Kwa tafsiri za kiulimwengu, ulimwengu wa roho Ni ulimwengu usioonekana kwa macho ambao unasadikika viumbe kama malaika, mapepo, au roho za wafu huishi na kutenda kazi. Na kwamba vyenyewe ndio vinavyoyaathiri maisha ya ulimwengu huu unaoonekana.
Na kwamba ili mtu aweze kutembea vizuri hapa duniani hana budi kufahamu au kuwasiliana navyo, ili viwape taarifa, au kushindana navyo pale vinapokinzana nao, kwa kuzingatia misingi Fulani maalumu ya kiroho. Na wengine wanaamini kuwa ni mahali ambapo pana mifumo kama hii ya kidunia, mfano majumba, magari, falme na mamlaka, isipokuwa tu hapaonekani kwa macho n.k. ipo mitazamo mingi.
Lakini kibiblia Mungu anataka tufahamu kwa picha ipi juu ya huu ulimwengu wa Roho?
Awali ya yote biblia inatuambia ulimwengu wa roho upo. Na hauonekani kwa macho.
Waebrania 11:3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
Umeona, kumbe vitu vyote tunavyoviona kwa macho vilitokea mahali ambapo hapaonekani. Na huko si pengine zaidi ya rohoni.
Lakini jinsi unavyotazamwa kiulimwengu ni tofauti na jinsi Mungu anavyotaka sisi tuutazame.
Mungu anataka tutambue kuwa ulimwengu wa Roho, ni mahali ambapo sisi tunakutana na yeye kuwasiliana, pia kumwabudu, na kumiliki, na kutawala, na kubarikiwa, kuumba, kujenga, kufunga na kufungua, na kupokea mahitaji yetu yote kutoka kwake. Kwasababu yeye ni Roho, zaidi ya kufikiri ni mahali ambapo tunakwenda kupambana na wachawi na mapepo au kuona vibwengo na mizimu.
Alisema..
Yohana 4:23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Hivyo, pale tu mtu anapoonyesha Nia ya kutaka kumjua Mungu (asiyeonekana), muumba wa mbingu na nchi. Tayari hapo anaanza hatua ya kuingia katika ulimwengu wa roho ambao Mungu aliuumba kwa ajili yake, na si kitu kingine.
Ndipo hapo sasa anapofahamu kuwa anauhitaji wokovu ili aweze kumkaribia Mungu. Anaanza kumwamini Yesu, anapokea msamaha wa dhambi, kisha Roho Mtakatifu, na baada ya hapo anaishi kwa kulifuata Neno la Mungu aliloliamini. Sasa huyu mtu ambaye Ameokoka, anaitwa mtu wa rohoni, lakini Yule ambaye anaishi katika Neno la Mungu kwa kulitii, huyu sasa ndiye anayetembea rohoni.
Hivyo haijalishi kama alishawahi kuona malaika, au pepo, au kusikia sauti, au kuona maono. Maadamu analiamini Neno la Mungu, na nguvu zake, na kuliishi. Huyo yupo katika ulimwengu wa Roho tena katika viwango vya juu sana. Kwasababu maandiko yanasema kwa kupitia hilo (NENO), vitu vyote viliumbwa.
Kuishi katika Neno ndio kuishi rohoni. Maana yake ni kuwa unaishi kwenye ulimwengu wa Neno.
Sasa utauliza, na haya mashetani sehemu yao ni ipi katika ulimwengu wa roho?
Haya nayo yanaingia rohoni, kwa lengo moja tu kuwapinga wale watu ambao wanatembea katika ulimwengu wa roho (yaani ulimwengu wa Neno). Hivyo yanajiundia mikakati, falme, ngome, na milki, ili tu yakuangushe wewe, uache kumwamini Mungu na Neno lake, na mpango wake wa wokovu kupitia Yesu Kristo. Uendelee kuwa mtu wa mwilini.
Ndio hapo sasa Bwana anatutahadharisha kuwa yatupasa tuwapo rohoni tusiwe hivi hivi tu. Bali tuhakikishe kweli silaha zote tumezivaa, kwasababu, mashetani haya pamoja na wajumbe wake wapo kwa lengo la kutuondoa kwenye Neno la Mungu.
Waefeso 6:10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa unapookoka, wewe tayari ni mtu wa rohoni. Ni mlango wa wewe kuonana na Mungu. Umeshaingia ulimwengu wa roho. Hivyo ili uweze kuona matunda yote ya Mungu, ni sharti uliishi kwa kuliamini Neno lake na ahadi zake, maisha yako yote yawe hivyo. Uwe mtu wa Neno. Lakini mtazamo wa kwamba siku unaona maono na malaika, au kusikia sauti ya Mungu kwenye masikio yako, au wachawi na mapepo ndio mara ya kwanza umeingia rohoni,. Si kweli. Bali Uanzapo kuliamini na kulitendea kazi Neno la Mungu.
Bwana akubariki.
Hivyo ni vifungu baadhi ambavyo utakutana na hilo neno, kwenye maandiko, vitakavyokusaidia kuelewa vema.
Waefeso 1:3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ULIMWENGU WA ROHO, ndani yake Kristo;
Waefeso 1:17 “Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; 19 na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; 20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ULIMWENGU WA ROHO”
Soma pia Waefeso 2:6, 3:10
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Uweza na nguvu ni vyake milele na milele. Amen.
Kuna mambo ambayo Mungu aliyaweka wazi, lakini pia kuna mambo ambayo Mungu aliyaficha ndani ya Kristo mpaka utimilifu wa wakati wake mwenyewe utakapofika. Hivyo ni vema ukafahamu siri hizo alizozificha tangu mwanzo, na ngapi zimeshatimia, na ngapi zipo mbioni kutimia.
Siri hizo hazipo kwa mwingine zaidi ya Yesu Kristo.
Wakolosai 2:2 “..wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo;”
Na hivyo ndani ya Kristo ziliandikwa siri kuu Nne, ambazo leo tutaziona.
Yesu ndio yeye mwenyewe:
1Timotheo 3:16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Mungu alijificha sana, kiasi kwamba hakuna aliyemtambua kuwa ndiye yeye Yehova katika umbo la kibinadamu, na ndio maana maandiko yanasema, kama watu wa ulimwengu huu wangemtambua kuwa yeye ndiye tangu mwanzo, wasingelimsulibisha.
1Wakorintho 2:7 bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; 8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;
Lakini bado tunaona ni jambo ambalo limejificha katika macho ya wengi hata sasa, lakini ashukuriwe Mungu tayari limeshafunuliwa hivyo hilo sio siri tena. Ni vizuri kuifahamu siri hii kwasababu wakati mwingine kushindwa kumtambua Kristo kama ndiye MUNGU mwenyewe. Hupunguza viwango vyako vya kutembea na yeye, na kumwelewa. Fahamu kuwa Yesu ni Mungu halisi Yehova mwenyewe kwenye umbile la kibinadamu ( Tito 2:13, Yohana 1:1, Wakolosai 2:9).
Mataifa nao ni warithi.
Waefeso 3:4 Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. 5 Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; 6 ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;
Wale wapagani, walioitwa makafiri na wayahudi, wafilisti, waashuru, wamisri, wakaanani, n.k. hao Mungu anakuja kuwafanya kuwa warithi wa uzima wa milele. Jambo ambalo halikujulikana na wanadamu au wayahudi kwa kipindi kirefu, wakidhani Mungu ni wakwao tu. Lakini leo hii anaabudiwa katika dunia nzima. Ilikuwa ni SIRI, lakini sasa imedhihirishwa. Soma (Wakolosai 1:27)
Siri hii ukiifahamu itakufanya usibague mtu wa kumuhubiria injili, kitu mwanadamu chini ya jua anastahili kumjua Mungu katika Kristo Yesu. Hivyo usibague kama wewe ambavyo hukubaguliwa. Hubiri kwa watu wa dini zote, kabila zote na lugha zote.
Wayahudi watarudiwa tena.
Warumi 11:25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. 28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.
Tuwaonapo sasa wayahudi wapo mbali na injili ya Kristo, haitakuwa hivyo kwao milele. Mungu anasema “utimilifu wetu utakapowasili”. Yaani mpango wa Mungu wa wokovu kwetu utakapotimia. Basi na wao pia watarudiwa. Na Mungu atasimama nao, na kuwatetea. Na kuwaokoa (Zekaria 12:10-14). Na Mungu anasema kurudiwa kwao kutakuwa na utukufu mwingi zaidi.
