SIKU ZA MWISHO WA DUNIA.

SIKU ZA MWISHO WA DUNIA.

Siku za mwisho wa dunia zitakuwaje?


Ukweli ni kwamba dalili zote zinaonyesha kuwa tunaishi katika siku hizo.

Shetani anawapufusha watu wengi macho wasilione hilo, ili waendelee kujiburudisha katika mambo maovu ya ulimwengu huu ili siku hiyo iwajilie kwa ghafla kama ilivyowajiliwa watu wa Sodoma na Gomora, na watu wa Nuhu.

Kabla ya hii dunia kuisha kuna mambo kadha wa kadha ambayo yatatangulia.

  • Kwa ufupi tukio la kwanza ambalo ni kuu tunalolingojea sasa hivi ni tukio la UNYAKUO.

Ikiwa bado hujafahamu Unyakuo ni nini, na litawahusu nani na nani bofya hapa ili ufahamu >> UNYAKUO.

Sasa ikitokea mfano Yesu amerudi leo, na ameshanyakua watakatifu wake, basi dunia hii itakuwa imebakiwa na muda mfupi sana usiozidi miaka 7 tu mpaka iishe, Hiyo ni kulingana na unabii wa Danieli (Soma Danieli 9:24-27). Ili kufahamu vema bofya hapa >> DANIELI: Mlango wa 9

  • Sasa ndani ya hicho kipindi cha miaka saba Mpinga-Kristo atanyanyuka ili kuleta dhiki kuu kwa wale ambao watakuwa wamebaki hapa duniani hawakwenda katika unyakuo. Yeye ndiye atakayelisimamisha chukizo la uharibifu..Kwa maelezo marefu fungua hapa kufahamu Zaidi >> CHUKIZO LA UHARIBIFU
  • Sasa mpinga-Kristo akishamaliza kazi yake, kutakuwa na mapigo mengine ya Mungu ya vitasa saba, mahususi kwa ajili ya kuwaadhibu wale wote watakaokuwa hai ulimwenguni kwa wakati huo bofya hapa ili kujua urefu wa mapigo hayo. >> SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!
  • Kisha baada ya hapo  itafuata Hukumu ya Mungu kwa mataifa. Na hapo ndipo Mungu atakapotenga mbuzi na kondoo.. Kondoo atawaweka mkono wake wa kuume, na mbuzi atawaweka mkono wake wa kushoto.

Siku za mwisho wa dunia.

  • Na baada ya hapo utaanza utawala wa Amani wa miaka 1000 duniani wa Yesu Kristo(Hiyo ni baada ya dunia na waovu wote kusafishwa). Bofya hapa >> UTAWALA WA MIAKA 1000.
  • Na mwisho wa ule utawala wa miaka 1000 shetani atafunguliwa kwa muda tena kuwajaribu watu watakaokuwepo ulimwengu wakati huo..Hapo ndipo atakapokamatwa na kutupwa katika lile ziwa la moto.
  • Kisha kitakachofuata ni hukumu ya kiti cheupe cha enzi cha mwana-kondoo. Hapo ndipo mataifa yote yatapokusanyika yahukumiwe.
  • Na kila kitu kikishakwisha, Ile Yerusalemu mpya itashuka kutoka mbinguni. Na ndipo maskani ya Mungu itakuwa Pamoja na wanadamu. Na watu wataishi na Mungu milele na milele na milele isiyokuwa na mwisho. >> UFUNUO: Mlango wa 21

Hakutakuwa na machozi tena wala vilio, wala misiba, wala huzuni,wala magonjwa wala majaribu. Bali tutaishi na Mungu wetu katika furaha isiyokuwa na kifani milele na milele, kipindi hicho ndicho tutakachojua nini maana ya Maisha..kwasasa umilele wote huo tutakaishi na Mungu tutayajua mengi sana.

Ni jukumu letu mimi na wewe, kukaza mwendo kipindi hichi, ili tuhakikishe kuwa Unyakuo hautupiti.

Kufahamu zaidi juu ya siku za mwisho wa dunia, angalia mada nyinginezo chini..

Mada Nyinginezo:

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MAONO YA NABII AMOSI.

BONDE LA KUKATA MANENO.

MPINGA-KRISTO

MIHURI SABA

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments