Swali: Je biblia takatifu inajichanganya katika habari ile ya binti wa Yairo?.. kwamaana katika Marko na Luka inaonyesha kuwa Binti alikuwa katika kufa! (Marko 5:23) Lakini katika Mathayo 9:18 inasema binti alikuwa amekwishakufa, sasa habari ipi ni sahihi kati ya hizo mbili?
Jibu: Awali ya yote ni muhimu kufahamu kuwa biblia haijichanganyi mahali popote, isipokuwa pambanuzi zetu, na tafakari zetu ndizo zinazochanganyikiwa. Sasa ili tuelewe vizuri, turejee mistari hiyo..
Marko 5:21 “Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng’ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.
22 Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,
23 akimsihi sana, akisema, BINTI YANGU MDOGO YU KATIKA KUFA; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi
24 Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa.”…..
Turuke mpaka mstari ule wa 35 na 36 ili tuimalizie habari hii kama ilivyoelezewa na Marko..
35 Hata alipokuwa katika kunena, WAKAJA WATU KUTOKA kwa yule mkuu wa sinagogi, WAKISEMA, BINTI YAKO AMEKWISHA KUFA; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu?
36 Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu”
Katika kisa hiki ni kweli tunaona taarifa zinaanza na binti kuwa katika HALI YA KUFA, na zinaishia na BINTI KUFA.. Lakini tukirejea katika kitabu cha Mathayo tunaona habari nyingine ambayo inaonekana kama ni tofauti kidogo..
Turejee…
Mathayo 9:18 “Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, BINTI YANGU SASA HIVI AMEKUFA; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.
19 Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake”……….
Hapa tunasoma kuwa Jumbe-Yairo anamwambia Bwana kuwa Binti yake amekwisha kufa, na si yu katika kufa!, hivyo aende kumwekea mikono afufuke.. sasa swali je! Biblia inajichanganya?
Jibu ni la!.. kama tulivyosema, biblia haijichanganyi, isipokuwa ni pambanuzi zetu.
Sasa ili tukiweke hiki kisa vizuri; ni kwamba Yairo alipotoka nyumbani mwake kumfuata Bwana YESU, binti yake alikuwa hajafa bado!, ila alikuwa katika hali ya kufa,..na alipokutana na Bwana akamwomba aende amwekee mikono ili apone, sawasawa na Marko alivyorekodi hapo katika Marko 5:23, tukio ambalo halijarekodiwa na Mathayo..
Lakini alipokuwa katika kumsihi Bwana kuna watu baadhi waliotokea nyumbani kwake na kumpa taarifa kuwa binti yake amekwisha kufa!…Sasa Yairo aliposikia kuwa mwanae kafariki hakukata tamaa, bali aliendelea kumsihi Bwana kuwa aende kumwekea mikono ili afufuke hata kama amekwisha kufa!, Na Bwana YESU aliposikia hayo akaahidi kwenda naye.
Lakini alipokuja mtu mwingine kutoka nyumbani mwake kumpa hizo hizo taarifa kuwa binti yake kashafariki hivyo asizidi kumsumbua mwalimu… (maana yake alikuwa anarudia rudia kumwambia, sasa hiyo kauli ya asizidi kumsumbua Marko 5:35) ndio iliyomfanya Bwana YESU amwambie ASIOGOPE!, kwani ndiyo inayokatisha tamaa, na yenye kuua Imani ya Jumbe (Marko 5:36).
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa Mwandishi wa kitabu cha Marko alianzia kuelekezea tukio kuanzia mwanzo kabla ya binti kufa, na kutaja kuwa watu walikuwepo Zaidi ya mmoja waliokuja kumpa taarifa Yairo za kifo cha mwanae (Marko 5:35),
Lakini mwandishi wa kitabu cha Mathayo alianzia kuelezea tukio katikati wakati ambao tayari binti amekwishakufa na hakuelezea kabla ya kufa kwake…..Hivyo hakuna mkanganyiko wowote hapo, na wala mahali pengine popote katika biblia.
Je umeokoka?.. Je unafahamu kuwa tunaishi katika majira ya siku za mwisho?, na Kristo yupo mlangoni?. Kama bado hujampokea unangoja nini?.. Mpokee leo na ubatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la BWANA YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako nawe utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 2)
Swali: Kwanini biblia ikataze kujiongezea hekima, kwani kuna ubaya gani katika kuongeza hekima?
Jibu: Turejee..
Mhubiri 7:16 “Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe?”.
Hekima inayozungumziwa hapo si hekima ya KiMungu, ambayo hiyo tumeagizwa tuitafute sana..
Yakobo 1:5 “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa”.
Tena maandiko yanasema mtu aonaye hekima (hiyo ya kiMungu), biashara yake ni Zaidi ya fedha..
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.
14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye”.
Kwahiyo hekima iliyozungumziwa hapo katika Mhubiri 7:16b ambayo mtu akiwa nayo nyingi inamharibu si hekima ya kiMungu, bali ni HEKIMA YA KIDUNIA.. Ambayo hiyo kwa Mungu ni upuuzi sawasawa na 1Wakorintho 3:18
1Wakorintho 3:18 “Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.
19 Maana HEKIMA YA DUNIA HII NI UPUZI MBELE ZA MUNGU. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.”
Umeona?.. kumbe hekima ya dunia ni upuuzi mbele za Mungu na hiyo mtu akijiongezea sana itamwangamiza!!!.
Sasa mfano wa hekima ya kidunia ni ile inayosema “mwanadamu asili yake ni nyani”.. sasa hii ni elimu/hekima ya kidunia..ambayo imetukuka miongoni mwa wasomi wengi wakubwa, kiasi kwamba mtu aliyezama sana katika hiyo hekima, anajiangamiza mwenyewe, kwani atafikia hatua ya kusema hakuna MUNGU.
Ndio maana hapo biblia inasema “usijiongezee mno”… Maana yake usizame sana katika kuzitafuta, kwani zimejaa upotofu mwingi na ukweli kidogo…
Bwana atusaidie.
Kwa maarifa Zaidi kwanini biblia iseme “usiwe na haki kupita kiasi” fungua hapa >>>>>USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kwanini Mungu alimkataa Sauli? (1Samweli 15:23)
NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?.
Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?
SWALI: Naomba kuelewa tafsiri ya mithali 30:32-33, isemayo;
Mithali 30:32 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.
33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.
JIBU: Hekima inatueleza matokeo ya kila tendo linapofanyiwa kazi liwe ni zuri au baya litaleta majibu fulani tu. Hapa anatumia mfano wa siagi ambayo inatolewa katika maziwa. Kwa kawaida siagi huwa imejificha ndani ya maziwa, hivyo ili kuipata tu ile siagi, ni kitendo cha kuipiga basi hutokea kwa juu yote,
Sasa kupiga hapo sio kuyachapa maziwa hapana, bali kuyakoroga, ndani chombo Fulani maalumu kwa muda mrefu, baadaye maziwa na siagi hujitenga vyenyewe.
Halikadhalika, pia damu huwa ipo ndani ya pua, lakini haiwezi kutoka yenyewe tu bila kuisumbua pua kwa kuipiga. Kwamfano mtu akikupiga ngumi ya pua ni wazi kuwa damu itatoka tu.
Ndivyo anavyofananisha na ugomvi, kwamba ni jambo ambalo lipo tu, wakati wowote katikati yetu. Mfano tu wa siagi ndani ya maziwa na damu ndani ya pua. Lakini mpaka ugomvi huo ujitokeze, unahitaji kuchochewa, kukorogwa, korogwa, kupigwa pigwa.
Anasema hasira inapoanza, aidha kwa kuzungumza maneno mabaya, mwenzako akakereka, haraka sana, weka mkono wako kinywani, usiendelee kuzungumza, kwasababu kitakachofuata ukiendelea sana ni ugomvi, yaani mapigano, na kudhuriana.
Mauaji, visasi, chuki, asilimia kubwa vimetokana na hasira zilizochochewa.
Lakini, uwezo huu wa kujizuia, una nguvu endapo mtu yupo ndani ya Kristo. Je! Umemwamini? Kama bado na upo tayari kumpokea leo, basi wasiliana nasi kwa namba zetu chini.
Bwana akubariki
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kwanini iwe ni nchi ibubujikayo maziwa na asali?
Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?
Mathayo 5:21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
JIBU: Katika vifungu hivi tunaona Bwana Yesu anatoa mtazamo mpya kuhusiana na dhambi ya uuaji. Hapo mwanzo ilidhaniwa kuwa pale mtu anapochukua hatua ya kumchinja ndugu yake, au kumpiga mpaka kufa kama alivyofanya Kaini, ndio umehitimu kuwa muuaji. Lakini Bwana Yesu anasema..
Kitendo tu cha kumwonea hasira ndugu yako, kumfyolea, na kumwapiza, tayari ni kosa la uuaji.
Sasa alikuwa na maana gani kwa maneno hayo matatu. “Hasira, kufyolea na kuapiza?”
Hasira kwa ndugu, huzaa mambo kama kinyongo, uchungu, na wivu. Kwahiyo kama mtu akiwa na mambo kama hayo kwa ndugu yake, mbele ya Kristo amestahili kuhukumiwa.
Lakini pia akimfyolea. Kumfyolea ni kumwita mwenzako mjinga wewe, au mpumbavu wewe. Ukilenga mtu asiye na akili, Kwa urefu wa tafsiri hii fungua hapa>> RACA Hilo nao ni kosa lililostahili kuketishwa kwenye mabaraza ya wazee, utoe hesabu.
Lakini mbaya zaidi kumwapiza. Hichi ni kitendo cha kumtamkia kabisa maneno ya laana. Kana kwamba ni mtu mwovu sana aliyepindukia. Kwamfano kumwita ndugu yako mwana-haramu wewe, au kumwita ‘shoga wewe’, kumwita msenge(neno lenye maana mtu anayeshiriki uovu kinyume na jinsia yake), kumwita pepo, kafiri wewe, n.k. maneno ambayo hayawezi kutamkika, ni sawa na tusi kwa mwenzako. Huko ndio kuapiza.
Adhabu yake Kristo anaifananisha na kutupwa katika jehanamu ya moto.
Hivyo hatupaswi kudhani kuwa, kuua ni mpaka tumwage damu, lakini twaweza kufanya hivyo tokea moyoni mwetu hadi vinywani mwetu, kabla hata hatujafikia kwenye kitendo chenyewe.
Tujazwe Roho Mtakatifu, tuwezi kuzishinda tabia hizi mbaya za mwili.
Katika agano la kale ilikuwa sio tu kumpiga mzazi wako, ilikupasa kifo (Kutoka 21:15), lakini pia kumwapiza huku, adhabu yake ilikuwa ni moja tu na hilo kosa la kwanza yaani kifo.
Kutoka 21:17 “Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa”
Shalom.
Je! Umeokoka? Fahamu kuwa usipomwamini Kristo, na kupokea msamaha wake wa dhambi, hauna uzima wa milele ndani yako. Kwasababu kamwe hutakaa umpendeze Mungu kwa nguvu zako au matendo yako mwenyewe. Na sababu ya Yesu kufa msalabani kwa ajili yako kukusaidia, kupokea msamaha wa dhambi, lakini pia nguvu ya kushinda mambo mabaya kwa Roho wake Mtakatifu tuliopewa. Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu akuokoe leo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala hiyo ya wokovu, Bwana akubariki >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Amen
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Bwana alimaanisha nini kusema “atazamaye mwanamke kwa kumtamani” amezini naye?
Je ni sahihi kumwita mtu “Mkuu”?
Jibu:Turejee,
Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13 KWA MAANA MANABII WOTE NA TORATI WALITABIRI MPAKA WAKATI WA YOHANA”.
Mstari huo haumaanishi kuwa Torati yote na Manabii wote walimtabiri Yohana Mbatizaji.. kwamba atakuja kutokea na kuhubiri, na kwamba atakuwa nabii mkuu kuliko wote. Hapana, bali ilimaanisha kuwa Torati iliendelea kuwepo na kufanya kazi, na manabii waliendelea kutokea na kutoa unabii, mpaka wakati wa Yohana kutokea duniani.. na baada ya Yohana ndipo likaanza agano lingine jipya la ufalme wa Mungu kutangazwa na kila mtu kujiingiza kwa nguvu.
Maneno hayo yamewekwa katika Kiswahili kirahisi Zaidi katika kitabu cha Luka..
Luka 16:16 “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu”.
Sasa kufahamu nini maana ya Torati na Manabii fungua hapa >>>Nini maana ya “Torati na manabii”?
Lakini ni kwanini aseme tangu wakati wa Yohana ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu na watu wanajiingiza kwa nguvu??..Ni kuonyesha kuwa hapo kwanza ilikuwa haiwezekani mtu kujiingiza katika ufalme wa Mungu..ilihitaji kuingizwa.. na waliokuwa wamesimama kama waingizaji wa watu katika ufalme wa Mungu ni Manabii na Torati..
Watu walisubiri maagizo ya Mungu kupitia Nabii au kuhani ndipo wapatanishwe na Mungu… lakini baada ya Bwana YESU kufa na kufufuka kiti cha rehema kimefunguliwa.. Watu hawahitaji tena manabii wala makuhani kumkaribia Mungu… (Maana yake kila mtu ana uwezo wa kumkaribia Mungu kupitia damu ya YESU).
Hatuhitaji tena kwenda Yerusalemu kwa makuhani ndipo tumsikie Mungu, hatuhitaji tena sanduku la agano, hatuhitaji tena nabii atokee ndipo atupe maagizo ya Mungu.. bali kupitia Roho Mtakatifu ndani yetu tunamkaribia yeye.
Kwa kadiri tunavyotia bidii ndivyo tunavyoukaribia na kuuteka ule ufalme..na wenye hekima na bidii ndio wanaoukaribia Zaidi ule ufalme.
Bwana atusaidie.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
SWALI: Nini Maana ya Isaya 24:16-18, inapomzungumzia mwenye haki, na anaposema Kukonda kwangu!
Isaya 24:16 Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana.
17 Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.
18 Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika
JIBU: Vifungu hivyo vinazungumzia unabii wa Masihi (Yesu Kristo) mwokozi wetu.
Katika mstari wa 16, nabii Isaya anaonyeshwa maono, ya nyimbo za “mwenye haki” ambaye si mwingine zaidi ya Kristo, Kwamba atukuzwe. Jambo ambalo ni la furaha, Kristo kuja duniani, ni tendo ambalo lilishangaliwa sio tu na malaika (Luka 2:8-14), lakini pia na wanadamu (Yohana 12:12-13).
Lakini tunaona katika sentensi inayofuata nabii Isaya, anaonyesha masikitiko yake, kwa kusema Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu, watenda hila wametenda hila. Akifunua kimifano hali ya taabu na huzuni inayompelekea hata kupoteza afya kwasababu ya mienendo ya watu waovu baada ya pale. Yaani badala wampokee mwokozi, wengi walimpinga na kumkataa, wakamsulubisha, na kuukata wokovu, ulioletwa na huyo mwenye haki.
Hivyo katika vifungu vinavyofuata 17-18, Anaeleza hukumu itakayowapata waliopo duniani, kwa kosa la kumkataa masihi, akilenga hasaa siku ile kuu ya Bwana, siku ya mwisho ya ghadhabu ya Mungu ambayo hii dunia itaharibiwa kabisa pamoja na watu waovu. Ambapo kwa urefu wake, inaelezwa pia katika vifungu vinavyofuata.
Unabii ambao ni kweli kabisa, unapompinga Kristo leo, aliye mwenye haki, aliyekuja kukuondolea dhambi zako, huwezi kuikwepa jehanamu ya moto, kwasababu matendo yako pekee hayawezi kukufanya mkamilifu, vilevile katika siku za mwisho ikiwa utakuwepo duniani, huwezi kuyakwepa mapigo ya Mungu juu yako.
Hivyo mpendwa ni heri ukampokea Yesu leo, akusamehe dhambi zako. Jina lako liandikwe kwenye kitabu cha uzima. Mwisho umekaribia sana, Jiulize ukifa leo katika hali ya dhambi utaenda kuwa mgeni wa nani huko ng’ambo ufikapo?
Ikiwa upo tayari kuupokea wokovu leo, upate msamaha wa dhambi zako basi fungua hapa kwa mwongozo huo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.
“Nami nikiinuliwa juu ya nchi,NITAWAVUTA WOTE KWANGU”(Yohana12:32).
JIBU: Yesu ni mtu ambaye alizungukwa na makutano mengi, hivyo isingekuwa rahisi kwao kumkamata wakati wa mchana, kwasababu walijua watakutana na upinzani mkubwa wa makutano.. kama maandiko yanavyosema katika vifungu hivi;
Mathayo 21:45-46
[45]Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao.
[46]Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
Hivyo njia pekee, ilikuwa ni usiku. Tena wakamwendea na marungu na mapanga kujidai kuwa wanakwenda kumtafuta mwizi, huku mioyoni mwao wakijua kabisa wanayekwenda kumfuata ni mtu wa haki.
Na hiyo ni kuthibitisha kwamba walikuwa hawajiamini kwa matendo yao, kwasababu waliyajua ni maovu ndio maana waliyafanya gizani.
Marko 14:48-49
[48]Yesu akajibu, akawaambia, Je! Ni kama juu ya mnyang’anyi mmetoka wenye panga na marungu, kunitwaa mimi? [49]Kila siku nalikuwa mbele yenu hekaluni nikifundisha, msinikamate; lakini haya yamekuwa ili maandiko yapate kutimia.
Hiyo ndio sababu kwanini wamfuate usiku, lakini hawakujua ndio walikuwa wanairahisisha njia ya wokovu. Kufunua kuwa giza kamwe haliwezi kuishinda nuru.
Yohana 1:4-5
[4]Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. [5]Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
Mwamini Kristo, Nuru yake ikuangazie moyoni mwako.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
Yesu kuvishwa taji la miiba kichwani, kulifunua nini?
Swali: Njia ya msalaba ni nini na Ipi historia ya njia ya msalaba?
JIBU..
Njia ya Msalaba ni Desturi iliyoanzishwa na kanisa Katoliki ambapo waumini wanapita katika mitaa ile Bwana YESU aliyosulubiwa, kuanzia alipotoka kwa Pilato mpaka mwili wake ulipowekwa kaburini.
Kulingana na kanisa Katoliki, kuna vituo 14 ambavyo Bwana YESU alipitia, ambapo kila inapofika Ijumaa kuu (ile ya pasaka) wakatoliki hupita katika vituo hivyo huko YERUSALEMU kuanzia mahali pajulikanapo kama “ngome ya Antonia” mpaka “kanisa la Roma la ufufuo” (karibia na mahali ambapo Kaburi la Bwana YESU lilikuwepo)..matembezi hayo ni ya mita 600.
Na wale wasiokuwepo Israeli basi watapita karibu na picha kumi na nne (14) zilizochorwa katika kuta za makanisa hayo ya Roma na kusema baadhi ya sala.
Vifuatavyo ni vituo hivyo kulingana na kanisa katoliki.
1. Yesu anahukumiwa kuuawa.
2. Yesu anapewa msalaba na maaskari wa kiroma
3. Yesu anaanguka chini kwa mara ya kwanza.
4. Yesu anakutana na mama yake (Mariamu)
5. Simoni Mkirene anashurutishwa kuubeba msalaba wa Yesu.
6. Veronika anapangusa damu katika uso wa Bwana Yesu.
7. Yesu anaanguka kwa mara ya pili.
8. Yesu akutana na wanawake wa Yerusalemu.
9. Yesu anaanguka mara ya tatu
10. Yesu anavuliwa mavazi yake
11. Bwana Yesu anagongomelewa msalabani
12. Yesu anaisalimu roho yake
13. Mwili wa Bwana Yesu unaondolewa msalabani.
14. Mwili wa Bwana Yesu wawekwa kaburini.
Hivyo ndivyo vituo 14, Bwana Yesu alivyovipitia kulingana na kanisa katoliki.
Lakini vituo baadhi hapo hatuvioni katika maandiko, kwamfano kituo cha 3,7 na 9 cha Bwana YESU kuanguka chini mara ya kwanza, na ya pili na ya tatu havipo katika maandiko..
Vile vile kituo cha 6 kinachomtaja Veronika kufuta damu katika uso wa Bwana YESU hakipo katika biblia..na hata kituo cha 4 cha Bwana YESU kukutana na mama yake hakipo katika biblia!.
Hivyo kama habari hizo hazipo katika biblia hatupaswi kuziamini wala kuzishika kwani huenda ni habari za kutungwa! au zimetolewa katika vyanzo visivyo sahihi, ambavyo havijahakikiwa na Roho Mtakatifu.
Kitabu cha biblia chenye vitabu 66, hiyo ndiyo iliyohakikiwa na Roho Mtakatifu lakini vitabu vingine nje na hivyo vya kwenye biblia ni potofu na vina udanganyifu.
Na Zaidi hatujapewa amri ya kuadhimisha vituo vya Bwana YESU alivyopitia, ndio! Tunaweza kutafakari lakini si kufanyia ibada,..sala za namna hiyo ni ibada za sanamu, kwani zinamfanya mtu aanguke katika zile picha au katika ile mitaa huko Yerusalemu, jambo ambalo ni machukizo.
Kufahamu njia ya Msalaba hasa kibiblia ni ipi fungua hapa >>> NJIA YA MSALABA
Shalom..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KUSAMBAA KWA ROHO YA MPINGA-KRISTO.
Matuoni ni nini katika biblia?
MSALABA NI ZANA YA UJENZI WA MAISHA YAKO.
UTHAMINI WITO WA PILI WA YESU ZAIDI YA ULE WA KWANZA.
Jibu: Turejee,
Walawi 19:32 “Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi Bwana”.
Maana ya kumwondokea ni “kumsogelea au kumkaribia ili kumsikiliza”. Hivyo biblia iliposema mwondokeeni mtu mwenye mvi, maana yake “tumsogeleeni mtu mwenye mvi na kumsikiliza”..
Na kwanini tumsogelee mtu/watu wenye mvi?..Ni kwasababu “kuna hekima katika wazee, kwani wameishi muda mrefu na kukutana na mengi na kujifunza mengi”. (wazee walio ndani ya KRISTO).
Ayubu 12:12 “Wazee ndio walio na hekima, Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu”.
Soma pia Ayubu 32:6-7 na Mithali 23:22.
Hivyo ukitaka mashauri sahihi kuhusu maisha basi watafute walio na mvi, (yaani wazee) walio ndani ya Kristo, watakuambia au ukutahadharisha na mengi…
> Vile vile ukitaka maarifa na ushauri sahihi kuhusu ndoa, kazi au elimu watafute wenye mvi walio ndani ya KRISTO watakushauri na kukutahadharisha mambo yaliyo sahihi na yale yasio sahihi.
> Vile vile ukitaka mashauri sahihi ya kiroho watafute wenye mvi za kiroho watakushauri mambo sahihi.
Na mambo mengine yote ni hivyo hivyo, wenye mvi wanafahamu Zaidi kuliko vijana.
Lakini hasemi tu! Kumwondokea mwenye mvi… bali pia anasema “heshimuni uso wa mzee”. Maana yake mzee/wazee wanapaswa kuheshimiwa sana…. ni kosa kumvunjia mzee heshima, hata kama kafanya jambo lisilo sahihi mbele ya macho yako. Si ruhusa kumkemea mzee kama wanavyokemewa vijana au watoto.
