Swali: Je sisi wakristo tunapaswa tuombe sala gani kabla kumchinja mnyama?, maana Imani nyingine tunaona kabla kuchinja wanatanguliza sala.
Jibu: Katika biblia hatujapewa maagizo yoyote ya kuomba sala, au kukiri maneno Fulani kabla ya kumchinja mnyama. Ndio zipo Imani zinazoelekeza kufanya hivyo, lakini si Biblia takatifu.
Maagizo tu yaliyopo katika biblia ni kushukuru kabla ya kula..lakini kupiga sala kabla ya kuchinja hatujapewa kwani hatuendi kutoa sadaka kwa miungu bali ni kwaajili ya kitoweo.
Katika agano la kale, wanyama waliombewa kabla ya kuchinjwa iwapo wanaenda kutolewa kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana (dhabihu).
Walawi 4:32 “Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu. 33 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake sadaka ya dhambi, kisha atamchinja awe sadaka ya dhambi, mahali hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa”.
Walawi 4:32 “Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu.
33 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake sadaka ya dhambi, kisha atamchinja awe sadaka ya dhambi, mahali hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa”.
Lakini katika agano jipya dhabihu ya mwili wa YESU ilishatolewa, (hiyo ndio dhabihu kamilifu)…sasa wanyama wanachinjwa kwaajili ya vitoweo, na si kwaajili ya sadaka.. na hakuna sala yoyote inayotangulia, na hata wanaoomba hizo dua bado kuna viumbe vitawafunga katika sheria hiyo, kwamaana samaki au dagaa au wadudu kama kumbikumbi au senene unawaombeaje dua kabla ya kutoa uhai wao?… utaombea dagaa mmoja mmoja??..ni jambo lisilowezekana vinginevyo hatutakula kabisa.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba hakuna sala inayotangulia kabla ya kuchinja au kuutoa uhai wa kiumbe chochote kwaajili ya chakula.. Na kufahamu kwa urefu kama wakristo anaruhusiwa kula nyama ya mnyama aliyechinjwa kwa dua, basi fungua hapa >>UKWELI KUHUSU UISLAMU Sehemu ya Pili: (Jiwe/Jabali la Kaaba).
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Print this post
Jibu: Turejee..
Mwanzo 15:16 “Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado”.
Ili tuelewe vizuri tuanzie ule mstari wa 13..
Mwanzo 15:13 “Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne. 14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi. 15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema. 16 NA KIZAZI CHA NNE KITARUDI HAPA, MAANA haujatimia uovu wa Waamori bado”
Mwanzo 15:13 “Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.
14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.
15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.
16 NA KIZAZI CHA NNE KITARUDI HAPA, MAANA haujatimia uovu wa Waamori bado”
Katika mistari hiyo Bwana MUNGU anamwambia Abramu kuhusiana na uzao wake kwamba utaenda utumwani katika nchi isiyo yake (ambayo ni nchi ya Misri) na utamtumikia Farao kwa muda wa miaka 400, na baada ya miaka hiyo watatoka Misri.
Sasa wakati Bwana anamwambia Abramu hayo maneno, Abramu alikuwa tayari yupo katika nchi hiyo ya ahadi, isipokuwa bado alikuwa hajaimiliki kwani uzao wake ulikuwa bado mdogo na ilikuwa ni sharti uende kwanza Misri, ukaongezeke huko na kukua, ndio maana Mungu anamwambia kuwa utapelekwa utumwani na kisha utarudi tena katika hiyo nchi Abramu aliyopo muda huo, na itawaondoa wenyeji wa nchi hiyo.
Sasa swali nini maana ya “Kizazi cha Nne kitarudi”..
Jibu: Zamani kizazi kimoja kilihesabika kwa miaka 100, hiko ni kizazi kimoja, kwahiyo vizazi vinne maana yake ni miaka 400.. na mwisho wa hiyo miaka 400 ndio wana wa Israeli walitoka Misri.
