SWALI: Ayubu alimaanisha nini kusema..Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Aliwezaje kurudi tena tumboni mwa mama yake tena uchi je hilo jambo linawezekana?
JIBU: Kauli hiyo aliisema Ayubu baada ya kupotelewa na familia yake na mali zake. Lakini Kwa ujasiri akamtukuza Mungu katika hali hiyo pia, kwa kusema maneno hayo;
Ayubu 1:21
[21]akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
Lakini swali lipo hapo, katika kurudi tumboni mwa mama yake uchi. maana yake ni nini?
Ikumbukwe kuwa sisi hatukutoka tu katika tumbo la wanamke bali pia katika tumbo la ardhi, hiyo ndio mama wa ulimwengu. yaani mama wetu wa kwanza.
soma;
Zaburi 139:15
[15]Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
[15]Mifupa yangu haikusitirika kwako,
Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
Mhubiri 12:7
[7]Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa,
Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Hivyo Ayubu aliposema nami nitarudi tena huko huko hakumaanisha mama yake mzazi, bali mama wa ulimwengu wote yaani ardhi.
Na ndivyo ilivyo kwa kila mmoja wetu, hukuja na kitu, utaondoka bila kitu chochote. Ukiwa uchi vilevile.
lakini jambo lingine la kufahamu kuwa, wale walio ndani ya Kristo, wafikapo kule ng’ambo hawataonekana uchi, bali watapewa vazi jipya la rohoni la Kristo Yesu, ndio ile miili mipya ya utukufu isiyoona uharibifu idumuyo milele.
2 Wakorintho 5:1-3
[1]Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. [2]Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; [3]ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.
[1]Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.
[2]Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;
[3]ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.
Swali ni je! Umeandaliwa vazi lako baada ya kuondoka?
Kumbuka unalipokea kwa kumwamini Yesu Kristo leo, okoka tubu dhambi zako, ubatizwe, kisha upokee kipawa cha Roho Mtakatifu. vazi lako liwe limekamilika., ili siku ile usionekane uchi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
SIFA ZA MAMBA YULE MKUBWA WA AYUBU.
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA MFUNGO.
Rudi Nyumbani
Print this post
SWALI: Je Daudi aliwachukia viwete na vipofu? Kama tunavyosoma katika 2Samweli 5:6-9. Je! habari hiyo tunaielewaje?
JIBU:
2 Samweli 5:6-9
[6]Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo. [7]Lakini Daudi aliipiga ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi. [8]Naye Daudi alisema siku hiyo, Yeye atakayewapiga Wayebusi, na apande kwenye mfereji wa maji, na kuwapiga viwete, na hao vipofu, ambao roho yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani. [9]Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani.
[6]Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo.
[7]Lakini Daudi aliipiga ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi.
[8]Naye Daudi alisema siku hiyo, Yeye atakayewapiga Wayebusi, na apande kwenye mfereji wa maji, na kuwapiga viwete, na hao vipofu, ambao roho yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani.
[9]Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani.
Habari hii inazungumzia wakati ule ambao Daudi alikwenda kuiteka Yerusalemu na kuufanya kuwa mji wa Mungu.
Alipofika na kukutana na wenyeji wa mji huo, walimdharau na kumsema kimafumbo kwa kauli ya mzaha kumwambia “Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe;”
Wakiwa na maana vita yake ni ya kupambanishwa na watu dhaifu kabisa wa mji, mfano wa vipofu na viwete, hao ndio apambane nao, lakini sio majemedari wa nchi ile. Akiweza hao walau ndio aingie sasa kujaribu kuuteka, huku wakijua kuwa hata hilo Daudi hataweza kwasababu walimwona ni dhaifu.
Na ukweli wakati huo Daudi hakuwa na nguvu yoyote, kwasababu ndio kwanza ametoka kuupokea ufalme. Hawakujua kuwa nguvu zake tangu zamani zina Mungu, ndio zile zilizomwangusha Goliathi ni silaha zake kwa jiwe moja.
Lakini Daudi aliipowafuatia na kuwapiga, na kuwaangamiza, naye alitumia pia jina hilo hilo la vipofu na viwete kimizaha akiwaita wayebusi waliomwonyeshea dharau..pamoja na hilo Daudi alionyesha kuwachia sana.
Lakini mistari hiyo hakumaanisha kuwa anawachukia viwete na vipofu. Hapana Kama ingekuwa hivyo asingemkaribisha Mefiboshethi mtoto wa Yonathani katika nyumba yake ya kifalme kuketi mezani pake daima..(2Samweli 9). Na ikumbukwe kuwa Daudi alikuwa anamcha Mungu na kuwakumbuka sana wanyonge.
Lakini pale inaposema….
“Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani”.
Ni kwamba kufuatana na Daudi kuwasema viwete na vipofu akiwarejea wayebusi, ukazuka msemo huo, ‘vipofu na viwete hawana ruhusu kuingia nyumbani mwa Mungu;. Lakini haikuwa hivyo’..
Misemo na namna hii ilikuwepo tangu zamani hata kuhusu ile habari ya mfalme Sauli, ya kutabiri (1Samweli 19:24), na kuhusu ike habari za mtume Yohana, pale wale mitume wengine waliposikia Kauli ya Bwana Yesu inayosema ikiwa nataka huyu awepo mpaka nijapo, wakadhani kuwa Yohana hata onja mauti kamwe, mpaka Yesu atakaporudi kumbe hawakumuelewa Bwana Yesu, hakumaanisha vile.(Yohana 21:22-23)
Na ndivyo ilivyodhaniwa kwa Daudi kwamba anawachukia vipofu na viwete, kumbe aliwamaanisha wayebusi.
Lakini ni nini hasaa tunaweza jifunza..katika tukio hilo?
Ni kawaida ya adui yetu anapokaribia kushindwa hunyanyua ujasiri wake kwa kiwango cha juu sana. Mji ambao uligeuzwa kuwa wa Bwana, na mwema kuliko yote, ulitanguliwa na dhihaka nyingi za kukatisha tamaa. Hata ukuta aliokuwa anaujenga Nehemia, ambao sehemu yake iliendelea kudumu kwa mamia ya miaka mbeleni ulitanguliwa na dhihaka nyingi za kuvunjishwa moyo. wakisema hata mbweha akipita juu yake utaanguka.
Silaha hiyo hiyo anaitumia adui leo, unapoona maono makubwa ya kuitenda kazi ya Bwana ndani yetu, vitisho vya adui huanzia hapo, aah wewe huna upako, wewe huwezi kuhubiri, huna pesa, huna elimu ya kukutosha, huna uzoefu, utafungwa..hizo zote ni dhihaka, Daudi alishazitambua toka kwa Goliathi, ndio maana akawashinda wayebusi.
Hivyo ni kusimama imara kuitetea injili, kwa imani tukijua hakuna linaloshindikana kwake yeye aaminiye. Na palipo na dhihaka nyingi ndipo palipo na mafanikio makubwa.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Wayebusi walikuwa ni watu gani?
Hanithi ni nini katika biblia? (kumbukumbu 23:17)
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
WhatsApp
Katika agano la kale, Israeli walikuwa na makusanyiko mengi, ambapo walikutanika kumfanyia Mungu ibada, na kuzishika sikukuu. Lakini pia yalichaguliwa makusanyiko mengine yaliyoitwa mikutano/makusanyiko ya makini. Makusanyiko haya yalifanyika katika siku ya saba ya sikukuu ya Pasaka, na siku ya nane, baada ya sikukuu ya vibanda. Katika siku hiyo hawakuruhusiwa kufanya kazi yoyote. Bali ilitengwa kwa ajili ya kujitakasa, au kujisogeza karibu na Mungu,
Hivi ni vifungu baadhi vinavyoielezea siku hiyo;
Hesabu 29:35 Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; 36 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba. Walawi 23:34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana. 35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. 36 Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi Kumbukumbu 16:8 Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa Bwana, Mungu wako, usifanye kazi yo yote.
Hesabu 29:35 Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi;
36 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba.
Walawi 23:34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana.
35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.
36 Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi
Kumbukumbu 16:8 Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa Bwana, Mungu wako, usifanye kazi yo yote.
Huo mkutano mtukufu ndio kusanyiko la makini.
Hekalu la kwanza pia lilipomalizika liliwekwa wakfu katika siku hii ya kusanyiko la makini
2Nyakati 7:9 Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba.
Sehemu nyingine mikusanyiko hii iliitishwa rasmi, kwa lengo la kujimimina kwa Mungu kuomba, kwa ajili ya maovu na majanga ambayo yanaipata nchi. (Yoeli 1:14 – 2:15). Kusanyiko hili liliitwa pia kama kusanyiko kuu.
Je! Ufunuo wake ni upi leo?
Kama vile tulivyo na mikusanyiko ya aina mbalimbali leo, mfano ya shule ya jumapili, ya semina, ya injili n.k. Vivyo hivyo hatuna budi kuwa na makusanyiko ya makini. Ambayo ni mikusanyiko ya mifungo na maombi. Ambapo tunapata muda wa kujimimina kwa undani kabisa uweponi mwa Mungu, kumtaka aingilie kati mambo yetu.
Je! unaithamini? Mungu aliyesema tusiache kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25). Hakumaanisha tu mikusanyiko ya jumapili, lakini pia ya mifungo na maombi.
SWALI: 2Timotheo 3:7, ina maana gani inaposema;
wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
JIBU: Katika kitabu cha 2Timotheo sura ya tatu(3), kuanzia mstari 1-9. Kinaeleza sifa za watu watakaozuka katika siku za mwisho. Tabia ambazo hapo mwanzo hazikuwepo. Sasa ukisoma pale utaona zimeorodheshwa baadhi ikiwemo kutokea watu wenye kupenda fedha, watu wakali, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu,..na nyinginezo
Lakini ipo sifa nyingine inatajwa pale, kuwa litazuka kundi la watu wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake..ndio hao ambao anaeleza sasa mbeleni, wanajifunza sikuzote ila wasiweze kuufikia ujuzi wa kweli.
Tusome;
2 Timotheo 3:5-9
[5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. [6]Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; [7]wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli. [8]Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani. [9]Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
[5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
[6]Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;
[7]wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
[8]Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
[9]Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
Maana ya ujuzi;
Ujuzi maana yake ni ufanisi au kukifanya kitu kwa utashi wote. Mtu anaweza akafanya jambo lakini akiwa hana ujuzi nalo litakuwa ni kituko kama sio hasara kabisa. Kwamfano mtu atasema, mimi naweza kujenga (na hajasomea ujenzi). Hivyo akaenda kununua tofali na kuanza kupandisha, unajua ni nini kitamkuta? kwasababu hajui kanuni za ujenzi anaenda kufanana na yule mtu aliyejenga nyumba yake juu ya machanga.
Ndivyo ilivyokuwa kwa hawa watu, hawakuufikia huo ujuzi wa kweli, kwasababu walikuwa na nia zao wenyewe za tofauti na sio ya Kristo, walilenga kuwakusanya wanawake waliokuwa na mizigo ya dhambi, kama daraja lao, na hifadhi yao ya kihuduma, ili watumize malengo yao. Sasa Kwa urefu wa tabia za wanawake hao bofya link hii uwasome >>> Wanaowachukua wanawake wajinga mateka ni akina nani?
Lakini huo ujuzi wa kweli ni upi?
ujuzi wa kweli ni UTAUWA/ UTAKATIFU. Mtu anayefikia kilele cha kuifahamu kweli ya Kristo huishia katika utakatifu wa kweli. Tunalisoma hilo katika;
Tito 1:1
[1]Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ‘ujuzi wa kweli’ ile iletayo utauwa;
Umeona ujuzi wa kweli, lazima ulete utauwa.
Lakini watu hawa walikuwa na mfano wa utauwa lakini walizikana nguvu zake kimatendo, ndio maana hawakufikia..waliitwa wakristo lakini wakristo jina, waliitwa mitume, wainjilisti, manabii, waalimu, watakatifu, lakini nia zao zipo penginepo. Walikuwa na elimu za vyuoni, wanajua kuyachambua maandiko, na vifungu vyote, lakini maisha ya utakatifu yapo mbali na wao.
Ndilo linalotendeka leo hii, maarifa tuliyonayo kuhusu Mungu ni mengi, zaidi hata watu wa kale, tuna wingi wa vyuo vya theolojia, na makanisa, na mafudisho mengi. Lakini maisha ya wengi hayamwakisi Kristo katika utakatifu wa kweli.
ndio hili neno linatimia,
wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli
Ni swali la kujiuliza na sisi, je! wokovu wetu umefikia ujuzi wa kweli? Kumbuka hizi ni siku za mwisho, mafundisho uliyonayo yanakusukuma kwenye nini? FUATA UTAKATIFU.
Bwana akubariki
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?
MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
SWALI: Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema.. “Yatosha kwa siku maovu yake”.
Mathayo 6:34
[34]Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
JIBU: Bwana, hataki tuwe na hofu ya vitu vya huko mbeleni (ambavyo bado havijafikiwa), si mpango wa Mungu tubebe mizigo mingi kwa wakati mmoja, kwasababu hatujaumbiwa asili hiyo, ndio maana hata katika ile sala ya Bwana tunasema; utupe “siku kwa siku” rikizi yetu.
Hasemi utupe riziki ya “mwaka mzima” kana kwamba tukikosa vyote leo hatutaishi.. bali siku kwa siku..
Kwanini iwe hivyo?
Sasa katika hali yetu ya kibinadamu tunajua kabisa mihangaiko yetu, taabu zetu, shughuli zetu za kila siku, mara nyingi huwa haziwi safi kama tunavyotarajia, wakati mwingine kama sio kujikwaa, basi tunakutana na mambo mengi pia ya kukosesha yasiyompendeza Mungu. Hayo ndio maovu yake.
Tunakutana na watukanaji, na wazinzi, na waharibifu, wenye mizaha, wasumbufu, n.k. hivyo kiuhalisia katika mambo yetu mema, maovu pia hutokea. Hivyo kitendo cha kuyataabikia sana ya mbeleni, tafsiri yake ni kuwa tunayaleta na maovu yake pia leo. Na matokeo yake tutalemewa na maovu kichwani Na kujikuta tunamkosea Mungu.
Bwana anataka tupambane kwanza na yale ya leo, ya kesho tutapewa nguvu ya kushindana nayo. Kwa tafsiri nyingine ikiwa wewe ni wa kubeba mambo mengi ya mbeleni, dhambi itakulemea na kukushinda.
Yatosha kwa siku maovu yake.
Ni kwa jinsi gani Mungu anapatiliza maovu ya baba zetu sawasawa na Kutoka 20:5-6?
Nilikuwa naomba kujua utofauti kati ya DHAMBI, UOVU na KOSA kibiblia.asante!!
HAMJAFAHAMU BADO?
Kama unao uhakika huo basi ni jambo jema lakini swali, ni kitu gani kinachokupa uhakika huo?.
Je! Ni imani uliyonayo?..au Ni dhehebu ulilonalo?, Au ni matendo unayoyafanya?…au ni nini?.
Kama ni Imani (kwamba unamwamini na akija ni lazima uende naye) basi fahamu kuwa anaweza akaja na usiende naye ijapokuwa unayo imani.
Kama ni dhehebu ndilo linalokupa uhakika wa kwenda na Bwana pindi atakaporudi, basi fahamu kuwa hio pekee haitoshi..
Pamoja na dhehebu lako bora, na jina lako bora bado unaweza usimwone siku atakaporudi..
Je ni Matendo yako mema ndiyo yanayokupa uhakika? (Kwamba hudhulumu mtu, hutukani,huibi, unasaidia wengine n.k)
Kama ni matendo tu, ndio yanayokupa uhakika wa kwenda na Bwana, basi fahamu kuwa atakaporudi unaweza pia usimwone.
Sasa ni kitakachopaswa kumpa mtu uhakika ya kwamba atakapokuja BWANA basi ataenda naye??.
Hebu tuangalie jibu lake katika biblia, kupitia maneno ya Bwana YESU (Atakayerudi).
Yohana 3:1 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. 3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”
Yohana 3:1 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.
2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”
Umeona sifa ya mtu atakayemwona Bwana siku ile?.
Si dhehebu kwasababu Nikodemo alikuwa ni wa dhehebu la Farisayo lililo bora (Matendo 26:5), wala si Imani kwa Mungu, kwasababu Nikodemo alikuwa tayari anamwamini Mungu na pia amemwamini YESU.
Lakini Bwana YESU anaonyesha kuwa hayo yote hayawezi kumsaidia mtu, isipokuwa kuzaliwa mara ya pili (kuwa kiumbe kipya katika roho).
Ni nini maana ya kuzaliwa mara ya pili???..Bwana YESU amefafanua katika mistari inayofuata kwamba ni kuzaliwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu (yaani ubatizo wa maji kama ishara ya utangulizi wa utakaso, na ubatizo wa Roho Mtakatifu).
Ubatizo wa Roho Mtakatifu ndio ukamilifu wa utakaso wa Mtu, na mtu anapoupokea huo pamoja na ubatizo wa Maji, anafanyika kuwa kiumbe kipya kupitia kazi za Roho Mtakatifu ndani yake.
Jambo hili limewekwa vizuri zaidi na Mtume Paulo kupitia waraka wake kwa Tito.
Tito 3:4 “Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu”.
Tito 3:4 “Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;
5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu”.
Je swali umejazwa Roho Mtakatifu kama tiketi ya kumwona Bwana na kwenda naye siku ile?.
Waliojazwa Roho Mtakatifu, wanaongozwa na Roho Mtakatifu, na mtu aliyejaa Roho Mtakatifu, hawezi kuwa mtu wa kidunia, wala kuupenda ulimwengu..kwasababu roho iliyopo ndani yake inamsukuma kufikiri yaliyo ya juu.
Mtu alijaa Roho mtakatifu kama muhuri wa kumwona Bwana, hawezi kufanana kimwonekano na watu wa ulimwengu, badala yake anakuwa nuru kwao, na hawezi kushirikiana na matendo ya giza.
Na kama hauna uhakika Bwana akirudi hautaenda naye, ni vizuri ukapata huo uhakika…
Pengine unaweza kuhitimisha kwa kusema siku atakapokuja, kama nitaenda naye au sitaenda naye…“Mungu anajua”…lakini hebu fikiri hili…
“Mwalifu anatangaza kuwa atakuja kukudhuru”
Halafu wewe unasema siku atakapokuja, “yeye anajua kama atanidhuru au hatanidhuru”.
Umeona?..kama hautachukua tahadhari ni wazi kuwa atatimiza lengo lake..lakini kama utajidhatiti basi utapata uhakika kama atatimiza lengo lake au la!.. wala huwezi kamwe kumwachia maamuzi afanye yeye!!.
Vivyo hivyo na sisi ni lazima tuwe na uhakika kwamba atakapokuja tutakwenda naye au hatutakwenda naye, na si kumwachia yeye atufanyie maamuzi..
Tukimwachia yeye tutakuwa tumemfanya yeye kuwa mwenye upendeleo, na yeye hana upendeleo.
1Petro 1:17 “Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni”
Maran atha.
NIMEOKOKA, ILA MUNGU NDIYE ANAYEJUA NITAKWENDA WAPI.
TUMAINI NI NINI?
Waoga ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani?(Ufunuo 21:8).
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
Nifanye nini ili niwe na uhakika nikifa naenda mbinguni?
Shetani huwa ana kauli zake, za uongo ambazo hupenda kuwaaminisha watu, kuwa kuna mambo mwanadamu hawezi kuyafanya akiwa hapa duniani hata iweje.
Tukisoma habari ya Ayubu wakati ule shetani alipokwenda kumshitaka kwa Mungu.
Mungu alipomuuliza kuhusu mwenendo wake, majibu ya shetani yalikuwa ni kwamba Mungu amemzungushia wigo, kutunza alivyonavyo, Na kama atapotezewa alivyonavyo, basi atamkufuru Mungu waziwazi. Hivyo Mungu akaruhusu shetani amjaribu Ayubu, amchukulie alivyo navyo vyote, lakini uongo wa kwanza, ukashindwa, alipoona Ayubu anamtukuza Bwana katika misiba yake. Hiyo ni kuonyesha kuwa mwanadamu yoyote anaweza kuishi bila msukumo wa mali,wala mtu wala kitu chochote katika hii dunia.
Lakini baadaye tena, akaendelea mbele kuzungumza uongo mwingine, alipoona Ayubu bado yupo na Mungu, akamwambia Mungu, yote yanawezekana kwa mwanadamu kuvumilia, lakini hili la kuugusa mfupa wake,kumtesa, kamwe hawezi kuvumilia atakukufuru tu. Mimi ninawajua wanadamu uwezo huo hawana, nilishawafundisha pia huko duniani.
Ayubu 2:4 Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. 5 Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako. 6 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake. 7 Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa. 8 Naye akashika kigae cha kujikunia; akaketi majivuni. 9 Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe. 10 Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Ayubu 2:4 Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
5 Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.
6 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake. 7 Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.
8 Naye akashika kigae cha kujikunia; akaketi majivuni. 9 Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe.
10 Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Hilo nalo likashindikana. Kumbe mtu, hata kuupoteza uhai wake kwa ajili ya Kristo, linawezekana.
Ni nini Bwana anatufundisha kwa mawazo ya adui kwetu sisi ?
Leo hii ni rahisi sana kusikia, kauli kama, hakuna mtakatifu duniani! Ni rahisi kuona mtu anaanguka ovyo katika dhambi, na kutumia kisingizio kuwa yeye sio malaika. Utasikia kauli kama haiwezekani mtu kuacha vyote alivyonacho kwa ajili ya Kristo. Ndugu tambua kuwa hizo ni kauli za ibilisi ndani ya moyo wako. Adui anapenda kumshusha thamani mtu, kumweka kama kiumbe ambaye hawezi kujisimamia, hafundishiki, haaminiki.
Ni kweli mwanadamu kuwa na ukamilifu wa Mungu haiwezekani (Ndio sababu Yesu akaja kutukomboa), lakini kuna viwango Fulani Mungu anajua tunaweza kuvifikia, akalithibitisha hilo kwa Ayubu. Kama Ayubu ameweza kwanini wewe ushindwe, usijishushe thamani.
Neema haijaja kutuambia kuwa sisi hatuwezi, bali imekuja kutuwezesha zaidi kuwa wakamilifu mbele za Mungu, yaani pale Ayubu aliposhindwa sisi tunasaidiwa kwa hiyo, na kutufanya tupokelewe kikamilifu mbele za Mungu, hiyo ndio kazi ya Neema (Soma Tito 2:11-12).
Kamwe usiruhusu hayo maneno ya kushushwa thamani na ibilisi, kwamba wewe huwezi mpendeza Mungu, huwezi kuacha vyote kwa ajili yake. Yesu alisema tutakuwa wakamilifu kama Baba yetu alivyomkamilifu. Tunachopaswa kufanya ni kuamini kuwa hilo linawezekana na kuonyesha bidii katika hilo kumpendeza yeye. Na neema ya Mungu itatusaidia kufikia kilele Hicho cha juu kabisa.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).
ILI TUONEKANE WAKAMILIFU MBELE ZA MUNGU.
Kwanini Labani aseme Yakobo ni Mfupa wake na nyama yake?(Mwanzo 29:14)
SWALI: Neno ‘huisingizia sheria na kuihukumu sheria’ maana yake nini? (Yokobo 4:11)
Yakobo 4:11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
JIBU: Ili kuelewa vifungu hivyo Mtume Yakobo kwa uongozo wa Roho alikuwa na maana gani aliposema Mtu amsingiziaye ndugu yake au amuhukumuye ndugu yake huisingizia sheria na kuihukumu sheria, Tafakari mfano huu.
Raisi ya nchi amendea mahali Fulani kwa ajili ya shughuli zake za kimaendeleo, lakini katika kupita pita kwake akaona familia moja iliyo fukara sana, na alipotathimini tatizo nini akaona walikuwa wote ni walemavu hawawezi kufanya kazi kabisa, hivyo kwa huruma zake akaagiza wajengewe nyumba, wapewe na msaada wa chakula kutoka serikali kila mwezi, walipiwe na pia bili za maji na chakula kwa kipindi chote wawapo hai.
Lakini Yule raisi alipoondoka, mkuu wa mkoa wa eneo lile, akaenda kuitazama ile familia ikoje, badala ya kutekeleza agizo la mkuu wake, akaanza kuwashitaki na kusema hawa hawana ulemavu wa kuwafanya wasifanye kazi, wanajifanya tu wadhaifu, ni wavivu, wanaweza kuendesha maisha yao, hakuna haja ya kuwapa chochote, hivyo akaanza kuwaonea na kuwashutumu, na kuwanyima mahitaji yao kwa wakati, na kuwashurutisha wajitume.
Sasa Kimsingi mtu kama huyu, ni rahisi kudhani, anawaudhi na kuwashutumu tu wale maskini, Lakini kiuhalisia anamudhi na kumshitaki raisi aliyetoa amri ile kwamba walishwe. Kwa tabia hiyo ni kwamba anamshtaki raisi hafikirii vizuri, anatumia fedha za uma vibaya, anatafuta sifa kwa watu, ana maamuzi yasiyokuwa na maana, hata kama huyo mkuu wa mkoa hawazi hivyo, anampenda raisi wake, na anathamini mali zake, lakini kitendo tu cha kuwashutumu wale, ni sawa na anamshutumu aliyewafadhili.
Ndivyo ilivyo na katika kifungu hicho, Wewe kama mwamini, unapomsingizia ndugu yako, Maana yake unakwenda kinyume na sheria ya Kristo tuliyopewa ya kupendana, unapomhukumu ndugu yako unakwenda kinyume na sheria ya Kristo inayosema Usikuhukumu (Mathayo 7:1).
Hivyo unaihukumu hiyo sheria kwamba ina makosa, wakati Bwana aliiona ni bora, lakini wewe unakwenda kinyume na hiyo.
Hivyo sisi kama wana wa Mungu hatujaitwa tuwashutumu watu, tutafute kasoro ndani ya ndugu zetu, kana kwamba sisi, hatuna maboriti kwenye macho yetu, ila tumeitwa tuitende sheria, na kuonyana, na kuelekezana, na kujengana, katika upendo, lakini sio kutoa hukumu kwa wengine, kana kwamba sisi ni mahakimu.
Tumeagizwa tunapomwona ndugu yetu ameghafilika tumrejeshe kwa upendo, sio kwa mashutumu, hiyo ndio sheria ya Kristo.
Wagalatia 6:1 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
2 Mchukuliane mizigo na KUITIMIZA HIVYO SHERIA YA KRISTO. 3 Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.
Je Yesu ni Mungu au Nabii?
MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?
JE! UMEYABATILISHA MAMBO YA KITOTO?
SWALI: Naomba kufahamu maana ya unabii unaozungumzia taifa la Tiro (Isaya 23). Kwamba litafanya ukahaba na falme zote ulimwenguni kisha utajiri wake utakuwa wakfu kwa Bwana. Tafsiri yake ni nini?
Isaya 23:17-18 inasema..
[17]Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. 18 Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.
[17]Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.
18 Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.
JIBU: Ukianza kusoma toka mstari wa kwanza wa hiyo sura ya ishirini na tatu (23), utaona Mungu anazungumzia adhabu, aliyoitoa kwa hilo taifa la Tiro lililokuwa na utajiri na mali nyingi kutokana na biashara zake lilizofanya na dunia nzima. Hata kuyakosesha na mataifa mengine, kwa bidhaa zake. Na jambo hilo Mungu akalihesabu kama ni ukahaba, hivyo akalipiga na kuliangusha kabisa likawa si kitu tena kwa muda wa miaka sabini(70).
Ni mfano tu, mataifa yanayokosesha ulimwengu sasa, kwa kuuza bidhaa ambazo ni machukizo kwa Mungu, utakuta taifa linazalisha nguo za mitindo ya nusu uchi, na kuyauzia mataifa mengine, au linatengeneza sinema zenye maudhui za kizinzi na kuyasambazia mataifa mengine yaliyokuwa na maadili.. Huo ndio mfano wa ukahaba ambao taifa la Tiro lilikuwa linafanya.
Isaya 23:15
[15]Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba.
Lakini baadaye Mungu alilirudia tena, na kuruhusu lifanikiwe, kama pale mwanzo. Likajikusanyia tena utajiri mwingi sana kwa biashara zake.. Lakini Kwasababu halikutubu, kitabia Mungu akalipiga kwa namna nyingine kwa kuzuia utajiri wao wasiule au kwa lugha nyingine hazina zao zisitunzwe kwa maendeleo yao, Bali Bwana atazizuia zije kutumika kwa kazi yake yeye mwenyewe na watu wake.
Na unabii huo ulikuja kutimia..
ndio maana ya huo mstari wa 18, unaosema..
[18]Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.
Hii ni kufunua nini?
Kufanikiwa kwake mwovu, kunatimiza makusudi mawili la kwanza ni aidha kwenda kujiangamiza mwenyewe (Mithali 1:32, Zab 92:7), au kumkusanyia mtu mwingine mwenye haki.
biblia inasema..
Mithali 28:8
[8]Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
Watu wengi wanaofanikiwa isivyo halali,mara nyingi mali zao, hula wengine..Ndicho alichokifanya Mungu kwa taifa la Tiro.
Ni kutufundisha pia fedha na dhahabu ni mali ya Bwana. Yeye ana uwezo wa kuzuia na kuachilia, anauwezo wa kuwapa watu wake hazina za gizani ambazo hawajazisumbukia, kwa ajili ya kazi yake.
Hivyo kumbuka Bwana akufanikishapo, tembea na Kristo, kinyume na hapo, mambo hayo mawili yanaweza kukukuta, aidha mafanikio hayo yazidi kukuangamiza ufe uende kuzimu, au yaliwe na watu wengine kabisa wema usiowajua na kazi yako ikawa bure.
Shalom.
Masomo mengine:
Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa?
Kwanini Herode aliwakasirikia watu wa Tiro na Sidoni? (Matendo 12:20)
Je ni halali kwa mkristo kufanya biashara ya Forex?
Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”.
Je unaelewa maana ya kukaa ndani ya YESU (kuwepo ndani ya YESU) ??kwasababu ipo tofauti ya Bwana YESU kukaa ndani yako, na wewe kukaa ndani yake.
Kukaa ndani si Kumpa YESU maisha yako!!!…Ni zaidi ya hapo!.
Je ulishawahi kusikia mtu akisema “fulani nimemtoa ndani yangu kabisa au moyoni”..??
Utakuwa unaelewa maana ya hiyo kauli kwamba huenda katendewa kitendo kibaya sana, au cha kuumiza au kudhalilisha…ikasababisha kumtoa huyo mru moyoni kabisa.
Vile vile kuna mtu utamsikia akisema “mtu fulani yupo sana moyoni mwangu”…
Maana yake mpaka kusema hivyo huenda huyo mtu kamfanyia jambo jema sana au la kugusa moyo wake, au la kumvutia, mpaka kufanya aingie moyoni mwake.
Na Bwana YESU ni hivyo hivyo, kuna watu wapo ndani yake (moyoni mwake)..na kuna watu hawapo kabisa moyoni mwake ijapokuwa wanaweza kukiri wanaye…
Kwanini?..
Jibu: Kwasababu hawajawahi kuugusa moyo wa Bwana hata kumfanya Bwana awaweke moyoni mwake..watu hawa kibiblia hawapo ndani ya YESU na Kristo ingawa wanaweza kukiri kwamba wanaye Kristo moyoni, na Bwana atawakana siku ile kwamba hawajui.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Yafuatayo ni mambo (Matendo) ambayo mtu anaweza kuyafanya yakaugusa moyo wa Bwana YESU , hata kumfanya mtu huyo awe ndani ya KRISTO (moyoni mwake).
Hili ni jambo la kwanza linalomzamisha mtu kwenye moyo wa KRISTO.
Yohana 6:56 “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. 57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi”.
Yohana 6:56 “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.
57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi”.
Kamwe usiidharau meza ya Bwana, lakini pia hakikisha unashiriki kulingana na Neno lake..Kwa kufanya hivyo utauteka moyo wa Bwana kwa kiwango kikubwa sana.
2.UMOJA.
Hili ni jambo la pili linalouteka moyo wa Bwana sana na kumzamisha mtu ndani ya moyo wake.
Yohana 17:21 “Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”.
Yohana 17:21 “Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”.
Hivyo jenga sana desturi ya kutafuta Umoja wa Roho, usipende kukaa peke yako peke yako (huendi kanisani, hushirikiani na wengine..ni hatari kubwa sana).
3. MATOLEO.
Kumtolea Mungu kwa hiari pasipo kulazimishwa wala kushinikizwa, ni kitendo cha tatu kinachougusa sana Moyo wa Bwana (hauwezi kutoka moyoni mwake daima).
Mathayo 26:12 “Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hiyo, ametenda hivyo ili kuniweka tayari kwa maziko yangu. 13 Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake”.
Mathayo 26:12 “Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hiyo, ametenda hivyo ili kuniweka tayari kwa maziko yangu.
13 Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake”.
Huyu mwanamke amekuwa ndani ya moyp wa Kristo kwa vizazi vyote, mpaka sasa tunavyozungumza.
Usikwepe matoleo (sadaka) shetani amevuruga sana eneo hili la matoleo kwasababu anajua endapo mtu akipata ufunuo mkamilifu basi ataingia ndani ya Kristo moja kwa moja.
Unyenyekevu ni wa kukiri makosa, na kurudi kitubu na kuyokurudia rudia machafu, ni tendo kubwa sana linamwingiza mtu ndani ya YESU.
Luka 23:40 “Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? 41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. 42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. 43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”
Luka 23:40 “Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?
41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.
42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”
Na yapo mambo mengine mengi katika maandiko yanayomwingiza mtu na kumdumisha ndani ya KRISTO.
Zifuatazo ni faida za kuwa ndani ya KRISTO.
Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”
2.Tunakuwa viumbe vipya.
2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya”.
Hasara za kutokuwa ndani ya KRISTO ni kinyume cha faida hizo.
Bwana atusaidie tuingie na kudumu ndani yake.
NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!
USIWE MKRISTO WA KUKAA TU GHALANI,
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.