1Timotheo 5:1 “Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;
2 wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
TUTAMKARIBIA MUNGU KWA IDADI YA MVI ZETU ROHONI.
HATA WAKATI WENU WA MVI NITAWACHUKUENI. (Isaya 46:3)
UTAKAPOKUWA MZEE, UTAINYOSHA MIKONO YAKO. NA MWINGINE ATAKUFUNGA
WALE WAZEE ISHIRINI NA WANNE (24), WANA KAZI GANI?
Huwenda ukawa unajiuliza, Bwana Yesu alikuwa na maana gani kusema, Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru? . Je huko gizani ni wapi, na sirini ni wapi? Je yeye huwa anazungumza gizani.
Mathayo 10:26 “Basi, msiwaogope, kwa maana hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana.
27 Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba”
JIBU: Ni vema tukaifahamu tabia ya Bwana wetu Yesu Kristo, katika kufundisha jinsi ilivyokuwa alipokuwa anazungumza na watu mbalimbali. Yapo maneno au mafundisho au mafunuo aliyoyaweka wazi kwa watu wote, lakini yapo ambayo hakuyaweka wazi kwa kila mtu.
Mahubiri yake mengi aliyazungumza hadharani, lakini mengine haikuwa hivyo, kwamfano upo wakati alijitenga akapanda milimani, na wale waliomfuata ndio aliowafundisha (Mathayo 5:1), wakati mwingine aliingia nyumbani, hakutana kujulikana kwasababu alikuwa akitaka kuwafundisha wanafunzi wake tu, peke yao (Marko 9:29-31), wakati mwingine aliwaponya watu akawataka wasimdhihirishe, (Marko 1:44), wakati mwingine alijifunua utukufu wake, kwa wale tu waliokwenda naye kuomba mlimani, uso wake ukawa unameta meta, kama jua, alipomaliza akawakataza wasimwambie mtu, mpaka atakapofufuka (Mathayo 16).
Hayo ni mazingira mbalimbali, ambayo Yesu alisema nao bila kujulikana na kila mtu, Sasa mazingira hayo ndio aliyaita “Gizani, au sirini”
Hii ni kufunua kuwa hata sasa Yesu anazungumza hadharani, lakini pia anazungumza sirini. Na yale ya sirini huwa ni makubwa zaidi na ndio maana haitaji yajulikane na kila mtu.
Watu wengi wanamsikia Yesu hadharani, lakini hawamsikii sirini. Hadharani, ni pale unaposikia mafundisho kanisani, mahubiri, semina, mkutano n.k. Ni kweli Yesu atakufundisha mengi kupitia matumishi wake mbalimbali, na yatakujenga na ni muhimu ufanye hivyo.
Lakini lazima pia sirini pa Yesu uwe napo.
Je hapo ni wapi?
“Ni eneo lako la utulivu la kimaombi na kutafakari”.
Ni muhimu sana kila mkristo, awe na wakati wake maalumu kila siku alioutenga wa kuzama uweponi, katika maombi, kusoma Neno na kutafakari shuhuda za Mungu maishani mwake. Ni muhimu sana.
Zaburi 91:1 AKETIYE MAHALI PA SIRI PAKE Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Mathayo 6:6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Hapa Yesu anataka uingie gharama, kidogo ili umsikie, au akuhudumie, au akufundishe. Ndio mfano wa wale waliomfata milimani. Vivyo hivyo na wewe, ingia gharama ya kudumu uweponi mwa Mungu. Ukiona mchana pana usumbufu, usiku ni muda mzuri sana, kuamka, tena masaa yako kadhaa kila siku,. Kumpa Bwana nafasi ya kukufundisha.
Ukiwa wa namna hii, hutamkosa Bwana popote pale. Kaa mahali pake pa siri. Kwasababu yupo pia sirini, akupe mambo mambo utayasema hadharani wakati fulani.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine: