Title Devis

Wakamchukua vile vile alivyo katika chombo.

Marko 4:35-36

[35]Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo.

[36]Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.

Vifungu hivi vinazidi kutueleza tabia ya Bwana wetu Yesu Kristo na huduma yake jinsi ilivyokuwa ya kitofauti sana hapa dunia.

Kujitoa kwake kulikuwa ni kwa gharama sana tofauti na sisi tunavyoweza kufikiri, embu fikiria kisa kile cha pale kisimani alipokutana na yule mwanamke msamaria, na kuanza kumshuhudia habari zake mpaka kupelekea wimbi kubwa la watu Samaria kumfuata.

Kwa jicho la kawaida unaweza kudhani ilikuwa ni huduma ya kawaida lakini kiuhalisia haikuwa ni jambo lililomruhusu sana kimwili. Kwani maandiko yanatuambia alichoka sana kwasababu alikuwa katika safari ndefu kutoka uyahudi Kwenye Galilaya.

Tunasoma akiwa na njaa na kuchoka ‘alijibwaga’ hivyo hivyo pale kisimani, akawaruhusu wanafunzi wake kwenda mjini kutafuta chakula..

Lakini Mwanamke yule alipokuja kisimani hakusema ngoja nipumzike kwanza, nivute pumzi, kinyume chake alianza muda ule ule kusema naye..hata baadaye alipoletewa chakula ale hamu yake ya kula ilikatwa na ile kazi ya Mungu Aliyokuwa anaifanya.

Yohana 4:6-8,30-33

[6]Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.

[7]Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.

[8]Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula…..

[30]Basi wakatoka mjini, wakamwendea.

[31]Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule.

[32]Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi.

[33]Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?

Vivyo Hivyo tena wakati mwingine alikuwa anawahubiria Makutano mchana kutwa, mpaka ilipofika jioni ambapo alipaswa aende kupumzika kidogo, ili kesho aendelee na huduma. Maandiko yanatuambia akawaambia wanafunzi wake “Tuvuke Ng’ambo”.

Kibinadamu jambo kama hilo la safari Nyingine mpya lingetemea kwanza maandalizi fulani labda ya chakula, au mavazi, au kushughulikia mahitaji mengine…lakini kwakua kusudi la Mungu lilimsukuma kwa nguvu wakamchukua Vilevile alivyo katika chombo Mpaka ng’ambo..hakuna kuoga, wala kupumzika, wala kuwatembelea marafiki na ndugu, ni kuunganisha ziara nyingine, sio kwamba alikuwa hachoki hapana alichoka sana, kuthibitisha hilo utaona akiwa katikati Ya safari ile alipitiwa na usingizi kwa sababu ya uchovu (4:38)

Hii inatuonyesha wazi utayari wa Kristo ambao uliathiri mpaka hali zake za kimwili.

Ni kutufundisha nini?

Kwasababu yeye ni yule yule jana na leo na hata Milele, utayari ule ule aliokuwa nao zamani anao hata leo.

Kristo haitaji maandalizi wala hali ya kimazingira, katika kutumika Na sisi. Ni rahisi Kudhani mpaka Bwana atende miujiza tunahitaji kwanza maandalizi ya Maombi na mifungo na mikesha, au mpaka Bwana amwokoe mtu tunahitaji tuwe na elimu nyingi ya biblia, au uzoefu kumbe si lazima..

Ni kweli mambo hayo ni muhimu katika baadhi ya mazingira lakini si yote. Anataka tuwe wepesi wa kumchukua yeye vilevile kama alivyo katika mazingira yoyote?

Yupo tayari kwenda na sisi popote, maadamu tu sisi tunakuwa tayari kumchukua katika safari zetu kwa imani. Hatupaswi kujali tutatolea Wapi fedha za huduma kumuhubiri Kristo.

Ikiwa umeokoka, ni nini unasubiri Usimtumikie Mungu wako?. Unataka uwe kama Martha ambaye alijisumbua na maandalizi mengi wakati lililohitajika ni moja tu, kumsikiliza Kristo? Kumchukua vilevile kama alivyo.

Yesu alipowaacha mitume hakuwapa mitaji ya maspika, au vyuo vya kusoma au majengo ya kuabudia…aliwaambia enendeni nami nitakuwa pamoja nanyi mpaka ukamilifu wa dahari. Msibebe fimbo wala mkoba, wala pesa kibindoni, wala kanzu mbili.(Mathayo 10:5-10)

Kwa tafsiri nyingine anasema nichukueni hivi hivi nilivyo, msijali hali yangu, nanyi mtaona Maajabu mbeleni.

Bwana atujalie kujua matamanio yake, ili tusizuiliwe kuhudumu naye popote, kwenye mazingira yoyote.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Masomo mengine:

RABI, UNAKAA WAPI?

Yesu alipopanda kuomba kwanini atokewe na Musa na Eliya na sio manabii wengine?

SAUTI NYUMA YA ISHARA.

Print this post

Nini maana ya “mtu atachukua dhambi zake” (Walawi 5:17).

Swali: Neno la MUNGU linamaanisha nini linaposema “mtu atachukua dhambi yake au uovu wake”?

Jibu: Turejee andiko hilo..

Walawi 5:17 “Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia vivyo, NAYE ATACHUKUA UOVU WAKE”

Tusome tena..

Walawi 24:5 “Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu awaye yote atakayemlaani Mungu wake ATACHUKUA DHAMBI YAKE”.

Utalisoma tena neno kama hilo katika Walawi 7:18, Hesabu 9:13, Ezekieli 44:10-12..

Katika  Agano la kale Bwana MUNGU aliruhusu mtu kulipizwa kisasi endapo amefanya jambo la kusudi lililo baya.. kwamba UHAI kwa UHAI.. jino kwa jino..jicho kwa jicho..

Maana yake kama mtu amemkata mwenzake mkono naye pia ni lazima akatwe mkono, kama mtu amemwua mwenzake sharti naye pia auawe..

Walawi 24:17 “Na mtu ampigaye mtu hata akafa, lazima atauawa;

18 na atakayempiga mnyama hata akafa atalipa; uhai kwa uhai.

19 Na mtu akimtia mwenziwe kilema; vile vile kama alivyofanya, naye atafanyiwa vivyo;

20 jeraha kwa jeraha, jicho kwa jicho, jino kwa jino; vile vile kama alivyomtia mtu kilema, naye atalipwa vivyo”.

Lakini yapo matukio ambayo yalikuwa yakifanyika yanakuwa HAYANA KISASI!, kwamfano mtu aliyesikika kamtukana MUNGU au kulilaani jina la MUNGU, mtu huyo sheria ilikuwa ni kuuawa kwa kupigwa mawe, sasa wale watu waliomwua kwa kumpiga mawe baada ya kuthibitika uasi wa Yule mtu, hao hawawezi kulipwa kisasi kwamba nao wauawe kwasababu sheria imesema uhai kwa uhai.

La! Bali wataachwa hai,.. sasa hiko kitendo cha hawa wauaji kuachwa Hai na kutokulipwa kisasi ndio tafsiri yake kwamba “Yule aliyekufa kauchukua uovu/dhambi yake mwenyewe”.. maana yake hajaacha dhambi kwa waliomwua!.

Lakini laiti kama atauawa pasipo hatia na ikathibitika hivyo, basi wauaji wale watabeba dhambi ya mauaji hivyo nao pia watauawa, kama sheria isemavyo kwamba uhai kwa uhai na jino kwa jino. Sasa kitendo hiko cha kuuawa kwa kosa la mauaji yasiyo na hatia, ndicho kinachoitwa kubeba dhambi ya aliyekufa.

(kumbuka si kwamba watabeba makosa ya Yule mtu, la!, Yule mtu atabaki na dhambi zake alizozifanya.. bali hawa wauaji watabeba lile kosa moja tu la mauaji ya mtu asiye na hatia), hivyo watahukumiwa tu kama wauaji waliomwua mtu asiye na hatia.

Na lugha nyingine ya kubeba dhambi ya mtu ni kubeba damu ya mtu. Hivyo mahali popote katika biblia Bwana MUNGU anaposema kuwa “nitaitaka damu mikononi mwa mtu” maana yake ni hiyohiyo kwamba “kwamba atamhukumu muuaji kwa kosa la kumwua asiye na hatia”.. na anaposema damu yake itakuwa juu yake mwenyewe aliyefanya kosa, maana yake ni kwamba aliyeuawa hatalipiwa kisasi kwa waliomwua.

Zifuatazo ni baadhi ya dhambi ambazo mtu akizitenda basi alibeba dhambi zake mwenyewe, wala waliomwua hawakuwa na hatia ya kulipwa kisasi wala kushtakiwa.

  1. Kulikufuru jina la MUNGU (Soma Walawi 24:5).
  2. Ibada za sanamu/miungu (soma Kumbukumbu 13:6-12).
  3. Kutoishika pasaka (Hesabu 9:13).
  4. Kufumaniwa katika uzinzi.
  5. Kulala na mnyama wa aina yoyote au ndugu yoyote wa karibu.(Kutoka 22:19)
  6. Kumlaani mzazi (Kutoka 20:9)

Je hata sasa (Agano jipya) sheria hizi zipo?.

Katika Agano jipya hatuna sheria yoyote ya kisasi, Bwana YESU alitufundisha hilo katika Mathayo 5:38-41, ikiwa na maana kuwa hatujapewa ruhusa ya kumwua mtu au kulipiza kisasi bali kisasi ni juu ya Bwana (soma Warumi 12:19).

Kwahiyo kama hatujapewa ruhusa ya kulipa kisasi, au kutoa hukumu ya aina yoyote  kama katika kipindi cha agano la kwanza, basi maana yake ni kwamba mtu yoyote Yule alipaye kisasi atakuwa na hatia pasipo kujalisha makosa aliyoyafanya ndugu yake!..

Muuaji wa aina yoyote ile, atabeba kosa la mauaji, (Bwana ataitaka damu ya aliyemwua mikononi mwake).. hata kama amemwua mtu aliyemlaani MUNGU, bado ni kosa!..katika agano la kale haikuwa makosa lakini agano jipya ni kosa!.

Kwahiyo hatujapewa ruhusa ya kuua kwa kosa lolote lile, tukifanya hivyo tutakuwa na hatia na Bwana ataitaka damu ya aliyekufa mikononi mwetu.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Orodha ya majina ya Miji ya Biblia (Agano la kale) na Sasa

Agano la Chumvi ni nini? (2Nyakati 13:5)

VUNJA AGANO LA MAUTI.

Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?

Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote

Print this post

Ipi tofauti kati ya Uhai na Uzima kibiblia?

Jibu: Turejee maandiko machache..

“Uhai” ni hali ya kuwa “HAI” (yaani kuishi) ili kiumbe kiwe kinaishi ni lazima kipumue, kile, kikue na hata kijongee. Hizo ndizo tabia chache za viumbe HAI,  Wanadamu, wanyama na mimea vyote vina uhai kwasababu vinapumua, vinaongezeka na pia kujongea.

Lakini “UZIMA” Umeenda mbali zaidi kuelezea UHAI wa kiroho ambao unapatikana kwa mtu kuwa na mahusiano na MUNGU.

Uhai unaelezea mwili lakini Uzima unaelezea roho. Mimea haina UZIMA bali ina UHAI.. wanyama hawana UZIMA bali wana UHAI maandiko yanaonyesha hivyo…

Mithali 12:10 “Mwenye haki huufikiri UHAI WA MNYAMA WAKE; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili”.

Na UZIMA unapatikana kwa mmoja tu ambaye ni YESU KRISTO,

Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili WAWE NA UZIMA, kisha wawe nao tele”.

ikiwa na maana kuwa wanadamu yoyote aliye nje ya YESU KRISTO anao “Uhai” tu kama wanyama lakini hawana “Uzima”… anapumua, anakula, anatembea lakini akisha kufa hana UZIMA tena.. Lakini aliye ndani ya KRISTO, hata akiwa amekufa ataendelea kwasababu anao  UZIMA wa MILELE alioupokea kutoka kwa YESU.

Je unao uzima wa milele ndani yako?…Je YESU ni sehemu ya maisha yako?

Yohana 17:2 “kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape UZIMA WA MILELE.

3 Na UZIMA WA MILELE ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na YESU KRISTO ULIYEMTUMA”.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! UPO KATIKA MAJI YA UTULIVU?

Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?

SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU.

Kwanini pawekwe MITI pale bustanini na si kitu kingine?.

Uzao wa Ibrahimu unamilikije mlango wa adui? (Mwanzo 22:17)

Print this post

Utakuwa Kichwa na si Mkia maana yake nini? (Kumbukumbu 28:13).

Jibu: Turejee..

Kumbukumbu 28:13 “Bwana atakufanya kuwa KICHWA, WALA SI MKIA; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;

14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia”.

Unaweza kutafakari kwanini hajasema Utakuwa KICHWA na wala si MGUU!.. kwasababu kichwa kipo juu na miguu ipo chini, na ndio sehemu ya mwisho ya mwili wa mtu… lakini badala yake anasema Utakuwa “kichwa”na si ”mkia”. Je kuna sifa gani mbaya katika mkia?

Sasa sote tunajua kuwa mwanadamu hajaumbwa na Mkia, bali kichwa tu peke yake, hivyo bila shaka hapo biblia imejaribu kutumia umbile la wanyama badala ya la mtu kufunua hali  ya mtu atakayemcha MUNGU na yule ambaye hatataka kumcha MUNGU, kwasababu wanyama ndio wenye kichwa na mkia na si mwanadamu.

Sasa kichwa cha mnyama yoyote ndicho kinachoongoza mwili wote, na ndio sehemu ya kwanza ya mwili wa mnyama. Lakini Mkia ni sehemu ya mwisho kabisa ya mwili wa mnyama, na sehemu hii imeungana na sehemu ya haja  kubwa ya mnyama. Kwahiyo wakati kichwa kinapokea chakula fresh, mkia unapokea uchafu (kinyesi).

Ikiwa na maana kuwa watu wanaomcha MUNGU, watapokea vilivyo  visafi na vya kwanza na vizuri, na wasiomcha MUNGU ni kinyume chake, watapokea vile vya mwisho na visivyo na heshima vilivyo haribika.

Pia watu wanaomcha MUNGU watakuwa wa kwanza, kulingana na sifa ya kichwa, lakini wasiomcha MUNGU watakuwa wa mwisho kama ilivyo nafasi ya mkia katika mwili wa mnyama, sasa hebu tafakari unakuwa wa mwisho na bado unapokea vilivyo vichafu (mfano wa vinyesi)..ni jambo baya sana..

Ni tahadhari kwetu tunaoishi, kwamba tuwekeze nguvu kubwa katika kumtafuta MUNGU ikiwa tutataka tuwe vichwa, lakini tusipotaka kufanya hivyo, maandiko yanasema tutakuwa mkia na maadui zetu MUNGU atawaweka juu yetu na sisi tutakuwa wa mwisho.

Kumbukumbu 28:43 “Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.

44 Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; YEYE ATAKUWA NI KICHWA, WEWE UTAKUWA MKIA.

45 Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza”

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

LAANA NI NINI KIBIBLIA?

MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

NI SAHIHI KABISA, HUU SI WAKATI WA TINI!

Maana ya Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao

Print this post

Je! Tutatambuana tukifika mbinguni?

Ndio Maandiko yanatuonyesha kuwa tutatambuana tukifika mbinguni. Ifahamike kuwa fahamu zetu au kumbukumbu zetu za hapa ulimwenguni hazitaondolewa kabisa, tufikapo mbinguni, kila pito tulipitialo, na kila jambo lililowekwa na Mungu sasa hapa duniani, lina sehemu kubwa ya fundisho la maisha yajayo. Hivyo maisha ya duniani yana thamani kama yalivyo tu maisha yatakayokuja. Ndio maana kabla ya kuingia kule ilitupaswa kwanza tupitie hapa.

Zipo sehemu kadha wa kadha katika maandiko zinatuthibitishia kuwa  tutatambuana kule mbinguni.

1). Kufufuka kwa Yesu.

Tunaona Bwana wetu Yesu Kristo alipofufuka na mwili mpya wa utukufu, aliweza kutambuliwa . Kwamfano siku ile ya kwanza ya juma Mariamu Magdalena, akiwa pale kaburini alimtambua Bwana Yesu alipozungumza naye.

Yohana 20: 16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu).

2) Mlima wa Mageuzi

Halikadhalika wakati ule Bwana Yesu anawachukua mitume wake watatu Petro, Yohana na Yakobo na kuwapeleka juu ya mlima ule mrefu, na kuwabadilikia sura, kama tunavyosoma watu wawili walitokea ambao ni Musa na Eliya.

Mitume waliweza kuwatambua ijapokuwa hawakuwahi  kuwaona uso kwa uso hapo kabla.

Mathayo 17:3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.

3) Fundisho la Paulo juu ya ufufuo

1Wakorintho 15:42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko

Mstari huo unatuonyesha  kuwa hatutaondolewa uhalisia wetu Tutabakia kuwa sisi sisi., isipokuwa tutavikwa utukufu wa juu zaidi. Maana yake ni kuwa tutatambuana.

4) Ahadi ya kukutanishwa tena

1Wathesalonike 4:16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana

hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

Tutarejeshwa, na kuonana. Hivyo kwa mujibu wa vifungu hivyo katika ulimwengu ujao sote tutajuana na kufahamiana.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

Ipi tofauti kati ya Sheria na kanuni kibiblia.

Sheria ni agizo la shuruti linalotolewa na mamlaka kuu…, na KANUNI ni mwongozo au utaratibu maalumu unaotolewa kuhusiana na utekelezaji wa sheria iliyowekwa au agizo lililotolewa..

Kwamfano katika biblia kulikuwa na Sheria ya “kuishika  Pasaka” lakini ilikuwepo pia kanuni (ambayo ni mwongozo wa namna ya kuiadhimisha hiyo siku), kwamba ni lazima kwanza iwe siku  ya 14 ya mwezi wa kwanza wa kalenda ya kiyahudi, na pia siku hiyo ni lazima achinjwe mwana kondoo na kumwoka motoni na aliwe pamoja na mboga zenye uchungu n.k (Soma Kutoka 12:1-12).

Sasa huo mwongozo wote wa jinsi ya kuiadhimisha hiyo siku ndio unaoitwa Kanuni, lakini sheria ni hiyo moja tu kwamba Waishike Pasaka..

Hesabu 9:14 “Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa Bwana; kama HIYO SHERIA YA PASAKA ILIVYO, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; MTAKUWA NA SHERIA MOJA, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi”.

Katika biblia kila Amri au sheria ilikuwa na Kanuni zake na hukumu zake.

Tunayo sheria na amri ya Kristo pia ambayo ni UPENDO, lakini huu upendo unao kanunini…ni lazima tuzitafutae kanuni za upendo  na tuzijue.

Isaya 28:13 “Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo”.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka?

PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA?

Nini tofauti kati ya kileo na divai?

FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.

Je! kuna mwanamke mwingine aliyempaka Bwana marhamu (manukato) zaidi ya Mariamu ndugu yake Lazaro?

 

Print this post

Ipi tofauti ya utakatifu na utukufu?

Jibu: Neno Utakatifu linatokana na Neno “utakaso”.. kitu lilichotakasika kinaitwa “kitakatifu”.. na kitu kilichotakasika/takata maana yake hakina uchafu.

Kwahiyo utakatifu kwa tafsiri rahisi maana yake ni “kuwa safi, (kutokuwa na uchafu)”..  Mtu anaweza kuwa msafi (mtakatifu) mwilini na rohoni.

Sasa kikawaida kitu chochote kinapokuwa safi, huwa kinatoa Mng’ao unaopendeza.. sasa ule mng’ao unaotafsiri usafi wa kitu kile ndio unaoitwa UTUKUFU, kwamfano dhahabu inaposafishwa na kuwa safi huwa inatoa mng’ao mzuri wa kipekee, sasa ule mng’ao ndio utukufu wa ile dhahabu au kito, na vitu vingine vyote ni hivyo hivyo.

Hali kadhalika mtu aliyetakaswa dhambi zake kwa damu ya YESU, na yeye mwenyewe kujilinda  na kujitenga na uchafu wote wa rohoni na mwilini,  basi mtu huyo ni mtakatifu na anao utukufu, ambao  ni NURU inayong’aa,  ambayo shetani na mapepo yake hayawezi kustahimili mwako wake.

Lakini zaidi sana MUNGU wetu aliyetuumba ndiye mwenye utukufu MKUU,  ambao huo unatokana UTAKATIFU alionao, uzidio viumbe vyake vyote.. Mng’ao wa utukufu wake hata malaika wanainama mbele zake na kujifunika kwa mbawa zao, na utukufu wake unang’aa mpaka duniani.

Isaya 6:1 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.

2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.

3 WAKAITANA, KILA MMOJA NA MWENZAKE, WAKISEMA, MTAKATIFU, MTAKATIFU, MTAKATIFU, NI BWANA WA MAJESHI; DUNIA YOTE IMEJAA UTUKUFU WAKE”.

Naam nasi tuliompokea YESU ni lazima tufanane naye, na hatuwezi kuwa na utukufu bila kuwa watakatifu, na hatuwezi kukosa utukufu tukiwa watakatifu, na kuwa mtakatifu duniani inawezekana..

Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA? 

NYUMBANI MWA BABA YANGU MNA MAKAO MENGI.

YESU NI ALFA NA OMEGA .

JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU

Print this post

Ipi tofauti kati ya Ahadi na Nadhiri?

Swali: Kuna tofauti gani kati ya Ahadi na Nadhiri, kwa mujibu wa Biblia?


Jibu: Ahadi ni Neno/tamko la hiari mtu analolitoa kwa mtu mwenzake, kwamba atalitenda katika wakati mfupi au mrefu ujao.

Kwamfano mtu anaweza kuahidi kuwa kesho atawasili katika hafla, na hiyo kesho kweli akafika kama alivyoahidi, hapo anakuwa ameitimiza ahadi yake, lakini asipowasili kama alivyoahidia anakuwa hajaitimiza ahadi, na ni dhambi ikiwa hakuwa na sababu za msingi za kuivunja ahadi yake.

Lakini katika upande wa Nadhiri, hii ni ahadi (yaani tamko ya hiari) mtu analolitoa kwa MUNGU, na si kwa mtu.

Kwamfano mtu anaweza kuahidi kuwa endapo akipona ugonjwa unaomsumbua atamtolea MUNGU sadaka ya shukrani, au endapo Mungu akimtendea jambo Fulani basi atamtolea MUNGU sadaka Fulani, hiyo inakuwa ni nadhiri.

Na mtu asipotimiza Nadhiri aliyomwekea MUNGU inakuwa ni dhambi..

Mhubiri 5:4 “Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; KWA KUWA YEYE HAWI RADHI NA WAPUMBAVU; BASI, UIONDOE HIYO ULIYOIWEKA NADHIRI.

5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe.

6 Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?”

Kwahiyo ni muhimu kuitimiza ahadi tunazozitoa na pia Nadhiri uliomwekea MUNGU.

Ikiwa kuna sababu zozote za msingi zilizojitokeza za kutotimiza ahadi basi ni vizuri kufanya mapatano na uliyemhadi mapema ili isigeuke kuwa uongo.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! USIPOTIMIZA NADHIRI ZAKO ZOTE KWA BWANA. HAWEZI KUKUSAMEHE?

Ipi tofauti kati ya sadaka ya dhambi na sadaka za hatia?

LISIMAMISHE JIWE.

AINA TATU ZA UTAKATIFU

FUVU LA KICHWA.

Print this post

Ipi tofauti ya Hasira na Ghadhabu ya MUNGU?.

Swali: Kuna utofauti gani uliopo kati ya Hasira ya MUNGU na Ghadhabu ya MUNGU?

Jibu:  Kujua tofauti yake turejee mistari michache katika biblia..

Zaburi 6:1 “Bwana, usinikemee kwa HASIRA YAKO, Wala usinirudi kwa GHADHABU YAKO”.

 “Hasira” ni hisia ya “kuchukizwa” inayompata mtu kutokana na tendo Fulani baya alilofanyiwa, au lililomtokea kinyume na matakwa yake.  Hii ni hisia ya ndani ambayo inaweza kumfanya mtu apoteze hamasa, au hamu au shauku ya jambo Fulani.

Lakini “Ghadhabu” yenyewe inaenda mbali zaidi haiishii kumfanya mtu ajisikie tu vibaya na kujitenga bali inampeleka kuadhibu, au kulipiza kisasi.

Kwamfano kuna mtu aliyepigwa na mwenzie, akaishia kukasirika na kujitenga na Yule mtu, (Huyu anahesabika kuwa anazo hasira, kakasirika).. Lakini kuna mwingine anaweza kupigwa na mwenzake asiishie tu kukasirika lakini akarudisha mapigo, sasa huyu maana yake kaghadhibika, hivyo hasira yake imerudisha majibu hasi kwa aliyemtendea.

Sisi wanadamu tuna hasira lakini pia tunazo ghadhabu.. Ila Biblia imetuonya tusiizalie matunda hasira hata kuwa ghadhabu.. kwasababu hasira iliyozidi hata kutenda dhambi ndio ghadhabu..

Waefeso 4:26 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;

27 wala msimpe Ibilisi nafasi”.

Kwanini Biblia imezuia tusiwe watu wa kuwa na hasira ya kupitiliza?… Ni kwasababu hisia zetu zina mapungufu na hukumu zetu si kamili..

Lakini hukumu za MUNGU ni kamili kwani MUNGU anayo hasira na pia Ghadhabu.. Lakini mpaka ghadhabu ya MUNGU imemwaga basi ni hakika kuwa tumestahili, lakini sisi wanadamu hatujapewa ruhusa ya kuwa na ghadhabu, kwasababu hukumu utakayompimia mwenzako MUNGU akikuangalia nawe pia unastahili hiyo hiyo kwa makosa yako mengine (Mathayo 7:1), Lakini yeye MUNGU akihuhukumu hana wa kumhukumu kwakuwa ni mkamilifu, hivyo hukumu zake ni kamili!.

Na pia ni kwa maarifa ya ziada ya kujua ni hasira ya namna gani ambayo tumepewa ruhusa ya kuwa nayo, fungua hapa>>MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.

Sasa Maandiko yanasema MUNGU aliyetuumba si Mwepesi wa hasira (maana yake hakasiriki haraka) lakini ni Mwingi wa hasira (maana yake hasira yake inafikia kiwango cha ghadhabu), cha kuadhibiwa na kujilipiza kisasi,.

Nahumu 1:2 “Bwana ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; Bwana hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA HUJILIPIZA KISASI JUU YA ADUI ZAKE, huwawekea adui zake akiba ya hasira.

3 BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake”.

Kilichowapata watu wa nyakati za Nuhu ni Ghadhabu ya MUNGU, kilichowapata watu wa nyakati za Sodoma na Ghomora  ni Ghadhabu ya MUNGU!, Ndio maana hawakupona, na kitakachotokea kwa dunia ya wakati wa Mwisho ni Gadhabu ya MUNGU, soma  (2Petro 3:6-7 na Ufunuo 16:1).

Na MUNGU anaweza kuimimina Ghadhabu yake kwa Mtu mmoja, na kwa watu wengi kwa pamoja au kwa dunia nzima.. Mtu anayefanya dhambi kwa makusudi yupo katika hatari ya kukumbana na ghadhabu ya MUNGU yeye kama yeye…

Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;

6 KWA AJILI YA MAMBO HAYO HUJA GHADHABU YA MUNGU”.

Hivyo Biblia  (Neno la MUNGU) linatufundisha kuiogopa Ghadhabu ya MUNGU kwa kutembea katika mapenzi yake na pia kujizuia sisi na ghadhabu kwasababu hasira ya mwanadamu haiitendei haki ya MUNGU.

Yakobo 1:19 “Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; WALA KUKASIRIKA;

20 KWA MAANA HASIRA YA MWANADAMU HAIITENDI HAKI YA MUNGU.

21 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu”.

Mithali 15:1 “Jawabu la upole hugeuza HASIRA; Bali neno liumizalo huchochea GHADHABU”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.

IEPUKE GHADHABU YA MUNGU.

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA.

NIMEAZIMIA KUWAKUSANYA MATAIFA. NIPATE KUWAMWAGIA GHADHABU YANGU

Biblia inamaana gani kusema ‘maana Mungu wetu ni moto ulao’ (Waebrania 12:29)

Print this post

Ipi tofauti kati ya sadaka ya dhambi na sadaka za hatia?

Katika agano la kale dhambi ilitokea na kuhesabiwa katika maeneo mbalimbali.

 Kwamfano 

> Kulikuwa na makosa ya jamii nzima. Yaani taifa zima kuasi. (Kutoka 32,)

> Makosa ya mtu binafsi. Mfano kutenda uzinzi, Wizi, uuaji n.k.

 > Makosa ya kuwatendea vibaya wanyonge: Mfano maskini, wageni, mayatima na wajane (Amosi 5:11-12),

>  Makosa ya kukaidi sherehe za kidini (Walawi 11-15), 

> Makosa ya kuvunja maagano (Yeremia 17:21-23), 

> Makosa ya kuabudu miungu mingine (sanamu). 

Lakini pia kulikuwa na aina nyingine mbili za makosa..

> Aina ya kwanza ni makosa ya kukusudia

> Aina pili ni yale ya kutokusudia.

 

Ikiwa mtu alitenda dhambi kwa kutojua, alihesabika kuwa ni dhambi, hivyo alilazimika atoe sadaka ya dhambi. Lakini kama alitenda dhambi ya makusudi kinyume na mwenzake, ili kuondoa kosa Ilipasa atoe sadaka ya hatia.

Aina ya sadaka hizi zinaelezwa kwa urefu kwenye kitabu cha Walawi 4:1 – 5:13

Dhambi za kutokusudia Mfano wake ilikuwa ni kama kuvunja amri bila kujua au kutojua Sheria ya vitu safi au najisi ilivyo. Hivyo mtu alijikuta tu anatenda kwa kukosa ufahamu.

Walawi 4:1-3

[1]BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 

[2]Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo; 

[3]kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng’ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.

Dhambi za kukusudia ni zote ambazo zilitendwa kinyume na mtu mwingine au mambo matukufu mfano wa hizi ni kama kuiba, kusema uongo, viapo Vya uongo, hivyo iliambatana pia na kutoa fidia ya vitu hivyo.

Sio tu kusamehewa bali pia kuweka mambo sawasawa kwa kulipia fidia.

Mfano wa tendo hili, tunaona kwa Zakayo, alipofikiwa na wokovu, alitubu kwa kurejesha mara nne ya vyote alivyodhulumu. (Luka 19:8) huo ni mfano wa sadaka ya hatia.

Katika agano jipya dhambi Zote Za kukusudia na kutokusudia na nyingine zote zinaondolewa  na sadaka moja  tu ya daima nayo ni DAMU YA YESU (Waebr 9:26, Isaya 53:10, 1Petro 2:24). Hiyo tu ndio inafuta hatia zote.

Lakini pamoja na hayo, sadaka hizi hutukumbusha pia kila tuombapo rehema, (kwa unajisi tunaojitia kila siku), hatuna budi kuomba sio tu kwa dhambi tuzijuazo bali pia kwa zile tusizozijua.

Kwasasa dhambi tusizokusudia ni kama vile kumkwaza  mwenzako bila kufahamu, Kutowaombea wengine(2Samweli 12:23), kuwaza vibaya, kutotumiza nadhiri zetu, au wajibu wetu N.k.

 

Bwana akubariki.

 

Je umesamehewa na kuondolewa dhambi zako? Kama ni la! basi wakati ndio sasa, unapomgeukia Bwana Yesu, anakuondolea kumbukumbu lote la makosa. Hivyo fungua hapa kwa msaada huo wa kumpokea yeye >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).

Nini maana ya dhabihu na matoleo hukutaka? (Waebrania 10:5).

Kwanini Mungu aliikubali sadaka ya Yeftha ya kumtoa binti yake kafara?

Print this post