Category Archive Uncategorized @sw-tz

Kwanini Yesu alikamatwa usiku, hawakuyafanya yale mchana?

JIBU: Yesu ni mtu ambaye alizungukwa na makutano mengi, hivyo isingekuwa rahisi kwao kumkamata wakati wa mchana, kwasababu walijua watakutana na upinzani mkubwa wa makutano.. kama maandiko yanavyosema katika vifungu hivi; 

Mathayo 21:45-46

[45]Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao.

[46]Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii. 

Hivyo njia pekee, ilikuwa ni usiku. Tena wakamwendea na marungu na mapanga kujidai kuwa wanakwenda kumtafuta mwizi, huku mioyoni mwao wakijua kabisa wanayekwenda kumfuata ni mtu wa haki.

Na hiyo ni kuthibitisha kwamba walikuwa hawajiamini kwa matendo yao, kwasababu waliyajua ni maovu ndio maana waliyafanya gizani.

Marko 14:48-49

[48]Yesu akajibu, akawaambia, Je! Ni kama juu ya mnyang’anyi mmetoka wenye panga na marungu, kunitwaa mimi? [49]Kila siku nalikuwa mbele yenu hekaluni nikifundisha, msinikamate; lakini haya yamekuwa ili maandiko yapate kutimia. 

Hiyo ndio sababu kwanini wamfuate usiku, lakini hawakujua ndio walikuwa wanairahisisha njia ya wokovu. Kufunua kuwa giza kamwe haliwezi kuishinda nuru.

Yohana 1:4-5

[4]Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. [5]Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza. 

Mwamini Kristo, Nuru yake ikuangazie moyoni mwako.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?

Yesu kuvishwa taji la miiba kichwani, kulifunua nini?

Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?

Rudi Nyumbani

Print this post

KIFUNGO CHA MWAMINI KIPO WAPI?

Unaweza kuuliza je! Mwamini anaweza kufungwa na adui?. Jibu ni ndio anaweza kufungwa. Utauliza tena, kama anafungwa sasa kazi ya Yesu msalabani ilikuwa ni nini ikiwa hajawekwa huru kweli kweli.

Jibu ni kwamba mwamini yeyote, hawezi kuwa na kifungo katika roho yake, yaani hawezi kufungwa roho aidha na mapepo, au wanadamu au chochote kile. Hawezi kuwa na laana yoyote ndani yake, aidha ya ukoo au ya mabibi. Kwasababu yeye ni mbarikiwa amewekwa huru na Yesu, na ndio kazi Yesu aliyokuja kuifanya kuwaweka huru walioonewa na ibilisi.Hivyo mtu yeyote aliyemwamini Yesu kwa ‘TOBA’, ubatizo na kupokea Roho. Huyo hana kifungo chochote kwasababu uhai wake unakuwa umefichwa ndani ya Kristo.

Lakini Shetani anauwezo wa kumzuia, katika mambo mengi, asipojua ni nini anapaswa afanye. Na hicho ndicho kifungo cha nje akifanyacho adui. Kukuzuia wewe mwamini, ndicho alichokifanya kwa Paulo wakati Fulani alipotaka kwenda kuhubiri  injili kwa Wathesalonike akasema shetani alinizuia (1Wathesalonike 2:8).

Lakini pia tunamwona Mtume mwingine aliyeitwa Petro.

sasa hebu tuangalie kisa hiki kwenye maandiko Kilichomhusu yeye, tuone ni maeneo gani huwa adui analenga mahususi.

Matendo 12:4  Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu.

5  Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.

6  Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakalilinda gereza.

7  Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika kule chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. MINYORORO YAKE IKAMWANGUKA MIKONONI.

8  Malaika akamwambia, Jifunge, KAVAE VIATU VYAKO. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, JIVIKE NGUO YAKO, ukanifuate.

9  Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono.

Umeona maeneo aliyofungwa Petro?

Wafungwa wa zamani, ilikuwa ili aitwe mfungwa, ni lazima mambo hayo matatu  yakamilishwe juu yake; nayo ni.

1) Kufungwa, Minyororo mikononi

2)Kuondolewa Mavazi, na kupewa mengine ya gerezani.

3)Kuondolewa viatu miguuni

Na hiki ndicho kitu anachokifanya  pia adui kwa mwamini. Anaanza kwa kukufunga mikono yako rohoni, kisha kuyaondoa mavazi yako, na mwisho viatu vyako miguuni. Baada ya hapo unakuwa tayari huna nguvu ya kumshinda.

Mikono ni nini?

Ni “maombi na mifungo”

Mikono ni viungo mama katika mwili. Husaidia viungo vingi kufanya shughuli zake. Silaha hushikwa na mikono,  hata ngumi hurushwa kwa mikono. Hivyo adui anajua akizuia mikono yako. Huwezi kufanya lolote. Mikono ya mwamini, ni “maombi na mifungo”.

Mtu ambaye ni mwombaji, kiwango cha Roho ndani yake huwa ni kikubwa, na hivyo hakuna mnyororo wowote, unaoweza kumshika. Ndio maana utaona baada ya kanisa kumwombea Petro kwa juhudi, akafunguliwa. Vilevile Paulo na Sila walipokuwa wamefungwa kipindi kile, hawakulala tu, bali usiku wa manane walikuwa wakiomba, na matokeo yake vifungo vikawaachia.

Matendo 16:25  Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 26  Ghafla pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.

Umeona, maombi, huondoa minyororo mikononi. Kuwa mwombaji, uzishinde nguvu za mwovu. Shetani anawaogopa waombaji

Mavazi ni nini?

Ufunuo 19:8  Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu

Mavazi, ni matendo mema. Ukikosa matendo mema,(Utakatifu), si rahisi kumshinda adui, utakuwa mwamini asiye na matunda yoyote, itaishi tu kama mwanadamu ambaye anamapungufu ya akili rohoni, hutaweza kufanya lolote.Ndani una makunyanzi, mawaa, ambazo katika hizo shetani anakuwa na haki ya kukulaumu.

Ishi kama mkristo, ukiwa rafiki wa dunia, fahamu kuwa unajifanya adui kwa Mungu moja kwa moja. Nuru yako isipoangaza nje, huwezi mshinda shetani. Ni lazima uwe kikombe safi, nje na ndani. Huwezi kusema umeokoka halafu matendo yako hayaendani na imani yako.Unajidanganya, bado hujaifahamu neema ya Mungu.

Miguu ni nini?

Waefeso 6:14  Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15  na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani.

Miguu ni utayari, wa kuhubiri. Adui anapenda kukawiisha nia za watu, kwa kuwavuta katika mambo yao mengine, na kusahau yaliyo ya msingi kwao, ndio hapo atawasonga kwa anasa, udanganyifu wa mali, na shughuli za ulimwengu huu. Na mwisho wa hapo wanabakia kuwa hawana matunda.

