Category Archive Mafundisho

IJUE KANUNI YA KUREJESHA NGUVU ZA KIROHO.

Je Imani yako imefifia?, je upendo wako umepoa?, je Amani yako imepungua?, na haki yako imepoa?.. Na hujui cha kufanya na ndani bado una haja sana ya kuwa na mambo hayo?.. Basi suluhisho lipo ndani ya biblia.

Ifuatayo ni kanuni moja nyepesi ya kurejesha joto la ROHO MTAKATIFU ndani yako. Kumbuka mtu aliyejaa Roho Mtakatifu ataonyesha matunda yafuatayo…

Wagalatia 5:22  “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23  upole, kiasi;…”.

Ikiwa mambo haya yalikuwa ndani yako lakini sasa huyaoni tena, au ikiwa hauna kabisa, basi tumia kanuni ifuatayo kuyarejesha/kuyajenga ndani yako.

KAA KARIBU NA WATU WATU WANAOMWITA BWANA.

Watu wanaomwita Bwana, kwa lugha nyingine ni watu waliookoka kikweli kweli,…Utauliza kwa namna gani?…Tusome maandiko yafuatayo..

2Timotheo 2:22  “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, PAMOJA NA WALE WAMWITAO BWANA KWA MOYO SAFI”.

Hapo mwisho anasema, ukatafute haki, Imani na upendo na amani “pamoja na wale wote wamwitao Bwana kwa moyo safi”.

Kumbe! Haki inapatikana kwa watu wanaomwita Bwana kwa dhamiri safi, kumbe tukikaa na watu waliomaanisha kumwita Bwana na kumtafuta basi Amani tutaipata, na upendo na Imani.

Kama maandiko yasemavyo kwamba “chuma hunoa chuma, Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake” (Mithali 27:17). Vivyo hivyo na sisi tunapokaa na watu wenye kumaanisha kumtafuta Mungu basi ule moto ulio ndani yao atahamia na kwetu pia.

Lakini tukijitenga na kubaki wenyewe, au tukijumuika na watu wengine wasio na nia ya dhati kumtafuta Bwana, ni ngumu kuuwasha ule moto wa Roho ndani yetu!, tutabaki kama tulivyo!.. Kanuni ni kukaa pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi!…Vile vile tunapojitenga na kuamua kukaa peke yetu kwa muda mrefu ni pia ni hatari!!.. Imani, amani, upendo na haki yako vinaweza kuathirika pakubwa.

Sasa tunawapatia wapi watu wamwitao Bwana kwa moyo safi?.

1.Katika kanisa lililo hai.

Hii ni sehemu pekee ambayo utawapata watu wamwitao Bwana kwa moyo safi, jiunge na kanisa la kiroho lililo karibu nawe, au hata lililo mbali ikiwa lililo karibu nawe halina utakatifu. Jumuika na watu hao, katika utii na unyenyekevu, na katika ibada zote, na hapo Roho Mtakatifu atakujenga ndani yako na kukujaza nguvu zake, utaona Imani yako inapata nguvu, upendo wako uliopoa unawaka tena, haki yako iliyopotea inarudi na Amani yako pia inahuika upya, na ifanye hiyo iwe desturi yako daima.

Waebrania 10:25 “wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine;..”.

Na utajuaje kanisa hilo, ni la kiroho?.

Kigezo cha kwanza ni mwonekano wa nje wa waabuduo wa mahali hapo!, ukiona mwonekano na mazungumzo ya waabuduo si ya kiMungu, kwamba wanazungumza kidunia na wanavaa kidunia, kiasi kwamba hauoni tofauti na mtu anayeenda disko na anayeshiriki mahali hapo, basi tuchukua tahadhari hapo si sehemu salama!.

Vile vile mafundisho yanayofundishwa mahali pale kama hayalengi TOBA, na UJIO wa PILI wa BWANA YESU, na UTAKATIFU wa MWILINI na ROHONI, pia hapo si sehemu salama, lakini kama kanisa lina vigezo hivyo vya Utakatifu wa kimafundisho na kimwonekano, basi ndani yake watakuwepo watu wamwitao Bwana kwa moyo safi, kaa hapo na utaona mabadiliko makubwa ya kiroho ndani yako.

Bwana akubariki.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

UTAYAFIKIAJE MANENO SAFI YA MUNGU?

KANUNI YA KUOMBA NA KUPOKEA.

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?.

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

Rudi nyumbani

Print this post

KAMA WEWE NI KIJANA, BASI FAHAMU YAFUATAYO NA UCHUKUE TAHADHARI!

Ikiwa wewe ni kijana basi fahamu basi fahamu mambo yafuatayo.

1.MAWAZO MABAYA YANAANZIA UJANANI.

Mwanzo 8:21 “Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, MAANA MAWAZO YA MOYO WA MWANADAMU NI MABAYA TANGU UJANA WAKE; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya”.

Mawazo ya kuidharau injili, mawazo ya ukaidi wa moyo na kiburi cha uzima yanaanzia ujanani.

Yeremia 22: 21 “Mimi nalisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako TANGU UJANA WAKO, KUTOKUITII SAUTI YANGU”.

   2. MUNGU ANATAFUTWA UJANANI NA SI UZEENI!.

Mhubiri 12: 1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”.

Maana yake katika uzee “haitawezekana kabisa” kumtafuta Mungu kama utapuuzia wito wa Mungu katika ujana wako!!!. Wakati wa Ujana ndio wakati wa kujifunga NIRA YA MUNGU iliyotajwa na BWANA YESU katika Mathayo 11:29.

Maombolezo 3:27 “Ni vema mwanadamu aichukue NIRA WAKATI WA UJANA WAKE.

28 Na akae peke yake na kunyamaza kimya; Kwa sababu Bwana ameweka hayo juu yake”.

   3. KAMA UTACHAGUA ANASA, BASI FAHAMU KUWA SIKU YA MWISHO UTASIMAMA HUKUMUNI.

Mhubiri 11:9 “Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya KWAMBA KWA AJILI YA HAYO YOTE MUNGU ATAKULETA HUKUMUNI”

Maana yake kama utachagua uzinzi katika ujana wako, au ulevi, au anasa nyingine yeyote basi pia jiweke tayari kusimama mbele ya kiti cha hukumu siku ile ya mwisho, ambapo maandiko yanasema kila mtu atatoa habari zake mwenyewe (Warumi 14:12), na tena kila neno la upuuzi litatolewa hesabu yake siku ile ya hukumu (Mathayo 12:36).

  4. NEEMA YA WOKOVU HAIKUBEMBELEZI.

Ufunuo 22:10 “ Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

11  MWENYE KUDHULUMU NA AZIDI KUDHULUMU; NA MWENYE UCHAFU NA AZIDI KUWA MCHAFU; NA MWENYE HAKI NA AZIDI KUFANYA HAKI; NA MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA”.

Ikiwa umechagua uchafu!, basi usiufanye kidogo!..ufanya sana, lakini kama umechagua USAFI, basi JITAKASE SANA, usiwe hapo katikati (vuguvugu!)..

   5. UTAKAPOKUWA MZEE UTAPELEKWA USIKOTAKA.

Yohana 21:18  “Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka”.

Uhuru ulionao si wa Daima, ipo siku utaisha, na wengine watakuwa na mamlaka juu yako…….

Je wewe kama kijana sasa umejipangaje?..je unawaza nini katika ujana wako huu? au unafikiri nini?…Kwanini usiamua kumgeukia Muumba wako leo!, na kuachana na udunia, na tamaa za ujanani, ambazo hazina faida yoyote Zaidi sana zina hasara nyingi?

2Timotheo 2:22 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi”.

Bwana Yesu akubariki.

Ikiwa unahitaji msaada wa kuokoka na ubatizo basi wasiliana nasi kwa namba zetu tajwa hapo chini.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.

Je! Mke wa ujana wako ni yupi kibiblia?

ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.

Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?

Nini tofauti ya Majira na Wakati?

Rudi nyumbani

Print this post

TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO.

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu katika mafundisho ya Neno la Mungu.

Ni vema tukafahamu tarajio la Mungu kwa kila mwanadamu ni lipi kabla ya kumaliza mwendo wake hapa duniani. Utaona kipindi kile kabla mfalme Hezekia hajafa, Neno la Mungu lilimjia kwa kinywa cha Nabii Isaya na kumwambia, atengeneze mambo yake, kwasababu kifo chake kimekaribia.

Isaya 38:1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona

Kwanini Mungu hakumwambia, “pumzika sasa usihangaike-hangaike” kwasababu kipindi si kirefu utaenda kufa? Lakini anamwambia “TENGENEZA”, mambo yako.

Mungu alijua kabisa  nyenzo pekee ya kuwa salama kule ng’ambo ya pili ni kutengeneza sasa mambo yako angali unaishi.

Inasikitisha kuona, watu wengi, wanaishi tu hohe-hahe, wakihubiriwa habari za wokovu, wanakuwa wepesi kusema, ‘siku moja nitaokoka!’ . Wakidhani kuwa mbinguni ni kuingia kama vile mtu aingiavyo kwenye basi/daladala, ambapo siku hiyo hiyo atakata tiketi, na siku hiyo hiyo utasafiri.

Mbingu ina maandalizi. Na maandalizi yake ni hapa duniani, ukiyakamilisha hayo utaonekana umestahili kuingia mule. Bwana anatazamia si tu Uokoke, halafu basi.  anatazamia pia Uache Urithi wa rohoni kwa vizazi vingine, huko ndiko kutengeneza mambo ya nyumbani mwako.  Kama vile tu mtu mwenye busara ambaye anajua anapokaribia kufa ni sharti aache urithi kwa watoto wake. Lakini kama hana urithi atawaachia nini?.

Lazima ujue umewekwa na Mungu pia umzalie matunda. Kwahiyo usiwe na amani kuondoka duniani, kienyeji-enyeji tu, anza kutengeneza wokovu wako leo, uwe na faida kwenye ufalme wa mbinguni. Hata utakapofika kule Bwana aone, ile talanta aliyokupa walau imeongeza jambo Fulani katika ufalme wa Mungu duniani.

Mathayo 25:20  Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. 21  Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 22  Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. 23  Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 24  Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; 25  basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. 26  Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; 27  basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. 28  Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. 29  Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. 30  Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno

Je! Mali zako, vitu ulivyo navyo, elimu yako, ujuzi wako, karama yako, vina sehemu gani katika kuundeleza ufalme wa Mungu?.  Kama mtu uliyeokoka Je! Moyo wako kimaombi upo wapi?, Usomaji wako wa Neno umeufichia wapi?. Ukuaji wako wa kiroho umekwama wapi. Tusijione salama katika hayo mazingira na angali muda unakwenda. Ipo hatari, tusipoyatengeneza maisha yetu ya kiroho. Upo wa kusimama mbele ya kiti cha enzi cha hukumu, ambapo kila mmoja atatoa hesabu ya mambo yake mwenyewe.

Hivyo huu ni wakati wetu kila mmoja kujitathimini ndani, kwasababu hapa duniani ni wapitaji tu, hatuna maisha marefu, hujui ni lini utaondoka, au Bwana atarudi lini. Tufahamu tu huko tuendako kama hatujajitengeneza vema sasa, kuingia haiwezekani.

Bwana atupigishe hatua.

Shalom.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?

ANGALIA JINSI USIKIAVYO:

TENGENEZA  NYAVU ZAKO, OSHA NYAVU ZAKO.

BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 14 (Yoeli, na Obadia).

Rudi nyumbani

Print this post

SI KILA KILICHO HALALI KINAFAA.

(Jihadhari na Marashi)

Si mambo yote yanayokubalika katika jamii basi yanafaa kwa mkristo.. Si mambo yote yanayokubaliwa na wengi basi yanafaa..ni muhimu kuchuja kila tunaloambiwa au tunayokutana nalo, kabla ya kulikubali, ndivyo biblia inavyotufundisha.

1Wakorintho 10:23  “Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo”.

Mojawapo ya jambo ambalo ni muhimu kuchukua nalo tahadhari ni “Matumizi makali ya marashi”. Unapojipulizia marashi ambayo mtu aliye mita 10 mbali nawe anayasikia, basi fahamu kuwa upo katika hatari kubwa sana.

Utauliza kivipi au kwa namna gani? Hebu turejee katika maandiko kidogo..

Utakumbuka ile habari ya yule mwanamke aliyemmiminia Bwana marhamu ya thamani nyingi mwilini mwake, na maneno Bwana Yesu aliyoyasema kuhusu kazi ya ile marhamu aliyomiminiwa?. Biblia inasema marhamu ile ilikuwa ni ya thamani kubwa, maana yake yenye kunukia sana na kwa eneo kubwa, kiasi kwamba mtu aliye mbali anaweza kuisikia harufu ya marhamu ile.

Tusome

Marko 14:3 “Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye KIBWETA CHA MARHAMU YA NARDO SAFI YA THAMANI NYINGI; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.

4  Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii?

5  Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung’unikia sana yule mwanamke.

6  Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema;

7  maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.

8  Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu MARHAMU KWA AJILI YA MAZIKO”.

Umeona hapo?.. wakati huyu mwanamke anadhani Marhamu ile ingeweza kumfanya Bwana anukie vizuri mbele za watu na aonekane mtanashati.. lakini Bwana aliyaona yale manukato tofauti na mwanamke alivyoyaona, Bwana Yesu aliona hayafai kwa utanashati, bali kwa MAZIKO!.

Lakini kwasababu mwanamke alikuwa na nia njema ya kutubu na kumthaminisha Bwana ndio maana akapata kibali kwa muda ule, lakini Ujumbe tayari tumeachiwa, “kuwa marhamu kama hizo ni kwaajili ya maziko” so kwaajili ya utanashati.

Hiyo ikimaanisha kuwa kumbe kuna vitu tunaweza kuvipaka mwilini, au kuvivaa, na kumbe ni malighafi za MAUTI, Na KIFO!!. Ijapokuwa kwa nje tunaweza kuonekana watanashati na tunaovutia, lakini kumbe tumejipaka au tumekivaa kifo!.

Bwana Yesu angeweza kuwaambia wale watu kuwa marhamu ile amepakwa kwa kuwekwa tayari kukutana na mkutano ili kwamba wasikie harufu nzuri itokayo mwilini mwake, kwani bado alikuwa na siku kadhaa za kuhubiri mbele za watu kabla ya kufa, lakini wala yeye hakuziona hizo siku bali aliona marhamu ile inafaa kwa matumizi ya MAZIKO! Na si utanashati kama wengine wote walivyotazamia.

Mama/dada jiulize hayo marashi unayojipulizia mwilini mwako je unajiweka tayari kwa nini?..je kwaajili ya maziko yako??..

Na asilimia kubwa ya watu wanaotumia marashi makali ni lazima wanakuwa wanasumbuliwa na roho za mauti au uasherati… hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari ya kiroho! Na si kila kitu kuiga kwasababu tu, tumeona ni kitu chenye kukubalika kila mahali.

Mama/dada Kama unatamani kujipamba basi jipambe kwa mapambo ya kibiblia, ambayo ndiyo yale yanayotajwa katika 1Timotheo 2:9 na 1Petro 3:3.

1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

4  bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; YAANI, ROHO YA UPOLE NA UTULIVU, ILIYO YA THAMANI KUU MBELE ZA MUNGU.

5  Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

6  Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote”.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada zinazoendana:

Mafundisho mengine:

Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?

SISI TU MANUKATO YA KRISTO.

Mawaa ni nini? Kama tunavyosoma katika biblia?

EPUKA KUCHELEWA IBADA.

Rudi nyumbani

Print this post

JINSI YA KUISHINDA HALI YA MSONGO WA MAWAZO.

Msongo wa mawazo ni nini? Ni shinikizo au mfadhaiko wa kiakili, unaomkumba mwanadamu, pale anapokutana  na  matatizo, au taabu, au dhiki au shida Fulani. Hivyo inapotokea mtu huyu anashindwa kuzitatua changamoto hizo, ndipo msongo huo huja.

Kwamfano labda mtu amegundulika, ana ugonjwa usiotubika, na kaambiwa na daktari hawezi kupona, mtu kama huyu ni rahisi kukumbwa na msongo wa mawazo,

Au labda mwingine  hana kazi na akiangalia familia inamtegemea, na bado hajafikia malengo yake kulinganisha na umri alionao, moja kwa moja mtu kama huyu ni rahisi kukumbwa pia na msongo wa mawazo. N.k.

Na kama tiba isipopatikana matokeo yake yanaweza kuwa mtu huyo, kupata matatizo ya kiafya, wengine kuchanganyikiwa, wengine kujitenga na watu, wengine kujifungia ndani kulia tu usiku kucha, wengine kutenda vitendo viovu,hata kujiua.

Je! Mkristo anaweza kuwa na msongo wa kimawazo? Jibu ni ndio anaweza kuwa nao. Lakini tiba imeshatolewa. Tutaona katika somo hili kwa namna gani, kwasababu yawezekana wewe ni mmoja wapo ambaye unakutana na hali hii na hujui cha kufanya.

Embu tuone kwanza baadhi ya watu katika maandiko ambao walipitia misongo ya mawazo

1) Eliya:

Eliya wakati amemaliza kuwaua manabii wa Baali, akatazama huku na huku na kujiona kama ni yeye peke yake ndiye nabii wa Mungu aliyebaki, hivyo ikampelekea ajitenge, na kukimbilia jangwani, akae huko mpaka afe.  Lakini Mungu alikuja kumtokea baada ya siku 40, akampa majibu ya faraja, kwamba asidhani yupo peke yake kuna wengine 7,000 amejisazia, rudi Israeli, kanitumikie.(1Wafalme 18-19)

2) Mfalme Daudi.

Alikumbwa mara nyingi na msongo wa mawazo katika maficho yake alipokuwa anawindwa na mfalme Sauli. Mara nyingi alifikia hatua ya kukata tamaa ya maisha. Embu tafakari haya maneno aliyoyasema Daudi.

Zaburi 69:1 Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu.  2 Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha.  3 Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu.  4 Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.  5 Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, Wala hukufichwa dhambi yangu

3) Ayubu

Baada ya kupotelewa na mali zake, na watoto wake, hadi mwili wake kubaki mifupa tu. Mkandamizo ulimjia. Ayubu anasema;

Ayubu6:2 Laiti uchungu wangu ungepimwa, Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja!  3 Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari; Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka

 Mpaka akanza kusema maneno magumu, ya kulaana siku aliyozaliwa. Mtu kama huyu alikuwa katika hali mbaya sana kifikra na kiakili.

