Title Devis

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

Umewahi kujiuliza kwanini Bwana Yesu alisema, Anakwenda kutuandalia makao? (Yohana 14:2), Na kwanini mbinguni kunafananishwa na karamuni?…Ni dhahiri kuwa utaratibu wa maandalizi ya karamu unafanana sana na utaratibu wa kuingia mbinguni. Kwahiyo tukizijua tabia za karamu ndio tutajua mbinguni kutakuwaje!

Kwanza Karamu ni lazima iandaliwe, siku gani itafanyika na wapi itafanyikia, na ni lazima iandaliwe kwa kupambwa vizuri, ni lazima pia iwe na vyakula na vinywaji, na ni lazima iwe na ndugu waalikwa…sherehe isiyokuwa na watu hiyo sio sherehe….

Na karamu kama Harusi sio ruhusa kila mtu kuingia, isipokuwa walioalikwa tu! Na ni kwanini sio watu wote wanaruhusiwa kuingia karamuni?..Ni kwasababu ya bajeti!…Waliochangia mara nyingi ndio wanaopewa kadi ya mwaliko. Na sherehe nyingi siku chache kabla ya tukio lenyewe, kadi zote zinakuwa zimeshagawiwa kwa wahusika, na hivyo hakuna nafasi tena ya mtu mwingine kuingia, Idadi ya viti imehesabiwa na Idadi ya watu imeshajulikana, mwingine yeyote akitaka kujichomeka kwenye karamu ile, siku ya Harusi atazuiliwa mlangoni…Na sababu ya kuzuiliwa mlangoni sio kwamba ni kwasababu anachukiwa, au kwasababu ni mtu mbaya sana hapana! Sababu pekee ni kwasababu nafasi yake haipo kwenye karamu hiyo, na hiyo inatokana na pengine hakuchangia, na hivyo akakosa kadi, na hata akiingia nafasi ya kiti hatapata humo ndani kwasababu Kila kitu kipo kwenye mahesabu, hivyo ataishia kuvuruga tu karamu badala ya kuipendezesha.

Kwasababu uwepo wa hiyo karamu ni kutokana na michango ya waalikwa..Gharama zote zimetokana na michango ya waalikwa.

Na katika ufalme wa Mbinguni ni hivyo hivyo… Ufalme wa Mbinguni unajengwa na michango ya Watakatifu. Bwana alipokwenda mbinguni yeye ni kama Mwana-kamati Mkuu, na Mkuu wa Sherehe..Gharama zote za maandalizi, zinatokana na Maisha ya watakatifu huku ulimwenguni…Kila atakayechangia gharama hizo, ndivyo anavyojiwekea nafasi nzuri ya kuwepo ndani ya ile karamu Mbinguni. Ndio maana Bwana Yesu mwenyewe alisema…

Mathayo 11: 12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”. Kwahiyo kama tunasubiri unyakuo wa ghafla, na hakuna chochote tunafanya kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, hicho kitu tuondoe kwenye akili..Watakaonyakuliwa ni wale tu watakaoalikwa, na walioalikwa ni wale waliochangia kitu katika ufalme wa Mbinguni.

Sasa tutachangiaje katika Ufalme wa Mbinguni ili tuweze kuuingia?

Biblia inasema katika kitabu cha Luka..

Luka 10:25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?

26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

27 AKAJIBU AKASEMA, MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, NA KWA ROHO YAKO YOTE, NA KWA NGUVU ZAKO ZOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE; NA JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.

28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi”

Kwahiyo Mchango mkubwa unaohitajika ili kujitengenezea nafasi katika Ufalme wa Mbinguni NI UPENDO WA MUNGU NA WA NDUGU..HIZO NDIZO TIKETI!.

Kumpenda Mungu kwa Nguvu zetu zote maana yake unatumia nguvu zako za mwilini na rohoni kutimiza mapenzi ya Mungu..Nguvu zako za ujana ambazo ungepeleka kutatufa mambo ya ulimwengu huu, unazitumia kumtafuta Mungu, Nguvu zako zote unazipeleka katika kuhubiria wengine injili, nguvu zako za kuimba, za kucheza, za kusoma..unazitumia kumwimbia Mungu, kumchezea Mungu, kusoma Neno la Mungu….. wakati huu ambao unaweza kutembea, kukimbia..Ndio wakati wa kukimbia kwenda kuihubiri Injili, wakati huu ambao mwili wako una nguvu na afya, ndio wakati wa kufunga, na kuomba katika kumtafuta Mungu.

Na inaposema Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, maana yake unampenda pasipo unafiki, Unapompenda mtu kwa moyo, huwezi kumuumiza, utajitoa kwake kwa kila kitu, huwezi kufanya jambo ukitazamia malipo, na unapofanya jambo kwa moyo siku zote huwezi kufanya kwa kulazimishwa kwasababu unafanya kwa moyo…. kadhalika tunapaswa tumpende Mungu kwa moyo, ikiwa na maana kuwa hatupaswi kumtafuta kwa kulazimishwa lazimishwa, wala hatutakiwi kufanya kazi yake kwa kusukumwasukumwa..walata hatutakiwi tumtafute kwasababu tunataka fedha kutoka kwake, au tunataka utajiri kutoka kwake, tunamtafuta kwasababu tunampenda kutoka moyoni, kwasababu yeye ni Mungu wetu, na tukimpenda kwa Namna hiyo atahakikisha anatutimizia mahitaji yetu pasipo hata sisi kumwomba kwani anajua tunayohitaji kabla hata hatujamwomba..

Tatu, tunapaswa tumpende Mungu kwa Akili zetu zote, Maana ya kumpenda Mungu kwa akili maana yake ni kutumia akili katika kumtafuta na kumtumikia Mungu..Na akili hiyo inatokana na kulinganisha mambo, unajifunza kuweka mambo mawili kwenye mizani na kuchagua moja lililo na uzito..Kwamfano kununua kiatu cha laki moja na huku huna biblia mkononi, huko ni kutotumia akili, kutokusoma Neno kwasababu huna Biblia na huku una smartphone mkononi mwako, huko pia ni kutokumia akili, kwasababu ungeweza kusoma kwa kutumia hata hiyo hiyo simu yako ya mkononi.. Kushindwa kumjua Mungu kwasababu tu hujakutana na mhubiri wa kukuhubiria barabarani, huko pia ni kutokutumia akili, kwasababu ungeweza kutumia simu yako hiyo hiyo kupata mafundisho yoyote yamhusuyo Kristo katika Mtandao. Kwahiyo kwa ulegevu kama huo unaweza kusababisha kukosa nafasi katika karamu ile.

Na tiketi ya nne ni kumpenda Mungu kwa roho yako yote. Kumpenda kwa roho ni Zaidi ya kumpenda kwa moyo, kwa roho maana yake unampenda mtu kwa utu wa ndani kabisa, (Utu wa Ndani unahusisha Ibada), ukimpenda mtu kwa moyo unakuwa humwabudu, lakini ukimpenda kwa roho ni unafikia kiwango cha kumwabudu….unakuwa tayari kufa hata kwaajili yake na kwaajili ya Injili, unakuwa na shauku ya kumwona Mungu, unakuwa na shauku ya kumwabudu na unakuwa pia na shauku ya kumaliza kazi ya Mungu kwa gharama yoyote ile ili ukamwone uso kwa uso. Kila siku unafikiria namna ya kuimaliza kazi ya Mungu kama alivyokuwa Bwana.

Na mwisho kabisa ni kuwapenda majirani zetu kama nafsi zetu..kama vile unavyojipenda wewe, hakuna hata siku moja umefikiria kujilipizia kisasi au kujisengenya mbele ya mwingine, au kujiangamiza mwenyewe vivyo hivyo tunapaswa tuwapende wale wanaotuzunguka kwa upendo wa viwango hivyo hivyo.

Vigezo hivyo vitano ndivyo vinavyotumika kuandaa nafasi za Wateule karamuni, mambo hayo 5 ndio kadi ya mwaliko…Kila mmoja, haijalishi ni Mtume,mchungaji, mwalimu, mwinjilisti, mwimba kwaya,Nabii, mpiga gitaa kanisani, au msafisha choo cha kanisa, au mtunza bustani wa kanisa…ni Lazima afanye mambo hayo ili aurithi uzima wa milele, ili aingie karamuni…Vigezo hivyo vitano ndio vinavyotumika kutengeneza kadi ya mwaliko wa kuingia kwenye mji ule.

Ndio maana Bwana Tangu wakati ule mpaka leo bado anaandaa makao…kila kizazi watu watu wajiingiza kwa nguvu, wanatengeneza tiketi zao na kujitwalia nafasi. Kila kizazi watu wanajiingiza kwa nguvu…Hakuna nafasi za watu wasiojishughulisha na ufalme wa Mbinguni.

Luka 16:16 “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu”.

Je! Na wewe umealikwa?..Unayo Kadi yako mkononi? Unayo nafasi katika ufalme wa Mbinguni? Umeingia kwa nguvu? Au unaendelea na matendo mabaya ya giza na huku unasubiria unyakuliwe?.. Biblia inasema pia waovu wana sehemu yao katika lile ziwa la moto, ikiwa na maana kuwa, hata kuzimu nako watu wanajitengenezea nafasi zao kule kuanzia sasa.

Ufunuo 21:8 “ Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Kama hujampa Kristo masha yako, mlango upo wazi sasa, Lakini upo karibuni kufungwa, karamu inakaribia kuanza, fanya hima upate kadi ya mwaliko, kwa kutubu dhambi zako zote, kubatizwa na kuishi kwa vigezo hivyo vitano hapo juu.

Bwana akubariki sana.

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group


Mada Nyinginezo:

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

JE! ADAMU ALIWASALIANA NA MUNGU KWA LUGHA IPI PALE BUSTANINI?

JE! KUCHORA TATTOO NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

NI KWANINI MUNGU HAONEKANI?

(Kwanini Mungu hatumuoni?)….Hili ni swali ambalo karibu kila mtu anajiuliza au alishawahi kujiuliza pengine kipindi Fulani nyuma, kwanini Mungu hajidhihirishi wazi wazi tukamwona kama tunavyoonana sisi kwa sisi?, au kwanini Mungu hatumsikii kama tunavyosikilizana sisi tunavyoongea?….Watu wanasema Ni rahisi kumwona Mungu kwa kazi zake lakini yeye mwenyewe ni ngumu sana ni kwanini kaamua kuwa hivyo? Na hiyo imewafanya watu wengi kuishia kutoamini kabisa kama kuna Mungu na wengine wameishia kusema Mungu amekufa..

Lakini Je! kutokumwamini Ndio kutaleta suluhisho la yeye kutokuonekana?, Jibu ni hapana, yeye atabakia kuwa Mungu tu haijalishi tunamfikiriaje au tunamzungumziaje,..Jambo la pekee tunaweza kufanya ni kujiuliza ni kwanini Mungu aonyeshe tabia kama hiyo

Ukweli ni kuwa Mungu hayupo hivyo wakati wote, upo wakati biblia inatuambia tutamwona, uso kwa uso, upo wakati tutakaa naye, upo wakati tutazungumza naye uso kwa uso, (Mathayo 5:8, 1Wakorintho 13:11-12), Ufunuo 21:3 inasema..

“Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.”

Lakini kwasasa yeye ametuweka tuishi katika hali hii ya kutomwona tujifunze kitu, Na siku tukilifahamu vizuri hilo wazo la Mungu, hatutafikiri kitoto tena..Embu jaribu kufikiria, wewe ulipokuwa mtoto, au kijana ambaye upo chini ya wazazi wako, jaribu kuwaza ingekuwa mzazi wako kila mahali ulipo au unapokwenda yupo nyuma yako kukufuatilia, ukienda kula mgahawani yupo hapo anakuangalia ni chakula gani unakula, ukienda shule yupo hapo nyuma yako anakuangalia, ukiingia darasani yupo pale nyuma ya darasa na yeye anakuangalia kuakikisha ni kitu gani unasoma au unaandika, ukiwa unazungumza na marafiki zako yupo hapo anakusikiliza mazungumzo yako na kukuambia zungumza nao hivi, au usizungumze nao vile, ukiwa upo kwenye michezo yupo pembeni yako kukuchunga usiumie, ukienda uwani, yupo hapo nje anakusubiria utoke,..kila kitu unachokifanya yupo hapo pembeni yako anakuangalia, anasema ni kwasababu anakupenda na anakujali na ndio maana hataki akae mbali na wewe hata sekunde moja..anataka kila wakati umuone na yeye akuone..

Sasa jiulize wewe kama mtoto utajisikiaje, cha kwanza ni kuwa japo mzazi wako anakupenda sana na kukujali sana, lakini kule kuwa na wewe kila sekunde kila dakika kunakufanya upoteze uhuru Fulani wa kufanya mambo yako hata yale ya msingi.., pili kunakufanya uboreke kwa sehemu Fulani, haijalishi nia ya mzazi ni nzuri kiasi gani..Kuna mahali utahijitaji uhuru wako sehemu Fulani ili ufanye mambo yako kwa ufasaha zaidi.

Na kwa Mungu ndivyo ilivyo, tunasema Ee Mungu naomba kila saa nikuone, naomba kila saa nisikie sauti yako, naomba kila saa unitokee, tunasema hivyo ni kwa vile tu hutujui tunachokiomba,..Wewe unaweza kuona ni jambo jema na zuri kumwona Mungu au kusikia kila dakika anasema na wewe, lakini katika upande wa pili utakuwa unamtumikia Mungu kwa presha na bila UHURU ambao Mungu anataka utembee nao, na hilo ndilo jambo ambalo Mungu hapendi.

Wengi tunatamani Mungu akishatuokoa tu, basi saa hiyo hiyo tuanze kumsikia akizungumza ndani yetu na kutupa maelekezo karibu ya kila kitu cha kufanya..hata tukitaka kupiga hatua tunataka tumsikie Mungu akituambia piga hatua tano kisha kunja mbili kulia, fanya hivi, fanye vile, sema hiki, usiseme kile..kama vile GPS, ambayo hiyo inakuongoza kama vile Roboti kugeuka kulia na kushoto ili kufika pale ulipoelekezwa…

Mungu hayupo hivyo, yeye anachofanya ni kutugawia sisi ramani mkononi, ambayo inatuonyesha mwanzo hadi mwisho wa safari yetu, na katika ramani hiyo hiyo anatuonesha na mwisho wa njia mbaya zote, na katika ramani hiyo hiyo ndani yake kaweka mashauri ya njia sahihi ya kuiendea, Hivyo hapo ni wewe kuchagua njia ipi inayokufaa, kama utachagua njia ya uzima hapo ni wewe, kama utachagua njia ya mauti hapo ni wewe mwenyewe, lakini ramani inaelekeza kila kitu na ramani yenyewe ni BIBLIA TAKATIFU.

Lakini leo hii ukimpa Kristo maisha yako na ukaufahamu ukweli usitazamie utasikia sauti inakuambia usiende disko, au usizini au usiibe, au usiabudu sanamu, au kula hichi au usile kile, au ukaanza kutokewa na Mungu kila siku, kwenye ndoto, ikitokea jambo kama hilo basi ufahamu kuwa ni Mungu anataka kukufundisha kitu lakini usidhani itakuwa ni jambo la sikuzote. Ni wajibu wako wewe kuishi kulingana na njia za uzima inavyoelekeza ili ufikie mwisho mwema, na ndivyo utakavyoishi kwa uhuru ambao Mungu anataka auone kwetu..Ni sawa na mwanamke mwerevu aliyeolewa, ambaye akishaingia tu ndani ya nyumba ya mumewe hasubirii kusikia mumewe akimwambia nipikie chai, au nenda sokoni, yeye mwenyewe tu atajua majukumu yake kama mwanamke na kuanza kujitumia sawasawa na alivyoitiwa vivyo hivyo na mwanamume mwenye akili ambaye ameona, hatangojea siku mkewe amwambie mume wangu nenda katafute ugali wa nyumbani, yeye mwenyewe tu atatoka na kwenda kupambana ili kuakikisha kuwa familia yake inakula na kufurahi.

