, miji ile ingekuwepo hadi leo, hivyo basi akasema itakuwa rahisi kwa watu wale kustahimili adhabu kuliko sisi tuliyoyaona na kuyakataa.

Ndugu salimisha maisha yako kwa Bwana kithabiti..Anapokuita sio kana kwamba anataka kukunyima haki yako ya kuchagua unayoyataka hapana, lakini anakupenda UPEO hataki upotee hata unywele wako, hataki uende kuzimu hilo tu!…Tubu sasa ukabatizwe katika ubatizo sahihi, uanze kuuishia wokovu katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho duniani. Usikubali uwe sehemu ya UZAO wa nyoka ambao hata uhubiriweje injili na kuona maajabu yote hauwezi kugeuka..Naamini wewe sio mmojawapo na kwamba utapoisikia leo hii utageuka na kumwishia Kristo.

Ubarikiwe sana. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki.


Mada zinazoendana:

UZAO WA NYOKA.

WATU WASIOJIZUIA.

UZAO WAKO UTAMILIKI MALANGO YA KUZIMU

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.

Shalom, Mtu wa Mungu, karibu tulitafakari kwa pamoja Neno la Mungu, biblia inasema Neno la Mungu ni Taa iongozayo miguu yetu na mwanga wa njia zetu (Zab.119:105), hivyo ni vyema tukalitafakari hilo kila kukicha ili njia yetu iwe safi na salama..(Zab.119:9 “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako”).

Kama tunavyojua wengi wetu kwamba tunaishi katika siku za mwisho, na sio siku za mwisho tu! Bali ukingoni mwa siku za mwisho…Kwasababu siku za mwisho zilianza tangu zamani, sasa tupo ukingoni mwa hizo siku..Na kama tunavyojua ishara kubwa ya kututambulisha kuwa tupo ukingoni ni KUNYANYUKA KWA TAIFA LA ISRAELI. Ukienda kila mahali utasikia Israeli, Israeli..dunia ina mataifa mengi lakini ki-nchi kidogo kama kile kinavumisha upepo wa dunia na kuwa mada ya kuzungumziwa katika siasa yote ya dunia? Kuna nini pale?…Ni wazi kuwa kuna jambo la kiroho linaendelea kwenye Taifa hilo…Ndugu yangu hebu kama hujafuatilia ni nini kinaendelea kwenye Taifa hilo hebu tenga angalau wiki moja usiingie hata kwenye mitandao kuchat, tenga muda ulifuatilie kwa makini, soma historia ya Taifa hilo kwenye Biblia na kwenye historia…Ndio utajua tunaishi kipindi gani.

Wengi wetu tumezaliwa kipindi ambacho tunaambiwa kuna Taifa la Israeli, lakini wengi wetu hatujui kuwa Waisraeli wenyewe halisi, hawakukaa kwenye taifa lao, na kuwa na Mfalme wao wenyewe kwa takribani miaka 2,500 mpaka ilipofikia juzi tu mwaka 1948 ndipo wakarudi kuwa Taifa huru na kuwa na Raisi wao wenyewe…Kabla ya hapo walikuwa wametawanyishwa kwenye mataifa yote.

Sasa kama tunavyojua Kuwa Hawa Waisraeli tunaowaona, hawakua hivi, kwenye karne kadhaa huko nyuma… walikuwa wametawanyishwa katika Mataifa yote duniani, maandiko yanasema hivyo….Sasa kwanini Mungu aliwatawanyisha kwenye mataifa yote?..Jibu ni ili sisi watu wa mataifa tupate Neema, kwani Baada ya wayahudi (yaani waisraeli) kumkataa Masia wao Yesu Kristo, Bwana aliwaambia maneno haya…

Luka 21:20 “Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.

21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.

22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.

23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.

24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara NA KUCHUKULIWA KATIKA MATAIFA YOTE; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia”

Sasa Swali lingine linakuja…Wayahudi/Waisraeli kutawanywa kwenye mataifa yote ina uhusiano gani na sisi watu wa mataifa kupata Neema?…Yaani wengine waumie ili sisi tupate Neema?..Wengine wachukuliwe mateka ndipo sisi tupate Neema?..Kwani Mungu hawezi kuwaacha tu wawe salama, na kutupa Neema wote sisi na wao?.

Ni swali zuri lakini ni vizuri pia kujua kuwa ili kimoja kipate uzima ni lazima kingine kife! Kwamfano ili ule tunda na kupata virutubisho vilivyomo ndani yake ni lazima ulichume kutoka kwenye mti, ulitafune na kulisagasaga…hapo ni sawa na umeliua…ili ule nyama ikusaidie kwa protini ni lazima mnyama Fulani auawe, huwezi kula kitu kizima…kadhalika ili upate kitu Fulani ni lazima hicho kitu kiwe kimepunguka kutoka sehemu Fulani, hata fedha mtu anazozotafuta ni kwamba zimepunguka sehemu Fulani zikaenda kwa huyo mtu, ikiwa na maana kuwa endapo ukifanikiwa kuzikusanya zote basi kwingine kutakuwa kumepunguka pia pakubwa, kwahiyo hakuna kuongezekewa kama hakuna kupunguka sehemu Fulani nyingine…wala hakuna kupata heshima Fulani kama mwingine hajapata dharau, hata cheo, au nafasi,ni lazima mmoja aondoke mwingine aingie…. Mambo ndivyo yanavyokwenda hivyo…Kwahiyo ili sisi watu wa Mataifa tupate heshima mbele za Mungu ni lazima wawepo wengine walioharibu mahali Fulani.

Kwahiyo Waisraeli walipomkataa Yesu na injili yake, wakawa wamejiharibia wenyewe hivyo hiyo ikawa faida kwetu sisi watu wa mataifa ndio maana Mtume Paulo aliwaambia..

Matendo 13:44 “Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.

45 Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.

46 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.

47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

49 Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote”.

Kwa dhambi hiyo walioifanya Mungu hakuishia tu kuwapokonya injili bali pia aliwatawanya kwenye mataifa yote, na hiyo pia ikawa ni faida ya PILI kwetu.

Kumbuka popote wayahudi wanapopelekwa, mahali pale lazima pabarikiwe hata kama wamepelekwa kwa makosa yao…mfano utaona Yusufu alipoingia Misri pamoja na wana wa Israeli wote, Taifa la Misri lilibarikiwa sana…Farao hakufa na njaa, na zaidi ya yote Farao aliyekuwa mtu wa Mataifa alipata nafasi hata ya kuoneshwa maono na Mungu mwenyewe, jambo ambalo si la kawaida Mungu kuzungumza na watu wamataifa.

Kadhalika utaona wakati Wana wa Israeli tena wamepelekwa Babeli utumwani, Mungu aliibariki Babeli kwa ajili ya wana wa Israeli waliomo mule, Babeli ilizidi kustawi, na pia Mfalme Nebukadneza alipata hadi Neema ya kuoneshwa maono na Mungu ya wakati ujao, jambo ambalo sio la kawaida Mungu kuzungumza na watu wa Mataifa, hiyo ni kutokana na waisraeli waliokuwepo kwenye hiyo nchi, ijapokuwa walipelekwa kule kwa dhambi zao lakini bado kulikuwa na Baraka Fulani za kimwili na kiroho zilizokuwa zinaambatana nao.

Kadhalika kipindi cha Esta, Mfalme Ahasuero alifanikiwa katika enzi yake kwasababu ya Esta, Mordekai pamoja na Wayahudi waliokuwepo kwenye ufalme wake..

Na sehemu zote ndio hivyo hivyo, popote Wayahudi walipokwenda kulibarikiwa mwilini na rohoni.

Vivyo hivyo katika siku zile baada ya kumkataa Yesu Kristo, walipotawanyishwa tena kwenye mataifa yote ulimwenguni, popote walipokaribishwa sehemu zile zilibarikiwa kimwili na kiroho, Ukiangalia mataifa mengi ya Ulaya, mafanikio yao yametokana na Wayahudi waliokuwemo kule kipindi kile, kadhalika na Marekani, na nchi nyingine zote…baraka zao ni kwasababu ya waisraeli waliowakaribisha kipindi wanatawanywa.. na Mungu kayabariki mataifa yote kwasababu ya Israeli na Baraka kubwa aliyowabaikia ya rohoni, ni KUWAPA MATAIFA ZAWADI YA YESU KRISTO. Hiyo ndio zawadi kubwa Mungu anayoweza kumpa mwanadamu…Kwahiyo sisi kuzawadiwa Yesu Kristo yaani kuzawadiwa hii Neema ya kumkubali Yesu Kristo ni kutokana na Wayahudi kuwemo humu mataifani, tulimo sisi.

Lakini cha kuogopesha ni kwamba wayahudi sasa wameshaanza kurudi nchini kwao, kidogo kidogo wameshaanza kuhisi makosa yao waliyoyafanya miaka 2000 iliyopia, mioyo ya kutubu kidogo kidogo imeanza kurudi ndani mwao, mamia kila siku wanamiminika kurudi kwao, hiyo ni ishara ya nini?..Ni ishara kuwa Neema inaondoka huku…Zile Baraka zinaondoka huku, baraka za rohoni na za mwilini…Kumbuka Baada ya majeshi ya Israeli kutoka Misri nini kilitokea huko nyuma?, jibu ni mapigo! ..hakuna Neema tena! Hujasikia tena tangu hapo na kuendelea Mfalme yeyote wa Misri anaota zile ndoto za kiMungu tena! Wala hujasikia chochote cha maana kilichokuwa kinaendelea Misri…Hiyo yote ni kwasababu Uzao wa Mungu umerudi kwao, na Bwana amewarudia watu wake.

Kadhalika wana wa Israeli waliporudi nchini kwao, baada ya kuchukuliwa Babeli, hutaona Mungu akishughulika tena na Babeli, au Umedi au Uajemi…Habari zao ndio zilikuwa zimeishia pale, sasa Mungu anarudi kushughulika na watu wake Israeli.

Ndugu, Hii Neema ipo ukingoni, hivi karibuni! Wayahudi wanakwenda kutubu kabisa kabisa! Na Bwana atawasamehe, na atawamwagia kipawa chake cha Roho, na wakati huo huo Roho Mtakatifu atakuwa ameshaondoka huku kwetu mataifani, yaani unyakuo utakuwa umeshapita! Kitakachokuwa kumesalia ni dhiki kuu na siku ya Bwana inayotisha!, Bwana akirudi leo hatutasema hatukusikia wala hatukuona, vyombo vya habari vinatuhubiria injili kila mahali, mtu asipotaka kuyatilia maanani basi ni kwa uzembe wake mwenyewe, mwenye macho haambiwi tazama, mwenye masikio haambiwi sikia

Ikiwa hii neema ambayo inafifia unaichezea, moja ya hizi siku itazima kabisa..Jitathimini wewe mwenyewe umesimama upande upi.

Maran Atha!

Tafadhali share na kwa wengine, Mungu akubariki.


Mada Zinazoendana:

Print this post

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

Biblia inatuambia moja ya kazi ya malaika ni kuwahudumia watakatifu, (Waebrania 1:14) na tunajua siku zote kama mtu ni muhudumu ni lazima akae eneo husika la wale anawahudumia, kwamfano Daktari anafanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa, japokuwa anao kwake mwenyewe lakini huwezi kumkuta masaa yote yupo nyumbani bali muda wake mwingi utakumkuta anakesha mahospitalini, kwasababu huko ndipo wagonjwa walipo. Vivyo hivyo na malaika wa Bwana, wamepewa jukumu la kuwahudumia watakatifu, sasa japo makazi yao ni mbinguni lakini muda wao mwingi wapo duniani wanazunguka huko na huko kuhakikisha yale yote yaliyokusudiwa na Mungu juu ya watakatifu yanatimia.

