Title September 2019

Je! Unaweza kubatizwa na usipokee Roho Mtakatifu?. Na Je! Unaweza kupokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono?

SWALI: Habari mtumishi…, ninaswali hapa naomba uniweke sawa.

Matendo ya mitume 8:14 “ na Mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu,wakawapelekea Petro na Yohana,

15.ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu,

16. kwa maana bado hawajashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.

17.Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu”.. 

Sasa swali langu limegawanyika katika vipengele 3..a) Je! unaweza kubatizwa na usimpokee Roho Mtakatifu kama hawa watu wa Samaria ilivyokua?. b) Je! unaweza mpokea Roho Mtakatifu kwa kuombewa kama Petro na Yohana walivyofanya?. c) Kwa jamii yetu ya kawaida ni kigezo gani kinatumika kwa mtu kuwabatiza wengine au awe na sifa zipi huyo mbatizaji ili tupate ubatizo sahihi?


JIBU: Shalom, Bwana akubariki kwa swali zuri, Kwanza ni muhimu kufahamu umuhimu wa ubatizo sahihi, Ubatizo sahihi ni kama Leseni ya Roho Mtakatifu kukaa ndani ya mtu, yaani mtu anapobatizwa katika ubatizo sahihi, amemhalalisha Roho Mtakatifu kuingia ndani yake na kuwa wake. 

Hivyo Roho Mtakatifu anaweza kushuka juu ya mtu kabla au baada ya kubatizwa, lakini uhalali wa kukaa moja kwa moja ndani ya mtu unakuja baada ya mtu kubatizwa. Sasa tukirudi kwenye swali la kwanza linalouliza “a) Je! unaweza kubatizwa na usimpokee roho mtakatifu kama hawa watu wa Samaria ilivyokua?” Jibu ni ndio! Kama umeamini na kutubu dhambi zako kwa kudhamiria kuziacha, na ukaenda kubatizwa, lakini hujawahi kusikia lolote juu ya Roho Mtakatifu, hapo hawezi kuingia ndani yako, kwasababu Roho hawezi kuja juu ya mtu ambaye hajawahi kabisa kuzisikia habari zake, ni sharti kwanza mtu huyo ahubiriwe Roho Mtakatifu ni nini, ndipo ashuke juu yake, Hata Bwana Yesu hawezi kuingia ndani ya moyo wa Mtu kama mtu huyo hajahubiriwa kabisa, au hajawahi kusikia kabisa habari za Yesu…. hivyo Kwa mtu aliyeamini na kutubu na kubatizwa ipasavyo, Roho Mtakatifu mwenyewe atahakikisha anamletea mhubiri ambaye atamweleza kuwa kuna kitu kinachoitwa Roho Mtakatifu ndipo ashuke ndani yake. Ndicho kilichotokea kwa hawa watu wa Samaria na wale Wakorintho Paulo aliokutana nao..

Matendo 19:1 “Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;

2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.

3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.

4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.

5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.

6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.

7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili”.

 Na pia Roho Mtakatifu anaweza kushuka juu ya mtu kabla hajabatizwa endapo tu atakuwa ameshasikia kuwa kuna kitu kinachoitwa ROHO MTAKATIFU, kama mtu ameshasikia kuwa kuna kitu kinaitwa Roho Mtakatifu na jinsi anavyotenda kazi, basi Roho anaweza kushuka juu ya huyo mtu kabla hata hajabatizwa, lakini ili awe na uhalali wa kukaa ndani ya huyo mtu ni lazima mtu huyo akabatizwe ili kukamilisha wokovu wake…Ndicho kilichotokea kwa Kornelio akida wa Kirumi wakati Petro amekwenda nyumbani kwake.. 

Matendo : 10:44 “Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno

45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.

46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu,

47 Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?

48 Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha”. 

Swali la pili linasema “Je! unaweza mpokea Roho Mtakatifu kwa kuombewa kama Petro na Yohana walivofanya?” Jibu ni ndio! Unaweza kupokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono, lakini sio wakati wote!.. mara nyingi watu wanapokea Roho pasipo hata kuwekewe mikono, mfano siku ya Pentekoste mitume hawakuwekewa mikono na mtu yeyote, na hata wakati Petro yupo nyumbani kwa Kornelio kama tulivyosoma hapo juu, wale watu hawakuwekewa mikono na mtu yeyote lakini Roho alishuka juu yao..hivyo Roho anaweza kushuka juu ya mtu aidha kwa kuwekewa mikono na watiwa Mafuta wake au bila kuwekewa mikono. Ni kwa jinsi Roho atakavyopenda!..Na kwa jinsi Roho atakavyomuongoza yule anayehudumu. Swali la tatu … “kwa jamii yetu ya kawaida ni kigezo gani kinatumika kwa mtu kuwabatiza wengine au awe na sifa zipi huyo mbatizaji ili tupate ubatizo sahihi?” 

