SWALI: Je! watu wanapaswa wakemewe au wasikemewe pale wanapofanya dhambi kulingana na 1Timotheo 5:1 na 20?
JIBU: Tusome,
1 Timotheo 5:1-2
[1]Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu; [2]wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.
[1]Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;
[2]wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.
Na,
1 Timotheo 5:20
[20]Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.
Mwandishi anatoa maelezo katika mazingira mawili tofauti. Mazingira ya kwanza ni katika eneo la marekebisho na mazingira ya pili ni katika eneo la makosa ya makusudi.
Kwamfano katika vifungu hivyo vya kwanza, anavyosema Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;analenga hasaa katika makosa ambayo yanajitokeza katikati ya huduma au maisha ya kikristo, kwamfano pengine mtu katika kuhudumu kwake kaonyesha uvunjifu fulani wa nidhani ya kimadhabahu, au kasema lugha isiyo ya staha, au kavaa vazi lisilo na heshima, au kabagua wengine, au kawadhulumu wengine, n.k. ambayo imesababishwa na uchanga wa kiroho au madhaifu ya kibinadamu.
Katika mazingira kama hayo Paulo anamhimiza Timotheo, kulingana na marika yao asitumie kukemea bali awaeleze kwa upole, nao watajirekebisha, akitambua kuwa wapo katika hatua za kuutafuta ukamilifu.
Lakini katika hivyo vifungu vya pili. Analenga Zaidi kwa wale wanaodumu kutenda dhambi. Wanaojua kabisa wanachokifanya sio sahihi, lakini wanaendelea kudumu kufanya hivyo, Paulo anasema hawapaswi kuvumiliwa bali kukemewa mbele ya watu wote.
Kwamfano mtu ni mzinzi, na tabia hiyo anaendelea nayo kanisani, au ni mlevi, au mchonganishi, sasa hawa wanapaswa wakemewe hadharani bila kujali marika yao, ili wengine wasiige Tabia hizo. Kwasababu wakiachwa wataendelea kulichachusha kanisa.
Makanisa mengi leo hii yamekumbwa na matatizo makubwa mpaka kusababisha jina la Kristo kutukanwa Nje, ni kutokana na kuvumiliwa kwa watu wa namna hii wanaodumu katika kutenda dhambi.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kuna hukumu za aina ngapi?
Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).
USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE.
Print this post
Swali: Madongoa kama inavyosomeka katika Ayubu 7:5, ni kitu gani, na ina ujumbe gani kiroho?.
Jibu: Turejee..
Ayubu 7:5 “Mwili wangu unavikwa mabuu na MADONGOA YA UDONGO; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena”.
Madongoa ni udongo ulioshikamana pamoja, sawasawa na Ayubu 38:38..
Ayubu 38:38 “Wakati mavumbi yagandamanapo, Na madongoa kushikamana pamoja?”
Kikawaida ardhi yenye Madongoa haifai kwa kilimo, bali mpaka madongoa hayo yatakapovunjwa na kulainishwa, ndipo mbegu ziweze kupandwa…
Isaya 29:23 “Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu. 24 Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima MADONGOA YA NCHI YAKE, na kuyavunja? 25 Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huko na huko kunde, na kutupa-tupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake? 26 Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha”.
Isaya 29:23 “Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu.
24 Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima MADONGOA YA NCHI YAKE, na kuyavunja?
25 Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huko na huko kunde, na kutupa-tupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake?
26 Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha”.
Neno hili pia tunaweza kulisoma katika kile kitabu cha Hosea 10:11..
Ni ni nini tunachoweza kujifunza??
Kama vile ardhi yenye madongo ilivyokuwa ngumu kwa kilimo, hali kadhalika mioyo yetu inafananishwa na shamba sawasawa na ule mfano wa Mpanzi (Mathayo 13:18-23), na kama mioyo yetu ni migumu kwa namna hiyo basi ni ngumu pia kumzalia MUNGU matunda.
Mfano wa moyo wenye madongoa ni ule ulio mgumu kusikia Neno, mtu mwenye moyo wa kupuuzia, na kutokujali pale asikiapo Neno la MUNGU, mtu wa namna hii anahitaji sana kusaidiwa.
Je ni wewe mtu huyo?. Kama ndio basi mkimbilie YESU leo kwa kumaanisha kabisa naye ataufanya maoyo wako kuwa mlaini, na utayaona matunda ya BWANA.
Tufanyaje ili tuonekane tunampenda Mungu?
KWANINI MIMI?
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?
MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.
JE UNA MATUMAINI YA KUPATA TENA KILE ULICHOPOTEZA?
Rudi Nyumbani
WhatsApp
Swali: Je Mungu ni mkaidi kulingana na Zaburi 18:26, au kwanini Mungu aseme maneno hayo?
Jibu: Tuanzie kusoma ule mstari wa 24, ili tupate maana kamili..
Zaburi 18:24 “Mradi Bwana amenilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake. 25 Kwa mtu mwenye fadhili UTAKUWA MWENYE FADHILI; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu; 26 KWAKE AJITAKASAYE UTAJIONYESHA KUWA MTAKATIFU; Na KWA MPOTOVU UTAJIONYESHA KUWA MKAIDI”
Zaburi 18:24 “Mradi Bwana amenilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
25 Kwa mtu mwenye fadhili UTAKUWA MWENYE FADHILI; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;
26 KWAKE AJITAKASAYE UTAJIONYESHA KUWA MTAKATIFU; Na KWA MPOTOVU UTAJIONYESHA KUWA MKAIDI”
Hapo anasema kwa mtu mwenye fadhili Bwana atajionyesha mwenye fadhili kwake, na kwa ajitakasaye Bwana atajionyesha ni mtakatifu kwake, vile vile na kwa mpotovu atajionyesha mkaidi.
Sasa kwa maneno hayo haimaanishi kuwa Bwana ni MKAIDI..La! yeye ni mwema siku zote na hawezi kufananishwa na sisi wanadamu…Lakini sasa swali ni kwanini aseme hivyo?
Ili tuelewe vizuri tafakari mfano huu; Unaye mtoto halafu ukaanza kuona anaonyesha tabia za kukosa nidhamu, na anafanya mabaya mengi, na ulipomwonya haonyeki, kisha ukaamua kumwambia kuwa endapo akiendelea kuwa na tabia hiyo, utakuwa mbaya kwake!..na akibadilika kuwa mzuri basi utakuwa mzuri kwake…
Je kwa kauli hiyo utakuwa umemaanisha kuwa wewe ni ni MTU MBAYA na MWOVU?.. bila shaka hutakuwa umemaanisha hivyo, bali utakuwa umemaanisha kuwa endapo akiendelea kufanya mabaya, basi utambadilikia na kumwadhibu, jambo ambalo ni baya machoni pa huyo mtoto, na ndicho Bwana Mungu alichomaanisha hapo kuwa kwa “mtu mpotovu atajionyesha kuwa Mkaidi”… Na si kwamba MUNGU ni Mkaidi.
Kwamba kwa mtu anayefanya mabaya Bwana na maovu na hakubali kuonyeka basi atapata mabaya kutoka kwa Mungu, kwani BWANA atamwadhibu,…Na adhabu za Bwana ni za lengo la kuonya, na kumfanya mtu aache njia mbaya, na si za kumpoteza mtu.
Waebrania 12:10 “Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. 11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. 12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, 13 mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe. 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”
Waebrania 12:10 “Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.
12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,
13 mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”
Na kinyume chake ni kweli, kwa mtu ajitakasaye, yeye Bwana atajionyesha mtakatifu kwake, Maana yake ataona mema mengi kutoka kwa Bwana..
Hivyo hiyo ni tahadhari kwetu na pia ni faraja kwetu, kwamba tukae katika usafi na utakatifu, ili tuuone wema wa Mungu, na tusikae katika upotovu, tusije tukauona ukaidi wa MUNGU, kwani Bwana atajionyesha kwa kila mtu sawasawasa na matendo yake.
ZIKUMBUKE FADHILI ZA MUNGU
Kama ulimwengu ujao utakuwa na watakatifu tu, sasa hao watakaotawaliwa watatoka wapi?
TAA YA MWILI NI JICHO
TULITAFUTE KWA BIDII TUNDA LA ROHO.
Mwandishi na Uchambuzi wa kitabu cha Wakorintho wa pili (2Wakorintho)
Kama kitabu kinavyojitambulisha, “Waraka wa pili wa Petro kwa watu wote”
Petro ndiye mwandishi. Ni waraka mfupi, aliouelekeza kwa watakatifu wote duniani.
Na haya ndio maudhui yake makuu;
Haya ndio maelezo ya kila kipengele kwa ufupi;
Petro anawahimiza watakatifu wasikwamwe kiroho bali waendelee kukua, mpaka kufikia utimilifu wao ambao ni upendo, Na kwamba mtu asipojitahidi kufanya hivyo matokeo yake ni kuwa atakuwa mvivu, na hatimaye atajikwaa.
2 Petro 1:3-8
[3]Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. [4]Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. [5]Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, [6]na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, [7]na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. [8]Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
[3]Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
[4]Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
[5]Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,
[6]na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,
[7]na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
[8]Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
Mtume Petro anatoa hakikisho la ushuhuda wao juu ya ujio wa Kristo, kwamba hawakuupokea katika hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali walishuhudia wao wenyewe kwa macho, walipotokewa na Musa na Eliya juu ya mlima ule mrefu na kuisikia sauti ya Mungu mbinguni moja kwa moja ikimshuhudia Yesu kuwa ndiye mwana wa Mungu, aliyependwa naye.