Hivyo ikiwa wewe ni mkristo, usisibiri Bwana akupe maagizo Fulani ya kufanya, utafunga sana, utaomba sana na usipate majibu yoyote, lakini tambua majukumu yako kama mkristo na uishi kulingana na ramani uliyopewa mkonono mwako yaani biblia!, na huko huko mbele ya safari ikiwa kuna kitu cha kuongezea au kina mapungufu ndipo Bwana atakuambia rekebisha hapa au rekebisha pale.

Kwamfano kama mkristo unajua kabisa tunapaswa kumzalia Mungu matunda ya aina zote (yaani ya haki na ya kazi), sasa tusisubirie kumngojea Mungu atuambie tukawashuhudie wengine waje kwake Hilo hutakaa ulisikie, Kwasababu Mungu anataka tuifanye kazi yake kwa uhuru..Hivyo tumia uhuru uliopewa kuifanya kazi ya Mungu pale ulipo kabla siku zako hazijaisha hapa duniani…Wapo wengi wanahitaji kumjua Mungu kama wewe ulivyo, lakini ukisubiria uone maono, hutafika popote.

2Wakorintho 3:17 Basi ‘Bwana’ ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.

Hizi ni siku za mwisho, Bwana wetu yupo mlangoni kurudi, hivyo tuzidi kuongeza nguvu katika kumtafuta yeye.

Bwana akubariki.


Mada Nyinginezo:

HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?

EPUKA KUTOA UDHURU.

DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

KWANINI BWANA YESU ALISEMA PALE MSALABANI NAONA KIU?

BIBLIA INAMAANA GANI KUSEMA “VILIVYOTAKASWA NA MUNGU, USIVIITE WEWE NAJISI”?


Rudi Nyumbani:

Print this post

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

Shalom, Mtu wa Mungu, karibu tujifunze biblia, Jukumu kubwa tulilopewa miongoni mwa mengi ni jukumu la kumfahamu sana YESU KRISTO, Na lengo kuu la kumfahamu sio kwasababu yeye anauhitaji sana wa Utukufu, au uhitaji sana wa kutafuta ajulikane, hapana! Hilo sio lengo…kwasababu pale tu alipo tayari anajulikana…Lakini bado anatuasa tunapaswa tumfahamu sana yeye…Hivyo hiyo ikimaanisha kuwa kwa jinsi tunavyomfahamu yeye ni tofauti na yeye anavyotaka sisi tumfahamu…

Kwasasa Mtu maarufu kuliko wote duniani kwa wakati wote ni YESU KRISTO, hakuna mwanadamu yeyote aliyewahi kufikia kiwango cha umaarufu alionao Bwana Yesu Kristo, ukienda kwa wachina, wahindu, wabudha wote wanamjua Yesu Kristo…Hata watu ambao sio wakristo kwa namna moja au nyingine walishawahi kumsikia Yesu Kristo katika Maisha yao..kwahiyo yeye ni maarufu tayari.

Biblia inasema katika…Waefeso 4: 13 “ …hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”

Na kwanini anataka sisi tumfahamu sana yeye? Mstari wa 14, hapo juu umetupa majibu… Ni ili tusiendelee kuwa Watoto wachanga, tukitupwa huku na huko, tukidanganywa na kila upepo wa elimu, na kuishia kuzifuata njia za udanganyifu.

Kwahiyo hakuna Elimu nyingine itakayoweza kutufanya tusiweze kudanganyika na elimu ya mashetani, isipokuwa Elimu ya kumfahamu Yesu Kristo, hakuna namna yoyote utakayoweza kuifahamu na kuidhibiti noti bandia pasipo kwanza kuijua noti halali ilivyo, ukishaifahamu noti halali ilivyo na tabia zake ndivyo utakavyoweza kuijua noti bandia..Kadhalika tunajukumu kubwa sana la kumfahamu Yesu Kristo kwa undani ili tuweze kuyadhibiti mafundisho ya mashetani na wapinga Kristo.

Leo tutajifunza kwanini Yesu Kristo, anajulikana kama Mwana wa Daudi na kwanini ni MFALME.

Sasa ni Dhahiri kabisa tunajua kuwa Yesu hakuwa na Baba wa kimwili, lakini kuna mahali kwenye maandiko kajitambulisha kuwa Mwana wa Daudi.. Sasa kwanini alijiita hivyo?

Sababu pekee ya Bwana Yesu kujulikana kama mwana wa Daudi, ni kutokana na Baraka Daudi alizozibeba, lakini si kutokana na undugu wa kidamu..Wewe unaitwa mwana wa Baba yako kutokana na uhusiano wa kidamu..lakini unaweza ukaitwa mwana wa Raisi wako, ila si kwa uhusiano wa kidamu bali wa pengine wa kiitikadi fulani….

Kwamfano pia sisi wakristo tunaitwa Wana wa Mungu, si kwasababu tumezaliwa familia moja na Muumba wetu,hapana au kwamba tuna damu moja na Mungu, hapana ni kutokana na Baraka za kimbinguni zinavyohusiana na sisi ndio maana tunaitwa wana wa Mungu.

Vivyo hivyo tunajulikana kwamba ni wana wa Ibrahimu , sio kwasababu sisi tuna damu moja na Ibrahimu, hapana bali ni kwasababu ni warithi wa Ahadi zile zile alizopewa Ibarahimu na Mungu, ndio maana na sisi tunajulikana kama wana wa Ibrahimu, Na Bwana Yesu ndio hivyo hivyo, Baraka alizopewa Daudi na mnyororo wa ukoo wake wote zilimhusu pia Bwana wetu Yesu Kristo…Daudi alikusudia kumjengea Mungu, Nyumba na hivyo Mungu akambarikia yeye na uzao wake kuwa uzao wa kifalme milele.(soma 2 Samweli 7:1-12)

kwasababu alizaliwa katika nyumba ya Yusufu ambaye alikuwa ni wa ukoo wa Daudi uliobarikiwa (ukoo wa kifalme),..Moja ya Baraka za ukoo wa Daudi ni kwamba utakuwa ni ukoo wa kifalme, kwamba wazao wote wa Kwanza wa Daudi walipakwa Mafuta na Mungu wawe wafalme soma (2 Wafalme 8:19,). Na ndio maana Bwana Yesu alipozaliwa katika nyumba ya Yusufu kama mzaliwa wa kwanza, roho ya kifalme ilikuwa juu yake. Kwahiyo kwa namna yoyote ile ni lazima angekuja tu kuwa Mfalme..

Je! Unajua kuwa Yusufu baba yake Yesu angepaswa awe mfalme wa Israeli kwa kipindi kile, kulingana na ahadi Mungu aliyomahidia Daudi?…Lakini kutokana na dhambi zao, Taifa la Israeli lilikatwa na uzao wa Daudi wa kifalme ukasimamishwa katika kutawala na ulisimamishwa kipindi gani?..

Kama ukisoma kitabu cha Wafalme, baada ya Daudi kufa, akafuata mwanawe Sulemani akawa mfalme kweli kulingana na ile Ahadi lakini naye pia akafa, na ikaendelea hivyo hivyo, kwa wajukuu na vitukuu vya Daudi, mpaka mfalme wa mwisho aliyetawala Yuda aliyeitwa Sedekia, ambaye alikuwa ni kitukuu cha 20 cha Daudi, huyu ndiye mfalme wa Mwisho kutawala Yuda, baada yake yeye, ndio Watu wakapelekwa Utumwani Babeli, hiyo ndiyo siku waliokatwa na waliporudi kukawa hakuna mfalme tena katika Israeli…vitukuu vya Daudi vilivyozaliwa baada ya Sedekia Mfalme wa Mwisho kufa, wakawa ni watu tu wa kawaida, kama watu wengine…

Ndio maana Yusufu baba yake Yesu alikuwa ni mtu wa kawaida tu maskini, ingawa alikuwa ni mwana wa kifalme…(Kwa urefu fuatilia ukoo huu wa Yesu kwenye kitabu cha Mathayo 1:1-17), laiti Israeli asingeasi na kupelekwa utumwani, Yusufu baba yake Yesu angekuwa mfalme wa Yuda, na Kristo angezaliwa huko…

Hivyo Israeli iliendelea kuwa kama mti uliokatwa baada ya kutoka Babeli…Wayahudi wakakaa mamia ya miaka bila mfalme….kukawa hakuna dalili yoyote ya Mfalme kunyanyuka katika uzao wa Daudi,..kwani Utawala wa Rumi ulikuwa umekamata dunia nzima, na Warumi waliwaweka watu wao kwenye makoloni yao yote, mpaka Israeli ilikuwa ni koloni la Warumi..Hivyo mtawala aliyetawala koloni la Israeli alikuwa ni Mrumi…jambo hilo liliendelea kwa miaka mingi…lakini Biblia ilitabiri katika Isaya Mlango wa 11 kuwa litatoka chipukizi katika shina la Yese….Kumbuka Yese alikuwa ni Baba yake Daudi, kwahiyo ni sawa na kusema litatoka chipukizi katika shina la Daudi au katika uzao wa Daudi. Tunasoma hayo katika…

Isaya11:1 “ Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.

