Karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu lililo Mwanga wa Njia zetu, na Taa iongozayo miguu yetu (Zaburi 119:105).
Neno hili lililo Taa linasema..
Yuda 1:5 “Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, ALIWAANGAMIZA BAADAYE WALE WASIOAMINI”
Maandiko hayo yanatufundisha kuwa KUOKOLEWA sio Mwisho wa safari. Kwani ni kweli wana wa Israeli waliokolewa kutoka Misri jeshi lote.. lakini si wote walioingia nchi ya Ahadi, bali watu wawili tu ambao ni Yoshua na Kalebu, na watoto wao ambao walizaliwa jangwani, lakini wengine wote MUNGU aliwaangamiza jangwani ijapokuwa aliwatoa Misri.
Leo wanaookolewa ni WENGI, wanaomkiri YESU ni wengi!, lakini pia ni wengi wanaoangamizwa na Bwana, kwasababu ya kutotembea na Mungu katika wokovu wao.
Wengi wa wana wa Israeli walijaa viburi (Mfano wa Dathani na Kora, soma Hesabu 16:1-50) na wengine walijaa mioyoni mwao manung’uniko na ibada za sanamu, na wengine walikuwa ni watu wa kumjaribu Mungu kila wakati..ingawa wote walikuwa wameokoka na utumwa wa Farao, lakini kwa bahati mbaya hawakuiona ile nchi ya Ahadi.
WALIOKOLEWA lakini baadaye WALIANGAMIZWA!…. WALIFUNGULIWA lakini baadaye WALIANGAMIZWA…. WALIPONYWA lakini baadaye WALIANGAMIZWA… Na jambo linalohuzinisha Zaidi ni kwamba waliangamizwa jangwani wakiwa bado wanakula Mana (Baraka za mbinguni), Vile vile waliangamizwa wakiwa chini ya WINGU NA NGUZO YA MOTO (Upako na Utumishi) na Zaidi ya yote walikuwa wameshabatizwa katika roho katika bahari ya Shamu.
Mambo haya yanabaki kuwa funzo na onyo kwetu ili tusifanya makosa kama hayo, kama maandiko yasemavyo..
1Wakorintho 10:1 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.
7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.
8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.
9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.
10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.
11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.
Je unajivunia ubatizo?… Unajivunia dhehebu?…unajivunia Karama uliyo nayo?… unajivunia upako?.. Vyote hivyo wana wa Israeli walikuwa navyo, lakini wengi wao waliangamizwa.
Utakase ukristo wako, kaa mbali na dhambi!, usimjaribu Mungu, usiabudu sanamu baada ya kuokoka, jitenge na mambo ya ulimwengu, tembea na Mungu kama Yoshua na Kalebu, na Bwana atusaidie sote katika hayo.
Amen.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
SHIKA SANA ULICHO NACHO, ASIJE MTU AKAITWAA TAJI YAKO.
Je Henoko aliyeenda na Mungu alikuwa ni mwana wa Kaini? (Mwanzo 4:16)
ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.
Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ni nani?
Kitabu cha Waebrania ni moja ya nyaraka ambazo waandishi wake hawajajitambulisha aidha ndani au mwanzoni au mwishoni mwa nyaraka hizo. Lakini kwa kutathimini baadhi ya nukuu za mwandishi, huwenda alikuwa ni mtume Paulo aliyeuandika. Kufuata na kumtaja Timotheo kwenye waraka huo, na tunajua Timotheo alikuwa chini ya utume wa Paulo, kwani ndiye aliyeongozana naye na kumtaja sana katika nyaraka zake nyingi.
Waebrania 13:23 Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; ambaye, akija upesi, nitaonana nanyi pamoja naye.
Na pia jinsi mwandishi alivyomalizia waraka wake, kwa kusema “neema na iwe nanyi nyote”. Ni salamu inafanana na nyaraka zote za mtume Paulo, kila alipomaliza alihitimisha na baraka hizo.
Japo wengine wanasema namna ya uandishi haifanani na mtume Paulo, yawezekana alikuwa ni Apolo, au Barnaba, au sila au mtu mwingine tofauti na Paulo.
Lakini kwa vyovyote vile kumtambua mwandishi, si lengo la uandishi, lengo ni kufahamu kilichoandikwa ndani humo.
Kwa ufupi, kama kitabu hichi kinavyoanza kujitambulisha, kinasema
WARAKA KWA WAEBRANIA.
Maana yake ni kitabu kilichoelekezwa kwa wayahudi-wakristo waliokuwa katika kanisa wakati ule. Ndio maana kwa jinsi ulivyoandikwa waraka huu, mwandishi anazungumza na mtu ambaye mwenye uelewa wa dini ya kiyahudi na taratibu zake za kiibada.
Dhumuni kuu ni kueleza UKUU WA YESU JUU YA WATU WOTE, NA MAMBO YOTE YA AGANO LA KALE.
Kwamfano anaeleza Yesu alikuwa mkuu juu ya;
Waebrania 1:1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu
Waebrania 1:13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? 14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Waebrania 10:11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.
12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;
13 tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. 14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
Hivyo kitabu hichi kinamfafanua Kristo kwa undani, jinsi alivyo na ukuu zaidi ya mambo yote ya agano la kale. Na kwamba watu wote tangu Adamu mpaka Ibrahimu wasingeweza kukamilishwa bila Kristo. Waliishi wa ahadi hiyo ya kuja mkombozi, wakiingojea kwa shauku na hamu (Waebrania 11).
Lakini pia kitabu hichi kinatoa angalizo kwa wayahudi wasirudi nyuma kwasababu ya dhiki na mateso yanayowapata kwa ajili ya imani ya Yesu Kristo. (Waebrania 12:1-13, 10:26-31), Bali wamtazame Kristo kama kielelezo chao, jinsi alivyostahimili mashutumu makuu namna ile. Hii ni kutuhamasisha na sisi kuwa tunapopitia dhiki leo basi nasi tumtazame Kristo aliyestahili, mapingamizi yale, wala hakuutupa ujasiri wake.
Waebrania 12:1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Zipo aina tatu za Utakatifu, na leo tutaangalia moja baada ya nyingine, na tutajua ni upi unaotufaa sisi.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Huwezi kufanya kazi zote peke yako..
Aliyeunda injini ya gari, alihitaji mwingine mwenye ubobezi katika utengenezaji wa matairi, lakini pia alimhitaji mbobezi wa umeme wa magari, hivyo ili gari lisimame na kuanza kutembea limegharimu mikono na ujuzi wa wataalamu wengi.
Vile vile, mtumishi wa Mungu mmoja hawezi kufanya mambo yote peke yake, kuna wakati wengine watahusika tu.
Katika biblia kuna mahali Filipo alihubiri na kubatiza, lakini lakini Petro na Yohana waliwaombea hao waliobatizwa ili wajazwe Roho Mtakatifu.
Matendo 8:12 ”Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.
14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;
15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;
16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu”
Umeona? mmoja Anabatiza wengine wanaombea ujazo wa Roho Mtakatifu..
Mambo yote yanakamilika namna hiyo katika ushirikiano na umoja wa Roho, na ndivyo kanisa la kwanza lilivyoenenda, hakukuwa na mashindano wala wivu katikati yao, tofauti na leo ambapo kila mtu anajiona bora kuliko mwingine.
Maandiko yanazidi kutuonyesha kuwa hata Paulo, hakupanda na kuwagia yeye, bali matunda yake yalipaliliwa na wengine.
1 Wakorintho 3:6-7 “Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.
7 Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye”.
Kama mtumishi wa Mungu, Je unaweza kuruhusu watumishi wengine wawajenge wale uliowatafuta wewe?…
Kumbuka si kila mtumishi ni wa kweli!…wengi ni wa uongo, lakini je inapotokea umehakiki kuwa kweli yule ni mtumishi wa Mungu, je waweza kuruhusu yule uliyemvua wewe ajengwe na mtumishi mwingine kama wewe?.
Kama hilo jambo gumu basi msaada wa haraka kutoka kwa Bwana unahitajika kwasababu ndivyo Mitume walivyofanya na sisi tunapaswa tufuate hivyo vielelezo.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.
JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?
(Masomo maalumu yahusuyo faida za matoleo).
Jifunze kutoa sadaka!!, jizoeze kutoa sadaka, jitaabishe kutoa sadaka!!.
Utoaji si agizo la washirika bali hata viongozi (wachungaji, waalimu, wainjilisti na watu wote wanaoujenga mwili wa Kristo), pasipo kujali Umri wala kipato. Hili ni agizo la Bwana YESU lenye baraka na laana nyuma yake (soma Mathayo 25:31-46).
Sadaka inayotolewa katika misingi ya Neno la Mungu, inafanya mambo makubwa zaidi ya yale tuyajuayo.
Sadaka inayotolewa katika msingi wa Neno la Mungu, inameza sadaka nyingine zilizotolewa na upande wa ibilisi.
Ile fimbo ya Musa ilibidi aitoe na kuitupa, ndipo ilipoweza kumeza zile fimbo nyingine za wachawi wa Farao.
Sasa zile fimbo zilizomezwa, laiti zingeendelea kuwepo zingeleta madhara mengine kwani zilikuwa ni za kichawi, na zilitumika na wachawi kwa shughuli za kichawi.
Sasa ilimgharimu Musa kuitoa fimbo yake kwanza ili imeze zile nyingine. Vile vile iliwagharimu wachawi kutoa fimbo zao za gharama ili wahindane na Musa.
Vile vile kuna mambo mengine yanahitaji tu matoleo yatatuke..(Kasome Waamuzi 20:20-40).
Sasa wale waganga wa Misri walizigharimia zile fimbo zao, hazikutokea tu… huenda walizinunua kwa fedha na kuzifanyia matambiko mengi.
Kitabu cha Matendo ya Mitume kinatuonyesha jinsi waganga wanavyougharimia uganga wao.
Matendo 19:17 “Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa.
18 Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.
19 Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu”
Hapo anasema gharama ya vile vitabu vya uganga vilivyochomwa ilikuwa ni elfu 50.
Sasa tukisema elfu 50, kwenye vichwa vya wengi inadhaniwa ni shilingi za kitanzania, zinazotosha tu gharama ya nauli kutola mkoa mmoja hadi mwingine..La!.
Kujua thamani halisi ya vipande vya fedha elfu 50…rejea kile kiasi Yuda alichoongwa ili amsaliti Bwana YESU, maandiko yanasema alipewa kiasi cha vipande 30 tu vya fedha na vipande hivyo vilitosha kununulia shamba (ambalo hatujui ni hekari ngapi) lakini tunajua ni hekari nyingi maana zilitumika kama eneo la makaburi..soma Mathayo 27: 3-7.
Sasa piga hesabu kama vipande 30 vya fedha ya Yuda vimenunua shamba, na hapo vitabu vya waganga gharama yake ni vipande vya fedha elfu 50..gawanya hapo uone waganga waliugharimia uganga wao kiasi gani…
Utaona hapo ni zaidi ya mashamba 1,600 na kama shamba moja litauzwa tu kwa gharama ya shilingi za kitanzania milioni moja…basi jumla yake vile vitabu vyote ni zaidi ya BILIONI MOJA.
Kwahiyo wale waganga waligharimia mabilioni kuusimamisha uganga wao!!!…..
Halafu wewe na mimi kuigharimia injili kidogo tu tunaona tabu!!!!…..Fikiri mara mbili…fikiri mara mbili!!!.
Jenga ufalme wa Mungu, kwani shetani anajenga ufalme wake kwa kasi na gharama.
Bwana atusaidie.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
Kupiga ramli ni nini katika biblia?
Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe.
Upo umuhimu wa kuhubiri injili mahali popote na katika mazingira yoyote kwasababu ni agizo la Bwana mwenyewe. Wapo wanaoamini kuwa injili ya mitaani na masokoni hazina faida yoyote kwasababu watu wanakuwa hawapo katika utulivu. Na pia wapo wanaoamini kuwa injili za kwenye mikutano au makanisani ndizo zilizo bora.
Lakini nataka nikuambie: Injili zote zina umuhimu. Za watu walio katika utulivu na utayari wa kusikiliza, na hata za wale ambao hawako tayari kabisa.
“Basi katika sinagogi akahojiana na Wayahudi na waliomcha Mungu, na wale waliokutana naye sokoni kila siku.”
(Matendo 17:17)
“Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu…”
(Luka 8:1)
Kikawaida ni ngumu kumsimamisha mtu barabarani na kumwambia asikilize. Lakini unapohubiri bila hata ridhaa yake, Neno linaweza kuingia ndani yake hata kama hataki. Lile Neno linaweza kuwa mbegu njema itakayochipuka kwa wakati wake.
Kwahiyo ni heri asikie moja kuliko kutokusikia kabisa. Wengine hawaendi kanisani, wengine ni wa imani tofauti, wengine wamejitosheleza – lakini kwa kuhubiri, unawafikia.
“Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana”
(Ezekieli 2:7)
Hata kama ni mara ya mia, huenda Neno moja tu likamgusa. Au wewe ndiye umeanza safari ya wokovu ndani yake ambayo itakamilika baadaye.
Wapo wanaohitaji kusikia mara nyingi. Ndio maana Bwana alituma manabii kupiga kelele:
“Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta…”
(Isaya 58:1)
Kazi ya kuhubiri si nyepesi. Lakini matokeo yake ni makubwa sana:
“Kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye”
(Luka 15:10)
Pengine umesikia injili mara nyingi lakini bado hutaki kubadilika. Injili ya kurudia rudia si tangazo, ni ushuhuda dhidi yako.
“Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja”
(Mathayo 24:14)
“Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu”
(Warumi 2:16)
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, basi wasiliana nasi:
📞 +255789001312
📞 +255693036618
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya hapa:
👉 https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mafundisho mengine:
Je! Watu ambao hawajawahi kusikia injili kabisa siku ya mwisho watahukumiwa?
INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?
Tangu mwanzo mwanadamu alikuwa akijaribu kujiokoa kwa njia yake mwenyewe ikiwemo kuonyesha matendo yake mazuri, na mwenendo wake mkamilifu lakini hakuweza. Pengine aliweza kushinda wizi kikamilifu lakini uongo ukamshinda, aliweza kushinda uzinzi wote, lakini tamaa zikamtawala, aliweza kushinda ibada za sanamu na vinyago, lakini kusamehe kukamshinda. Alipoweza kushinda kimoja, nyuma yake kulikuwa na elfu vinavyo mhukumu.
Na hiyo ilimfanya asikidhi vigezo vya kuingia mbinguni, kwasababu watakaoiona mbingu na Mungu ni watakatifu asilimia mia wasio na doa lolote. Ndio maana maandiko yanasema wote wameoza,wamepotoka hakuna amtafutaye Mungu. Bali tunahesabiwa haki bure kwa neema ya Bwana Yesu Kristo.
Warumi 3:11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. 12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
Ndio sababu ya Yesu kuja duniani, ili kwa kupitia kumwamini yeye tuipokee hiyo neema ya kuitwa watakatifu, bila kuonyesha kwanza kipimo chochote kwa Mungu.
Maana yake ni kuwa mimi na wewe tunapomwamini Yesu Kristo, ni moja kwa moja tunaitwa watakatifu, tuliosamehewa dhambi zetu, na kuondolewa pia.
Ikiwa umemwamini leo Yesu Kristo, moja kwa moja Mungu hakuhesabii tena dhambi yoyote kama mkosaji. Ijapokuwa utakuwa hujakamilika bado. Hii ndio maana ya neema, yaani kukubaliwa kusikostahili. Ilikupasa kwanza uwe na matendo makamilifu asilimia 100 kama Bwana Yesu, ndio uitwe mtakatifu uliyestahili kumwona Mungu. Lakini sasa kwa kuupokea ukombozi wa Yesu Kristo, dhambi zako, zimefuta unaitwa mtakatifu, kabla hata ya ukamilifu wa utakatifu wenyewe kukufikia. Ndio maana sisi tulio ndani ya Kristo hatuna budi kuwa na amani, na furaha wakati wote. Kwasababu ule mzigo mzito wa kujitahidi sisi wenyewe kuingia mbinguni umeondolewa na Yesu Kristo Bwana wetu, kwa kifo chake pale msalabani.
Lakini sasa, katika nyakati hizi za mwisho suala hili la neema limetafsirika vibaya, kama tu nyakati zile za zamani, na hapo yatupasa tuwe makini sana. Ni sawa na taifa litangaze neema kwa nchi yake na kusema, sasa huduma zote za maji ni bure, hakuna kulipia bili,matumizi ni kama unavyotaka. halafu uone watu wanatumia fursa hiyo kwenda kufungulia mabomba yatiririshe maji kwenye mitaro na mabarabarani, kila mahali kuwe ni maji tu, Bila shaka utasema hawa watu wamerukwa na akili, hawana sifa ya kupewa huduma hiyo tena.
Ndivyo ilivyo kwa jambo linaloitwa neema, tusijipojua kanuni zake, tutajikuta badala ya kupokea wokovu, tunapokea maangamizi. Badala ya kukazana kumpendeza Mungu, tunastarehe katika dhambi, Na ndicho kinachoendelea sasa kwa sehemu kubwa miongoni watu na madhehebu.
Yafuatayo ni mambo ambayo ujiepushe nayo kwa nguvu zote, wewe uliyeipokea neema ya Mungu.
2 Wakorintho 6:1
[1]Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.
Ukisoma vifungu vichache vya nyuma anasema mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya.
Mtu ambaye hataki geuko, baada ya kusamehewa dhambi zake, huyo ni mtu ambaye ameipokea neema bure, haithamini, ameitwa mtakatifu, halafu hataki kuishi maisha matakatifu, anaendelea na maisha yake yale yale ya kale.. Mtu kama huyo asijidanganye neema hiyo ni batili. Mtu yeyote aliyeokoka wakati huo huo una wajibu wa kuanza kupiga hatua za mabadiliko, na unapaswa uithamini sana hiyo zaidi ya vyote, kwasababu ni Mungu ndiye akutakasaye baada ya hapo.
Lakini pia mtu ambaye amekaa muda mrefu hamzalii Mungu matunda, anahesabika kama aliyeipokea neema ya Mungu bure, na hivyo mwisho wake unakuwa ni kukatwa.
Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Je! Umeitii neema hii inayokufundisha kukataa machafu ya duniani?. Leo yapo madhehebu yanayosema, ukiokoka umekoka milele, kazi yako imeisha, hata usipoonyesha bidii nyingine yoyote kwa Mungu,huwezi potea. Ndugu yangu kuwa makini sana na imani hizi. Neema haipokelewi bure.
Epuke pia kuipungukia neema.
Waebrania 12:15-17
[15]mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
[16]Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.
[17]Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.
Kuipungukie neema Ni tabia ya kuishusha thamani neema, na kuilazimisha itende kazi hata katika kiwango ambacho si chake.
Hii hasa huja kwa watu ambao wanazoelea kufanya dhambi mara kwa mara wakiamini kuwa kwasababu Mungu hawahesabii makosa basi hata wakifanya kosa lolote hawawezi kupotea.
Ndugu, neema si kuhalalisha maisha ya dhambi.
Biblia inasema..
Warumi 6:1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Usitende dhambi za mazoelea, ukadhani neema itakuwa sikuzote kukufunika. Ukiifanyia jeuri neema, itaondoka kwako.
Waebrania 6:4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
Yuda 1:4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.
Neema ya Mungu inaweza badilishwa ikamaanishwa kivingine kabisa. Kwamfano utaona leo hata mashoga, wanavyama vyao wakisema sisi tupo chini ya neema. Walevi nao, wenye dhambi nao wanasema neema ya Yesu ipo duniani sasa, kumwokoa kila mtu.
Hivyo watakuambia maneno kama usihukumu usije ukahukumiwa. Na wana amani na ujasiri katika hayo wanayoyafanya na wengine wanajiita maaskofu na wachungaji, wakihalalisha kila kitu kiovu kufanyika kwa kivuli cha neema.
Hao ndio waibadilishao neema ya Bwana Yesu kuwa ufisadi, hilo Neno ufisadi ni zaidi ya uasherati, Ni pamoja na matendo yote maovu kupita kiasi. Lakini neema ya Yesu,.haikuja kufunuki dhambi, bali ilikuja kuondoa dhambi ndani ya mtu. Usiwe mmojawapo aibadilishaye neema ya Mungu.
Hivyo kwa vifungu hivyo itoshe kusema kuwa NEEMA tunaipokea bure, lakini ili iweze kufanya kazi lazima tujue sifa zake, kisha tuzikubali, vinginevyo tutajidanganya na kuangamia. Ni sawa na mtu akupe gari bure, lakini usipoliweka mafuta, na kujua kuliendesha linakuwa halina tofauti na mdoli wa gari.
Lakini ukiithamini neema, itakutunza, itakuhifadhi na kuyaficha makosa yako yote, Hivyo utaendelea kuonekana mkamilifu asilimia mia mbele za Mungu, na hata ukifa, ni moja kwa moja mbinguni.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.
MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?
JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.
Zipo kanuni za ki-Mungu tunaweza kuzifuata na zikaleta matokeo kabisa halisi, lakini zisiwe na manufaa kwetu katika suala la wokovu. Sasa kabla ya kuangalia ni kwa namna gani?
chukulia mfano wa kawaida.
Mwanamke yeyote anaweza kubeba ujauzito katika mazingira mbalimbali, kwamfano anaweza akatwezwa nguvu (akabakwa), na akapata ujauzito, lakini pia anaweza kwenda kujiuza kama kahaba na bado akapata ujauzito, vilevile anaweza akasubiri aolewe kwanza katika ndoa halali ndipo apokee ujauzito na likafanikiwa vilevile tu, kuleta kiumbe duniani, kama angefanya hayo kabla ya ndoa, au atokapo nje ya ndoa yake.
Sasa unaweza jiuliza, katika njia zote hizo ambazo angepata ujauzito ni ipi iliyo halali inayokubalika mbele za Mungu na wanadamu. Bila shaka ni hiyo njia ya mwisho ambayo ni ya kuolewa kwanza, ndipo apokee ujauzito kutoka kwa mume wake mmoja wa halali. Na ndio mtoto huyo hujulikana kama halali sio haramu.
Lakini cha ajabu ni kuwa ijapokuwa njia halali ipo lakini feki pia huleta matokeo yaleyale mfano wa halali. Kwasababu gani? Kwasababu kanuni ya kupata mtoto, si kanuni ya uhalali. Hivyo ni vitu viwili tofauti,
Hata Ibrahimu, alikuwa na watoto wengi, alitangulia Ishmaeli, kisha baadaye wakazaliwa na watoto wengine sita kwa suria mwingine, mbali na Isaka. Wote walikuwa wanadamu, viumbe wa Mungu, wenye akili na nguvu na baraka, wasio na hatia. Lakini lilipokuja suala la urithi, ndipo kubaguliwa kulipokuja, Watoto wote wa masuria walifukuzwa wakapewa zawadi tu bali Isaka alipewa vyote.
Mwanzo 25:5-6
[5]Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo.
[6]Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
Zipo kanuni nyingi sana za kiroho ambazo mtu yeyote, hata ambaye hajamwamini Yesu anaweza zitumia na zikatoa matokeo yaleyale sawa tu na mtu ambaye ameokoka.
Kwamfano, kufanya miujuza na ishara kwa jina la Yesu. Watu hawajui kuwa jambo hili huhitaji imani tu, katika jina lake. Hivyo wale wafikiao kiwango hicho haijalishi ni mwizi, ni mpagani, anaweza pokea muujiza na akafanya pia muujiza sawa tu na yule aliyeokoka.
Kwasababu gani? kwasababu amefanikiwa kufuata kanuni ambayo ni Imani.
Akijua lile neno linalosema ‘yote yawezekana kwake yeye aaminiye’’ (Marko 9:23). Ndio maana walikuwepo watu wengi wasiokuwa wayahudi kipindi kile cha Yesu walipokea miujiza mikubwa, zaidi ya wayahudi kwasababu tu ya ukubwa wa imani zao. Na sio haki zao.
Vivyo hivyo hata katika kuomba. Mtu yeyote aombaye hupokea. Ni kanuni ya asili ya rohoni, haijalishi ni nani.
Mathayo 7:8
[8]kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Watu hawajui hata kufanikiwa kwa shetani hutegemea maombi, na yeye pia huenda mbele za Mungu kuomba na hupewa..hajiamulii tu mambo yake ovyo ovyo bila idhini ya Mungu, kwasababu hii dunia si yake… utauliza kwa namna gani, ? unamkumbuka shetani kipindi cha Ayubu, yeye naye alikwenda kujihudhurisha mbele za Mungu, ndipo akaleta uharibifu. Akapeka haja zake akasikiwa, dua zake na magoti yake.
Ayubu 1:6
[6]Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao.
Watu wengi wanapoona wanamwomba Mungu wanajibiwa wanadhani, ndio wamekubaliwa na Mungu. Kumbe unaweza kuomba kama mwana-haramu usiyekuwa na urithi wa uzima wa milele, bali haki ya kupokea tu unachokiomba.
Unaweza ukafanya miujiza kama mwana-haramu. Lakini usiende mbinguni.
Mathayo 7:22-23
[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
[23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Unaweza ukamwamini Yesu, na kumuhofu, lakini ukaamini kama mashetani.
Yakobo 2:19
[19]Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
unaweza ukawavuta watu kwa Kristo na wakaokoka, lakini ukawa mtu wa kukataliwa kama tu Paulo alivyosema katika;
1 Wakorintho 9:27
[27]bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
Kanuni Mungu anayoitazama kwetu ni Wokovu uliokamilishwa kwa matendo yake.
Angalia mwishoni pale kwenye Mathayo 7:23 Bwana Yesu alichokisema;
“ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Umeona je unaishi maisha gani?. hicho ndio kipimo cha ki-Mungu,
Alisema pia.
Yakobo 2:24
[24]Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
Hakikisha maisha yako yanaendana na ukiri wako, wa imani yako, usiishi tu kama mtu ambaye hajaamini ukijitumainisha, kuona maombi yako yanajibiwa, karama yako inafanya kazi, imani yako inatenda kazi..hizo ni kanuni za kupokea lakini sio kanuni za uhalali wa kuurithi uzima wa milele. Ishi kama mtu ampendezaye Bwana wake kimwenendo, ndipo hayo mengine yakifuata huna hasara.
Nyakati hizi za mwisho, adui anaweka uzito kwenye mioyo ya watu wasipende kutafuta maisha matakatifu, kinyume chake wabakie tu kwenye miujiza, uponyaji, utabiri…Siku ile hivyo vitu havitafuata na wewe ndugu, bali matendo yako.
Ufunuo wa Yohana 14:13
[13]Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Tuanze sasa kujipima mienendo yetu. Kisha tutumie nguvu nyingi hapo kujirekebisha, sawasawa na imani tuliyoipokea, ili tuwe wana halali waliozaliwa kweli ndani ya Kristo, watakaorithi uzima wa milele.
Wokovu wa kweli hufunuliwa kwa mwenendo mzuri. Tuitazame sana kanuni hii.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine: