JIBU: Neno hilo halimaanishi kuwa hatupaswi kabisa kumwita mtu yeyote baba duniani hata wazazi wetu, hapana kama ni hivyo basi Mungu angekuwa anapingana na Neno lake pale aliposema “Waheshimu baba yako na mama yako (Kutoka 20:12)”
unaona?. Lakini tunapaswa kufahamu maneno hayo Bwana aliwalenga watu wa namna gani, ukisoma mistari hiyo kuanzia juu utaona kuwa aliwalenga wale mafarisayo na masadukayo ambao wao, walipenda kuchukua nafasi ya Mungu duniani kwa kila kitu, walitaka watu wawaone kama pasipo uwepo wao, hawawezi kumjua Mungu, pasipo watu kuongozwa na wao hawawezi kumfikia Mungu, yaani kwa ufupi walikuwa wanachukua nafasi ya Kristo duniani. Na ndio maana tukisoma tangu juu tunaona Bwana akiwaambia maneno haya..
Mathayo 23:1 “Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema,
2 Waandishi na Mafarisayo WAMEKETI KATIKA KITI CHA MUSA;
3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.
4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.
5 Tena matendo yao yote huyatenda ILI KUTAZAMWA NA WATU; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,
7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.
8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.
9 WALA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI; MAANA BABA YENU NI MMOJA, ALIYE WA MBINGUNI.
10 WALA MSIITWE VIONGOZI; MAANA KIONGOZI WENU NI MMOJA, NAYE NDIYE KRISTO”.
Mambo hayo hayo ndio tunayoweza kuyaona leo hii katika Kanisa la kirumi (Katoliki), ofisi ya kiPapa inajulikana kama “ofisi ya baba mtakatifu” na watu humweshimu yeye kama mpatanishi wa dhambi zao, na anaonekana kama ni mtu aliye na kibali cha karibu zaidi kwa Mungu zaidi ya watu wengine wote, hivyo amepewa heshima ya kipekee, anaketi mbele katika masinagogi (Katika umoja wa makanisa) ili atazamwe na ulimwengu wote kuwa yeye ni baba mtakatifu. Sasa Heshima kama hizo ambazo zinazohusianishwa na uhusiano na vyeo mbele za Mungu kwamba mtu Fulani ni mwenye cheo Fulani cha kipekee mbele za Mungu zaidi na wengine, ndizo Kristo alizokuwa anazikemea, kwamba tusimwite mtu yeyote Baba kwa namna hiyo, au kiongozi, au Rabi. Kwasababu sisi sote ni ndugu na hakuna aliye juu ya mwenziwe.
Pale Mtume Paulo alipomwita Timotheo na Tito wanae, alikuwa anaonyesha uhusiano aliokuwa nao kama mtumishi wa Mungu aliyewazaa katika injili, na kuwalea, kwa mfano wa Baba kwa mwanawe, lakini hakuwa na maana kuwa yeye yupo juu ya mwenzake, wala hakutanua hirizi zake wala kuongeza matamvua yeye, kiasi cha kukaa masokoni kupewa heshima na watu, kwamba ni sharti aanze yeye mbele za Mungu kisha wao, na kwamba pasipo yeye hawawezi kumfikia Mungu, Hapana na hakuna mahali popote Paulo alisisitiza yeye aitwa aitwe Baba.
Utaona nyaraka zake zote Mtume Paulo, alianza na “Mimi Paulo, mfungwa na Mtumwa wa Yesu, sehemu nyingine anasema mimi Paulo mtume wa Yesu Kristo”..Lakini hutaona sehemu yoyote anaanza kwa kusema “Mimi Paulo, Baba Mtakatifu wa kanisa takatifu korintho”..hapana hutaona hicho kitu.
Lakini inasikitisha zaidi kusikia leo hii watu wanagombania kuitwa baba, na wengine kwa nguvu, hata kama huyo mtu hana mahusiano yeyote ya kiiamani na yeye anayetaka amwite, bado atataka aitwe tu baba, hayo ndiyo Kristo aliyoyakataa, hiyo ni roho ya mpinga-kristo.
Lakini ikiwa ubaba wowote hautahusianishwa na kuchukua nafasi yoyote ya Kristo, huo hauna shida yoyote, ni kama tu vile unavyomwita mzazi wako baba au mama, hiyo haikuchukui nafasi yeyote linapokuja suala la kumwabudu Mungu, kwasababu unajua Baba yako aliye mbinguni ndiye anayestahili kupewa heshima zote za ibada na za kiungu.
Vivyo hivyo ikiwa utatoa heshima yako kwa kiongozi wako yeyote, au mwalimu wako, kanisani, hakikisha kuwa hilo halichukui nafasi ya Kristo, mnapokuja kwenye suala la kumwabudu Mungu basi sisi wote ni ndugu na tunapaswa kupeleka heshima zote, shukrani zote, na maombi yote kwa Mungu na sio kwa mwanadamu yeyote kama kanisa katoliki lifanyavyo kwa mapadre wao na Papa, na baadhi ya makanisa ya kiroho ambayo yanamfanya mtu mmoja kama ndio kila kitu kwao, huku wakimwita baba na pasipo yeye wanajihisi hawawezi kumwabudu Mungu. Hizo ni ibada za sanamu.
Ubarikiwe sana.
Mada Nyinginezo:
KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?
MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
JIBU: Embu tutafakari mfano huu, utatusaidia kupata majibu ya maswali yetu. Tunajua kuwa Dunia tunayoishi sasa hivi ni dunia ya utandawazi na kugunduliwa kwa Kompyuta kumefanikisha kurahisisha mambo mengi sana, Komputa sasa inAaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu pekee angeweza kufanya, unaweza ukaiuliza swali lolote na ikakusaidia kupata sehemu kubwa ya majibu yako, inaweza kukusaidia kufanya mahesabu yako, inaweza ikakusaidia kuwasiliana na mtu mwingine aliye mbali, inaweza ikakuonyesha picha, inaweza ikakuhifadhia kumbukumbuku zako, inaweza ikakusaidia kutafiti, na hata kufanya kazi n.k. Kwa ufupi komputa sasa tunaweza kusema ni chombo ambacho kina ufanisi mkubwa karibia na mwanadamu, tunaweza kusema kina uhai fulani, Na uhai huo ni wazi kabisa hakijapewa na mwingine zaidi ya mwanadamu.
Lakini pamoja na hayo tunajua hata kiwe na ufanisi mkubwa kiasi gani, bado tu uhai wake hauwezi kuwa halisi kama wa mwanadamu mwenyewe, vipo vitu vingi kitashindwa kufanya ambavyo mwanadamu angeweza kufanya, kwamfano Komputa haiwezi kufariji, haiwezi kupima hisia za mtu, komputa haiwezi kuonyesha fadhili, komputa ukiiomba chakula haiwezi kukupa, komputa haiwezi kuona mambo ya mbeleni ili kuchukua tahadhari n.k..yenyewe inaongozwa na kwa yale tu mwanadamu aliyoyapachika ndani yake, nje ya hapo haiwezi kujichagulia mambo yake yenyewe. Vivyo hivyo tukirudi kwa Mungu wetu.
Tunajua sisi sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, na kama vile alivyo hai, na sisi basi tutakuwa hai, lakini uhai tulionao si kama ule wa kwake, sisi ni mfano wa Komputa zilizotengenezwa na Mungu, tunaouwezo wa kuonyesha tabia zote za Mungu lakini haimaanishi tutakuwa na ule uhai halisi kabisa kama wa Mungu mwenyewe, wa kufikia hatua ya kuweza hata kuumba, kufanya kila kitu, kuona mambo yote ya mbeleni yanayokuja, kuchipusha chakula ardhini, hatuwezi pia kujihakikishia uzima wetu wa milele kama sio kutoka kwake. Hivyo tunavyosema Tunamwabudu Mungu aliye HAI, tunamaanisha Mungu awezaye kufanya mambo yote, Mungu anayetoa uhai katika mambo yote, Mungu ambaye hashindwi na lolote,Shetani hawezi kuumba chochote,japo anaishi, hajui hata kesho yake itakuwaje sasa ataitwaje mungu aliye hai? Yeye kapewa tu sehemu ya uhai kama sisi tulivyopewa, hawezi kusema sasa nataka jua lizime, au leo mimea yote duniani ikauke,hana uwezo huo hivyo hawezi kuitwa Mungu aliye hai.. Neno zuri labda linaweza kumstahili yeye kuitwa nao hao wanaomwabudu ni “mungu aliyepewa pumzi”, lakini sio Mungu aliye hai aliye hai ni mmoja tu! anayekaa mbingu za mbingu.
Isaya 46:9 “kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; 10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote. 11 Nikiita ndege mkali kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyo mbali; naam, nimenena, nami nitatekeleza; nimekusudia, nami nitafanya.”
Ubarikiwe.
Mada zinazoendana:
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
SWALI: Kaini baada ya kumuua ndugu yake Abeli, alikimbilia katika nchi ya Nodi, Naomba kufahamu Je! Huko alipatia wapi mke na kuzaa naye watoto? (Mwanzo 4:16).
JIBU: Ukisoma Mwanzo 5:1-5 utaona inasema….
“1Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, AKAZAA WANA, WAUME NA WAKE
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na the lathini, naye akafa.”
Sasa kwenye Mstari huo wa 4 utaona kuwa kumbe mbali ya Kaini na Abeli kuzaliwa na Adamu kulikuwa na wana wengine wa kike na wakiume waliokuja kuzaliwa kwenye familia yao pia, na ndio huko huko Kaini alipojitwalia mke.
SWALI: Kama KAINI alitwaa mke ambae alizaliwa na Adamu na Hawa ambao ni wazazi wake kwahiyo alimuoa dada yake je,kwahiyo nihalali kumuoa mwanamke ambae ni dada yangu wa damu?”.
JIBU: Kumbuka hata Adamu mwenyewe hakwenda kumtwaa mke kutoka kwenye familia nyingine, bali katika ubavu wake mwenyewe, hivyo kama ni undugu basi Adamu na hawa wana undugu mkubwa zaidi ya Dada na kaka…
Unaona? Mungu aliruhusu iwe hivyo mwanzoni kwa ajili ya uzazi, ili watu waongezeke, lakini baadaye Mungu alitoa maagizo kuwa ni makosa mtu kutwaa ndugu wake wa karibu na kumfanya kuwa mke wake..
Mambo ya walawi 18:6 “Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana”.
Na pia mstari wa 9 unasema…
9″ Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue”.
Kwahiyo ni machukizo kuoa ndugu yako yoyote yule wa karibu.
Ubarikiwe
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
JIBU: Mungu alimpa maagizo nabii Hosea kuoa mke aliye kahaba, sio kwasababu Mungu, anahalalisha usherati, hapana! Kusudi la Mungu kufanya vile ni kutaka kuwaonyesha wana wa Israeli ni jinsi gani wao wanavyofanya uasherati katika roho zao mbele zake kwa kuyaacha maagizo yake.. Kwahiyo nabii Hosea alipooa mke wa uzinzi, ilikuwa kama ishara ya Bwana kutaka kuwaonyesha wana wa Israeli mambo wanayoyafanya mbele zake…
Sasa Bwana alitaka endapo watu watakapomwuliza Hosea kwanini ameoa mke ambaye ni mzinzi…ndipo Hosea awajibu, kama mimi ninavyoudhiwa na huyu mwanamke mzinzi ndivyo na ninyi (wana wa Israeli) mnavyomuudhi Bwana kwa kufanya uzinzi mbele zake kwa kulihalifu agano lake na kuabudu miungu migeni, ukisoma habari ile yote kwa urefu utaona jambo hilo.
Sio mara ya kwanza Bwana kutoa ishara kupitia maisha ya watu, ukisoma biblia mahali pengine utaona Nabii ezekieli Bwana anamwagiza ale kinyesi, mahali pengine akate nywele zake kwa upanga azigawanye sehemu tatu….sehemu nyingine anaambiwa ahame nyumba yake kwa kutoboa ukuta, huku amejifunika macho kumwonyesha Mfalme wa Yuda Sedekia kwamba wakati majeshi ya wakaldayo yatakapouzingira mji kwa miaka miwili, yeye atatoroka kwa njia ya kutoboa ukuta wa mji, na hatimaye watamkamata na kumtoboa macho yake sawasawa na nabii Ezekieli alivyoonyesha…
Ezekieli 12:1 Neno la Bwana likanijia tena, kusema,
2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.
3 Basi, mwanadamu, funga tayari vyombo kwa uhamisho, ukahame wakati wa mchana mbele ya macho yao; nawe utahama toka mahali pako hapa mpaka mahali pengine mbele ya macho yao; labda watafahamu, wajapokuwa ni nyumba iliyoasi.
4 Nawe utatoa vyombo vyako, wakati wa mchana, mbele ya macho yao, kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa; nawe mwenyewe utatoka, wakati wa jioni, mbele ya macho yao, kama watu watokavyo katika kuhamishwa.
5 Toboa mahali ukutani mbele ya macho yao, ukachukue vitu kwa kuvipitisha pale.
6 Mbele ya macho yao utajitwika begani pako, na kuvichukua nje gizani; utafunika uso wako, hata usiione nchi; kwa maana nimekuweka uwe ishara kwa nyumba ya Israeli.
7 Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nalitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavitoa gizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao.
8 Asubuhi neno la Bwana likanijia, kusema,
9 Mwanadamu, nyumba ya Israeli, je! Nyumba ile iliyoasi, hawakukuambia, Unafanya nini wewe?
10 Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Ufunuo huu wamhusu mkuu wa Yerusalemu, na nyumba yote ya Israeli walio kati yao.
11 Sema, Mimi ni ishara kwenu; kama mimi nilivyotenda, wao nao watatendwa vile vile; watahamishwa, watakwenda kufungwa.
12 Naye mkuu aliye kati yao atachukua begani katika giza; naye atatoka kwenda zake; watatoboa mahali ukutani, wapate kuvichukua vyombo vyao nje; atafunika uso wake, kwa sababu hataiona nchi kwa macho yake.
13 Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, angawa atakufa huko.
14 Nami nitawatawanya kwa pepo zote wote wamzungukao ili wamsaidie, na vikosi vyake vyote; nami nitaufuta upanga nyuma yao.
15 Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; nitakapowatawanya kati ya mataifa, na kuwatupa-tupa katika nchi zote”
Ukizidi kusoma utaona mahali pengine Nabii mmoja Bwana alimwagiza amwambie mtu ampige mpaka atoke majeraha.
1 Wafalme 20: 35 “Basi, mtu mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake kwa neno la Bwana, Nipige, nakusihi. Akakataa yule kumpiga.
36 Akamwambia, Kwa sababu hukuisikiliza sauti ya Bwana, angalia, mara ukitoka kwangu simba atakuua. Na mara alipotoka kwake, simba alimwona, akamwua.
37 Ndipo akaona mtu mwingine, akasema, Nipige, nakusihi. Yule mtu akampiga, hata kumpiga na kumtia jeraha.”
Sasa mambo haya yote ni ishara ya Bwana kutaka kuzungumza na wana wa Israeli kwa kupitia maisha ya watu, kwahiyo hiyo ndio sababu ya Mungu kumwambia Nabii Hosea akaoe mke wa kikahaba..na pia kumbuka Hosea mwenyewe hakuwa mzinzi ni yule mwanamke aliyeambiwa amwoe ndiye aliyekuwa ni kahaba. Kwa jinsi hiyo hiyo mambo hayo yanavyochukiza mbele za watu ndivyo hivyo hivyo yanavyochukiza mbele za Mungu, pale watu wanapoasi maagano yake.
Ubarikiwe!
Mada zinazoendana:
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
JIBU: Biblia haituelezi kuwa kama kuna mtu yeyote anayejuwa mawazo ya mtu isipokuwa mtu mwenyewe na Mungu peke yake basi. Mungu peke yake ndio yupo kila mahali, yeye peke yake ndio anajua kila kitu, na yeye peke yake ndiye anayeweza mambo yote..Kwasababu yeye ndio muumba wa vyote. Hilo tunalithibitha katika vifungu hivi vya maandiko.
Zaburi 139: 1 “Ee Bwana, umenichunguza na kunijua.
2 Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.
4 Maana hamna neno ulimini mwangu Usilolijua kabisa, Bwana.
5 Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.
6 Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia. 7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?
8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika.
11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; 12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu”.
Unaona ni sawa tu! na mtu ambaye anamiliki account ya facebook,sasa mwenye uwezo pekee wa kuiingia na kutoka ni mmiliki wa account hiyo na aliyetoa account hiyo ambao ni facebook basi! Hao wawili tu ndio wenye uwezo wa kufanya lolote juu ya account hiyo lakini mtu mwingine wa nje! hata kama na yeye atakuwa anamiliki shirika kubwa kiasi gani linaloweza kufanana na facebook, hawezi hata kidogo kuwa na uwezo wa kudukua taarifa za account yako ya facebook, labda wewe umfunulie au shirika la facebook lenyewe limpe taarifa zako.
Vivyo hivyo moyo wa mwanadamu shetani hawezi kuuingia wala kufahamu mawazo yaliyopo ndani yake, isipokuwa wewe mwenyewe umfunulie au Mungu.
Lakini pia kumbuka biblia inamwita shetani lile joka la zamani, Hii ikiwa na maana kuwa amekuwepo duniani tangu zamani na hiyo inampa faida kuwatazama wanadamu kwa muda mrefu na kuelewa baadhi ya tabia walizonazo, hivyo anaweza akawa anauwezo wa kuhisi mawazo ya mtu yakoje na haraka akamuundia njia ya kumwangamiza kulingana na anachokitamani, lakini kufahamu moja kwa moja fikra za mtu kama vile Mungu hilo hawezi, uwezo huo wa kuyasoma mawazo ya mtu mwingine hata sisi wanadamu tumepewa,..unaweza ukamuangalia mtu katika mazingira Fulani ukajua anachowaza, lakini huwezi kuingia ndani ya kichwa chake na kujua kila kitu ndani yake.
Na ndio maana utaona shetani alipokuwa anamjaribu hata Yesu alikuwa anamwambia ikiwa wewe ndiwe! Kuonyesha kuwa alikuwa hana hata uhakika wa uhusiano wa Yesu na Baba yake ulivyo maana kama angelijua hilo asingepoteza hata muda wake kumuuliza Bwana maswali yaliyoonekana kuwa ni ya kitoto kwa Bwana .
Lakini pia shetani anaowezo wa kutuma fikra zake ndani ya mtu, anaweza akatuma kwa kupitia ndoto, kwa kutumia mawazo, au hata kwa njia ya maono. Na hayo huwa yanakuja na nguvu Fulani kukushawishi kufanya mambo yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. Kama mtu akiwa anaendelea kuyatafakari badala ya kuyakataa basi ndivyo anavyompa shetani wigo mpana wa kuyamiliki maisha yake.
Na ndio maana biblia inasema inatupaswa tuwe na uwezo wa kuteka kila fikra ipate kumtii Kristo. Jambo lolote linalokuja kwenye mawazo yetu, au ndoto, au chochote kile kama kinapingana na kanuni za Mungu ni kutokipa nafasi, kukikataa kwa nguvu, na chenyewe mwisho wa siku kitaondoka.
2 Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;”.
Hivyo, kuhusu shetani kufahamu mawazo ya mtu kana kwamba anasikia radio, hilo jambo haliwezi, japo anao uwezo wa kuhisi mtu au anachokiwaza au kumsoma mawazo yake kwa kuchunguza tabia za huyo mtu na mienendo yake, na mazungumzo yake mara kwa mara.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
TUNAMWABUDU MUNGU ALIYE HAI ,JE! WALE WANAOMWABUDU SHETANI SIO MUNGU WAO ALIYE HAI?
JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?
JIBU: Ndio atamuhukumu kama mkosaji, na ndio maana utaona zile adhabu zote zilimpata!! Hata kufiwa na mtoto wake wa kwanza…Na baada ya kufa kama hakupewa moyo wa kutubu, basi bado ataenda jehanamu ya moto. Kumbuka Moyo wa kutubu na moyo wa kumtafuta Mungu, ni Mungu mwenyewe ndio anaotoa sio sisi tunaoamua kwa juhudi zetu..ndio maana Bwana Yesu alisema katika
“Yohana 6:44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka;”
Umeona hapo? Nguvu ya mtu kumfuata Mungu ni Mungu mwenyewe ndiye anayekujalia..vinginevyo haiwezekani kumtafuta Mungu wala kumfuata.Sasa Kwanini Mungu amjalie Musa moyo mlaini wa kumkubali na Farao ampe moyo mgumu wa kumkataa??..hatujui na wala hatuwezi kumuuliza Mungu hayo maswali, ndivyo ilivyompendeza yeye, ni sawa na tumuulize Mungu alitokea wapi?? Hayo ni maswali tusiokuwa na majibu nayo….Yapo juu ya upeo wa fikra zetu. Na ndio maana mtume Paulo alisema katika..
Warumi 9.13 “Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.
14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!
15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.
16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.