4) Petro

Petro na Yuda walipitia jambo moja, kukana na kusaliti, ni dhambi pacha. Isipokuwa Yuda alikwenda kujinyonga kwasababu msongo wa mawazo ulimshinda, lakini Petro hakujinyonga. Yeye alikwenda kujificha na kulia sana kwa “majonzi”.  Tengeneza picha ni wewe unamkana Mungu wako, tena kwa maneno ya dhihaka mbele za watu. Hali hiyo unadhani itakufanya ujionaje kama sio mateso ya kiakili baada ya hapo?. Wengine wanapitia hali kama hizi, wanapojiona wamemtenda Mungu dhambi kubwa sana, isiyosameheka, wakidhani kuwa Mungu hawajali tena, hawathamini.(Mathayo 26:75)

5) Mitume 11.

Baada ya Bwana Yesu kufa, hofu ya wayahudi ikawavaa mitume, wakiona kuwa wao ndio wanaofuata kuuliwa baada ya kiongozi wao kufa.. Hivyo hiyo ikawapelekea kujifungia ndani, wasitoke. Msongo mkubwa sana wa mawazo uliwavaa, kutoka kwa wayahudi.(Yohana 20:19-29)

Itoshe tu kutumia mifano hiyo michache, kwani wapo wengine wengi sana katika biblia waliopitia hali kama hizi, mfano ni Musa, Yusufu, Yeremia, Nebukadreza, Hana(mamaye Samweli),  Danieli, Mtume Paulo wote hawa ukisoma habari zao katika biblia utayathibitisha hayo.

Lakini Je! Waliwezaje kuzishinda hizo hali.

Utagundua, walipopotia taabu zao, walilikumbuka TUMANI la Mungu. Ndilo lililowapa nguvu ya kuweza kuvuka nyakati hizo mbaya walizozipitia.  Waliyazingatia haya maneno;

1Petro 5:6  Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; 7  HUKU MKIMTWIKA YEYE FADHAA ZENU ZOTE, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Na lile alolilisema Yesu..

Mathayo 11:28  Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha

Pale akili zilipogoma, fikra kuzima, moyo kuwa baridi, walijifunza kumtwika Mungu, huzuni zao, mateso yao, shida zao. Hata pale ambapo hazikutatulika kwa wakati walioutarajia, lakini waliendelea na mwisho wa siku Bwana alikuja kuyaweka yote sawa. Kwasababu yeye mwenyewe alisema.

Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi TUMAINI siku zenu za mwisho

Hivyo ndugu, ikiwa na wewe upo katika hali hii ya msongo wa kimawazo, katika eneo lolote lile, iwe la kiroho, kihuduma, kifamilia, kikazi, kiafya, kimaendeleo. Umeshindwa kuendelea mbele, Usiogope. Kwa Mungu lipo TUMAINI, zaidi ya Matumaini yote ya kibinadamu.

Haijalishi msongo huo, umekupata kutokana na dhambi zako, au kutokana na hali zilizo nje ya uwezo wako. Usiogope. Mponyaji, mfajiri, mtatuaji wa matatizo yupo. Huyu si mwingine zaidi ya YESU KRISTO mwokozi.

Mungu akikupa tumaini, ujue ni lazima litokee, lakini mwanadamu akikupa tumaini, ni kusudi tu kukufariji, lakini tatizo linaweza kubaki palepale.  Yesu hayupo hivyo. Mtazame tu yeye. Wakati wa shida, ndio wakati wa kukimbilia chini ya mbawa zake, sio kuwakimbilia wanadamu.

JE! UFANYEJE?

  1. Katika hali hiyo, Usiache kuomba sana  & Kumsifu Mungu & Kushukuru, siku zote za maisha yako. Ongeza kiwango chako katika eneo hili.
  2. Soma sana Biblia: Utapata faraja ya Roho katika uwezo wa Mungu aliowatendea wengine.
  3. Usiwe mtu wa kutanga-tanga sana. Tuliza akili zako, si lazima utafute ushauri kwa kila mtu, jiachie kama vile huna tatizo lolote, ukimkabidhi Bwana yote, ukijua yeye yupo kazini.
  4. Kila wakati Jiambie, “Mungu wangu atayaweka yote sawa mwisho wa siku”.
  5. Mawazo ya kushindwa/kujihukumu yanapokuja yapinge.  Sema “Bwana ndiye boma langu na ngome yangu, na mwamba wangu sitatikisika”.

Na hakika, katika muda fulani, utaona Mungu anakuvusha, anakuponya, anakufariji, anakuondolea huo mzigo. Huo ni uhakika sio makisio. Usiache tu kuendelea na Bwana..

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Mafundisho Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

TUMAINI NI NINI?

UKIOKOKA,HIZI FIKRA ZIKIJA NDANI YAKO, ZIKATAE.

VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI

TUUTAFUTE UMOJA WA ROHO.

Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?

Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

UTAJUAJE KAMA WEWE NI MTUMISHI WA MUNGU NA KRISTO YU PAMOJA NAWE?.

(Masomo maalumu kwa watumishi).

Jina la Mwokozi YESU KRISTO Lihimidiwe daima.

Je unajua namna yakujipima kama kweli wewe ni mtumishi wa Mungu na Kristo yu pamoja nawe?

Je unadhani ni ishara na miujiza ndio utambulisho pekee ya kwamba Kristo yu pamoja nawe?

Nataka nikuambie La!..Ishara na mijuiza si uthibitisho wa kwanza wa Kristo kuwa pamoja nawe, kwasababu biblia inasema Yohana Mbatizaji hakufanya ishara hata moja lakini bado alikuwa mkuu kuliko manabii wote waliotangulia.

Yohana 10:41 “Na watu wengi wakamwendea, wakasema, Yohana kweli hakufanya ishara yo yote, lakini yote aliyoyasema Yohana katika habari zake huyu yalikuwa kweli”.

Na pia wapo watakaofanya ishara lakoini atawakana kuwa hawajui…

Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Umeona kumbe kufanya ishara au kutofanya si tija!..Si uthibitisho wa kwanza kuwa Kristo yu nawe!.

Sasa ni kipi kinachotupa uthibitsho kuwa tunatembea na YESU katika utumishi tunaoufanya?.

Jibu tutalipata katika maandiko yafuatayo..

Yohana 12:26 “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu”.

Hapo Bwana mtu akitaka kumtumikia, yani kuwa mtumishi wake BASI AMFUATE!!… Na yeye alipo ndipo na mtumishi wake alipo, au kwa lugha nyepesi “Yeye yupo pamoja na wale waliomfuata”.

Sasa tunamfuata vipi YESU?.

Tusome tena maandiko yafuatayo..

Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote AKITAKA KUNIFUATA, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.

24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha”.

Kumbe ili tuwe watumishi wa kweli wa Mungu, ambao Kristo atakuwa nasi muda wote ni lazima TUJIKANE NAFSI KILA SIKU??.

Sasa swali ni je tumejikana nafsi zetu?au tunazipenda nafsi zetu na kuzishibisha kwa kila tunachokitaka.

Huwezi kumtumikia Mungu na huku hutaki kuacha mila, huwezi kumtumiia Mungu na huku unaupenda ulimwengu.
Huwezi kuwa mtumishi wa Mungu na huku hutaki kuacha mizaha, na wala dhambi.

Huwezi kumtumikia Mungu na bado unaishi na mke/mume asiye wako. Fahamu kuwa Kristo hayupo na wewe hata kama unaona ishara na miujiza katika maisha yako..hiyo ni kilingana na maneno ya Kristo mwenyewe.

Kanuni ya kutembea na Kristo, itabaki kuwa ile ile MILELE! Nayo ni KUJIKANA NAFSI, KUBEBA MSALABA NA KUMFUATA YEYE!. Kwasababu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele (Waebrania 13:8).

Na hiyo ni kwa faida yetu na si yake! (Ayubu 35:7).

Huenda umeshamwamini Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako!.. Hiyo ni nzuri sana, lakini bado haitoshi, ni lazima uongezee hapo “KUJIKANA NAFSI!”. Na baada ya kufanya hivyo pia ujiandae kwa dhiki kwaajili yake.

Jiandae kuchekwa, kudharaulika, kuonekana mshamba, mjinga na usiyejielewa. Usiogope maana hizo ndizo chapa zake Yesu, (Wagalatia 6:17), na wewe sio wa kwanza, zilianza kwa Kristo BWANA WETU NA AKAZISHINDA.

Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

“Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

MAHANAIMU (Jeshi la Mungu)!.

Rudi nyumbani

Print this post

NI KIJIJI CHA AINA GANI UPO?

Yapo makazi ambayo si rafiki sana kwaajili ya uponyaji wa maisha yako!.

Kuna mahali/vijiji/mitaa ambayo ukikaa ni ngumu kupokea chochote kutoka kwa Mungu, isipokuwa Mungu mwenyewe amekuambia uishi hapo!. Lakini kama hakuna msukumo wowote wa KiMungu kuishi hapo, basi kuwa makini na mahali utakapopachagua!, kama ni mtaa, mji au kijiji.

Utauliza kwa namna gani?

Utakumbuka yule kipofu aliyepelekwa kwa Bwana ili aponywe!, biblia inasema “Bwana Yesu alimtoa nje ya kijiji kabla ya kumponya” na hata baada ya kumponya alimzuia asirudi kile kijiji alichokuwepo!.

Marko 8:22 “Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.

23  Akamshika mkono yule kipofu, AKAMCHUKUA NJE YA KIJIJI, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?

24  Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda.

25  Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi.

26  Akampeleka nyumbani kwake, akisema, HATA KIJIJINI USIINGIE”

Umeona?..sababu ya Bwana kumtoa huyu kipofu nje ya kijiji si kwasababu ya ghasia ya watu!, hapana bali ni kutokana na hali ya kiroho ya mahali pale, maana yake mazingira ya kile kijiji yalikuwa ni magumu kwa yule mtu kupokea uponyaji! (Maana yake ukinzani uliokuwepo pale ulikuwa ni mkubwa sana), Ndio maana Bwana akamtoa kwanza nje ya kijiji kabla ya kumponya!

Hali kama hiyo inaendelea hata leo!, ipo mitaa ambayo ina vita vikali vya kiroho kuliko mingine, vipo vijiji vilivyo vizito kuliko vingine, na sisi kama wana wa Mungu ni lazima tuongozwe na roho mahali pa kwenda na mahali pa kuishi.

Aina ya vijiji/mitaa ifuatayo kuwa makini nayo!

1. Yenye watu wengi wasio na hofu ya Mungu.

Ukiona mtaa/kijiji hakuna hofu ya Mungu, maana yake watu wa mahali hapo ni watu wasiojali, na hata kuidharau injili, na kuipinga kazi ya Mungu, kuwa makini na huo mtaa au hicho kijiji. Kwasababu mitaa inayoikataa Injili mara nyingi inakuwa chini ya vifungo vya laana (Mathayo 10:14-15), na mwisho wake huwa inaharibiwa na Mungu aidha kwa mapigo ya magonjwa au majanga au hali za kiuchumi!.

2. Yenye kiwango kikubwa cha ushirikina na uasherati.

Uchawi na uasherati ni ibada kuu mbili za shetani. Mahali palipojaa kiwango kikubwa cha uasherati na ushirikina fahamu kuwa hiyo ni kambi ya adui asilimia zote. Kuwa makini na mahali hapo!. Kama Roho wa Bwana amekuongoza uishi, basi ishi hapo na utafanikiwa, maana ni mapenzi yake!..lakini kama sio, basi usiishi hapo, ili ubaki salama na familia yako!, (mara nyingi adui anatumia mitaa/vijiji kuharibu watoto au ndoa), hivyo kuwa makini!

Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake”

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?

AINA ZA MAJINI, MAJINA YAO, KAZI ZAO, NA TIBA ZAKE.

Aina za dhambi

UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.

Rudi nyumbani

Print this post

JINSI YA KUIBEBA MIZIGO MIZITO YA KIMAISHA.

Kila mwanadamu, kuna aina Fulani ya mizigo anayo. Mizigo tunayoizungumzia hapa sio mizigo ile ya dhambi n.k. Hapana, bali ile ya kimajukumu. Kama vile utafutaji wa rizki, kodi, ada, elimu, ujenzi n.k. Hii ni mizigo ambayo inatufanya tusiwe katika hali Fulani ya utulivu.

Wakati mwingine haiepukiki, ni lazima tukumbane nayo. Lakini kosa linafanyika ni pale tunapotaka kuibeba mizigo hiyo yote ndani ya siku moja. Au tuyatatue matatizo yote kwa kipindi kifupi.

Ukiwa mtu wa namna hiyo hata ukiwa tajiri wa namna gani, Bado utaona maisha ni magumu, tena yenye shida na taabu isiyokuwa ya kawaida, na wengine wanaishia hadi kujinyonga kwa namna hii. Kwasababu gani? Kwasababu Mungu hajatuumbia tuibebe mizigo kwa namna hiyo? Leo tutaona ni kwa namna gani tunaweza kuibeba mizigo yote.

Kwamfano unapofikiria, changamoto za chakula cha mwaka mzima uzimalize leo, hivyo unafikiria ni wapi utapata pesa ya kununua mapipa 5 ya mahindi, wakati huo huo unafikiria ada za watoto za miaka 5 mbele itakuwaje, hivyo unahangaika uzipate nazo leo, tena wakati huo huo unafikiria uende katika mafunzo ya kujiongezea aina 7 za elimu, ambazo ungepaswa uzisomee kwa miaka 10, unataka uzimalize ndani ya miezi 3. Tena uanze kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanja vya watoto wako watano, ambapo ndio kwanza wananyonya, na wengine wapo tumboni.

Yaani kwa ufupi ufanye mambo yote chap-chap ndani ya kipindi hiki hiki kifupi. Ukweli ni kwamba kamwe hutakuwa na raha katika maisha yako. Utaona maisha ni mazito sana, hayabebeki, hata kama utakuwa unapata vingi kiasi gani. Kumbuka, Kusema hivi haimaanishi tusifikirie kuwekeza, hapana, lakini fikiria hivyo tayari kipo mkononi, lakini kama hakipo, usijijengee akili hiyo.

Hivyo Mungu ametusaidia kwa kutupa njia ya kuibeba mizigo hiyo yote. Nayo si nyingine zaidi ya ile ya “kuimega siku kwa siku”.

Luka 11:3  Utupe siku kwa siku riziki yetu.

Bwana ameivunja vunja mizigo yetu katika siku. Ametaka kukupa rizki ya siku, kesho usiwe na presha nayo sana, Bwana ataifungulia milango yake, amekupa ada ya muhula mmoja, shukuru,  ile ya muhula wa pili ikifika atakupa, usiwe na wasiwasi wa ada ya miaka 3 mbele, atapata ugonjwa wa moyo. Acha hata kufikiria kodi ya miaka 2 mbele, ikiwa umejaliwa ya mwezi mmoja, shukuru. Hujua mwaka ujao utahama hapo, au Bwana atakufungulia milango ya Baraka zaidi ukanunua pako.  

Jukumu lolote ulilonalo, embu livunje vunje kwenye vipindi vifupi, Kwasababu hujaumbiwa uibebe mizigo yote kwa wakati mmoja. Ukiitabikia sana “kesho yako” leo, ujue unajijengea mazingira ya stress.

 Ni kwa faida yako mwenyewe., Lakini ukiwa mtu wa kushughulika na siku yako utashangaa tu mbeleni  umeweza litatua hilo tatizo kubwa kirahisi, kwa njia mbalimbali Mungu atakazokufungulia, kwasababu ni hekima ya Mungu imetumika hapo si ya mwanadamu.

Mathayo 6:31  Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32  Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33  Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34  Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?

JE UNATAMANI KUMJUA MUNGU, NA HUJUI PA KUANZIA?

Fahamu Namna ya Kuomba.

Kupiga ramli ni nini katika biblia?

Watu wenye kuvunja maagano ndio watu wa namna gani? (Warumi 1:31)

Rudi nyumbani

Print this post

TUYASHIKE SANA MAUNGAMO YETU.

Waebrania 4:14  “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu

Kuungama maana yake ni kukiri kwa wazi jambo fulani mbele ya wote… Katika ukristo tunaungama kwa “kukiri kwa vinywa vyetu kuwa Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha yetu, na kukiri kwa vinywa vyetu kuwa sisi ni wenye dhambi, na kutubu!”.. sawasawa na Warumi 10:10.

Warumi 10:9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”.

Biblia inazidi kutufundisha kuwa ni lazima TUYASHIKE MAUNGAMO YETU, maana yake tusikiri tu kwa vinywa na kusahau, bali yale tuliyoyakiri mbele za Mbingu na Nchi, hayo TUYAISHI siku zote za maisha yetu.

Sasa swali tunayashikaje/tunayaishije Maungamo yetu?.

Tusome 1Timotheo 6:12.

1Timotheo 6:12 “PIGA VITA VILE VIZURI VYA IMANI; SHIKA UZIMA ULE WA MILELE ULIOITIWA, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi

 13  Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato”.

Kumbe tunayashika Maungamo yetu kwa kuvipiga vita vya Imani, na kushika ule uzima wa milele tulioitiwa!. Hebu tutazame moja baada ya lingine.

1.PIGA VITA VYA IMANI.

Vita vipo vingi, lakini kama wakristo tumeagizwa kupigana vita vya aina moja tu!, NAVYO NI VILE VYA IMANI!. Na vita hivyo hatupambani na wanadamu wenzetu, bali na roho za mapepo na falme zao katika ulimwengu wa roho…

Waefeso 6:11  “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

12  Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”.

Kwa maelezo marefu kidogo kuhusiana na vita hivi vya Imani na jinsi ya kupambana fungua hapa >>> TUZIDI KUWA HODARI KATIKA BWANA.

 2) SHIKA UZIMA WA MILELE.

Yohana 17:2 “kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.

3 Na uzima wa milele ndio huu, WAKUJUE WEWE, MUNGU WA PEKEE WA KWELI, NA YESU KRISTO ULIYEMTUMA”.

Uzima wa milele maana yake ni “kumjua sana Mungu na Yesu Kristo aliyemtuma”… Hivyo tunavyodumu katika kutafuta kumjua Mungu na siri iliyopo ndani ya mwanae Yesu Kristo ndivyo uzima wa milele unavyozidi kudumu ndani yetu. Lakini tutakapopunguza kumtafuta Mungu, ndivyo ule uzima wa milele unavyozidi kufifia ndani yetu.

Je unayashika Maungamo yako?.

Bwana atusaidie.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.

VITA DHIDI YA MAADUI

USIMPE NGUVU SHETANI.

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

Kuungama ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 14 (Yoeli, na Obadia).

Jina Kuu la ukombozi wa roho zetu, (Jina la YESU KRISTO) lihimidiwe daima!

Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa vitabu vya biblia, tumekwisha kuvitazama vitabu kadhaa vya nyuma na leo tutavitazama vitabu vitatu vya mbele, ambavyo ni kitabu cha Yoeli, Amosi na Obadia. Hivyo ni vizuri kwanza kusoma vitabu hivi mwenyewe katika biblia, ndipo ukapitia uchambuzi huu, na kumbuka uchambuzi huu ni ufupisho tu!, na si wa kutegemea kama darasa kamili au ufunuo kamili wa vitabu hivi, hivyo ni muhimu sana kusoma biblia na kumruhusu Roho Mtakatifu afunue, ndipo masomo mengine yafuate juu yake.

Ikiwa bado hujavipitia vitabu vya awali, ni vizuri ukavipitia kwanza kabla ya vitabu hivi ili tuweze kwenda pamoja.

KITABU CHA YOELI:

Kitabu cha Yoeli, ni kitabu cha 29 katika orodha ya vitabu vya agano la kale, na kimeandikwa na Nabii Yoeli mwenyewe, mapema katika karne ya 8 kabla ya Kristo, kipindi cha Mfalme Uzia wa Yuda, na maana ya jina “Yoeli” ni “Yahwe ni Mungu”.  

Kitabu cha Yoeli kina Milango (Sura) tatu tu!, na kila sura/mlango una ujumbe tofauti.

Yoeli: Mlango wa kwanza.

Katika mlango wa kwanza Nabii Yoeli, anaelezea madhara yaliyoletwa na Nzige, na parare, na madumadu waliotokea Israeli. Historia inaonyesha kipindi cha miaka kadhaa kabla ya Yoeli kuandika kitabu hiki, kulitokea Janga ambalo lililetwa na Mungu kutokana na maasi.

Na janga hilo lilikuwa la Kuzuka kwa Nzige, parare na madumadu ambao walikula mazao yote, na kutokusaza chochote, Uharibifu wa Nzige hao uliwashangaza wote, kwani walikula mazao yote.

Na baada ya pigo hilo, ndipo Mungu anampa Nabii Yoeli ujumbe wa kuwaambia watu wake, kwamba watafakari hayo yaliyotokea, na wapate akili, na kutubu,.. watafakari jinsi wadudu hao walivyoharibu mazao kiasi kwamba makundi yote ya watu waliathirika, mpaka makuhani pia waliadhirika kwani hakikupatikana hata cha kutoa katika nyumba ya Mungu, maana yake zile sadaka za unga zilizokuwa zinatolewa ndani ya hekalu hazikutolewa tena..(Yoeli1:9).

Yoeli 1:1 “Neno la Bwana lililomjia Yoeli, mwana wa Pethueli. 

2 Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi. Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu? 

3 Waarifuni watoto wenu habari yake, Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine.

4 Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu. 

5 Levukeni, enyi walevi, mkalie; Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai; Kwa sababu ya divai mpya; Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu. 

6 Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu, Lenye nguvu, tena halina hesabu; Meno yake ni kama meno ya simba, Naye ana magego ya simba mkubwa. 

7 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe”.

Kutokana na pigo hilo la Nzige, Mungu anawaita watu wake wote watubu!, ikiwemo makuhani, wafunge kwa kulia na kuomboleza, na tena wafunge katika saumu ya kweli (Yoeli 1:13-14).

Yoeli: Mlango wa 2.

Katika mlango wa Pili, Mungu analifananisha jeshi hilo la Nzige na jeshi atakalolinyanyua la watu ambao watavamia Israeli na kuharibu watu na vitu, kwa jinsi hiyo hiyo ya Nzige walivyoharibu mazao! Kwasababu ya maasi ya Israeli. Hivyo anazidi kuwaasa watubu!, kwa kupiga mbiu kwa watu wote, kwani jeshi hilo la watu ambao Bwana analifananisha na nzige litakapopita litapageuza Israeli jangwa (Yoeli 2:3), na Mungu atalipa uwezo wa kuharibu kwa uharibifu mkuu (Soma Yoeli 2:4-10).

Lakini katika Mstari wa 12, Bwana anarudia kutoa shauri la kutubu! Ili aiponye nchi kutokana na pigo la nzige, waliokula mazao, vile vile kwa pigo ambalo atakwenda kulipiga Taifa hilo kwa jeshi la watu wabaya atakaowatuma kuwadhuru.

Yoeli 2:12 “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;

 13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya. 

14 N’nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu?

15 Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; 

16 Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, Na bibi arusi katika hema yake.

17 Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?

Mstari wa 17-32: (Ahadi ya kuponywa miaka ya njaa)

Bwana anatoa ahadi ya marejesho ya chakula katika miaka iliyoliwa na parare na nzige (katika pigo la Nzige). endapo watatubu!

Yoeli 2:25 “Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. 

26 Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.

27 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe”.

Lakini haiishii tu kutoa ahadi ya kuponya miaka iliyoliwa na Nzige, bali pia Bwana anatoa ahadi nyingine ya kipekee ya kuwabariki watu katika roho, (yaani kuwamwagia Roho wake Mtakatifu).

Yoeli 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu”.

Mlango wa 3 wote unahusu ahadi ya Bwana ya kuwapigania Israeli dhidi ya majeshi yaliyowaonea, baada ya wao kutubu, na kumrudia yeye.

Sasa tukirudi katika biblia, tunasoma baada ya Nabii Yoeli kuondoka, Israeli hawakutubu kikamilifu, ijapokuwa walipigwa na janga hilo la Nzige, na parare na madumadu na tunutu..lakini waliendelea kuwa vile vile, mpaka Bwana alipotimiza neno lake hilo la kuleta jeshi la watu ambao wataharibu nchi mfano wa hao nzige waliotangulia, na jeshi halikuwa lingine Zaidi ya lile la Wakaldayo, ambalo Bwana Mungu aliliruhusu lifike Yuda na kuharibu hekalu na kuwaua wayahudi wengi na baadhi yao kuwachukua utumwani Babeli.

