Jibu: Tusome,
Waamuzi 18:2 “Basi wana wa Dani wakatuma watu wa jamaa zao, watu watano katika hesabu yao yote, watu mashujaa, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli, ili kuipeleleza hiyo nchi, KUIAUA; wakawaambia, Haya, endeni mkaikague nchi hii; basi wakaifikilia nchi ya vilima vilima ya Efraimu, hata nyumba ya huyo Mika, Wakalala huko”
Kuiaua nchi maana yake ni KUITEMBELEA NCHI au KUIZURU. Kwahiyo watu wanaozunguka zunguka ndani ya nchi kwa lengo la kuipeleleza au kwa lengo la utalii, maana yake ni WAMEIAUA HIYO NCHI.
Mungu wetu anaiaua dunia hii tunayoishi, kutafuta watu wanaomcha yeye, kuwatia nguvu na kuonyesha uweza wake juu yao.
2Nyakati 16:9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake…”
Lakini pia adui yetu shetani ANAIAUA dunia nzima kutafuta mwenye haki mmoja amwangushe..
Ayubu 1:6 “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.
7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.
8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu”
Hivyo hatuna budi kuutunza ukamilifu wetu ili tusije tukanaswa katika mitego ya shetani na hatimaye kuanguka kabisa.
Maran atha!
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
TABIA ZITAKAZOMTAMBULISHA MPINGA-KRISTO AJAYE.
Marago ni nini? ( Waamuzi 10:18)
KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.
Jibu: Tusome,
1Samweli 28:24 “Naye yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na unga, akaukanda, akafanya MKATE WA MOFA kwa unga huo”.
Mkate wa Mofa ni mkate uliotengenezwa bila kuwekwa “Hamira”. Hamira kwa lugha ya kibiblia inaitwa “Chachu” kazi yake ni kuchachusha au kuumua unga uliokandwa, kama biblia inavyosema katika..
Mathayo 13:33 “Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia”
Na tena biblia inasema.. “Chachu kidogo huchachua donge zima (Wagalatia 5:9)”
Kwahiyo Mikate ya Mofa ni mikate iliyotengenezwa bila kuwekwa hamira, mfano wa chapati. Kwa wayahudi baada ya sikukuu ya pasaka kupita, sikukuu iliyokuwa inafuata ilikuwa ni sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu (yaani Mofa), Ndani ya siku 7 Wana wa Israeli waliambiwa wale mikate ya Mofa, na mtu yeyote ambaye alionekana anakula mikate mingine zaidi ya hiyo, aliuawa kulingana na sheria ya torati.
Na ndani ya kipindi hicho pia mtu yeyote akionekana na Viungo vya Hamira ndani kwake, hata kama atakuwa hajaviweka kwenye unga, kitendo tu cha kuiweka ndani ilikuwa pia adhabu yake ni kifo
Kutoka 12: 15 “Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli”.
Soma pia Walawi 23:5-6.
Lakini je! Mkate wa Mofa unawakilisha nini kiroho?
Mkate wa Mofa unawakilisha Mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo, Na ndio uliotumika na wakristo wa kanisa la kwanza katika kushiriki Meza ya Bwana, na ndio unapaswa utumike hata sasa katika kushiriki meza ya Bwana, na si biskuti au maandazi!.
Luka 22:19 “Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu”.
Sasa kwanini Bwana Yesu achague mkate wa Mofa, kuwakilisha Mwili wake?
Ni kwasababu Mwili wa Bwana Yesu haubadiliki wala hauwezi kubadilishwa maumbile. Hamira/chachu kazi yake ni kubadilisha maumbile ya vitu, ndio maana inapowekwa kwenye unga uliokandwa baada ya muda Fulani utakuta ule unga umeumuka!
Sasa mwili wa Kristo hauumushwi, wala hauwezi kubadilishwa kimaumbile..bali siku zote ni ule ule!(Waebrania 13:8).. Maana yake kanuni za Bwana Yesu ni zile zile, hazibadilishwi na mazingira wala na mtu, Neno lake ni lile lile jana na leo na hata milele.
Hatuwezi kutia hamira Neno la Mungu, Neno la Mungu likisema ulevi ni dhambi!, hatuwezi kuliwekea hamira hapo na kusema ulevi sio dhambi!..likisema “mtu anapaswa avae mavazi ya kujisitiri” hatuwezi kulitia hamira kwa kusema “Mungu haangalii roho bali anaangalia mwili (1Timotheo 2:9)”
Na mambo mengine yote, biblia iliyoyataja ni lazima tuyazingatie yabaki kama yalivyo bila kuumuliwa na hamira za mafundisho ya uongo.
Bwana Yesu atusaidie katika hayo.
Maran atha!
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?
Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zilikuwaje?
HII NDIO TABIA YA WATU WA KEILA, USIIGE
Nini tofauti kati ya Bustani ya Edeni (Mwanzo 2:8) na bustani ya Adeni (Ezekieli 28:13 na Yoeli 2:3)
Jibu:Tusome
Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa EDENI, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya”.
Isaya 51:3 “Maana Bwana ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama BUSTANI YA EDENI, na nyika yake kama bustani ya Bwana; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba”.
Hapa tunaona ikitajwa bustani ya “Edeni” lakini tukisoma mahali pengine tunaona ikitajwa bustani nyingine ya “Adeni”
Ezekieli 28:13 “Ulikuwa ndani ya ADENI, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari”
Yoeli 2:3 “Moto unakula mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na BUSTANI YA ADENI mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao”.
Na pia katika Ezekieli 31:9, Ezekieli 31:16-18, na Ezekieli 36:35 utaona ikitajwa Adeni na si Edeni, swali je kuna utofauti wowote?
Jibu ni la! hakuna utofauti wowote iliyopo kati kati ya “Adeni” na “Edeni”, hayo ni maneno mawili yenye maana moja, sehemu moja biblia imetaja Edeni, sehemu nyingine Adeni lakini maana ni ile ile..Na maana ya neno Edeni au Adeni ni “paradiso ya raha”.
Mungu alipoiumba dunia, alimweka mwanadamu wa kwanza katika bustani ya Edeni, na alikusudia mahali pale pawe Paradiso yake ya milele. Dunia yote ilikuwa ni nzuri, lakini pale Edeni palikuwa ndio kitovu cha utukufu wa mwanadamu.
Lakini baada ya shetani kumdanganya Hawa, ndipo Uovu ukaingia na kusababisha mwanadamu kuondolewa katika bustani ile, na Mungu kuitowesha kabisa!
Lakini Bwana ameahidi kuumba Mbingu Mpya na Nchi mpya (Isaya 65:17), ambayo itakuja baada ya utawala wa miaka elfu kuisha hapa duniani. Katika mbingu mpya na nchi mpya, Bwana ametuandalia mambo mazuri kuliko yaliyokuwepo Edeni, maandiko yanasema jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia mambo ambayo Mungu kawaandalia wale wampendao..(1Wakorintho 2:9).
Lakini ahadi hiyo kulingana na Neno lake ni kwa wale waliomwamini Yesu Kristo na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake.
Je umempokea Yesu?..kama bado unasubiri nini?. Mwamini leo na ukabatizwe katika ubatizo na ujazwe Roho Mtakatifu kulingana na Matendo 2:38.
Maran atha.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Bustani ya Edeni ipo nchi gani?
Je! Ni kweli Yesu alirejesha kila kitu kama pale Edeni?
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
Swali: Kukaramkia ni nini?
Jibu: Tusome,
2Wakorintho 7:2 “Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu.
3 Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja”
“Kukaramkia” ni Kiswahili kingine cha neno “Utapeli” (ambao unahusisha kuchukua fedha kutoka kwa mtu kwa njia ya ulaghai wa maneno). Mfano wa watu wanaokaramkia watu ni manabii wa uongo, na makristo wa uongo!, ambao wanaweza kutumia chochote kile kudanganya nacho watu, ili lengo lao wapate fedha kutoka kwao. ( Na fedha hizo ndizo zijulikanazo Kama mapato ya aibu, ambayo yanatajwa katika kitabu Cha Tito 1:7)
Katika siku hizi za mwisho manabii wa uongo wanatumia maji, mafuta, udongo na vyote vijulikanavyo kama visaidizi vya upako kulaghai watu, hivyo wanawakaramkia watu na kuchukua fedha zao na mali zao, huku wakiwaaminisha kuwa matatizo yao yameondoka.
Watumishi hawa wa uongo, maandiko yanasema kuwa mungu wao ni tumbo!!..
Wafilipi 3:17 “Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.
18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.
20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo”
Mitume wa kanisa la kwanza hawakumkaramkia mtu yeyote, ili kupata faida.. Zaidi walihubiri injili kamili yenye kumgeuza mtu kutoka katika dhambi kuingia katika haki kupitia Yesu Kristo.
Na sisi hatuna budi kuwa kama hao, tuifanye kazi ya Mungu bila kumkaramkia mtu yeyote.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kwa namna gani mauti hufanya kazi ndani yetu na uzima kwa wengine? (2Wakorintho 4:12).
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.
Swali: Kudhili ni nini, au mtu aliyedhiliwa anakuwaje?
Jibu: Kudhili maana yake ni “kushusha chini” Mtu aliyeshushwa chini maana yake “kadhiliwa”.
Katika biblia, maandiko yanaonesha kuwa Mungu huwadhili watu wote wanaojikweza, na wenye kiburi..na wale wote wanaojishusha (yaani wanaojidhili) basi yeye huwakweza, kwa kuwapandisha juu!!.
Mathayo 23:11 “Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu.
12 Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa”
Ayubu 40:11 “Mwaga mafuriko ya hasira zako, Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili”.
Zaburi 75:7 “Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu”.
Unaweza kusoma pia juu ya Neno hilo katika Zaburi 107:39, na Wafilipi 4:12.
Hivyo na sisi hatuna budi kujishusha siku zote mbele za Mungu, na mbele za watu ili Bwana atukweze.. Kwasababu Mungu hapendi watu wanaojiinua, na wenye majivuno na wanaojiona wao ni bora kuliko wengine wote.
Luka 18:9 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
NI MAONO YAPI HAYO UNAYOSUBIRIA?
JE UNA MATUMAINI YA KUPATA TENA KILE ULICHOPOTEZA?
Nini maana ya kuabudu malaika? (Wakolosai 2:18)
Swali: Hivi viungo tunavyovisoma katika Mathayo 23:23, ni viungo gani na vina ujumbe gani kiroho?
Jibu: Tusome
Mathayo 23:23 “ Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za MNANAA na BIZARI na JIRA, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
24 Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia”.
Hapa tunaona ni viungo vitatu vimetajwa ambavyo ni; Mnana, Bizari na Jira. Tutazame kiungo kimoja baada ya kingine.
1.MNANAA:
Mnanaa ni aina ya majani ambayo yanatumika kama tiba ya magonjwa ya tumbo na kinywa. Asilimia kubwa ya dawa za Meno zinazotumiwa na wengi zinatengenezwa kwa majani haya ya mnanaa, pamoja na karafuu… watu hutumia majani ya mnanaa katika kimiminika kama chai mfano wa (mchaichai unavyowekwa) na kuuchemsha pamoja na kisha kunywa.. ambapo inasaidia kupunguza harufu ya kinywa, kuua bacteria mdomoni.
Pia Mimea ya Mnanaa ulitumika na unatumika hata sasa kusafisha tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo, na kuondoa gesi tumboni. Zao hili ni zao kongwe ambalo lilitumika enzi na enzi, na lilikuwa ni zao la biashara, ingawa upatikanaji wake haukuwa mgumu.
2. BIZARI:
Bizari ni aina nyingine ya Mmea, ambayo majani yake yanatumika kama Kiungo cha kuongeza ladha katika chakula, na pia faida yake katika mwili ni kupunguza magonjwa ya moyo. (Tazama picha chini)
3. JIRA:
Jira ni kiungo ambacho ni maarufu zaidi kuliko viungo viwili vilivyotangulia.. Kiungo hiki ni kiungo kinachowekwa katika baadhi ya vyakula kama Wali, Mikate na Maandazi kwaajili ya kuongeza ladha na pia kupunguza kiwango cha mafuta mwilini. (Tazama picha chini).
Sasa kwanini Bwana Yesu aseme “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za MNANAA na BIZARI na JIRA,” Ni kwasababu viungo hivi vilikuwa vinapatikana kirahisi sana na pia havikuwa vya gharama kubwa.. ni sawa tu na zao la Mchai chai, ambalo yeyote anaweza kulipanda nyumbani mwake, si kama maharage ambayo upatikanaji wake ni lazima ukayanunue tena kwa gharama kubwa.
Mazao haya katika maeneo ya Mashariki ya kati yanapatikana kirahisi sana, na hata mtu akiyalima na kuyapeleka sokoni basi faida yake si kubwa ni ndogo sana, kuliko mazao yote, kwahiyo hata zaka yake ni ndogo sana..
Sasa Mafarisayo wenyewe walikuwa wanahakikisha wanatoa ZAKA hata kwa viungo vidogo kama hivyo..hawaachi hata senti, ni waaminifu katika kulipa zaka.. Sasa ndio Bwana Yesu akawaambia, mambo hayo wanayoyafanya ni mazuri, (yaani kuzingatia kulipa zaka bila kuiba chochote, hata kama ni kidogo) lakini pia pamoja na kuwa waaminifu katika kulipa zaka, wanapaswa pia wasiyaache mambo mengine ya msingi kama Rehema, Adili na Imani.. Vinginevyo watakuwa ni wanafiki.
Kwasababu haitakuwa na maana kama Utakuwa mwaminifu katika kulipa Zaka, halafu huna Rehema, au Msamaha au Imani au Upendo.. Vyote hivyo vinapaswa viende sambamba.
Ni nini tunajifunza hapo?
Na sisi pia hatuna budi kufanya mambo yote sawasawa yaani kufanya mambo ya sheria kama Imani, Adili, Upendo, Utakatifu, uaminifu, utu wema n.k lakini pia ni lazima KULIPA ZAKA kwa uaminifu bila kuiba chochote, Ndicho Bwana Yesu alichokuwa anakimaanisha hapo kwa Mafarisayo pamoja na sisi pia..
Swali ni Je! unalipa Zaka?..(Fahamu kuwa Zaka si agizo la agano la kale pekee bali pia ni la agano jipya, na lililoelekezwa na Bwana Yesu mwenyewe) Kama hulipi basi fahamu kuwa unaenda kinyume na hilo andiko la Mathayo 23:23, kwasababu hapo Bwana Yesu hapo kaelekeza kwamba ni lazima tulipe Zaka. Vile vile ni lazima tufanye mambo sheria kama Rehema, imani, adili na upendo.. Mambo haya yote ni lazima yaende sambamba.
Bwana Yesu akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
IPELEKE SADAKA YAKO MAHALI SAHIHI, ILI UBARIKIWE.
JE! KUNA UMUHIMU WOWOTE WA KULIPA ZAKA?
UTARATIBU WA KUTOA FUNGU LA 10 UPOJE?.
NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?
Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?
Je! neno Masihi linamaanisha nini?
“Masihi” ni Neno la Kiebrania, linalomaanisha “Mpakwa mafuta” (Yaani mtu aliyeteulewa na Mungu kwa kusudi Fulani). Katika biblia watu walioteuliwa na Mungu rasmi kuwa Wafalme, hao waliitwa masihi wa Bwana, vile vile waliochaguliwa na Mungu kuwa manabii, nao pia waliitwa masihi wa Bwana.
Tafsiri nyingine ya neno Masihi ni “Kristo”. Kwahiyo katika biblia mamasihi (yaani makristo au watiwa mafuta) walikuwa wengi lakini aliyekuwa MASIHI KIKWEKWELI alikuwa ni Mmoja tu! Ambaye ni YESU KRISTO.
Mamasihi wengine ni kweli walipakwa mafuta na Mungu lakini hawakuwa wakamilifu asilimia zote..Daudi alikuwa ni masihi wa Bwana (Soma 1Samweli 16:6-13) lakini hakuwa mkamilifu asilimia zote, kwani aliua na pia alimtwaa mke wa Uria na kumfanya wake.
Vile vile Mfalme Sauli maandiko yanasema alikuwa ni masihi wa Bwana lakini tunasoma alikuja kukengeuka na kumdharau Mungu na maagizo yake..
1Samweli 24:9 “Daudi akamwambia Sauli, Kwa nini unasikiliza maneno ya watu wasemao, Tazama, Daudi anataka kukudhuru?
10 Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi Bwana alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA”.
Soma pia 1Nyakati 16:22
Hawa wote walikuwa ni watiwa mafuta lakni walikuwa na kasoro nyingi, Lakini Yesu Kristo alikuwa ni mkamilifu kuliko hao wote..Kwahiyo yeye ndiye aliyetiwa Mafuta Makuu kuliko wote, ndio maana tunasema aliye Masihi peke yake ni YESU.
Waebrania 1:8 “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio”.
Kwahiyo Wayahudi wote, na wasamaria wote, walikuwa wanautazamia ujio wa huyu Masihi mmoja ambaye atakuwa mkamilifu, asiyekuwa na dhambi hata moja, ambaye atawafundisha sheria za Mungu na kuwaokoa na dhambi zao.
Yohana 4:25 “Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.
26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye”
Yohana 1:40 “Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.
41 Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). .
Huyu Masihi Yesu Kristo, alishakuja miaka zaidi ya elfu 2 iliyopita, akapaa mbinguni, na sasa yupo hai, na pia amekaribia sana kurudi. Atakapokuja hatakuja tena kwa kusudi la wokovu, bali kwa HUKUMU.
Yohana 5:22 “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote”
Je umemwamini Masihi Yesu?.. Umetii agizo lake la ubatizo?, na je umempokea Roho wake Mtakatifu.. Fahamu kuwa kama umekosa vitu hivyo vitatu, bado hujaokolewa kulingana na Neno lake. Hivyo ni vyema ukafanya uamuzi wa kumwamini na kutubu leo na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, na mambo mengine yaliyosalia Roho Mtakatifu utakayempokea atakuongoza katika kweli yote.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JUMA LA SABINI (70) LA DANIELI
Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi?
Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?
Jibu: Tiro na Sidoni ni miji iliyokuwa katika nchi inayoitwa LEBANONI. Tofauti na nchi nyingine ambazo zilibadilika majina baada ya miaka mingi kupita, lakini nchi ya Lebanoni, imeitwa kwa jina hilo hilo tangu nyakati za biblia hata leo.
Tiro na Sidoni ni miji ambayo ipo karibu karibu, (Kusini Mashariki mwa Nchi ya Lebanoni), na miji hii enzi za biblia ilikuwa ni miji ya kibiashara, lakini iliyojaa machukizo mengi.
Kwasasa nchi ya Lebanoni ina miji mikubwa minne, Ambayo ni Beiruti, Tripoli, Sidoni na Tiro. Mji wa Sidoni ni mkubwa kuliko Tiro na katika Lebanoni ndiko ulipokuwepo pia Mji wa Tarshishi, ule ambao Yona aliukimbilia ili apate kujiepusha na uso wa Bwana.
Kwasasa nchi hii ya Lebanoni inakaliwa na Waarabu, na ni nchi ambayo ipo katika upande wa Kaskazini mwa Israeli, Eneo kubwa la Nchi ya Lebanoni, ni misitu na ndio huko Mfalme Sulemani alipotolea Miti aina ya Mierezi kwaajili ya ujenzi wa Hekalu la Mungu.
Nchi ya Lebanoni kwasasa ina uadui mkubwa sana na Nchi ya Israeli. Na unabii unaonyesha katika Ezekieli 38 na 39 kuwa siku za mwisho Lebanoni pamoja na nchi za kando kando zitashirikiana na Nchi ya Urusi kwa lengo la kuifuta Israeli katika uso wa dunia, lakini zitapigwa zote, kwasababu Mungu wakati huo atasimama upande wa watu wake Israeli.
Kwaufupi miji ya Tiro na Sidoni imebeba ufunuo mkubwa katika matukio ndani ya biblia. Kasome Mathayo 11:21-22, Yoeli 3:4, Zekaria 9:1-4, na Matendo 12:20
Lakini lililo kubwa zaidi ni ufunuo mji huo uliobeba, kumhusu shetani.. Biblia inamtaja mkuu wa Mji wa Tiro katika ulimwengu wa roho, kwamba ni shetani mwenyewe.
Ezekieli 28:1 “Neno la Bwana likanijia tena, kusema,
2 Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu……
13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.
14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako”.
Na shetani si mkuu tu wa Tiro, bali biblia imezidi kutupa mwangaza kuwa ni mungu wa ulimwengu mzima (2Wakorintho 4:4).. Yaani mifumo yote ya kishetani iliyopo duniani ni yeye muasisi.
Je umempokea Yesu?
Kumbuka hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo Mlangoni.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Kwanini Herode aliwakasirikia watu wa Tiro na Sidoni? (Matendo 12:20)
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
Swali: Katika Mwanzo 3:20 na Mwanzo 4:1 mkewe Adamu ni Hawa. Nmekuwa nikisikia mkewe Adamu pia ni Eva. Je! jina Eva na Hawa ni sawa?
Jibu: Hawa na Eva ni jina moja isipokuwa katika lugha mbili tofauti ni sawa na jina YESU na JESUS; ni jina moja isipokuwa katika lugha mbili tofauti, yaani ya kiingereza na ya kiswahili.
Kadhalika na Eva (au Eve) ni kiingereza na HAWA ni kiswahili chake.
Sasa swali ni kwanini, tafsiri zake zionekane kama mbalimbali, yaani Kutoka Eve mpaka Hawa ni kama hazikaribiani?. Kwanini Eve isingetafsiriwa tu Eva kwa lugha ya kiswahili badala yake ikawa Hawa?
Jibu ni kwamba lugha ya kiswahili sehemu nyingi imeitafsiri herufi “V” kwa “W” katika majina ya watu au vitu. Kwamfano utaona jina “LAWI”, kwa lugha ya kiingereza ni “LEVI”.
Vilevile mji wa “Ninawi” kwa lugha ya kiingereza ni “NINEVEH”n.k
Kwahiyo hata Eva kiswahili chake ni lazima kirudi kwenye herufi “w” na kuwa “Hawa”
Ni kama vile majina yote yanayoanza na herufi “J” yanavyobadilika na kuanza na herufi “Y” yanapokuja katika lugha ya kiswahili…Kwamfano Jina Jesus-Yesu, Jonah-Yona, Joshua-Yoshua, Jezebel- Yezebeli n.k Ndivyo ilivyo kwa majina yote yenye herufi “V”, yalibadilika na kuwa “W” yanapoletwa katika lugha ya kiswahili.
Kwahiyo kwa hitimisho mtu anayetumia Jina Hawa na anayetumia Eva wote wapo sahihi, na wanamlenga mtu mmoja.
Je umempokea Yesu?..je umebatizwa?..je umepokea Roho Mtakatifu?..Kama bado unasubiri nini?. Kumbuka hizi ni nyakati za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi.
Maran atha!.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!
Je! dhambi zote ni sawa Kuna dhambi kubwa na ndogo?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;(Mithali 16:2)
Jibu: Tusome kuanzia ule wa 2 ili tuweze kuelewa vizuri.
Ayubu 24:2 “Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.
3 Humfukuza punda wake asiye baba, Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.”.
Hapa Ayubu anazungumzia juu ya kundi la watu wabaya ambao wanawaonea Mayatima na kuwadhulumu wajane.
Ndio hapo anasema wapo (watu duniani) ambao.
1. Wanaondoa alama za Mipaka, na kuyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.
Maana yake wanawadhulumu watu mashamba/ardhi kwa kuondoa mipaka iliyokuwepo na kuweka mipaka ya uongo!,..na baada ya kumiliki ardhi kwa dhuluma namna hiyo bado wanalisha mifugo yao juu ya hizo ardhi za dhuluma.
2. Humfukuza punda wake asiye baba,
Maana yake humfukuza Punda wa Yatima, (mtoto asiye na Baba). Punda wake anapoingia mahali kula vichache vilivyosalia katika mashamba yao, wao humfukuza punda Yule, pasipo kuzingatia kuwa Yule ni yatima asiye na uwezo wa kujimudu mwenyewe, asiye na uwezo wa kununulia chakula punda wake, lakini wao hawajali hayo yote, bali wanazifukuza punda zake.
3. Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.
Hawa watu pia wanachukua Ng’ombe za wanawake wajane, ambao wamefiwa na waume zao, na hata nguvu za kufanya kazi tena hawana!.. wanachukua Ng’ombe zao na kuwaweka Rehani, kutokana na mikopo wanawake hao waliyoichukua.. Jambo ambalo ambalo si jema machoni pa Mungu..Wangepaswa wawahurumie na kuwapa mikopo bila kuwawekea rehani chochote kwasababu wao hawana tumaini msaada wowote wapo wao kama wao, na umri wao umeshakwenda..
Kumbukumbu 24:17 “Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;
18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili”
Hivyo watu wa namna hii ambao wanawatesa Wajane na Mayatima, Bwana Mungu alitaja hukumu yao katika kitabu cha Kutoka 22:22
Kutoka 22: 22 “Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.
23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima”.
Hivyo na sisi hatuna budi kuwatendea Mema watu hawa, na kuwapenda ili na Bwana atubariki
Shalom
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?
Kwanini wajane vijana hawakupaswa kuandikwa?
NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?
TENDA AGIZO LA YESU, HILO NDIO LITAKALOKULINDA.