Hivyo ndugu uliyeokoka, usiruhusu adui kukuzuia popote. Jijengee desturi ya kuwa mwombaji wa kila siku. Mikono yako isifungwe. Penda kuishi maisha matakatifu, vazi lako lisibadilishwe, kuwa tayari kuhubiri injili wakati wowote, ukifaao na usiokufaa, epuka udhuru wa mwili au kazi, pinga sana hapo jiwekee ratiba yako, ili upate sehemu ya kuwaeleza wengine habari za Yesu Kristo anayewaokoa wanadamu.

Tukizingatia hayo. Tutakuwa tumemshinda shetani ndani na nje. Hatujafungwa ndani wala nje.

Bwana akubariki

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

Kongwa ni nini kwenye biblia?(Wagalatia 5:1)

VITA DHIDI YA MAADUI

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

Rudi Nyumbani

Print this post

Nini maana ya sulubu/ sulubisha?

Neno sulubu huzaa kusulibisha/kusulubisha,

Maana ya Sulubu, ni kuadhibisha kwa kuning’iniza kwenye mti wa msalaba, au nguzo iliyonyooka, kwa kufungwa au kugongelewa miguu na mikono, na kuacha hapo mpaka ufe.

Hii ni aina ya adhabu ya kifo, ambayo ilitumika zamani, kwenye falme zilizokuwa na nguvu na katili kama Rumi.

Watu walioshitakiwa kwa makosa makubwa ikiwemo uhaini, au uuaji, uvunjaji amani, hawakupewa adhabu ya kawaida ya kifo kama vile kukatwa kichwa na kufa mara moja,. Bali walipewa adhabu kali kama hii, lengo lake ni kumfanya Yule mshitakiwa kupitia mateso makali ya muda mrefu kabla ya kufa, kwasababu, baada ya kuning’inizwa kwake pale msalabani itamchukua siku tatu mpaka wakati mwingine wiki hadi kufa. Hivyo kipindi chote hicho unatakuwa unateseka tu pale mtini.

Hiyo ndio adhabu waliyoichagua kwa mwokozi wetu Yesu Kristo, ambaye hakuwa na hatia yoyote, wala kosa, jambo ambalo hata mtawala yule Pilato alilishuhudia kuwa hakukuwa na uovu wowote ndani yake. (Luka 23:4). Lakini kwasababu ilipasa maandiko yatimie ili sisi tupate ukombozi mkamilifu, ndio maana ilimpasa Yesu aadhibiwe vikali, ili mimi na wewe tupokee ONDOLEO LA DHAMBI. Kwa kifo chake.

Gharama aliyoilipa ni kubwa sana, kusulubiwa uchi wa mnyama, bila nguo, kudhalilishwa na kupigwa, na kuharibiwa mwili wote. Ni kwasababu mimi na wewe tupokee msamaha wa dhambi, tuepushwe na hukumu ya milele ya jehanamu ya moto.

Ndio maana maandiko yanasema..

Waebrania 2:3  sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia.

Je! Umempokea Yesu maishani mwako?

Ikiwa ni la! Basi waweza kufanya hivyo sasa, kwa kubofya hapa ili upate mwongozo wa sala hiyo. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

Tofuati kati ya kifo na mauti ni ipi?

NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU.

Rudi Nyumbani

Print this post

SIFA SITA (6), ZINAZOIKAMILISHA ILE SIKU YA BWANA ITISHAYO.

Nyakati tunazoishi ni za hatari kubwa, zaidi hizo zinazokuja wakati si mwingi ndio za hatari mno. Watu wengi hawajui kuwa mwisho umekaribia sana, dunia imekwisha, na kwamba SIKU YA BWANA, ipo mlangoni.

Siku ya Bwana ni nini?

Siku ya Bwana ni kipindi fulani maalumu ambacho Mungu amekiandaa ili kuuharibu huu ulimwengu pamoja na watu wote waovu waliopo duniani, na mifumo yao mibovu. Na hiyo itakuja baada ya kanisa la Kristo kunyakuliwa 

Tukisoma katika kitabu cha Sefania tunaelezwa kwa urefu juu ya sifa kuu za siku hiyo itakavyokuja. 

Ametaja sifa zake sita (6), kwa kuziita “siku ya”..”siku ya”…”siku ya”

Tusome..

Sefania 1:14-16

[14]Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!

[15]Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,

[16]Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.

1) Anaanza kwa kusema ni Siku ya ghadhabu.

Ghadhabu ni zao la hasira, na hasira hufuatana na mapigo. ndio hapo tunaposoma kitabu cha ufunuo 16, tunaona kipindi hicho kikifika wale malaika saba watavimimina vile vibakuli vyao saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi. na kitakachofuata kwa tendo lile ni mapigo, ndio hapo utaona majipu mabovu, yanawatokea wanadamu, na tena jua linashushwa na kiwaunguza watu, mpaka wanafikia hatua ya kumtukana Mungu.

Ufunuo 16:8-9

[8]Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto. 

[9]Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu. .

2) Siku ya fadhaa na dhiki.

Dhiki na fadhaa ni taabu ambazo mtu anazipata hususani kutoka katika mazingira ya nje. Ukiendelea kusoma sura ile ya 16, utaona mito, chemchemi na bahari zote zinageuzwa kuwa damu, wanadamu wanakosa maji. hofu na mashaka ya mabadiliko ya nchi. Duniani hatakuwa ni mahali penye utulivu, tengeneza picha unaishi katika dunia ya namna hii, utastahimili vipi. Bwana anasema wanadamu watafuta kifo, lakini kifo kitawakimbia.

Ufunuo 16:3  Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.

4  Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu. 5  Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;

6  kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili

3) Siku ya uharibifu na ukiwa

Sio tu mapigo na dhiki, lakini pia kuharibiwa kwa huu ulimwengu na mifumo yake kutafuata, kwasababu biblia inasema siku hiyo kutatokea tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijawahi kutokea tangu dunia kuumbwa, mpaka visiwa kuhama, inasema moto utatokea kuharibu huu ulimwengu, mfano wa sodoma na gomora na mfano wa kipindi cha gharika.

2 Petro 3:10-12

[10]Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 

[11]Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, 

[12]mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? 

4) Siku ya giza na utusitusi.

Giza na utusitusi unaozungumziwa hapa ni ule wa rohoni. ni kipindi ambacho watu watautafuta uso wa Mungu lakini hawatauona, ndio maana Yesu alisema imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyetupeleka maadamu ni mchana, usiku waja asioweza mtu kufanya kazi. watu watamwita Mungu, lakini hakutakuwa na majibu yoyote.

Mithali 1:27 Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.  28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.  29 Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha Bwana.  30 Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote

5) Siku ya mawingu na giza kuu. 

Vilevile kwa jinsi dunia hii itakavyoharibiwa jua na mwezi na nyota vitazuiliwa.. duniani kutakuwa na giza ambalo halijawahi kutokea, na hayo ndio yatakuwa yale mapigo ya mwisho mwisho kabisa yatakayokuwa yanaukaribisha ujio wa pili wa Yesu duniani.

Vilevile wingu zito litatandaa angani, mawe mazito yatashuka duniani kama talanta, jiwe lenye uzito wa kg 34, hatujui itakuwa ni mvua ya namna gani, hiyo.

Ufunuo 16:18-21

[18]Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. 

[19]Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 

[20]Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 

[21]Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.

6) Anasema pia ni siku ya tarumbeta na ya kamsa.

Kamsa ni kelele za vita. Maana yake katika kipindi hicho cha siku ya Bwana, vita vitakuwepo, ndio ile vita ya mwisho ijulikanayo kama Harmagedoni.Mataifa yote yatahusika. lakini Bwana awataua watu wengi sana. damu nyingi sana zitamwagika. ni nyakati ambayo hakutakuwa na shujaa, kila mtu ataomboleza mpaka mashujaa, wafalme na matajiri wote hao watalia sana, pesa zao hazitawasaidia wataomba milima iwaangukie wafe haraka, kuliko kushuhudia huo mfululizo wa mapigo ya Mungu mwenyezi.

Na ndio maana ukimalizia kusoma mistari inayofuata pale kwenye kitabu cha Sefania anasema

Sefania 1:17-18

[17]Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. 

[18]Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha. 

Ndugu yangu, ikiwa unyakuo ukipita leo, fahamu haya utayashuhudia, wakati huu si wa kumbelelezewa wokovu, ni kuamka na kuikimbilia neema, nyakati mbaya zimekaribia, haya mambo ya duniani yatakufikisha wapi? uhai wako umefichwa wapi? Ukifa leo huko uendako utakuwa mgeni wa nani.Kwasababu huko nako kuna mateso makali vilevile kama hapa.

Embu dhamiria kutubu na kumgeukia Bwana Yesu leo, akupe msamaha wa dhambi bure. Hukumu ya Mungu inatisha. 

Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu maishani mwako. Na unatamani leo Yesu akutue hiyo mizigo ya dhambi. Basi waweza kusali sala hii kwa imani. Ukijua Kristo wakati wote yupo kutuokoa. Kumbuka kinachotangulia ni kuamini. Kisha ndipo kukiri.

Hivyo

Hapo ulipo piga magoti, kisha dhamiria moyoni mwako kuyasema maneno haya, na moja kwa moja leo, utapokea msamaha wa dhambi zako hapo hapo ulipo, 

Sema.

Ee Bwana Yesu asante kwa kuja kwako duniani, kutukomboa sisi wanadamu tuliokuwa tumepotea, kwa kifo chako pale msalabani na kufufuka kwako. Ninaamini kuwa wewe ndio Bwana na mwokozi, nami napokea neema uliyonipa bure ya ondoleo la dhambi, tangu leo ninakubali kufanyika mwana wako, na kugeuka kuacha njia mbaya za kale. Asante kwa kuwa unanipa nguvu hiyo na kuliandika leo jina langu katika kitabu cha uzima. Nami nafanyika kiumbe kipya. Asante kwa kunipokea, asante kwa kunisamehe, Asante kwa kunifanya mwana wako.  Ninaomba nikiamini katika jina la Yesu Kristo Amen.

Basi ikiwa umesema sala hiyo toka moyoni kwa imani. Tayari umeshaupokea wokovu. Na hivyo hatua zilizobakia kwako ili kuitimiza haki yote, ni wewe kubatizwa. Tafuta mahali wabatizwapo kwa maji tele, na kwa jina la Yesu Kristo.  Ikiwa utahitaji msaada pia waweza kuwasiliana nasi kwa namba zetu chini.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani

Print this post

NI NJIA GANI MTU AITUMIE AWEZE KUSHINDA TAMAA NA VISHAWISHI?

Nakusalimu katika jina la Bwana Yesu,

Ni swali ambalo linaulizwa na wengi, je ni kweli mtu anaweza kuzishinda tamaa za mwili? Au vishawishi vyake?  Anaweza kweli kuacha dhambi ya uzinzi, au kujichua,au kutazama picha za ngono, au ulevi, au miziki, n.k.?

Jibu la kibinadamu ni hapana! Na ndivyo ilivyo.. Lakini jibu la Mungu ni ndio, kwasababu alisema kwake yote yanawezakana.(Mathayo 19:26).

Akili yako itakuambia haiwezekani, kwasababu hujajua kanuni ya kuwezekana. Mimi niliwahi pia kufikiri hivyo hapo nyuma. Lakini nikathibitisha kile maandiko yanasema, kuwa hilo jambo linawezakana, Mungu hasemi uongo. Sasa utauliza ni kwa namna gani?

Awali ya yote ni vema ukafahamu kuwa hakuna mwanadamu yoyote aliyeumbwa na uwezo wa kuzishinda tamaa za mwili.  Hayupo. Vilevile anayejaribu kufanya hivyo kwa akili zake, na kwa nguvu zake peke yake, pia anajidanganya mwenyewe kwasababu, utafika wakati atayarudia yaleyale tu. Ikiwa wewe ni mmojawapo unayejaribu kupambana kwa nguvu zako, utavunjika moyo ni heri leo ujue kanuni sahihi ya kuitumia.

Sasa ni kwa namna gani tutaweza kushinda hali hizo za mwili?

Kanuni imetolewa kwenye mistari huu.

Wagalatia 5:16  BASI NASEMA, ENENDENI KWA ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17  Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

Anasema “Enendeni kwa Roho”, biblia ya kiingereza inatumia neno “Walk in spirit” akiwa na maana “Tembeeni katika Roho”

Wakristo wengi, wanampokea kweli Roho Mtakatifu, wanajazwa Roho kabisa, lakini ni wachache sana “wanaotembea katika Roho Mtakatifu”.

Ni sawa, na mgeni unayemkaribisha nyumbani mwako. Halafu unapokwenda kazini, au matembezini unamwacha nyumbani, hajui kingine chochote kuhusu wewe zaidi ya maisha ya palepale unayokutana naye nyumbani. Ndivyo anavyofanywa Roho Mtakatifu na waamini wengi.

Tunamtambua Roho tu, pale tunapokuwa ibadani, lakini maisha nje ya ibada, sisi ni watu wengine kabisa. Na hapo ndipo linapokuja tatizo kwanini vishawishi na tamaa zinatushinda. Kwasababu hatutembei na  Roho Mtakatifu.

Ukweli ni kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayekusaidia wewe kuua nguvu ya tamaa ndani yako. Na hivyo anahitaji uwepo wake uwe nawe wakati wote, ili hilo liwezekane.  Ni sawa na GANZI, anayopigwa mgonjwa, wakati ganzi, ipo mwilini hawezi kusikia maumivu, lakini inapoisha maumivu yanamrudia kwa kasi, hivyo anahitaji kuongezewa ganzi nyingine, ili aendelee tena kukaa bila maumivu.