Lakini swali lingine ni hili: Ni kwasababu gani uzao wa Abramu ukae Misri miaka muda mwingi hivyo? (400).. Jibu tunalipata katika ule mstari wa 16 unasema..“Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado”
Kumbe ilihitajika UOVU WA WAAMORI UTIMIE!!..Na hiyo yote ni kuonyesha huruma za MUNGU, kwamba si mwepezi wa hasira, mpaka aachilie ghadhabu yake maana yake ni kwamba kiwango cha maasi kimezidi sana..kile kikombe cha ghadhabu kinakuwa kimejaa..
Kwahiyo hapo aliposema haujatimia uovu wa Waamori, maana yake kiwango cha maasi cha Waamori bado hakikuwa kingi kiasi cha kupigwa na MUNGU.. Lakini baada ya miaka 400 kile kiwango cha maovu na maasi ya Waamori, na ya watu wengine waliokuwa wanaishi Kanaani kilifika kilele, na ndipo MUNGU akaachilia hukumu yake kwa kuwaondoa.
Utazidi kuona MUNGU anawakumbusha wana wa Israeli kuwa sababu ya wenyeji wa Kanaani kuondolewa katika ile nchi, si kwasababu ya utakatifu wa wana wa Israeli, bali ni kwasababu ya maasi ya waliokuwa wanaikalia ile nchi.
Kumbukumbu 9:3 “Basi jua siku hii ya leo kuwa Bwana, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia Bwana. 4 USISEME MOYONI MWAKO, BWANA, MUNGU WAKO, ATAKAPOKWISHA KUWASUKUMIA NJE MBELE YAKO, UKASEMA, NI KWA HAKI YANGU ALIVYONITIA BWANA NIIMILIKI NCHI HII; KWANI NI KWA AJILI YA UOVU WA MATAIFA HAYA BWANA AWAFUKUZA NJE MBELE YAKO. 5 Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya Bwana, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno Bwana alilowaapia baba zako Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo. 6 Basi jua ya kuwa Bwana, Mungu wako, hakupi nchi hii nzuri uimiliki kwa ajili ya haki yako, kwa maana u taifa lenye shingo ngumu”.
Kumbukumbu 9:3 “Basi jua siku hii ya leo kuwa Bwana, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia Bwana.
4 USISEME MOYONI MWAKO, BWANA, MUNGU WAKO, ATAKAPOKWISHA KUWASUKUMIA NJE MBELE YAKO, UKASEMA, NI KWA HAKI YANGU ALIVYONITIA BWANA NIIMILIKI NCHI HII; KWANI NI KWA AJILI YA UOVU WA MATAIFA HAYA BWANA AWAFUKUZA NJE MBELE YAKO.
5 Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya Bwana, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno Bwana alilowaapia baba zako Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.
6 Basi jua ya kuwa Bwana, Mungu wako, hakupi nchi hii nzuri uimiliki kwa ajili ya haki yako, kwa maana u taifa lenye shingo ngumu”.
Umeona?… Na MUNGU ni yule yule hajabadilika, kama alivyowavumilia Waamori, na waanaki na Wahiti waliokuwa wanaikalia ile nchi ya ahadi kwa miaka 400, anatuvumilia hata sasa, lakini uvumilivu wake ni ili sisi tutubu, kwasababu hapendi hata mmoja apotee..
Warumi 2:4 “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? 5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu”.
Warumi 2:4 “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu”.
Je umeitikia wito wa YESU?, Kama bado hujageuka na kumfuata YESU basi usipoteze muda Zaidi, huu ndio wakati, duniani imefikia kilele kabisa cha maovu na maasi, muda wowote parapanda italia na kile kikombe cha ghadhabu ya MUNGU kitamiminwa duniani.
Bwana atusaidie tusiwe miongoni mwa watakaokabiliana na mkono wa BWANA.
SWALI: Yusufu aliwezaji kutafsiri ndoto? Je ni kwa hekima aliyokuwa nayo au kwa kuangalia ishara fulani, au kwa usomaji wa vitabu, au kwa saikolojia?
JIBU: Biblia inatuonyesha sifa kuu, ya Yusufu iliyokuwa ndani yake ni uwezo wa kutafsiri ndoto.
Lakini swali linaloulizwa je uwezo huo alitolea wapi, ulikuwa ndani yake mwenyewe au ulitoka kwingine.
Tukisoma Mwanzo 41:15, tunaweza kupata majibu;
Farao akamwambia Yusufu, Nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri.16 Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani.
Hapo Yusufu anasema si mimi, Mungu atampa Farao majibu. Kuonyesha kuwa uwezo huo ulitoka kwa Mungu wala sio katika akili zake, elimu , saikolojia , au hekima ya kibinadamu.
Alimtegemea Mungu asilimia mia kumfunulia, mfano tu wa Danieli alipokwenda kuomba juu ya tafsiri ya ndoto ya Nebukadreza katika sala akafunuliwa. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yusufu, katika kutafsiri ya ndoto ya Farao, pamoja na za wale watumishi wawili wa mfalme waliokuwa wanahudumu mezani pa mfalme. Hakubuni tu tafsiri kulingana na mazingira, bali alifunuliwa moja kwa moja aidha kwa ndoto au kuona maono.
Lakini ni kwanini Yusufu apokee neema hiyo kirahisi kwa Mungu, tofauti na wengine.
Jibu lipo katika TABIA yake, Ni wazi Roho ya Mungu huvutika sana katika tabia njema ya mtu. Yusufu tangu udogo alijitahidi kujiepusha na tabia zisizofaa, jambo lililopelekea mpaka ndugu zake kumchukia kwasababu alikuwa anatoa siri za mambo yao mabaya, hata alipouzwa kwa akida wa Farao, bado aliendeleza tabia yake ileile, pale mke wa Potifa alipomtamani akakataa, mwishowe akatupwa gerezani. Kwa njia hiyo Yusufu hakuacha kulitunza joto la ROHO ndani yake. Mfano tu wa Danieli naye, ambaye hakutaka kujitia unajisi kwa vyakula vya kifalme, na ndani ya hakukuonekana kosa lolote (Danieli 6:3).
Akashuhudiwa na mfalme kuwa Roho njema sana, na iliyo bora inakaa ndani yake.
Danieli 5:12 kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danielii, naye ataionyesha tafsiri.
Hivyo ili na sisi tushiriki sehemu bora na njema za vipawa mbalimbali vya Roho Mtakatifu, hatuna budi kujijenga kimwenendo, katika maisha matakatifu yampendezayo Mungu.
Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?
KWA KUWA ROHO BORA ILIKUWA NDANI YAKE.
WALA HAKUSIMAMA MTU PAMOJA NAYE, YUSUFU ALIPOJITAMBULISHA KWA NDUGUZE
JIBU: Safina ya Nuhu ilikuwa ni mfano wa Meli kubwa iliyojengwa katika deka tatu, ambayo vipimo vyake vilikuwa ni mikono mia tatu urefu wake, na mikono hamsini upana, na mikono thelathini kwenda juu.
Mwanzo 6:13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami. 15 Hivi ndivyo utakavyoifanya; mikono mia tatu urefu wa safina, mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake.
Ambayo kwa vipimo vya sasa ni sawa na makadirio ya;
> Mita 137 urefu
> Mita 23 upanda
> Mita 14 kimo.
Ukubwa wa ile Safina, kwa sasa tunaweza kuifananisha na hizi meli kubwa za mizigo.
Yapo mambo manne ya kufahamu;
1). Jambo la kwanza ni kuwa hawakuingizwa wengi wengi, bali wawili wawili, na wengine saba saba, hivyo ni idadi ndogo tu ya kila jamii ndio iliyoingizwa.
2) Lakini pia kuna uwezekano Nuhu aliwaingiza wale wadogo wadogo tu, na sio wale wakubwa, Hivyo ikaachilia nafasi ya wanyama wote kujitosheleza ndani ya safina.
3) Tatu alipoambiwa awaingize wanyama kwa “namna” zao, (Mwanzo 6:20). Kwa lugha ya kibiblia si lazima imaanishe kila familia za wanyama ziingie, mfano familia mbalimbali za mbwa, wenye manyoya marefu, wenye asili ya ufupi, wawindaji, n.k. hapana, bali walipoingizwa mbwa, ni namna moja tu, iliwakilisha wote, Na baadaye walipoongozeka waliweza kuonekana wa maumbile tofauti tofauti tena, hilo linawezekana, ni sawa na sisi wanadamu tulitoka katika asili ya baba mmoja na mama mmoja, lakini leo hii kuna waafrika, wazungu, wachina, waarabu n.k. Hivyo ikiwa aliwaingiza kwa njia hiyo basi kisayansi inawezekana kabisa.
4) Lakini hoja ya mwisho iliyo na nguvu kuliko zote, ni kuwa hata kama ni namna zote na familia zao waliingia, bado Mungu anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyafanya, ikiwa katika uzazi wa mwanaume mmoja Mungu amehifadhi mamilioni ya mbegu za kibinadamu, na ndani ya tumbo la mwanamke mmoja hadi watoto tisa wanakaa kwa ujauzito mmoja. Hivyo hatuwezi kushangaa, Mungu kuvihifadhi viumbe vyote katika meli ile, inayoonekana haijitoshelezi. Kwasababu yeye ni Mungu asiyeshindwa na chochote.
Ni kwa yeye haathiriwi na nafasi ya udogo au ukubwa, kusudi lake litasimama tu. Kwa vile vichache vilivyokuwa kwenye safina, ulimwengu leo umejawa na viumbe vingi na watu wengi. Wengine wanasema mimi nabanwa na muda hivyo siwezi kumtumikia Mungu, mimi nabanwa na masomo hivyo siwezi kufanya kitu kwa Mungu, mimi nimefungwa gerezani, siwezi kulitimiza kusudi lolote la Mungu. Ndugu Neno la Mungu halifungwi.
Ndugu Paulo alifungwa gerezani akazuiwa kwenda kuhubiri injili katika mataifa kama ilivyo desturi yake, lakini akiwa gerezani aliandika nyaraka ambazo mpaka leo hii zinaendelea kuhubiri injili, zaidi hata ya ziara zake.
Amini uweza wote wa Mungu mahali popote ulipo, bila kuathiriwa na mazingira.
NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?
SAFINA NI NINI?
Mvinje ni mti gani? (Mwanzo 6:14)
Swali: Je mtu akifanya dhambi katikati ya mfungo, mfano dhambi ya uzinzi, je ule mfungo unakuwa umeharibika?
Jibu: Awali ya yote ni vizuri kufahamu kuwa kufunga ni kitendo cha kuyatiisha chini mapenzi ya mwili na kuruhusu mapenzi ya roho yaje juu, kwasababu roho siku zote hushindana na mwili..
Wagalatia 5:16 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka”
Wagalatia 5:16 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka”
Sasa unapokula chakula katikati ya mfungo, huo mfungo unakuwa umeharibika, kwasababu unakuwa umeyaruhusu mapenzi ya mwili, hali kadhalika unapofanya dhambi kama ya uzinzi katikati ya mfungo, pia mfungo huo unakuwa umeharibika kwasababu uzinzi ni dhambi inayohusisha mwili kwa asilimia zote.
1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”.
Kwahiyo mtu anayefanya zinaa anakuwa ameuharibu mfungo wake, na hivyo anapaswa atubu kwa kumaanisha kuacha hiyo dhambi kisha kwa uongozo wa Roho Mtakatifu apange mfungo mwingine.
Kwa urefu kuhusiana na njia bora ya kufunga, fungua hapa >>>NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
WhatsApp
(Mafunzo maalumu kwa watoto na walezi).
Kama wewe ni mtoto basi jifunze haya, na kama ni mzazi basi pia jifunze haya na pia mfunze mwanao…
Mambo ya Walawi 19:3 “Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu”
Biblia imetumia neno “kumcha” kuonyesha msisitizo wa jambo hilo, jinsi lilivyo la msingi.
“Kumcha mzazi” sio “kumwabudu” bali ni kumpa heshima ya hali ya juu sana, ikiwemo kumsikiliza, kumtii na kufanya yale anayosema bila kumsumbua sumbua ikiwa jambo hilo si nje na mapenzi ya MUNGU.
Maana yake kama tunavyomcha MUNGU, kila atuambiacho tunakizingatia, kwasababu tunajua kwake kuna baraka na laana, kadhalika na wazazi hivyp hivyo wanaweza kutubariki na kutulaani.
Sasa wengi wetu inapofika eneo hili la kutafakari mzazi na mtoto akili zetu huwa zinalenga kufikiri wale watoto walio chini ya malezi ya wazazi, pasipo kujua kuwa hata uwe na miaka 70 na kama mzazi wako yupo hai bado hiyo amri inakuhusu hata wewe ya kumcha mzazi wako, kwani wewe bado ni mtoto kwake.
Amri ya watoto kuwatii na kuwaheshimu wazazi inawahusu hata wenye ndevu na hata wazee wenye mvi, haijalishi wewe sasa ni bibi au babu na unao wajukuu…kama mzazi wako yupo hai unayo amri ya kumcha..
Lakini ukimvunjia heshima mzazi kwasababu ni mzee, basi fahamu kuwa bado hujayajua maandiko.
Mithali 23:22 “Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee”
Jifunze kumcha Mzazi, wapo watu wanapambana na wazazi wakati wote, wanagombana na wazazi, na hata kuwaita wachawi, usiwe jamii ya hao watu waliotabiriwa..
Mithali 30:11,”Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao”.
Yafuatayo ni madhara machache ya kutomcha Mzazi.
1. Jicho kung’olewa.
Mithali 30:17 “Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa Na vifaranga vya tai watalila”
Mtu aliyetolewa macho ni kipofu, hawezi kuona ya mbele wala ya nyuma katika maisha yake, atabaki anapapasa tu.
2. Kifo.
Mithali 20:20 “Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu”.
Maana ya Taa kuzimika ni “kifo”. (Soma Ayubu 21:17).
Yapo na madhara mengine mengi ikiwemo kukosa Heri mashani..
Je unamcha mzazi wako?..je unameombea?..je umepatana naye?. Kama bado hujafanya hayo yote basi anza leo.
Bwana akubariki na atusaidie.
JE! UNA MHESHIMU MUNGU?
WAZAZI WA YOHANA NA YAKOBO.
Uchaji ni nini kama tunavyosoma katika 1Timotheo 2:10?
BARAKA ZA WAZAZI KWA WATOTO.
Jibu: Turejee…
Walawi 24:3 “Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu”.
“Pazia la ushahidi” au kwa lugha nyingine “Pazia la Sitara” lilikuwa ni pazia lililotenga “patakatifu” na “Patakatifu pa patakatifu”.
Pazia hili lilisitiri eneo la ndani kabisa ya hema mahali palipokuwepo sanduku la Agano au sanduku la ushahidi.
Kipindi wana wa Israeli wapo jangwani wakitaka kuondoka eneo moja kwenda lingine walikuwa hawana budi kulivunja hema, na ili kulisitiri sanduku la agano mbali na macho ya watu wakati wanatembea, Bwana aliwaambia watumie pazia hilo la ushahidi linalotenga patakatifu na patakatifu pa patakatifu kulifunika hilo sanduku.
Na walipopiga makambi tena walilitengeneza hema na kilitumia hilo pazia kusitiri sehemu hizo mbili, hiyo ndiyo ilikuwa desturi yao.
Hesabu 4:5 “hapo watakapong’oa safari, Haruni ataingia ndani, na wanawe, nao watalishusha pazia la sitara, na kulifunika sanduku la ushahidi kwa hilo pazia”
Sasa Pazia la sitara kiroho liliwakilisha kiambazi kulichotutenga sisi na rehema za Mungu, kwamba hapo kwanza hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kupaingia patakatifu (ndani ya pazia) na kudai rehema isipokuwa kuhani mkuu tu, tena mara moja kwa mwaka, na dhambi zilifunikwa tu na hazikuondolewa.
Lakini Kristo alipokufa pale msalabani maandiko yanaonyesha kuwa hili Pazia la sitara lilipasuka kati kwa kati, vipande viwili.
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. 51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka”.
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka”.
Hiyo nikufunua kuwa sasa watu wote tunaweza kukikaribia kiti cha neema kupata rehema..
Waebrania 4:14 “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu”
Ni neema kubwa sana tuliyonayo sasa ambayo haikuwepo zamani, watu wa kale walitamani kuipata neema hii tuliyonayo lakini hawakuipata.
Lakini swali kuu linabaki kwetu…Je tunaithamini hii Neema, au tunaichukulia tu kama kitu cha kawaida?.
Waebrania 10:29 “Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”.
Bwana atusaidie tusimame imara.
Sadaka ya kinywaji ilikuwaje? Na inawakilisha nini?.
Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?
AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?.
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA
Walawi 7:9 “Na kila sadaka ya unga iliyookwa MEKONI, na yote yaliyoandaliwa chunguni, au kaangoni, yote yatakuwa ya huyo kuhani aliyeyasongeza”.
Mekoni ni jiko la kuokea mikate kwa lugha ya kiingereza ni “oven”.
Katika agano la kwanza sadaka zote za unga zilizotengenezwa kwa kupikwa ….Bwana Mungu aliagiza ziwe ni riziki za makuhani wanaofanya kazi yake katika nyumba yake.
Walawi 7:10 “Na kila sadaka ya unga, kama umeandaliwa na mafuta, au kama ni mkavu, watautwaa wana wote wa Haruni kuutumia, kila mtu sawasawa”
Katika agano jipya pia Bwana ameruhusu wanaohudumu madhabahu wale kupitia madhabahu..
1 Wakorintho 9:13 “Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? 14 Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili”
1 Wakorintho 9:13 “Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?
14 Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili”
Unapotoa riziki kwa wanahubiri injili unafanya jambo lenye thawabu kwasababu ni maagizo ya Bwana na si sheria.
Shetani kaliharibu hilo eneo la matoleo na kuwafanya watu wasitoe kabisa wakiamini kuwa ni biashara zinafanyika..
Ni kweli wapo wanaofanya injili kama biashara lakini si wote, hatuwezi kuacha kutimiza majukumu kwa Bwana kwasababu ya uharibifu wa shetani, tutaendelea mbele kwasababu Ukristo ni mapambano.
NIMEYATUNZA MANENO YA KINYWA CHAKE ZAIDI YA RIZIKI YANGU.
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
MADHABAHU NI NINI?
Tofauti kati ya makuhani na walawi ni ipi?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Swali: Je malaika wana damu na nyama na mifupa kama tuliyonayo sisi wanadamu?
Jibu: Malaika wanayo miili kama wanadamu tulivyo na miili, isipokuwa miili ya Malaika imeumbwa kwa malighafi za kimbinguni na hii yetu imeumbwa kwa udongo.
