Category Archive Mafundisho

Roho ya kukataliwa ni nini?

Swali: Je kuna roho ya kukataliwa katika biblia?.. na kama ipo je mtu anawezaje kufunguliwa kutoka katika hiyo roho?


Jibu: “Kukataliwa” kwa lugha nyingine ni ile hali ya “kukosa kibali”.

Mtu anaweza kukosa kibali “kwa Mungu” au “kwa wanadamu”.

  1. KUKOSA KIBALI KWA MUNGU.

Sababu kuu ya Mtu kupoteza kibali (kukataliwa) na Mungu ni “DHAMBI/MAOVU”. Dhambi inapoweka mizizi katika maisha ya mtu inampotezea kibali kwa Mungu.. Mtu huyu anaweza kumwomba Mungu na asione majibu anayoyategemea…anaweza kupambana na asione matokeo ya kile anachokipambania.

Isaya 59:1 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;

2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, HATA HATAKI KUSIKIA”.

Mfano wa mtu aliyepoteza kibali mbele za Mungu na kuwa mtu wa kukataliwa mbele zake ni Mfalme Sauli (1Samweli 16:1) na pamoja na Kaini (Mwanzo 4:10-12).

Sasa mtu anapopoteza kibali cha kiMungu vilevile hawezi kupata kibali kwa watu, hivyo atakuwa mtu wa kukataliwa na watu sahihi (lakini anaweza kukubalika na watu wasio sahihi, jambo ambalo ni hatari kubwa). Mfano wa watu hao katika biblia ni Kaini..

Mwanzo 4:10 “Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.

14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; HATA ITAKUWA KILA ANIONAYE ATANIUA”

Umeona hapo?..Kaini alijua madhara ya “kukataliwa na Mungu” ni “kukataliwa na watu pia”… ndio maana anasema “watu watakapomwona watamwua”.

Kwahiyo DHAMBI au MAASI ndio msingi mkubwa wa mtu kupoteza kibali. Na kwasababu dhambi zote zinaasisiwa/kuchochewa na roho ya Ibilisi na mapepo yake, hivyo basi ni sahihi kabisa kusema kukataliwa ni roho..

Kwahiyo mtu anapojigundua kuwa kila mahali hakubaliki, anakataliwa na kila mtu, na hata wakati mwingine hajui sababu… ni muhimu kulitafakari hilo kwa jicho la pili, kwasababu ni roho ipo nyuma yake inayopalilia dhambi juu ya maisha yake, ambayo matokeo yake huyo mtu ni kukatalika kwa kila anayemwona, au kila anachokipanga..

Hivyo suluhisho pekee la kuiondoa hiyo roho ya kukataliwa ndani ya mtu ni KUOKOKA KIKWELI KWELI.. Na maana ya kuokoka ni KUACHA DHAMBI!!!.. Mtu anayetaka kuokoka lakini hataki Kuziacha dhambi zake, hataki kuacha uzinzi, ulevi, wizi, usengenyaji, matukano, kutokusamehe, chuki, wivu, usengenyaji, fitina n.k hawezi kupokea wokovu mkamilifu. Lakini anayetubu kwa kudhamiria kuziacha dhambi zake ndiye anayepokea wokovu mkamilifu.

Na matokeo ya kupokea wokovu mkamilifu ni kuondoa roho ya kukataliwa ndani yako, na si tu roho ya kukataliwa bali na roho nyingine zote ambazo zimekaa ndani yako zinazochochea tabia na mienendo mingine isiyofaa.

Je umeokoka?

Kama bado na unatamani kufanya hivyo basi waweza wasiliana nasi kwa namba zetu kwa msaada Zaidi au ukafuatiliza sala hii >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mistari ya biblia kuhusu kibali.

NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.

TENDA JAMBO LA ZIADA.

MAPAMBO YA WANAWAKE WALIOUKIRI UCHAJI WA MUNGU.

NUHU WA SASA.

Rudi Nyumbani

Print this post

KIFUNGO CHA MWAMINI KIPO WAPI?

Unaweza kuuliza je! Mwamini anaweza kufungwa na adui?. Jibu ni ndio anaweza kufungwa. Utauliza tena, kama anafungwa sasa kazi ya Yesu msalabani ilikuwa ni nini ikiwa hajawekwa huru kweli kweli.

Jibu ni kwamba mwamini yeyote, hawezi kuwa na kifungo katika roho yake, yaani hawezi kufungwa roho aidha na mapepo, au wanadamu au chochote kile. Hawezi kuwa na laana yoyote ndani yake, aidha ya ukoo au ya mabibi. Kwasababu yeye ni mbarikiwa amewekwa huru na Yesu, na ndio kazi Yesu aliyokuja kuifanya kuwaweka huru walioonewa na ibilisi.Hivyo mtu yeyote aliyemwamini Yesu kwa ‘TOBA’, ubatizo na kupokea Roho. Huyo hana kifungo chochote kwasababu uhai wake unakuwa umefichwa ndani ya Kristo.

Lakini Shetani anauwezo wa kumzuia, katika mambo mengi, asipojua ni nini anapaswa afanye. Na hicho ndicho kifungo cha nje akifanyacho adui. Kukuzuia wewe mwamini, ndicho alichokifanya kwa Paulo wakati Fulani alipotaka kwenda kuhubiri  injili kwa Wathesalonike akasema shetani alinizuia (1Wathesalonike 2:8).

Lakini pia tunamwona Mtume mwingine aliyeitwa Petro.

sasa hebu tuangalie kisa hiki kwenye maandiko Kilichomhusu yeye, tuone ni maeneo gani huwa adui analenga mahususi.

Matendo 12:4  Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu.

5  Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.

6  Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakalilinda gereza.

7  Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika kule chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. MINYORORO YAKE IKAMWANGUKA MIKONONI.

8  Malaika akamwambia, Jifunge, KAVAE VIATU VYAKO. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, JIVIKE NGUO YAKO, ukanifuate.

9  Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono.

Umeona maeneo aliyofungwa Petro?

Wafungwa wa zamani, ilikuwa ili aitwe mfungwa, ni lazima mambo hayo matatu  yakamilishwe juu yake; nayo ni.

1) Kufungwa, Minyororo mikononi

2)Kuondolewa Mavazi, na kupewa mengine ya gerezani.

3)Kuondolewa viatu miguuni

Na hiki ndicho kitu anachokifanya  pia adui kwa mwamini. Anaanza kwa kukufunga mikono yako rohoni, kisha kuyaondoa mavazi yako, na mwisho viatu vyako miguuni. Baada ya hapo unakuwa tayari huna nguvu ya kumshinda.

Mikono ni nini?

Ni “maombi na mifungo”

Mikono ni viungo mama katika mwili. Husaidia viungo vingi kufanya shughuli zake. Silaha hushikwa na mikono,  hata ngumi hurushwa kwa mikono. Hivyo adui anajua akizuia mikono yako. Huwezi kufanya lolote. Mikono ya mwamini, ni “maombi na mifungo”.

Mtu ambaye ni mwombaji, kiwango cha Roho ndani yake huwa ni kikubwa, na hivyo hakuna mnyororo wowote, unaoweza kumshika. Ndio maana utaona baada ya kanisa kumwombea Petro kwa juhudi, akafunguliwa. Vilevile Paulo na Sila walipokuwa wamefungwa kipindi kile, hawakulala tu, bali usiku wa manane walikuwa wakiomba, na matokeo yake vifungo vikawaachia.

Matendo 16:25  Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 26  Ghafla pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.

Umeona, maombi, huondoa minyororo mikononi. Kuwa mwombaji, uzishinde nguvu za mwovu. Shetani anawaogopa waombaji

Mavazi ni nini?

Ufunuo 19:8  Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu

Mavazi, ni matendo mema. Ukikosa matendo mema,(Utakatifu), si rahisi kumshinda adui, utakuwa mwamini asiye na matunda yoyote, itaishi tu kama mwanadamu ambaye anamapungufu ya akili rohoni, hutaweza kufanya lolote.Ndani una makunyanzi, mawaa, ambazo katika hizo shetani anakuwa na haki ya kukulaumu.

Ishi kama mkristo, ukiwa rafiki wa dunia, fahamu kuwa unajifanya adui kwa Mungu moja kwa moja. Nuru yako isipoangaza nje, huwezi mshinda shetani. Ni lazima uwe kikombe safi, nje na ndani. Huwezi kusema umeokoka halafu matendo yako hayaendani na imani yako.Unajidanganya, bado hujaifahamu neema ya Mungu.

Miguu ni nini?

Waefeso 6:14  Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15  na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani.

Miguu ni utayari, wa kuhubiri. Adui anapenda kukawiisha nia za watu, kwa kuwavuta katika mambo yao mengine, na kusahau yaliyo ya msingi kwao, ndio hapo atawasonga kwa anasa, udanganyifu wa mali, na shughuli za ulimwengu huu. Na mwisho wa hapo wanabakia kuwa hawana matunda.

Hivyo ndugu uliyeokoka, usiruhusu adui kukuzuia popote. Jijengee desturi ya kuwa mwombaji wa kila siku. Mikono yako isifungwe. Penda kuishi maisha matakatifu, vazi lako lisibadilishwe, kuwa tayari kuhubiri injili wakati wowote, ukifaao na usiokufaa, epuka udhuru wa mwili au kazi, pinga sana hapo jiwekee ratiba yako, ili upate sehemu ya kuwaeleza wengine habari za Yesu Kristo anayewaokoa wanadamu.

Tukizingatia hayo. Tutakuwa tumemshinda shetani ndani na nje. Hatujafungwa ndani wala nje.

Bwana akubariki

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

Kongwa ni nini kwenye biblia?(Wagalatia 5:1)

VITA DHIDI YA MAADUI

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

Rudi Nyumbani

Print this post

Mwujiza wa kwanza wa Bwana YESU ni upi, na una ujumbe gani?

Swali: Muujiza wa kwanza wa Bwana YESU ulikuwa ni upi?


Jibu: Mwujiza wa kwanza wa Bwana YESU ni ule wa Kana ya Galilaya, ambapo aligeuza maji kuwa Divai.

Yohana 2:1 “Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.

2  Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.

3  Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.

4  Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.

5  Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.

6  Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.

7  Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.

8  Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.

9  Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,

10  akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.

11  MWANZO HUO WA ISHARA YESU ALIUFANYA HUKO KANA YA GALILAYA, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini”.

Mstari huo wa 11 unatudhihirishia wazi kuwa hiyo ndio iliyokuwa ishara ya kwanza kufanywa na BWANA YESU mbele ya wanafunzi wake.

Sasa kujua kwa mapana ujumbe uliopo nyuma ya muujiza wa kwanza wa Bwana YESU wa Kana ya Galilaya fungua hapa >>Kwanini Bwana YESU ageuze maji kuwa Divai? Na ni ujumbe gani tunapata?

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NI NINI BWANA ANATAKA KUTOKA KATIKA MUUJIZA ALIOKUFANYIA?

JE UMEJIANDAA KUTIMIZA UNABII UPI?

Kumaka ni nini katika biblia? (Mathayo 8:27)

SIRI KUU NNE (4), UNAZOPASWA UZIFAHAMU NDANI YA KRISTO.

UFUNUO: Mlango wa 3 part 3

MIMI NIKO AMBAYE NIKO

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini Bwana YESU ageuze maji kuwa Divai? Na ni ujumbe gani tunapata?

Swali: Kuna nini katika Divai mpaka Bwana YESU ayageuze maji kuwa Divai?


Jibu: Hakukuwa na chochote maalumu au cha kipekee katika Divai.

Sababu ya Bwana YESU kuyageuza maji kuwa Divai na si kinywaji kingine ni kwasababu ndicho kinywaji kilichokuwa kimepunguka pale! (Kulingana na zile taarifa alizoletewa na mama yake).. Endapo kama ingekuwa ni chakula ndicho kilichopunguka basi Bwana YESU angefanya muujiza wa chakula kuongezeka cha kuutosha ule umati wote, huenda angefanya muujiza kama ile ya  Mikate na Samaki, alipolisha maelfu ya watu. (Marko 6:38-44 na Luka 9:13-17).

Sasa kabla ya kuangalia ni ujumbe gani tunapata kwa mwujiza ule, hebu kwanza tuangalie matokeo ya kukosa Divai katika ile Harusi.

Kufahamu kwa kina matumizi ya Divai katika biblia fungua hapa >>MATUMIZI YA DIVAI.

Kulingana na Desturi za kiyahudi ilikuwa ni aibu kubwa sana arusi ikose Divai, au chakula…Hivyo ni aibu kubwa sana kwa wanafamilia, sawasawa tu sasa sherehe ikipungukiwa na chakula inakuwa ni aibu kubwa kwa walioandaa na huzuni na karaha!..

Sasa kitendo cha Bwana YESU kubadili yale maji na kuwa Divai, tena yenye kuwatosha watu wote ni kitendo KILICHOWAONDOLEWA AIBU WANA ARUSI NA WAZAZI.. vile vile ni kitendo kilichowaondolewa huzuni, na masononeko na fadhaa.. na ni kitendo kilichowapa heshima. Ndio maana utaona yule mkuu wa Meza alimfuata Bwana arusi kumsifu badala ya Bwana YESU.

Sasa ni ujumbe gani mkuu tunaupata hapo?

Ujumbe mkuu si upekee wa Divai.. bali ni Faida ya BWANA YESU ndani yetu au katikati yetu. Kuwa yeye anapoingia ndani yetu anazichukua aibu zetu, na fadhaa zetu na masikitiko yetu, na kutuheshimisha na kutuondolea aibu zetu..

Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.

Unauona upendo wa YESU kwetu pale tunapomkaribisha na kumtwika fadhaa zetu?.. Wale wanaharusi waliona thamani ya YESU na kumwalika katika sherehe yao, na pale walipopungukiwa ndipo Kristo alipozuchukua fadhaa zao na aibu yao..

Wenye harusi , (wao hawakumwalika Bwana kwasababu walijua divai itaisha ili baadaye wamwite awageuzie maji kuwa Divai).. La! Ile ilitokea tu kama dharura na ndipo Bwana akafanya miujiza.. Wao lengo lao kubwa lilikuwa ni kumwitaji YESU ndani ya harusi yao, na si wamtumie.

Na sisi leo hatupaswi kumfuata BWANA YESU kwasababu tu tunataka uponyaji, au heshima au kuinuliwa kimaisha (watu wote waliomfuata Bwana YESU kwa haja kama hizo aliwakimbia Soma Yohana 6:25-26)..Lakini tumfuate Bwana YESU kwasababu tunataka uzima kwanza, na kuyafanya mapenzi yake na hayo mengine yawe ni dharura tu, kama wale waliomwalika.

Ukishahikiki kwamba uzima upo ndani yako, ndipo tumtwike hayo mengine..

1Petro 5:7 “huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Manabii walisema “Neno la Mungu likanijia” ..Maana ya hili neno ni nini?.

Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.

WENGINE WANAKESHA KWAAJILI YAKO.

BUSTANI YA NEEMA.

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.

Rudi Nyumbani

Print this post

Bwana Yesu alizaliwa katika nchi gani?

Bwana YESU KRISTO alizaliwa katika Nchi/Taifa la ISRAELI, lililopo mashariki ya kati. Na mji aliozaliwa ni Bethlehemu ambao ulikuwa katika urithi wa kabila la YUDA.

Mika 5:2 “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”.

Pamoja na kwamba Bwana YESU alizaliwa Bethlehemu kulingana na unabii huo wa Mika, lakini hakulelewa katika huo mji wa Bethlehemu badala yake wazazi wake waliishi mahali palipojulikana kama NAZARETI, Mji mdogo sana uliopo kaskazini mwa Taifa hilo la Israeli, na huko ndiko Kristo alikokulia, ndio maana mahali pengine anajulikana kama Mnazorayo (yaani mtu wa Nazareti).

Mathayo 2:23 “akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo”.

Lakini pia Mji huo wa Nazareti ulikuwa ndani ya Wilaya iitwayo Galilaya, wakati mji wa Bethlehemu aliozaliwa Bwana YESU ulikuwa katika Wilaya iliyoitwa Yudea au Uyahudi.

Wilaya ya Galilaya ndio uliyojumuisha miji mingine midogo midogo kama Kapernaumu na Korazini na Bethsaida, ambapo wanafunzi wengi wa Bwana YESU walitokea katika hiyo miji, na ndio miji ambayo iliona miujiza mingi ya Bwana YESU lakini haikutubu (Mathayo 11:21)…. Wakati Wilaya ya Uyahudi ndio iliyobeba miji ya Bethlehemu pamoja na Yerusalemu.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba BWANA YESU alizaliwa Bethlehemu ya Uyahudi na kulelewa Nazareti ya Galilaya, na alifia YERUSALEMU na kuzikiwa hapohapo, na kufufuka hapo hapo YERUSALEMU. Na sasa yupo hai na atarudi tena mara ya pili na siku hizo zimekaribia kulingana na unabii wa biblia.

Je umeokoka?

Bwana YESU ANARUDI.

Kama unatamani kuokoka basi fuatiliza sala hii >>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Bwana Yesu alizaliwa mwaka gani?

Raheli aliwalilia vipi watoto wake?

BADO UPO YERUSALEMU TU..GALILAYA HUTAKI KWENDA

Yerusalemu ni nini?

AKAZIDI KUENDELEA KATIKA HEKIMA NA KIMO.

Rudi Nyumbani

Print this post

Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru.

Huwenda ukawa unajiuliza, Bwana Yesu alikuwa na maana gani kusema, Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru? . Je huko gizani ni wapi, na sirini ni wapi? Je yeye huwa anazungumza gizani.

Mathayo 10:26  “Basi, msiwaogope, kwa maana hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana.

27  Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba”

JIBU: Ni vema tukaifahamu tabia ya Bwana wetu Yesu Kristo, katika kufundisha jinsi ilivyokuwa alipokuwa anazungumza na watu mbalimbali. Yapo maneno au mafundisho au mafunuo aliyoyaweka wazi kwa watu wote, lakini yapo ambayo hakuyaweka wazi kwa kila mtu.

Mahubiri yake mengi aliyazungumza hadharani, lakini mengine haikuwa hivyo, kwamfano upo wakati alijitenga akapanda milimani, na wale waliomfuata ndio aliowafundisha (Mathayo 5:1), wakati mwingine aliingia nyumbani, hakutana kujulikana kwasababu alikuwa akitaka kuwafundisha wanafunzi wake tu, peke yao (Marko 9:29-31), wakati mwingine aliwaponya watu akawataka wasimdhihirishe, (Marko 1:44), wakati mwingine alijifunua utukufu  wake, kwa wale tu waliokwenda naye kuomba mlimani, uso wake ukawa unameta meta, kama jua, alipomaliza  akawakataza wasimwambie mtu, mpaka atakapofufuka (Mathayo 16).

Hayo ni mazingira mbalimbali, ambayo Yesu alisema nao bila kujulikana na kila mtu, Sasa mazingira hayo ndio aliyaita  “Gizani, au sirini”

Hii ni kufunua kuwa hata sasa Yesu anazungumza hadharani, lakini pia anazungumza sirini. Na yale ya sirini huwa ni makubwa zaidi na ndio maana haitaji yajulikane na kila mtu.

Watu wengi wanamsikia Yesu hadharani, lakini hawamsikii sirini. Hadharani, ni pale unaposikia mafundisho kanisani, mahubiri, semina, mkutano  n.k. Ni kweli Yesu atakufundisha mengi kupitia matumishi wake mbalimbali, na yatakujenga na ni muhimu ufanye hivyo.

Lakini lazima pia sirini pa Yesu uwe napo.

Je hapo ni wapi?

Ni eneo lako la utulivu la kimaombi na kutafakari”.

Ni muhimu sana kila mkristo, awe na wakati wake maalumu kila siku alioutenga wa kuzama uweponi, katika maombi, kusoma Neno na kutafakari shuhuda za Mungu maishani mwake. Ni muhimu sana.

Zaburi 91:1 AKETIYE MAHALI PA SIRI PAKE Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

Mathayo 6:6  Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Hapa Yesu anataka uingie gharama, kidogo ili umsikie, au akuhudumie, au akufundishe. Ndio mfano wa wale waliomfata milimani. Vivyo hivyo na wewe, ingia gharama ya kudumu uweponi mwa Mungu. Ukiona mchana pana usumbufu, usiku ni muda mzuri sana, kuamka, tena masaa yako kadhaa kila siku,. Kumpa Bwana nafasi ya kukufundisha.

Ukiwa wa namna hii, hutamkosa Bwana popote pale. Kaa mahali pake pa siri. Kwasababu yupo pia sirini, akupe mambo mambo utayasema hadharani wakati fulani.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kujazi ni nini? (Mathayo 6:4)

UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?

AGIZO LA UTUME.

MKUU WA GIZA.

Rudi Nyumbani

Print this post

SIFA SITA (6), ZINAZOIKAMILISHA ILE SIKU YA BWANA ITISHAYO.

Nyakati tunazoishi ni za hatari kubwa, zaidi hizo zinazokuja wakati si mwingi ndio za hatari mno. Watu wengi hawajui kuwa mwisho umekaribia sana, dunia imekwisha, na kwamba SIKU YA BWANA, ipo mlangoni.

Siku ya Bwana ni nini?

Siku ya Bwana ni kipindi fulani maalumu ambacho Mungu amekiandaa ili kuuharibu huu ulimwengu pamoja na watu wote waovu waliopo duniani, na mifumo yao mibovu. Na hiyo itakuja baada ya kanisa la Kristo kunyakuliwa 

Tukisoma katika kitabu cha Sefania tunaelezwa kwa urefu juu ya sifa kuu za siku hiyo itakavyokuja. 

Ametaja sifa zake sita (6), kwa kuziita “siku ya”..”siku ya”…”siku ya”

Tusome..

Sefania 1:14-16

[14]Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!

[15]Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,

[16]Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.

1) Anaanza kwa kusema ni Siku ya ghadhabu.

Ghadhabu ni zao la hasira, na hasira hufuatana na mapigo. ndio hapo tunaposoma kitabu cha ufunuo 16, tunaona kipindi hicho kikifika wale malaika saba watavimimina vile vibakuli vyao saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi. na kitakachofuata kwa tendo lile ni mapigo, ndio hapo utaona majipu mabovu, yanawatokea wanadamu, na tena jua linashushwa na kiwaunguza watu, mpaka wanafikia hatua ya kumtukana Mungu.

Ufunuo 16:8-9

[8]Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto. 

[9]Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu. .

2) Siku ya fadhaa na dhiki.

Dhiki na fadhaa ni taabu ambazo mtu anazipata hususani kutoka katika mazingira ya nje. Ukiendelea kusoma sura ile ya 16, utaona mito, chemchemi na bahari zote zinageuzwa kuwa damu, wanadamu wanakosa maji. hofu na mashaka ya mabadiliko ya nchi. Duniani hatakuwa ni mahali penye utulivu, tengeneza picha unaishi katika dunia ya namna hii, utastahimili vipi. Bwana anasema wanadamu watafuta kifo, lakini kifo kitawakimbia.

Ufunuo 16:3  Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.

4  Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu. 5  Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;

6  kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili

3) Siku ya uharibifu na ukiwa

Sio tu mapigo na dhiki, lakini pia kuharibiwa kwa huu ulimwengu na mifumo yake kutafuata, kwasababu biblia inasema siku hiyo kutatokea tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijawahi kutokea tangu dunia kuumbwa, mpaka visiwa kuhama, inasema moto utatokea kuharibu huu ulimwengu, mfano wa sodoma na gomora na mfano wa kipindi cha gharika.

2 Petro 3:10-12

[10]Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 

[11]Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, 

[12]mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? 

4) Siku ya giza na utusitusi.

Giza na utusitusi unaozungumziwa hapa ni ule wa rohoni. ni kipindi ambacho watu watautafuta uso wa Mungu lakini hawatauona, ndio maana Yesu alisema imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyetupeleka maadamu ni mchana, usiku waja asioweza mtu kufanya kazi. watu watamwita Mungu, lakini hakutakuwa na majibu yoyote.

Mithali 1:27 Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.  28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.  29 Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha Bwana.  30 Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote

5) Siku ya mawingu na giza kuu. 

Vilevile kwa jinsi dunia hii itakavyoharibiwa jua na mwezi na nyota vitazuiliwa.. duniani kutakuwa na giza ambalo halijawahi kutokea, na hayo ndio yatakuwa yale mapigo ya mwisho mwisho kabisa yatakayokuwa yanaukaribisha ujio wa pili wa Yesu duniani.

Vilevile wingu zito litatandaa angani, mawe mazito yatashuka duniani kama talanta, jiwe lenye uzito wa kg 34, hatujui itakuwa ni mvua ya namna gani, hiyo.

Ufunuo 16:18-21

[18]Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. 

[19]Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 

[20]Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 

[21]Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.

6) Anasema pia ni siku ya tarumbeta na ya kamsa.

Kamsa ni kelele za vita. Maana yake katika kipindi hicho cha siku ya Bwana, vita vitakuwepo, ndio ile vita ya mwisho ijulikanayo kama Harmagedoni.Mataifa yote yatahusika. lakini Bwana awataua watu wengi sana. damu nyingi sana zitamwagika. ni nyakati ambayo hakutakuwa na shujaa, kila mtu ataomboleza mpaka mashujaa, wafalme na matajiri wote hao watalia sana, pesa zao hazitawasaidia wataomba milima iwaangukie wafe haraka, kuliko kushuhudia huo mfululizo wa mapigo ya Mungu mwenyezi.

Na ndio maana ukimalizia kusoma mistari inayofuata pale kwenye kitabu cha Sefania anasema

Sefania 1:17-18

[17]Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. 

[18]Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha. 

Ndugu yangu, ikiwa unyakuo ukipita leo, fahamu haya utayashuhudia, wakati huu si wa kumbelelezewa wokovu, ni kuamka na kuikimbilia neema, nyakati mbaya zimekaribia, haya mambo ya duniani yatakufikisha wapi? uhai wako umefichwa wapi? Ukifa leo huko uendako utakuwa mgeni wa nani.Kwasababu huko nako kuna mateso makali vilevile kama hapa.

Embu dhamiria kutubu na kumgeukia Bwana Yesu leo, akupe msamaha wa dhambi bure. Hukumu ya Mungu inatisha. 

Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu maishani mwako. Na unatamani leo Yesu akutue hiyo mizigo ya dhambi. Basi waweza kusali sala hii kwa imani. Ukijua Kristo wakati wote yupo kutuokoa. Kumbuka kinachotangulia ni kuamini. Kisha ndipo kukiri.

Hivyo

Hapo ulipo piga magoti, kisha dhamiria moyoni mwako kuyasema maneno haya, na moja kwa moja leo, utapokea msamaha wa dhambi zako hapo hapo ulipo, 

Sema.

Ee Bwana Yesu asante kwa kuja kwako duniani, kutukomboa sisi wanadamu tuliokuwa tumepotea, kwa kifo chako pale msalabani na kufufuka kwako. Ninaamini kuwa wewe ndio Bwana na mwokozi, nami napokea neema uliyonipa bure ya ondoleo la dhambi, tangu leo ninakubali kufanyika mwana wako, na kugeuka kuacha njia mbaya za kale. Asante kwa kuwa unanipa nguvu hiyo na kuliandika leo jina langu katika kitabu cha uzima. Nami nafanyika kiumbe kipya. Asante kwa kunipokea, asante kwa kunisamehe, Asante kwa kunifanya mwana wako.  Ninaomba nikiamini katika jina la Yesu Kristo Amen.

Basi ikiwa umesema sala hiyo toka moyoni kwa imani. Tayari umeshaupokea wokovu. Na hivyo hatua zilizobakia kwako ili kuitimiza haki yote, ni wewe kubatizwa. Tafuta mahali wabatizwapo kwa maji tele, na kwa jina la Yesu Kristo.  Ikiwa utahitaji msaada pia waweza kuwasiliana nasi kwa namba zetu chini.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani

Print this post

NI NJIA GANI MTU AITUMIE AWEZE KUSHINDA TAMAA NA VISHAWISHI?

Nakusalimu katika jina la Bwana Yesu,

Ni swali ambalo linaulizwa na wengi, je ni kweli mtu anaweza kuzishinda tamaa za mwili? Au vishawishi vyake?  Anaweza kweli kuacha dhambi ya uzinzi, au kujichua,au kutazama picha za ngono, au ulevi, au miziki, n.k.?

Jibu la kibinadamu ni hapana! Na ndivyo ilivyo.. Lakini jibu la Mungu ni ndio, kwasababu alisema kwake yote yanawezakana.(Mathayo 19:26).

Akili yako itakuambia haiwezekani, kwasababu hujajua kanuni ya kuwezekana. Mimi niliwahi pia kufikiri hivyo hapo nyuma. Lakini nikathibitisha kile maandiko yanasema, kuwa hilo jambo linawezakana, Mungu hasemi uongo. Sasa utauliza ni kwa namna gani?

Awali ya yote ni vema ukafahamu kuwa hakuna mwanadamu yoyote aliyeumbwa na uwezo wa kuzishinda tamaa za mwili.  Hayupo. Vilevile anayejaribu kufanya hivyo kwa akili zake, na kwa nguvu zake peke yake, pia anajidanganya mwenyewe kwasababu, utafika wakati atayarudia yaleyale tu. Ikiwa wewe ni mmojawapo unayejaribu kupambana kwa nguvu zako, utavunjika moyo ni heri leo ujue kanuni sahihi ya kuitumia.

Sasa ni kwa namna gani tutaweza kushinda hali hizo za mwili?

Kanuni imetolewa kwenye mistari huu.

Wagalatia 5:16  BASI NASEMA, ENENDENI KWA ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17  Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

Anasema “Enendeni kwa Roho”, biblia ya kiingereza inatumia neno “Walk in spirit” akiwa na maana “Tembeeni katika Roho”

Wakristo wengi, wanampokea kweli Roho Mtakatifu, wanajazwa Roho kabisa, lakini ni wachache sana “wanaotembea katika Roho Mtakatifu”.

Ni sawa, na mgeni unayemkaribisha nyumbani mwako. Halafu unapokwenda kazini, au matembezini unamwacha nyumbani, hajui kingine chochote kuhusu wewe zaidi ya maisha ya palepale unayokutana naye nyumbani. Ndivyo anavyofanywa Roho Mtakatifu na waamini wengi.

Tunamtambua Roho tu, pale tunapokuwa ibadani, lakini maisha nje ya ibada, sisi ni watu wengine kabisa. Na hapo ndipo linapokuja tatizo kwanini vishawishi na tamaa zinatushinda. Kwasababu hatutembei na  Roho Mtakatifu.

Ukweli ni kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayekusaidia wewe kuua nguvu ya tamaa ndani yako. Na hivyo anahitaji uwepo wake uwe nawe wakati wote, ili hilo liwezekane.  Ni sawa na GANZI, anayopigwa mgonjwa, wakati ganzi, ipo mwilini hawezi kusikia maumivu, lakini inapoisha maumivu yanamrudia kwa kasi, hivyo anahitaji kuongezewa ganzi nyingine, ili aendelee tena kukaa bila maumivu.

Ndivyo alivyo Roho Mtakatifu, huna budi kufahamu ni namna gani atakupiga ganzi, ili uweze kuishi maisha ya ushindi hapa duniani. Na kanuni si nyingine zaidi ya Kuenenda katika Roho. Kuanzia leo acha kupambana na hizo tamaa kivyako, hutazishinda, pambania kujawa na Roho lakini pia kutembea naye maishani mwako.

Sasa Tunatembeaje katika Roho?

Kwa kuzingatia mambo makuu matatu.

1). KWA KUWA WAOMBAJI WA DAIMA:

Watu wengi wanapofikiria maombi akili zao zinakwenda moja kwa moja kudhani ni wasaa kwa  kuwasilisha mahitaji yao. Lakini maombi si mahali tu pa mahitaji, bali ni mahali pa kujazwa Roho. Hivyo kama mtoto wa Mungu uingiapo kwenye maombi yako kila siku tumia nafasi ya kuomba ujazwe Roho Mtakatifu, akuongoze, akupe nguvu, akujenge nafsi yako, uimarike. Hivyo yakupasa uingie katika maombi ya ndani kabisa sio juu juu ya kutimiza ratiba, bali ya kuweka mawazo yako yote kwa Roho Mtakatifu, akujawe ndani yako, hili ni muhimu sana, kwasababu yeye ndio atakayekusaidia.

Sasa kwa jinsi unavyoomba kwa muda mrefu, na kwa mara kwa mara, ndivyo unavyozidi kumpa nafasi Roho wa Mungu kukujaza nguvu, na mwisho unaona vitu kama tamaa ni vidogo sana, kwasababu ganzi imeshaingia vya kutosha ndani yako.

Jambo hili linatakiwa liwe ni la kila siku(Waefeso 6:18). Kama wewe sio mwombaji, kiwango cha Roho kitakuwa kidogo ndani yako, mwili utakulemea tu, haijalishi upo kwenye wokovu kwa miaka 50, utasumbuliwa tu na tabia za mwilini, Ndio maana tunasisitizwa tuombe kila wakati. Maombi ni kila wakati, kila saa, omba kwa akili, pia omba wa kunena kwa lugha kwa jinsi Bwana atakavyokujalia. Lakini elekeza mawazo yako katika kujazwa na yeye, ukiwa ni mwombaji wa wiki mara moja uendapo kanisani jumapili, au mwezi mara moja, hapo unapoteza muda, hutembei katika Roho. Uthibitisho wa anayetembea kwa Roho ni Yule ambaye ni mwombaji wa kila siku.

2) LIWEKE NENO LA MUNGU AKILINI MWAKO WAKATI WOTE.

Neno la Mungu, husisimua roho zetu wakati wote. Na adui anachohakikisha ni kutufanya sisi tulisahau, hivyo mambo mengine yatawale akili zetu. Anajua akili yako ikiwa inatafakari habari na maonyo katika biblia, itakaa mbali na njia mbovu.

Pale adui anapotaka kukujaribu ukifiria wema Mungu aliomtendea Yusufu, kwa kuukimbia uzinzi, anajua utapata nguvu, pale Mungu alipomtukuza Ayubu kwa kukaa mbali na maovu, utapata nguvu, jinsi Danieli alivyokuwa mwaminifu, Mungu akamwinua anajua utaendelea katika uaminifu wako . Hivyo hapendi, wewe utawaliwe na Neno kichwani, anataka utawaliwe, na movie, utawaliwe na mipira, utawaliwe na siasa, na  mambo ya mitaani, basi. Akili yako izunguke hapo, lakini isizunguke kwenye BIBLIA.

Ukijizoesha kilizungusha Neno la Mungu, na ahadi za Mungu kichwani mwako. Tafsiri yake ni kuwa unamzungusha Roho Mtakatifu, katika ulimwengu wako wa maisha. Na ni nini atakachokifanya kwako kama sio kukusimua roho yako, kwa Neno lile. Hivyo unayashinda yote kirahisi. Watu hawajui Neno la Mungu ndio Roho Mtakatifu mwenyewe wanasema nao.

Yohana 6:63  Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA NI ROHO, TENA NI UZIMA.

Soma sana Neno, lakini zaidi, lidumu kichwani pako, kutwa nzima. Huu ni ulinzi kamili, na silaha madhubuti ya mambo yote ya mwilini.

3) FANYA MAAMUZI YA GEUKO LA KWELI.

Maamuzi ni kutii. Ukiwa mtu wa nia nia mbili, unataka kumfuata Yesu, na wakati huo huo hutaki ulimwengu ukuache nyuma. Hapo napo unamzuia Roho wa Mungu kufanya kazi yake vema ndani yako. Unaweza ukawa ni mwombaji kweli lakini kama moyoni mwako hujaamua kufanya maamuzi, bado ni kazi bure.

1Yohana 2:15  Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16  Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

17  Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele

Ukiamua kumfuata Yesu, fahamu kuwa hii dunia sio fungu lako tena, anasa sio rafiki tena kwako. sio tu na ulimwengu lakini pia na nafsi yako.Ndipo hapo unachukua hatua za dhahiri kabisa katika  imani yako, kama ulikuwa na vichocheo vyote vinavyokusababishia utende dhambi, ndio hapo Yesu anakuambia ukate, usione huruma kutupa hizo nguo za kizinzi ulizozoea kuzivaa, kuachana na huyo girlfriend, kuacha hizo muvi za kizinzi, unazoangalia, usione shida kuacha kampani zako za walevu, usijihurumie hata kidogo, huku ukiwa na mawazo kuwa unafanya hivyo kwasababu ya Kristo ndiye atakayekupa neema ya kushinda.

Ijapokuwa mwanzoni utaona shida kwasababu unafanya kimwili, kwa utiifu wako huo baadaye Roho wa Mungu atakunasa, kwasababu umempa umiliki wote wa maisha yako. Ganzi kubwa sana itaingia ndani yako,.

Ukizingatia mambo hayo matatu, kila siku katika maisha yako. Basi wewe unaenenda kwa Roho. Hakuna litakalokuwa gumu kwako. Kwasababu si kwa nguvu zako bali kwa nguvu za aliye ndani yako, unayashinda hayo.

Wagalatia 5:25  Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.26  Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

KWANINI MUNGU HAJIBU MAOMBI?

Roho Mtakatifu ni nani?.

Rudi Nyumbani

Print this post

MIMI NIKO AMBAYE NIKO

Musa alipomwuliza Mungu kuhusu jina lake, alitarajia kuwa atapewa jina Fulani maalumu kama vile jina la miungu mingine yoyote ijulikanayo mfano wa Baali, au arishtoreth, n.k.

Lakini tunaona Mungu alimjibu kwa ujumla na kumwambia, wakikuuliza jina langu waambie kuwa MIMI NIKO AMBAYE NIKO

Kutoka 3:14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.

Sasa kama ukitazama biblia yako kwa chini utaona imeeleza kwa tafsiri nzuri zaidi hiyo sentensi. Akiwa na maana kuwa NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA.

Yaani mimi sina jina moja maalumu, lenye sifa Fulani. Bali nitatambulika pindi niwapo katika hilo tukio, au tatizo au haja hiyo jina langu. Na kweli ndivyo ilivyokuwa baada ya pale. Tunaona Farao alipogoma tu, kuwaruhusu wana Israeli kutoka Misri tena kwa adhabu ya kuwaongezea kazi, ndipo hapo Mungu akaanza kujifunua kwa majina yake. Akamwambia Musa, kwa jina langu Yehova nilikuwa sijajifunua, sasa nitakwenda kujifunua, kwa jina hilo,

Kutoka 6:1 Bwana akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake. 

2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 

3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao. 

4 Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni. 

5 Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu. 

6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa; 

7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri. 

8 Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA

Umeona? Jina la Mungu lililowatoa wana wa Israeli Misri ni jina la Yehova. Na baada ya hapo tunaona sehemu mbalimbali akijifunua kwa majina mengine mengi, kama Yehova yire, Yehova Nisi, Yehova shama, Yehova shalom, Ebenezeri, n.k. nyakati za vita, za mahitaji, za huzuni n.k. Kulingana na jinsi alivyowasaidia watu wake, walipomlilia.

Na mwisho kabisa akajifunua kwa jina kuu la UKOMBOZI, ambalo ni YESU, lenye maana ya Yehova-mwokozi.  

Hii ni kufunua nini?

Yatupasa tumwelewe Mungu wetu sikuzote kama “NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA”. Hana mipaka ya kujifunua kwake kwetu, nyakati za mahitaji atajifunua, nyakati za raha atajifunua, nyakati za magumu atajifunua, mabondeni atajifunua tu kwako, milimani ataonekana tu, yeye ni vyote katika yote. Uwapo visiwani, uwapo jangwani, uendapo mbinguni, ushukapo mahali pa wafu utamwona tu Mungu wako. Hakuna mahali hatajidhihirisha kwako. Pindi tu umwaminipo. Huhitaji kuwa na hofu na wasiwasi na kumwekea mipaka kwamba kwenye jambo hili au hili hataweza kuwepo au kujidhihirisha.

Swali ni je! Umemwamini Mungu aliyejifunua kwako kama mwokozi? Yaani Kristo? Kumbuka, kabla hujasaidiwa kwingine kote na yeye , unahitaji kwanza uokolewe, kwasababu umepotea katika dhambi, na mshahara wa dhambi ni mauti. Leo hii ukimwamini Yesu atakupa ondoleo la dhambi zako, utakuwa na uzima wa milele. Na utaufurahia wokovu kwasababu utakuwa tayari umevukishwa kutoka mautini kwenda  uzimani. Kumbuka hizi ni siku za mwisho. Itakufaidia nini uachwe katika UNYAKUO, angali nafasi unayo leo.Geuka umfuate Kristo.

Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu maishani mwako, basi wasiliana na namba zetu chini kwa msaada bure wa kuokoka.

Ubarikiwe.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?

Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.

JE! MUNGU NI NANI?

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.

Rudi nyumbani

Print this post

FAHAMU SEHEMU NNE (4)  APANDWAPO MWAMINI.

Shalom.

Sisi kama waamini tunafananishwa na mche, au zao Fulani linalopandwa. Kwamfano ukisoma

Zaburi 1:1-3 Inasema..

1 Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 

2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3 NAYE ATAKUWA KAMA MTI ULIOPANDWA KANDOKANDO YA VIJITO VYA MAJI, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

Hii ni kufunua kuwa mtu yeyote mwenye haki (Aliyeokoka), huwa anapandwa mahali Fulani rohoni.

Sasa ni vema kufahamu maeneo Mungu aliyoyaruhusu/ aliyoyakusudia sisi tupandwe, na hii ni muhimu kujua ili tuwe na amani, kwasababu wakristo wengi wanapoona kwanini baadhi ya mambo yapo hivi, huishia kurudi nyuma, au wengine kukata tamaa kabisa, au wengine kupoa, na wengine kulegea legea. Lakini kwa kufahamu haya, nguvu mpya itakuja ndani yako.

Hizi ni sehemu nne (4), Ambazo sisi kama waamini tunapandwa.

1) TUTAPANDWA PALIPO NA  MAGUGU

Mathayo 13:24  Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;

25  lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

26  Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.

27  Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?

28  Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?

29  Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.

30  Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.

Ukiendelea mbele mstari wa 36-43, utaona Yesu anatolea ufafanuzi, wa mstari huo akisema hizo mbegu njema ni wana wa Ufalme, na konde hilo ni ulimwengu, na magugu ni wana wa ibilisi. Hivyo vyote viwili vimeruhusiwa vimee katika shamba hilo hilo moja la Mungu. Vishiriki neema sawa sawa, lakini mwisho, ndio vitofautishwe.

Kufunua kuwa tumewekwa pamoja na waovu, kamwe hatutakaa tuwe sisi kama sisi tu duniani, na hivyo basi tuwe tayari kusongwa na shughuli zao mbaya, kuudhiwa nao wakati mwingine, tuwapo kazini, majumbani, mashuleni, na wakati mwingine hata makanisani, watakuwepo. Na kibaya zaidi tuwe tayari kuona wakibarikiwa kama sisi tu tubarikiwavyo, watapokea mema yote kama tu wewe, kwasababu mvua ileile inyweshayo kwako itawapata na wao.

 Lakini Bwana anataka nini?

Anataka tuwapo katika mazingira hayo ya watu waovu tusifikirie kujitenga, na kutafuta mahali petu wenyewe tuishi, Yesu alisema Baba siombi uwatoe ulimwenguni, bali uwalinde na Yule mwovu, Bwana atakata tuwapo katikati yao tuzae matunda ya haki, kama Danieli alivyokuwa Babeli kwa wapagani, kama Yusufu kwa Farao, kama Kristo kwa ulimwengu. Vivyo hivyo na wewe kwa mume/mke wako asiyeamini, kwa majirani zako wachawi, kwa wafanyakazi wenzako walevi. Angaza nuru yako usijifananishe na wao, wala usingoje siku utengwe nao, jambo hilo linaweza lisitokee. Hivyo weka mawazo yako mengi katika kuangaza Nuru kuliko kutengwa na waovu. Kwasababu ni mapenzi ya Mungu tuwepo miongoni mwao.

2) TUTAPANDWA KATIKATI YA MITI MINGINE MEMA.

Bwana Yesu alisema tena, mfano huu;

Luka 13:6  Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.

7  Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?

8  Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi;

9  nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.

Tafakari huo mfano, Mtu huyu alikuwa na shamba la mizabibu tu! Lakini akajisikia moyoni mwake apande na mti mmoja wa TINI katikati ya shamba lake. Matokeo yake ni kwamba ule mtini ukagoma kuzaa. Baadaye  akataka kuukata. Akitufananisha na sisi. Upo wakati utapandwa katikati ya jamii nyingine ya watu. Na Mungu atatarajia uzae matunda yaleyale ya wokovu wako uliopokea mwanzo. Je! Utafanya hivyo au utalala?

Hili ni jambo ambalo linawaathiri waamini wengi, pale panapohama na kwenda ugenini, mfano labda kasafiri kaenda mkoa mwingine, sasa kwasababu kule hakuna wapendwa wa namna yake, basi anaamua kuwa vuguvugu hamzalii Mungu matunda yoyote, kwasababu kule  hawapo wakristo. Mwingine amesafiri nje ya nchi. Mbali sana na watu wenye imani ya Kristo. Kwasababu yupo kule anasema mimi nipo peke yangu, siwezi kufanya lolote la Kristo. Ndugu usifikiri hivyo, Bwana anakutaka uzae matunda sawasawa, bila kuangalia ni wewe tu peke yako upo hapo. Kama ni kuwashuhudia wengine habari njema, wewe fanya. Timiza wajibu wako, usiangalie kundi au dhehebu, au jamii nyingine ya waamini waonaokuzunguka. Wewe timiza wajibu wako hivyo hivyo. Bwana akuone unazaa. Kwasababu kwa namna moja au nyingine hatuwezi kuyaepuka mazingira mapya, ambayo tutajikuta tupo sisi tu wenyewe. Tufanye nini? Kumbuka tu mtini ulio katikati ya mizeituni. Usiwe mlegevu.

3) TUNAPANDWA  JUU YA MITI MINGINE.

Tofauti na sehemu mbili za kwanza, ambazo ni katikati ya magugu, na katikati ya miti mingine. Lakini pia tunapandwa juu ya miti mingine. Hii ikiwa na maana, “tunapachikwa” juu ya mti uliokatwa. Wana wa Israeli, walifananishwa na mzeituni halisi, na sisi mataifa mizeituni mwitu. Hivyo wao walipoikataa neema, basi wakakatwa,tukapachikwa sisi, neema ikatufikia pia.

Warumi 11:17  Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,

18  usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe

Na hivyo hapa tulipo tumepachikwa juu ya shina lingine. Na hivyo yatupasa tuwe makini, na kuuchukulia wokovu wetu kwa kumaanisha  sana, kwasababu na sisi tusiposimaa tutakatwa. Mhubiri mmoja wa Injili wa kimataifa aliyejulikana kwa jina la Reignhard Bonnkey, mwanzoni mwa huduma yake, Mungu alimwambia nenda kanitumikie, yeye akawa anasua-sua, Mungu akamwambia neema hii niliyokupa alipewa mwingine akaikataa, na hivyo itaondoka kwako na kwenda kwa mwingine usipotii. Aliposikia vile alikubali kutii kwa moyo wote, akaenda kuhubiri injili. Kuonyesha kuwa sisi ni wa kupachikwa, sio shina. Tuipokee neema kwa kuogopa na kutetemeka (Wafilipi 2:12). Usiwe mkristo vuguvugu, tumia muda wako vema, mzalie Mungu matunda. Kwasababu ulipachikwa tu, kwa kosa la mwingine.

4) TUNAPANDWA KWENYE UDONGO ULIORUTUBISHWA SANA.

Fuatilia habari hii,

Marko 11:12  “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.

13  Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.

14  Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”

Kama tunavyoifahamu hiyo habari asubuhi yake Bwana Yesu alipopita karibu na njia hiyo, ule mti ulionekana umekauka kabisa kabisa. Lakini swali la kujiuliza ni kwanini aulaani, wakati haukuwa msimu wake wa kutoa matunda? Mbona ni kama ameuonea tu?

Ukweli ni kwamba Yesu aliona mti ule kwa mazingira uliokuwepo ulistahili kuwa na matunda hata kabla ya msimu. Kwa namna gani, chukulia mfano wa mazao ambayo yanastawishwa  kwa kilimo cha kisasa, mfano “banda kitalu”(green house), kulingana na matunzo yake, huwa yanastawi kwa haraka na kuzaa ndani ya muda mfupi. Kwasababu yamerutubishwa sana, kwa madawa na mbolea na kuwekewa mazingira rafiki mbali na wadudu waharibifu, mfano wa kuku wa kisasa, ndani ya wiki 6 wamekomaa, lakini matunzo yao hayawezi kama ya wale kuku wa kienyeji ambao wanaachwa wakajitafutie.

Sasa fikiri kama muda wote huo unapita halafu hawazai/hawakui, wanafanana na wale wa kienyeje, ni nini watarajie? Kama sio kuondolewa.

Ndivyo ilivyo kwetu sisi, tunapookoka, muda huo huo tunapokea ROHO MTAKATIFU. Huyu ndiye anayetupa uwezo na nguvu, ya kumshuhudia, na kuzaa matunda ya haki. Hivyo hatuhitaji tena kusubiri mpaka miaka Fulani ipite kama watu wa zamani, ambao walikuwa bado hawajakaliwa na Roho. Bali wakati huo huo tunapookoka na sisi tunawafanya wengine kuwa wanafunzi.

Hatupaswi kujiona sisi ni wachanga kiroho, au watoto, Bwana atakuja ghafla akikosa matunda atatuondoa, na sisi tutabakia kudhani wakati ulikuwa bado.

Hivyo ndugu, fahamu kabisa tayari tumesharutubishwa, usingoje wakati Fulani ufike, hapo hapo fanya jambo kwa Bwana, waeleze wengine habari ya wokovu wamjue Mungu. Wataokoka, usihofu kiwango chako cha kujua maandiko, anayewashawishi watu ni Mungu na sio wewe. Hivyo hubiri kwa ujasiri na Mungu atakuwa na wewe.

Bwana akubariki.

Kwa kufahamu sehemu hizo kuu nne (4), itoshe kutukumbusha mwenendo wetu hapa duniani, uzidi kuwa katika uvumilivu, hofu, wajibu na bidii. Ili tusijikwae, au kufa moyo.

Maran Atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

UTENDAJI KAZI MWINGINE WA ROHO MTAKATIFU USIOUFAHAMU

SIRI YA KUASI KATIKA KANISA LA MUNGU.

JE! WEWE NI MBEGU HALISI YA KRISTO?

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

Rudi nyumbani

Print this post