Title Devis

Je! ni kweli Bwana alimaanisha hatutaonja mauti kabisa tukimwamini?(Yohana 11:25)

Naomba ufafanuzi wa huu mstari Yohana 11:25-26″  Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? “

hususani hapo anaposema (naye kila aishiye na kuniamini mimi hatakufa kabisa hata milele.) ana maana gani?


JIBU: Tunajua Yesu Kristo ndio ule mti wa uzima uliozungumziwa katika bustani ya Edeni kule mwanzo kwamba ukila matunda yake utaishi milele, na matunda yake leo hii tunayajua ni NENO lake, na neno lake ndio UZIMA wenyewe na siku zote palipo na uzima hapana kifo. 

Tukichunguza katika mstari huo tunaona Bwana Yesu alizungumza kwa watu wa aina mbili tofauti,

Aina ya kwanza: ni “yeye aniaminiye mimi ajapokufa atakuwa anaishi”. Hili ni kundi ambalo linajumuisha watu wote waliomwamini Bwana watakaokufa watakuwa wanaendelea kuishi katika paradiso wakingojea ufufuo wa mwisho lakini kundi hili halikufanikiwa kufikia utimilifu wa imani ya kumwamini Mwana wa Mungu, hivyo basi itawapasa wafe lakini kwa kuwa walimwamini Mungu kwa sehemu ya imani watakuwa wanaendelea kuishi huko paradiso. Na ni watu wengi leo hii wanakufa katika hali hii.

Aina ya pili : “naye kila aishiye na kuniamini mimi hatakufa kabisa hata milele”. Hili ni kundi lililofikia imani timilifu ya kumwamini na kumjua sana mwana wa Mungu inayozungumziwa katika kitabu cha…

 (waefeso 4:13”hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; )


hata kufikia hatua ya kushinda kifo na mauti. Mfano wa watu kama hawa tunawaona kama Henoko, Eliya, na kanisa ambalo litakuja kunyakuliwa siku ya mwisho. Hata leo hii inawezekana mtu kutokuonja mauti kabisa tukimwamini mwana wa Mungu (YESU KRISTO) katika utimilifu wote, tutachukuliwa juu hatutakufa kama  ilivyokuwa kwa Eliya na Henoko, maana biblia inasema Eliya alikuwa ni mtu mwenye tabia sawa na sisi lakini kwa bidiii na kwa imani akachukuliwa juu. Mahali pengine Bwana Yesu alisema katika…

 Yohana 8:51 “Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.

52 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

54 Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. ” mstari huu unaelezea jinsi Bwana alivyokuwa akijaribu kuwaeleza juu ya jambo hili lakini wayahudi hawakutaka kulipokea.

Sehemu nyingine Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake,

Mathayo 16:28″Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake. “

leo hii zipo shuhuda nyingi duniani za watu waliochukuliwa na Bwana pasipo kuonja mauti lakini shetani anataka kuwafanya watu waamini kuwa hilo jambo haliwezekani kwamba ni manabii tu wa zamani ndio walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo siku hizi hayo mambo hamna. usidanganyike katika kila kizazi Bwana ana watu wake wanaoshinda. Hivyo maneno haya yanatupa changamoto ya sisi kuongeza uhusiano wetu na Mungu kwasababu hata kanisa litakalokuja kunyakuliwa halitaonja mauti na ni lazima liwe na hiyo imani swali je! wewe unayo? kama hauna ndio wakati wa kuitafuta sasa maana Bwana Yesu mwenyewe alisema

Luka 18:8”……walakini atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?”

kwahiyo ni lazima aione imani kwanza ndipo aje hivyo tuitafute hii imani vinginevyo hatutakwenda kwenye unyakuo kumbuka ni Kristo anayetungojea sisi tuwe wakamilifu ndipo aje kutuchukua na sio sisi tunayemngojea yeye.

Mungu akubariki.


 

Mada Nyinginezo:

UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?

KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?

KUPAYUKA PAYUKA KUNAKOZUNGUMZIWA KWENYE BIBLIA NDIO KUPI?

MWANZI ULIOPONDEKA.

HADITHI ZA KIZEE.


Rudi Nyumbani:

Print this post

KUONGEZEKA KWA MAARIFA.

Habari ya uzima wako mtu wa Mungu, katika hizi siku za mwisho na za hatari kama bado upo nje ya wokovu jiulize sana, Na kama bado unaishi kwa kushikilia mapokeo ya kidini jifikirie mara mbili..Kwasababu biblia inatuambia dalili nyingine kubwa inayofungua ukarasa wa siku za mwisho ni Kuongezeka kwa maarifa.. Na maarifa ya kwanza biblia iliyomaanisha ni maarifa ya rohoni, lakini tunajua mambo ya mwilini sikuzote huwa yanafunua yale ya rohoni hivyo tunapoona maarifa yakiongezeka duniani kwa kasi basi tunajua kuwa ule wakati umeshawasili . Sehemu nyingine biblia inatuambia tujifunze katika ‘Maumbile, yaani vitu vya asili (NATURE)’ 1Wakorintho 11:14..

Ni wazi kuwa vitu tunavyoviona karibu vyote ulimwenguni kwa namna moja au nyingine vinatuhubiria injili pengine pasipo hata sisi kujua..Tunamwona Bwana Yesu alitumia mifano mingi ya asili kutufundisha sisi, kwamfano aliposema watafakarini ndege ni mfano wa maumbile ya asili, aliposema tena

“Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo.

55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.

56 Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya?”(Luka 12:54-56)

Unaona Yote hayo ni maumbile yakituhubiria injili..

Vivyo hivyo biblia pia inaposema Maarifa yataongezeka katika siku za mwisho, inamaanisha tunapaswa tujifunze katika hayo, kwasababu na rohoni ndivyo ilivyo.. tunasoma hilo katika

Danieli 12:4 “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, NA MAARIFA YATAONGEZEKA.”

Hakuna mtu asiyejua ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa ushindani, ili uweze kuishi au kufanikiwa ni lazima uwe na akili timamu vile vile uwe mshapu, na hiyo yote ni kwasababu teknolojia iliyopo sasa ndiyo inayotufanya tuwe watu wa namna hiyo..

Embu jaribu kutafakari, siku hizi unaweza kusoma tangazo kwenye gazeti, au internet, linasema linahitaji wafanyakazi Fulani watakaojaza nafasi za wafanyakazi Fulani walioachishwa kazi,..na linawahitaji ndani ya saa 5-7 wawe wameshafika eneo la shirika kwa ajili ya mahojiano na watakaokidhi vigezo wataanza kazi mara moja Eneo husika ni Daresalaam..

Ukijiangalia wewe upo Kigoma kwa wakati huo, na mwingine yupo Bukoba, na mwingine Afrika ya kusini…. Je! Kwa akili ya harakaharaka unadhani usafiri utakao tumika hapo ni upi ili kufika eneo la kazi?, Je! Ni miguu?, au Baiskeli au gari?..Ni wazi kuwa hapo itahitajika kifaa kinachokwenda kasi zaidi nacho si kingine zaidi ya ndege tu,..Ukitumia usafiri mwingine utachelewa tu..

Sasa ndivyo itakavyokuwa kwa habari ya unyakuo. Kipindi kifupi kabla ya Unyakuo, Bwana atawaita watu wake kwa sauti nyingine kuu..Na sauti hiyo inajulikana kama Sauti ya Malaika mkuu ukisoma (Ufuno 10:3) utaliona hilo, Hicho ndicho kipindi ambacho watu wote waliovuguvugu na walio moto wataisikia hiyo sauti kwa mahubiri ya kipekee yatakayokuwa yanafundishwa na watumishi wa Mungu waaminifu duniani kote..Na wito huu utakuwa ndani ya Muda mchache sana, Bwana Yesu alitumia mfano wa wale wanawali 10, kueleza tukio hilo litakavyokuwa ambapo tunasoma 5 walikuwa werevu na 5 wapumbavu, pindi wote waliposikia sauti ya Bwana harusi tokea mbali, wote walinyanyuka kuzitengeneza taa zao, lakini wale wapumbavu walipoona wameishiwa mafuta walijaribu kuwaomba wale werevu wawapunguzie walau hata kidogo, lakini wale werevu waliwaambia hayatutoshi sisi na nyie, ni heri mkanunue ya kwenu ndani ya hichi kipindi kifupi kabla Bwana harusi hajatokea..

Lakini kwa bahati mbaya walikuwa wameshachelewa waliporudi walikuta mlango umeshafungwa.

Sasa ndivyo itakavyokuwa ndani ya hicho kipindi kifupi, Sauti kuu italia karibia ulimwengu mzima, tunapozungumza inaweza ikawa siku yoyote kuanzia sasa, Na watu watafahamu kabisa kuwa Bwana siku yoyote anawanyakuwa watu wake, lakini kwa bahati mbaya wakati huo wapo watu ambao watakuwa tayari wapo nyuma ya teknolojia ya kimbinguni,..Wakati wenzao wanatumia kifaa cha ndege kumfikia Mungu wengine watakuwa bado wapo kwenye miguu wengine bado kwenye baiskeli, wengine kwenye gari…

Na hiyo itawachelewesha kufikia malengo yao katika hicho kipindi kifupi sana..Na siku ya kuitwa juu mbinguni itakapofika Mlango utakuwa umeshafungwa, hakutakuwa na udahili tena..Hapo ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno kama biblia inavyosema utakapoona mbona Fulani niliyemjua hayupo, mbona huyu nilikuwa ninakwenda naye kanisani hayupo, wewe ndiye utakayeumia zaidi kuliko Yule mlevi wa Bar..kwasababu mlevi wa Bar hataamini chochote.

Na ndio maana ni muhimu tuyajue hayo kwamba suala la kwenda mbinguni sio jambo la kuotea tu, bali ni jambo la kimkakati, na mkakati huo ulishaanza tangu zamani na bado hata sasa unaendelea. Leo hii unaambiwa tafuta Roho Mtakatifu maana huyo ndio muhuri wa Mungu na ndiye atakayekuongoza na kukufanya kuwa mkamilifu unasema dhehebu langu linanitosha..Unapohubiriwa juu ya mambo ya ufalme wa mbinguni, unasema sisi tupo duniani, hatuishi mbinguni, injili unazozipenda ni za kuambiwa njoo pokea, unapoambiwa tengeneza mambo yako sasa hizi ni nyakati za hatari, unasema mbona hakuna dalili yoyote ya mwisho wa dunia, lakini biblia inasema siku hiyo itakuja katika siku ambazo zinaonekana kuwa za amani ndipo uharibifu unapokuja kwa ghafla.(1Wathesalonike 5:3).

Hivyo kama ikitokea leo hii Injili hiyo ya ajabu inahubiriwa duniani kote, na bado upo vuguvugu, basi hesabu kuwa utaachwa siku ile, na utabaki tu hapa duniani kwa ajili ya dhiki kuu…Tubu leo, ili saa ile itakapokaribia uwe mfano wa wale wanawali werevu waliokuwa na mafuta ya ziada katika taa zao. Na maarifa ya kutosha kwa ajili ya kumlaki BWANA MAWINGUNI..

Ubarikiwe.

Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine. Na Bwana atakubariki.


Mada Nyinginezo:

DANIELI: MLANGO WA 12.

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA

SAUTI NYUMA YA ISHARA.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.

CHUKIZO LA UHARIBIFU.

MIHURI SABA.

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUZAA MATUNDA.

Shalom mtu wa Mungu, karibu tutafakari maandiko pamoja.
 
Biblia inasema katika Kitabu cha Yohana 15:16 kwamba “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni”
 
Tumepewa jukumu la kuzaa matunda, na matunda hayo yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, sehemu ya kwanza ni matunda ya Haki, ambayo hayo yanatokana na utakatifu, tunayasoma hayo katika
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
 
Na aina ya pili ya Matunda, ni matunda ya KAZI, ambayo hayo yanatokana na kuwaleta watu kwa Kristo,
 
Wafilipi 1:21 “Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
 
22 Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui.”
 
Hivyo Kristo ametuweka tuzae aina hizi mbili za matunda…Matunda ya HAKI na Matunda ya KAZI..Hivi viwili vinakwenda pamoja…Na vyote vinahitaji Mafuta ya Roho Mtakatifu ili viweze kufanyika. Ili tuwe watakatifu tunahitaji Mafuta ya Roho Mtakatifu…Kwasababu kama jina lake lenyewe lilivyo..Roho Mtakatifu, hivyo kila ampataye yeye ni lazima atakuwa mtakatifu tu.
 
Kadhalika ili tuweze kuleta matunda mengi kwa Kristo tunamhitaji Roho Mtakatifu, kwasababu yeye ndiye anayehusika katika kumshawishi mtu ndani ya moyo wake amgeukie Kristo.. 1 Wakorintho 2:4 “Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu”
Na leo tutajifunza umuhimu wa Roho Mtakatifu katika kuzaa matunda katika hizi siku za mwisho.
Kazi ya kuwavuta watu kwa Kristo imefananishwa na kazi ya uvuvi…Sharti ni kwamba ili mtu akavue samaki ni lazima atimize masharti makuu 5..
 
Sharti la kwanza ni lazima awe na mtumbwi unaoelea, sharti la pili ni lazima awe anajua kuogolea, sharti la tatu ni lazima awe na nyavu au ndoano, sharti la 4 Ni lazima aende usiku na sharti la 5 na la mwisho ni lazima awe na TAA..Akitimiza masharti hayo 5 basi ni lazima apate samaki..hawezi kukosa chochote aendapo anavua baharini…
 
Masharti hayo hayo pia yanatumika katika roho kwa uvuvi wa watu…
 
Sharti la kwanza: Kama vile mvuvi ni lazima awe na mtumbwi unaoelea na ni lazima akae juu ya huo mtumbwi ili aweze kuvua…vivyo hivyo katika Uvuvi wa watu ni lazima mtu awe juu ya Mtumbwi unaoitwa YESU KRISTO, na ni lazima mtu awe juu ya huo mtumbwi sio mbali au nje ya huo mtumbwi…huko nje ni kwa watu wasiomjua Mungu, ulimwengu unafananishwa na bahari ambayo imejaa watu wasiomjua Mungu ambao wanahitajika kuvuliwa..Hivyo haiwezekani mtu aliye nje ya Kristo kuwahubiria watu waje kwa Kristo kama vile ilivyo ngumu mvuvi kuwa nje ya mtumbwi na kuvua samaki.
 
Sharti la pili: Ni lazima mvuvi awe anajua kuogelea kabla hajaenda kuvua samaki…awe na uwezo endapo ikitokea ajali akaanguka ghafla majini awe na uwezo wa kurudi tena mtumbwini…sio endapo Kazama ndio anapotelea huko moja kwa moja…Kadhalika na mvuvi wa Roho za Watu ni lazima awe na uwezo wa kujihadhari na dunia, kwasababu dunia ni kama bahari, ukizama na ukiwa hujui namna ya kujitoa huko unazama moja kwa moja na kufia huko…Kwahiyo Ni kama tunaonywa kamwe tusidhubutu kwenda kuhubiri injili kama tunajua hatujaacha sisi wenyewe mambo ya ulimwengu huu, kama tunajua hatuwezi kuushinda na kujinusuru na ulimwengu…ni afadhali tusiende kuhubiri injili kabisa kuliko kwenda na kuzama huko… kwasababu endapo tukianguka tunakuwa tumeanguka moja kwa moja hakuna kurudi tena..
 
2 Petro 2:20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
 
21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa”
 
Sharti la Tatu: Ni lazima mvuvi awe na ndoano au nyavu…Ndoano au nyavu zinawakilisha Neno la Mungu, pamoja na ishara na miujiza…Vitu hivi biblia inasema waaminio wote vitaambatana nao…Ni lazima tulifahamu Neno ndipo tuende kuwahubiria wengine…
 
Sharti la Nne: Ni lazima mvuvi aende usiku kuvua, wavuvi wote wanaomaanisha kupata samaki huwa hawaendi mchana kwani wanajua hawatapata kitu, ni lazima aende usiku, kadhalika hata wakati huu wa sasa tunapaswa tuende ulimwenguni kote kulikojaa giza…Matendo ya dhambi yote ni matendo ya giza, na dunia yote imejaa giza kutokana na dhambi za wanadamu…lakini leo Utashangaa mtu anapambania awe mhubiri kanisani kila siku, lakini hataki kwenda mitaani mahali ambapo makahaba wapo, mahali penye giza…tukihubiri kanisani mahali ambapo kuna mwanga ni sawa tunaingia na mshumaa ndani ya nyumba ambayo tayari ina bulb inayowaka sana..Hivyo ni lazima tuenda na mitumbwi yetu, na nyavu zetu sehemu zenye giza mbali sana huko kuvua roho za watu. Na sisi wenyewe tukijihadhari tusipotelee huko.
 
Na Sharti la Tano Na la mwisho: Ni lazima mvuvi aende na TAA..Nyavu peke yake haitoshi kuwaleta samaki, ndoano peke yake haitoshi inahitajika taa…Wataalamu wa masuala ya uvuvi wanasema wakati wa usiku samaki wanapenda kufuata mahali penye mwangaza, hivyo wavuvi wengi hutwaa taa zao juu na kwenda nazo vilindini na hivyo samaki wanapoiona ile Nuru wanaisogelea na hivyo kunaswa…Na sisi tunahitaji Taa yenye Mafuta ili kuwavuta samaki wengi kwenye nyavu zetu, NA Mafuta yanawakilisha Roho Mtakatifu. Hivyo tunahitaji Roho Mtakatifu sana ili Taa zetu ziwe zinawaka sana, katika dunia hii ya giza ili waovu waonapo wamgeukie Bwana.
 
Wafilipi 2:15 “….mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao MNAONEKANA KUWA KAMA MIANGA KATIKA ULIMWENGU”
 
Ukiwa na Mtumbwi, ukiwa na ndoano, ukiwa na nyavu, na ukiwa na ujuzi wote wa kuogelea, kama huna TAA ni kazi bure…utakuwa umwekwenda baharini kubarizi tu na si kuvua..Kadhalika hata tukiwa na tumempa Bwana Maisha yetu, hata tukiwa tunalijua Neno vizuri na kujiepusha na dunia vizuri kama hatuna Roho Mtakatifu, kamwe shughuli ya kuwaleta wengine kwa Kristo itakuwa ngumu sana kwetu.
Hivyo leo tunajifunza tumtafute sana Roho Mtakatifu ajae ndani yetu, kwa maana pasipo yeye hakuna mtu yeyote atakaye vutwa kwa Mungu.
 
Yohana 6: 44 “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho”.
Bwana akubariki sana. Wahubirie na wengine habari njema, waujue wokovu wa Bwana Yesu.
 
Bwana akubariki.



Mada nyinginezo:

TUTAWEZAJE KUMZALIA MUNGU MATUNDA?

TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.

UMUHIMU WA KUISHI MAISHA YAMPENDEZAYO MUNGU SASA.

MUNGU MWENYE HAKI.

MLINZI, NI HABARI GANI ZA USIKU?

LILE TUMAINI LILILO NDANI YETU LINAPOULIZIWA.

NGUVU YA UPOTEVU.


Rudi Nyumbani:

Print this post

MAFUMBO YA MUNGU.

Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tuyatakari maandiko pamoja, lakini kabla hatujaendelea mbele zaidi naomba ulitafakari fumbo hili fupi kwa muda kidogo, ukipata au ukikosa jibu endelea kusoma habari hii, nitakupa majibu mbeleni… Fumbo lenyewe ni hili “Daudi ananyoa hata mara mia kwa wiki lakini kidevu chake bado kina ndevu nyingi, Je! Unaweza kunielezea ni kwanini? ”….Tafakari kisha utanipa jibu baadaye.

Lengo la kusema hivi ni kuwa kitabu kinachoitwa biblia ni kitabu kilichobeba mafumbo mengi sana, ambayo wakati mwingine majibu yake yanaweza yakawa ni marahisi kama tu tukimruhusu yeye aliyeyatunga kutufunulia, lakini pale tunapokosa kupata majibu sahihi, hatutaki kukiri kuwa hatufahamu, matokeo yake tunaishia kuona labda biblia ilikosewa au pengine tunaishia kutoa tafsiri zisizo sahihi ili tu tuonekane tunafahamu kile kilichoandikwa, hakuna asiyejua biblia imejaa mafumbo mengi sana, lakini miongoni mwa hayo ni suala la uungu wa kiMungu, kama vile biblia inavyosema Mungu ni MMOJA tu, lakini inakuwaje Yesu naye anaonekana kuwa ni Mungu, Roho Mtakatifu naye ni Mungu kama Mungu ni mmoja…

Sasa tunapokosa majibu ya maswali kama haya huwa tunaishi kusema Mungu ni mmoja ila kagawanyika katika nafsi tatu zinazojitegemea..Majibu tunayoyatoa ni marahisi sana, lakini hatujui kuwa tunazua maswali mengi, hata kwa wale ambao hawamjui Mungu wa wakristo, ndio linawafanya waende mbali zaidi ya ukristo wanapopata majibu kama hayo ambayo hayaoenekani kwenye biblia..Lakini hiyo yote ni kwasababu tumeukwepa uongozo wa Roho Mtakatifu kutufundisha ni jinsi gani Kristo ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu Yule Yule asiyekuwa na mshirika mwingine pembeni.

Kipengele kingine ambacho nacho kimezua utata mwingi, tunakipata katika mstari huu:

Mathayo 16:13 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?

14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.

15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?

16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.

17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”.

Mstari huu, unatafsiriwa na wengi hususani kanisa Katoliki kuwa mwamba huo unaozungumziwa kuwa Bwana Yesu atalijengea kanisa lake ni Petro, hivyo inaamika tangu zamani kuwa sisi sote tumejengwa juu ya Petro, na yeye ndiye PAPA wa kwanza, na kanisa la Kwanza ndio kanisa Katoliki.. Lakini kiuhalisia hapo Kristo hamzungumzii Petro bali anazungumzia juu ya UFUNUO ambao Petro alifunuliwa na Baba yake wa mbinguni wa kumjua YESU KRISTO ni nani, ambao wengi sana walishindwa kuuju, huo ndio mwamba ambao kanisa linajengwa juu yake?….Kwamba kwa ufunuo huo ndio atakalolijengea kanisa lake na malango ya kuzimu hayatalishinda…

Hivyo pale alikuwa hazungumziwi Petro na Petro hakuwa Papa, yeye alioa ma-papa huwa hawaowi, Yeye hakusujudia sanamu mahali popote wala kumwomba Mariamu dua mahali popote, lakini Mapapa wanafanya hivyo….vile vile Petro alimkana Bwana, lakini kanisa haliwezi kumkana Bwana, vilevile injili kwetu kwa mataifa ililetwa na mtume Paulo kuliko hata Mtume Petro , hivyo ambaye angestahili zaidi kuwa mjenzi wa kanisa basi angekuwa ni Paulo na sio Petro…Hivyo tunapaswa tumwombe Roho Mtakatifu atusaidie sana katika kuyachambua maandiko..

1Wakorintho 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata MAFUMBO YA MUNGU.

11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.”

Kadhalika leo hii tukikosa shabaha ya ufunuo wa Roho kumhusu Yesu Kristo katika katika maisha yetu, hatutaweza kusimama wala kumshinda shetani, Tunapomwona Yesu Kristo kwa kiganja chake, mtoa rizki tu, wa kubariki tu, wa kutusaidia kutatua matatizo yetu ya kimwili tu!…Na hatumfahamu kama mwana wa Mungu aliyetumwa kutuokoa, na kututakasa na dhambi zetu, kisha atupe uzima wa milele.. hatutakaa kamwe tumshinde shetani. Tutakuwa matajiri wa mali, lakini maskini wa roho.

Sasa tukirudi kwenye fumbo letu juu, linalouliza “Daudi ananyoa hata mara mia kwa wiki lakini kidevu chake bado kina ndevu nyingi, Je! Unaweza kuelezea ni kwanini”?..Jibu ni kuwa Daudi ni KINYOZI, huwa ananyoa vichwa vya watu wengi kila siku, hivyo basi hilo halihusiani na kidevu chake…je! ulifikiri hivyo? Au ulifikiri kwamba Kidevu cha Daudi ndicho kinachonyolewa mara mia kwa wiki?..Kama ulifikiri kuwa ni kidevu cha Daudi ndicho kinachonyolewa mara mia kwa wiki, na ukatafuta na ukajitafutia sababu za nywele hizo kuota kwa kasi kiasi hicho basi fahamu kuwa ulikosea… Na biblia sehemu nyingi ndio ipo kwa mafumbo kama hayo hayo…Unasoma hivi, na kufikiri hicho unachokisoma ndio tafsiri yenyewe kumbe, umekosea pakubwa, tafsiri yake ni nyingine tofauti na hiyo uliyokuwa unaifikiria wewe, na Yesu Kristo kumwelewa haihitaji kumhakiki kwa andiko peke yake bali kwa Roho Mtakatifu, kwasababu maandiko pasipo Roho yanapotosha.

2 Wakorintho 3: 6 “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, BALI WA ROHO; KWA MAANA ANDIKO HUUA, BALI ROHO HUHUISHA”.

Bwana atusaidie sote tuweze kumwelewa yeye kwa utimilifu wote, kama anavyotaka yeye sisi tumwelewe.

Ubarikiwe na Bwana.

Kama hujampa Kristo Maisha yako, mlango upo wazi sasa, lakini hautakuwa wazi hivyo si siku zote, parapanda ya mwisho inakaribia kulia, na Kristo kuchukua watu wake waliokombolewa kwa damu yake, je! Una uhakika umo miongoni mwao?..una uhakika wa kwenda na Bwana atakapokuja?..Uamuzi ni wako.

Maran atha! Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

ANGALIA JINSI USIKIAVYO:

FIMBO YA HARUNI!

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?


Rudi Nyumbani

Print this post

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

Shalom! Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze maandiko, Katika kitabu cha Warumi Mlango wa 7, tunaona biblia imetaja kuwepo kwa vitu viwili, ambapo cha kwanza ni SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI, na cha pili ni SHERIA YA ROHO WA UZIMA Hizi ni sheria kuu mbili zinazofanya kazi ndani ya mtu. Leo tutazitazama hizi sheria ni zipi, na ni jinsi gani zinafanya kazi. Naomba usome taratibu, ukisoma haraka hutaelewa chochote!

Sasa kabla ya kuingia kuzitazama hizi sheria mbili hebu kwanza tujifunze nini maana ya sheria?..

Sheria ni mfumo au utaratibu uliowekwa na jamii Fulani au mtu Fulani ufuatwe bila shuruti, kwamfano jua kuchomoza mashariki na kuzama magharibi hiyo ni sheria iliyowekewa jua, ni lazima litii hiyo sheria pasipo shuruti, kadhalika maji ya mvua kutoka juu kuja chini hiyo ni sheria iliyowekewa, ni lazima yatii, haiwezekani siku moja mvua ikanyesha kutoka chini kwenda juu…kadhalika giza kukimbia mwanga hiyo ni sheria iliyowekewa giza, haiwezekani hata siku moja giza likazidi mwanga kwa nguvu….n.k, Sasa katika maandiko pia zipo sheria hizi mbili zinazotenda kazi katikati ya wanadamu..

1)SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI.

Hii ni sheria ya kwanza inayotenda kazi ndani ya mtu. Sheria hii kama jina lake lilivyo ni sheria ya dhambi na Mauti, yaani maana yake ni kwamba sheria hii inamlazimisha mtu kutenda dhambi hata kama hataki…kama vile jua linavyotii sheria ya kulimulikia jua, hiyo litatii hata kama lingekuwa na uwezo wa kukataa lisingeweza kubatilisha hiyo sheria..Na kadhalika sheria hii ya dhambi ilianza kufanya kazi baada ya anguko pale Edeni.

Adamu na Hawa walipokula tunda sheria hii iliingia kwao na kwa Watoto wao, kwamba ni lazima utende dhambi tu hata kama hutaki, na sheria hii inatenda kazi katika viungo vya mwili….

Ndio maana utaona mtoto mdogo anapozaliwa tayari kitendo cha kuzaliwa tu, hapo hapo anaanza kutenda dhambi, utaona siku kadhaa au miezi kadhaa, anaanza kuwa na hasira zisizokuwa na sababu, kabla hajaelewa jema na anaanza kuwa na kiburi ukimwita anakataa, ukimwambia afanye kitu saa nyingine hafanyi au anasusa vitu na kuwa na chuki na vitu visivyokuwa hata na sababu…. au utaona anaanza kuwa mkatili, anaweza kuona mjusi pale akamrushia hata jiwe na kumwua kikatili, Watoto wengine utaona wana miaka 5 lakini wameshaanza kutamani uasherati.n.k…Hiyo yote hafanyi kwa kupenda! Hapana! Ni sheria ambayo tayari kashazaliwa nayo ambayo inafanya kazi katika mwili wake…Inamlazimisha yeye kufanya dhambi hata kama hapendi au hajui. Hata kama mtu moyoni mwake hapendi hicho anachokifanya atajikuta tu anarudi kukifanya tena na tena…

Mtume Paulo aliitaja sheria hii na kusema katika

Warumi 7:20

“Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

21 Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.

22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,

23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.

24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?”

Na sheria hii mtu anazaliwa nayo na anaendelea nayo mpaka siku ile atakapozaliwa mara ya pili..na kupokea sheria mpya ya pili ambayo tutakuja kuiona mbeleni kidogo. Na kama mtu hatazaliwa mara ya pili basi sheria hii ya dhambi na mauti ataendelea nayo mpaka siku anakufa..Hakuna namna yoyote mtu wa kawaida anaweza kushindana na dhambi!! Hakuna!, Mtu yeyote hawezi kuishinda dhambi kwa nguvu zake, ni lazima atakuwa chini ya utumwa wa sheria ya dhambi…

Na kumbuka sheria hii haiitwi tu sheria ya dhambi peke yake hapana bali inaitwa sheria ya dhambi na mauti! Ikiwa na maana kuwa, ni sheria inayozaa mauti! Ya kimwili na kiroho…Kama Biblia isemavyo “Mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23)”..Na tena “roho itendayo dhambi itakufa (Ezekieli 18:4)”

Sasa mtu anayefanya punyeto, anayefanya uasherati unaojirudia rudia, anayetazama mara kwa mara picha za ngono, anayerudia rudia kutukana, anayerudia rudia kusengenya na kuchukia watu, na anayerudia rudia kuwekea watu vinyongo, na hapendi kufanya hivyo lakini anajikuta anafanya, mtu huyo yupo chini ya HII SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI! na ANAKUWA NI MTUMWA WA DHAMBI..Na mshahara wake ni MAUTI na ZIWA LA MOTO!!..

Lakini ipo sheria ya pili ambayo ilitengenezwa na Mungu mwenyewe kuimaliza nguvu hii sheria ya dhambi na Mauti, na hiyo si nyingine Zaidi ya SHERIA YA ROHO.

2) SHERIA YA ROHO

Sheria hii ilikuja Baada ya Bwana Mungu, kuona hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kushindana na dhambi wala kuishinda dhambi kwa nguvu zake..Kwa kupitia Roho wake Mtakatifu aliileta sheria hii mpya, ambayo ilimpasa Kristo aje kufa msalabani, na kutuachia sisi kipawa cha Roho wake Mtakatifu, Roho huyu Mtakatifu kazi yake ni kuleta sheria ambayo itatufanya sisi KUTIMIZA Sheria za Mungu na amri zake pasipo kusukumwa sukumwa wala pasipo kutumia nguvu nyingi…Yaana mtu tu unajikuta unaichukia dhambi na kuipenda haki!….wakati sheria ya dhambi na mauti ni kinyume chake, yenyewe inakufanya uchukie haki na kupenda dhambi hata kama ndani ya moyo wako huipendi ile dhambi. Lakini sheria hii ya Roho inafanya kazi kinyume chake..

Inamfanya mtu kujikuta tu! Anampendeza Mungu hata kama hajahubiriwa! Inamfanya mtu anajikuta anauchukia uasherati hata kama hajahubiriwa, inamafanya mtu anajikuta anamwogopa na kumheshimu Mungu pengine Zaidi hata ya mchungaji wake..Ndio hapo unamkuta binti anavaa tu nguo za kujisitiri hata kama hajaonyeshwa andiko lolote kwenye biblia. Kwanini? Kwasababu sheria ya mpya ya Roho inafanya kazi ndani yake…na hiyo ndio maana ya kuishi kwa Roho, kuishi kwa Roho sio kuishi kwa kuona maono! Au kwa kunena kwa lugha! Au kwa kutabiri hapana bali ni kuishi katika sheria mpya ya Roho wa uzima haleluya!!

Waefeso 5: 16 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sharia”.

Sasa jambo pekee la kufahamu lisilojulikana na wengi ni kwamba Mtu aipokeaye sheria hii mpya ya Roho wa Uzima ndani ya moyo wake, haimaanishi kwamba ile ya kwanza ya dhambi imeondolewa!! Hapana sheria ile ya dhambi na mauti bado ipo!, isipokuwa imefunikwa na sheria hii mpya! Ikiwa na maana kuwa endapo mtu huyu aliyeipokea sheria hii mpya ya Roho akizembea na kumhuzunisha Roho Mtakatifu hata kuondoka basi huyu mtu anairudia ile sheria ya kwanza ya dhambi na mauti ambayo bado ipo ndani yake! Ndio maana inahitajika umuhimu mkubwa sana wa kushika kile tulichozawadiwa.

Ndio maana utaona mtu alikuwa moto! Hata uasherati alikuwa hafanyi lakini kapoa na kuanza kuwa baridi na kurudia matapishi ya kwanza! Kuna hatari kubwa sana juu ya huyu mtu!!

Kwahiyo sheria hii mpya ya Roho kazi yake sio kuondoa sheria ile ya zamani ya dhambi bali kazi yake ni kuifunika!

Sasa swali linakuja nitaipataje sheria hii mpya ya Roho ndani ya Moyo wangu itakayonisaidia kushinda sheria hii ya dhambi?

Mtume Paulo aliendelea kusema katika…

Warumi 7:24 “Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.…..

Warumi 8 :1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;

4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho”

Umeona hapo? Dawa ya dhambi ni Kristo Yesu, kwanza kumwamini yeye, pili kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi! Wengi hawapokei msamaha wa dhambi kwasababu wanatubu tu kwa midomo na si toba halisi itokayo mioyoni mwao inayoambatana na kuacha vile walivyokuwa wanavifanya…Na cha tatu baada ya Toba, ni ubatizo sahihi, na cha mwisho ni kupokea Roho Mtakatifu…

Na baada ya kupokea Roho Mtakatifu ni kuishi kwa kutomzimisha Roho Mtakatifu(Waefeso 4:30)..hapo dhambi haitakuwa na nguvu juu yako! Hutahitaji mhubiri akuhubirie kuwa ulevi ni dhambi, hutahitaji askofu akuambie kuwa kuishi na mwanamke/mwanamume ambaye hamjaoana ni dhambi! Hutahitaji mtu akuhakikishie katika maandiko kwamba uvaaji mbaya ni dhambi na upakaji uso rangi, hamu ya kuwa mtakatifu na ya kujiepusha na uovu itakuwa inamiminika tu ndani yako…Msukumo wa kutamani uasherati wala wa kufanya punyeto na kutukana hutauona tena. Hilo Ndio agano jipya lililoletwa na Bwana wetu Yesu Kristo kwamba sheria za Mungu tuzimize ndani yetu pasipo kusukumwa sukumwa wala pasipo kuwa watumwa wa sheria..

Yeremia 31:31 “ Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”

Bwana akubariki.


Mada zinazoendana:

JE! “MAJIRA NA SHERIA” MPINGA-KRISTO ATAKAYOKUJA KUBALISHA NI KUPINDUA SIKU YA SABATO NA KUWA JUMAPILI?

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

BIBLIA ITUAMBIA TUSALIMIANE KWA BUSU TAKATIFU. HILI BUSU NDIO LIPI?


 

Rudi Nyumbani:

 

Print this post

DALILI NYINGINE INAYOUTAMBULISHA UZAO WA NYOKA

Shalom mtu wa Mungu, karibu tena tuyatafakari maandiko, leo tutaona dalili nyingine kubwa inayoutambulisha UZAO WA NYOKA..kama biblia inavyosema ulimwenguni kuna watu ambao wanafanya dhambi kwa makusudi huku wakijua kabisa watu wanaofanya hivyo wanastahili hukumu ya mauti lakini wao wanaendelea kufanya hivyo kwasababu ile hali ya kujali au kuchukua tahadhari haipo ndani yao(ukisoma Warumi 1:32 utaona jambo hilo), hao watu sio wachache ni wengi sana..Embu tuitazame hii habari fupi itatukumbusha kitu  kingine cha msingi.

