Title May 2019

CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.

Chachu ni nini?. Chachu kwa lugha ya sasa ni HAMIRA, na kwa kawaida ukiitazama hamira unaweza ukadhani ni unga Fulani hivi, lakini kiuhalisia ule si unga bali ni mkusanyiko wa wadudu wenye uhai kwa lugha ya kitaalamu wanaitwa YEAST, hawa wanadudu ndio wanaofanya kazi ya kumengenya ule unga, na kutoa gasi maalumu ambayo ndiyo inaufanya ule unga uumuke. Kwahiyo hamira sio kama chumvi au sukari ambavyo havina uhai ndani yake, Hamira ni kitu chenye uhai kwasababu ni wadudu wale. Na ndio maana ikiwekwa mahali inaweza kubadili maumbile ya kitu na kukifanya kuwa kingine kabisa..

Kwamfano unga wa ngano ukitiwa hamira, ukila kalmati sio sawa na utakavyokula keki, na sio sawa na utakavyokula tambi au maandazi. Yote hii inafanywa na kazi moja ya Hamira (CHACHU). Kubadilisha maumbile.

Na ndio maana Bwana alitumia Neno “chachu” kuonyesha madhara yanayoweza kumtokea mtu asipojihadhari na hayo atakayoonywa.

Tukisoma.

Marko 8:15 inasema “Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode”.

Mathayo 16:12 “Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo”.

Mahali pengine anasema:

Luka12 :1 “Wakati huo, makutano walipokutanika elfu elfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni UNAFIKI”.

Kwahiyo kumbe chachu anayoisemea alikuwa anamaanisha kuwa ni MAFUNDISHO YA KINAFKI. Ambayo yanaletwa na hayo makundi mawili, kundi la kwanza ni watu wa kidini na kundi la Pili ni wana SIASA.

Na leo kwa neema za Mungu tutaliangalia zaidi hili kundi la PILI. Tunajua makundi yote haya wakati wa BWANA YESU na ule wa mitume yote yalifanyika kuwa maadui wakubwa wa kazi ya Mungu, tunaona wakati tu Bwana Yesu anazaliwa Herode alitaka kumuua lakini mpango wake ukashindikana, baadaye mtoto wake akafanikiwa kumuua Yohana Mbatizaji, na ndio huyo huyo alitaka tena kuja kumuua Yesu, lakini Yesu alimwita Mbweha..halikadhalika mafarisayo na waandishi walikuwa wanamvizia siku zote za huduma yake wamwangamize mpaka baadaye mwishoni wakafanikiwa wote wawili kuungana (yaani Herode na mafarisayo) ili kumuua YESU.

Lakini heri wangekuwa wanafanya vile kwa ujinga, Lakini Bwana alikuwa anasema wanafanya kinafki, ikiwa na maana kuwa wale ambao wangepaswa wawe watenda haki na watunza sheria za Imani na za nchi wao ndio wanaokuwa wa kwanza kutokusimamia haki, kwa nje wanaonekana ni watenda haki na wanasiasa bora lakini kumbe ndani yao ni wanafki…Na kwasababu hiyo basi Yesu akawaonya wanafunzi wake wajitenge na njia zao, kwasababu kama wakiambatana nao, wao pia muda si mrefu wategeuzwa kwa unafki wao na kufanana nao, na mwisho wa siku watajikuta wanamkosea Mungu.

Jambo hilo hilo tunaonywa hata na sasa, TUJIEPUSHA NA WANASIASA, sio kwamba tusionge nao kabisa, au tusile nao au tusialikwe nao hapana…Bali tusikubali CHACHU yao iingie ndani yetu.. Kwasababu hiyo inaweza ukatubalisha maumbile yetu ya kiroho na kuwa watu tofauti kabisa, tofauti na tulivyokuwa hapo mwanzo. Na sisi tutaanza kuwa wanafki, tutaanza kufanana na wao,.na mwisho wa siku tutaangamia.

Hilo ni kosa mojawapo linalofanywa na watumishi wengi wa Mungu sasa, ikiwa Mungu amekupa ujumbe kwa mwanasiasa, basi utoe kulingana na maagizo ya ki-Mungu, na usiwe wakati wa wewe kila jambo la kisiasa upo, kampeni upo, jeshi la polisi upo, bungeni upo, ..n.k..vikao vya kisiasa mtaani kwako upo, mijadala ya kisiasa upo, Hayo ni mambo ambayo kwa nje unaweza ukaona upo sahihi lakini nyuma yake unajiangamiza mwenyewe.

Ukiwa umeamua kuwa mtumishi wa Mungu, na mtumishi wa Mungu siye anayehubiri tu madhabahuni, bali yeyote Yule anayemtumikia Mungu kwa karama aliyopewa (huyo ni mtumishi wa Mungu) weka mbali mambo ya SIASA, tuwache wao na shughuli zao na sisi tuendelee na shuhuli zetu za kutangaza habari za haki, na injili..Na ndivyo tutakavyo fanikiwa kutumika pasipo kujikwaa.

1Wakorintho 5:7 “ Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;

8 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli”.

Ubarikiwe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP



Mada Zinazoendana:

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.

NINI TOFAUTI KATI YA MYUNANI, MFARISAYO NA MSADUKAYO.

WAFAHAMU MANABII WA UONGO

TUSIFUNGWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 22

Bwana wetu YESU KRISTO apewe sifa, Karibu katika mfululizo wa mwendelezo wa kitabu cha ufunuo leo tukiwa katika sura ya 22 na ya mwisho, Tusome..

    Ufunuo 22

1 Kisha akanionyesha MTO WA MAJI YA UZIMA, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo MTI WA UZIMA, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia;

4 nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.

5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.

6 Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.

Tukirejea kidogo kwenye historia ya Edeni, tunafahamu kuwa katikati ya Bustani, kulikuwa na ule mti wa uzima, na pia kulikuwa na mto kando ya mti wa uzima ambao ulikuwa unaitilia bustani yote maji, na kisha baada ya hapo uligawanyika na kuwa vichwa 4 (Mwanzo 2),ambavyo vilikwenda kuimwagilia dunia yote. Hivyo tunajua kuwa ule mti wa uzima, haukuwa mti kama mti wa matunda ya asili kama vile zabibu au peasi, la! bali ulikuwa ni mti wa rohoni, ambao matunda yake mtu akila anapata uzima wa milele, vyakula vya mwilini haviwezi kumpa mtu uzima wa milele, ukisoma kwa makini pale utaona Mungu alichepusha miti ya aina tatu: wa kwanza ulikuwa ni kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa(haya ndio matunda ya asili kama vile zabibu, embe, tufaa, n.k.)..aina ya pili ni mti wa uzima, na aina ya tatu ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya,(Mwanzo 2:9), sasa hii miti aina 2 za mwisho ni miti ya rohoni.

Hivyo ule “mti wa uzima” ulikuwa ni NENO LA MUNGU ambao ndio baadaye ulikuja kuuvaa mwili ukaitwa YESU KRISTO, Sasa hili NENO LA MUNGU ndilo lililokuwa sheria na maagizo yote ambayo Adamu na Hawa walipewa na Mungu ili wakidumu katika hayo waishi milele. Hivyo pale Edeni Adamu na Hawa walikula matunda ya kawaida ya asili pamoja na maji ya asili kuwapa uzima miili yao, lakini pia walikula chakula cha rohoni (Matunda ya mti wa uzima), na maji ya rohoni, kuwapa uzima katika roho zao.

Lakini baada ya Adamu kuasi(kukaidi sheria ya MUNGU) tunaona njia ya mti wa uzima ilifungwa(kumbuka mti wenyewe haukuondolewa), ilipofika wakati uliokusudiwa ile njia ilifunguliwa tena, na tunajua huyu si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, Yohana 14:6″Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA, na kweli, na UZIMA; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. ”

Hivyo YESU KRISTO ni NENO/maagizo yale yale ya Mungu yaliyouvaa mwili.

Yeye ndiye ule mti wa uzima, na pia ndio anayetoa yale maji ya uzima.

ukisoma Yohana 4:14″

13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;

14 walakini ye yote atakayekunywa MAJI YALE nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia UZIMA WA MILELE. “

Sasa tukirudi juu, katika kitabu cha UFUNUO, tunasoma..

1 Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo MTI WA UZIMA, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

Hapa tunaona mto wa maji ya uzima unaonekana ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha mwanakondoo, kumbuka kama tulivyosoma katika sura iliyopita kwamba katika ile Yerusalemu mpya(ambayo ni BIBI-ARUSI) ndipo patakapokuwa makao ya Mungu

(Ufunuo 21:3-4″Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, TAZAMA, MASKANI YA MUNGU NI PAMOJA NA WANADAMU, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. ),

hivyo kiti chake cha enzi cha Mungu kitakuwepo huko, Na MTI wa UZIMA pamoja na mto wa maji wa uzima utatokea huko.

Kwahiyo bibi-arusi wa Kristo ambaye ndo ile Yerusalemu mpya na ndio watu wale wote watakaoshinda kutoka katika nyakati mbalimbali za Kanisa, Kama Bwana Yesu alivyoahidi katika Ufunuo 2:7 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu. ”

Hii Ikiwa na maana kuwa wale watakaoshinda tu ndio watakula mema yote na kuzishiriki baraka zote ambazo Mungu alimwahidia YESU KRISTO atakapokuja kuumiliki ulimwengu, Yaani kwa lugha rahisi hawa watu watakatifu watafanana na YESU KRISTO mwenyewe. Kwa kuwa maisha yao walipokuwa hapa duniani yalifanana sana na mwana wa Mungu, hivyo watavuna walichokipanda kwa kula matunda yake.(yaani matunda ya mti wa uzima-YESU KRISTO mwenyewe.)

Lakini pia majani yatakuwa ni ya kuwaponya mataifa, kama tunavyofahamu mti wowote wa matunda, kwa mfano mti wa mwembe, huwezi ukala majani, ukasema, huu mwembe ni mzuri pengine yanaweza kukusaidia kama dawa ukiyatwanga, au kuongeza tu virutubisho fulani mwilini, lakini anayekula EMBE ndie anayejua uzuri wa mwembe, Vivyo hivyo kwa YESU KRISTO yeye kama mti wa UZIMA matunda yake watakayoyafurahia aliyopewa na BABA yake ni BIBI-ARUSI tu, wengine wote watamfahamu YESU katika sehemu ya matawi yake, kama biblia inavyosema yatakuwa ni kwa ajili ya kuwaponya tu, waendelee kuishi milele, lakini BIBI-ARUSI atakuwa na vyote.

Kama ilivyokuwa katika bustani ya Edeni mto ulitoka katika bustani na kusambaa duniani kote, vivyo hivyo na huu mto utokao katika kiti cha Enzi cha mwanakondoo katika ile YERUSALEMU MPYA, maji yake yatasambaa ulimwenguni kote kuwanywesha mataifa, ikiwa na maana kuwa yale maji ya uzima ambayo chanzo chake ni YESU KRISTO, kwa kupitia bibi-arusi wake, yataenea duniani kote kwa kufandisha mataifa kanuni zote za Mungu na utukufu wake.

Hivyo hawa watu ambao wanaaunda huu mji Yerusalemu mpya, watakuwa wametawanyika duniani kote . Unaona uzuri wa kuwa bibi-arusi wa Kristo? Kama dunia ya leo ni wasomi tu, ndio wanaotoa mwongozo wa mataifa ya dunia na kupewa kipaumbele, vivyo hivyo na kule ni BIBI-ARUSI tu, ndiye atakayetawala na KRISTO, na litakuwa ni kundi dogo, ni kwa wale watakaoshinda tu!

Tukiendelea..

Ufunuo 22:7-21 7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.

8 Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo.

9 Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.

10 Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

Ndugu hapa Bwana anatoa angalizo, Hili neno “TAZAMA NAJA UPESI” ..na thawabu yangu ipo mkononi mwangu kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo, Linaonyesha kwamba wakati umeisha, je! wewe kazi yako ni ipi?, je! umeipima thawabu yako?, je! unastahili kuitwa bibi-arusi ?, je! kazi yako inakupeleka mbinguni au kuzimu?.

maana hapa anaendelea kusema…

15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.

17 Na “ROHO na BIBI-ARUSI” wasema, NJOO! Naye asikiaye na aseme, NJOO! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

Huu ni wakati wako wewe mkristo uliyevuguvugu, kimbilia kwenye chemchemi ya maji ya uzima unywe maji yaliyo hai na ufue nguo zako, ufanyike kiumbe kipya, wakati umeisha Bwana yu karibu kurudi.

Hivyo ni vyema kujua kalenda ya Mungu na ujumbe wa Mungu kwa wakati tunaoishi. Kwa kulijua hilo utaishi maisha ya uangalifu tukijua kuwa BWANA wetu yu karibu kurudi kumchukua bibi-arusi wake safi asiye na hila wala mawaa.

Bwana anaendelea kusema…

18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.

19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

20 Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.

21 Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.

Huu ni wakati wa kupiga mbio kweli kweli tuhakikishe hatukosi kuwa katika hiyo YERUSALEMU MPYA bibi-arusi wa Kristo ambayo Bwana anaendelea kuiandaa hadi sasa, na watakaokuwa huko ni kundi dogo, biblia inasema..

Waebrania Mlango 12:

1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu. “

Amen.

Maran Atha!

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.

MWISHO WA MAELEZO JUU YA KITABU CHA UFUNUO.

   Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Zinazoendana..


MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

NINI MAANA YA USIPUNGUZE WALA USIONGEZE NENO LA MUNGU?


Rudi Nyumbani.

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 21

Bwana YESU KRISTO atukuzwe, Karibu katika mafunzo ya kitabu cha Ufunuo, leo tukiwa katika ile sura ya 21,

Tukisoma..

Mlango 21:1-8

1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.

6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.

7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Sura hii inaelezea juu ya MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, ikiwa na maana kuwa hapo mwanzo kulikuwa na mbingu ya zamani na nchi ya zamani, na hizi si nyingine zaidi ya hizi zilizopo sasa, kama mtume Petro alivyosema katika 2 Petro 3:5-6″…

5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;

6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.

7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.

9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?

13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, ambayo haki yakaa ndani yake.

14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake. “

Kwahiyo kwa maneno hayo tunaona dunia ya wakati ule wa Nuhu iliangamizwa kwa maji, vivyo hivyo na hii dunia tuliyopo sasa itaangamizwa kwa moto, kisha ndio ije mbingu mpya na nchi mpya ambaye HAKI yakaa ndani yake. Kumbuka DUNIA haitakunjwa kunjwa kama karatasi na kutupwa kuzimu kama watu wengine wanavyofikiria, hapana bali itakuwa ni dunia hii hii isipokuwa itarekebishwa na kurejeshwa katika utukufu usioneneka ambao Mungu alishaukusudia kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, Hivyo Dunia hii ndiyo makao ya mwanadamu ya milele, Mbinguni tutakaa kwa kitambo tu, kisha tutarudi kutawala na Kristo hapa duniani milele.

Mbingu mpya na nchi mpya itakuja mara baada ya ule utawala wa miaka 1000 kuisha, vilio, misiba, mauti, uchungu, biblia inasema havitakuwepo tena, kwasababu shetani atakuwa ameshatupwa katika lile ziwa la moto pamoja na waovu wote, huko ng’ambo kutakuwa na mambo mapya kabisa ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, Vitu kama Bahari havitakuwepo tena, Mambo mazuri yasiyoneneka yatakayokuwepo huko, itapelekea hata zile taabu za kwanza zisiingie akilini. Ndugu sio sehemu ya kukosa, uchungu hautakuwa kwasababu utaangamizwa milele, uchungu utakuja pale utakapogundua unayakosa mambo matamu ya Mungu ya umilele.

Lakini tukisoma mstari wa 2, tunaona jambo jingine...” Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.”

.. Mstari huu unafunua kuwa huu mji mtakatifu si mwingine zaidi ya BIBI-ARUSI, na ndio maana ukisoma mstari wa 9-10 tunaona jambo hilo likiendelea kwa urefu,”

“9 Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule BIBI-ARUSI MKE WA MWANA-KONDOO,

10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule MJI MTAKATIFU, YERUSALEMU, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;”

..Unaona hapo Yohana alionyeshwa bibi-arusi mke wa mwana-kondoo mfano wa MJI.

Kwahiyo hii YERUSALEMU MPYA inayozungumziwa hapo ni BIBI-ARUSI wa Kristo na sio mji tu kama mji mfano wa Ninawi au Nazareti. Pengine itakuwepo miji mikubwa na mizuri huko, lakini sio huo unaozungumziwa hapo…huo ni Bibi arusi wa Kristo.

Kumbuka mji huu Mungu amekuwa akiuundaa tangu vizazi na vizazi, na Mungu hakai katika maskani yenye muundo wa mfano wa kibinadamu, bali maskani ya Mungu ni KANISA lake TAKATIFU, kama tunavyosoma katika waefeso 2:19-22″

19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.

20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni JIWE KUU LA PEMBENI.

21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe HEKALU TAKATIFU katika Bwana.

22 Katika yeye ninyi nanyi MNAJENGWA PAMOJA KUWA MASKANI YA MUNGU KATIKA ROHO. “

Kwahiyo sisi kwa pamoja, (wakristo) tunajenga mwili mmoja maskani ya Mungu ambayo yeye mwenyewe anakaa ndani yake, na ndio mji ambao Ibrahimu aliuona tokea mbali akasema..Waebrania 11:8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia MJI WENYE MISINGI, AMBAO MWENYE KUUBUNI NA KUUJENGA NI MUNGU.”. Hivyo upo mji wenye misingi ambao Mungu anaundaa.

Na pia tunaona Mtume Paulo kwenye wagalatia 4, akifananisha wakristo kama watoto wa ile Yerusalemu ya mbinguni iliyofananishwa na Sara,

Wagalatia 4:25-31

25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.

26 Bali YERUSALEMU WA JUU NI MWUNGWANA, naye ndiye mama yetu sisi.

27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.

28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.

29 Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.

30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.

31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, BALI TU WATOTO WA HUYO ALIYE MWUNGWANA. “ .

Mtume Paulo pia alionyeshwa hilo kwamba watakatifu ni watoto wa ahadi wa ule mji utokao juu(Yerusalemu mpya.)

Hivyo kwa mistari hiyo mpaka hapo tunaweza kupata picha kuwa MJI MTAKATIFU YERUSALEMU MPYA ambao Mungu alikuwa akiiunda kwa muda mrefu sio makasri ya kifahari na barabara nzuri zenye kupendeza bali hayo yote ni picha inayoelezea uzuri wa wateule wake bibi-arusi safi asiye na mawaa aliyemnunua kwa thamani ya damu yake mwenyewe.

Sasa tukiendelea na mistari inayofuata katika ile sura ya 21 tunasoma..

Mlango 21:9-14

9 Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.

10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;

11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri;

12 ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.

13 Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu.

14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.

Kama tunavyosoma hapo juu mji huu unaonekana wenye misingi 12, na wenye majina 12 ambao ni mitume 12 wa Bwana Yesu Kristo, kumbuka kama tulivyotangulia kusoma kwenye Waefeso 2:20 inasema..”Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”. Hivyo hawa waliojengwa juu ya huu msingi wa mitume na manabii ni sisi watu wa mataifa, lakini pia kuna wayahudi ambao ni wazao wa ahadi ambao pia walikuwa wakiutazamia mji huu, vivyo hivyo nao walijengwa juu ya wale wana 12 wa Yakobo, ambao kwa ujumla wanatengeneza taifa la Israeli, Hivyo wote kwa pamoja (yaani wakristo na wayahudi ) wataunda ile YERUSALEMU MPYA ya mbinguni. Na ndio maana ule mji hapo unaonekana ukiwa na msingi 12, na milango 12 ambao ni mitume 12 na wana 12 wa Yakobo.

Tukiendelea….

MLANGO 21:15-17

15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.

16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.

17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika”.

Tunaona picha nyingine hapa huu mji unaonekana ukipimwa, na vipimo vyake vinaonekana kuwa ni sawasawa, havijazidiana,wala kupungukiana kuashiria kwamba uko sawa umejengwa katika utashi wa hali ya juu hivyo ni wa kudumu milele, lakini kama ungepimwa na kuonekana umepunguka, HAKIKA usingedumu milele, ungeanguka tu kama BABELI Mji ule mkuu ulivyopimwa na kuonekana umepunguka, ukaanguka. ukisoma Danieli 5:24-28″ Ndivyo Babeli ilivyoanguka kwasababu vipimo vyake vilionekana vimepunguka, lakini mji huu mtakatifu ambao Mungu ameubuni na kuujenga kwa muda mrefu VIPIMO VYAKE VIPO SAWASAWA, HALELUYA.!!!. na ndio tunafahamu kwanini biblia inasema huko hakitaingia KINYONGE.

Kwasababu mji huo(bibi-arusi) ni mkamilifu.

Tukimalizia kusoma..

MLANGO 21:18-27

18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.

19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;

20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.

21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.

22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.

23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.

24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.

25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.

26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.

27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

Amen.

Na kama inavyoonekana mji huo hauhitaji jua wala mwezi kuangaza, bali UTUKUFU wa Mungu huutia nuru ikiwa na maana kuwa hili kundi linalounda BIBI-ARUSI wa Kristo litapelekwa katika kiwango kingine kikubwa cha UTUKUFU, Kumbuka duniani wakati huo watakuwepo watu wengine wa kawaida, mbali na bibi-arusi, watu hawa watakuwa wametoka katika kumshinda shetani katika ule utawala wa miaka 1000, na baadhi ya waliohukumiwa katika hukumu ya kiti cheupe ambao majina yao yalionekana katika kile KITABU CHA UZIMA. kundi hili ni mbali na BIBI-ARUSI, hawa ndio watakaotawaliwa na kuleta heshima na utukufu kwa Mungu kupitia BIBI-ARUSI wake(Ambaye ndiye YERUSALEMU MPYA).

Kwahiyo bibi-arusi pekee ndiye atakayezichukua siri za Mungu na kuwafundisha mataifa pamoja na hayo utukufu wa miili yao itakuwa ni tofuauti sana na wale wengine, hawa watakuwa na uwezo na ujuzi mwingine wa kipekee kutoka kwa BWANA.

Hivyo ndugu kundi linalounda bibi-arusi wa Kristo ni dogo sana, ni wale tu wanawali werevu waliokwisha kuweka taa zao tayari pamoja na mafuta ya ziada kwenda kumlaki BWANA wao, Huu ni wakati wa kuyaangalia tena maisha yako na kujiweka sawa, Bwana yupo mlangoni kuja na mwanawali mwerevu tu, ndiye atakayemlaki BWANA, na baada ya hapo mlango utafungwa, (Mathayo 25). Biblia inasema Luka 13:23″ Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,

24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; “

JE! HAPA BWANA ALIMAANISHA NI MLANGO UPI TUJITAHIDI KUUINGIA?

Jibu: ni kuingia katika milango ya MJI WA YERUSALEMU MPYA ambaye ni bibi-arusi safi. kwasababu itafika wakati nafasi ya kuwa bibi-arusi haitakuwepo tena.. Ufunuo 22:14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na KUINGIA MJINI KWA MILANGO YAKE. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. “

Kama tulivyosoma hapo juu biblia inatuambia:

7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Hivyo maombi yangu sisi sote tufanye bidii tuwe mojawapo wa bibi-arusi wa Kristo.

AMEN!

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.

Mungu akubariki.


Mada Zinazoendana.


MJI WENYE MISINGI.

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.

NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 19

Karibu tujifunze biblia na huu ni mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika ule mlango wa 19,

Tunasoma..

1 Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina BWANA MUNGU wetu.

2 kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana AMEMHUKUMU YULE KAHABA MKUU aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.

3 Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele.

4 Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya.

5 Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. “

Katika mistari hii ya mwanzo tunaona mbingu ikishangalia kuanguka kwa yule mwanamke kahaba ambaye aliyewakosesha watu wote na kuiharibu nchi kwa uasherati wake, kama tulivyoona katika sura iliyotangulia ya 18. Na kahaba huyu si mwingine zaidi ya kanisa Katoliki

na ni kwa jinsi gani alihukumiwa? Tunasoma Mungu alitumia zile pembe 10 (Ufunuo 17:16) ambayo ni mataifa 10 yatakayounda umoja wa ulaya kwa wakati huo, ndio yatakayomkasirikia yule mwanamke kahaba na kumtekeza kabisa kwa moto,kwa maelezo marefu juu ya hukumu ya yule kahaba fautilia link hii >>> UFUNUO 18

Na ndio sababu tunaona mbingu zikishangalia, zikisema hukumu za Mungu ni za haki kwa kuwa kahaba huyu alimwaga damu za watakatifu wengi wa Mungu na ndio maana hukumu yake ikaja na moshi wake hupaa juu hata milele na milele kuashiria kuwa pigo lake haliponyeki ni la kifo cha milele wala hata kaa anyanyuke tena kuwakosesha watu wanaokaa juu ya nchi kwa uasherati wake. Mstari wa 5 unasema..

5 Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.

KARAMU YA HARUSI YA MWANA-KONDOO.

Tukiendelea kusoma mstari wa 6-10.

6 Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.

7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.

10 Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.

Katika vipengele hivi, Arusi ya mwanakondoo inazungumziwa na mkewe amekwisha jiweka tayari, kumbuka kuna tofauti kati ya Arusi na Karamu,. Siku zote ndoa ikishafungwa (Arusi), kinachofauta ni KARAMU, Kwahiyo Karamu ni sherehe ya kuifurahia “ndoa/arusi mpya”. Vivyo hivyo na kwa YESU KRISTO kama Bwana Arusi yeye naye ana bibi-arusi wake ambaye ndio KANISA lake TAKATIFU bikira safi asiye na mawaa.

Kwahiyo katika ukristo NDOA hii inaendelea sasa hivi kufungwa duniani na hii ilishaanza tangu kipindi BWANA YESU alichopaa kwenda mbinguni mpaka leo, katika vile vipindi vyote 7 vya makanisa , na amekuwa akikusanya bibi-arusi wake kwa kila kipindi na kila nyakati na hadi sasa anaendelea kufanya hivyo,takribani miaka 2000 sasa. Na kuoana huko ni kati ya MTU na NENO LA MUNGU, na kama tunavyofahamu NENO ni YESU KRISTO MWENYEWE, hivyo wale walishikao na kuliishi NENO ndio waliooana na KRISTO

Na sio mkristo vuguvugu anayesema mimi nimeokoka halafu haliishi na halipokei NENO LA MUNGU, kwa mfano ukimwambia mtu biblia inasema hivi yeye anasema dhehebu langu halinifundishi hivyo, ukimuuliza ni kwanini ubatizo wa watoto wachanga haulingani na NENO la Mungu atakwambia dini yetu haifundishi hivyo. Mtu anajiita mkristo lakini anaupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu, ukimuuliza kwanini unakunywa pombe, atasema dini inaruhusu kunywa pombe, acha kuhukumu, hapo mtu huyo anakuwa ameoana na ulimwengu badala ya Kristo (NENO), Hivyo anafanya uasherati mkuu wa kiroho.

Kwahiyo fahamu ndoa inaendelea sasa hivi katika roho, usipoana na KRISTO (NENO LA MUNGU), utaona na shetani kwa mafundisho yake ya uongo yanayolipinga NENO LA MUNGU. Kwahiyo ni vizuri sasa hivi ukajitambua upo upande upi?.

Mtume Paulo alisema katika 2Wakorintho 11:2-4″ Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi”.

Hivyo ni jukumu kwa kila nayejiita mkristo sio tu kuwa bikira bali kuwa BIKIRA SAFI!!

Tukisoma katika mathayo 25 tunaona mfano ya wale wanawali li kumi (10), watano werevu na watano wakiwa wapumbavu. Kumbuka wote 10 walikuwa MABIKIRA wakimngoja Bwana wao, lakini kilichowatofautisha ni kwamba wale wapumbavu hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao ambayo ni “ufunuo wa NENO LA MUNGU katika ROHO MTAKATIFU”,. jambo hilo tu liliwafanya wasiingie KARAMUNI japo wote walikuwa ni mabikira, kwahiyo kujiita mkristo tu haitoshi ni lazima pia uwe na ufunuo wa NENO LA MUNGU, na ndoa inafanyika hapa duniani lakini KARAMU itafanyika mbinguni pale bibi-arusi safi atakapokwenda kwenye unyakuo.

Kama tunavyosoma wale 5 werevu waliingia karamuni bali wale wapumbavu walifungiwa nje vivyo hivyo katika hichi kipindi cha mwisho kutakuwa na makundi mawili ya wakristo, werevu na wapumbavu, werevu ni wale wanaolishika na kuliishi NENO LA MUNGU bila kujali kitu kingine chochote, hao wataenda na Bwana na kuingia katika KARAMU YA MWANAKONDOO, Lakini wale wapumbavu wasiojiweka tayari, kwa kukataa uongozo wa Roho Mtakatifu katika NENO lake, hawa watatupwa giza la nje! kwenye dhiki kuu, wakati wenzao wanafurahi na Bwana katika utukufu mbinguni na kupewa thawabu zao za milele na ndio maana mstari wa 8 tunasoma bibi-arusi ” ..amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.”

Katika hii karamu kutakuwa na mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia mambo ambayo Kristo kawaandalia hao wateule wake (yaani bibi-arusi wake safi), hawa watakuwa na miili ya utukufu sana na ndio baadaye watashuka na BWANA kuja kutawala aulimwengu kwa muda wa miaka 1000 wakiwa kama makuhani na wafalme wa dunia nzima,uzao mteule, watu wa milki ya Mungu, na BWANA YESU KRISTO, akiwa kama BWANA WA MABWANA, na MAFALME WA WAFALME. haleluya!!. Kosa kila kitu ndugu lakini usiikose hiyo karamu, uchungu siku hiyo hautakuwepo sana katika mateso ya dhiki kuu, hapana bali uchungu utakuja sana pale utakapogundua kuwa umekosa thawabu za milele, na usidanganyike eti huko tunapokwenda wote tutakuwa sawa tunafanana! hayo mawazo futa, kule kutakuwa na madaraja tofauti tofauti, wapo watakaokuwa wakuu sana, na wakawaida sana na ni itakuwa hivyo milele, kwanini leo hii unang’ang’ana na vitu vinavyoharibika usijiwekee hazina mbinguni?.

Mstari wa 9 unasema “.. Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.”

VITA YA HAR-MAGEDONI

11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo ala mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;

18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.

19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake.

20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;

21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.

Katika aya hizi tunaona Yohana akionyeshwa mbingu zikifunguka na kuona farasi mweupe, na yeye aliyempanda, anaitwa Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Huyu sio mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO na hapo anaonekana akiwa na vilemba vingi juu ya kichwa chake ikiashiria kuwa anamiliki juu ya wafalme wengi,

Na anaonekana pia akishuka pamoja na jeshi la mbinguni, sasa kumbuka hili jeshi sio malaika bali ni wale watakatifu (bikira safi) waliokuwa wamekwishanyakuliwa mbinguni sasa baada karamu kuisha watarudi duniani wakiwa kama MIALE ya moto kama BWANA alivyo, jambo hili tunaona Henoko miaka mingi iliyopita alionyeshwa Yuda 1:14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake. “

Kwahiyo Bwana atakapokuja wafalme wote wa dunia watakuwa wamekusanyika tayari kupigana naye, mahali panapoitwa Harmagedoni huko Israeli (Ufunuo 16:16) pale zile pembe 10 za yule mnyama pamoja na wafalme kutoka mawio ya jua ambazo ni nchi za mashariki ya mbali kama Japan, China, Korea, Singapore n.k.

Ufunuo 16:12-16″ Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.

13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.

14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.

15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)

16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.

lakini vita hii itadumu ndani ya muda mfupi sana, kwamaana KRISTO hapigani kwa kutumia silaha za kibinadamu, bali siku zote yeye anatumia NENO, kwasababu yeye mwenyewe ni NENO, na ndio maana tukisoma hapo juu jina lake anaitwa NENO LA MUNGU, kwahiyo kwa kuzungumza tu pale megido kutakuwa ni bahari ya damu, mabilioni ya watu watakufa, na kama tunavyosoma katika mstari wa “17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;

18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.

Ndege wengi wataalikwa kuja kula nyama za watu wanajiona majemedari na wafalme wa nchi, kwahiyo unaweza ukatengeneza picha yatakuwa ni mauaji ya namna gani yeye ndiye atakayekanyaga lile shinikizo la ghadhabu ya Mungu, na ukisoma ufunuo 14:20, utaona shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, DAMU ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kwa mwendo wa maili 200, “hii ni picha kuonyesha kwamba damu nyingi sana itamwagika kiasi cha kwamba ndege wengi wa angani watakusanyika kula nyama za mizoga ya watu.Hivyo vita hii ndio itakayohitimisha utawala mbovu wa dunia hii na kuleta utawala mpya wa BWANA YESU KRISTO duniani.

Na katika ule mstari wa mwisho tunasoma

20 “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;

21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.”

Kwahiyo zile roho mbili kati ya zile tatu chafu kama vyura, zilishikwa na kutupwa katika lile ziwa la moto, kumbuka hapo anaposema mnyama na nabii wa uongo anamaanisha zile roho zilizokuwa zinawaendesha huyu mnyama na nabii wa uongo, lakini ile roho ya tatu ambayo ni roho ya shetani itafungwa kwa muda wa miaka 1000, kisha itafunguliwa tena kwa muda mfupi habari hii tutaisoma zaidi katika sura inayofuata ya 20,

Hivyo ndugu fahamu kuwa kanisa tunaloishi leo ni kanisa la mwisho la 7 linaloitwa LAODIKIA, na mjumbe wake ameshapita, muda wowote BWANA anakuja kumchukua bibi-arusi wake safi tu, aliyekwisha kujiweka tayari kwa kupokea Roho Mtakatifu na kuishi kwa NENO tu, je! umejiweka tayari kwenda naye? au utakuwa mwanamwali mpumbavu (yaani mkristo mpumbavu) vuguvugu?. Maombi yangu Bwana akufanye kuwa BIKIRA SAFI. ili sote siku ile kwa neema za BWANA TUKUTANE KATIKA ILE KARAMU YA MWANA KONDOO.

MUNGU AKUBARIKI.

Kwa mwendelezo >> UFUNUO: Mlango wa 20

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Zinazoendana..


KARAMU YA MWANA-KONDOO.

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.

KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.


Rudi Nyumbani.

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 18

Tukirejea kwenye ile sura ya 17 tunamwona yule mwanamke KAHABA aliyeketi juu ya yule mnyama mwekundu na kwenye paji la uso wake ana jina limeandikwa kwa “siri” BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI, na tulishaona huyu mwanamke si mwingine zaidi ya KANISA KATOLIKI, lenye makao yake makuu VATICAN, na ni kwanini hajulikani kwa wazi? ni kwasababu jina lake lipo katika SIRI, na pia BABELI hii ipo rohoni, kumbuka BABELI ya kwanza ilikuwa ya mwilini na ilishaanguka wakati ule wa utawala wa mfalme Nebukadneza(Tunasoma katika kitabu cha Danieli). Lakini katika Mlango huu wa 18, tunaona hukumu ya BABELI hii ya rohoni ambayo ndiyo inayotawala hata sasa.

Tusome.

Mlango 18:1 “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.

6 Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu.

7 Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.

8 Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.

9 Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;

10 wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.

Kumbuka Babeli ya kwanza ambao ulikuwa (kwasasa ni maeneo ya Iraq) ngome pekee yenye nguvu iliyokuwa inatawala dunia nzima kwa wakati ule, ndio ilikuwa chimbuko la mambo yote maovu na dini zote za kipagani, ikiwemo kuabudu sanamu, na uchawi, zaidi ya yote ndiyo iliyohusika kuuhamisha hata uzao wa Mungu(Israeli) na kuupeleka utumwani na kuliteketeza HEKALU la Mungu, na kutumia vyombo vya madhabahuni vitakatifu kwa kufanyia anasa na uchafu kwa miungu yao, Kwasababu hiyo basi Babeli ulionekana kuwa ni mji wenye MACHAFUKO na MACHUKIZO makubwa sana mbele za Mungu.

Pamoja na hayo ulizidi kuwa kuendelea sana, miji yake ilikuwa imetengenezwa kwa utashi wa hali ya juu hata leo tunafahamu moja ya maajabu 7 ya dunia kwa wakati wote tukiachia mbali zile Piramidi za Misri nyingine ni “BUSTANI ZINAZOELEA ZA BABELI”. Mji huu ulitukuzwa sana, mpaka kufikia kiwango cha watu kuuita “BABELI MJI WA MILELE”, na ni kweli kwa jinsi ulivyokuwa na nguvu ilikuwa ni ngumu kutabiri kama kweli ungekuja kuanguka na kuwa makao ya mbuni na hayawani wa mwituni. Leo hii maeneo yaliyokuwa ni Babeli ni jagwa lisilokuwa na kitu.

Lakini Jambo hili tunaona Mungu alilitolea unabii kwa kinywa cha nabii Yeremia miaka 70 kabla ya Babeli kuanguka alisema…,

Yeremia 51:6 “Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha Bwana, atamlipa malipo.

7 Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Bwana; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu.

8 Babeli umeanguka na kuangamia ghafula; mpigieni yowe; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa.

9 Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni. “

Na pia tunamwona Nabii Isaya alishatabiri miaka 200 kabla ya Babeli kuanguka alisema…

Isaya 13:19 “Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza.

20 Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.

21 Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko.

22 Na mbwa-mwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka.”

Kwahiyo unabii wote huu ulikuja kutimia kama ulivyo kwa wakati wake, pale wakuu wa Babeli walipokuwa wanafanya anasa tena kibaya zaidi wakiwa wanatumia vyombo vitakatifu vya Hekalu, kulitokea kile kiganja ukutani kikiandika MENE, MENE, TEKELI na PERESI, na usiku ule ule Waamedi wa waajemi waliuvamia mji kwa njia ambayo hawakuitegemea na ndio hapo ikawa mwisho wa BABELI na katika usiku mmoja tu! uliteketezwa, mji ule waliosemea UTAISHI MILELE ndio ulikuwa mwanzo wa kuwa makao ya mbuni, na wanyama wa mwituni,(Danieli 5). Hii ikithibitisha kuwa BWANA akisema jambo ni lazima litimie tu!.

Sasa hiyo iliyoangamizwa ilikuwa ni BABELI ya kwanza, lakini BABELI iliyopo sasa hivi ni ya ROHONI na ipo katika “SIRI”, Kumbuka ile ya kwanza iliwachukua wayahudi wa kimwili utumwani na kuchukua vyombo vya hekalu la Mungu kutumia kwa karamu zao za kipagani lakini hii ya sasa hivi inawachukua wayahudi wa rohoni(WAKRISTO) utumwani na kuchukua vyombo vitakatifu vya rohoni (Ibada Halisi ) na kuzitumia pamoja na ibada za masanamu, haya ni MACHUKIZO mbele za Mungu, na kama vile ile ya kwanza iliandikiwa MENE, MENE, TEKELI na PERESI vivyo hivyo na hii ya rohoni IMESHAHUKUMIWA na hivi karibuni tu itateketezwa na kuwa ukiwa.

Na ndio maana tukisoma kwenye hiyo mistari hapo juu tunaona;… “9 Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake; wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja. “

Kanisa Katoliki makao yake makuu yakiwa VATICAN ni dini iliyojichanganya na SIASA, na ina utajiri mkubwa sana, kumbuka hazina kubwa ya dunia ipo VATICAN karibu kila taifa duniani lina mkono wa dola ya Rumi nyuma yake, kwamfano hata hapa Tanzania ukiangalia karibu miradi mikubwa mingi na mataasisi ya kijamii na mabiashara, mashule, mahospitali,n.k yanafadhiliwa au kuasisiwa na kanisa Katoliki na yapo karibu kila mkoa,limefanya hivi dhumuni lake kubwa ikiwa ni kueneza dini yake ya uongo na kutaka kutawala kama MALKIA.

Na kama maandiko yanavyosema “. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.” Kanisa Katoliki limejiweka kama MALKIA, si ajabu hata ishara ya kanisa hili ni mwanamke (bikira Mariam) wakimfanya kama malkia wa mbinguni.

Na jambo hili lipo katika mataifa yote duniani, hivyo wafalme wote na mataifa yote duniani yamelewa kwa mvinyo wa uasherati wake na ndio maana tunaona hapo wataomboleza watakapoona uharibifu wake utakapokuja kwa ghafla ndani ya siku moja,

Kama vile Mungu alivyowatumia waamedi na waajemi kuiangusha ile BABELI YA KWANZA, vivyo hivyo Mungu ataenda kutumia zile PEMBE 10 zilizokuwa juu ya kichwa cha yule mnyama (ambayo ndiyo yale mataifa 10 ya ulaya) kuiangusha hii BABELI ya PILI ambaye ndio yule MAMA WA MAKAHABA aketiye juu ya yule mnyama(KANISA KATOLIKI), na KITI chake cha ENZI kikiwa VATICAN. Hivyo kwa siku moja VATICAN itateketezwa kwa moto pengine kwa bomu la ATOMIC. Na wale watu waliopata utajiri kupitia yeye biblia inasema watamwombolezea kwasababu watastaajabia imewezekanikaje ngome kubwa kama hiyo kuanguka ndani ya siku moja na pia utajiri waliokuwa wanaupata kwa kupitia yeye hawataupata tena..

 Tukiendelea mistari inayofuata.. UFUNUO 18:11-24 tunasoma..

“11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;

12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;

13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.

14 Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe.

15 Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza,

16 wakisema, Ole, ole, mji ule mkuu! Uliovikwa kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu;

17 kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa. Na kila nahodha na kila aendaye mahali popote kwa matanga, na mabaharia, nao wote watendao kazi baharini, wakasimama mbali;

18 wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa!

19 Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.

20 Furahini juu yake, enyi mbingu, nanyi watakatifu na mitume na manabii; kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.

21 Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.

22 Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;

23 wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana-arusi na bibi-arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.

24 Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi.”

Kama vile ile BABELI YA KWANZA ilivyoangamizwa kwa ishara Mungu aliyompa Seraya kwa mkono wa YEREMIA

 ukisoma….Yeremia 51:61-64″ Naye Yeremia akaandika katika kitabu habari ya mabaya yote yatakayoupata Babeli, maneno hayo yote yaliyoandikwa juu ya Babeli.

61 Naye Yeremia akamwambia Seraya, Utakapofika Babeli, basi angalia uyasome maneno haya yote.

62 ukaseme, Ee Bwana, umenena habari za mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele.

63 Tena itakuwa utakapokwisha kukisoma kitabu hicho, utakifungia jiwe, NA KUKITUPA KATIKA MTO FRATI;

64 nawe utasema,Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watngachoka. Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.

Habari hiyo hiyo tunaona inajirudia tena kwa Babeli ya pili kama tunavyoona katika kitabu cha UFUNUO; 

Ukaisoma mstari wa 21 unasema ” Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, UTATUPWA BABELI, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.” Hivyo Historia inajirudia tena..

Na pia mstari wa mwisho unasema.. 24 “Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi.”

Ni dhahiri kuwa kuwa dini ya Katoliki ndio dini pekee iliyohusika na mauaji mengi ya wakristo historia inaonyesha zaidi ya wakristo milioni 68 waliuliwa kikatili na dini hii kwa kujaribu tu kwenda kinyume na desturi zao za kipagani, na isitoshe bado huko mbeleni katika kipindi cha dhiki kuu itamwaga damu nyingi za watu wote watakaokataa kumsujudia. kwa namna hiyo kwanini Mungu asiiteketeze?

Hivyo ndugu biblia inasema kwenye ule mstari wa 4 ” TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.”

tena ni kwanini tuondoke??.. kwasababu biblia inasema pale kwenye Yeremia 51: 9 “Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni. ” unaona hapo?

Kitabu cha Danieli 2:34 inasema jiwe lilichongwa pasipo kazi ya mikono ikalipiga miguu ya ile sanamu na kuteketea yote na tunajua lile jiwe si mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO akiihukumu BABELI ya rohoni katika siku za mwisho inayowakilishwa na ule utawala wa chuma kilichochanganyikana na udongo ambayo ni RUMI ya kidini (UKATOLIKI).

Kwahiyo Huu ni wakati wa kutoka katika mifumo ya dini na madhehebu na kuligeukia NENO LA MUNGU ambalo ndio NURU yetu itakayotupeleka mbinguni, sio kutoka kwa miguu, bali ni kutoka kwa “ROHO”, kumbuka BABELI hii ipo rohoni, hatumfikii Mungu kwa mapokeo ya dini yoyote au dhehebu lolote, ibada za sanamu ni machukizo, kusali rozari ni machukizo, kwenda toharani ni uongo, ubatizo wa vichanga haupatani na maandiko,pamoja na ibada za wafu n.k..jambo pekee litakalokutoa huko ni kuifanya biblia kuwa KATIBA YAKO TU!

Mungu ni ROHO nao wamwabuduo biblia inasema imewapasa kumwabudu katika roho na kweli, kuwa mkristo halafu bado unakuwa mwasherati,unavaa vimini, suruali, msengenyaji, unapenda anasa, mtukanaji, mlevi unakula rushwa n.k. ni ishara kabisa kuwa na hapo bado hujatoka BABELI, Na kumbuka Tafsiri ya Neno BABELI ni MACHAFUKO, hivyo wafanyao haya machafuko yote wataharibiwa.

Mungu akubariki.

Kwa Mwendelezo >>UFUNUO: Mlango wa 19

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Nyinginezo…


DANIELI: Mlango wa 2

MNARA WA BABELI

NINI MAANA YA KUISHI KWA NENO?

ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 17

Karibu tujifunze kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika mwendelezo wetu wa sura ya 17, Biblia inasema…

Ufunuo 17:1-6″
1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;

2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.

3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.

4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.

Tukirudi nyuma kidogo kwenye ile sura ya 13, tunamwona yule mnyama aliyetoka baharini mwenye vichwa saba na pembe 10, akielezewa, jambo hilo hilo tunaliona tena katika hii sura ya 17 mnyama yule yule mwenye vichwa 7 na pembe 10 na majina ya makufuru ametokea tena, isipokuwa hapa katika sura hii ya 17 tunaona kuna jambo lingine limeongezeka; anaonekana MWANAMKE  AKIWA AMEKETI JUU YAKE.

 Kwahiyo msisitizo mkubwa katika sura hii ni juu ya huyo mwanamke aliyepambwa kwa dhahabu, lulu na vito vya thamani aliyeketi juu ya huyo mnyama.

Sasa mwanamke huyu ni nani?

Mwanamke katika biblia anawakilisha KANISA, Sisi wakristo tunatambulika kama BIBI-ARUSI wa KRISTO,(2Wakoritho 11:2 Paulo anasema “..Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo BIKIRA SAFI. “) Na pia..

Ufunuo 19:7 inasema..” Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na MKEWE amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.  Pia Taifa la Israeli Bwana alilitambua kama MKE WAKE” [soma ezekieli16:1-63, ezekieli 23] utaona jambo hilo. Hivyo mahali popote Mungu anapozungumza juu ya kundi la watu wake huwa analifananisha na mwanamke.

Lakini hapa tunaona mwanamke mwingine ametokea ambaye anaonekana ni KAHABA,  amelewa kwa DAMU za watakatifu na za mashahidi wa YESU, na tena wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.  Na katika kipaji cha uso wake ana jina limeandikwa, la SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

Hivyo tunaona tabia ya huyu mwanamke (ambaye anawakilisha KANISA fulani) kuwa ni KAHABA, Na kama tunavyofahamu kanisa la KRISTO haliwezi kuwa kahaba, kwasababu ni BIKIRA SAFI, na haliwezi kuua watakatifu wa Mungu, kwasababu lenyewe ni TAKATIFU, Hivyo hili Kanisa haliwezi kuwa lingine zaidi ya KANISA KATOLIKI chini ya uongozi wa PAPA.

Kwanini ni Kanisa  KATOLIKI na si kitu kingine?

Tunajua siku zote shetani anatabia ya kuunda “copy” inayofanana na ya Mungu ili aabudiwe kirahisi, au kudanganya watu kirahisi, vinginevyo asingeweza kupata wengi, ili noti feki iweze kufanya kazi ni lazima ifanane sana na orijino, shetani anataka kuabudiwa kama Mungu hivyo atatumia njia zote zinazofanana na za Mungu  ili apate wafuasi wengi. Na ndio maana Mungu alikataza Mtu kutengeneza mfano wa Kitu chochote kama Mungu ili kukiabudu kwasababu mtu anaweza akadhani anamwabudu Mungu kumbe anamwabudu shetani mwenyewe kwa kivuli cha ile sanamu pasipo kujua.ZIKIMBIE IBADA ZA SANAMU. Mimi sipo kinyume na wakatoliki, wala siwahukumu ndugu zangu wakatoliki, bali nipo kinyume na mifumo ya kanisa Katoliki kwasababu Mungu alishaihukumu, na kupiga mbiu watu wake watoke huko wasishiriki mapigo yake!.

Sasa mpango wa Mungu aliouunda tangu awali ni kumleta “MTU” atakayesimama kwa niaba yake ili kuwakomboa wanadamu (VICAR) katika dhambi zao hivyo akamleta mwanae anayeitwa YESU KRISTO, ambaye kwetu sisi ni Mungu mwenyewe katika mwili..shetani kuona hivyo akaanza kuiga kwa kumtengeneza mtu wake (VICAR), ambaye naye atasimama kwa niaba yake hapa duniani, na akampa jina lililo maarufu (VICARIUS FILII DEI) yaani tafsiri yake,  ni “Badala ya mwana wa Mungu duniani”, hivyo huyu mtu wake anasimama hapa duniani badala ya mwana wa Mungu (yaani YESU KRISTO), na  shetani akamvika uwezo wake bandia kwamba na yeye anaweza kusamehe dhambi duniani kama vile BWANA WETU YESU KRISTO alivyo na uwezo wa kusamehe dhambi.

Na kama vile Mungu alivyounda kanisa lake takatifu kwa kupitia BWANA YESU KRISTO, ambalo ndilo linaloitwa BIBI-ARUSI safi, vivyo hivyo shetani naye alilitengeneza Kanisa lake kwa kupitia huyu (VICARIUS FILII DEII) yaani PAPA, Kutimiza kusudi lake la kutaka kuabudiwa na kupeleka watu kuzimu na hilo KANISA  ndilo KAHABA, Na si lingine zaidi ya KANISA KATOLIKI. 

Na tunajua Kanisa la Kristo safi linaongozwa na ROHO MTAKATIFU kwa kupitia zile huduma na karama za roho, yaani mitume, manabii,wachungaji, wainjilisti na waalimu lakini hili kanisa kahaba na lenyewe limevuviwa vyeo vya uongozi  kama Upapa, Ukadinali, upadre, paroko, ukasisi n.k.

Kwahiyo unaweza ukaona ni jinsi gani cha uongo kinavyofanana na cha ukweli, na watu wengi wamepofushwa macho na shetani wakidhani kuwa wanamwabudu Mungu hapo kumbe ni shetani.

Na ni kwasababu gani ni kahaba?

Ni kahaba kwasababu biblia inasema wafalme wa nchi wamezini naye nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo wa usherati wake, si ajabu Kanisa hili lina nguvu nyingi katika mataifa mengi kwa utajiri wake kwa jinsi linavyotoa misaada na miradi mingi ya kimaendeleo na ya kijamii, linajenga mashule na mahospitali linatoa misaada ya majanga na kusapoti siasa za nchi, linafanya hivi kwa lengo moja tu! kupumbaza mataifa na wafalme wa nchi ili kuwalewesha kwa kupenyeza mafundisho na itikadi zake za uongo kwa watu ambazo zipo nje ya MANENO MATAKATIFU YA MUNGU.

Na ndio maana tunaona mwanamke huyu ana jina limeandikwa kwa SIRI katika kipaji cha uso wake “BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA, NA MACHUKIZO YA NCHI”..Umeona hapo, jina lake lipo katika SIRI, hivyo inahitaji HEKIMA kumtambua, kwasababu shetani huwa hafanyi vitu vyake kwa wazi wazi, anatumia kivuli cha “orijino” ili kuwadanganya watu.

Ni BABELI mkuu kwasababu tafsiri yenyewe ya neno BABELI ni “MACHAFUKO”, Hivyo Mji wa Babeli ndio ulikuwa chimbuko la machafuko yote, ibada za kipagani za kuabudu miungu mingi na uchawi ndipo zilipozaliwa, Nimrodi akiwa muasisi wa mji ule na mke wake Semiramis pamoja na mtoto wao Tamuzi, waliabudiwa kama miungu, ndipo baadaye Waroma wakaja kutohoa mfumo huo wa kuabudu miungi mingi, na sio ajabu tunaona baadaye wakaja kumweka Yosefu kama Nimrodi, Semiramis kama Mariam na Tamuz kama mtoto YESU ili kutimiza matakwa yao ya ibada zao za sanamu ambazo walikuwa nazo tangu zamani, kwakweli haya ni machafuko makubwa sana katika KANISA LA KRISTO.

Na mji huu huu wa Babeli baadaye ndio uliohusika kuutesa na kuuchukua uzao wa Mungu (ISRAELI) mateka, sasa hii ilikuwa ni Babeli ya mwilini iliyolichukuwa Taifa la Israeli mateka sasa hii iliyopo leo ni  BABELI YA ROHONI(ambayo ni kanisa Katoliki ) inawachukua wakristo wengi mateka kwa kuwafanya waabudu miungu mingine mbali na YAHWE  YESU KRISTO MUNGU WETU. 

Lakini Biblia inasema hakika BABELI HII ya sasa itaangushwa tu! kama ilivyoangushwa ile ya kwanza ya mwilini. Nadhani kuanzia hapo utakuwa umeanza kupata picha ni kwanini mwanamke yule anajulikana kama BABELI MKUU. Sasa tuone ni kwa nini anaitwa “MAMA WA MAKAHABA”.

Ni Mama wa makahaba kwasababu amezaa wabinti ambao nao pia ni makahaba kama yeye na si mengine zaidi ya madhehebu yote yanayoshirikiana naye, wale waliokuwa wanajiita ma-protestants mwanzo  sasa hivi hawapo hivyo tena, wanashirikiana naye kwa namna zote. Kanisa Katoliki limefanikiwa kuwalewesha na kuwavuta tena kwake, lutheran imeshaungana na katoliki rasmi, pamoja na madhehebu mengine mengi,na ndio maana linaitwa “KANISA MAMA”. Sasa ni rahisi kuelewa hapo kwanini ni “MAMA WA MAKAHABA”..Kwasababu yeye ameshakuwa kanisa mama, na mabinti wake wameshafuata mifumo yake ya ibada zisizotokana na NENO la Mungu.

Na ni kwanini ni “Mama wa Machukizo ya nchi”?.

Hili kanisa lenyewe ndio linalohusika na machukizo yote ya nchi yanayovuta ghadhabu yote ya Mungu juu ya nchi, kama ya kuwauwa watakatifu wa Mungu, kimwili na kiroho, kwa ibada zake za sanamu, kanisa hili limeua zaidi ya wakristo milioni 68 katika historia hiyo ni idadi kubwa sana, hata Bwana YESU  alishatabiri juu yao alisema..Yohana 16:1-3″Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania KILA MTU AWAUAYE YA KUWA ANAMTOLEA MUNGU IBADA. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. ” 

Hiyo ndio sababu ya yule mwanamke kuonekana amelewa kwa damu za watakatifu ..Haya yote ni machukizo makuu mbele za Mungu, na yule  mpinga-kristo atakayetokea huko ndiye atakayelisimamisha lile CHUKIZO LA UHARIBIFU lililotabiriwa na nabii Daneli na BWANA wetu YESU KRISTO, ndio  maana anajulikana kama “MAMA WA MACHUKIZO YA NCHI”.

SIRI YA YULE MNYAMA.

Tukiendelea Ufunuo 17:7-18 “7 Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi.

8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.

9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.

10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.

11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu

12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.

13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.

14 Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.

15 Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.

16 Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.

17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.

18 Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi. “

Hapa pia tunaona Yohana anaonyeshwa siri ya yule mnyama ambaye ndio yule yule aliyeonyeshwa katika ile sura ya 13 ambaye ana vichwa 7 na pembe 10, isipokuwa hapa zile pembe 10 zinaonanekana hazina vilemba ikiwa na maana hazijapokea ufalme bado, na ndio maana tukisoma mstari wa 12 inasema watakuja kupokea ufalme(yaani kuvikwa vilemba) saa moja na yule mnyama.

Kumbuka vile vichwa saba vya mnyama, ni FALME 7, ambazo shetani alizikalia kuutesa au kutaka kuungamiza kabisa uzao wa Mungu, ambazo ni 1) MISRI   2)ASHURU  3)BABELI   4)UMEDI & UAJEMI  5) UYUNANI   6)  RUMI-ya-KIPAGANI   7) RUMI-ya KIPAPA…

kwa maelezo marefu juu ya huyu mnyama kama anavyoonekana kwenye sura 13 fungua hapa >> UFUNUO: Mlango wa 13

Lakini tunaona hapo wakati Yohana anaonyeshwa maono hayo aliona watano wameshakwisha anguka, na mmoja yupo na mwingine hajaja bado. Kumbuka wakati ule Yohana anapewa haya maono  AD 90 ,utawala uliokuwa unaitawala dunia wakati ule  ni RUMI ya kipagani, kwahiyo zile tawala tano za kwanza zilikuwa  zimeshapita yaani Misri, Ashuru, Babeli, Umedi&uajemi pamoja na Uyunani. Hivyo ule wa Urumi ndio uliokuwepo na ndio ule uliomsulibisha KRISTO.

Na kama alivyoambiwa mmoja bado hajaja(ambaye ni wa 7), Na kwamba atakapokuja itampasa akae muda mchache, sasa  huo  si mwingine bali ni ule utawala wa RUMI ya kidini chini ya upapa ulioongoza dunia nzima kuanzia kile kipindi cha karne ya 4, ni ule ule tu wa RUMI sema hapa umegeuka ukawa wa kidini chini ya upapa.

Tukiendelea kusoma mstari wa 11 inasema..” Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.”.Hivyo tunaona mnyama mwingine wa 8 anajitokeza hapo, lakini biblia inasema huyu wa 8 ndio yule yule wa 7, hii ikiwa na maana kuwa ni kile kile kichwa cha saba isipokuwa kimebadilisha taswira, kwasababu yule mnyama tayari anavyo vichwa saba hawezi akawa tena na vichwa nane,

Na huyu mnyama wa 8 biblia inasema ambaye alikuwako naye hayupo naye anaenda kwenye uharibifu, tukirudi kwenye historia tunamwona  huyu mnyama (ambaye ndio kile kichwa cha 7 -Rumi ya kidini chini ya Upapa wa Kanisa Katoliki) ulikuwa na nguvu kipindi kile cha utawala wake, lakini baadaye ulikuja kutiwa jeraha la mauti na wale wanamatengezo, hivyo nguvu zake za kutawala dunia nzima zilikufa, lakini tunaona lile jeraha lilianza kupona tena, kuanzia kile kipindi cha vita vya pili vya dunia mpaka leo linaendelea kupona, utakapofika wakati atakaporejeshewa nguvu zake tena alizopoteza ndipo atakapoingia katika UHARIBIFU, naye ataitawala dunia kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu na nusu ndio kile kipindi cha dhiki kuu, ndio maana biblia inasema alikuwepo naye hayupo, naye anajiandaa kwenda kwenye uharibifu. Kwasababu hapo mwanzo alishawahi kutawala na atakuja kutawala tena.

Sasa Zile pembe 10 za yule mnyama ambayo ni yale mataifa 10 ya ULAYA(EU), Biblia inasema  yatakuja kupata nguvu wakati mmoja na yule mnyama. Na haya ndiyo mpinga-kristo PAPA atakayoyatumia kuwatesa wale ambao hawataipokea chapa ya mnyama katika kile kipindi cha dhiki kuu.

Lakini mstari 16 tunaona jambo lingine..” Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.” 

Mwisho wa yote baada ya dhiki kuu kukaribia kuisha yale mataifa 10 ya Ulaya yatagundua kuwa utawala wa mpinga-kristo(PAPA) Chini ya kanisa katoliki hauna manufaa yoyote wala haujasaidia chochote kutimiza matakwa yao, na suluhu zao za AMANI, sasa kwa pamoja yatamchukia yule mwanamke(yaani PAPA) na Makao yake VATICAN  na kumwangamiza kabisa, hiyo ndio HUKUMU ya YULE KAHABA MKUU kama mstari wa kwanza unavyosema.

” Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;”

Huo utakuwa ndio mwisho wa Utawala wa Upapa na Kanisa Katoliki, kwasababu makao makuu yake VATICAN yatakuwa yameshateketezwa, hukumu hii imeelezewa kwa urefu kwenye SURA YA 18, jinsi Babeli ulivyoanguka na kuwa ukiwa mfano wa ile Babeli ya kwanza ilivyokuwa.

Baada ya huyu mwanamke Babeli mkuu kuhukumiwa, sasa mstari wa 14 unasema. zile pembe 10 (yaani yale mataifa ya ulaya)” ndio yatafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.” Kumbuka hii itakuwa ndio ile vita ya MUNGU MWENYEZI yaani “HARMAGEDONI”  inayozungumziwa kwenye ufunuo 16:16.

Ufunuo 18:1-5″

1 Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.

5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.”

Hivyo ndugu unaona ni HATARI! gani  iliyo mbele yetu?, ni wazi kabisa muda umeshaisha Yule mnyama siku yoyote anaingia katika uharibifu, kumbuka wakati huo kanisa ambaye ni BIBI-ARUSI safi atakuwa ameshanyakuliwa, bibi-arusi asiyeabudu sanamu, bibi-arusi aliyebikira kwa NENO tu na sio pamoja na mapokeo mengine yaliyo nje na NENO LA MUNGU Kama kusali Rosari na ibada za wafu. Bibi-arusi Anayemwabudu Mungu katika Roho na kweli  sio katika mifumo ya ki-DINI  na ya-kimadhehebu, Bibi-arusi aliyepokea kweli ubatizo wa Roho Mtakatifu, na kama tunavyofahamu asili ya bibi-arusi ni kuvaa vazi refu la kujisitiri, je! na wewe mwanamke mavazi yako ni ya kujisitiri?, Utakuwa mkristo na bado uwe  kahaba kwa mavazi unayovaa? kumbuka fashion zote ni dhambi! lipstic,vimini, wigy,suruali, wanja nk. vitakupeleka kuzimu mwanamke.

BWANA YESU ANASEMA…

12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, NA HAO WAABUDUO SANAMU, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.

17 NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO!  Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

TUBU ANGALI MUDA UPO.

Mungu akubariki. Kwa mwendelezo >>UFUNUO: Mlango wa 18

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada zinazoendana…


MNARA WA BABELI

CHAPA YA MNYAMA

SIRI YA KUASI KATIKA KANISA LA MUNGU.

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.

UFUNUO: Mlango wa 18


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 15

Karibu tujifunze mwendelezo wa kitabu cha ufunuo, leo tukiendelea na sura ya 15;

Ufunuo 15:1-4 

1 Kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, na ya ajabu; malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana Katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia.

2 Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.

3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.

4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.

Katika sura hii ya 15 tunaona Yohana akionyeshwa ishara nyingine kuu mbinguni kama vile alivyoonyeshwa kwenye ile sura ya 12 juu ya yule mwanamke aliyekuwa na utungu wa kuzaa ambaye tuliona anawakilisha taifa la Israeli, na ishara nyingine kuu aliyoonyeshwa mbinguni ni juu ya lile joka kubwa jekundu lililokuwa limejiandaa kummeza yule mtoto pindi atakapozaliwa, na huyu si mwingine zaidi ya shetani akipingana na YESU KRISTO na uzao wa Mungu.

Lakini katika sura hii ya 15 tunaona Yohana akionyeshwa ishara nyingine tena mbinguni iliyo kubwa na ya ajabu “malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia.”

Hawa Malaika 7 wanaoonyeshwa hapa ndio wale watakaohusika katika kumimina vile vitasa 7 vya ghadhabu ya Mungu, kumbuka katika kipindi cha ile miaka mitatu na nusu ya mwisho kati ya ile saba, Mungu atamuhukumu yule KAHABA MKUU, (utawala wa mpinga-kristo chini ya Kanisa Katoliki ) kwa kupitia zile pembe 10 ambazo zitakuja kumchukia yule mwanamke na kumtowesha kabisa kama inavyoelezewa katika (ufunuo 16:10, pamoja na Ufunuo 17 & 18),

Sasa itakayofuata ni HUKUMU YA MATAIFA yote yaliyozini na huyu mwanamke kahaba Babeli mkuu, biblia inasema…

Ufunuo 14:9-11″ Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,

10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.

11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.

Hivyo hii HUKUMU YA MATAIFA itatekelezwa na Hawa malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho ambayo katika hayo ghadhabu ya Mungu itatimia, na mapigo haya tunayaona yakitekelezwa katika sura inayofuata ya 16.

Tukiendelea mstari wa 2-4 tunaona Yohana akiona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.

Hii bahari ya kioo iliyochanganyikana na moto inaonyesha watakatifu waliosafishwa kwa moto (yaani waliopitia dhiki kuu), ndio maana ile bahari imeonekana kama imechanganyikana na moto, kama vile tunavyoona kwenye ufunuo 4:6 bahari nyingine ya kioo mfano wa bilauri na sio ya moto. Kwahiyo hawa ni watakatifu waliotoka kwa yule mpinga-kristo.

Na pia ukiendelea kusoma utaona wameshinda kutoka kwa yule mnyama na sanamu yake na hesabu ya jina lake, hawa ndio waliokataa kushirikiana na yule mnyama hivyo iliwapasa kutoa maisha yao, kwa ushuhuda wa Yesu Kristo. Kumbuka wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita yule mwanamwali mwerevu atakuwa ameshaondoka(kwenye unyakuo), amebaki yule mpumbavu (ukisoma Mathayo 25 utaona jambo hilo), hivyo kwasababu ya upumbavu wake wa kutokuwa na mafuta ya ziada kwa kujiweka tayari kumlaki Bwana wake wakati ajapo, aliachwa!, kumbuka tayari alikuwa ni mwanamwali wa Bwana isipokuwa alikuwa ni mpumbavu, hivyo itambidi akumbane na ghadhabu ya mpinga-kristo ambayo asingepaswa apitie.

Wakati unyakuo unapita sio watu wote watafahamu, utakuwa ni wa siri, na ni wachache tu watakaonyakuliwa wala hakutakuwa na ajali, wala mshtuko wowote duniani maana watakuwa ni wachache sana, Bwana Yesu alisema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na kama ilivyokuwa katika siku za luthu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu, sasa jiulize? katika siku za Nuhu walipona watu wangapi? ni watu 8 kati ya mamilioni, siku za Luthu walipona wangapi? ni 3 kati ya mamilioni na Bwana Yesu anasema ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake. Je! na wewe utakuwa miongoni mwa hao wachache watakaokwenda na Bwana katika Karamu yake?..

Mstari unaofuata unasema ..”3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.”

Hapo tunaona kuna aina mbili za nyimbo zikiimbwa 1) wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu ikiashiria watu wam Israeli watakaouawa kipindi hicho na mpinga-kristo kwa kukataa kumsujudia, 2) Wimbo wa mwana-kondoo ikifunua wakristo watakaouawa wakati wa dhiki kuu watakaokataa kuipokea ile chapa na kumsujudia. Kwahiyo hayo ni makundi mawili yatakayopitia dhiki kuu.

Tukiendelea mlango wa 15 kuanzia ule mstari wa 5 hadi wa 8 ambao ndio wa mwisho tunasoma habari ifuatayo.

Ufunuo 15:5-8

5 Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa;

6 na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung’aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.

7 Na mmoja wa wale wenye uhai wanne akawapa wale malaika saba vitasa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu, aliye hai hata milele na milele.

8 Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale a malaika saba.

Hapa tunaona hekalu la hema la ushuhuda mbinguni likifunguliwa na kujazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu ikiwa na maana kuwa ni hukumu ya Mungu, kumbuka popote palipo na hekalu la Mungu au hema ya ushuhuda utukufu wa Mungu huwa unashuka kama “wingu” kuashiria neema na rehema za Mungu mahali hapo aliposhukia lakini hapa tunaona hekalu limejaa “moshi” ikiashiria ghadhabu na hukumu ya Mungu, na kama vile inavyosema wala hakuna mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu mpaka yatimizwe yale mapigo ikionyesha kuwa mlango wa rehoema na neema mbaada ya haupo utakuwa umeshafungwa,

Na tunaona wale malaika saba walipewa vile vitasa 7 ili kumimina ghadhabu ya Mungu juu ya nchi ili kuleta mapigo yale yote Mungu aliyoyakusudia kwa wale wote waliomsujudia yule mnyama na kupokea chapa yake au hesabu ya jina lake. Katika kipindi hicho huruma Mungu haitakuwepo na watu wengi sana wataangamia. Kwa mwendelezo wa sura inayofuata ya 16 inayohusu juu ya ghadhabu ya Bwana ambayo ndio vile vitasa saba tutajifunza katika sura inayofuata…

Ndugu tunaishi katika muda wa nyongeza, na KARAMU YA MWANAKONDOO imekaribia, na watakaoshiriki ni wale watakaokwenda katika UNYAKUO TU!. Wakati wateule wa Mungu wanapokea thawabu zao na kuwa wafalme na makuhani wa Mungu milele, wewe nafasi yako saa hiyo itakuwa wapi?,

wakati watakatifu wanafutwa machozi yao na Bwana YESU wewe utakuwepo wapi?. Huu ni wakati wa kutengeza taa zetu na kujiweka tayari kwenda kumlaki Bwana, huu sio wakati wa kuambiwa uumpe Bwana maisha yako bali ni wakati wa KUFANYA IMARA UTEULE WAKO NA WITO WAKO(2petro 1:10), vinginevyo utakuwa mwanamwali mpumbavu ambaye alibeba TAA pasipo mafuta ya ziada,

Kumbuka chapa ya mnyama imeshaanza kufanya kazi, na inaanzia ndani kisha ije nje Kumalizia! na hii inatenda kazi katika madhehebu yote yaliyofanya uzinzi na kanisa kahaba KATOLIKI, ni mara ngapi unaambiwa biblia inasema hivi, wewe unasema dhehebu letu haliamini hivyo?, ni mara ngapi unaulizwa wewe ni mkristo unajibu mimi ni wa-dhehebu fulani? Je unadhani ni ROHO MTAKATIFU ndiye aliyeleta hiyo migawanyiko? jibu ni hapana shetani ndiye aliyeleta hiyo migawanyiko, na bila kujua hilo dhehebu lako lina ushirika kamili na lile kanisa mama kahaba na ndio tunaona lile jina MAMA WA MAKAHABA limezaliwa huko. Sasa kwa dizaini hii utaachaje kushawishika kuipokea ile chapa?..umeshaipokea tayari moyoni mwako kilichobaki ni udhihirisho wa nje tu! ambao hauna tofauti na ule wa ndani. Biblia inasema tokeni kwake enyi watu wangu wala msishiriki dhambi zake, kutoka sio kwa miguu tu, bali kutoka moyoni kwanza kwa kubadilisha namna ya kumwabudu Mungu, Mungu ni ROHO nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli, na sio kwa kupitia sanamu, wala dhehebu wala papa wala bikira Mariamu, wala kwa mapokeo wala kwa mtu mwingine yoyote, bali katika roho na kweli (ndani ya YESU KRISTO).

Na pia Kumbuka kanisa tunaloishi sasa ni kanisa la mwisho linaloitwa LAODIKIA, na mjumbe wake ameshapita na ujumbe wetu tuliopewa na BWANA YESU KRISTO ni huu..

Ufunuo 3:15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. “

Umeona hapo?, hili ni kanisa vuguvugu, anasema ni heri uwe moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu, hivyo chagua moja,

Ufunuo 22:10″ Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.

17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. “

Amen!

Kwa Mwendelezo >>> UFUNUO: Mlango wa 16

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada zinazoendana..


KARAMU YA MWANA-KONDOO.

UNYAKUO.

WALIOITWA NI WENGI, ILA WATEULE NI WACHACHE.

UMEITIKIA WITO INAVYOPASWA?

KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.


Rudi Nyumbani.

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 14

Kama tunavyofahamu baada ya wakati wa mataifa kuisha yaani unyakuo kupita itakuwa imebaki miaka 7 tu mpaka dunia kuisha, ndani ya hicho kipindi kifupi Mungu atakuwa anashughulika na Taifa la Israeli, na kuwatia muhuri wale wayahudi 144,000 kama tunavyosoma katika sura ya 7 ya kitabu cha Ufunuo, kwahiyo ile miaka mitatu na nusu ya kwanza itakuwa ni injili kwa wayahudi na ile miaka mitatu na nusu ya mwisho itakuwa ni wakati wa ile DHIKI KUU.

Tukiendelea na ufunuo sura ya 14 ambayo ni mwendelezo wa habari ya wale wayahudi 144000 waliotiwa muhuri na Mungu, kama haujapitia sura ya 7, unaweza ukaanzana nayo kwa kufuata link hii kisha ndio tuendelee na sura hii ya 14 >>> Ufunuo: Mlango wa 7

Ufunuo 14:1-5″ Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

2 Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao;

3 na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi.

4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.

5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.

Hapa tunaona wale wayahudi 144000 wakionekana wakiwa na mwanakondoo juu ya mlima Sayuni ikifunua nafasi za hawa wateule wa Mungu mbele za YESU KRISTO,katika utawala unaokuja wa miaka 1000, watakapomiliki na kutawala na YESU katika mlima Sayuni (yaani Yerusalemu), pia hawa wanaonekana ni bikira ikiwa na maana kwamba hawajajitia unajisi wowote na mafundisho ya dini za uongo,

Na pia kama tunavyoona walijifunza wimbo mpya ambao ni wao tu waliouweza kuuimba, sasa huu wimbo unamaana kuwa ni “furaha ya Roho Mtakatifu”, kama vile sisi wakristo tunapompokea Kristo na Bwana anapotuokoa na kutupa pumziko pale tunapomfurahia na kumshukuru wimbo mpya wa Mungu unazalika ndani ya mioyo yetu ambao hakuna mwingine anayeweza kuuimba isipokuwa mwenye Roho wa Mungu kama sisi

..Daudi alisema katika Zaburi 40:1 “Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.

2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

3 AKATIA WIMBO MPYA KINYWANI MWANGU, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana “.

Kwahiyo hawa 144000 baada ya kutiwa muhuri wa Mungu kwa kupokea Roho Mtakatifu na kupata ufunuo kwamba mwokozi wao anaishi na ndiye atakayekuja kuwapigania wimbo mpya utazaliwa ndani ya mioyo yao ambao hakuna mwingine yoyote atakayeweza kujifunza isipokuwa wao,

Na pia kumbuka watu hawa hawakuwa mbinguni, bali ni hapa hapa duniani, ukisoma kwa makini utaona sio wale 144000 ndio waliokuwa mbinguni mbele ya kiti cha enzi wakiimba hapana bali ni sauti ilisikiwa mbinguni wakiimba na hawa si wengine zaidi ya malaika, na ndio wale 144000 walionekena wakijifunza wimbo ule. Hivyo hawa 144000 hawakunyakuliwa mbinguni, bali watakuwa hapa hapa duniani.

INJILI YA MILELE:

Tukiendelea..

Ufunuo 14:6-13″ 6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,

7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.

8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.

9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,

10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.

11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.

12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.

Katika mistari hii tunaona baada ya wale 144,000 kutiwa muhuri, na Bwana akiwaweka mbali na yule mnyama watafunguliwa pia na mlango wa kuhubiri INJILI YA MILELE. Na ndio wale malaika watatu tunaona wakiruka katikati ya mbingu wakihubiri injili ya milele juu yao wakaao juu ya nchi, kumbuka Mungu hajawahi kutumia malaika kuhubiri injili duniani, siku zote huwa anawatumia wanadamu, biblia inasema malaika ni roho zitumikazo kuwahudumia watakatifu(waebrania 1:14). Hivyo watakaozihubiri hizi jumbe za wa hawa malaika warukao ni wale wayahudi 144000.

Kumbuka Injili tuliyonayo sasa ni Matendo 2:38 “…Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu “. Injili hii ni ya kuwafanya watu kuwa wakristo lakini INJILI YA MILELE ni kwa watu wote na inayojulikana na watu wote, kwamfano inajulikana kuwa ushoga ni kosa,usagaji, kuua ni kosa, kuzini, kutukana,ufiraji, kuzini na wanyama,kufanya maasi ni kosa, dhamiri ya mtu ikimshuhudia kabisa kuwa anachokifanya sio sahihi bila hata kuhubiriwa n.k. ni injili ambayo kwa ufupi hahiitaji biblia kuijua, inajulikana na watu wote wenye dini na wasio na dini. Hiyo ni hofu ya Mungu ambayo ipo kwa kila mwanadamu.

Kwahiyo INJILI hii ya MILELE itahubiriwa tena kwa mara ya mwisho kwa wanadamu wote waliopo ulimwenguni wanaotenda maasi ili mtu asiwe na udhuru wa kusema sijasikia, kwa maana kwa wakati huo maasi yatakuwa ni mengi sana duniani kama tunavyoyaona leo…

Warumi 1:18 “Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.

19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana YAMEKUWA DHAHIRI NDANI YAO , kwa maana Mungu aliwadhihirishia.

20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, UWEZA WAKE WA MILELE NA UUNGU WAKE; hata wasiwe na udhuru; ……..

32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao. “

Hivyo injili hii ya MILELE itagusa makundi yote hata wasiokuwa na dini, kwasababu ni mambo yaliyodhahiri ambayo yanajulikana na kila mtu.

Malaika wa pili akafuAata akisema “8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.”

Hawa watu 144000 baada ya kupokea ufunuo wa Mungu kuwa anayetawala dunia nzima na dini zote ni mpinga-kristo (PAPA) na jinsi kanisa Katoliki lilivyohusika kuwaua watakatifu wengi na litakapokwenda kuishia, kwamba Mungu ameshalihukumu hivyo watahubiri ujumbe wao katika dunia nzima, hukumu ya Babeli mkuu.

Tukiendelea mstari wa 9-11 tunasoma..

“9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,

10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.”

Sasa hili ni onyo la mwisho litakalohubiriwa kwa watu wote, kwamba mtu yoyote atakayemsujudia yule mnyama na sanamu yake (yaani Kushirikiana na Kanisa Katoliki na mafundisho yake au kuwa mshirika wa umoja wa madhehebu) au kuipokea chapa katika mkono wake au katika kipaji cha uso wake, atashiriki mapigo yote ya Mungu yanatakayofuata huko mbeleni.

Kumbuka hapo kanisa litakuwa limeshaondoka, watanyakuliwa watu wachache sana wakati huo ulimwengu hautajua chochote, dhiki zote zitawakuta wale waliobaki duniani, je umeokolewa?. kama biblia inavyoendelea kusema.. “13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao. “

SHINIKIZO LA GHADHABU YA MUNGU:

14 Kisha nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali.

15 Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa.

16 Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya nchi, nchi ikavunwa.

17 Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali.

18 Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana.

19 Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.

20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili. “

Mistari wa 14-20 unaelezea maandalizi juu ya ile vita ya Harmagedoni, vitakavyopigwa Israeli, Hapa tunaona malaika akiwa ameshika mundu mkali na kuvuna mzabibu wa nchi kuashiria maovu ya wanadamu yamefikia kilele, kikombe cha ghadhabu ya Mungu kimejaa wakati wa rehema hakuna tena, kinachofuata ni hasira ya Mungu kumwagwa juu ya nchi, na ndio maana unaona zile zabibu zikatupwa katika lile shinikizo kubwa la ghadhabu ya Mungu na damu ikatoka pale mpaka kwenye hatamu za farasi kwa mwendo wa maili 200, kumbuka farasi anawakilisha vifaa vya kijeshi, hii ni picha halisi inayoonyesha jinsi hiyo vita itakavyokuwa ya kumwagika damu nyingi hayo yatatimia katika kumiminwa kile kitasa cha sita kati ya vile saba vya ghadhabu ya Mungu..

Ufunuo 16:12-16″

12 Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.

13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.

14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.

15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)

16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.

Pia Ufunuo 19:11-16 Inasema…”11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, NAYE ANAKANYAGA SHINIKIZO LA MVINYO LA GHADHABU YA HASIRA YA MUNGU MWENYEZI .

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.”

Hii itakuwa ni vita ya mwisho mabilioni ya watu watakufa, na baada ya kumiminwa kile kitasa cha mwisho cha saba mwisho wa dunia utakuwa umefika. 

Hivyo ndugu kumbuka shetani hapendi ukifahamu kitabu cha UFUNUO kwasababu anajua siku ukiyajua mambo ya kutisha yanayokuja huko mbeleni utatubu na kuishi maisha ya uangalifu hapa duniani, yeye anachotaka ujue ni kuwa dunia itadumu milele na ni raha tu siku zote lakini biblia usisahau inasema 1wathesalonike 5:3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.”

Huu ni wakati wa jioni sana BWANA YESU yupo mlangoni kurudi kulinyakua kanisa lake je! na wewe utakuwa miongoni mwa wale watakaokwenda naye? Ni mara ngapi umesikia injili ubadilike lakini bado unaabudu sanamu, unapenda mambo ya ulimwengu huu zaidi ya Mungu , unavaa vimini, unapaka lipstick, unazini, mlevi, msengenyaji, mtukanaji,? Injili hiyo halitadumu milele, upo wakati mlango wa neema utafungwa hapo ndipo Bwana Yesu anasema kutakuwa na kilio na kusaga meno.

Mpe Bwana maisha yako leo uokolewe.

Mungu akubariki.

Kwa Mwendelezo >> UFUNUO: Mlango wa 15

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada zinazoendana..


INJILI YA MILELE.

ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.

JE! KUBET NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 13

Tukisoma kitabu cha Ufunuo mlango wa 13 tunaona kuna wanyama wawili wanaozungumziwa pale; wa kwanza akiwa ni yule mwenye vichwa saba na pembe 10 aliyetoka baharini na wa pili ni yule aliyekuwa mfano wa mwanakondoo mwenye pembe 2 akitoka katika nchi.

Kwa ufupi tuwatazame hawa wanyama wanawakilisha nini na wanachukua nafasi gani katika siku hizi za mwisho:

MNYAMA WA KWANZA:

Ufunuo 13:1-5″ Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.

2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.

3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.

4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?

5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.

6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.

7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.

8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.

9 Mtu akiwa na sikio na asikie.

10 Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu. “

Hapa tunamwona huyu mnyama akiwa na vichwa saba na pembe 10, na juu ya zile pembe zake ana vilemba 10, sasa hivi vichwa 7 inafahamika vinawakilisha ngome/mamlaka ambazo shetani alizikalia na kuzitumia kupambana na kuuharibu uzao wa Mungu hapa duniani tangu taifa la Israeli lilipoundwa. Na tawala hizi tunaweza tukaziona katika biblia nazo ni 1) MISRI   2) ASHURU, 3) BABELI 4) UMEDI & UAJEMI   5) UYUNANI   6) RUMI   7) RUMI -KIDINI.

Lakini Yohana alimwona yule mnyama akiwa na PEMBE 10 katika kichwa chake, kumbuka zile pembe 10 hazikuwa zimesambaa juu ya vichwa vyote saba kama inavyofikiriwa na watu wengi, bali zote 10 Yohana alizoziona zilikuwa juu ya kichwa KIMOJA TU! na sio kingine zaidi ya kile kichwa cha saba. Kwahiyo kile kichwa cha saba ndicho Yohana alichokikazia macho kwasababu kilikuwa ni tofauti na vingine vyote.

Hivyo zile pembe 10 kulingana na maono aliofunuliwa Danieli juu ya ile sanamu ya Nebukadneza alioiona yenye miguu ya chuma na nyayo zenye vidole 10 zilizochanganyikana nusu chuma, nusu udongo, kama inavyojulikana ile miguu ya chuma ni utawala wa RUMI na vile vidole ni utawala wa RUMI uliokuja kugawanyika na kuwa yale mataifa kumi ya ULAYA wakati ule ambayo yalikuwa bado hayana nguvu kwasababu yalikuwa bado hayajavikwa vilemba(CROWNS). Hivyo vile vidole 10 ndio zile pembe 10 zinazoonekana juu ya yule mnyama na ni mataifa 10 yaliyopo katika umoja wa ULAYA (EU), na kama tunavyoona sasa kwa huyu mnyama zile pembe 10 zimetiwa VILEMBA inaashiria kuwa utakuja wakati haya mataifa yanayounda umoja wa ulaya yatapewa nguvu ya utawala na yule mnyama kutenda kusudi la kuwaua watakatifu katika kipindi cha ile miaka mitatu na nusu ya mwisho ya dhiki kuu.

Leo hii tunaona umoja wa ulaya unaundwa na mataifa zaidi ya 10, lakini yatakuja kuishia kuwa 10 tu ili kutimiza unabii wa kwenye biblia na yapo mbioni kuvikwa vilemba( yaani kupewa utawala wa dunia) yakiwa chini ya yule mnyama ( RUMI) chini ya utawala wa PAPA ambaye ndiye mpinga-kristo biblia inayomwitwa “mtu wa kuasi”, mwana wa uharibifu ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.(2Thesalonike 2). Leo hii bado hayana nguvu kwasababu Danieli alionyeshwa kuwa vile vidole kumi nusu yake vitakuwa na nguvu na nusu yake vitakuwa vimevunjika ndivyo ilivyo sasa hivi Umoja wa ulaya hauna nguvu sana, lakini utakuja kupata nguvu duniani kote ili kutimiza kusudi la yule mnyama(mpinga-kristo)

Tukiendelea kusoma mstari wa tatu tunaona moja ya kichwa chake (ambacho ndio kile kichwa cha saba) kimetiwa jeraha la mauti nalo likapona. Kumbuka Rumi-ya kidini(UKATOLIKI) iliyokuwa chini ya UPAPA katika historia ilikuwa inatawala dunia nzima, na ilifanikiwa kupata nguvu dunani kote kiasi cha kwamba mtu yeyote aliyeonekana anakwenda kinyume na hiyo dini adhabu ilikuwa ni kifo tu, mamilioni ya wakristo waliouwa wote waliokataa kuisujudia miungu yao ya kipagani, jambo hili liliendelea na hii dini ilizidi kupata nguvu hadi kufikia karne ya 16 wakati wa matengenezo ya kanisa ambapo Mungu alianza kuwanyanyua watu wake kama Martin Luther ambaye alianza kufundisha watu “kuhesabiwa haki kwa imani” na kukosoa mafundisho potofu ya kanisa Katoliki lakini PAPA alipotaka kumuua mfalme wa Ujerumani alisimama kumuhifadhi Luther, ndipo watu wengi wakaanza kuacha hii dini ya uongo na kuligeukia NENO la Mungu hivyo Ukatoliki ukaanza kupungua nguvu, na wakati huo huo Mungu aliwanyanyua wengine kama Calvin, Zwingli, Knox n.k. ili kulitengeneza tena kanisa lililokuwa limeharibiwa na mafundisho ya uongo ya Kanisa katoliki.

Hapo ndipo ulipokuwa mwanzo wa lile jeraha la yule mnyama lakini pigo hasa lilikuja karne ya 18 mwaka 1798 katika mapinduzi huko Ufaransa Jenerali Berthier alipeleka vikosi vyake Roma na kumng’oa PAPA katika utawala wake, akamchukua mateka pamoja na mali zake zote za dini yake, Hivyo ikapelekea dini ya kikatoliki iliyokuwa inatiisha dunia kuwa karibuni na kutoweka kabisa, hilo lilikuwa pigo kubwa sana lilofananishwa na jeraha la mauti lakini tunaona Biblia inasema lile JERAHA LA MAUTI lilipona,

 Je! Jeraha hili liliponaje na lilipona lini?.

Wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia, matatizo yalikuwa mengi duniani, uchumi ulishuka sana, mataifa ya ulaya yaliaanza kuanguka na kupoteza nguvu zao kutokana na athari ya vita, Hivyo kiu ya kutafuta amani duniani ikaongezeka kumbuka wakati huo huo Marekani ilianza kupata nguvu, na likiwa kama taifa la kikristo (protestant) lenye nguvu kubwa ya kiuchumi na kijeshi hivyo kwa kushirikiana na mataifa ya ulaya kwenye harakati za kutafuta amani, (isiyokuwa ya kivita) walianza kuutambua umuhimu wa PAPA Kwasababu alionekana kuwa ni mtu mwenye mvuto na anayekubalika na watu wengi duniani, hivyo mataifa mengi yakaanza kutuma mabalozi wake kwa papa ajihusishe na masuala ya AMANI YA DUNIA. Sasa kuanzia hapo jeraha lake la mauti likaanza kupona, wale ambao walikuwa wanafanya mageuzi kinyume chake(protestants) wakaanza kushirikiana nae tena, uprotestant ukabakia kuwa jina tu na ndio huko inapoundiwa ile sanamu ya mnyama nitakayoielezea zaidi mbeleni…

Tukiendelea mstari 4 & 5, Tunaona lile joka ambaye ni Shetani mwenyewe alimpa nguvu yule mnyama naye akaanza kunena maneno makuu ya makufuru. Tukisoma pia kitabu cha Danieli alizungumziwa kama ile PEMBE ndogo iliyozuka na kungo’a wale wafalme watatu na kunena maneno ya makufuru Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. “ Na huyu si mwingine zaidi ya mpinga-kristo ambaye ni PAPA,..Si ajabu PAPA leo anasimama “badala ya mwana wa Mungu duniani”..Vicarivs filii Dei, ..Papa leo amejivika uwezo wa kusaheme dhambi jambo ambalo BWANA YESU KRISTO mwenyewe ndiye anayeweza kulifanya ..haya yote ni maneno ya makufuru, na yapo mambo mengi zaidi ya hayo ambayo ni makufuru. Kumbuka ninaposema PAPA namaanisha kile “CHEO”..kwahiyo yeyote anayekikalia hicho cheo amejitwika cheo cha mpinga-kristo mwenyewe.

Na tunaona wakati wa mwisho atapewa uwezo wa kutenda kazi miezi 42, hii ni miaka mitatu na nusu, kati ya ile miaka saba ya mwisho ya lile juma la 70 la Danieli. Hichi kitakuwa kipindi cha DHIKI KUU, sasa hivi PAPA anaonekana kama mtu asiyekuwa na madhara yoyote, anakuja kwa njia ya kujipendekeza ili apate nguvu kiurahisi, kama kitabu cha Danieli kinavyomtabiri, leo hii duniani kote anajulikana kama “MTU WA AMANI”, Ni mtu mwenye wafuasi wengi duniani, na aneyekubalika kuliko mwanasiasi yoyote duniani, dini nyingi zimeanza kuvutiwa naye, hata waislamu sasa wanamwona kama ni mtetezo wao mtu anayejali watu wote, PAPA anasema wote tunamwabudu Mungu mmoja ila kwa njia tofauti tofauti (yaani wakristo, waislamu wahindu, wabudha tunamwabudu Mungu mmoja), angali biblia inasema YESU ndiye njia pekee ya kumfikia Mungu, na cha ajabu umaarufu wake unaongozeka na watu wanamfurahia ili kutimiza ule unabii kwamba “watu wote ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio watakaomsujudia.” Na kumsujudia sio kumpigia magoti bali ni kukubaliana na mifumo yake na imani yake.

Ndugu yangu mpinga-kristo hatakuja na mapembe kichwani, akilazimisha watu wamwabudu, kumbuka biblia inasema shetani ana HEKIMA kuliko Danieli, na sehemu nyingine biblia inasema ile roho itataka kuwadanganya yamkini hata wateule. Siku zote anakuja kama malaika wa nuru, usitazamie kuwa mpinga-kristo atakuwa muislamu au muhindi au freemason, hapana ndugu yupo kanisani amebeba biblia na anafanya kampeni za amani duniani na watu wanamshangilia na kumbusu, biblia inasema hapo ndipo “PENYE HEKIMA ” .

Kwahiyo inahitajika Hekima kumjua vinginevyo utachukuliwa na mafuriko yake kama wengi walivyochukuliwa huu ni wakati wa kuwa macho sana, jali maisha yako ya umilele yanayokuja. Chunguza maandiko kama watu wa Beroya, sio kila roho inayoshabikiwa na wengi unaipokea moyoni mwako kwasababu biblia inasema IPO NJIA IONEKANAYO KUWA NJEMA MACHONI PA WATU..LAKINI MWISHO WAKE NI UPOTEVU, na BWANA YESU alisema njia iendayo upotevuni ni PANA na wengi wanaiendea hiyo.

MNYAMA WA PILI:

Ufunuo 13:11-18″

11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.

12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.

13 Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.

14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.

15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.

16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;

17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. “

Tunaona huyu mnyama wa pili ana pembe kama mwanakondoo, lakini sio mwanakondoo, na huyu anaonakana ametoka katika nchi na sio katika bahari na yeye hana vichwa saba Kama yule mnyama wa kwanza, ikiwa na maana kuwa utawala wake haukuanzia mbali kama yule mnyama wa kwanza bali ulizuka mwishoni. Hivyo huyu mnyama si mwingine zaidi ya MAREKANI. Ukiangalia katika ile nembo ya Marekani katika ile dola yao utaona yule tai akiwa ameshika mishale 13, ile piramidi kuna ngazi 13, kuna nyota 13 juu ya yule tai, matawi 13 ya ule mzeituni ulioshikwa ..nk. kila mahali 13..13… na taifa la Marekani linaonekana katika UFUNUO 13.

Pia huyu mnyama alipewa uwezo wa kufanya watu wote wakaao duniani wamsujudie yule mnyama wa kwanza na kuunda ile SANAMU YA YULE MNYAMA.

Sasa Sanamu ya mnyama ni ipi?

Marekani kama taifa lilokuwa la kiprotestant ambalo hapo kwanza lilikuwa halishakamani wala halishirikiani na kanisa Katoliki kwa namna yoyote, lakini katika karne ya 20 baada ya vita ya pili Vya dunia liliacha njia ya kweli ya NENO LA MUNGU, na kurudi kuiga tabia za yule mnyama,kazi nzuri na juhudu zote zilizofanywa na wale wana-matengenezo zikawa ni bure, ni sawa na mbwa aliyerudia matapishi yake.

Baada ya kuibuka jopo kubwa la madhehebu ya kiprotestant duniani, viongozi wa madhehebu ya kimarekani walikutanika kwa agenda ya kutaka kuondoa tofauti katikati ya wakristo ili kufikia muafaka mmoja wa IMANI, ndipo walipounda BARAZA LA MAKANISA ULIMWENGUNI (World Council Of Churches), na NATIONAL COUNCIL OF CHURCHES , na ndio chimbuko la EKUMENE. (Ecumenical council)

Na Kanisa Katoliki likiwa kama washirika wao wa karibu wakiwasaadia.

Baraza hili la UMOJA WA MAKANISA liliazimu kuyarudia mambo yale yale ya ukahaba yaliyofanywa na kanisa Katoliki, Iimekuwa ni SHIRIKA LA KI-DINI, na Linasheria zake na itakadi zake ambazo zinaenda kinyume na mpango na NENO LA MUNGU. Kwahiyo UMOJA HUU ndio unaoitwa SANAMU YA MNYAMA..Kwasababu tabia zote zilizokuwa katika kanisa kahaba katoliki zipo nazo kule na hivi karibuni yule mnyama (America) ataenda kuipa PUMZI ILE SANAMU INENE, ili watu wote waiabudu, hii ikiwa na maana siku sio nyingi watu wote duniani watenda kulazimishwa kuwa washirika wa muunganiko wa hayo makanisa mtu yeyote atakayeonekana kwenda kinyume atauawa.

Na kama tunavyoona huyu mnyama wa pili (MAREKANI) anaweza kufanya ishara kubwa hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni, jambo hili linatupa picha nguvu za kijeshi walizonazo Marekani kama uwezo wa kushusha makombora makubwa ya vita kutoka angani mabomu ya atomic n.k.

Hili baraza la makanisa duniani sasa linafanikiwa kuzivuta dini zote ulimwenguni pamoja, ikiasisiwa na PAPA kiongozi wa kanisa katoliki duniani, itafika wakati kama hautakuwa mshirika wa dini au kanisa ambalo halijaunganishwa katika huu UMOJA WA MAKANISA NA DINI hutaweza kuuza wala kununua wala kuabudu, wala kuishi katika jamii,

Leo hii tunaona vitendo vya kigaidi na vya mauaji vikiongezeka, wanasiasa wameshindwa kuirejesha amani ya dunia, na matatizo yote yahusuyo amani yanatokana na mizozo ya kidini tunaweza kuona mambo yanayoendelea mashariki ya kati mfano Israeli, syria-kuna ISIS,Iraq, Lebanoni-kuna hezbolah, myanmar huko Asia kuna warohighya, sehemu za Afrika nchi kama Nigeria kuna Boko kuna haramu, Somalia-alshabaab, central Africa- antibalaka ..na makundi mengine mengi sana,. tunaona mizizi yote ya migogoro inaanzia katika DINI. Hivyo atahitajika mtu wa KIDINI mashuhuri kutatua migogoro ya kidini na sio wanasiasa au watu wa kijamii – Na huyu atakuwa si mwingine zaidi ya PAPA kwasababu yeye ndiye anayekubaliwa na dini zote pamoja na wafalme wote wa dunia.

Hivyo atapokwisha kupata nguvu, ataibua mfumo mmoja wa kutambua watu wote duniani kwa imani zao, kwa kivuli cha kuleta amani na kukomesha vitendo vya uvunjifu amani duniani kumbe nia yake itakuwa ni kuwateka watu wote duniani na kuwatia ile CHAPA YA MNYAMA. Wakati huo watu wengi duniani wataufurahia huo mfumo pasipo kujua ndio wanaipokea chapa hivyo. Wengi watasajiliwa katika madhehebu na dini zao zilizokuwa na ushirika huo wa UMOJA WA MAKANISA ULIMWENGU , Vitatumika vitu kama CHIPS, IDS, na utambulisho mwingine utakotengenezwa ili kuyafikia makundi yote, sasa wale watakaokaidi ndio watakaopitia dhiki kuu, hao ndio watakaoonekana magaidi na wavunjifu amani, kama sivyo kwanini wasikubali utambulisho huo mpya? na kumbuka watakuwa ni wachache sana watakaogundua kuwa ndio CHAPA YENYEWE ,

Hivyo ndugu injili tuliyonayo sasa hivi inasema ..UFUNUO 18:4-5″ Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU,MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, wala msipokee mapigo yake.Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “

Ndugu toka katika mifumo ya madhehebu kwasababu yameshirikiana na yule mnyama(kanisa katoliki) kufanya ukahaba, na kuua watakatifu wa Mungu wengi, yeye anaitwa BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA ikiwa na maana kama yeye ni mama wa makahaba ni dhahiri kuwa anao mabinti na wao pia ni makahaba kama mama yao alivyo na hao mabinti sio wengine zaidi ya madhehebu yote yaliacha uongozo wa Roho mtakatifu na kuandamana na desturi za kanisa kahaba Katoliki, hivi karibuni tumesikia WALETHERANI wameungana rasmi wakatoliki.!! Biblia inasema TOKENI KWAKE ENYI WATU WANGU, kama ukishirikiana naye inamaanisha kwamba na wewe pia utashiriki mapigo yake ndivyo Mungu anavyokuchukulia.

Ufunuo 14:9 ” Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. “

Bwana ametuita kuwa BIKIRA SAFI, na bikira tu ndiye atakayeingia katika karamu ya mwanakondoo, toka kwenye mifumo ya madhehebu umwabudu Mungu katika ROHO NA KWELI.

Mungu akubariki, na Mungu atusaidie katika safari yetu tuumalize mwendo salama

Amen.

Kwa Mwendelezo >> UFUNUO: Mlango wa 14

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada zinazoendana…


CHAPA YA MNYAMA

DANIELI: Mlango wa 2

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

UFUNUO: Mlango wa 21


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 12

MAELEZO JUU YA “UFUNUO 12”

Ufunuo 12

1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.

2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.

3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.

4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.

5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.

6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.

7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.

12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.

13 Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.

14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.

15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.

16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.

17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.

Ukisoma Ufunuo mlango wa 11, utaona habari ya wale MASHAHIDI WAWILI wakifanya kazi ya kuwahubiria injili wale Wayahudi 144,000 na kutiwa muhuri (Ufunuo 7). Na tunaona walifanya kazi yao miezi 42, (yaani miaka mitatu na nusu) na baada ya kumaliza ushuhuda wao yule mnyama atokaye kuzimu atawaua lakini baada ya siku tatu na nusu tunaona Mungu atawafufua.

Kumbuka baada ya kanisa kunyakuliwa, injili itahamia Israeli na itakuwa imebakia miaka 7 tu mpaka mwisho wa dunia utakapofika kulingana na unabii wa Danieli 9:27, kwenye lile juma moja la mwisho kati ya yale majuma 70 aliyoonyeshwa.

Hivyo ndani ya hii miaka 7, nusu yake yaani miaka mitatu na nusu ya kwanza, hawa manabii wawili watafanya kazi ya kuwahubiria wayahudi, na nusu ya pili iliyobaki itakuwa ni kipindi cha ile DHIKI KUU (yaani miaka 3.5 ya mwisho).

Sasa tukiendelea kusoma kitabu cha Ufunuo 12 tunaona Yohana akiona ishara kuu mbinguni, yule mwanamke aliyevikwa jua na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake na juu ya kichwa chake taji ya nyota 12.

Ukiangalia huyu mwanamke anawakilisha taifa la Israeli, ukisoma mwanzo 37:9 utaona ile ndoto aliyoota Yusufu aliona jua na mwezi na zile nyota 11 zikimwinamia ambayo tafsiri yake tunafahamu ilikuwa ni Yakobo kama jua, mwezi kama mama zake, na wale wana 11 wa Israeli kama zile nyota. Hivyo yule mwanamke ni taifa la Israeli.

Ukiendelea kusoma mstari wa pili utaona yule mwanamke alikuwa na mimba, na katika hali utungu wa kutaka kuzaa, na akamzaa mtoto mwanamume ambaye atawachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Maana ya ule utungu ni unabii au matarajio ya kuzaliwa masiya katika Israeli ambaye alikuwa akisubiwa kwa muda mrefu, Na huyu mtoto mwanamume si mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO yeye ndiye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma katika ule utawala wa miaka 1000 (Ufunuo 2:27).

Ukizidi kusoma utaona pia katika mstari wa 3-6, utaona ishara nyingine ilionekana lile joka kubwa jekundu (ambalo ni shetani) likiwa limejiandaa pale atakapozaliwa yule mtoto limmeze, lakini halikufanikiwa, jambo hili tunaliona lilitimia wakati Bwana YESU anazaliwa Mfalme Herode, alipopata habari kuwa mfalme aliyetabiriwa kazaliwa katika Israeli alifadhaika na kutaka kumwangamiza mtoto YESU, Lakini hakufanikiwa mpaka Mungu alipomchukua juu mbinguni katika kiti chake cha enzi.

Tukiendelea kusoma kuanzia ule mstari wa 7-12, Tunaona habari nyingine inayohusu vita vinavyoendelea mbinguni, kati ya Malaika watakatifu na shetani pamoja na malaika zake, kwa maelezo marefu juu ya vita hivyo unaweza kufungua hapa >> Vita vinavyoendelea mbinguni

Lakini tukiendelea mstari wa 13 tunaona baada ya yule mtoto kunyakuliwa juu (yaani Yesu kupaa AD 30) yule joka aliendelea kumuudhi yule mwanamke,tunaona katika historia alizidi kumuudhi kwa takribani muda wa miaka 2000 mpaka sasa, aliwatesa na kuwaua wayahudi katika nyakati tofauti tofauti, mfano wakati wa utawala wa Adolf Hitler aliwaua wayahudi zaidi ya milioni 6, katika historia tunaona wayahudi ni watu wamekuwa wakichukiwa na mataifa mengi n.k.

Mstari wa 14, tunasoma mwanamke yule baada ya kuudhiwa muda mrefu akapewa MABAWA MAWILI YA TAI yule mkubwa ili aruke aende mbali na yule Joka aliyetupwa chini ili kufanya vita na watakatifu kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Yale mabawa ya Tai ni injili ya wale manabii wawili wa ufunuo 11, watakaowahubiria wayahudi ili kuwafanya wamjue yule joka kubwa jekundu ni nani (MPINGA-KRISTO), na utendaji kazi wake na namna ya kumuepuka, na ndiye anayetaka kukaa katika Hekalu la Mungu kuabudiwa kama Mungu.

Kumbuka wale manabii wawili katika injili yao ndio watakaomfunua yule mpinga-kristo kwa wayahudi kuwa si mwingine zaidi ya kiongozi maarufu anayetoka katika utawala wa RUMI, mwenye kivuli cha Amani kumbe ndani yake ni joka linalotaka kuabudiwa, Kama tu vile lile joka lilivyokuwa ndani ya HERODE-Mrumi kutaka kumwangamiza YESU vivyo hivyo hilo joka litakuwa ndani ya mpinga-kristo atakayetoka katika utawala ule ule wa Rumi kutaka kuwaangamiza wayahudi.

Hivyo wale wayahudi 144,000 (ufunuo 7), watakapoamini ile injili ya wale manabii wawili watakayoihubiri ile miaka mitatu na nusu ya kwanza, pamoja na zile ishara na yale mapigo yatakayofuatana nao, Hawa wayahudi wachache 144,000 watafahamu kuwa yule joka anawawinda, na kwamba DHIKI KUU itaanza hivi karibuni, hivyo Mungu atawafungulia mlango wa kuwaficha mbali na yule JOKA pale dhiki itakapoanza,

Kwahiyo hili kundi dogo litaondoka ISRAELI, Mungu atawapeleka mahali alipowaandalia mahali ambapo yule mpinga-kristo hataweza kuwafikia (hii ndio maana ya kupewa mabawa ya Tai), lakini kumbuka sio wayahudi wote wataikubali ile injili ya wale manabii wawili bali ni wale tu 144,000 tu.

Watakaosalia ile miaka mitatu na nusu ya mwisho itakapoanza (ambacho ndio kipindi cha dhiki kuu), watapata mateso mengi yasiyokuwa na mfano tangu ulimwengu kuumbwa na hayatakuwepo hata baada ya hapo, kumbuka dhiki hii itajumuisha pia watu wote wa mataifa watakaokataa kuipokea ile chapa ya mnyama wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita.

Kama tu vile kipindi cha kuzaliwa kwa YESU wale mamajusi walipomletea Herode habari ya kuzaliwa mfalme Israeli, malaika walimwonya Mariamu na mwanawe waondoke Israeli kwasababu mpinga-kristo(Herode) anakwenda kuleta dhiki, walikimbilia Misri kabla ya ile dhiki kuanza, lakini yule Herode alipoona kuwa wale mamajusi wamemlaghai, alikasirika akaenda kufanya vita na uzao wote uliobakia wa watoto wa Israeli,

Tunaona kulikuwa na maombolezo makuu Yerusalemu watoto wote walichinjwa. Vivyo wale manabii wawili (Ufunuo 11) wanafananishwa na wale MAMAJUSI ambao walimtangazia Herode habari mbaya za kuzaliwa mfalme, na wakati wa mwisho wale MANABII WAWILI pia watamtangazia mpinga-kristo kwamba mfalme kazaliwa tena mioyoni mwa WAISRAELI na kwamba anayepaswa kuabudiwa ni yule mtoto na sio yeye, na kama vile Herode alivyowakasirika mamajusi pamoja na Mariamu na mtoto vivyo hivyo mpinga-kristo wakati wa mwisho atawakasirikia wale MASHAHIDI WAWILI na kuwaua, lakini baadaye hakufanikiwa kuwaangamiza kabisa kwani walifufuka kama vile wale mamajusi walivyopewa njia ya kumtoroka Herode,

Na kama vile ni mwanamke mmoja tu (Mariamu) kati ya wanawake wote wa Israeli ndiye aliyekuwa na mimba ya mwokozi ndani, vivyo hivyo ni lile kundi dogo tu (144000) ndio litakalokuwa na ufunuo wa YESU mioyoni mwao utakaoletwa na wale manabii wawili wanaofananishwa na mamajusi.

Na pia kama tunavyoona Mariamu alipelekwa peke yake Misri mbali na Herode vivyo hivyo na wale 144,000 ndio tu watakaopelekwa mbali na mpinga-kristo wakati wa dhiki itakapoanza walioabakia wote yaani mamilioni ya waisraeli itawapasa wapitie DHIKI KUU kama tu wale wanawake wengine wa Israeli walivyouliwa wana wao.

Kwahiyo hawa 144,000 hawataguswa na yule joka kubwa jekundu na ndio maana tunawaona katika Ufunuo 14 wakiwa wamesimama na mwanakondoo juu ya mlima Sayuni, bikira safi wa Mungu, hawa wataingia katika ule utawala wa miaka 1000, pasipo kupitia madhara yoyote.

Kwa ujumla Ufunuo sura ya 12, inaelezea ISRAELI na jinsi yule mwanamke alivyofananishwa na taifa la Israeli.

Kwahiyo ndugu tazama ni wakati gani tunaishi, je! umepokea kweli Roho Mtakatifu? umebatizwa katika ubatizo sahihi? Maisha yako yanastahili unyakuo?. Kumbuka sasa Taifa la Israeli linanyanyuka, dalili zote zinaonyesha kuwa unyakuo upo mlangoni na injili inakaribia kurudi Israeli, Maombi yangu utubu,

Fahamu tu yule JOKA kubwa jekundu alishatupwa chini akiwa na ghadhabu nyingi akijua muda wake umebaki mchache, Hivyo utendaji wake wa kazi wa sasa sio kama ule wa zamani anatafuta kukupeleka kuzimu kwa gharama zozote, hivyo ni wakati wako wewe kusimama imara na kuuthibitisha wokovu wako.

Mungu akubariki.

Kwa mwendelezo >> UFUNUO: Mlango wa 13

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada zinazoendana..


MARIAMU

UZAO WA NYOKA.

MPINGA-KRISTO

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.


Rudi Nyumbani

Print this post