Huu ni waraka wa Pili ambao mtume Paulo aliuandika kwa mwanae Timotheo akiwa kama mfungwa kule Rumi (2Timotheo 1:17)
Ni waraka wa Kitume zaidi, akimweleza Timotheo mambo mengi anayopaswa ayafanya, na ayaelewe kuhusiana na kazi ya Mungu.
Maudhui makuu ya Paulo yalikuwa ni haya;.
Haya ni maelezo mafupi katika maeneo hayo makuu:
> Paulo Anaanza kwa kumtaka Timotheo aichochee karama iliyo ndani yake, aliyoipokea kwa kuwekewa mikono na yeye. Akionyesha kuwa huduma ni kama moto ambao ili kuufanya uendelee kuwaka inahitaji wakati wote uchochewe.(2Timotheo 1:6-8)
> Anamsihi kama askari mwema, ajikite katika kazi moja ya injili, Asipeleke fikra zake katika shughuli za kidunia, akimtaka afahamu hilo ili aweze kuvipiga vita vizuri vya imani, bila kuvutwa na mambo mengi.
2 Timotheo 2:3-7
[3]Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.
[4]Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
[5]Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali.
[6]Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda.
[7]Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.
> Anamtaka pia ajionyeshe Kuwa amekubaliwa na Mungu, Mtu awezaye kuligawanya Neno la Mungu vema, (2:15)
> Azikimbie tamaa za ujanani (2:22)
> Awe tayari kuhubiri injili Wakati wote ufaao na usiofaa.(4:1-2)
> Awe na kiasi katika mambo yote, avumilie mabaya, atimize huduma yake. (4:5)
> Akumbuke pia akikubali kuishi maisha ya utauwa ataudhiwa.(3:12)
Paulo anatoa habari za tabia alizokutana nazo kwa baadhi wa wahudumu wenza,
makundi hayo ni kama yafuatayo;
> Walioshirika na yeye nyakati zote kwa uaminifu, mfano wa hawa ni Onesiforo na watu wa nyumbani mwake, pamoja na Luka(1:16).
> Waliotengana naye kwasababu njema za mtawanyiko wa kihuduma mfano wa hawa ni Kreste na Tito,(4:9b)
> Lakini wapo ambao walimwacha kwa kupenda dunia mfano wa hawa ni Dema.(4:9)
> Na wengine kwa kujiingiza kwenye mafundisho ya uongo mfano wa hawa ni Himenayo na Fileto.(2:17-18)
> Na wengine walifanyika kabisa wapinzani wake. Mfano wa hawa ni Iskanda mfua shaba.(4:14)
Lengo la Paulo kumjuza juu ya watu hawa ni kumtaka ajifunze kuvumilia, na pia kujiepusha nao hususani wale wapingamizi, na kuweka misingi ya kimafundisho kwa kuwatahadharisha watu wasiyafuatishe mafundisho mengine, kwani makundi hayo atakutana nayo, na yatakuwepo.
Paulo anampasha habari Timotheo uhalisia juu ya nyakati za mwisho, ambazo tangu wakati ule zilikuwa tayari zimeshaanza..
2 Timotheo 3:1-5
[1]Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
[2]Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
[3]wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
[4]wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
[5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
makusudi yake ni kumtaka avumilie, na kusimama imara katika huduma, kwasababu nyakati ngumu atakutana nazo za watu wengi kujiepusha na mafundisho ya uzima.
Anasema pia kutazuka wimbi la waalimu wa uongo, wapinzani wa injili mfano wa Yane na Yambre, ambao watashindana na kweli, (3:8-9).
Hatua za kuchua:
> Adumu katika mafundisho na mwenendo wote alioupokea kwake (3:10, 14)
> Awakabidhi wengine mapokeo hayo. .(2:1)
> Ajiepushe na mashindano ya kidini, na maneno yasiyokuwa na maana (2:16, 23-26)
Mwisho.
Paulo anaeleza mwisho wake, na sababu ya kuvipiga vita vema na kusimama imara katika Imani, ni kwasababu aliiona ile taji ya haki aliyowekewa Na Mungu mbinguni. Akitumai na Timotheo atasukumwa kuvipiga vita vema kwa kuiona thawabu hiyo hiyo aliyowekewa mbinguni.
2 Timotheo 4:6-8
[6]Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
[7]Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
[8]baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Uchambuzi wa kitabu cha kwanza cha Paulo kwa Timotheo (1Timotheo)
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Yeremia alikuwa na umri gani alipoitwa?
Mithali 27:19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
JIBU: Anaanza kwa kutoa mfano halisi, ili kueleza vema jambo la kitabia. Anasema kama vile maji yanavyoweza kuwa kioo kiakisicho, vivyo hivyo mioyo ya watu walio pamoja.
Kama tunavyojua ukiyatazama maji, utauona uso wako vilevile kama ulivyoyatazama, wala hayawezi kudanganya, ukiyaangalia umekunja sura, utaonekana hivyo hivyo, ukiyaangalia umevaa kofia, utajiona hivyo hivyo.
Ndivyo Mungu anavyowaona watu wawili waliojiungamanisha katika kitu kimmoja,(urafiki), tabia ya mmoja itamwakisi mwingine, mwisho wa siku watafanana tu na kuwa na mwenendo sawa. Akiwa mmoja ni mwizi, Yule mwingine atakuwa kama yeye tu, akiwa mmoja ni mwamini mwombaji Yule mwenzake atakuwa naye mwombaji, akiwa ni mkarimu, mwenzake naye atakuwa hivyo hivyo.
Ndio sababu biblia inasema wawili hawawezi kukaa pamoja isipokuwa wamepatana (Amosi 3:3). Hivyo vifungu hivi vinatukumbusha umuhimu wa kuchagua watu sahihi wa kuambatana nao, imesisitiza tusifungwe nira ya watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwasababu kwa njia hiyo watatuambukiza tabia zao.
Hata katika kuoa/kuolewa, ikiwa umeokoka, tafuta wa kufanana na wewe, au mbadilishe kwanza awe kama wewe ndio umwoe/uolewe naye vinginevyo, unajiandaa kugeuzwa tabia kama ilivyokuwa kwa Sulemani kuoa wake wa kimataifa.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NI UTUKUFU WA MUNGU KUFICHA JAMBO.
Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri.
Amali, na kila kazi ya ustadi, inatokana na mtu kupingana na mwenzake.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
SWALI: Kwanini sehemu kadha wa kadha wana wa Israeli walipoonekana wanakwenda kinyume na Torati hutumia kauli ya
“atakatiliwa mbali na watu wake”. Nini maana ya hii kauli?
Mambo ya Walawi 7:27
[27]Mtu ye yote alaye damu, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.
JIBU: Ni kauli ya ujumla inayomaanisha huyo mtu atatengwa na kusanyiko la Israeli. Kutengwa huko kunaweza kuwa Kwa namna mbalimbali kutegemeana na aina ya kosa.
Hizi ndio aina kuu tatu za kukatiliwa mbali
Kifo kilihusika katika baadhi ya hukumu, ambazo Nyingine ni Mungu mwenyewe aliyezitekeleza (Walawi 20:3-6). Na nyingine Wanadamu. Kwamfano mtu yeyote aliyefumaniwa katika uzinzi, adhabu yake ilikuwa ni kupigwa Mawe Mpaka kufa.
Vivyo hivyo katika kuihalifu sabato, adhabu ilikuwa ni hiyo soma;
Kutoka 31:14
[14]Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.
Hii nayo ilikuwa ni aina nyingine ya kukatiliwa mbali, ambapo ulifutwa katika hesabu ya waisraeli, inayokufanya kupoteza haki ya kushiriki Ibada yoyote katika makusanyiko, au vipaumbele.
Hesabu 19:20
[20]Lakini mtu atakayekuwa najisi, naye hataki kujitakasa, mtu huyo atakatiliwa mbali katika mkutano, kwa sababu amepatia unajisi mahali patakatifu pa BWANA; hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake; yeye yu najisi.
Maana yake ni kuwa hauwi mshirika tena wa baraka za maagano ya Mungu, kama vile ulinzi na ahadi.
Mwanzo 17:14
[14]Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.
Hata leo, katika agano jipya mambo mambo tunaweza kufanya yakatusababishia kukatiliwa mbali na rehema za Mungu.
Na adhabu hizo zinaweza kutekelezwa na wanadamu(watakatifu), na nyingine Mungu mwenyewe.
Kwamfano Biblia inatoa ruhusu kanisa kumtenga mtu ambaye anazoelea dhambi, (1Wakorintho 5:1-5)
Mungu mwenyewe anaweza kutekeleza hukumu hiyo, kwamfano tunaweza kuona kwa Anania na Safira, ambao walitumia njia ya hila katika mapatano ya Roho.(Matendo 5:1-11). Lakini pia kwa mtu ambaye anakusudia kuurudia ulimwengu baada ya kuipokea neema, hukumu kama hii huweza kumkuta. (Waebrania 10:26-27)
Kwahiyo jambo hili halikuwa tu kwa wana wa Israeli, lakini lipo hata sasa rohoni. Tusiwe watu wa kuzoelea dhambi tukidhani kuwa wakati wote Mungu ataturehemu. Usidanganyike ukishakatiliwa mbali si rahisi tena kumgeukia Mungu wako.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Tofauti kati ya makuhani na walawi ni ipi?
Maana ya Mithali 25:25 Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu
ALIPOKUWA ANGALI MBALI, BABA YAKE ALIMWONA.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Tofauti na nyaraka nyingi za mtume Paulo, ambazo aliziandika kwa Makanisa, waraka huu aliuelekeza kwa Timotheo ambaye alisimama sio tu kama msaidizi wake wa kihuduma bali pia kama mwanae Katika vifungo vya injili. Ni waraka wa kichungaji zaidi ya wa kimafundisho,
Katika waraka huu Paulo anamwagiza Timotheo namna ambavyo kanisa linapaswa likae katika utaratibu, Mungu alioukusudia.(1Timotheo 3:15)
Maudhui makuu ya Paulo kwa Timotheo yalikuwa ni haya;
Haya ni maelezo mafupi Kwa kila kipengele.
Paulo anamhiza Timotheo lengo kubwa la kumtaka abaki Efeso ni ili awazuie watu wasifundishe elimu nyingine.
1 Timotheo 1:3
[3]Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine;
Elimu hiyo potofu aliyoina iliegemea kuwazuia watu wasile aina ya vyakula, Wasioe, pamoja na kuhubiriwa Hadithi za kizee, na nasaba (1:4, 4:7)
Kwa urefu wa mafundisho Hayo bofya hapa >>> HADITHI ZA KIZEE.
1 Timotheo 4:1-3
[1]Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
[2]kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
[3]wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
Kwa wanaume: Paulo anatoa agizo la kwamba wao wanajukumu la kusalisha kila mahali, lakini bila hasira wala majadiliano, yaani wawe safi kiibada (2:8)
Kwa Wanawake: Paulo anatoa agizo kuwa hawana ruhusa ya kufundisha katika kanisa (2:12), halikadhalika wanawajibu wa kuvaa mavazi ya kujisitiri, mapambo yao yawe yale ya rohoni na sio ya mwilini (2:9-10).
Anaendelea kusema Wanawake ambao ni wajane waandikwe katika kanisa ili Wahudumiwe kimahitaji, lakini wale ambao si wajane kwelikweli hawapaswi kuandikwa (5:4-16)
Wazee, na vijana wafanyapo makosa wasikemewe, Bali Waonywe kwa upole Kulingana na marika yao(5:1), lakini pale wafanyapo dhambi. kwa kukusudia au kuzoelea wakemewe mbele ya wote. (5:20),
Watumwa wote wanawajibu wa kuwaheshimu mabwana zao, si tu kwa wale wasiamini bali pia kwa wale waaminio wawaheshimu wote. (6:1)
Kanisa lina wajibu wa kuwaombea watu wote, na watawala, ili liishi katika utulivu, na amani, katika utauwa wote.(2:1-4)
Sehemu hii Paulo anamwagiza Timotheo juu ya vigezo vya maaskofu, na Mashemasi namna wanavyopaswa wawe, kwamba wawe watu wasio laumika, wameshuhudiwa mema na watu wa nje, waume wa wake mmoja mmoja, si watu wa kupenda fedha,si walevi, si waongofu wapya, wanapaswa wawe wakaribishaji,, wastahivu, wenye kiasi, waaminifu, wawasimamiao watoto wao vema, na wake zao, (3:1-13).