Hivyo tusichokujua tu ni kuwa hata sasa tunapozungumza kuna mamilioni ya malaika wanaozunguza duniani kila siku, na kazi yao ni moja kuhakikisha kusudi la Mungu linatimia kwa namna zote. Na malaika kama biblia inavyotuambia ni viumbe wa rohoni hivyo Mungu amewapa uwezo wa kuchukua maumbile tofauti tofauti, wanaweza wakatembea kama nguzo ya moto, au wingu, au taswira za mnyama, au taswira ya mwanadamu. Kwahiyo katika sikuzote za maisha yako, kwa namna moja au nyingine ulishawahi kukutana au kupishana na malaika wa Mungu wengi pasipo hata wewe kujijua, Na ndio maana Mtume Paulo anasema:

Waebrania 13:1 “Upendano wa ndugu na udumu.

2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.”

Tukimwangalia Ibrahimu siku moja wakati amekaa nyumbani kwake ghafla aliona watu watatu wamesimama nyumbani kwake, Lakini Ibrahimu hakuwafukuza au kuwaita wapepelezi badala yake yeye ndiye aliyewashurutisha waangie nyumbani mwake wale na wanywe, na kumbe walikuwa ni malaika wa Bwana pamoja na Bwana mwenyewe wakiwa katika safari yao ya kwenda kuupeleleza mji..

Vivyo hivyo hao hao waliposhuka Sodoma, Lutu alipowaona kuwa ni wageni sio wenyeji wa pale hakusubiri wafike nyumbani kwake bali yeye ndiye aliyewakimbilia na kuwaambia waingie kwake! Wale na wanywe na walale, lakini wale watu walikataa kata kata, lakini Lutu hakuacha kuwashurutisha sana, na walipokubali baadaye ndipo Lutu alipojua kuwa wale hawakuwa watu wa kawaida.. Na Kuwafadhili wageni

 Sio lazima tu iwe wale wanaotaka kuja kulala nyumbani kwetu, lakini pia kuwatendea ukarimu wale ambao wanaonekana wanahitaji msaada kwa wakati huo, hususani wale tusiowajua….na ukarimu huo unaweza ukawa chakula, fedha, ushauri, n.k.

Biblia inatukumbusha tuwe wakarimu, ni wazi kuwa dunia ya sasa upendo umepoa kila mtu anajipenda nafsi yake, zamani ilikuwa mwenyeji ndio anamshurutisha mgeni aje kwake, lakini sikuhizi mwenye hitaji ndio anamshurutisha mwenye nacho amsaidie, na bado anaweza asiambulie chochote, utakuta muda mwingine unapishana na mtu barabarani anakuambia ninasikia njaa sijala, na hakuombi hata pesa anakuomba tu ukamnunulie muhogo mmoja pale apooze njaa! Utasikia huyo mtu anasema, mimi sina kitu na ukiangalia mfukoni ana kiasi tu kikubwa cha fedha ambayo haina matumizi imekaa tu kwenye pochi.. mwingine atakuambia naomba unilipie nauli, utaona mtu anasema sina pesa, lakini ukweli ni kuwa anayo lakini hataki kumpa, Ndugu kama unacho chochote wewe mpe tu! Sio lazima kiwe kingi, hata kama kakudanganya usijali chochote, kwa maana hujui huyo aliyekuomba ni nani?.

Mwingine hataonyesha dalili ya kukuomba chochote, lakini wewe ukimtazama utaona anao uhitaji Fulani, na huku ukiangalia una vichenchi chenchi vimebaki mfukoni wewe mpe tu, kwasababu hujui huyo unayempa ni nani…Lakini simaanishi  kwamba uumpe tu kila mtu, hata kama mtu anahitaji pesa ya sigara au pombe au madawa ya kulevya uumpe hapana!..Mtu wa namna hiyo hapaswi kupewa chochote kwasababu mtu mwenye shida kweli ya msingi hawezi kuomba vitu kama hivyo, vilevile hata malaika wa Bwana hawawezi kufanya hivyo. Ukimkuta Mtu kalewa halafu anakuomba kitu usimpe chochote, ukimkuta mtu kashika sigara halafu anakuomba usimpe! Mpe kwanza injili n.k

Lakini mbali na hao asilimia kubwa ya wengi wanaotuomba wanao matatizo..pengine hata wewe ilishakukuta ulifika wakati ulitamani mtu akusaidie kitu Fulani, pengine hata sio chakula, bali kitu Fulani kingine cha muhimu sana ambacho unahitaji tu kwa muda huo na hauna….sasa watu wa namna hiyo wapo mamia kwa mamia… tuwasaidie kwa vidogo tulivyo navyo. Utajisikiaje siku ile umefika mbinguni halafu malaika kama 100 wanatokea kila mmoja anakuambia ulishawahi kunisaidia mara 2 nilipokuwa duniani. Ni furaha kiasi gani unadhani Bwana Yesu ataona fahari juu yako kiasi, lakini siku ile mfano unafika na unaona malaika hawana habari na wewe, wakati unashangaa hilo  wanakuambia ulishawahi kutufukuza, au ulishawahi kutunyima kitu Fulani tulichowahi kukuomba tukiwa  duniani. Na wakati haukutani na malaika bali na MKUU mwenyewe Bwana Yesu, sasa tukiwa wabinafsi kila wakati kuna hatari kubwa sana ya kukosa mema Mungu aliyotuandalia..

Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.

34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?

40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”

Bwana akubariki. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine.


Mada zinazoendana:

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

JE! BAADA YA ULIMWENGU HUU KUISHA MALAIKA WATAKUWA NA KAZI GANI TENA?

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

MALAIKA WA MAJI NI NANI? (UFUNUO 16:5)


Rudi Nyumbani:

Print this post

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.

Watu wengi sana sio tu wasiomjua Mungu bali hata miongoni mwa wakristo, wakisikia jambo hili kuwa siku moja kuna kusimama hukumuni huwa linawatesa sana, na kuwahuzunisha sana na hilo linawafanya waishi Maisha ya wasiwasi mwingi. Lakini habari njema ni kwamba biblia inatumbia hukumu inakwepeka
.
 
Leo tutajifunza ni kwa jinsi gani tunaweza kuikwepa hukumu ya Mungu inayotisha, Na andiko pekee linalotuambia habari hiyo ni hili..
 
Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.”
 
Kama wengi tunavyofahamu huyu aliyesema maneno hayo ni Bwana wetu Yesu Kristo, lakini swali linakuja palepale je! Huko kumwamini Bwana kukoje, je! Ni kuamini tu kama yeye yupo?, au kumwamini tu kama yeye ni mwokozi mpaka kutufanya tusihukumiwe au vipi?. Mbona tumesikia wengi wamemwamini Kristo lakini wapo kuzimu?
 
Tusisahau kuwa biblia inatuambia hata mashetani wanaamini na kutetemeka, (Yakobo 2:19 ) wanaamini Yesu ni mwokozi, wanaamini maneno ya Mungu kuwa ni kweli,..hivyo hapo tunapaswa tujue biblia inapotuambia tumwamini Yesu na yeye aliyempeleka ni Zaidi ya kumfahamu tu wasifa wake.. Mfano ni sawa na umekutana na njia mbili mbele yako ukaona kibao kimoja kinasema kushoto ni shuleni, na kulia ni Sokoni, na wewe ukiangalia ulikuwa unatafuta mahali soko lilipo…Ni wazi njia ile ya kibao kinachokuelekeza sokoni utaiamini Zaidi kuliko ile ya kibao kinachokuelekeza shuleni..Sasa hiyo ni hatua ya kwanza, hatua ya pili ili ufike unapotaka kwenda ni sharti uifuate ile njia kwa gharama zozote hata kama itakuwa ina vumbi, na mikunjo kunjo haipendezi kama ile ya shule, utaifuata tu, lakini ikiwa hutaifuata na huku bado unataka ufike sokoni, ni wazi kuwa hutafika popote haijalishi umeifahamu njia sahihi kiasi gani.
 
Vivyo hivyo na kwa Bwana Yesu kumwamini tu pekee yake kuwa amekuokoa kwa kuongozwa sala ya toba, haikufanyi wewe usisimame hukumuni siku ile..Ni sharti uonyeshe kwa vitendo kuwa umemwamini yeye kwa kuifuata njia ya uzima, na vitendo hivyo ndivyo vinavyojulikana kama TOBA.
 
Toba ni kitendo cha kugeuka na kuanza safari kule ambako haukuwepo.. Sasa ikiwa mtu atakamilisha tu agizo hio basi Hukumuni hataingia.
 
Na hiyo inakujaje, mfano ikiwa leo hii umempa Kristo Maisha yako kwa mara ya kwanza, ukatubu dhambi zako zote ukaenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, kumbuka muda huo bado mbingu haifanya chochote juu yako, bali inakuangalia kwanza, mwenendo wako, je! Ni kweli alichotubia na alichobatiziwa unakitelekeza kwa vitendo, je ni kweli huendi disco tena, je ni kweli huangalii picha chafu tena kwenye mitandao?, je ni kweli hauendi bar tena, je ni kweli hufanyi uasherati tena…sasa Mungu akishaona mtu huyu kageuka anazidi kupiga hatua kila siku katika kuielekea njia ya uzima…mtu wa namna hiyo hata kama hatakuwa mkamilifu wote, tayari mtu huyo anahesabiwa haki na mbingu kama mtakatifu..na hiyo ndio maana ya neema.
 
Hata ikitokea hajafikia ule utimilifu wote halafu akafia njiani mtu huyo moja kwa moja siku ile hataingia hukumuni. Kwasababu alikuwa anaonyesha nia ya kuelekea katika njia ya uzima..Mfano hai ni ule wa kipindi cha Sodoma na Gomora pale Lutu alipofuatwa na wale malaika, hawakumteketeza Lutu na wale watoto wake wawili sio kwamba walikuwa ni wenye haki sana mbele za Mungu hapana lakini pindi walipoonyeshwa tu njia ya uzima wao, wa kujiponya nafsi zao waliindea njia hiyo hiyo bila kugeuka nyuma, na mwisho wa siku wakajikuta wameokoka,Lakini mke wa Lutu aliyatamani ya nyuma japokuwa alitokewa na malaika japokuwa aliiamini ile njia kweli lakini moyo wake haukudhamiria kwa dhati kuifuata ile njia na ndio maana akawa jiwe la chumvi.
 
Ndugu ikiwa umemwamini Kristo halafu bado unatembea huku unageuka geuka nyuma, haijalishi ulitokewa na malaika wangapi siku ile ulipoamini,haijalishi ulitokewa na YESU mwenyewe, Kwenda hukumuni hakukwepeki, na unajua anayepandishwa hukumuni sikuzote ni mshtakiwa na hakuna mtu yeyote anayeweza kuyakwepa au kuyashinda mashtaka ya Mungu juu yake…bali wote watakaopanda hukumuni wataingia kwenye ziwa la moto..
 
Fahamu kuwa Mungu hatuhesabii haki kwa matendo yetu, vile vile usisahau hatuhesabii haki kwa matendo yetu maovu, lakini anaangalia ule moyo unaotamani kuhesabiwa haki ndio anaupa Haki, na moyo wowote wa namna hiyo siku zote utajitahidi kuishi Maisha ya haki kwa gharama zozote na ndipo Mungu anamalizia kuupa haki yote kwa neema yake.
 
Ikiwa hukulifahamu hilo basi huu ndio wakati wako sasa wa kuonyesha Imani yako kwa matendo, acha kwa moyo mmoja mambo yote mabaya na ya aibu uliyokuwa unayafanya huko nyuma, ulikuwa unaangalia picha za ngono, acha ulikuwa unafanya mustarbation acha, ulikuwa unafanya uzinzi acha, ulikuwa unavuta sigara acha, ulikuwa unatoa mimba acha, ulikuwa unauza madawa ya kulevya au unatumia acha, ulikuwa unatukana tukana ovyo acha, ili Mungu akuone nia yako amalizie kukupa HAKI YOTE bure,..hata ukifa leo uwe na ukakika wa kuingia uzimani bila kupita hukumuni.
 
Warumi 8:1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu”.
 
Ubarikiwe sana.
 
Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki.

Mada zinazoendana:

KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?

UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.

UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.

KAMA MHUBIRI NI WOKOVU UPI UNAUPELEKA KWA WATU?

Rudi Nyumbani:

Print this post

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

Wakati mwingine, unaweza ukapitia hali ya kusemwa vibaya, kwa siri au hadharani, Tambua tu hiyo ni hali ya kawaida, wewe sio wa kwanza, hata walio watu wakuu na wakubwa na wanaoheshimika wanasemwa vibaya, hata kama wamefanya mazuri mangapi katika jamii, eneo la kuzungumziwa vibaya, haliepukiki katika Maisha yao.
 
Mtu aliyekuwa mkamilifu, na asiye na dhambi, na Zaidi ya yote ni Mungu, (Bwana wetu Yesu Kristo) alisemwa vibaya mara nyingi sana, sasa kama yeye alisemwa vibaya na alikuwa hana dhambi hata moja! Wewe ni nani usizungumziwe vibaya?..Kwahiyo hilo ni jambo ambalo halikwepeki maadamu bado tupo hapa duniani..Wakati mwingine unaweza ukaambiwa maneno makali hata na watu wako wa karibu sana, ambao usingeweza kutazamia kama wangekwambia maneno hayo…
 
Mfano katika Biblia tunamwona mtu mmoja aliyeitwa YEFTHA, Huyu alikuwa mzaliwa wa kwanza kwa Baba yake, lakini mama yake alikuwa ni kahaba, kwahiyo alizaliwa na mama kahaba, na baadaye Baba yake akaoa mke wa halali akazaa naye Watoto, lakini hao Watoto walipokuwa mkubwa wakamtamkia hadharani Yeftha kwamba hatakuwa mrithi pamoja nao kwasababu yeye ni mwana wa mwanamke mwingine kahaba, wakamfukuza..Na niwazi kuwa pia walitaka kumdhuru maana aliwakimbia na kuhamia kabisa nchi nyingine, na sio tu ndugu zake walimchukia, bali na Taifa zima lilimtenga. (Habari hizi utazipata katika kitabu cha Waamuzi Mlango wa 11 na kuendelea).
 
Kwahiyo Yeftha akaondoka katika nchi yake, akiwa peke yake, watu maskini wasio na maana (mabaradhuli) waliochoka kama yeye, wakaenda kuungana naye huko alikokwenda… Lakini Mungu alilitazama teso lake, wakati ulipofika alimnyanyua Yeftha kama alivyomnyanyua Yusufu, na akawa MWAMUZI katika Taifa Teule la Mungu (Israeli)..Shujaa wa Bwana,haleluya!!..Wale wote waliomfukuza walikuja kumwomba msaada kwa kumsihi sana, Taifa zima lilikuja kumwomba msaada katika vita. Kwasababu maandiko yanasema katika
 
1Samweli 2 :6 “Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.
8 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake”.
 
Sasa leo tutajifunza ni namna gani tutashinda hali ya kusemwa au kutamkiwa maneno mabaya. Unajua wanadamu wote tumeumbwa na moyo, moyo kwa lugha nyingine tunaweza kusema ni (utu wa ndani), sasa uwezo wa moyo kuhifadhi hisia au maumivu ni mkubwa kuliko mwili, kidonda cha mwili kikipona kimepona kikishabaki kovu kinakuwa sio kidonda tena, hata upaguseje pale hapawezi kusababisha maumivu tena, Zaidi ya yote pakipona ndio panaweka gamba gumu zaidi(sugu)…kwasababu kidonda kimeshapona…Lakini moyo haupo hivyo, vidonda vyake haviponi kirahisi hivyo na inaweza ikapita miaka hata 10, lakini pale palipoumizwa pakiguswa tena kidogo tu! Ni kama umeanza mwanzo tena.
 
Kwahiyo hapo ni kuwa makini sana..Vinginevyo tusipofahamu namna ya kushughulika na utu wetu wa ndani, tutakuwa tunaishi Maisha ya maumivu na kutokusamehe kila siku…
Sasa dawa ya kuzuia kuumizwa ni ipi?
Ni kujitahidi kutokuweka jambo moyoni, au kwa lugha nyingine unakuwa unajitahidi kuyapotezea kwenye kichwa chako baadhi ya mambo, unakuwa huyachukulii kwa uzito..Kwamfano mtu amekwambia labda neno la “kukudhalilisha au kukushushia heshima”..jambo lile kabla ya kuanza kuliweka moyoni na kuanza kulitafakari na kujiuliza uliza kwanini mtu yule kaniambia vile, kwani kanionaje?….Utumie muda huo kufikiri ingekuwa ni wewe umemwambia vile, ungekuwa na maana gani?.
 
Ukiona mtu kakutukana, hebu fikiria wewe uliowatukana moyoni mwako, je! ulikuwa una nia gani mbaya nao?..utagundua basi tu! Uliwatukana pengine kwa hasira za pale pale na iliishia hapo tu!…huwezi kufikiri kwamba mtu uliyemtukana kwamba afikiri unamchukia, au una kinyongo naye… au umemtafakari sana, au yupo kwenye akili yako muda wote, na umekusudia kumwumiza, kwa kiwango anachokifikiria moyoni mwake…..wewe ulimtukana tu kwasababu zako… basi imeishia hapo tu!.
 
Kadhalika na wewe unapotukanwa au unapodharauliwa, hupaswi kuliweka jambo moyoni, kwasababu yule aliyekudharau, pale alipokudharau pengine haikupita hata dakika tano kashasahau kwamba alikudharau…Hivyo wewe unabaki na majeraha, wakati mwenzako moyo wake umeshasafishika siku nyingi, na pengine anampango wa kuja kuendelea kuwa na wewe, na kushirikiana na wewe kwa mambo mengine.
 
Hiyo ndio namna ya kujiponya majeraha yako…Hekima hiyo tunaisoma pia katika maandiko matakatifu, Sulemani Mwana wa Daudi aliiandika…
 
Mhubiri 7:21 “Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana.
22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine”.
 
Na mambo mengine yote! Yachukulie tu juu juu, jiweke kama ingekuwa ni wewe umemfanyia mwingine. Lakini endapo kila kitu kinachozungumzwa mbele yako wewe unakitafsiri tu na kukiweka moyoni mwako! Na kusema aaa anamaanisha nini kusema vile?…aa kwanini aseme vile?…aa kwani kaona nini kwangu?…au kwasababu niko hivi ndio maana kasema vile?…au kwasababu yeye ana kile na mimi sina?…Ukiishi kwa utaratibu huo, sura yako kila siku haitakosa huzuni, na uchungu, na macho hayataisha machozi, na kununa, na utakuwa mtu wa kunung’unika na kufurahia mabaya ya watu wengine, na hatimaye kutafuta namna ya kulipa kisasa na wengine wanaishia kwenda kwa waganga wa kienyeji na manabii wa uongo, kutafuta dawa ya kushughulika na maadui zako.
 
Lakini ukjifunza kuishi Maisha hayo Biblia inayotufundisha, kamwe hutapata majeraha ya moyo na utaishi Maisha ya msamaha na kuvumilia, na kupendana na watu, na ndivyo pia utakavyozidi kupendwa na watu, na hutaona kama kila mtu ni adui yako, Na hata kama utakuwa unajiona upo chini na wengine wapo juu kumbuka Bwana anaziona njia zako njema…na hivyo wakati ukifika Bwana atakunyanyua tu kama alivyomnyanyua Yusufu au Yeftha, haijalishi itachukua miaka mingapi, lakini atakuja kukulipa mema tu!. Yusufu alipokuwa Misri hakuwahi kunung’unika kwa wale ndugu zake kwa kumuuza, Zaidi baadaye aliwakaribisha wote na kula pamoja nao.
 
Bwana akubariki sana.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
 

Mada zinazoendana:

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

KWANINI PALE BWANA YESU ALICHUKUA HATUA YA KUMSAMEHE DHAMBI KWANZA KABLA YA KUMPONYA YULE MTU MWENYE KUPOOZA?(MARKO 2).

KISASI NI JUU YA BWANA.

EPUKA MUHURI WA SHETANI


Rudi Nyumbani:

Print this post

UPUMBAVU WA MUNGU.

1Wakorintho 1:25 “Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu’’.
 
Swali ni je! Mungu ni mpumbavu, au Mungu anao udhaifu?. Kwa mtu mwenye akili timamu akiangalia jinsi hii dunia ilivyoumbwa na sayari zake na nyota zake nyingi, akiangalia jinsi milima na mabonde na mito ilivyoumbwa kwa namna ya kushangaza, akaangalia vile vile Mungu alivyoumba vitu vyote na jinsi yeye mwenyewe alivyoumbwa na kupewa akili nyingi namna hii mpaka za kugundua ndege na kwenda huko juu mbali sana angani, hawezi kufiria kuwa Mungu ana upumbavu au anayo madhaifu yoyote..Na ndivyo ilivyo.
 
Lakini kwanini biblia inasema upumbavu wa Mungu, au Udhaifu wa Mungu?. Je! Inazungumzia katika Nyanja gani?..Inazungumziwa katika Nyanja yetu sisi jinsi tunavyomwona Mungu, hata wewe hapo kweli unaweza ukawa upo sahihi sana kwa kile unachokifanya, lakini hiyo haikufanyi watu wengine wote wakuone upo sahihi, wengine watakuona unafanya kitu cha kipumbavu haijalishi ni cha maana kiasi gani..Ndivyo ilivyo kwa Mungu wapo watu japo wanamfahamu kuwa Mungu ni mweza wa yote lakini wanayadharau mambo yake ya msingi ambayo yeye ndio kayatukuza..
 
Sasa ukisoma mistari ya juu yake kidogo utaona wayahudi walikuwa wanamtazamia Mungu kuwa atakuja kwa Ishara madhubuti itokayo mbinguni kama vile kung’aa kama jua,au kutoa Ishara kubwa zaidi hata ya zile za kina Musa na Eliya, lakini alipokuja na kumwona mbona ni mpole, mbona hajazaliwa kwenye familia ya kitajiri, mbona ni maskini, halafu, isitoshe hatma yake inaanishia kwenye kifo cha aibu cha kutundikwa msalabani uchi, moja kwa moja wakamdharau wakasema huyu hawezi kuwa masihi…Vile vile Wayunani nao (ambao wanawawakilisha watu wa mataifa yote), walitazamia kuona hekima ndani yake yaani walitazamia wasikie kutoka kwake kanuni mpya za ki-fizikia na kikemia na hesabati ambazo zitawafanya wafikie viwango vingine vya ustaarabu wa dunia na kuwafanya waishi maisha mengine ya kipekee..lakini walipomsikia anasema “Msisimbukie maisha watafakarini ndege, hawapandi wala hawavuni” wakamwona kama huyu ni kichaa kwao zikawa kama habari za kipuuzi zisizoongeza chochote katika jami..
 
1Wakoritho 1:22 “Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima;
23 bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi;
24 bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.
25 Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.”
 
Hivyo kwa ujumla Dunia nzima habari za Yesu zilikuwa kama za kipuuzi tu, haziingii akilini sio tu kwa watu wasiomjua Mungu lakini pia hata kwa watu wa kidini..Ni upuuzi..Ndio maana Bwana Yesu aliwaambia mahali Fulani makutano (HERI MTU YULE ASIYECHUKIZWA NAMI!… Mathayo 11:6), au kwa lugha nyingine heri mtu yule asiyechukizwa na ujio wangu au utendaji wangu kazi!
 
Lakini wayahudi na wayunani…hawakujua kuwa hapo ndipo misingi ya mbingu na nchi ilipolala, hapo ndipo chanzo cha hekima yao kilipo, hapo ndipo ukombozi wa Roho zao zilipo, hapo ndipo kiti cha enzi cha Mungu wao kilipo..Na chanzo cha vitu vyote na viumbe vyote..
 
Na ndio maana Biblia inaweka wazi kabisa mfano laiti wangelijua hilo wasingedhubutu kumsulibisha Bwana wa utukufu..
 
1Wakorintho 2:7 “bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
 
8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;”
 
Ni sawa tu na mtu asiyeijua Almasi, hata akikutana nayo shambani kwake atailima tu na kuitupa nje kama mawe mengine tu..Lakini kama angejua kuwa wapo watu wanaokaa miezi na miezi chini ya ardhi, usiku na mchana hawaona jua wala mwezi, wakipitia hatari nyingi za kufukiwa na vifusi vya udongo, kuitafuta, hawaipati lakini hawakati tamaa wakiamini siku moja watapata walau kipande kidogo tu cha dini hilo, kwasababu wanajua thamani yake ni zaidi ya hata ya mshahara wa watu elfu wanaolipwa mishahara mizuri ofisini kwa miaka mingi….Kama vile Yule mtanzania ambaye hajaenda shule aliyepata almasi ya sh. Bilioni Tatu, fedha ambayo mameneja 10 na wakurugenzi 10 wanaweza kuitafuta katika makumpuni yao mpaka kustaafu kwao na wasiipate…
 
Na hiyo yote ni kwasababu kaelewa tu thamani ya almasi. Vivyo hivyo na kwa Mungu, huwa anaificha thamani ya almasi yake yaani (YESU KRISTO) machoni pa watu wengi, na wakati mwingine inaonekana haina thamani kabisa, inaonekana kama ni upuuzi Fulani hivi, yaani mtu ambaye anampa leo Kristo maisha yake anaonekana kama kapoteza dira ya maisha, au amepungukiwa akili,..au mtu ambaye anataka kumjua Kristo na kulishika Neno lake, anaonekana sasa huyu ndio mpumbavu kabisa na mvivu..
 
Lakini hawajui kuwa jinsi mtu huyo anavyozidi kufikia kile kilele cha utimilifu wa kumjua Kristo ndivyo anavyozidi kuwa mbali kuliko upeo wa ufahamu wao ulipo..Kwasababu yeye kakiendea moja kwa moja chanzo cha mambo wanayoyatafuta wao kwa miaka mingi, hivyo uwezekano wa yeye kupata kila kitu ni mkubwa kuliko huyo akidharauye chanzo..
 
Nataka nikuambie hakuna mtu yeyote aliyemfuata Bwana Yesu akajuta baadaye, kwa upande wangu mimi sijaona, Daudi naye hakuliona hilo mpaka akasema
 
Zaburi 37:25 “Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.”
 
Na bado hatujaona utukufu alionao Bwana Yesu Kristo vizuri, tukifika huko ndio tutamwelewa kwanini anaitwa Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa wafalme, na wamwendeao wanaitwa makuhani wake, uzao mteule, watu wa Milki ya Mungu. Je! Unamkataa leo hii Bwana Yesu ambaye alikufia, ambaye alikupa uzima, ambaye mpaka sasa uhai wako upo mikononi mwake, unakimbilia vitu visivyokupa uhai, unavihangaikia hivyo kana kwamba siku ukifa vitakuhifadhia…kumbuka maandiko haya yanatimia juu yako 1 Wakorintho 1: 18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu”.
 
Mgeukie Bwana Yesu akupendaye, anapokuita usikatae, yeye ni HEKIMA YA MUNGU, iliyokataliwa na ulimwengu lakini mbele za Mungu ni LULU YA THAMANI…Anakupenda UPEO kiasi kwamba hakuna mtu yeyote alishawahi kufikia kiwango hicho cha upendo.
 
Ubarikiwe.

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

BASI MUNGU AKAMUADHIMISHA SANA..

NJIA YA MSALABA

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Kumwambia mtu mwenye dhambi kuwa atakwenda kuzimu asipotubu Je! ni kuhukumu?

JIBU: Kumhukumu mtu ni kitendo cha kumshtaki mtu mbele za Mungu kuwa anakasoro Fulani zinazopaswa adhabu. Na wengi wanao hukumu wanalengo la kujihesabia wao haki, na hawana lengo la kumwonesha mtu njia bali wanalengo la kuhitimishia kwamba yeye yupo hivi au vile.au atapatwa na hili au lile, na wala hawatoi njia ya mtu kuepukana na hatari hiyo.
 
Lakini kumfundisha mtu mambo anayopaswa kujiepusha nayo sio kumhukumu, au kumweleza mtu asipofanya jambo Fulani zuri, litampata jambo Fulani baya huko sio kuhukumu. Ni sawa na Mzazi anayemwambia mwanaye usipokuwa mtiifu sasa, mambo mabaya yatakukuta katika Maisha yako huko mbeleni, hivyo hapo hajamhukumu bali amemwonya!. Haijalishi atamhorodheshea mambo mangapi mabaya au mazuri…hata kama atamworodheshea mambo 100 mabaya, hapo bado hajamhukumu, bali amempa angalizo la mambo ya mbeleni.
 
Kadhalika Biblia haijatupa sisi ruhusa ya kuhukumu, Mhukumu ni mmoja tu! Lakini imetupa ruhusa ya kuonyana kwa Neno, Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.
 
2 Timotheo 4:1 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”
 
Kwahiyo Unaposikia unahubiriwa kuwa wala rushwa sehemu yao ni katika ziwa la moto, hapo hujahukumiwa bali umeonywa, walevi wote, waasherati wote na waabudu sanamu hawataurithi uzima wa milele, wasipotubu! fahamu tu ni umeonywa yatakayokupata mbele endapo ukiendelea kushupaza shingo yako, Kwasababu ndivyo Biblia inavyosema katika,
 
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
 
Hivyo usione unahubiriwa dhambi zako ukadhani kuwa unahukumiwa, kinyume chake ni unapendwa ili ugeuke usiangamie. Vile vile usiogope kumweleza mtu matokeo ya dhambi zake kwa kuogopa labda utakuwa unahukumu.
 
Mungu akubariki.

Mada zinazoendana:

KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?

Biblia inasema ” HAMJUI YA KUWA MTAWAHUKUMU MALAIKA? (1Wakorintho 6:2-3) ”. je! sisi tutawahukumuje Malaika?.

NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?

KUZIMU NI MAHALI PA NAMNA GANI ,JE! HUKO WANAISHI WATU WAKIFA NA KWENDA KUPATA MATESO AU NI VINGINEVYO?

NI HALALI KUBATIZA WATOTO WADOGO?

USHUHUDA WA RICKY:


Rudi Nyumbani:

 

 

Print this post

WAFALME WATOKAO MAWIO YA JUA.

Ufunuo 16:12 “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni”
 
Tukizunguza kwa lugha ya rohoni mto au bahari sikuzote unasimama kama kizuizi, Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Jangwani kuingia Nchi ya Ahadi walikutana na kizuizi cha Mto Yordani..Na kwa umati mkubwa kama ule wa mamilioni ya watu, pamoja na watoto wao, na mizigo yao mikubwa na mifugo yao mingi ilikuwa ni ngumu sana kuuvuka ule mto kwa njia ya kawaida ya mitumbwi, , ingekuwa ni rahisi kama ingekuwa ni mtu mmoja au wachache tu, lakini kwa wingi ule ilikuwa ni ngumu ilihitaji kitendo cha muujiza.. Na hilo ndio lililowapa matumaini watu wa Yeriko kwasababu walijua shughuli nzito itawakuta pale, ni lazima wakwame tu, lakini tunaona muujiza Mungu alioufanya wa kuukausha mto ule wa Yordani ili watu wake wavuke, na ule ndio ilikuwa mwisho wa Taifa lijulikanalo kama Yeriko.
 
Vivyo hivyo hata sasa katika Roho ipo mito mingi ambayo inasimama kama ukingo mbele yetu , ipo mito iliyowekwa na Mungu ili kutuzuia sisi na mashambulizi ya ibilisi na vilevile ipo mito iliyopandwa na shetani ili kutuzuia sisi tusifikie malengo yetu aliyotuwekea Mungu.. Tukisoma kitabu cha Mwanzo tunaona pale Edeni Mungu alitokeza mto mmoja mkubwa kuulitilia bustani maji ambao baadaye uligawanyika na kuwa vichwa vinne wakwanza uliitwa Pishoni, wa pili uliitwa Gihoni, wa tatu uliitwa Hidekeli na wa nne ambao ndio wa mwisho uliitwa Frati. Sasa hii mto inamaana kubwa katika roho. Adamu na hawa walipoasi pale bustanini, ilianza kukauka mmoja baada ya mwingine na ilipokauka ndio ilikuwa chanzo cha shambulizi moja baada ya lingine.
 
Sasa tukirudi kwenye kitabu cha Ufunuo tunaona malaika wa sita akiamuriwa kumimina kitasa chake juu ya nchi, na alipokimimina tu maji ya mto ule wa mwisho uitwao Frati ukakauka na njia ikapatikana kwa wafalme watokao katika mawio ya jua kupanda kuleta uharibifu..Ukisoma kitabu cha Ufunuo utaona kuwa hawa wafalme wa mawio ndio watakaoenda kusababisha Vita ile ya mwisho ya Harmagedoni. Na siku hiyo Biblia inasema litakusanyika jeshi kubwa, yaani wanajeshi MILIONI 200 watahusika katika vita hii, usidhani hilo jeshi dogo, jaribu kifikiria jeshi tu la ulinzi la Tanzania linaowanajeshi kama laki na kumi hivi, piga hesabu hili la Harmagedoni ni mara ngapi ya letu..Ni zaidi ya mara 1800 ya Jeshi letu, na hapo bado silaha za vita na makombora yatakayotumika.
 
Watu walioishi miaka ya mwanzoni mwa karne ya 19/20 ilikuwa ni ngumu sana kufahamu hawa wafalme watokao mawio ya jua watakuwa ni wakina nani hasa, kwasababu mawio siku zote ni mashariki jua linapochomozea, na kwa wakati ule hakukuwa na taifa lolote la mashariki ambalo lilikuwa hata na dalili ya kuwa na nguvu kijeshi au kiuchumi au kisiasa, kwani mataifa ya Magharibi kama tunavyofahamu katika historia kama vile Ulaya na Marekani ndio yaliyokuwa yana nguvu kwa namna zote, na mataifa karibu mengine yote yalikuwa ni makoloni yao, lakini leo hii tunaona sasa ni jinsi gani huu unabii unavyokwenda kutimia kwa haraka sana, mataifa ya Mashariki ndiyo yanayozidi kuwa utiishio kwa dunia ya sasa, taifa kama Korea, Japan na China.. ni tishio kwa usalama wa dunia.. Leo hii tunaona vuguvugu na vitisho vya vita kati ya mataifa haya na yale ya magharibi lakini huo ni mwanzo tu wa uchungu…Vita hasaa vyenyewe vinakuja kuwa kati yao wakiongoza mataifa mengine duniani dhidi ya taifa teule la Mungu Israeli.
 
Na mambo hayo hayapo mbali kutokea..Inasubiriwa amri moja tu itolewe ya kukauka huu mto wa rohoni Frati, hapo ndipo matendo halisi yatafuata..Teknolojia iliyopo sasa bomu moja tu la Hydrogen likiachiwa katika mji wenye idadi ya wastani wa watu inauwa zaidi ya watu milioni 34, hilo ni moja, silaha kama hizo zipo maelfu duniani katika mataifa mbalimbali..
 
Ni wakati gani huu tunaishi?, na ni kwanini tunajikumbusha haya? Ni kwasabab mwisho wa mambo yote umekaribia, ya nini kujitumainisha na mambo yanayopita ya hapa duniani, hata ukipata ulimwengu wote Kristo akiwa mbali na wewe ni hasara siku ile ukaachwa hivyo vyote vitakusaidia nini, kama sio vilio na maombolezo.
 
Mguekie Kristo sasa kabla mlango wa neema haujafungwa.
 
Maran Atha.
 

Mada zinazoendana:

UFUNUO: Mlango wa 16.

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

Naomba kuuliza kati ya Unyakuo wa kanisa, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?

UNYAKUO.

MAMBO YATAKAYOTOKEA ISRAELI SIKU ZA HIVI KARIBUNI.


Rudi Nyumbani:

Print this post