Biblia inatuambia tabia mojawapo ya shetani ni “kuzunguka zunguka”, na sikuzote tunajua mzungukaji huwa na tabia Fulani ya udadisi na hiyo inafanya mwisho wa siku kuwa na tabia ya kupenda kuteka pia, kwasababu mahali alipo anaona hapamtoshi na hivyo anaamua kutoka na kwenda kuchunguza chunguza maeneo mengine na huko huko akiona upenyo mdogo tu au fursa fulani huwa anaitumia ipasavyo kutimiza matakwa yake mwenyewe..Na ndio maana jina Mzungu, limetokana na Neno mzungukaji, watu waliotoka bara la ulaya zamani walikuwa wakizunguka zunguka nchi mbalimbali na mabara mbalimbali duniani ili kutafuta rasilimali kwa ajili ya nchi zao, Na walipofika maeneo kama Afrika, na kuona kuna kila kitu na vile vitu walivyokuwa wanavitafuta ndipo wakatua hapo, na kufanya yaliyo yao na hata kutumia fursa hiyo kuteka watu na kuwatawala…
Vivyo hivyo na shetani naye, ni mzungukaji kufanikiwa kwake kunategemea kuzunguka zunguka huku na huko duniani, anajua asipofanya hivyo kabisa hawezi kufanikiwa kuuimarisha ufalme wake, Tukisoma kwenye maandiko katika kitabu cha Ayubu tunaona wakati Fulani malaika wa Bwana walipokwenda kujihudhurisha mbele za Mungu, shetani naye alikwenda katikati yao, ndipo Mungu akamuuliza maneno haya..
Ayubu 1:7 “Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo”.
Unaona hapo, anasema duniani, ikiwa na maana kila kona ya dunia alikuwa anazunguka zunguka, inamaana hata katika kila taasisi, kila shirika, kila dini, na katika kila nchi, na ndio maana hatushangai kumwona shetani yupo hata katikati ya kanisa la Mungu. Na lengo lake kubwa sio kutalii, hapana bali ni kuchukua mateka, na kuharibu kile kinachoonesha dalili ya kuinuka na kufanikiwa kwa ajili ya Bwana..Ukitaka kujua ukali wa shetani na jinsi anavyomchukia mwanadamu kwa namna isiyokuwa ya kawaida angali tu kitu alichomfanyia Ayubu baada ya Mungu kuuondoa ule ulinzi wake kwake..
Utaona bila kupoteza muda alimletea radi, ikawapiga wale kondoo wake wote, akanusurika Yule mtu mmoja aliyemletea taarifa ambaye alimwambia nimeona moto wa Mungu umeshuka, ilikuwa ni radii ile, sio moto tu kama moto, Hata wewe vile vile anaweza kukutengenezea radi ikiwa tu upo nje ya ulinzi wa Mungu, yaani nje ya wokovu, hiyo ndio kazi inayomfanya azungukezunguke duniani.
Utaona tena Muda huo huo akaandaa majeshi ya maadui, yakawavamia wafugaji wake yakawaua wote, halafu yakaondoka na mifugo, vivyo hivyo hata wewe anaweza akakuundia tu kikundi cha vibaka wakati unakatiza usiku umetoka labda kwenye shughuli zako, wakakuvamia na kukuchoma visu wakaondoka na fedha zako na wewe ukafa saa hiyo hiyo ikiwa tu haupo ndani ya wokovu..
Wakati huo huo tena Shetani akamletea upepo wenye nguvu ukaipiga ile nyumba ikawaangukia watoto wake wote wakafa, hashindwi kukuletea kipunga hapo ulipo umekaa kwa amani, au mafuriko, na kukusababishia tu ajali ambayo chanzo chake hakieleweki, hata gesi tu kukulipukia nyumbani, hashindwi kukufanyia hivyo au shoti kutokea nyumbani au kung’atwa na nyoka tu njiani na habari yako ikawa imeishia hapo,..hashindwi kufanya hivyo vyote kwa mtu ambaye ulinzi wa Mungu haupo juu yake.
Utaona tena Shetani akimeletea Ayubu mpaka magonjwa ambayo hajawahi kuumwa, Leo hii usijione unayo afya na bado upo nje ya wokovu ukadhani wewe unayo kinga kubwa zaidi ya wengine waliopo mahospitalini ndio maana huugui ugui ovyo, shetani anao uwezo wa kukutupia hapo hata kansa usijue imetokea wapi, au ugonjwa wa ajabu ajabu usiojulikana, na ukafa ndani ya siku tatu tu…
Hayo ndio matunda ya shetani ya kuzunguka zunguka kwake ni ili tu kutafuta mtu wa kummeza basi.. Na kumbuka lengo lake sio kukuangamiza tu halafu basi hapana bali ni anataka ufe haraka katika hiyo hali hiyo hiyo ya dhambi uliyonayo sasa ili uende kuzimu moja kwa moja hilo ndio lengo lake…kwasababu anajua akizidi kuchelewa pengine neema ya Mungu inaweza kukupitia ukatubu siku moja.
Na ndio maana Biblia inazidi kutuhimiza maneno haya..
1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
9 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.’’
Unaona ni jinsi gani shetani anavyokuchukia wewe uliye kwenye dhambi, kama sio huruma za Mungu tu kumzuia shetani tayari angeshakuangamiza siku nyingi…
Hivyo kama unahitaji kumruhusu leo Bwana aingie maishani mwako, utakuwa umefanya uamuzi wa busara, hapo ulipo tubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote, na kwamba unamaanisha kutokurudia yale yote maovu uliyokuwa unayafanya huko nyuma, Kisha mwambie Bwana Yesu nisamehe na nakukaribisha uje katika maisha yangu….Na ukishamaliza kumweleza mambo hayo yote kwa kumaanisha kabisa, hatua inayofuata tafuta mahali ukabatizwe ili kukamilisha wokovu wako, kumbuka ubatizo ni muhimu, na ni maagizo ya msingi kwa yeyote aliyempokea Bwana, Usipuuzie, ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi ni wa kuzingatia na uwe ni kwa jina la BWANA YESU KRISTO sawasawa na maandiko haya (Matendo 2:38, 8:16, 10:48, 19:5).
Hivyo ukikamilisha hayo, Bwana mwenyewe atakupa Roho wake Mtakatifu, naye atakaa na wewe milele kukulinda dhidi ya Yule adui azururaye huko na huko, mpaka ile siku ya mwisho ya kwenda mbinguni itakapofika.
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
UNALITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI?.
Shalom mtu wa Mungu, karibu tujifunze Maandiko..Biblia inatuasa tuwe tunajikumbusha kila siku yale ambayo tumeshajifunza ( 2 Petro 1:12-13, Yuda 1:5), hiyo itatusaidia kutompa nafasi shetani kuziiba zile mbegu ambazo zilishapandwa ndani yetu tayari…Leo kwa Neema za Bwana tutajikumbusha ni kwa jinsi gani Ulimwengu utahukumiwa na watakatifu.
Ni jambo la kufurahisha kuona bado kuna watakatifu ulimwenguni, watu wanaojitunza na kumweshimu Mungu, kwa viwango vya juu…kuona bado kuna watu wanamcha Mungu, kuna wanawake na wanaume wanaojiheshimu, kuona kuwa bado kuna watu ni wapole, ni wasomaji na watendaji wa Neno, ni wavumilivu, wasikivu, wenye huruma, wasiolipiza kisasi, wenye mioyo ya Toba, na wenye kuwahurumia wengine n.k Haijalishi watakuwa ni wachache kiasi gani, lakini uwepo wao tayari ni Tiba kubwa kwa ulimwengu.
Jambo lisilojulikana na wengi ni kuwa Uwepo wa Watakatifu duniani leo hii, ndio unaosababisha ulimwengu usiangamizwe…Bwana akitazama katika mji mmoja na kuona maovu yaliyomo ndani ya huo mji, na akaona huko watakatifu watano, basi huo mji wote unaweza ukasalimika kwasababu tu ya hao watakatifu watano waliopo ndani ya Huo mji. Na siku maangamizi ya Huu ulimwengu yatakapokuja Bwana atakuwa ameshawaondoa watakatifu wake kwa kuwanyakua, haiwezekani kuwaangamiza watakatifu wake pamoja na waovu. Ndio maana utaona Bwana alitamani kuuhurumia mji wa Sodoma na Ghomora endapo tu angekuta huko watu kumi tu walio wakamilifu, lakini hawakuwepo hata hao kumi..Na zaidi ya yote, hata Lutu huyo mmoja aliyesalia walimdharau. Na hivyo kujisababishia maangamizi yao….Hiyo ndiyo Neema wanayoibeba watakatifu waliopo katika ulimwengu sasa…
Lakini katika upande wa pili wa shilingi, Uwepo wa Watakatifu mahali fulani pia ni Ishara mbaya kwa ulimwengu…Kwasababu hao hao watakatifu ambao kwa kupitia wao Mungu anairehemu dunia, hao hao siku ya Hukumu watauhukumu Ulimwengu. Biblia inasema hivyo katika
1 Wakorintho 6:2 “Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu?……”
Sasa utauliza Watakatifu wataihukumu vipi dunia?..Na nafasi ya Bwana Yesu ya kuhukumu itakuwa ni ipi Kama watakatifu wataihukumu dunia?, Na pia inawezekanikaje siku ile mtu amhukumu ndugu yake ambaye alikuwa anamfahamu?.
Kuelewa Hukumu itakuwaje siku ile, hebu tafakari mfano ufuatao.
Mwalimu alikuwa na darasa lake la wanafunzi 10 la wanafunzi wa Bweni, akawafundisha kwa mwaka mzima, kisha mwisho wa mwaka akawapa mtihani, wawili kati ya hao 10 walipata alama ‘A’ na nane kati yao wakapata alama ya mwisho kabisa ‘F’. Mwalimu akafurahi kuona amepata wanafunzi wawili waliofaulu vizuri, lakini akahuzunika kuona Zaidi ya robo tatu wamefeli na kupata alama ya mwisho kabisa ‘F’…tena miongoni mwa hao waliopata F kuna wengine wamepata sifuri kabisa. Akawapatia zawadi wale wawili, kwa kuwapandisha daraja la juu na wale 8 akawapa barua ya kuwafukuza shule.
Lakini wale waliofukuzwa wakaanza kumlalamikia kwanini tumefukuzwa…Mwalimu akawaambia ni kwasababu mmefeli mtihani, wakaanza kila mmoja kulalamika…oo ni kwasababu Umetoa kitu ambacho hujatufundisha, wengine wakasema oo ni kwasababu mazingira ya shule hayakuwa mazuri, wengine wakasema oo ni kwasababu chakula kilikuwa kibovu kila siku mlo ule ule tu! Ndio maana tukashindwa kula vizuri na kupelekea kufeli, wengine wakasema tunaomba utupe nafasi ya pili.
Mwalimu akawauliza swali moja wote! Je! Hao waliopata alama ‘A’ hawakuwa kwenye mazingira kama hayo hayo ya kwenu? Ndio mwalimu akaamua kumuita mmoja wa hao waliopata alama ‘A’ mbele yao na kuanza kumhoji na kumwuliza…
Je! Wewe ulikuwa unakula chakula kizuri sana tofuati na hawa ndio ikakusababishia kufaulu, yule akajibu hapana mwalimu, nilikula chakula kimoja na hao, isipokuwa mimi nilikuwa sio mnung’unikaji kama wao nilijua tu hapa shuleni napita hivyo nilivumilia tu shida za kitambo hizi na nikaweka jitihada yangu yote kwenye masomo…akaulizwa tena je! Ulikuwa unalala kwenye kitanda kizuri Zaidi ya wengine, akasema hapana!..akaulizwa na swali la mwisho je! Katika mtihani uliofanya ulikutana na swali ambalo mimi sikuwahi kuwafundisha darasani?…akasema hapana! Maswali yote uliyoyatoa uliyafundisha darasani ndio maana mimi nimeweza kuyajibu mengi ya hayo kifasaha..
Baada ya mwalimu kumwuliza hayo maswali, akawageukia wale wanafunzi 8 waliofeli akawaambia..mnasikia anachosema mwenzenu?..Huyo ndiye anayewahukumu sio mimi…mlilala wote pamoja, mlikula wote chakula kimoja, wote mlikuwa darasa moja…lakini tofauti yenu ni kwamba ninyi hamkuwa makini na shule, na pia hamkujua kilichowapeleka shuleni ndio maana mkafeli kwahiyo ni haki yenu kufukuzwa shule. Kwasababu mlipitia mazingira sawasawa na ya wenzenu waliofaulu lakini nyinyi hamkuzingatia, mlipaswa mvumilie na kujituma kama wenzenu hata kama chakula kilikuwa ni mlo mmoja kila siku. Wale wanafunzi walikosa cha kujitetea na wakaondoshwa shuleni.
Ndugu yangu ndivyo itakavyokuwa siku ile ya Hukumu, Bwana atawahukumu wenye dhambi wote kulingana na matendo yao mbele ya kile kiti cheupe! Atawaambia wamefeli mtihani wa haya Maisha, na hivyo watashushwa daraja la chini (ambalo ni ziwa la Moto), Majina yao hayataonekana katika Kitabu cha uzima hivyo wataondolewa mbele yake, Kwasababu kila mtu sasahivi anafanya mtihani wake na kuandika kitabu chake…Na wengi watakaosikia hiyo hukumu wataanza kulalamika kuwa wanaonewa, wengine watasema Ulimwengu ulikuwa umejaa vishawishi tungewezaje kushinda! Wakubwa kwa wadogo, matajiri kwa maskini, kila mtu ataanza kutoa malalamiko yake..Ndipo yule aliyeketi katika kile kiti cha hukumu, atawaita watakatifu walioshinda ulimwenguni na kuwahoji mbele yao. Na hao waliohukumiwa watakosa cha kujitetea mbele yao, Kwahiyo wataenda kwenye lile ziwa la moto kwa huzuni na majuto makubwa, wakijua kuwa ni kweli wamestahili.
Ndugu wakati leo hii unaona wapo watakatifu wanaojituma kweli katika Mungu, hao sio ishara nzuri kwako, siku ile ya Hukumu watakuhukumu…Utasema Bwana mbona ilikuwa ni ngumu sana mimi kuacha uasherati kwenye kizazi changu ambacho kila kona ya barabara nilipishana na wanawake wapo nusu uchi? Nikifungua tv, internet, radio nakutana na mambo yavishawishi vya uasherati? Bwana atamleta mmoja ambaye alikuwepo kwenye hicho hicho kizazi chako, ambaye naye pia alikuwa anapitia majaribu kama ya kwako na hata pengine Zaidi hata na hayo yako kama vile Yusufu na akashinda uasherati na wewe utakosa cha kujitetea siku hiyo..
Utasema mbona mimi nilikuwa mzuri sana ningewezaje kushinda vishawishi mahali ambapo kila kona watu walikuwa wananitaka?..simalizi hatua mbili kila mwanamume ananijaribu? Siku ile watasimamishwa waliokuwa wazuri kuliko wewe mfano wa Sara katika kizazi chako, na pamoja na kwamba walikuwa ni wazuri sana, lakini walishinda vishawishi, na kujihadhari na ulimwengu, utakosa cha kujitetea siku ile.
Utasema nitawezaje kutubu na kumgeukia Kristo ninaposikia injili, si kila mtu atanicheka na kuniona mwendawazimu, nitawezaje kuacha Imani yangu na dini yangu, na dhehebu langu nililolizoea? Na kutubu na kumgeukia Kristo kikamilifu?…Biblia inasema katika Mathayo 12: 41 “Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona”
Utasema tena Bwana mimi nilikuwa ni Tajiri sana, nilikuwa ni Mkuu wa Wilaya, ningewezaje kupata muda wa kukutafuta wewe?..Siku ile watasimamishwa waliokuwa matajiri kuliko wewe katika wakati wako na katika utajiri wao wote walimtafuta Mungu na kujiepusha na ulimwengu. Biblia inasema katika..
Mathayo 12: 42 “Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani”
..Malkia anasafiri maelfu ya Maili…kwenda kuitafuta Hekima ya Mungu, wewe Balozi wa nyumba kumi huna muda! Siku ile hutakuwa na la kujibu.
Kwahiyo uonapo! Mtu mwema anafanya wema katika mazingira yasiyostahili wema..usiishie kufurahia tu! Bali pia Ujiulize nawe pia unafanya wema kama yeye katika mazingira kama yake?..Kwasababu kama hufanyi hivyo siku ile hutakuwa na cha kujitetea, na wala hutapata mtetezi…Dada uonapo kuna mwanamke mzuri kuliko wewe anavaa kwa kujisitiri pamoja na uzuri wake wote..usifikiri utakuwa na cha kujitetea siku ile ya hukumu mbele za Mungu, utaelekea kwenye Ziwa la Moto, na utasema ni kweli umestahili.
Unapoona kuna watu wanamtafuta Mungu katika kizazi chako cha uovu..Usiishie kufurahia tu! Na kusema nakushukuru Mungu!…Tambua kuwa kitendo wafanyacho huko mbeleni kitakuja kugeuka kuwa mashitaka kwa wasiomtafuta Mungu katika kizazi hicho hicho kigumu.
Bwana akubariki sana. Ni matumaini yangu kuwa umepata kitu, kama hujampa Kristo Maisha yako, mlango wa Neema haujafungwa, lakini siku si nyingi utafungwa, watakatifu wataondolewa duniani na kunyakuliwa juu mbinguni, na dhiki kuu kuanza duniani. Je! Bado ni vuguvugu?..bado unaupenda ulimwengu na anasa zake! Shetani anakudanganya kuwa hakuna watu wanaomcha Mungu duniani leo?…usidanganyike Mungu ana watu wake kila mahali, shetani anachotaka ni wewe uendelee kufikiri hivyo ili siku ile ya hukumu, uhukumiwe vizuri na Maisha ya watakatifu waliopo leo duniani.
Baada ya kutubu kama ulikuwa hujatubu, ni Ubatizo, ubatizo sahihi ni ule wa kuzama mwili wote katika maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu.
Mada Nyinginezo:
Danieli 12:3 “Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.”
Yuda 1:12 “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa;
13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; NI NYOTA ZIPOTEAZO, AMBAO WEUSI WA GIZA NDIO AKIBA YAO WALIOWEKEWA MILELE”.
Amosi 5: 8 “mtafuteni YEYE AFANYAYE KILIMIA NA ORIONI, NA KUKIGEUZA KIVULI CHA MAUTI KUWA ASUBUHI, NA KUUFANYA MCHANA KUWA giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; Bwana, ndilo jina lake;”
Ayubu 9:7 “Aliamuruye jua, nalo halichomozi; Nazo nyota huzipiga muhuri.
8 Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu, Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9 Yeye afanyaye hizo NYOTA ZA DUBU, na ORIONI, na hicho KILIMIA, Na makundi ya nyota ya kusini”.
Ayubu 38: 31 “Je! Waweza kuufunga mnyororo wa KILIMIA, Au kuvilegeza vifungo vya ORIONI?
32 Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake?….”
Mada Nyinginezo:
INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA.
HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).
MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.
SIRI YA KUASI KATIKA KANISA LA MUNGU.
Kwanini maombi ya Usiku yana nguvu kuliko ya mchana?
Kadhalika usiku wakati watu wamelala ndio wakati Adui anaiba vipawa vya watu..Kwahiyo unapokwenda kusali usiku, maana yake, unaingia kwenye uwanja wa mapambano uso kwa uso na Adui yako na ni rahisi kumwangusha..Kwahiyo yanakuwa ni maombi ya shabaha..Na yana madhara makubwa kwa shetani na ufalme wake.
Shetani hapendi watu wasali usiku kwasababu anajua madhara yatakayomfikia.
Bwana akubariki. Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP
Mada Nyinginezo:
Mbinguni ni mahali mbali sana na upeo wetu wa kufikiri, na umbali huo haupo katika mfumo wa kilometa, au maili hapana! bali kiufahamu…Katika miili hii ya damu na Nyama hatuwezi kufika mbinguni. Ni sawa uwaambie paka wote duniani au mbwa wote duniani, wajikusanye wafanye bidii wafike kwenye wafike kwenye kifaa kilichotengenezwa na wanadamu kinachoitwa satelite kilichopo kule juu sana mawinguni..
Unaona? jambo hilo haliwezekani..kwanini? kwasababu wao upeo wao upo mbali sana na upeo wa wanadamu…Ili wafike kwenye satelite kule mbinguni ni sharti kwanza wawe wanadamu, wawe na ufahamu kama wa wanadamu ndipo waweze kufika kule.
Kadhalika na sisi tunahitaji kubadilishwa miili yetu, ifanane na malaika ndipo tuweze kufika mbinguni. Kwa jitihada zetu sisi kamwe hatuwezi kufika mbinguni, Malaika watakatifu walipo
Ubarikiwe!
Mada Nyinginezo:
NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?
JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?
JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?
JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?
KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?
Mpaka umefikia kuuliza hili swali, naimani ni mtu unayependa kuabudu kitu unachokifahamu..Na pia naamini unapouliza dini ya kweli ni ipi unamaanisha kuwa ni Imani ipi ya kweli..Leo duniani zipo dini zaidi ya 4300 zinazofuatwa na wengi, hiyo ni mbali na madhehebu na vikundi vidogo vidogo, vikihesabiwa na hivyo hata laki vinafika..Na kila moja inadai kuwa Mungu wake ni sahihi..Mpaka unashindwa kujua Mungu wa kweli yupo wapi,
Upo katika tovuti hii, ambayo ni ya kikristo, mfano nikikupa jibu la haraka kuwa ukristo ndio Imani sahihi, bila shaka unaweza ukaamini kuwa huyu mtu anataka kunivuta kwake. Vivyo hivyo ukienda na kwingine, Hivyo maneno matupi hata yakijaza dunia, hayawezi kubatilisha ukweli wa maneno matano tu.
Hivyo ikiwa kweli umekusudia kufahamu Dini ya kweli, na Mungu wa kweli, jambo ni rahisi, Mungu aliye Mungu wa kweli sikuzote huwa anajitetea mwenyewe na wala hajitetei…Hivyo kama umemaanisha kweli kumtafuta Mungu huyo tenga muda wako mwenyewe binafsi kisha piga magoti, halafu omba kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni, usipomaanisha hakuna kitu kinachoweza kukutokea mwambie Ee Mungu wa kweli jidhihirishe kwangu na nionyeshe njia ya kweli na dini ya kweli ya kukufikia wewe..
Ukishamaliza kuomba basi wewe tulia, njia atakayoileta mbele yako ifuate, mimi siwezi kukuelezea atakujibuje jibuje lakini akikujibu utafahamu kuwa amekujibu kwa mambo yatakayofuatana na wewe baada ya hapo.
Fanya hivyo na Mungu wa kweli bila shaka atajidhihirisha kwako, na huyo ndiye umfuate kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote na kwa roho yako yote.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
Dini ni nini? Dini ya kweli ni ipi? na Imani ya kweli ni ipi?
Dini ni tendo linalotokana na Imani fulani (mambo ya rohoni), pale tu mtu anapoamini uwepo wa Mungu au hata uwepo wa shetani au hata kitu chochote kisichoonekana cha kuabudiwa basi hapo hapo dini inazaliwa, ndipo hapo utaona mtu anajiwekea miiko Fulani ya kufuata au utaratibu Fulani au ustaarabu Fulani kwamfano wanaoamwamini Buddha utaona wanao taratibu zao za kufuata ili kumwabudu mungu wao ipasavyo ndipo hapo utakuta ni lazima wote wavae mavazi Fulani, au wapitie madarasa Fulani, au waishi maisha Fulani ya kujinyima au kutokushirikiana na jamii Fulani ya watu au kufunga, au kutokula aina Fulani ya vyakula n.k sasa hiyo ndiyo inayoitwa dini..
Vivyo hivyo na katika ukristo, mtu yeyote mwenye imani ya kweli ya YESU Kristo ni lazima atakuwa na kiwango Fulani cha dini ndani yake, kwamfano ukiwa mkristo ni lazima utajikuta wewe mwenyewe unajijengea utaratibu wa kuomba kila siku, utajikuta unajijengea utaratibu wa kufunga mara kwa mara, licha tu ya biblia kuagiza lakini utajikuta unahudhuria ibada kanisani kila wakati, utajikuta unajijengea utaratibu wa kutoa sadaka na kuwasaidia na wengine n.k.…Na ndio maana biblia inasema..
Yakobo 1:26 “Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.
27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”
Hivyo dini ya kweli ni ipi? Ni hiyo hapo juu kwenye mstari wa 27..Lakini sasa hiyo haimpi tiketi ya moja kwa moja kwenda mbinguni , bali inamrahishia tu njia ya kwenda mbinguni..tofauti na Imani nyingine kwao kushika dini ndio kuokoka, lakini katika ukristo usipomwamini YESU KRISTO na kuoshwa dhambi zako katika damu yake hata kama unashika dini vipi mbinguni huwezi kwenda…
Unaweza ukawa unafunga lakini kama maisha yako yapo mbali na Kristo kuzimu utakwenda, unaweza ukawa unahudhuria ibada kila siku na kushika mambo yote unayoambiwa kanisani kwako kufanya lakini kama hauna Roho Mtakatifu ni bure…Tofauti na dini nyingine ambao kwao dini ni kitu cha kujivunia..
Hivyo kwa ufupi Dini ni njema kama itakuwa imeambata na imani ya kweli ipasavyo, ni sawa na shule yenye maabara na walimu wazuri, inamjengea mwanafunzi mazingira mazuri ya kufaulu siku za mwisho lakini shule pekee haimfanyi mwanafunzi afaulu mitihani kama hatakuwa na bidii yake binafsi..
Baada ya kujua dini ni nini na dini ya ukweli ni ipi…Ni vizuri kujua Imani ya kweli ni ipi?..Imani ya kweli ni ile iliyopo katika kumwamini Yesu Kristo kama mwana wa Mungu na aliyetumwa kuja kuwaokoa wanadamu. Hiyo ndiyo imani ya kweli..Imani nyingine tofauti na hiyo ni imani ya uongo na unayopotosha na kupeleka watu mautini.
Hivyo huu Si wakati wa kijivunia dini tena…bali kujivunia wokovu katika Yesu Kristo…Hivyo kama hujaokoka na kuingia katika Imani ya kumwamini Yesu Kristo..Bado hujachelewa ingawa mlango wa Neema upo karibuni kufungwa hivyo mgeukie Kristo leo kwa kutubu dhambi zako zote na kuoshwa kwa damu yake, naye atakusamehe na kukurehemu.
Bwana akubariki sana.
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
KUNA TOFAUTI GANI KATI YA SALA NA DUA?
JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
NI NINI KINAKUPATA UNAPOIPUUZIA INJILI?
KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.
Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia;tukiomba kwa Babaye, maombi asikiyaLakini twajikosesha, twajitweka vibaya; kwamba tulimwomba Mungu, dua angesikia.
Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia.Haifai kufa moyo, dua atasikia.Hakuna mwingine mwema, wa kutuhurumia;atujua tu dhaifu; maombi asikia.
Je hunayo hata nguvu, huwezi kwendelea,ujapodharauliwa, ujaporushwa pia.Watu wangekudharau, wapendao dunia,hukwambata mikononi, dua atasikia.
Joseph Scriven alizaliwa mnamo 1819 katika familia ya kitajiri huko Banbridge, County Down, Ireland. Alihitimu digrii yake kutoka Chuo cha Trinity, huko Dublin mnamo 1842. Mpenzi wake alizama kwenye maji na kufa kwa bahati mbaya mnamo 1843, usiku kabla ya kuolewa.
Mnamo 1845, akiwa na umri wa miaka 25, aliondoka nchi yake ya asili na kuhamia Canada, na kukaa Woodwood, Ontario. Alibaki Canada kwa muda mfupi tu baada ya kuugua, lakini akarudi mnamo 1847
Mnamo 1855, alipokaa na James Sackville huko Bewdley, Ontario, kaskazini mwa Port Hope, alipokea habari kutoka kwa Ireland ya mama yake kuwa mgonjwa sana. Aliandika shairi la kumfariji mama yake inayoitwa “Omba bila Kukata tamaa”. Baadaye iliwekwa kwa muziki na ikabadilishwa jina na Charles Crozat Converse, ikawa wimbo wa “Yesu kwetu ni Rafiki”. Scriven hakuwa na dhamira yoyote wala ndoto kwamba shairi lake litakuja kuchapishwa kwenye gazeti na baadaye kuwa wimbo unaopendwa kati ya mamilioni ya Wakristo ulimwenguni.
Mada Nyinginezo:
NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE
JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?
SWALI: Mwanzo 29:16 “Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni Lea, na jina la mdogo ni Raheli. 17 Naye Lea macho yake yalikuwa DHAIFU, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso. 18 Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo.”
Hapo Anaposema macho ya Lea yalikuwa dhaifu:Ni Udhaifu wakutokuona mbali au ni udhaifu wa namna gani huo??
JIBU: Biblia haituambii macho yake yalikuwa ni dhaifu kwa namna gani, kwamba ni makengeza, au yaliyolegea, au yenye kasoro ya kimaumbile kwamba ni makubwa sana au madogo sana au yanayoona karibu au mbali, hatujui lakini tunachojua ni kuwa alipofananishwa na mwenzake, Raheli alionekana ni mzuri kuliko yeye,…
Lakini Mungu hakuangalia hilo kama kigezo cha kuliunda taifa la Israeli, kwamba ampendelee Raheli zaidi ya Lea katika wana, kisa tu yeye ni mzuri wa sura na kwamba Yakobo kampenda zaidi…hapana kwanza utaona Lea ndiye aliyepewa uzao mkubwa zaidi, karibu nusu ya makabila yote ya Israeli yalitoka kwake isitoshe lile kabila la Bwana wetu Yesu Kristo kabila la YUDA lililoshinda makabila yote lilitoka kwa Lea…
Hivyo hiyo inatufundisha pia kutokukubaliwa na watu haimaanishi kuwa hatujakubaliwa na Mungu, Yabesi alikuwa ni mtu aliyezaliwa katika huzuni mpaka mama yake akamwita jina hilo ambalo lilimaanisha huzuni, Lakini Yabesi alijitahidi kuishi katika amani kwa heshima, kuliko ndugu zake wote, mpaka ikafikia wakati akamuomba Mungu dua amfanikishe katika mambo yake na Mungu akaisikia dua yake, mpaka habari yake leo hii tunaisoma katika biblia (1Nyakati 4:9-10,) …Hivyo ulemavu wowote mtu alionao haimaanishi kuwa hawezi kuwa jemadari katika ufalme wa mbinguni.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
Kama mkristo ili uweze kuenenda kikamilifu katika safari yako ya wokovu hapa duniani bila dosari zozote zisizokuwa na sababu, ipo mistari miwili ya kuzingatia..
Wa kwanza ni huu:
Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.
Na wa pili ni huu
Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate KUISHI KWA KIASI, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Tukiweza kutembea na kanuni hizo mbili yaani kuishi kwa Kiasi na kufanya jambo lolote kwa kumshirikisha Mungu, basi tuwe na uhakika kuwa njema zetu zitanyooka, Sasa tukirudi kwenye swali lililoulizwa kuhusu picha za video (movies), hatuwezi kusema moja kwa moja usiangalie kabisa, ni kweli hakuna asiyejua movie nyingi hazina maudhui yoyote ya kumfaa au kumjenga mkristo lakini bado hatuwezi kusema ni zote, ni kama tu vipindi vya TV vipo vilivyo vizuri na vipo vilivyo vibaya, hivyo hatuwezi kumwambia mtu asiangalie TV kabisa kwasababu kuna vipindi vibaya vingi, hapo tutakuwa tumepoteza shabaha ya kulitibu tatizo..kwasababu kwenye TV pia kuna vipindi vya mahubiri na taarifa ya habari ambavyo kwa namna moja au nyingine vinaweza kumjenga mtu kiroho au kumfunza au kumjuza.
Lakini tukiwa na kiasi, inamaana kuwa hata tukitazama movie tutazama kwa kiasi tena zile tu ambazo zinaonekana kuwa na manufaa kwa mkristo, lakini leo hii utaona mtu anatazama series, kuanzia asubuhi mpaka jioni, hana muda wa kusali, hana muda wa kujisoma biblia, hana muda wa kwenda kanisani, hana muda wa kwenda fellowship, sasa hapo hata kama movie hiyo inayo maadili kiasi gani, lakini kwa kukosa tu kile kitu kinachoitwa kiasi tayari imekuwa ni kikwazo kwake na dhambi..
Vilevile utamwona mwingine anatazama tamthilia za mapenzi, au movie zilizojaa mambo maovu maovu tu, hajui kuwa moyo wa mwanadamu unatabia ya kujazwa na kile kinachofanywa, au kinachozungumzwa au kinachowazwa muda mrefu, kwa mfano ukiwa mtu wa kutafakari Neno la Mungu kila saa na kila wakati basi lile Neno linakuwa sehemu ya maisha yako..Vivyo hivyo ukiwa ni mtazamaji wa movie ambazo hazina vimelea vyovyote vya ki-Mungu ndani yake basi utakuwa mtu wa kufuatana na hivyo unavyovitazama,..Huko huko ndipo roho za uzinzi zinapozaliwa, na uuaji, na ulevi na matusi n.k…Na hiyo yote ni kwasababu hujazingatia lile Neno linalosema lolote mfanyalo kwa Neno au Kwa tendo fanyeni yote kwa jina la Yesu Kristo…Yaani kwa lugha nyepesi kufanya kwa jina la Yesu Kristo ni kabla hujafanya unaangalia je! Hichi ninachokitazama kina umuhimu gani katika maisha yangu ya rohoni…kama hakina unakiacha, kama kinayo unakitazama, huko ndio kufanya kwa jina la YESU.
Ukiweza kutembea na mistari hiyo miwili basi hakuna jambo lolote litakalokuwa dhambi kwako, sio movie, sio radio, sio tv, sio simu, sio computa n.k.
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?
JE NI SAWA KWA MKRISTO KUUZA MAZAO YA KUTENGENEZEA POMBE KAMA VILE MTAMA?
NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?