2 Petro 1:16-17
[16]Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. [17]Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. [18]Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.
[16]Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.
[17]Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
[18]Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.
Lakini pia anawahimiza kujiepusha na manabii wa uongo, ili wasije wakachukuliwa na makosa Yao, wakaangamia tena. Ambao sifa zake nyingi ameziorodhesha pale (kwenye sura yote ya pili), Sifa zao ni pamoja na tamaa na uzinzi, akiwataja kama watu wasiokoma kutenda dhambi, wasaliti wa Bwana, wenye uhodari wa kutunga maneno wenye werevu, ili wawavute watu kwao, wenye kupenda ujira wa udhalimu kama Balaamu, watoao maneno ya makufuru, watu wa kujikinai, wasio na hofu ya Mungu, watu wa anasa, wa kuhadaa watu waliosimama imara, ili wawaaungushe.
2 Petro 3:17
[17]Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu.
Petro pia anawahimiza watakatifu wawe na tumaini juu ya uthabiti wa kurudi kwa Bwana,
akiwatahadharisha juu ya kuibuka kwa kundi la watu wenye kudhihaki, wanaosema iko wapi ile ahadi,mbona muda mrefu umepita? lakini Petro analirekebisha kwa kulitolea maelezo kuwa Mungu hakawii kutimiza ahadi yake bali anavumilia ili watu wote wafikie toba. Lakini siku hiyo itakuja kama mwizi, na ulimwengu ukaliwao na waovu utaharibiwa.
2 Petro 3:9-13
[9]Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. [10]Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. [11]Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, [12]mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? [13]Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
[9]Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
[10]Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
[11]Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
[12]mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
[13]Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
Mwisho, mtume Petro anaeleza uthabiti wa yale anayowaeleza, akiwatolea mfano kwa kurejea pia nyaraka za mitume wengine (akimtaja Paulo).Kama pia anayaeleza mambo hayo hayo ayasemayo katika nyaraka zake.
Petro 3:15-16
15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenziPaulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katikanyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu,wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu waowenyewe.
Hivyo kwa ujumla maudhui ya waraka huu ni kuwahimiza watakatifu kufanya bidii katika ukamilifu na kujiepusha na manabii wa uongo, na kuchoka kungojea ahadi za Mungu. Bali waendelee mbele kutibitika katika ukamilifu bila wala wala hila hadi siku ya kutokea kwake Bwana Yesu mara ya pili.
Je wewe kama mkristo unayemngojea Bwana. Unafanya imara wito wako na uteule wako, kwa kukua kila siku katika neema kiasi cha kukufanya ujione huna mawaa wala aibu, katika siku ile ya Bwana?
Kama sio, basi wakati ndio huu, Maanisha kugeukia kumfuata Kristo.
Mwandishi na Uchambuzi wa kitabu cha kwanza cha Petro.(1Petro)
Fahamu Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ni nani.
Mwandishi na uchambuzi wa kitabu cha Wakorintho wa kwanza (1Wakorintho)
SWALI: Konstantino mkuu ni nani, na je umuhimu wake katika ukristo ni upi?
JIBU: Konstantino mkuu ni Mmoja wa wafalme waliotawala chini ya dola ya Rumi, Kuanzia mwaka wa 306BK mpaka 337BK.
Dola hii ya Rumi ndiyo dola iliyokuwa na nguvu sana, zaidi ya zote zilizowahi kutokea katika historia, ilifanikiwa kutawala kikamilifu katika nyanja karibia zote, za kijeshi, kisiasi hadi kiuchumi, na ndio ngome iliyodumu kwa muda mrefu kuliko zote.
Itakumbukwa kuwa hata wakati Kristo anakuja duniani, dola hii ndio ilikuwa inatawala ulimwenguni kote na Kaisari ndiye aliyekuwa mfalme. Israeli wakati huo halikuwa taifa huru kama tunavyoliona sasa, bali ilikuwa koloni la Rumi, na watalawa na maliwali wake wote akiwemo, Pilato na Herode walikuwa ni Warumi.
Utawala huu ndio uliomsulubisha Kristo kwa shinikizo la wayahudi. Lakini tunaona katika historia, injili ilipoanza kuhubiriwa na jamii kubwa ya watu kugeuzwa kuwa wakristo duniani kote, Utawala huu ulianza kulitesa kanisa, na hata baadhi ya wafalme wao waovu waliotokea walitunga sheria kwamba ikionekana mtu yeyote anajiita mkristo, basi adhabu yake ilikuwa ni kifungo kama sio kifo.
Mfano wa watawala hawa alikuwa Nero, trajan, na Domitian, Na hiyo ilipelekea jamii kubwa sana ya wakristo kuuawa kikatili, wengine kuchomwa moto, wengine kusulubiwa, wengine kuwekwa katika viwanja vya mauaji na kuachiwa wanyama wakali wawaue, idadi ya mamilioni ya wakristo walipoteza maisha kwa njia hii. Historia hiyo utaipata vema katika kitabu maarufu kijulikanacho kama (Foxes book of martyrs). Kumbuka utawala uliohusika ulikuwa ni huu wa Rumi, chini ya watawala wao mbalimbali.
Hivyo kwa wakati wote huo ukristo ulionekana kama imani ya vikundi fulani vya wavuruga amani..
Wakati huo Rumi lilikuwa ni taifa la kipagani likiongozwa kisiasa, chini ya dini zao za miungu mingi.
Lakini alipokuja kutokea huyu mtawala mpya aliyeitwa Kostantino baada ya watawala 59 kupita nyuma yake,
Kwa mujibu wa ushuhuda wake anasema wakati anakwenda kupigana vita mojawapo kuu iliyomkabili, katika maono aliona..msalaba angani, akaambiwa kwa ishara hii utashinda. Hivyo Konstantino akaichukua nembo ya ukristo na kuipachika katika ngao za jeshi lake, na hivyo akashinda vita ile iliyokuwa inamkabili, ushindi huo ulimuimarishia sana ufalme wake.
Huo ndio ukawa mwanzo wake wa kuwa mkristo. Aliendelea kuupa sana kipaumbele ukristo, Kuanzia huo wakati ndio ukawa mwisho wa mauaji ya watakatifu. Na mwanzo wa dini ya Kikatoliki.
Lakini historia inaonyesha Konstantini hakuwa ameupokea ukristo katika ukamilifu wote, kama madhehebu baadhi yanavyoamini. Bali ukristo wake ulikuwa na msukumo wa kisiasi pia nyuma yake, ambao ulilenga kuwaunganisha wakristo na warumi wakipagani, kwasababu hakuacha pia kuabudu miungu yake ya kirumi. Ndio maana ibada gheni za miungu zilichanganywa na imani ya mitume, kwa kuzaliwa kanisa katoliki na kulipelekea kanisa kuingia katika kipindi kirefu sana cha ukimya kijulikanacho kama kipindi cha giza.
Pamoja na hayo ni kweli alifanikiwa kukomesha mateso kwa wakristo, na kuuthaminisha ukristo, na wakati mwingine kuruhusu mabaraza ya Wakristo, kuthibitisha vipengele kadha wa kadha vya imani, vilivyoleta msaada mwingi.
Lakini pia hakuuingiza Ukristo Katika misingi yake yote, ndio maana kanisa liliongia katika kipindi cha giza.
Hata hivyo kwa sehemu yake alisimama kuanzisha Imani ijapokuwa hakufanya katika utimilifu wote. Ilikuwa ni wajibu wa mabaraza Na wazee na watakatifu, Kuyatengeneza yaliyosalia, lakini hawakupiga hatua yoyote zaidi ya pale kwa miaka mingi.
Lakini ashukuriwe Mungu wakati wa matengenezo ulipofika (Karne ya 15)..Bwana aliwanyanyua watu wake mbalimbal8 mfano wa Martin Luther, Zwingli, Calvin na wengineo kulitengeneza upya kanisa kutoka katika misingi mibovu Mpaka wakati wa Pentekoste, ambapo kanuni zote za Kibiblia zilirejeshwa. Na mpaka sasa Kanisa linazidi kupanda katika utumilifu wake wote.
Hivyo ni wajibu wetu, sote kusoma biblia na kuifahamu kwa kina kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu, lakini pia kuhubiri injili kwasababu kwa njia hiyo ndivyo tutakavyoujenga ufalme Wa Kristo Na kuufanya uenee duniani kote, kiufasaha.
Naliupata wenyeji huu kwa mali nyingi, maana yake nini (Matendo 22:28)
UKristo Ni Nini?
Je! Mtume Paulo alikuwa ni Mrumi, Myahudi au raia wa Tarso?
Kichwa cha kitabu hichi kinasema “Waraka wa kwanza wa Petro kwa watu wote” Kutuonyesha kuwa Petro Ndiye mwandishi.
Waraka huu mfupi aliuelekeza kwa watakatifu wote waliotawanyika, na kuishi kama wageni maeneo ya Asia ndogo ambayo kwasasa ni nchi ya Uturuki.
Maudhui makuu ya waraka huu tunaweza kuyagawanya katika sehemu kuu nne(4):
1) Ni kuwafariji watakatifu kwa kuwaeleza juu ya utukufu walioandaliwa mbinguni utakaofunuliwa siku ya mwisho. Na kwamba kwa kulitambua hilo basi wafurahi Katika majaribu mbalimbali ya imani, yaliyo ya kitambo tu.
2) Lakini pia unalenga kuwahimiza kuishi maisha ya utakatifu ya kumpendeza Mungu katika wakati wao wa kuishi hapa duniani.
3) Vilevile wajibu wakuishi maisha ya nidhamu katika Jamii ya wasioamini inayowazunguka.
4) Halikadhalika wajibu wa viongozi kulichunga kundi la Kristo kwa uaminifu wotena wajibu wa kanisa lote kumpinga shetani.
Haya ni maelezo mafupi juu ya kila kipengele:
Petro anawahimiza watakatifu kwamba wafurahi katika majaribu mbalimbali (kuliko kuhuzunika) kwa sababu ya uthamani mkuu wa imani yao itakayolipwa siku ile ya mwisho ambayo Yesu atafunuliwa kwetu.
1 Petro 1:6-7
[6]Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; [7]ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
[6]Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
[7]ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
> Petro Anahimiza kuiga kielelezo cha Kristo ambaye yeye alikubali kuteswa ijapokuwa hakutenda Dhambi, hata alipotukanwa hakurudisha majibu. Vivyo hivyo na sisi tukubali teso lolote kwa ajili yake katika upole wote, uvumilivu na ustahimilivu.
1 Petro 2:19-21
[19]Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki. [20]Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu. [21]Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
[19]Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki.
[20]Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.
[21]Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
1 Petro 4:12-16
[12]Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. [13]Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. [14]Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. [15]Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. [16]Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
[12]Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.
[13]Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.
[14]Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.
[15]Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.
[16]Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
Sehemu hii ya pili Mtume Petro anawahimiza watakatifu, kuwa kwasababu wanatazamia neema itakayofunuliwa siku ya mwisho ya kuja kwake Yesu Kristo (1:13), hivyo hawana budi kuishi maisha ya kiasi na utakatifu hapa duniani.
1 Petro 1:13-16
[13]Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. [14]Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; [15]bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; [16]kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
[13]Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.
[14]Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu;
[15]bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
[16]kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
1 Petro 2:1-2
[1]Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. [2]Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
[1]Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
[2]Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
> Petro anaendelea kuwasihi watakatifu waishi kama wapitaji duniani, kwa kuziepuka tamaa za mwili.
1 Petro 2:11
[11]Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
1 Petro 4:2-3
[2]Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. [3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
[2]Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
[3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
> Anaeleza pia Wajibu wa kupendana kuhurumiana, kunyenyekeana, tuwe watu wasiolipa baya kwa baya, bali wenye kubariki(3:8-12, 4:7)
> Kadhalika pia anaeleza wajibu wa wanandoa. Kwamba wake wawatii Waume zao, na kujipamba kwao kunapaswa kuwe kwa mapambo ya rohoni, Lakini pia waume kuishi na wake zao kwa akili. (3:1-7)
Katika sehemu hii ya tatu anahimiza watakatifu kuwa na mwenendo unaopasa kwa watu wasioamini, ili wakose nafasi ya kutushitaki au kutulaumu kwa lolote.
> Anagusia katika eneo la watumwa Kwamba wawatii bwana zao, si wale tu wapole bali pia wale wakali.(2:18)
> Lakini pia Watakatifu waitii kila kilichoamriwa na mamlaka.
1 Petro 2:13-15
[13]Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; [14]ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema. [15]Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;
[13]Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;
[14]ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.
[15]Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;
> Lakini pia anahimiza watakatifu wawaheshimu watu wote(2:17)
Mwishoni Petro anatoa wito wa waangalizi wa kanisa la Mungu (wazee), kwamba walichunge kundi kwa hiari, sio kwa kulazimishwa au kutazamia malipo ya kifedha, bali kwa moyo.
1 Petro 5:1-3
[1]Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; [2]lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. [3]Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.
[1]Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;
[2]lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.
[3]Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.
> Pamoja na hayo anasisitiza watakatifu wote wawe na kiasi na kukesha, kwasababu adui yetu ibilisi ni mfano wa simba angurumaye akitafuta mtu ammeze, hivyo wana wajibu wa kumpinga sikuzote.(5:8-9)
Hitimisho:
Hivyo kwa maelezo machache ni kwamba Petro analihimiza kanisa kutembea katika uvumilivu wote na uthabiti Wa imani, pamoja na utakatifu, na kutimiza wajibu wao katika utakatifu na adabu kwa wanadamu wote, katika wakati ambao kanisa linasubiria neema kuu itakayofunuliwa siku ya mwisho Yesu atakaporudi.
Na ndivyo ambavyo sote tunapaswa tuishi hivyo sasa.
Kama mkristo je unaendelea kufurahi katika majaribu? Unaishi maisha matakatifu? Unaishi vema na jamii yako? unaifanya kazi ya Mungu? Unampinga shetani kwa kudumu katika sala?
Ikiwa hayo, unayazingatia basi, wewe ni mshirika wa neema hiyo kuu ya Mungu itakayofunuliwa siku ya mwisho.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mwandishi na uchambuzi wa kitabu cha Wakolosai
MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.
JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE
Je wewe ni miongoni mwa waliochaguliwa sawasawa na andiko hili?…
Waefeso 1:11 ”na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake”.
Kama wewe ni miongoni mwa waliochaguliwa basi fahamu lengo/kusudi la kwanza la wito wa MUNGU kwako ni lipi?..
Hebu tuusome wito wa Mtumishi wa Mungu Paulo, tuweze kujua nia ya Kristo ipi…
Matendo 22:13 “Akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu yangu Sauli, uone. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile. 14 Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate KUJUA MAPENZI YA MUNGU, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake”.
Matendo 22:13 “Akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu yangu Sauli, uone. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile.
14 Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate KUJUA MAPENZI YA MUNGU, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake”.
Hapo anasema “Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua MAPENZI YAKE..”...Jiulize kwanini ataje jambo la kwanza “mapenzi ya Mungu”.
Kumbe lengo la kwanza la Mungu kumwita Paulo ni yeye “kuyajua mapenzi ya Mungu”. Na mengine ndiyo yafuate..
Na ni sahihi kabisa kwani Bwana YESU mwenyewe alituambia maneno yafuatayo…
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye AFANYAYE MAPENZI YA BABA YANGU ALIYE MBINGUNI”. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye AFANYAYE MAPENZI YA BABA YANGU ALIYE MBINGUNI”.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Umeona?..kwahiyo kumbe Bwana anataka tuyajue sana mapenzi yake na tuyafanye..
Je unayajua mapenzi ya Mungu??…na je unayafanya pia?.
Mapenzi ya MUNGU ni haya…
1 Wathesalonike 4:3 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
1 Wathesalonike 4:3 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
1. Utakaso ni sehemu ya mapenzi ya MUNGU kwako.
(Na unatakasika kwa maombi, mifungo, kusoma Neno, na kuhudhuria ibada).
2. Pia Kuuweza mwili katika utakatifu na heshima ni sehemu ya mapenzi ya MUNGU kwako.
(Maana yake mwili wako kuuweka katika hali ya heshima, ikiwemo kuvaa mavazi ya heshima na staha, ikiwemo kutojichubua, na kutofanya uasherati na mambo yote yanayohusika kuuchafua mwili”.
Yajue mapenzi ya MUNGU, yafanye mapenzi ya MUNGU.
Kwa urefu zaidi kuhusu Mapenzi ya MUNGU fungua hapa》》MAPENZI YA MUNGU NI YAPI?
Sura hii inaeleza maono aliyoonyeshwa nabii Zekaria, kuhusu ujenzi wa hekalu la pili. Anaanza kwa kuonyeshwa na malaika kinara cha taa cha dhahabu, chenye taa saba juu yake. Ambacho pia kina mirija saba, inayotoka katika matawi ya mizeituni miwili inayohusika kuleta mafuta katika kinara hiyo.
Hivyo nabii Zekaria kuona maono hayo, alitamani kuelewa tafsiri yake ni nini. Tusome.
Zekaria 4:1 Na yule malaika aliyesema nami akanijia mara ya pili, akaniamsha, kama mtu aamshwavyo katika usingizi wake. 2 Akaniuliza, Unaona nini? Nikasema, Nimeona, na tazama, kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kinabakuli juu yake, na taa zake saba juu yake; tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwa taa zote zilizo juu yake; 3 na mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume walile bakuli, na mmoja upande wake wa kushoto. 4 Nami nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini? 5 Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. 6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala sikwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi. 7 Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe lakuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie. 8 Tena neno la Bwana likanijia, kusema, 9 Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu. 10 Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote. 11 Ndipo nikajibu, nikamwambia, Ni nini mizeituni hii miwili iliyo upande wa kuume wa kinara cha taa kile na upande wake wa kushoto? 12 Nami nikajibu mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao? 13 Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. 14 Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.
Zekaria 4:1 Na yule malaika aliyesema nami akanijia mara ya pili, akaniamsha, kama mtu aamshwavyo katika usingizi wake.
2 Akaniuliza, Unaona nini? Nikasema, Nimeona, na tazama, kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kinabakuli juu yake, na taa zake saba juu yake; tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwa taa zote zilizo juu yake;
3 na mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume walile bakuli, na mmoja upande wake wa kushoto. 4 Nami nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini?
5 Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu.
6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala sikwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.
7 Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe lakuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.
8 Tena neno la Bwana likanijia, kusema,
9 Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe
utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu.
10 Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote.
11 Ndipo nikajibu, nikamwambia, Ni nini mizeituni hii miwili iliyo upande wa kuume wa kinara cha taa kile na upande wake wa kushoto?
12 Nami nikajibu mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao?
13 Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu.
14 Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.
Tafsiri yake ni kuwa matawi yale mawili walimwakilisha Yoshua kuhani mkuu, na Zerubabeli liwawi wa Yuda. Hawa ndio wana wawili wa mafuta. Yoshua alisimama katika mambo yote yahusuyo dini na ibada na Zerubabeli katika mambo yote ya kiutawala,
Na ile mizeituni miwili iliwakilisha Neno la Mungu lililowajia wao, kuwaongoza na kuwatia nguvu. aidha kwa njia ya Torati au kwa Manabii. Maana yake ni kuwa Yoshua kama kuhani mkuu akiongozwa na Torati na Zerubabeli kama akida akiongozwa na manabii waliopokea ujumbe kutoka kwa Mungu ili walisimamie kusudi lake. Na manabii ambao walihusika hapa kuwatia nguvu walikuwa ni Hagai na Zekaria.
Katika ono hili Mungu alikuwa anamfunulia Zerubabeli uweza wake, kwamba si yeye atendaye hiyo kazi kubwa ambayo inaonekana kibinadamu haiwezekani, kutokana na hofu ya maadui zao, kupungukiwa fedha, na lile agizo lililotolewa na mfalme kuwa mji ule usiendelezwe. Bali ni Roho wa Mungu atendaye kazi yote, kwasababu si kwa uweza wao wala kwa nguvu.
Mungu akamuhakikishia Zerubabeli kuwa mikono yake ndiyo imetia msingi, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza nyumba ile yote. Akimwonyesha kimaono jinsi wao wanavyosimama tu kama matawi ndani ya mzeituni (Zerubabeli na Yoshua), ambayo yanapokea mafuta na kutoa kuelekea kwenye mirija. Lakini hayahusiki katika kutengeneza mafuta au kuwasha taa yoyote.
Na ndivyo ilivyokuwa kwao ujenzi huo ulienda ukakamilika bila taabu zao wenyewe walizozitarajia, bali Mungu alihakikisha anawapatia kibali, pamoja na vitendeakazi vyote(Mali) kiasi kwamba utukufu wa hekalu hilo la pili ukawa mkubwa sana kuliko ule wa kwanza, pamoja na udhaifu wao.
Vivyo hivyo hata sasa, ni lazima tufahamu kuwa jambo lolote kuu tunalotamani kumfanyia Mungu, aidha kujenga nyumba yake, kusapoti injili, kuhubiri injili sehemu za taabu na nguvu n.k. Tusifirie sana hali zetu, bali tumfikirie Roho Mtakatifu, kwasababu yeye mwenyewe aliahidi kuwa atatupa nguvu ya kuyatenda hayo yote, na kuyatimiliza.(Matendo 1:8), ili utukufu wote umrudie yeye.
Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu (Zekaria 13:7-9)
DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.
Mafuta mabichi ni mafuta ya aina gani? (Zaburi 92:10)
Jibu: Turejee…
1 Wakorintho 6:17 “Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye”.
Maana ya kuwa roho moja na Bwana ni kama maandiko yafuatayo yanavyoeleza..
Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema Njoo!…..”.
Hapa anasema Roho (yaani wa Roho wa Mungu) na bibi-arusi (yaani kanisa la Mungu)…Wasema Njoo!!…
Maana yake hawa wawili (Roho pamoja na bibi arusi) wote wanatoa Kauli moja!.. ya Njoo!..
Maana yake Bibi arusi akisema ni Roho wa Mungu kasema na Roho wa Mungu akisema ni Bibi arusi kasema…kwanini?…kwasababu wameungwa pamoja.
Ndio sababu Bwana YESU alisema, tukiwapokea waliotumwa na yeye, tumempokea yeye, na tukiwakataa waliotumwa na yeye, tumemkataa yeye kwasababu wameungwa na yeye.
Mathayo 10:40 “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma”.
Je umemwamini Bwana YESU?. Je unasubiri Bwana YESU mwenyewe akutokee ndio uamini?..
Kama ndicho unachosubiri basi upo hatarini, kwasababu YESU yupo anafanya kazi ndani ya watu wake, mtumishi wa MUNGU wa kweli kukujia na kukupa habari za uzima wa milele, tayari YESU ameshakutokea kwasababu maneno akuambiayo si yake bali ya Roho wa Mungu.
Na anapokuita uingie kwenye imani/wokovu si yeye bali ni Roho wa MUNGU ndani yake..
Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”
Shalom.
VIASHIRIA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU KUWEPO NDANI YAKO.
NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?
Pale mwanandoa mmoja anaposhindwa kutimiza wajibu wake ufanyaje?
NDOA TAKATIFU NI MKE MMOJA/MUME MMOJA.
Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”
Matendo 7:58 “wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi WAKAWEKA NGUO ZAO MIGUUNI PA KIJANA MMOJA ALIYEITWA SAULI. 59 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu”.
Matendo 7:58 “wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi WAKAWEKA NGUO ZAO MIGUUNI PA KIJANA MMOJA ALIYEITWA SAULI.
59 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu”.
Zipo tafiti zinasema kuwa zamani za biblia, akipatikana mtu na kosa la kustahili kuuawa kwa kupigwa mawe, basi wale mashahidi waliolishuhudia kosa la huyo mtu, kabla ya kutekeleza mauaji walivua nguo zao kama ishara ya kiapo walichokitoa/ushahidi kuwa ni kweli.
Lakini dhana hiyo haina marejeo yoyote ya biblia, hivyo si ya kusadikika.
Lakini sababu pekee yenye kuleta maana ya mavazi ya mashahidi kuwekwa miguuni mwa Sauli ni ili wawe wepesi katika kutekeleza zoezi hilo la mauaji.
Ni kawaida wana michezo au wapiganaji kupunguza mavazi yao kabla ya mchezo kuanza ili wawe wepesi, ndicho walichokifanya hawa mashahidi, walipunguza mavazi yao ya nje, na kumpatia kijana Sauli awahifadhie kwa muda na baadae wazichukue baada ya kumuua Stefano.
Na tunasoma Sauli (ambaye baadaye ndiye aliyekuja kuwa Paulo), alikubali kuwatunzia..
Matendo 22:20 “Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao waliomwua”.
Sasa ni kwanini Bwana MUNGU aruhusu mavazi ya wauaji yatunzwe na Sauli?.
Sababu kuu ni kwamba Bwana MUNGU alijua Sauli atakuja kugeuka baadaye na kuwa mtumishi wake kwa watu wa Mataifa.
Hivyo kitendo cha zile nguo kuwekwa miguuni mwa Sauli ni kuweka sababu baadae ya Wayahudi pamoja na wakristo waliopo Yerusalemu kumkataa, ili aende kwa watu wa mataifa…
Kwani watakapokumbuka lile tendo la kushiriki kwake kumuua Stefano, wamkatae na kumwona hafai..
Matendo22:17 “Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemu, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa hali ya kuzimia roho, 18 nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, KWA SABABU HAWATAKUBALI USHUHUDA WAKO katika habari zangu. 19 Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikiwafunga gerezani wale wanaokuamini na kuwapiga katika kila sinagogi. 20 Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao waliomwua. 21 Naye akaniambia, Enenda zako; KWA KUWA NITAKUTUMA UENDE MBALI KWA WATU WA MATAIFA”.
Matendo22:17 “Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemu, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa hali ya kuzimia roho,
18 nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, KWA SABABU HAWATAKUBALI USHUHUDA WAKO katika habari zangu.
19 Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikiwafunga gerezani wale wanaokuamini na kuwapiga katika kila sinagogi.
20 Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao waliomwua.
21 Naye akaniambia, Enenda zako; KWA KUWA NITAKUTUMA UENDE MBALI KWA WATU WA MATAIFA”.
Na utaona faida ya Paulo kuhubiri kwa watu wa Mataifa ndio mazao ya nyaraka zote za Paulo, ambazo mpaka leo zimekuwa msingi wa Neno la Mungu.
Tunachojifunza zaidi kuwa yapo makosa ambayo yalitokea zamani, na MUNGU aliyaruhusu yatokee kwasababu yamebeba kusudi kubwa mbeleni.
Makosa mengine yaliruhusiwa zamani ili yatuondolee viburi leo, mengine yaliruhusiwa ili tupate fursa njema leo, na mengine ni ushuhuda kwa wengine na maonyo kwa wengi e n.k
Hivyo kila jambo lina kusudi lake.
Maziara ni nini? Je! Na Tunaruhusiwa kuyajenga kwenye makaburi yetu?
Ni sahihi kusema sikuitiwa kuhubiri ubatizo kama Paulo alivyosema (1Wakorintho 1:17)?
Nini maana ya “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi”?
ANTIPA SHAHIDI WANGU, MWAMINIFU WANGU.
MWOMBENI BWANA WA MAVUNO APELEKE WATENDA KAZI.