Hivyo kuifahamu siri hii, itakuwasadia wewe ambaye umepata neema hii bure kutoichezea, bali kuithamini sana, kwasababu ikiwa wale waliipoteza, vivyo hivyo na sisi tunaweza ipoteza kwa kutokuamini kwetu. Na ndivyo itakavyokuja kuwa baadaye. Israeli watakaporudiwa kwa kipindi kifupi, sisi tutakuwa tumekwenda kwenye unyakuo, watakaobaki watalia na kuomboleza. Hivyo ni muhimu kuutimiza wokovu wako kwa kugopa na kutetemeka, kama maandiko yanavyotuambia (Wafilipi 2:12). Ithamini neema ya Kristo.
Kurudi kwa Bwana.
Kipindi kile Bwana alipokuwa duniani, wanafunzi walimuuliza kuhusiana na siku ya kurudi kwake, ndipo akawaeleza wazi kuwa hakuna mtu aijuaye, isipokuwa Baba tu (Mathayo 24:36). Lakini Kristo alipopaa juu alipokea ufalme na enzi na nguvu, maana yake pia alitambua mpango wote alipowekewa na Baba yake, tunalithibitisha hilo katika kuvunjwa kwa ile mihuri saba (Ufunuo 6).
Na baadaye tunaona biblia inasema..
Ufunuo 10:7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo SIRI YA MUNGU ITAKAPOTIMIZWA, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.
Hii siri ya Mungu itakayotimizwa ndio hiyo inayohusiana na kutambua wakati husika wa Bwana kurudi. Na ndio maana ukisoma katika vifungu vya juu kidogo utaona yapo mambo ambayo Yohana aliyasikia lakini akakatazwa kuyaandika. Kuonyesha kuwa ipo sehemu ya Neno la Mungu, ambayo haijafunuliwa kwetu sisi, Mungu atakuja kufanya hivyo baadaye.
Ufunuo 10:3 Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao. 4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.
Hivyo hii ndio siri moja tu, ambayo ipo ndani ya Kristo hatujafunuliwa bado. Lakini wakati u karibu.
Je! Unatambua kuwa hizi ni siku za mwisho, umejiandaaje na karamu ya mwana-kondoo mbinguni kwa tukio la unyakuo. Tubu dhambi zao, umegukie Kristo akupe ondoleo la dhambi zako bure. Ikiwa upo tayari leo kumpokea Yesu maishani mwako, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>>
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
SWALI: Nini maana ya Mithali 25:13
Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
JIBU: Kwa wanaoishi maeneo ambayo kuna misimu ya theluji, wanafahamu kuwa vipindi hivyo vya baridi vinapofika, huwa kunakuwa na upepo-baridi unaovuma.
Sasa kwa mujibu wa vifungu hivyo, anasema, Kama upepo huo ukivuma kipindi cha mavuno, ambacho kimsingi ni wakati wa kiangazi,na sio baridi, kingekuwa ni shangwe kubwa sana kwa wavunaji.
Kwa namna gani?
Kazi ya uvunaji inafanyika wakati wa jua kali, kwasababu mazao pia wakati huo yanakuwa yamekauka. Lakini pia mfano jua lile likapoozwa na upepo wa baridi, huuburudisha sana moyo wa mvunaji.
Vivyo hivyo anafananisha na wajumbe waaminifu wanaotumwa kupeleka habari fulani anasema;
“Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao”.
Mjumbe wa kwanza mwaminifu aliyetumwa ni Bwana wetu Yesu Kristo. Alimburudisha Baba moyo wake, kwasababu yote, na kusudi alilopewa kulifanya la kutukomboa sisi alilitimiza lote.
Vivyo hivyo na sisi, tumewekwa kuwa wajumbe wa Bwana, wa kuenenda kuihubiri injili ya Kristo kwa kila kiumbe, ulimwenguni kote. Yatupasa tuwe waaminifu, mfano wa Bwana na mitume wake, ili moyo wa Kristo wetu ufurahi.
Na thawabu ya kuuburudisha moyo wa Bwana ni sisi kupewa mamlaka kubwa kule ng’ambo tufikapo, kwa mfano ambao Bwana Yesu aliutoa katika vifungu hivi;
Luka 19:12-26
[12]Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
[13]Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.
[14]Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.
[15]Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.
[16]Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.
[17]Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
[18]Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.
[19]Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.
[20]Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.
[21]Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
[22]Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
[23]basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?
[24]Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.
[25]Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.
[26]Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.
Je na sisi tunaweza kuwa mbele za Bwana Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; ?
Bwana atusaidie.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Je! Umeokoka?
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?
