Neno sulubu huzaa kusulibisha/kusulubisha,
Maana ya Sulubu, ni kuadhibisha kwa kuning’iniza kwenye mti wa msalaba, au nguzo iliyonyooka, kwa kufungwa au kugongelewa miguu na mikono, na kuacha hapo mpaka ufe.
Hii ni aina ya adhabu ya kifo, ambayo ilitumika zamani, kwenye falme zilizokuwa na nguvu na katili kama Rumi.
Watu walioshitakiwa kwa makosa makubwa ikiwemo uhaini, au uuaji, uvunjaji amani, hawakupewa adhabu ya kawaida ya kifo kama vile kukatwa kichwa na kufa mara moja,. Bali walipewa adhabu kali kama hii, lengo lake ni kumfanya Yule mshitakiwa kupitia mateso makali ya muda mrefu kabla ya kufa, kwasababu, baada ya kuning’inizwa kwake pale msalabani itamchukua siku tatu mpaka wakati mwingine wiki hadi kufa. Hivyo kipindi chote hicho unatakuwa unateseka tu pale mtini.
Hiyo ndio adhabu waliyoichagua kwa mwokozi wetu Yesu Kristo, ambaye hakuwa na hatia yoyote, wala kosa, jambo ambalo hata mtawala yule Pilato alilishuhudia kuwa hakukuwa na uovu wowote ndani yake. (Luka 23:4). Lakini kwasababu ilipasa maandiko yatimie ili sisi tupate ukombozi mkamilifu, ndio maana ilimpasa Yesu aadhibiwe vikali, ili mimi na wewe tupokee ONDOLEO LA DHAMBI. Kwa kifo chake.
Gharama aliyoilipa ni kubwa sana, kusulubiwa uchi wa mnyama, bila nguo, kudhalilishwa na kupigwa, na kuharibiwa mwili wote. Ni kwasababu mimi na wewe tupokee msamaha wa dhambi, tuepushwe na hukumu ya milele ya jehanamu ya moto.
Ndio maana maandiko yanasema..
Waebrania 2:3 sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia.
Je! Umempokea Yesu maishani mwako?
Ikiwa ni la! Basi waweza kufanya hivyo sasa, kwa kubofya hapa ili upate mwongozo wa sala hiyo. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
Tofuati kati ya kifo na mauti ni ipi?
Swali: Kusaga kunakozungumziwa katika Ayubu 31:10 ni kupi?..na maandiko hayo kwa ujumla yana maana gani?
Jibu: Turejee kuanzia mstari ule wa 9.
Ayubu 31:9 “Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;
10 Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine, Na wengine na wainame juu yake.
11 Kwani hilo lingekuwa kosa kuu; Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi”
Maneno haya ni ya Ayubu kwa rafiki zake watatu, ambapo alikuwa anajaribu kuwaambia ukamilifu wake kuwa hajawahi hata kumtazama mwanamke kwa kumtamani (Ayubu 31:1) wala hajawahi kumchukua mke wa jirani yake… Hivyo majaribu yaliyompata si kwasababu ya dhambi au makossa.
Na hapo mstari wa 9 anazidi kujithibitisha kuwa kama “moyo wake ulishawishwa kwa mwanamke, Na ameotea mlangoni pa jirani yake; Ndipo hapo mke wake na asage kwa mwingine, Na wengine na wainame juu yake”.
Akimaanisha kuwa kama yeye aliotea mlango kwa jirani yake, maana yake alisubiri mume wa mke wa jirani yake aondoke kisha aingia na kulala na mwanamke huyo.. basi na yeye pia mke wake na achukuliwe na akasage kwa nyumba ya mwanaume mwingine.
Sasa kusaga kunakozungumziwa hapo ni “kule kusaga nafaka”.. Kumbuka shughuli maarufu ya wanawake wa zamani katika nyumba zao zilikuwa ni kusaga nafaka kama ngano au mtama..
Ndio maana utaona katika lile tukio la unyakuo limefananishwa na wanawake wawili kukutwa wakisaga, na si wanaume..
Luka 17:34 “Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.]