17 Kwa maana maandiko YASEMA JUU YA FARAO, ya kwamba, nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.
18 BASI, KAMA NI HIVYO, ATAKAYE KUMREHEMU HUMREHEMU, NA ATAKAYE KUMFANYA MGUMU HUMFANYA MGUMU.
19 Basi, utaniambia, MBONA ANGALI AKILAUMU? Kwa maana NI NANI ASHINDANAYE NA KUSUDI LAKE?
20 La! Sivyo, Ee binadamu; WEWE U NANI UMJIBUYE MUNGU? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?”
Unaona hapo? Biblia inasema pia wapo watu ambao hawajakusudiwa uzima wa milele, watu ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu (Ufunuo 17:18 na Ufunuo 13:8)..Swali ni Ni wakina nani hao?? Jibu ni kwamba Hatuwajui, Mungu ndie anayewajua…sisi sio kazi yetu kuwafahamu, jukumu tulilopewa ni kuhubiri injili kwa kila kiumbe kana kwamba wote wote wamekusudiwa uzima wa Milele,…Na kujitahidi kuishi kulingana na maagizo yake na amri zake,ili tuwe na uhakika sisi sio miongoni mwa hilo kundi lililoandikiwa kupotea milele.Kwasababu dalili kuu inayotambulisha kuwa umekusudiwa uzima wa milele ni pale mtu anapoitii na kubadilika, kadhalika dalili kubwa inayoweza kumtambulisha kama mtu huyo hajakusudiwa uzima wa milele, ni pale anapoupinga wokovu ndani ya moyo wake.
Ubarikiwe!
Mada zinazoendana:
MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU:
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
JIBU: Shalom!, Kwa hali ya kawaida tunafahamu sanduku kazi yake huwa ni kuhifadhi vitu Fulani, inaweza ikawa ni fedha,vito,nguo, hazina, miili n.k. na ndio maana tukirudi kwenye biblia tunaona biblia inataja masanduku ya aina mbali mbali, kwa mfano pale Yusufu alipokufa biblia inatuambia mwili wake waliuweka kwenye sanduku (Mwanzo 50:26), hivyo kuna masanduku ya miili. Hali Kadhalika kulikuwa na masanduku ya kuhifadhia sadaka, ambayo yaliitwa masanduku ya sadaka au masanduku ya hazina, mahususi kwa kazi ya sadaka tu!. (Marko 12:41).
Vivyo hivyo na masanduku mengine yalikuwepo, ya fedha, ya vito n.k.. Sasa tukirudi kwenye sanduku la agano lililokuwepo Israeli katika agano la kale, mpaka limeitwa sanduku la agano ni wazi kuwa ndani yake lilikuwa limehifadhi maagano Fulani. Na kama ukisoma biblia utaona ndani ya sanduku lile ambalo Musa alipewa maagizo alichonge lilikuwa na vitu vitatu: kimoja ni zile mbao zenye zile amri 10 Mungu alizompa Musa akiwa mlimani, zilizoandikwa kwa kiganja cha Mungu mwenyewe, cha pili ni ile mana, na cha tatu ni ile fimbo ya haruni iliyochipuka.
Na kila mojawapo hapo ilikuwa na maana yake. Musa aliagizwa avitunze vitu hivyo vitatu kwenye sanduku lile liwe kama kumbukumbuku la agano Mungu alilofanya na wana wa Israeli tangu walipotoka Misri mpaka walipoingia katika nchi ya ahadi. Vitu hivyo aliagizwa vikae kwenye sanduku kwa vizazi vyote kama ukumbusho.
Waebrania 9:2 “Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu.
3 Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu,
4 yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;
5 na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja”.
Fimbo ile ikimaanisha ukombozi wao waliopewa na Mungu kwa njia ya mti ule, Mungu alitumia kipande kile cha mti ule kumwadhibu Farao mpaka kuwaachilia watoke katika utumwa ule mgumu ambao kwa namna ya kawaida ilikuwa haiwezekani wao kutoka Kwahiyo fimbo ya Haruni ndio ile ile fimbo ya Musa).
Kadhalika amri zile kumi zikufunua sheria zote na maagizo yote Mungu aliowapa wana wa Israeli walipokuwa jangwani kwamba waziendee hizo siku zote za maisha yao.
Na mana, inafunua chakula cha kiroho Mungu alichokuwa anawapa kule jangwani kilichoshuka kutoka mbinguni, ambacho kiliwapa nguvu ya kusonga mbele katika hali zozote walizokuwa wanapitia. Sasa tukirudi katika agano jipya kama swali lilivyoulizwa Sanduku la agano linawakilisha nini katika agano jipya?.
Jibu ni kuwa mambo yote yaliyotendeka katika mwili kwenye agano la kale yalikuwa yanafunua mambo yanayoendelea katika roho kwenye agano jipya sasa. Hivyo sisi sote tunaoishi katika agano jipya, Na sisi pia Mungu aliingia agano na sisi na kutugawia FIMBO, AMRI, na MANA. Na hizo zote akazihifadhi katika sanduku lake moja litembee nasi. Na sanduku hili si lingine zaidi ya BIBLIA neno la Mungu.
Fimbo yetu ni msalaba ule ambao kwa huo Mungu aliutumia kumpiga shetani siku ile pale Golgotha, siku ile Bwana aliposema IMEKWISHA! Baada ya damu yake kumwagika Basi siku hiyo ulikuwa mwisho wa kila kitu kwa shetani, Bwana aliyotuweka huru mbali na utumwa na vifungo vya shetani (Farao).
Kadhalika amri zile ni maagizo yote tuyasomayo katika Biblia Bwana aliyotupa,kila siku tuyafuate na Mana na ufunuo wa Roho ambao huo unashuka moja kwa moja kutoka mbinguni kwa Baba kutupa sisi nguvu ya kudumu katika IMANI. Hivyo vitu hivyo vitatu vinakamilisha agano jipya na vyote hivyo vipo katika sanduku moja nalo ndio BIBLIA TAKATIFU.
Na kama vile mahali popote wana wa Israeli walipoenda sanduku la agano lilifuatana nao kadhalika mtu yeyote aliye mkristo na anakaa mbali na biblia maneno ya Mungu ni wazi kabisa bado hajaingia kwenye hili agano jipya la damu ya Yesu Kristo.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO
MUNGU KUSEMA NA WEWE PEKEE, HAITOSHI KUKUPA USHINDI.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA TATU WA YOHANA.
KWANINI SAMWELI ALIRUHUSUIWA KUHUDUMU HEKALUNI KAMA VILE WALAWI WAKATI YEYE NI MU-EFRAIMU?
NINI MAANA YA HUU MSTARI “NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA;”?
JIBU: Hii ni kuonyesha kuwa Bwana hakuja kukomboa roho zetu tu basi, bali hata miili yetu pia..Na aliposema hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea, alikuwa anaamanisha kuwa hata kile kinachoonekana kuwa hakina thamani katika mwili wetu hakitapotea..vyote vitarejeshwa tena, ..Ikiwa ni mwamini alikufa hana mguu, basi siku ile ya ufufuo mguu wake utarejeshwa ikiwa alikufa na upara juu ya kichwa chake, basi nywele zake zote zitarejea katika siku ile na kuwa kama kijana. Na baada ya kurejeshwa ndipo miili mipya ya utukufu kutoka mbinguni ambayo asili yake ni mbinguni na sio ardhini itakuja kuivaa hii miili yetu ya ardhini. Kuonyesha kuwa hakuna kilichopotea hata kimoja…
1Wakoritho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
53 MAANA SHARTI HUU UHARIBIKAO UVAE KUTOKUHARIBIKA, NAO HUU WA KUFA UVAE KUTOKUFA.
54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?”
Lakini pia ikiwa Bwana anasema “Walakini HAUTAPOTEA hata Unywele” alimaanisha kuwa wapo ambao UTAPOTEA..Na hao ndio wale wanampinga YESU mfalme wa uzima sasa hivi wakijua kabisa yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kuokoa roho zao na miili yao. Siku ile wakifa katika dhambi basi miili yao na roho zao vyote kwa pamoja zitateketea katika lile ziwa la Moto milele. Watapotea milele wala hakutakuwa na kumbukumbu kama hata hao watu walishawahi kuishi duniani.
Ubarikiwe
Mada zinazoendana:
UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.
TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.
MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.
NI MAONO YAPI HAYO UNAYOSUBIRIA?
SWALI: Shalom!.Ndugu zangu Biblia inatuambia kuhusu kazi yakutoa jasho aliyopewa Nuhu ya”KUVIINGIZA KATIKA SAFINA”VIUMBE VIRUKAVYO-Vya kiume na vyakike kwa jinsi yake” “KILA NAMNA YA WANYAMA-Wakiume na Wakike kwa jinsi yake” .
Swali Ni je! Nuhu Alipata wapi ujuzi huo wa kuvitambua hivyo viumbe vyote, na je! Hao wanyama wote aliwatolea wapi?
JIBU: Ukisoma mstari wa 20 sura ya 6 wa kitabu kile cha Mwanzo Biblia inasema : 20 Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna WATAKUJA KWAKO ILI UWAHIFADHI. Unaona hapo, hilo neno WATAKUJA KWAKO ILI UWAHIFADHI
Ni kuthibitisha kuwa sio wanyama wote Nuhu alikwenda kuwachunguza kujua jinsia zako au kuwakamata, hapana wengine walikuja wenyewe Mungu ndiye aliyewaleta,isipokuwa wale wa kufungwa, lakini wengi wa hao waliosalia Mungu aliwaleta mwenyewe kwa Nuhu, kazi ya Nuhu ilikuwa ni kuwaingiza tu ndani.
Ubarikiwe.
Mada zinazoendana:
JE! VIUMBE VINATAZAMIAJE KWA SHAUKU KUFUNULIWA KWA MWANA WA MUNGU?
JE! VITABU VYA BIBLIA VILIWEZAJE KUKUSANYWA PAMOJA?
HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.
SEHEMU YA MAANDIKO ILIYOFICHWA.
JIBU: Ili kupata jibu ya swali hilo, ni vizuri pia tujiulize baadhi ya maswali ambayo ni rahisi kabisa kuyajibu yanayoonekana katika maisha yetu ya kila siku. Tuchukulie mfano Leo hii nikimuuliza daktari je! Utanithibitishiaje kuwa kama kuna kitu kinachoitwa kirusi au bacteria.?..
Tunafahamu hataniita na kuniambia angali kwa makini utaviona hewani , vikielea, vinginevyo nitamuona ni mwendawazimu lakini yeye kama daktari atajua kabisa kwa macho yangu ya asili siwezi kuviona virusi au bacteria hivyo jambo yeye atakalolifanya ni moja kwa moja kunichukua na kunipeleka mahabara na kunionyesha KIFAA maalumu kinachoitwa HADUBINI (Microscope), ambacho hicho kimeundwa mahususi kwa ajili ya kuvuta vitu visivyoonekana kwa macho. Hivyo pale nitakapoitazama labda tusema damu kwenye hadubini hiyo na kuona vijidudu vidogo vidogo vikitembea ndipo hapo nitakapoamini kuwa kuna viumbe vinaitwa Bacteria au virusi.
Kadhalika leo hii mtaalamu wa masuala ya Anga, akaniambia kuna sayari inayoitwa Pluto inayofanana na dunia, ni wazi kuwa siwezi kuamini kwasababu kwa macho yangu hayalithibitishi hilo lakini pindi atakapotumia kifaa chake maalumu kinachoitwa DARUBINI (Telescope). Ambacho hicho ni mahususi kwa kuvuta magimba yote yaliyo angani ndipo nitakapoamini kuwa kweli kuna sayari inayoitwa Pluto kwasababu ninaiona kwenye darubini. Vivyo hivyo na mambo ya rohoni, hatuwezi kuyatambua kwa jinsi ya mwilini biblia inatuambia hivyo katika
1Wakoritho 2: 14 “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni”.
Hivyo ili sasa tuweze kujua kuwa kuna mbingu au kuzimu basi yatupasa nasi pia tutumie kifaa maalumu kinachoweza kuvuta mambo ya rohoni na hicho si kingine zaidi ya BIBLIA TAKATIFU. Tatizo linakuja ni pale watu wasipotaka kuliamini NENO LA MUNGU na huku bado wanataka wamwone Mungu, ni sawa na mtu anayetaka kuona kirusi na huku bado haiamini Hadubini. Iamini kwanza biblia, ndipo utakapopata uthibitisho kweli kama kuna mbingu au kuzimu vinginevyo hata mtu atoke mbinguni au kuzimu akuambie hutaamini wala hutaweza kulithibitisha hilo.
Ubarikiwe sana.
Mada zinazoendana:
JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?
NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.