Na kwasababu miili ya Malaika imeumbwa kwa malighafi ya kimbinguni, basi uwezo wake au fahari yake ni kubwa kuliko hii yetu ya udongo, yenyewe haimwi, haichoki, haina tamaa, wala haifi…
1Wakorintho 15:40 “Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali”.
Miili ya Malaika inaweza kubadilika na kuwa ya kibinadamu kwa muda, na kwa kusudi maalumu, ndio maana katika biblia tunaona Malaika wakiwatokea watu kama wanadamu (Soma Mwanzo 18:1-3, Mwanzo 32:24, na Yoshua 5:14)… Lakini hii ya udongo haiwezi kubadilika na kuwa ya viumbe wengine, mabadiliko ya miili ya udongo ni unene, wembamba na urefu basi, hivyo ni dhaifu sana..
Lakini pamoja na hayo yote, wanadamu tuliomwamini Bwana YESU na kumfuata tunayo ahadi ya kubadilishwa hii miili na kupewa kama ile ya Malaika watakatifu isiyo na kasoro, (miili ya kimbinguni).. na ahadi hiyo itatimia katika ile siku ya ufufuo kulingana na maandiko..
1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa”
1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa”
Soma pia Mathayo 22:30..
Sasa tukirudi kwenye swali! Je Malaika wana damu na nyama kama sisi wanadamu?, jibu tumeshapata kuwa HAPANA!, Kwasababu miili yao si ya duniani, inayohitaji oksijeni ili iishi, hivyo hawana damu na nyama.
Je umempokea BWANA YESU?.. Je unaishi katika ahadi hiyo ya kubadilishwa mwili katika siku ile?.. Kama upo nje ya KRISTO, na ikitokea umekufa, basi hutakuwa miongoni mwa watatakaofufuliwa na kuvikwa miili ya kimbinguni.
Bwana atusaidie tusiikose ile ahadi.
Ubarikiwe.
Nini Maana ya Adamu?
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
WEWE SI MALI YAKO MWENYEWE!
ZIDI KUTAFUTA UTAKASO WA MWILI.
Swali: Je Malaika watakatifu walioko mbinguni wanao uongozi, kama sisi wanadamu tulivyo na viongozi wanaotuongoza?.
Jibu: Kama vile sisi binadamu tulivyo na Uongozi duniani biblia inatuonyesha pia Malaika wanao uongozi mbinguni, maana yake wapo walio viongozi na wasio viongozi.
Kwa mfano tukisoma kitabu cha Ufunuo 12, tunaona Mikaeli anatajwa akiwa pamoja na malaika zake, hiyo ni kuonyesha kuwa Mikaeli ni kiongozi.
Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni”.
Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni”.
Soma pia Yuda 1:9, utaona Mikaeli anatajwa tena kama Malaika Mkuu..
Na pia wakati ule Yoshua anakutana na yule Malaika wa Bwana baada ya kuvuka Yordani, Malaika yule alijitambulisha kuwa ni AMIRI wa jeshi la Bwana…Sasa Amiri maana yake ni kiongozi wa jeshi.
Yoshua 5:13 “Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? 14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la BWANA. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? 15 Huyo amiri wa jeshi la BWANA akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo”
Yoshua 5:13 “Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?
14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la BWANA. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?
15 Huyo amiri wa jeshi la BWANA akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo”
Hivyo huyu Malaika alikuwa ni kiongozi wa Malaka wengine wa vita mbinguni, ndio maana akajitambulisha kama “Amiri”.
Lakini pamoja na kwamba upo uongozi katikati ya Malaika, hiyo bado haiwafanyi waabudiwe au wasujudiwe au kusifiwa.
Anayestahili kusifiwa na kusujudiwa duniani na mbinguni ni MUNGU peke yake.
Wakolosai 2:18 “Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, NA KUABUDU MALAIKA, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili”.
YESU KRISTO anarudi mwamini na mtumikie.
Shalom.