Mto Yordani uko nchi gani kwa sasa duniani?
Mto Yordani upo katika eneo la Mashariki ya kati, ni mto ambao unasimama kama mpaka wa mataifa mbalimbali, Ikiwemo Lebanoni, Syria, Israeli, na Yordani.
Ni kama vile ziwa Tanganyika lilivyo simama kama mpaka wa nchi 4, Congo, Burundi, Tanzania, na Zambia ndivyo ilivyo hata na kwa mto Yordani,
Nchi ya Yordani, unayoisikia leo hii pale mashariki ya kati, imechukua jina lake kutoka katika mto huu.
Mto huu chanzo chake ni kwenye chemchemi kadhaa zinazotiririka kutoka katika mlima Hermoni ulio mpakani mwa Lebanoni na Syria.Kisha kutoka hapo unateremsha maji yake mpaka Israeli kwenye bahari ya Galilaya/Tiberia/Genesareti. Na kutoka hapo unaibukia upande wa pili na kuendelea na safari yake moja kwa moja mpaka bahari ya Chumvi.
Tazama picha chini.
Mto huu, umekuwa kitovu katika historia ya Israeli kuanzia agano la kale mpaka agano jipya. Yoshua aliusimamisha mto huu na wana wa Israeli wakavuka kuelekea Yeriko.
Vilevile mto huu huu katika agano jipya ndio makutano mengi yalikuwa yanavuka kumwendea Yesu ili waponywe.(Mathayo 19:1-2), Na ni mto ambao Yesu mwenyewe alibatiziwa.
Kuonyesha kuwa ili nawe upate wokovu na ushindi dhidi ya maadui zako,na ili uponywe nafsi yako, ni lazima Uvuke Yordani yako ya Rohoni..Ili ukakutane na Yesu ng’ambo ya pili huna budi kuvuka Yordani, Na Unavukaje Yordani? Ni kwa kubatizwa, kama Yesu alivyobatizwa kwenye mto ule.
Hivyo na wewe sharti ukishamwamini Yesu moja kwa moja ukabatizwe, mahali popote penye maji tele kama ishara ya kuwa umeokoka kweli kweli. Na kuwa unakwenda kuwashinda maadui zako.
Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Wengi wanapuuzia maagizo haya ya msingi, wanadhani kuamini tu inatosha, Ndugu kubatizwa ni tendo lenye maana kubwa sana kwako rohoni, aliyetupa maagizo hayo hakuwa amekosa cha kutuagiza bali alijua umuhimu wake.
Swali Nji wewe umebatizwa ipasavyo? Kama sivyo basi kafanye hivyo.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda masomo yetu yawe yanakufikia njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Israeli ipo bara gani?
Wafilisti ni watu gani.
MJUMBE WA AGANO.
Zile mbao mbili za mawe Musa alizoambiwa achonge zilikuwaje?
Mlima sinai upo nchi gani? Na Je unaijua Sinai yako ya rohoni?
CHUKIZO LA UHARIBIFU
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
UNYAKUO.
Rudi Nyumbani:
Print this post
SWALI: Neno “Korbani” linalozungumziwa katika Marko 7:11 lina maana gani?
JIBU: Ili tupate picha nzuri ya Neno hilo embu tusome sehemu zote mbili zinazozungumzia jambo hilo hilo moja.
Mathayo 15 :1-6
1 “Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema, 2 Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula. 3 Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? 4 Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. 5 Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu, 6 basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu”.
1 “Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema,
2 Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.
3 Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
4 Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.
5 Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,
6 basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu”.
Marko 7:8-13
“8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. 9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. 10 Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. 11 Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, NI KORBANI, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; 12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; 13 huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.
“8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.
9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.
10 Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe.
11 Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, NI KORBANI, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi;
12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye;
13 huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.
Kama tunavyosoma hapo, biblia imeshatoa tafsiri ya hilo Neno Korbani mbele kidogo kuwa linaamanisha WAKFU.
Kitu chochote kilichowekwa wakfu ina maana kuwa hakitumiwi kwa mtumizi mengine yoyote isipokuwa kwa Mungu tu. Sasa katika habari hiyo, utaona Bwana Yesu alikuwa anawelenga sana sana Mafarisayo na waandishi kwa unafki wao kwa kujifanya kuwa wanaishika torati yote, wakati yapo mambo mengine mengi ya torati walikuwa wanayakaidi.
Na ndio hapo Bwana Yesu akawatolea mfano mmojawapo, ambao ulihusu kuwaheshimu wazazi, kama mojawapo ya amri ambazo Mungu alizitoa zishikwe na watu wote. Na biblia iliposema kuwaheshimu wazazi, ilikuwa sio tu kuwaonyeshea heshima na utiifu, hapana ilikuwa ni zaidi ya hapo ikiwemo kuwahudumia kifedha, hususani wakiwa wazee.
Sasa hawa waandishi walikuwa wanayapindisha hayo maagizo, kwa kuwashurutisha watu, kuepuka majukumu yao ya kuwahudumia wazazi wao, kinyume chake walikuwa wanawaambia hayo wanayoyapata kwa ajili ya wazazi wanaweza tu kuyafanya kuwa wakfu(Korbani) mbele za Mungu, na ikawa ni sawa tu na kama wamewahudumia wazazi wao, isiwe dhambi mbele za Mungu.
Hivyo kama mtu alikuwa ametenga fedha yake kiasi kwa ajili ya matumizi ya baba yake au mama yake kule kijijini, basi walihimiziwa walizete Hekaluni kwa ajili ya Mungu kama wakfu..
Na mzazi akimuuliza, mbona huniletei matumizi, basi Yule kijana atasema, fedha hii au nafaka hii niliyoivuna ni wakfu kwa Mungu.
Hivyo watu wengi wakawa wanawaacha wazazi wao katika hali ya shida na umaskini wa hali ya juu. Jambo ambalo Mungu hakuliagiza.
Ndipo Yesu anawakemea hawa waandishi kwa kuyapindua maagizo ya Mungu, ya kutotimiza majukumu yao ya kuwahudumia wazazi kwa kanuni zao walizojitungia.
Nini tunajifunza?
Kumbuka biblia haifundishi watu wakimbie majukumu yao ya kifamilia kwa wazazi wao hususani pale wanapokuwa wazee kwa kisingizio kuwa wanamtolea Mungu.. Biblia inasema usipowahudumia watu wa nyumbani kwako, wewe ni kuliko hata mtu asiyeamini(1Timotheo 5:8).. Lakini pia biblia haifundishi kuwa watu waache kumtolea Mungu kwa kisingizio kuwa wanayo majukumu mengi ya kifamilia.
Lazima ujue kila utoaji una sehemu yake, na Baraka zake. Watu wa nyumbani kwako wana sehemu yao, maskini wana sehemu yao, na Mungu pia anayosehemu yake..Usipojua hilo utakuwa nawe pia unatangua torati kwa kufuata mawazo yako mwenyewe uliyojitungia. Kwasababu wapo watu wengi leo hii, wameacha kupeleka fedha zao kanisani, au kwenye huduma za Mungu, wanasema sitoi sadaka yangu, na ukiwauliza ni kwanini?, wanasema mbona hatuoni zikienda kuwahudumia maskini na wajane kama ilivyokuwa katika kanisa la kwanza la mitume…Lakini mtu huyo huyo hajui kuwa watakatifu wa kanisa la kwanza sio kama hawa wa sasahivi, wale walikuwa wapo tayari kuuza mashamba yao na viwanja vyao na kuleta kwa Mungu, hivyo kwa namna ya kawaida nishati ya kutosha ni lazima iwepo nyumbani kwa Mungu hata kuwahudumia mpaka wajane.
Lakini kama wewe unampelekea Mungu shilingi, wakati hiyo fedha hata gharama za umeme kanisani hazijitoshelezi, unapata wapi ujasiri wa kutaka kujua mfuko wa kanisa unatumikaje?? Fikiria tu. Je wewe unaweza kuuza shamba lako kule kijijini, umletee Mungu?
Bwana atusaidie,.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Je! Mwanamke anapaswa afunikwe kichwa anapokuwa ibadani?
WANA JUHUDI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA.
MIJI YA MAKIMBILIO.
JE KUVAA PETE NI DHAMBI?
MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.
YOTE NAMTOLEA YESU_Tenzi za Rohoni.
Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?
Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu. (Blessed assuarance)
Wimbo huu ulindikwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Fanny Crosby, Mwanamke huyu japo aliishi kwa miaka 95 akiwa kipofu,lakini hakuacha kuitumia neema Mungu aliyompa kutangaza injili kwa njia ya Nyimbo zenye muundo wa Tenzi za rohoni na nyinginezo, katika maisha yake alifanikiwa kuandika nyimbo zaidi ya 8000, Na hii nyimbo “Ndio dhamana Yesu wangu” Ikiwa mojawapo, Nyingine inayojulikana sana mpaka leo ni “Usinipite mwokozi” yeye pia ndio aliyeiandika nyimbo hii alipokuwa amewatembelea wafungwa gerezani(angalia historia yake chini).
Phoebe Knapp
Sasa Siku moja alipokuwa amemtembelea rafiki yake nyumbani kwake aliyeitwa Phoebe Knapp, ambaye alikuwa ni mtunzi wa sauti za nyimbo, wakiwa nyumbani kwake Phoebe alianza kupiga mdundo wake aliokuwa ameutunga, kisha baada ya muda alimuuliza Fanny, Je unaweza kuniambia mdundo huu ni wa nyimbo gani?
Ndipo Fanny akamwambia “Ndio dhamana Yesu wangu”. Basi hapo ndio pakawa mwanzo wa mdundo na utunzi wa wimbo huo (1873).
Ndio dhamana Yesu wangu.
*****
Uimbapo wimbo huu kumbuka ni kipofu ndiye aliyeuandika, nawe pia unaposema “Ndio dhamana Yesu wangu” Basi awe kweli wokovu wako. Mpende yeye bila unafki na kumtumikia kwasababu ndiye aliyekufa kwa ajili yako.
Je! Umeokoka? Unajua kuwa Unyakuo upo karibu sana, kwasababu tunaishi katika kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia? Na kwamba hatutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili? Siku hizi zimekwisha, Hivyo kama upo tayari kumpa Yesu maisha yako leo ili wimbo huu uwe na maana kweli kwako. Basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
USINIPITE MWOKOZI Lyrics
BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics
CHA KUTUMAINI SINA lyrics
KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
MPINGA-KRISTO
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
UFUNUO: Mlango wa 1
Yote namtolea Yesu_tenzi za rohoni|Swahili hymn.
Wimbo huu uliandikwa na ndugu mmoja wa kimarekani aliyeitwa Judson W. Van DeVenter, Ndugu huyu alilelewa katika mazingira ya kikristo, aliokoka akiwa na miaka 17, kuanzia huo wakati wito wa kujitoa kikamilifu ulianza kuita ndani yake,lakini bado hakufanya uamuzi huo. DeVenter alifanikiwa kusoma mpaka chuo kikuu na kutunikiwa shahaba ya Sanaa, aliajiriwa kama mwalimu na mwongozaji katika shule za sanaa, hiyo ilimfanya aweze kusafiri sehemu nyingi mbalimbali katika bara la Ulaya kutokana na kazi yake ya sanaa.
Zaidi ya hilo alisomea pia na kufundisha elimu ya muziki, ilimchukua miaka 5 mpaka “Kumtolea yote Yesu”, Na hiyo ilikuwa ni baada ya marafiki zake kumshawishi sana, aingie katika kazi ya kumtumikia Mungu.
Mwaka 1896 Siku moja alipokuwa anafanya huduma ya muziki katika kanisani, hii ndio siku aliyoamua kuyasalimisha maisha yake ya ki-utumishi moja kwa moja kwa Kristo akiwa na miaka 41, aliamua kujitoa moja kwa moja kwa ajili ya kuifanya kazi ya unjilisti, na ndipo hapo huu wimbo “Yote namtolea Yesu” ulipozaliwa ndani ya moyo wake.
YOTE WA YESU.
Je! Na sisi tunapouimba wimbo huu tunaweza kumtolea Yote Yesu?. Je! mali zetu tunaweza kumpa yeye, nguvu zetu tunaweza kuzielekeza kwake?, akili zetu tunaweza kuzitumia ziitende kazi ya Mungu? Kama sivyo basi wimbo huu tutauimba kinafki.
Bwana atutupe kutambua hayo.
Shalom.
Je! Umeokoka? Ikiwa bado hujaokoka na unahitaji kuokoka leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo mbalimbali ya Neno la Mungu, kwa njia ya whatsapp yako, basi tutumie ujumbe kwa namba hii :+255 789001312
YESU KWETU NI RAFIKI
NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MAONO YA NABII AMOSI.
Kuwa mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe, ni muhimu sana!.
Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe. Karibu tujifunze biblia.
Mwinjilisti mmoja alichukuliwa katika maono mbinguni akakutana na Bwana Yesu, alionyeshwa mambo mengi yatakayotokea baada ya Maisha haya, kwa wema na waovu, lakini Pamoja na hayo kuna mambo mengine aliambiwa ambayo naamini leo tukiyatafakari yatatusaidia.
Na jambo mojawapo aliloambiwa lilikuwa ni kuhusu “uaminifu”…kulingana na maelezo yake, anasema Bwana Yesu alimwambia haya maneno;
“Neno langu ni nguvu inayoshikilia vitu vyote. Kwa kiwango ambacho unavyoamini Neno langu ni kweli, ndivyo unavyoweza kufanya vitu vyote. Wale ambao wanaamini kwamba maneno Yangu ni kweli, basi watakuwa pia wakweli kwa maneno yao wenyewe, Ni asili yangu kuwa kweli, na uumbaji huliamini Neno Langu kwa sababu mimi ni mwaminifu na kwake. Wale ambao ni kama mimi, pia huwa ni wakweli kwa maneno yao wenyewe. Neno lao ni hakika, na ahadi zao ni za kuaminika. ‘ndio’ yao inamaanisha ‘NDIO!’ na ‘hapana’ yao inamaanisha ‘HAPANA!’. Ikiwa maneno yako mwenyewe sio kweli, ni lazima pia utaanza kutilia shaka maneno Yangu, kwa sababu udanganyifu uko moyoni mwako. Ikiwa wewe sio mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe, ni kwa sababu bado hujanijua kabisa mimi ni nani, mimi ni mwaminifu kwa maneno yangu. Ili kuwa na imani, lazima uwe mwaminifu kwa maneno yako. Nimekuita utembee kwa imani kwa sababu mimi ni mwaminifu. Hiyo ni asili yangu”.
“Neno langu ni nguvu inayoshikilia vitu vyote. Kwa kiwango ambacho unavyoamini Neno langu ni kweli, ndivyo unavyoweza kufanya vitu vyote. Wale ambao wanaamini kwamba maneno Yangu ni kweli, basi watakuwa pia wakweli kwa maneno yao wenyewe, Ni asili yangu kuwa kweli, na uumbaji huliamini Neno Langu kwa sababu mimi ni mwaminifu na kwake.
Wale ambao ni kama mimi, pia huwa ni wakweli kwa maneno yao wenyewe. Neno lao ni hakika, na ahadi zao ni za kuaminika. ‘ndio’ yao inamaanisha ‘NDIO!’ na ‘hapana’ yao inamaanisha ‘HAPANA!’. Ikiwa maneno yako mwenyewe sio kweli, ni lazima pia utaanza kutilia shaka maneno Yangu, kwa sababu udanganyifu uko moyoni mwako. Ikiwa wewe sio mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe, ni kwa sababu bado hujanijua kabisa mimi ni nani, mimi ni mwaminifu kwa maneno yangu. Ili kuwa na imani, lazima uwe mwaminifu kwa maneno yako. Nimekuita utembee kwa imani kwa sababu mimi ni mwaminifu. Hiyo ni asili yangu”.
**mwisho**
Ndugu moja ya tatizo kubwa linalowakabili wakristo wengi wa sasa, ni kukosa UAMINIFU. Na uaminifu unaanza kwa mtu kukosa uaminifu kwa mambo yake mwenyewe kwanza. Kwamfano mtu baada ya kumpa Yesu Maisha yake, akaahidi kwamba hatasengenya tena, hatatukana, hataiba, hatafanya hichi au kile anaahidi pia atamtumikia Mungu, au atakuwa mtu wa kumtolea Mungu sana n.k..lakini baada ya muda kupita anaanza kwenda kinyume na kile alichokisema au alichokipanga. Ndugu hiyo ni hatari sana.
Maneno hayo ya mwinjilisti huyo aliyoambiwa na Bwana, nayaamini asilimia mia kuwa ni kweli. Hata katika hali ya kawaida kama huwezi kuwa mwaminifu kwa mali yako mwenyewe ni Dhahiri kuwa haiwezekani kuwa mwaminifu kwa mali ya mwingine. Kama kiatu chako mwenyewe hukitunzi wala hukijali utakijali vipi kiatu cha mwingine aliyekuazima ukivae kwa muda tu!. Uaminifu wa mtu unaanza kwa kile alichonacho yeye mwenyewe, ndipo aweze kuwa mwaminifu kwa kitu cha mwingine.
Kadhalika huwezi kuwa mwaminifu kwa Maneno ya Mungu, kama sio mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe.
Katika Luka 16:10 Bwana Yesu alisema maneno haya..
“Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia”.
Hivyo tujifunze kuyashika maneno yetu wenyewe..Ndipo tutakapoona Neno la Mungu likiwa na nguvu juu ya maisha yetu… Ukisema sitaki hichi au kile!, au nataka hichi!..basi kishikilie hicho kweli kweli usiwe na mawazo mawili mawili… Hiyo nguvu ya Maamuzi ndio chanzo cha nguvu zako za kiroho. Hata likitokea jambo mbele yako, na ukanukuu mstari Fulani kwenye biblia kwa Imani, basi jambo lile ulilolitamka kufuatia mstari huo uliounukuu, litatimia kama ulivyolisema kwasababu wewe pia huwa ni mkweli katika maneno yako…Hivyo Mungu atahakikisha na yeye analifanya neno lake kuwa kweli juu yako. Lakini tusipokuwa wakweli kwenye maneno yetu, basi kuna uwezekano pia neno la Mungu lisiwe kweli juu yetu. Tunaweza tukalinukuu sana na tusiona matokeo yoyote.. kwasababu sisi wenyewe sio waaminifu.
Bwana atusaidie, na atubariki.
Maran atha!
Je! Ni ipi tarehe sahihi Evil-merodaki alimtoa Yekonia gerezani?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
ZABURI 91, NI ZABURI YENYE NGUVU NYINGI.
SABATO TATU NI NINI?
Je! Mtume Paulo alikuwa ni Mrumi, Myahudi au raia wa Tarso?
JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?
NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,
Hakuna mtu anenaye katika Roho,kusema Yesu amelaaniwa
Kwanini Amelaaniwa aangikwaye msalabani?
Kutundikwa msalaba au kwa jina lingine kutundikwa mtini, ilikuwa ni adhabu iliyotekelezwa kwa watu wenye makosa ya hali ya juu sana.
Adhabu hii ilikuwa sio tu ilikuwa inatekelezwa na watu wa mataifa mengine kama wengi wanavyodhani ni Warumi tu, hapana bali pia ilikuwa inatekelezwa na Israeli pia.
Ni adhabu yenye mateso mengi sana, na vilevile ni adhabu ya aibu. Waliokuwa wanatundikwa msabani walikuwa sana sana ni wauaji. Makosa ambayo yalikuwa yanathibitisha kuwa wamelaaniwa na Mungu.
Kumbukumbu 21:22 “Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti; 23 mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako”.
Kumbukumbu 21:22 “Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti;
23 mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako”.
Utasoma sehemu nyingi, katika biblia mifano ya watu waliangikwa msalabani. (Mwanzo 40:18-19, Esta 2:22-23, Esta 7:10)
Jambo hilo hilo tunaliona mpaka katika kipindi cha karibu na agano jipya, katika ule ufalme wa Rumi, wafungwa wote waliokuwa na kesi kubwa za mauaji au wizi, n.k. Adhabu yao ilikuwa ni kuangikwa/kutundikwa msalabani ukiwa hai.
Lakini cha ajabu ni kwamba, adhabu zilizokuwa zinawahusu watu waliolaaniwa, zilimkuta mtu ambaye hakuwahi kutenda dhambi hata moja..Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO
Wagalatia 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, AMELAANIWA KILA MTU AANGIKWAYE JUU YA MTI; 14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani”.
Wagalatia 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, AMELAANIWA KILA MTU AANGIKWAYE JUU YA MTI;
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani”.
Lakini ni kwanini yamkute hayo yote?
Je ni ilikuwa ni bahati mbaya tu? Au Mungu alishindwa kumzuia? Jibu ni la, ilitokea vile kwa makusudi kabisa, ili ile hati ya mashitaka ya waliolaaniwa ifutwe juu yetu, aliibeba yeye ile hati ya laana, na ndio maana pale ambapo Baraba muuaji alipopaswa auawe, Yesu aliuawa badala yake, pale ambapo wewe mzinzi ungepaswa uhukumiwe milele kwa makosa yako, Yesu aliichukua laana hiyo siku ile msalabani, pale ambapo wewe uliye na dhambi ambazo nyingine ni aibu kuzitaja, Yesu alizichukua, hatia zote kwako.
Lakini hizo haziwezi kufutika juu yako, hivi hivi tu, bali ni mpaka uende kuzisalimisha msalabani.
Na ndio maana unahitaji kumpokea Yesu maishani mwako, vinginevyo hati ya mashitaka ya dhambi zako zitaendelea kubakia juu yako hadi siku ya mwisho, na utahukumiwa kama mkosaji.
Lakini ikiwa leo upo tayari kumpokea Yesu maishani mwako, basi leo leo atazifuta dhambi zako bure kabisa, haijalishi wewe ni mwenye dhambi kiasi gani.
Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Hivyo kama upo tayari leo kumpa Yesu maisha yako, basi uamuzi huo ni wa busara, hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali Share na wengine, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au katika namba hii hii +255 789001312
KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?
Nifanye nini ili niwe na uhakika nikifa naenda mbinguni?
MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.
UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.
Je! Watoto wa Ibrahimu/Wana wa Ibrahimu walikuwa ni wangapi?
Jumla ya wana wa Ibrahimu walikuwa ni nane (8). Kulingana na Biblia.
Mwana wa kwanza alikuwa ni Ishmaeli, ambaye alizaliwa na kijazi wa mke wake Sara aliyeitwa Hajiri (Mwanzo 16:1-4).
Mwana wa Pili, alikuwa ni Isaka,(Ndiye mwana wa Ahadi) ambaye alizaliwa miaka 14 baada ya Ishmaeli kuzaliwa.
Mwanzo 21:1 “Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema. 2 Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. 3 Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia”.
Mwanzo 21:1 “Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema.
2 Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. 3 Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia”.
Sara alipofariki, Ibrahimu akaoa mke mwingine, aliyeitwa Ketura. (Mwanzo 25:1-2)
Huyu Ketura ndiye aliyemzaliwa Ibrahimu wana wengine 6. Kufanya jumla ya watoto wote wa Ibrahimu kuwa 8, Biblia haielezi kuwa alikuwa na wana wengine wa kike.
Lakini katika wana hao wote, ni mmoja tu, aliyekuwa mrithi wa Ibrahimu, naye ni Isaka. Na siri moja ni kuwa wale wana wengine Ibrahimu aliwapa zawadi nyingi, lakini Isaka alipewa vyote, zawadi pamoja na urithi, kwasababu yeye ndiye aliyekuwa mwana wa Ahadi kutoka kwa Mungu.
Mwanzo 25:5 “Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo. 6 Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu”.
Mwanzo 25:5 “Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo.
6 Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu”.
Vivyo hivyo na sisi, tunaweza sote tukawa ni watu wa Mungu, tulioumbwa na Mungu, lakini si sote tukawa wana wa ahadi wa Mungu mfano wa Isaka. Wana wa ahadi ni wale waliozaliwa mara ya pili (yaani waliokoka). Na hao ndio Mungu kawaandalia vyote, thawabu pamoja na urithi wa ufalme wa mbinguni.
Ambapo Yesu alikwenda kuwaandalia waliompokea, Na siku atakaporudi, atawagawia urithi huo ambao alikuwa akiwaandalia kwa miaka 2000. Mambo ambayo jicho halijawahi kuoa wala sikio kusikia.
Swali la kujiuliza Ni je! na wewe ni mmojawapo wa wana wa Ahadi? Kama hujaokoka na kusimama, bado hujawa mwana wa ahadi, Lakini habari njema ni kuwa nafasi bado ipo lakini haitakuwepo siku zote ya wewe kufanyika hivyo.. Kama upo tayari leo hii kufanyika mtoto wa Mungu, na kuachana na dunia, na kutaka Yesu akuokoe, basi uaumuzi huo ni wa busara kwako, unachopaswa kufanya ni kufungua hapa ili upate maelekezo ya sala ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tazama chini kwa masomo mengine ya rohoni.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp yako mara kwa mara tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
WATOTO WA YESE KATIKA BIBLIA.
KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?
NENO NI LILE LILE, LAKINI UJUMBE NI TOFAUTI.
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
Watoto wa Yese katika biblia walikuwa ni wangapi?
Kitabu cha Samweli kinaonyesha Yese alikuwa na wana nane(8), Daudi akiwa ndio mwana wa mwisho kabisa, Lakini kitabu cha Mambo ya Nyakati wa kwanza kinaonyesha Yese alikuwa na Wana saba (7). Sasa swali linakuja Je! takwimu zipi ni sahihi? Je! biblia inajichanganya yenyewe?
Jibu ni hapana..
Tusome..
1Samweli 16:10 “Yese akawapitisha WANAWE SABA mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. 11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, AMESALIA MDOGO WAO, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku”.
1Samweli 16:10 “Yese akawapitisha WANAWE SABA mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.
11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, AMESALIA MDOGO WAO, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku”.
Soma tena.
1Nyakati 2:13 “na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama; 14 na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai; 15 na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi; 16 na maumbu yao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.”
1Nyakati 2:13 “na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;
14 na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai;
15 na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;
16 na maumbu yao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.”
Sasa ukiangalia hapo utaota kitabu cha Mambo ya Nyakati hakijatoa idadi Fulani kwamba wana wa Yese kuwa walikuwa ni saba tu, hapana badala yake kimeorodhesha majina, Sasa kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia utagundua kuwa kitabu cha mambo ya Nyakati kiliandikwa miaka ya mbeleni sana ukilinganisha na kitabu cha Samweli. Na kitabu hicho cha Mambo ya Nyakati wa kwanza kilikuwa kimejikita zaidi katika kuelezea uzao wa makabila ya Israeli(Vizazi vya wana wa Israeli).
Hivyo ilikuwa ni kawaida mtu asiyekuwa na uzao hakuweza kuorodheshwa katika orodha hiyo. Kwahiyo ni sahihi kusema Yese alikuwa na wana 9, lakini mmojawapo alifariki, pengine akiwa bado hajapata uzao, na hivyo mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati akaona hakukuwa na haja ya kumworodhesha pale. Ni kama tu Samweli alivyoacha kuwaorodhesha dada zao wawili. Kama isingekuwa kitabu cha Mambo ya Nyakati kuwaorodhesha ni rahisi kudhani walizaliwa wana wa kiume tu kwao, lakini kulikuwa hakuna haja ya kuwaorodhesha pale, kutokana na muktadha ya maudhui ya pale, kwamba waliokuwa wanahitajika na wana wa kiume, tu.
Ndivyo ilivyokuwa hata kwa mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati, walioorodheshwa na wale wenye uzao tu.
Kwahiyo kwa kuhitimisha ni kuwa Yese alizaa watoto nane (8) wakiume, na wawili (2) wa kike, Lakini mmoja baadaye alikuja kufa, wakabakia wana wa kiume 7 ndio wale walioorodheshwa katika 1Nyakati.
Tafadhali, angalia masomo mengine chini, ujifunze zaidi;
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo mballimbali kwa njia yaWhatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Adamu alikuwa na watoto wangapi?
Nuhu alikuwa na watoto wangapi?
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 8 (Kitabu cha Ezekieli)
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
YAKINI NA BOAZI.
MANENO ALIYOWEZA KUTAMKA YESU TU PEKE YAKE.
Jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, Natumai u mzima, karibu tujifunze Maneno ya Uzima kama ilivyo wajibu wetu, maadamu siku ile inakaribia.
Leo tutatazama kwa ufupi juu ya aliyoyatenda mwanamke mmoja aliyeitwa Rispa, mwanamke huyu alikuwa ni suria wa mfalme Sauli. Sasa ilitokea siku moja Israeli ilipitia katika njaa ya mfulilizo wa miaka mitatu, hakuna mvua yoyote juu, mpaka wakajiuliza ni nini hiki? Maandishi ya zamani tofauti na biblia yanasema Daudi akajiuliza pengine kuna watu wanaabudu miungu kwa siri, wakaangalia wakaona mbona sio, wakaangalia kwa kila namna, na wakachunguza kila kitu lakini bado hakuna kilichowapa jibu,
Ndipo Daudi akaona aende moja kwa moja kumuuliza Mungu, pengine labda ni yeye kamkosea, Lakini Mungu akamjibu na kumwambia kuwa kosa lipo katika nyumba ya mfalme Sauli, kwa kuwa yeye alikwenda kuwaua watu ambao walishaingia nao maagano tangu zamani kwamba hawatawaua kwa kinywa cha akina Yoshua (Yoshua 9:15)
Lakini mfalme Sauli hilo hakulijali, akawaua hao watu (wagibeoni), ndipo Mungu akaliona hilo na kuifanya nchi ya Israeli ikae katika njaa kwa miaka mitatu mfufulizo..
Sasa Daudi alichokifanya ni kuwaendea wale wagibeoni, na kuwauliza wawafanyie nini, ili hiyo laana indoke juu yao, ndipo Wagibeoni hawakutaka kitu kingine chochote, bali walitaka tu kumlipizia kisasi Sauli kwa uzao wake, hivyo wakamwomba wapewe wazao wa Sauli waliobaki wawaue kwa kuwatundika kwenye miti milimani. Ndipo Daudi akawajalia haja yao, akawapa wana 7 wa Sauli.
Sasa wawili kati ya hao wana 7 walikuwa wa huyu suria mmoja wa Sauli aliyeitwa Rispa. Tusome.
2Samweli 21:9 “akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za Bwana, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri. 10 Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku”.
2Samweli 21:9 “akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za Bwana, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri.
10 Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku”.
Unaweza kutengeneza picha mama anayeona watoto wake wakiuliwa kikatili mbele ya macho yake, kwa makosa ya watu wengine, halafu hawazikwi, wameachwa pale msalabani ni uchungu kiasi gani, anausikia..
Lakini kama tunavyosoma hapo huyu Rispa, hakuondoka pale mlimani, bali tangu siku hiyo watoto wake walipotundikwa, alikaa pale pale, kuhakikisha kuwa maiti za wanawe zinaheshimiwa, hakuruhusu ndege aje kula mizoga yao, wala usiku fisi waje kula mifupa.. Na zamani zile ilikuwa mizoga haiondolewi kwenye miti, mpaka hapo Mungu atakapojibu maombi, hivyo kama majibu yakija baada ya wiki moja, ndipo inashushwa pale mtini, yakija baada ya mwezi mmoja ndipo itakaposhushwa, vivyo hivyo hata yakija baada ya mwaka mzigo hiyo itaendelea kubakia pale mtini kwa mwaka mzima.
Na maandiko yanatuambia, mama yule hakuondoka pale mchana wala usiku tangu mwanzo wa mavuno ya shayiri mpaka mvua iliponyesha.. Mwanzo wa mavuno ya yashiri ni mwenzi wa 3-4, na mvua kunyesha ni mwezi 10..Hivyo mwanamke huyu alikaa pale mlimani kwa kipindi kisichopungua miezi 6..
Tengeneza picha, usiku na mchana, unafanya kazi ya kulinda, kuhakikisha maiti za wanao hazivunjiwi heshima kama mizoga ya wanyama, kwa kuliwa na ndege au fisi..alikaa pale mpaka ikawa ni mifupa tu imening’inia lakini hakuruhusu fisi achukue hata kidole cha wanawe.
Lakini tukirudi huku upande wa pili, Daudi akashangaa japokuwa tumewatimizia Wagibeoni haja zao, lakini mbona kama mvua inachelewa tena kwa miezi kadhaa?
Ndipo akasikia kuwa kumbe mama wa wale watoto wawili, tangu kipindi kile cha mauaji, hakuondoka pale mlimani akilinda maiti za wanawe.
Hilo likamfikirisha sana Daudi,, akawaza, kama mama huyu anazithamini maiti na mifupa ya wanawe waliotundikwa mitini na wao sio kitu kikubwa sana, Si zaidi mimi kuthamini mifupa ya Mfalme Sauli aliyeuliwa vivyo hivyo kama wao, (1Samweli 31:10-13) isitoshe ni mtiwa mafuta wa Mungu, mfalme wa Israeli na mimi sijui hata mifupa yake ilipo, Ndipo Daudi akatuma watu kwenda kuichukua mifupa ya Sauli iliyokuwa mbali sana, ng’ambo ya mto Yordani, akaileta Israeli, wakaifanyia maombolezo ya kitaifa, akaichanganya akaichukua ni mifupa ya wale watoto 7 waliouliwa, wakaenda kuzikiwa pamoja.
2Samweli 21:11 “Kisha akaambiwa Daudi hayo aliyoyafanya huyo Rispa binti Aya, suria wa Sauli. 12 Akaenda Daudi, akaitwaa mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe mikononi mwa watu wa Yabesh-gileadi; waliyoiiba katika njia ya Bethshani, hapo Wafilisti walipowatungika, katika siku hiyo waliyomwua Sauli huko Gilboa; 13 naye akaileta toka huko hiyo mifupa ya Sauli, na mifupa ya Yonathani mwanawe; nao wakaizoa mifupa yao waliotundikwa. 14 Kisha wakaizika mifupa ya Sauli na ya Yonathani mwanawe katika nchi ya Benyamini, huko Zela, kaburini mwa Kishi babaye; wakafanya yote aliyoyaamuru mfalme. Na baadaye Mungu aliiridhia hiyo nchi”
2Samweli 21:11 “Kisha akaambiwa Daudi hayo aliyoyafanya huyo Rispa binti Aya, suria wa Sauli.
12 Akaenda Daudi, akaitwaa mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe mikononi mwa watu wa Yabesh-gileadi; waliyoiiba katika njia ya Bethshani, hapo Wafilisti walipowatungika, katika siku hiyo waliyomwua Sauli huko Gilboa;
13 naye akaileta toka huko hiyo mifupa ya Sauli, na mifupa ya Yonathani mwanawe; nao wakaizoa mifupa yao waliotundikwa.
14 Kisha wakaizika mifupa ya Sauli na ya Yonathani mwanawe katika nchi ya Benyamini, huko Zela, kaburini mwa Kishi babaye; wakafanya yote aliyoyaamuru mfalme. Na baadaye Mungu aliiridhia hiyo nchi”
Na kwa tukio hilo likapelekea Mungu kuileta mvua juu ya nchi.
Ni nini tunajifunza?
Bidii ya mwingine, na kujali kwa mwingine, kunaweza kukawa sababu ya wewe Mungu kukuzuilia baraka zako. Unasema wewe ni mkristo, umeokoka, Lakini Mungu akimtazama mtu mwingine ambaye hamwabudu Mungu mkuu unayemwabudu wewe lakini ana bidii usiku na mchana ya kumtafuta mungu wake, ujue kuwa mbingu itazuliwa juu yako.. Haijilishi utasema umeokoka kiasi gani.
Ikiwa watu wa dini nyingine wanamfanyia mungu wao dua mara 5 mpaka 10 kwa siku, lakini wewe unaambiwa uombe lisaa limoja kwa siku, huwezi unategemea vipi mbingu isifungwe juu yako?, Hata kama utakuwa umetimiza vigezo vingine vyote, yule mwingine atabakia kuwa hukumu tu kwako.
Yatupasa tujirekebishe, ikiwa wao wanafunga siku 30 kila mwaka, sisi tunapaswa tuende zaidi ya hapo, lakini kama inapita mwaka mzima hujawahi kufunga hata wiki moja, mbingu zitafunga tu juu yako.
Ikiwa wanazingatia kushika aya za vitabu vyao vya dini kwa bidii, lakini wewe mkristo hujui hata biblia inavitabu vingapi, hujawahi hata kusoma kitabu kimoja cha biblia ukakimaliza chote, unasubiria tu kuhubiriwa, mbingu zitafungwa juu yako. Mpaka siku utakapojua tatizo ni nini.
Hivyo sote tujitathmini, Na Bwana atusaidie.
Maran Atha.
JE TATIZO LA KULA KUCHA NI ISHARA YA KUWA NA MAPEPO?
SAUTI AU NGURUMO?
CHOCHOTE UMFANYIACHO KRISTO KINA THAMANI.
JINSI YA KUJIWEKA KARIBU NA MUNGU.
HATUTAACHA KUJIFUNZA NENO KILA INAPOITWA LEO.
IJUE NGUVU YA IMANI.
WhatsApp
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tuyatafakari maandiko pamoja.
Katika maisha, hakikisha unarekebisha vitu vinne. 1) Kazi unayoifanya 2) Kabila unalotoka 3) Nchi unayotoka 4) Mahali unapotoka.
Haya ni mambo makuu manne ambayo ni nguzo katika kuyajenga au kuyaharibu maisha. Na kimojawapo kisipokaa sawa mbele za Mungu, basi kitakuletea tufani kubwa katika maisha.
Hebu tuisome kidogo habari ifuatayo..
Yona 1:7 “Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona. 8 Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? 9 Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu. 10 Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha. 11 Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka“
Yona 1:7 “Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.
8 Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani?
9 Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu.
10 Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha.