2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana”.

Kama ni msomaji mzuri wa maandiko utagundua kuwa…hilo shina linalozungumziwa hapo si lingine Zaidi ya BWANA YESU KRISTO mwenyewe…Biblia inasema litatoka shina, ikiwa na maana kuwa ni kutoka katika mti uliokatwa, nalo litazaa sana matunda… Kama ulishawahi kuona mti mkubwa uliokatiwa chini kabisa..linakuwa linabaki tu kama gogo…halafu baada ya kipindi fulani unaona kitawi kidogo cha kijani kinajitokeza ubavuni mwa lile gogo, na kama hakitakatwa na chenyewe, baada ya kipindi fulani kitakuwa kikubwa na hatimaye kuwa tena mti mkubwa kama ulivyokuwa mwanzo…

Ndicho kilichotokea baada ya uzao wa Daudi kukatwa na kupelekwa Babeli…ni sawa na mti uliokatwa…lakini chipukizi likatoka, katika uzao huo huo wa Daudi..

Bwana Yesu, Mwana wa Daudi, mzao wa kifalme, mwenye ahadi ya kifalme juu yake, alizaliwa huko Bethlehemu, alikuwa ni mfalme aliyetoka katika shina lililokatwa ndio maana utaona alizaliwa katika zizi la ng’ombe, familia ya kimaskini, laiti Yusufu baba yeke angekuwa mfalme basi naye pia angezaliwa katika familia ya kifalme..Lakini kinyume chake alizaliwa katika ufalme uliokatwa…

Lakini maandiko yanatabiri, huyo atakuja kuwa mti mkubwa na utazaa sana matunda, na ufalme wake utaenea duniani kote…kipindi alichokuja miaka 2000 iliyopita, roho ya Bwana ilikuwa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana” Kwa hekima, na maarifa aliyoyabeba alituletea sisi Wokovu…ambao mpaka sasa tunanufaika nao…., Lakini katika utawala wa miaka 1000 ijayo, ndio tutamwona vizuri kama Mfalme, aliyeketi katika kiti cha Kifalme…katika wakati huo, yeye pamoja na sisi ambao sasa tumemwamini, tutatawala naye, sisi tutakuwa wafalme nay eye atakuwa kama Mfalme wa wafalme.

Wakati huo Mamlaka yote ya kifalme atakuwa nayo yeye, utakuwa sio wakati wa wokovu tena bali wakati wa utawala, sasa hivi ndio tupo wakati wa wokovu, nyakati hizo zitakuwa ni nyakati za utawala mkuu wa Yesu Kristo. Dunia yote itajawa na kumcha Bwana, kutakuwa hakuna vurugu, kutakuwa na Amani isiyo ya kawaida..simba na kondoo watakaa pamoja na hawatadhuriana, mtoto atacheza na nyoka, na hakutakuwa na madhara yoyote.

Tusome tena Isaya hii 11 Mpaka mwisho..

“1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.

2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;

3 na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;

4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.

5 Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.

6 Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.

7 Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe.

8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.

9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari.

10 Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu”.

Ufunuo 3:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, KAMA MIMI NILIVYOSHINDA NIKAKETI PAMOJA NA BABA YANGU KATIKA KITI CHAKE CHA ENZI.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”

Na pia alisema..

Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.

17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”

Kama hujampa Yesu Kristo Maisha yako, jua umechelewa sana, lakini mlango bado hujafungwa ingia kabla mlango hujafungwa..mwisho wa mambo yote umekaribia, na Kristo yupo Mlangoni kurudi, atakaporudi nyakati hii ya mwisho atakuja kama mfalme na mtawala mkuu hatakuja tena kama mwokozi.

Bwana akubariki.

Tafadhali share kwa wengine


Mada Nyinginezo:

MWANA WA MUNGU.

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

JIWE LA KUSAGIA

HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.

JE! MTU KUSIKIA SAUTI ZA WATU WALIO MBALI, KUNAWEZA TOKANA NA MUNGU?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “HERI WALIOTASA, NA MATUMBO YASIYOZAA, NA MAZIWA YASIYONYONYESHA”?


Rudi Nyumbani:

Print this post

MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, Leo ni siku nyingine Bwana ametupa neema  mimi na wewe kuiona, hivyo ni wajibu wetu kiutimia vizuri siku yetu kwa kujifunza maneno yake ambayo ndio nuru yetu na uzima wetu hapa duniani kila siku.

Leo kwa neema za Bwana tutajifunza juu ya huu mwaka wa Bwana uliokubaliwa ni upi ambao Bwana Yesu aliuzungumzia katika…

Luka 4:18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa”.

Sasa ni vizuri kufahamu kuwa biblia inaposema mwaka sio kila mahali inamaanisha kuwa ni mwaka Fulani mahususi labda 2018 au 2019 hapana, bali inamaanisha kipindi Fulani cha wakati kilichotengwa mahususi kukamilisha lengo Fulani chenye mwanzo wake na mwisho wake ambacho kimefananishwa na mwaka..

Hivyo hapo ni sawa na kusema “kuutangaza wakati wa Bwana uliokubaliwa”..Ikiwa na maana kuwa kama huo ndio wakati uliokubaliwa, basi pia  zilikuwepo nyakati nyingine ambazo hazikukubaliwa…. Na pia tunapaswa kufahamu ulikubaliwa kwa kusudi lipi?

Katika agano la kale kila mwaka wa 50 uliitwa Yubilee, mwaka huu ulikuwa ni mwaka wa maachilio, haikuruhusiwi kulima wala kupanda, ardhi ilikuwa inastarehe, ni mwaka ulioitwa mwaka wa maachilio ya watumwa, na kusamehe watu madeni yao (Walawi 25:11),

Na ndicho Bwana Yesu alichokuja kukifanya katika agano jipya, kuleta maachilio ya vifungo vyote, vya rohoni na mwilini, vile vile alikuja kuutangaza huo mwaka Bwana uliokubalika, yaani wakati wa Mungu kumkubali mwanadamu, kumwokoa na kumfunulia uso wake na mapenzi yake amjue yeye..Hiyo ililetwa na Bwana YESU tu peke yake, kumbuka  hapo kabla Mungu alikuwa hampokei Mwanadamu yeyote haijalishi ni kuhani au nabii au rabi kiasi gani, hakukuwa na mwanadamu yeyote ambaye aliwahi kumkaribia  Mungu na kutoa hoja zake pasipo kuwa na deni la dhambi ndani yake, na ndio maana ilimpasa kuhani mkuu peke yake aingie patakatifu pa patakatifu mara moja tu kwa mwaka afanye upatanisho wa dhambi za watu, pamoja na dhambi zake mwenyewe ambazo kimsingi zilikuwa haziondolewa bali zinafunikwa, baada ya hapo shughuli imeishia hakuna mashauri wala mahojiano, unaondoka mbele ya madhabahu ya Mungu ambayo ilikuwa duniani na wala sio mbinguni..

Lakini Bwana Yesu alipokuja yeye alisimama kama kuhani mkuu, na hivyo sasahivi sio tu tumepata ondoleo la dhambi na  maombi yetu kusikiwa bali pia tunaketi na kula na kunywa na Mungu katika ulimwengu wa Roho kama vile Baba na mtoto wake wa pekee ampendaye.. Haleluya!.

Kwahiyo tunaishi bado katika kipindi cha Mwaka wa Bwana uliokubalika…Lakini huu wakati hautadumu milele, mwaka Bwana uliokubalika hautadumu milele, kuna wakati Bwana Yesu kama kuhani mkuu atasimama kutoka katika kiti chake cha ukuhani, na kuanzia huo wakati na kuendelea hakutakuwa na rehema tena, na wala Mungu  hatakuwa na nafasi ya kuwatazama waasi, kinachobakia tu ni ghadhabu ya Mungu kumiminwa juu ya waovu wote..Na huo wakati upo karibu sana ndugu, Unyakuo ukishapita tu basi fahamu kuwa kiti cha rehema kilishaondolewa..

Luka 13.24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25 Wakati mwenye nyumba ATAKAPOSIMAMA na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.

Na ndio maana biblia inasema wakati uliokubalika ndio sasa, ndio huu tulionao mimi na wewe,  yaani leo kwasababu kesho hatujui itakuwaje….

2 Wakorintho  6:2 “(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)”..

Usisubirie wakati ambao haukubaliki ndio umkumbuke Mungu, utakuwa umeshachelewa ndugu. Ikiwa bado upo mbali na Kristo wakati ndio huu wa sasa tubu dhambi zako, jitwike msalaba wako umfuate YESU, atakusamehe dhambi zako, kisha hakikisha baada ya kutubu kwako unabatizwa  kisha yeye mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu bure kama alivyoahidi katika (Matendo 2:38)…

Bwana akubariki sana.


Mada Nyinginezo:

NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?

CHANZO CHA MAMBO.

WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA.

JE! TARATIBU ZA KUFUNGA NDOA [YAANI HARUSI] NI AGIZO LA MUNGU AU NI MAPOKEO TU YA KIBINADAMU?

KUNENA KWA LUGHA KUKOJE?


Rudi Nyumbani:

Print this post

UKristo Ni Nini?

Ili kuelewa Nini maana ya Ukristo, tutafakari kwanza maana ya Neno UTAIFA…Neno utaifa limetokana na Nomino Taifa…Kwahiyo kitendo chochote kinachofanyika kinachohusisha mapenzi na Taifa, kitendo hicho kinaitwa Utaifa..

Tukirudi katika UKristo, Neno Ukristo nalo pia limetokana na Nomino Kristo…Na maana ya Kristo ni “Mtiwa Mafuta” au “Masihi” na wala sio Yesu,…Mtu aliyetiwa Mafuta na Mungu zamani hizo aliitwa kristo  na hata sasa kibiblia bado wanajulikana hivyo hivyo kama makristo.. Chimbuko la neno hilo Masihi au kristo Ni lugha ya Kigiriki.

Hivyo walikuwepo makristo wengi, sana zamani..Katika Biblia Daudi alijulikana kama ni kristo (yaani masihi wa Bwana) 1Samweli 16:6, kadhalika Mfalme Sauli (1Samweli 24:6) na wengine wengi, walijulikana kama ni makristo/masihi wa Bwana.

Lakini alipokuja mmoja ambaye alikuwa ni mkuu kuliko hao wote, aliyetiwa mafuta na Mungu mwenyewe kuwa juu ya vitu vyote, huyo naye aliitwa masihi au Kristo, isipokuwa ili kumtofautisha na masihi na makristo wengine, huyu jina lake lilianza kwa Herufi kubwa, yaani aliitwa Kristo badala ya kristo. Na huyo si mwingine zaidi ya YESU. Ndio maana mahali popote katika biblia panapomtaja Kristo Yesu ni lazima hilo neno Kristo lianze kwa herufi kubwa, kuwatofautisha na makristo wengine.

Kwahiyo tukirudi kwenye swali, U-Kristo ni nini? Jibu ni kuwa U-Kristo ni kitendo mtu anachokifanya kinachohusisha mapenzi yake na mtu mmoja anayeitwa Kristo Yesu, zingatia hilo neno Kristo Yesu na sio “kristo yesu”…kwasababu makristo wapo wengi, na ma-yesu wapo wengi  lakini Kristo yupo mmoja na Yesu yupo Mmoja.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

DINI NI NINI?

JE! UKIMWI UNATIBIKA?

SHETANI NI NANI?

JE! UBATIZO SAHIHI NI UPI?

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Biblia ni nini?

Biblia ni nini?

Ni neno la Kigiriki, lenye maana ya “mkusanyiko wa vitabu vitakatifu”..kikiwa kitabu kimoja kinaitwa Biblion lakini vikiwa vingi vinaitwa Biblia..

Hivyo Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vitakatifu..Vitabu hivyo vimeandikwa na wanadamu, lakini kwa Uongozo wa Roho Mtakatifu, kwasababu Mungu anafanya kazi ndani ya watu..(Warumi 8:28), Wanadamu wachache Mungu aliowachagua waliandika habari za Mambo yahusuyo sheria za Mungu, Maneno ya Mungu, Uweza wa Mungu, Upendo wa Mungu, huruma ya Mungu, Utukufu wa Mungu, na Ukuu wa Mungu..

Bwana Mungu aliwachagua waandishi hao kutoka katika makundi yote, kwa nyakati tofauti tofauti..Iliandikwa na Wafalme, Manabii, Matabibu, Wavuvi wa samaki, Wakusanyaji wa kodi n.k

Biblia imegawanyika katika sehemu mbili:  Agano la Kale na Agano Jipya, au Agano la Kwanza na Agano la Pili..

Agano la kale lina jumla ya vitabu 39, na Agano la Jipya lina jumla ya vitabu 27 kufanya jumla ya vitabu 66 vya Biblia Nzima.

Kiini cha Biblia yote ni mtu mmoja tu anayeitwa YESU KRISTO, Kila kitabu katika Biblia Takatifu kimeandika kwa wazi au kwa kinabii, habari za Yesu Kristo. Maonyo na Mafundisho yaliyomo ndani yake ni maonyo ya Yesu Kristo Mwenyewe.

Biblia ndio kitabu pekee, kilichobeba sauti ya Mungu ndani yake..Hakuna kitabu kingine chochote duniani kilichobeba kusudi la Mungu juu ya mwanadamu zaidi ya Biblia Takatifu. Na hakuna njia nyingine yoyote mwanadamu anaweza kumfikia Mungu tofauti na kitabu hicho


Mada Nyinginezo:

SHETANI NI NANI?

SIKU YA HUKUMU ITAKUWAJE?

DINI NI NINI

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE


Rudi Nyumbani:

Print this post

KIFAA BORA CHA MATUMIZI.

Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, maandiko yanasema,

Mhubiri 10:10 “Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa”.

Katika tafsiri nyingine hilo Neno Chuma limetafsiriwa kama shoka, ikiwa na maana kuwa kama shoka ni butu au halinolewi mara kwa mara basi itampasa mtu kutumia nguvu zaidi katika kukata vitu au kuchonga, au kuchanja kama anakata nyama itampasa atumie nguvu zaidi kuikata nyama ile, kama anakata mti basi itampasa atumie jitihada ya ziada yenye kuchosha kuudondosha mti kwasababu Shoka ni butu haliwezi kupenya kwa haraka ndani ya shina..Tofauti na kama kifaa hicho kingekuwa ni kikali, angetumia nguvu chache tu na matokeo kuwa makubwa ndani ya muda mfupi…

Ni kama tu kisu au kiwembe kikiwa ni kakali basi ukipitisha hata kwenye karatasi ni mara moja tu limegawanyika, lakini kama ni butu basi utakipeleka mbele na nyuma, na utachukua muda, na bado halitachanika vizuri kama lile lililochanwa na kiwembe kikali..

Lakini Mhubiri anaendelea kwa kusema, “walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa”,.. Ikiwa na maana usipoweza kutumia hekima, kuamua maisha yako kwa kukifanya kisu chako kuwa kikali basi mambo yako, licha tu ya kuwa magumu lakini pia utatumia nguvu nyingi kuyafikia…

Duniani Vipo visu vingi tofauti tofauti na mashoka tofuati tofauti na kila mtu analo lake, ambalo kwa namna moja au nyingine linamsaidia kufanya mambo yake kuwa mepesi, wengine ni elimu, wengine ni ujuzi, wengine ni fedha n.k..Lakini hasara moja ya vifaa hivyo vyote sio vya kudumu, huwa vinakuwa butu kwa jinsi muda unavyokwenda na kwa jinsi vinavyotumika…. Mtu akiviacha vinachakaa na pia isitoshe havitumiki kila mahali…huwezi kutumia elimu kutibu kifo, vile vile huwezi tumia pesa kununua furaha, au upendo au amani..

Ni kifaa kimoja tu ambacho Mtu mwenye akili na Hekima anaweza kukitumia kwa matumizi yote na kukata kila kitu pasipo kutumia nguvu, na bado kutokupungua ubora wake na makali yake…Nacho ni Neno la Mungu..

Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.”

Mtu akiwa na Neno la Mungu peke yake, hiyo ni salaha tosha, ya kurahisisha mambo yako..hili haliwi butu kama vile mengine, linao uwezo sio tu wa kukata kwa ukali zaidi ya upanga wowote, bali pia linaweza kuchoma hata kuzigawanya nafsi na roho, yaani linaingia ndani ya moyo wa mwanadamu na kugawanyisha kila kitu na kutambua mawazo yake, kitu ambacho pesa haiwezi kufanyi, elimu ya dunia hii haiwezi kufanya, ujuzi wowote ule wa mwanadamu hauwezi kufanya..

Ndio maana mtu yeyote aliyejaa Neno la Mungu ndani yake, hakuna jambo lolote linaloweza kumlemea hata liwe gumu kiasi gani kwasababu anafahamu vizuri silaha aliyonayo inaubora kiasi gani..

Mhubiri anatushauri NI HERI KUTUMIA HEKIMA NA KUFANIKIWA, tunapaswa tujue ni kifaa gani kitakachotufaa katika maisha yetu, katika mapori yanayotuzunguza mbele yetu ambayo yanapaswa yafyekwe kweli kweli, kifaa ambacho tunaweza kukabiliana na adui yetu ibilisi na kummaliza haraka sana bila kutumia nguvu nyingi… silaha hiyo si nyingine zaidi ya Neno la Mungu. Waefeso 6: 17 “Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;”

Tunapoliishi Neno la Mungu, maisha yetu hatutayaona ni magumu, hatutasumbuka kama ulimwengu unavyosumbuka, Kwani ni Mungu mwenyewe ndiye atakayekuwa anatupigania,,Lakini tunapoliweka Neno la Mungu kando, tunapolidharau na kuchagua mambo mengine, au kuyaona mambo mengine ni ya muhimu zaidi ya Neno lake, tuwe na uhakika kuwa safari yetu itaishia ukingoni…Ni kutumia kifaa butu, kuufyeka msitu…Mambo yatakuwa magumu tu, huo ndio ukweli, Nira iliyo nyepesi ipo kwa Bwana Yesu tu, pengine kote ni Nzito na mateso yasiyoelezeka..(Mathayo 11:28)

Ndugu/Kaka Ikiwa hujayakabidhi maisha yako kwa BWANA Mlango wa Neema upo wazi, usisubiri baadaye au kesho, muda umekwenda sana kama unyakuo hautakukuta moja ya hizi siku, hujui baadaye yako itakuwa vipi, waliokufa leo asubuhi sio kwamba walikuwa waovu zaidi yako wewe, au walikuwa wameshajiandaa kwa safari ya kwenda huko ng’ambo, hapana lakini kifo kiliwakuta kwa ghafla tu, na ndivyo kitakavyotukuta wote walio haki na wasio haki…Hivyo fanya uamuzi wa busara wakati huu kwa kutubu dhambi zako kama hujatubu na kumgeukia Bwana sasa hivi.. kumgeukia Bwana Yesu sio kuwa vuguvugu, ni kitendo cha kumaanisha kabisa….Kisha utafute mahali wanapobatiza ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa Jina la YESU KRISTO, kama pia bado hujafanya hivyo..Upate ondoleo la dhambi zako, kulingana na (Matendo 2:38) ili Bwana akupe kipawa cha Roho wake Mtakatifu ambaye ndio muhuri wetu, Mungu anaotutia mpaka ile siku wa ukombozi wetu (Waefeso 4:30).

Bwana Azidi kukubariki.

Maran atha! Bwana wetu anakuja.


Mada Nyinginezo:

MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA?

USIWE SABABU YA WATU KUMKUFURU MUNGU.

LAANA YA YERIKO

NINI MAANA YA USIPUNGUZE WALA KUONGEZA NENO LA MUNGU?

JE! NI DHAMBI KUSHEREKEA SIKU YA KUZALIWA? BIRTHDAY!


Rudi Nyumbani

Print this post

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

Jina la Bwana YESU litukuzwe daima. Karibu tujifunze Neno la Mungu, leo kwa neema za Bwana tutajifunza juu ya njia sahihi ya kufunga.

Zipo aina nyingi za kufunga lakini kwa vyovyote vile, hatufungi ili Mungu atusikie au atujibu maombi yetu, Mungu hasubiri kwanza tuteseke ndio atusikie hapana kwani alishaweka wazi katika Neno lake, kuwa yeye anajua tunachohitaji kabla hata hatujamwomba (Mathayo 6:8)…Lakini pamoja na hayo Kufunga kunasaidia kuongeza uwezekano wa wewe kupata majibu ya maombi yako au kupata unachokitafuta kwa haraka tofuati na yule asiyefunga. Ni sawa tu na mwanafunzi anayesomea maktaba na Yule anayesomea nyumbani, anayesomea maktaba anaongeza uwezekano mkubwa wa kufaulu mitihani kuliko Yule anayesomea nyumbani, kwasababu kule maktaba kunakuwa na utulivu mkubwa na mazingira mazuri ya kujisomea kuliko nyumbani..Lakini hiyo haimfanyi afaulu mtihani moja kwa moja Yule wa nyumbani anaweza kufanya vizuri kushinda hata yeye..Lakini itampasa awe mtu wa kujitambua sana.

Vivyo hivyo na katika kufunga, Mtu mwenye desturi ya kuomba kwa kufunga anajijengea daraja zuri la yeye kuwasiliana na Mungu kuliko Yule apelekaye dua zake kwa Mungu bila kufunga, Kwasababu Kufunga kunampa utulivu Fulani wa Roho tofauti na mtu asiyefunga.

Na hiyo yote ni Kutokana na kutokuwa na Mungu katika mwili, au kutokumwona Mungu katika mwili ndio maana inatupelekea tumtafute Mungu kwa umakini zaidi kuliko kama tungekuwa tunamwona kwa macho…Mitume walipokuwa na Bwana duniani hakukuwa na sababu ya kufunga, ufunge ya nini wakati unayemtafuta upo naye hapo? Mpaka watu wengine wakashangaa inakuwaje hawa ni mitume wa Bwana lakini hawafungi, Ndipo Bwana alikawaambia wanachokifanya hawajakosea kwasababu mimi nipo, Siku zitakuja nitakapoondoka ndipo watakapofunga kama wengine…

Marko 2:18 “Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?

19 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga.

20 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile.”

Hivyo kitendo cha kufunga hakikwepeki sasa kwa mkristo yeyote. Na zipo aina nyingi za kufunga, lakini aina iliyozoeleka ni ile ya kuacha kula chakula. Lakini mfungo huu unafanywa kimakosa na wengi kwasababu ya kutokufahamu ni kwanini mtu anaacha kula..Na ndio hapo mtu mmoja atafunga vizuri kweli hata wiki tatu au mwezi au siku arobaini, lakini anafanya kama desturi za dini nyingine wanavyofanya, ukiangalia huku nyuma utamwona anaendelea na maisha yake ya kidunia anadhani kusikia kule njaa ndo Mungu anampa thawabu,. Hajui kuwa Mungu hamjibu mtu kwa mateso,(Maombolezo 3:31-35) sasa hapo mtu wa namna hiyo kaamua tu kujitesa bure..Hakuna chochote atakachokipata kutoka kwa Mungu.

Au unakuta mwingine anafunga kwa lengo la kumuomba Mungu mambo ambayo sio sawa na mapenzi yake, mwingine atamwomba Mungu ampe mali, lakini ndani ya moyo wake anawaza aitumie kwa anasa, mwingine atamwomba Mungu ampe hiki au kile, lakini nia yake moyoni ni kutumia kwa mambo maovu.. mtu wa namna hiyo pia asitazamie kupata kitu.

Isaya 58:3 “Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.

4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.

5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?

6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?

7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?

8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.

9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;

10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.”

Unaona? Dhumuni la msingi kabisa la kujizuia kutokula mtu anapaswa afahamu ni kuyaleta mapenzi ya mwili chini na kuruhusu mapenzi ya Mungu yaje juu, ile njaa inakukumbusha kwenda mbele za Mungu kwa unyenyekevu mwingi , sikuzote mtu mwenye njaa anakuwa katika uhitaji sana kuliko mtu aliye shiba, hivyo mtu wa namna hiyo anapokwenda mbele za Mungu kumaanisha kwake kunakuwa kwa kiwango cha juu zaidi kuliko mtu aliyeridhika, hata maombi yake yanakuwa marefu sana, jaribu hata kwako utaligundua hilo..Na hiyo ndio faida kubwa ya kutokula wakati wa maombi. Hivyo inapelekea maombi yako kuwa na nguvu zaidi mbele za kuliko wengine.

Vile vile kuna kufunga ambako sio kwa kula, bali kwa kujizuia na mambo mengine yanayoweza kukusonga usiisikie sauti ya Mungu. Kufunga kwa namna hii kumekuwa kwa kawaida kwa watumishi wengi wa Mungu, Nabii Elisha ilimpasa atumie muda mwingi kujitenga na mazingira ya watu ili kudumisha joto la uhusiano wake na Mungu. Sio kwamba kuna shida kujihusisha na mambo ya kawaida ya kila siku, hapana lakini ni utaratibu wa Mungu kuzungumza katika sauti ya utulivu, na kama ni sauti ya utulivu hivyo naye huwa anahitaji mazingira tulivu ya kumwelewa.

Ufunuo wowote Mungu anaompa mwanadamu, hampi akiwa katika mazingira ya usumbufu wa akili, Usijidanganye kuwa Mungu atakupa ufunuo wowote katika hali ya masumbufu, kama utaisoma biblia na huku unasikiliza miziki ya kidunia, au huku una chat, au huku unafanya mambo mengine, Ni heri uifunge uje usome baadaye usiku peke yako…. inahitaji utulivu wa fikra na mawazo..Na hapo ndipo inakupasa ufunge baadhi ya vitu unavyovifanya, au ulivyozoea kuvifanya..Na kwa jinsi unavyovifunga kwa muda mrefu zaidi ndivyo unavyoongezeka uwezekano wa Mungu kusema na wewe kwa haraka na kwa mara nyingi zaidi.

Kufunga ni kuna faida kwasababu yeye mwenyewe anasema wote wafanyao hivyo huwapa thawabu kama hawatafanya kinafki na kwa nia mbaya..(Mathayo 6:16)

Ni ahadi yake kukulipa, Funga tu kwa kumaanisha kumsogelea Mungu zaidi, utapata zaidi ya kile ulichomwomba. Kuna mtu aliuliza swali je! Maandiko yanasema tunapaswa tufunge kuanzia saa ngapi hadi saa ngapi na ni kwa siku ngapi?..Jibu ni kuwa Biblia haijatoa masharti yoyote juu ya muda wa kufunga au siku za kufunga..Imezoeleka siku 3, siku 21 na siku 40 kwasababu ndio siku ambazo zimeonekana zikifungwa na wengi..Lakini hiyo haimaanishi kuwa nawe ufunge muda huo, ni vile Roho atakavyokuongoza na kulingana na aina ya dua uipelekayo kwa Mungu, unaweza ukafunga, siku moja, au wiki, au mwezi, au mwaka, na Mungu akaridhia, vile vile unaweza ukafunga saa 6 kwa siku, saa 12, au siku tatu bila kula, au siku 40 bila kula , ni vile tu Mungu atakavyokupa neema..Lakini vyovyote vile kufunga ni muhimu kwa kila mkristo. Na kuna manufaa na thawabu nyingi.

Ubarikiwe sana. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki.


Mada Nyinginezo:

FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU

KAZI YA UZURURAJI WA SHETANI.

RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.

NINI MAANA YA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI?

KAINI ALIPATIA WAPI MKE?


Rudi Nyumbani:

Print this post

IPO NGUVU ITUVUTAYO KWA KRISTO, ITHAMINI!.

Kuna nguvu ya kipekee sana, inayoendelea duniani kote leo, hiyo inawavuta watu kwa Kristo, Nguvu hiyo ni nguvu ya Roho Mtakatifu, inazungumza mioyoni mwa watu, ikiwashawishi kuwavuta kwa Mungu. Nguvu hiyo ndio ile ile nguvu iliyokuwa inawavuta wale Wanyama kipindi cha Nuhu, waielekee Safina.

Kipindi kifupi kabla ya gharika kushuka juu ya nchi, ghafla tu Nuhu alianza kuona Wanyama wanasogea karibu na mahali Safina ilipokuwa inatenengenezwa, pengine kaamka asubuhi ghafla anaona simba wawili wakike na kiume wamelala pembezoni mwa kichaka Fulani kilichopo karibu na Safina ilipokuwepo, na wamekaa kama wanasubiri kuingia mahali Fulani hivi, halafu wamekuwa wapole jambo ambalo si la kawaida.

Mita kadhaa mbele pengine anaona tembo wamesimama kama vile wanahaja na kitu Fulani, nao hawana madhara…baada ya siku moja nyingine au mbili anaona chui, swala…na wote wakiwa na shauku ya kuingia ndani ya Hiyo nyumba yao mpya (safina). Kama vile kuku, au ng’ombe au mbuzi wanavyokuwaga na shauku ya kuingia mabandani mwao kila inapofika jioni..Giza linapoingia utaona kuku wamekusanyika mlangoni mwa banda lao wakingoja mlango ufunguliwe waingie…

Ndivyo ilivyokuwa kipindi kile cha gharika, shauku ya wale Wanyama kuingia ndani ya Safina, ilikuwa ni kubwa mpaka ikazima ukali wao, wote wakawa wapole wakitii na kusubiri amri ya kuingia ndani ya Safina.

Sasa ni nani aliowaongoza hao Wanyama mpaka wafike mlangoni mwa Safina?..je! walihubiriwa na watu kwamba kuna gharika inakuja hivyo wajiepushe?..Jibu ni hapana!…Kuna nguvu Fulani ndani yao iliyokuwa inawasukuma waende mahali ambapo ni salama Zaidi…Kuna mazingira Fulani yaliwafanya wahisi kuwa mwisho umefika na kuna mauti kubwa inakuja mbeleni(hukumu), na Zaidi ya hayo kuna kitu kiliwafanya pia wahisi kuwa kuna Maisha yataendelea baada ya hukumu hiyo, ili kuendelea kuishi hayo Maisha yanayokuja, daraja lake ni kutafuta hifadhi sasa.

Unajua hata watabiri wa vimbunga na matetemeko, wanatumia ishara ya Wanyama kutabiri maafa?..Endapo wakiona kuna tabia ya kipekee ya Wanyama imezuka mahali Fulani, labda ndege wote wameondoka mijini na kukimbilia milimani au mahali pa mbali, na wakati si jambo la kawaida, wanatangaza kuwa kuna janga litatokea siku si nyingi, hivyo watu wachukue tahadhari, na kweli baada ya kipindi Fulani kifupi labda wiki, mwezi au mwaka janga linatokea mahali hapo.

Kama Mungu, aliiachia hii nguvu ya wokovu hata kwa Wanyama (Warumi 8:19-22), si Zaidi wanadamu?…Hata sasa hii nguvu ipo, Wewe mwenyewe unajua ndani yako kuna nguvu Fulani inakushuhudia kwamba tunaishi siku za mwisho! Na kwamba siku moja mwisho wa mambo yote utafika, na ulimwengu utahukumiwa….Na hiyo nguvu haiishii hapo, inazidi kukushuhudia kwamba kutakuwa na maisha baada ya hukumu…Na pia haiishii hapo, inakusukuma kuifuata Safina mahali popote ilipo…Usiipuuzie hiyo sauti!!.

Nuhu wetu wa Sasa ni Yesu Kristo, Safina ni Neno lake, Wote aliopewa Nuhu walikwenda kwake kadhalika wote aliopewa Bwana Yesu na Baba walikwenda kwake na wanakwenda kwake sasa hivi..

Yohana 6:37 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.

38 Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka”.

Yohana 6: 43 “Basi Yesu akajibu, akawaambia, Msinung’unike ninyi kwa ninyi. Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho”.

Muda unakwenda kwa kasi sana! Je! Hii nguvu bado ipo ndani yako? Au umeizimisha? Je! Kama ipo Umeikaribia Safina kiasi gani?..Umemkaribia Nuhu kiasi gani?, Jibu unalo..Fanya maamuzi thabiti kabla hazijafika siku za hatari, ambazo wengi watatamani waingie safinani na watashindwa…

Luka 13:23 “Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,

24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.

Biblia inaposema kama zilivyouwa siku za Nuhu ndivyo itakavyokuwa siku za kuja kwake mwana wa Adamu, tunapaswa tujifunze pia tabia kama hizi, za kuvutwa safinani, vile vile tunapaswa tujue kuwa sio wanyama wote waliingia bali ni wachache..Vivyo hivyo leo hii wanaoitii hiyo sauti ni wachache,..Tujitahidi na sisi tuwe miongoni mwao, kwa kuitikia wito huo wa Mungu uitao mioyoni mwetu kila siku.

Tafadhali share na wengine

Bwana akubariki.


Mada Nyinginezo:

NUHU WA SASA.

FAHAMU KINACHOMGHARIMU MUNGU, KUTOA URITHI WAKE.

JE! MUNGU ATAIANGAMIZA DUNIA TENA BAADA YA GHARIKA YA NUHU?

MANENO HAYA YANA MAANA GANI? “..KWA SABABU HAMTOI ROHO KWA KIPIMO. (YOHANA3:34)

JE! MUNGU ANAUPENDELEO KWA WANAUME ZAIDI YA WANAWAKE?

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! UKIMWI UNATIBIKA?

Kwanza ni vizuri kufahamu kuwa hakuna jambo lolote linaloshindikana hapa duniani,  lakini habari mbaya ni kuwa yapo mambo mengi yanayotushinda sisi wanadamu, na hiyo ni kutokana na kuwa kwa namna moja au nyingine tumekosa kujua njia sahihi ya kutatua matatizo hayo au wakati mwingine kukosa maarifa ya kutosha juu ya tatizo husika, kwa mfano watu wawili wanaweza kuumwa Malaria lakini mmoja akawa na ufahamu kuwa huu ni ugonjwa wa malaria, hivyo akaenda hospitali akapewa dawa akanywa akapona, na mwingine kwa kuwa hajawahi kufahamu au kusikia juu ya ugonjwa huo akadhani amelogwa akaenda kwa mganga, akaambiwa leta unyayo wa jirani yako, lakini mwisho wa siku akajikuta anakufa katika hali ile  ile, hiyo ni kwasababu alikosa maarifa ya kujua chanzo cha tatizo na njia sahihi  ya kulitatua..

Vivyo hivyo na magonjwa mengine yote yasiyotibika, kama vile ukimwi, kansa, Kisukari n.k. sio kwamba hayana tiba, hapana tiba yanayo ukimwi unatibika isipokuwa tu tumekosa maarifa ya kutosha ya kujua mahali pa kuyatatua na njia sahihi,..Na hiyo imetufanya tuhangaike huku na huko na mwisho wa siku tunaangamia…Madaktari wetu wanafanya kazi njema ya Mungu, lakini upo wakati ambao uwezo wao kutibu unafika kikomo, hivyo inahitaji mtu mwingine ambaye mwenye uwezo mkubwa zaidi ya yeye kukusaidia hapo.

Habari  njema ni kuwa yupo anayeweza kuyaondoa yote pasipo gharama yoyote na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO. Zipo shuhuda nyingi, na bado zitaendelea kuwa nyingi za watu wanaoponywa magonjwa hayo kwa damu yake. Anachotaka kwako sio tu kukuponya mwili wako lakini pia kuiponya roho yako, kwasababu hiyo ndiyo ya muhimu zaidi.

Kwani kuna makundi mawili ya watu wanaopatwa na matatizo haya, kundi la kwanza ni wale waliopata kutokana na dhambi zao, kwamfano mtu amekuwa mzinzi na mwasherati matokeo yake akapata Ukimwi, sasa watu wengi wa namna hii wakati mwingine wanataka Mungu awaponye, lakini hawezi kuwaponya kama hawatakuwa tayari kutubu na kuacha dhambi zao, kundi la pili, ni wale wanaopatwa kwa njia za kawaida tu sio kwa dhambi, sasa hawa kama mtu atakuwa bado yupo nje ya Kristo ni vizuri akaokoka na kama yupo ndani ya Kristo asiwe na wasiwasi Bwana atamponya tu.

Jambo ni moja tu ni kumwamini Bwana YESU..Kwasababu ndiye pekee aliyekufa kwa ajili yetu, hakuna kiongozi yoyote, au mtume yeyote, au nabii yeyote ambaye aliyewahi kuyatoa maisha yake makamilifu kwa ajili ya shida za watu wengine, hakuna haijawahi kutokea katika historia na wala haitakaa itokee, Ni mmoja tu ambaye ni YESU KRISTO. Yeye ndiye aliyeyachukua magonjwa yetu yote na madhaifu yetu.

Mathayo 8:16 “Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,

17 ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.”

Isaya 53:4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Wewe Unajuaje kuwa ni huyo huyo YESU ndiye aliyekupitisha katika ukurasa huu?, Ameona shida zako na magonjwa yako unayopitia kuwa muda mrefu, Hivyo usiogope leo hii ugonjwa huo utaondoka, Jambo la kwanza unalopaswa kufanya kama hajatubu basi tubu leo hapo ulipo kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako na kumwishia yeye, kwasababu hapo ulipo anakuona, na anakutazama, anajua kila kitu kilichopo ndani ya moyo wako, hivyo tubu makosa yako yote kwa kumaanisha ikiwa upo nje ya Kristo, na yeye atakusamehe, kisha baada ya maombi ambayo nitaomba na wewe muda si mrefu, ukatafute mahali wanapobatiza ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO ili ukamilishe wokovu wako, na baada ya hapo Mungu mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu.

Sasa nataka ufanya jambo moja hapo ulipo weka mkono wako wa kuume mahali pale unapoumwa,..kama ni mwili mzima au ndani ya damu weka mkono wako katika kifua chako.. Kisha Sema kwa sauti maneno haya kwa IMANI.

BWANA YESU, NAJA KWAKO, NINAKIRI KUWA WEWE NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NA TENA WEWE NI MPONYAJI WANGU, WALA SINA MPONYAJI MWINGINE ILA WEWE, UMEWAPONYA WENGI NA SHUHUDA ZAO KILA SIKU NINAZISIKIA NA KUZIONA MBELE YA MACHO YA WATU, NAMI LEO HII NATAKA UNIPONYE NA MIMI EE YESU MPENZI, NIMEONA KUWA HAKUNA MWINGINE ANGEWEZA KUNIPENDA KAMA WEWE ULIVYONIPENDA, KWA KUJITOA NAFSI YAKO, MAISHA YAKO, NA UHAI WAKO ILI MIMI NIPATE UKOMBOZI WA BURE, NA LEO HII NINAKIRI KUWA SITAKUACHA, NITATEMBEA NA WEWE SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU. ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPONYA.

AMEN.

Ikiwa umefuatiliza sala hiyo, sasa hapo ulipo jiangalie mahali ulipokuwa unaumwa, au nenda hospitali kapime, na huo ugonjwa ulionao utakuta umeshaondoka. Hivyo usiache kututumia shuhuda zako kwa namba hizi:

+255789001312

+255654555788,

Au kwa barua pepe hii:

email: watakatifuwasikuzamwisho@gmail.com

Pia unaweza soma shuhuda mbalimbali hapo chini zitakazokusaidia kujenga imani yako kwa Bwana.


 

Mada Nyinginezo:

USHUHUDA WA UPONYAJI WA UKIMWI.

USHUHUDA WA UPONYAJI WA KANSA.

NAMNA GANI NITAPOKEA NGUVU ZA BWANA YESU?

YESU MPONYAJI.

JE! NI KWELI BWANA ALIMAANISHA HATUTAONJA MAUTI KABISA TUKIMWAMINI?(YOHANA 11:25)

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post