Mathayo 28:1 “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.

2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.

3 Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji.

4 Na kwa kumwogopa, wale walinzi WAKATETEMEKA, WAKAWA KAMA WAFU.

5 Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa”………

11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka.

12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi,

13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. 14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.

15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.”

Sasa kama tukiwatazama hawa askari ambao walikuwa wanalilinda kaburi la Bwana Yesu, pindi tu walipomwona Yule malaika kashuka pale, walitetemeka kwa hofu kubwa wakawa kama wafu, Na unajua mfu tabia yake ikoje?, Mfu huwa hawezi kufanya lolote anakuwa ameganda tu hapo chini, ndivyo ilivyowatokea hawa, ile hofu iliwafanya washindwe hata kukimbia au kufanya kitendo kingine chochote isipokuwa kungojea tu lolote litakalotokea, ni wazi maono yale ya wazi yaliwaingia sana moyoni, walitamani ingekuwa ni ndoto lakini haikuwa hivyo lilikuwa ni jambo la wazi kabisa mbele ya macho yao..

Waliona walichokiona, walisikia walichokisia, kulikuwa hakuna namna yoyote ungewashawishi kuwa Bwana Yesu hajafufuka kwa tukio lile, lakini kwa kuwa walipenda pesa kama Yuda, wakajiamulia tu kuudanganya uma kwamba hakuna kitu kama hicho, japo  ukweli wote ulikuwa ndani yao..Hiyo ni mbaya sana. Ndugu Uzao wa Nyoka sikuzote huwa na tabii hii, hata kama ukizungumza na Mungu uso kwa uso, hata kama ukaona uweza wake wote na ukuu wake wote ni rahisi kuchukuliwa na jambo dogo sana, na hata kukana alichokiona dakika chache tu hapo nyuma.

Walichokiona askari hawa hakina tofauti na alichokiona Sauli wakati anaelekea Dameski kuwaua watakatifu, tofauti yao ni kwamba Sauli alitubu na kugeuka kwa mono yale, kuonesha kuwa yeye ni uzao wa Mungu, lakini hawa wengine walikwenda kusambaza uzushi pamoja na kwamba wameona maono makubwa kama yale… kuonesha kuwa wao sio uzao wa Mungu, ni uzao mwingine wa nyoka.

Wapo watu wengi leo Mungu kajidhihirisha kwao kwa namna nyingi sana, wengine Mungu kasema nao kwenye ndoto wazi wazi, wengine wametokewa na malaika, wengine wameonyeshwa maono mengi,wengine wameuona mkono wa Mungu waziwazi katika mambo yao, wengine wameepushwa na hatari nyingi na kusema kabisa hakika huyu ni Mungu wala hakuna pingamizi, wengine hata walimwomba Mungu awafanikishe katika vitu vyao akawafanikisha sawasawa na walivyomwomba kwa wakati waliomwomba, wakatetemeka na kusema kweli Mungu yupo… wakaogopa kweli kweli wakalia, wakazimia, wakawa kama wafu wakasema Mungu wangu kuanzia leo nitakutumikia, wengine wakasema ukinipa nafasi ya pili basi mimi nitakutumikia milele, mimi sitatenda dhambi tena kuanzia leo, lakini cha kushangaza akitoka hapo siku chache baadaye, au miezi michache mbeleni, pengine kakutana tu na vitu vidogo vidogo visivyokuwa na maana vya ulimwengu huu vinavyopita, utamwona karudi nyuma kwa kasi kubwa kana kwamba  hajawahi kukutana na Mungu hapo nyuma hata siku moja…

Tena anaweza akawa ndio wa kwanza kuzungumza maneno ya mzaha kuhusu kazi ya Mungu au watumishi wake, lakini ndani ya moyo wake anajua kabisa Mungu alishawahi kumtembelea na kumwambia atubu. Watu kama hao wapo wengi sana inawezekana mmojawapo ni wewe unayesoma habari hii… Fanya utafiti uangalie utaona wale ambao hawajawahi kuuona uweza wa Mungu mwingi wale ambao Mungu anajihirisha kwao mara chache sana hao ndio wanaodumu na wanaomtumikia Mungu kwa moyo thabiti kuliko hawa wengine….na ndio maana Bwana Yesu alimwambia Tomaso heri wale ambao wameamini bila kuona..kwasababu alijua ugumu wa hawa wengine..

Ndugu unaendelea bado kumtumikia shetani na umesahau Mungu aliyokutendea hapo nyuma..Usidhani yataendelea kujirudia rudia hivyo kila siku, wakati utafika Roho wa Mungu ataondoka moja kwa moja ndani yako, utakachokuwa unangojea ni adhabu kubwa kuliko hata ile ya watu wa Sodoma na Gomora, Bwana Yesu ndio alisema  hivyo kama wale wangeona Ishara na maajabu Mungu anayowatendea watu leo hii, miji ile ingekuwepo hadi leo, hivyo basi akasema itakuwa rahisi kwa watu wale kustahimili adhabu kuliko sisi tuliyoyaona na kuyakataa.

Ndugu salimisha maisha yako kwa Bwana kithabiti..Anapokuita sio kana kwamba anataka kukunyima haki yako ya kuchagua unayoyataka hapana, lakini anakupenda UPEO hataki upotee hata unywele wako, hataki uende kuzimu hilo tu!…Tubu sasa ukabatizwe katika ubatizo sahihi, uanze kuuishia wokovu katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho duniani. Usikubali uwe sehemu ya UZAO wa nyoka ambao hata uhubiriweje injili na kuona maajabu yote hauwezi kugeuka..Naamini wewe sio mmojawapo na kwamba utapoisikia leo hii utageuka na kumwishia Kristo.

Ubarikiwe sana. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki.


Mada zinazoendana:

UZAO WA NYOKA.

WATU WASIOJIZUIA.

UZAO WAKO UTAMILIKI MALANGO YA KUZIMU

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.

Shalom, Mtu wa Mungu, karibu tulitafakari kwa pamoja Neno la Mungu, biblia inasema Neno la Mungu ni Taa iongozayo miguu yetu na mwanga wa njia zetu (Zab.119:105), hivyo ni vyema tukalitafakari hilo kila kukicha ili njia yetu iwe safi na salama..(Zab.119:9 “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako”).

Kama tunavyojua wengi wetu kwamba tunaishi katika siku za mwisho, na sio siku za mwisho tu! Bali ukingoni mwa siku za mwisho…Kwasababu siku za mwisho zilianza tangu zamani, sasa tupo ukingoni mwa hizo siku..Na kama tunavyojua ishara kubwa ya kututambulisha kuwa tupo ukingoni ni KUNYANYUKA KWA TAIFA LA ISRAELI. Ukienda kila mahali utasikia Israeli, Israeli..dunia ina mataifa mengi lakini ki-nchi kidogo kama kile kinavumisha upepo wa dunia na kuwa mada ya kuzungumziwa katika siasa yote ya dunia? Kuna nini pale?…Ni wazi kuwa kuna jambo la kiroho linaendelea kwenye Taifa hilo…Ndugu yangu hebu kama hujafuatilia ni nini kinaendelea kwenye Taifa hilo hebu tenga angalau wiki moja usiingie hata kwenye mitandao kuchat, tenga muda ulifuatilie kwa makini, soma historia ya Taifa hilo kwenye Biblia na kwenye historia…Ndio utajua tunaishi kipindi gani.

Wengi wetu tumezaliwa kipindi ambacho tunaambiwa kuna Taifa la Israeli, lakini wengi wetu hatujui kuwa Waisraeli wenyewe halisi, hawakukaa kwenye taifa lao, na kuwa na Mfalme wao wenyewe kwa takribani miaka 2,500 mpaka ilipofikia juzi tu mwaka 1948 ndipo wakarudi kuwa Taifa huru na kuwa na Raisi wao wenyewe…Kabla ya hapo walikuwa wametawanyishwa kwenye mataifa yote.

Sasa kama tunavyojua Kuwa Hawa Waisraeli tunaowaona, hawakua hivi, kwenye karne kadhaa huko nyuma… walikuwa wametawanyishwa katika Mataifa yote duniani, maandiko yanasema hivyo….Sasa kwanini Mungu aliwatawanyisha kwenye mataifa yote?..Jibu ni ili sisi watu wa mataifa tupate Neema, kwani Baada ya wayahudi (yaani waisraeli) kumkataa Masia wao Yesu Kristo, Bwana aliwaambia maneno haya…

Luka 21:20 “Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.

21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.

22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.

23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.

24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara NA KUCHUKULIWA KATIKA MATAIFA YOTE; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia”

Sasa Swali lingine linakuja…Wayahudi/Waisraeli kutawanywa kwenye mataifa yote ina uhusiano gani na sisi watu wa mataifa kupata Neema?…Yaani wengine waumie ili sisi tupate Neema?..Wengine wachukuliwe mateka ndipo sisi tupate Neema?..Kwani Mungu hawezi kuwaacha tu wawe salama, na kutupa Neema wote sisi na wao?.

Ni swali zuri lakini ni vizuri pia kujua kuwa ili kimoja kipate uzima ni lazima kingine kife! Kwamfano ili ule tunda na kupata virutubisho vilivyomo ndani yake ni lazima ulichume kutoka kwenye mti, ulitafune na kulisagasaga…hapo ni sawa na umeliua…ili ule nyama ikusaidie kwa protini ni lazima mnyama Fulani auawe, huwezi kula kitu kizima…kadhalika ili upate kitu Fulani ni lazima hicho kitu kiwe kimepunguka kutoka sehemu Fulani, hata fedha mtu anazozotafuta ni kwamba zimepunguka sehemu Fulani zikaenda kwa huyo mtu, ikiwa na maana kuwa endapo ukifanikiwa kuzikusanya zote basi kwingine kutakuwa kumepunguka pia pakubwa, kwahiyo hakuna kuongezekewa kama hakuna kupunguka sehemu Fulani nyingine…wala hakuna kupata heshima Fulani kama mwingine hajapata dharau, hata cheo, au nafasi,ni lazima mmoja aondoke mwingine aingie…. Mambo ndivyo yanavyokwenda hivyo…Kwahiyo ili sisi watu wa Mataifa tupate heshima mbele za Mungu ni lazima wawepo wengine walioharibu mahali Fulani.

Kwahiyo Waisraeli walipomkataa Yesu na injili yake, wakawa wamejiharibia wenyewe hivyo hiyo ikawa faida kwetu sisi watu wa mataifa ndio maana Mtume Paulo aliwaambia..

Matendo 13:44 “Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.

45 Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.

46 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.

47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

49 Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote”.

Kwa dhambi hiyo walioifanya Mungu hakuishia tu kuwapokonya injili bali pia aliwatawanya kwenye mataifa yote, na hiyo pia ikawa ni faida ya PILI kwetu.

Kumbuka popote wayahudi wanapopelekwa, mahali pale lazima pabarikiwe hata kama wamepelekwa kwa makosa yao…mfano utaona Yusufu alipoingia Misri pamoja na wana wa Israeli wote, Taifa la Misri lilibarikiwa sana…Farao hakufa na njaa, na zaidi ya yote Farao aliyekuwa mtu wa Mataifa alipata nafasi hata ya kuoneshwa maono na Mungu mwenyewe, jambo ambalo si la kawaida Mungu kuzungumza na watu wamataifa.

Kadhalika utaona wakati Wana wa Israeli tena wamepelekwa Babeli utumwani, Mungu aliibariki Babeli kwa ajili ya wana wa Israeli waliomo mule, Babeli ilizidi kustawi, na pia Mfalme Nebukadneza alipata hadi Neema ya kuoneshwa maono na Mungu ya wakati ujao, jambo ambalo sio la kawaida Mungu kuzungumza na watu wa Mataifa, hiyo ni kutokana na waisraeli waliokuwepo kwenye hiyo nchi, ijapokuwa walipelekwa kule kwa dhambi zao lakini bado kulikuwa na Baraka Fulani za kimwili na kiroho zilizokuwa zinaambatana nao.

Kadhalika kipindi cha Esta, Mfalme Ahasuero alifanikiwa katika enzi yake kwasababu ya Esta, Mordekai pamoja na Wayahudi waliokuwepo kwenye ufalme wake..

Na sehemu zote ndio hivyo hivyo, popote Wayahudi walipokwenda kulibarikiwa mwilini na rohoni.

Vivyo hivyo katika siku zile baada ya kumkataa Yesu Kristo, walipotawanyishwa tena kwenye mataifa yote ulimwenguni, popote walipokaribishwa sehemu zile zilibarikiwa kimwili na kiroho, Ukiangalia mataifa mengi ya Ulaya, mafanikio yao yametokana na Wayahudi waliokuwemo kule kipindi kile, kadhalika na Marekani, na nchi nyingine zote…baraka zao ni kwasababu ya waisraeli waliowakaribisha kipindi wanatawanywa.. na Mungu kayabariki mataifa yote kwasababu ya Israeli na Baraka kubwa aliyowabaikia ya rohoni, ni KUWAPA MATAIFA ZAWADI YA YESU KRISTO. Hiyo ndio zawadi kubwa Mungu anayoweza kumpa mwanadamu…Kwahiyo sisi kuzawadiwa Yesu Kristo yaani kuzawadiwa hii Neema ya kumkubali Yesu Kristo ni kutokana na Wayahudi kuwemo humu mataifani, tulimo sisi.

Lakini cha kuogopesha ni kwamba wayahudi sasa wameshaanza kurudi nchini kwao, kidogo kidogo wameshaanza kuhisi makosa yao waliyoyafanya miaka 2000 iliyopia, mioyo ya kutubu kidogo kidogo imeanza kurudi ndani mwao, mamia kila siku wanamiminika kurudi kwao, hiyo ni ishara ya nini?..Ni ishara kuwa Neema inaondoka huku…Zile Baraka zinaondoka huku, baraka za rohoni na za mwilini…Kumbuka Baada ya majeshi ya Israeli kutoka Misri nini kilitokea huko nyuma?, jibu ni mapigo! ..hakuna Neema tena! Hujasikia tena tangu hapo na kuendelea Mfalme yeyote wa Misri anaota zile ndoto za kiMungu tena! Wala hujasikia chochote cha maana kilichokuwa kinaendelea Misri…Hiyo yote ni kwasababu Uzao wa Mungu umerudi kwao, na Bwana amewarudia watu wake.

Kadhalika wana wa Israeli waliporudi nchini kwao, baada ya kuchukuliwa Babeli, hutaona Mungu akishughulika tena na Babeli, au Umedi au Uajemi…Habari zao ndio zilikuwa zimeishia pale, sasa Mungu anarudi kushughulika na watu wake Israeli.

Ndugu, Hii Neema ipo ukingoni, hivi karibuni! Wayahudi wanakwenda kutubu kabisa kabisa! Na Bwana atawasamehe, na atawamwagia kipawa chake cha Roho, na wakati huo huo Roho Mtakatifu atakuwa ameshaondoka huku kwetu mataifani, yaani unyakuo utakuwa umeshapita! Kitakachokuwa kumesalia ni dhiki kuu na siku ya Bwana inayotisha!, Bwana akirudi leo hatutasema hatukusikia wala hatukuona, vyombo vya habari vinatuhubiria injili kila mahali, mtu asipotaka kuyatilia maanani basi ni kwa uzembe wake mwenyewe, mwenye macho haambiwi tazama, mwenye masikio haambiwi sikia

Ikiwa hii neema ambayo inafifia unaichezea, moja ya hizi siku itazima kabisa..Jitathimini wewe mwenyewe umesimama upande upi.

Maran Atha!

Tafadhali share na kwa wengine, Mungu akubariki.


Mada Zinazoendana:

Print this post

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

Biblia inatuambia moja ya kazi ya malaika ni kuwahudumia watakatifu, (Waebrania 1:14) na tunajua siku zote kama mtu ni muhudumu ni lazima akae eneo husika la wale anawahudumia, kwamfano Daktari anafanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa, japokuwa anao kwake mwenyewe lakini huwezi kumkuta masaa yote yupo nyumbani bali muda wake mwingi utakumkuta anakesha mahospitalini, kwasababu huko ndipo wagonjwa walipo. Vivyo hivyo na malaika wa Bwana, wamepewa jukumu la kuwahudumia watakatifu, sasa japo makazi yao ni mbinguni lakini muda wao mwingi wapo duniani wanazunguka huko na huko kuhakikisha yale yote yaliyokusudiwa na Mungu juu ya watakatifu yanatimia.

Hivyo tusichokujua tu ni kuwa hata sasa tunapozungumza kuna mamilioni ya malaika wanaozunguza duniani kila siku, na kazi yao ni moja kuhakikisha kusudi la Mungu linatimia kwa namna zote. Na malaika kama biblia inavyotuambia ni viumbe wa rohoni hivyo Mungu amewapa uwezo wa kuchukua maumbile tofauti tofauti, wanaweza wakatembea kama nguzo ya moto, au wingu, au taswira za mnyama, au taswira ya mwanadamu. Kwahiyo katika sikuzote za maisha yako, kwa namna moja au nyingine ulishawahi kukutana au kupishana na malaika wa Mungu wengi pasipo hata wewe kujijua, Na ndio maana Mtume Paulo anasema:

Waebrania 13:1 “Upendano wa ndugu na udumu.

2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.”

Tukimwangalia Ibrahimu siku moja wakati amekaa nyumbani kwake ghafla aliona watu watatu wamesimama nyumbani kwake, Lakini Ibrahimu hakuwafukuza au kuwaita wapepelezi badala yake yeye ndiye aliyewashurutisha waangie nyumbani mwake wale na wanywe, na kumbe walikuwa ni malaika wa Bwana pamoja na Bwana mwenyewe wakiwa katika safari yao ya kwenda kuupeleleza mji..

Vivyo hivyo hao hao waliposhuka Sodoma, Lutu alipowaona kuwa ni wageni sio wenyeji wa pale hakusubiri wafike nyumbani kwake bali yeye ndiye aliyewakimbilia na kuwaambia waingie kwake! Wale na wanywe na walale, lakini wale watu walikataa kata kata, lakini Lutu hakuacha kuwashurutisha sana, na walipokubali baadaye ndipo Lutu alipojua kuwa wale hawakuwa watu wa kawaida.. Na Kuwafadhili wageni

 Sio lazima tu iwe wale wanaotaka kuja kulala nyumbani kwetu, lakini pia kuwatendea ukarimu wale ambao wanaonekana wanahitaji msaada kwa wakati huo, hususani wale tusiowajua….na ukarimu huo unaweza ukawa chakula, fedha, ushauri, n.k.

Biblia inatukumbusha tuwe wakarimu, ni wazi kuwa dunia ya sasa upendo umepoa kila mtu anajipenda nafsi yake, zamani ilikuwa mwenyeji ndio anamshurutisha mgeni aje kwake, lakini sikuhizi mwenye hitaji ndio anamshurutisha mwenye nacho amsaidie, na bado anaweza asiambulie chochote, utakuta muda mwingine unapishana na mtu barabarani anakuambia ninasikia njaa sijala, na hakuombi hata pesa anakuomba tu ukamnunulie muhogo mmoja pale apooze njaa! Utasikia huyo mtu anasema, mimi sina kitu na ukiangalia mfukoni ana kiasi tu kikubwa cha fedha ambayo haina matumizi imekaa tu kwenye pochi.. mwingine atakuambia naomba unilipie nauli, utaona mtu anasema sina pesa, lakini ukweli ni kuwa anayo lakini hataki kumpa, Ndugu kama unacho chochote wewe mpe tu! Sio lazima kiwe kingi, hata kama kakudanganya usijali chochote, kwa maana hujui huyo aliyekuomba ni nani?.

Mwingine hataonyesha dalili ya kukuomba chochote, lakini wewe ukimtazama utaona anao uhitaji Fulani, na huku ukiangalia una vichenchi chenchi vimebaki mfukoni wewe mpe tu, kwasababu hujui huyo unayempa ni nani…Lakini simaanishi  kwamba uumpe tu kila mtu, hata kama mtu anahitaji pesa ya sigara au pombe au madawa ya kulevya uumpe hapana!..Mtu wa namna hiyo hapaswi kupewa chochote kwasababu mtu mwenye shida kweli ya msingi hawezi kuomba vitu kama hivyo, vilevile hata malaika wa Bwana hawawezi kufanya hivyo. Ukimkuta Mtu kalewa halafu anakuomba kitu usimpe chochote, ukimkuta mtu kashika sigara halafu anakuomba usimpe! Mpe kwanza injili n.k

Lakini mbali na hao asilimia kubwa ya wengi wanaotuomba wanao matatizo..pengine hata wewe ilishakukuta ulifika wakati ulitamani mtu akusaidie kitu Fulani, pengine hata sio chakula, bali kitu Fulani kingine cha muhimu sana ambacho unahitaji tu kwa muda huo na hauna….sasa watu wa namna hiyo wapo mamia kwa mamia… tuwasaidie kwa vidogo tulivyo navyo. Utajisikiaje siku ile umefika mbinguni halafu malaika kama 100 wanatokea kila mmoja anakuambia ulishawahi kunisaidia mara 2 nilipokuwa duniani. Ni furaha kiasi gani unadhani Bwana Yesu ataona fahari juu yako kiasi, lakini siku ile mfano unafika na unaona malaika hawana habari na wewe, wakati unashangaa hilo  wanakuambia ulishawahi kutufukuza, au ulishawahi kutunyima kitu Fulani tulichowahi kukuomba tukiwa  duniani. Na wakati haukutani na malaika bali na MKUU mwenyewe Bwana Yesu, sasa tukiwa wabinafsi kila wakati kuna hatari kubwa sana ya kukosa mema Mungu aliyotuandalia..

Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.

34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?

40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”

Bwana akubariki. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine.


Mada zinazoendana:

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

JE! BAADA YA ULIMWENGU HUU KUISHA MALAIKA WATAKUWA NA KAZI GANI TENA?

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

MALAIKA WA MAJI NI NANI? (UFUNUO 16:5)


Rudi Nyumbani:

Print this post

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.

Watu wengi sana sio tu wasiomjua Mungu bali hata miongoni mwa wakristo, wakisikia jambo hili kuwa siku moja kuna kusimama hukumuni huwa linawatesa sana, na kuwahuzunisha sana na hilo linawafanya waishi Maisha ya wasiwasi mwingi. Lakini habari njema ni kwamba biblia inatumbia hukumu inakwepeka
.
 
Leo tutajifunza ni kwa jinsi gani tunaweza kuikwepa hukumu ya Mungu inayotisha, Na andiko pekee linalotuambia habari hiyo ni hili..
 
Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.”
 
Kama wengi tunavyofahamu huyu aliyesema maneno hayo ni Bwana wetu Yesu Kristo, lakini swali linakuja palepale je! Huko kumwamini Bwana kukoje, je! Ni kuamini tu kama yeye yupo?, au kumwamini tu kama yeye ni mwokozi mpaka kutufanya tusihukumiwe au vipi?. Mbona tumesikia wengi wamemwamini Kristo lakini wapo kuzimu?
 
Tusisahau kuwa biblia inatuambia hata mashetani wanaamini na kutetemeka, (Yakobo 2:19 ) wanaamini Yesu ni mwokozi, wanaamini maneno ya Mungu kuwa ni kweli,..hivyo hapo tunapaswa tujue biblia inapotuambia tumwamini Yesu na yeye aliyempeleka ni Zaidi ya kumfahamu tu wasifa wake.. Mfano ni sawa na umekutana na njia mbili mbele yako ukaona kibao kimoja kinasema kushoto ni shuleni, na kulia ni Sokoni, na wewe ukiangalia ulikuwa unatafuta mahali soko lilipo…Ni wazi njia ile ya kibao kinachokuelekeza sokoni utaiamini Zaidi kuliko ile ya kibao kinachokuelekeza shuleni..Sasa hiyo ni hatua ya kwanza, hatua ya pili ili ufike unapotaka kwenda ni sharti uifuate ile njia kwa gharama zozote hata kama itakuwa ina vumbi, na mikunjo kunjo haipendezi kama ile ya shule, utaifuata tu, lakini ikiwa hutaifuata na huku bado unataka ufike sokoni, ni wazi kuwa hutafika popote haijalishi umeifahamu njia sahihi kiasi gani.
 
Vivyo hivyo na kwa Bwana Yesu kumwamini tu pekee yake kuwa amekuokoa kwa kuongozwa sala ya toba, haikufanyi wewe usisimame hukumuni siku ile..Ni sharti uonyeshe kwa vitendo kuwa umemwamini yeye kwa kuifuata njia ya uzima, na vitendo hivyo ndivyo vinavyojulikana kama TOBA.
 
Toba ni kitendo cha kugeuka na kuanza safari kule ambako haukuwepo.. Sasa ikiwa mtu atakamilisha tu agizo hio basi Hukumuni hataingia.
 
Na hiyo inakujaje, mfano ikiwa leo hii umempa Kristo Maisha yako kwa mara ya kwanza, ukatubu dhambi zako zote ukaenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, kumbuka muda huo bado mbingu haifanya chochote juu yako, bali inakuangalia kwanza, mwenendo wako, je! Ni kweli alichotubia na alichobatiziwa unakitelekeza kwa vitendo, je ni kweli huendi disco tena, je ni kweli huangalii picha chafu tena kwenye mitandao?, je ni kweli hauendi bar tena, je ni kweli hufanyi uasherati tena…sasa Mungu akishaona mtu huyu kageuka anazidi kupiga hatua kila siku katika kuielekea njia ya uzima…mtu wa namna hiyo hata kama hatakuwa mkamilifu wote, tayari mtu huyo anahesabiwa haki na mbingu kama mtakatifu..na hiyo ndio maana ya neema.
 
Hata ikitokea hajafikia ule utimilifu wote halafu akafia njiani mtu huyo moja kwa moja siku ile hataingia hukumuni. Kwasababu alikuwa anaonyesha nia ya kuelekea katika njia ya uzima..Mfano hai ni ule wa kipindi cha Sodoma na Gomora pale Lutu alipofuatwa na wale malaika, hawakumteketeza Lutu na wale watoto wake wawili sio kwamba walikuwa ni wenye haki sana mbele za Mungu hapana lakini pindi walipoonyeshwa tu njia ya uzima wao, wa kujiponya nafsi zao waliindea njia hiyo hiyo bila kugeuka nyuma, na mwisho wa siku wakajikuta wameokoka,Lakini mke wa Lutu aliyatamani ya nyuma japokuwa alitokewa na malaika japokuwa aliiamini ile njia kweli lakini moyo wake haukudhamiria kwa dhati kuifuata ile njia na ndio maana akawa jiwe la chumvi.
 
Ndugu ikiwa umemwamini Kristo halafu bado unatembea huku unageuka geuka nyuma, haijalishi ulitokewa na malaika wangapi siku ile ulipoamini,haijalishi ulitokewa na YESU mwenyewe, Kwenda hukumuni hakukwepeki, na unajua anayepandishwa hukumuni sikuzote ni mshtakiwa na hakuna mtu yeyote anayeweza kuyakwepa au kuyashinda mashtaka ya Mungu juu yake…bali wote watakaopanda hukumuni wataingia kwenye ziwa la moto..
 
Fahamu kuwa Mungu hatuhesabii haki kwa matendo yetu, vile vile usisahau hatuhesabii haki kwa matendo yetu maovu, lakini anaangalia ule moyo unaotamani kuhesabiwa haki ndio anaupa Haki, na moyo wowote wa namna hiyo siku zote utajitahidi kuishi Maisha ya haki kwa gharama zozote na ndipo Mungu anamalizia kuupa haki yote kwa neema yake.
 
Ikiwa hukulifahamu hilo basi huu ndio wakati wako sasa wa kuonyesha Imani yako kwa matendo, acha kwa moyo mmoja mambo yote mabaya na ya aibu uliyokuwa unayafanya huko nyuma, ulikuwa unaangalia picha za ngono, acha ulikuwa unafanya mustarbation acha, ulikuwa unafanya uzinzi acha, ulikuwa unavuta sigara acha, ulikuwa unatoa mimba acha, ulikuwa unauza madawa ya kulevya au unatumia acha, ulikuwa unatukana tukana ovyo acha, ili Mungu akuone nia yako amalizie kukupa HAKI YOTE bure,..hata ukifa leo uwe na ukakika wa kuingia uzimani bila kupita hukumuni.
 
Warumi 8:1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu”.
 
Ubarikiwe sana.
 
Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki.

Mada zinazoendana:

KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?

UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.

UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.

KAMA MHUBIRI NI WOKOVU UPI UNAUPELEKA KWA WATU?

Rudi Nyumbani:

Print this post

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

Wakati mwingine, unaweza ukapitia hali ya kusemwa vibaya, kwa siri au hadharani, Tambua tu hiyo ni hali ya kawaida, wewe sio wa kwanza, hata walio watu wakuu na wakubwa na wanaoheshimika wanasemwa vibaya, hata kama wamefanya mazuri mangapi katika jamii, eneo la kuzungumziwa vibaya, haliepukiki katika Maisha yao.
 
Mtu aliyekuwa mkamilifu, na asiye na dhambi, na Zaidi ya yote ni Mungu, (Bwana wetu Yesu Kristo) alisemwa vibaya mara nyingi sana, sasa kama yeye alisemwa vibaya na alikuwa hana dhambi hata moja! Wewe ni nani usizungumziwe vibaya?..Kwahiyo hilo ni jambo ambalo halikwepeki maadamu bado tupo hapa duniani..Wakati mwingine unaweza ukaambiwa maneno makali hata na watu wako wa karibu sana, ambao usingeweza kutazamia kama wangekwambia maneno hayo…
 
Mfano katika Biblia tunamwona mtu mmoja aliyeitwa YEFTHA, Huyu alikuwa mzaliwa wa kwanza kwa Baba yake, lakini mama yake alikuwa ni kahaba, kwahiyo alizaliwa na mama kahaba, na baadaye Baba yake akaoa mke wa halali akazaa naye Watoto, lakini hao Watoto walipokuwa mkubwa wakamtamkia hadharani Yeftha kwamba hatakuwa mrithi pamoja nao kwasababu yeye ni mwana wa mwanamke mwingine kahaba, wakamfukuza..Na niwazi kuwa pia walitaka kumdhuru maana aliwakimbia na kuhamia kabisa nchi nyingine, na sio tu ndugu zake walimchukia, bali na Taifa zima lilimtenga. (Habari hizi utazipata katika kitabu cha Waamuzi Mlango wa 11 na kuendelea).
 
Kwahiyo Yeftha akaondoka katika nchi yake, akiwa peke yake, watu maskini wasio na maana (mabaradhuli) waliochoka kama yeye, wakaenda kuungana naye huko alikokwenda… Lakini Mungu alilitazama teso lake, wakati ulipofika alimnyanyua Yeftha kama alivyomnyanyua Yusufu, na akawa MWAMUZI katika Taifa Teule la Mungu (Israeli)..Shujaa wa Bwana,haleluya!!..Wale wote waliomfukuza walikuja kumwomba msaada kwa kumsihi sana, Taifa zima lilikuja kumwomba msaada katika vita. Kwasababu maandiko yanasema katika
 
1Samweli 2 :6 “Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.
8 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake”.
 
Sasa leo tutajifunza ni namna gani tutashinda hali ya kusemwa au kutamkiwa maneno mabaya. Unajua wanadamu wote tumeumbwa na moyo, moyo kwa lugha nyingine tunaweza kusema ni (utu wa ndani), sasa uwezo wa moyo kuhifadhi hisia au maumivu ni mkubwa kuliko mwili, kidonda cha mwili kikipona kimepona kikishabaki kovu kinakuwa sio kidonda tena, hata upaguseje pale hapawezi kusababisha maumivu tena, Zaidi ya yote pakipona ndio panaweka gamba gumu zaidi(sugu)…kwasababu kidonda kimeshapona…Lakini moyo haupo hivyo, vidonda vyake haviponi kirahisi hivyo na inaweza ikapita miaka hata 10, lakini pale palipoumizwa pakiguswa tena kidogo tu! Ni kama umeanza mwanzo tena.
 
Kwahiyo hapo ni kuwa makini sana..Vinginevyo tusipofahamu namna ya kushughulika na utu wetu wa ndani, tutakuwa tunaishi Maisha ya maumivu na kutokusamehe kila siku…
Sasa dawa ya kuzuia kuumizwa ni ipi?
Ni kujitahidi kutokuweka jambo moyoni, au kwa lugha nyingine unakuwa unajitahidi kuyapotezea kwenye kichwa chako baadhi ya mambo, unakuwa huyachukulii kwa uzito..Kwamfano mtu amekwambia labda neno la “kukudhalilisha au kukushushia heshima”..jambo lile kabla ya kuanza kuliweka moyoni na kuanza kulitafakari na kujiuliza uliza kwanini mtu yule kaniambia vile, kwani kanionaje?….Utumie muda huo kufikiri ingekuwa ni wewe umemwambia vile, ungekuwa na maana gani?.
 
Ukiona mtu kakutukana, hebu fikiria wewe uliowatukana moyoni mwako, je! ulikuwa una nia gani mbaya nao?..utagundua basi tu! Uliwatukana pengine kwa hasira za pale pale na iliishia hapo tu!…huwezi kufikiri kwamba mtu uliyemtukana kwamba afikiri unamchukia, au una kinyongo naye… au umemtafakari sana, au yupo kwenye akili yako muda wote, na umekusudia kumwumiza, kwa kiwango anachokifikiria moyoni mwake…..wewe ulimtukana tu kwasababu zako… basi imeishia hapo tu!.
 
Kadhalika na wewe unapotukanwa au unapodharauliwa, hupaswi kuliweka jambo moyoni, kwasababu yule aliyekudharau, pale alipokudharau pengine haikupita hata dakika tano kashasahau kwamba alikudharau…Hivyo wewe unabaki na majeraha, wakati mwenzako moyo wake umeshasafishika siku nyingi, na pengine anampango wa kuja kuendelea kuwa na wewe, na kushirikiana na wewe kwa mambo mengine.
 
Hiyo ndio namna ya kujiponya majeraha yako…Hekima hiyo tunaisoma pia katika maandiko matakatifu, Sulemani Mwana wa Daudi aliiandika…
 
Mhubiri 7:21 “Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana.
22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine”.
 
Na mambo mengine yote! Yachukulie tu juu juu, jiweke kama ingekuwa ni wewe umemfanyia mwingine. Lakini endapo kila kitu kinachozungumzwa mbele yako wewe unakitafsiri tu na kukiweka moyoni mwako! Na kusema aaa anamaanisha nini kusema vile?…aa kwanini aseme vile?…aa kwani kaona nini kwangu?…au kwasababu niko hivi ndio maana kasema vile?…au kwasababu yeye ana kile na mimi sina?…Ukiishi kwa utaratibu huo, sura yako kila siku haitakosa huzuni, na uchungu, na macho hayataisha machozi, na kununa, na utakuwa mtu wa kunung’unika na kufurahia mabaya ya watu wengine, na hatimaye kutafuta namna ya kulipa kisasa na wengine wanaishia kwenda kwa waganga wa kienyeji na manabii wa uongo, kutafuta dawa ya kushughulika na maadui zako.
 
Lakini ukjifunza kuishi Maisha hayo Biblia inayotufundisha, kamwe hutapata majeraha ya moyo na utaishi Maisha ya msamaha na kuvumilia, na kupendana na watu, na ndivyo pia utakavyozidi kupendwa na watu, na hutaona kama kila mtu ni adui yako, Na hata kama utakuwa unajiona upo chini na wengine wapo juu kumbuka Bwana anaziona njia zako njema…na hivyo wakati ukifika Bwana atakunyanyua tu kama alivyomnyanyua Yusufu au Yeftha, haijalishi itachukua miaka mingapi, lakini atakuja kukulipa mema tu!. Yusufu alipokuwa Misri hakuwahi kunung’unika kwa wale ndugu zake kwa kumuuza, Zaidi baadaye aliwakaribisha wote na kula pamoja nao.
 
Bwana akubariki sana.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
 

Mada zinazoendana:

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

KWANINI PALE BWANA YESU ALICHUKUA HATUA YA KUMSAMEHE DHAMBI KWANZA KABLA YA KUMPONYA YULE MTU MWENYE KUPOOZA?(MARKO 2).

KISASI NI JUU YA BWANA.

EPUKA MUHURI WA SHETANI


Rudi Nyumbani:

Print this post