11 Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka“
Walipoanza kwenye nchi, aliwaambia yeye ni Mwebrania..hivyo wakajua moja kwa moja ni mtu wa Taifa la Israeli,ametokea katika mojawapo ya miji ya kule, alipoendelea mbele kidogo, kwenye shughuli anayoifanya akasema yeye anamcha Mungu (yaani maana yake ni mtumishi wa Mungu), anayehudumu katika shamba la Mungu, na kwamba ameikimbia kazi ya Mungu, ndipo walipoelewa tatizo lipo hapo, wakaogopa na kutafuta suluhisho kabla mambo hayajazidi kuharibika.
Sasa endapo Yona ingekuwa hajaikimbia kazi ya Mungu na baharini imewachafukia vile, basi tatizo ni lazima lingekuwa aidha kwenye kabila analotokea, na kama sio kwenye kabila basi kungekuwa na tatizo kwenye nchi anayotokea..au mahali anapotokea.
Hivyo Nataka uone leo kwamba kazi yako unayoifanya inaweza kuwa chanzo cha Tufani na misukosuko, hakikisha kazi unayoifanya yoyote ile aidha ya mikono, iwe inampendeza Mungu kwa viwango vyote, uwe mwaminifu katika kazi yako na pia jiepushe na hila na wizi. Vilevile kama unafanya kazi ya Mungu hakikisha hukwepi majukumu yako kama mtumishi, wala huifanyi kwa ulegevu vinginevyo utakumbana na tufani kama iliyokuta Yona.. Na mkristo yoyote ni lazima awe na jukumu katika kazi ya Mungu. Hivyo jihakiki sana.
Yeremia 48:10 “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu”
Vile vile kabila unalotoka linaweza kuwa chanzo cha matatizo. Makabila mengi yana mila na desturi zilizo kinyume na Neno la Mungu, makabila mengi yana matambiko na ushirikina, jiepushe na hayo yote baada ya kuokoka. Zipo mila nyingine ambazo ni aibu hata kuzisema hapa..Hizo zote ni rahisi kukusababisha tufani katika maisha yako, na hasira ya Mungu kuwaka juu yako. Jiepushe na hizo mila…Sisemi kwamba ujiepushe na ndugu zako au wazazi wako wanaofanya hizo mila!, na uwachukie na kuwasema Hapana!..endelea kubaki na ndugu zako, waheshimu,wapende, watunze, waombee, na ishi nao kwa furaha zote na kushirikiana nao kwa mambo mengine yote mazuri wanayoyafanya lakini usishiriki mila hizo zilizo kinyume na neno la Mungu.
Pia nchi unayotokea au mahali ulipo panaweza kuwa chanzo cha tufani katika maisha yako..Hivyo ni wajibu wa kushiriki mambo mazuri yanayoendelea katika nchi yako, na kuyakataa yale mabaya yote, Nchi inaweza kuhalalisha ndoa za jinsia moja kisheria kabisa!, nchi inaweza kuhalalisha uvutaji wa bangi, nchi inaweza kuhalalisha utoaji mimba, nchi inaweza kuhalalisha ndoa za wanadamu na wanyama n.k.
Nchi ya namna hiyo tayari ipo chini ya laana na hasira ya Mungu na watu wake ni hivyo hivyo..Hivyo ni wajibu wa wewe uliyeokoka unayeishi ndani ya nchi kama hiyo, kujitenga kwa kutofanya hayo mambo au kukubaliana nayo, ili usiwe miongoni mwa wanaomwudhi Bwana Mungu. Na kujitenga sio kutoongea nao, au kutofanya nao kazi kwenye kampuni moja!..hapana..bali kujiepusha na njia zao, mfano wa Danieli, Meshaki, Shedraka na Abednego jinsi walivyoishi katikati ya taifa la Babeli lakini hawakushiriki matendo ya watu wa Babeli, na walifanikiwa sana katikati ya Taifa lile ovu.
Bwana atusaidie na Bwana atubariki
Na mwisho kabisa kama umejaliwa kupata watoto, au unampango wa kuwa na watoto..kumbuka kuwalea katika njia inayowapasa, angali wakiwa wadogo, kwasababu wakiwa wakubwa hawataiacha biblia inasema hivyo, Na pia wewe mwenyewe kama hujaokoka!. Mlango wa Neema upo wazi, usiidharau injili hata kidogo inayohubiriwa kwako bure! Bila kutozwa chochote… Hata vitu vingi vinavyoishiaga kutolewa bure mara nyingi huwa ni vya gharama sana na vya muhimu sana, kwasababu kama vingeuzwa basi hakuna mtu angeweza kununua..
Hata madawa yanayotolewa bure! Mengi ni ya gharama ya juu sana, yananunuliwa ghali sana aidha na serikali au mashirika binafsi lakini yanakuja kutolewa bure tu kwa watu ili kuokoa maisha!. Na wokovu ni wa gharama sana na wa muhimu kwa kila mtu, ndio maana tunapewa bure!, hivyo usiudharau, Laiti tungetozwa fedha ili kuupata, basi hakuna ambaye angeweza kuununua, hata dunia nzima tungekusanya nguvu zetu zote, tusingeweza kununua wokovu wa mtu mmoja tu! Licha ya watu wa dunia nzima. Mpokee Yesu leo kama hujampokea, na ukabatizwe na kupokea Roho Mtakatifu. Kwa usalama wa maisha yako.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
YONA: Mlango 1
YONA: Mlango wa 2
JINA LA MUNGU NI LIPI?
USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.
KUMCHA MUNGU NI NINI? NA MTU ANAMCHAJE MUNGU?
JE NI LAZIMA MKRISTO AOE/AOLEWE?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA ZA LUTU.