Nafasi ya mwanamke katika kanisa ni ipi? Je anaruhusiwa kuwa mchungaji, au askofu?
Mtume Paulo alisema,..
1Wakoritho 14;34 “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana”
Hapa maandiko yanaweka wazi kabisa mwanamke hana nafasi ya uongozi wowote katika kanisa, au kutatua tatizo lolote katika kanisa, Mungu aliuweka huu utaratibu, kulifundisha kanisa, maana mwanamke anawakilisha kanisa la Kristo, na kama vile kanisa limtiivyo Kristo katika kila Neno vivyo hivyo na wanawake wanapaswa kujitiisha chini ya waume zao ikiwemo kuongozwa kwa kila jambo kama maandiko yanavyosema kwenye..
Waefeso 5:22-23“Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Kwahiyo mwanamke hajapewa mamlaka yeyote ya kumtawala mwanamume iwe kanisani au nyumbani, Kichwa cha mwanamke ni mwanamume na kichwa cha mwanamume ni Kristo.
Sasa zile huduma tano zilizozungumzwa katika waefeso 4:11( “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”) hizi zilitolewa kwa wanaume tu ,ofisi hizi tano ni za uongozi katika kanisa hakuna hata moja inayomhusisha mwanamke. ikiwemo maaskofu na mashemasi wote wanapaswa wawe wanaume.
Na Bwana Yesu alitoa sababu katika
1timotheo 2:11-14 ” Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.”
kwahiyo hapa tunaona kuwa Hawa ndiye aliyedanganywa na sio Adamu. Na Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, kama tu vile sisi tunavyowatii wazazi wetu pasipo shuruti na kuwaheshimu na kuwapa mamlaka yote katika familia ni kwasababu wao ndio waliotutangulia kwanza duniani na ndio waliotuzaa, lakini tunawapa heshima yao je! si zaidi kwa mwanamke kumtii Adamu aliyetoka katika ubavu wake na ndiye aliyeumbwa wa kwanza??..
Kuna baadhi ya wanaojiita watumishi wa Mungu wanaoingiza harambee za kijamii katika kazi ya Mungu na kufundisha kuwa kila kitu mwanaume anachofanya, mwanamke pia anaweza kufanya, hawajui kwamba wanaenda nje ya mpango wa Mungu kwa maana kila jambo Mungu aliweka kwa utaratibu na kwa kulifundisha kanisa.
Tunaona mitume 12 wote wa Bwana Yesu walikuwa ni wanaume, katika agano la kale hakuwahi kuwa na kuhani mwanamke, ilikuwa inafahamika hivyo tangu awali shughuli zote zinazohusu madhabahu ya Bwana zilikuwa zinafanywa na wanaume, lakini mambo haya yalianza kujitokeza ilipofika kuanzina karne ya 20 mpaka leo wanawake walipoanza kutafuta haki sawa ndipo hapo walipoanza kujiingiza katika siasa, na leo hii shetani amefanikiwa kuingiza hiyo roho katika kanisa na kufanya madhabahu ya Mungu itawaliwe na wanawake. Haya ni machukizo mbele za Mungu, na ni dhambi yenye uzito ule ule sawa na wasiokuwa wa kabila la walawi kuhudumu katika nyumba ya Mungu kwenye agano la kale.
Swali ni je! wanawake wanaofanya hivyo Mungu hayupo nao??
Ni siri kubwa imekaa hapo ambayo watu wengi hawaijui, wanapoona mtu anatenda miujiza, vipofu wanaona, unabii unatolewa n.k. wakidhani ndio uthibitisho kuwa mtu huyo yupo katika njia sahihi biblia inasema
Mathayo 7:22-23 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”
Kwahiyo tunaona haijalishi unatenda miujiza kiasi gani, uthibitisho pekee wa Mungu kuwa na wewe ni kuyatenda mapenzi ya Mungu ambayo ni kuishi katika Neno lake, na NENO lake ndilo hilo
“Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu ”
Kwahiyo yoyote aendaye kinyume na hayo anaenda nje ya maagizo ya Bwana haijalishi ni miujiza kiasi gani inatendeka kwenye huduma yake, anafanya kazi isiyokuwa na faida.
Je! kazi ya mwanamke ni ipi katika kanisa?
Kuna zile karama Mungu alizitoa kwa wote, kwa mwanaume na mwanamke. (ijulikane kuwa karama ni tofauti na huduma) ukisoma..
1wakoritho 12:4-10 ” Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.
5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.
6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; ”
Hivyo basi Mungu anaweza kumtumia mwanamke kutoa unabii/ujumbe katika kanisa lakini sio kufundisha. Mungu anaweza kumtumia mwanamke kuponya wagonjwa, kunena kwa lugha, kutoa unabii, hizi zote ni karama za Mungu na anaweza kumtumia yeyote, lakini zile huduma ambazo ni ofisi kuu tano yaani, mitume, manabii, wainjilisti,waalimu na wachungaji, ikiwemo na mashemasi, hizi ni huduma za uongozi wa kanisa, na hazimuhusu mwanamke hata kidogo.
Wanawake wanapaswa kujifunza, kwa kuuliza maswali kwa mtu yeyote ikiwemo mchungaji wake yahusuyo masuala yake ya kiroho na pia kuruhusu karama za Mungu kutenda kazi ndani yake, ikiwemo, kunena kwa lugha, kutoa unabii, uponyaji, ishara na miujiza, ndoto,kumsifu na kumwimbia Mungu wao, na kushuhudia wengine katika nafasi uliyopo kwa jinsi Mungu atakavyokujalia.
Isipokuwa kufundisha au kuhubiri kanisani au kumtawala mwanaume kwa namna yoyote na kufungua huduma na kujiita mchungaji, au mwinjilisti au askofu au mwalimu au mtume ni makosa, kama ulishawahi kufanya hivyo pasipo kujua jirekebishe na ukae katika nafasi uliyoitiwa.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
KWANINI MUNGU ANAMPA NABII HOSEA MAAGIZO YA KUMUOA MWANAMKE KAHABA? (HOSEA 3)
Imekuwa ikijulikana na wengi kuwa unyakuo utakuwa ni tendo la ghafla. kufumba na kufumbua mamilioni ya watu watatoweka, watu watakuwa wakikimbia mabarabarani, ulimwengu mzima utataharuki, ndege zitaanguka, ajali nyingi zitatokea duniani, amani itapotea ghafla na watu watakuwa wakilia na kuomboleza, wakimwona mpinga-kristo akipanda kutoka kuzimu kuleta uharibifu duniani kote. Lakini Je! ni kweli unyakuo utakuwa kwa namna hiyo kulingana na maandiko?. Tukisoma;
1wathesalonike 4:16-17 “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na MWALIKO, na SAUTI YA MALAIKA MKUU, na PARAPANDA YA MUNGU; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”.
Tukiyachunguza haya maandiko hapa juu tunaona kuwa kuna hatua tofauti tatu zitakazoambatana na kuja kwa Bwana Yesu kulichukua kanisa lake: Hatua ya kwanza: Bwana atashuka kutoka mbinguni na ‘MWALIKO’.na hatua Ya pili: Bwana atashuka na ‘SAUTI YA MALAIKA MKUU’..na hatua Ya tatu: Bwana atashuka na ‘PARAPANDA YA MUNGU’. Hii inaashiria kwamba kuja kwa Bwana kutakuwa ni kwa hatua za kufuatwa.na sio ghafla tu kama inavyodhaniwa. Tunapaswa tuzitambue ili tusiwe gizani kwa jinsi siku zinavyokaribia, Hebu tuzitazame hizi hatua tatu kwa undani zaidi.Vinjari Miwani yetu inayofadhiliwa na mshirika, yenye chaguo mbalimbali ili kuendana na kila ladha na bajeti, zinazopatikana kununua mtandaoni
Biblia inasema 1wathesalonike 4:16 “Bwana atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko” sasa hili neno “mwaliko” kama linavyozungumziwa hapo halimaanishi ule mwaliko wa kama mtu anaalikwa kwenye sherehe fulani hapana! Bali inamaanisha Kilele za nguvu zinazoambatana na nderemo na vifijo kuashiria kuwa mtu fulani wa kipekee anakaribia kuwasili mfano,Raisi, Bwana arusi n.k,… Hii ni kwa kusudi la kumfanya mtu anayemngojea kujiweka tayari kumlaki atakapofika langoni mwake, ili isiwe ghafla ghafla.
Hivyo Tukisoma kwenye tafsiri nyingine za biblia, mfano ile biblia ya kiingereza KJV inatuambia..
”For the Lord himself shall descend from heaven with a SHOUT, with the voice of the archangel, and with the trump of God: and the dead in Christ shall rise first:”
Sasa Hapo neno ‘Shout’ linamaanisha ni kupaza sauti kuu za kelele kwa nguvu, ili kumfanya mlengwa aamke au awe makini kujianda na tukio linalokwenda kutokea mbele.
Ili tuelewe vizuri juu ya maneno haya na jinsi mwaliko ulivyo, tupitie baadhi ya vipengele vya maandiko, kama tunavyosoma mfano wa wale wanawali kumi. Katika Mathayo 25,
Mathayo 25:1-13″ 1 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.
2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.
3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;
4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.
5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.
6 Lakini usiku wa manane, PAKAWA NA KELELE, Haya, bwana arusi; TOKENI MWENDE MKUMLAKI.
7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa. “
Hivyo turudi katika kizazi hichi tuishicho, sote tunajua kuwa kuja kwa Bwana wetu YESU KRISTO kumefananishwa na wale wanawali kumi waliokuwa wakingoja kumlaki Bwana wao atakapokuja waende naye arusini, Na tunaona ilipofika usiku wa manane wote waliishiwa nguvu, na kusinzia kwa kuona Bwana wao anakawia kwa kungojea sana, Lakini ghafla usiku ule ule pakawa na ”KELELE kubwa ikisema Tazama! Bwana arusi anakuja”.
Kwahiyo kitendo kile cha zile kelele kuwaamsha hawa wanawali 10 kutoka usingizini huo ndio ule ‘Mwaliko’ unaozungumziwa pale kwenye ( 1wathesalonike 4:16-17). ambapo biblia inasema, Bwana atashuka pamoja na mwaliko… ni kwa dhumuni la kumwamsha bibi arusi ili ajiweke tayari kwa kwenda kumlaki Bwana wake. Na kama huo mwaliko usingepita kwanza hakuna mwanawali yoyote angeweza kutambua kuja kwa Bwana wake, wote ingewajia kama mwivi, Hivyo jambo hili kutangulia ni mahususi ili kumfanya aamke usingizini na kuaacha mambo yake anayoyafanya yote aanze kuiweka taa yake sawa, kwasababu muda waliokuwa wanauongojea umewasili.
Kanisa lilipokuwa limelala katika vipindi vyote vya nyuma baada ya roho ya mpinga Kristo kuliharibu, na kulipindua kama tunavyosoma katika historia ya ukristo jinsi kanisa lilivyopitia katika kipindi kirefu cha giza, na jinsi lilivyoingia katika mafundisho ya upotofu pale ukristo ulipooana na upagani na kuendelea hivyo kwa muda mrefu sana wa mamia ya miaka..
Sasa muda wote huo ulikuwa ni muda kanisa lilikuwa limelala, Lakini ulipofika wakati wa Bwana kushuka kulijilia kanisa lake tena, hakuja ghafla, kwasababu hakuna ambaye angestahili kwenda naye, alianza kwanza na kutanguliza Mwaliko wake, ni ujumbe wa kumwamsha kwanza bibi arusi kutoka usingizini yaani (mwaliko) na kumfanya aiweke tayari taa yake na ahakikishe pia inayo mafuta ya ziada (mafuta ni Roho Mtakatifu na mafuta ya ziada ni ufunuo wa Roho wa Mungu).
kwahiyo huu MWALIKO ni UAMSHO wa Roho ambao unatangaza ujio wa Bwana Yesu kulichukua kanisa lake na watu wajiweke tayari kumpokea Bwana wao. Kama tulivyoona katika
(Mathayo 25:6..na ilipofika usiku wa manane pakawa na ”KELELE Bwana arusi anakuja”). Sasa huu mwaliko ulianza na Martin Luther mjumbe wa kanisa la tano, ukaendelea hivyo hivyo na John Wesley mjumbe wa kanisa la sita, Na mwisho Bwana aliutoa tena kwa kupitia mjumbe wa kanisa la saba William Branham,..
Kumbuka sauti hiyo ya mwaliko ilianza kusikika kutoka mbali, na ilivyokuwa inazidi kukaribia ndivyo ilivyozidi kuwa kubwa zaidi, Hivyo sauti ya mwaliko wa kanisa hili la mwisho la Laodikia ni kali, kuliko ilivyokuwa kwa kanisa la tano au la sita. Kwasababu Bwana yupo mlango kufika amtwae Yule mwanawali mwerevu aliyeitii sauti ya mwaliko. Kumbuka ndugu Ujumbe tulionao sasa hivi ni KUTOKA kabisa katika mifumo ya dini na madhehebu na kuanza kuishi maisha ya utakatifu, kama mtu anayemngojea Bwana wake, Huko ndiko kuzitengeneza Taa zetu.
Luka 12: 35 “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA
36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, ATAKAPORUDI KUTOKA ARUSINI, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao”.
Unaona hapo?..MWALIKO wa kuja kwa Bwana ulishaanza tangu wakati wa kanisa la tano, na la sita, na unaendelea na la saba. Ulianza na Martin Luther, kwa ujumbe wa kuwahubiria watu watoke, kutoka katika ile dini ya uongo(Katoliki). Ndipo kuanzia huo wakati bibi-arusi wa kweli wakaanza kuzitengeneza TAA zao, lakini cha kusikitisha ni baadhi yao hawakuwa na mafuta ya kuwatosha ya ziada (Ufunuo wa Roho),kuwawezesha kudumu katika hayo mpaka Bwana wao atakapokuja, hivyo kilichowatokea ni wao kudumu katika dhehebu linaloitwa Lutherani, hawamruhusu tena Roho wa Mungu kufanya kazi ndani yao, wakawa wametosheka na mapokeo yao tu, hawakujua kuwa inawapasa wapige hatua nyingine katika kumjua Mungu,..[Wanadamu tumeumbiwa kukua kila siku, katika mambo yote, kadhalika na mambo ya rohoni ukiona hukui jua tu kuna tatizo mahali Fulani.]
Kadhalika John Wesley mjumbe wa kanisa la sita naye pia aliutangaza ule mwaliko kwa nguvu zaidi kuliko Luther wengi walitengeneza taa zao lakini ulipofika wakajitengenezea dini na kusababisha taa zao nao kuzima, na katika kanisa la mwisho la Laodikia Bwana alimnyanyua mjumbe wake tena Ndugu. William Branham na sauti kubwa na ya mwisho ya mwaliko kuwaambia watu watoke wakamlaki Bwana wao maana ameshafika na muda umekwisha, sasa bibi-arusi wa kweli atatoka katika hili kanisa la mwisho kwa kutii sauti ya mtumishi wake na kwenda katika hatua inayofuata yaani ya “sauti ya Malaika Mkuu”.
Lakini pia kama makanisa mengine ya nyuma yalivyomzimisha Roho kwa kujiundia madhehebu kadhalika na katika kanisa hii la Mwisho wapo waliojiundia dhehebu, na kujiita wa-Branhamu, kama tu wafuasi wa Luther walivyojiita wa-luther.
kadhalika na kundi hili pia halitafika katika hatua inayofuata ya sauti ya malaika mkuu. Kundi hili litaishia njiani, kwasababu limemzimisha Roho, kumbuka Bwana hajawahi kuleta dhehebu lolote, Bwana huwa analeta UAMSHO kama ilivyotokea siku ya Pentekoste, madhehebu yote ni mifumo ya wanadamu inayodai kumtafuta Mungu lakini ndani yake imejaa mapokeo ya wanadamu na kumzimisha kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba anaonekana mwanadamu au mapokeo zaidi ya YESU KRISTO Mungu wetu,na ndio maana Bwana kayakataa.