Ndivyo alivyo Roho Mtakatifu, huna budi kufahamu ni namna gani atakupiga ganzi, ili uweze kuishi maisha ya ushindi hapa duniani. Na kanuni si nyingine zaidi ya Kuenenda katika Roho. Kuanzia leo acha kupambana na hizo tamaa kivyako, hutazishinda, pambania kujawa na Roho lakini pia kutembea naye maishani mwako.

Sasa Tunatembeaje katika Roho?

Kwa kuzingatia mambo makuu matatu.

1). KWA KUWA WAOMBAJI WA DAIMA:

Watu wengi wanapofikiria maombi akili zao zinakwenda moja kwa moja kudhani ni wasaa kwa  kuwasilisha mahitaji yao. Lakini maombi si mahali tu pa mahitaji, bali ni mahali pa kujazwa Roho. Hivyo kama mtoto wa Mungu uingiapo kwenye maombi yako kila siku tumia nafasi ya kuomba ujazwe Roho Mtakatifu, akuongoze, akupe nguvu, akujenge nafsi yako, uimarike. Hivyo yakupasa uingie katika maombi ya ndani kabisa sio juu juu ya kutimiza ratiba, bali ya kuweka mawazo yako yote kwa Roho Mtakatifu, akujawe ndani yako, hili ni muhimu sana, kwasababu yeye ndio atakayekusaidia.

Sasa kwa jinsi unavyoomba kwa muda mrefu, na kwa mara kwa mara, ndivyo unavyozidi kumpa nafasi Roho wa Mungu kukujaza nguvu, na mwisho unaona vitu kama tamaa ni vidogo sana, kwasababu ganzi imeshaingia vya kutosha ndani yako.

Jambo hili linatakiwa liwe ni la kila siku(Waefeso 6:18). Kama wewe sio mwombaji, kiwango cha Roho kitakuwa kidogo ndani yako, mwili utakulemea tu, haijalishi upo kwenye wokovu kwa miaka 50, utasumbuliwa tu na tabia za mwilini, Ndio maana tunasisitizwa tuombe kila wakati. Maombi ni kila wakati, kila saa, omba kwa akili, pia omba wa kunena kwa lugha kwa jinsi Bwana atakavyokujalia. Lakini elekeza mawazo yako katika kujazwa na yeye, ukiwa ni mwombaji wa wiki mara moja uendapo kanisani jumapili, au mwezi mara moja, hapo unapoteza muda, hutembei katika Roho. Uthibitisho wa anayetembea kwa Roho ni Yule ambaye ni mwombaji wa kila siku.

2) LIWEKE NENO LA MUNGU AKILINI MWAKO WAKATI WOTE.

Neno la Mungu, husisimua roho zetu wakati wote. Na adui anachohakikisha ni kutufanya sisi tulisahau, hivyo mambo mengine yatawale akili zetu. Anajua akili yako ikiwa inatafakari habari na maonyo katika biblia, itakaa mbali na njia mbovu.

Pale adui anapotaka kukujaribu ukifiria wema Mungu aliomtendea Yusufu, kwa kuukimbia uzinzi, anajua utapata nguvu, pale Mungu alipomtukuza Ayubu kwa kukaa mbali na maovu, utapata nguvu, jinsi Danieli alivyokuwa mwaminifu, Mungu akamwinua anajua utaendelea katika uaminifu wako . Hivyo hapendi, wewe utawaliwe na Neno kichwani, anataka utawaliwe, na movie, utawaliwe na mipira, utawaliwe na siasa, na  mambo ya mitaani, basi. Akili yako izunguke hapo, lakini isizunguke kwenye BIBLIA.

Ukijizoesha kilizungusha Neno la Mungu, na ahadi za Mungu kichwani mwako. Tafsiri yake ni kuwa unamzungusha Roho Mtakatifu, katika ulimwengu wako wa maisha. Na ni nini atakachokifanya kwako kama sio kukusimua roho yako, kwa Neno lile. Hivyo unayashinda yote kirahisi. Watu hawajui Neno la Mungu ndio Roho Mtakatifu mwenyewe wanasema nao.

Yohana 6:63  Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA NI ROHO, TENA NI UZIMA.

Soma sana Neno, lakini zaidi, lidumu kichwani pako, kutwa nzima. Huu ni ulinzi kamili, na silaha madhubuti ya mambo yote ya mwilini.

3) FANYA MAAMUZI YA GEUKO LA KWELI.

Maamuzi ni kutii. Ukiwa mtu wa nia nia mbili, unataka kumfuata Yesu, na wakati huo huo hutaki ulimwengu ukuache nyuma. Hapo napo unamzuia Roho wa Mungu kufanya kazi yake vema ndani yako. Unaweza ukawa ni mwombaji kweli lakini kama moyoni mwako hujaamua kufanya maamuzi, bado ni kazi bure.

1Yohana 2:15  Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16  Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

17  Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele

Ukiamua kumfuata Yesu, fahamu kuwa hii dunia sio fungu lako tena, anasa sio rafiki tena kwako. sio tu na ulimwengu lakini pia na nafsi yako.Ndipo hapo unachukua hatua za dhahiri kabisa katika  imani yako, kama ulikuwa na vichocheo vyote vinavyokusababishia utende dhambi, ndio hapo Yesu anakuambia ukate, usione huruma kutupa hizo nguo za kizinzi ulizozoea kuzivaa, kuachana na huyo girlfriend, kuacha hizo muvi za kizinzi, unazoangalia, usione shida kuacha kampani zako za walevu, usijihurumie hata kidogo, huku ukiwa na mawazo kuwa unafanya hivyo kwasababu ya Kristo ndiye atakayekupa neema ya kushinda.

Ijapokuwa mwanzoni utaona shida kwasababu unafanya kimwili, kwa utiifu wako huo baadaye Roho wa Mungu atakunasa, kwasababu umempa umiliki wote wa maisha yako. Ganzi kubwa sana itaingia ndani yako,.

Ukizingatia mambo hayo matatu, kila siku katika maisha yako. Basi wewe unaenenda kwa Roho. Hakuna litakalokuwa gumu kwako. Kwasababu si kwa nguvu zako bali kwa nguvu za aliye ndani yako, unayashinda hayo.

Wagalatia 5:25  Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.26  Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

KWANINI MUNGU HAJIBU MAOMBI?

Roho Mtakatifu ni nani?.

Rudi Nyumbani

Print this post

Kulaumu/ Lawama ni nini kibiblia?

Je! wakristo tunalaumiwa?

JIBU: Ni mashtaka au maneno  Fulani yanayotolewa dhidi yako, yanayolenga kutoridhishwa na mwenendo, au maneno au tabia yako.

Tunaweza tukawa watoto wa Mungu, na bado siku ile ya mwisho tukalaumiwa na Mungu.  Utauliza ni kwa namna gani?

Ni kweli deni letu la mashtaka limeondolewa pale msalabani kwa Kifo cha Yesu Kristo. Na kwamba mtu anapomwamini tu Yesu Kristo haukumiwi, bali anaingia uzimani. Tafsiri yake ni kuwa hana lawama la hukumu ya jehanamu (Wakolosai 1:21-22)

Lakini, kumbuka wewe “unahesabiwa” kuwa mwenye haki. Lakini kiuhalisia “huna haki ndani yako”. Yaani kwa asili wewe huna kitu chochote kizuri ndani yako mbele za Mungu, na kimsingi huo sio mpango Mungu aliokusudia kwa mwamini. Mungu anataka amwokoe mtu wake, na wakati huo huo awe mkamilifu kama yeye.

Ndio hapo hatupaswi kuichukulia NEEMA ya Mungu kama fursa ya sisi kupumzika katika dhambi, au kupuuzia matendo ya haki. Au kutokuonyesha bidii yoyote ya Kufanana na Kristo.

Maandiko yanasema watu wengi wataonekana kuwa na lawama, mbele za Kristo, kwa kushindwa tu kurekebisha baadha ya mienendo yao, walipokuwa hapa duniani.

Kwa mfano maandiko haya yanaeleza baadhi ya mienendo, hiyo; moja wapo ni  kukaa katika  Mashindano, au manung’uniko ndani ya wokovu hupelekea utumishi wako,kulaumiwa .

Wafilipi 2:14  “Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano,  mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu”

Vilevile kutofikia upendo  na  Utakatifu, ni zao la lawama.

1Wathesalonike 3:12  Bwana na awaongeze na KUWAZIDISHA KATIKA UPENDO, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;

13  apate kuifanya imara mioyo YENU IWE BILA LAWAMA KATIKA UTAKATIFU mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.

Tufanye nini ili tuweze kuepuka lawama, na tuwe na ujasiri, mbele za Kristo siku ile?

Ni kuitendea kazi neema ya Kristo maishani mwetu. Kwa kumtii yeye, na kumfuata kwa mioyo yetu yote, nguvu zetu zote, akili zetu zote na roho zetu zote, Ambayo inafuatana pia na bidii katika kujitenga na maovu, Ndipo itakuwa rahisi sisi kuyashinda,kwasababu ataiachilia nguvu yake ya ushindi itende kazi ndani yetu, na hivyo tutajikuta tunakaa mbali na mambo ya kulaumu.

1Wathesalonike 5:22  jitengeni na ubaya wa kila namna.

23  Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu MHIFADHIWE MWE KAMILI, BILA LAWAMA, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

Hivyo ndugu uliyeokoka, tambua kuwa kila mmojawetu atatoa hesabu yake mbele za Mungu, siku ile. Hatuna budi sasa kuishi kama watu wanaotarajia TAJI bora, na sio watu wasio na mwelekeo wowote. Bwana asije akaona “neno ndani yetu”, mfano wa yale makanisa 7  tunayoyasoma katika Ufunuo 2&3, ambayo Yesu aliyapima akaona mapungufu. Hivyo tuishi kama watu wenye malengo, sio tu wa kukombolewa, bali pia wa kukamilishwa.

2Wakorintho 6:3  TUSIWE KWAZO LA NAMNA YO YOTE KATIKA JAMBO LO LOTE, ILI UTUMISHI WETU USILAUMIWE; 4  bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;

5  katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga;

6  katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki;

7  katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;

8  kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli.

Bwana akubariki.

Hivi ni baadhi ya vifungu vingine utakavyokutana na Neno hilo pia (1Timotheo 3:1-7, Luka 1:5-6)

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!

Mtakatifu ni Nani?

HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.

MUNGU MWENYE HAKI.

Rudi nyumbani

Print this post

FAHAMU SEHEMU NNE (4)  APANDWAPO MWAMINI.

Shalom.

Sisi kama waamini tunafananishwa na mche, au zao Fulani linalopandwa. Kwamfano ukisoma

Zaburi 1:1-3 Inasema..

1 Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 

2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3 NAYE ATAKUWA KAMA MTI ULIOPANDWA KANDOKANDO YA VIJITO VYA MAJI, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

Hii ni kufunua kuwa mtu yeyote mwenye haki (Aliyeokoka), huwa anapandwa mahali Fulani rohoni.

Sasa ni vema kufahamu maeneo Mungu aliyoyaruhusu/ aliyoyakusudia sisi tupandwe, na hii ni muhimu kujua ili tuwe na amani, kwasababu wakristo wengi wanapoona kwanini baadhi ya mambo yapo hivi, huishia kurudi nyuma, au wengine kukata tamaa kabisa, au wengine kupoa, na wengine kulegea legea. Lakini kwa kufahamu haya, nguvu mpya itakuja ndani yako.

Hizi ni sehemu nne (4), Ambazo sisi kama waamini tunapandwa.

1) TUTAPANDWA PALIPO NA  MAGUGU

Mathayo 13:24  Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;

25  lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

26  Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.

27  Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?

28  Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?

29  Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.

30  Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.

Ukiendelea mbele mstari wa 36-43, utaona Yesu anatolea ufafanuzi, wa mstari huo akisema hizo mbegu njema ni wana wa Ufalme, na konde hilo ni ulimwengu, na magugu ni wana wa ibilisi. Hivyo vyote viwili vimeruhusiwa vimee katika shamba hilo hilo moja la Mungu. Vishiriki neema sawa sawa, lakini mwisho, ndio vitofautishwe.

Kufunua kuwa tumewekwa pamoja na waovu, kamwe hatutakaa tuwe sisi kama sisi tu duniani, na hivyo basi tuwe tayari kusongwa na shughuli zao mbaya, kuudhiwa nao wakati mwingine, tuwapo kazini, majumbani, mashuleni, na wakati mwingine hata makanisani, watakuwepo. Na kibaya zaidi tuwe tayari kuona wakibarikiwa kama sisi tu tubarikiwavyo, watapokea mema yote kama tu wewe, kwasababu mvua ileile inyweshayo kwako itawapata na wao.

 Lakini Bwana anataka nini?

Anataka tuwapo katika mazingira hayo ya watu waovu tusifikirie kujitenga, na kutafuta mahali petu wenyewe tuishi, Yesu alisema Baba siombi uwatoe ulimwenguni, bali uwalinde na Yule mwovu, Bwana atakata tuwapo katikati yao tuzae matunda ya haki, kama Danieli alivyokuwa Babeli kwa wapagani, kama Yusufu kwa Farao, kama Kristo kwa ulimwengu. Vivyo hivyo na wewe kwa mume/mke wako asiyeamini, kwa majirani zako wachawi, kwa wafanyakazi wenzako walevi. Angaza nuru yako usijifananishe na wao, wala usingoje siku utengwe nao, jambo hilo linaweza lisitokee. Hivyo weka mawazo yako mengi katika kuangaza Nuru kuliko kutengwa na waovu. Kwasababu ni mapenzi ya Mungu tuwepo miongoni mwao.

2) TUTAPANDWA KATIKATI YA MITI MINGINE MEMA.

Bwana Yesu alisema tena, mfano huu;

Luka 13:6  Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.

7  Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?

8  Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi;

9  nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.

Tafakari huo mfano, Mtu huyu alikuwa na shamba la mizabibu tu! Lakini akajisikia moyoni mwake apande na mti mmoja wa TINI katikati ya shamba lake. Matokeo yake ni kwamba ule mtini ukagoma kuzaa. Baadaye  akataka kuukata. Akitufananisha na sisi. Upo wakati utapandwa katikati ya jamii nyingine ya watu. Na Mungu atatarajia uzae matunda yaleyale ya wokovu wako uliopokea mwanzo. Je! Utafanya hivyo au utalala?

Hili ni jambo ambalo linawaathiri waamini wengi, pale panapohama na kwenda ugenini, mfano labda kasafiri kaenda mkoa mwingine, sasa kwasababu kule hakuna wapendwa wa namna yake, basi anaamua kuwa vuguvugu hamzalii Mungu matunda yoyote, kwasababu kule  hawapo wakristo. Mwingine amesafiri nje ya nchi. Mbali sana na watu wenye imani ya Kristo. Kwasababu yupo kule anasema mimi nipo peke yangu, siwezi kufanya lolote la Kristo. Ndugu usifikiri hivyo, Bwana anakutaka uzae matunda sawasawa, bila kuangalia ni wewe tu peke yako upo hapo. Kama ni kuwashuhudia wengine habari njema, wewe fanya. Timiza wajibu wako, usiangalie kundi au dhehebu, au jamii nyingine ya waamini waonaokuzunguka. Wewe timiza wajibu wako hivyo hivyo. Bwana akuone unazaa. Kwasababu kwa namna moja au nyingine hatuwezi kuyaepuka mazingira mapya, ambayo tutajikuta tupo sisi tu wenyewe. Tufanye nini? Kumbuka tu mtini ulio katikati ya mizeituni. Usiwe mlegevu.

3) TUNAPANDWA  JUU YA MITI MINGINE.

Tofauti na sehemu mbili za kwanza, ambazo ni katikati ya magugu, na katikati ya miti mingine. Lakini pia tunapandwa juu ya miti mingine. Hii ikiwa na maana, “tunapachikwa” juu ya mti uliokatwa. Wana wa Israeli, walifananishwa na mzeituni halisi, na sisi mataifa mizeituni mwitu. Hivyo wao walipoikataa neema, basi wakakatwa,tukapachikwa sisi, neema ikatufikia pia.

Warumi 11:17  Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,

18  usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe

Na hivyo hapa tulipo tumepachikwa juu ya shina lingine. Na hivyo yatupasa tuwe makini, na kuuchukulia wokovu wetu kwa kumaanisha  sana, kwasababu na sisi tusiposimaa tutakatwa. Mhubiri mmoja wa Injili wa kimataifa aliyejulikana kwa jina la Reignhard Bonnkey, mwanzoni mwa huduma yake, Mungu alimwambia nenda kanitumikie, yeye akawa anasua-sua, Mungu akamwambia neema hii niliyokupa alipewa mwingine akaikataa, na hivyo itaondoka kwako na kwenda kwa mwingine usipotii. Aliposikia vile alikubali kutii kwa moyo wote, akaenda kuhubiri injili. Kuonyesha kuwa sisi ni wa kupachikwa, sio shina. Tuipokee neema kwa kuogopa na kutetemeka (Wafilipi 2:12). Usiwe mkristo vuguvugu, tumia muda wako vema, mzalie Mungu matunda. Kwasababu ulipachikwa tu, kwa kosa la mwingine.

4) TUNAPANDWA KWENYE UDONGO ULIORUTUBISHWA SANA.

Fuatilia habari hii,

Marko 11:12  “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.

13  Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.

14  Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”

Kama tunavyoifahamu hiyo habari asubuhi yake Bwana Yesu alipopita karibu na njia hiyo, ule mti ulionekana umekauka kabisa kabisa. Lakini swali la kujiuliza ni kwanini aulaani, wakati haukuwa msimu wake wa kutoa matunda? Mbona ni kama ameuonea tu?

Ukweli ni kwamba Yesu aliona mti ule kwa mazingira uliokuwepo ulistahili kuwa na matunda hata kabla ya msimu. Kwa namna gani, chukulia mfano wa mazao ambayo yanastawishwa  kwa kilimo cha kisasa, mfano “banda kitalu”(green house), kulingana na matunzo yake, huwa yanastawi kwa haraka na kuzaa ndani ya muda mfupi. Kwasababu yamerutubishwa sana, kwa madawa na mbolea na kuwekewa mazingira rafiki mbali na wadudu waharibifu, mfano wa kuku wa kisasa, ndani ya wiki 6 wamekomaa, lakini matunzo yao hayawezi kama ya wale kuku wa kienyeji ambao wanaachwa wakajitafutie.

Sasa fikiri kama muda wote huo unapita halafu hawazai/hawakui, wanafanana na wale wa kienyeje, ni nini watarajie? Kama sio kuondolewa.

Ndivyo ilivyo kwetu sisi, tunapookoka, muda huo huo tunapokea ROHO MTAKATIFU. Huyu ndiye anayetupa uwezo na nguvu, ya kumshuhudia, na kuzaa matunda ya haki. Hivyo hatuhitaji tena kusubiri mpaka miaka Fulani ipite kama watu wa zamani, ambao walikuwa bado hawajakaliwa na Roho. Bali wakati huo huo tunapookoka na sisi tunawafanya wengine kuwa wanafunzi.

Hatupaswi kujiona sisi ni wachanga kiroho, au watoto, Bwana atakuja ghafla akikosa matunda atatuondoa, na sisi tutabakia kudhani wakati ulikuwa bado.

Hivyo ndugu, fahamu kabisa tayari tumesharutubishwa, usingoje wakati Fulani ufike, hapo hapo fanya jambo kwa Bwana, waeleze wengine habari ya wokovu wamjue Mungu. Wataokoka, usihofu kiwango chako cha kujua maandiko, anayewashawishi watu ni Mungu na sio wewe. Hivyo hubiri kwa ujasiri na Mungu atakuwa na wewe.

Bwana akubariki.

Kwa kufahamu sehemu hizo kuu nne (4), itoshe kutukumbusha mwenendo wetu hapa duniani, uzidi kuwa katika uvumilivu, hofu, wajibu na bidii. Ili tusijikwae, au kufa moyo.

Maran Atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

UTENDAJI KAZI MWINGINE WA ROHO MTAKATIFU USIOUFAHAMU

SIRI YA KUASI KATIKA KANISA LA MUNGU.

JE! WEWE NI MBEGU HALISI YA KRISTO?

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

Rudi nyumbani

Print this post

Yesu kuvishwa taji la miiba kichwani, kulifunua nini?

SWALI: Yesu kuvishwa taji la miiba kichwani alipokuwa anasulubiwa kulikuwa kuna funua nini rohoni?


JIBU: Kila tendo alilotendewa Yesu katika kipindi cha mateso yake lilikuwa lina ufunuo wake rohoni. Tunajua wale askari waliposikia kuwa yeye ni mfalme, muda ule ule walimvisha vazi la kifalme, kisha wakampa fimbo, na baada ya hapo wakasokota taji la miiba, wakamvisha kichwani, kisha wakaanza kumdhihaki, huku wakimpiga wakisema..  Salamu! Mfalme wa Wayahudi!

Yohana 19:2  “Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. 3  Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi”

Tunajua lengo la wale maaskari kumvisha miiba ni kumfanya aumie zaidi, lakini upo ufunuo mkubwa rohoni, pengine kwanini asingevishwa la matambara mabovu, au taji la udongo, au la vyuma vyenye ncha kali, badala yake wakaona miiba.

Kibiblia, miiba, huwakilisha “mahali palipolaaniwa”.

Adamu alipoasi, Mungu alimwambia ardhi imelaaniwa kwa ajili yako, hivyo itatoa miiba na michongoma. Na matokeo yake ni kwamba italimwa kwa shida

Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;  18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;

Ndio maana shamba ambalo  halipaliliwi  au halitunzwi, matokeo yake ni kuwa linatoa miiba.

Mithali 24:30 Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.  31 Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka.  32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho.  33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! 34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha

Na vivyo hivyo rohoni, mioyo yetu inafananishwa na mashamba. 

Ukisoma ule mfano wa mpanzi, utaona mbegu(Neno la Mungu), lilipopandwa, zipo ambazo ziliangukia kwenye miiba (yaani mahali ambapo hapajafyekwa na kupapaliwa), ndipo pale kwenye miiba, na mwishowe zikakua na kumea. Lakini zikasongwa na ile miiba hazikashindwa kuzaa.

Yesu akatoa tafsiri yake, akasema, miiba ile ni “anasa, udanganyifu wa mali, na shughuli za ulimwengu huu”.

Luka 8:14  “Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote”.

Sasa Yesu alipokuja kufa msalaba, alishughulika na jambo hilo kubwa, kubeba laana hiyo kubwa kwenye kichwa chake.

Akimaanisha kuwa ile nchi iliyolaaniwa (yaani mioyo wa mtu), kuanzia sasa ni mwisho. Imekwisha.

Miiba iliyokuwa inatoka mimi nimeichukua kichwani mwangu.

Moyo wa mtu kuanzia sasa, utaanza kuzaa matunda, na wala hautasongwa na anasa, wala udanganyifu wa mali, wala shughuli za ulimwengu huu, usiivishe chochote.

Hii ikiwa ni kweli kabisa.

Sisi tunaomwamini Yesu, moja kwa moja tunapewa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu (Yohana 1:12), na matokeo ya uwezo huo ni kuwa,  nguvu ya kusongwa na ulimwengu inakuwa ndogo, kwasababu Roho Mtakatifu aliyemwagwa ndani yetu anatusaidia, Kuukataa ulimwengu, na kuishi maisha ya utauwa. Utakuwa ulimwenguni lakini, hutasongwa na mambo yake. Kwasababu utafundishwa pia “kiasi” na Roho Mtakatifu.

Hivyo uwezo huu utakuja ndani yako, pindi tu unapomgeukia Kristo kwa kumaanisha kabisa, ambapo panaanza na kwa KUTUBU kwanza dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kugeuka,na kumfuata Kristo tangu huo wakati, na kisha kubatizwa, na kupokea Roho wake. Lakini nje ya hapo, huwezi kwenda popote.

Je! Umempokea Yesu?

Pasipo yeye huwezi ndugu kuushinda ulimwengu kwa nguvu zako, haiwezekani hata kidogo, hata ufanyeje haiwezekani,miiba itakusonga tu, dunia itakulemea tu, Unahitaji nguvu zake, kwa Roho wake Mtakatifu. Ili kuzipata maanisha tu kumgeukia,  na kusudia kutembea naye moyoni mwako.

Utaushinda huu ulimwengu. Wala hakuna mwiba wowote utakaomea kwenye moyo wako. Kwasababu Kristo alishayakomesha yote. Je! upo tayari kuokoka leo? Basi fungua hapa kwa mwongozo wa kimaombi>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.

Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?

Je vazi alilovikwa Bwana Yesu lilikuwa la Zambarau au Jekundu?

Mbaruti ni mmea gani? (Mathayo 7:16)

Rudi nyumbani

Print this post

Anaposema zijapokuwa nyekundu kama bendera, ana maana gani?

SWALI: Mungu anaposema dhambi zetu zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Ana maana gani, kwenye hilo neno bendera?

Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.  19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;


JIBU: Hapa ni Mungu anaeleza mambo mawili hayuhuso dhambi walizotenda watu wake.

  • Jambo la kwanza ni ukubwa/wingi wa dhambi walizonazo. Ndio hapo anafananisha rangi nyekundu sana, ukilinganisha na kitu kilicho cheupe sana mfano wa theluji.

Tunajua theluji inang’aa sana mfano wa jua, Kuonyesha ni jinsi gani hawa watu walivyokuwa mbali sana na ukamilifu, yaani jinsi gani walivyokuwa hawakaribii hata kidogo kuwa wema mbele za Mungu, walau wangeonekana wa rangu ya kijani, basi wangekuwa na afadhali, lakini ni mbali sana, wana rangi ya damu. Ndivyo ilivyokuwa Israeli yake.

  • Jambo la pili ni usugu wa dhambi uliokuwa ndani yao.Ndio hapo anafananisha na Bendera, ukilinganisha ni sufu nyeupe.

Zamani bendera nyingi zilichovywa katika rangi nzito nyekundu, inayodumu sana, kwasababu ni kitu cha kudumu muda mrefu, hivyo haikuhitajika rangi inayofubaa haraka. Sio tu bendera, lakini mpaka mavazi ya kifalme, au nguo za thamani za sufu.

Hivyo unaposoma habari za bendera hapo, si bendera ya kila rangi, mfano wa bendera tulizonazo sikuhizi zina rangi mbalimbali, zamani nyingi zilichovya kwa rangi  nyekundu. Hivyo Mungu anawaambia ijapokuwa ni nyekundu kama bendera, basi zitageuzwa na kuwa nyeupe kama Sufu, (akiwa na maana ambayo haijachovywa), Yaani Mungu anaweza kuiondoa hiyo rangi sugu, kwenye hicho kitambaa kana kwamba hakijachovywa kabisa.

Kufunua nini,

Yesu Kristo mwokozi wetu ndiye aliyetimiza huo unabii. Kuonyesha kuwa dhambi zote tulizotenda haijalisha ni nyingi kiasi gani, haijalishi ni mbaya namna gani yeye kwa damu yake anaweza kuzifuta kabisa kabisa. Dhambi tulizotenda haijalishi hazisameheki namna gani, hazineneki, ni sugu namna gani, yeye anao uwezo wa kuziondoa, kwa neema yake.

Swali ni je! Umesamehewa dhambi zako? Kama ni la! Unangoja nini kuipokea neema hii, ya WOKOVU mkuu namna hii? Pokea sasa msamaha wa dhambi kwa kutubu dhambi zako, na kumaanisha kuishi maisha mapya ya wokovu. Kisha moja kwa moja atakupokea na kukupa ondoleo la dhambi zako. Na baada ya hapo unahesabiwa kuwa huna dhambi yoyote, umestahili uzima wa milele, bure.

Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo basi, fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa maombi mafupi, na kwa kupitia sala hiyo kwa imani utakuwa umeshampokea Yesu Kristo, na amekusamehe dhambi zako zote.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Wale Nyoka wa Moto jangwani, walikuwa ni wa namna gani?

ALAMA ZA BENDERA YA ISRAELI ZINAWAKILISHA NINI?

MAANA YA RANGI KIBIBLIA.

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

Rudi nyumbani

Print this post

Merikebu ya Iskanderia kwanini itajwe jina lake ‘Ndugu Pacha’?

SWALI: Je kulikuwa na umuhimu wowote wa ile merikebu ya Iskanderia  walioipanda Paulo na wafungwa wengine kutajwa jina lake ‘ndugu Pacha’,?

Matendo 28:11  Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha. 12  Tukafika Sirakusa, tukakaa siku tatu. 13  Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli. 14  Huko tukakuta ndugu, wakatusihi tukae nao siku saba; na hivi tukafika Rumi.


JIBU: Safari ya mtume Paulo kama mfungwa, kutoka Kaisaria kwenda Rumi kuhukumiwa, haikuwa rahisi, iligubikwa na misuko suko mikubwa ambayo ilihatarisha maisha yao ukisoma Matendo 27, utaona mtume Paulo alionywa na Roho Mtakatifu kuhusu hatari hiyo lakini alipomwambia akida na manahodha, walipuuzia agizo lake, kwasababu watu wale hawakuamini habari za “miungu kabisa”. Maandiko yanasema walipoona upepo wa kusi umevuma kidogo tu, unaoruhusu kusafiri, wakadhani itakuwa hivyo mbeleni.

Lakini tunaona walipofika katikati, ghafla ile bahari iliwachafukia sana, upepo wa nguvu ukavuma merikebu yao ikawa karibu na kuzama, baadaye ilivunjika kabisa, na wakaokoka kwa shida kwasababu Mungu alimuhakikishia Mtume Paulo kuwa hakuna hata mmoja wao atakayeangamia.

Walipookoka na kufika kisiwa kile kilichoitwa Melita, walikaa miezi mitatu pale, kuruhusu hali ya hewa kutulia, kabla ya kuondoka. Lakini tunaona walipotaka kuondoka, safari hii wale mabaharia pamoja na maakida, hawakuichukulia safari yao kirahisi rahisi, yaani hivi hivi tu bila uongozo wowote. Ndipo walipojifunza kuchagua merikebu yenye “ulinzi wa kiroho”. Wakaipata hiyo ya Iskanderia iliyokuwa na nembo ya “Ndugu Pacha” kwa mbele.

Ndugu Pacha ni miungu ya kipagani ya kiyunani, ukisoma tafsiri nyingine za biblia imewataja moja kwa moja miungu hiyo kama Castor na Pollux. Ni miungu ambayo waliamini inahusika na ulinzi wa  safari za majini. Hivyo kwa imani yao ya kipagani, wakachukua nembo yao kuonyesha tunaiabudu na kuiheshimu hii miungu, na kutaka iwaongoze  salama katika safari yao, hawategemei tena elimu zao na nadharia zao.

Sasa tukirudi kwenye swali, linalouliza, kulikuwa ni umuhimu gani, hiyo merikebu ya Iskanderia kutajwa hadi nembo yake ya ndugu Pacha. Sababu ndio hiyo, Sio kwamba biblia inatufundisha, na sisi tukaweke miungu ya kipagani, kwenye vyombo vyetu vya usafiri kutuhakikishia ulinzi, hapana!

Bali inatufundisha Safari ya maisha hapa duniani. Kila mwanadamu anasafiri, lakini Je! Katika safari yako ni kitu gani kinakuongoza na kukulinda ili kukufikia ng’ambo yako salama?

Hakuna mwanadamu ambaye anaweza kujiongoza mwenyewe. Na ndio maana utaona hawa kwasababu hawakumjua Mungu wa kweli iliwabidi wakatafuta vinyago visivyoweza kuwasaidia kitu viwaongoze, na kama sio mtume Paulo kuwepo ndani ya Merikebu ile, safari yao ndio ingekuwa mbaya mara mbili zaidi. Hawakujua tu waliongozwa na Kristo Yesu pasipo wao kujua kwa neema tu!. Kwasababu watumishi wa Mungu walikuwa ndani.

Na sisi, hapa tulipo, fahamu kuwa maisha yako, bila KRISTO ni mauti mbele. Shetani hakuwazii mema, wala akili zako mwenyewe hazikusaidii ndugu, hiyo elimu ni kazi bure, huo uzoefu na ujuzi ulionao ni bure rafiki. Unamuhitaji Kristo, yeye ndio awe nembo  ya maisha yako. Mwamini leo akupe msamaha wa dhambi, mwamini leo akuokoe, safari yako iwe salama hapa duniani. Ukifa leo katika hali hiyo, fahamu ni jehanamu moja kwa moja. Umesikia injili ikihubiriwa mara ngapi, kwamba Yesu ni mwokozi lakini unapuuzia? Walio kuzimu wanatamani hata dakika moja, watubu hawawezi kwasababu kule hakuna maisha ya kuishi. Lakini wewe unaishi.

Usikiapo maneno haya, ugeuze moyo wako, umruhusu Kristo leo akuokoe, ikiwa upo tayari kumgeukia Bwana Yesu , na unatamani upate mwongozo wa kimaombi kwa ajili ya wokovu wako. Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii, bure.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

Rudi nyumbani

Print this post