Jina la BWANA wetu YESU KRISTO lihimidiwe.
Katika sura zilizotangulia (yaani ya 1-6), tuliona zikielezea sana sana historia za maisha ya watakatifu waliyopitia zaidi kuliko unabii lakini kuanzia Mlango huu wa 7 na kuendelea tunaona Danieli akionyeshwa maono ya mambo yatakayokuja kutokea katika siku za mwisho. Tukisoma..
Danieli 7:1-8” Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.
2 Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.
3 Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.
4 Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.
5 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.
6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.
7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
Tukirejea kwenye ile sura ya pili tunaona jinsi Mfalme Nebudreza akionyeshwa katika ndoto Falme nne zitakazotawala dunia mpaka hapo ALIYE JUU(YESU KRISTO) atakapochukua Falme zote za dunia, hivyo Danieli alimpa tafsiri yake, Ufalme wa kwanza ukiwa ni Babeli, wa pili ukiwa ni Umedi na uajemi, wa tatu ukiwa ni ufalme wa uyunani na wa nne ni Rumi. Jambo hili hili tunaona linajirudia tena katika sura hii ya 7, Danieli akifunuliwa zile zile Falme 4 zitakazotawala ulimwengu wote mpaka mwisho wa dunia isipokuwa hapa anaonyeshwa kwa undani zaidi.
Hapa aliona wanyama 4, wakitoka baharini, kumbuka bahari inawakilisha mikusanyiko ya watu wengi(makutano){ufunuo 17:15, } hivyo hizi falme zitanyanyuka kutoka katikakati ya watu.Kumbuka wanyama hawa 4 Danieli aliowaona ndio yule yule mnyama Yohana alioonyeshwa akitoka Baharini mwenye vichwa 7 na pembe 10, wa kwenye Ufunuo 13 isipokuwa hawa wameunganishwa wote pamoja..
“ufunuo 13:1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa MFANO WA CHUI, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya DUBU, na kinywa chake kama kinywa cha SIMBA, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. “
Tutazame wanyama hawa.
MNYAMA WA KWANZA:
Kama tunavyosoma yule mnyama wa kwanza alionekana kama mfano wa SIMBA na akiwa na mabawa ya tai, kumbuka utawala wa kwanza Babeli ndio uliohusika kuwapeleka wana wa Israeli utumwani, ulifananishwa na simba ukisoma Yeremia 4:5-6 inaelezea kuwa watu walioichukua Israeli mateka na kuwapeleka Babeli walifananishwa na kama simba aangamizaye mataifa. Na pia kama anavyoonekana na mabawa ya tai hii inaashiria uharaka wake katika kuteka, kitu kinachopaa siku zote kina kasi kuliko vinavyokwenda kwa miguu hivyo Babeli ulikuwa mwepesi wa kuteka.
Habakuki 1:6″ Kwa maana, angalieni, nawaondokesha Wakaldayo {wakaldayo ni wa-babeli}, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao.”
7 Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe.
8 Farasi zao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwa-mwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; HURUKA KAMA TAI AFANYAYE HARAKA ALE. ”
Kwahiyo tunaona hapo yule mnyama wa kwanza ni ufalme wa Babeli ambao ulikuja kuanguka baadaye na kunyanyuka mwingine wenye nguvu kushinda huo.
MNYAMA WA PILI:
Mnyama huyu anaonekana akifanana na Dubu, na pia anaonekana kama ameinuliwa upande mmoja ikiwa na maana kuwa anazo pande mbili na upande mmoja imezidi mwingine, na tunafahamu utawala huu si mwingine zaidi ya ufalme wa UMEDI na UAJEMI, na historia inaonyesha ufalme wa Uajemi ulikuwa na nguvu zaidi kuliko Umedi , hivyo zilipoungana zikaja kuundoa ufalme wa Babeli katika mamlaka yake na kuimiliki dunia upya, na pia yule Dubu anaonekana akiwa na MIFUPA MITATU ya mbavu kinywani mwake hizi ni ngome tatu walizoziangusha hawa wafalme wa Umedi na Uajemi, nazo ni Lidya, Misri na Babeli.
Ukisoma Isaya 13:15 ilishatabiri ukatili wake hata kabla ya utawala huo kunyanyuka.inasema ..
“15 Kila mtu atakayeonekana atatumbuliwa, na kila mtu atakayepatikana ataanguka kwa upanga.
16 Na watoto wao wachanga watavunjwa-vunjwa mbele ya macho yao, nyumba zao zitatekwa nyara, na wake zao watatendwa jeuri.
17 Tazama, nitawaamsha WAAMEDI juu yao, ambao hawaoni fedha kuwa kitu, wala hawafurahii dhahabu.
18 Na nyuta zao zitawaangusha vijana; wala hawatahurumia mazao ya tumbo; jicho lao halitawahurumia watoto.
19 Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza.”
ukizidi kusoma utaona huyu mnyama anaambiwa “ainuke ale nyama tele” ikiwa na maana kuwa atapewa uwezo wa kuteka mataifa mengi, na ndivyo ilivyokuja kuwa, katika historia inaonyesha Umedi na Uajemi uliteka na kutawala mataifa mengi Kuanzia India mpaka Ethiopia majimbo 127 (Esta 1:1) inaelezea vizuri.
MNYAMA WA TATU:
Mnyama huyu wa tatu Danieli alimwona akiwa mfano wa chui mwenye vichwa vinne, tukisoma..”6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”
Huu ni utawala wa UYUNANI (UGIRIKI) ambao ulikuja kunyanyuka baada ya mtawala wa Uyunani “Alexander the great” kuiangusha ngome ya Umedi na Uajemi, ni mtawala aliyekuwa na nguvu sana, kama chui alivyo mwepesi wa kushika mawindo yake, ndivyo ilivyokuwa kwa huyu mtawala mdogo, kila alipokwenda kupigana na maadui zake alifanikiwa, kwa muda wa miaka 12 tu alikuwa tayari amekwishafanikiwa kuiteka dunia nzima. Lakini naye pia hakudumu sana katika utawala wake, alipokuwa na miaka 31 alipata ugonjwa na kufa, hivyo hakuacha mtu wa kumrithi baada yake, Hivyo ikasabisha wale majemedari waliokuwa chini yake kupigania ufalme lakini hakufanikiwa kutokea mwenye nguvu kama za Alexander hivyo ufalme ule ukagawanyika katika pande NNE, Ambavyo ndio vile vichwa vinne vya yule mnyama; Cassander, Lysimachus ,Ptolemy na Seleucus.
MNYAMA WA NNE:
“7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
Mnyama huyu ni utawala wa RUMI, ndio ile miguu ya chuma kwenye yale maono aliyoyaona Mfalme Nebukadreza kwenye Danieli 2, na mnyama huyu hapa anaonekana akiwa na meno ya chuma, ikiashiria ana nguvu nyingi za kuharibu na kusagasaga, na pia hapa anaonekana na pembe 10, ambavyo ndio vile vidole 10 vya kwenye ile sanamu ya Nebukadreza. Kumbuka utawala huu ndio uliokuwa utawala katili kuliko yote iliyotangulia, na ndio unaotawala hata sasa katika roho,Lakini Katika historia, utawala wa Rumi ya magharibi ulikuja kugawanyika katika mataifa 10 yanayojitegemea AD 476, ambayo ni
1) Alemanni– kwa sasa ni Ujerumani
2) Franks – kwa sasa ni Ufaransa
3) Burgundians-Kwa sasa ni uswizi
4) Visigoths -Hispania
5) Lombards-Italia
6) Anglo-Saxons– Uingereza
7) Suevi- Ureno
8) Vandals -iling’ofolewa na ile pembe ndogo iliyozuka
9) Ostrogoths-ilingom’ofolewa na ile pembe ndogo iliyozuka
10) Heruli– iling’ofolewa na ile pembe ndogo iliyozuka
Lakini tukiendelea kusoma mstari wa 8 tunaona kuna PEMBE nyingine ndogo ikizuka
“8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake PEMBE TATU katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
Hivyo baada ya Danieli kuona haya alitamani kufahamu ile pembe ndogo maana yake ni nini??, Kama tunavyosoma Danieli 7:19 Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;
20 na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake.
Kumbuka Pembe zinawakilisha ufalme au mfalme, Hivyo zile pembe 10 zinasimama kama wafalme wenye falme, vivyo hivyo na ile pembe ndogo ya 11 iliyoonekana kuzuka na kung’oa pembe nyingine tatu ni mfalme atakayenyanyuka na kuangusha wafalme wengine watatu. Historia inaonyesha mara baada ya utawala wa RUMI kugawanyika katika zile Falme 10, utawala wa KIPAPA ulizuka na kungusha tatu ya hizo ngome 10, pale zilipotaka kushindana na utawala wa PAPA aliziharibu kabisa na kuzishinda na hizo si nyingine zaidi ya Vandals, Ostrogoths na Heruli.
Na kama tunavyosoma pembe hiyo ilijitukuza sana na kunena maneno makuu ya makufuru, tunafahamu cheo pekee kinachosimama kama Mungu duniani ni cheo cha UPAPA, leo hii katika enzi yake yeye anasimama kama ” badala ya Kristo duniani”, anao uwezo wa kusamehe dhambi, anafahamika kama mtawala wa mbinguni, duniani, na chini ya nchi, N.K. hayo yote ni maneno ya makufuru mbele za Mungu. watu wanamtazama duniani yeye kama Mungu.
Lakini Mstari wa 21 unasema. ” Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; “ hakuishia tu katika kujitukuza lakini aliendelea hata kufanya vita na watakatifu Hili ni jambo limekuwa likijirudia katika historia tangu utawala wa KIPAPA chini ya Kanisa Katoliki uanze, wakristo wengi wamekuwa wakiuliwa kikatili pindi tu pale walipoonekana wanaenda kinyume na Dini hiyo. Wakristo zaidi ya milioni 68 waliuawa kikatili walipoonekana tu wanalishika Neno na kupinga mafundisho ya uongo ya kanisa hilo. Kumbuka wakatoliki sio wapinga-kristo isipokuwa ule mfumo wa lile kanisa na kile cheo anachokikalia kiongozi wa lile kanisa ndio cha MPINGA-KRISTO MWENYEWE.
Mstari wa 25 unasema ” Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa WAKATI, NA NYAKATI MBILI, NA NUSU WAKATI “. Hii inafunua siku mpinga-Kristo yule PAPA wa mwisho atakaposimama kutenda kazi.
Kumbuka hawa PAPA waliopo sasa hivi na waliopita wamekaa katika viti vya mpinga-kristo lakini yupo MMOJA atakayesimama na kubadilisha majira, na sheria, biblia inasema
( 1Yohana 2:18 “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba MPINGA KRISTO YUAJA , hata sasa WAPINGA KRISTO WENGI wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho).
Na siku sio nyingi atasimama atawale na kuitesa dunia kwa nyakati na nyakati mbili na nusu wakati, ambayo ni miaka mitatu na nusu, kwasababu kibiblia nyakati moja ni mwaka mmoja.
Hivyo hiyo itakuwa ni miaka mitatu na nusu ya dhiki kuu,. labda anaweza akawa ndio huyu PAPA aliyepo sasa au mwingine muda utaeleza yote.. Huu ni wakati wa kujiweka tayari muda wowote mambo yanabadilika, Hauoni sasa hivi anavyozunguka kuleta DINI zote pamoja, akiwa kama mtu mwenye wafuasi wengi kuliko wote duniani. Kilio chake ni AMANI! AMANI! kwa kivuli hicho anatafuta ufalme ili baadaye aje kupambana na uzao wa Mungu.
Biblia inasema..1Wathesalonike 5:1-3″ Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.Wakati wasemapo, KUNA AMANI NA SALAMA, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. “
Ndugu wakati umeisha usidanganyike na watu wanaosema dunia haishi leo wala kesho, geuka weka mambo yako sawasawa yahusuyo wokovu.Huu ulimwengu unapita na mambo yake yote.
Mstari wa 9-10. unasema…” Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na VITABU VIKAFUNULIWA.
Hapa tunaona mwisho wa yote vitabu vitafunguliwa vihusuvyo maisha yetu, kila mtu na kitabu chake na utahukumiwa katika hicho, je! kitabu chako unakiandikaje? Biblia inasema sisi ni barua, na kila siku tunafungua kurasa mpya wa vitabu vyetu, na siku ile utakapokufa kitafungwa kikingojea kufunguliwa tena katika siku ile ya HUKUMU.
Hivyo tukiona mambo haya tunajua kabisa ule mwisho umekaribia UTAWALA USIOWEZA KUHARIBIKA wa mwokozi wetu ,hivi karibuni utakuja hapa ulimwenguni,.BWANA wetu YESU KRISTO MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA, atamiliki pamoja na watakatifu wake milele tunasoma..
27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; UFALME WAKE NI UFALME WA MILELE, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
2Petro 1:10” Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”
AMEN!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara, kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.
Jina KUU la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe.
Ndugu mpenzi karibu tujifunze Neno la Mungu na leo tukiwa katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli, kama Biblia inavyosema, katika 2 Timotheo 3:16″ Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa MAFUNDISHO, na kwa kuwaonya watu makosa yao, NA KWA KUWAONGOZA, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”
Hivyo kila habari tunayoisoma katika biblia kwa namna moja au nyingine ina mafunzo tosha ya kutufanya sisi tuenende kiukamilifu katika safari yetu hapa duniani pasipo kukwazwa na majaribu ya aina yoyote ya shetani, na ndio maana maandiko yanasema ” Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. (1Wakoritho 10:11) “. Kwahiyo mambo yote waliyoyapitia watakatifu wa kale ni kwa ajili ya kutuonyesha sisi njia ya kupita tunapokumbwa na majaribu kama ya kwao.
Katika sura hii ya sita Danieli licha ya kwenda katika ukamilifu wake wote lakini bado tunaona akiingizwa katika majaribu mazito, kama tunavyoweza kusoma habari hii:
Danieli 6:1-18″
1 Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;
2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
5 Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, TUSIPOIPATA KATIKA MAMBO YA SHERIA YA MUNGU WAKE.
6 Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.
7 Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.
8 Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.
9 Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.
10 Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
11 Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.
12 Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika.
13 Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku.
14 Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.
15 Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme.
16 Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.
17 Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danieli.
18 Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.
Kama tukifuatilia habari hii tunaona Danieli alitumika kikamilifu katika kazi zote za uliwali pasipo dosari yoyote, alikuwa mwaminifu, hakuruhusu jambo lolote ovu limkoseshe katika kazi zake za uliwali siku zote za maisha yake, hakuwa anakula rushwa, wala kuwa na matumizi mabaya ya fedha za ufalme katika mamlaka aliyopewa, na ndio maana mfalme ilibidi atafute watu watatu waaminifu ambao wataweza kuzisimamia hizo hazina kubwa za fedha ili mfalme asipate hasara katika mahesabu yake na mmojawao alikuwa ni Danieli.
Lakini haikuwa hivyo kwa wale wakuu wenzake waliokuwa na Danieli, wao walikuwa wanatafuta faida zao wenyewe, mambo kama ufisadi, rushwa, na ubadhilifu wa fedha vilikuwa ni sehemu ya maisha yao, Hivyo mtu kama Danieli alikuwa ni kikwazo kikubwa kwao. Pengine walipojaribu kuhujumu fedha za nchi Danieli aliwakemea na kuwashitaki kuwa wanachokifanya sio sawa, Hivyo ikawapelekea kumchukia Danieli sana na kuanza kumuundia visa, kwasababu nuru na giza haviwezi kuchangamana.
Kumbuka huo ulikuwa ni mpango wa shetani ndani ya watu, alipoona kuwa Danieli ni mkamilifu na hawezi kuuacha ukamilifu wake, akaamua kubadilisha kinyago chake na kuja na mbinu mpya, isipokuwa hii ni katika IMANI YAKE. Na hapo ndipo vita vinapokuwa vikali, pale unapolazimika kuchukua maamuzi ya NDIO AU HAPANA juu ya IMANI yako.
Na ndio maana ukisoma pale kwenye ule mstari wa 5 “Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, TUSIPOIPATA KATIKA MAMBO YA SHERIA YA MUNGU WAKE”.(Danieli 6:5)
Kwahiyo wale wakuu tunaona waliunda SHERIA moja madhubuti ihusuyo IMANI katika DUNIA YOTE ili tu kumnasa mtu mmoja wapate kumuangamiza. Lakini Danieli alipoona kuwa ile amri imeshapitishwa hakuacha msimamo wake zaidi ya yote alifungua madirisha yake kuelekea YERUSALEMU na kuendelea kusali kutwa mara tatu kama ilivyokuwa desturi yake, alichukua uamuzi wa kukubali kufa kwa ajili ya imani yake, na walipomwona bado anashikilia uamuzi wake wakamtupa katika Tundu la Simba, lakini tunaona Bwana ni mwaminifu alikuja kumwokoa.
Vivyo hivyo mambo hayo waliyoyakuta akina Danieli na sisi pia yatatukuta kwa namna moja au nyingine, Kama hao walikuwa ni watoto wa Mungu waliopendwa wameyapitia hayo vivyo na sisi pia tutayapitia kama hayo. Kumbuka ikiwa wewe ni mkristo na unajiona umesimama katika imani yako, fahamu kuwa shetani anakuchunguza maisha yako kila siku, ni kweli unaweza ukawa hauli rushwa kazini kwako, au haufanyi uasherati, au haunywi pombe, au hauvai mavazi ya kikahaba au hauabudu sanamu au haukosi kwenda ibadani au kusali n.k. Hivyo vyote shetani anaviangalia na atakapokujaribu kwa ushawishi wa muda mrefu ili uache msimamo wako na kuona unazidi tu kuvishinda, atatafuta njia mbadala ambayo moja kwa moja itaathiri UHUSIANO wako wewe na Mungu, aidha ukiache uishi au uendelee nacho uangukie MATATIZO MAKUBWA.
Kwamfano umekuwa mwaminifu kwa bosi wako kazini kwa muda mrefu na anafahamu kuwa wewe ni mkristo, lakini hapa ghafla anakuletea ripoti ya kukulazimisha usaini mapatano ya rushwa, kumbuka yule ni bosi wako na ukimkatalia utafukuzwa kazi,mkumbuke Danieli,
Au wewe wewe desturi yako ni kujisitiri lakini ghafla sheria mpya inakuja ofisini ni lazima kuvaa suruali au vimini, na usipofanya hivyo ni kuhatarisha kazi yako, sasa hilo ni jaribu shetani anakuletea la kutumia nguvu ili umtendee Mungu wako dhambi kwamaana ameona kwa utaratibu huwezi, hivyo anakuja kwa nguvu.
Au pengine kiongozi/mwalimu wako anakulazimisha ufanye naye uasherati usipokubali anakufelisha mitihani, au anakuzushia mabaya yatakayokupelekea hata pengine kufungwa. Katika mazingira kama hayo mkumbuke Yusufu, Kimbia! ni heri upoteze kila kitu kuliko kuipoteza nafsi yako.
Au wewe ni mwombaji mzuri, unasoma Neno, unafunga lakini unashangaa ghafla mzazi anatoa sheria nyumbani hakuna kuomba muda mrefu tena, hakuna kufunga, au hakuna kusoma NENO, unalazimishwa kurudia ibada za sanamu ambazo hapo mwanzo ulishaziacha, na ukijaribu kukataa tu, unatengwa na wazazi au unafukuzwa nyumbani. Usiogope kufukuzwa wala kutengwa hayo ni mapito ya muda tu! Bwana anakuwazia yaliyo mema.
Fahamu tu yatakapokutokea hayo yote usione kama Mungu amekuacha, wewe mkumbuke Danieli, mkumbuke Yusufu, mkumbuke Shedraka, Meshaki na Abednego, mkumbuke na Ayubu, mkumbuke Mordekai, hawa wote baada ya kuonekana wamesimama katika imani yao, shetani aliwaletea SHERIA ZA MASHARTI YA NGUVU. aidha ukubali kuabudu sanamu au ufe, aidha ukubali kuzini au uende gerezani, aidha ukuendelee kumtumikia Mungu wako kwa dua na sala au uishie kwenye matundu ya simba na moto. Lakini kumbuka mwisho wao hawa wote ulikuwa ni wa faraja, badala ya kuangamia kabisa walinyanyuliwa mara dufu. Hivyo usiogope yatakapokupata.
Na mambo hayo hayatamkuta kila mtu isipokuwa ni wale tu watoto wa Mungu waliosimama imara katika Imani ya YESU KRISTO, haya hayana budi kuja na ndio maana Bwana Yesu mwenyewe alisema.
Yohana 16:1-4 ” Maneno hayo nimewaambia, MSIJE MKACHUKIZWA.
2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.
4 Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.
Unaona hapo, shetani hatoweza kuvumulia kumuona mtoto wa Mungu anadumu katika utakatifu wakati wote hivyo ni lazima ameletee majaribu yatakayohusu imani yake na wakati mwingine Mungu anaruhusu kama vile Ayubu kwasababu biblia inasema. Wafilipi1:29 “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; “
Na pia inasema kwenye 2 Timotheo 3:12 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.”
Kumbuka pia jambo kama hili hili litajitokeza tena wakati wa kipindi cha dhiki kuu pale mpinga-kristo atakaponyanyuka na kuunda SHERIA MOJA YA SHARTI inayohusu IMANI, na shabaha yake itakuwa sio kila mtu aliye duniani bali ni kwa wale waliobaki (wasiokwenda kwenye unyakuo) wakristo vuguvugu wanawali-wapumbavu ambao watajaribu kutoshirikiana naye hao ndio watakaopitia dhiki kuu kwa kuteswa kwa mateso ambayo hayajawahi kuwako tangu ulimwengu kuumbwa. Na sheria itakuwa ni moja tu aidha uisujudie sanamu yake na kupokea chapa yake, ili uendelee kuisha au ukatae kuisujudia na kuteswa na kuuawa kikatili.
Kumbuka lile neno : Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. (1Wakoritho 10:11) “. Mambo ya kale ni kivuli cha mambo yanayokuja.
Hivyo ndugu kuna wakati unakuja mbeleni ulio mgumu sana, wa ulimwengu mzima kujaribiwa na yule mwovu shetani( katika dhiki kuu), Na huu ndio wakati wa kuziweka taa zetu sawa kwa kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu ili Bwana atuepushe na hiyo saa itakapofika (kwa kutunyakua). Kwasababu muda umeisha na wakati wowote Bwana anakuja kulichukua kanisa lake. NI WATAKATIFU TU! NDIO WATAKAOEPUKA HIYO DHIKI KAMA BWANA ALIVYOSEMA..
Ufunuo 3:10-11″ Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, UTOKE KATIKA SAA YA KUHARIBIWA ILIYO TAYARI KUUJILIA ULIMWENGU WOTE, KUWAJARIBU WAKAAO JUU YA NCHI. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.”
Kama bado haujatubu ndugu, ni vema ukafanya hivyo leo angali muda upo.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa Mwendelezo >>> Mlango wa 7
Mada Nyinginezo:
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO.
MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.
INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA.
NGURUMO SABA
DANIELI 5: KUANGUKA KWA BABELI:
Tukisoma katika Historia na kwenye biblia tunapata picha jinsi mji wa Babeli ulivyokuwa mkubwa, wenye maboma yenye nguvu, na ngome Imara iliyokuwa imezungukwa na kuta ndefu zenye njia katikati pande zote, mpaka kufikia wenyeji wa mji ule kusema kuwa ni “mji udumuo milele”,
Lakini tunaona wakati mmoja Mfalme wa Taifa hilo (BELSHAZA) alipokuwa amestarehe na kujifurahisha kwa anasa katika fahari yake tunaona uharibifu ulimkuta kwa ghafla, habari hii tunaisoma katika kitabu cha Danieli mlango wa 5, pale ambapo kiganja cha mkono kilipotokea na kusimama ukutani na kundika maneno yale magumu ambayo hakuna mchawi, wala mwenye hekima aliyeweza kuyasoma na kuyatafsiri maneno yale isipokuwa Danieli peke yake kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU.
Danieli 5:1-8″ Belshaza, mfalme, aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa akanywa divai mbele ya elfu hao.
2 Belshaza, alipokuwa akionja ile divai, akaamuru wavilete vile VYOMBO VYA DHAHABU NA FEDHA, ambavyo baba yake, Nebukadreza, ALIVITOA KATIKA HEKALU LILILOKUWAKO YERUSALEMU; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea.
3 Basi wakavileta vile vyombo vya dhahabu, vilivyotolewa katika hekalu la nyumba ya Mungu lililokuwako Yerusalemu; na mfalme na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wakavinywea.
4 Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.
5 Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu, vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme, mahali palipokikabili kinara; naye mfalme akakiona kitanga cha ule mkono ulioandika.
6 Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana.
7 Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme.
8 Basi wakaingia wenye hekima wote wa mfalme; lakini hawakuweza kuyasoma yale maandiko, wala kumjulisha mfalme tafsiri yake.”
Kama tunavyosoma hapo Mfalme Belshaza aliona haitoshi kujifurahisha katika anasa pamoja na masuria wake tu, lakini aliongezea kwenda kuchukua vyombo vya nyumba ya Mungu ambavyo baba yake (Nebukadreza) aliona vema kuvitunza visitumiwe kwa namna yoyote kwasababu viliwekwa wakfu kwa Bwana mpaka wana wa Israeli watarejea katika nchi yao, ni vyombo vilivyotumiwa na makuhani tu katika nyumba ya Mungu kwa ajili ya ibada. Lakini ijapokuwa Belshaza ALIYAFAHAMU HAYO YOTE, na kwamba vitu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wa Israeli havipaswi kutumiwa kwa namna yoyote. Lakini kwa kiburi chake cha kufanya moyo wake kuwa mgumu kwa kutokujali na kumdharau Mungu, alikwenda kuvitumia kwa anasa zake, tukiendelea kusoma..
Danieli 5:9-31″
9 Ndipo mfalme Belshaza akahangaika sana, uso wake ukambadilika, na wakuu wake wakaona fadhaa.
10 Basi malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike.
11 Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako, naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu;
12 kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danielii huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danielii, naye ataionyesha tafsiri.
13 Ndipo Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Na Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Je! Wewe ndiwe Danieli yule, aliye mmoja wa wana wa Yuda waliohamishwa, ambao mfalme, baba yangu, aliwaleta huku toka Yerusalemu?
14 Nimesikia habari zako, kwamba roho ya miungu imo ndani yako, na kwamba nuru na ufahamu na akili bora zimeonekana kwako.
15 Basi sasa, watu wenye hekima na wachawi wameletwa mbele yangu, wapate kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake; lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri ya jambo hili.
16 Lakini nimesikia habari zako, kwamba waweza kuleta tafsiri, na kufumbua mafumbo; haya! Kama ukiweza kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake, utavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utakuwa mtu wa tatu katika ufalme.
17 Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.
18 Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu;
19 na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.
20 Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.
21 Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng’ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.
22 Na wewe, mwanawe, Ee Belshaza, hukujinyenyekeza moyo wako, ijapokuwa ulijua hayo yote.
23 Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.
24 Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa.
25 Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE MENE TEKELI, NA PERESI.
26 Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.
27 TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.
28 PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.
29 Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.
30 Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, AKAUAWA.
31 Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.
Amen.
Habari hiyo imejifafanua yenyewe, huo ndio ulikuwa mwisho wa Babeli, historia inasema usiku ule ule Danieli alipokuwa anawapa tafsiri ya maneno yale, kumbe jeshi la waamedi na waajemi lilikuwa limeshauzingira mji kwa mbali, hao hawakujua lolote kwasababu walishajitumainisha katika ulinzi wa kuta zao ndefu zinazouzunguka mji huku geti kubwa la kuingilia njia za miji ukiwa umefungwa,
Hivyo walijua hakuna namna yoyote taifa lolote lingeweza kuwavamia kwa njia yoyote ile, lakini hawakufahamu jambo moja, kwamba kwa Mungu hakuna lolote linaloshindikana, akisema mji huu utaanguka, ni kweli utaanguka! Hivyo Danieli alipomwambia maneno yale: “ufalme wako umeanguka na wamepewa waamedi na wajemi”, Mfalme alichukulia kama ni jambo ambalo ni gumu kutokea kwa wakati ule hivyo pengine ifikiria kichwani kwake kwamba kuta zake ndefu na majeshi yake imara yanayokesha usiku kucha kuulinda mji hayawezi kuvamiwa, na hakuna taifa lolote duniani lingeweza kupigana nalo , hivyo akastarehe tena na kutaka kumtukuza Danieli pasipo kujali maneno yale kwa kuanguka na kutubu saa ile ile.
Pia tazama..
Lakini hakujua maabaya yatakayomkuta muda mfupi baadaye, kulikuwa na mto mkubwa uliokuwa unaingiza maji katika mji ule, na tunafahamu siku zote hauwezi kuziba njia ya maji kupita, lazima kuachwe tundu kuruhusu maji kupita yaingie mjini, na ndivyo ilivyokuwa Babeli.
Palikuwa na mto mkubwa (FRATI) uliokatiza mji ule hivyo maadui zao walipokuja (Waamedi na waajemi) hawakupita kwa njia ya mageti au kubomoa kuta za miji, kwasababu kule zilikuwa zinalindwa na maaskari wengi waliomakini, Hivyo njia waliyoitumia waamedi na wajemi ni kwenda kukausha maji ya ule mto kwa kuyaundia mchipuko mwingine, hivyo yakaanza kupungua kidogo kidogo pasipo wao kujua, na mwisho kufikia kiwango cha watu kuweza kupita kwa miguu, jeshi kubwa la waamedi na wajemi liliweza kuingia kiurahisi kuuteka mji, na usiku ule ule Mfalme Belshaza aliuliwa bila kujua watu wameingilia wapi? na ufalme wake ukachukuliwa. Na Babeli kuishia hapo.
Wengi wanasema unabii wa Mungu huwa unachelewa kutimia, lakini si kweli ukichelewa ni kukufanya wewe utubu, kumbuka hapa tunaona mara tu baada ya Danieli kumtabiria Belshaza kuanguka kwake pengine alidhani ingekuwa kama ya Baba yake, kwamba yatatimia baada ya miezi au miaka kadhaa, lakini haikuwa hivyo kwake yeye ilitimia usiku ule ule.
Vivyo hivyo na BABELI ya rohoni (Utawala wa dini ya RUMI -UKATOLIKI ) iliyopo sasa, ambayo inapeleka mamilioni ya watu kuzimu, kama biblia inavyomwita katika
Ufunuo 17,“BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI”. NAYO PIA uharibifu wake utakuja ndani ya siku moja Biblia inasema
Ufunuo 18:6-8″ Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu.
7 Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.
8 KWASABABU HIYO MAPIGO YAKE YATAKUJA KATIKA SIKU MOJA, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu. ” AMEN.
Kumbuka pia jambo lingine lilolosababisha Mungu kuihukumu Babeli ni pale VYOMBO VYA NYUMBA YA MUNGU vilipochanganywa na SANAMU na kusababisha CHUKIZO kubwa lililoleta UHARIBIFU, Vivyo hivyo pia katika Babeli ya rohoni itakuja pale yule mtawala wake yaani mpinga-kristo (PAPA wa wakati huo) atakapojiinua na kuingia katika hekalu la Mungu kule YERUSALEMU na kutaka kuabudiwa kama Mungu, litakuwa ni chukizo kubwa kwa Mungu ambalo litapelekea uharibifu wake moja kwa moja hilo ndilo CHUKIZO LA UHARIBIFU.
Habari zake zinazungumziwa hapa na mtume Paulo;
2 Wathesalonike 2:1-4″ Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,
2 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.
3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa YULE MTU WA KUASI, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.”
Vivyo hivyo kuutumia MWILI wako kwa uasherati, au fashion (vimini, suruali, hereni, wigy,) au ulevi, au wizi, au anasa, au rushwa,ulanguzi, NI SAWA NA KUVICHUKUA VYOMBO VYA NYUMBA YA MUNGU NA KWENDA KUVITUMIA KWA ANASA, haya yote ni machukizo yatakayokuletea uharibifu wa ghafla, Kwasababu Bwana alisema katika 1Wakoritho 6 kuwa “mwili ni kwa BWANA na BWANA ni kwa mwili na atakayeliharibu hekalu la hilo, Mungu atamuharibu mtu huyo.”
Au unapotumia Karama za Mungu kwa ajili ya faida zako mwenyewe, kwamfano unajiita mchungaji/nabii/mwinjilisti na bado ni unazini na washirika wako, au unatumia karama/vipawa hivyo kuwachukulia watu fedha,au kuwalaghai, huko ni SAWA NA KUVICHUKUA NA KUVITUMIA VYOMBO VYA NYUMBA YA MUNGU KWA ANASA, kama alivyofanya Belshaza hayo yote ni machukizo makubwa ambayo yatakupelekea kuanguka kwako haraka sana.
Hivyo ujumbe tulionao kwa kizaazi hiki cha mwisho ni huu:
2 Wakorintho 6:14 -18″ Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
16 TENA PANA MAPATANO GANI KATI YA HEKALU LA MUNGU NA SANAMU? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
17 Kwa hiyo, TOKENI KATI YAO, MKATENGWE NAO, ASEMA BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,
Ukisoma tena Ufunuo 18:4 inasema;
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “
Hivyo Jitenge na DINI za uongo, na pia jitenge na mienendo ya watu watendao dhambi.
Ubarikiwe na Bwana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Kwa mwendelezo >>> Mlango wa 6
Mada Nyinginezo:
KITABU CHA YASHARI KINACHOZUNGUMZIWA KATIKA 2SAMWELI 1:17-18, NI KITABU GANI?
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
Danieli 4:
JINA LA BWANA wetu YESU KRISTO, Mkuu wa milki zote za dunia lihimidiwe.
Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli;
Sura hii inaelezea Maono Mfalme Nebukadreza aliyoyaona na kumpelekea kubadili fikra zake na kuwa mtu mkamilifu mbele za Mungu, aliandika barua hii..
Danieli 4:1 Mfalme Nebukadreza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu.
2 Mimi nimeona vema kutangaza habari za ISHARA NA MAAJABU, aliyonitendea Mungu aliye juu.
3 Ishara zake ni kubwa kama nini! Na maajabu yake yana uweza kama nini! Ufalme wake ni ufalme wa milele; na mamlaka yake ni ya kizazi hata kizazi.
Hapa tunaona Nebukadreza anaanza kwa kushuhudia ISHARA na MAAJABU Mungu aliyomtendea alipokuwa amestarehe katika ufalme wake, tunajua siku zote jambo fulani Baya Mungu akitaka kulileta kwa mtu/watu kabla ya kulileta jambo hilo huwa anatanguliza ishara kwanza kama onyo, na kazi ya ishara ni kumfanya mtu atubu, kwamfano tunaona wakati wa kipindi cha Yona,
Kabla ya Mungu kuiangamiza Ninawi ndani ya siku 40, Mungu alitangulia kuwapa ishara kwanza ya Yona kukaa ndani ya tumbo la samaki siku tatu, ili watakapoiona ishara kama hiyo watubu,na wasipotubu wataangamizwa, lakini tunaona walitii na kutubu na Mungu akaghahiri kuleta ubaya ule.
Vivyo hivyo na kwa Nebukadreza katika utawala wake Mungu alishatangulia kumpa ISHARA nyingi ili aache uovu wake lakini hakutubu, Kwamfano ile ndoto aliyoota ya kwanza “ya sanamu KUBWA” ilikuwa ni ishara kuwa ufalme wake siku moja utaangushwa, hivyo amgeukie Mungu lakini hakufanya hivyo, na Mwishoni pia Mungu alimpa ISHARA nyingine ya ndoto juu ya ule mti mrefu sana, uliokatwa na kuachwa kisiki tu, ambao ulimuhusu yeye moja kwa moja ili atubu aache maovu yake lakini hakutubu..Na ndio maana hapa tunaona anashuhudia na kusema ISHARA ZAKE NI KUBWA KAMA NINI!!.
Pia tazama..
Licha ya Ishara alionyeshwa pia na maajabu, ambayo ni miujiza mfano wa ya akina Shedraka, Meshaki na Abednego ya kukaa katika moto mkali pasipo kuteketea, mambo ambayo hakuwahi kuyaona hata kwa wachawi wake aliokuwa nao Babeli na ndio maana alisema anaona vizuri kuandika maajabu Mungu aliyomtendea, yenye UWEZA MKUBWA.
Vivyo hivyo hata kwa mtu yeyote kabla ya Mungu kufanya jambo huwa anatanguliza kwanza ISHARA NA MAAJABU kama ONYO kumfanya mtu huyo atubu, lakini asipotubu mambo mabaya yatamkuta kama yalivyomkuta Mfalme Nebukadreza. Na kizazi tunachoishi sasa hivi kilishapewa ISHARA kama ya NINAWI ili kitubu na ishara hiyo si nyingine zaidi ya YESU KRISTO mwenyewe Ukisoma..
Mathayo 12:38-42″ Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.
39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ISHARA YA NABII YONA.
40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.
41 Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao WALITUBU kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.
42 Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani. “
Na MAAJABU pia Mungu anatutenda, tunayaona kila siku katika maisha yetu, wafu wanafufuliwa, viwete wanatembea, vipofu wanaona, watu wanaponywa magonjwa yao, wenye UKIMWI, Cancer, magonjwa yasiyotibika yote yanapona, n.k. Hivi vyote Mungu anavifanya ili watu watubu na kumgeukia yeye, lakini wengi wanakimbilia kwa Mungu ili watendewe miujiza tu na sio kwa ajili ya TOBA, Lakini Bwana alisema…
Mathayo 11:20 -24 “Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu HAIKUTUBU.
21 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.
22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.
23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama MIUJIZA iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe. “
Kwahiyo dhumuni KUBWA la Mungu Kuruhusu ishara na maajabu sio kututimizia mahitaji yetu pekee, bali ni KUTUONYA na kutufanya TUTUBU, ili tusije tukaangukia hukumu, jiulize, Mungu amekufanyia Ishara na Maajabu mara ngapi katika maisha yako? na Je! yalikufanya wewe utubu na kuacha dhambi au umkaribie Mungu zaidi? Kama sivyo jitathimini tena.
Tukirejea kwenye ule mstari wa nne tunaona Nebukadreza aliendelea na kusema:
Danieli 4:4-17″
4 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi.
5 Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.
6 Basi nikatoa amri kwamba wenye hekima wote wa Babeli, waletwe mbele yangu, ili kunijulisha tafsiri ya ndoto ile.
7 Ndipo wakaingia waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu; nikawahadithia ile ndoto; wao wasiweze kunijulisha tafsiri yake.
8 Bali hatimaye Danieli akaingia mbele yangu, ambaye jina lake ni Belteshaza, kwa kufuata jina la mungu wangu; tena ndani yake inakaa roho ya miungu watakatifu; nikamhadithia ile ndoto, nikisema,
9 Ee Belteshaza, mkuu wa waganga, kwa sababu ninajua ya kuwa roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako, na ya kuwa hapana neno la siri likushindalo, niambie njozi za ndoto yangu niliyoiona, na tafsiri yake.
10 Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; naliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana.
11 Mti ule ukakua, ukawa na nguvu, urefu wake ulifika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka mwisho wa dunia.
12 Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake.
13 Nikaona katika njozi za kichwa changu kitandani mwangu, na tazama, “MLINZI”, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka mbinguni.
14 Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.
15 Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi;
16 moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake.
17 Hukumu hii imekuja kwa AGIZO LA WALINZI, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge. “
Baada ya Mfalme Nebukadreza kumsimulia Danieli ndoto hii, ndipo tunasoma Danieli mkuu wa waganga alimpa tafsiri yake na kumwambia ule mti mkubwa wenye nguvu ambao wanyama wote wa kondeni walipata uvuli chini yake, unamwakilisha yeye, na kwamba ulionekana umekatwa kwa agizo la WALINZI, ikiwa na maana kuwa ataondolewa katika enzi yake ya kifalme, naye atakaa mwituni na kula majani kama ng’ombe mpaka nyakati saba zitakapotimia ( yaani miaka 7), hadi hapo atakapofahamu kuwa aliye juu ndiye anayetawala falme zote za dunia.
Lakini tunaona pamoja na kupewa ISHARA hii na Danieli kumshauri ATUBU aache njia zake mbaya kwa kuwahurumia MASKINI, Hakutubu aliendelea kuwa na kiburi, kuwanyanyasa maskini na kutokuwa na huruma kwa watu, mpaka kiwango cha maovu yake kilipofikia kilele, tunasoma baada ya miezi 12 jambo hilo lilimtokea kama lilivyo.
Danieli 4:28-30″
28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza.
29 Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli.
30 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?
31 Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.
32 Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.
33 Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.
AGIZO LA WALINZI:
Kama tunavyosoma habari hii kuwa kulikuwa na WALINZI mbinguni waliokuwa wanatazama mienendo yote Ufalme wa Nebukadreza, mema yake yote na mabaya yake yote aliyoyafanya, Kumbuka Hawa ni MALAIKA WATAKATIFU walioko mbinguni, wanaotazama kila cheo, nafasi au mamlaka mtu aliyonayo, je! anavitumiaje?. Kama mtu anatenda mema Mungu kwa mkono wa hao walinzi anakulipa, lakini kama unatenda maovu au unaitumia vibaya nafasi yako uliyopewa, Mungu kwa mkono wa hao walinzi utapokea HUKUMU. Na mambo hayo ni hapa hapa duniani kabla ya hukumu kuu ya siku ya mwisho.
Kama wewe ni Raisi fahamu tu kuna WALINZI mbinguni wanakutazama kama vile wale waliokuwa wanamtazama Mfalme Nebukadreza, kama wewe ni waziri,mbunge, mkuu wa mkoa, balozi, diwani, m/kijiji, mjumbe, n.k. fahamu tu wapo walinzi juu wanakutazama mienendo yako kama je unaenenda katika haki au la!..Kama wewe ni mchungaji, mwinjilisti, Nabii, mwalimu, shemasi, mwimba kwaya, mfanya usafi kanisani, mwandishi, n.k. fahamu tu wapo walinzi mbinguni wanakutazama kama je! unasimama katika njia ya haki au la!, Kama wewe ni baba, au mama, au mlezi au boss, jua tu kuna walinzi watakatifu mbinguni wakifuatilia nyendo zako kama kweli hao unaowalea unawatendea haki au la!….n.k.
Kwahiyo katika nafasi yoyote uliyopewa na Mungu ni muhimu kuendana nayo kwa umakini ukijua kuwa, hakuna mamlaka iliyojiweka yenyewe (Warumi 1:1 “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana HAKUNA MAMLAKA ISIYOTOKA KWA MUNGU; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.). Mfalme Nebukadreza alipuuzia hilo na kusahau kuwa anatazamwa juu na kwamba Bwana ndiye anayetoa mamlaka yote, matokeo yake thamani yake ikashushwa kuliko hata mnyama wa porini kwa muda wa miaka 7, lakini alipogundua kosa lake, alitubu na kuwa mnyenyekevu hivyo Mungu akamrehemu na kumrejeshea vyote na enzi kupita kiasi. Sasa huyu alifanyika kama mfano,neema hiyo inaweza isiwepo kwako, kama utatumia vibaya nafasi uliyopewa.
Ndipo Mfalme Nebukadreza alimalizia na kusema:
Danieli 4:34 Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;
35 na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?
36 Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi.
37 Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.
Kwahiyo ndugu kumbuka ishara na maajabu(ndoto, Maono, mafanikio, uponyaji, kuepushwa na mabaya, kutendewa miujiza Mungu anayokuonyesha ni kukutaka ufikie toba, utubie uasherati wako, ulevi wako, sanamu zako, vimini vyako, makeup zako na usengenyaji wako n.k. Pia usisahau katika nafasi uliyopewa wapo walinzi juu wanakutazama.
Ubarikiwe na Bwana Yesu.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Kwa Mwendelezo >>> MLANGO WA TANO:
Mada Nyinginezo:
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.
Jina la Bwana wetu na Mkuu wetu Yesu Kristo libarikiwe.
Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli. Leo tukiutazama ule mlango wa tatu, Tunasoma baada ya Mfalme Nebukadreza kuota ile ndoto ya kwanza, inayohusu zile falme 4 zitakazotawala mpaka mwisho wa dunia,lakini hapa kwenye sura hii tunaona akitimiza maono yake kwa kunyanyua SANAMU kubwa ya dhahabu, na kulazimisha watu wa dunia yote waiabudu, Na mtu yeyote atayeonekana amekaidi adhabu yake ni kwenda kutupwa katika tanuru la Moto. Kama tunavyosoma.
Danieli 3:1-6″ Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.
2 Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.
3 Ndipo maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
4 Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi,
5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
6 Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.
Lakini pamoja na hayo walionekana watu baadhi waliokaidi amri ya mfalme nao ni Shedraka Meshaki na Abednego. watu hawa tunasoma walikuwa ni wacha Mungu tangu awali, tunaona walikataa kula vyakula najisi vya mfalme, na hapa pia wanakataa kuabudu sanamu ambayo ni kinyume na sheria ya Mungu aliyowapa, kwa mkono wa Musa kule jangwani ikisema..
Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Hivyo Mfalme aliposikia habari yao alighadhibika na kuwatupa katika tanuru la Moto, lakini tunaona Bwana aliwaokoa na ukali wa moto ule.
Kumbuka Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya, (wakolosai 2:17) yaliyotokea katika mwili agano la kale, yatakuja kutokea katika roho kwenye agano jipya, na ndio maana tunaona hapa inatajwa BABELI ya NJE, lakini tukisoma katika kitabu cha Ufunuo 17 &18 Tunaona inatajwa BABELI nyingine itakayokuja kunyanyuka nayo ni ya rohoni. Hivyo tabia inayojitokeza kwenye hiyo ya mwilini itafanana na hiyo ya rohoni.
Na kama Babeli ile ya kwanza ilivyounda sanamu na kulazimisha watu wa dunia nzima waiabudu na yeyote asiyeabudu atatupwa katika tanuru kali la moto vivyo hivyo na hii ya rohoni itaunda SANAMU yake na mtu yeyote atakayekaidi kuiabudu, adhabu yake itakuwa ni mateso ambayo biblia inasema hayajawahi kuwepo tangu dunia kuumbwa (DHIKI KUU)..Habari hii tunaweza kuisoma katika…
Ufunuo 13:15 Akapewa kutia pumzi katika ile SANAMU YA MNYAMA, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao WOTE WASIOISUJUDIA SANAMU YA MNYAMA WAUAWE.
16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao:
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Kumbuka Mnyama huyu ni RUMI na dini yake ni KATOLIKI, ndio BABELI ya rohoni iliyopo sasa. Itafika kipindi itapata nguvu kwa kuunganisha DINI zote na Madhehebu yote ulimwenguni ili kuunda DINI moja (ambayo ndio SANAMU YA MNYAMA), ambayo pasipo hiyo hakuna mtu yeyote atakayeweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa, na yeyote atakayeonekana hana chapa(utambulisho) wake, adhabu yake itakuwa ni mateso makali na vifo. Kama vile amri ya Mfalme ilivyokuwa kali juu ya akina Shedraka mpaka moto ukachochewa mara saba, ndivyo mateso yao yatakavyokuwa makali kwa wale wote watakaokataa kusujudia ile SANAMU ya Mnyama au kupokea CHAPA YAKE.
Pia tazama..
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa Historia utaona mateso waliopitia wayahudi wakati wa utawala wa kimabavu wa Adolf Hitler, jinsi wayahudi walivyouawa kikatili kwenye magereza maalumu (CONCENTRATION CAMPS), walivuliwa nguo uchi wa mnyama na kuingizwa katika matanuru ya Gesi, wengine walikuwa wanapasuliwa wazima kama kuku kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara mifupa na msuli inachomolewa pasipo ganzi na kuwekwa kwa mwingine,
wengine walitiliwa sumu machoni, wengine wanadondoshwa kwenye ndege maili nyingi kutoka hewani( zote hizi ni kwaajili ya utafiti wa kijeshi na kibaolojia), wengine wanafungiwa kwenye mashehena yenye kemikali kwa muda mrefu ili tu wafe taratibu kwa maumivu makali, wengine walikuwa wanaachwa kwenye barafu uchi, wengine wanafanyishwa kazi ngumu kwa muda mrefu bila chakula mpaka wafe, wengine wanaachwa na kiu kwa muda mrefu na kupewa maji ya chumvi tu kuchunguza kama mtu anaweza kuishi kwa maji ya chumvi kwa muda gani?, watoto wanafungwa na kugongwa nyundo kichwani kidogo kidogo kwa muda mrefu mpaka kufa, au ukichaa ili tu kuchunguzwa ni kwa muda gani mwanadamu anaweza akavumilia maumivu n.k. embu fikiria ni mateso ya aina gani hayo?, tazama picha hapo chini..
Kumbuka Adolf Hitler aliwafanyia hivyo kwasababu tu ni wayahudi, kwasababu wao ni taifa teule la Mungu, na si vingine, sasa hayo yote ni kivuli cha yatakayokuja huko mbeleni, huo ni mfano mdogo sana, Biblia inasema kutakuwepo na dhiki ambayo haijawahi kutokea na wala haitakuja kutokea tena baada ya hapo, Hivyo hawa wa mwisho watakuja kuuliwa kwasababu wanashikilia ushuhuda wa Kristo kwa kukataa kuisujudia SANAMU ya yule mnyama na kupokea chapa yake.
Ni mambo ya kutisha yanakuja huko mbele usitamani uwepo, anza kuweka sawa mambo yako yahusuyo wokovu leo kabla wakati haujaisha.
Lakini jambo lingine tunaweza kulisoma katika hii habari, Ni kwamba DANIELI haonekani kuwepo wakati sanamu ile inasimamishwa na watu walipolazimishwa kuiabudu. je! hii inafunua nini??.
Kama vile tulivyoona agano la Kale ni kivuli cha Agano jipya. Danieli ni mfano wa BIBI-ARUSI wa Kristo aliyekwisha jiweka tayari na kwenda kwenye UNYAKUO. Na ndio maana hatumwoni Danieli miongoni mwa wakina Shedraka, Meshaki na Abednego,.
Hivyo kabla ya hii DHIKI KUU kuanza kuna kundi dogo sana(BIBI-ARUSI wa KRISTO) watakuwa wameshanyakuliwa kwenye utukufu , watu hawa ni wale waliokuwa wamejiweka tayari, kwa UTAKATIFU, na Kudumu katia NENO na UFUNUO wa Roho Mtakatifu, ni watu walioshi kama vile wapitaji duniani wanaomngojea Bwana wao, Hawaabudu sanamu, sio walevi, sio wavutaji sigara, sio waenda disco na wasikilizaji wa miziki ya dunia hii, wasengenyaji, sio wezi wala walarushwa, sio wazinzi, sio watukanaji, n.k.
Kumbuka ndugu huyu mnyama anafanya kazi ndani ya DINI YA KATOLIKI, na atakayeisimamisha SANAMU yake atakuwa ni mpinga-kristo(katika kiti cha UPAPA)..na sanamu yake itakuwa ni “Muungano wa dini zote na madhehebu yote duniani (Ekumene)” .Na sanamu hii ilishaanza kuundwa tangu miaka ya 1900. kilichobaki ni “KUSIMAMISHWA TU” ili watu waiabudu.Na hivi karibuni itasimamishwa, lakini kinachohuzunisha zaidi ni watu wameshaanza kuiabudu hata kama haijasimamishwa, na ndio maana Bwana anasema tokeni kwake enyi watu wangu..(Ufunuo 18:4) kwa ufahamu jinsi gani chapa ya mnyama itatenda kazi fungua hapa >> Chapa ya Mnyama
Unaweza ukaona ni jinsi gani siku zilivyokwisha, matunda ya nchi yamekwisha iva, Tunapoona vikundi vya kigaidi vinakirithiri, vikundi kama ISIS, Boko Haramu, Alshabaab, n.k. migogoro ya kidini kati ya taifa na taifa, Israeli na wapalestina, wabudha & waislamu, wakristo & waislamu n.k. yote haya yanazidi kumfungulia njia mpinga-kristo kuleta muafaka wa AMANI-FEKI, Juu ya masuala ya dini ambao wanasiasa wa dunia nzima wameshindwa kuyatatua. Kwa jinsi yanavyoendelea kuongezeka mpinga-kristo (PAPA wa wakati huo) atapewa nguvu na mataifa ya dunia yote, ndipo atakapoleta utaratibu mpya (NEW WORLD ORDER) ambao katika huo watu wote watalazimika kuufuata na mtu yeyote atakayekaidi, ni mateso yasiyoelezeka yatamkumba.
Hivyo NENO la Mungu linasema
1Wakorintho 7:29 Lakini, ndugu, nasema hivi, MUDA UBAKIO SIO MWINGI; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;
30 na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu.
31 Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.
Tujiweka tayari kwasababu siku ya Bwana itakuja kama mwivi..
1Wathesalonike 5:1 Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 Wakati wasemapo, KUNA AMANI NA SALAMA, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi”.
Uzidi kubarikiwa na BWANA YESU.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Kwa Mwendelezo >>> Mlango wa 4
Mada Nyinginezo:
ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU.
WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.
UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.
Kulikuwa na sababu kwanini Mungu aliinyanyua Babeli kuwa taifa lenye nguvu kuliko yote duniani na kutawala falme zote za dunia kwa wakati ule, hata kudhubutu kulichukua taifa teule la Mungu Israeli kulipeleka utumwani, pamoja na kuteketeza mji na Hekalu la Mungu..Aliruhusu kwasababu alitaka kuonyesha kuwa ijapokuwa ni mji uliokuwa umetukuka sana, lakini siku moja kwa wakati ulioamriwa mji huo utaanguka na kuwa makao ya mbuni, na hayawani wote wa mwituni usioweza kukalika na watu . Hivyo ndivyo itakavyokuwa pia kwa BABELI YA ROHONI iliyopo leo ijapokuwa imetukuka sana, biblia inasema kwenye ufunuo 18 itaanguka na kuwa ukiwa na watu wote watauomboleza kwa kuanguka kwake.
Tunasoma miaka kadhaa kabla ya kuanguka kwake Mungu alishaanza kutoa maonyo kwa watawala wa Taifa hilo, na ndio maana tunaona ndoto zote na maono waliyoyaona yaliwafadhaisha sana, kwasababu walikuwa wanafahamu kwa namna moja au nyingine zinawahusu wao na utawala wao. Na kibaya zaidi ni kuona jinsi yale maono yalivyokuwa yanaishia.
Kama tunavyosoma katika sura hii ya pili Mfalme Nebukadneza aliota ndoto, ambayo ilimhuzunisha sana mpaka kufikia kwenda kuwaita waganga, na wachawi pamoja na watu wote wenye hekima waliokuwa Babeli wampe tafsiri ya ndoto ile, lakini hakuonekana hata mmoja ambaye angeweza kutoa tafsiri, waganga wote na wachawi walikiri kuwa hakuna awezaye kuingia katika vyumba vya ndani vya moyo wa mwanadamu isipokuwa Mungu peke yake. Na ni kweli ndivyo ilivyo shetani hana uwezo wa kuingia ndani ya mtu na kuyafahamu mawazo yake, ndio anaweza kutuma mawazo mabaya lakini hawezi kutambua fikra za mtu zikoje, mwenye uwezo huo ni Mungu tu,
Waebrania 4:12-13″ Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. “
Kwahiyo Mfalme alipoona hakuna mtu wa kumtafsiria ndoto yake, akakusudia kuwaangamiza waganga na wenye hekima wote wa Babeli lakini Mungu akamjalia Danieli na wenzake neema ya kufahamu tafsiri ya ile ndoto, na kuipeleka kwa mfalme. Tunasoma..
Danieli 2:26″ Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake.
27 Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu;
28 lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi;
29 Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa.
30 Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako.
31 Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha.
32 Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba;
33 miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.
34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.
35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.
36 Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme.
37 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;
38 na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.
39 Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.
40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta.
41 Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.
42 Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika.
43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.
44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
45 Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.
46 Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danielii, akatoa amri wamtolee Danielii sadaka na uvumba.
47 Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii.
48 Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.
49 Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danielii alikuwa akiketi katika lango la mfalme.
Katika ndoto hii tunaona Danieli akifunuliwa na Mungu Falme 4 zitakazokuja kutawala mpaka mwisho wa dunia, Kumbuka hakutakuwa na falme nyingine zaidi ya hizo, na ule wa tano ambao ndio uleule wa nne isipokuwa umechanganyikana na udongo ndio utakuwa wa mwisho kabla ya lile jiwe lilolochongwa mlimani pasipo kazi ya mikono kuupiga na kuuharibu kabisa.
Kama Danieli alivyomtafsiria mfalme kwamba kile kichwa cha dhahabu kinamwakilisha yeye(yaani ufalme wake wa Babeli),ambao kulingana na Historia ulidumu kuanzia mwaka 605BC hadi mwaka 539BC, Hichi ni kipindi cha miaka 66 , na baada ya hapo ukaanguka kama kitabu cha Danieli sura ya tano kinavyoelezea pale Mfalme Belshaza alipokuwa anafanyia anasa vyombo vya hekalu la Mungu kukatokea kiganja na kutoa hukumu juu ya kuanguka kwa ufalme wake, tunasoma katika usiku huo huo ufalme wake ulianguka.
Kisha ukanyanyuka utawala mwingine baada yake, tukisoma katika biblia ulikuwa ni utawala wa (Umedi na Uajemi) ambao ndio unawakilishwa na kile kifua na mikono ya fedha, Huu ulianza kutawala pindi tu Babeli ilipoanguka kuanzia mwaka 539BC hadi 331 BC. Nao ulienda kwa kipindi cha miaka 208, Pia kumbuka mwanzoni mwa utawala huu ndio Taifa la Israeli lilipokea Uhuru wake ili kutimiza unabii wa miaka 70 ya kukaa kwake utumwani kama Yeremia alivyotabiri, na kurejea tena katika nchi yake, ili kuijenga nyumba ya Bwana iliyokuwa imeharibiwa na Nebukadreza mfalme wa Babeli.
Agizo hilo la kurejea na kuijenga tena nyumba ya Mungu, liliasisiwa na mfalme Koreshi wa Uajemi. Tunasoma..
Ezra 1:1 Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,
2 Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi;
3 Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu.
4 Na mtu awaye yote aliyesalia mahali po pote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. “
Lakini baadaye mwishoni historia inaonyesha ulikuja ukaanguka.
kisha baada ya huo ulikuja Utawala mwingine wa tatu chini ya Mfalme “Alexander the great” aliyekuwa mfalme mwenye nguvu, tunasoma katika historia na katika biblia ulikuwa ni utawala wa Uyunani ambao unawakilishwa na kile kiuno na shaba, Huu ulianza kutawala kuanzia mwaka 331 BC hadi 168 BC, Ni kipindi cha miaka 163,
Na baada ya huu ufalme wa Uyunani kuanguka ulinyanyuka utawala mwingine uliokuwa na nguvu kama za chuma, uliowakilishwa na ile miguu ya chuma, na huu haukuwa mwingine zaidi ya utawala wa RUMI ya kipagani.Utawala huu ulidumu tangu kipindi cha 168 BC hadi kipindi cha 476 AD, ni zaidi ya miaka 644 na huu ndio utawala uliomsulibisha Bwana Yesu, uliwaua watu wengi kikatili kwa kuwasulibisha misalabani, wengine kwa kuchomwa moto n.k. na ndio maana biblia inasema ulikuwa ni mgumu kama CHUMA.
Tukiendelea tunasoma utawala mwingine wa tano na wa mwisho ulifuatia ambao ni chuma kilichochanganyikana na udongo, huu ni utawala ule ule wa nne isipokuwa hapa unaonekana kama umechanganyikana na udongo, Hivyo ni ule ule wa Rumi lakini umechanganyikana ndio unaowakilishwa na zile nyayo na vidole vya miguu ..
JE! huu udongo uliochanganyikana na chuma ni nini?.
Mstari wa 43 unasema..
43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.
Kumbuka hapo kabla, Taifa la Rumi lilikuwa haliingiliani na Taifa la Mungu kiimani kwa kipindi chote lilipokuwa linatawala dunia kama chuma, wakati huo lilikuwa lipo kisiasa na kiuchumi zaidi, lakini lilikuja kubadilika baadaye na kubadili tasira yake kwa kupitia DINI ili kujiingiza katikati ya taifa la Mungu (wakristo na wayahudi)
1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, TAIFA TAKATIFU, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, BALI SASA NI TAIFA LA MUNGU; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.
Kumbuka hii ilikuwa ni agenda ya shetani alipoona mambo yamehamia Rohoni na yeye akahamia rohoni.
Kwahiyo ule UDONGO unawakilisha WATU WA MUNGU au TAIFA LA MUNGU, na ndio zile mbegu za wanadamu.
Hivyo taswira hii ya kujigeuza ilianza kujidhihirisha wakati wa utawala wa Costantine, pale upagani wa kirumi ulipoingizwa rasmi katika Ukristo, hapo ndipo mafundisho ya kweli ya NENO la Mungu yalipoanza kuchanganywa na mafundisho ya kipagani ya kirumi ili tu kuwafanya watu wabebe taswira ya ufalme wa Rumi na wakati huo huo bado wabebe taswira ya Ufalme wa Mungu (Ukristo), Na ndio maana leo mtu akiulizwa wewe ni nani? atakuambia mimi ni MROMA, badala ya kuwa na utambulisho wa taifa lake la mbinguni (yaani kuitwa mkristo), atakuambia ndio mimi ni mkristo na pia ni Mroma, unaona hapo tayari ameshachanganyikana na ule ufalme wa chuma (ambao ndio Babeli ya rohoni ya sasa), na ndio wenye watu wengi duniani leo.
Kumbuka huu utawala ndio wa mwisho na hakutakuwa na mwingine baada ya huo (BABELI YA ROHONI) inayozungumziwa katika Ufunuo 17 & 18, Hivyo hii Rumi iliyochanganyikana na udongo ni UKATOLIKI. DINI hii imechukua desturi za Roma za kipagani ikazileta katikati ya watu wa Mungu, kwamfano ibada za sanamu ambazo Mungu alizikemea akilionya taifa lake lisifanye mambo kama hayo ni machukizo (Kutoka 20) lakini hili limeyaleta katikakati ya watu wa Mungu, ibada kama kusali rozari na kuomba kwa wafu, mafundisho ya kwenda toharani, kukataa uongozi wa Roho Mtakatifu kwa kuua karama za Roho na kuweka vyeo vya uongozi wa kibinadamu badala yake, n.k. Haya yote yalipenyezwa katika NENO la Mungu na kuleta mchanganyiko mkubwa sana katika Kanisa la Kristo.
Lakini mwisho wa lile ONO lilionekana JIWE likiwa limechongwa Mlimani na kushuka, tukisoma..
34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.
35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.
Na jiwe hili si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, yeye ndiye atakayebatilisha hizi falme zote mbovu kwa kuupiga ule ufalme wa mwisho kuleta utawala mpya Duniani ambao huo utadumu milele. Kwasababu yeye ni BWANA WA MABWANA, na MFALME WA WAFALME. Haleluya!!..Na jiwe lile lilionekana likiwa milima mikubwa ikishiria kuwa Kristo atatawala duniani kote pamoja na wafalme wengi(wateule wake) milele na milele.
Mstari wa 44 unasema..
” Danieli 2:44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.”
Hivyo ndugu kama tunavyosoma hakitasalia chochote katika ile sanamu?, na wewe je! upo kwenye ile sanamu kumbuka utawala wa shetani uliopo leo ndio ule wa tano uliochanganyika yaani chuma na udongo(shetani ni mdanganyifu, haji kwako moja kwa moja,)..Udongo ni wewe unayejiita mkristo, na chuma ni ROMA, chini ya mwamvuli wa dini ya katoliki, je na wewe umejichanganya humo? kumbuka lile jiwe lilisaga saga chuma na udongo vyote kwa pamoja, hivyo kama na wewe umejichanganya naye utasagwasagwa kama yeye hakitasalia kitu.
Kumbuka yule mnyama anayezungumziwa kwenye Ufunuo 13 & 17 ni dola ya Rumi inayounda ile chapa ya mnyama, na yule mwanamke aliyeketi juu ya yule mnyama ni Kanisa Katoliki, na anafahamika kama mama wa makahaba, ikiwa na maana kuwa anao mabinti wenye tabia kama za kwake za kikahaba, na hawa mabinti si wengine zaidi ya madhehebu mengine yote yaliyoacha uongozi wa Roho wa mtakatifu na kufuata desturi zisizoendana na NENO LA MUNGU.
Na ndio maana NENO LA MUNGU linasema Ufunuo 18:4″ Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “
Kanisa tulilopo ni la mwisho linaloitwa LAODIKIA, na Bwana alilikemea kuwa ni kanisa vuguvugu (lililochanganyikana), na Bwana amesema atalitapika kama lisipotubu,
Ufunuo 3:14-20″14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. “
Huu ni wakati wa kuwa bibi-arusi safi wa Bwana asiye na mawaa, kwa kujitenga na mafundisho ya uongo pamoja na kuishi maisha matakatifu( waebrania 12:14″ Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;” ) ili BWANA atakapokuja tuwe tayari kwenda naye katika unyakuo.
Jina la Bwana wetu YESU KRISTO na MKUU wa Dunia yote libarikiwe,
Karibu katika kujifunza kitabu cha Danieli, leo tukianza na ile Sura ya kwanza, Kwa ufupi tunasoma mlango huu wa kwanza kama wengi tunavyofahamu unaeleza jinsi wana wa Israeli walivyochukuliwa utumwani mpaka Babeli kutokana na wingi wa maovu yao, na Mungu kwa kupitia kinywa cha Nabii wake Yeremia alishawatabiria kuwa wangekaa huko kwa muda wa miaka 70 mpaka watakaporudi tena katika nchi yao wenyewe. Lakini mara tu baada ya kwenda utumwani tunasoma mfalme Nebukadneza alitamani kuwa na watu ambao watamsaidia katika Elimu za utafiti pamoja na utabiri wa mambo yanayokuja katika ufalme wake, hivyo akaazimu kwenda kuwatafuta watu wenye ujuzi mwingi na maarifa pamoja na wanajimu na wachawi wote waliosifika, kutoka katika majimbo yote ya dunia aliyokuwa anayatawala.
Lakini tunaona walipofika kwa watu walioamishwa wa kabila la Yuda, walionekana huko vijana wanne, wenye sifa ya kuwa na ujuzi na hekima zilizotoka kwa Mungu nao ni Shedraki, Meshaki, Abednego pamoja na Danieli ambaye alikuwa na ujuzi katika ndoto na Maono yote.
Hivyo tunasoma walipopelekwa katika jumba la kifalme kwa mafunzo ya lugha na Elimu za wakaldayo, kama tunavyojua maeneo kama hayo havikosekani vyakula vya kila namna, vinono vyote kama nguruwe, nyama za wanyama wasiopasuka miguu kama bata, divai, na ng’ombe, kuku n.k vilikuwepo ambavyo vingi kati ya hivyo vilikuwa ni Najisi kwa Taifa la Israeli.
Kwahiyo Danieli na wenzake kwa kuwa walikuwa wanamcha Mungu hawakudhubutu kuvunja torati ya Mungu kwasababu ya vyakula, Hivyo wakaazimu kumuomba mkuu wa Matowashi wasivitumie vile vyakula, ndipo wakajaribiwa kwa mtama na maji kwa muda wa siku 10, na tunaona licha ya kwamba MTAMA na MAJI ni vyakula visivyokuwa na virutubisho kamili lakini tunaona waliweza kunona na kunawiri kuliko wale wengine wote waliokuwa wanajishibisha na vyakula vyote vya kifalme.
Na yule mkuu wa Matowashi alipouona muujiza ule na ujasiri wao, moja kwa moja aliwatolea ile posho ya vyakula najisi na kuwalisha vyakula walivyokuwa wanataka wao. Na baada ya ile miaka 3 kuisha ya mafunzo, walipowasilishwa mbele ya MFALME ili kuzungumza nao, hawakuonekana waliokuwa mfano wa Danieli, Meshaki, Shedraki na Abednego watakaomfaa katika baraza lake la washauri.
Amen.
TUNAJIFUNZA NINI KATIKA MAMBO HAYA?.
Tunapomuweka Mungu nyuma kwasababu ya fursa fulani au mazingira fulani yaliyopo mbele yetu, tukidhani kuwa ndio tutafanikiwa ukweli ni kwamba hatutafanikiwa tutakwama tu!!, Inawezekana mazingira yanayokuzunguka kama nyumbani au kazini au popote pale yanakulazimisha wewe mwanamke uvae vimini au suruali, au kuweka makeup, angali ukifahamu kuwa sheria ya Mungu hairuhusu hayo mambo, ni najisi, kwakuwa unaogopa kutengwa, au kufukuzwa kazi, au kuonekana wewe ni mshamba sio mzuri, unajitia unajisi kwa kufanya vitu ambavyo Mungu hakukuagiza ufanye ukidhani kuwa ndio utafanikiwa au utaonekana mzuri au utapandishwa cheo n.k., ukweli ni kwamba hautafanikiwa kwa lolote, safari yako ni fupi.
Danieli na wenzake, waliazimu kula mtama na maji tu, lakini ndani ya siku 10 tu walinawiri kuliko wale wengine wote, kuonyesha kuwa vyakula vya unajisi havimfanyi mtu kunawiri badala yake ndio vinamfanya mtu KUFUBAA.
Na sisi leo vyakula vyetu najisi ni nini??..Sio nguruwe, wala bata, bali ni Uasherati, ibada za sanamu,Ulevi, sigara, Ufisadi, usengenyaji,utukanaji,wizi, Rushwa, Fashion{vimini, suruali, makeup, wiggy}, ushoga, pornoghaphy, musterbation,disco, kamari,anasa, n.k. Hivi vyote vitakupelekea UFUBAE rohoni na mwilini, kwamaana vinatoka rohoni Bwana Yesu alisema..
Mathayo 15:16-20″ Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi;… “
Hivyo usidhani kwamba kwa kufanya hivyo utakubalika, au utaonekana mzuri, au utafanikiwa, la!! bali itakuwa ni kunyume chake.”
Kumcha Mungu ndio chanzo cha mafanikio yote na Hekima yote, kwa kadiri tutakavyozidi kuendelea kutazama sura zinazofuata tutaona jinsi Danieli alivyokuwa mwaminifu mpaka Mungu akampa kujua SIRI ya mambo yatakayokuja kutokea mpaka mwisho wa dunia, na kupewa cheo cha kuwa mkuu wa maliwali na waganga wote wa dunia.
Ni maombi yangu leo katika nafasi uliyopo, USIJITIE UNAJISI NA VITU VYA ULIMWENGU HUU, Bali uwe na msimamo kama Danieli na wenzake walivyokuwa, na watakapouona msimamo wako, watakuacha uendelee nao, lakini usipoonyesha msimamo wako, shetani atakuchezea kama anavyotaka.
Ubarikiwe na Bwana YESU
Kwa mwendelezo >>MLANGO WA PILI.
Mada Nyinginezo:
NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!
JE! INAWEZEKANA MTU AKAWA ANAONA MAONO NA KUFANYA MIUJIZA NA BADO ASINYAKULIWE?
NINI MAANA YA KUBATIZWA KWA AJILI YA WAFU? (1WAKORINTHO 15:29)
Jina la BWANA wetu na mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe milele daima.
Karibu katika kujifunza maneno ya Mungu, leo tukiwa katika mwendelezo wa kitabu cha Yuda tunapomalizia sehemu ile ya mwisho. Tunasoma.
Yuda 1: 14 “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.
16 Watu hawa ni wenye kunung’unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.
17 Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo,
18 ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu.
19 Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.
20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,
21 jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.
22 Wahurumieni wengine walio na shaka,
23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.
24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;
25 Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina. “
Kama tulivyotangulia kusoma sehemu zilizopita tuliona watu wa aina TATU, mwovu aliowapandikiza katika kanisa la Mungu, waliofananishwa na nyota zipoteazo ambao weusi wa giza ndio akiba waliyowekewa milele, ambao wanafananishwa pia na miti ipukutishayo isiyo na matunda iliyokufa mara mbili, na visima visivyo na maji na miamba yenye hatari..wanafananishwa na magugu yaliyopandwa katikati ya ngano.
Na maonyo haya kumbuka waliandikiwa watu ambao wapo katika safari ya Imani, wakafananishwa na wana wa Israeli walipokuwa safarini, Na kama tunavyosoma wengi wao hawakuweza kuishindania Imani yao na kuilinda Enzi yao wakaishia kuanguka kwa makosa mengi, ikapelekea kutokuiona ile nchi ya AHADI Mungu aliyowaahidia.
Na tuliona watu waliotumiwa na shetani kuwakosesha wana wa Israeli Jangwani, walikuwa ni KORA na BALAAMU. Hawa walikuwa ni manabii, Na ndio maana kitabu cha Yuda kimewataja watu 3, na mwingine alikuwa ni KAINI. Tukisoma mstari wa 11 unasema
“Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.
12 Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ” .
Sasa huduma za watu hawa 3, ndizo zinazotenda kazi katika kanisa la Mungu leo, ili kuwapindua watu waliosimama katika Imani, na zinatenda kazi kwa udanganyifu wa hali ya juu kiasi kwamba ni ngumu kuzigundua. Katikati ya Huduma hizi ndipo kiti cha enzi cha shetani kilipo,(Ufunuo 2:13-14).
Wana wa Israeli walipokuwa kule jangwani wapo waliotii mafundisho ya Kora, ndio walioangamizwa naye, wapo pia waliousikiliza udanganyifu wa Balaamu nao pia wakaangamizwa, kadhalika katika kanisa wapo watakaopotea kwa kudanganywa na kwa kuyafuata mafundisho yatokayo kwa wachungaji wa uongo, mitume wa uongo, waalimu na manabii wa uongo, Huu ni wakati wa kuwa makini sana. Na utajuaje! kuwa hawa ni watumishi wa uongo? ni pale wanapoenda mbali na Neno, mfano wa Kora na Balaamu.
Biblia inasema katika ule mstari wa 18 “…….Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu”.
Jambo lingine linalo tutambulisha kuwa tunaishi siku za mwisho, ni kutokea kwa watu wenye kudhihaki, na hawa hawatoki mbali! bali ni ndani ya kundi linalojiita kundi lililopo safarini, kumbuka waliomdhihaki Mungu ni Kora na wenzake baada ya kuona kuwa safari imekuwa ndefu, yenye shida, ambayo ingepasa ichukue wiki kadhaa tu kumaliza lakini imechukua miaka 40, wakaanza kudhihaki na kusema hiyo nchi tuliyoahidiwa mbona hatufiki hata sisi tunaweza tukajiongoza wenyewe??. Mfano huo huo wa baadhi ya watu wanaojiita wakristo, utasikia wanasema “Unakuja umekuwa YESU?“…”Yesu mbona haji?”.n.k. na cha kusikitisha huyu ni mtu anayejiita mkristo ndio anafanya hivyo, hawaogopi hata kulitamka hilo jina lililo kuu, katika mambo yao ya kipumbavu. Moja kwa moja utafahamu watu kama hao wameshaanguka katika maasi ya Kora, na wala hawapo katika Imani japo wanajiita wakristo.
Mtume Petro pia alisema.
2Petro 3:1 “Wapenzi, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika zote mbili naziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha,
2 mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi iliyoletwa na mitume wenu.
3 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,
4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;”
Unaona hapo?. Uvumilivu wake Mungu ni kutuvuta sisi tutubu dhambi zetu, Lakini siku ya BWANA inakuja, inayotisha sana, kuwatekeza watu wote waasi, walioacha enzi yao. Wakati huo Bwana atakuja na watakatifu wake maelfu elfu, hao watakuwa ni wale waliokwisha nyakuliwa kabla, ndio watakaorudi na Bwana kuuhukumu ulimwengu wote, Kama HENOKO yule mtu wa 7 aliyenyakuliwa alivyoonyeshwa.(Ufunuo 19:11-20)
Yuda 1:14 “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.”
Ndugu huu ni wakati wa kufanya wito wako, na uteule wako imara(2Petro 1:10), angali upo safarini, Sio wakati wa kutanga tanga huku na kule, kila wimbi la mafundisho unapokea..Unaweza ukaona mafundisho fulani ni mazuri yanavutia na kukupa faraja, lakini hujui kidogo kidogo yanakutoa katika njia ya IMANI,..Hapo mwanzoni ulikuwa unasali, ulikuwa unafunga, ulikuwa unawasaidia watu, ulikuwa mnyenyekevu,ulikuwa na huruma, ulikuwa unaogopa hata kuvaa mavazi ya aibu na kutembea nayo barabarani, ulikuwa ukisikia Neno la Mungu tu, unatetemeka lakini baada ya kufika sehemu fulani! na kusikia mahubiri fulani tu! kutoka kwa watumishi fulani, kuanzia hapo hayo mambo yote yakafa kabisa,Yesu kwako amekuwa kama kitu cha ziada, hana sehemu kubwa katika maisha yako kama zamani, hata ule uwepo wa ki-Mungu uliokuwa unausikia kwanza umetoweka, hamu ya kutamani mambo ya mbinguni imekufa. fahamu tu hapo umeiacha imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu! geuka haraka. kwasababu hapo ulipo ndipo penye kiti cha enzi cha shetani alipo Balaamu na Kora. Hivyo ondoka haraka sana, Rudi katika imani,..Ishindanie hiyo kwasababu shetani ndiyo anayoiwinda.
Tafuta uhusiano wako binafsi na Mungu, kwa kudumu katika maonyo ya biblia, Na BWANA ni mwaminifu safari aliyeianzisha mioyoni mwetu ataitimiliza..kama alivyosema.
Yuda 1: 24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;
25 Yeye aliye MUNGU PEKEE, MWOKOZI WETU, KWA YESU KRISTO BWANA WETU; UTUKUFU UNA YEYE, NA UKUU, NA UWEZO, NA NGUVU,TANGU MILELE, NA SASA, NA HATA MILELE. AMINA.
Mungu akubariki sana.
Unaweza pia uka-Share kwa wengine, mafundisho haya, ili nao pia wanufaike, na Mungu atakubariki.
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.
ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:
NAPENDA KUJUA MAANA NA TOFAUTI KATI YA MYUNANI, MFARISAYO NA MSADUKAYO.
JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?
Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Yuda, leo tukiendelea na sehemu ya pili. Kama tulivyokwisha kuona ile sehemu ya kwanza, Yuda mtumwa wa BWANA, alitoa angalizo na maonyo kwa watu wa Mungu kwamba waishindanie imani waliokabidhiwa watakatifu mara moja tu, na kwamba maonyo hayo hawakupewa watu wote (yaani watu waovu na wema), hapana bali waraka ule uliandikwa kwa watu wa Mungu tu walioitwa peke yao (yaani wakristo). Hivyo ni vizuri ukafahamu hilo unapokisoma hichi kitabu,tukiendelea na mistari inayofuata tunasoma..;
“Yuda 1:7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.8 Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, HUUTIA MWILI UCHAFU, HUKATAA KUTAWALIWA, NA KUYATUKANA MATUKUFU.
9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.
10 Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama wanyama wasio na akili.
11 Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika NJIA YA KAINI, na KULIFUATA KOSA LA BALAAMU pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika MAASI YA KORA.
12 Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa;
13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao WEUSI WA GIZA ndio akiba yao waliowekewa milele”.
Kama ukichunguza watu hawa ambao Yuda anawazungumzia, ambao wanakataa kutawaliwa, wanaoenenda kwa kufuata mambo ya mwili, na wanaotukana matukufu, watu wanaofananishwa na nyota zinazotea ambao weusi wa giza ni sehemu yao waliowekewa milele, wanaonena maneno makuu magumu wasiyoyajua, Utaona kuwa Yuda amewapata kutoka katikati ya hawa watu watatu (yaani KAINI, BALAAMU na KORA). Kuna kitu kikubwa cha ajabu katikakati ya hawa watu.
Sasa tuwatazame ni kwa namna gani wamefananishwa na mawingu yasiyokuwa na maji, yachukuliwayo na upepo, na miamba ya hatari, na miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa; Kumbuka hawa watu wanaozungumziwa ni watu waliopo katikati ya kundi la Mungu waliojiingiza kwa siri.
NJIA YA KAINI;
Kumbuka Kaini hakuwa wa uzao wa Adamu kwa asili tangu mwanzo bali wa nyoka. Na nyoka kabla hajalaaniwa alikuwa hatembei kwa matumbo,bali alisimama wima kama mtu na alikuwa anazungumza kama mtu, ni kiumbe kilichokuwa karibu sana kufanana na mwanadamu, alikuja kuwa reptilia (nyoka tunayemwona sasa) baada ya kulaaniwa. Lakini Habili ndiye aliyekuwa mwana halisi wa Adamu, na uzao wake baada yake ndio ulioitwa “WANA WA MUNGU”, na uzao wa Kaini baada yake uliitwa “WANA WA BINADAMU “,
Na kama tunavyosoma tabia zote zilizokuwa kwa Kaini na uzao wake hazikutoka kwa Mungu, mfano tabia ya uuaji, alimuua ndugu yake kwasababu ya wivu, na ukichunguza uzao wake baada yake ulikuwa na tabia hiyo hiyo, mtoto wake Lameki alisema kama Bwana akimlipa Kaini kisasi mara 7 hakika Lameki atalipwa mara 77, sasa unaweza ukaona jinsi huyu mtu alivyokuwa muuaji kushinda hata baba yake.(Mwanzo 4:23), Ikiwa na maana kuwa kama baba yake aliweza kumuua mwenye haki mmoja (Habili), basi yeye ataua wenye haki 77.
Kadhalika tabia ya kuoa wake wengi ilianzia katika uzao wa Kaini, Ukisoma utaona huyu Lameki alikuwa na wake wawili jambo ambalo Mungu hakuliagiza. Lakini uzao wa Adamu (ambao ndio wana wa Mungu), walikuwa ni watu wanaomcha Mungu na kuutafuta uso wa Mungu siku zote soma(Mwanzo 4:25). Lakini agenda ya shetani siku zote ni kuwatafuta watu wa Mungu, na sio watu wa ulimwengu kwasababu hao tayari alishawapata. Na njia pekee anayoweza kutumia ni kuwakosesha wao na Mungu wao. Ili Mungu mwenyewe aamue kuwaangamiza, na ndio maana tunasoma katika mwanzo 6 utaona wana wa Mungu(yaani uzao wa Adamu) waliwatamani binti za binadamu (yaani uzao wa kaini) ambao ulikuwa ni mwovu, na kwenda kuwaoa na kusababisha kitendo cha kuchanganyika kwa mbegu. Hilo ndio likawa jambo pekee lililosababisha Mungu kuleta gharika kwa kuona mbegu takatifu imeharibika. Tunaona hapo japokuwa ulimwengu ulikuwa ni mwovu lakini hasira hasaa ya Mungu iliwaka juu ya wana wa Mungu kutoilinda enzi yao. Kumbuka “wana wa Mungu” kama wanavyozungumziwa pale sio malaika, kwasababu malaika hawazai wala hawazaliani. Na Mungu angewaadhibu malaika ingekuwa ndio wao waliozini, lakini badala yake waliadhibiwa wanadamu. Hivyo wana wa Mungu wanaozungumziwa pale ni wana wa uzao wa Adamu.
Ndio jambo linaloendelea leo katikati ya watu wanaojiita wakristo, shetani akishagundua upo katika mstari wa Imani, hali akijua wewe ni mzao mteule wa Mungu, atakuja kwa NJIA YA KAINI. Atakuletea jamii ya Viongozi wa Dini/Imani mfano wa Kaini, atakuletea wahubiri watakaokuhubiria kuoa wake wengi ni sawa watatumia Biblia kukuhakikishia jambo hilo, watakufundisha kuoa/kuolewa na mwanamke yeyote ni sawa tu! kumbuka hiyo ni njia mwovu siku zote wale binti wa Kaini ndio waliowakosesha wana wa Mungu, na ndio waliomkosesha pia na Sulemani,.Watakuhubiria kunywa pombe ni sawa biblia inaruhusu, watakufundisha Mungu haangalii mavazi, anaangalia moyo, hivyo hata ukivaa kimini na suruali na kupaka rangi usoni ni sawa….Na wewe hujui kwamba shetani ameshakumaliza..kukukosesha wewe na Mungu umeishindwa kuilinda enzi na IMANI yako uliyokabidhiwa mara moja tu! kwa kutokudumu katika maagizo yake, jambo litakalokutokea ni kuwekwa katika vifungo vya giza, kama watu wa Nuhu walivyofanywa na wale malaika walioasi..Na Bwana Yesu alisema kama zilivyokuwa katika siku za Nuhu…….
KOSA LA BALAAMU:
Kama wewe ni mwanafunzi wa biblia utajua kabisa Balaamu alikuwa ni nabii lakini sio mwisraeli, Alikuwa ni nabii na bado alikuwa ni mchawi vile vile biblia inasema hivyo! sasa unaweza ukauliza je! Mtu anaweza akawa ni mchawi na bado akawa ni nabii?? JIBU NI NDIO!! (soma Kumbukumbu 13),ni nabii kabisa na anapokea mafunuo kutoka kwa Mungu lakini alikuwa ni mchawi. Sasa wakati wana wa Israeli walipokuwa jangwani wanakaribia kupita katika nchi ya Moabu, yule Balaki mfalme wa Moabu aliwazuia wasikatize katika nchi yao. Hivyo Wamoabu wakaongezea kwa kumuajiri Balaamu aje kuwalaania(kuwaloga) wana wa Israeli. Lakini Mungu alimwoonya asifanye hivyo, kama alivyomwonya Kaini tu, lakini kwasababu ni mtu aliyependa fedha, akatafuta njia mbadala ya kuwakosesha watu wa Mungu.
Ndipo akaja na wazo jipya la kishetani zaidi, kama lile linalofanana na uzao wa Kaini, Akamwambia Balaki mfalme wa Moabu watu hawa (Waisraeli) hawalaaniki kwa namna yoyote isipokuwa kwa njia ya kuwakosesha wao na Mungu wao. Na njia pekee ni kuwaalika na kuwapa binti zenu wale walio wazuri wakaolewe na wana wao, ili watoe sadaka kwa miungu yao, na kufanya karamu za anasa, kitu ambacho Mungu wao amewakataza wasifanye. Na baada ya hapo Mungu wao atakasirishwa nao na kuwaangamiza. Na kweli njama zao zilifanikiwa baada ya kitendo kile walidondoka waisraeli elfu 24, (Hesabu 22-25).
Unaona hapo balaamu ni aina ya wahubiri wa uongo waliopo duniani sasa, ni kweli wanaweza wakawa na karama za kinabii,wanaona maono saa nyingine wanakutabiria jambo na linatimia, lakini kumbe ni wachawi walioajiriwa na shetani kuwaharibu watu waliosimama katika imani. Agenda yao kubwa ni kwa wakristo wa kweli waliosimama. Mafundisho yao yanakupeleka moja kwa moja kufanya uzinzi wa kiroho,(Kumchanganya Mungu na ibada za sanamu), watakuhubiria ibada za miungu mingi, kuwaomba watakatifu waliokufa zamani na walio hai, watakufundisha kuna nafasi ya pili baada ya kifo, watakufundisha hakuna kuzimu, n.k na wengine wanakutabiria na inatokea..
Na ndio maana Bwana alisema katika
Ufunuo 2: 13 Napajua ukaapo, NDIPO PENYE KITI CHA ENZI CHA SHETANI; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu WASHIKAO MAFUNDISHO YA BALAAMU, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa SADAKA KWA SANAMU, NA KUZINI.
15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.
16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.
17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Umeona hapo Bwana anazungumza na watu ambao wameishikilia IMANI, na akawaonya watubu watu wote wanaoshikilia mafundisho ya balaamu. Hivyo ndugu umeona kiti cha enzi cha shetani kilipo?? Hakipo freemason, kipo kwenye dini na mafundisho yote ya uongo katikati ya kanisa la Mungu. Hivyo kama unayashikilia toka huko, vinginevyo Bwana anasema atakuja kufanya vita na wewe kwa huo upanga wake.
MAASI YA KORA:
Kora naye alikuwa ni nabii kama Balaamu isipokuwa huyu sasa anatoka katikati ya wana wa Israeli tena katika uzao wa kikuhani (wana wa Lawi),alikuwa ni kuhani naye pia aliaminiwa na kupewa heshima kubwa katikati ya umati wa wana wa Israeli, Lakini aliinuka moyo na kuona kuwa MAMLAKA iliyowekwa na Mungu haistahili kuwaongoza, akaidharau TORATI ya Mungu na mtumishi wake, na kupeleka mashtaka juu ya mtu wa Mungu Musa,na kutoa maneno makuu ya kufuru, sasa kilichotokea alikusanya watu na kutaka kuwaundia MAMLAKA yake mwenyewe na kuwaongoza katika nchi yake ya ahadi anayoijua yeye. Lakini tunasoma mwisho wa siku ardhi ilipasuka na kummeza yeye pamoja na wafuasi wake wote waliomfuata (Hesabu 16).
Hii inafunua nini? Kora ni mfano wa viongozi wa dini wanaokataa MAMLAKA KUU, wanaokataa kutawaliwa na katiba maalumu ambayo Mungu kaiweka ambayo ni BIBLIA TAKATIFU. Wanayapinga yaliyoandikwa huko kwa faida zao wenyewe, Kama vile Kora, alivyoikinai njia Mungu aliyoiweka ya kupita nyikani, vivyo hivyo wahubiri hawa wataipinga njia ya msalaba kwa mafundisho yao,..hawawafundishi watu watubu, wajitwike misalaba yao wamfuate YESU, badala yake watawafundisha watu wajitwike mabunda ya pesa wamfuate Yesu ndio uthibitisho kwamba wanaelekea kaanani. Kumbuka Kora alikuwa anaona kama vile Musa anawatesa jangwani, wanapitia shida, na taabu, hiyo siyo njia ya Mungu..Vivyo hivyo na hawa wanapoona Watoto wa Mungu wanapitia magumu katika Imani zao wanakuja kuwavunja moyo na kuwafundisha,waache uongozi wa njia ya Mungu aliyoiweka, na wafuate uongozi wa kibinadamu.
Kora mahubiri yake yalikuwa ni kuwafariji kuwa wote ni watakatifu(Hesabu 16:3). Vivyo hivyo na hawa mafundisho yao ni kuwafariji watu na kuwaambia yote ni sawa, nyie ni watakatifu hata ukiishi maisha ya kawaida tu, utaenda mbinguni wewe bado ni mtakatifu kwanini kujiumiza kuishi maisha ya kilokole?.
Hivyo tukishafahamu tabia za hawa watu katikati ya kundi la Mungu, tunaonywa tujiepushe nao kwasababu ni nyota zipoteazo.
Biblia imerudia kuelezea habari hii ya kitabu cha Yuda katika kitabu cha 2Petro 2 soma kwa utaratibu itakusaidia sana kulinganisha yote mawili.
Inasema..
Mlango 2:1 “Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.
3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.
4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;
6 tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;
7 akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu;
8 maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;
9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;
10 na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka.
11 Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa malaika ambao ni wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele za Bwana.
12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;
13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;
14 wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;
15 wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;
16 lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule.17 Hawa ni visimavisivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.
18 Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;
19 wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.
20 Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.
Hivyo ndugu, Kanisa tunaloishi ni la hatari sana, je! umeufanya imara wito wako na uteule wako?. Unaishindania imani?. Kama hujatubu dhambi zako fanya hivyo sasa.
Mungu akubariki.
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
Kwa mwendelezo >>> KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
Mada Nyinginezo:
HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).
DALILI NYINGINE INAYOUTAMBULISHA UZAO WA NYOKA.
Biblia inamaanisha nini kusema Yeye aliye na sikio, na asikie?
Karibu katika kujifunza NENO la Mungu, leo tukikiangalia kitabu cha Yuda, kilichojaa maonyo makubwa kwa kanisa la leo. Yuda aliyeandika kitabu hichi sio Yule Yuda mwanafunzi wake YESU au yule aliyemsaliti hapana, bali ni Yuda yule aliyekuwa ndugu yake Bwana Yesu kwa kuzaliwa(Marko 6:3). Hivyo kwa uongozo wa Roho Mtakatifu aliuandika waraka huu mfupi kwa WATU WALIOITWA TU!! (yaani wakristo) na sio watu wote wa ulimwengu ambao sio wakristo, Leo tutasoma mstari wa 1-6″, Bwana akitupa neema tutaendelea na mistari inayofuata katika sehemu ya pili na ya tatu.
Biblia inasema…
Mlango 1:1-6″ Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, KWA HAO WALIOITWA, WALIOPENDWA, katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo.
2 Mwongezewe rehema na amani na upendano.
3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ILI NIWAONYE KWAMBA MWISHINDANIE IMANI WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU.
4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.
5 Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, ALIWAANGAMIZA BAADAYE WALE WASIOAMINI.
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, AMEWAWEKA KATIKA VIFUNGO VYA MILELE CHINI YA GIZA KWA HUKUMU YA SIKU ILE KUU”.
Kama tulivyotangulia kusema waraka huu uliandikwa kwa watu walioitwa peke yao, yaani watu waliokwisha kumwamini Bwana Yesu Kristo, Ikiwa na maana wakristo wote (mimi na wewe). Hivyo tunaposoma maandiko haya tufahamu kuwa maonyo haya yanatuhusu sisi tunaojiona kuwa tupo katika IMANI na kwa namna moja au nyingine haziwahusu watu ambao wapo nje ya ukristo. Kwahiyo unaposoma usilichukulie kiwepesi wepesi na ndio maana Yuda alianza na kusema “Napenda kuwakumbusha ijapokuwa mmeyajua haya yote.” Kwahiyo inawezekana umeyajua, lakini unakumbushwa tena.
Sasa Tukisoma ule mstari wa 3 anasema
“Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ILI NIWAONYE KWAMBA MWISHINDANIE IMANI WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU. “
Umeona hapo anazungumza juu ya IMANI waliyopewa watakatifu, ambayo wamepewa mara moja tu! na kama ni mara moja inapaswa ishindaniwe kwa bidii na kushikiliwa kwa maana ikidondoka tu! hakutakuwa na nafasi ya pili ya kuipata tena. Huo ndio msisitizo mkubwa hapo.
Na kushindania Imani ni nini?. Ni kudumu katika kile ambacho umekiamini na kujiangalia usianguke, Na ndio maana ukiendelea kusoma Yuda aliuchukua mfano wa Wana wa Israeli akifananisha na safari ya wakristo (yaani walioitwa), alisema, ” Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, ALIWAANGAMIZA BAADAYE WALE WASIOAMINI. “
Sasa tukichunguza habari ya wana wa Israeli, tunaona wote waliokolewa kweli, wote walibatizwa, wote walikuwa wanashiriki baraka zote za rohoni, wote walikuwa chini ya Neema, wote walikula chakula cha Bwana n.k. lakini “WENGI” wa hao Mungu hakupendezwa nao na kuangamizwa jangwani, kumbuka sio wachache bali ni “WENGI”. Kama tunavyosoma katika biblia.
1Wakoritho 10:1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
5 LAKINI WENGI SANA KATIKA WAO, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.
7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.
8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.
9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.
10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.
11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.
Umeona hapo biblia inasema mambo hayo yameandikwa ili kutuonya sisi, Wana wa Israeli ni mfano wa wakristo wote ulimwenguni, ambao kwa pamoja tulipoamini tulitoka Misri na siku tulipobatizwa tulivuka bahari ya Shamu. Lakini huo ndio ulikuwa mwanzo wa safari yetu sio kwamba ndio tumefika, la! bali kuanzia hapo ndio IMANI INAANZA KUSHINDANIWA.
Kama tunavyosoma katika maandiko waliofika Kaanani, ni wawili tu kati ya mamilioni ya watu waliotoka Misri, Kadhalika na kanisa la siku za mwisho, japo kuna mamilioni ya watu wanaojiita wakristo na wameokoka, na wamebatizwa kweli katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa, wanaoupako, wanaona kabisa wakibarikiwa na Mungu katika mambo yao yote (huko ndiko kula mana kwenyewe kutoka mbinguni), wananena kwa lugha, wanatenda miujiza, wanayajua maandiko, n.k. lakini biblia imetabiri katika siku za mwisho watakaofika ng’ambo ya pili ni wachache sana kwasababu walioitwa ni wengi, lakini wateule ni wachache. Lakini ni sababu ipi itakayowafanya watu wengi washindwe kuilinda imani, ni kwasababu kama hizo hizo tu za wana wa Israeli.
Tuzitazame:
> Ibada za sanamu: Wana wa Israeli walitengeneza sanamu za dhahabu wakiwa katikati ya safari yao ya Imani na kuanza kuziabudu, Hivyo Mungu akakasirishwa nao kuliko hata watu wa mataifa, ikapelekea kufanya dhambi isiyosameheka, mfano halisi wa leo mkristo upo safarini, Unafahamu kuwa ibada za sanamu, kuabudu picha au sanamu za watakatifu fulani waliokufa zamani angali unajua kufanya hivyo ni dhambi. Kuna hatari kubwa mno ya kuangamizwa na Mungu mwenyewe.
> Sababu nyingine ni Uasherati: Wana wa Israeli walifika mahali wakasahau maagizo ya Mungu na kuanza kuzini na wanawake wa kimataifa: Kadhalika na watu wanaojiita wakristo kuzini au kufanya uasherati nje ya ndoa takatifu, pamoja na kuvaa mavazi ya kikahaba yanayowasababishia wengine kutenda dhambi za uzinzi nafsini mwao vile vile ni kujiangamiza mwenyewe, ipo hatari kubwa ya kuondolewa kabisa katika neema.
> Manung’uniko: Hili nalo liliwafanya wana wa Israeli wakataliwe na Mungu, japo ni kweli waliitwa na Mungu mwenyewe na kubatizwa lakini manung’uniko yalifamfanya Mungu achukizwe nao. Ni mfano halisi wa sasa wakristo wengi wanapopitia na mitikisiko kidogo tu, wanasahau fadhili zote Mungu alizowatendea nyuma. Pengine anapitia misiba, anaanza kutoa maneno ya makufuru, anapitia, kuugua kidogo anaanza kulaumu Mungu kamuacha, mtu kapungukiwa kidogo tu! anaanza kunung’unika moyoni mwake anasahau kuwa miaka mingine nyuma Mungu alikuwa anamfanikisha n.k.. Sasa mambo kama hayo ndio yanayosababisha safari kuwa fupi…Biblia inasema atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka..Safari ya ukristo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.
> Pia tabia ya kutamani mabaya na kumjaribu Mungu. Ni kikwazo kingine kilichowafanya wengi wa wana wa Israeli wasimalize safari yao. Kwa mfano Mungu aliwakusudia wale mana tu! mpaka wakati watakapoingia nchi ya ahadi, wao wakawa wanataka nyama tena kwa njia ya kumjaribu, wakijua kabisa Bwana anaweza kufanya hivyo. Vivyo hivyo watu wa leo Hawataki kuridhika katika njia Mungu aliowakusudia wapitie, wanataka wakiwa wakristo bado wafanane na watu wa kidunia, wanaenda kanisani leo kesho wanaenda disko, wanaongea vizuri leo kesho wanatukana n.k. Hizi zote ni sababu kubwa zinazokwamisha safari. Ni heri mtu kama huyo asingeanza safari kabisa, kuliko kuingia na kufanya machukizo, maana nafasi ya pili haipo kwasababu IMANI INAKABIDHIWA MARA MOJA TU.
Na ndio maana tukiendelea kusoma tunaona Yuda aliwafananisha watu hawa na watu WALIOJIINGIZA KWA SIRI katikati ya kundi la Mungu, ni magugu katikati ya ngano, Alisema;
” 4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.
5 Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu “
Hivyo mtu yeyote anayefanya hayo na bado anajiita mkristo ni sawa na mtu aliyejiingiza kwa siri katikati ya kundi la Mungu mfano wa akina Kora, na dathani katikati ya wana wa Israeli ambao walishaandikiwa hukumu yao tangu zamani. Na biblia imewafanisha hawa na wale malaika walioasi (Shetani na malaika zake), ambao hawakuilinda enzi yao. sasa hivi wamefungwa katika vifungo vya giza wakisubiria ile hukumu ya siku ile watakapotupwa wote kwa pamoja katika lile ziwa la moto. Katika kanisa la kwanza walikuwepo watu waliojiingiza kwa siri, na hata sasa wapo wengi.
Hivyo ndugu kwanini unaendelea kuichezea au kuichukulia Imani yako juu juu, kumbuka upo safarini na imani umekabidhiwa mara moja tu, na wanaomuudhi na wanaompendeza Mungu siku zote huwa ni wale walio safarini na sio wasiomjua Mungu, hao Mungu atawahukumu mwenyewe siku ya mwisho. Na ndio maana anasema ni heri uwe moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu. Hatari kubwa ipo kwako wewe uliye mkristo vuguvugu, usipoilinda ENZI YAKO, na KUISHINDANIA IMANI utafananishwa na wale malaika walioasi ambao wameandaliwa ziwa la moto.
Huu ni wakati wa KUTUBU na kufanya IMARA WITO WAKO, NA UTEULE WAKO. Tunaishi katika siku za mwisho na Bwana yupo karibu kuja, Je! utaenda nae?.
Mungu akubariki.
Tafadhali share kwa wengine ujumbe huu.
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
Kwa mwendelezo >>> KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 2
Mada Nyinginezo:
KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.
MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.