Bwana alimaanisha nini katika Mathayo 5:20 aliposema..
[20]Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Ni haki ipi hiyo.
JIBU: Katika andiko hilo tunaona Bwana akiainisha kigezo cha mtu kuingia kwenye ufalme wa Mungu..kwamba kigezo chenyewe ni “HAKI” …
Haki ni kitu kinachomstahilisha mtu kupokea kitu fulani. Kwamfano tunasema mtoto ana haki ya kulindwa…ikiwa na maana kilichomsababishia apate haki ya kulindwa ni ile hali ya utoto wake.
Mfano mwingine, tunasema ni mtu mzima ana haki ya kuoa au kuolewa na mtu amtakaye, katika wakati auchaguaye yeye. Tafsiri yake ni kwamba kinachompa haki ya kuwa hivyo ni kwasababu yeye ni “mtu-mzima”. Angekuwa mtoto asingekuwa na haki hiyo.
Sasa tukirudi katika habari hiyo tunaona kilichowafanya waandishi na mafarisayo wajihesabie haki kwamba wao ni warithi wa ufalme wa mbinguni. Ilikuwa ni kuitimiza sheria kwa matendo yao. Ambayo kimsingi wao wenyewe hawakuweza kuishika..kwa nje walionekana sawa lakini ndani walikuwa mbali na sheria yao. Kwasababu hakuwahi kutokea mtu hata mmoja aliyeweza kumpendeza Mungu kwa matendo yake, yeye mwenyewe.
Hivyo njia yao ya kupata haki, ambayo ni kwa matendo ya sheria haikuwa sawa. Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake na wale waliomsikia kwamba haki “ yao” isipozidi ya mafarisayo na waandishi kamwe hawataweza kuuingia ufalme wa mbinguni.
Swali je ya kwao inapaswa iweje. Je ya matendo ya sheria zaidi ya yale au vinginevyo?
Haki Yesu aliyoileta ambayo itampelekea mtu kurithi uzima wa milele ni kwa njia yake yeye mwenyewe .Ambayo sisi tunahesabiwa haki kwa kumwamini, kama mwokozi wa maisha yetu. Bila kutegemea matendo yetu ya haki. Yaani ni haki tuipatayo kwa neema.
Hivyo, wote wanaoipokea haki hiyo basi uzima wa milele ni wao. Na kwasababu ndio njia ambayo sisi tutamfikia Mungu. Basi neema yenyewe inatufundisha pia kuyazaa matunda ya Roho. Na hivyo tunaitimiza sheria ya Mungu mioyoni mwetu bila unafiki. Mbali na mafarisayo ambao walitegemea akili zako na nguvu zao.
Hata sasa ikiwa unategemea jitihada zako, zikupe haki mbele za Mungu, ndugu umepotea. Hutaweza Itegemee neema ya Mungu. Na hiyo itakusaidia kuyatimiza hayo mengine kwa Roho Mtakatifu.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.
FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.
Swali: Mafuta Mabichi yapoje, na yanafunua nini kiroho?
Jibu: Tureje..
Zaburi 92:10 “Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa MAFUTA MABICHI”.
Mafuta mabichi yanayozungumziwa hapo si mafuta ambayo hayajapitishwa kwenye moto yakaiva na kuchemka… La!.. bali ni mafuta yaliyo mapya (yaani freshi) ambayo yayajakaa muda mrefu.
Nyakati za biblia na hata sasa wayahudi wanatumia mafuta ya Mizeituni kwa matumizi ya chakula na ibada.
Asilimia kubwa ya vyakula vya wayahudi na baadhi ya jamii za mashariki ya kati wanatumia mafuta ya Mizeituni kama kiungo cha mboga, na wakati jamii nyingine mbali na hizo wanatumia mafuta ya Alizeti au mimea mingine katika mapishi.
Chakula kilichoandaliwa kwa mafuta mabichi (yaani mapya) ya Mizeituni kinakuwa ni kitamu na chenye ladha… utaona hata ile MANA jangwani, ladha yake ilifananishwa na ladha ya mafuta mapya. (soma Hesabu 8:11).
Vile vile katika shughuli za kiibada, pale ambapo mtu anatawazwa kuwa mfalme basi alipakwa Mafuta haya ya mizeituni kama ishara ya kuruhusiwa kuchukua madaraka hayo,
1Samweli 9:15 “Basi Bwana alikuwa amemfunulia Samweli, siku moja kabla Sauli hajamwendea, akisema,
16 Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, NAWE MTIE MAFUTA ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia”
Soma pia1Wafalme 16:12, 1Wafalme 1:34, na 1Wafalme 19:15-16 utaona jambo hilo hilo..
Vile vile makuhani walitiwa mafuta kama ishara ya kuchaguliwa na Mungu kutumika katika nyumba yake.
Zaburi 133:2 “Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake”.
Sasa ilikuwa ni heshima na jambo jema kutiwa mafuta ambayo ni mapya.. Kwani Mafuta ya Mizetuni kama yamehifadhiwa vizuri yanadumu kwa miaka 2 tu, ukipita huo muda yanaharibika na kutoa harufu nyingine. Kwahiyo chakula kilichoandaliwa kwa mafuta yaliyokaa kinakuwa hakina ladha na pia kinatoa harufu mbaya…
Vile vile mtu aliyepakwa mafuta yaliyokaa sana au kuharibika si jambo la utukufu… lakini mafuta mabichi ilikuwa ni jambo la utukufu kwasababu ni freshi.
Sasa mafuta mabichi (yaani mapya) na yale yaliyokaa (yaani ya zamani) yanawakilisha nini sasa kiroho?..
Mafuta yanamwakilisha ROHO MTAKATIFU. Hivyo mafuta yaliyokaa (ya zamani) yanawakilisha utendaji kazi wa Roho Mtakatifu katika Agano la kale… na Mafuta mapya ni utendaji wa ROHO MTAKATIFU katika agano jipya.
Na sisi tunayahitaji mafuta mabichi katika UTUMISHI WETU, na si yale yaliyokaa… kwasababu hayatatufaa sana..
Mafuta mapya yanatufundisha kuwa wakamilifu zaidi na katika kuyafanya mapenzi ya Mungu..kuliko yale ya zamani.
Mathayo 5:27 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu”.
Je umempokea YESU KRISTO, aliye mjumbe wa Agano jipya?, kumbuka huwezi kuwa na ROHO MTAKATIFU, kama YESU KRISTO hayupo ndani ya maisha yako.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza
Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi?
MAANA YA KRISTO/ JINA KRISTO LINA MAANA GANI?
Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?
Swali: Je ni kweli kwamba kiganja cha mkono wa kushoto au wa kulia kikiwasha basi ni ishara ya kupata pesa?
Jibu ni LA!.. hakuna uhusiano wowote kiganja kuwasha na fedha kumjia mtu. Labda kama mtu huyo ana pepo la utambuzi ndani yake..
Kama mtu ana pepo la utambuzi basi anaweza kuhisi kitu Fulani kikimjia, ikiwemo pesa kutoka katika chanzo kisicho cha kiMungu, au akahisi hatari kutoka katika upande wa maadui zake (maana yake upande wa Mungu), na ishara hizo anaweza kuzihisi kwa njia kama hizo za kuwashwa mkono, au kuwashwa sehemu nyingine ya mwili.
Lakini mtu mwenye Roho wa Mungu hisia zake zipo katika Neno la Mungu..Anaposoma Neno la Mungu na kudumu katika uwepo huo basi anaweza kuhisi Baraka zijazo, au hatari ijayo.
Kwamfano Neno hili katika biblia linaweza kukupa hisia za Baraka zijazo…
Mithali 13:11 “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”.
Mtu akilisoma hili Neno la kulishika, tayari atakuwa anajua ni nini kitafuta katika shughuli anayoifanya.. lakini si kukisikilizia kiganja kinasema nini!.. Na maneno mengine yote ya Mungu ni hivyo hivyo..
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba, Elimu ya kusoma viungo vya mwili na kutabiri mambo yajayo ni elimu ya adui na ya kupotosha..
Lakini pia kumbuka si kila anayewashwa mkono basi ana pepo la utambuzi!.. La!, mkono unaweza kuwasha kwa sababu nyingine yoyote ya kibaolojia, na mtu asiwe na pepo!.. (Hata hivyo asilimia kubwa ya wanaowashwa mikono hawana mapepo). Hivyo kilicho kikubwa na cha msingi ni kudumu katika Neno la Mungu.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?
Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)
Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).
SWALI: Naomba kufahamu nini maana ya Isaya 40:12 inaposema maji kwa konzi ya mkono, na mbingu kwa shubiri?
Isaya 40:12 “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani”?
JIBU: Ukianzia kusoma vifungu vya juu na kuendelea vile vya chini, utaona Mungu anawaambia watu wake Israeli kuwa atawajilia kama mchungaji awachungaye kondoo wake , na kuwalisha, na kuwakuongoza, na kuwakusanya kifuani mwake, hata wale walio wachanga, ndivyo atakavyowatendea watu wake na hilo litawezekana.
Lakini Israeli waliona kama jambo hilo linaweza lisiwe rahisi, Ndio hapo akawaambia sasa katika vifungu vifuatavyo maneno hayo. Kwamba “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake”? Maji anayoyazungumzia hapo ni maji mengi, mfano wa bahari, na maziwa Je! Kuna mtu yeyote anayeweza kuyakusanya maji mengi namna hiyo kwenye viganja vyake? Jibu ni hapana! Lakini kwa Mungu ni jambo dogo sana.
Vilevile anawauliza ni nani awezaye ‘kuzikadiri mbingu kwa shubiri’?. Shubiri ni kipimo cha urefu, wa kiganja, toka kidole gumba mpaka kile cha katikati vinaponyooshwa. Na ni wazi hakuna mtu anayeweza kupima ukubwa wa mbingu, toka sayari moja hadi sayari nyingine, kwa kipimo chochote kile cha kibinadamu. Lakini kwa Mungu hilo ni jambo dogo sana, ni kama kuzipima kwa shubiri.
Halikadhalika anauliza ni nani awezaye kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi?. Pishi ni kopo dogo, je kuna mwanadamu anaweza kuyakusanya mavumbi yote duniani, kama vile akusanyavyo yale machache kwenye kopo lake. Ni wazi hakuna awezaye kuwa na pipa la uwezo huo.
Vilevile anauliza ni nani anayeweza kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?. Je! Kuna mizani yoyote ya kibinadamu inaweza kuiweka milima juu yake, na kutoa vipimo?. Jibu ni hakuna. Lakini kwa Mungu ni jambo dogo sana. Milima ni kama vipunje vidogo sana vya mchanga.
Ikiwa haya yanaonekana magumu kwa mwanadamu, lakini kwa Mungu ni mepesi. Vivyo hivyo jambo la kuwakusanya watu wake, au kuwasaidia, lisitizamwe kibinadamu, kwasababu uweza wa Mungu ni mkuu sana usioweza kufikirika kibinadamu. Maswali ya namna hii ndio kama yale Mungu aliyokuwa anamuuliza Ayubu, (Ayubu 38-41), na katika Mithali 30:4
Yesu kama mchungaji wetu mkuu, anauwezo wa kutukusanya kama kondoo wake. Haijalishi tutaonekana tumetawanyika mbali kiasi gani, lakini akisema jambo ni lazima liwe. Halikadhalika na katika mambo yetu yote ya kiroho na kimwili.
Hivyo kitabu cha Isaya sura ya 40 yote, kinaeleza uweza wa Mungu, usiopomika kibinadamu. Lakini Swali ni Je! Kristo amekusamehe dhambi zako? Kama ni la! Basi nafasi bado unayo leo. Mwamini yeye akuokoe. Na kukupa ondoleo la dhambi zako.
Kwa mwongozo wa namna ya kupokea wokovu basi fungua hapa>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Nini maana ya mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe? (Mathayo 24:35).
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
SWALI: Naomba kufahamu maana ya 1Wakorintho 4: 7
Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?
JIBU: Ukianza kusoma tokea sura ya kwanza utaona Paulo, anakemea sana baadhi ya tabia ya matengano ambayo ilionekana katika kanisa hili la wakorintho. Iliyozuka kutokana na aina ya mafundisho au utendaji kazi wa waasisi wa huduma, au waliowabatiza, na sana sana kati ya Paulo na Apolo.
Hivyo matabaka haya yakawafanya wajivunue wanadamu, na mafundisho yao. Bila kufahamu kuwa kanisa ni la Kristo na si la wanadamu.
Ndipo Paulo, akaweka wazi kuwa kila mmoja aliitwa kwenye utumishi wa Kristo Yesu, ambao una mchango wake katika kanisa, lakini si kwamba huduma ya mmoja ni bora kuliko nyingine. Akasema mmoja anapanda mwingine anatia maji, lakini mkuzaji ni Mungu.
Sasa katika vifungu hivi anaendelea kuwaambia tabia ya kupambanua watumishi, au huduma, si sawa. Ndio hapo anasema “Nawe una nini usichokipokea?”. Akiwa na maana je! Kuna kipawa gani, au kitu gani chema katika kanisa ambacho hawakukipokea kutoka kwa Mungu,?
Lakini anasema..
“Iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?. Yaani kama vyote vilitoka kwa Mungu na sio kwa wanadamu, mbona basi mnajisifia kana kwamba vimekuja kwa uweza wa kibinadamu?.
Kama tumepewa kwa neema iweje sasa tujisifie, kana kwamba tumevipokea kwa nguvu zetu na utashi wa watumishi wetu, na ukuu wao, na uwezo wao wa kuhubiri vizuri? Karama hizi za rohoni hakuna hata mmoja imetoka kwa mwanadamu, wenyewe wamefanyika vyote tu. Hivyo wa kujivunia hapo na kusifiwa hapo ni Mungu wala si Paulo au Apolo.
Jambo ambalo hata leo huonekana kwa baadhi ya watu wa kanisa la leo. Ikiwa tuna msingi katika Kristo, iweje kujivunia makanisa au huduma, na kujiona sisi ndio bora zaidi ya wale wengine?
Ni kweli zipo huduma ambazo si za kweli, hazina msingi sahihi wa Kristo Yesu. Lakini ikiwa wote Injili yetu ni ya Kristo aliyesulubiwa kutukomboa sisi, basi tofauti za kiutendaji kazi, au kiujuzi, zisitufanye tujione bora, kwasababu sio hao wanadamu walitoa hivyo vipawa bali ni Roho Mtakatifu. Na anatenda kazi kama apendavyo yeye, anampa huyu hiki, anampa Yule kile.
Mmoja atapanda, mwingine atatia maji, mwingine mbolea, mwingine mvunaji, lakini atakuzaye ni Mungu mmoja, katika shina la Yesu Kristo Bwana wetu.
Kama mkristo ukijiona una vita vya kiuhuduma, ujue bado ni mchanga kiroho, bado unatabia za mwilini.
Bwana atusaidie.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
SWALI: Biblia inamaana gani inaposema “Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango”.
Yakobo 5:9 Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
JIBU: Neno la Mungu halitoi nafasi ya sisi, kunung’unikiana kwasababu yoyote. Aidha ya kuonewa, au kudhulumiwa, kuaibishwa au kufanyiwa jambo ambalo halikupasa utendewe, Manung’uniko ni zao la kutokuwa na uvumilivu. Na kwamba tukifanya hivyo basi, tafsiri yake ni kuwa tunamfanya Mungu naye aghahiri uvumilivu wake kwetu.
Lakini anatoa, suluhisho, kwamba hayo tuyaache mikononi mwake. Kwasababu yeye ndio mwamuzi wetu. Na kwamba, sio tu mwamuzi lakini ni mwamuzi ambaye yupo mlangoni. Akiwa na maana kuwa Kristo yupo karibu sana na maonevu, au dhuluma hizo, na kwamba yeye mwenyewe atalipa, wala hatakawia, kwasababu yupo mlango.
Atalipa aidha kwa wakati huu huu duniani, au siku ile ya mwisho wa Hukumu. Kwake yeye ni lazima haki itendeke. Pia kwa upande mwingine anataka uogope kwasababu ukinung’unika yeye hayupo mbali kukusikia.
Wafilipi 4:5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa, popote tusimamapo kutoa malalamiko, laumu, kuhesabu makosa, n.k. basi tutambua kuwa Kristo yupo hapo hapo katikati yetu kutusikia. Hivyo tusiwe wepesi ya kunena, bali tujifunze kuwa wavumilivu katika mambo yote. Ili Mungu atuachilie neema yake.
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka? Je, umebatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo? Kama ni hapana, basi wakati ndio huu, tubu dhambi zako, kwa kumwamini Yesu upokee ondoleo la dhambi zako, Na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.
Ikiwa upo tayari kumkabidhi leo maisha yako. Basi fungua hapa kwa mwongozo huo. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Je! Umejengwa kweli juu yake?
Ukimuuliza mtu, mwamba ni nini, ni rahisi kukujibu YESU. Jibu ambalo ni sahihi, maandiko yanatuthibitishia hilo Yesu kuwa Yesu ni mwamba (Mathayo 21:42, 1Wakorintho 10:4). Lakini lazima ufahamu pia MWAMBA mwenye anasemaje, kuhusu yeye mwenyewe alivyo.
Ni maneno ambayo tunayasoma lakini si rahisi kuyatafakari kwa ukaribu, embu tusome tena, halafu utaona mwamba alimaanisha nini. (Zingatia vifungu vilivyo katika herufi kubwa) Soma kwa utulivu.
Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na KUYAFANYA, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu ASIYAFANYE, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
28 Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.
Umeelewa? Vema hayo maneno?
Kumbe mtu yeyote anayesikia maneno ya Yesu. Hapo hapo huwa anaanza ujezi.
Lakini tofauti inakuja mahali anapokwenda kujengea,. Yule aliyejenga kwenye mchanga tafsiri yake Yesu anasema, anasikia, lakini hayatendei kazi (Hayafanyi), aliyoyasikia. Hivyo hapo Mchanga, ni KUTOTENDA.
Lakini Yule mwingine aliyekwenda kwenye mwamba tafsiri yake ni anasikia lakini pia anatenda. Hivyo MWAMBA, ni kutenda.
Mwamba sio kumjua Yesu ndugu, mwamba sio kusoma sana biblia na kujua mafumbo na siri zote zilizo katika biblia, mwamba sio kujua kujua tafsiri zote za kigiriki na kiebrania kwenye maandiko, mwamba sio kujua kufundisha vema biblia,.. Sio hivyo vyote.
Mwamba ni KULITENDEA KAZI NENO, Unalolisikia kwake. Hilo tu. Sio kumjua Yesu.
Hatari iliyopo leo, miongoni mwa wakristo wengi, ni kwamba tumejengwa juu ya mafundisho mengi. Lakini hatujajengwa juu ya kutendea kazi mafundisho tunayofundishwa. Ndugu fundisho halikusaidii kuyashinda majaribu, au tufani za mwovu, au dhoruba, au pepo, hapo unafanya kazi ya kuchosha tu,kudumu katika kusikia, kusoma, kusikiliza, bado si suluhisho, kusema nimebarikiwa, nimefunguliwa ufahamu, bado hakukufikishi popote, kama HUTALIISHI hilo Neno.
Ukiwa ni wa kufanya bidii kuliishi NENO moja, wewe ni imara sana kuliko Yule mwenye kujiona anaijua biblia yote
Penda Utakatifu, penda usafi wa moyo, penda kupiga hatua rohoni. Penda matendo mema.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)
Swali: Kwanini katika biblia lisitumike neno “Mwizi” na badala yake linatumika neno “Mwivi”…Mwivi ni nini?
Jibu: Mwivi na Mwizi ni Neno moja, lenye maana moja.. isipokuwa ni lugha mbili za nyakati mbili tofauti.
Kiswahili kilichotumika katika kutafsiri biblia ni Kiswahili cha zamani, kilichoitwa “kimvita” ambacho ndicho kimebeba maneno ambayo hatuyaoni katika Kiswahili cha sasa, na mojawapo ya maneno ndio kama hayo “Mwivi na wevi” ikimaanisha “mwizi na wezi”. Ndio maana katika biblia yote huwezi kukuta neno Mwizi, badala yake utakuta mwivi (Soma Kutoka 22:2, Ayubu24:14, Zaburi 50:18, Mithali 6:30, Yoeli 2:9, Luka 12:39 n.k )
Maneno mengine ya kimvita (Kiswahili cha zamani) ambayo mengi ya hayo hayatumiki sasa ni pamoja na “jimbi” badala ya “Jogoo”… “Kiza” badala ya “Giza”….”Nyuni” badala ya “ndege”…. “Kongwa” badala ya “Nira” na mengine mengi.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba “Mwivi” na “Mwizi” ni Neno moja, lenye maana ile ile moja (ya mtu anayeiba).
Lakini mbali na hilo, maandiko yanatufundisha kuwa Bwana YESU atakuja kama “Mwivi”..
Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake)”
Je umewahi kujiuliza ni kwanini aje kama Mwivi na si Askari?.. Kwa upana juu ya hilo basi fungua hapa >>ANAKUJA KAMA “MWIVI” NA SI KAMA “ASKARI” FANYIKA CHOMBO CHA THAMANI.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Nini maana ya Mithali 6:30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha
Wale waliowekewa tayari ufalme ni akina nani?. (Mathayo 20:23).
Swali: Je Neno “Kalvari” tunalisoma wapi katika biblia?, na tofauti yake na Golgotha ni ipi?
JIbu: Katika biblia ya Kiswahili hakuna neno “Kalvari”, bali kuna neno “Golgotha” ambalo tunalisoma katika kitabu cha Yohana 19:17
Yohana 19:17 “Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, GOLGOTHA.
18 Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati”.
Maana ya Neno “Golgotha”, tayari biblia imeshatoa tafsiri yake hapo kwenye mstari wa 17 kuwa ni “Fuvu la Kichwa”
Sasa neno “Kalvari” maana yake ni nini?
Neno Kalvari linapatikana katika tafsiri chache za lugha ya kiingereza, ambalo asili yake ni lugha ya Kilatini “CALVARIAE” lenye maana ile ile ya “Fuvu la kichwa cha mtu”.
Hivyo “Kalvari” na “Golgotha” ni Neno moja lenye maana moja, isipokuwa lugha tofauti, ni sawa na neno “church” na “kanisa” ni kitu kimoja ila lugha tofauti.
Kufahamu kwa upana ufunuo uliopo nyuma ya Golgotha, (Fuvu la kichwa), basi fungua hapa >>>FUVU LA KICHWA.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
Swali: Je wale waliowekewa tayari ni akina nani na kwanini Bwana Yesu aseme maneno yale?
Jibu: Tuanzie kusoma mstari wa 20..
Mathayo 20:20 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.
21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.
22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.
23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, SINA AMRI KUWAPA, BALI WATAPEWA WALIOWEKEWA TAYARI NA BABA YANGU”.
Ili tuelewe vizuri, hebu tafakari mfano huu.. “wanafunzi wawili wamemfuata mwalimu wao wa darasa na kumwomba washike nafasi ya kwanza kitaifa na mwingine ashike ya pili kitaifa katika mitihani yao ya mwisho wa kuhitimu”.. Unadhani jibu la mwalimu litakuwa ni lipi?..
Bila shaka mwalimu atawauliza.. je! Mtaweza kusoma kwa bidii??.. Na kama wale wanafunzi watajibu NDIO!.. Bado Mwalimu hataweza kuwapa hizo nafasi, bali atawaambia mimi sina mamlaka ya kuwapa bali “Wasahishaji watakaosahisha mitihani ya wote ndio watakaotoa majibu ya mitihani yenu na kuwapanga kama mmestahili hizo nafasi au la”..
Ndicho Bwana YESU alichowaambia hawa wana wa Zebedayo!.. ambao walienda kumwomba nafasi ya kuketi pamoja naye katika kiti chake.. na jibu la Bwana YESU likawa, ni “kukinywea kikombe”.. maana yake kukubali mateso kwaajili yake!.. Na wao wakajibu “wataweza”.. Lakini jibu la Bwana likawa “Nafasi hizo watapewa waliowekewa tayari”..maana yake waliostahili.
Na hao waliostahili ni akina nani?
Ni wale watakaofanya vizuri Zaidi ya wengine wote katika mambo yafuatayo.
1. KUKINYWEA KIKOMBE.
Kikombe alichokinywea Bwana Yesu ni kile cha Mateso ya msalabani (Soma Mathayo 26:39), kutemewa mate, kupigwa Makonde, kuvikwa taji ya miiba, na kugongomelewa misumari mikononi..
Na yeyote ambaye atakubali kuteswa kwaajili ya Kristo, na si kwaajili ya mtu au kitu kingine chochote, basi yupo katika daraja zuri la kumkaribia Kristo katika siku ile kuu.
2. KUBATIZWA UBATIZO WA BWANA YESU.
Marko 10:38 “Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au KUBATIZWA UBATIZO NIBATIZWAO MIMI?”
Swali Ubatizo aliobatizwa Bwana YESU KRISTO ni upi?…. si mwingine Zaidi ya ule wa kufa, kuzikwa na siku ya tatu kufufuka, na kupaa juu (soma Luka 12:50), Na ubatizo huu mpaka sasa hakuna rekodi ya wazi ya yoyote aliyeupitia..
Ubatizo tubatizwao sasa ni ule wa maji mengi, ambao ni ishara ya kufa na kufufuka na Kristo (Wakolosai 2:12), kwamba tunapozamishwa katika maji mengi na kuibuka juu, ni ishara ya kufa pamoja na Kristo na kufufuka pamoja naye… Lakini Ule hasa wa kufa na kufufuka na kupaa, hakuna rekodi ya wazi ya aliyeupitia.
Isipokuwa unawezekana ndio maana tunasoma katika Ufunuo 11, kuwa wale washahidi wawili, ni miongoni mwa watakaoupitia..
Ufunuo 11:10 “….Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.
11 NA BAADA YA SIKU HIZO TATU U NUSU, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.
12 WAKASIKIA SAUTI KUU KUTOKA MBINGUNI IKIWAAMBIA, PANDENI HATA HUKU. WAKAPANDA MBINGUNI KATIKA WINGU, ADUI ZAO WAKIWATAZAMA”.
Je umempokea YESU?, Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho, na Kristo yupo mlangoni.
Maran atha!
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA