Shalom, mtu wa Mungu, Biblia inasema mtu hataishi kwa mkate tuu, bali kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Bwana, hivyo pale tunapojifunza Neno la Mungu kwa dhati tuwe na uhakika kuwa Roho zetu zinanenepa na hivyo kujiongezea siku za kuishi hapa duniani (1Wafalme 3:14)..
Tukisoma kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza tunaona jinsi Bwana alivyofanya kazi yake ya kuumba ulimwengu kwa siku 6, na ilipofika siku ya 7 aliacha kazi zake zote akastarehe, tena akaibariki siku hiyo kuonyesha kuwa kila kitu kimekamilika, Vile vile ukisoma sura ya pili utaona jinsi Bwana anavyompa Adamu maagizo ya kuishi katika bustani ile, akamletea na Wanyama wote awape majina, naye akafanya hivyo, basi Maisha ya Adamu na viumbe vyake vyote yakaendelea hivyo siku zinakuja siku zinakwenda..
Lakini kilipita kipindi Mungu akamtazama Adamu akasema neno hili “SI VEMA”..Tunasoma hilo katika..
Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”
Embu jaribu kufikiria mtu akisema Neno “si vema” anaashiria nini?, Ni wazi kuwa atakuwa ameona mapungufu, na hivyo anahitaji kufanya marekebisho fulani ili mambo yaende kama anavyotaka..
Ndivyo ilivyokuwa kwa Mungu, japo alikuwa tayari ameshamuumba mwanamke katika mawazo yake tangu siku nyingi, ukisoma Mwanzo 1:27-28 utalithibitisha hilo, Mwanamke alikuwa tayari kashaumbwa kabla hata ya uumbaji wenyewe kuanza, lakini Mungu aliruhusu kwa makusudi kabisa asitokee katika uumbaji ule wa mwanzo alipokuwa anamuumba Adamu na viumbe vyake vyote, kana kwamba alisahau hivi, ili tu alitumie hili neno SI VEMA, kutufundisha sisi jambo..
Mwanamke alikuja kuumba baadaye kabisa, Maisha yameshaendelea edeni kwa kipindi fulani pengine cha mwaka 1 au 10 au 100 hatujui, lakini mwanamke siku alipokuja kuumbwa, uumbaji ulikuwa umeshamalizika siku nyingi sana huko nyuma.
Kwanini Mungu alifanya hivyo? ni kwasababu alikuwa anatufundisha kuwa yeye anapendezwa na marekebisho, embu jaribu kufikiria marekebisho yake yake jinsi yalivyo na manufaa makubwa kwetu sisi leo hii, jaribu kuwazi hii dunia mfano isingekuwa na wanawake tungeishije ishije huku duniani, mfano usingeupata upendo wa mama leo hii wewe ungekuwaje, usingeupata upendo wa dada leo hii wewe ungekuwaje, usingeuonja upendo wa mke leo hii wewe mwanamume ungekuwa mtu wa namna gani? N.k, hakuna mnyama yeyote au kiumbe chochote kingeweza kukupa faraja duniani kama sio mwanamke..
Tunamshukuru Mungu kwa kutupa zawadi hii, lakini hiyo yote ni kutokana na marekebisho, kama Mungu angesema mimi nimeshamaliza uumbaji wangu, na siku ya 7 nimeshastarehe, hichi tunachokiona leo hii kisingekuwepo?.
Vivyo hivyo na sisi Mungu anatarajia tuwe tunafanya marekebisho katika ukristo wetu, katika huduma zetu za kuujenga ufalme wa mbinguni, tusione haya kusema SI VEMA…Mungu asiyeweza kukosea alisema hivyo wewe kwanini uone kila kitu kipo vyema?. Kwanini uridhike na ukristo ule ule ambao ulikuwa nao miaka 10 iliyopita, hadi leo unaendelea nao, na huku unaona kabisa unayo mapungufu mengi ndani yako ya kufanyiwa marekebisho?
Kazi ya Mungu inalala, miundo mbinu ya kanisa kila siku inaporomoka, kwanini usiseme SI VEMA hichi kiwe vile, au kile kiwe vile? Natoa mchango wangu wa fedha, au nguvu zangu kupakarabati hapa, au akili uzoefu wangu kufanikisha kile…Mungu anata tuwe hivyo..Unajuaje kuwa hicho unachokirekebisha kitakuwa na manufaa makubwa ya kuleta maelfu wa watu wa Kristo, kama vile mwanamke alivyo na manufaa makubwa sana leo hii kuleta roho nyingi za watu duniani?.
Ukiona umeokoka na muda mrefu upo vilevile, huongezi kiwango chako cha kusali huongezi kiwango chako cha kuwapelekea wengine injili, huongezi kiwango chako cha kufunga, basi ujue umeshatoka nje ya kusudi la Mungu alilotaka wewe uliendee…Tunapaswa tukue toka Imani, hadi Imani, toka utukufu hadi utukufu,..lakini tukiona kila kitu kipo sawa tu ndani yetu, tumeridhika basi tunajidanganya wenyewe.
Ni maombi yangu mimi na wewe, tutaanza kujifunza kusema SI VEMA, Na kuanzia leo kwa msaada wa Bwana tutahakikisha tunaboresha Maisha yetu ya rohoni pamoja na hudumu za kuipeleka injili.
Amen.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine, kama umeona pia SI VEMA, ushiriki baraka hizi peke yako.
Mada Nyinginezo:
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
KUOTA UMEPOTEA.
JE KUJIUA NI DHAMBI?
Bwana Yesu alikuwa na wanafunzi wengi, lakini alikuwa na Mitume 12 tu! Matume hawa 12 wote walichaguliwa kwa ufunuo wa Roho, kwani tunasoma kwamba Bwana kabla ya kuwachagua mitume hao alikwenda kuomba kwanza, ndipo akafunuliwa majina ya mitume hao.
Lakini jambo la kushangaza kidogo ni kwamba miongoni mwa hao mitume 12, alikuwemo mtume mmoja wa Uongo, ambaye aliitwa Yuda Iskariote. Sasa swali linakuja? kwanini Roho Mtakatifu amchague Mtume wa Uongo katikati ya mitume wa ukweli?..Ukitafakari hilo kwa makini kama ni mtu wa kufikiri mambo litakuogopesha kidogo!..Roho Mtakatifu anawapaka mafuta mitume wa uongo na kuwatuma?..Maana Yuda naye alikuwa anatumwa kuhubiri na kutoa pepo kama mitume wengine wote..Na Bwana alimpenda tu kama alivyowapenda mitume wengine…Na bila shaka endapo watu wangemwuliza Bwana eti huyu Yuda naye ni mwanafunzi wako? Ni wazi kuwa angejibu ndio! Asingemkana kwasababu ni yeye ndiye aliyemchagua.
Na ni wazi kuwa mahali pa siri ambapo Bwana alikuwa anakaa, mahali ambapo haruhusu watu wengine kufika isipokuwa mitume wake tu angemruhusu Yuda..Kwahiyo kwa ufupi ni kwamba upendeleo wote ambao Mitume wa kweli walikuwa wanaupata Yuda naye alishiriki.
Na cha ajabu ni kwamba Yuda Iskariote mwenyewe ambaye ni mtume wa Uongo, hakuna aliyekuwa anamjua kuwa ni mtume wa uongo, isipokuwa Bwana Yesu tu peke yake! Hata mitume wenzake walikuwa hawajui!..Ndio maana utaona wakati Bwana anawaambia mmoja wao atamsaliti…wale mitume 11, walishindwa hata kumhisi kuwa ni Yuda, walijihisi ni wao, kila mmoja alijidhania ni yeye!…ikionesha ni jinsi gani Yuda ilikuwa ni ngumu kumgundua.
Marko 14:18 “Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja nami, atanisaliti.
19 Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia mmoja mmoja, Je! Ni mimi?”
Yohana 17:12 “Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie”.
Ni andiko gani hilo ili litimie? Ni hili:
Yohana 13:18 “Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, ALIYEKULA CHAKULA CHANGU AMENIINULIA KISIGINO CHAKE”.
Unabii huo uliandikwa katika kitabu cha Zaburi 41: 9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake”.
Yuda akamwinulia kisigino Bwana, akamsaliti kwa vipande 30 vya fedha…akasema
Mathayo 26:14 “Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani,
15 akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.”
Na Mitume hawa wauongo wapo katika hizi siku za mwisho ili kutimiza hili andiko ! Kazi yao ni kumgeuzia Bwana kisigino na kumwuza kwa vipande vya fedha!..wanawafuata watu na kuwaambia mna shilingi ngapi niwapatie Maji ya Upako?….kama Yuda alivyofanya..badala ya kwenda kuwahubiria wakuu wa makuhani watubu dhambi zao, na kumwamini Yesu, yeye anakwenda kuwahubiria injili ya kuwauzia Yesu..Mfano dhahiri wa mitume na manabii wa uongo wa leo…wanawahubiria watu injili za kumwuza Yesu, una shilingi ngapi nikutolee pepo, una shilingi ngapi nikupe maji ya upako, unashilingi ngapi nije kufanya maombi ya ufumbuzi nyumbani kwako n.k?
Ndugu, epuka injii ya Yuda Iskariote, ya mafanikio kila kukicha? Jiangalie tangu umeanza kutumia hayo maji, mafuta ni nini umenufaika katika roho yako?..Kama umeona yamekusaidia kuacha dhambi, kuacha usengenyaji, kuacha rushwa, kuacha wizi, kuacha matusi, kusamehe, kuacha uasherati basi yatumie lakini kama umeyatumia na hali yako ya kiroho ipo vile vile basi fahamu kuwa Umeuziwa Bwana Yesu kama Yuda alivyowauzia mafarisayo…na wewe umemnunua kwa dhumuni la kwenda kumsaliti na kumsulibisha mara ya pili kutokana na dhambi zako.
Ikiwa hujampa Yesu Kristo maisha yako na unataka kufanya hivyo bado hujachelewa, hapo ulipo, tubu kwa kudhamiria kuacha dhambi zako zote na kisha tafuta mahali ukabatizwe kama hujabatizwa, kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa kuzama mwili wote na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38, na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, na baada ya hapo hakikisha unadumu katika kujifunza Neno la Mungu, katika kusali, na kufanya ushirika na wakristo wengine kanisani, kama tulivyoagizwa katika Matendo 2:42
Shalom! jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Nifanyaje ili nijue kuwa uamuzi ninaokwenda kuchagua kufanya ni mapenzi ya Mungu?
Kuota umepotea mjini, au kuota umepotea shuleni, au kuota umepotea msituni, au kuota umepotea njia panda au kuota umepotea katika riadha au kuota umepotea sehemu usiyoijua, kwa vyovyote vile maadamu ni ndoto ya kupotea basi fahamu kuwa ndoto za namna hii mara nyingi zinatokana na Mungu.
Na huwa zinakuja kwa makundi yote ya watu, (Yaani wale walio ndani ya Kristo na wale walio nje ya Kristo).
Zaburi 37: 18 Bwana anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele.
19 Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba.
20 Bali WASIO HAKI WATAPOTEA, Nao wamchukiao Bwana watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
Unaona wasio haki sikuzote huwa wanapotea, hivyo kuota umepotea ni ujumbe ambao Mungu anakuonyesha hali yako ilivyo rohoni, na kama vile huko ndotoni unavyojiona unahangaika huku na kule kutafuta njia sahihi ya kufika mahali unapotaka kufika na unashindwa, unateseka sana huku na kule, unaonyeshwa kuwa kuna wakati utafika utautafuta huo wokovu ulioupoteza na hautauona milele…na kibaya zaidi wakati huo utakuwa umeshachelewa.
Zaburi 1:6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.
Mungu anakupenda na ndio maana anakuonyesha mambo kama hayo mapema ili utengeneze njia zako sasahivi, maadamu upo hai, maadamu imeitwa leo, Kesho inaweza isiwe yako, unaweza ukajiona upo sawa sasa katika Maisha yako, labda umejiendeleza, umefika mbali, una afya nzuri, umefanikiwa, unayo familia nzuri, lakini Mungu anakuambia umepotea, haijalishi upo katika mafanikio gani leo hii, Unachopasw kufanya ni ugeuke uombe msaada kwa Mungu naye atakuonyesha njia…na njia yenyewe ni YESU KRISTO.
Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.
Mathayo 18:10 “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
11 [Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea”.]
Kwahiyo ikiwa leo utakubali kutii na kumpa Maisha yako, basi atayaokoa na kukusamehe kabisa, ikiwa upo tayari sasa, hapo ulipo piga magoti kisha chukua dakika chache tafakari mambo yote maovu ulioyomfanyia Mungu, kisha kwa Imani, zungumza na Mungu, mwombe rehema,usimfiche chochote mwambie akusamehe maanisha kabisa kwasababu hapo ulipo anakusikia…Kisha ikiwa toba yako imetoka moyoni kwa dhati, na kwamba upo tayari kuacha yote ya nyuma uliyoyafanya basi fahamu kuwa Mungu amekusamehe, hivyo tu,
Ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na (Matendo 2:38) Ili ukamilishe wokovu wako uwe milki halali ya YESU KRISTO, ndipo Mungu akumwagie kipawa chake cha Roho Mtakatifu. Hivyo zingatia hayo maagizo yote ni muhimu sana kuyafanya, ikiwa hufahamu vizuri ni wapi utapata ubatizo sahihi, basi wasiliana na sisi kwa namba hizi 0789001312 au 0654555788.Tutakusaidia kutafuta maeneo karibu na wewe.
Vile vile ikiwa wewe tayari ulishaokoka, na ndoto kama hizi, kuota umepotea shuleni, au kuota umepotea msituni, au kuota umepotea njia panda au kuota umepotea katika riadha au kuota umepotea sehemu usiyoijua zinakujia, basi fahamu kuwa Mungu anakukumbusha kuwa, unakaribia kuiacha njia ya wokovu, aidha kuna uamuzi unaokwenda kuufanya ambao utakupotezea ramani yako ya wokovu moja kwa moja, au umeshaanza kuifanya..au kuna dhambi unaitenda ambayo haimpendezi Mungu sasahivi,Hivyo kuwa makini sana.. Shika sana ulicho nacho asiye mwovu akalitwaa taji lako.
Ezekieli 44: 9 Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli.
10 Lakini Walawi waliofarakana nami, hapo Waisraeli walipopotea, waliopotea na kuvifuata vinyago vyao, watachukua uovu wao wenyewe.
Kwahiyo jitazame, kumbuka Bwana alipokutoa, usimwache yeye..Mungu anakuonya kwa njia hiyo kwasababu anakupenda..Hivyo ukiona unalolijfanya sasahivi linakutenga na Mungu kama linakushinda nguvu ya kulitawala basi liweke kando mtafute muumba wako kwanza kwa usalama wa roho yako na hayo mengine yawe baadaye kama yatakuwa na umuhimu.
Ubarikiwe sana.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
NYOTA ZIPOTEAZO.
KUOTA UPO UCHI.
Kuota unafanya Mtihani.
KUOTA UNA MIMBA.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
Katika Biblia Injili ni nini maana yake?
Neno Injili limetokana na Neno la kigiriki “euaggelion” lenye maana ya “Habari Njema”. Hivyo Injili maana yake ni habari njema…Tukirudi katika biblia Injili maana yake ni “Habari Njema za Yesu Kristo”
Luka 2:8 “Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.
9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana“.
Habari yoyote inayomhusu Bwana Yesu Kristo, kuzaliwa kwake, kuishi kwake, mahubiri yake, kufa kwake na kupaa kwake, na kurudi kwake mara ya pili hiyo ndiyo Injili ya kweli na ndio habari njema.
Injili ya kweli ina nguvu ambayo inaleta wokovu..
Warumi 1:16 “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.
Kinyume chake injili yoyote isiyomwelezea Yesu kuzaliwa kwake, kuishi kwake, kufa kwake, kupaa kwake na kurudi kwake mara ya pili, injili hiyo ni injili ya uongo ya yule Adui shetani ambayo katika nyakati hizi za mwisho imezagaa kila mahali.
Injili ya uongo inaelekeza kutafuta na kuyapenda mambo ya ulimwengu huu, haielekezi Toba na msamaha wa dhambi, Injili ya uongo haizungumzii hata kidogo kurudi kwa Kristo mara ya pili, badala yake inawalewesha watu wasikumbuke wala kufahamu kuwa Yesu Kristo atarudi tena kama alivyosema..
Injili ya uongo kamwe haigusii kwamba tunaishi katika siku za hatari na za mwisho, siku zote inafundisha kuwa bado sana mpaka mwisho ufike. Na injili hii inahubiriwa na wanadamu, ipo injili nyingine inayohubiriwa na vitu vya asili ijulikanayo kama Injili ya Milele, ambayo hatuna nafasi leo ya kuizungumzia hapa…
Injili (au Habari Njema) sasa imeshahubiriwa katika mataifa yote, hakuna nchi ambayo Injili ya kweli ya Yesu Kristo haijafika, hivyo ule mwisho umekaribia sana, tunaishi katika muda wa nyongeza, saa yoyote wakati wowote Unyakuo utapita. Je una uhakika wa kunyakuliwa endapo parapanda ikilia leo? Jibu unalo
Mathayo 24:14 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja”.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.
Luka 12:47b“………Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na Zaidi”.
Kila siku tunapolisikia Neno la Mungu tujue kabisa tunajiongezea deni mbele zake, kama vile biblia inavyosema Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu (Waebrania 4:12), inamaanisha kuwa pindi tu Neno la Mungu linapoingia ndani yetu linatazamiwa litoe matunda ya uhai, yaani lionyeshe mabadiliko ndani ya mtu, na pili watu wengine wabadilishwe kupitie Neno hilo hilo lililoingia ndani yetu.
Sasa kama inatokea leo hii tunalisikia Neno la Mungu, kisha hatulitendei kazi, tunasikia tu au tunasoma tu kama habari fulani ya kusisimua, tukitoka hapo, tunafikiria mambo mengine, tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida, Kesho tena tunasoma vile vile kama habari fulani iliyojiri mpya, kisha baada ya hapo tunaendelea kuwa kama tulivyokuwa, Kesho kutwa nayo vivyo hivyo, tunasoma tunaondoka, siku zinakwenda, miezi inakwenda, miaka inakwenda, ukiangalia jumla ya mahubiri au mafundisho uliyosoma au kuyasikia hayahesabiki,nabado hakuna badiliko lolote ndani yako, leo hii tunaangalia kichwa cha somo ni kipi, tunasoma, tunapita, tunachukulia ni kawaida tu, tukidhani Mungu naye anachukulia hivyo kama sisi…..Ndugu Mungu anahesabu kila Neno lake linaloingia katika masikio yetu, kwasababu yeye mwenyewe anasema hakuna Neno lake linalokwenda bure bure (Isaya 55:11), ni lazima limrudishie majibu, na majibu hayo yatamrudia siku ile tutakaposimama katika kiti cha hukumu.
Biblia inasema kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na Zaidi…
Mungu anatazamia hicho unachokisikia na mwingine akisikie kupitia wewe kwa ile karama Mungu aliyoiweka ndani yako, lakini unakihifadhi tu, ni sawa na mtu anayetupa chakula wakati wengine wanakufa na njaa, ni sawa na kufuru, hujui kuwa mahali fulani kuna mama ambaye ni mwabudu sanamu, na anafanya vile kwa kutokujua laiti angefahamu ukweli huo kutoka kwako angebadilika na kuwa shujaa wa Bwana, lakini kwa kuwa hana wa kumwelezea habari hizo anakufa katika sanamu na kwenda kuzimu..
Mahali fulani yupo kijana ambaye anadhani kwa kushika dini yake fulani tu ndio tiketi ya kwenda mbinguni, lakini hajui kuwa hata pamoja na dini yake aliyonayo anaweza kwenda kuzimu kwasababu njia pekee ya kufika mbinguni ni kwa YESU tu, lakini kwasababu hakuna wa kumuhubiria yeye anaendelea kujitahidi na dini yake na mwisho wa siku anakufa na kwenda kuzimu na mtu wa kumweleza ulikuwepo..
Sehemu nyingine mtu fulani amekata tamaa ya Maisha, pengine kwa magonjwa anataka kujinyonga, anasema hakuna tumaini tena la kuishi, lakini hajui kuwa tumaini pekee lipo kwa YESU kwake huyo hakuna mzigo wowote usiotua, lakini anaenda kuishia kujinyonga kwasababu hakukuwa mtu wa kumsaidia…Vivyo hivyo wapo wengi wanateswa katika hali nyingi kama hizo na shetani..ambao wanahitaji maneno machache tu yahusuyo habari za YESU, ili wabadilike, lakini sisi ambao tumeshiba tukiachilia mbali ya kuwahubiria na wengine, sisi wenyewe hatulitendei kazi hilo tunalolisikia kila siku..
Hebu leo mwambie mtu amhubirie mwingine anayepotea kuhusu habari za Yesu, utasikia anakwambia hana karama ya kuhubiri au hana karama ya kichungaji, lakini hebu aone mtoto wake anazama kwenye matumizi ya madawa ya kulevya uone kama hatamhubiria kila siku kwa masaa mengi kwa uchungu na kwa kuhuzunika..
Siku ile tutaficha wapi nyuso zetu..wakati wale wengine ambao wamekuwa waaminifu wanapoambiwa Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.(Mathayo 25:21)
Mathayo 25:26 “Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Tunapaswa tusilizoelee Neno la Mungu,..Pale tunapolisikia tulitendee kazi, kwasababu utafika wakati ambao Bwana akitazama na asipoona matunda yoyote, basi tutakatwa na tukishakatwa ndio milele hivyo hakuna tumaini tena baada ya hapo…
Wafilipi 2:13 “………utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.”
Kila siku tunapaswa tujitathimini, na tupige hatua moja mbele..
Maran Atha!.
Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
ESTA: Mlango wa 1 & 2
Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?
USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?
Rudi Nyumbani:
Je Kujiua ni dhambi?
Ili kufahamu kuwa kujiua ni dhambi au la! Hebu tutafakari mstari ufuatao.
1Wakorintho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.
Mstari huu unatosha kutupa jibu la swali letu! Hebu tafakari ni sahihi kutumia vibaya mali ya mwingine?..Mtu akikuambia chukua kiatu changu hichi kivae ukitunze akakupa na mashari na wewe ukasema kwasababu umeshakabidhiwa basi una mamlaka ya kukitumia utakavyo na kukiharibu je mwenye kiatu atakuwa na hatia kukulipisha?
Ndivyo ilivyo na miili hii tuliyonayo Biblia inasema hapo juu kwamba SIO MALI YETU WENYEWE. Na hivyo kama sio mali yetu wenyewe hatuna mamlaka yoyote ya KUIUA. Je kujiua ni dhambi? Jibu ni ndio! kujiua ni dhambi kubwa sana mbele za Mungu, kwasababu mtu anayejiua anakuwa anaitumia mali ya Mungu isivyopaswa.
Na sio tu kujiua, bali hata kuichora chora au kuivalisha mavazi yasiyoipasa…Mwanamke akivaa mavazi ya mwanamume hapo ameitumia isivyopaswa mali ya Mungu, na kadhalika mwanamume naye vivyo hivyo..na mwanamke anayetoboa masikio baada ya kuujua ukweli, na anayevaa hereni na bangili wanaitumia mali ya Mungu isivyopasa..Mungu atawahukumu watu wote wasiotumia vyema miili waliyopewa.
1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
Je unautunza mwili wako? Je Roho Mtakatifu anakaa ndani yako? Je una uhakika wa kwenda mbinguni?
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Ndoto kama hizi ambazo unajiona umechelewa mahali fulani, aidha kuota umechelewa kufanya mtihani, au kuota umechelewa kusafiri, au kuota umechelewa kwenda kazini, au kuota umechelewa kwenye appointment fulani, au kuota umechelewa airport au kuota umechelewa interview, au umechelewa mahakamani n.k. huwa zinatoka kwa Mungu na Na kama zinajirudia mara kwa mara basi zidi kuzitilia maanani kwasababu bado hujavuka hapo.
Biblia inasema, Katika Ayubu 33:14-18
“Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;
18 Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
Unaona Mungu huwa anasema na mtu hata Zaidi ya mara moja katika ndoto ile ile, na hiyo ni kumtilia msisitizo kuwa anapaswa aizingatie kugeuka.
Kuota umechelewa mahali fulani muhimu, ni ishara kuwa kuna mahali unalegalega kufanya uamuzi wa kuokoka, au kama umeokoka basi unazembea wokovu wako, na hiyo itayagharimu Maisha yako ya milele kama usipokuwa makini, ukisoma katika kile kitabu cha Mathayo sura ya 25, utaona habari ya wale wanawali 10 ambao walikuwa wanamngojea Bwana wao aje kuwachukua waingie karamuni, biblia inatuambia watano wao walikuwa ni werevu na watano wao walikuwa wapumbavu…Wale werevu walibeba taa zao pamoja na Mafuta ya ziada katika vyombo vyao, lakini wale wengine wapumbavu, waliliona hilo halina maana sana, wakapuuzia, wakaenda hivyo hivyo na taa zao, lakini Bwana wao alipokuwia kidogo na usiku wa manane, ulipofika wakasikia kelele kwa mbali za shangwe kwamba Bwana wao anakuja, sasa wale ambao walikuwa na Mafuta ya ziada wakazitengeneza taa zao, kwenda kumlaki Bwana, lakini wale wengine baada ya kujiona taa zao zinazima, ndio wakaanza kupata akili kumbe tulipaswa kuwa na Mafuta ya ziada kwenye chupa zetu, na walipowaomba wenzao wawagawie kidogo, wale wengine wakasema hayawezi kututosha sisi na nyinyi, ni heri mwende sokoni mkanunue haraka mrudi labda mtamuwahi…
Lakini biblia inatuambia walipokwenda na kurudi walikuwa tayari wameshachelewa, wakakuta mlango umeshafungwa..kilichoendelea huko nje ni kilio na kusaga meno.
Sasa ndoto yako inaendana kabisa na mfano huu Bwana Yesu alioutoa isipokuwa tu imekuja katika taswira nyingine..Na mara nyingi katika ndoto hiyo wakati umeshachelewa utajiona jinsi unavyopambana ili uwahi lakini inashindikana kama tu vile ilivyowatokea wale wanawali watano wapumbavu, walikuwa wanafanya harakaharaka mambo ambayo wangepaswa wawe wameshayafanya tangu zamani lakini ilishindikana.
Hivyo nawe pia kama upo nje ya Kristo, nakushauri, mgekie muumba wako leo, kabla hazijakaribia siku za hatari ambazo utatamani kweli umjue Mungu wako, lakini hutaweza tena, na siku hiyo ikifika wewe mwenyewe utajisikia hali ya kujiona umepoteza jambo la msingi katika Maisha yako hapo ndipo majuto yatakapoanza…Je! Ni kitu gani kinachokuchelewesha sasa? Je ni utafutaji mali? Je Ni ndugu, Je, ni kazi yako?..Kama ndivyo basi biblia inasema ni heri kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili mzima ukatupwe katika Jehanamu ya moto, hivyo ni heri hiyo kazi ukaipoteza lakini umpate Yesu, Hizi ni nyakati za mwisho, Parapanda inakaribia kulia, watakatifu kwenda mbinguni usisibirie mpaka hayo yakukute, Tubu sasa mpe Kristo maisha yako ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38 upate ondoleo la Dhambi zako, ili Bwana akupe kipawa cha Roho wake Mtakatifu, kukusaidia kukulinda katika siku hizi mbaya.
Halikadhalika ikiwa wewe tayari upo katika wokovu, Jiangalie vizuri kwasababu kuna mahali unarudi nyuma, kuna vitu ambavyo unavifanya, au pengine unataka kwenda kuvifanya vinakucheleweshea taji lako, hivyo nawe pia, uimarishe wokovu wako, uisafishe njia yako, acha kuwa vuguvugu, Bwana anakuonya kwasababu hataki mwisho wa siku uangamie, kuota umechelewa kufanya mtihani au umechelewa kwenda kazini, au umechelewa kwenye interview, au umechelewa stendi ni dalili kuwa unachelewa katika safari yako ya mbinguni..Hivyo jirekebishe na Bwana atakusaidia.
Ubarikiwe sana.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?
Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?
UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
Mbali na mtu kuona maono au kuota ndoto Kuna mambo mengine ambayo nimeshawahi kuona yakitokea kwa watu wengi, na wengine walikuwa wakiniuliza ni nini maana yake lakini wasifahamu, hata mimi mwenyewe yamenitokea mara nyingi, na sikujua maana yake mpaka Bwana alipokuja kunipa ufahamu wa kuelewa…
Na hata pengine yalishawahi kukutokea na wewe, kuna wakati Fulani labda umekaa mahali unazungumza na watu, au unafanya kitu Fulani, na mara kunatokea tukio mbele yako ambao linalohusiana na tukio hilo, pengine katikati ya mazungumzo au shughuli mfanyayo na hapo hapo unapata ufahamu wa kujua kama vile tukio hilo ulishawahi kuliona mahali fulani, na sasa linatimia, ni kama vile linajirudia hivi au unaona tukio fulani na ghafla unajua hatma yake ni nini, na kweli inatokea hivyo, na hiyo huwa haidumu sana, ni kitendo cha sekunde mbili tatu, imekwisha..
Au inatokea tena wakati mwingine, ukitazama kitu chochote cha asili aidha mbingu, miti, milima, bustani, habari,wanyama, watu n.k.. hapo hapo unajikuta kuna hisia nzuri inakujia ndani yako usijue ilipotoka inakuwa kama ulishawahi kuishi sehemu Fulani nzuri yenye amani na furaha na utulivu kam hiyo hapo kabla n.k. na hiyo nayo huwa haidumu muda mrefu ni kitendo cha sekunde kadhaa tu imekwisha.
Sasa kama hautaelewa maana ya hayo mambo, utabakiwa na maswali mengi kichwani. Lakini hujui kuwa ni Mungu ndiye anayezungumza na wewe na kukuonyesha uhalisia wa mambo jinsi ulivyo.
Kuna siku moja nilikuwa ninacheza na mtoto wa Dada yangu nje, nilikuwa ninamrusha rusha juu na kumkamata, lakini baada ya muda kidogo mawazo yangu yalihama nikawa ninafikiria mambo mengine, nikawa kama nimepoteza amani kama vile mtu aliyeachwa kwenye unyakuo…na mara Yule mtoto ambaye nilikuwa ninacheza naye pale nje, akatulia kwa muda mfupi, halafu akawa anaangalia mbinguni pale pale mbele yangu. Kisha akazungumza maneno haya mara tatu “HUKUMU, HUKUMU, HUKUMU”..na baada ya hapo akaendelea na michezo yake, kama kawaida. Nikapata wasiwasi kidogo huyu mtoto mdogo wa miaka mitatu haya maneno ya ndani kayajulia wapi na huku hata kuongea vizuri alikuwa hawezi ni mzito hata wa kuongea..
Yale maneno yaliniingia ndani ya moyo wangu, nikafiria sana na tena linaendana na jambo nililokuwa ninawaza muda huo huo, hapo ndipo nikajua kuwa ni Mungu alikuwa anazungumza na mimi.
Sasa kwanini ninasema hivi, ndugu zipo njia nyingi sana usizozidhania tofauti na ulizizoe Mungu kusema nawe kila siku, na hizo pia zitatuhukumu katika siku ile ya mwisho. Unaweza kuikwepa Injili ya msalaba, unaweza ukakwepa mahubiri ya Neno la Mungu,akasema sikujua, Mtu atakwepa kila kitu kwa kisingizio cha kuwa hajasikia injili lakini hatakwepa SAUTI ya Mungu inayosema naye kila siku katika maisha yake kwa namna ambazo asizozitazamia yeye.
Sasa ni kwanini mtu anapata hisia kama hizo za kuona vitu vinavyoweza kutokea muda mfupi au sekunde chache mbeleni, ni kwasababu Mungu anamwonyesha kuwa pia una ouwezo wa kuona mambo yatakayokuja kutokea huko mbeleni kabisa hata baada ya kifo, kama hatopuuzia. Ikiwa umeona ya muda mfupi kidogo mbeleni kwanini usione ya muda mrefu yanayokuja huko mbeleni?. Kwanini usione ipo dhiki kuu inakuja huko mbeleni, Kwanini usione lipo ziwa la moto mbeleni?. kwanini usione ipo mbingu imeandaliwa kwa wale watakaoshinda, kama ikiwa kuna wakati mwingine unapata hisia nzuri kama alishawahi kuishi mahali Fulani kuzuri?, Kwanini asijue kuwa upo utawala wa amani wa miaka 1000 unakuja huko mbele wa Kristo na bibi-arusi wake na umilele ujao..
Ndugu Kila mwanadamu ameumbwa ni kiwango Fulani cha Imani, haijalishi awe ni mwenye dhambi, au mwema, haijalishi awe ni mwaminio au sio mwaminio, hata mtu anayeamini kuwa hakuna Mungu imemgharimu Imani, kuamini kuwa Mungu hayupo. Hivyo hakuna ambaye atanusurika siku ile ya Hukumu, hakuna hata mmoja.
Sikia maneno ya Mungu yanavyosema:
Isaya 65: 12 “mimi nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu NILIPOITA HAMKUITIKA; NILIPONENA, HAMKUSIKIA; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia.
Unaona Mungu amekuwa akinena na wewe kwa njia mbalimbali, wakati mwingine ulipokuwa katika shughuli zako na mihangaiko umeshawahi kusikia sauti kama mtu akuita jina lako kwa nguvu, na ulipotazama usione mtu, Sauti kama hizo ni kukuonyesha kuwa Mungu anakuita umtazame yeye, lakini wewe husikii, hata leo hii anazidi kunena na wewe lakini bado unataka kuufanya moyo wako mgumu usitubu dhambi zako na kumgeukia Mungu. Kumbuka Kuna wakati Mungu kauandaa wa kuuawa kwa waovu wote, na huko si kwingine zaidi ya kwenye ziwa la moto.
Usisubiri hizo nyakati mbaya zikukute, usiitamani hukumu ya Mungu,ambayo hakuna mtu hata mmoja aliye mwovu atapona, itii sauti yake leo, mpe Bwana maisha yako, anza mwanzo mwema, weka mbali maisha ya dhambi, yanakusaidia nini hayo? utubu kabisa kwa kumaanisha kuacha dhambi zako, kisha haraka iwezekanavyo katafute mahali utakapoweza kwenda kubatizwa ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kama hujabatizwa, wengi shetani kawapofusha macho na kufikiri ubatizo haujalishi, au hauna maana sana, ndugu yangu usidanganyike.
Ubatizo ni wa umuhimu sana, biblia inasema “aaminiye na kubatizwa ataokoka” sio aaminiye tu! peke yake hapana! Bali aaminiye na kubatizwa…utasema mbona Daudi hakubatizwa? ina maana hataokoka?..Daudi hakubatizwa kwasababu yeye hakuifahamu hii neema ingawa alitamani kuijua, hivyo yeye na watu wote ambao hawakuijua hii neema ya Ubatizo, Bwana atawapa neema ya wokovu kwasababu hawakujua, kadhalika Daudi aliua maadui zake kwasababu hakuijua hii neema tuliyonayo sisi ya kufahamu kuwa hata kumwonea hasira ndugu yako ni sawa na kuwa muuaji, hali kadhalika Daudi alioa wake wengi kwasababu hakuijua hii neema ya kuwa mtu anapaswa awe na mke/mume mmoja tu!!
Lakini leo hii wewe unayesikia haya, ukiua na umeshaufahamu ukweli kwa kisingizio cha kujilinganisha na Daudi, utakwenda kwenye ziwa la moto, vivyo hivyo ukimwacha mume wako/mke wako na kwenda kuoa mwingine au kuongeza wake wengi kwa kisingizio cha kujilinganisha na Daudi, utakwenda katika ziwa la moto, kadhalika wewe unayesema leo ubatizo sio wa lazima sana kwa kujilinganisha na Mfalme Daudi na yule mtu aliyekufa na Bwana pale msalabani utaenda kwenye ziwa la moto. Kwasababu umeujua ukweli na bado ukaukataa. Na leo hii umeusikia ukweli hapa siku ile hutasema hukuusikia.
Na ubatizo sahihi sio wa kunyunyiziwa, ni wa kuzamishwa mwili wote katika maji mengi na ni kwa jina la YESU Kristo kama maandiko yaagizavyo katika (Matendo 2:38, 8:16, 10:48, 19:5).Jina la Yesu ndio jina la Baba,Mwana, na Roho Mtakatifu, hakuna lingine Wengi wanapuuzia maagizo hayo lakini wewe usiwe hivyo, suala la wokovu wa roho yako usilichukulie kidini, au kiwepesi wepesi hayo ni maandiko kabisa na ni maagizo ya Mungu kwa ajili ya uzima wa roho yako. Mtu yeyote anayemaanisha kumfuata Kristo hataona ni masharti magumu, lakini waliovuguvugu ndio watatoa udhuru.Na ndio hao mwisho wa siku wokovu wao hauthibitiki.
Lakini wewe ukizingatia hayo kwa moyo mweupe Bwana atakupa kipawa cha Roho wake na huyo ndiye atakayekuongoza siku zote katika kuijua kweli. Na kubatizwa si lazima kupitia mafunzo yoyote ya muda mrefu, halafu baadaye upokee cheti Fulani, kama dini zinavyofanya..tiketi ya kubatizwa ni KUAMINI NATOBA BASII!!. Pindi tu mtu anapoamini na kutubu dhambi zake na kuamua kumwishia Kristo wakati huo huo anapaswa akabatizwe.
Na pia kama umempa Bwana maisha yako tayari na umebatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, ni wajibu wetu sote kuwahubiria wengine habari njema za ufalme, hivyo popote pale ulipo waambie wengine kuhusu wokovu ulio katika Bwana wetu Yesu Kristo
Ikiwa kama hujabatizwa na hujui mahali utakapopata huduma hiyo, unaweza pia kuwasiliana nasi, tukuelekeze mahali karibu nawe.
Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?
UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.
USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
https://wingulamashahidi.org/2019/08/30/maswali-na-majibu-2/
Huu ni mfululizo wa maswali machache yamhusuyo Bwana Yesu, ambayo yamekuwa yakiulizwa na watu wengi hususani wale wasio Wakristo, ambao hawamjui Bwana Yesu kwa mapana, na Baadhi ya maswali hayo ni pamoja na 1)Bwana Yesu alizaliwa wapi? 2) Bwana Yesu alizaliwa mwaka gani? 3) Bwana Yesu alikuwa dini gani 4) Yesu alizikwa wapi? 5) Je Yesu aliteswa msalabani au juu ya mti ? n.k
Maswali yote na mengine mengi tutayapata majibu yake hapa, hivyo karibu!
Tukianza na swali la kwanza linalouliza
Swali la Yesu alizaliwa wapi..Jibu lake lipo wazi katika Biblia kwamba alizaliwa huko Bethlehemu ya Uyahudi…Bethlehemu ulikuwa ni mji aliozaliwa Mfalme Daudi, uliokuwepo maili chache sana kutoka mji wa Yerusalemu…Hivyo Kutokana na Daudi kuupendeza sana moyo wa Mungu, Mungu aliubariki mji wake aliozaliwa na kuufanya kuwa mji atakaokuja kuzaliwa Masihi yaani Yesu Kristo.
Mathayo 2:1 ‘Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu’
Sasa ingawa Bwana Yesu alizaliwa Bethlehemu lakini maisha yake yote hakuishi huko Bethlehemu bali aliishi mji mwingine uliokuwepo mbali sana unaoitwa Nazareti, hivyo alijulikana sana kama Yesu Mnazareti kuliko Mbethlehemu.
Biblia haijaeleza Bwana Yesu alizaliwa mwaka gani, lakini tukisoma hiyo Mathayo 2:1 hapo juu inasema…Yesu alizaliwa zamani za Mfalme Herode..Hivyo inaaminika na wanathelojia wengi kuwa Kristo alizaliwa kati ya mwaka 4-6 KK. Lakini katika Kalenda yetu tunafahamu kuwa umeshapita zaidi ya Miaka elfu 2 tangu Kristo awepo duniani…Hivyo ni kusema kwamba Kristo alizaliwa miaka 2019 iliyopita, kama leo hii ni mwaka 2019..
Ahadi ya kuzaliwa Mwokozi walipewa wayahudi (yaani Waisraeli) Lakini ahadi hiyo haikuishia kuwa Baraka kwa Waisraeli tu peke yao, bali kwa watu wote hata wa Mataifa kwasababu maandiko yanasema..Mataifa yote ulimwenguni yatamtumainia, na yeye atakuwa wokovu kwa mataifa yote…Lakini sharti kwanza Wokovu huo uanze kwa Wayahudi ambao ndio walioahidiwa kwanza na kisha uje kwa watu wa mataifa mengine.
Hivyo wayahudi walikuwa na Dini yao ya kiyahudi ambayo ndio ile waliyopewa na Musa, ya kushika sheria na Torati..Lakini Ahadi ya ujio wa Masihi ni kurekebisha pale palipopunguka..Hivyo alipozaliwa alizaliwa katika dini ya kiyahudi, lakini kwa uweza wa Roho aliitimiliza torati pale palipopunguka na pale palipoeleweka vibaya…Ndio maana akasema katika
Mathayo 5:17 ‘Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza’.
Hivyo dini ya kiyahudi Bwana Yesu alikuja kuitimiliza kwa kuwaambia amchukiaye ndugu yake ni sawa na muuaji, hivyo chuki haitakiwi kabisa, amtazamaye mwanamke kwa kumtamani tayari kashazini naye hivyo kutamani hakutakiwi kabisa licha tu ya kuua,..Hiyo ndiyo ilikuwa dini Bwana Yesu aliyokuwa nayo na ndio aliyokuwa anahubiri watu wawe nayo…Hakuhibiri Dini ya kiyahudi kwamba watu wawe wayahudi au wajina fulani…Bali alihubiri watu wabadilike na kuwa wema, watakatifu wenye upendo n.k…hiyo ndio Dini ya Bwana Yesu..
Yakobo 1:26 ‘Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.
27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa’.
Kwahiyo dini ni matendo sio Jina! au kikundi fulani cha waabudio fulani..
Bwana Yesu alizikwa wapi? Jibu: alizikwa Yerusalemu, mji uliokuwepo karibu sana na mji aliozaliwa Bethlehemu…soma Luka 13:33 na Mathayo 27:60
Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa Msalaba unatengenezwa kwa mti, hivyo mahali popote kwenye biblia panaposema Bwana aliangikwa juu ya mti kama kwenye Wagalatia 3:13, basi fahamu kuwa inazungumzia msalaba kwasababu msalaba unatengenezwa kwa mti. Na msalaba ulikuwa unatengenezwa kwa vipande viwili vilivyokatana kama alama ya kujumlisha…na sio kipande kimoja kilichosimama wima kama inavyoaminika na ‘mashahidi wa Yehova’
Utamaduni wa kuwatundika Watu msalabani haukuanzia kwa Bwana Yesu bali ulikuwepo kabla yake, kwamba wahalifu waliokosa sana walikuwa wanauawa kwa kutundikwa msalabani vile vile kama Bwana Yesu alivyotundikwa, ndio maana utaona siku ile aliposulibiwa kulikuwepo pia kuna wengine wawili waliosulibiwa pamoja naye..Kwahiyo Bwana Yesu aliteswa msalabani wenye mfano wa alama ya kujumlisha.
Kumbuka Bwana YESU alikufa kwaajili ya dhambi zako na zangu, alisulubiwa na kuteswa na alikufa na siku ya tatu akafufuka, naye hatakufa tena..sasa hivi tunavyozungumza yupo hai, na anakutazama wewe na mimi, ametuma Neno lake kutuponya..Hivyo kama hujampa maisha yako ni vyema ukafanya hivyo sasa kama unatamani kuishi milele..
Yeye atakupokea na kukusafisha dhambi zako zote bure! alisema
Mathayo 11:28 ‘Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi’.
Je mzigo wako ni mzito? unasubiri nini usiende kuutua kwa Yesu sasa?
Bwana akubariki.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?
Unatafuta kujua namna ya kuvunja maagano ya ukoo?. Upo sehemu sahihi fuatilia somo hili hadi mwisho kabisa utafahamu njia rahisi ya kuondokana na hizo laana milele zisikurudie tena.
Biblia inasema:
Yohana 8:36 “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”
Unaweza ukajiuliza ni kwanini pale msalabani Bwana Yesu alisema neno moja tu IMEKWISHA!!(Yohana 19:30), Na sio YAMEKWISHA?…Ukilifahamu hilo utajua ndio sababu kwanini huwezi kuona maneno kama laana za ukoo, laana za kifamilia, laana za mababu, laana za mapepo, kifungo vya kikabila n.k katika biblia..kwasababu hayo yote yamejumuishwa katika hicho kitu kimoja kilichokwisha pale msalabani nacho si kingine Zaidi ya DHAMBI.
Dhambi ndio mzizi wa matatizo imefananishwa na ugonjwa wa ukimwi, Ambao vijidudu vyake vinafanya kazi moja tu nayo ni kwenda kushambulia kinga ya mwili basi, havileti madhara mengine yoyote mwilini, havisababishi kutokwa na vidondo, havisababishi kutapika, havisababisha kuugua, havisababishi kukohoa La!..Lakini vinaua kinga ya mwili, sasa ile kinga ikishakufa, ina maana kuwa mwili hauna ulinzi tena, hapo ndipo kila aina ya ugonjwa unapata nafasi ya kuingia, mara malaria, mara Tb, mara mkanda wa jeshi, mara homa ya ini n.k. n.k. Na hivyo ndivyo mwisho wa siku vinakwenda kummaliza mtu…
Ogopa sana ugonjwa mmoja unaokwenda kushambulia kinga ya mwili kuliko magonjwa 99 yanayokwenda kushambulia sehemu nyingine zote mwilini.
Sasa dhambi na yenyewe ndio inafanya kazi hiyo hiyo, Adamu na Hawa walipoasi pale Edeni, dhambi iliingia ndani yao, ikamaliza kinga yao yote ya ulinzi Mungu aliokuwa amewawekea pale Edeni, Na ghafla uuaji ukaingia, dhuluma ikaingia, magonjwa yakaanza, uchawi ukaanza, laana zikaingia, vita vikaingia, matabaka na matambiko yakajitokeza ndio maagano zote za ukoo zikatokea huko huko n.k. Na hili likawa ni tatizo lisilokuwa na tiba kwa vizazi na vizazi, kwa karne na karne..Dawa ya dhambi haikupatika kama vile dawa ya ukimwi usivyopatikana leo, kwa Zaidi ya maelfu ya miaka.
Lakini Bwana Yesu alipokuja miaka karibia 2000 iliyopita hakuja kushughulika na tawi Moja la dhambi labda tuseme maagano ya ukoo, au laana za kifamilia, hapana angefanya hivyo basi tatizo lote lisingeondoka, lakini alikuja kuung’oa mzizi wote wa DHAMBI, kiasi kwamba mfano mtu aking’olewa mzizi huo ndani yake basi hakuna vimelea vyovyote vya laana yoyote ile itakayomwandama.
Jambo ambalo watu wengi hawafahamu, ni kuwa wanadhani kwenda kuombewa au kufanyiwa maombi fulani ya muda mrefu labda tuseme ya kufunga, na kukaa milimani na kutumia masaa mengi kuomba na kukemea ndio kunaondoa laana na maagano ya ukoo au maagano ya kifamilia, wengine wanadhani kutoa sadaka fulani maalumu ndio kunaondoa maagano ya kiukoo hapana, mtu anaweza akafanya hivyo na bado hayo mambo yasiondoke ndani yake, kama ikiwa bado yupo nje ya wokovu.
Kama mtu hajakusudia kweli kuokoka, mambo hayo hayawezi kuondoka hata iweje, yataendelea kumfuata tu, lakini kama leo hii ukasema mimi na dhambi basi, nimeamua kujitwika msalaba wangu na kumfuata YESU popote atakapotaka mimi niende, sirudi nyuma tena, ukatubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote, kisha ukatii agizo la Ubatizo, ukaenda kubatizwa katika ubatizo wa kuzamishwa kwenye maji mengi, na Kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na Matendo 2:38, ili upate ondoleo la dhambi zako, na kuanzia huo wakati ukawa unaishi Maisha ya kama mkristo aliyeokoka, nataka nikuambie, sio tu maagano ya ukoo yatafutwa juu yako, bali pia hata na yale maagano mengine usiyoyajua ya kipepo yaliyokuwa juu yako yote hayo yatafutwa..
Usihangaike kwenda kuombewa huku na kule, ukifika kule kila mmoja atakuambia hichi, mwingine kile. Kumbuka Wokovu ni muujiza mkubwa sana ambao unatokana na neema ya Kristo tunaoupata bure bila kujisumbua wala kugharamia chochote, wewe ni kutii tu, hivyo pale ulipotubu basi jua vyote vimefutika,..Lakini kitu shetani anachokifanya ni kukutisha, kukufanya ujione kuwa bado upo chini ya maagano hayo, atakuletea hichi na kile, hapo unapaswa usimsikilize wewe sema tu maneno haya..
“Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”
Atafanya hivyo kwa muda tu, lakini kwa jinsi unavyozidi kujifunza maneno ya Mungu na biblia, kwa bidii Zaidi ndivyo utakavyomfanya aende mbali na wewe Zaidi na mwishoni asikusumbue kabisa, kwasababu shetani huwa anamsumbua mtu na kumletea vitisho kutokana na ujinga wake, kutokana na uzembe wake wa kutokuzingatia kujifunza maandiko,..hivyo unapaswa ujifunze sana maandiko ili uweze kumshinda atakapokuletea majaribu yake.. Na ndio maana biblia inasema.
Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.
Na “KWELI” ni Neno la Mungu biblia inasema hivyo katika (Yohana 17:17)..Hivyo ukiwa ni mtu wa kujifunza na kuyatafakari Maneno ya Mungu kwa bidii shetani atakaa mbali na wewe sikuzote. Hiyo ndio njia pekee ya kuvunja maagano ya ukoo, ukiipata hiyo huhitaji kwenda kuombewa, wala kufanyiwa maombi yoyote ya ukombozi, lakini kama Maisha yako ya wokovu yapo mbali na Kristo halafu unatafuta njia mbadala ya kuondoa tatizo hilo, kumbuka hayo mambo yalishafanyika zamani sana, na yakashindikana..Hivyo na wewe pia usijaribu kuyarudia hayo..bali Mkaribishe leo YESU maishani mwako, awezaye kuondoa mzizi wote wa dhambi na laana zake zote. Na kukufanya kuwa kiumbe kipya. Na hakika atayavunja maagano yote ya ukoo, babu zako, na mababu zako waliyoingia na kuapa iwe ni katika afya, au mafanikio, au furaha vyovyote vile vitakwisha ndani yako.
Ubarikiwe sana.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Kwanini kuna watu wanafanyiwa deliverance (Maombi ya kufunguliwa), lakini baada ya muda wanarudiwa tena na hali ile ile sababu ni nini?
VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.
IPO NGUVU ITUVUTAYO KWA KRISTO, ITHAMINI!.
KWANINI MOTO NA UPEPO VINAWAKILISHA TABIA ZA MUNGU?
UNYAKUO.