Na kule utumwani walikaa miaka 70, na baada ya ile miaka 70, Danieli alisimama kutubu kwa niaba yao baada ya kuujua unabii wa Yeremia kuhusu muda wao wa kukaa utumwani, na waliporejea Bwana aliwapa majuma 69 (ambayo ni miaka 483) ya kuujenga Yerusalemu kabla ya kutimiza ahadi yake ya kumwanga Roho Mtakatifu.

Na miaka hiyo ilipotimia Bwana aliachilia Roho wake mtakatifu sawasawa na ahadi yake aliyoiahidi, katika Yoeli 2:28, ambapo ilitimia ile siku ya Pentekoste (Matendo 2:17).

Matendo 2:14  “Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.

15  Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;

16  lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,

17  Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.

18  Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri”.

Na mpaka leo hii Roho Mtatifu yupo, na ndiye Muhuri wa Mungu juu ya mtu (Warumi 8:9, Waefeso 4:30, 2Wakorintho 1:22).

Kwa undani Zaidi kuhusiana na wadudu hawa (parare, nzige, madumadu na tunutu) na ujumbe gani wa ziada wamebeba kiroho, fungua hapa >>>Nzige, Parare, madumadu na tunutu ni wadudu gani? (Yoeli 2:25)?

KITABU CHA OBADIA:

Kitabu cha Obadia ni kitabu kilichoandikwa na Nabii Obadia mwenyewe, na kina Mlango mmoja tu!, hivyo kukifanya kuwa kitabu kifupi kuliko vitabu vyote vya agano la kale. Maana ya jina ‘Obadia’ ni “Mtumishi wa Bwana”.

Kitabu cha Obadia kinahusu Hukumu Mungu alioitangaza juu ya Taifa la Edomu (Nchi ya Edomu sasahivi ni maeneo ya kusini-magharibi mwa nchi ya Yordani).

Kwaasili Edomu ulikuwa ni urithi wa Esau aliyekuwa ndugu yake Yakobo! (Mwanzo 25:30 na Mwanzo 36:8)... Na tangu Esau na Yakobo wakiwa tumboni mwa mama yao, walikuwa wakipambana!.

Mwanzo 25:22 “Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana.

23 Bwana akamwambia,Mataifa mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo. 

24 Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake”

Kutokana na unabii huo wa Esau kupambana na Israeli, ulifika wakati kiburi cha wana wa Esau (Edomu) kilinyanyuka kwa kiwango kikubwa..kwani walijinyanyua mbele za Mungu na kufanya dhambi na vile vile kuwafanyia mabaya makubwa wana wa ndugu yao Yakobo (yani wana wa Israeli). Na hivyo Mungu kutamka hukumu juu yao kwa kinywa cha Nabii wake Obadia.

Obadia 1:1 “Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa Bwana, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema,Haya,inukeni ninyi;Na tuinuke tupigane naye. 

2 Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana. 

3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi? 

4 Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana”.

Lakini mbali na hilo, historia inaonyesha kuwa kipindi Wakaldayo wameuhusuru Yerusalemu na baadaye kuivamia na kuharibu mali, wana wa Edomu walishirikiana na wakaldayo kushirikiana nao, na hata kuchukua mali nyingi za wana wa Israeli, sawasawa na unabii huo alioutoa Obadia miaka mingi kabla ya wana wa Israeli kuchukuliwa utumwani..

Obadia 1:11 “Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao”. 

Hivyo kwa kosa hilo na mengine ambayo hayajatajwa katika biblia, Bwana Mungu alitangulia kuwaonya lakini hawakutubu, hivyo ulipofika wakati Edomu iliadhibiwa sawasawa na hukumu hiyo, lakini pia iliyopo sasa itakuja kuadhibiwa katika vita vya mwisho vya Ezekieli 38.

Maelezo kwa kina kuhusu Edomu fungua hapa >>>Edomu ni nchi gani kwasasa?

Na baada ya Bwana kuiadhibu Edomu, kutokana na mabaya waliyoifanyia Israeli, Bwana anatoa ahadi ya kuijenga Yerusalemu, baada ya ubaya wao kupita.

Obadia 1:18 “Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema hayo”.

Ni nini tunajifunza katika kitabu hiki cha Obadia?..

Tunachoweza kujifunza kikubwa ni kwamba Mungu anatoa unabii unaokuja kama onyo!, ili yamkini mtu au Taifa lisije kuangukia katika hukumu ya Mungu, Watu wa Edomu walipewa unabii huu kama ushauri kwamba wakati wa msiba wa Israeli wasishirikiane na watu wakaldayo, na onyo hilo walipewa miaka mingi kabla ya Israeli kuja kuvamiwa na wakaldayo, lakini hawakutii unabii huo, na wakafanya waliyoyafanya na leo hii hawapo!.. Wanaoishi Edomu sasa si wana wa Esau bali wana wa Ishmaeli, ambao kulingana na unabii wa kibiblia watafutwa katika vile vita vya Ezekieli 38, na 39, kama walivyofutwa hawa wana wa Edomu.

Na sisi vile vile hatupaswi kutweza unabii (yaani kudharau unabii wa kibiblia). Unabii wa biblia unasema kuwa siku za mwisho watatokea watu wa dhihaka, watu wasiotii wazazi wao, wakaidi, wasiotaka kufanya suluhu, watukanani n.k (soma 2Timotheo 3:4), na kwamba watu wa namna hii hawataurithi ufalme wa Mungu.

Sasa unabii huu ni kweli utatimia, hivyo si wa kuutweza/kuupuzia..kwasababu ni kweli siku za mwisho, ambazo ndizo hizi hawa watu wametokea, hivyo hatupaswi kuwa miongoni mwa watakaotimiza unabii huo wa watakaodhihaki na kupotea, badala yake tutimize unabii wa watakaokolewa kwa kumfuata Mungu na kuitii Injili.

1Wathesalonike 5:20 “ msitweze unabii;”

Bwana atusaidie.

Usikose mwendelezo..

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 13 (Kitabu cha Hosea).

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 12 (Kitabu cha Isaya)

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)

Vitabu vya Deuterokanoni ni vya kiMungu?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5

Rudi nyumbani

Print this post