Jibu: Vigezo vinavyotumika vya mtu kuwabatiza wengine ni vigezo vile vile vya mtu anayetaka kuwa mhubiri!..Mtu akitaka kuwa mhubiri, au mwalimu kwa wengine ni sharti kwanza awe mwanafunzi wa Kristo, pili awe na uwezo wa kufundisha wengine kitu ambacho yeye mwenyewe anakiishi, na awe na uelewa wa kutosha wa kitu anachokwenda kukifanya, Awe Ameitwa na Mungu kweli na anafahamu kuwa anafanya kazi ya Mungu na si ya mwanadamu…

Kadhalika mtu anayetakiwa kubatiza wengine anapaswa na yeye mwenyewe kwanza awe amebatizwa katika ubatizo sahihi, na awe na uelewa wa kutosha kuhusu ubatizo yaani faida za kubatizwa na hasara za mtu kutokubatizwa ili aweze kuwafundisha vyema wale ambao watakuja kubatizwa naye!. Mtu mwingine yoyote asiyekuwa na vigezo hivyo haruhusiwi kifanya kitendo hicho kitakatifu. 

Bwana akubariki!


Mada Nyinginezo:

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.

UPEPO WA ROHO.

JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?

FAIDA ZA MAOMBI.

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.

 


Rudi Nyumbani:

Print this post

Katika Yakobo 1:13 Biblia inasema Mungu hamjaribu mtu, lakini tukirudi kwenye kitabu cha Mwanzo 22:1 tunaona Mungu alimjaribu Ibrahimu. Hapo naomba mwanga zaidi.

JIBU: Tunapaswa tufahamu mistari hiyo ilikuwa inalenga katika Nyanja gani, mfano kama tukisoma huo wa Yakobo1:13 Unasema  

“Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.

14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.”  

Unaona ukiangalia hapo kwa makini utagundua kuwa analenga katika mambo maovu, kwamfano uzinzi, au ulevi, uchawi, usengenyaji, wizi,n.k. Kwamfano utakuta mtu ni mkristo, na hapo mwanzo alikuwa hazini wala hanywi pombe, lakini pengine ghafla mbele yake kikapita kichocheo kimojawapo cha zinaa labda tuseme kahaba, au picha chafu za ngono, sasa yeye badala avikatae na avikimbie hivyo vichochezi yeye kidogo kidogo anavutiwa navyo na kuanza kuvifuatilia au kudokoa na kuvitazama, huko ndiko kuvutwa na kudanganywa kwenyewe kunakozungumziwa hapo, na kama akizidi kuendelea kuviendekeza hivyo vichocheo baadaye vinazaa dhambi hapo ndipo unakuta mtu wa namna hiyo anaingia katika uzinzi moja kwa moja, na anakuwa mbaya kuliko hata wale aliowakuta huko na mwisho wa siku anazaa mauti kwasababu ile dhambi ilisha komaa hapo hawezi kugeuka tena kilichosalia ni kwenda kwenye ziwa la moto.  

Sasa mtu kama huyo hawezi kusema Mungu alikuwa anamjaribu,kumletea kahaba, kwasababu Mungu hashikamani na ouvu wa aina yoyote..bali ni tamaa ya mambo yake ndio iliyokuwa inamvuta huko. Yusufu alipojaribiwa na mke wa Potifa sio Mungu aliyekuwa anamjaribu pale, bali ni ouvu, lakini yeye aliishinda kwasababu hakuiendekeza hiyo roho.

Lakini pia ifahamike kuwa mtu yeyote anapoamua kumfuata Mungu, inamaanisha kuwa anakuwa mwanafunzi wa Kristo moja kwa moja, na tunajua kuwa hakuna mwanafunzi yeyote anayesoma tu bila kujaribiwa kwa mitihani, hiyo haipo?, Mwalimu atajuaje kuwa huyu mwanafunzi ameelewa au la, Vinginevyo shule itajikuta inaandaa watu wasiokuwa na uwezo wa kitaaluma, Vivyo hivyo kwa Mungu pia kuna mitihani,unajaribiwa kuangaliwa kama umekidhi vigezo au la!   Na kujaribiwa huko hakuna lengo la kukuangusha, bali kukuimarisha. Mwalimu yoyote mwenye akili timamu hawezi kuwajaribu wanafunzi wake kwa kuwachanganya kwenye bweni moja wanafunzi wa kike na wa kiume walale humo humo, kwa lengo la kupima kiwango chao cha elimu..huko ni kuwapoteza na sio kuwafundisha, bali atawapa mitihani kulingana na wanachofundishwa darasani,   Na ndivyo Mungu anavyofanya kwa watoto wake wote, hawajaribu kwa maovu, bali kwa yale waliyokuwa wanafundishwa na kuyapitia katika imani yao, na ndio yaliyomkuta Ibrahimu na ndiyo yaliyowakuta wana wa Israeli na ndiyo yatakayokukuta wewe ambaye unasema umeamua kumfuata Kristo..

Mwanzo 22:1 “Ikawa baada ya mambo hayo Mungu ALIMJARIBU Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.

2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”  

Ukisoma tena habari ya wana Israeli walipokuwa jangwani utaona Mungu akiwaambia hivi…  

Kumbukumbu 8:2 “Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, KUKUJARIBU kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.

3 Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana.

4 Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini.”  

Vivyo hivyo leo hii unaweza kusema umemfuata Yesu, lakini kusema hivyo tu haitoshi, Mungu ataipima imani yako kwake,..pengine anaweza kuruhusu ukachekwa kwa ajili ya wokovu wako, aangalie je! Utauacha?, ataruhusu uchukiwe na kutengwa na ndugu, aangalie je! Kweli ulimaanisha kumfuata?, ataruhusu upitie kupungukiwa aangalie je! Unampenda wakati wa raha tu, au hadi wakati wa mateso, ataruhusu upitie hiki au kile..Huko ndio kujaribiwa na Mungu. Lakini Mungu hawezi kukuletea pombe, au kahaba, au hirizi au pesa haramu, ukasema ni Mungu anakujaribu,,ukikutana na mambo ya namna hiyo maovu fahamu kuwa unajaribiwa kwa tamaa zako mwenyewe sio kwa ajili ya IMANI yako.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO.

AYUBU ALITESEKA KATIKA MAJARIBU KWA MIAKA MINGAPI?

TUTAWEZAJE KUMZALIA MUNGU MATUNDA?

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?

MSHAHARA WA DHAMBI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Mungu anasema hatagharikisha dunia na maji tena,.Kwanini watu wanasema dunia itaangamizwa?

SWALI: Shalom watumishi wa Mungu Leo nina swali nataka niulize maana linanitatiza jambo hili ni kutoka kitabu cha Isaya. 

Isaya 54:9 “ Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea.

10 Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye”

 Je! swali lina kuja hivi mtumishi Leo hii kuna watu nimewaskia wakisema hakuna ghadhabu ya Mungu tena mana amekwisha sema maji ya Nuhu hayatapita tena na tunajua maji ya Nuhu ilikua ni siku ya mwisho ya dunia je! ni kweli Mungu hata shusha hasira yake tena? kuna watu wana sadiki kujitetea na maovu yao kupitia neno hli wakisema hakuna hukumu tena maana Mungu amekwisha apa!


JIBU: Shalom! Ni kweli Mungu hataingamiza dunia tena kwa maji, kama Neno lake hilo linavyosema hapo juu! Lakini hiyo haimaanishi kuwa dunia haitaangamizwa, itaangamizwa lakini sio kwa maji, bali na kwa kitu kingine, kwasababu Neno linasema kama zilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu (yaani siku za mwisho) kwahiyo kama siku za Nuhu ulimwengu uliangamizwa kwa maovu yake, kadhalika na siku hizi za mwisho ulimwengu utaangamizwa vile vile kwa maovu yake..lakini si kwa maji. Na kama si kwa maji basi ni kwa kitu gani?…Jibu lipo kwenye biblia hiyo hiyo..tusome:

 2 Petro 3:5 “Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;

6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.

7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu” 

Kwahiyo siku sio nyingi dunia hii itakwenda kugharikishwa KWA MOTO!..Usidanganyike hata kidogo kuwa hakuna hukumu inayokuja!..Hukumu ni lazima ije kwasababu Mungu alishasema ni lazima ije!..Hivyo ni kuwa macho na kukesha katika roho ili siku hiyo isitujie kama mwivi. 

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

PEPETO LA MUNGU.

LAANA YA YERIKO.

BIDII YA MFALME YOSIA.

Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Mstari huu una maana gani? “Tupa chakula chako usoni pa maji; Maana utakiona baada ya siku nyingi”. (Mhubiri 11:1)

JIBU: Shalom, utaona katika mstari huo anatumia neno “Tupa” na sio hifadhi au weka, ikiwa na maana ya kupoteza kitu chako cha thamani, chakula chako, na hapo anaendelea kusema kitupe usoni pa maji, ukisoma tafsiri nyingine utaona anasema kwenye habari, au maji mengi, na tunafahamu sikuzote ukitupa kitu mtoni au ziwani au baharini hapo ni kuhesabu kuwa umekipoteza hutakipata tena, sembuse chakula, ambacho kinayenyuka na kuoza haraka..

Lakini kinyume chake mhubiri anatuambia, “maana utakipata baada ya siku nyingi”..Ili kuelewa vizuri huo mstari tusome mistari inayofuata baada ya hiyo, 1 Tupa chakula chako usoni pa maji; Maana utakiona baada ya siku nyingi.

(Mhubiri 11: 2 Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane; Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi.

Maji mengi kwenye biblia yanawakilisha “watu wengi au mataifa, au makutano (soma Ufun.17:15)”….Unaona, kumbe alimaanisha uwagawie watu sehemu ya fungu lako, bila kujali malipo au watakurudishia nini, unafanya kama unapoteza, Kwamfano unaweza ukawa unavi hazina kidogo kwenye mfuko wako na pengine anatokea mtoto wa ndugu yako anaomba msaada wa ada ya shule, huku mwingine anakuomba chakula, mwingine anakuomba nguo, mwingine anakuomba hifadhi, maadamu vipo ndani ya uwezo wako fanya kuwapa tu kama vile huna matumizi na hiyo fedha, kwasababu biblia inasema hujui mbeleni kutakuwaje, pengine huyo mtu unayemsaidia sasa anaweza akawa msaada mkubwa sana kwako au kwa watoto wako, au kwa ndugu zako.  

Tajiri mmoja wa kidunia ambaye leo hii anajulikana duniani kote anayeitwa Bill Gates, zamani alipokuwa kijana mdogo, alipenda kwenda kusoma magazeti, lakini kwa bahati mbaya alikuwa hana pesa ya kununa gazeti lakini mahali hapo kulikuwa na mzee mmoja mwafrika mweusi, alimnunuliza magazeti, hilo lilimwingia sana moyoni, miaka mingi ikapita akaanza kufanikiwa na kuwa tajiri sana kwa ugunduzi wake wa Microsoft, akakumbuka wema aliofanyiwa na huyo mzee, alingarimika kumtafuta popote alipo, alipomwona alimpatia kiasi cha dolla milioni moja, ambayo kwa pesa yetu ni zaidi ya sh. Bilioni 2,.Unaona gazeti la sh.1000, linakuja kumzaliwa Bilioni 2. Miaka mingi baadaye.  

Hivyo Mhubiri anatufundisha hekima ya maisha ya kawaida, kuna usemi unaosema “kinachokwenda nje ndicho kinachokurudia”, leo hii mtu ukiwa mbinafsi na kuwadharau wengine kwa mafanikio yako kidogo uliyopewa na Bwana, ziangalie pia siku za mbeleni kwa jinsi ya kibinadamu. Na ndio maana hapo anasema sehemu, uwagawie watu 7 hata nane,.Hii Ikimaanisha usichague aina Fulani tu ya watu, tupa kokote,poteza kokote utakuja kupata hicho ulichokipoteza baada muda Fulani, haijalishi itachukua miaka mingi, lakini mwisho wa siku utakipata tu. Hata chakula vyenye asili ya mbegu kama maharage au mahindi, ukivitupa mahali penye ardhi yenye asili ya maji maji baada ya muda Fulani vitakuja kukuwa na kuzaa, na hivyo kukipata kile ulichokipoteza na Zaidi.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.

JIRANI YAKO NI NANI?

NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

WATU WASIOJIZUIA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Maneno haya yana maana gani? “Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu HAMTOI ROHO KWA KIPIMO. (Yohana3:34)”

JIBU: Tukianzia mistari ya juu anasema: 

Yohana 3:31 “Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote.

32 Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake.

33 Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli.

34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo

.35 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.

36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia”. 

Kama tukichunguza hapo tunaona ni Kristo pekee ndiye anayeshuhudiwa katika biblia nzima kuwa “aliyaona na kuyasikia” mambo yote ya Mungu, Na hiyo ni kwasababu yeye alitoka huko, na asili yake ni huko, tofauti na wanadamu wengine wote, hivyo hata kile atakachokishuhudia duniani ni lazima kitakuwa ni Ukweli mtupu usiokuwa na chembe chembe yoyote ya mapungufu, Na ndio maana kila kilichotoka katika kinywa chake kilikuwa ni Neno la Mungu halisi kabisa.. Tofauti na manabii wake na watu wengine wote ambao wakati mwingine iliwapasa watafiti, tafiti wachunguze chunguze, 

1Petro 1:10 “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.

11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.

 Matendo 17:26 “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;

27 ili wamtafute Mungu, INGAWA NI KWA KUPAPASA-PAPASA, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu”. 

Vile vile mitume nao, japo walifunuliwa mambo yote na Roho mtakatifu lakini bado walikuwa hawana ufahamu wote wa mambo yote, 

1Wakoritho 13.9 “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;

10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika…….wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana”. 

Umeona, aliyefahamu mambo yote ni YESU KRISTO mwenyewe,ambaye hapo mwanzo alikuwapo kwa Mungu, yeye alikuwa ashuhudiwi kwanza na Roho ndipo aseme kama vile mitume walivyofanya, bali kilichokuwa kinatoka kwenye kinywa chake ni maneno ya ROHO mwenyewe akizungumza mbele za watu ndio maana aliwaambia mahali fulani, maneno yangu ni Roho tena ni uzima.

Yohana 6.63 “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”Hivyo mtu yeyote akiyasikia maneno ya Kristo, na kuyashika, ni Roho wa Mungu mwenyewe ndio anayejaa ndani yake..

Na ndio maana Yohana akamshuhudui, kuwa hamtoi Roho kwa kipimo. Leo hii ukisikiliza maneno ya watumishi wote wa Kristo, utapata kipimo cha Roho wa Mungu, kwasababu maneno yanayotoka katika vinywa vyao hajakamilika yote, lakini ukisikiliza maneno ya Kristo, utapata kiwango kamili cha Roho wake, kwasababu ni Neno lililotakasika lisilo la chembe ya uchafu, lisilo na kipimo …Na maneno ya Kristo ndio BIBLIA TAKATIFU,..ukiisioma hiyo, na kuiishi hiyo utapokea kiwango kamili cha Roho wake, bila kipimo…Kwasababu maneno yake ni ROHO. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?

JE MUNGU ANAMJARIBU MTU?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! ni halali kutoa cheti kwa wakristo wanaooa?

JIBU: Ndio ni halali, Tunapaswa tutofautishe kati ya yale maagano ya mwilini na yale ya rohoni. Tunapookoka na kubatizwa katika ubatizo halali, hapo ni sawa na tumefungishwa ndoa na kuwa mwili mmoja na Kristo, ni hiyo ni ndoa ya kimbinguni kwasababu haitambuliki katika mwili, hata karamu yake haifanyiki huku bali kule mbinguni, vivyo hivyo nacheti chake ni lazima kiwe cha kule, na cheti chenyewe ndio ule uzima wa milele, pale tunapojua majina yameandikwa katika kitabu cha uzima.

Lakini mtu anapooa, au anapoolewa, haowi mbinguni au haolewi mbinguni bali ni hapa hapa duniani, hivyo kuwa na ushahidi au uthibitisho wa uhalali wa ndoa hiyo ni muhimu kuwepo, ni moja ya vigezo vya kuzingatiwa katika hatua za mwisho za ndoa. Na sio lazima kiwe ni cheti kabisa lakini walau waraka wa makubaliano uliothibitishwa na mashahidi kanisani (Mchungaji wako na waumini). Ikiwa tu kitendo cha kuachana katika Israeli kilihitaji “hati/cheti” (Mathayo 19:7, Kumbu 24:1) si zaidi kukubaliana?.  

Na Hiyo faida yake ipo katika mwili, mojawapo ni hii unaweza kwenda mahali ugenini na mkeo, mkashindwa kuruhusiwa kuingia, au kushirikiana katika mambo Fulani, au kulala pamoja kwa kuwa tu hamna cheti cha ndoa, hususani katika nyumba za wageni.   Pili hata ikitokea mmojawapo amefariki, hatua za kimirithani, yaani urithishaji mali, kama hakuna cheti inamaanisha, Serikali ya kidunia inaweza kukuzuia usiwe na haki ya kumiliki mali za mwenza wako ambazo mlizichuma pamoja.   Hivyo japo katika roho cheti kinaweza kisiwe na maana yoyote, Na wala biblia haijaagiza lolote kuhusu hilo, lakini katika mwili kina umuhimu mkubwa, na pia ili kuiheshimisha ndoa yako, na kuipa thamani yake, ni vizuri ukapewa hati ya ndoa kanisani kwako.(Waebrania 13:4).

Bwana akubariki.


Mada Nyinginezo:

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

NDOA NA TALAKA:

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.

JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?.

SIFA TATU ZA MUNGU.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Ni kwa jinsi gani Mungu anapatiliza maovu ya baba zetu sawasawa na Kutoka 20:5-6?

SWALI:Kule katika kitabu cha KUTOKA 20:5-6.Mungu alisema”NAWAPATILIZA WANA MAOVU YA BABA ZAO.. Sasa hivi Baba wa Fulani akimwiba mke wa jirani yake na kumwua..Mungu Atawapatiliza adhabu hao watoto wa baba Fulani Kwa huo wizi na uuaji wake?? Shalom.


JIBU: Ukisoma mistari yote inasema hivi 

Kutoka 20:4“Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia”.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE CHA WANICHUKIAO,

6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Mwishoni mwa mstari wa 5 inasema hata kizazi cha tatu na cha nne cha “wanichukiao”. Kumbe cha hao wamchukiao, na sio cha wampendao, kama baba yako alikuwa ni mwovu anaabudu sanamu, halafu na wewe mtoto kwa kulijua hilo unafanya yale yale ambayo baba yako alikuwa anayafanya, hapo laana ya baba yako pamoja na yako mwenyewe itakupata…

Na ndivyo ilivyokuwa kwa wana wa Israeli, enzi zile za wafalme, jambo kuu lililowafanya wachukuliwe utumwani, kupelekwa Ashuru na Babeli ni kutokana na kuwa walikuwa hawampendi Mungu, Kwani baada ya kuona Baba zao na wafalme wao wanatenda maovu wanasimamisha maashera na kuabudu miungu mingine, wao badala ya kutubu wakayaiga yale yale waliyokuwa wanayafanya, hivyo Mungu alikasirika akayaketa maovu ya Baba zao wote yakawapata hao, mpaka walipotawanywa katika mataifa yote..

 Lakini pia ukisoma mstari wa 6 anasema “nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”. Ikiwa na maana kuwa hata kama Baba zako walikuwa ni waovu vipi, Hivyo Mungu akakusudia kuulaani uzao wao wote, ikatokea wewe (mtoto) anampenda Mungu na kumcha, basi rehema zake zinakuwa juu yake, kana kwamba hujazaliwa katika kizazi chenye laana. Hapo linatimia hili neno.

Ezekieli 18: 20 “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake”.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001312.

 

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


SIKU ZA MAPATILIZO.

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA.

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

UNYAKUO.

LILE TUMAINI LILILO NDANI YETU LINAPOULIZIWA.

JE! VIUMBE VINATAZAMIAJE KWA SHAUKU KUFUNULIWA KWA MWANA WA MUNGU?


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; Mstari huu unamaana gani?.

JIBU: Zipo thawabu za aina nyingi na tofauti tofauti katika biblia, Kuna thawabu za kukubali kushutumiwa au kuteswa kwa ajili ya Kristo (Luka 6:22),Si wengi wanazipenda hizi, Kuna thawabu ya kutenda mema (Luka 6:35), vilevile kuna thawabu za utumishi (1Wakorintho 3:8), kuna thawabu za wanaomtafuta Mungu kwa bidii tu(Waebrania 11:6), kuna thawabu ya kumfanyia Mungu kitu bila unafki, mfano kufunga, kusali, na kutenda wema,…Kuna thawabu za kuisapoti kazi ya Mungu(Malaki 3:10), na nyingine nyingi..Hivyo ni mtu tu kuchagua ni ipi au zipi zitakazomfaa. 

Vile vile zipo thawabu nyingine kama hizi, mfano kumpokea Nabii,(Akimaanisha watumishi wote wa Mungu), na kupokeo huko kupo kwa namna mbili, ya kwanza ni kumpokea kwa alichokibeba, na kumpokea kwa alichopungukiwa..kile alichokibeba ni ujumbe wa Mungu..

Mtu akiupokea ule ujumbe ambao mtumishi wa kweli wa Mungu anamletea, tayari moja kwa moja utayaathiri maisha yake na kumbadilisha,na kumbariki, hiyo ni thawabu ya kwanza iliyo kuu, lakini pia namna ya pili ni pale anaponyoosha mkono wake kwa kile alichopungukiwa, yaani kumuhudumia aidha kwa kwa malazi, mavazi, fedha, chakula, hiyo ni thawabu ya pili ambayo Mungu atahakikisha ni lazima amlipe mtu anayefanya hivyo. Halikadhalika, mtu akimstahi mwenye haki, (hapa anamaanisha mkristo mwenzake), atapokea thawabu kulingana na wema aliomtendea, vile vile haiishii hapo, hata akimstahi mzazi wake, atapata thawabu ya mzazi, akimstahi jirani yake, atapata thawabu ya jirani, akiwastahi maskini, Mungu atampa thawabu ya maskini, kipimo kile kile apimacho ndicho hicho hicho atakachopimiwa..hata ukiwastahi wanyama,mimea, mazingira utapata thawabu ya vitu hivyo.n.k. Lakini iliyokuu kati ya hizi zote, ni hiyo ya kuiendeleza kazi ya Mungu, na ya pili yake ni kuwastahi watumishi wake, kwasababu hapo utakuwa umemfanyia Kristo mwenyewe.. Na ndio maana ukisoma mstari wa juu yake na ule wa mwisho utaona anasema.. Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma…Na pia anasema..

Mathayo 10:40 “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.

41 Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.

42 Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.”..

Hapo anasema kwa kuwa ni “MWANAFUNZI”..sio kwa kuwa ni “maskini au mkulima” hapana bali kwa kuwa ni mwanafunzi….Ikiwa na maana kuwa kumpokea mtu wa Mungu kuna thawabu kubwa kuliko kuwapokea watu wengine wa kawaida.

Sehemu nyingine Bwana alisema maskini mnao sikuzote, lakini mimi hamnami (Yohana 12:8), hivyo unapoligawa fungu lako Mungu aliokubariki kwa wengine, aidha wazazi, maskini, marafiki, ndugu, ambao hao sikuzote unao, usisahau fungu lako kubwa kulirudisha mikononi mwa Mungu, kwasababu huko ndiko kwenye thawabu kubwa na nyingi zaidi tena zidumuzo.. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.

MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.

NAMNA GANI NITAPOKEA NGUVU ZA BWANA YESU?.

JINA LA MUNGU NI LIPI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Shetani anatolea wapi fedha, angali tunajua Fedha na dhahabu ni mali ya Bwana?.

SWALI: Watu hawa wanao mtumaini shetani na kupata utajiri na Mali, shetani anavitoa wapi?, Na wakati Neno linasema Mali na fedha na dhahabu ni vya Mungu?, Wakolosai 1 :16-17 je shetani anavichukuaje kwa Mungu na kuwapa watu hawa, ingali yeye hana vitu?Je! shetani ana Mali, fedha na dhahabu anavyowapa watu wanaomwabudu?.


JIBU: Ni kweli fedha na dhahabu ni mali ya Bwana (Hegai 2:8). Lakini swali ni kwa namna gani shetani anamiliki fedha? Kama fedha yote ni mali ya Bwana.….Tofauti na watu wengi wanavyofikiri kuwa shetani anakiwanda cha kutengeneza fedha mahali Fulani kuzimu na hivyo mtu akitaka anakwenda kuzimu na kupewa kitita Fulani kama begi na hivyo akirudi huku duniani anakuwa Tajiri ghafla…… lakini kiuhalisia shetani hamiliki mali kwa namna hiyo. Hakuna kiwanda chochote kuzimu cha kutengeneza fedha, wala hakuna fedha zozote zinazofichwa kuzimu…..

Mfumo wa shetani wa kumiliki fedha na mali upo hapa hapa duniani na unatenda kazi hivi;…shetani anawaingia watu wake (wanaweza kuwa wachawi au watu waovu) na kuwashawishi kutengeneza mfumo au taasisi fulani ambayo ni ya kishetani ambayo kwa kupitia hiyo ataweza kukusanya fedha nyingi…ndio hapo kwa kupitia watu wake wadogo atawashawishi watengeneze vitu kama Bar, Casino, sehemu za anasa na starehe n.k ambazo kwa kupitia hizo atawarushia watu mapepo waende kwenye hivyo vitega uchumi! Na hivyo huyo mtu kupata faida Fulani ya haraka kwa kupitia hiyo kazi ya kishetani!…sasa Hizo fedha au mali mtu atakayopata kupitia hiyo taasisi ya kishetani ndio fedha ambazo kapewa na shetani. 

Sasa kwa watu wakubwa na wasomi, hatawapeleka kwenye biashara ndogo ndogo hizo, atawaingiza kwenye mitandao yake mikubwa Zaidi labda biashara za madawa ya kulevya, na makampuni ya utengenezaji wa pombe na sigara, ambayo hayo yanatengeneza faida kubwa sana duniani kutokana na wanunuzi wake kuwa wengi…. 

Na haishii hapo tu! Anakazana kila siku kukusanya utajiri wa ulimwengu kwa nguvu zote, kila siku anatafuta njia ya kuvuta fedha nyingi na mali nyingi kuzipeleka kwenye taasisi zake hizo. Na anabuni taasisi mpya kila siku na kuzianzisha hapa hapa duniani…Na anatafuta viongozi wa serikalini wa juu na wa kidini kuwaweka kama viongozi na waongozaji wa taasisi zake hizo, na ili kazi zake ziende vizuri… Sasa endapo mtu wa kawaida akienda kuomba kazi katika mojawapo ya hizo taasisi zake anampa mtu huyo masharti Fulani na endapo akikubaliana nayo ndio anapata kazi na akikataa anaikosa…ndio hapo kama ni mwanamke ataambiwa pengine aanze kuvaa kikahaba, au aachane na mume wake na aolewe na mshirika wa hiyo taasisi nk.. 

Na kuna sehemu nyingine na mashirika mengine ambayo huwezi kupata nafasi ya kazi au fursa mpaka umekuwa mshirika kamili wa kikundi hicho. Na utakitambuaje kuwa ni kikundi cha kichawi? Ni pale utakapoona unapewa masharti Fulani pengine ya kutoa kutoa kafara, kuabudu vitu usivyovijua au kulazimishwa kusema maneno fulani…sasa ukishajiunga kwenye kikundi chao basi wanakuajiri na kukupa mshahara mkubwa, sasa hizo fedha mtu atakazozipata kutokana na kazi hiyo ya kishetani ndio fedha za kishetani zenyewe hizo, ambayo shetani alishaziwekeza kupitia hayo mashirika yake maovu. Na anampa yeyote kwa jinsi atakavyo.

Lakini hana kiwanda cha kutengeneza fedha. Na kuna sehemu nyingine na mashirika mengine ambayo huwezi kupata nafasi ya kazi au fursa mpaka umekuwa mshirika kamili wa kikundi hicho. Na utakitambuaje kuwa ni kikundi cha kichawi? Ni pale utakapoona unapewa masharti Fulani pengine ya kutoa kutoa kafara, kuabudu vitu usivyovijua au kulazimishwa kusema maneno fulani…sasa ukishajiunga kwenye kikundi chao basi wanakuajiri na kukupa mshahara mkubwa, sasa hizo fedha mtu atakazozipata kutokana na kazi hiyo ya kishetani ndio fedha za kishetani zenyewe hizo, ambayo shetani alishaziwekeza kupitia hayo mashirika yake maovu. Na anampa yeyote kwa jinsi atakavyo.

Lakini hana kiwanda cha kutengeneza fedha. Na baadhi ya mashirika mengine yanayobeba utajiri mkubwa wa shetani ni mashirika yote ya betting, mashirika ya kutengeneza vipodozi, mashirika ya Rotary, mashirika ya Samaritani, mashirika ya kutengeneza filamu, na MASHIRIKA YA DINI ZA UONGO na kuna dini ambazo ukikubali kujiunga tu kwa tamaa ya kulipwa mshahara na kufuata taratibu zao utapewa misaada mikubwa ambayo gharama zake hutajua zilipotoka…atapata na fursa na channels nyingi, lakini kumbe unatumika katika ufalme wa giza…. kwahiyo pia ni muhimu kabla ya kuingia kwenye shirika Fulani kufanya kazi ni vizuri kulitathmini kwanza shirika hilo au kampuni hilo, misingi yake ni nini? Pia mshirikishe Mungu katika maamuzi yako.. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.

MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.

CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.

SEHEMU YA MAANDIKO ILIYOFICHWA.

MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini, tuimbe, je! kuna ulazima wowote wa kufanya hivyo?

SWALI: Bwana Yesu asifiwe wingu la mashahidi. Nmekutana na swali naomba upana wa somo hili. Kwa nini tunaimba na kuna sura nyingi zinasisitiza kuimba mfano Luka 19 :37-38 na vitabu vya zaburi na ufunuo. Na tofauti ya kuimba na kuongea au kusema mf ufunuo 5:12-14 n.k. naomba ufunuo juu ya mambo hayo. Amen.


JIBU: Shalom ndugu yangu..   Hatuimbi kwasababu tumeagizwa, lakini tunaimba kwasababu ni kitu tulichoumbiwa ndani yetu.. Ni kama vile kucheka, kukasirika, kuona huruma, hivi vitu haviji kwasababu tumeagizwa na Mungu, au tunapoambiwa tuvifanye. hapana bali ni vitu vinavyotoka vyenyewe ndani, ndivyo ilivyo katika kuimba kila mwanadamu haijalishi ni mwema au mwovu, atapenda tu kuimba, asipopenda kumwimbia Mungu basi atapenda kumwimbia shetani.…. Na hili ni lango la haraka sana linalomchukua mtu rohoni naweza kusema zaidi ya malango mengine, kama vile kufunga, …kuimba ni lango linalomwingiza katika roho haraka sana.  

Na ndio maana Mungu anapotuagiza tumsifu, anasisitiza tumsifu kwa nyimbo, kumbuka sifa za Mungu kiuhalisia sio nyimbo, sifa ni kitu kinachokuja kutoka ndani ya moyo na hiyo ni aidha baada ya kuuona uweza na ukuu wa Mungu, au kuona wema wake kwako..hapo ndipo sifa zinapokuja, na hizo zinaweza kudhihirishwa nje kwa njia mbali mbali aidha kwa kuzungumza au kwa vitendo mfano kuruka ruka mbele zake, kusujudu, au kuimba, ambapo kunajumuisha kuabudu.  

Lakini kwanini Mungu anasisitiza tumsifu kwa nyimbo, ni kwasababu kuimba kunaleta bubujiko la haraka zaidi kuliko kuzungumza kwasababu kuimba kunahusisha na hisia za mtu za ndani kabisa..Wanaomwimbia shetani, wakiimba nyimbo zao huwa wanakuwa kama vichaa, ni kwasababu wanamwimbia katika roho, Na ndio maana Mungu anasisitiza tumsifu yeye kwa aina mbalimbali za vinanda na ustadi wa kila namna umpendezao..kwa kadri ya wingi wa ukuu wake.  

Zab 150: 1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. 2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. 3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; 4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; 5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.  

Ubarikiwe.

Print this post