Swali: Je, Mtume Paulo alimaanisha Nini kusema Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno Bali katika nguvu?.
Jibu: Turejee mstari huo..
1 Wakorintho 4:20 “Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu”.
Hapo anaposema kuwa Ufalme wa Mungu hauwi katika “neno” hamaanishi “Neno la Mungu”...kwasababu Ufalme wa Mbinguni unajengwa na NENO LA MUNGU kama nguzo ya msingi…na pasipo hilo hakuna ufalme wa Mungu…kinyume chake ni ufalme wa giza unajengwa.
Hivyo biblia inaposema ufalme wa Mungu hauwi katika neno, inamaanisha kuwa hauwi katika “MANENO MATUPU YASIYO NA NGUVU ZA MUNGU”...Bali unakuwa katika maneno yenye nguvu za Mungu.
Maana yake ishara na miujiza inafuatana na Neno la Ufalme…
Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho alizidi kuliweka hilo vizuri katika 1Wathesalonike 1:5.
1 Wathesalonike 1:5 “ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika MANENO TU, bali na KATIKA NGUVU, na KATIKA ROHO MTAKATIFU, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu”.
Vile vile na sisi tunapaswa tuhubiri injili isiyo ya maneno matupu au yenye ushawishi wa maneno ili kuvuta watu… bali yenye dalili na udhihirisho wa Roho.
Maana yake ishara na miujiza vifuatane nasi…Na muujiza wa kwanza ni watu kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha…
1 Wakorintho 2:4 “Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Elewa maana ya mstari huu;
Mithali 10:12 Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote.
Mstari huu unalenga kutufundisha sifa za kipekee sana za upendo. Ambazo zinazungumziwa pia sehemu mbalimbali.
Kwamfano hapo anasema kuchukiana hakuzai kingine zaidi ya fitina,( yaani uchongezi, na kudhuriana), lakini upendano husitiri MAKOSA YOTE. Anaposema yote. Ni kweli yote. Endapo upendo utatoka kwelikweli katika kilele chake. Hiyo ndio sifa ya ajabu ya upendo ambayo kitu kingine chochote chema hakiwezi kutoa, kwamfano imani, nguvu, mamlaka, uweza n.k. haviwezi kusitiri “makosa yote”. Ni upendo tu peke yake.
Neno hilo hilo pia limerudiwa katika agano jipya.
1Petro 4:8 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi
Ndio maana Bwana Yesu alisema Torati yote imelalia hapo, katika kumpenda mwenzako kama nafsi yako, alisema vile unavyotaka wewe utendewe watendee wenzako. Utashangaa tu, wivu unayeyuka wenyewe, hasira inakufa, vinyongo vinaondoka, mashindano yanapotea, wizi, uzinzi unafutika, kwasababu umegundua kuwa mwenzako ni kama hiyo nafsi yako mwenyewe, kama vile wewe unavyopenda kufanikiwa vivyo hivyo usichukie kuona mwenzako amefanikiwa.
Lakini Jambo hili linaweza kutoka ndani yetu kwa njia tatu. Ya kwanza ni kujazwa Roho Mtakatifu. Kwasababu tunda mojawapo la Roho Mtakatifu ni upendo (Wagalatia 5:22). Hivyo unapokuwa mwombaji sana, hususani wa “masaa” sio dakika, unajazwa Roho Mtakatifu vema. Na matokeo yake ni kuwa urahisi wa kuudhihirisha upendo unakuja.
Lakini hilo peke yake halitoshi, unapaswa uambatanishe na usomaji wa Neno kila siku. Neno ni njia nyingine ya Roho Mtakatifu kukukumbusha, yale unayopaswa kufanya, kwamfano ukidhihirisha hasira ukisoma Neno utajifunza uvumilivu, utajifunza unyenyekevu, kuachia, na madhara ya kutokusamehe. Hivyo litakufanya uweze kurejea kwenye mstari haraka pale unapokaribia kuteleza. Usipuuzie kusoma Neno kila siku.
Tatu, ni kutendea kazi. Lazima ujiwekee malengo. Kwasababu ukiwa mwombaji tu, na msomaji peke yake bado haitakusaidia sana , kama huna mikakati ya kukifanyia kazi. Ndio maana hapo anasema iweni na JUHUDI nyingi katika kupendana,.Juhudi ni lazima yaani unaanza kuchukua hatua ya kushindana na vipinga-upendo, na hapo hapo utaanza kuona, wepesi umekuja ndani yako,
Sisi kama watoto wa Mungu, tumeagizwa tukue kila siku kuufikia upendo wa ki-Mungu ndani yetu. Ndio ukomavu wetu na kilele cha imani yetu. Kwasababu hii ndio dawa ya dhambi zote.(2Petro 1:5-11)
Bwana atuongezee neema.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
Malaika watakatifu waliopo mbinguni, wanaompa Mungu utukufu usiku na mchana, ni WAALIMU wazuri wa SIFA, na KWAYA kwetu!.. Hao wamewekwa ili kutufundisha sisi namna ya kumwimbia Mungu katika viwango vya kimbinguni. Huenda wasitufundishe namna ya kuhubiri, lakini katika kusifa, wanayo mafunzo kwaajili yetu.
> FUNZO LA KWANZA: Wanajisitiri!.
Malaika wa Sifa, (yaani Maserafi na Makerubi) sehemu kubwa ya mbawa walizopewa wanazitumia kujisitiri.. na wanajisitiri kuanzia kichwani mpaka miguuni…wanaposimama mbele za MUNGU KUMPA UTUKUFU..
Isaya 6:1“Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; KWA MAWILI ALIFUNIKA USO WAKE, NA KWA MAWILI ALIFUNIKA MIGUU YAKE, NA KWA MAWILI ALIRUKA”
Ikimaanisha kuwa kabla ya kupeleka sifa mbele za MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi, kigezo cha kwanza ni KUJISITIRI!!. Lakini leo hii watu watasimama mbele za MUNGU kumwabudu na kumsifu, vifua vikiwa wazi, mgongo ukiwa wazi, mapaja yakiwa wazi, mauongo yakiwa wazi..na wanawake vichwa vikiwa wazi..
Swali la kujiuliza je ni nani amewafundisha hayo????.. kuabudu, na kusifu wakiwa nusu uchi, je wamefundishwa na nani?..na Malaika watakatifu wanaomwimbia Mungu au nani?..jibu rahisi ni kwamba wamefundishwa na shetani, na wanayempa sifa si MUNGU wa Mbinguni bali ni shetani wa duniani na kuzimu!.
> FUNZO LA PILI: Wanahubiri utakatifu.
Malaika wa Sifa mbinguni, (Maserafi na Makerubi) wanaonekana “wakiitana” (maana yake wakiambiana) Mtakatifu…Mtakatifu… Mtakatifu…
Na zingatia hili: si kwamba walikuwa wanamwambia Mungu, kwamba ni Mtakatifu!!.. la! Walikuwa wanaambiana wao!.. maana yake wanakumbushana wao kwa wao!, wanajitangazia na kuwatangazia wengine kuwa Bwana ni mtakatifu, hivyo “kila mmoja adumu katika huo utakatifu”..kwasababu Mungu ni mtakatifu na hakai katika uchafu..
Ufunuo 6:3 “Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake”.
Huo ndio wimbo wa MALAIKA mbinguni usiku na mchana!!… UTAKATIFU, UTAKATIFU, UTAKATIFU…
Na ndizo zinazopasa kuwa NYIMBO za watakatifu waliopo duniani… Sio kumwambia Mungu MTAKATIFU!!, Kana kwamba tunampa taarifa asiyoijua!!… yeye tayari ni mtakatifu na atabaki kuwa hivyo daima… bali tunapaswa tujikumbushe na kujitangazia sisi kuwa MUNGU NI MTAKATIFU, NA HIVYO TUZIDI KUJITAKASA… SIFA ZA NAMNA HIYO NDIZO ZINAZOMPENDEZA MUNGU!!..
Na sio mtu unaimba huku una mambo mengine ya kando kando!!.. sio unaimba huku unaishi na mke/mume ambaye si wako, sio unaabudu na kuimba kwaya huku ni mzinzi na mwabudu sanamu na unafanya mambo mengine yaliyo machukizo.
Neno la Mungu linasema pasipo huo utakatifu, hakuna mtu atakayemwona MUNGU…
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.
Nyimbo au Mahubiri yasiyohubiri utakatifu ni “Ngojera za ibilisi:”.. zinazotoa thawabu za kishetani, haihitaji kuwa mchawi ndio uwe wa shetani… kumwimbia tu ibilisi tayari wewe ni wake!..kuhubiri huku unasifia na kuzitenda dhambi wewe ni wa shetani.
Kama una karama ya uimbaji acha usanii, kazi ya MUNGU lebo!!, si brand! Ni huduma..kwahiyo usijitengeneze na kuwa mfano wa wasanii wa kidunia ambao wamepewa lebo na brandy na shetani ili wafanye mapenzi yake. (Hao wanahitaji kusaidiwa waokoke, na sio kuigwa).
Ukiamua kumwimbia MTAKATIFU aliye juu, VAA NGUO KAMILI!!!, HUBIRI UTAKATIFU, ISHI UTAKATIFU..
BWANA ATUSAIDIE!
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)
MAKABURI YAKAFUNUKA; IKAINUKA MIILI MINGI YA WATAKATIFU WALIOLALA;
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
TAFUTA KWA BIDII KUWA MTAKATIFU.
Jibu: Turejee..
Yohana 12:3 “Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya NARDO SAFI yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.
4 Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema,
5 Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa DINARI MIA TATU, wakapewa maskini”
“Nardo” ni jamii ya mmea mdogo ujulikanao kama “Nardostachys”. Mmea huu hutoa maua madogo ya rangi ya “Pinki” (Tazama picha juu), na vijimatunda vidogo vyeusi ambavyo ndivyo chanzo cha mafuta aina ya “Nardo” yanayotumika kutengenezea madawa ya asili pamoja na marhamu (yaani Perfumes/pafyumu) iliyo ya gharama kubwa kuliko nyingine nyingi.
Pafyumu iliyotengenezwa kwa “Nardo”, ilikuwa ni ya gharama kubwa na hata sasa ni ya gharama kubwa kutokana na upatikanani wa mimea hiyo.
Mimea ya Nardostachy, inapatikana katika safu za milima ya Himalaya, iliyopo nchini Nepali, na sehemu chache za “nchi ya India” pamoja na “Uchina”. Na inamea kuanzia kwenye kimo cha Mita 3,000 mpaka mita 5,000 kutoka katika usawa wa bahari (Mita 5,000 ni karibia na kimo cha Mlima Kilimanjaro).. Hivyo upatikanaji wake ni mgumu sana, kutokana na sehemu chache unazomea na kimo unapopatikana!.
Kutokana na sababu hizo, ndizo zinazoifanya Marhamu ya Nardo kuwa ya gharama. Mpaka hapo tutakuwa tumeshafahamu kuwa ile Marhamu yule mwanamke aliyompaka Bwana iliagizwa kutoka mbali sana (maana yake nje ya Israeli) na ilikuwa ya gharama sana… Dinari 300 ni sawa na shilingi Milioni 6 za kitanzania.
Mistari mingine inayozungumzia Marhamu ya Nardo ni pamoja na Wimbo ulio bora 1:12, na 4:13-14
Sasa kufahamu kwa urefu ni nini tunajifunza kupitia tukio la mwanamke yule kukivunja kile kibweta fungua hapa >>AKAKIVUNJA KIBWETA AKAIMIMINA KICHWANI PAKE.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
AKAZIDI KUENDELEA KATIKA HEKIMA NA KIMO.
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.
Jibu: Turejee,
Wimbo 2:9 “Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala. Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu, Achungulia dirishani, atazama kimiani”.
“Kimiami” ni dirisha kubwa lililo katika “ghorofa”..
Madirisha makubwa yaliyo katika maghorofa tofauti na yale yaliyo katika nyumba za chini ndiyo yaliyoitwa “kimiami”.
Mfano wa dirisha la Kimiami ni lile ambalo mfalme Ahazia aliloanguka na kuugua..
2Wafalme 1:2 “Na Ahazia AKAANGUKA KATIKA DIRISHA la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu”.
Na lile ambalo Yezebeli alianguka, baada ya kuangushwa na wale matowashi..
2Wafalme 9:30 “Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.
31 Hata Yehu alipoingia lango la mji, alisema, Je! Ni amani, Ewe Zimri, mwenye kumwua bwana wako? 32 AKAINUA USO WAKE KULIELEKEA DIRISHA, akasema, Aliye upande wangu ni nani? Matowashi wawili watatu wakachungulia.
33 Akasema, Mtupeni chini. Basi wakamtupa chini; na damu yake ikamwagika nyingine juu ya ukuta, na nyingine juu ya farasi, naye akamkanyaga-kanyaga”.
Tazama pia shubaka hapa >>>Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
Swali: Je ni kwamba Mungu anafurahia Mauti ya watu wake mpaka aseme hivyo?
Jibu: Turejee mstari huo…
Zaburi 116:15 “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake”
Sasa ili tupate vizuri maana ya huu mstari hebu tuweke msingi kwa kusoma tena mstari ufuatao…
Ezekieli 33:11 “Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, SIKUFURAHII KUFA KWAKE MTU MWOVU; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?”
Kama Bwana hakufurahii kufa kwake MTU MWOVU, basi kinyume chake ni kweli!! kuwa “KUFA KWAKE MTU MWENYE HAKI ikiwa amemaliza kusudi lake duniani NI JAMBO LINALOMPENDEZA MUNGU”… Na Ndio hapo kwenye Zaburi 116:15 anasema “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake”.
Sasa kwanini MAUTI YA WENYE HAKI NI YA THAMANI MACHONI PA MUNGU?
1. DUNIANI NI MAHALI PA DHIKI.
Hii ndio sababu KUU..Duniani si mahali pa raha kwa “Wanaomcha Mungu”.. Kwa wengine wasiomcha Mungu panaweza kuwa mahali pao kwa raha ya kitambo..lakini kwa wacha Mungu si sehemu ya faraja hata kidogo..
Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. ULIMWENGUNI MNAYO DHIKI; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.
Kutokana na kwamba ulimwenguni ni mahali pa dhiki, na tena pa mapito, ni mahali pa kutaabika kupambana na dhambi na kutaabika kuhubiri injili.. hivyo MAUTI ni sehemu ya mapumziko kwa wanaomcha Mungu kutokana na taabu hizo za ulimwengu…ndivyo maandiko yanavyosema..
Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA TANGU SASA. NAAM, ASEMA ROHO, WAPATE KUPUMZIKA BAADA YA TAABU ZAO; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
Hiyo ndiyo sababu kwanini KIFO ni sehemu bora kwa WANAOMCHA MUNGU KULIKO KUENDELEA KUSHI DUNIANI. Na Mkristo yeyote yule wa kweli, ni lazima atamani kuondoka katika haya maisha kuliko kuendelea kubaki hapa!!, ni lazima atamani kila siku ile siku ya unyakuo ifike, au siku ya kulala kwake (kufa) ifike akamwone Bwana.
Kitu pekee ambacho kinapaswa kutufanya tuendelee kutaka kubaki duniani ni “kuimaliza kazi yake”, (maana yake tusiondoke kabla ya kuimaliza kazi yake aliyotuitia, kwani kuna hatari ya kufa bila kuifanya kazi yake au kuimaliza).. na hakuna sababu nyingine tofauti na hiyo…
Ukiona unatamani uendelee kubaki duniani, ili uwe milionea, au ili uendeshe na kumiliki magari, au utengeneze majumba kwa fahari yako, kuna shida katika Imani yako!..(Ni muhimu kujipambanua upya).. wewe utakuwa wenyeji wako ni hapa duniani, sio mbinguni.
Walio wa mbinguni wanatamani ya mbinguni, na walio waduniani wanatamani, na kuwekeza, na kusifia vya duniani…
Wafilipi 3:20 “Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo”
Soma pia 1 Petro 2:11 utaona jambo hilo, hivyo jihakiki ni nini kinakupa sababu ya wewe kuendelea kubaki hapa duniani?..ni vitu vya dunia hii au vile vijavyo?.
Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho aliandikia kuwa “kuishi kwake ni Kristo na kufa ni faida”,..Maana yake kusudi lake kuu la kuendelea kubaki duniani ni Kristo (yaani kufanya kazi Kristo aliyomuitia na kuimaliza)..Nje na hapo kufa ni FAIDA KUU!
Wafilipi 1:21 “Kwa maana kwangu mimi kuishi ni KRISTO, NA KUFA NI FAIDA.
22 Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui.
23 Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana;
24 bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu”.
Hapo anasema kudumu katika mwili (yaani kuendelea kuishi) kwahitajika kwaajili yao, na si kwaajili yake (maana yake kwaajili ya kuwahubiria wao injili).
Je mimi na wewe kubaki kwetu katika mwili kwahitajika kwaajili ya nini??…je ni kwaajili ya matumbo yetu, na tamaa, na anasa au kwaajili ya Bwana?..
Kumbuka pia, ni hasara kubwa sana kufa katika dhambi!.. na hakuna maombi yoyote ya kumtoa mtu aliyekufa kutoka katika mateso ya moto wa jehanamu na kumingiza paradiso. (Hayo maombi hayapo usidanganyike).
Hakuna maombi yoyote ya Mchungaji, au Askofu, au Nabii, au Mtume, au Papa, au Padre, au Kadinali, au Mwalimu, au Rabi, au Mwinjilisti, au Kuhani au Malaika wa mbinguni…. yatakayomtoa mtu kwenye mateso ya moto wa jehanamu na kumwamisha kumwingiza peponi, Mtu akifa katika dhambi!, habari yake ndio imeishia hapo..
Bwana YESU Kwa kinywa chake mwenyewe ametupa tahadhari hiyo katika kitabu cha Yohana..
Yohana 8:24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba MTAKUFA KATIKA DHAMBI ZENU; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, MTAKUFA KATIKA DHAMBI ZENU”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?
WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU
Amosi 5:23 “Niondoleeni KELELE ZA NYIMBO ZENU; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu”.
Je ni kwamba Mungu wetu hapendezwi na nyimbo tunazomwimbia??
Jibu ni la! Yeye anapendezwa na nyimbo na tena anaketi katika SIFA.
Zaburi 22:3 “Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli”.
Lakini kwanini aseme “niondoleeni kelele za nyimbo zenu?”… Ni wazi kuwa kuna nyimbo ambazo kwa Mungu ni kama kelele.
Sasa ni aina gani za nyimbo ambazo kwa Mungu ni kelele?.
1. NYIMBO ZA UNAFIKI.
Nyimbo za kinafiki ni zile mtu anazoimba kwa kupaza sauti, lakini maisha yake hayaendani na kile anachokiimba, kuanzia, uzungumzaji, uvaaji, utendaji na maisha yake yake siri. Mtu mwenye tabia hiyo halafu akasimama na kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu, iwe ni nyimbo alizozitunga yeye, au za mwingine, mtu huyo anapiga kelele mbele za Mungu na hivyo anafanya dhambi.
2. NYIMBO ZENYE MIDUNDO YA KIDUNIA.
Kuna nyimbo ambazo zinafanana sana na za kidunia, kiasi kwamba mtu akisikiliza anafananisha na nyimbo Fulani ya kidunia ambayo alishawahi kuisikia mahali fulani. Nyimbo za namna hiyo ni kelele, na si kelele tu, bali pia ni machukizo… mfano wa hizo ni nyimbo aina ya rege, rap, pop, taarabu na nyingine zinazofanana na hizo, Nyimbo za namna hii zinajulikana kama nyimbo za upuuzi (Amosi 6:5). Hivyo wakristo hatupaswi kutumia midundo hiyo kumwimbia MUNGU.
3. NYIMBO ZINAZOSHIRIKISHA WASANII WA KIDUNIA.
Wasanii wa kidunia ni watu wanaoimba nyimbo za zinazotukuza na kusifia mambo ya ulimwengu huu, na ulimwengu upo chini ya shetani, sasa mtu anayewashirikisha waimbaji hao wa kidunia, waliozoea kumwimbia shetani, kisha wakapewa mashairi ya kumsifu Mungu pamoja na watu wa kiMungu, hizo ni kelele na machukizo mbele za Mungu, haijalishi nyimbo hiyo itakuwa na beti nzuri kiasi gani na ujumbe mzuri kiasi gani, au zenye kumsifia MUNGU kwa kiasi gani, bado ni kelele mbele za Mungu na hazina matunda yoyote.
Nyimbo zenye kumtukuza Mungu ni zile zilizobeba ushuhuda wa Neno kuanzia kwa MWIMBAJI, beti na mdundo. Na zinapoimbwa zinamtukuza Mungu na kuwabariki wasikiao.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.
Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?
Fahamu maana 1Wakorintho 14:20 “Ndugu zangu msiwe watoto katika akili zenu;
Jibu: Turejee,
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, UCHAFU, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Dhambi zote ni “uchafu” lakini zipo dhambi ambazo ni “chafu Zaidi”, hizo ndizo zinazoitwa “Uchafu” Mfano wa hizo ni zile zilizotajwa katika Mambo ya Walawi 18 na 20…(Dhambi za kulala na mnyama na ndugu wa karibu).
Walawi 18:23 “Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; NI UCHAFUKO”.
Walawi 20:12 “Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo UCHAFUKO; damu yao itakuwa juu yao”.
Utaona dhambi nyingine zimetajwa tu kama ni “Machukizo” mfano lakini hizi zimetajwa kama “Uchafuko” maana yake zimezidi machukizo.. Ni uchafu mkuu mbele za Mungu.
Kulala na Mnyama, ni uchafu, vile vile kulala na mama mkwe au baba mkwe ni uchafu..na wachafu wote hawataurithi uzima wa milele sawasawa na maandiko hayo.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni ipi?
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
Ninyi ni chumvi ya dunia, Andiko hilo lina maana gani?
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Swali: Huyu Tirano tunayemsoma katika Matendo 19:9 alikuwa ni nani, na darasa lake lilikuwaje?
Jibu: Tuanzie kusoma mstari ule wa 8 hadi ule wa 11 ili tuweze kuelewe vizuri..
Matendo 19:8 “Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa MUDA WA MIEZI MITATU, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.
9 Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika DARASA YA MTU MMOJA, JINA LAKE TIRANO.
10 Mambo haya yakaendelea kwa MUDA WA MIAKA MIWILI, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.
11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida”.
Baada ya Paulo kuingia Efeso, aliingia katika sinagogi moja la wayahudi ili kuhubiri habari za BWANA YESU, na wachache walioamini na kuitii injili, lakini wengi walikaidi na hata kuitukana kabisa injili mbele ya watu wote..
Mtume Paulo alipoona kuwa wameikataa injili, aliliacha sinagogi hilo (la wayahudi) ambalo pengine lingekuwa ndio sehemu bora kwa watu kujifunzia habari za Bwana YESU, lakini kutokana na ubishi na ugumu wa watu wa sinagogi (wayahudi).. Paulo aliondoka pamoja na wale wachache walioamini (wanafunzi)..na kuhamia kwenye darasa lingine la mtu mmoja wa mataifa aliyeitwa TIRANO. (na kipindi ambacho Paulo alihudumu katika Sinagogi la wayahudi mpaka alipoondoka na kuhamia kwenye darasa la Tirano ni muda wa miezi 3)
Kumbuka hapo biblia inaposema “darasa la Tirano” inamaanisha “jengo” lililokuwa maalumu kwaajili ya kufundishia la mtu aliyeitwa Tirano.
Sasa swali huyu Tirano alikuwa nani?
Biblia haijaeleza kwa kina huyu Tirano alikuwa ni nani, lakini ni wazi kuwa alikuwa ni mmoja wayunani aliyeamini injili na hivyo akatoa darasa lake hilo liweze kutumika kama mahali pa kufundishia watu injili.. Kama tu Petro alivyoalikwa nyumbani kwa Simoni mtengeneza ngozi kule Kaisaria (Matendo 9:43).
Na mpaka atoe darasa hilo, maana yake hapo kwanza inawezekana alikuwa ni mwalimu wa Falsafa za Kiyunani (kwani wayunani walikuwa ni watu wasomi na wenye kutafuta elimu sana).
Na baada ya Paulo kuhama kutoka kwenye lile Sinagogi na kuhamia kwenye darasa hilo la Tirano, injili ilipata mafanikio makubwa sana, kwani baada ya miaka miwili tu, Watu wote wa Asia waliisikia injili na kuitii..
Matendo 19:10 “Mambo haya yakaendelea kwa MUDA WA MIAKA MIWILI, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.
11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida”.
Ikifunua kuwa kuna mambo au mifumo ndani ya masinagogi (au madhehebu) ambayo inazuia kutembea kwa Roho Mtakatifu, zipo tabia ambazo zinazuia injili kusambaa, ipo mienendo inayokinzana na nguvu za Roho Mtakatifu kutembea.. na mojawapo ya hiyo ni tabia ya kupingana na Neno la Mungu (kama ilivyokuwa kwa hawa wayahudi ndani ya Sinagogi)..walikuwa wanashindana na Paulo kutwa kuchwa.
Walikuwa wanaikejeli injili, hata kama wanaona kinachohubiriwa ni kweli kabisa..
Na hata katika madhehebu na makanisa leo ni hivyo hivyo, utakuta mtu au kiongozi anaweza kuiona kweli lakini bado akashindana nayo na kuipinga!..Kiongozi anaweza kuona jambo Fulani sio sawa lakini bado akalipalilia, na kushindana na ile kweli, watu wanaweza kufunuliwa maandiko lakini bado wakawa hawabadiliki wapo vile vile, bado maisha yao ni yale yale NA KWA MATENDO YAO WANAITUKANA INJILI (ingawa midomo yao inakiri).. mambo hayo yanazuia injili kusambaa na kutembea kwa Roho Mtakatifu.
Bwana atusaidie tuzidi kutembea katika kweli yake.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)
TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?
INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?
Sinagogi kufumakana maana yake nini? (Matendo 13:43).
Swali: Mathayo 21:19 inasema “mtini ulinyauka mara (maana yake muda ule ule uliolaaniwa)”.. lakini katika Marko 11:20 biblia inasema “mtini ulinyauka kesho yake, na sio siku ile ile ulipolaaniwa”.. Je mwandishi yupi yupo sahihi na yupi hayupo sahihi?.
Jibu: Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa biblia haijichanganyi mahali popote na wala haijawahi kujichanganya mahali popote, isipokuwa pambanuzi zetu, fahamu zetu na tafakari zetu ndizo zinazojichanganya pale tunaposoma pasipo kutafakari kwa kina.
Sasa turejee habari hizo moja moja na kisha tuzitafakari tena..
Mathayo 21:18 “Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa.
19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. MTINI UKANYAUKA MARA.
20 WANAFUNZI WALIPOONA, WALISTAAJABU, WAKISEMA, JINSI GANI MTINI UMENYAUKA MARA?
21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka”.
Hapa tunaona mtini ulinyauka “Mara”.. Lakini turejea kitabu cha Marko ni kama tunasoma habari tofauti…
Marko 11:12 “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.
13 Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.
14 Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”
Turuke mpaka mstari wa 19-23..
“19 Na kulipokuwa jioni alitoka mjini.
20 NA ASUBUHI WALIPOKUWA WAKIPITA, WALIUONA ULE MTINI UMENYAUKA TOKA SHINANI.
21 PETRO AKAKUMBUKA HABARI YAKE, AKAMWAMBIA, RABI, TAZAMA, MTINI ULIOULAANI UMENYAUKA.
22 Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu.
23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake”
Hapa tunasoma “MTINI ULINYAUKA SIKU INAYOFUATA na si muda ule ule”.. Sasa swali? habari ipi ni sahihi kati ya hizo mbili?
Jibu ni kwamba habari zote ni sahihi, waandishi wote wote wapo sahihi, hakuna hata mmoja aliye mwongo..…
Sasa kwa ufupi ni kwamba mtini haukunyauka muda ule ule Bwana alipoulaani, bali mpaka kufikia kesho yake ndio ulikuwa umekwisha nyauka kabisa..…Sasa swali, kama ni hivyo kwanini Mathayo aseme ulinyauka MARA?…
Jibu la swali hili ni kwamba…si kila mahali panapotumika neno “Mara” panamaanisha “dakika ile ile, au sekunde ile ile, au muda ule”… Hapana!.. Bali neno “Mara” linaweza kumaanisha kipindi fulani cha muda/wakati… ili tuelewe vizuri, tusome habari ifuatayo..
Marko 1:26 “Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka.
27 Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii!
28 Habari zake ZIKAENEA MARA KOTEKOTE KATIKA NCHI ZOTE kandokando ya Galilaya”
Hapo biblia inasema habari za Bwana YESU zikaenena “MARA KOTE KOTE KATIKA NCHI ZOTE”… Sasa swali??…Je zilienea sekunde ile ile, au muda ule ule, aliotoa Pepo?..Jibu ni la!...bali ni baada ya kipindi Fulani cha wakati labda masaa kadhaa mbele au siku moja mbele au siku kadhaa???… Kwani isingewezekana ndani ya sekunde ile ile muujiza ulipotokea, habari zifike Galilaya yote ambayo ilikuwa na vimiji vidogo vidogo Zaidi ya 400 kulingana na historia na miji hiyo ikiwemo Nazareti, Kapernaumu, korazini na Bethasaida, Na tena si Galilaya tu!, na hata nje ya Galilaya, maana hapo anasema taarifa zilifika miji yote ya kandokando ya Galilaya (maana yake nje ya Galilaya).
Kwa mantiki hiyo basi tutakuwa tumeelewa kuwa Mathayo alipotumia neno “kunyauka Mara” hakumaanisha sekunde ile ile, bali alimaanisha kuwa ni kwa kipindi Fulani cha masaa kadhaa, (haraka sana, ambako sio kwa kawaida kwa desturi ya miti kunyauka)… kwa maana kikawaida mpaka mti unyauke unachukua siku kadhaa, na huo ni kama umekatwa…sasa ule haukuonekana kama umekatwa, lakini ulinyauka kabisa (Hivyo ni muujiza).
Kwahiyo kwa hitimisho ni kuwa mtini mpaka kufikia asubuhi ndio ulionyesha kunyauka na wanafunzi walishagaa hiyo asuhubi hivyo biblia haijichanganyi mahali popote..
Je unaliamini Neno la Mungu?.. Na je umeokoka?…Kama bado ni nini kinachokusubirisha usimpokee Bwana YESU??.. Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na YESU yu mlangoni.. hivyo usiyachezee maisha yako wala mtu mwingine yoyote asiyachezee..
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.