SWALI: Biblia inamaana gani kusema..maana Mungu wetu ni moto ulao?
Waebrania 12:29
[29]maana Mungu wetu ni moto ulao.
JIBU: Andiko hilo linaeleza sifa nyingine ya Mungu, kwamba si tu anajifananisha na maji, au nuru, au mafuta bali pia na “moto” tena ule “moto ulao”.
Kwanini aseme hivyo?
Ukianzia kusoma mistari ya juu utaona anaeleza madhara ya kuikataa sauti ya Kristo, kwamba ghadhabu yake inapokuja huwa ni mbaya mfano tu wa ile ghadhabu aliyoidhihirisha kwa wana wa Israeli kule jangwani walipoasi.
Waebrania 12:25
[25]Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni;
Neno hili la moto ulao, mwandishi alilinukuu kwenye vifungu hivi vya agano la kale.
Kumbukumbu la Torati 4:23-24
[23]Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu cho chote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu, [24]kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.
[23]Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu cho chote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu,
[24]kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.
Mungu alijitambulisha kwa wana wa Israeli kwa sifa hii, ndio sababu hata mwanzoni kabisa alipomtokea Musa kule jangwani alijifunua kama kijiti kinachoungua lakini hakiteketei. Kufunua kuwa wakitembea katika njia zake moto wake hauwezi kuwala, hivyo wasiwe na hofu, bali utawalinda na kuwaimarisha,lakini wakiasi utawala hakika.
Moto huo ndio ule uliokuwa nguzo mbele yao kuwalinda. Na walipokosea waliadhibiwa kwa huo, wakaanguka watu wengi jangwani kwa yale mapigo tunayoyasoma.
Sasa tukirudi kwenye kitabu cha Waebrania. mwandishi anatoa angalizo pia kwamba tusiipuuzie sauti ya Mungu katika Kristo Yesu, kwasababu sasa hivi Mungu anazungumza na sisi moja kwa moja kutoka mbinguni, sio tena kwenye mahema au milimani,kama kule jangwani, hivyo tuongeze umakini
Tukikumbuka kuwa sifa zake ni zile zile…Yeye ni moto ulao hata sasa. Tunapofanya dhambi kwa makusudi tunapokengeuka na kudharau wokovu (Waebrania 6:4-8)…tuogope kwasababu moto wa wivu wake unaweza pita juu yetu, na kutuharibu kabisa, na kujikuta tupo katika ziwa la moto.
Lakini tunapotii, moto wake hautuharibu bali unatulinda na kutuimarisha..tunafananishwa na dhahabu, inayopitishwa kwenye moto kutakaswa.
Hivyo, maaana ya vifungu hivyo ni tunafahishwa kuwa Mungu ana sifa ya moto, tukilifahamu hilo tutautumiza wokovu wetu kwa kuogopa na kutetemeka. (Wafilipi 2:12). Wala hatutakwenda kutenda dhambi kwa makusudi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’?
Je ni Mungu au Malaika?
Fahamu Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ni nani.
Print this post
SWALI: Wanawake wenye cheo wanaotajwa kwenye biblia ni akina nani? (Matendo 17:12)
JIBU: Mitume walipoanza kulitekeleza agizo kuu la Bwana Yesu la kuenenda ulimwenguni kote kuhubiri injili, biblia inatuonyesha walikutana na makundi mbalimbali ya walioamini.
Sasa mojawapo ya kundi hilo ambalo liliipokea injili, walikuwa ni hawa wanawake wenye cheo.
Kwamfano tunaweza kuona jambo hilo katika ziara ya mtume Paulo kule Beroya.. alipofika kule alikutana wa wanawake wa namna hii, na akawahubiria wakaipokea injili.
Matendo ya Mitume 17:10-12
[10]Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. [11]Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. [12]Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.
[10]Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi.
[11]Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
[12]Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.
Wanawake wenye cheo ni wanawake waliokuwa na sifa ya aidha nafasi za juu za kiutalawa, au ushawishi mkubwa kwenye jamii zao au wenye mali nyingi.
Wengi wao walipokutana na injili ya kweli ya Bwana Yesu Kristo waliipokea na kugeuka.
Lakini tunaona mahali pengine, mtume Paulo alipokwenda, wayahudi walimfanyia fitina kwa kuwatumia watu wa namna hii ili kuwataabisha..Kwamfano alipofika kule Antiokia mji wa Pisidia, na kuhubiri injili kwa ushujaa na wengi kuokoka. Wayahudi kwa sababu ya wivu wakawashawishi baadhi ya wanawake na wanaume wa namna hii..Ili wawapinge akina Paulo. Kwasababu walijua nguvu yao kijamii ni kubwa kiasi gani, hivyo itakuwa rahisi kutekeleza adhma yao.
Matendo ya Mitume 13:50
[50]Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.
Hivyo hiyo ni kututhibitishia hata sasa, Watu wenye vyeo wana nafasi ya kuwa washirika wa injili. Hivyo tusibague wa kumuhubiria, kwasababu wote Kristo amewafia msalabani. awe ni mbunge, au waziri, awe ni tajiri, au maskini, msomi, au asiye na elimu,. wote ni wa Mungu na wanastahili wokovu, wasipotumiwa na Mungu wao, shetani atawatumia. Hivyo nguvu zetu za injili ziwe sawasawa kwa watu wote.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MWANAMKE ABIGAILI ANAFUNZO GANI KWA WANAWAKE?
Apitaye cheo ni mtu wa namna gani?
Wale waliowekewa tayari ufalme ni akina nani?. (Mathayo 20:23).
Rudi Nyumbani
Somo la nyuma tuliona msingi wa Ukristo ni nini.. kwamba Yesu Kristo Bwana wetu ndiye msingi wenyewe..Yeye huitwa jiwe kuu la pembeni, na mwamba ambao juu yake sisi sote tumewekwa, pasipo Yesu hakuna ukristo. Yeye ndio msingi wa imani yetu.
Lakini pia kikawaida msingi ukishakaa chini, huwa nguzo zinafuata juu yake, kazi ya nguzo ni kulifanya jengo liweze kushikamana na kusimama vema toka juu kwenye paa mpaka chini kwenye msingi wenyewe.
Hivyo wewe kama mkristo ukishaweka msingi chini wa nyumba yako ya kiroho, fahamu pia moja kwa moja utanyanyua na nguzo zake, ili kuliunda jengo. Je nguzo zenye ni zipi?
Hizi ndizo nguzo kuu saba (7), za ukristo .
Ni wajibu wa kila mwamini aliyekombolewa na Kristo, pindi tu alipookoka aanze kukua ki-upendo. Hii ndio nguzo mama, kwasababu Mungu mwenyewe ni upendo (1Yohana 4:8). Zaidi sana anapaswa afahamu kuwa, upendo wa ki-Mungu sio kama ule wa kibinadamu
wa kupenda wanaokupenda, hapana ..huu ni upendo unaozidi usio na sharti wa kujitoa, ambao unapenda mpaka maadui, zaidi na kuwaombea wanaokuudhi.
Mtu asiyejijenga katika huu, haijalishi atajitaabisha vipi kwa Kristo, kazi yake itakuwa ni ya hasara siku ile ya mwisho.
1 Wakorintho 13 : 1-13
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi
cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama
sina upendo, hainifaidii kitu.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha,
zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
Ili maisha ya mkristo yasimame vema, maombi ni nguzo nyingine inayomkamilisha. Biblia inasema maombi yanapaswa yawe ni jambo la daima.
Wakolosai 4:2 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;
Maombi ni sawa na maji mwilini, au mafuta kwenye gari, vikikosekana hivi vitu hakuna utendaji kazi wowote utakaoendelea, vivyo hivyo ukristo wako usipokuwa wa maombi, hautaendelea sana. Utakufa tu siku moja
Ili tujengeke vizuri kiwango cha chini Bwana alichotaka tuombe kwa siku ni saa moja (Mathayo 26:40). Bwana Yesu alikuwa mwombaji, mitume walikuwa waombaji, sisi yatupasaje?
Ukishaokoka, jambo linalofuata ni kuwa karibu na biblia yako. Katika hiyo utapata kuelewa mpango kamili wa Mungu katika maisha yako. Huku ukisaidiwa na waalimu na wakufunzi wako kwenye usomaji wako wa biblia, kama Bwana wetu Yesu alivyokuwa mdogo akifanya bidii kuwasikiliza waalimu wake.
Kujifunza na kusoma kunapaswa kuwe ni tendo la kila siku. Neno ni kama chakula na maombi ni maji. Hivi viwili ndivyo vinakukuza kiroho na kukujenga nafsi. Hupaswi kuacha kusoma.. Mkristo asiyeifungua biblia yake ni rahisi sana kuchukuliwa na upepo wa ibilisi kwa mafundisho potofu. Kwasababu hamjui Mungu.
Hekima, maarifa, imani, ufahamu,na mamkala vinatoka katika kulijua Neno na mafundisho. Hivyo soma hiyo kila siku, pia sikiliza mafundisho kutoka kwa waalimu wako sahihi wa kweli, kwasababu ni muhimu sana kuvipata.
Matendo 2:41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Matendo 2:41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
1Timotheo 4:13 Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha
Ushirika ni kukutana pamoja na wenzako kujengana. Ushirika ni umoja wa Roho katikati yetu.
Waebrania 10:25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Kama mtakatifu, hupaswi kujiaminisha utakuwa na utimilifu wote wa ki-Mungu ndani yako kivyako. Utahitaji kukamilishwa na wengine kwa sehemu baadhi, Ndio hapo suala la ushirika linakuja.
Ndio sababu Mungu ameweka karama tofauti tofauti ili tujengane. Katika ushirika mtaombeana, kushiriki meza ya Bwana pamoja, mtafarijiana, mtasaidiana n.k.
Na pia biblia inasema wawili walalapo watapata joto.
Mhubiri 4:9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. 10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! 11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? 12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatuhaikatiki upesi.
Mhubiri 4:9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona
moto?
12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatuhaikatiki upesi.
Muwapo pamoja kuna ulinzi wa kipekee unaongezeka juu yenu. Hivyo kamwe usijaribu ule ukristo wa kivyako-vyako. Ni lazima tuwe washirika wa kanisa. Kama kanisa la kwanza lilivyoweza kusimama kwa kanuni hiyo.
Utakatifu ni utambulisho wa ukristo. Huwezi kuwa mkristo, halafu ukawa mwovu, huwezi kupokea Roho Mtakatifu halafu sifa za utakatifu usizionyeshe ndani yako. Kwasababu maandiko yanasema Mungu tunayemtumikia ni Mtakatifu hivyo na sisi pia hatuna budi kuenenda katika utakatifu. Bwana Yesu pamoja na watakatifu wa kwanza walizingatia viwango vyote vya usafi na ukamilifu. Vivyo hivyo na sisi
1Petro 1:16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Ushuhudiaji unaanza pindi tu unapookoka. Kila mkristo ameitwa kuitenda kazi ya Bwana. Na ni lazima afanye hivyo kama sehemu ya maisha yake, ili safari yake ya wokovu hapa duniani iwe imara ni lazima azae matunda. Uwakili ni kazi yetu ya daima. Ukristo bila uinjilisti hauwezi kuwa imara. Kanisa la kwanza lilikuwa la kiinjilisti. Kila mmoja alitambua wajibu wake wa kuisambaza injili kila mahali walipokuwa wakilizingatia lile agizo la Bwana.
Matendo 8:4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.
.
Sifa ya Mungu ni utoaji, ndio maana mpaka leo tunanufanika na mengi katika ulimwengu wake. Hata tulipopotea katika dhambi alijitoa kwa ajili yetu kwa kumtoa mwanawe awe fidia.
Na sisi kujitoa kihali na kifedha kwa ajili ya injili na kanisa la Kristo, ni nguzo muhimu sana. Unawajibu wa kuisapoti huduma inayokukuza kiroho, kwa zaka na changizo zako, pamoja na kuwasaidia ndugu (maskini). Kwasababu, Bwana Yesu na kanisa la kwanza lilikuwa na desturi hiyo.
1 Wakorintho
16:1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo
Hivyo sisi sote tukizitendea kazi nguzo hizo muhimu, basi tuwe na uhakika jengo letu la Imani litakuwa imara sana, linaloweza kustahili tufani na majaribu yote, lililoundwa vyema, kwa utukufu wa Mungu, hata siku ile ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.
USIKWEPE USHIRIKA NA MADHABAHU YA KRISTO.
MKARIBIE BWANA ZAIDI ILI UFANYIKE NGUZO.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu tuyatafakari maneno ya uzima. Leo napenda tujifunze tabia nyingine ya Bwana Yesu. Kwasababu yeye mwenyewe alituambia ‘tujifunze kwake’. Hivyo naamini tuna mengi ya kuyajua kuhusu yeye.
Habari hiyo tunaisoma katika vifungu hivi;
Luka 9:51 Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu; 52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. 53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu. 54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]? 55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] 56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Luka 9:51 Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;
52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.
53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.
54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia utakumbuka kuwa kuna wakati ulifika, ilikuwa wazi kwa watu wote, kuwa Yesu anatafutwa ili auawe, (hususani kule Yerusalemu). Na hilo lilimfanya mara kadha wa kadha asitembee kwa uwazi wote mbele ya makutano (Yohana 7:10), kwasababu, saa yake ya kuuawa ilikuwa bado haijafika.
Yohana 11:54 Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Lakini mambo yalikuja kubadilika baadaye, hilo halikuendelea kwa wakati wote. Alipoona sasa kazi aliyopewa na Mungu ameimaliza, alionyesha tabia nyingine ambayo haikuwa ya kawaida. Biblia inatuambia, “aliukaza uso wake kuelekea Yerusalemu”, kule kule alipokuwa anatafutwa auawe.
Jambo ambalo lilileta mshtuko hata kwa mitume wake;
Yohana 11:7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. 8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? 9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.
Yohana 11:7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena.
8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?
9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.
Walishangaa, ujasiri huo ni wa namna gani? Ni sawa na wanajeshi waliokwenda vitani, halafu maadui wakawaua wanajeshi wote, akabakia mmoja tu, halafu huyo mmoja anasema nitakwenda kupambana na jeshi lote hilo peke yangu sitajificha. Ukweli ni kwamba inahitaji nguvu nyingine ya ziada ndani ya huyo mtu.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu, aliukaza uso wake, kwenda kututetea sisi. Embu Fikiria kama angeulegeza, na kuendelea kuzunguka mahali pengine na sio kule uyahudi(Yerusalemu), wokovu wetu tungeupatia wapi?
Ilibidi, alazamishe mambo, japo mwili wake ulikuwa hautaki, ndio maana akiwa pale bustanini, anaomwomba Baba, akisema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, ni kuonyesha kuwa hata mwili wake ulikuwa unagoma kuwepo kule Yerusalemu, na si mwili tu, bado mazingira pia hayakutaka, alipokuwa anakatiza kwa Wasamaria wenyeje wa pale hawakutaka kumruhusu akae kwao, kwasababu waliona kama anawaletea matatizo, ikumbukwe kuwa watu hao hao ndio waliokuwa wanataka kumfanya mfalme hapo mwanzo. Kuonyesha kuwa mazingira yalimgomea. Si mazingira peke yake, hata mitume wake nao, walifanya kama kumsindikiza tu, lakini mioyo yao walishajiandaa kuchukua hatua yoyote lolote litakapotokea, ndio maana pale bustanini, wale watu walipokuja kila mmoja akakimbia na njia yake.
Kwa ufupi kila kitu kilikataa, isipokuwa roho yake tu. Ndio sababu ya kwanini maandiko yanatuambia ‘aliukaza uso wake’ kwasababu haikuwa rahisi, si jambo tena la kuomba, au kubembeleza, au kushawishi, au kusubiri msimu mzuri. Bali ni kujitoa tu wote wote, katika hayo. Watu wengi tunadhani Yesu aliuchukua msalaba wake siku ile alipobebeshwa ule mti, hapana, aliuchukua msalaba wake Kwa kitendo hichi cha kuamua kuukaza uso wake, kuelekea kifoni. Hata aliposema tujitwike misalaba yetu, alilenga, eneo hilo.
Ni nini na sisi tunapaswa tukipokee kwa Bwana Yesu?
Kwa kuwa Roho wake naye yupo ndani yetu, hatuna budi kufahamu kuwa yapo majira katika safari yetu ya wokovu, hatutahitaji mazingira yawe mazuri, ndio tulitimize kusudi la Mungu, au ndugu kutukubalia, au marafiki kuafikiana na sisi, au miili kutuambia sasa ndio wakati, hapana..bali ni kujitwika misalaba yetu, “kwa kukaza nyuso zetu” na kumfuata Yesu.
Tukingoja vikwazo viondoke, au viondoshwe, tutajidanganya, na tutangoja sana, kwani vita vitaendelea kuwepo mpaka mwisho, mapambano hayaishi, tutashinda tu kwa kukaza tu nyuso zetu. Na Bwana atakuwa pamoja na sisi, ijapokuwa itaonekana ni kujipoteza lakini mwisho wake utakuwa ni uzima kama ulivyokuwa kwa Bwana Yesu.
RABI, UNAKAA WAPI?
MFALME ANAKUJA.
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?
SWALI: Biblia inamaana gani kusema jivikeni silaha ya nia ile ile? (1Petro 4:1)
1 Petro 4:1-3
[1]Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. [2]Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. [3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
[1]Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.
[2]Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
[3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
JIBU: Tukiangalia undani wa hilo neno hapo anaposema silaha ya nia. Ni kutuonyesha kuwa kumbe “Nia ”, inaweza kuwa silaha.
Mara nyingi tunapofikiria silaha kibiblia mawazo yetu moja kwa moja yanakimbilia zile za Waefeso 6:10-18, silaha za haki, kama vile upanga wa Roho ambalo ni Neno la Mungu, chapeo ya wokovu, ngao ya imani, dirii ya haki n.k.
Lakini hapa tunaonyeshwa kuwa ipo pia silaha ndani ya Nia, ambayo nayo tunashauriwa tuwe nayo, kwasababu ilikuwa kwanza ndani ya Kristo.
Na silaha yenyewe ilikuwa ni kukubali kuteswa katika mwili ili kuiua dhambi.
Bwana wetu Yesu Kristo alijua dhambi ina nguvu sana pale mwili unapopewa raha zake. Hivyo aliikubali Nia ya kuteswa, ili dhambi ife.
Kumbuka sababu ya yeye kuchukiwa na watu, kuudhiwa, kuwindwa auawe, kuteswa mpaka kusulubiwa ni kwasababu alitangaza uadui na dhambi, Vinginevyo asingepitia maudhi yale katika mwili. Na tunaona mwisho wake ulikuwa ni ushindi. Kwani kwa kifo chake dhambi ilihukumiwa kabisa kabisa.
Alisema..
Yohana 7:7
[7]Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.
Hivyo maandiko yanatuambia na sisi pia, tujivike nia ile ile ya kukubali pia mateso kwa ajili ya Kristo. Kwasababu tukifanya hivyo tunaonyesha kuwa tumeachana na dhambi(tumeihukumu dhambi).
Kwa ufupi ni kuwa ukichukia maisha ya dhambi, tafsiri yake ni kukubali dhiki katika mwili kwa ajili ya Kristo. Hivyo zipende sasa dhiki hizo kama Kristo alivyozipenda, ili dhambi isikutawale. Hiyo ni Silaha kubwa sana.
2 Timotheo 3:12
[12]Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.
kubali shida, kwasababu umeamua kuacha ile biashara haramu, furahia kutengwa na kuonekana mshamba, kwasababu umeamua kuacha mienendo ya marafiki wabaya, penda kupigwa na kufungwa kwasababu unahubiri kweli. Hiyo ndio SILAHA YA NIA. iwezayo kuishinda dhambi.
Ndio maana vifungu vinavyofuata anasema..
“Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. [3]Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
“Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
Daima tujivike silaha hii, tukikumbuka kuwa vita vyetu si vikali tena kama vile alivyovipiga Kristo.
Waebrania 12:4
[4]Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;
Shalom.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
NDUGU,TUOMBEENI.
DHABIHU ZA ROHO NI ZIPI? (1Petro 2:5)
KIKWAZO CHA EUODIA NA SINTIKE.
Kitabu cha Wagalatia ni moja ya nyaraka ambazo mtume Paulo aliziandika kwa makanisa aliyoyapanda. Tunaona mwanzoni kabisa mwa waraka huu Paulo mwenyewe anajitambulisha akionyesha kuwa yeye ndiye mwandishi.
Waraka huu unamwonyesha Paulo akiwastaajabia watakatifu wa kanisa la Galatia kwa kuacha Imani ambayo aliwaachia hapo mwanzo, alipokuwa analisimamisha kanisa hilo, jambo ambalo lilimfanya mpaka imani yake impelekee kufikiri kuwa wamelogwa(Wagalatia 3:1), kwa jinsi tu walivyoiacha imani kwa haraka.
Kwa mujibu wa waraka huu, tunaona Paulo alilijenga kanisa hilo katika msingi wa imani katika neema ya Yesu Kristo.Na si katika msingi wa matendo ya sheria kama kigezo cha kukubaliwa na Mungu.
Kutokana na kuwa kanisa hili lilikuwa na mchanganyiko wa wayahudi pamoja na watu wa mataifa waliomwamini Kristo.Hapo ndipo tatizo lilipoanzia baada ya baadhi ya wakristo wa kiyahudi kuanza kuwashurutisha watu wa mataifa kwa kuwaambia kwamba hawawezi kuokolewa kama hawataishika torati ya Musa, kama hawatatimiza maagizo kama tohara, kushika siku, miezi, na miaka.(Wagalatia 4:8-10)
Hivyo hiyo ikawafanya watu kuacha kuishi tena kwa Imani iliyo katika neema ya Kristo Yesu, na kuangalia matendo ya sheria kama ndio kigezo cha kukubaliwa na Mungu?
Hivyo Paulo alipojua mageuzi hayo, ndio akawaandikia waraka huo kwa ukali, akiwaambia wokovu wetu huja kwa imani iliyo katika Yesu Kristo itendayo kazi katika upendo. Na si katika matendo ya sheria. Kwasababu kama ingekuwa hivyo Kristo alikufa bure. Torati ingeendelea tu kutawala.
Wagalatia 5:6
[6]Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Akasema torati, haikuwahi kumkamilisha mtu, na mtu anayeishi kwa hiyo ametengwa na Kristo, bado yupo chini ya laana.
kuishi kwa sheria ni kurudia mafundisho manyonge.
Lakini Swali ambalo alitarajia lingeulizwa na wagalatia, ni hili;
Je sasa hatuna haja ya kuyatazama matendo mema, tuishi tu, kama tunavyotaka kwasababu tunahesabiwa haki kwa neema ya Kristo tu?
Mbeleni kabisa katika sura ya tano, Mtume Paulo alitolea ufafanuzi, na kuwaambia tukishaokolewa, Maana yake ni kuwa tumeusulubisha mwili pamoja na tamaa zake mbaya..Hivyo hakuna nafasi ya dhambi kupata nguvu ndani yetu.
Wagalatia 5:24
[24]Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Je hilo inawezekanaje? kama hatuna sheria?
Linawezekana kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Ambaye tumepewa na Mungu.
Wagalatia 4:6
[6]Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
Hivyo Paulo anaendelea kueleza ni wajibu wa kila mwamini kutembea katika Roho. Ili awasaidie Roho kuzishinda tamaa zote za mwili, na mambo maovu.
Wagalatia 5:16-21
[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. [17]Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. [18]Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. [19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, [20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, ,[21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
[17]Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
[18]Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
[20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
,[21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Je waraka huu ulilenga hasa nini?
Kwamba kwa nguvu zetu, au dini zetu au torati kamwe hatuwezi kumpendeza Mungu bali tuitegemee neema ya Kristo ambayo kwa hiyo tumepokea Roho awezaye kutufanya wakamilifu.
Hivyo ni wajibu wako kama mkristo. Kila wakati wote kujawa Roho (Waefeso 5:18). Ambayo hiyo huja kwa kuwa waombaji, wasomaji Neno, na kufanya ibada mioyoni mwetu wakati wote..
Tukiwa watu wa namna hiyo sheria wala dhambi inakuwa haina nguvu ndani yetu. Kwasababu tunakuwa chini ya neema ya Yesu Kristo.
Ni uchafu gani unaozungumziwa katika Wagalatia 5:19?
je! Paulo aliwalaani Wagalatia na Wakorintho?
Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).
Wapelelezi wa uhuru wa wakristo ni watu gani (Wagalatia 2:4)?
WhatsApp
Swali: Kulikuwa na sababu gani ya Bwana MUNGU kuuweka mti wa mema na mabaya katikati ya bustani ili hali anajua kuwa mti huo ndio utakaowakosesha Adamu na Hawa, kwanini Mungu asingeondoa, na kuubakisha tu ule mmoja wa uzima katikati ya bustani?
Jibu: Ni kweli inaweza kuonekana ni busara mti mmoja tu kuwepo pale bustanini lakini ukweli ni kwamba endapo Mti mmoja tu ungekuwepo pale bado MTI WA UZIMA, usingeeleweka na wala maana yake isingekuwepo..
Kwani ili kuuthibitisha wema lazima uwepo ubaya mahali fulani… kwasababu wema hauwezi kujilikana kama ubaya haujadhihirishwa, vinginevyo ule wema utaonekana ni kitu cha kawaida, lakini ukifunuliwa ubaya ndipo wema unapopata kujulikana na kueleweka.
Nuru haiwezi kujulikana kama ni njema na kitu kizuri, kama giza halipo.. lakini ili Nuru ipate sifa, na kuheshimika ni lazima giza liwepo mahali ili nuru ilishinde giza.
Vile vile Mungu aliuweka ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambao matunda yake ni MAUTI, ili kuuthibitsha MTI WA UZIMA ambao matunda yake ni UZIMA.
Adamu na Hawa wasingeweza kuelewa nini maana ya UZIMA kama kisingekuwepo kingine kinachoelezea/kuhubiri MAUTI, vile vile hata sisi leo tusingejua Uzima ni nini kama MAUTI isingekuwepo, vile vile hatuwezi kujua Amani ni nini, kama hatujawahi kusikia kuhusu vita, au kupitia vita..
Hatuwezi kujua umaskini ni nini kama hatujawahi kuona utajiri, vile vile hatuwezi kujua utajiri ni nini kama hatuwahi kuona au kupitia umasikini,.. hatuwezi kujua kuwa tuna afya kama hatujawahi kuona wagonjwa, wala hatuwezi kujijua kuwa tuna ugonjwa kama hatujawahi kuona wenye afya, au sisi wenyewe kuwa na afya, huwezi kujua hiki ni kirefu kama kifupi hakipo, wala huwezi kujua hiki ni kirefu kama kifupi hakijawekwa mahali kama mfano.
Hivyo utaona kuwa uwepo wa vibaya au vyenye kasoro ni ili kuvithibithisha vile vilivyo vizuri na visivyo na kasoro.. Na lengo la Mungu kuuweka mti ule wa ujuzi wa mema na mabaya lilikuwa ni kuwapa kuelewa Adamu na Hawa Uzima ni nini, na thamani yake, na ili wauthamini na kuushika… na wala lengo lake si kuwatega!.
Hebu pia tengeneza picha miili yetu isingekuwa na maumivu, je unadhani ni nini kingetokea?…bila shaka hakuna mtu ambaye angehangaika kuutunza… hakuna mtu angeogopa kujikata na kisu, au kutembea peku kwenye miiba, au kunywa maji ya moto yale yanayotokota… lakini maumivu yamewekwa ili tujue na kutamani kuwa katika hali ya kutokuwa na maumivu na vile vile kuitunza miili yetu na kuushikilia uzima vizuri .
Hali kadhalika uwepo wa mti ule wa ujuzi wa mema na mabaya ni ili kuuthaminisha mti wa UZIMA. Ili mtu ajue umuhimu wa UZIMA, na RAHA ya Uzima, faida za uzima.
Je wewe umempokea YESU, na kuoshwa dhambi zako? Kumbuka YESU ndiye njia ya Mti wa UZIMA, na yeyote anayempokea humpa matunda hayo na kuishi milele, ndani yake.
Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.
Ufunuo 2:7 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu”
Kujua kwanini BWANA MUNGU awazuie wasile matunda ya Mti wa Uzima baada ya kula ya ujuzi wa mema na mabaya fungua hapa >>>
Kwanini Bwana MUNGU aliwazuia Adamu na Hawa wasile matunda ya Mti wa uzima waishi milele?
Swali: Katika Mwanzo 22:17, MUNGU anasema kuwa uzao wa Ibrahimu utamiliki malango ya adui, sasa unamiliki vipi huo mlango wa adui?.
Jibu: Turejee…
Mwanzo 22:17 “katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao”.
Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa Mzao wa Ibrahimu aliyebeba ahadi kamili za Ibrahimu ni BWANA YESU KRISTO.
Wagalatia 3:16 “Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo”.
Wengine wote, akina Isaka na Yakobo,(yaani Israeli katika mwili). walibeba sehemu za baraka hizo lakini si zote.. Iliweza kumiliki baadhi ya milango ya adui katika mwili lakini si yote.
Sasa kwa namna gani Israeli ya mwilini ilimiliki malango ya adui?
Kwa njia ya vita: kumbuka zamani miji ilikuwa inazungukwa na kuta, na mageti makubwa, hivyo nguvu na udhaifu wa mji ulikuwa katika mageti ya mji, hivyo lango la mji likitekwa na kumilikiwa basi tayari ule mji umeshatekwa,
Na Mungu aliwapa ahadi wana wa Israeli kwa jinsi ya mwili, kumiliki mlango/malango ya adui, ndio maana waliweza kuangusha miji ya kanaani iliyo mikubwa na yenye nguvu, na hatimaye kuiteka nyara miji hiyo.
Lakini mbali na hayo, lipo Lango ambalo Israeli ya mwilini asingeweza kumiliki, na mlango huo si mwingine zaidi ya ule wa MAUTI na KUZIMU.
Na kawaida mtu mwenye miliki ya mlango, ni yule mwenye FUNGUO ZA HUO MLANGO.
Mtu akikosa funguo hawezi kuwa na milki ya mlango wowote ule.
Hivyo Israeli ya mwilini alikuwa na Funguo za kufungua Mageti ya Wakaanani na Yeriko na mageti ya Wafilisti na kuwapiga na kuwatoa katika ardhi yao, lakini hakuwa na FUNGUO za MAUTI na KUZIMU,
Hakuweza kuzuia watu wasiingie kuzimu wala kuwatoa huko na kuwarudisha tena juu sawasawa na Ayubu 7:9.
Ayubu 7:9 “Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa”
Hivyo Israeli ya mwilini haikuweza kumiliki malango yote…. alikwama hapo kwenye Mauti na Kuzimu, sawasawa na maneno ya Bwana Mungu katika Ayubu 38:17.
Ayubu 38:17 “Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?”
Sasa swali la msingi, kama Israeli ya mwilini imeshindwa kumiliki milango hiyo, ni nani basi mwenye uwezo huo sawasawa na Mwanzo 22:17?.
Jibu la swali hili tunalipata katika kitabu kile cha Ufunuo 1:17-18.
Ufunuo 1:17 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU”
Ufunuo 1:17 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU”
Huyo mwenye hizo funguo za Mauti na kuzimu, ndiye mwenye milki ya Mlango wa Adui.
Maana adui wa kwanza na wa mwisho wa mwanadamu ni MAUTI ambaye analetwa na dhambi, huyu ndiye aliyeanza na Adamu pale Edeni na atamalizwa na Mwana wa Adamu siku ya mwisho.
1 Wakorintho 15:26 “Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”.
Na matokeo ya Mauti katika dhambi ni KUZIMU.
Kwahiyo YESU KRISTO ndiye mwenye funguo za Mauti na Kuzimu.
Wafu wote wanamilikiwa na Bwana YESU, na KUZIMU ipo chini ya mamlaka ya Bwana YESU, utauliza kivipi?..Mtu anayekufa sasa katika dhambi si shetani anayemtupa katika lile shimo la kuzimu, bali mamlaka ya YESU kupitia malaika wake ndio wanaowatupa watu katika lile shimo la kuzimu.
Kwasasa shetani hana mamlaka yoyote na wafu, hizo milki alishapokonywa na Bwana siku ile aloposhuka kuzimu, na hayo malango sasa yanamilikiwa na YESU KRISTO (Mkuu wa Uzima).
Warumi 14:9 “Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia”.
Nguvu za Bwana YESU kwasasa ni KUU SANA!!!, ukitaka kufahamu kwa sehemu kiwango cha nguvu alizonazo juu ya Mauti, ikumbuke ile kauli aliyosema..
Yohana 10:17 “Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. 18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu”.
Yohana 10:17 “Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.
18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu”.
Tafakari mtu anakuambia anao uwezo wa kuitoa roho yake na kuirudisha tena,…yaani kama vile mtu anavyozima taa na kuiwasha….na tena anasema “hakuna mtu aniondoleaye”..Maana yake Bwana YESU hakuuawa, bali yeye mwenyewe ndiye aliyeitoa roho ndani ya mwili wake.
Ndio maana akasema yale maneno…
Luka 23:46 “Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu”
Sasa mtu aliyeuawa hawezi kusema maneno hayo…lakini Bwana YESU hakuuawa bali yeye mwenyewe aliiondoa roho yake katika ule mwili, na ndio maana hata wale askari walishangaa imekuwaje amekufa mapema vile kabla ya kuvunjwa miguu.
Sasa ni kweli yapo maandiko yanayosema kuwa Bwana YESU aliuawa, lakini fahamu kuwa popote yanapotaja hivyo ni kuitia nguvu mada iliyoanza, lakini ukweli ni kwamba Bwana hakuuawa na mtu bali aliitoa roho yake mwenyewe.
Hiyo yote ni kuonyesha kuwa Mlango wa Adui wa Mauti, Bwana anao funguo zake.
Hivyo basi tukitaka mauti na kuzimu zisiwe na nguvu juu yetu, hatuna budi kumwendea yeye mwenye funguo hizo, na hatimaye atupe wokovu.
Lakini tukimkataa yeye mwenye funguo hizo, tujue kuwa hatutaokoka hata kidogo.
Malango ya adui, ni malango ya kuzimu, na ni malango ya mauti na yote chanzo chake ni dhambi.
Je umempokea Bwana YESU na kuoshwa dhambi zako?.
Kama bado unasubiri nini?.
Je Adamu na Hawa waliokoka?
Je mtu anaweza kupoteza wokovu?
USIWE ADUI WA BWANA
ANDALIZI LA MWISHO LA UJIO WA MPINGA KRISTO.
MUNGU HAJARIBIWI NA MAOVU BALI MEMA.
1Petro 4:12 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho”.
Neno “Msiba” kama linavyozungumziwa hapo halimaanishi ule Msiba wa mtu kufa. La! Bali neno hilo limetumika hapo kuwakilisha “jaribu zito”.
Kama tu lile lililompata yule mwanamke aliyetokwa na damu mda wa miaka 12.
Marko 5:27 “aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; 28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. 29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule………………… 33 Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. 34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena”
Marko 5:27 “aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.
29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule…………………
33 Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote.
34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena”
Hivyo tukirejea andiko hilo la 1Petro 4:12 msiba unaozungumziwa hapo “Ni jaribu zito”.
Kwahiyo kwa kiswahili kingine mstari huo unaweza kusomeka hivi…
“Wapenzi, msione kuwa ni ajabu lile jaribu zito lililo kati yenu, linalowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho”
Na msiba huo (au jaribu hilo)…Ni “Kuteswa kwaajili ya Kristo”…tunalithibitisha hilo katika mstari unaofuata wa 13.
1 Petro 4:13 “Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia”.
1 Petro 4:13 “Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.
14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia”.
Soma pia 1Wathesalonike 3:7 unataja msiba wa dhiki katika Kristo.
Na hata leo wote watakaotaka kuishi maisha ya kumpendeza MUNGU na utauwa, watakutana na misiba ya Kuudhiwa kwaajili ya imani.
2 Timotheo 3:12 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa”.
Lakini ukiishi maisha ya kuupenda ulimwengu, basi ulimwengu nao utakupenda kwasababu ulimwengu unawapenda walio wake.
Bwana atusaidie.
PIGO LA KUFA KWA WAZALIWA WA KWANZA
NYWELE ZAKO ZIKUFUNDISHE, SAUTI YA MUNGU.
VIASHIRIA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU KUWEPO NDANI YAKO.
MTAKENI BWANA NA NGUVU ZAKE.
HEKIMA NANE(8) ZA KIUINJILISTI, KATIKA KUWAVUA WATU KWA KRISTO.
Swali: Hili lango la samaki linalotajwa katika Sefania 1:10 lilikuwaje na lilikuwa linahusika na nini?.
Jibu: Yalikuwepo malango kadhaa ya Kulikuwa mji wa Yerusalemu nyakati za zamani, ambayo yalizunguka pande zote za mji.
Baadhi ya malango hayo ni “Lango la samaki”, “Lango la kale”, “Lango jipya” “Lango la Efraimu” na “Lango la kondoo”, ambalo liitumika kupitishia kondoo katika mji, kwa maelezo marefu juu ya lango hilo fungua hapa >>>
Mlango la kondoo ulikuwaje?(Yohana 5:2)
Lakini kuhusu “Lango la Samaki” turejee maandiko.
Sefania 1:10 “Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani”.
Hili “Lango la Samaki” halikuwa na matumizi kama lile “Lango la Kondoo”…kwamba linatumika kupitisha samaki ndani ya mji.
La! Bali ni lango la mji wa Yerusalemu ambalo lilikuwa upande Kaskazini-magaribi, karibu na “Soko la Samaki”..Hivyo liliitwa jina hilo kufuatia soko la samaki lililokuwa karibu na lango hilo.
Ingawa pia kwasababu lilikuwa upande wa kaskazini, wafanya biashara kutoka Galilaya walilitumia hili, na wengi waliotoka Galilaya walikuwa ni Wavuvi..
Hivyo lilitumika pia na wafanya biashara wa samaki, lakini halikuitwa kwasababu hiyo bali kutokana na soko hilo la samaki lilikokuwa karibu na lango hilo.
Lango la samaki kwanza limeanza kuonekana kipindi cha Mfalme Manase ambaye alikuja kuujenga ukuta wa nje wa mji wa Daudi (Yerusalemu), aliujenga upande wa magharibi mpaka kufikia mlango huo wa samaki.
2 Nyakati 33:12-14 “Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi BWANA, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake. 13 Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba BWANA ndiye Mungu. 14 Hata baada ya hayo akaujengea mji wa Daudi ukuta wa nje, upande wa magharibi wa Gihoni, bondeni, hata kufika maingilio ya LANGO LA SAMAKI; akauzungusha Ofeli, akauinua juu sana; akaweka maakida mashujaa katika miji yote ya Yuda yenye maboma”.
2 Nyakati 33:12-14 “Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi BWANA, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.
13 Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba BWANA ndiye Mungu.
14 Hata baada ya hayo akaujengea mji wa Daudi ukuta wa nje, upande wa magharibi wa Gihoni, bondeni, hata kufika maingilio ya LANGO LA SAMAKI; akauzungusha Ofeli, akauinua juu sana; akaweka maakida mashujaa katika miji yote ya Yuda yenye maboma”.
Baada ya miaka mingi kupita, tunakuja kusoma, kipindi ambacho mji wa Yerusalemu umebomolewa na Nehemia amerudi kuujenga ukuta, tunaona biblia inataja kuwa sehemu ya ukuta ya upande wa “Lango la samaki” ulijengwa na wana wa Senaa..
Nehemia 3:3 “Na lango la samaki wakalijenga wana wa Senaa; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake”.
Utaona tena lango hilo linatajwa kipindi cha mji kuwekwa wakfu (Nehemia 12:39).
Je umempokea Bwana YESU?..Je unafahamu kuwa tunaishi katika majira ya kurudi kwa YESU kwa pili?.
Je akija leo na kukukuta hivyo ulivyo utakwenda naye??
Bwana atusaidie sote.