Hizi ni nyakati za mwisho, utafika wakati utatamani sekunde moja ya kuwa mtakatifu utakosa, siku hiyo utakapogundua kuwa umeachwa, leo unahubiriwa tunaishi katika siku za mwisho unadhihaki unasema Bwana Yesu hawezi kurudi kizazi hiki,bado sana, ni kweli hatujui siku wala saa lakini alitupa majira ya kuja kwake na dalili zote zinaonyesha kuwa tunaishi katika kizazi ambacho tukashuhudia kuja kwa pili kwa Yesu Kristo.
Kwahiyo kama hautaweza kuitikia hii sauti ya MWALIKO kwa kujiweka tayari kumpokea Bwana sasa kama mwokozi wako, na kwa kupokea Roho Mtakatifu na kuishi maisha yampendezayo Mungu ya utakatifu sawa sawa na NENO na sio sawasawa na dhehebu lako au dini yako, hautawezi kuendelea hatua inayofuata, na wala hautaijua, utafanana na wale wanawali wapumbavu waliokosa mafuta katika taa zao.
Tunaishi katika wakati wa matenganisho, Bwana anawatenga wanawali werevu kutoka katika wanawali wapumbavu, anatenga magugu na ngano, magugu atawatuma watu (manabii wa uongo) wayafunge matita matita (madhehebu) na ngano atawatuma watumishi wake wayakusanye(kwa ajili ya unyakuo) ghalani mwake. Je! Wewe upo kundi gani?
1 wathesalonike 4:16 “BWANA ATASHUKA NA SAUTI YA MALAIKA MKUU
Hii ni hatua ya pili na itawahusu tu wale waliokwisha kuisikia sauti ya mwaliko(yaani wanawali werevu), wale ambao wamekwisha weka taa zao tayari wakiwa na mafuta ya ziada ambayo ni Roho Mtakatifu na Roho ya ufunuo (ya kutaka kumjua Mungu zaidi na zaidi pasipo kumzimisha ndani yao) hawa ndio wale wanawali wenye busara.
Tunapaswa tujiulize hii sauti ya Malaika Mkuu ni ipi??
Tukisoma Katika kitabu cha
Ufunuo 10:1-7 ” Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.
2 Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi.
3 Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao.
4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.
5 Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni,
6 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya;
7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.”
Huyu Malaika mwenye nguvu anayezungumziwa hapa akishuka kutoka mbinguni ni BWANA YESU KRISTO, kumbuka neno malaika maana yake ni “mjumbe” na Bwana Yesu anajulikana kama “mjumbe wa Agano” Malaki 3: 1 “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule MJUMBE WA AGANO mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi”.
Na hapa kwenye ufunuo anaonekana akiwa ameshika kitabu kidogo, na hichi kitabu si kingine zaidi ya kitabu cha ukombozi wa mwanadamu, ndio kile kilichokuwa kimetiwa mihuri saba, Ufunuo 6 na tunasoma pia aliapa “hakutakuwa na wakati baada ya hapa” kuashiria kuwa muda utakuwa umeisha wakati atakapokuwa anazungumza, tunaona pia alipolia kwa sauti kuu kama simba angurumavyo zile NGURUMO SABA zikatoa sauti zao ambazo Yohana aliambiwa asiziandike, hizo ni siri ambazo hazijarekodiwa mahali popote katika biblia ni siri zitakazokuja kufichuliwa katika hatua hii ya pili, na ni kwa ajili tu ya kumpa bibi arusi imani ya kwenda katika unyakuo. Chapisho hili limefadhiliwa na https://www.fakewatch.is/product-category/richard-mille/rm-005/ washirika wetu.
Kwahiyo hii ya SAUTI YA MALAIKA MKUU ni siri ya zile ngurumo saba, ambazo zitakuja kuhubiriwa kwa bibi-arusi aliyeko ulimwenguni kote,Hizi ngurumo saba zitakapotoa sauti zao ndipo bibi arusi atapata imani kamili ya kwenda kwenye unyakuo, katika uamsho huu yatahubiriwa mambo ambayo hayajaandikwa katika biblia. Haimaanishi kwamba yatapingana na biblia hapana bali ni mambo ambayo hayajarekodiwa katika biblia yatakuwa ni ufunuo wa mambo mapya mahususi tu kwa wale wakristo ambao wameitikia wito wa sauti ya mwaliko.
Uamsho huo hautakuwa wa watu wote wa dunia nzima, hapana bali utakuwa ni wa kikundi kidogo sana Bwana alichokipa neema kuvuka hatua ya kwanza ya mwaliko.
Mungu alikuwa na makusudi kwanini alimwambia Yohana asiziandike zile ngurumo saba kwa wakati ule, ni kwa sababu maalumu zije zifunuliwe kipindi cha siku za mwisho katika hatua hii ya pili,kwa bibi arusi wa Kristo aliyewekwa tayari, ni siri zilizoandikwa katika kile kitabu kidogo kilichokuwa kimeshikwa na yule malaika mkuu(Yesu Kristo). Wakati huo hizo ngurumo zitakapokuwa zinatoa sauti zao, hawa wengine hawatafahamu chochote, kwao wataona kama ni imani mpya imezuka duniani..Lakini walio na Roho Mtakatifu kweli kweli watafahamu kwa uweza wake, kutaambatana na maagizo ya kufuata mahususi kwa bibi-arusi wa Kweli.
kwahiyo hiyo Huyu MALAIKA MKUU tuliyemsoma kwenye 1Thesalonike 4:16 , ndiye huyo tunayemwona katika kitabu cha ufunuo sura ya kumi aliyetoa zile ngurumo saba. Na si mwingine zaidi ya Bwana Yesu Kristo.
Hatua hii ni ya mwisho na inahusu PARAPANDA YA MUNGU .Tukisoma 1wathesalonike 4:16″ Inasema..Bwana atashuka na parapanda ya Mungu. nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”
Hii ni sauti ya parapanda ya YESU kwa wafu kwa ajili ya ufufuo, hapa ndipo wafu watakapoisikia sauti ya Mungu ikiwaita huko waliko nao watafufuka na kuivaa miili ya utukufu na kuungana pamoja na wale walio hai na kwenda kumlaki Bwana mawinguni, kama vile Lazaro alivyoisikia sauti ya Bwana ilipomwambia njoo huku nje Yohana 11:43 naye akafufuka. ndivyo itakavyokuwa kwa wafu waliokufa katika Kristo siku ile watakapoisikia sauti ya parapanda ya mwisho.
Yohana 5:25 Inasema.. “Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.”
Hii ndio hatua ya mwisho na sisi tulio hai miili yetu itabadilika kufumba na kufumbua na kuungana na waliofufuliwa kwenda mbinguni kwa BWANA WETU YESU KRISTO.
Na sio wakristo wote watanyakuliwa bali wale tu walioitikia mwaliko, na sauti ya malaika Mkuu, na hatua hii inafananishwa na “check-in procedures” katika safari za ndege.
Na kumbuka sio watu wote watafahamu kama unyakuo umepita watu wasiofahamu wataendelea na shughuli zao kama kawaida, itakuwa ni siri hakutatokea vurugu wala ajali mabarabarani, kama kukitokea vurugu mpinga-kristo atafanyaje kazi sasa hapo?.
Ni dhahiri kuwa hakuna atakayeshawishika kwasababu watu wote watamjua mpinga-kristo amefika, na unyakuo hapo utakuwaje wa siri tena?? lakini siku hiyo wengi hawatamjua mpinga-kristo wala chapa yake kwasababu hatakuja akiwa na mapembe, atakuwa ni mtu anayeheshimika,na kukubalika na dunia, atakuja na kivuli cha amani, na atapendwa na wengi, na atakuwa ni mtu wa kidini, na anashika biblia, lakini ndani yake ni utendaji kazi wa shetani wenyewe, atawadanganya wengi waipokee ile chapa, na ni muhimu pia kufahamu namba 666 sio chapa ya mnyama, hilo ni jina la mnyama na sio chapa yake, chapa yake ni kitu kingine kabisa.
Ikiwa namba 666 ndio chapa yake, watu wengi pia siku hiyo wataikataa, lakini siku hiyo mamilioni ya watu wataipokea kwasababu hawataijua, Hivyo ni kuwa makini sana na hizi nyakati.
Ndugu mpendwa ujue mpaka wakati huu tuliopo unyakuo umeshakwisha kuanza,na hatua ya kwanza ya mwaliko ndiyo tuliyopo sasa ni wakati wa kutengeneza taa zetu tuhakikishe tumepokea Roho Mtakatifu na tumeitikia vizuri UJUMBE WA SAA HII ambao ni KURUDI KATIKA UKRISTO WA BIBLIA na kutoka katika mifumo ya madhehebu ambayo yamewapofusha wengi macho na yamewasababishia wafanye uasherati na yule mama wa makahaba( ufunuo 17) ambalo ni kanisa la roman katholiki. Hivyo basi kwa kuitikia hivyo inatufanya sisi kuwa bikira safi waliotayari kumlaki Bwana.
Hatua inayofuata itakuwa ni zile Ngurumo saba na watakaoweza kuzipokea ni wale bikira safi tu na ndiyo hatua tunayoisubiria sasa na iko mbioni kutokea, uamsho mkubwa unakuja mbeleni, siri hizo hazitaweza kueleweka na mtu wa kawaida asiyekuwa na Roho wa Kristo.Kisha baada ya hapo ni parapanda ya mwisho ya kwenda kumlaki Bwana mawinguni wafu watafufuliwa na sisi tutaungana nao kwenda mbinguni ndio siku hiyo mmoja atatwaliwa na mmoja ataachwa, kama Eliya alivyotwaliwa na Elisha kuachwa kama Henoko alivyotwaliwa na Nuhu kuachwa.
Ni kwasababu Eliya alikuwa na ufunuo wa ziada zaidi ya Elisha, na kadhalika Henoko alimpendeza Mungu na alikuwa ana ufunuo wa ziada zaidi ya Nuhu, hivyo wakashuhudiwa kwamba hawataonja mauti ni bibi-arusi wa siku za mwisho aliyepita hatua ya kwanza, atashuhudiwa kuwa hatakufa hata atakapomwona Bwana akija mawinguni, kuja kwa Bwana kwake hakutakuwa siri, atajua siku atakapoondoka,
1 Wathesalonike 5: 1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.
8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu”.
je! bado unafanya mzaha na haya maisha katika hichi kipindi cha hatari tunachoishi sasa cha kuja kwa BWANA YESU KRISTO kwa mara ya pili,? bado unaupenda ulimwengu unaokwenda kuisha, unaendelea kuwa mwasherati, mlevi,mwongo,mwizi, una majivuno,mlafi,kusengenya, kuvaa vimini, mawigi na mahereni, na kupaka wanja, lipstick, na fashion??.
Bado unaendelea kuwa mlevi,na mtazamaji pornography, bado unaendelea kuwa msagaji, mlawiti na mfanyaji masturbation? Bado unaendelea kuwa mtukanaji, Kuzimu! Ipo usidanganyike!Tafuta Roho Mtakatifu Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, Muda umeenda sana. Leo hii tubu kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi kwa jina la Yesu Kristo, kisha Bwana mwenyewe atakupa ahadi ya Roho Mtakatifu aliyowaahidia waitakayo.
Mungu akubariki sana.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Washirikishe na wengine habari hizi
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE
Kabla hatujaliangalia juma la 70 hebu tufahamu kwa ufupi haya majuma 70 ni yapi?
Tukisoma Danieli
9:24-27 “24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.
27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu”
Katika lugha ya biblia juma moja linawakilisha miaka 7.Hivyo majuma 70 ni sawasawa na 7*70=490
kwahiyo miaka 490 imeamuriwa kwa watu wake,sasa hawa watu wake wanaozungumziwa hapa ni wayahudi na sio watu wa mataifa. Majuma haya sabini yalianza kuhesabiwa baada tu ya danieli kupokea hayo maono.
MAJUMA 7 YA KWANZA:
Majuma 7 ya kwanza ambayo ni miaka 49 Danieli aliambiwa Yerusalemu utajengwa tena upya na njia zake kuu katika kipindi cha taabu na shida. katika hichi kipindi Hekalu la pili lilijengwa upya na kumalizika ndani ya hii miaka 49 ya kwanza baada ya kutoka uamishoni babeli.
MAJUMA 62:
Haya yalianza kuhesabiwa pale tu baada ya hekalu kumalizika kujengwa ndani ya yale majuma 7 ya kwanza. katika haya majuma 62 yaani miaka 434 ikishakwisha masihi yaani YESU KRISTO atakatiliwa mbali. Mpaka hapo majuma 69 yatakuwa yameisha. kwahiyo masihi yaani Yesu Kristo atakuwa ameshazaliwa na mwisho wa hilo juma la 69 yaani 62+7=69, atakatiliwa mbali, hili lilitokea pale alipopelekwa kalvari.AD 33
JUMA 1 LA MWISHO:
Majuma 69 yalipoisha Mungu aliacha kushughulika na wayahudi na neema ikahamia kwa mataifa kwasababu wayahudi walimkataa Masihi wao,kwahiyo kikaanza kipindi cha mataifa ambacho mpaka sasa tunaendelea nacho takribani miaka 2000 sasa. Na Neema itakaporudi Israeli ndipo juma moja la mwisho litakapoanza kuhesabiwa tena yaani miaka 7 ya mwisho, kutimiza majuma sabini. majuma haya 70 yaliamuriwa kwa watu wa Daniel yaani wayahudi na sio pamoja na watu wa mataifa. Na katikati ya hili juma la mwisho yaani miaka mitatu na nusu ya kwanza injili itapelekwa Israeli, na katika miaka mitatu na nusu ya mwisho mpinga kristo atavunja agano atakaloingia na wayahudi na kukomesha sadaka na dhabihu na ndipo ile dhiki kuu itakapoanza.
MTAZAMO AMBAO SIO SAHIHI
Kuhusu juma la mwisho la 70, watu wengi waaminio wa ujumbe wa William Branham wananukuu baadhi ya sehemu alizohubiri katika vitabu vya ujumbe, mfano katika kitabu cha “ufunuo wa mihuri saba” katika zamu ya maswali na majibu, alisema kuwa lile juma la 70 lilishaanza na BWANA YESU alishalitimiza nusu ya juma hilo alipokuwa duniani katika ile miaka mitatu na nusu ya kwanza aliyohubiri ulimwenguni.na miaka mitatu na nusu iliyobaki itatimizwa baada tu ya kanisa kunyakuliwa.
Lakini pia tukinukuu ndugu William Branhama alichofundisha katika kitabu cha “LILE JUMA LA 70 LA DANIELI” agosti 6 mwaka 1961 alisema kuwa lile juma la sabini litaanza baada tu ya utimilifu wa mataifa(yaani kanisa kwenda kwenye unyakuo) na itabaki miaka 7 ambapo miaka mitatu na nusu ya kwanza injili itapelekwa Israeli na wale manabii wawili wa ufunuo 11 na mitatu na nusu ya mwisho itakuwa ni wakati wa ile dhiki kuu baada ya mpinga kristo kulivunja lile agano atakaloingia na wayahudi.
Hapa tunaona kuwa ndugu Branham alizungumza vitu viwili tofauti vinavyoonekana kama kupingana..sasa tuchukue lipi tuache lipi?. Je! ni ujumbe unashida?? hapana ni watu wasioulewa ujumbe na kushikilia vipengele vya vitabu tuu pasipo kuomba msaada wa Roho Mtakatifu ndio wanaoufanya ujumbe usieleweke, Hata ndugu William Branham alisema mwenyewe “biblia ndio muongozo wangu” na pia alisema “hata mimi nikizungumza neno lolote kinyume na biblia usilichukue” Mambo mengi aliyoyazungumza nabii alipewa na BWANA ila sio yote aliyokuwa anazungumza yalikuwa ni “HIVI ASEMA BWANA”.. ni mara ngapi tuliona akikiri kuwa mambo mengine hafahamu, anayefahamu kila kitu na asiyekosea ni BWANA YESU KRISTO peke yake. Aleluya.!
.Ni dhahiri kabisa tunajua kuwa NENO LA MUNGU haliwezi kujichanganya Mungu aliyaruhusu haya makusudi ili kutupima sisi kama tumelielewa NENO na kama kweli tunampenda BWANA YESU, na kurejeza kila kitu kwenye NENO lake
Sasa ili kuondoa huo mkanganyiko inatupasa kurudi kwenye biblia tuangalie inasemaje na sio kuangalia vitabu vinasemaje, vitabu vinapaswa kuturudisha kwenye NENO na sio NENO liturudishe kwenye vitabu. Ni jukumu letu sisi kuhakiki kila neno linalosemwa na mtu yeyote kwa NENO na nabii mwenyewe ndivyo alivyotufundisha wote. Nabii hakumvumilia wala kumuonea haya mtu yeyote anayetoa mapokeo yake nje ya neno.
Biblia inasema danieli 9:26 ” Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji” Hapa tunaona dhahiri Masihi atakatiliwa mbali mara baada ya majuma 62 kukamilika, kukamilisha majuma 69 yaani (7+62=69) kuisha, na sio baada ya majuma 62.5 yaani(7+62.5=69.5).unaona biblia inasema baada ya yale majuma 69 kuisha ndipo masihi atakapokatiliwa mbali.
Na huyo mkuu atakayekuja baada ya Masihi kukatiliwa mbali atakuwa ni mpinga kristo naye atafanya agano na watu wengi katika juma moja yaani miaka 7. na nusu ya juma hilo atalivunja hilo agano na kuikomesha sadaka na dhabihu, kumbuka Masihi na mkuu atakayekuja ni watu wawili tofauti.chukizo la uharibifu ni mpinga kristo atakapoingia lile agano na israeli.
Tukisema masihi ni sawa na mkuu wa watu atakayekuja tutakuwa hatujaielewa biblia vizuri kwasababu, maandiko yanasema watu wa huyo mkuu atakayekuja ndio watakoutekeza mji, na tunafahamu katika historia warumi ndio waliouteketeza mji 70AD kutimiza ule unabii Bwana Yesu aliousema mtakapouna mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi mjue uharibifu wake umefika.(luka 21:20).
Hivyo sio watu wa Yesu Kristo(yaani wayahudi) walioteketeza mji bali ni watu(warumi), wa yule “mkuu atakayekuja” yaani mpinga kristo. ambaye kwa kipindi hicho alikuwa bado hajaja lakini baadaye atakuja na kuingia agano na wayahudi katika lile juma moja la mwisho lililobaki.
Kwahiyo kulingana na NENO juma la sabini litaanza baada tu ya injili kumalizika kwa mataifa na ndivyo hata nabii alivyohubiri katika ujumbe aliofundisha agosti 6 mwaka 1961″LILE JUMA LA SABINI LA DANIELI”. Hivyo mtazamo unaosema kuwa Bwana Yesu alishakamilisha nusu ya juma akiwa hapa duniani sio sahihi.
2 petro 1:10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.”
Mungu akubariki!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
MANABII WALISEMA “NENO LA MUNGU LIKANIJIA” ..MAANA YA HILI NENO NI NINI?.
NINI MAANA YA HILI ANDIKO “USHUHUDA WA YESU NDIO ROHO YA UNABII” (UFUNUO 19:10)?
Mungu amekuwa akizungumza na wanadamu kwa njia tofauti tofauti na kwa wakati tofauti tofauti,
Katika historia ya kanisa ujumbe Mungu alioutoa kwa kanisa la kwanza sio sawa na ujumbe alioutoa kwa kanisa la pili..na wala sio sawa na ujumbe alioutoa kwa kanisa la mwisho. Mungu anaongea kulingana na wakati, ni muhimu sana kulitambua hilo. Kwa mfano wakati ulipotimia wa Mungu kumleta mwana wake katika agano jipya watu wengi ikiwemo waalimu wa torati na mafarisayo hawakuweza kuiamini injili yake kwasababu hawakuuelewa ujumbe wa saa yao. Walishikilia torati ya Musa lakini walisahau kuwa Musa alisema ”atakuja nabii mwingine kama mimi mwaminini yeye”. Lakini waliukataa ujumbe wa Yesu Kristo wakabaki kushikilia mapokeo yao.
Katika hichi kipindi cha siku za mwisho tunaona kuwa yote yaliyotabiriwa na BWANA YESU KRISTO yanaenda kutimia, Licha ya kwamba Bwana kumtuma mjumbe wake(William Branham) kutuamsha kujiweka tayari kwa ajili ya kumlaki Bwana mawinguni tunaona pia Mungu amekuwa akizungumza na sisi kwa kupitia maumbile ya ulimwengu (nature) kutufundisha na kututhibitishia kuwa nyakati hizi tunazoishi ni za mwisho.
Kwa mfano maendeleo makubwa ya teknolojia tunayoyaona sasa hivi yana hubiri dhahiri injili ya kuja kwa BWANA YESU KRISTO. Baadhi ya hayo ni:
Leo hii sio jambo la kushangaza kuona mtu mmoja anawasiliana na mwingine aliye taifa la mbali maelfu ya maili. Kwa sekunde tu!, watu wanaweza wakaonana na kuzungumza kwa mfumo wa video (yaani video chat).Watu wanaweza kupelekeana taarifa na habari kwa mfumo wa televisheni ndani ya dakika chache tu na dunia nzima ikapata habari ya mambo yanayoendelea ulimwenguni, teknolojia imefanikiwa kuifanya dunia kuwa kama kijiji.
Mungu kayaruhusu haya yote kutokea kwa kasi kubwa katika karne hii ya 20 na ya 21 ili kutufundisha na sisi watoto wa Mungu ya kuwa katika kipindi chetu cha mwisho mawasiliano yetu na Mungu yanapaswa yawe makubwa kuliko vipindi vyote vya nyuma vilivyotutangulia, tunajua kwa dunia ya sasa kuwa na chombo cha mawasiliano (kama simu) ni muhimu kwa ajili ya kujuzana habari sana sana kwa matukio ya gafla, pasipo hicho hauwezi kuendana na jamii/maisha ya sasa vivyo hivyo na sisi kama wana wa Mungu tumefika wakati ambao kila mtu anapaswa awe na Roho Mtakatifu kama chombo chake cha mawasiliano katika hichi kipindi cha uovu na mafundisho ya uwongo kuenea kila mahali.
Leo hii mtu anaweza kutafuta ukweli wa jambo fulani kwa kutumia mtandao (internet) na sisi pia kama wana wa Mungu tunahitaji Roho Mtakatifu kutufundisha na kutuongoza katika kweli yote, na kama vile zamani ujumbe ni lazima upelekwe na mtu fulani(mjumbe) lakini sasahivi mjumbe haitajiki tena kwasababu kuna simu ambazo zimerahisisha mambo kupata habari kwa haraka vivyo hivyo katika wakati wetu tunaoishi sasa hivi Mungu alishawapeleka wajumbe wengi sasa tupo katika hatua ya sisi kuwasiliana na Mungu moja kwa moja mjumbe haitajiki tena kama kuna Roho Mtakatifu.
Yeremia 31:33 ” Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.
Tumeona hapa katika hizi siku za mwisho ni muhimu kuwa na Roho Mtakatifu kukufundisha ndani yako binafsi na kukuongoza katika kweli yote, maana saa tunayoishi ni ya hatari manabii wa uwongo waliotabiriwa na mafundisho mengi ya uwongo yameenea kila mahali hichi ndicho kile kipindi Bwana alichosema.
Mathayo 24:23-26 “Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki”.
Ni wakati wa kutafuta uhusiano wako binafsi na Mungu, leo hii ukitaka kumwita mtu kwa haraka mahali fulani mbali ni lazima umpigie simu, kama hana simu basi hawezi kujua kama unamhitaji kwa wakati huo, vivyo hivyo usipokuwa na Roho wa Mungu hutaweza kufahamu wakati utakapoitwa haraka kwenda kumlaki Bwana mawinguni, watakaoenda ni wale tu wenye mahusiano na mawasiliano mazuri na Mungu.
Kwa vizazi vya nyuma suala la mtu kupaa hewani lilikuwa ni jambo lisilowezekana lakini sasa mtu kusafiri kwenda kwenye magimba ya nje ya dunia limekuwa ni jambo la kawaida kwa kutumia roketi.
Hii inatufundisha kuwa kama sayansi imefanikiwa kufanya hivi, na sisi wakristo tunaomngojea Bwana wakati wetu wa kupaa mawinguni umekaribia, kama vile wanasayansi walivyokuwa wakitafiti kwa miaka na miaka huko nyuma ni jinsi gani wangeweza kuruka juu hewani na kufika kwenye magimba mengine nje ya dunia na kufanikiwa katika kizazi hichi baada ya kutaabika kwa muda mrefu, inatufundisha sisi wana wa Mungu kuwa ndege yetu ya kwenda mbinguni imeshaandaliwa na iko tayari katika hichi kizazi chetu baada ya kusubiria kwa muda mrefu, na kama vile mtu akitaka kusafiri kwa ndege ni lazima awe na tiketi naye amekata mapema(booking).
Vivyo hivyo na sisi tunapaswa sasa hivi kuwa na Roho Mtakatifu kama tiketi yetu ya kuingia katika ndege hiyo ya mbinguni na tunapaswa tu-book mapema kabla ya ndege kuondoka ili tuwe na uhakika wa safari yetu kabla nafasi hazijajaa.
Jiulize ewe ndugu..simu yako ni ipi?? kama hapo ulipo hukosi kuwa na simu mfukoni na unajua kabisa katika dunia ya sasa usipokuwa na simu hauwezi kuendana na jamii inayokuzunguka lakini hutaki kuwa na simu ya roho ambayo ni Roho Mtakatifu unatazamia nini hapo??..
Jibu ni dhahiri kwamba unategemea siku ile ikujie gafla kama mtego unasavyo..wakati wengine wakiwa na Roho wa Mungu akizungumza nao katika hichi hichi kizazi unachoishi wewe wakijiweka tayari kuchukuliwa juu wewe utakuwa huna habari…habari itakufikia baadae wakati wakristo wa kweli wameshaondoka kwasababu huna simu yako mwenyewe (Roho Mtakatifu) ingekupasa upigiwe simu ya kuondoka lakini kwasababu huna Roho Mtakatifu utasubiria uletewe habari kwasababu hiyo basi itakupasa uingie katika ile dhiki kuu..mimi binafsi nisingependa kubaki kwenye dhiki kuu sijui wewe??
Kumbuka ndege ipo tayari na ina nafasi chache tu (limited number of seats) na kumbuka ndege sio gari uende saa hiyo hiyo na kupanda uondoke, ina process. Hivyo inahitaji booking mapema, wanashauri walau ukate tiketi wiki moja au mbili kabla kwa uhakika wa safari yako, na katika siku ya safari unapaswa ufike airport masaa 3 kabla kwa ajili ya hatua ya makaguzi (check-in process) usipozingatia hivi vigezo huwezi kusafiri. Vivyo hivyo katika safari yetu ya kwenda mbinguni ndege yetu ipo tayari hatua tuliyopo sasa ni ya booking kwa ajili ya kupata nafasi katika sehemu ya ufalme.
Na hatua hii inakaribia kumalizika unatakiwa uwe na tiketi yako mkononi (Roho Mtakatifu) nafasi zinaenda kujaa, na zikishajaa hatua itakayofuatia ya makaguzi(check- in). Ni kwa wale tu walio na tiketi zao wengine wasio na tiketi haitawahusu, na hatua zote hizi zinafanyika tukiwa hapahapa duniani. kabla ya kwenda kupanda ndege yetu ya kwenda mbinguni.
Tukumbuke Mungu karuhusu haya mabadiliko makubwa ya teknolojia yatokee katika kizazi chetu. Ili sisi tujifunze, tusipojifunza yatakuja kutuhukumu katika siku ile ya Bwana..Je! hauoni ni wakati gani huu wa hatari tunaouishi??..Na bado unaendelea kuupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu. unakuwa mwasherati wakati Mungu anasema “hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu”.
Unatazamiaje Roho wa Mungu aje juu yako, una kuwa mlevi, vuguvugu haueleweki wewe ni mkristo au ni nani, una kuwa msengenyaji, unajichanganya na watu waovu wa ulimwengu huu hao ndio rafiki zako wakati biblia inasema ‘msifungwe nira pamoja na wasio amini”.
Una kaa na watu wenye mizaha, maneno machafu yanatoka midomoni mwako na bado unajiita mkristo, unavaa mavazi yasiyo na heshima na kufanana na wanawake wa ulimwengu huu.
Huna muda wa kusoma neno na kusali na kuomba lakini unapata muda mwingi wa kuchati kwenye mitandao katika vitu visivyokuwa na maana, shetani amekupofusha akikudanganya kwamba wewe ni bibi arusi wa Kristo na kwamba yote ni sawa.
Lakini jua jambo moja katika kizazi hichi hichi unachoishi wewe kuna wakristo kweli kweli ulimwenguni kote waliojazwa Roho Mtakatifu wanaushinda ulimwengu katika mazingira kama hayo hayo yakwako unayoishi wewe na watatuhukumu maana biblia inasema ‘watakatifu ndio watakaoouhukumu ulimwengu’.
Umehubiriwa injili kila siku unaisikia bado unaishi maisha unayoishi sasa. Kristo alisema ”itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako?” mambo ya ulimwengu huu yanakusonga mpaka unashindwa kuwa mkristo kama unavyopaswa uwe,
Tubu! badilika muda umeenda kuliko tunavyodhani mambo yote yameshakuwa tayari. Huu sio wakati tena wa sisi kumngojea Bwana bali Bwana ndiye anayetungojea sisi.
TAFUTA ROHO MTAKATIFU MAANA HUO NDIO MUHURI WA MUNGU!
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
JE UMEYABATILISHA MAMBO YA KITOTO
BWANA ALIPOSEMA KUWA YEYE NI “MUNGU WA MIUNGU” ALIKUWA NA MAANA GANI?..JE! YEYE NI MUNGU WA SANAMU?
JE! WATAKAOENDA MBINGUNI NI WENGI?
1Yohana 3:1 “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye”
Katika maisha ya kila mmoja wetu, kuna ushuhuda ambao Mungu ameuandika.Bwana ameruhusu kila mtu apitie hatua mbili kuu muhimu maishani mwake nazo ni KUWA MTOTO, NA KUWA MZAZI ( BABA/MAMA) Mungu hakuona vema mtu atokee tu duniani akiwa mtu mzima bali aliruhusu kwa makusudi kabisa mtu apitie hatua zote hizi mbili,ya kwanza awe mtoto, na kisha awe baba/mama,
Ili kusudi kwamba Mungu atakapojifunua kwetu kama Baba tuweze kumuelewa, kwa namna gani Baba ana nafasi yake katika maisha yetu kwakuwa tumeshayapitia hayo maishani ya kuwa na baba wa mwilini na kufahamu vizuri nafasi yake kwetu, ndio maana akasema ni pendo la namna gani alilotupa baba sisi kuitwa wana wa Mungu, kwasababu malaika hawajafananishwa na wana wa Mungu, kwakuwa hawajapitia njia tunazozipitia sisi wanadamu kama vile kuzaliwa na kuwa baba.
Wao waliumbwa tu katika hali zao walizopo sasa Mtume Paulo alieleza wazi kabisa katika
Waebrania 1:5 “Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?”
kwahiyo tunaona hapa malaika hawakuitwa wana wa Mungu, kwasababu hawajaumbiwa ile hali ya kuwa wana, wala kupitishwa katika maisha ya kuwa wana, biblia inasema wao ni roho zitumikazo ( waebrania 1:14 ” Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”)
TABIA YA MWANA:
Kama sisi tumepewa neema hii kubwa ya kuitwa wana wa Mungu inatupasa sisi tufahamu jinsi Mwana anavyopaswa kuwa kwa Baba yake ili ampendeze Baba yake, inajulikana kuwa tabia ya mtoto yoyote mdogo hafikirii atakula nini wala atakunywa nini,wala atavaa nini, wala atalala wapi,wala hafikirii kesho itakuwaje, wala hafikirii kuhusu afya yake.
Hizi ni tabia za watoto wote ikiwemo hata mimi na wewe tulivyokuwa watoto wadogo. Ujasiri huo wa maisha anao kwasababu anajua Baba yake yupo na ndiyo yeye anajukumu la kumlisha, kumvisha, kumnywesha,kuiangalia afya yake na kumlinda..mtoto haitaji kumweleza baba yake kuwa anaumwa ni jukumu la baba yake yeye kufahamu, mtoto hawezi kwenda kumsaidia baba yake kuleta chakula nyumbani hiyo haimuhusu mtoto kwasababu mtoto hayatambui hata hayo, na baba hachukizwi kumuona mtoto kuwa hivyo kwasababu anajua huyu ni mtoto tu, hawezi kufanya lolote.
Mtoto siku zote anaujasiri mkubwa sana kwa baba yake, kiasi cha kwamba anaona hakuna mtu mwingine yeyote anaweza akawa mkubwa kuliko baba yake, mtoto hana tabia ya kuweka kinyongo akiadhibiwa na baba yake baada ya muda mfupi ameshasahau, mtoto siku zote huwa anajishughulisha na vitu vidogo vidogo na huwa hatafuti ukubwa na ana tabia ya kupenda kukaa nyumbani na kuamini chochote atakachoambiwa na mzazi wake.
Na sisi kama wazazi tunachukuliana na watoto wetu na kuwapenda sana wakiwa katika hali kama hizo, tunawapenda pale tunapowaona watoto wetu wanavyojitoa kikamilifu kwetu,watiifu na wasio na kiburi, wanaojiachia kwetu..sidhani kama kuna mzazi yeyote anaweza akamchukia mtoto wake akiwa katika hali hiyo kwasababu anajua huyo ni mtoto tu hajiwezi na anahitaji uangalizi wote, na hakuna mzazi asiyemuhurumia mtoto wake, akimwona mtoto wake hana chakula yuko radhi alale njaa yeye ili mtoto wake ashibe, akimwona mtoto wake ana dalili tu ya kuumwa anamuhurumia na kumpeleka hospitali haraka sana. JE! SI ZAIDI KWA BABA YETU ALIYE MBINGUNI??
kumbuka Mungu alitupitisha makusudi katika hatua hizi za kuwa mtoto au mzazi ili tumuelewe Mungu kama Baba yetu ana nafasi gani na umuhimu gani kwetu.
Kama Baba zetu wa mwilini wanaweza kututendea mema yote hayo, kutuangalia na kutuhudumia maisha yetu bure, kutuvisha,kutulisha, kutunywesha, kutupa malazi na kutupa afya pasipo kumlipa chochote si zaidi sana kwa Baba yetu aliye mbinguni??
Kuna mafundisho mengi ya uongo ya shetani na yanafundishwa hata na baadhi ya wanaojiita wahubiri wakisema Mungu wetu ni baba wa rohoni na kwamba yeye anatuhudumia tu kwa mambo ya rohoni na kwamba ya mwilini inatupasa tujihudumie wenyewe.
Lakini biblia inasema
waefeso 3:14-15 “Kwa hiyo nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa”
Unaona hapo ni ubaba wote unaozungumziwa wa mbinguni na wa duniani sio tu wa mbinguni bali hata na wa duniani pia. Kwa namna ile ile uliyokuwa una mtegemea baba yako hapa duniani akulishe, akunyweshe, akuvishe, na akulinde na kukupa afya vivyo hivyo inakupasa umtegemee Mungu ambaye ni Baba yako hapa duniani kwa mahitaji yako yote ya mwilini na ya rohoni kwa kuwa ni baba wa rohoni pia.
Yesu Kristo alisema katika
Mathayo 6:25-34 ” Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”
Neno hili shetani ameligeuza na kutoa tafsiri nyingi zinazopingana na maana ya maneno yaliyopo hapo juu.Maneno hayo Bwana Yesu aliyoyazungumza yana maana kama yalivyoandikwa, shetani anafahamu kuwa hii ni SIRI inayobeba uhusiano mkubwa kati ya Baba na Mwana, BWANA YESU anasema msisumbukie maisha yenu mle nini au mnywe nini kwamba baba yetu anajua kuwa hayo yote tunayahitaji, kama vile baba zetu wa mwilini tulivyokuwa watoto walikuwa wanajua yote kwamba tunahitaji kula na kunywa je! si zaidi kwa Baba yetu aliye mbinguni?
Embu jaribu kufikiri juu ya hilo ndugu kwa undani. Pamoja na mambo mengi Bwana Yesu Kristo aliyosema tujifunze kwayo, alisema pia tujifunze kwa kunguru, n.k alisema tutazame kunguru, tujifunze jinsi wanavyokula, na kunywa, na kuishi hawapandi, hawavuni, hawana bima, hawana maghala lakini kila siku wana kula, kunguru anauwezo wa kuishi hadi miaka 80 na hajawahi kumeza kidonge katika maisha yake yote.
Na maua ya mashambani hayafanyi ”KAZI” lakini yanatoa harufu nzuri na rangi nzuri na kuuzwa kwa bei ghali kumbuka hayasogei hata inchi moja..Mungu ambaye ni baba yetu anasema “sisi si zaidi kuliko hao??”
Mathayo 18:3 ” Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema, Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni?
Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.”
Hapa tunaona Kristo anazungumzia aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni ni yule atakayejinyenyekeza kuwa kama mtoto mdogo. Unyenyekevu uliozungumziwa hapa ni maisha ya mtoto kwa baba yake, ni tabia ya mtoto kwa baba yake na sio kumpigia mtu magoti au kuonyesha utiifu fulani hapana. Kwetu sisi kujinyenyekeza kama watoto ni kujiweka/kujiachia kama watoto kwa baba yetu aliye mbinguni, na kuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni ni kuweza kuyashika na kuyaishi hayo maneno yote BWANA YESU aliyoyazungumza hapo juu kwenye mathayo 6:25-34.(huko ndio kujinyenyekeza kama mtoto) lakini kuwa na upako, au kuwa muhubiri mkubwa, au kuwavuta watu kwa Kristo au kuwa mchungaji au kuona maono au kuomba sana, au kufunga sana, au kwenda kanisani sana hakukufanyi wewe kuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. unapaswa uwe mtoto kwa Mungu(Baba wa mbinguni) kama vile mtoto alivyo kwa baba yake wa duniani.Hivyo ndivyo BWANA YESU KRISTO alivyokuwa hapa duniani kujiachia kwa baba yake wa mbinguni.
Uthibitisho mmoja wapo kuwa wewe umempokea Roho Mtakatifu ni wewe KUFANYIKA KUWA MWANA WA MUNGU
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”
na pia katika Warumi..
warumi 8 :14-16 inasema “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;”
Kwa hiyo uthibitisho kuwa wewe ni mtoto wa Mungu, ni Mungu kwako kuwa kila kitu na unamwona katika maisha yako akikuhudumia kwa mahitaji yote ya mwilini na ya rohoni( kumbuka! sio ya rohoni tu bali hata ya mwilini) hautasumbukia maisha kwasababu unaye baba, wewe sio yatima, baba yako atakuvisha, atakulisha, atakunywesha sikwambii wewe ufanye kazi akunyweshe hapana! ana njia zake mwenyewe, unaweza usifanye kazi kabisa wala kujishughulisha na jambo lolote na akakulisha na kukuvisha, unaweza usiwe na fedha hata kidogo na bado akakuvisha, akakulisha na akakuvisha, njia zake sio njia zetu, unaweza usiende hospitali kabisa na bado akakupa afya,
BWANA YESU alisema Baba yetu anajua kabisa kuwa tunahitaji haya yote yaani tule, tunywe, tuvae, tulale, tuwe na afya, kasema mwenyewe kama yeye anaweza kuwafanyia hivyo ndege wa angani na maua ya kondeni je! sisi sio zaidi?? usimruhusu shetani autangue uhusiano wako wewe na Baba yako aliye mbinguni kwa kumwekea Mungu vikwazo na mipaka kwamba yeye hawezi kukuhudumia mpaka ufanye kazi..sipo kinyume na kazi, unaweza ukafanya kazi lakini Mungu hatumii hivyo tu kukuhudumia wewe…
Je! mtoto anajihangaikia mwenyewe?? ..Mungu alitupitisha huko ili tujue nafasi ya baba kwa mtoto ni ipi?.. Yeye ni Mungu tu na ni baba yako, kama wewe ulivyokuwa mtoto ulikuwa huwezi kuzichunguza njia za baba yako lakini ulikuwa una kula, ulikuwa hufikirii wala kuyasumbukia ya kesho wewe..kwanini leo kesho ikufikirishe sana mpaka ukakosa hamu ya kuishi?.
BWANA YESU alisema msisumbukie ya kesho, kwa kuwa ya kesho itajisumbukia yenyewe..huko ndio kufanyika kuwa mwana.
Sasa sikufundishi kuwa mvivu…Lakini kuwa kama Mwana…Weka mipango yako, ya leo na ya kesho, pia fanya shughuli zako kwa bidii kama kawaida, lakini usisahau kuwa unaye Baba mbinguni, hata hizo shughuli zako zikikwama, hatashindwa kukulisha, wala kukuvisha wala kukutunza… Baba anamfurahia mtoto mwenye malengo yake na mipango yake aliyojiwekea, lakini hafurahii kuona mtoto wake ajihisi kama vile hana mzazi ambaye siku mambo yake yakiharibika atakosa hifadhi..
Petro alipewa ufunuo mkubwa kuwa YESU KRISTO ni nani! ambao Bwana alimwambia Petro juu ya ufunuo huo atalijenga kanisa lake na milango ya kuzimu haitaiweza
Mathayo 16:18 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?
Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.
Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia,
Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”
Ufunuo huu Petro aliopewa sio wa Yesu Kristo kuwa ni Mungu, wala Yesu Kristo kama Mwokozi bali alipewa ufunuo kuwa yeye ndiye MWANA WA MUNGU aliye hai.
Petro kwa kuona jinsi Kristo alivyokuwa anamtegemea baba yake kwa kila kitu, na jinsi baba yake alivyokuwa ana muhudumia kwa mambo yote, akatambua kuwa ule uhusiano ulikuwa ni wa kipekee kama vile wa BABA NA MTOTO WAKE. Hakukuwahi kutokea mtu yeyote katika torati au huko nyuma ambaye alishawahi kuwa na mahusiano ya kama baba na mtoto kwa Mungu, hiyo ilionekana kwa Yesu Kristo tu na ndio maana Petro alipewa ufunuo huo na Mungu jambo ambalo lilifichwa hata kwa baadhi ya mitume.
Sauti ilisikika kutoka mbinguni Yohana alipokuwa akibatiza na Yohana pekee yake ndiye aliyeusikia huo ufunuo
Mathayo 3:17 “na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye”.
Hapa Kristo hakushuhudiwa kama yeye ni Mungu au mfalme(ingawa Yesu Kristo alikuwa ni Mungu na Mwokozi) bali alishuhudiwa yeye kuwa ni Mwana wa Mungu .
Chunguza tena maisha yako je! wewe ni kweli mwana halali au mwana haramu. mwana halali anaonekana kwa maisha yake anayoyaishi na uhusiano wake yeye na baba yake vilevile na mwana haramu anaonekana kwa maisha yake jinsi alivyo na mambo yake mwenyewe, hapendi kujishughulisha na mambo ya baba yake, asiyeweza kuadhibiwa anapokosea(kurudiwa), hamtegemei baba yake,
Je! Umepokea Roho Mtakatifu?? kama umepokea Roho wa Mungu atakushuhudia katika maisha yako kuwa wewe ni mtoto wa Mungu kwasababu maandiko ndivyo yanavyosema
Warumi 8 :14-16 inasema “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;“
MUNGU AKUBARIKI!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
NIFANYAJE ILI NI NIJUE KUWA UAMUZI NINAOUFANYA NI MAPENZI YA MUNGU?
NI KOSA GANI DAUDI ALILOLIFANYA KATIKA KUWAHESABU WATU?
Wito wa Mungu kwa mtu unakuja kwa namna tofauti tofauti kulingana na kusudi la Mungu juu ya maisha yake, na kazi mtu atakayokuja kuifanya baadaye katika kazi ya huduma. Huduma ya mtu inategemea na jinsi mtu alivyoitwa.
UTUMWA/UHURU
1wakorintho 7:20-24″ Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa.
21 Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.
22 Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.
23 Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu.
24 Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo. “
Kuna watu ambao wameitwa katika hali ya utumwa lakini sio utumwa ambao utaathiri imani yake kwa Mungu yaani utumwa wa kuwa chini ya mtu fulani mfano kujishughulisha na kazi za kidunia kama kuajiriwa ambazo zitahusisha muda mwingi wa huyo mtu kuitumikia kazi yake, hivyo basi kwa kuwa amekuwa mtumwa wa mtu mwingine basi mtu huyo amefanyika kuwa huru kwa Mungu (tunazungumzia katika kazi ya utumishi) kulingana na biblia, yaani mtu huyo hawezi kutumika kwa muda wote katika kazi ya Mungu (au kuwa mnadhiri wa Mungu) biblia inasema mtu hawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja
Mathayo 6:24, ” Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. “…
Kwahiyo wakristo kama hawa hawawezi wakawa watumwa wa Kristo lakini Mungu atawabariki katika huduma nyingine za mwilini kama za utoaji n.k katika utakatifu wote (ukisoma 2wakorintho 9:11″mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; “,..pia soma 1Timotheo 6:17-19),
Na pia watu hawa wanao uwezo wa kuhudumu katika kazi nyingine za kanisa kwa jinsi Mungu atakavyowajalia kwa karama zote za rohoni kama miujiza,uponyaji, neno la maarifa,unabii kunena kwa lugha,au wakawa mashemasi n.k lakini zile huduma tano kuu kama tukisoma katika Waefeso 4:11-16 inasema;
” Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; “
hizi huduma kuu tano ni ofisi za Mungu, kwahiyo zinahitaji muda wote wa uangalizi wa watakatifu, na Mungu anazitumia kwa jinsi apendavyo yeye, Hawa wameitwa katika hali ya utumwa kwa Mungu kwa hiyo ni lazima wawe huru na mambo mengine yote ya ulimwengu mfano shughuli za ulimwengu huu zinazoweza kumtinga mtu na kuathiri kazi ya huduma.
Na hawa hawatakiwi kujiingiza katika shughuli yoyote ambayo itawachukulia muda wao wote mbali na Mungu, hawa ni watiwa mafuta wa Bwana kazi yao ni moja tu kuifanya kazi ya Mungu na sio kitu kingine. Mungu pekee ndiye anayejua jinsi ya kuwalisha na kuwavisha na ndio maana mahali pengine Mungu ameruhusu kwasehemu wapate fungu lao kutoka katika vitu vya madhabahu na pia Mungu ana njia nyingine mbali na hizo za kuwahudumia hao watu, kama vile hakuna mwajiri yeyote asiyemlipa mfanyakazi wake, vivyo hivyo na kwa Mungu hatazidi sana kuwajali watendakazi wake?
1Wakorintho 9:12-14 “Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili. “.
Kwa ufupi neno hili Bwana aliwaambia mapema wanafunzi wake kuwa mtu hawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, kwamfano mtu hawezi kuajiriwa katika ofisi mbili tofauti na zote mbili akatumika asubuhi mpaka jioni, lazima moja ya hizo iwe ni ya part time tu! au aamue kufanya moja na aache nyingine, ni dhahiri kabisa inajulikana hivi kuwa hakuna manager yeyote anayeweza kumuajiri mtu anayetumika na shirika lingine full time mbali na lake, na vivyo hivyo kwa Mungu.
Kwahiyo biblia inasema 1 wakorintho7:20-23 “Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia. “.
Kwahiyo kama umeitwa katika hali ya utumwa usione ni vibaya kuwa mwaminifu na muhubiri Kristo katika hali uliyoko, tenda wema,ukristo wako ujulikane na watu wote wanaokuzunguka ili watazamapo mwenendo wako wengi waokolewe katika wewe,biblia inazungumzia
1 Timotheo 6:1-2,waefeso 6:5-8,” Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;
6 wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;
7 kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;
8 mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru. “
kumbuka maneno haya Paulo alikuwa anawaandikia wakristo na sio watu wa mataifa.
pia Mungu anaweza akakutumia kuhudumu katika kanisa kwa karama ya Roho aliyoiweka ndani yako kwamfano uimbaji, utoaji,ushemasi na kwa namna nyingine yeyote ambayo unaweza ukaona unawito wa kufanya katika kanisa lakini sio huduma yoyote ya uongozi katika kanisa kama kuwa mchungaji, mwalimu, nabii, muinjilisti,mitume hizi hazijishikishi na mambo mengine yoyote nje na kazi za kanisa. Ni ofisi za Mungu katika kanisa. kwahiyo kama ukitaka kuwa na mojawapo ya huduma hizo ni lazima ujitoe kikamilifu, ni lazima uachane na moja ushikamane na lingine, hauwezi ukatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
WITO WA MTU BINAFSI
Kuoa/ kutokuoa
Mungu pia anaweza akamwita mtu katika hali ya kuoa au kutokuoa, wahubiri wengi wanafundisha kuwa ni lazima watu wote waoe au kuolewa, lakini wanasahau pia kufundisha kuwa Mungu ana wito tofauti tofauti kwa watu tofauti tofauti, wako walioitwa waoe na pia wapo walioitwa kutokuoa au kutokuolewa. BWANA YESU KRISTO alisema
Mathayo 19:10-12.”Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa. Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;
tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee. “
..Katika agano la kale matowashi walikuwa ni watu walioasiwa kwa ajili ya kazi ya Mungu (aidha kazaliwa hivyo,au kaasiwa na watu wake au kaamua kujiasi mwenyewe kwa ajili ya Mungu) lakini katika agano jipya jambo hili linaweza likawa kwa mtu yeyote aliyeasiwa au ambaye hajaasiwa lakini anaweza akayaweza mapenzi yake( kujizuia na tamaa)..hivyo mtu wa namna hii haoi wala haolewi kajiweka mwenyewe wakfu au mnadhiri kwa Bwana..mfano wa watu hawa tunaye Bwana wetu YESU KRISTO, Mtume Paulo,Yohana mbatizaji n.k
Hapa tunaona Bwana Yesu alisema sio wote wawezao kulipokea hilo neno la kutokuoa ila wale tu waliojaliwa, Bwana alisema ‘awezaye kulipokea neno hilo na alipokee’
Pia Mtume Paulo alisema katika..
1 wakorintho 7:1,8,32-35(1 Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke……
8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo…..
32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.
34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine. )
.Hivyo tunaona Mtume Paulo anashauri kuwa kutokuoa au kutokuolewa ni vizuri zaidi kwa sababu mtu kama huyo atajishughulisha zaidi na mambo ya Mungu zaidi ya Mtu aliyeoa au kuolewa.Lakini pia sio vibaya au dhambi mtu kuoa au kuolewa, wala mtu hapaswi kulazimishwa kutokuoa wala kutokuolewa, Mtume Paulo alisema kuwa kila mtu ana karama yake jinsi alivyoitwa, lakini tunaona jinsi vile Bwana YESU KRISTO, Mtume Paulo,Eliya,Yohana Mbatizaji hawakuoa na tunaona matunda makubwa waliyotoa ya kazi zao, Mtume Paulo hakupata nafasi ya kutembea na Kristo kama Mitume wengine lakini yeye ndiye aliyefanya kazi kubwa kushinda mitume wengine wote.
Kwahiyo ndugu kama ukiwa na wito ndani yako wa kutokuoa au kutokuolewa, na unajiona kupata amani kuhusu jambo hilo, na unaweza ukajizuia, na unatamani kumtumikia Mungu katika hali hiyo usimzimishe Roho,hiyo ni kazi ya Roho wa Mungu ndani yako kuwa mwaminifu tu, inawezekana hiyo karama Mungu ameiweka ndani yako. Na hii ni kama tu unaona amani na unaona uko huru zaidi kuliko kuoa/kuolewa sasa huo ndio wakati wa kupeleka mapenzi yako yote kwa Mungu (Bwana YESU awe mpenzi wako) naye Bwana siku zote ni mwaminifu atakutunza. Kumbuka hiyo inakuwa kama nadhiri kwahiyo usiwe mtu wa kusitasita leo huku kesho kule kuwa na uhakika na maamuzi unayoyafanya naye Bwana atazidi kukuimarisha kidogo kidogo nawe utakuwa imara katika jambo hilo. Wito wa namna hii ni kwa mtu binafsi na ni kama moja ya nadhiri ya hiari mbele za Bwana, na ina thawabu kubwa sana,
Isaya 56:3-5 “Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu.
4 Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu;
5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. “
Hapa tunaona Bwana amewaahidia watu wa namna hii(matowashi) kuwa atawapa jina lililo jema lidumulo milele,zaidi ya kuwa na wana na binti.
kumbuka maaskofu(wachungaji) na mashemasi kama wakitaka kuwa na wake wanapaswa wawe na mke mmoja kulingana na kazi ya huduma walizoitiwa za uangalizi wa makanisa, hivyo ni lazima waonyeshe vielelezo kwanza kwenye familia zao, kisha ndio waje kulichunga kanisa. lakini pia kama wanaweza kujizuia wasioe ni vizuri zaidi kwa ajili ya kazi ya Bwana.
Kwahiyo ndugu mkristo ukitaka kuwa na huduma yeyote katika ofisi kuu za Mungu kama vile uchungaji, uinjilisti, ualimu, utume, na unabii fahamu tu ni lazima ujitoe kikamilifu na ndio maana Bwana Yesu alisema hauwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja..tusijidanganye kama hatuwezi kuwatumikia mabosi wawili wa kiduniani kwa wakati mmoja, si zaidi Mungu wetu aliye mkuu kushinda Bosi yeyote duniani na aliye na ofisi kuu kushinda ofisi yoyote duniani na bado tunataka kuigeuza kazi yake kuwa part time,
Hauwezi ukawa ni mchungaji — na bado ukawa mbunge
Hauwezi ukawa ni mchungaji—na bado ukawa mwana siasa
Hauwezi ukawa ni mchungaji—na bado ukawa mwajiriwa wa full time kutumikia shirika fulani
Hauwezi ukawa ni mchungaji—na bado unajihusisha na harambee za kijamii
Hauwezi ukawa ni mchungaji—na bado ukawa mtu wa kupenda pesa
Kuwa mtumwa wa Kristo ni kuwa huru na shughuli za ulimwengu na kuwa mtumwa wa shughuli za ulimwengu ni kuwa huru wa Kristo..“.Lakini Paulo alisema kama unaweza ukawa huru ni afadhali kuutumia huo uhuru, TUMENUNULIWA KWA THAMANI TUSIWE WATUMWA WA WANADAMU”.
Jiangalie ni utumishi wa namna gani wewe uliopo?..
Mungu akubariki!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto”?
Mwinjilisti mmoja alisema kuwa kuipokea chapa ya mnyama/Alama ya Mnyama ni kuukataa muhuri wa Mungu ambao ni Roho Mtakatifu, alisema kuna pande mbili tu, upande wa Mungu na upande wa shetani, hivyo ukikosa kuwa na Roho wa Mungu, maana yake ni una roho ya shetani nayo ndiyo chapa ya mnyama. Na ndivyo ilivyo
Kwahiyo roho ya mpinga kristo ambayo ndani yake imebeba chapa ya mnyama iliyozungumziwa kwenye kitabu cha ufunuo 17:1-6 tusome..
” Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu”.
Habari hii inamwonyesha mwanamke aliyeketi juu ya mnyama mwekundu sana, na juu ya paji la uso wake, alikuwa na jina limeandikwa la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA, NA MACHUKIZO YA NCHI,
Sasa huyu mwanamke anayezungumziwa katika sura hii, ni KANISA fulani kwasababu mwanamke siku zote katika biblia anawakilisha kanisa, na pia mwanamke huyu tunaona anaitwa MAMA WA MAKAHABA, Hii ikiwa na maana kwamba ni kanisa-kahaba mama, na ikiwa ni “mama” basi ana “MABINTI”, na hao mabinti ni makahaba kama mama yao alivyo. Kwahiyo kahaba ni mwanamke anayezini na wanaume wengi mbali na mume wake. Na tunaona kuwa kanisa pekee lililofanya uasherati kwa kuchanganya mafundisho ya Mungu na mafundisho ya kipagani ni kanisa Katoliki,
Hivyo basi yule mama wa makahaba aliyezungumziwa pale ni kanisa Katoliki, Na wale mabinti ni madhehebu mengine yote ya dini yaliyobakia, yaliyoacha uongozi wa Roho Mtakatifu na kuiga desturi zile zile za kipagani kama za mama yao kahaba yaani kanisa katoliki. Na sasa hivi tunaona madhehebu yote ulimwenguni na dini zote ulimwenguni zinaungana, pamoja na mama yao mkuu kahaba katoliki (ecumenical council) na KUIUNDA ILE CHAPA YA MNYAMA.
Chapa ya mnyama ipo rohoni na mwilini, (nje na ndani). kwa NDANI ni kama hauna Roho Mtakatifu, umeshaipokea ile chapa ya mnyama(Au Alama ya Mnyama), kwahiyo ndugu tafuta kuwa na Roho wa Mungu angali muda upo, maana biblia inasema huo ndio muhuri wa Mungu, (soma waefeso 4:30). Na pia kuipokea chapa ya mnyama(Alama ya Mnyama) kwa NJE ni kama upo au umejiunganisha au umejifunga na mifumo yote ya madhehebu ambayo yameuacha uongozi wa Roho Mtakatifu, na kuweka mifumo ya kipagani, pamoja na taratibu za kibinadamu na desturi zisizoendana na NENO la Mungu. hivyo kuipokea chapa ya mnyama ni kujishona na madhehebu na kuwa na utambulisho mwingine wowote nje ya UKRISTO mfano, kujitambulisha kama mlutheri, mwanglikana, msabato,mbaptisti, mkatoliki, mbranhamite n.k. badala ya kujitambulisha kama MKRISTO.
(kumbuka maana ya haya majina sio mbaya, lakini madhehebu ambayo yamebeba hayo majina yana ile chapa ya mnyama ndani yake kwasababu yameshafanya uasherati kama wa mama yao katoliki, na Mungu ameyakataa soma ufunuo 3:1 ” …Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. “) kwahiyo kwa kujiita tu hivyo tayari umeshakwisha kubaliana na ile alama ya mnyama bila ya wewe mwenyewe kujijua. Fikiria tu hili kama sisi sote ni WAKRISTO huo utambulisho mwingine unatoka wapi?. Ujue tu unatoka kwa mpinga kristo ambao mwisho wake unapelekea kuiunda ile alama ya mnyama. Na nguvu ya hii alama ya mnyama itakuja kujidhihirisha sana katika kipindi cha dhiki kuu, baada ya kanisa (bikira safi) kunyakuliwa.
Kwahiyo hii alama ya mnyama kwasasa ipo sana katika roho na watu wanaendelea kuipokea kwa kukosa Roho Mtakatifu, lakini kwa nje, ipo wanakubaliana nayo ila itakuja kutenda kazi kwa Nguvu katika kipindi cha dhiki kuu. pale mpingakristo atakaponyanyuka na kupewa mamlaka juu ya ulimwengu mzima, na huyu mpinga kristo atakuwa sio mwingine zaidi ya Papa kiongozi wa kanisa katoliki wa Roma. Sio kwamba wakatoliki ni watu wabaya, Hapana ni watu wazuri wote bali ni vizuri kujua roho inayoliendesha kanisa katoliki ni roho ya mpinga kristo na haitokani na Mungu, Hivyo watu wa Mungu lazima waujue ukweli watoke huko.
Tunaweza tukaona leo hii, mambo mengi ya ajabu, yakitokea ulimwenguni ikiwemo vitendo vya kigaidi vikizidi kukithiri, amani inazidi kutoweka duniani,watu wanaishi kwa hofu za machafuko na vita, siasa na umoja wa mataifa umeshindwa kuihifadhi amani ya dunia, dunia inatafuta suluhisho la mambo hayo na bado haijapata, hivyo anatafutwa kiongozi atakayeonekana ana uwezo wa kurejesha amani duniani naye atakuwa si mwingine zaidi ya PAPA ili maandiko yatimie. Kama tunavyomwona leo hii anajulikana ulimwenguni kote kama mtu wa amani (MAN OF PEACE).
Hivi karibuni tunaweza tukaona jinsi kiongozi huyu wa kanisa Katoliki (papa Francis), akirejesha mahusiano kati ya Marekani na Cuba, ambayo yalikuwa yamevunjika kwa muda mrefu. Leo analeta dini zote ulimwenguni pamoja, anakubalika na kuheshimika na watu wote, Ni kiongozi mwenye ufuasi mkubwa wa watu kushinda kiongozi yeyote ulimwenguni.
(papa akiwa na viongozi wa dini mbalimbali duniani)
Kwahiyo katika kipindi cha ile dhiki kuu, atakuja na wazo la kukomesha ugaidi na vitendo viovu duniani akitaka watu wote, wasajiliwe kulingana na madhehebu yao na mashirika yao ya dini, kwasababu vitendo vinavyosababisha amani kutoweka vinasababishwa na dini na ndivyo ilivyo. kwahiyo ni lazima tatizo litatuliwe kwa namna ya KIDINI na si vinginevyo. Hivyo itahitaji kiongozi wa kidini na hakuna mwingine anayekidhi hivi vigezo zaidi ya Papa kiongozi wa kanisa katoliki.
Leo hii duniani vita vya kidini vimeiweka dunia katika mtazamo mpya, mfano mabomu ya kujitoa muhanga, na vikundi vya kigaidi, kama ISIS, Alqaeeda, Alshabaab, Boko haram Anti-balaka, LRA n.k.vimekuwa ni tatizo sugu kwa dunia nzima, ni mada iliyopo mezani kila siku sio kwa mataifa maskini wala matajiri wote wamevamiwa na tatizo hili .Hivyo kiongozi huyu atapewa nguvu kwa kujipendekeza (danieli 11:21), Jambo hili litatimiza ule unabii wa Daniel 9:27 “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja;….. “ Agano hili la amani litafurahiwa na dunia nzima, kwani litadhaniwa kuwa litaleta amani duniani,
UJIO WA USTAARABU MPYA WA ULIMWENGU
Hapo ndipo utakapowekwa utaratibu mpya wa ulimwengu (NEW WORLD ORDER). chini ya uongozi wa papa (mpinga kristo) baada ya kupewa nguvu na mataifa yote duniani kumbuka hatajiita mpingakristo wala hatakuwa na uso wa shetani, wala usidanganyike kama atakuwa freemason au illuminati, au kikundi chochote cha kichawi hapana bali ATATOKEA NDANI YA KANISA ni mtu anayekubalika na watu, anaonekana mpenda amani, anapenda dini, anajali watu wote wa dini zote, anabusu watoto na zaidi ya yote ataonekana ni mnyenyekevu kuliko watu wote duniani, lakini ndani yake ni SHETANI katika utendaji kazi wake. Biblia inasema “Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ufunuo17:8″
Kumbuka shetani ananyanyua sasa hivi kwa kasi vikundi vya kuvunja amani na ugaidi duniani kama mbinu yake ya sasa ya kutafuta kuwaangamiza wakristo, kama alivyofanya kwa wakristo katika kanisa la kwanza kwenye utawala ule ule wa KIRUMI chini ya Nero (AD 64),ambapo wakristo wengi waliuawa baada ya kusingiziwa kuwa wameuchoma mji, na ANGALI sio wao waliofanya hivyo. Na kwa njia kama hiyo hiyo shetani anawatafuta wakristo leo hii awaangamize, kwa vitu vya KUSINGIZIWA, maana anajua hakuna namna yeyote mkristo anaweza akashitakiwa na kuuawa kwa makosa yeyote ya kihalifu kwasababu wakristo sikuzote wanaishi maisha ya haki. Hivyo sasa hivi ameunyanyua ugaidi katika uislamu na vikundi vingine kama anti-balaka, ISIS, alshabaab,Boko Haramu, Al-qaeda, Hizbolah,Ku klax klan, pamoja na vikundi vyote vya siri vinavyouchafua ulimwengu, ili baadaye aweze kuwasingizia wakristo kwa urahisi kuwa wao ndio magaidi na kuwaangamiza wote).
(wakristo wasingiziwa kuuchoma mji, kusababisha wapitie dhiki kubwa ya kuuawa kikatili dhidi yao chini ya utawala wa Nero AD 64)
Hivyo basi utaratibu huo mpya utakapokuja watu wote watapaswa wahakikiwe taarifa zao muhimu zinazohusiana na DINI ZAO, itahusisha pia na kazi mtu anayofanya, kwenye makampuni, na mashirika. Kila mmoja ni lazima atambuliwe yeye ni dhehebu gani au dini gani katika shughuli anayoifanya kwa dhumuni la kuwapata watu wachafuaji wa amani duniani, kwamfano waislamu wenye itikadi kali, wanaojihusisha na vikundi vya kigaidi, pamoja na vikundi vya kihalifu vinavyohusisha vita vya kidini na mauaji ya kikatili ya watu watambulike na kukamatwa. Lakini nia ya shetani itakuwa sio kuleta amani wala kuwalenga waislamu au makundi mengine BALI NI KUWALENGA WAKRISTO, (kama ilivyotokea kwenye utawala wa NERO,)
Lakini wale ambao hawatakubaliana kujiunga na huo mfumo wa yule mnyama ambao ni MUUNGANIKO WA MADHEHEBU NA DINI ZOTE. Mtu huyo hataweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa asipokuwa na huo utambulisho, Hataruhusiwa kuabudu kwenye kanisa ambalo halijasajiliwa na muungano wa madhehebu, ndugu Branham alitabiri akasema itafika wakati haya makanisa tuliyonayo sasa yatafungwa yote.kwahiyo huu usajili utaanza karibu duniani kote, katika kila nyanja na kila taasisi, kwa waajiriwa na wasio waajiriwa, katika vitambulisho vya taifa,kura na serikalini na taasisi binafsi kama mabenki, ATM cards, VISA n.k. na sehemu nyingine zitatumika MICRO-CHIPS sana sana kwa mataifa yaliyoendelea.
Itakuwa ni sheria kila raia lazima ahakiki taarifa zake za kidini, na huo mfumo mpya. watu wengi wataukubali na kuupenda na kuhakiki taarifa zao pasipo kujua kuwa ndio wanaipokea ile chapa ya mnyama (au alama ya mnyama), na mfumo huo utafanikiwa kukamata wahalifu wengi.Ni wazi kuwa itakuwa ni ngumu kwa mtu kufanya biashara yeyote ya kuuza wala kununua wala kuajiriwa usipokuwa na huo utambulisho wa kidini. kwahiyo ukishahakikiwa taarifa zako utakuwa huru kufanya shughuli yako yoyote unayotaka.lakini sio kujiita MKRISTO tu! haitafanya kazi tena kipindi hicho, huko kutakuwa ni kuonyesha tu ID au CHIP ambayo imebeba taarifa zako zilizohakikiwa na huo mfumo mpya wa mpingakristo,
Lakini wale wakristo watakaokuwepo watamtambua yule mpingakristo na chapa yake, watakataa kuupokea huo utambulisho na usajili wake (chapa ya mnyama/alama ya mnyama). Sasa hao ndio watakaotafutwa na kuitwa magaidi, na hao tu ndio watakaopitia dhiki kuu wakati dunia inaendelea kufurahi. Na hawa hawatauliwa ovyo ovyo tu, kama inavyodhaniwa. bali watachukuliwa na serikali,(maana serikali itawatambua kama wahalifu na sio raia wa kawaida kwa maana serikali itashirikiana na mpingakristo kufanya kazi). Maana hawatakuwa wengi, na watapelekwa kwenye magereza maalumu ya mateso ya siri (concentration camps), huko ndiko kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea wala haitakaa itokee kama Bwana YESU KRISTO alivyosema.
Wakristo wengi watateswa kama magaidi, watasingiziwa wao ndio wanaoharibu amani ya dunia kama sivyo kwanini wakatae kusajiliwa, lazima kuna mambo ya siri wanayo. watakataliwa na jamii nzima, hata ndugu za hao jamaa hawatawaelewa.Hapo ndipo ndugu atamsaliti ndugu ili auawe, Tunaona kama vile wayahudi walivyofanyiwa na Adolf Hitler katika vita ya pili ya dunia kwenye zile concentration camps. watu jinsi walivyokuwa wakiuliwa kikatili na mateso makali yasiyoelezeka ndivyo itakavyokuwa tena na zaidi ya hapo katika wakati wa dhiki kuu kwa wakristo , mpinga kristo atawaua wote, (Na dhiki hii kuu itawahusisha na wayahudi pia) na itadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu ya mwisho wa lile juma la 70 la Danieli.
Na kwa mataifa yote yaliyobaki ambayo yamepokea ile chapa (yaani kwa kuukubali mfumo na utambulisho wa yule mnyama katika vitambulisho vyao na ID, na CHIP zao na vyeti vyao). wataingia katika ile siku ya KUOGOFYA ya BWANA ambayo itaanza mara tu baada ya ile miaka mitatu na nusu kuisha (baada ya dhiki kuisha),hapo ndipo hukumu ya mataifa itakapoanza.
(wayahudi katika mateso kipindi cha utawala wa Hitler)
Kanisa Katoliki ndio linaloongoza kwa kuwaua na kutesa wakristo wengi, na inakadiriwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68 katika historia ya kanisa. Na ndivyo linavyofanya hata sasa kwa siri na litakavyokuja kufanya katika kile kipindi cha dhiki kuu ambacho kipo karibuni kuanza.
Na ndio maana yule mwanamke aliyeonekana kwenye ufunuo 17 alionekana amelewa kwa damu ya watakatifu. Kuna wakristo wengi wanaoteswa na kuawa kwa siri duniani kote, kwa ajili tu wao ni wakristo na sio jambo lingine.
Shetani hapendi kuona mtu anajiita MKRISTO, kama vile asivyopenda kuona watu wakibatizwa kwa jina la YESU KRISTO, na ndivyo asivyopenda kumwona mkristo anautambulisho wa asili wa KUMKIRI KRISTO, Hakuna mahali popote mkristo katika biblia alikuwa anajiita mpaulo au mpetro au m-yohana mbatizaji, au m-eliya au m-timotheo, biblia inasema wote walikuwa wanaitwa wakristo. Kwahiyo utambulisho mwingine zaidi ya huo unatoka kwa shetani, na hiyo ndiyo chapa ya mnyama yenyewe. amina.
Papa akiwa kama kiongozi wa kanisa katoliki ana nembo katika enzi yake inayojulikana na kusomeka kama VICARIUS FILII DEI. tafsiri yake kwa kiswahili ni “BADALA YA MWANA WA MUNGU.”
Kwahiyo papa kulingana na kanisa katoliki anasimama hapa duniani badala ya mwana wa Mungu, anauwezo kama vile, kusamehe dhambi, kubariki, na kusujudiwa n.k.
Haya ni machukizo mbele za Mungu,. Na hesabu ya hilo jina, kwa kirumi ni 666. unaweza ukaona hesabu yake hapa chini.
kwahiyo kutiwa chapa katika mkono wa kuume au kwenye kipaji cha uso, ni kukubaliana na ule mfumo kichwani kwako,(hiyo ni kwenye kipaji cha uso) na kukubali kuutumia huo mfumo kama kitu cha kujipatia riziki au chakula (hiyo ni kwenye mkono wa kuume) tunafahamu kama vile mkono tunautumia kwa kula, kukubaliana na kitu, kusaini mikataba n,k kwa wale watakaokubali kuuza na kununua ndio watapokea hiyo chapa (666). Kumbuka hii 666 ni namba inayomtambulisha mpingakristo na chapa yake, na sio chapa yenyewe.
ukiulizwa wewe ni dhehebu gani, sema mimi ni mkristo usione haya Bwana Yesu alisema katika marko 8:38″Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu”. Uvae ukristo umfuate Yesu usiuvae udhehebu utakupeleka jehanum.
Bwana Yesu anasema mathayo 16:24-26 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?.”
Tubu ndugu mgeukie Mungu haya mambo yote, yatatokea kizazi tunachoishi sisi, unaona jinsi gani MPINGAKRISTO kashaweka mambo yake yote tayari, ni kutekeleza tu! mambo yaishe. YESU KRISTO YUPO MLANGO KURUDI, MUDA UMEENDA SANA KUSHINDA UNAVYOFIKIRI.
MUNGU AKUBARIKI!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.
CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZIUSIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.
Mungu amekuwa akisema na watu mara nyingi kwa kutumia ishara, kwa kusudi la kuonya au kuhadharisha watu wake jambo ambalo litakuja kutokea endapo watu hawatatubu, wageuke na kuziacha dhambi zao. Kwahiyo Mungu amekuwa akiwatumia watu wake wafanyike ishara ili kizazi hicho kiamini na kutubu, na kwamba kisipoamini na kutubu kitaadhibiwa kwa sababu ya kutokusadiki sauti nyuma ya hiyo ishara ambayo Mungu amekipa kizazi hicho.
ISHARA YA YONA:
Yona 1-4,Tunaona katika biblia mfano hai ni Yona, Mungu alipompa maagizo ya kwenda kukionya kizazi cha watu wa Ninawi kiache uovu na kitubu, kimgeukie Mungu kwa kuwa maovu yake yamekuwa mengi, lakini tunafahamu kuwa Yona alikaidi na kukimbilia Tarshishi lakini tunaona ule ulikuwa ni mpango wa Mungu Yona kufanya vile ili amezwe na yule samaki kule baharini na akae tumboni mwa samaki siku tatu, mchana na usiku ili kusudi kwamba Mungu amfanye yeye kuwa ishara kwa faida ya watu wa Ninawi ili kwa kuona ile ishara watubu, maana pasipo ile ishara watu wa Ninawi wasingeamini na wangeishia kuangamizwa,
Lakini tunafahamu ile habari kuwa baada ya wale watu kuisikia ile ishara ya Yona ya kukaa tumboni mwa samaki siku tatu waliogopa na kutubu na kuacha njia zao mbaya. Ile ishara ilikuwa ni neema ya Mungu kwa watu wa Ninawi.Vivyo hivyo ishara kama hiyo wangeonyeshwa watu wa Sodoma na Gomora wasingeangamizwa kwani wangetubu wote, kama Bwana Yesu Kristo alivyosema mathayo 21:11.
ISHARA YA YESU KRISTO:
Baada ya maovu kuwa mengi Mungu alimtuma mwanawe Yesu Kristo ulimwenguni kufanyika ishara ili vizazi vyote vilivyobakia vitubu, watu waokoke na ghadhabu ya Mungu ambayo itakuja kuupata ulimwengu wote hivi karibuni, ilikuwa ni ngumu sana kwa wakati ule kumwamini Kristo kuwa ndiye mwokozi wa ulimwengu kama asingefanyika kuwa ishara kwa dunia nzima iamini, na ishara hiyo ilikuwa ni kufa na kukaa siku tatu kaburini na kufufuka, kama yeye mwenyewe alivyotabiri katika
Mathayo 12:38-40″ Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. “
Kwahiyo Bwana Yesu Kristo alipomaliza kazi yake hapa duniani alipaswa apae aondoke lakini angeondoka bila kufanyika ishara ulimwengu tusingeamini, hivyo basi ilimpasa afe akae kaburini siku tatu kama Yona kisha afufuke ndipo apae, ili sisi kwa kuiona ile ishara tumuamini Yesu kuwa yeye ndiye masihi kweli na katumwa na Mungu, ili kwa maneno yake tutubu na kumgeukia Mungu tuiepuke ghadhabu inayokuja. kwahiyo kwa ishara ya Yesu Kristo mpaka sasa sisi tunaokolewa, na asiyemwamini atahukumiwa kama walivyohukumiwa watu wa kizazi cha Nuhu na watu wa Sodoma na Gomora, mpe Yesu Kristo maisha yako leo.
ISHARA KWA KIZAZI CHETU:
Katika kizazi chetu pia Bwana amekuwa akiwatumia watu wake mbali mbali kama ishara kwenye mataifa mbalimbali na jamii mbalimbali, kwa kusudi la kukionya kizazi kimgeukie Mungu, kiache njia zake mbaya.Tunaona katika Taifa letu hili la Tanzania Bwana alitupa ishara, inawezekana haujawahi kuisikia habari hii, au kama ulishawahi kuisikia pengine haukuelewa sauti ya Mungu nyuma ya hiyo ishara.
Mnamo Tarehe 9/10/2015 . Wahanga 6 wakiwa katika harakati za kuwaokoa wenzao waliokuwa wamefunikwa na kifusi katika mgodi wa madini huko Nyangalata wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kifusi kilishuka na kuwafunika hao watu sita ambao walienda kuwaokoa wenzao, na baada ya muda mrefu kupita walidhaniwa wameshakufa, mule chini shimoni umbali wa zaidi ya mita 120, Walikaa siku 41 usiku na mchana, katikati ya giza nene, pasipo msaada wowote. Lakini katika hali yao humo shimoni walikuwa wakimlilia Bwana, wakifanya ibada, chakula chao kilikuwa ni mende na vyura, hawakujua hewa ilikuwa inatoka wapi ni dhahiri kuwa ulikuwa ni muujiza wa Mungu..
Kumbuka ndugu Mungu hakuwaacha hawa ndugu mule shimoni siku 41, kuwaburudisha watanzania, Mungu angeweza kuwatoa siku ile ile ya kwanza waliyomlilia lakini Mungu aliwaacha siku zile zote ili kwa kupitia wale tuisikie sauti ya Mungu nyuma ya ile ishara, ili tutubu na kumgeukia Mungu.
Lakini cha ajabu ishara hizi tunaziona kawaida. kama ishara ya Yona kukaa siku tatu tu! watu wa Ninawi waliamini na kutubu kwa kuvaa nguo za magunia je! si zaidi hawa ndugu waliokaa siku 41 usiku na mchana katika moyo wa nchi?? Je! masikio yetu yamezibwa? tunaliona hili jambo kuwa la kawaida, hatuelewi sauti iliyo nyuma ya ishara kwamba Mungu anatuvuta sisi tutubu na tumgeukie yeye..kibaya zaidi kizazi chetu hichi cha siku za mwisho ndio kile kilichotabiriwa kufanana na sodoma na gomora Bwana Yesu alisema
Mathayo 12:41-42″ Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.”
Mungu ametuma manabii wake na watumishi wake wengi, sauti yake imesambaa kila mahali kwa ishara nyingi na miujiza. Pia tunaona Kwa kizazi chetu Mungu alimtuma mjumbe wake ndugu William Branham na kumpa ishara mbili kama alizopewa Musa ili watu waamini, na Mungu aliruhusu kitendo cha kimiujiza kinaswe katika kamera na kihakikiwe na wanasayansi kuwa ni kweli ili watu watazame na waamini.Tazama video na picha hapa chini.
sikiliza video hii usikie ishara mbili alizopewawilliam branham kwa uthibitisho wa huduma yake, na ujumbe aliopewa.
Malaika wa Mungu katika mwanga juu ya kichwa cha william branham, uliomtokea juu yake alipokuwa akihubiri. picha hii ilipopigwa ilihakikiwa na wanasayansi kuwa ni ya kimiujiza mwaka 1950, jambo hili la kimiujiza lilishuhudiwa na mamia ya watu waliokuwa mkutanoni siku hiyo
Hakika Mungu hawezi kufanya jambo lolote bila kuwafunulia watumishi wake hao manabii amosi 3:7, Kwa ishara zote hizi Mungu amezungumza na kizazi chetu kwa njia tofautitofauti, hata hatuna udhuru wa kujitetea siku ya hukumu, Tutawezaje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii
Lakini bado unaendelea kuwa mwasherati, mlevi,mwizi,mwongo,mchawi, mzinzi, msengenyaji, unaupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu, uko kwenye tamaa na udanganyifu wa mali vinavyokusonga ukae mbali na Mungu, unaishi maisha ya uvuguvugu haujulikani kama wewe ni mkristo au la,Bwana Yesu alisema katika ufunuo: 3 kwamba watu kama hao atawatapika, na unajua matapishi hayarudiwagi, jichunguze biblia inasema yeye ajionaye kuwa amesimama, na aangalie asianguke. Kama hujazaliwa mara ya pili ni bora ufanye hivyo angali muda upo, Kristo yupo mlangoni kulichukua kanisa lake, ndugu tunaishi katika kizazi ambacho kinaweza kikashuhudia kuja kwa Bwana Yesu mara ya pili, kwamaana dalili zote zinaonyesha na maandiko yanatimia, pengine hatutakuwa na kizazi baada ya hiki, je! utakuwa wapi siku hiyo? jiulize!
Ubarikiwe!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
KWANINI MUNGU AWACHOME WATU KWENYE ZIWA LA MOTO NA HALI YEYE NDIYE ALIYEWAUMBA?
Majaribu matatu Yesu aliyojaribiwa na shetani akiwa njikani siku 40, yanaweza yakachukuliwa kivyepesi lakini ukiyachunguza kwa undani yana tafsiri kubwa sana na maana kubwa sana katika maisha ya kila mkristo akiwapo hapa duniani, na yanahitaji uongozo wa Roho Mtakatifu kuyaelewa yale majaribu yana maana gani kama yalivyoandikwa pale.
Wengi wetu tunafikiri kuwa Yesu alipandishwa nyikani siku 40, kujaribiwa na ibilisi, na alipomaliza kujaribiwa alirejea katika maisha yake ya kawaida halafu basi yaliishia pale. Watu pia wanafikiria kuwa shetani alimtokea Yesu kwa mfano wa nyoka au vinginevyo na kuanza kumjaribu kumpa yale majaribu matatu.
Lakini hiyo sio kweli dhumuni kuu la Yesu kupandishwa nyikani ni kwenda kukutana na Mungu wake kwa dhumuni la kupokea maagizo fulani au ufunuo fulani, Tunaona sehemu fulani kristo aliwaambia wanafunzi wake mwenyewe Mathayo 17:21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] Yesu Kristo hakuongozwa na Roho na kufunga siku 40 nyikani kwenda kukutana na shetani hapana bali ni kwenda kukutana na Mungu wake.
Tunaweza tukaona mfano mwingine kama Musa alivyoitwa na Mungu mlimani kwenda kuchukua zile amri 10, alifunga siku 40 usiku na mchana, na alikuja kufunga tena siku nyingine 40 mchana na usiku kuwaombea wana wa israeli kwa makosa waliyoyafanya ya kuabudu sanamu. Kwahiyo Bwana Yesu Kristo kufunga nyikani siku 40 ilikuwa ni kwa ajili ya huduma yake iliyokuwa inakaribia kwenda kuanza, ndipo huko Mungu alipomfunulia huduma yake itakavyokuwa pamoja na yale majaribu makuu matatu atakayokutana nayo katika maisha yake ya huduma.
JARIBU LA KWANZA:
Tunasoma katika luka 4:1-4 “1 Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,
2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.
3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.
4 Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu.”
Hapa tunaona Bwana Yesu baada ya siku 40 kuisha aliona njaa na alipoona njaa akiwa kama mwanadamu alitamani chakula, lakini safari yake ya nyikani ilikuwa bado haijakwisha kwahiyo shetani alipoona kuwa huyu mtu anauhitaji wa chakula alimletea ushawishi moyoni wa kugeuza jiwe kuwa mkate kwasababu alifahamu kuwa anaweza kufanya hivyo.
Sasa hapa inadhaniwa kuwa shetani alimtokea akamwambia hivyo la! hakumtokea bali alimletea ushawishi moyoni kufanya vile, biblia inasema mtu anajaribiwa kwa tamaa zake mwenyewe,(yakobo 1:14 ). Yesu kama asingeona njaa asingejaribiwa, njaa ilipokuja shetani naye akapata nafasi lakini pamoja na hayo Bwana alishinda kwa kuwa aliyajua maneno ya Baba yake kuwa “mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litakalotoka katika kinywa cha Mungu”, aliona sio vema kuyakatiza mapenzi ya Mungu kwa sababu ya chakula, alitambua kuwa ni Mungu ndiye aliyempeleka kule kwa hiyo hata kama siku za kukaa kule nyikani zingeongezeka mpaka kufikia 60,au 70 au 100. angeendelea kuishi kwasababu anaishi kwa neno linalotoka katika kinywa cha baba yake na sio kwa chakula cha mwilini tu. Kwahiyo tunaweza kuona Yesu Kristo aliweza kushinda kwa namna hiyo.
Lakini jaribu hili sio kwamba liliishia pale nyikani tu, ule ulikuwa kwake ni kama ufunuo wa mambo atakayokwenda kukutana nayo mbeleni katika huduma yake, Mungu alimuonyesha ni moja ya jaribu kuu ambalo shetani atampelekea katika maisha yake ya huduma.
Maana ya kugeuza jiwe kuwa mkate ni ipi?
kugeuza jiwe kuwa mkate inatokea pale mtu anayopitia hali ya uhitaji au shida ya kitu fulani na anafahamu kuwa ni Mungu ndiye aliyempitisha katika hiyo hali, lakini yeye anatafuta njia mbadala ya kujing’amua na hiyo shida angali iko katika uwezo wako wa kufanya hivyo, mfano Yesu Kristo alitambua kuwa anapitia katika hali ya taabu na alikuwa na uwezo wa kugeuza lile jiwe kuwa mkate lakini hakufanya vile kwasababu alijua kuwa angeenda nje ya mapenzi ya Mungu sio kana kwamba hakuwa na njaa au alikuwa anajinyima au hakuweza kufanya la! bali alijinyenyekeza chini ya Mungu katika hali ngumu aliyokuwa nayo..
Tunaona jaribu kama hili liliwapata wana wa Israeli lakini walilishindwa pale walipopitishwa miaka 40 nyikani wakaanza kumnung’unikia Mungu wakitaka watimiziwe matakwa yao wenyewe na sio matakwa ya Mungu. Tunaona katika hali ngumu waliyokuwa nayo nyikani ukafikia wakati wakasikia njaa kama Yesu Kristo alivyosikia njaa, na kwajinsi Yesu alivyokuwa na uwezo wa kubadilisha jiwe kuwa mkate vivyo hivyo na wao pia walikuwa na uwezo huo huo wa kubadilisha jiwe kuwa mkate mfano huu tunawaona badala ya kujinyenyekeza chini ya mapenzi ya Mungu wakaanza kumnung’unikia Mungu wakitaka nyama nyikani na Mungu aliwapa nyama, alikuwa akiwapa chochote walichokuwa wanakihitaji(huku ndio kugeuza jiwe kuwa mkate)..
Kumbuka wana wa israeli walikuwa wanajua kuwa lolote watakalomwomba Mungu atawapa kama vile Yesu alivyojua kuwa lolote atakalomwomba Baba yake atampa, tunaona wana wa israeli walikuwa wanashushiwa mana kule jangwani kwa hiyo wakatumia kigezo hicho kwa tamaa zao kutaka vitu ambavyo sio sawasawa na mapenzi ya Mungu kwa kisingizio kuwa wanasikia njaa lakini hawajui kuwa shetani ameshawashinda kwa kutoweza kulishinda hilo jaribu.
kumbukumbu 8:1-5″Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.
2 Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.
3 Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana.
4 Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini.
5 Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo.”
Vivyo hivyo kristo katika huduma yake ambayo Mungu alikuwa akimtuma alijifunza kutokutazama vitu vya nje kama mali,chakula, mavazi hakujali hata sehemu ya kulala japokuwa alikuwa na uwezo wa kupata mali, kula na kunywa, na sehemu za kulala kwasababu alihesabu kutenda mapenzi ya Mungu kwanza ni bora kuliko njaa ya vitu vya nje
yohana 4:30-34 Basi wakatoka mjini, wakamwendea.
31 Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule.
32 Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi.
33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?
34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.”
Kwahiyo alifahamu eneo shetani atakalomtesea katika maisha yake ya huduma ni hapo kwenye njaa ya mambo ya nje, lakini kwa kujua ufunuo huo alikuja kuweza kuyashinda yote. Na ndio maana aliwaambia mahali fulani wanafunzi wake
mathayo 6:26″ Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? ” aleluya!!
Jambo hili hili linajirudia kwa Mkristo anayesema ameamua kumtumikia Mungu, kumbuka haya majaribu matatu kila mkristo lazima ayapitie na hakuna majaribu makubwa zaidi ya hayo shetani anaweza akamjaribu mtu, vivyo hivyo kwa mkristo aliyeamua kumtumikia Mungu atambue kuwa ni lazima akutane na hili jaribu, pale shetani anapokuona upo karibu na Mungu wako sana na upo katika hali ya nyikani(kumbuka nyikani ndipo Mungu anaposhushia mana, na nyikani ni sehemu yoyote isiyokuwa na tumaini lolote,
Inawezekana katika maisha sana sana katika safari ya wokovu mtu anapoanza kumwangalia Kristo) hapo ndipo shetani analeta ushawishi kama huo alioupata Bwana ili uache njia yako, anatumia Neno kukufanya wewe utimize tamaa yako ambayo sio sawasawa na mapenzi ya Mungu, atakwambia fanya hivi au fanya vile ili uishi vizuri ndipo umtumikie Mungu, atakwambia acha hicho unachokifanya fanya kwanza hichi ujikwamue kimaisha..
Atakwambia sasa tafuta kwanza maisha ndipo uje kumtumikia Mungu baadaye, tafuta pesa kwanza maana unashida ya pesa sasa hivi halafu Mungu utamtafuta baadaye, atakwambia jiweke vizuri kiuchumi kisha utaenda baadaye kuhubiri injili, atakwambia huoni watumishi wote wanafanya hivyo,?? na atakupa sababu zote kwamba una uwezo wa kufanya hayo yote na ni kweli ukiangalia unao huo uwezo lakini nia yake yeye sio wewe kuyakidhi mahitaji yako bali ni kukufanya utoke katika kusudi la Mungu la kumtazama yeye, anakufanya usilifahamu neno la “mtu hataishi kwa mkate tu,”
kwahiyo anatumia tamaa zako kukufanya uende kinyume na mapenzi ya Mungu. kumbuku wana wa israeli walivyokuwa Mungu kuwapitisha nyikani ilikuwa sio kwenda kuwakomoa, lakini wangejuaje kama Mungu anaweza kuwalisha pasipo kazi ya mikono? wangelifahamu vipi hilo neno la MTU HATAISHI KWA MKATE TU ?? kama wasingepitishwa nyikani. unaona ni kusudi kabisa la Mungu kumpitisha mtoto wake nyikani ili ajifunze kumtegemea lakini shetani anavumbua njia mbadala kumchonganisha na Mungu haya ndiyo yaliyowakuta wana wa Israeli.
Jambo hili hili linawatokea wakristo wengi wanapopitishwa nyikani(kumbuka kila mkristo lazima apitishwe nyikani) wanashindwa na hili jaribu la shetani wanashindwa kufahamu kuwa mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litakalotoka katika kinywa cha Mungu, mtu hataishi kwa pesa tu, mtu hataishi kwa kazi tu, mtu hataishi kwa mifumo tuliyoizoea tu, mtu hataishi kwa gari na nyumba tu, mtu hataishi kwa umaarufu wala chochote cha ulimwengu huu, bali mtu ataishi kwa neno la Mungu tu!! Mungu ni zaidi ya mali na kila kitu Kristo anasema .
(Mathayo16:25-26..”Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? ).
kila siku unasema ngoja nisubirie kidogo, nisubirie kwanza nifanye kitu fulani nikishakipata ndipo nianze kumtafuta Mungu, mwingine yupo katika taabu anasema ngoja kwanza nitafute pesa nitoke katika hii tabu ndipo nianze kumtafuta Mungu huko ndiko kugeuza jiwe kuwa mkate, unadhania kuwa mtu ataishi kwa pesa tu pasipo pesa huwezi kuishi(wana wa israel hawakuwa na fedha lakini walilishwa miaka 40 jangwani), unasema pasipo nyumba huwezi kuishi(yesu alilala milimani ambaye ndiye tunayemwita Bwana wetu na mfalme wetu),
Yesu alisema
mathayo 6:31-34″ Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”
Na pia Yesu alisema chakula changu ni kuyatenda mapenzi ya baba yangu (yohana 4:34) vivyo hivyo na sisi tuseme hivyo chakula chetu ni kuyatenda mapenzi ya baba yetu na kuyamaliza. Tusigeuze jiwe(vitu visivyo na uhai) kuwa mkate. Mungu anapotuita tuwe tayari kutii na kusema ndio pasipo kuangalia mambo mengine ya kando kando, kwa kufanya hivyo ndivyo tutakavyoshinda hilo jaribu la mkate vinginevyo hatutaweza.
JARIBU LA PILI:
Luka 4:5-6″ Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.
6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.7 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. “
Kwenye Jaribu hili tunaona Kristo akihamishwa kutoka nyikani mpaka kwenye milki zote za ulimwengu akaonyeshwa fahari zote za ulimwengu. Hapa sio shetani alimchukua katika mwili bali ni alichukuliwa na Mungu katika maono kuonyeshwa lile jaribu la shetani litakavyokuwa katika maisha yake ya huduma”. Kwa namna ya kawaida ni vigumu adui yako akuambie nisujudie halafu nitakupa vitu vyote, unafahamu kabisa huwezi kumsujudia kwasababu unajua kabisa anakujaribu kwahiyo ni wazi kabisa shetani hakumtokea Yesu bali ni Mungu ndiye aliyemwonyesha yale maono, na hili jambo lilikuja kutimia katika maisha yake kule mbeleni pale huduma yake ilipoanza kuwa kubwa, alipojulikana kila mahali na watu wote mfano huu tunaona alipokwenda Samaria wale watu wa ule mji walitaka kumshika na kumfanya mfalme
(Yohana 6:14-15 “Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.
15 Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake. “)
Jaribu kufikiria leo hii kama Bwana Yesu angekuwa mfalme wa wasamaria msalaba tungeujulia wapi, kwahiyo tunaliona hilo ni jaribu shetani alilomletea lakini alikumbuka alionyeshwa na baba yake akiwa jangwani, ya kwamba utamsujudia Bwana Mungu wako yeye peke yake, sasa kusujudia pale sio kwenda kumpigia magoti shetani bali ni kukubaliana na jambo lolote shetani atakalokuletea mbele yako kinyume cha mapenzi ya Mungu, tunaona hata leo hii watu wanamsujudia shetani pasipo hata wao kujua pale wanapotenda dhambi, unadhani shetani angemtokea mtu na kumwambia nisujudie nani angekubali?? yeye siku zote anatumia hila kuabudiwa anamfanya mtu adhani kuwa anamwabudu Mungu kumbe anamwabudu shetani.
Vivyo hivyo shetani alivyokuwa anajaribu kufanya kwa Bwana Yesu Kristo kwa kutaka kusujudiwa kwa kupitia ufahari,lakini Kristo alishinda, aliona ni vyema kuiendea njia ya msalaba aliyowekewa na baba yake kuliko kukubali sifa na heshima na vyeo na ukuu na ufalme kutoka kwa watu.Lakini leo hii angeonekana ni mtu anayechezea bahati.
Vivyo hivyo jaribu hili pia linawakuta wakristo sana sana watumishi wa Mungu walio katika huduma, mwanzoni wataanza vizuri katika huduma na Mungu atatembea nao lakini shetani anapoona hivyo ili kumwaribu anamletea jaribu kama hili lililomkuta Bwana Yesu, anaanza kwa kumpa umaarufu wa ghafla, watu watakuja kumwambia njoo uwe kiongozi wetu tutakupa pesa, nyumba, magari, tutakufanya kuwa maarufu kushinda hapo ulipo, tutaikuza huduma yako zaidi ya hapo ilipo, ila acha tu huo mtindo wako wa kale wa kuhubiri, punguza ukali wa maneno tutakupa kila kitu, we hubiri tu kama sisi tunavyohubiri, wengine wanaitwa na wanasiasa wawasaidie katika siasa zao na wanaahidiwa kupewa pesa nyingi.
Kwahiyo mtu huyu badala ya kukaa chini na kutafakari kama huduma yake itaathirika au la! yeye anakubali bila kufahamu kuwa hizo ni hadaa za shetani kutaka asujudiwe. Na watumishi wengi wa Mungu wameshindwa hili jaribu wameacha kusudi lao la kufundisha, na kuiendea njia ya msalaba, wakaiendea njia ya watu wa mataifa ili kupata umaarufu na heshima. luka 6:26″ Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo. “
JARIBU LA TATU:
Luka 4:9-12″ Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini;
10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde;
11 na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. “
Katika jaribu la tatu tunaona Yesu Kristo akipelekwa katika kinara cha hekalu, unaweza ukajiuliza kwa nini alipelekwa Yerusalemu, na ni kwanini kwenye kinara cha hekalu na sio penginepo?
Ono hili alipewa kuonyeshwa mwisho wa safari yake ya huduma, kwamba mwishoni atawekwa kwenye kinara cha hekalu ambacho ni msalaba, Yesu Kristo safari yake ya mwisho ilikuwa ni msalabani(hata sio ajabu kuyaona makanisa yakiwa na msalaba juu, hii inaleta picha kuwa pale juu ya kinara cha hekalu alipowekwa Yesu ni msalabani) na kumbuka hata pale msalabani shetani alikuwa akimjaribu kwa maneno hayohayo kama tunayoyaona hapo juu, shetani alimwambia kipitia vinywa vya wale watu
Mathayo 27: 39-44″ Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa vyao, wakisema,
40 Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani.
41 Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe.
42 Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
43 Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.
44 Pia wale wanyang’anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile. “
Lakini kama Bwana Yesu Kristo asingetambua hayo majaribu ambayo alionyeshwa na baba yake akiwa nyikani angejishusha chini msalabani na watu wote wangeamini kwasababu alikuwa anao huo uwezo, picha hii hii tunaiona pale usiku ule walipokuja kumshika Yesu na petro alipotaka kumwokoa Bwana alimwambia (mathayo 26:52-54 ”
Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?” ) Kwahiyo tunaona Yesu Kristo alikuwa ana huo uwezo wa kujishusha msalabani lakini je! angejishusha msalabani mapenzi ya baba yangetimizwaje? na sisi tungepataje wokovu?.
Vivyo hivyo na kwa mkristo yeyote anayeipenda njia ya msalaba(japo sio wote watakayoipitia ) jaribu kama hili atakutana nalo ndilo la mwisho kumbuka shetani hatakuacha hata katika dakika ya mwisho ya wewe kukata roho atakuwa karibu yako kukufanya uanguke. Msalaba ndio hatua yetu ya mwisho, Yesu alisema mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba isipokuwa kwa njia ya mimi, njia hapo anayoizungumzia ni maisha yake yeye sasa tunayaamishia kwetu, na alisema pia mtumwa sio mkuu kuliko Bwana wake, kama yeye walimwita belzebuli, mwenye pepo, alienda msalabani kufa kifo cha aibu je! inatupasaje sisi? hatupaswi kuionea haya njia ya msalaba, watazame mitume na manabii na wakristo wa kale kwa kuitetea kweli na kuisimamia kweli hawakupenda maisha yao hata kufa, walihesabu kuwa utukufu wa Mungu ni bora kuliko utukufu wa wanadamu, Kristo alisema mtu yeyote akitaka kunifuata ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake anifuatae kila siku (mathayo 16:24),na unajua msalaba ni nini?, mwisho wake ni golgotha.
Kwahiyo utakapofikia katika jaribu la tatu na la mwisho ambalo shetani atakuacha ni pale utakapoona unaenda kutiwa mikononi mwa shetani kama Yesu Kristo na mitume na manabii. walivyofanyiwa, angali una uwezo wa kujiepusha nalo kama Yesu tunaweza kuona shetani alimvaa hata Petro akijaribu kumshawishi Yesu asiipitie njia ya msalaba, lakini Yesu alimwambia nenda nyuma yangu shetani huyawazi ya Mungu bali ya wanadamu, lakini Yesu alijinyenyekeza kama kondoo aendaye kuchinjwa na ndivyo walivyofanya mitume watu wa Mungu kama stephano, yohana n.k huko ndiko kulishinda hilo jaribu( na kumalizia kusema Baba wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo).
Yesu Kristo anasema
(ufunuo 3:20-22″ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. ). kwahiyo kushinda ni nini?? kushinda ni kule kushinda yale majaribu matatu kama Bwana Yesu alivyoyashinda.”
Sio kwamba usipopitia hiyo njia itakufanya usiende mbinguni la! Labda utaenda lakini utakuwa hujashinda kwasababu hujapigana kikamilifu, thawabu yako itapunguzwa kama utashindwa na majaribu hayo ya shetani,
1wakorintho 9:24″ Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.
26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;
27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
Na pia mtume Paulo anasema,
2timotheo 2:5″4 Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
5 Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali. “
mtume Paulo pia aliandika..
wafilipi 3:10-14″10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;
11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. “
mwisho mtume Paulo aliandika
2timotheo 4:6-8″ Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. “
Mungu akubariki sana ndugu yetu mpendwa.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?
JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA??
ZIFAHAMU NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE SABA
Mathayo 24:32-35 ” Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
34 Amin, nawaambia, KIZAZI HIKI HAKITAPITA, hata hayo yote yatakapotimia.
35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Mambo haya Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake walipokuawa wameketi katika mlima wa Mizeituni, akiwaonya mambo yatakayokuja kutokea siku za mwisho kabla ya kurudi kwake, yakaandikwa kwaajili yetu sisi tusiwe gizani ili wakati huo ukifika mambo hayo yasitujie kama mwivi. Yapo mambo mengi Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kama tunavyoyaona katika vitabu vya injili na vitabu vingine kuhusu siku za mwisho zitakavyokuja kuwa.
Lakini katika kitabu cha Mathayo 24 Bwana Yesu alisema katika siku za mwisho kutatokea vita na matetesi ya vita (mathayo 24:6), Hii ni sahihi hivi vita tumekuwa tukiviona vikipiganwa kwa karne na karne kati ya mataifa na mataifa, lakini vita vingi na vikubwa vimekuja kukithiri zaidi katika karne ya 20 na 21,tunaona mfano wa vita vya kwanza (1914-1918) na vya pili vya dunia (1939-1945) ambavyo vimesababisha mauaji ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote, kitu ambacho hata hakijawahi kuonekana katika historia ya vizazi vyote vya nyuma., lakini Bwana alieleza wazi yatakapoanza kutokea haya msitishwe ule mwisho bado,alisema kuwa huo ndio mwanzo wa utungu.
Bwana Yesu alisema pia siku za mwisho kutakuwa na njaa (mwilini na rohoni), matetemeko ya nchi, kutakuwa na magonjwa mengi, mambo ambayo tumekuwa tukiyaona kila kukicha matetemeko kila mahali, magonjwa mapya yanazuka kila siku((kama cancer, kisukari,presha,zika,ukimwi,ebola,sars,kimeta, n.k) ambayo hayakuwepo katika vizazi vya zamani, lakini haya yote Bwana Yesu pia alisema ni mwanzo wa utungu, kwamba ule mwisho unakaribia lakini bado haujafika.
Jambo lingine Bwana Yesu alilolisema ni kuwa manabii na makristo wengi wa uwongo watatokea na kuwadanganya wengi, Kila mtu anafahamu kama tunavyowaona leo mafundisho mengi ya uwongo yamezagaa kila mahali, alisema pia upendo wa wengi utapoa, ni dhahiri kabisa upendo(shauku) ya watu kumpenda Mungu na kupendana wao kwa wao imetoweka,na tamaa mbaya za ulimwengu huu zimewasonga watu na kumsahau Muumba wao, alisema pia watu watakuwa wakijipenda wenyewe, wakisalitiana na kuchukiana.
Aliwaambia wanafanzi wake pia,
luka 21:20-24 “ Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.
21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.
22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.
23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.”.
Hili jambo lilitimia kama lilivyo mwaka 70 BK pale majeshi ya Rumi yalipouzunguka mji wa Yerusalemu na kuharibu mji na hekalu kuliteketeza kwa moto, na wayahudi wote waliokuwa wamesalia Yerusalemu walitawanywa katika mataifa yote duniani hivyo basi Israeli wakawa wageni katika mataifa mengine, mpaka Mungu alipowarejesha tena nchini kwao mwaka 1948 kuwa kama taifa huru tena linalojitegemea.
Mwisho Bwana Yesu alisema habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Lakini hapa kuna jambo kuu na la muhimu sana tunatakiwa tulione,
Tukisoma katika
Luka 21:29-33 inasema “29 Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote.
30 Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.
31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.
32 Amin, nawaambieni, KIZAZI HIKI HAKITAPITA, HATA HAYO YOTE YATIMIE.
33 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Alisema kwa mtini jifunzeni, “Mtini” siku zote kwenye biblia unawakilisha Taifa la Izraeli,(soma yeremia 24), na aliposema utazameni mtini na miti mingine,hii miti mingine ni mataifa mengine, sasa aliposema mtini utakapoanza kuchipua alikuwa na maana Taifa la Israel kuzaliwa tena upya baada ya kukaa katika mataifa mbalimbali kwa muda mrefu. Tunaona jambo hili lilitimia mwaka 1948 pale Izraeli waliporejea katika nchi yao wenyewe kama ilivyotabiriwa na Bwana, hiyo ndiyo maana ya kuchipuka kwa Israeli. Hivyo basi kuanzia huo mwaka wa 1948 mpaka sasa tunaona mataifa mengi yalianza kupata uhuru wao ikiwemo mataifa karibu yote ya Afrika, baadhi ya Asia na Marekani ya kusini hii inatimiza ule unabii Yesu aliosema mjifunze pia kwa miti mingine (miti mingine ni sisi mataifa mengine mbali na Israeli).
![]() |
Taifa la Israeli likisherekea siku ya uhuru wao 1948 |
Sasa baada ya mtini kuchipuka(Izraeli) hapo ndipo Bwana aliposema “Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Hichi kizazi kinachozungumziwa hapa sio kile kizazi cha Yesu alichokuwa anazungumza nacho, bali ni kile kizazi kilichoshuhudia Izraeli ikichipuka yaani Izraeli kuwa Taifa huru tena kama ilivyokuwa hapo mwanzo zaidi ya miaka 2500 iliyopita.
Na kizazi kilichoshuhudia hayo ni kuanzia watu waliozaliwa mwaka 1948 na kuendelea hadi sasa, kwahiyo tumeshafahamu kuwa kizazi cha wale waliozaliwa mwaka 1948 Bwana Yesu ndicho alichosema hakitapita. Na tunajua kizazi mpaka kitoweke kabisa katika dunia ni miaka 100,kwa dunia ya sasa, tukiangalia tangu mwaka 1948 hadi leo ni miaka 69 imeshapita, na hapa Bwana Yesu alisema kizazi hiki hakitapita hakusema kitatimia ndio mwisho uje bali alisema hakitapita,
Kwahiyo hii ina maanisha hapa hapa katikati kabla ya kufikia hicho kipindi cha kizazi kutoweka Bwana Yesu Kristo atakuwa ameshakuja, ni wazi kabisa wengi waliozaliwa chini ya mwaka 1948 ni asilimia 7% tu inayoishi duniani sasa (kwa mujibu wa takwimu za dunia), kwahiyo hili rika la hawa watu linakaribia kupotea, lakini Bwana Yesu Kristo aliapa kuwa hili rika halitapita,
aliweka msisitizo kabisa akasema Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”..
Na baada ya hapo ndipo Bwana Yesu aliposema mtakapoona hayo yanaanza kutokea tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu, kwa hiyo ndugu tambua hilo wewe unayesema bado sana Yesu kurudi, wewe ambaye unasitasita kwenye mawazo mawili, maneno haya yanaonyesha wazi kabisa kuwa kuja kwa Bwana kuko mlangoni, Baada ya hayo maneno Bwana Yesu Kristo alimalizia kwa kusema
“ Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
36 Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
Bwana Yesu Kristo hakutoa muda wala saa ya kuja kwake lakini alitupa majira kwamba yatakapokuja yasitujie kama mwivi au kama mtego unasavyo, je! wewe ambaye unatambua kabisa tunaishi katika kizazi ambacho tutashuhudia kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili, umejiwekaje tayari, umebatizwa kweli kwa Roho Mtakatifu?? umeufanya imara kweli uteule wako na wito wako? Bwana Yesu akija leo una uhakika wa kwenda naye??.
Huu ni wakati wa wale wanawali werevu kutengeneza taa zao kwenda kumlaki Bwana Yesu, je! na wewe una uhakika kuwa taa yako iko sawa?? Tambua ya kuwa Bwana akija leo na taa yako haipo sawa utabaki hapa na kuingia katika ile dhiki kuu? Kumbuka ujumbe huu unakuhusu wewe mkristo unayesema umeokoka, kumbuka wale walikuwa wote ni wanawali na wote walikuwa wanamsubiria Bwana wao isipokuwa watano walikuwa werevu na watano walikuwa wapumbavu (mathayo 25)
kwahiyo hao wanawali 10 wote ni wakristo na sio watu wasioamini, fahamu tu uchungu utakuwa kwa wale ambao walidhani wangeenda katika unyakuo lakini wakabaki, na sio wale wasioamini, hivyo ndivyo itakavyowakuta wakristo wote ambao ni vuguvugu sasa wanachofahamu tu ni madhehebu yao lakini hawataki kumjua Kristo katika neno lake, hawataki kujazwa Roho Mtakatifu ili awaongoze katika kweli yote uteule wao uwe wa uhakika, Roho Mtakatifu ndio muhuri wa Mungu (waefeso 4:30) pasipo Roho Mtakatifu hakuna unyakuo. je! wewe ni mmoja wa wanawali mwerevu au mpumbavu? wanawali wote werevu wanajivunia kuwa wakristo wa NENO na sio wakristo wa madhehebu, wanawali wapumbavu wanaona aibu kuitwa wakristo, wanajivunia madhehebu ukimwuliza yeye ni nani atakwambia mimi nimlutheri,mkatoliki,msabato,mbranhamite,m-eagt,morovian., hawafahamu jambo lingine lolote nje ya madhehebu yao, ukiwaambia biblia inasema hivi wanasema dhehebu letu halifundishi hilo,
Lakini BWANA YESU KRISTO leo anatuita tuwe WANAWALI WEREVU(SAFI)…..na ujumbe tulionao sasa kwa wakati wetu ni
Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.”
Jihadhari na mafundisho ya uongo.
Ndugu tubu, mgeukie Bwana muda ndio huu, usidanganyike na mafundisho yanayosema kuwa Kristo bado sana kurudi.
Mungu akubariki!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=9K3Zsu-btLs[/embedyt]
Mada Nyinginezo:
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE
JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?