Kwahiyo kusagan ilikuwa ni shughuli ya siku zote ya wanawake wa nyumbani, Na walikuwa wanasaga kwa kutumia mawe maalumu yajulikanayo kama “Mawe ya kusagia”
Kwa maelezo ziadi kuhusiana na Jiwe/mawe ya kusagia fungua hapa >>>JIWE LA KUSAGIA
Kwahiyo Ayubu alimaanisha kama aliiba mke wa mtu mwingine, basi wake pia achukuliwe na kutumikia nyumba nyingine, (kwa shughuli hizo za kusaga na nyingine kama za mama wa nyumbani).. na si tu asage, bali pia na wengine wainame juu yake, (maana yake walale naye).
Lakini hayo yote Ayubu hayakumpata kwasababu alikuwa mkamilifu katika njia zake, na wala hakuwahi kulala na mke wa jirani yake, wala kudhulumu, wala kumnyima maskini mkate..njia zake zote zilikuwa ni kamilifu kama Bwana Mungu alivyomshuhudia..
Ayubu 1:1 “Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu”
Ni mambo gani tunajifunza kwa maisha ya Ayubu?
Jambo la kwanza: ni roho ya kumcha Mungu na kuepukana na Uovu.. Watu wanaomcha Mungu na kuepukana na uovu ndio wanaosifiwa naye..
pili: ni Uvumilivu wa Ayubu…Pamoja na majaribu yote yale, alimngoja BWANA, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu (Ayubu 1:22), na mwisho wa siku Bwana alimwokoa na majaribu yale yote.
Yakobo 5:11 “Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”
Je umempokea YESU?..kama bado unasubiri nini?.. Fahamu kuwa mlango wa wokovu hautakuwa wazi siku zote, ipo siku utafungwa, na siku hiyo imekaribia sana, huwenda ikawa leo?..Je parapanda ikilia na ikikukuta ukiwa katika hali hiyo, utakuwa mgeni wa nani?..au ukifa katika hali hiyo kule uendako utakuwa mgeni wa nani?.. Tafakari sana na ufanye maamuzi, kama bado hujaokoka.
Bwana YESU ANARUDI.
Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia”.
Maran atha!.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba.
MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
Biblia inamaana gani inaposema “Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu?”
Swali: “Kigutu” ni mtu wa namna gani kama tunavyosoma katika Marko 9:43?
Jibu: Turejee,
Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima U KIGUTU, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;
44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]”
“Kigutu” ni mtu aliyekatwa mkono au aliyekatika mkono, tazama picha juu.
Biblia inatufundisha kuwa kiungo chetu kimoja kikitukosesha tukiondoa ili kisitupeleke katika jehanamu ya moto.
Sasa ni kweli kiungo kinaweza kuwa tabia, au marafiki, au vitu vya kimwili ambavyo vimejiungamanisha na mtu kiasi kwamba vinamkosesha katika Imani. Lakini pia biblia iliposema kiungo, imemaanisha pia kiungo kama kiungo, ikiwa na maana kwamba kama ni mkono ndio unakukosesha basi uondoe!, kama mkono wako umezoea kuiba, baada ya kutubu!, basi uondoe! Na hautaiba tena.
Kama ni jicho pia liondoe, na viungo vingine vyote… Na sababu ya Bwana kusema hivyo ni ili mtu aokoke na ziwa la moto, ambao kule kuna funza wasiokufa!, na moto wa kule hauzimiki, na wote wanaoshuka huko moshi wa maumivu yao unapanda juu milele na milele.
Ufunuo 14:10 “yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; NAYE ATATESWA KWA MOTO NA KIBERITI MBELE YA MALAIKA WATAKATIFU, NA MBELE ZA MWANA-KONDOO
11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake”.
Kwa upana juu ya viungo vinavyokosesha fungua hapa >>YESU alimaanisha nini aliposema “mkono wako ukikukosesha ukate?
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Nini tofauti kati ya moyo na roho?
Bwana alimaanisha nini kusema “kila mtu atatiwa chumvi kwa moto”
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
(Maswali yahusuyo pasaka)
Swali: Je kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka, kwamfano mwaka 2023 pasaka ilikuwa ni Aprili 13, lakini mwaka huu 2024 ni Marchi 31, na inategemewa kubadilika tena katika mwaka ujao na miaka yote inayokuja, kwanini iwe hivyo, wakati Krismasi ni tarehe ile ile 25 miaka yote?
Jibu: Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa pasaka ni moja ya sikukuu 7 za wayahudi, na inasheherekewa na wayahudi katika kila terehe 14 ya mwezi wao wa Kwanza, ambapo mwezi wao wa kwanza unaangukia katikati ya mwezi Machi na Aprili kwa kalenda tunayoitumia sisi.
Lakini kuhusiana na kwanini tarehe za pasaka zinabadilika kila mwaka kwa upande wa wakristo, ni kutokana na MWONEKANO WA MWEZI.
Mwezi unapozuka mzima (yaani angavu/full moon) basi jumapili inayofuata ndiyo inayosherekewa na wakristo wengi kama jumapili ya pasaka.
Kuna miaka ambapo “mwezi mwangavu” unawahi kuchomoza na kuna miaka unachelewa. Ikiwa na maana kuwa kama mwezi mwangavu utaonekana jumatano basi jumapili inayofuata itakuwa jumapili ya pasaka, ambayo itakuwa ni baada ya siku nne, Kwamfano kwa mwaka 2023 mwezi mwangavu ulionekana jumatano ya Tarehe 5 Aprili, hivyo jumapili iliyofuata ya tarehe 9 ndio ikawa jumapili ya pasaka.
Lakini kwa mwaka 2024, Mwezi mwangavu umewahi kuonekana, kwani umeonekana Jumatatu ya tarehe 25 Machi, hivyo jumapili inayofuata ya tarehe 31 Machi, ndio itakayokuwa jumapili ya pasaka.
Lakini pia kwa mwaka 2025, Mwezi mwangavu unatarajiwa kuonekana jumapili ya tarehe 13 Aprili, hivyo jumapili itakayofuata ya tarehe 20 Aprili ndio itakayokuwa jumapili ya pasaka.
Kwahiyo hiyo ndio sababu kwanini tarehe hizo zinabadilika badilika kila mwaka, (ni kutokana na mwonekano wa mwezi).
Sasa kujua pasaka ni nini na kama wakristo ni halali kuiadhimisha fungua hapa >>PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA?
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)
Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
SWALI: Yesu kuvishwa taji la miiba kichwani alipokuwa anasulubiwa kulikuwa kuna funua nini rohoni?
JIBU: Kila tendo alilotendewa Yesu katika kipindi cha mateso yake lilikuwa lina ufunuo wake rohoni. Tunajua wale askari waliposikia kuwa yeye ni mfalme, muda ule ule walimvisha vazi la kifalme, kisha wakampa fimbo, na baada ya hapo wakasokota taji la miiba, wakamvisha kichwani, kisha wakaanza kumdhihaki, huku wakimpiga wakisema.. Salamu! Mfalme wa Wayahudi!
Yohana 19:2 “Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. 3 Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi”
Tunajua lengo la wale maaskari kumvisha miiba ni kumfanya aumie zaidi, lakini upo ufunuo mkubwa rohoni, pengine kwanini asingevishwa la matambara mabovu, au taji la udongo, au la vyuma vyenye ncha kali, badala yake wakaona miiba.
Kibiblia, miiba, huwakilisha “mahali palipolaaniwa”.
Adamu alipoasi, Mungu alimwambia ardhi imelaaniwa kwa ajili yako, hivyo itatoa miiba na michongoma. Na matokeo yake ni kwamba italimwa kwa shida
Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
Ndio maana shamba ambalo halipaliliwi au halitunzwi, matokeo yake ni kuwa linatoa miiba.
Mithali 24:30 Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. 31 Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka. 32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho. 33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! 34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha
Na vivyo hivyo rohoni, mioyo yetu inafananishwa na mashamba.
Ukisoma ule mfano wa mpanzi, utaona mbegu(Neno la Mungu), lilipopandwa, zipo ambazo ziliangukia kwenye miiba (yaani mahali ambapo hapajafyekwa na kupapaliwa), ndipo pale kwenye miiba, na mwishowe zikakua na kumea. Lakini zikasongwa na ile miiba hazikashindwa kuzaa.
Yesu akatoa tafsiri yake, akasema, miiba ile ni “anasa, udanganyifu wa mali, na shughuli za ulimwengu huu”.
Luka 8:14 “Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote”.
Sasa Yesu alipokuja kufa msalaba, alishughulika na jambo hilo kubwa, kubeba laana hiyo kubwa kwenye kichwa chake.
Akimaanisha kuwa ile nchi iliyolaaniwa (yaani mioyo wa mtu), kuanzia sasa ni mwisho. Imekwisha.
Miiba iliyokuwa inatoka mimi nimeichukua kichwani mwangu.
Moyo wa mtu kuanzia sasa, utaanza kuzaa matunda, na wala hautasongwa na anasa, wala udanganyifu wa mali, wala shughuli za ulimwengu huu, usiivishe chochote.
Hii ikiwa ni kweli kabisa.
Sisi tunaomwamini Yesu, moja kwa moja tunapewa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu (Yohana 1:12), na matokeo ya uwezo huo ni kuwa, nguvu ya kusongwa na ulimwengu inakuwa ndogo, kwasababu Roho Mtakatifu aliyemwagwa ndani yetu anatusaidia, Kuukataa ulimwengu, na kuishi maisha ya utauwa. Utakuwa ulimwenguni lakini, hutasongwa na mambo yake. Kwasababu utafundishwa pia “kiasi” na Roho Mtakatifu.
Hivyo uwezo huu utakuja ndani yako, pindi tu unapomgeukia Kristo kwa kumaanisha kabisa, ambapo panaanza na kwa KUTUBU kwanza dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kugeuka,na kumfuata Kristo tangu huo wakati, na kisha kubatizwa, na kupokea Roho wake. Lakini nje ya hapo, huwezi kwenda popote.
Je! Umempokea Yesu?
Pasipo yeye huwezi ndugu kuushinda ulimwengu kwa nguvu zako, haiwezekani hata kidogo, hata ufanyeje haiwezekani,miiba itakusonga tu, dunia itakulemea tu, Unahitaji nguvu zake, kwa Roho wake Mtakatifu. Ili kuzipata maanisha tu kumgeukia, na kusudia kutembea naye moyoni mwako.
Utaushinda huu ulimwengu. Wala hakuna mwiba wowote utakaomea kwenye moyo wako. Kwasababu Kristo alishayakomesha yote. Je! upo tayari kuokoka leo? Basi fungua hapa kwa mwongozo wa kimaombi>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
Je vazi alilovikwa Bwana Yesu lilikuwa la Zambarau au Jekundu?
Swali: Kuna tofauti gani ya “kutakabari” na “kutakabali”, sawasawa Warumi 1:30 na Mwanzo 4:4-5?
Jibu: Tuanze na 1) kutakabari..
Warumi 1:30 “wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao”.
“Kutakabari” maana yake ni “kuwa na kiburi” kinachokuja kutokana na kuwa na kitu Fulani, au kujiamini sana..
Matokeo ya kutakabari ni kuanguka..
Mithali 16:18 “Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
19 Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi”.
Mfano wa mtu kwenye biblia aliyetakabari na akaanguka ni Mfalme wa Ashuru aliyeitwa Senakeribu.. Huyu alijiinua mbele za Mungu kwa kiburi kikuu na anguko lake likawa kubwa. (Soma 2Wafalme 19:28-37).
Unaweza kujifunza Zaidi juu ya kutakabari kwa kufungua hapa >>Kutakabari ni nini katika biblia?.
Mistari mingine inayozungumzia juu ya kutakabari ni pamoja na 1Samweli 2:3, Nehemia 9:10, Isaya 13:3, na 1Wakorintho 13:4.
2. KUTAKABALI.
“KUTAKABALI” ni tofauti na “kutakabari”…. Kutakabali ni “kukubali kitu”.. Utaona sadaka ya Habili Mungu aliitakabali (maana yake aliikubali na kuiheshimu zaidi ya ile ya Kaini).
Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana AKAMTAKABALI Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini HAKUMTAKABALI, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”
Na sisi tunapomtolea Mungu sawasawa na Neno lake, Sadaka zetu atazitakabali, lakini tukitoa nje na neno lake hatazitakabali kama vile sadaka ya Kaini alivyoikataa..
Yeremia 14:12 “Wafungapo, mimi sitasikia kilio chao; na watoapo sadaka za kuteketezwa na sadaka ya unga, sitazitakabali; bali nitawaangamiza kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni”
Vile vile tukimwomba Mungu sawasawa Neno lake basi Maombi yetu atayatakabali na kutujibu, lakini tusipoomba kulingana na Neno basi hata maombi yetu hayatajibiwa..
Zaburi 6:9 “Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu”.
Kujua kuomba kulingana na Neno la Mungu fungua hapa >>>>KWANINI MUNGU HAJIBU MAOMBI?
Mistari mingine inayohusu KUTAKABALI ni pamoja na Zaburi 20:3, Mhubiri 5:20, Ezekieli 20:41, Hosea 14:2 na Malaki 2:13.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Kiburi cha Uzima ni nini? (1Yohana 2:16)
SWALI: Mungu anaposema dhambi zetu zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Ana maana gani, kwenye hilo neno bendera?
Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. 19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
JIBU: Hapa ni Mungu anaeleza mambo mawili hayuhuso dhambi walizotenda watu wake.
Tunajua theluji inang’aa sana mfano wa jua, Kuonyesha ni jinsi gani hawa watu walivyokuwa mbali sana na ukamilifu, yaani jinsi gani walivyokuwa hawakaribii hata kidogo kuwa wema mbele za Mungu, walau wangeonekana wa rangu ya kijani, basi wangekuwa na afadhali, lakini ni mbali sana, wana rangi ya damu. Ndivyo ilivyokuwa Israeli yake.
Zamani bendera nyingi zilichovywa katika rangi nzito nyekundu, inayodumu sana, kwasababu ni kitu cha kudumu muda mrefu, hivyo haikuhitajika rangi inayofubaa haraka. Sio tu bendera, lakini mpaka mavazi ya kifalme, au nguo za thamani za sufu.
Hivyo unaposoma habari za bendera hapo, si bendera ya kila rangi, mfano wa bendera tulizonazo sikuhizi zina rangi mbalimbali, zamani nyingi zilichovya kwa rangi nyekundu. Hivyo Mungu anawaambia ijapokuwa ni nyekundu kama bendera, basi zitageuzwa na kuwa nyeupe kama Sufu, (akiwa na maana ambayo haijachovywa), Yaani Mungu anaweza kuiondoa hiyo rangi sugu, kwenye hicho kitambaa kana kwamba hakijachovywa kabisa.
Kufunua nini,
Yesu Kristo mwokozi wetu ndiye aliyetimiza huo unabii. Kuonyesha kuwa dhambi zote tulizotenda haijalisha ni nyingi kiasi gani, haijalishi ni mbaya namna gani yeye kwa damu yake anaweza kuzifuta kabisa kabisa. Dhambi tulizotenda haijalishi hazisameheki namna gani, hazineneki, ni sugu namna gani, yeye anao uwezo wa kuziondoa, kwa neema yake.
Swali ni je! Umesamehewa dhambi zako? Kama ni la! Unangoja nini kuipokea neema hii, ya WOKOVU mkuu namna hii? Pokea sasa msamaha wa dhambi kwa kutubu dhambi zako, na kumaanisha kuishi maisha mapya ya wokovu. Kisha moja kwa moja atakupokea na kukupa ondoleo la dhambi zako. Na baada ya hapo unahesabiwa kuwa huna dhambi yoyote, umestahili uzima wa milele, bure.
Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo basi, fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa maombi mafupi, na kwa kupitia sala hiyo kwa imani utakuwa umeshampokea Yesu Kristo, na amekusamehe dhambi zako zote.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Wale Nyoka wa Moto jangwani, walikuwa ni wa namna gani?
ALAMA ZA BENDERA YA ISRAELI ZINAWAKILISHA NINI?
Ni muungamaniko wa maneno makuu mawili. (Yaani Christian na Islamic). Likachukuliwa Neno la kwanza Chris katika Christian, likaunganishwa na Neno la katikati “slam” kutoka katika Islamic. Kuunda Christlam
Hii ni imani iliyozuka, katika taifa la Nigeria miaka ya 1970. Kufuatana ni migongano ya kiimani baina ya makundi haya mawili ya dini, ikizingatiwa kuwa Taifa La Nigeria ndio lenye watu wengi barani Africa, na takribani Nusu kwa Nusu, dini hizi mbili ndio zimechukua jamii kubwa ya watu.
Hivyo waasisi ya umoja huu walikuwa na madhumuni ya kuondoa tofauti za kidini, husani zilizo katika mataifa ya magharibu na ya mashariki ya kati, Lakini pia kwasababu hizi ndio dini kubwa duniani, basi pia zikiungana zinaweza kusaidia kuushinda upagani kwa sehemu kubwa.Na ukweli ni kwamba imani hii imepata umaarufu mkubwa duniani, hususani kwa kipindi cha sasa.
Waanzilishi walisukumwa kuunda umoja huu, wakiamini kuwa, sehemu kubwa ya dini ya kikristo inatajwa katika Quran, wakimrejea Yesu mwenyewe pamoja na manabii wa kale, kama Ibrahimu na wengineo. Lakini pia uislamu unamwingiliano mkubwa wa kitamaduni ambao hata katika ukristo upo. Hivyo kwa mujibu wa hoja zao hakuna sababu ya kuwa na utofauti wowote katika mashindano ya kidini.
Imani ya Kikristo na dini ya kiislamu haviwezi kuchangamana, ni sawa na chuma na udongo. Kwasababu kiini cha imani ya ukristo ni KRISTO mwenyewe, na kwamba mtu hawezi kwenda mbinguni pasipo kumwamini YESU kama mwokozi PEKEE anayewaokoa wanadamu. Jambo ambalo linakinzana na dini ya Kiislam, katika imani ya kufika mbinguni, ambapo kwa waislam Kristo ni kama mmojawapo wa manabii tu wengine. Na hivyo mbingu si kupitia Kristo, bali ni kupitia matendo mazuri kama vile kukaa mbali na uovu n.k.
Uislamu haumtambui Kristo kama Mungu, huamini kuwa yoyote anaye amini kuwa Yesu ni Mungu, ni makufuru, kwasababu Mungu hajazaa, wala hana mshirika. Hivyo aaminiye uungu wa Yesu, pepo haimuhusu.
Kwa vigezo hivyo, uislamu na ukristo ni imani mbili tofauti kabisa, ijapokuwa zitaonekana kushea baadhi ya desturi, lakini bado haziwezi kuletwa pamoja kuwa kitu kimoja.
Je! Hatupaswi kuwa waamini wa Chrislam
Ndio wewe kama Mkristo,, imani yako haipaswi kuchanganywa na nyingine yoyote, ukifanya hivyo ni Kosa kiimani. Sisi tunaamini, wokovu ni kwa kupitia Yesu Kristo anaotupa BURE kwa neema katika kumwamini Yeye, kwa kifo chake pale msalabani.
Tunamtegemea Kristo kutuokoa, kutupa nguvu ya kuishi maisha makamilifu, kutuongoza, kwa asilimia zote. Hivyo hatuna msingi au tegemeo lingine nje yake yeye. Na hata hivyo kibiblia, yoyote asiyekubaliana na Kristo Yesu, kama ndiye mwokozi pekee. Huyo ni mpinga-Kristo.
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa wewe kama mwana wa Mungu, usijihusishe ni imani yoyote nje ya Kristo Yesu mwokozi wako.
Matendo 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?
Praitorio ni nini? Na Kwanini ilikuwa ni najisi kwa wayahudi kuingia humo? (Yohana 18:28)
SWALI: Je kulikuwa na umuhimu wowote wa ile merikebu ya Iskanderia walioipanda Paulo na wafungwa wengine kutajwa jina lake ‘ndugu Pacha’,?
Matendo 28:11 Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha. 12 Tukafika Sirakusa, tukakaa siku tatu. 13 Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli. 14 Huko tukakuta ndugu, wakatusihi tukae nao siku saba; na hivi tukafika Rumi.
JIBU: Safari ya mtume Paulo kama mfungwa, kutoka Kaisaria kwenda Rumi kuhukumiwa, haikuwa rahisi, iligubikwa na misuko suko mikubwa ambayo ilihatarisha maisha yao ukisoma Matendo 27, utaona mtume Paulo alionywa na Roho Mtakatifu kuhusu hatari hiyo lakini alipomwambia akida na manahodha, walipuuzia agizo lake, kwasababu watu wale hawakuamini habari za “miungu kabisa”. Maandiko yanasema walipoona upepo wa kusi umevuma kidogo tu, unaoruhusu kusafiri, wakadhani itakuwa hivyo mbeleni.
Lakini tunaona walipofika katikati, ghafla ile bahari iliwachafukia sana, upepo wa nguvu ukavuma merikebu yao ikawa karibu na kuzama, baadaye ilivunjika kabisa, na wakaokoka kwa shida kwasababu Mungu alimuhakikishia Mtume Paulo kuwa hakuna hata mmoja wao atakayeangamia.
Walipookoka na kufika kisiwa kile kilichoitwa Melita, walikaa miezi mitatu pale, kuruhusu hali ya hewa kutulia, kabla ya kuondoka. Lakini tunaona walipotaka kuondoka, safari hii wale mabaharia pamoja na maakida, hawakuichukulia safari yao kirahisi rahisi, yaani hivi hivi tu bila uongozo wowote. Ndipo walipojifunza kuchagua merikebu yenye “ulinzi wa kiroho”. Wakaipata hiyo ya Iskanderia iliyokuwa na nembo ya “Ndugu Pacha” kwa mbele.
Ndugu Pacha ni miungu ya kipagani ya kiyunani, ukisoma tafsiri nyingine za biblia imewataja moja kwa moja miungu hiyo kama Castor na Pollux. Ni miungu ambayo waliamini inahusika na ulinzi wa safari za majini. Hivyo kwa imani yao ya kipagani, wakachukua nembo yao kuonyesha tunaiabudu na kuiheshimu hii miungu, na kutaka iwaongoze salama katika safari yao, hawategemei tena elimu zao na nadharia zao.
Sasa tukirudi kwenye swali, linalouliza, kulikuwa ni umuhimu gani, hiyo merikebu ya Iskanderia kutajwa hadi nembo yake ya ndugu Pacha. Sababu ndio hiyo, Sio kwamba biblia inatufundisha, na sisi tukaweke miungu ya kipagani, kwenye vyombo vyetu vya usafiri kutuhakikishia ulinzi, hapana!
Bali inatufundisha Safari ya maisha hapa duniani. Kila mwanadamu anasafiri, lakini Je! Katika safari yako ni kitu gani kinakuongoza na kukulinda ili kukufikia ng’ambo yako salama?
Hakuna mwanadamu ambaye anaweza kujiongoza mwenyewe. Na ndio maana utaona hawa kwasababu hawakumjua Mungu wa kweli iliwabidi wakatafuta vinyago visivyoweza kuwasaidia kitu viwaongoze, na kama sio mtume Paulo kuwepo ndani ya Merikebu ile, safari yao ndio ingekuwa mbaya mara mbili zaidi. Hawakujua tu waliongozwa na Kristo Yesu pasipo wao kujua kwa neema tu!. Kwasababu watumishi wa Mungu walikuwa ndani.
Na sisi, hapa tulipo, fahamu kuwa maisha yako, bila KRISTO ni mauti mbele. Shetani hakuwazii mema, wala akili zako mwenyewe hazikusaidii ndugu, hiyo elimu ni kazi bure, huo uzoefu na ujuzi ulionao ni bure rafiki. Unamuhitaji Kristo, yeye ndio awe nembo ya maisha yako. Mwamini leo akupe msamaha wa dhambi, mwamini leo akuokoe, safari yako iwe salama hapa duniani. Ukifa leo katika hali hiyo, fahamu ni jehanamu moja kwa moja. Umesikia injili ikihubiriwa mara ngapi, kwamba Yesu ni mwokozi lakini unapuuzia? Walio kuzimu wanatamani hata dakika moja, watubu hawawezi kwasababu kule hakuna maisha ya kuishi. Lakini wewe unaishi.
Usikiapo maneno haya, ugeuze moyo wako, umruhusu Kristo leo akuokoe, ikiwa upo tayari kumgeukia Bwana Yesu , na unatamani upate mwongozo wa kimaombi kwa ajili ya wokovu wako. Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii, bure.
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)
Jibu: Turejee.
Mithali 20:1 “Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima”.
Hili ni andiko linaloelezea mambo makuu mawili yanayowakosesha watu waliopungukiwa na Hekima.. na Mambo hayo ni “Mvinyo” pamoja na “Kileo”. Na vitu vyote hivi viwili vina madhara kwa mtu anayevitumia..
Sasa ni ipi tofauti kati ya Mvinyo na Kileo? Na madhara yake ni yapi kwa mtumiaji?.
“Mvinyo” (kwa lugha ya kiingereza ni “wine”) ni kilevi kinachotengenezwa kwa “Matunda yaliyosagwa” kama Zabibu, mananasi, maembe n.k Mfano wa mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu ni “Divai”.
Wakati “Kileo” (Kwa lugha ya kiingereza Beer/Bia) ni kilevi kinachotengenezwa kwa nafaka kama Ngano, mahindi, ulezi, mtama, mchele n.k
Kikawaida Mvinyo ndio wenye kilevi kingi kuliko Kileo. Na matokeo ya mtu anayetumia mvinyo au kileo yanakaribiana. Hebu tuangalia madhara ya kimoja baada ya kingine kibiblia.
1. MVINYO
Biblia anasema “Mvinyo hudhihaki”.. maana yake ni kuwa mtu anayetumia mvivyo anakuwa ni mtu wa kudhihaki na kudhihakiwa!.. kwasababu ya wingi wa maneno yao yasiyo na maana yatokayo midomoni mwao.
Ndio maana utaona kile kipindi cha Pentekoste, walipowasikia wanafunzi wa Bwana YESU wakinena kwa lugha, walidhani wamelewa kwa mvinyo mpya na hivyo wakaanza kuwadhihaki..
Matendo 2:12 “Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? 13 WENGINE WALIDHIHAKI, WAKISEMA, WAMELEWA KWA MVINYO MPYA.
14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.
15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli”.
Umeona hapo?.. walianza kuwadhihaki wakidhani wamelewa kwa MVINYO MPYA, ikimaanisha kuwa Mvinyo huleta dhihaka kwa anayekunywa. Na mtu anayelewa kwa mvinyo atapokea dhihaka nyingi katika maisha yake..
2. KILEO
Biblia inaendelea kusema kileo huleta “UGOMVI”. Asilimia kubwa ya watu wanaogombana mpaka kufikia hatua ya kudhuriana ni walevi wa pombe, mafarakano mengi yanatoka kwa watu waliolewa..
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba, Ulevi wa aina yoyote ile uwe wa “Mvinyo” au wa “Kileo” matokeo yake ni mabaya katika maisha ya ulimwengu huu na ule ujao…. Kulingana na biblia walevi wote hawataurithi uzima wa milele (soma 1Wakorintho 6:9-10 na Wagalatia 5:19-20)..
Warumi 13:13 “Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ULAFI NA ULEVI, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake”.
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
“Si watu wa kutumia mvinyo sana”, je tunaruhusiwa kutumia mvingo kidogo?(1Timotheo 3:8).
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?