Lakini pia anawahimiza wazee wanaotawala vema wahesabiwe kuwa wamestahili heshima mara dufu (5:17).
Paulo anamwagiza Timotheo wajibu wake kama mwangalizi kuwa na upendo, Imani isiyo na unafki, na dhamiri njema, upole, saburi, na haki (1:5, 18-20, 6:11),
Anamwagiza afanye mambo yote bila upendeleo (1Timotheo 5:21).
Ajizoeshe kupata utauwa (4:8).
Awe kielelezo katika usemi na mwenendo (4:12)
Asiwaekee watu mikono kwa haraka,(5:22)
Akimbie tamaa ya fedha, na mashindano ya kidini (6:20).
Hitimisho.
Hivyo kwa ufupi, waraka huu ni wa kikanisa zaidi, na kwamba vigizo hivyo vikisimamiwa vema kanisa litakuwa imara, lenye heshima lisiloshitakiwa mabaya nje.
Ikiwa viongozi watachaguliwa hodari, na kila rika na jinsia likahudumu katika nafasi yake, yaani wanawake Kudumu katika upole, kujisitiri na kiasi na wanaume kuhudumu bila hasira wala majadiliano, huku waangalizi wakihakikisha mafundisho potofu hayapati nafasi. Ni ukweli kwamba kanisa hilo litakuwa imara sana.
Bwana akubariki
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mada nyingine:
Nasaba ni nini kibiblia?(1Nyakati 9:1, Tito 3:9)
Timotheo alikuwa wapi wakati anaandikiwa nyaraka zake na mtume Paulo?
Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)
JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE
Fahamu kanuni muhimu ya kufungua milango ya Baraka za rohoni na mwilini.
Neno la MUNGU linasema..
Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ALIYETUBARIKI KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI, KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, NDANI YAKE KRISTO”.
Ni lini tulibarikiwa na baraka zote za rohoni?..Je ni jana au leo??.. Nataka nikuambie kuwa si jana, wala juzi wala mwaka uliopita wala si siku ile ulipozaliwa…. bali ni tangu siku ile damu ya Mwokozi YESU ilipomwagika msalabani tayari tulishabarikiwa,
Na si kubarikiwa tu, bali pia tayari tulishaponywa tangu siku ile Kristo aliposulibiwa, tayari tulishashinda tangu siku ile Kristo aliposulibiwa..
Sasa swali ni hili, kama tayari Baraka na ushindi tulishapewa tangu siku ile ya pale Kalvari, kwanini sasa hatuzioni hizo Baraka zetu katika roho na katika mwili?
Hili ndilo swali la msingi kujiuliza.. kwanini hatuzioni hizo Baraka tulizobarikiwa miaka mingi iliyopita.
Sababu kuu ya sisi kutoshiriki Baraka zote za rohoni ambazo tayari zilishaachiliwa juu yetu, miaka elfu mbili (2) iliyopita pale Kalvari ni “shetani”.
Anachokifanya adui ni kuzuia kupokea zile Baraka, na si kuzuia zisitoke!.. Tayari Mungu alishatubariki..wala hatuwezi kumwomba tena atubariki, ni sisi kupambania kilicho chetu.
Sasa ili tuweze kupokea kilicho chetu, ni lazima tupambane vita, na vita hivyo ni vile vya kiroho, kwani shetani na majeshi yake yamesimama kuhakikisha hatupokei kilicho chetu.. shetani hamzii MUNGU kutoa, bali anatuzuia sisi kupokea… Na MUNGU tayari alishatoa, ila shetani anazuia tusipokee..
Ni sawa na mzazi aliyemtumia mwanae aliyeko shuleni fedha za matumizi kupitia anwani ya shule, halafu mwalimu mmoja azifiche zile fedha zisimfikie mtoto, hapo mtoto mwenye busara akishajua katumiwa fedha ana wajibu wa kuzifuatilia, na kuulizia na kama kuna shida kwa mwalimu, na kama akiona kuna shida basi aweza kushitaki ili tatizo litatuke, kwasababu atajua shida si mzazi bali ni mwalimu (sasa huu ni mfano tu).
Na mambo ya rohoni ni hivyo hivyo, BWANA MUNGU wetu alishatubariki kwa Baraka zote za rohoni.. kazi tuliyobakiwa nayo ni kushughulika na vizuizi vya sisi kupokea hizo Baraka.
Na silaha zifuatazo ndizo zinazoweza kuvunja vizuizi vyote na kuachia kilicho chetu.
1. MAOMBI
Maombi (hususani yanayohusisha mfungo) ni silaha ya kwanza ya kuzipinga hila za adui zinazozuia Baraka zetu.. Mtu aliyejizoeza kuomba ni rahisi kupokea Baraka zote zilizoahidiwa na MUNGU, na mtu anayepungukiwa maombi ni kinyume chake.
2. KUSOMA NENO.
Maombi bila Neno la Mungu ni sawa na bendera iliyokosa mlingoti… Mtu aombaye huku Neno la Mungu limejaa ndani yake, ni rahisi sana kuteka Baraka zake tofauti na yule asiyekuwa msomaji wa NENO, na kusoma Neno kunakozungumziwa hapa si kushika vifungu vya biblia, La!.. Unaweza kuwa umeshika vifungu elfu vya biblia na bado usiwe umelijua Neno.
Bali kusoma Neno kunakozungumziwa hapa ni kule kujifunza kitabu baada ya kitabu na kujua maudhui ya kila kitabu katika ufunuo wa Roho.
3. UTAKATIFU
Utakatifu wa mwilini na rohoni ni mkuki wa kumpiga yule mwovu aachie vinavyotuhusu.. kinyume chake uchafu na maisha ya dhambi ni kifungo kinachozuia Baraka zetu.
Sasa utauliza Baraka za rohoni na mwilini ni zipi?
Mfano wa Baraka za rohoni ni Amani, furaha, upendo, uvumilivu, upole, utu wema na mambo mengine yote mema yanayofanana na hayo, kwa ufupi ni Roho Mtakatifu na matunda yake (Wagalatia 5:22).
Na baraka za mwilini hamna haja ya kuziandika maana zinajulikana, ambazo ni zile zote zinazohusu mahitaji ya mwilini.
Je umepungukiwa na Baraka?…fahamu kuwa Maombi, Neno na Utakatifu ndio dawa ya kutibu hilo tatizo, wala usimnung’unikie MUNGU kwanini hakubariki.. yeye tayari alishatubariki, ni sisi kupambana kupata vilivyo vyetu..Anza mapambano hayo kuanzia sasa ikiwa tayari umeshampokea Bwana YESU.
Na kumbuka mapambano haya hamna siku yatapoa, hata baada ya kuwa mtumishi.. ni jambo endelevu daima mpaka safari ya maisha inaisha, kwani pia kuna kupokonywa na yule aliyetuzuia tusipokee, ikiwa hatutasimama katika mambo hayo makuu matatu, na mengine yanayofanana na hayo.
Hivyo ukristo ni mapambano, ni vita, lakini vyenye nafasi kubwa ya kushinda Zaidi ya kushindwa kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Warumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote TUNASHINDA, NA ZAIDI YA KUSHINDA, kwa yeye aliyetupenda”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.
MILANGO YA KUZIMU.
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
CHAKULA CHA ROHONI.
MILANGO YA KUZIMU.
SWALI: Je! watu wanapaswa wakemewe au wasikemewe pale wanapofanya dhambi kulingana na 1Timotheo 5:1 na 20?
JIBU: Tusome,
1 Timotheo 5:1-2
[1]Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;
[2]wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.
Na,
1 Timotheo 5:20
[20]Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.
Mwandishi anatoa maelezo katika mazingira mawili tofauti. Mazingira ya kwanza ni katika eneo la marekebisho na mazingira ya pili ni katika eneo la makosa ya makusudi.
Kwamfano katika vifungu hivyo vya kwanza, anavyosema Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;analenga hasaa katika makosa ambayo yanajitokeza katikati ya huduma au maisha ya kikristo, kwamfano pengine mtu katika kuhudumu kwake kaonyesha uvunjifu fulani wa nidhani ya kimadhabahu, au kasema lugha isiyo ya staha, au kavaa vazi lisilo na heshima, au kabagua wengine, au kawadhulumu wengine, n.k. ambayo imesababishwa na uchanga wa kiroho au madhaifu ya kibinadamu.
Katika mazingira kama hayo Paulo anamhimiza Timotheo, kulingana na marika yao asitumie kukemea bali awaeleze kwa upole, nao watajirekebisha, akitambua kuwa wapo katika hatua za kuutafuta ukamilifu.
Lakini katika hivyo vifungu vya pili. Analenga Zaidi kwa wale wanaodumu kutenda dhambi. Wanaojua kabisa wanachokifanya sio sahihi, lakini wanaendelea kudumu kufanya hivyo, Paulo anasema hawapaswi kuvumiliwa bali kukemewa mbele ya watu wote.
Kwamfano mtu ni mzinzi, na tabia hiyo anaendelea nayo kanisani, au ni mlevi, au mchonganishi, sasa hawa wanapaswa wakemewe hadharani bila kujali marika yao, ili wengine wasiige Tabia hizo. Kwasababu wakiachwa wataendelea kulichachusha kanisa.
Makanisa mengi leo hii yamekumbwa na matatizo makubwa mpaka kusababisha jina la Kristo kutukanwa Nje, ni kutokana na kuvumiliwa kwa watu wa namna hii wanaodumu katika kutenda dhambi.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kuna hukumu za aina ngapi?
Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).
USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE.
Swali: Madongoa kama inavyosomeka katika Ayubu 7:5, ni kitu gani, na ina ujumbe gani kiroho?.
Jibu: Turejee..
Ayubu 7:5 “Mwili wangu unavikwa mabuu na MADONGOA YA UDONGO; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena”.
Madongoa ni udongo ulioshikamana pamoja, sawasawa na Ayubu 38:38..
Ayubu 38:38 “Wakati mavumbi yagandamanapo, Na madongoa kushikamana pamoja?”
Kikawaida ardhi yenye Madongoa haifai kwa kilimo, bali mpaka madongoa hayo yatakapovunjwa na kulainishwa, ndipo mbegu ziweze kupandwa…
Isaya 29:23 “Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu.
24 Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima MADONGOA YA NCHI YAKE, na kuyavunja?
25 Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huko na huko kunde, na kutupa-tupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake?
26 Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha”.
Neno hili pia tunaweza kulisoma katika kile kitabu cha Hosea 10:11..
Ni ni nini tunachoweza kujifunza??
Kama vile ardhi yenye madongo ilivyokuwa ngumu kwa kilimo, hali kadhalika mioyo yetu inafananishwa na shamba sawasawa na ule mfano wa Mpanzi (Mathayo 13:18-23), na kama mioyo yetu ni migumu kwa namna hiyo basi ni ngumu pia kumzalia MUNGU matunda.
Mfano wa moyo wenye madongoa ni ule ulio mgumu kusikia Neno, mtu mwenye moyo wa kupuuzia, na kutokujali pale asikiapo Neno la MUNGU, mtu wa namna hii anahitaji sana kusaidiwa.
Je ni wewe mtu huyo?. Kama ndio basi mkimbilie YESU leo kwa kumaanisha kabisa naye ataufanya maoyo wako kuwa mlaini, na utayaona matunda ya BWANA.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Tufanyaje ili tuonekane tunampenda Mungu?
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?