WALIYATWAA MAVAZI YAKE, WAKAFANYA MAFUNGU MANNE,
Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?
SWALI: Je! ni sahihi kwa mkristo kufanya biashara za kifedha mitandaoni kama vile Forex, na crypto-currency mfano wa bitcons?
JIBU: Ni vema kufahamu biashara za kifedha mitandaoni kama forex ni nini?
Ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni katika soko la dunia. Yaani ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni, sawa tu ile tuliyowahi kuisikia, ijulikanayo kama Bureau de change, ambayo watu wanakwenda kununua/kuuza pesa za kigeni, isipokuwa hii hufanyika mitandaoni, tofauti na bureau ambayo hufanyika kwa makarati ndani ya ofisi Fulani maalumu. Biashara hii ya forex na nyinginezo Mara nyingi hufanywa na taasisi kubwa za kifedha kama mabenki na makampuni, lakini pia hata watu binafsi.
Ni biashara ya bahati nasibu, inayofanana na michezo ya kubahatisha kitabia.. Lakini ni tofauti kabisa kimaudhui.
Biashara hii ni ya uwekezaji, ambayo imehalalishwa ki-ulimwengu, japokuwa hatusemi kuwa kila biashara iliyohalalishwa na taifa kuwa ni halali kwa mkristo kufanya, hapana mfano zipo pombe zimehalalishwa kitaifa lakini kwa mkristo sio sawa kufanya biashara kama hizo.
Lakini, biashara hii, haihusishi katika kumdhulumu mtu, au kumlaghai mtu kiakili, apoteze kitu Fulani ili wewe ujilimbikizie fedha zake ambazo hazina mzungumko wowote wa kimaendeleo. Mfano wa hizo ni kama vile “Betting na kamari”. Kwa mkristo kushiriki katika biashara hizo za betting na kamari sio sawa. Kwa urefu wa somo lake pitia link hii >>>JE! KUBET NI DHAMBI?
Lakini Forex na nyinginezo zijulikanazo kama biashara za uwekezaji, zinahitajika sana, kwasababu kama zikikosekana, basi mzunguko wa fedha za kigeni, ungekuwa mgumu sana, na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji uchumi, katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia.
Hivyo tukirudi kwa mkristo, je kufanya biashara hii ni dhambi?
Kimsingi ikiwa anafanya kwa lengo la uwekezaji wake, huku akijua pia ni kwa faida ya uchumi, na hamdhulumu au kumlaghai mtu. Hafanyi kosa. Lakini akiwa na fikra za kikamari, kama vile afanyavyo kwenye betting, Kwake itakuwa ni kosa, kwasababu dhamiri yake inamshuhudia, ameigeuza kama kamari moyoni mwake.
Ndio hapo hili andiko linakuja.
Warumi 14:22 Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.
23 Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. NA KILA TENDO LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI.
Maana yake ni kuwa ukiwa na mashaka moyoni mwako kuifanya kazi hii, basi ni heri usifanye kabisa, kwasababu mashaka yoyote ni dhambi. Lakini kimsingi biashara hii sio kosa kwa mkristo, ambaye ana maarifa/elimu ya kutosha juu ya biashara za kifedha katika ulimwengu wa sasa.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)
KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.
Hesabu 16:20 Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 21 Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja. 22 Nao WAKAPOMOKA kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?
Soma pia
Yoshua 5:13 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?
14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua AKAPOMOKA kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?
Neno hilo utalisoma pia katika vifungu hivi baadhi; Hesabu 16:4, 16:45,
Ni Kiswahili cha zamani cha Neno kuporomoka. Yaani kuanguka chini, kwamfano maji yanayoelekea chini kwa wingi tunasema maporomoko ya maji, au udongo unaoanguka kutoka milimani kwa wingi tunasema maporomoko ya udongo.
Hivyo, katika vifungu anaposema Musa na Haruni wakapomoka kifudifudi, anamaanisha wakaanguka chini kifudi fudi mbele za Mungu kumlilia Bwana rehema.
Je! Na sisi tuombapo rehema au tumtakapo Bwana kwa jambo Fulani muhimu ni lazima tupomoke chini ili tusikiwe ?
Jibu lake ni kwamba sio takwa kufanya hivyo. Kwasababu Mungu anaangalia moyo, kupomoka kwetu kunapaswa kuwe moyoni. Lakini pia si vibaya kuomba kwa namna hiyo, na ni vema, kwasababu pia ni ishara moja wapo ya unyenyekevu wa moyo. Ni sawa tu na tunapopiga magoti, au kunyosha mikono juu wakati wa kumwomba Mungu, kama ishara ya unyenyekevu mbele zake.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Ni kwanini tunambariki Mungu? Je! Mungu huwa anabarikiwa?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2
Tunapokisoma kisa cha Daudi, cha kumwiba mke wa shujaa wake (Uria), na kumlazimisha kuzini naye kwa siri, na baadaye kumuua mumewe , (2Samweli 11) tunaishia kuona picha mbaya sana ya Daudi. Na kumshutumu, na wengi wetu kusema Daudi ni mzinzi sana, iweje apendwe na Mungu namna ile, tena awe kipenzi cha Mungu?
Ni kweli kabisa alichokifanya Daudi hakistahili kufanywa na mtu yeyote, ambaye anamjua Mungu, mfano wa Daudi. Lakini kuna funzo kubwa sana ambalo wengi wetu hatulioni nyuma ya maisha ya Daudi baada ya pale.
Daudi alipozama katika dhambi ile, na kugundua makosa yake. Alikuwa na badiliko lisilo kuwa la kawaida. Sio kule alikokuwa anaomboleza usiku kucha, Hapana, lile lingekuwa la “kufoji” tu, ambalo yoyote anaweza kulifanya hata leo. Kinyume chake Daudi alikuwa na badiliko la kimatendo. Na hilo ndilo lililomfanya apendwe sana na Mungu.
Kwa namna gani?
Sasa angalia Daudi Yule Yule ambaye alikuwa ni mzinzi, mwenye tamaa ya hali ya juu,akiona tu mwanamke mzuri hajali, huyu ni mke wa mtu au la yeye alimwiba na kuzini naye. Lakini Dakika zake za mwisho hazikuwa hivyo. Alibadilika kwelikweli baada ya dhambi ile.
Utakumbuka hata alipokuwa mzee, Wakuu wa Israeli walikwenda kumtafutia Binti mzuri bikira katika taifa lote la Israeli, ili amlalie Daudi ampe joto kwasababu nguo za joto hazikutosha. Lakini biblia inasema Daudi alipolala naye ‘hakumjua’.
Kwa jinsi ya kibinadamu, binti alale, na mtu mwenye sifa ya tamaa kama Daudi, halafu asimwingilie. Lazima kutakuwa kuna jambo lingine limetendeka ndani ya maisha ya huyo mtu.
Tusome;
1 Mfalme 1:1
“Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto.
2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto.
3 Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.
4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua”
Ni wazi kuwa habari hiyo ilijulikana Israeli nzima, Daudi amelala na binti bikira mrembo miaka kadhaa lakini hajamwingilia. Ni shujaa kiasi gani. Hawakujua kuwa anawathibitishia Israeli kuwa yeye sio Yule wa zamani, sio Yule mzinzi mliyemzoea, ameshabadilika. Si mtu wa kulipuka lipuka tamaa ovyo kama alivyokuwa hapo mwanzo.
Hiyo ndio sababu Mungu alimpenda Daudi. Kwasababu alikuwa na badiliko la dhati Kwa Mungu wake. Je! Na sisi, tunaweza kusema tumeuacha ulimwengu kweli kweli pale tunapomgeukia Mungu, au tutakuwa na vimelea vya kidunia ndani yetu, pale tunapokutana na majaribu kama yale yale ya mwanzo. Tulipokuwa wazinzi na sasa tumeokoka, Je! Tuna ujasiri wa kuishi maisha ya mbali zinaa, au bado tupo nusu nusu.
Tuwe na badiliko la dhati, leo tumeanguka katika dhambi Fulani mbaya, sasa tumetubu, tusiwe tena walewale wa kuanza kuangalia angalia nyuma kama mke wa Lutu. Mungu atakuchukizwa na sisi na mwisho wa siku tutakuwa jiwe la chumvi kama sio kutapikwa mfano wa kanisa la Laodikia.
Tumaanishe kwelikweli kuacha mambo maovu tuliyoyazoelea. Jifunze kwa Daudi. Yule sio mzinzi kama wewe unayejitumaisha kwa visa vyake vya zamani, ukadhani kuwa utanusurika hukumu ikiendelea na tabia hiyo.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?(Opens in a new browser tab)
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 4
Kwanini Daudi achukue mawe matano, na malaini na sio vinginevyo?
(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.(Opens in a new browser tab)
Manabii Wanaume katika biblia walikuwa wengi kiidadi kuliko manabii wanawake.
UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA JEDWALI:
Kutazama Jadwali zima, basi Slide kuelekea upande wa kushoto.
N/A | JINA | WAFALME WALIOTAWALA ENZI ZAKE | MIJI/MATAIFA ALIYOYATOLEA UNABII | MAJIRA ALIYOTOA UNABII |
---|---|---|---|---|
1. | ELIYA | Ahabu, Ahazia na Yoramu | ISRAELI | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
2. | ELISHA | Yoramu, Yehu na Yehoahazi | ISRAELI | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
3. | YONA | Yeroboamu wa Pili | NINAWI (Ashuru) | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
4. | NAHUMU | Manase, Amosi na Yosia | NINAWI (Ashuru) | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
5. | OBADIA | Sedekia | EDOMU | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
6. | HOSEA | Yeroboamu wa Pili, Zekaria, Shalumu, Menahemu, Pekahia,Peka na Hoshea | ISRAELI | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
7. | AMOSI | Yeroboamu wa Pili | ISREALI | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
8. | ISAYA | uzia, Yothamu, Ahazi, Hezekia na Manase | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
9. | YEREMIA | Yosia, Yehoahazi,Yehohakimu, Yekonia na Sedekia. | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
10. | YOELI | Yoashi | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
11. | MIKA | Yothamu, Ahazi, Hezekia na Manase. | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
12. | HABAKUKI | Yehoyakimu na Yekonia | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
13. | SEFANIA | Amoni na Yosia | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
14. | EZEKIELI | Yekonia na Sedekia | YUDA (Ikiwa utumwani Babeli) | Wakati YUDA Ikipelekwa utumwani Babeli |
15. | DANIELI | Yehohakimu, Yekonia na Sedekia. | YUDA (Ikiwa utumwani Babeli) | Wakati YUDA ikiwa utumwani Babeli |
16. | HAGAI | Liwali ZERUBABELI | YUDA (Masalia waliorudi Yerusalemu kutoka utumwani) | Baada ya YUDA kutoka utumwani Babeli |
17. | ZEKARIA | Liwali ZERUBABELI | YUDA (Masalia waliorudi Yerusalemu kutoka utumwani) | Baada ya YUDA kutoka utumwani Babeli |
18. | MALAKI | Liwali NEHEMIA | YUDA (Masalia waliorudi Yerusalemu kutoka utumwani) | Baada ya YUDA kutoka utumwani Babeli |
Mbali na hawa walioorodheshwa katika Jedwali hilo hapo juu, walikuwepo pia Manabii wengine ambao hawakuonekana wakitajwa katika kutoa Nabii za Nchi au Taifa.. Mfano wa hao tunawaona katika Jedwali lifuatalo.
N/A | JINA | MFALME ALIYETAWALA WAKATI WAKE | HALI KIROHO | MAREJEO |
---|---|---|---|---|
1. | MUSA | Isreli wakiwa Misri na Jangwani | WA KWELI | Kutoka, M/Walawi, Kumbukumbu na Hesabu |
2. | MIKAYA | Ahabu | WA KWELI | 1Wafalme 22:13 |
3. | AHIYA | Yeroboamu | WA KWELI | 1Wafalme 1:45 |
4. | NATHANI | Sauli | WA KWELI | 2Samweli 7:2 |
5. | Nabii wa Yuda (Asiyetajwa jina) | Yeroboamu wa Kwanza | WA KWELI | 1Wafalme 13:1-9 |
6. | Nabii MZEE (Asiyetajwa jina) | Yeroboamu wa kwanza | MCHANGANYIKO | 1Wafalme 13:11-14 |
7. | HANANIA | Yekonia na Sedekia | WA UONGO | Yeremia 28:15-17 |
8. | Manabii 400 (wasiotajwa majina) | Ahabu | WA UONGO | 1Wafalme 22:6 |
9. | BALAAMU | Israeli wakiwa Jangwani | WA UONGO (Mchawi) | Yoshua 13:22 |
10. | BAR-YESU | Nyakati za kanisa la Kwanza | WA UONGO (Mchawi) | Matendo 13:9 |
11. | AGABO | Nyakati za kanisa la Kwanza | WA KWELI | Matendo 11:28 na Matendo 21:10 |
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU
Nini maana ya Mithali 11:17 inaposema;
Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake.
JIBU: Mwenye rehema ni mtu wa huruma, mwenye kusamehe, mwenye kuachilia hata kama tendo alilofanyiwa linastahili adhabu kwa yule mwingine.
Biblia inasema mtu kama huyo huipa faida nafsi yake. Huitendea mema nafsi yake. Ambayo huipata kwanza hapa hapa duniani, kwasababu Bwana alisema kipimo kile tupimacho ndicho tutakachopimiwa na watu.
Marko 4:24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.
Maana yake ni anajijengea wigo mpana wa yeye naye kukutana na rehema nyingi mbeleni.
Vilevile anapata faida katika ulimwengu ujao, Bwana alisema..
Mathayo 5:7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
Lakini anasema pia, mtu mkali hujisumbua mwili wake. Mtu mkali ni kinyume cha mtu mwenye rehema, ni mtu asiye na huruma, mwenye visasi, asiyejali, mkorofi, akiudhiwa anarudisha Maudhi, akikosewa kidogo, analipiza mara mbili, maneno yake hayana staha, kugombeza wengine kwake ni jambo la kawaida n.k.
Sasa matokeo ya mtu wa namna hii ni kuadhibiwa na Mungu, aidha hapa hapa duniani, au kule aendapo.
Bwana alisema…auaye kwa upanga, atauwawa kwa upanga, ukimtendea mtu kwa ukali na wewe ukali utakurudia, ukimpiga mwingine kwasababu kakuudhi kidogo, na wewe utapigwa mahali fulani kwasababu ulimuudhi mwingine.. (hicho huitwa kisasi cha Mungu).
Hivyo tendea mema nafsi yako, lakini pia mwili wako, kwa kumpenda Bwana. Na kuwa mwema.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.(Opens in a new browser tab)
Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)
(Opens in a new browser tab)NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.(Opens in a new browser tab)
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?(Opens in a new browser tab)
SWALI: Nini maana ya Mithali 20:11 inaposema;
Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.
JIBU: Mwandishi anatuonyesha kuwa tabia ya mwanadamu yoyote, huwa haijifichi kufuatana na umri wake, kwamba yaweza kukaa ndani tu kipindi cha utotoni isionekane ikaja kudhihirika ghafla ukubwani. Hapana, anasema “Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili”.
Ikiwa na maana katika utoto ule ule unaweza kuuchunguza mwenendo wa mtoto, ukautambua. Na hiyo itakupa fursa ya kuurekebisha ukiwa ni mbaya, au kuuimarisha ukiwa ni mzuri, akiwa katika vipindi kile kile. Usione mwanao anayotabia ya udokozi, ukasema huyu ni mtoto tu, haelewi anachokifanya. Hapana unapaswa umrekebishe mapema, kwasababu hicho kitu kipo ndani yake, Ukiona mtoto anapenda kutazama biblia, anapenda kukaa kanisani, anapenda kusikiliza nyimbo za injili. Usiseme, huyu ni mtoto, ukampuuzia tu, kwa kuishia kusema ‘ubarikiwe mwanangu’ kinyume chake, mwendelezee mazingira hayo, kwasababu mwelekeo wa maisha yake, ni huko.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo, tabia zake zilianza kuonekana tangu utotoni, wazazi wake walimstaajabia, kumwona katika umri ule mdogo, yupo hekaluni, amekaa na waalimu na wakuu wa dini akiwauliza maswali, Kinyume chake wazazi wake hawakumkemea, bali waliyaweka yote mioyoni mwao, na kukubali kuutambua mwelekeo wa mtoto wao.
Hii ni kufundisha nini?
Lipo funzo la rohoni, lakini pia la mwilini.
La mwilini ni kuwa yatupaswa tuwatazame watoto, bila kupuuzia kitendo chochote wanachokidhihirisha katika umri ule wa chini. Ikiwa ni chema tukipalilie, ikiwa ni kibaya, tukikemee, na kushughulika nacho kwelikweli kabla hakijaweka mizizi. Hivyo hakuna mzazi au mlezi anaweza kusema, huyu mwanangu kabadilika tu ghafla. Ukweli ni kwamba mabadiliko yalianza kuwepo tangu zamani, isipokuwa kwa namna moja au nyingine tulipuuzia, tulipoyaona ndani yao tukadhani ni tabia za utoto tu. Wazazi wanaowajenga wanao katika maadili na vipawa tangu utotoni, ukiwatazama watoto wao wanapokuwa watu wazima, huwa wanakuwa na ufanisi na ujuzi wa hali ya juu sana, zaidi ya wale ambao watajijengea wenyewe wanapokuwa watu wazima. Hivyo mzazi jali maisha ya kiroho ya mwanao.
Vilevile rohoni, wapo ambao ni wachanga kiroho. Ikiwa na maana katika kanisa ni wale ambao wameokoka hivi karibuni. Halikadhalika hawa nao utaweza kutambua karama zao, sio mpaka wawe wakomavu kiroho. Aliye Mwinjilisti, utaona anapenda kushuhudia, lakini pia anauwezo wa kuwavuta wengine kwa Bwana. Aliye mwalimu, utaona anapenda sana kujifunza, aliye nabii, utaona karama za maono, ndoto, huwa zinamjia mara kwa mara, hata kwa namna ambazo hazielewi elewi, mwimbaji atapenda wakati mwingi kujifunza kuimba hata kama hawezi. Hivyo, kila mmoja wetu, kitu ambacho Mungu amekiweka ndani yake, hujidhihirisha mapema sana pindi ameokoka. Sio mpaka awe amekomaa sana kiroho kama wengi wanavyodhani.
Pindi unapookoka, kipindi hicho hicho karama yako inaanza kufanya kazi, unapachopaswa tu, ni kujishughulisha na utumishi wa Bwana, ndivyo utakavyoruhusu mambo hayo kutokea kwa wepesi na urahisi zaidi?
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
(TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
MAANA WEWE, BWANA HUKUWAACHA WAKUTAFUTAO”.(Opens in a new browser tab)
Wafalme waliotawala ISRAELI, ukiwatoa wale watatu wa Mwanzo (Yaani Sauli, Daudi na Sulemani) walikuwa ni Wafalme 19 tu, na hakukuwa na Malkia aliyetawala Israeli kama ilivyokuwa kwa YUDA.
Kati ya Wafalme hao 19 waliotawala Israeli, hakuna hata mmoja aliyekuwa Mkamilifu mbele za MUNGU katika ukamilifu wote kama ilivyokuwa kwa baadhi ya Wafalme waliotawala YUDA. Isipokuwa Mfalme mmoja tu aliyeitwa YEHU ndiye angalau alionekana kufanya Mema lakini pia alifanya na Mabaya.
UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA TAKWIMU.
JINA | MIAKA ALIYOTAWALA | MATENDO | MAREJEO | |
---|---|---|---|---|
1. | YEROBOAMU | 22 | MABAYA | 1Wafalme 12:25-33 |
2. | NADABU | 2 | MABAYA | 1Wafalme 15:25-31 |
3. | BAASHA | 24 | MABAYA | 1Wafalme 15:33-16:7 |
4. | ELA | 2 | MABAYA | 1Wafalme 16:8-14 |
5. | ZIMRI | 7 | MABAYA | 1Wafalme 16:15-20 |
6. | OMRI | 12 | MABAYA | 1Wafalme 16:21-27 |
7. | AHABU | 22 | MABAYA | 1Wafalme 16:29-33 |
8. | AHAZIA | 2 | MABAYA | 1Wafalme 22:51-53 |
9. | YORAMU | 12 | MABAYA | 2 Wafalme 1:17, 3:1-3 |
10. | YEHU | 28 | Nusu Mema- Nusu Mabaya | 2 Wafalme 9:30, 10:36 |
11. | YEHOAHAZI | 17 | MABAYA | 2 Wafalme 13:1-9 |
12. | YEHOASHI | 16 | MABAYA | 2 Wafalme 13: 10-25 |
13. | YEROBOAMU II | 41 | MABAYA | 2 Wafalme 14:23-29 |
14. | ZEKARIA | 6 | MABAYA | 2 Wafalme 15:8-12 |
15. | SHALUMU | Mwezi 1 | MABAYA | 2 Wafalme 15:13-16 |
16. | MENAHEMU | 10 | MABAYA | 2 Wafalme 15:17-22 |
17. | PEKAHIA | 2 | MABAYA | 2 Wafalme 15:23-26 |
18. | PEKA | 20 | MABAYA | 2 Wafalme 15:27-31 |
19. | HOSHEA | 9 | MABAYA | 2 Wafalme 17:1-7 |
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine: