Mata ni kitu gani na imebeba ujumbe gani kiroho?
Jibu: Turejee,
Mwanzo 27:2 “Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.
3 Basi, nakuomba, chukua MATA yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; 4 ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa”.
“Mata” Ni jina jingine la “Silaha”. Kwahiyo badala ya kutumia neno “silaha” ni sahihi pia kutumia neno “Mata”.
Kwahiyo mstari huo wa tatu (3) ni sahihi kuuweka hivi,… “chukua SILAHA yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo ”
Na silaha hiyo inaweza kuwa mkuki, mshale au upanga, lakini katika andiko hilo silaha (Mata), iliyomaanishwa pale ni “Mshale”. Na kwanini ni mshale na si upanga wala mkuki?.. ni kwasababu kuna Podo imetajwa pale na upinde..
Maana yake huwezi kubeba upanga na upinde bila mshale, hivyo ni wazi kuwa Mata iliyomaanishwa pale ni mshale, kwasababu kuna upinde na Podo.
Sasa kwa maarifa kuhusu “Podo” na ufunuo wake kiroho waweza fungua hapa >>> Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?
Sasa hizi zote ni silaha za mwili, lakini biblia inatufundisha kuwa zipo silaha za roho ambazo kila mkristo ni lazima azivae, na silaha hizo tunazisoma katika kitabu cha Waefeso 6:10-18, ambazo ni Chapeo ya Wokovu, Dirii ya Haki, Ngao ya Imani, Kweli, Upanga wa Roho, na Utayari miguuni pamoja na sala na maombi.
Na kwa silaha hizo pekee ndio tutaweza kumshinda adui yetu shetani, kwa mapana kuhusiana na silaha hizi jinsi ya kuvizaa na namna zinavyotenda kazi fungua hapa >>>MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.
Nini maana ya Mithali 21:1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana;
Swali: Biblia ina maana gani kusema Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa? Je hiki kiti cha Musa ndio kipi?
Jibu: Turejee,
Mathayo 23:2 “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa”
“Kiti cha Musa” maana yake ni “Nafasi ya Musa”.. Leo hii tukisema mtu kaketi katika kiti cha Uraisi, maana yake ni kuwa “kachukua nafasi ya Uraisi”.
Sasa Musa alikuwa na nafasi gani?
Musa alikuwa na nafasi kuu mbili (2) mbele za wana wa Israeli.
1) UALIMU.
Mtu wa Kwanza kuwafundisha wana wa Israeli HUKUMU, AMRI NA SHERIA za Mungu alikuwa ni MUSA.
Kumbukumbu 4: 14 “Bwana akaniamuru wakati ule NIWAFUNDISHE maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.
15 Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile Bwana aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;
16 msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke”.
Na mahubiri yake yaliendelea kuwa msingi wa marejeo kwa vizazi na vizazi mbeleni.
2) UONGOZI.
Hii ni nafasi ya pili aliyokuwa nayo Musa mbele ya wana wa Israeli:
Maandiko yanasema Mungu alimfanya Musa kuwa “Mkuu sana” mbele ya Misri na mbele ya wana wa Israeli. Kiasi kwamba maamuzi ya mwisho yalikuwa yanatoka kwake, kwa lugha nyepesi alikuwa ni kama Mfalme.
Kutoka 11:3 “…Zaidi ya hayo, huyo Musa ALIKUWA NI MKUU SANA katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake”.
Soma pia Kutoka 18:13-24, utaona nafasi ya Musa katika kuwaamua Israeli.
Sasa baada ya Musa kuondoka (yaani kufa), Mafarisayo na Waandishi wakajiweka katika nafasi yake, maana yake wao ndio wakawa WAALIMU kama alivyokuwa Musa, na pia wakajiweka kuwa VIONGOZI kama alivyoukwa Musa, kiasi kwamba maamuzi ya mwisho yalikuwa yanatoka kwao.
Lakini ni heri kama wangekuwa wameketi kwenye nafasi hiyo ya Musa, na wakawa kama Musa..(yaani wacha Mungu kama Musa, au wapole kama Musa)..
Lakini wao walikuwa ni kinyume chake, walikuwa wanawatawala watu na kuwahukumu kwa sheria ya Musa lakini wao wenyewe ni wanafki mioyoni mwao.. mioyo yao ilikuwa ipo mbali na Mungu ingawa kwa nje wanaonekana ni waamuzi wazuri na viongozi wazuri wenye kusifiwa, lakini ndani yao wamejaa unafiki!.
Na Bwana YESU anatuonya tusiwe kama wao..
Mathayo 23:2 “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa”
3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi
4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.
5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,
7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.
8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.
9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.
10 Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.
11 NAYE ALIYE MKUBWA WENU ATAKUWA MTUMISHI WENU.
12 Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa”.
Je YESU KRISTO ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako?..Je una uhakika jina lako lipo katika kitabu cha uzima?.. Kama bado YESU hayupo maishani mwako ni heri ukampokea leo, maana saa ya wokovu na wakati uliokubali ni sasa.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Jibu: Turejee,
Wimbo 8:6 “Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni MIALI YA YAHU”.
“YAHU” ni jina lingine la “YAHWE” ambalo ndilo “YEHOVA”.
Kutoka 6:2 “Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;
3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao”.
Kwahiyo YAHU, YAHWE na YEHOVA ni jina Moja!
Lakini hapo katika Wimbo 8:6 maandiko yanasema kuwa “upendo una nguvu kama mauti”.. maana yake kama vile mauti ilivyo na nguvu kiasi kwamba wanaokufa ni ngumu kurudia uzima! Vile vile Upendo wa Mungu kwetu ni mkuu kiasi kwamba akitupenda ametupenda!, hakuna wakati atatuchukia, anaweza asipendezwe na sisi lakini si kutuchukia!.
Warumi 8:35 “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?………
38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Lakini pia anasema wivu ni mkali kuliko Ahera..Ahera ni “Kaburi”, Kwa urefu Zaidi fungua hapa >>>Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.
Na miali yake ni miali ya YAHU. Maana yake ni kuwa Mungu ana upendo lakini pia anawivu, huwezi kamwe kutanganisha vitu hivi viwili, UPENDO na WIVU.
Kwahiyo kama Mungu ametupenda, basi hapendi kuona tunaabudu miungu mingine, tukifanya hivyo tunamtia yeye wivu, umbao unaweza kutupeleka kaburini (Ahera).
Kutoka 20:3 “Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, NI MUNGU MWENYE WIVU; NAWAPATILIZA WANA MAOVU YA BABA ZAO, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE CHA WANICHUKIAO,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.
YAHU atusaidie tusimtie Wivu, lakini tumpende, na vile vile upendo wake utubidiishe katika kuyafanya mapenzi yake.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Maran atha.
Mafundisho Mengine:
Wivu ni nini na kuna aina ngapi za Wivu?
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
IJUE HEKIMA YA MUNGU KATIKA KUKUINUA KIMAISHA.
WEKA KUMBUKUMBU YA MAMBO BWANA ANAYOKUFANYIA KWASABABU YATAKUFAA MBELENI.
Falaki ni nini katika biblia?
Jibu: Turejee,
Isaya 47:12 “Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda.
13 Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na WASIMAME HAO WAJUAO FALAKI, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata”.
“Falaki” ni “elimu ya nyota na sayari na jua”.
Wanaofanya Falaki, wanaamini kuwa “mpangilio wa nyota, mwezi na jua na sayari angani, unaathiri tabia ya nchi na tabia ya mtu/watu”. Jambo ambalo kwa sehemu moja ni kweli na sehemu nyingine uongo!.
Ni kweli Mpangilio wa Jua na mwezi, unaweza kuathiri tabia ya nchi, kama vile vipindi vya mvua, kiangazi, au kipupwe….ipo miezi ambayo mvua inanyesha, na miezi ambayo mvua hainyeshi, ipo miezi ya kiangazi na miezi ya kipupwe…Majira ya mwezi wa 6 na 7 ni Kipindi ambacho jua linakuwa mbali na dunia na kweli nchi inaathirika na baridi kali, katika ukanda wa kusini wa dunia.
Vile vile tabia za mimea zinaathiriwa na majira na nyakati, yanayotokana na mpangilio wa mwezi na jua angani, mfano tabia za miembe kuzaa maembe zinaathiriwa na mwezi wa 12, kwamba yanapofika majira ya mwezi huo wa 12 mpaka wa 1 basi miti yote ya miembe inazaa sana, tofauti na kipindi kingine chote (kwahiyo kwa sehemu ni kweli).
Sasa kwa mantiki hiyo wana-falaki wanaamini kuwa kama mpangilio wa jua, mwezi na nyota angani unaweza kuathiri mazingira na hali ya hewa, basi vile vile mpangilio huo huo unaweza kuathiri tabia za watu, na hisia zao, na maamuzi yao na hata hatima yao!.
Kwamba kila tarehe na mwezi unabeba matukio yake kulingana na mtu na mtu, na pia kulingana na tarehe aliyozaliwa, vile vile mpangilio wa nyota na mwezi unaweza kuelezea ni kitu gani mtu atafanya, au atakitenda, au kitampata, vile vile ni bahati gani ipo mbele yake au hatari gani inamkabili.
Kwahiyo wote waliohitaji kujua mambo yatakayowapata mbeleni waliwatafuta hawa wana-Falaki, au kwa lugha nyingine wanajimu kujua hatima zao.
Lakini swali ni je! Elimu hii ina ukweli wowote na je wakristo ni sahihi kuitafuta, ili kujua hatima zetu kupitia falaki?
Jibu ni LA! Elimu hii haina ukweli wowote, mpangilio wa sayari na nyota, na mwezi hauwezi kuelezea tabia, hisia, maamuzi au hatima ya Mwanadamu!…mpangilio huo unaweza kufaa katika utabiri wa hali ya hewa na misimu ya kupanda na kuvuna (tena kwa sehemu ndogo) lakini hauwezi kutabiri maisha ya mtu.
Maisha ya mtu hayatabiriwi wala kusomwa kwa kutazama jua, au mwezi au nyota au sayari, kama ndivyo kulikuwa hakuna haja ya Kristo kuja, au hata kama angekuja basi angetuhubiria sana hiyo elimu, bali maisha ya mtu yanatabiriwa kwa KULITAZAMA NENO LA MUNGU peke yake!.
Ukitaka kujua kesho yako itakuwaje, isome biblia, itakuambia sio tu kesho utakuwa wapi, bali MILELE UTAKUWA WAPI!!!.
Utauliza vipi wale Mamajusi, mbona walioiona nyota ya Bwana YESU kutoka mashariki?.
Mungu alipenda kutumia ishara ya nyota kuelekeza utukufu wa mwanae alipozaliwa, lakini hakuwa anahubiri elimu ya nyota pale!, ni sawa na alivyotumia ishara ya Nguzo ya wingu au nguzo ya moto juu ya wana wa Israeli walipokuwa jangwani,.. ilikuwa ni kwa lengo la kuelekeza utukufu wa wana wake mahali walipo, lakini hakuwa anahubiri elimu za mawingu na moto, kwamba zikasomwe kwa bidii ili kuelezea utukufu juu ya mtu/watu.
Vile vile leo hii shetani anapenyeza elimu hii ya Nyota(Falaki) ndani ya kanisa kwa kasi sana!. Elimu hii inatoka kwa waganga na inahamia kanisani kwa kasi sana..Watu hawasomi tena biblia wanatafuta kusomewa nyota zao! Hawaombi tena kulingana na Neno wanaombea nyota kwa kurejea elimu ya falaki.
Ndugu usidanganyike!..Elimu ya nyota (Falaki) ni elimu ya shetani asilimia mia.
Kama unataka kusafisha hatima yako itii biblia, wala usitafute maombi ya kutakasiwa nyota!, hiyo ni elimu nyingine!… Vile vile ukitaka kujua kesho yako itakuwaje kasome biblia, usitafute utabiri wa kusomewa nyota kutoka kwa yoyote yule iwe mganga au anayejiita mtumishi wa Mungu.. Biblia pekee ndiyo itakayokuonyesha tabia yako na kukupa utabiri sahihi wa maisha yako ya kesho na ya milele.
Je umemwamini Yesu?, je umebatizwa ubatizo sahihi? Je umepokea Roho Mtakatifu?.
Bwana Yesu anarudi.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?
Jibu: Tusome,
1Samweli 26:11 “Hasha! Nisiunyoshe mkono wangu juu ya masihi
12 Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile GUDULIA LA MAJI, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia”.
Gudulia ni chombo maalumu kilivyotengenezwa kwa lengo la kuhifadhia maji ya kunywa ya watu wachache, kwa lugha ya sasa hivi tunayaita “majagi”
Magudulia/majagi ya zamani yalitengenezwa kwa malighafi tofauti na ya zama hizi. Zamani majagi/magudulia waliyatengeneza kwa kutumia udongo wa (mfinyanzi tazama picha juu), lakini sasa yanayotumika mengi yao yametengenezwa kwa glasi au plastiki.(tazama picha chini).
Mistari mingine inayotaja chombo hiki (gudulia) ni pamoja na 1Wafalme 19:6, Yeremia 19:1 na Yeremia 19:10.
Je umemwamini Bwana Yesu?, je unajua kuwa tunaishi katika majira ya kurudi kwa YESU mara ya pili, na wakati wowote unyakuo wa kanisa utatokea?.
Bwana atusaidie.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
WALA HAKUACHA MTU ACHUKUE CHOMBO KATI YA HEKALU.
Ni nani aliyemshawishi Daudi akawahesabu Israeli? Ni Mungu au shetani?
Uadilifu ni neno pana linalomaanisha, nidhamu, utu, auminifu, yaani kutenda kile ambacho jamii husika inataka wewe ukitende.
Kibiblia uadilifu ni utiifu katika sheria ya Mungu. Vilevile uaminifu na nidhamu katika mambo yote ya ki-Mungu. Mtu wa namna hiyo anaitwa mwadilifu, au mcha Mungu.
Kwamfano watu ambao walikuwa waadilifu katika biblia ni kama Yusufu, Ayubu, Danieli pamoja na wengine, ambao waliweza kutembea katika sheria za Mungu bila lawama yoyote.
Baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na Neno hilo ni hivi;
2Nyakati 26:3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na miwili; na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 4 Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Amazia babaye
Zaburi 64: 10 “Mwenye haki atamfurahia Bwana na kumkimbilia, Na wote wenye moyo wa adili watajisifu”
Zaburi 112: 2 Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. 3 Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele. 4 Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki
Soma pia 2Nyakati 27:2,29:2 Zaburi 140:13.
Lakini cha kujua kuhusu tabia hii, ni kwamba Bwana Yesu alisema ni wajibu pia wa kila kiongozi wa kiroho/ Mhubiri kufundisha mafundisho ya adili, zaidi ya mafundisho ya utoaji.
Luka 11:42 Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili.
Mafundisho ya adili, ni kama vile, utakatifu, uaminifu, haki, utu wema, amani, umoja na kiasi, uvumilivu, fadhili, upole, unyenyekevu. na yote yanayofanana na hayo. Kwasababu ndicho Bwana anataka kukiona ndani ya mioyo ya watu wake, wawe waadilifu kama yeye alivyo mwadilifu (Zaburi 25:8).
Je! Wewe ni mwadilifu? Kumbuka huwezi kuwa hivyo kama upo nje ya Kristo. Yeye ndio pekee anayeweza kukupa nguvu ya kutenda mema. Hivyo ili uitwe mwadilifu sharti kwanza umpokee Yesu akuokoe, akusamehe dhambi zako. Ndipo Bwana akupe nguvu ya kumcha yeye.
Ikiwa upo tayari leo kuokoka, basi fungua hapa kwa mwongozo wa Sala ya Toba. >> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
JE KUHUDUMU KWA NYIMBO ZA INJILI KUKOJE?
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Maana ya Neno Ebenezeri ni jiwe la msaada.
Wakati ule Israeli wanamlilia Bwana awarudie, Wafilisti walipata taarifa wakakusanyika pamoja ili wawaangamize, Israeli walivyoona hivyo wakaogopa sana, wakamsihi Samweli awalilie kwa Bwana ili wasaidiwe kwasababu wanakwenda kuangamia. Na Mungu akasikia kilio chao, akawatetea, kwa kutoa ngurumo kubwa sana, zilizowadhoofisha wafilisti, hivyo wakapigwa na kuharibiwa, mpaka miji ambayo wafilisti walikuwa wameiteka ikarudishwa yote kwa Israeli. Ndipo Samweli akachukua jiwe kubwa akalisimamisha Kati ya Mispa na Sheni, akaliita Ebenezeri, akasema hata sasa Bwana ametusaidia.
1Samweli 7:12 Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri, akisema, Hata sasa Bwana ametusaidia.
Lakini la kujiuliza kwanini Samweli anyanyue jiwe, na sio kitu kingine labda nguzo au bendera? Na pia alikuwa na maana gani kusema “Hata sasa Bwana ametusaidia”? Na sio maneno mengine?
JIBU: Alinyanyua jiwe kwasababu alipata ufunuo wa aliyemsaidia, na huyo si mwingine zaidi ya Kristo ambaye ndio jiwe letu (Warumi 9:33). Alitambua ni yeye ndiye aliyewapigania vita kwa kunguruma, Kwasababu ndiye simba wa Yuda.
Lakini pia kwanini aseme “Hata sasa Bwana ametusaidia” ni kwasababu alitambua kuwa Mungu ni msaada wao sikuzote, hadi ule wakati walioufikia bado alikuwa ni msaada wao, ndio maana akasema “Hata sasa Bwana ametusaidia”, yaani sio tu jana, au zamani bali hata sasa Bwana yupo pamoja nasi.
Ikiwa na maana kuwa hata na sisi tukiwa ndani ya Kristo wakati wote atatulinda, sio jana tu peke yake, hadi leo na hata kesho. Ni furaha iliyoje kuwekwa chini ya huu mwamba Yesu Kristo?
Je! Kristo ni jiwe lako? Je! Ni Ebenezeri wako? Kama sio, embu mkaribishe leo maishani mwako akuokoe, upate uzima wa milele. Akulinde mbali na Yule mwovu. Ikiwa upo tayari kutubu na kumpokea Yesu basi fungua hapa kwa msaada wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.
BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
Neno hili utalisoma katika vifungu kadha wa kadha,
Hivi ni baadhi ya vifungu hivyo ambavyo utakutana nalo;
Mwanzo 37:6 “akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. 7 Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. 8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake”.
Walawi 23: 10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; 11 naye atautikisa mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. 12 Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.
Tafsiri ya Neno mganda, ni matita ya mazao yoyote yaliyovunwa ambayo yamefungwa pamoja. Kwamfano ngano zilipovunwa, katika mashamba, zilifungwa kwanza katika matita matita, baadaye zikakusanywa zote pamoja, ndipo zikaenda kukobolewa na kusagwa. Sasa hayo matita matita ndio huitwa miganda. (Tazama picha juu)
Kwamfano katika vifungu vifuatavyo utaelewa biblia ilimaanisha nini;
Kumbukumbu 24: 19 Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili Bwana, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.
Maana yake ni kuwa ikitokea, umeenda shambani kuvuna, ukafanikiwa kukusanya miganda kumi, sasa wakati unaondoka ukasahau mmoja, Ilikatazwa kurudi nyuma na kuuchukua, bali uuache kwa ajili ya mayatima na wageni. Kwasababu maskini waliruhusiwa kuingia kwenye mashamba kuokota vile vinavyosalia.
Hii inatufundisha nini?
Wakati mwingine Mungu ataruhusu usichukue kila kitu ulichonacho / ulichokikusanya, ikawa umesahau fahamu kuwa ni Mungu ametaka, ili wengine wafaidike, usipende kukomba kila kitu, wakati mwingine utajiepusha na Baraka zako. Ukisafiri usiondoke na kabati lote la nguo, ulikuwa unakwenda mahali Fulani umebeba vingi, na kwa bahati mbaya ukakisahau kimoja, usiwe mwepesi kukirudia kukichukua, hujui ni kwanini Mungu amekusahaulisha.
Wewe ni boss, umeona, vichenji vimebaki, si lazima uvikombe vyote, waachie waajiriwa wako. Itakuwa ni Baraka kwako.
Lakini pia ni kutuelekeza mioyo yetu imtegemee yeye zaidi ya miganda yetu. Utakumbuka mitume wa Kristo, walipofanyiwa miujiza ya mikate, wakaagizwa wakusanye vipande, kisipotee hata kimoja, lakini baadaye walipoondoka, wakakumbuka wamesahau,wakaanza kulalamikiana wao kwa wao watakula nini. Lakini Yesu akawaambia mmesahau miujiza Mungu aliyowafanyia kama hiyo? Mna wasiwasi gani? Mungu anaweza kuwapa na vingine.
Mathayo 16:5 Nao wanafunzi wakaenda hata ng’ambo, wakasahau kuchukua mikate. 6 Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. 7 Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate. 8 Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache, kwa sababu hamna mikate? 9 Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota?
Hivyo na sisi pia tusiwe na tabia ya kubeba miganda yote.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Mofa ni nini? na inafunua nini kiroho?(1Samweli 28:24).
Mashonde ni nini? (Ezekieli 4:15).
YEYE ATAWABATIZA KWA ROHO MTAKATIFU NA KWA MOTO.
TUYATENDE MAMBO YOTE KWA UZURI NA UTARATIBU.
Azali ni neno linalomaanisha milele, isiyokuwa na mwanzo, wala mwisho.
Hivyo, watu wanaposema Yesu mwana wa Azali wa Mungu, wanamaanisha Yesu mwana Mungu asiyekuwa na mwanzo.
Neno hili utalisikia sana katika, ukiri wa Imani ya Nikea, (kwa makanisa ya kiprotestanti), Imani ya Nikea imetokana na baraza la maaskofu wa kidini waliokaa chini mwaka 325, ili kuunda kanuni moja mama ya imani, ambayo watatembea nayo wakristo wote duniani.
Na huu ndio ukiri wenyewe unavyosema;
“Twamwamini Mungu mmoja, Baba Mwenyezi, Muumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Twamwamini Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu, Mwana wa Azali wa Baba: yu Mungu kutoka Mungu, yu Nuru kutoka Nuru, yu Mungu kweli kutoka Mungu kweli; Mwana wa Azali asiyeumbwa, mwenye uungu mmoja na Baba: Kwa Yeye huyu vitu vyote viliumbwa. Aliyeshuka kutoka mbinguni kwa ajili yetu wanadamu na kwa wokovu wetu; akatwaa mwili kwa uweza wa Roho Mtakatifu katika Bikira Mariamu, akawa mwanadamu: Akasulibiwa kwaajili yetu zamani za Pontio Pilato; aliteswa, akafa, akazikwa. Siku ya tatu akafufuka kama yanenavyo Maandiko Matakatifu: Akapaa mbinguni; ameketi mkono wa kuume wa Baba: Naye atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu walio hai na wafu. Na ufalme wake hauna mwisho; Twamwamini Roho Mtakatifu Bwana mtoa uzima, atokaye katika Baba na Mwana, anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana, aliyenena kwa vinywa vya manabii; Twaamini Kanisa moja, takatifu, la Kikristo la ulimwengu wote na la kimitume. Twakiri ubatizo mmoja kwa ondoleo la dhambi, Twatazamia kufufuliwa kwa wafu, na uzima wa ulimwengu ujao. Amen”
Je! Ni kweli Kristo ni mwana wa Azali wa Mungu?
Jibu ni ndio. Yeye hana mwanzo wa siku wala mwisho wa Siku. Amefananishwa na Melkizedeki kama maandiko yanavyosema (Waebrania 7:3). Yesu ndio Yehova, na ndio Elohimu katika umbile la kibinadamu. Wala hana tofauti yoyote na Mungu. Ni ofisi tu tofauti za utendaji kazi wa Mungu, lakini ni yeye Yule milele na milele. Wala si Miungu mitatu, katika umoja. Bali ni mmoja katika utendaji kazi wa aina tatu tofauti. Alikuja akakaa kwetu ili kutufundisha namna ambavyo sisi tunavyoweza kuwa wana kamili wa Mungu.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?
Huyu Azazeli ni nani tunayemsoma katika(Walawi 16:8)
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
Vyemba kama lilivyotumika hapo ni mkuki.
Absalomu mwana wa Daudi alipomwasi baba yake, na kusababisha vita vikubwa katika Israeli, Tunasoma, alipokuwa vitani, akiwa amepanda mnyama wake, alipita chini ya mti mmojawapo akanaswa, mnyama alipoendelea mbele yeye akabaki ananing’inia pale pale, pasipo mafanikio yoyote ya kujinasua, baadhi ya askari wa Daudi walipomwona waliogopa kumuua, kufuatana na kiapo cha Daudi alichowaagiza wasimuue. Lakini jemedari wa mfalme aliyeitwa Yoabu yeye alikaidi amri, na kwenda kumwua kumpiga hivyo vyemba vitatu, moyoni. Kisha akamaliziwa na wasaidizi wake.
2Samweli 18:14 Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua vyemba vitatu mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa akali hai katikati ya ule mwaloni. 15 Kisha vijana kumi, waliomchukulia Yoabu silaha zake wakamzunguka, wakampiga Absalomu, na kumwua
Hivyo Yoabu alimchoma mikuki mitatu Absalomu kifuani mwake.
Lakini katika habari hii tunajifunza nini?
Upendo wa Daudi kwa mwanae ni sawa na Upendo wa Mungu kwetu sisi. Ijapokuwa Absalomu alimuudhi sana baba yake mpaka kumvunjia heshima ya kulala na wake zake, na kuuasi ufalme wake mtukufu, Daudi bado moyo wake ulikuwa kwa Absalomu kutaka atubu. Lakini Absalomu mwenyewe hakutaka, na hivyo alikutana na majeshi yakamwangamiza kwa tabia zake za uasi ulioendelea. Laiti angekuwa mtoto mtii, asingekufa kwasababu baba yake angeweza kumlinda.
Tunapomwasi Mungu, tunajitenga na rehema zetu wenyewe, Kama vile Yona alivyosema katika (Yona 2:8),. Kamwe usimwasi Mungu ndugu, tembea katika njia zake, kwasababu hakika huko unapokimbilia kifo kipo. Na utakapovamiwa na adui yako ibilisi Mungu hataweza kukutetea kwa lolote. Utakufa na kuangamia milele kwa vyemba hivyo rohoni.
Nje ya Kristo hakuna usalama. Mrudie Mungu wako, kwa kumfuata Bwana Yesu, Tubu dhambi zako leo, ubatizwe, upokee ondoleo la dhambi zako. Uishi maisha ya neema siku zote ndani ya pendo lake. Acha uasi, neema haitadumu kwako daima kukulinda katika hiyo mitego adui anayokutegea kila siku akuue.
Je ungependa kuupokea wokovu leo? Kwa Yesu kuwa mwokozi wako na mtetezi? Kama ni ndio basi fungua hapa kwa mwongozo huo wa Sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
ANGALIA UZURI WAKO, USIGEUKE KUWA KITANZI CHAKO.
UVUMILIVU NA MIKAKATI YA ABSALOMU, INA FUNZO NYUMA YAKE.
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.