Category Archive Mafundisho

USIIGE TABIA YA NAAMANI

Unajua Kwanini Naamani atake kuingia tena katika nyumba ya Rimoni baada ya kuponywa? (2Wafalme 5:18)

Turejee..

2Wafalme 5:18 “Jambo hili Bwana amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, Bwana amwachilie mtumwa wako jambo hili”.

Katika kitabu hiki cha 2Wafalme 5, tunasoma uponyaji wa mtu mmoja aliyeitwa Naamani, aliyekuwa Jemedari wa jeshi la mfalme wa Shamu. Lakini huyu Naamani alikuwa ni mtu mwenye ukoma ingawa alikuwa shujaa wa vita.

Siku moja alienda kutafuta uponyaji kutoka kwa Mungu wa Israeli, kupitia taarifa alizozipitia kutoka kwa kijakazi wake aliyekuwa Mwishraeli kwa asili, na alipokutana na Nabii Elisha, kwa uongozo wa Roho wa Mungu aliagizwa akajichovye katika mto Yordani mara saba na ugonjwa wake (wa ukoma) utaondoka.

Mwanzo alikataa lakini baadaye alikubali na Bwana MUNGU akamponya ule ukoma, na ngozi yake ikarudi kama ya mtoto mchanga.

2Wafalme 5:14 “Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi”.

Kwa uponyaji huo alioupata aliahidi kutotoa tena sadaka kwa miungu aliyokuwa anaitumikia hapo mwanzo ambayo haikumsaidia kitu. (na mungu aliyekuwa anamtumikia hapo mwanzo kabla ya kuponywa na Bwana alikuwa anaitwa rimoni) .

2Wafalme 5:17 “Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana”.

Lakini pamoja na ahadi hiyo, aliona tatizo moja mbele yake..

Alijua atakaporudi kwa mfalme, bado atakuwa chini ya mfalme kama jemedari wake, na mara zote alikuwa anaongozana naye kuingia katika hekalu la mungu rimoni, naye pia alikuwa anasujudu.. Hivyo akajua atakaporudi hiyo desturi itaendelea.

Kwahiyo akatangulia kuomba radhi kwamba endapo jambo hilo likitokea basi Mungu amsamehe (yaani amwachilie), kwasababu hajadhamiria kufanya hivyo isipokuwa tu ni kwa kutimiza matakwa ya mfalme, lakini yeye ndani ya moyo wake au kwa hiari yake mwenyewe hajakusudia kumtolea mungu rimoni sadaka wala kumsujudia..

Hivyo Elisha akamruhusu aende na afanye kama anayoyaona moyoni mwake.

Ni jambo gani tunalojifunza?..

Ni kweli kwa Naamani tunajifunza Imani ya kupokea uponyaji baada ya kukubali mashauri, kwani kitendo cha kuamini tu taarifa kutoka kwa kijakazi, hiyo ni Imani kubwa, (kwamaana si wote wanaweza kuwasikiliza na kuwaamini watu walio chini yao kiuwezo, kielimu na hata kiufahamu), lakini Naamani aliweza hilo..Na hata sisi ili tuvute msaada wa Mungu na muujiza wake ni sharti tuwe watu wa Imani kama Naamani.

Na ndio Bwana YESU anakuja kurejea habari ya Imani yake katika kitabu cha Luka 4:27

Luka 4:27 “Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu.”

Lakini pamoja na hayo pia, lipo ambalo hatupaswi kujifunza kwa Naamani,..

NAAMANI MOYONI ALIMKIRI MUNGU WA ISRAELI kwa muujiza aliofanyiwa LAKINI KWA MATENDO ALIMTUMIKIA MUNGU RIMONI kwa heshima ya Mfalme.

Kwahiyo alikuwa ni VUGUVUGU..Moyo wake upo kwa Mungu wa Israeli,…lakini viungo vyake na utumishi wake upo kwa rimoni (mungu wa nchi yake).

Mfumo wa nchi yake ulimbana!, kazi aliyoifanya ilimfunga!..ijapokuwa alikuwa anatamani kweli kutotumika katika hekalu la mungu ambaye hakumsaidia, lakini tayari alikuwa ameshafungwa Nira, na hakuwa tayari kuikata hiyo nira.

Katika kitabu kile cha 2Wakorintho 6:15 Neno la Mungu linasema, tusifungwe Nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa.

2Wakorintho 6:14 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

15  Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

16  Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

17  Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha”

Na sisi kama wakristo ni lazima tutoke katika mahekalu ya sanamu, ni lazima tutoke katika kazi zinazotulazimu kusujudia sanamu au kumwabudu shetani, ni lazima tuache makundi yanayoturudisha kumwabudu shetani.

Ni kweli inagharimu, lakini hiyo ndio maana ya “kuubeba msalaba na kujikana nafsi”, kama kazi inakuuzisha pombe, au mwili wako, au inakuabudisha sanamu…IACHEEE!!. Ili uondokane na uvuguvugu. Kwasababu Bwana YESU alisema atawatapika wale wote walio vuguvugu.

Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16  Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa change”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.

Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?

MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.

Orodha ya Miji ilivyojulikana Agano Jipya na inavyojulikana sasa

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

Rudi Nyumbani

Print this post

KWA KUWA ROHO BORA ILIKUWA NDANI YAKE.

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu tujifunze maneno ya uzima.

Katika nyakati hizi za hatari na udanganyifu mwingi, ni vizuri kujichunguza sana, ni Roho ipi umeipokea ndani yako. Kwasababu tabia unazozionyesha ni matokeo ya roho iliyopo nyuma yake, ikiwa wewe ni mpenda dunia basi roho ya dunia ipo ndani yako.

1Wakorintho 2:12  Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

Vivyo hivyo ukijiona wewe ni mwizi, ujue roho ya wizi ipo nyuma yako.

Lakini maandiko yanasemaje kuhusu Danieli?

Yanasema ROHO BORA ilikuwa ndani yake.

Danieli 6:3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote

Maana yake ni kuwa Roho iliyozidi viwango, ndio iliyokuwa ndani yake.. Unajua mpaka inasema bora, maana yake zipo ambazo hazina ubora, kwa tafsiri nyingine “feki”, zenye mfano wa ile orijino. Ndicho shetani anachokibuni sana, ili awapoteze watu, wadhani wanaye Roho Mtakatifu, kumbe ni bandia.

Sehemu nyingine, inasema “Roho njema kupita kiasi”. Ilikuwa ndani yake..

Danieli 5:12 kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danieli, naye ataionyesha tafsiri.

Umeona sifa ya roho hiyo ni lazima iwe ya ‘kupita kiasi’, sio ya kawaida, vinginevyo ni feki. Sifa za Roho wa Mungu, anapita kiasi. Katika ubora na wema.

Ndio iliyomfanya Danieli awe mkamilifu kama tunavyomsoma kwenye maandiko. Kiasi cha watu kutafuta kosa ndani yake, bila mafanikio.

Danieli 6:4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.

Na mtu yeyote anayesema ameokoka,  Roho hii naye ni lazima imkalie. Roho iliyo bora, na njema kupita kiasi. Uthibitisho wa kwanza wa Roho uliyempokea ni Roho Mtakatifu, atakusukuma, kuwa Mtakatifu kama jina lake lilivyo.

Lakini iweje tunasema, tumepokea Roho, tunanena kwa lugha usiku kucha, tunatabiri, lakini Ubora wa huyo Roho hauonekani ndani yetu? Cha kushangaza utaona  huyo mtu anasema haiwezekani kuishi maisha matakatifu hapa duniani, ndio hapo tunamhubiri Kristo, wakati huo huo, tunaishi kidunia, tunafunga na kuomba wakati huo huo, tunavaa ovyo ovyo, tunaabudu pamoja lakini chini kwa chini tunavisasi na vinyongo. Tunatoa sadaka lakini nyuma kwenye biashara zetu ni za rushwa rushwa.

Je! Hiyo ni Roho bora?  Au imechakachuliwa?. Tumepewa ruhusu ya kujipima (1Yohana 4:1). Jihakiki, tangu ulipookoka hadi leo je, kuna mabadiliko yoyote ndani yako? Kama huna ni aidha ulimzimisha alipokuwa anaugua ndani yako ugeuke, au huna kabisa Roho Mtakatifu.

Habari njema ni kuwa Roho bora, ukimwita, huja ndani yako, au huamka tena. Ni wewe kuamini, na kutii kwa moyo wako wote. Kuwa tayari kuacha vyote(vya kidunia), na kumgeukia yeye. Na hatimaye atakuongoza na kukuweka sawa. Lakini sharti kwanza uaminifu kuwa utakatifu unawezekana, lakini pia ulimwengu utaukana.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VIASHIRIA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU KUWEPO NDANI YAKO.

OMBA, TAFUTA NA BISHA.

JE UMEUPOKEA UWEZA WOTE WA UUNGU NDANI YAKO?

Rudi Nyumbani

Print this post

HEKIMA NANE(8) ZA KIUINJILISTI, KATIKA KUWAVUA WATU KWA KRISTO.

Bwana ametupa agizo na wajibu wa kwenda kuihubiri injili ulimwenguni kote, na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wake.(Mathayo 28:19)

Alisema pia mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache. Ikiwa na maana lengo lake ni yeye apate mavuno mengi kutoka kwetu. Lakini huwenda tukaona sisi ni shida, kufanya hivyo.

Hata kama itakuwa kwetu ni shida kuvuta watu, bado Yesu anaona ni rahisi kwetu..Kwani mahali pengine alisema mashamba yameshakuwa meupe tayari kwa mavuno, wapo ambao tayari walishayataabikia, sisi ni kumalizia tu. Hivyo ni rahisi sana.

Lakini ili injili yetu itoe matokeo aliyoyakusudia, yatupaswa tujifunze kanuni zote za kiuinjilisti na kuzitumia, kisha  miongoni mwa hizo Bwana azitumie kuleta matokeo yake. Kuliko kutegemea kanuni moja tu Fulani na kupuuzia nyingine.

Ni sawa na mvuvi ambaye anashikilia  uvuvi wa ndoano tu, lakini hajui kuna wa nyavu, au wa mkuki au wa kutegea, lakini pia kuna wa majira mbalimbali ya kuvua, kuna ya usiku, au ya mchana.

Na sisi katika utumishi wetu wa kuwavuta watu kwa Yesu, tufahamu pia njia zote.

Sasa kibiblia zipo kanuni kuu (8), zinazovuta watu.

1) Kutangaza/Kushuhudia.

Hii ndio njia kuu na ya kwanza, ambayo ndio inasimama kama uti wa mgongo wa uinjilisti. Kwamba ni sharti kila mmoja wetu atumie kinywa chake, ujuzi wake, elimu yake, ufahamu wake, kumuhubiri Kristo kwa watu kwa namna yoyote. Utashuhudia shuleni, nyumba kwa nyumba, masokoni, barabarani, vijiweni, mitandaoni n.k. Ni agizo la Bwana na linapaswa lifanywe na wote.

2) Kuangaza Nuru.

Mathayo 5:16

[16]Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Wapo watu si rahisi kugeuka kwa kusikia unawaelezea habari za Yesu, ni rahisi kugeuka wanapomwona yule anayewahubiria mwenendo wake ni tofauti na wa kwao. Na hilo likamchoma moyo na kumfanya amgeukie Kristo moja kwa moja.

Hivyo angaza mwenendo wako, kwa watu, ikiwa hawataamini kwa lile Neno, basi waamini kwa mwenendo wako mzuri.

1Petro 3:1  Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2  wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu

3) Kujichanganya.

Ni ile hali ya kujaribu kuchukuliana na mawazo ya wale watu, na wakati mwingine hali zao, kana kwamba ni mmojawao, kisha kutumia fursa hiyo kuwaeleza habari za Yesu. Wengine huvitiwa kwanza na jinsi unavyothamini hali zao, sio kwa jinsi unavyo eleza vema Neno au mwenendo wako. Ni njia ambayo aliitumia Paulo na ikamletea matokeo mengi sana ya waongofu.

1Wakorintho 9:19  Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.

20  Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.

21  Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.

22  Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.

23  Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.

Zingatia kujichanganya sio kushirikana na dhambi zao, hapana, bali kuwepo katikati yao ili kuwaondoa huko, huku wewe mwenyewe ukijilinda nafsi yako usitekwe na dhambi zao.

4) Kuifuata dira ya Roho Mtakatifu.

Unaweza kudhani kila eneo unaweza kuhubiri na kuleta matokeo unayoyatazamia. sio kweli, Mitume walivua samaki usiku kucha lakini hawakupata kitu, baadaye Yesu akawaambia tupeni jarife upande wa kuume mtapata (Yohana 21), sehemu nyingine aliwaambia waende vilindini. Na walipofanya vile walipata samaki wengi. Paulo mwanzoni aliegemea injili yake kwa wayahudi sana, akapitia ukinzani, lakini kumbe Mungu alimkusudia aende kwa mataifa, na alivyotii agizo lile matokeo yakawa makubwa. (Matendo 22:21)

Hivyo ni muhimu kuomba Bwana akupe dira, lakini pia katika kuhubiri kwako utaona eneo Fulani lina matunda mengi, basi ujue hapo ni dira yako. Au njia Fulani ukiitumia wengi huvutiwa kwa Kristo, basi fanya hivyo. Lakini hili ni kuendelea kuomba na kuhubiri Mungu mwenyewe ataielekeza dira yako, kama ni hapo au kwingine, kama ni njia hiyo au njia nyingine, la kuzingatia  ni kuwa mwepesi kutambua upepo wa Roho unakufanikisha wapi. Kisha ongeza nguvu nyingi sana hapo, kuliko kule kwingine.

5) Ishara na miujiza

Yapo makundi ambayo, Mungu anajua yakiona tu muujiza au ishara fulani huvutika kirahisi. Na hili pia ni eneo la kumwomba Bwana, ajalie kunyosha mkono wake kuponya maana lina mvuto mkubwa na wa haraka sana.

Kanisa la kwanza liliomba maombi ya namna hiyo.

Matendo 4:29  Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, 30  ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu

Hivyo popote uendapo pia hakikisha unawaombea na watu, shida zao. Kwasababu kwa njia  hiyo Roho Mtakatifu hupata nafasi ya kupenyeza mvuto huo, kwao.

6) Busara.

Busara ni  namna nzuri kunena, hadi kuushawishi moyo wa mtu. Bwana Yesu anataka na sisi tujae busara ndani yetu aliyoifananisha na kama ile ya nyoka.

Mathayo 10:16  Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.

Nyoka alijua akimwendea Hawa kwa ukali, au kulazimisha isingewezekana, lakini alijishusha na kujifanya kama mtu wa mashauri, afichuaye siri, Jambo ambalo ni uongo. Na sisi hatuna budi kujua kunena kwa hekima, ili wale tuwahubirio tuishawishi mioyo yao, mpaka kumgeukia Kristo ambaye ndiye kweli.  Tujifunze kueleza uzuri wa Yesu. Lakini pia tusiwe watu wa kauli mbaya kwa tunaowahubiria hata kama watatupinga.

7) Kujihatarisha: 

Kuna la watu hatutaweza kulipata kama hatutaingia gharama kubwa kwa ajili yao. Wakati mwingine hata kuhatarisha  maisha. Kwasababu mahali walipofungwa na adui, pana ngome nzito. Mfano wa hawa ni wale waliofungwa katika vifungo vikali sana vya kidini.

Kuwang’oa huko ni kujiandaa na dhiki. Cha kuomba hasaa hapa kwa Mungu ni ujasiri kwa kanisa la kwanza lilivyoomba.

Hichi ndio kilele cha juu kabisa cha kiuinjilisti. Ndio wito Yesu aliowaitia mitume wake utakaowafanya wafikie kona zote. Kuwa tayari kufa kwa ajili ya walio dhambini. Ndio maana si wote waliweza kuambatana nao, Bali walibakia tu kuwaadhimisha.

Matendo 5:12  Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;

13  na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha;

8) Maombi.

Kuna wengine si rahisi kuokoka ki-uinjilisti tu, bali pia kuwaombea. Hii ni njia inayolegeza  nira za mwovu mioyoni mwa watu. Injili yako inaweza isiwe na shida lakini mioyo yao ya jiwe ikawa vile, hata uhubirije hawewezi kukuelewa.

Paulo alikuwa ni mtu wa kuwaombea sana watu wake wayahudi waokolewe. Maandiko yanasema ombeaneni ninyi kwa ninyi mpate kuponywa.

Warumi 10:1  Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.

2  Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.

Usione shida kuwaombea ndugu zako ambao hawajaokoka, wafanyakazi wenzako, majirani zako, jamii yako n.k. Ni maombi yasiyo  na ukomo fanya hivyo kila siku, maombi yako ni silaha kubwa sana ya kiuinjilisti.  Lakini usiombe tu na kukaa ukasema namwachia Bwana. Hapana unawaombea na huku unawahubiria.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba, tukijifunza njia zote hizi, na kuziachilia katika maisha yetu ya kiutumishi ni hakika kuwa lipo kundi litaokoka tu.  Lakini kutegemea njia moja peke yake huubana utendaji kazi wa Roho Mtakatifu ndani yetu, . Ukihubiri changanya na hizo nyingine, kisha yeye aamue ni ipi itamvuta mtu kwa wakati huo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI

UFUATILIAJI NI SEHEMU YA HUDUMA MUHIMU KWENYE UINJILISTI

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Rudi Nyumbani

Print this post

JE UMEUPOKEA UWEZA WOTE WA UUNGU NDANI YAKO?

2 Petro 1:3

[3]Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 

Kuna mambo makuu sana ya kujifunza ndani ya vifungu hivi;

Hapo tunaonyeshwa kuwa Mungu anao Uweza wake. Kama vile tu mwanadamu alivyo na uweza wake usiokuwa sawa na mbwa. Kwamfano mwanadamu anaweza kuunda silaha, ambayo inaweza teketeza mji mzima kwa maarifa yake. Anauwezo wa kuruka angani zaidi ya kiumbe chochote duniani kwa vyombo alivyovibuni, anaweza kuwasiliana na mtu aliye mbali sana hata na kuona uso wake kwa vyombo vya mawasiliana alivyojibunia.Mambo ambayo mnyama hawezi. Huo ni uweza wake wa kibinadamu.

Vivyo hivyo na Mungu wetu, anao uweza wake wa uungu, ambao ametukirimia sisi, Tunapoupokea huo  tunakuwa na sifa kama zake.

Ndio hapo anasema…

“Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.

Lakini sasa nataka uone hapo uweza huo umeshushwa juu yetu, si katika kila kitu bali  katika mambo mawili makuu.

1) La kwanza ni uzima.

2) la pili utauwa.

Yaani mambo yote yanayohusiana na uzima wetu, ametuwezesha yeye mwenyewe. Ndio maana kwa kumwamini Yesu tunapokea msamaha wa dhambi. Tunakuwa tumevuka kutoka  mautini kuingia uzimani. Hatuangamii, tunakuwa na uzima wa milele ndani yetu.

Kwasababu Hatuna kifo ndani yetu, tunalala tu, kupumzishwa ili baadaye tuamshwe. Lakini Uzima huu hauwezi kuupokea kwa juhudi zako, au kwa elimu yako, au kwa matendo yako mema, au kwa dini yako nzuri, hapana..Ni zawadi ya Mungu kupitia Kristo Yesu. Pale unapomwamini tu, unapokea msamaha wa dhambi zako, kwa neema, huu ni uweza wake wa ajabu, ambao wanadamu wanausumbukia hawaupati, kwasababu mwanadamu hana matendo mema ya kutosha kuununua uzima. Isipokuwa Yesu tu peke yake alitununulia kwa damu yake.

Yohana 3:36

[36]Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. 

Lakini sio tu Uzima, uweza huo umetukirimia pia na katika Utauwa wote. Utauwa ni utakatifu. 

Mtu ambaye hajaokoka hawezi yatoa maisha ya utakatifu ndani yake. Vinginevyo atajitahidi sana kwa kuutumikisha mwili kwa nguvu, na hatimaye atashindwa, au atafanya kinafki kama mafarisayo na waandishi, ambao walikuwa wananena mambo ambayo hawayatendi,.kwasababu uweza huu haukuwa ndani yao.

Utauwa haswaa ni kazi ya Mungu mwenyewe mioyoni mwetu kupitia Roho Mtakatifu. Ni pale mtu anapompokea Kristo kama mwokozi wake, kisha kukubali kumtii, kwa kujikana nafsi yake. Ndio hapo hapo yeye mwenyewe anakuongezea nguvu, ambayo inakufanya uyakimbie yale maisha ya kale ya dhambi. Lakini kumbuka hiyo inakuja kwa kukubali kumtii Yesu, kukubali kuwa kiumbe kipya. Wakristo wengi wanataka Bwana awasaidie lakini hawataki kujikana nafsi zao wasaidiwe na Bwana. Ukimpokea kwa mdomo tu uweza huu hautakuwa na matunda ndani yako. Lakini ukiwa ni wa geuko la kweli, uweza huo ni lazima utende kazi ndani yako.

Utaweza kushinda zile dhambi ambazo ulikuwa huwezi ziacha.

Yohana 1:12

[12]Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 

Unaposema Yesu ni BWANA wangu. Ni lazima, ujue unajifanya kuwa mtumwa wake.. sikuzote bwana yoyote humiliki mtumwa, chochote anachoagizwa.huwa ni amri kwake sio ombi. Kumbali kuongozwa na Yesu, acha kabisa wokovu wa mdomoni.

Kama mkristo, kuwa mtakatifu ni lazima sio chaguzi, ndio kitambulisho chako kuwa umepokea uzima wa milele. Kwasababu pasipo huo huwezi kumwona Mungu (Waebrania 12:14).

Hakikisha uweza wote huu umeupokea ndani yako. Usiseme hicho kingine cha utakatifu hakinihusu, vinginevyo utakuwa hujakamilika

Shalom.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

INJILI NI UWEZA WA MUNGU, UULETAO WOKOVU.

Je! Utatu mtakatifu upo kibiblia?

Rudi Nyumbani

Print this post

MKATAE MWAJIRI HUYU MBAYA.

Hebu tengeneza picha umeajiriwa, halafu aliyekuajiri anakutumikisha kwa mateso makali na mwisho wa siku anakulipa mshahara wa kifo!, Je kabla ya kuanza hiyo kazi, utakubali kutia sahihi mkataba huo??

Bila shaka kwa mtu mwenye akili timamu, hawezi kukukubali.

Lakini ajabu ni kwamba Zaidi ya nusu ya wanadamu wa kizazi chetu, wametia sahihi na huyu boss, ambaye anawatumikisha halafu anawalipa mshahara wa kifo. Je unataka kumjua huyu boss mkatili, na tena mwenye mshahara mbaya wa kifo?.. Biblia imemtaja ni nani katika Yohana 8:34-35 na Mshahara wake ni upi katika Warumi 6:23.

Yohana 8:34 “Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni MTUMWA WA DHAMBI”.

Mtu anayetenda dhambi, tajiri wake ni DHAMBI!.. Dhambi ni boss mbaya asiye na huruma…na huu ndio mshahara wake..

Warumi 6:23 “Kwa maana MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI….”.

Huyu boss hamdhulumu mtu, bali “anamlipa mtu mshahara tena kwa wakati”… kwasababu kila anayefanya kazi anastahili malipo biblia inasema hivyo katika (Luka 10:7 na 1Timotheo 5:18).

Dhambi inaua.., dhambi inaua.., dhambi inaua…, dhambi inaua..! Dhambi inaua,..Dhambi inaua…

> Dhambi inaua ule Upendo mdogo uliopo ndani yako

> Yale mahusiano madogo uliyoyaanza na Mungu wako, dhambi inayaua, inakusababisha kabisa usioune uso wa Mungu,… Tena biblia inasema inasema “Inafarikisha”…kufarikisha sio “kufarakanisha”… Kufarikisha inatokana na neno “kufariki” yaani “kufa/kutengwa”

Isaya 59:2 “lakini maovu yenu YAMEWAFARIKISHA ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”

> Dhambi inaua “furaha” ndogo na kubwa uliyonayo..

> Dhambi inaua “amani” na kuleta hofu.

> Dhambi inaua “wema” mtu alionao.

> Dhambi inaua “ndoa”

> Dhambi inaua huduma/karama/kipawa.

> Dhambi inaua “Heri” za mtu.

> Dhambi inaondoa “Baraka” za mtu

Mwisho dhambi inaua “Mwili”….. huyu ni boss asiyefaa, mwenye mkataba Mbovuuu!!!!…Tumkimbie! Na kumwendea Bwana YESU, ambaye yeye anasema Nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi, nasi tutapata raha nafsini mwetu (Mathayo 11:28).

Tukimkimbilia Bwana YESU anatufungua kutoka kwa huyu mwajiri mbaya (dhambi) na kutuweka huru.

Yohana 8:35  “Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.

36  Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”

Bwana YESU anatulipa UZIMA badala ya KIFO…. na si Uzima tu, bali UZIMA WA MILELE.

Bwana anamlipa mtu uzima katika Nafsi yake.

Unaongeza uzima juu ya upendo wa mtu, lakini dhambi inaua!

Bwana YESU anaongeza Uzima juu ya Amani ya mtu, lakini dhambi inaua!

Bwana YESU anaongeza Uzima juu ndoa ya mtu na maisha kwa ujumla, lakini dhambi inaua!

Na Zaidi ya yote, Bwana YESU anamlipa Mtu UZIMA WA MILELE (Yaani maisha baada ya hapa)..Kwanini tusimchague huyu??.

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Je unaye tayari?..kama bado unangoja nini?.. kwanini dhambi ikukaushie uzima wako wa hapa duniani na ule wa milele ujao??..na matunda ya dhambi ni yale yote yaliyotajwa katika Wagalatia 5:19-20.

Wakati uliokubalika ni sasa, mkaribishe YESU leo maishani mwako akuweke huru.

Ikiwa bado hujampokea Bwana YESU na unahitaji msaada huo basi wasiliana nasi, tutakusaidia buree.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TENDA JAMBO LA ZIADA.

ROHO MBAYA KUTOKA KWA BWANA.

Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.

Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?

UFALME WAKO UJE.

Rudi Nyumbani

Print this post

NAMNA YA KUNENA KWA LUGHA MPYA

bofya, juu, “download” ufungue makala yake usome..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

OMBA, TAFUTA NA BISHA.

KILINDI CHAPIGIA KELELE KILINDI.

Rudi Nyumbani

Print this post

OMBA, TAFUTA NA BISHA.

Mwokozi wa ulimwengu (BWANA YESU KRISTO) atukuzwe.

Bwana YESU alisema katika Mathayo 7:7, maneno yafuatayo..

Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa”

Na kwanini aseme hivyo??…anaendelea mstari wa nane (8) kwa kusema..

“kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”.

Kwahiyo kwanini tunapaswa tuombe?…jibu tumepata “kwasababu kila aombaye atapewa”… Lakini kwanini “Tutafute”..kwasababu kila “atafutaye ataona” na kwanini tubishe??… ni kwasababu “kila abishaye atafunguliwa”.

Kwahiyo matokeo ya Kuomba, Kutatufa na kubisha ni  KUPEWA, KUONA, na KUFUNGULIWA.

Je unataka KUPEWA unachokitaka, na KUKIONA, na KUFUNGULIWA?...basi usikwepe mambo hayo matatu; Kuomba, kutafuta, na kubisha…usichukue moja na kuacha lingine??.. ipo sababu kwanini Bwana ayaorodheshe yote matatu.

Unataka kumjua Mungu, na kutembea katika kanuni zake? Kuwa mtu wa KUOMBA, lakini si kuomba tu bali pia na KUTAFUTA!… Unamtafutaje Mungu?, kwa kuhudhuria katika makusanyiko kila wakati kwa uaminifu, na kwa kuyasoma maneno yake usiku na mchana…na KUBISHA!..

Kubisha kunakozungumziwa hapo si “kulumbana” bali “kugonga mlango”..kwa lugha rahisi ni kitendo cha kutumia maarifa yoyote uliyonayo kufikisha ujumbe kwa aliye ndani kwamba unataka kuingia!.. Na katika kumtafuta Mungu, kubisha kwetu ni pamoja na kumtolea yeye sadaka, na kuhubiria wengine habari njema, na kufanya mambo mengine yanayofanana na hayo.

Wengi wanapenda kuomba tu na kuombewa, lakini wao wenyewe kutenga muda wa kumtafuta Mungu hawawezi.. watu wa namna hii ni ngumu sana kumpata Mungu katika maisha yao..  wanaishi kwa YESU aliyeko ndani ya mchungaji wao, au kiongozi wao (ndio maana kila kitu wanasubiri kuombewa)…lakini si hawaishi kwa YESU aliyeko ndani yao.

Hawa wataishia kuomba/ kuombewa na kupata kile wakitakacho lakini hawatamwona YESU katika maisha yao (hawataijua sauti yake wala kuongozwa na yeye)..lakini kama wangeomba na kuombewa na wangeongeza bidii katika kumtafuta MUNGU, wangepata faida zote.. kupata na kuona.

Je unaomba, na kutafuta na kubisha?

Kama hayo bado huuyafanyi basi anza kuyafanya leo, na Bwana atajifunua kwako.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

NIFANYE NINI NIMSHINDE SHETANI?

TAFUTA KUMJUA MUNGU ZAIDI YA SHETANI

NIFANYE NINI ILI MUNGU AYAJIBU MAOMBI YANGU?

MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.

Rudi Nyumbani

Print this post

NYUMBANI MWA BABA YANGU MNA MAKAO MENGI.

Bwana Yesu karibu na kuondoka alizungumza maneno haya;

Yohana 14:1  Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2  Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3  Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

Kwa mara ya kwanza anawafunuliwa wanafunzi wake, kuhusu mambo yaliyo kwa Baba yake tuliyoandaliwa sisi. Na hapo anasema huko kuna “makao mengi”. Hasemi kuna “kao”kana kwamba ni moja, bali “makao” tena mengi.. Hatujui idadi labda ni mia, au elfu, au milioni, au bilioni. Yesu kusema mengi, amini ni mengi kwelikweli.

Ndio maana kumaliza mambo mema Mungu aliyotuandalia inahitaji umilele.

Sasa kibiblia tumepewa kuyajua makao ya aina tatu tu.

Moja, alituletea tayari, Lakini Mengine mawili yatakuja baadaye.

Kao la kwanza: Lilikuwa ni yeye kutukaribisha ndani yake.

Hilo lilitimia muda mfupi sana, baada ya kuondoka, Tunaona baada ya siku 10, siku ile ya pentekoste, alirudi tena juu yetu kama Roho Mtakatifu. Akaingia ndani yetu, Kwa mara ya kwanza sisi ndio tulipokea mahusiano binafsi ya moja kwa moja na Mungu, tukaingia nyumbani mwake.

Matendo 2:1  Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2  Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

3  Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4  Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

Mtu aliye na Roho Mtakatifu, huishi tofauti na mtu ambaye hana Roho. Kwasababu ulimwengu wake ni mwingine kabisa na ule wa kwao, Kao lako ni kuu zaidi ya kao lao la kidunia. Raha na pumziko analolipata, walimwengu hawawezi kulipata. Hekima na upeo ulionao wewe,wale hawana, Hakika kao hili ni zuri sana. Unapojazwa Roho vema, ndio unaona uzuri wa kao hilo maishani mwako.

Kao la pili: Ni kao la roho zetu.

Kumbuka roho hizi zipo ndani ya miili hii ya mavumbi. Lakini Yesu aligundua udhaifu wa miili hii hivyo, alikwenda kutundalia miili ya utukufu itokayo juu, ambayo hiyo tutavishwa, siku ile ya unyakuo itapofika, miili ambayo haijatengenezwa kwa malighafi za duniani, bali zile za kimbinguni. Miili isiyozeeka, isiyougua, isiyo sikia njaa, wala isiyokufa. Haleluya. Ni kao zuri ambalo hakuna hata mmoja wetu anapaswa alikose.

2Wakorintho 5:1  Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.

2  Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;

3  ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.

4  Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.

Kao la Tatu: Ni mazingira mapya ya watakatifu, ndio ile mbingu mpya na nchi mpya.

Na ule mji wa kimbinguni, Yerusalemu mpya ishukayo kutoka juu kwa Baba. Uzuri ulioko huko hauna kifani. Ni mji unawaka na kumeta-meta utufukufu wa Mungu.

Ufunuo 21:15  Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.

16  Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.

17  Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.

18  Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.

19  Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;

20  wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.

21  Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.

22  Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.

23  Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.

24  Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.

25  Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.

26  Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.

27  Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo

Haya ni matatu tu! Vipi kuhusu hayo mengine ambayo hatujafunuliwa? Ukiyajua hayo, hutauchukulia wokovu kirahisi-rahisi, utafanya bidii uingie ndani ya Kristo. Mfuate Kristo akupe uzima wa milele. Ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi wasiliana  nasi kwa mawasiliano unayoyapata mwisho wa makala hii, bure

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.

Nini maana ya Mithali 19:21Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.

Jiepushe na tamaa ya Mali/kupenda fedha.

TUMAINI NI NINI?

Rudi Nyumbani

Print this post

UKWELI KUHUSU UISLAMU, Sehemu ya Tatu: Kisima cha Zamzam.

Kisima cha Zamzam ni nini, na ukweli wake ni upi?


Angalizo: Makala hii haina lengo la kushambulia Imani Fulani, wala kushabikia Imani Fulani, pia haina lengo la kumchafua mtu yoyote, wala kumdhalilisha, bali kutoa elimu sahihi kuhusiana na tunayoamini na yanayoaminiwa.


Kisima cha “Zamzam”, ni kisima kilichopo katika msikiti wa Al Haram uliopo Makka, katika nchi ya Saudi Arabia. Kisima hiki kipo umbali mfupi kutoka katika jiwe/jabali jeusi la Kaaba. (umbali wa mita 20 mashariki mwa jiwe hilo).

Kulingana na Uislamu, kisima hiko kilijitokeza hapo kimiujiza kipindi kile Hajiri kijakazi wa Sara alipoachwa na Abramu katika lile jangwa (katika vilima vya Safa na Marwah) na akakosa maji ya kunywa yeye na mwanae Ismaili.

Na Hajiri alipoona mwanae anakaribia kufa, akaanza kuzunguka vilima hivyo vya Safa na Marwah mara saba, na alipokuwa katika mzunguko wa saba, ndipo Malaika Jibra’il (Gabrieli) akatokea na kukitokeza kisima hiko kimiujiza na kilipotokea, Hajiri akaanza kusema zamzam, maana yake “acha kutiririka”

Hadithi za kiislamu zinazidi kusema kuwa kisima hiko kilikauka, lakini kikaja kuvumbuliwa tena na babu yake Muhamad aliyeitwa Muttalib katika karne ya sita(6).

Lakini pia binamu yake Muhamad aliyeitwa “Ibn Abbas” alisema “Maji ya zamzam yanafaa kwa nia yoyote ile, mtu akinywa kwa lengo la kupona ugonjwa basi mungu atamponyesha kupita maji hayo, kama mtu atakunywa kwa lengo la kuondoa njaa, basi mungu ataiondoa njaa yake, kama mtu atayanywa kwa lengo la kukata kiu basi mungu ataikata kiu yake kwasababu hata Ismail alikunywa maji hayo na kukata kiu yake kali”.

Na kwasababu hiyo maelfu ya watu wanayatumia maji hayo wakiamini yamebeba uponyaji wa kimungu ndani yake??. (Je ukweli wa mambo haya ni upi)?

Awali ya yote tufahamu kuwa Ishamaeli, mwana wa Hajiri hakuwa mwana wa Ahadi kulingana na biblia, hali ISAKA, mwana wa Sara ndiye aliyekuwa mwana wa Ahadi.  Hadithi zote zilizopo na zinazotungwa zinazoshinikiza kuwa Ishamaeli ndiye mwana wa Ahadi, si za kweli.

Ishmaeli aliahidiwa Baraka nyingine za Mungu lakini si za Mzaliwa wa kwanza. Baraka za mzaliwa wa kwanza zilikuwa kwa Isaka aliyekuwa mwana wa Sara.

Sasa ukweli wa kisima hiko kibiblia ni upi na je kuna muujiza wowote katika kisima hiko?

Habari ya kisima hiko, ambako biblia haisemi kwamba kinaitwa “Zamzam” inapatikana katika kitabu kile cha Mwanzo 21, Hebu tuianzie ile habari mbali kidogo katika ule mstari wa 9 ili tuielewe habari..

Mwanzo 21:9 “Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.

10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.

11 Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe.

12 Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.

13 Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.

14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.

15 Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.

16 akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.

17 MUNGU AKASIKIA SAUTI YA KIJANA. MALAIKA WA MUNGU AKAMWITA HAJIRI KUTOKA MBINGUNI, AKAMWAMBIA, UNA NINI, HAJIRI? USIOGOPE, MAANA MUNGU AMESIKIA SAUTI YA KIJANA HUKO ALIKO.

18 ONDOKA, UKAMWINUE KIJANA, UKAMSHIKE MKONONI MWAKO, KWA KUWA NITAMFANYA KUWA TAIFA KUBWA. 

19 mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.

20 mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.

21 akakaa katika jangwa la parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya misri”.

Sasa kulingana na maandiko hayo matakatifu, ni Dhahiri kuwa Ishmaeli (au Ismail), hakuwa mwana wa ahadi ndio maana aliondolewa katika hema ya Sara, na Mungu alikuwa upande wa Sara. Lakini kwasababu Mungu ni wa rehema asingeweza kumwacha kabisa Hajiri na Ishamaeli kwani nao pia ni uzao wa Ibrahimu, ndio maana akawaokoa na mauti katika jangwa lile lisilo na maji.

Na utaona Malaika wa Mungu alimfumbua macho Hajiri ili akione kisima, na si kwa “alikitokeza kisima kile kimiujiza”.. Maana yake ni kwamba kisima kile tayari kilikuwepo pale, isipokuwa macho ya Hajiri hayakukiona, na yalipofumbuliwa ndipo akakiona na kumshukuru Mungu.

Sasa swali la Msingi ni hili, je kisima hiko kiliendelea kuwepo?, na je Mungu aliagiza chochote juu ya kisima hiko, kwamba watu waende huko kuchota maji yake?

Jibu ni kwamba kisima hiko kiliendelea kuwepo, kwasababu kilikuwepo kabla ya hapo pia!..na ulipofika wakati kilipotea kama tu visima vingine vilivyopotea… Na wala maji yake hayakuwa na muujiza wowote kwa Ishmaeli Zaidi ya maji mengine yoyote.

Yale yalikuwa ni maji ya kawaida tu, ambayo mtu akinywa anakata kiu, na ndilo lililokuwa lengo la Mungu, kwa Hajiri na Ishmaeli, kwamba wanywe wakate kiu basi, waweze kuokoka na mauti ya kukosa maji, na si kwamba wakifanye kuwa kisima kitakatifu cha kufanyia ibada.

Sasa kulingana na hadithi za kiislamu, wanakiri kuwa kilipotea hiko kisima, lakini ajabu ni kwamba kimekuja kugunduliwa na kufukuliwa karne ya 6, (Jambo hilo si kweli, ni uongo wa adui).

Huenda hiko kisima kilichopo sasahivi ni kisima tu kilichoibuliwa na watu, na zaidi hata kama kingekuwa ni chenyewe (halisi) kile alichoonyeshwa Hajiri na Malaika, kisingekuwa na Uungu wowote ndani yake kwani Mungu hajawahi kuweka agano lake katika visima! Au mito au bahari.

Ingekuwa ndivyo basi ule mto Yordani ambao Naamani-Mkoma aliokwenda kuoga mara saba na ukoma wake kuondoka basi hata leo wakoma na wagonjwa wangetiririka pale kuoga ili kupona magonjwa yao…

2Wafalme 5:9 “Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha.

10 Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi………………

14 Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi”.

Sasa huo ni mto Yordani ambao mpaka leo upo! Na ndio mto Bwana YESU aliobatizwa na Mbingu zikafunuka juu yake kumshuhudia.. Lakini maji yake leo hayawezi kutumika kama maji ya kiungu.. Vipi hayo mengine?.

Na pia kisima hiko cha Hajiri hakikuwepo Saudi Arabia, bali kilikuwepo Parani katika jangwa la Sinai.

Kwahiyo maji hayo ya zamzam, yanayotoka huko Saudi Arabia, (Makka), si maji ya kiungu na  mkristo/asiye mkristo hapaswi kuyatumia kwa matumizi yoyote, matokeo ya kutumia maji hayo kwa lengo la kupata uponyaji, au utatuzi wa tatizo lingine lolote ni KUONGEZA TATIZO HILO!.

Inasadikika pia maji haya yanatumika katika baadhi ya misiba, (yanatiwa katika vyakula vya misibani), na katika baadhi ya vyakula vya biashara, na matumizi mengine,

Ikiwa unahudhuria mazishi yoyote yale (yawe ya kikristo au sio ya kikristo), hakikisha unatakasa vyakula vyote kwa Imani kwa damu ya YESU kabla ya kula!.. Usile tu!..Vile vile kila ununuacho kama bidhaa ya chakula, pasipo kujua asili ya utengenezaji wake, kabla ya matumizi, takasa kwa Imani kwa damu ya YESU.

Lakini si maji ya zamzam tu yenye shida kiroho, bali pia na maji yajulikanayo kama “ya upako yauzwayo katika baadhi ya makanisa”..yote yanabeba sifa moja na haya ya ZAMZAM.

Ukiona maji yanauzwa kwa kivuli cha upako, kwamba uyatumiapo utapata uponyaji au ufunguzi!, kuwa makini sana!.

Watumishi wa kweli wa Mungu, wanatumia maji kwa uongozo maalumu wa Roho Mtakatifu, na si kama utaratibu au mwenendo wa mara zote, kwamba kila tatizo ni maji na tena yanauzwa!, na tena yanaaminishwa kuwa ndio kitu kiponyacho!, hayo ni mafundisho ya ibilisi, ambayo ni muhimu kuwa nayo makini!.

Ukikuta maji yanauzwa usinunue!, ukikuta mafuta yanauzwa usinunue!..Ibilisi ni yule yule, anayefanya kazi kwenye kila kitu kilicho kinyume na Neno la Mungu.

Usikose Makala zijazo…

Je umempokea YESU kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako?..kumbuka yeye pekee ndiye Njia ya kufika mbinguni, na si mwanadamu yoyote aliye hai au aliyekufa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UKWELI KUHUSU UISLAMU Sehemu ya kwanza: (Msikiti wa AL-Aqsa).

HAJIRI NI KAMA MLIMA SINAI ULIOKO ARABUNI.

JE! NI CHEMCHEMI IPI INATOKA NDANI YAKO, YA MITO AU YA KISIMA?

JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?

LAKINI NINYI, NDUGU, MSIKATE TAMAA KATIKA KUTENDA MEMA.

Rudi Nyumbani

Print this post

KILINDI CHAPIGIA KELELE KILINDI.

Zaburi 42:7

[7]Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maboromoko ya maji yako, Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tutafakari pamoja Neno la Mungu.

Biblia inatuambia kila jambo tunalolifanya lina matokeo sawa rohoni. Ikiwa wewe ni mwizi malipo ya wizi utayapata rohoni, ikiwa wewe ni muuaji, malipo ya uuwaji utayapokea vilevile rohoni, mito ya maji inapoelekea huko huko ndipo inaporudia.

Ufunuo 13:10

Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.

Sasa hapo tumeona katika eneo la ubaya, je vipi katika upande wa Mema?

Maandiko hayo hayo yanatuambia kwamba Kilindi hupigia kelele kilindi.

maana yake ni nini?

kilindi ni mahali pa katikati kabisa mwa bahari. Sasa mwandishi wa zaburi  anatumia mifano ya kitu halisi kana kwamba kinaongea… anasema Kinaita chapigia kelele kilindi. Na cha kushangaza ni kwamba hakiiti eneo lingine lolote la maji labda ufukweni.. au kwenye rasi, au ghuba.. hapana bali kinapigia kelele kilindi chenzake.

Kilindi chapigia kelele kilindi

Maana yake ni nini?

Tukitaka mambo ya ndani ya Mungu, mambo ya vilindini, lazima na sisi tuwe vilindini. Ni muunganiko wa ki-Mungu. kila kiwango kina sauti yake. kamwe hizo sauti haziingiliani, ni sawa na mbwa amwite tai kwa sauti yake ya kubweka, haiwezekani kuja inahitaji, ajifunze sauti yake ili yule tai aelewe, vinginevyo atakuwa anapiga kelele tu.

Na sisi vivyo hivyo kwa Mungu, wengi tunatamani tumwone Mungu kwa undani katika maisha yetu, lakini hatutaki tuzame ndani yake.

Mwandishi wa Zaburi mwanzoni kabisa kabla hajasema maneno hayo kwenye hiyo sura 42 anasema

Zaburi 42:2-3

[2]Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?

[3]Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako.

Kuonyesha ni mtu ambaye alimtamani sana Mungu wake.

Sehemu nyingine Daudi anasema..

Zaburi 63:1-8

[1]Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,

Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.

[2]Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako.

[3]Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.

[4]Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.

[5]Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.

[6]Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku.

[7]Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.

[8]Nafsi yangu inakuandama sana; Mkono wako wa kuume unanitegemeza.

Umeona, usiku kucha, anamtafakari Mungu, kuonyesha ni mtu ambaye moyo wake upo kwa Mungu asilimia mia..unategemea vipi mtu kama huyo Mungu asijifunue kwake kwa viwango vile?

Nafasi hii pia mimi na wewe tunayo. Tumfuate Mungu wetu vilindini, ili ajifunue kwetu katika viwango vingine..

Na hiyo inakuja kwa kile Bwana Yesu alichosema..Tujitwike misalaba yetu tumfuate, tuwe tayari kuacha vyote visivyompendeza yeye na kumtii. Na kwa kufanya hivyo rohoni tunatafsirika kuwa tunamwita Mungu wa vilindini.

Anza sasa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.

Ni kelele gani zinazozungumziwa hapo katika Waefeso 4:31.

NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)

Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?

Rudi Nyumbani

Print this post