Category Archive Maana ya maneno

Vyusa ni nini? (Ayubu 41:7)

Ayubu 41:7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa?

Vyusa ni mikuki maalumu iliyoundwa kwa ajili ya kunasia samaki, ambayo wavuvi hutembea nayo, kuvizia samaki, hususani wale waliokaribia na kilele, kisha huwachoma kwa nguvu, na kuwavuta nje ya maji, na kwasababu ya ukali na mvuvi, na wepesi wa ngozi zao, mara nyingi mkuki ule hauwezi kunasuka mwilini mwao.

Sasa katika habari hiyo, ukianzia mistari ya juu hata katika sura nzima na zile zilizotangulia, ni Ni mahojiano kati ya Ayubu na Mungu, ambapo Mungu anamuuliza maswali Ayubu ayajibu, ni maswali ambayo mpaka sasa hayana majibu, mambo makuu ya Mungu na uweza wake usiofafanulika kwa ufahamu wa kibinadamu. Sasa moja ya mambo aliyokuwa anamuuliza Ayubu ni kuhusu, mnyama “Mamba”, kwa jinsi alivyomuumba kwa namna ya kipekee, tofauti na samaki wengine, Anamweleza  jinsi alivyo jasiri, asiye na woga, anamuuliza Ayubu je unaweza kutupa ndoano yako ukamvua kama vile ufanyavyo kwa samaki wengine?(Ay 41:1).

Kwa jinsi magamba yake yalivyo magumu, anasema hata upanga ukipita juu yake haumwingii..

41:26 Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.

Ndio hapo sasa mbeleni anasema tena, je! Je unaweza kukitoba kichwa chake kwa vyusa, kama vile ufanyavyo kwa sangara, na perege? Si itakuwa sawa na unautoboa ukuta na chelewa.

Mungu kwa urefu ameeleza sifa zake mnyama huyu katika sura yote ya 41 (japo kimsingi alikuwa anamwelezea Kristo Yesu, kwa mfano wa wanyama), akimfananisha na mnyama huyu jinsi alivyokuwa thabiti kiasi kwamba hakukuwa silaha yoyote ya adui iliyompata, na jinsi alivyotisha na kuwa na nguvu za kushinda hata mauti..

Kwa uerfu wa habari hiyo fungua hapa usome>>>> SIFA ZA MAMBA YULE MKUBWA WA AYUBU.

Je! Umempokea mfalme huyu moyoni, mwenye nguvu za kutisha, asiyetikiswa na kitu chochote?. Kumbuka wokovu ni kwa faida yako mwenyewe, hakuna njia unaweza ukamshinda adui, kama Kristo hajakuficha ndani yake. Utavuliwa tu na adui kama samaki dhaifu, lakini uwapo ndani ya Kristo hakuna awezaye kukuvua. Ikiwa upo tayari kuyasalimisha maisha yako kwa Bwana Yesu..wasiliana na sisi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii.

Pia kwa maana za maneno mengine ya kwenye biblia fungua hapa >>>> Maana ya Maneno Kwenye Biblia

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Madongoa ni nini? (Ayubu 7:5)

Nini maana ya Selahamalekothi?

Ayubu alimaanisha nini kusema ‘nami nitarudi tena huko uchi vilevile;?

Print this post

Nini maana ya ‘kupelekea mkono’ (Esta 2:21)

SWALI: Nini maana ya “kupelekea mkono” kama ilivyotumika kwenye maandiko. Esta 2:21

Esta 2:21

[21]Ikawa siku zile, Mordekai alipokuwa akiketi mlangoni pa mfalme, wawili katika wasimamizi wake mfalme, Bigthana na Tereshi, wangoje mlango, walighadhibika, wakataka kumpelekea mikono mfalme Ahasuero.

JIBU:

Kupeleka Mkono, ni neno linalomaanisha “kutaka kudhuru”. Kwamfano katika hiyo habari tunaona Mordekai kama msimamizi wa malangoni pa mfalme aligundua njama za watumishi wenzake wengine ambao walitaka kwenda kumuua mfalme..hatujua aidha kwa kumwekea sumu, au kumchoma upanga, au hatua nyingine yoyote ilitayo madhara.

Kitendo hicho kibiblia, huitwa “kupeleka mkono”

Tunaweza kuona jambo lingine kama hilo, wakati fulani Daudi alimkaribia sana mfalme kwa kiwango ambacho angeweza kumuangamiza kama angetaka..lakini akasema nisinyoshe mkono wangu kwa masihi wa Bwana. Maana yake nisimuue.

1 Samweli 24:4-7

[4]Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia BWANA, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yo yote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri.

[5]Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.

[6]Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA. 

[7]Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaache kumwondokea Sauli. Kisha Sauli akatoka pangoni, akaenda zake.

Bwana akubariki..

Je umempokea Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako?

Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo.. basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii.. Pia kufahamu tafsiri ya maneno mengine ya kibiblia tazama chini.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ESTA: Mlango wa 1 & 2

Uchambuzi wa kitabu cha kwanza cha Paulo kwa Timotheo (1Timotheo)

Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?

Print this post

Kuseta ni nini?

Kuseta kama ilivyotumika kwenye maandiko maana yake ni kukiharibu kitu, aidha kwa kukiponda, kukikanyaga, au Kukivunja vipande vipande.

Kwamfano kwenye maandiko kama haya tunaweza kuona neno hilo..

Warumi 16:19-20

[19]Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.

[20]Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]

Hapa Mungu anaonyesha kwamba pale tunapokuwa mbali na mambo mabaya ndivyo anavyomponda shetani chini ya miguu yetu..

Kuonyesha kuwa njia kuu ya kumshinda shetani sio kumkemea bali ni kujitenga na mambo maovu.

Vifungu vingine ni kama hivi..

Zaburi 110:5

[5]Bwana yu mkono wako wa kuume;  Ataseta wafalme,  Siku ya ghadhabu yake.

Hapa Mungu anaonyesha ukali wa ghadhabu yake juu ya watu waovu..hata wale wanaoonekana ni wakuu, hawataikwepa hasira yake atawaharibu kwa kuwaponda- ponda.

kwa hitimisho ni kuwa kuseta ni kuharibu kabisa Kabisa ..Na Mungu amekusudia kufanya hivyo sio kwetu bali kwa shetani… Ni sisi tu kuishi maisha yanayomlingana yeye ikiwa tayari tumeshaokoka…Lakini ikiwa ni kinyume na hapo tutaingia katika mkondo huo huo wa shetani, wa kuharibiwa endapo hatutamwamini Yesu Kristo leo.

Je upo tayari kumpokea Yesu leo? Kama ni ndio basi bofya hapa >> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MWEKE SHETANI MBALI NA WEWE.

SI SHETANI BALI NI WEWE. (CHAGUA MEMA)

DANIELI: Mlango wa 2

Print this post

Nini maana ya Selahamalekothi?

Ilikuwa ni desturi ya wayahudi kuyapa majina, maeneo yote ambayo walikutana na Mungu kipekee.

Kwamfano Yakobo alipokutana na Mungu mahali fulani palipoitwa Luzu, kwa kuona maono yale ya ngazi kushuka kutoka mbinguni, na malaika wanashuka na kukwea, hakuondoka hivi hivi bali alipaita mahali pale Betheli yaani ‘ nyumba ya Mungu’ (Mwanzo 28:10-22).

Sehemu nyingine Mungu alipowasaidia Israeli kuwapiga wafilisti kwa kishindo kikubwa, Samweli alilisimamisha jiwe na kuliita Eneb-ezeri akimaanisha ‘hata sasa Bwana ametusaidia’ na 1Samweli 7:12.

Hivyo pia tukisoma kisa cha Mfalme Sauli na Daudi, tunaona mara nyingi Daudi alipowindwa ili auawe alifanikiwa kumtoroka Sauli, lakini upo wakati ambao alihusuriwa pande zote, Daudi akawa hana namna isipokuwa kungojea tu kuuliwa palepale pangoni, sasa wakati ambapo Sauli amemkaribia sana Daudi. Taarifa za ghafla zilimfikia na kuambiwa kwamba wafilisti wamevamia Israeli, hivyo ikambidi aache kumfuatilia Daudi arudi Israeli kupambana na adui zake.

Sasa tendo hilo la wokovu halikumwacha Daudi awe vilevile kinyume chake, alipaita mahali pale Selahamalekothi

1 Samweli 23:26-28

[26]Sauli akaenda upande huu wa mlima, na Daudi na watu wake wakaenda upande huu wa mlima; naye Daudi akafanya haraka sana kwenda zake kwa hofu ya Sauli; kwa sababu Sauli na watu wake wakamzunguka Daudi na watu wake ili kuwakamata.

[27]Lakini akaja mjumbe kwa Sauli, kusema, Njoo upesi, kwa kuwa Wafilisti wameishambulia nchi.

[28]Basi Sauli akarudi kutoka kumwinda Daudi, akaenda kinyume cha Wafilisti; kwa hiyo wakapaita mahali pale, Selahamalekothi.

Selahamalekothi ni neno la kiebrania lenye maana ya MWAMBA WA KUTOROKEA.

Daudi na watu wake walipaita mahali pale hivyo kufuatana ba jinsi Mungu alivyowaepusha na mkono wa Sauli, kwa njia isiyodhaniwa/ kutegemewa hata kidogo.

Ni kwanini wayaite majina maeneo hayo?

Ni Ili kuendelea kukumbuka matendo makuu Mungu aliyowatendea wasizisahau wafidhili zake kabisa.

Je na sisi ni alama gani tunaacha mahali ambapo tunamwona Mungu ametutendea makuu. PENDA kuandika shuhuda zako, ili wakati ujao zikusaidie kukumbuka fadhili za Mungu umshukuru.

Kikawaida Mungu huwa anatufanyia maajabu mengi Sana kila siku, lakini tunakuwa wepesi kuyasahu, ni vema tujifunze kwa namna yoyote kutunza kumbukumbu, hata kama si kwa kuandika lakini kwa njia zozote zile, mfano wa mababa zetu hawa.

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Pango la Makpela ni lipi, je lina umuhimu wowote kwetu?

HII NDIO TABIA YA WATU WA KEILA, USIIGE

SIKU YA HOFU YANGU NITAKUTUMAINI WEWE.

Print this post

Theofania ni nini?

Theofania ni neno la kiyunani lenye muunganiko wa maneno ya mawili “theos (Mungu)” na “faino (kuonekana)”. Hivyo ukiunganisha linazalika neno “kuonekana kwa Mungu”

Theofania sio kuonekana kwa Mungu katika ule utimilifu wake wote, hapana, kwasababu maandiko yanasema hakuna mtu awezayo kumwona Mungu akaishi (Kutoka 33:20). Hivyo Theofania ni njia mbadala (isiyo ya moja kwa moja) ambayo Mungu  aliitumia kujitokeza na kuongea na watu, kuthibitisha agano lake, au kuwapa maagizo.

Mfano wa njia hizo,

> Ni kijiti cha moto, alichotumia kuzungumza na Musa kule jangwani. (Kutoka 3)

> Mtu Yule aliyeshindana na Yakobo mweleka (Mwanzo 32:24-30)

> Melkizedeki (Mwanzo 14: 18-20)

> Yule mtu wanne aliyewatokea Shedraka, Meshaki na Abednego ndani ya moto (Danieli 3)

> Nguzo ya moto na wingu jangwani (Kutoka 13:21-22)

> Mungu kumtokea Samweli  (1Samweli 3:10)

> Maono ya Ezekieli (Ezekieli 1)

Je! theofania ipo hadi sasa?

Yesu Kristo alipozaliwa katika mwili, sio tena theofania, Bali ni utimilifu wote wa Mungu katika mwili.

Wakolosai 2:9 Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.

Hapo mwanzo watu hawakumwona Mungu katika utimilifu huo, kwasababu kama wangemwona Mungu wangekufa kwasababu ya dhambi. Lakini Kristo alipokuja kuondoa dhambi kwa damu yake, wanadamu wote tunamwona Mungu katika utilimilifu wote, kwa Roho Mtakatifu aliyemweka ndani yetu.

Tunakikaribia kiti cha rehema, na neema kwa ujasiri bila kufa kama kule mwanzo, kwasababu damu ya Yesu inanguvu ya kuzificha dhambi zetu zote. Ukimwona Kristo(moyoni) umemwona Mungu (Yohana 14:6-11)

Ndio maana ni kwanini leo hii mtu huwezi kumfikia Mungu bila Yesu Kristo.

Okoka leo upokee neema hii, ikiwa upo tayari kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya toba. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Theolojia ni nini?. Na je ni sahihi kuisoma?

Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?

NINI TUNAJIFUNZA KWA THEOFILO MTUKUFU?

Print this post

Wanethini ni watu gani kwenye biblia?

Wanethini ni kundi la watu ambao walitumika katika hekalu, ambao sio asili ya wayahudi. Wanatajwa sana kwenye kitabu cha Nehemia na Ezra. Maana ya neno ‘Nethini’  kwa kiyahudi linamaanisha “waliotolewa”. Wakimaanisha watu waliotelewa kuwasaidia walawi katika shughuli za hekaluni.

Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyowataja;

Ezra 8:20 na katika Wanethini, ambao Daudi, na wakuu, walikuwa wamewaweka kwa ajili ya utumishi wa Walawi, Wanethini mia mbili na ishirini; wote wametajwa kwa majina yao.

Nehemia 7:73 Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao. Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Israeli walikuwa wakikaa katika miji yao.

Soma pia, (Ezra  2:43, 2:58, 7:24)

Asili yao:

Biblia haituonyeshi moja kwa moja asili yao ni wapi, lakini wanazuoni wengi huamini walitokea katika chimbuko la wale wagibeoni waliowadanganya Israeli wakati ule mpaka wakafanya nao maagano, Ambao Yoshua aliwapa kazi ya kupasua kuni, na kuteka maji.

Yoshua 9:27 Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua

Mbali na hawa wagibeoni wengine wanaweza wakawa ni wageni au mateka., ambao baadaye wakaja kuwekwa kwenye utumishi wa hekaluni.

Kazi yao:

Wanethini hawakufanya kazi zozote za kikuhani, ikumbukwe kuwa ilikuwa ni kosa, mtu ambaye sio myahudi tena wa kabila la Lawi kufanya shughuli zozote za kihekalu, Hawa walikuwa wanafanya kazi za usaidizi ule wa nje, kama vile kutweka maji, kukusanya kuni, usafi, na kazi nyingine zilizohitaji msaada wa pembeni.,Ili kuwaruhusu walawi wasilemewe  wajikite zaidi katika kazi za hekaluni.

Maandiko yanaonyesha walikuwa na makao yao maalumu palipoitwa Ofeli kule Yerusalemu karibu na hekalu (Nehemia 3:26)

Hata Baadaya ya uhamisho wa Babeli, tunaona mabaki yaliyorudi Israeli kufanya shughuli za kihekalu, hawa wanethini pia walirejea

Kwa ufupi wanethini walikuwa ni la watu (wasio-wayahudi) waliowekwa kwa ajili ya kusaidia shughuli za hekaluni.

Kwanini Bwana aruhusu jambo hili?

Licha ya kwamba Mungu ameliita kanisa lake na amelitenga, limtumikie lenyewe katika shughuli zote za kimadhabahu. Lakini Bado Bwana anaweza kunyanyua watu wengine nje ya kanisa, kusaidia kanisa kusonga mbele. Mfano wa hawa ni Yule akida wa kirumi ambaye alilipenda taifa la Israeli na  kulijengea sinagogi (Luka 7:1-5). Hakuwa myahudi lakini aliwasaidia wayahudi.

Hata sasa wanethini wapo wengi, hawapaswi kuzuiliwa, endapo wanasaidia kanisa au kazi ya Mungu, kwasababu ni Bwana ndiye aliyewavuta.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

Nini maana ya neno kumwamba (Zaburi 78:19)

Zaburi 78:18-19

[18]Wakamjaribu Mungu mioyoni mwao Kwa kutaka chakula kwa tamaa zao. [19]Naam, walimwamba Mungu, wakasema, Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani? 

Kumwamba kama ilivyotumika hapo ni “kuzungumza kinyume”

Hivyo hapo anaposema 

“Naam, walimwamba Mungu, wakasema, Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?”

Ni sawa na kusema..

Naam, walizungumza kinyume na Mungu, wakisema Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?

Wana wa Israeli kule jangwani, vinywa vyao havikuwa vya shukrani au vya kuomba, bali vivywa vya kumjaribu Mungu na manung’uniko, ijapokuwa walijua uweza wake wote, lakini walijifanya kama Mungu wao hawezi kuwaokoa, wakawa wanauliza maswali yaliyoonekana magumu, kumbe nafsini mwao wanajua yote yanawezekana, wanafanya tu makusudi ili waone Yehova atafanya nini. Na ndio sababu iliyomfanya Mungu asipendezwe nao.

Na sisi pia tusiwe watu wa kumwamba Mungu, kwa kusema maneno ya kutoamini.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

Kama Musa aliandika vitabu vya torati, Je! kifo chake alikiandikaje mule?

BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.

Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?

Rudi Nyumbani

Print this post

msalaba ni nini.

Msalaba ni kipande cha mti, kilichochongwa kwa kupishanishwa na kingine kwa juu. chenye lengo la kumuulia mwanadamu kwa kifo cha mateso.

Tofauti na sasa, ambapo adhabu nyingi za kifo kwa mataifa mbalimbali huwa ni kunyongwa, au kupigwa risasi, au kuwekwa kwenye kiti cha umeme, n.k.. Lakini katika falme za zamani watu waovu kupita kiasi, kwamfano wauaji, au wenye makosa ya uhaini, adhabu yao, ilikuwa ni kutundikwa au kugongelewa pale msalabani mpaka ufe. Ni mateso ambayo utataabika hapo kwa saa nyingi sana kabla ya kufa, hata siku mbili.

Hivyo kwa lugha rahisi tunaweza kusema msalaba ni chombo cha kuulia mtu.

Kwetu sisi tuliomwamini Kristo. Msalaba ni ishara kuu ya ukombozi tulioupata kwa kifo cha mwokozi wetu. Kufahamu kwa undani ni kwanini fungua link hizi; usome..

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

Nini maana ya sulubu/ sulubisha?

nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> 

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.


Mafundisho mengine:

Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?

Je! msalaba kaburini una umuhimu wowote?

Print this post

Simo ni mtu gani? (Ayubu 17:6).

Swali: Simo ni nini, au ni nani kama tunavyosoma katika Ayubu 17:6.

Jibu: Tusome mistari hiyo mpaka ule wa saba (7).

Ayubu 17:6 “Amenifanya niwe simo kwa watu; Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi. 

7 Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli”

Neno hili “Simo” linasomeka tena katika Ayubu 30:9.

Ayubu 30:9 “Na sasa mimi nimekuwa wimbo wao, Naam, nimekuwa simo kwao

10 Wao hunichukia, na kujitenga nami, Hawaachi kunitemea mate usoni”.

Na maana ya neno hilo (simo) ni “MTU ANAYEDHARAULIKA”

Wakati Ayubu mtumishi wa MUNGU anapitia yale majaribu ya kufiwa na wanawe na kupoteza mali zake zote, na zaidi ya yote kupitia matatizo ya kiafya, ile fahari yake yote iliisha na kusababisha watu wengi kumdharau ikiwemo mke wake, mpaka hatimaye naye kuliona hilo na kusema hayo maneno.

Lakini pamoja na kuwa SIMO mbele ya watu, kwa MUNGU alikuwa LULU kubwa sana, kwani majaribu yale hayakuwa kwasababu ya yeye kumwacha MUNGU bali ni kwasababu ya yeye kumkaribia Mungu zaidi, na wakati ulipofika alipata mara mbili, ya alivyovipoteza na miaka mingi zaidi ya kuishi (Ayubu 42:12-16).

Na sisi tunajifunza mambo hayo hayo, kuwa tujaribiwapo kwaajili ya haki tuna heri…

Lakini tupitiapo majaribu mfano wa yale ya Ayubu tukiwa katika dhambi, tunapaswa tujifikiri mara mbili, kwani huenda ni mapigo na laana kutoka kwa Mungu ili tutubu na si kwa lengo la kuzijaribu imani zetu kama Ayubu.

Ndivyo Neno linavyoma katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 28.

Kumbukumbu la Torati 28:15-16,37-39 “Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. 

16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. 

37 Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA. 

38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila. 

39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?

Kwanini Mungu alimkataa Sauli? (1Samweli 15:23)

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

Rudi Nyumbani

Print this post

Neno Siuze linamaanisha nini kwenye biblia?

Siuze ni ‘Sembuse’, kwa uandishi mwingine.

Kwamfano mtu anaposema kauli hii

 “Kama Bwana Yesu alikuwa mwombaji siuze mimi, kuzidi hapo?


.Ni sawa tu  na kusema “Kama Bwana Yesu alikuwa mwombaji sembuse mimi, kuzidi hapo?

Maana ya Neno hilo ni. “Si zaidi

‘Kama Bwana alikuwa mwombaji si zaidi mimi kuzidi hapo’.

Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu ambavyo utalisoma neno hili kwenye biblia;

 

2 Mambo ya Nyakati 6:18

[18]Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga! 

 

2 Wakorintho 3:9

[9]Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi. 

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Neno vuruvuru linamaanisha nini katika biblia?

Nini maana ya mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe? (Mathayo 24:35).

Kuna Mbingu ngapi?

Rudi Nyumbani

Print this post