Title November 2020

Wakaldayo ni watu gani?

Wakaldayo ni wenyeji wakongwe wa Mji wa Babeli. Mji wa Babeli ulikuwepo maeneo ya nchi ya Iraq kwasasa.

Hawa wakaldayo ndio waliowachukua mateka wana wa Israeli na kuwapeleka utumwani Babeli..

Yeremia 21:8 “Nawe waambie watu hawa, Bwana asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti.

9 Yeye atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atakayetoka, na kujitia pamoja na Wakaldayo wanaowahusuru, yeye ataishi, na maisha yake yatakuwa nyara kwake.

10 Maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu niuletee mabaya, wala nisiuletee mema, asema Bwana; utatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza”.

Ezra 5:12 “Lakini hapo baba zetu walipomkasirisha Mungu wa mbingu na nchi, hata akaghadhibika, akawatia katika mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Mkaldayo, naye ndiye aliyeiharibu nyumba hii, akawachukua watu mateka mpaka Babeli”

Pia Ibrahimu kabla ya kuhamia nchi ya Kaanani, alikuwa anaishi huko Uru ya Wakaldayo. Kwasababu Babeli tayari ilikuwepo miaka mingi kabla hata ya Taifa la Israeli kuwepo, ndipo ule Mnara wa Babeli ulipotengenezewa.

Mwanzo 11:31 “Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko”.

Hivyo popote biblia inapowataya Wakaldayo ina maanisha Wenyeji wa Babeli.

Je una habari kuwa Babeli iliyowachukua wana wa Israeli mateko kwa namna ya kimwili, ipo leo kwa namna ya kiroho?..Kama ulikuwa hujui basi kasome kitabu cha ufunuo mlango wa 17 na kuendelea.

Na Babeli hiyo ya rohoni inawachukua utumwa watu wengi leo pasipo wao kujua, na mwisho wa siku inawaua kiroho na kuwapeleka kuzimu. Na Babeli hii sasa inafanya kazi kwa nguvu katika dini na madhehebu, na Bwana ataihukumu katika siku za mwisho.

Ufunuo 14:8 “Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake”.

Kwa urefu kuhusu Babeli hii ya rohoni fungua hapa >> BABELI YA ROHONI

Je umeokoka?.  Kumbuka Kristo anarudi saa na wakati usiodhani?..Wakati unafikiri bado sana ndio wakati anaokuja..

Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia”.

Kama hujampokea ni vizuri ikampokea sasa hivi, wala usisubiri hata dakika 5 mbele, kwasababu hujua yatakayojitokeza dakika mbili mbele. Hivyo hapo ulipo piga magoti, kisha tubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na Bwana wa huruma na Neema atakusamehe bure, na kukutakasa. Na baada ya hapo tafuta ubatizo sahihi, wa maji mengi na kwa jina la Yesu, na  tafuta kanisa la Kristo la kiroho, lililo karibu nawe,  jiunge hapo na wakristo wenzako ili ujengeke kiroho, na Roho Mtakatifu atakuongoza kufanya yaliyosalia.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

MNARA WA BABELI

Mto Frati upo nchi gani, Umuhimu wake katika biblia ni upi?

Kongwa ni nini kwenye biblia?(Wagalatia 5:1)

NENO LA MUNGU NI DAWA ILIYO TOFAUTI NA DAWA NYINGINE.

JUKUMU LA MUHIMU LINALOKWEPWA NA WENGI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Wibari ni nani?(Mithali 30:26)

SWALI: Wibari ni nani? Na kwanini wanatajwa kama moja wa viumbe wanne wenye akili nyingi?(Mithali 30:26)


JIBU: Wibari ni wanyama wadogo wanaokaribia kufanana na sungura, kwa jina lingine wanajulikana kama pimbi, au kwanga, au perere, tazama kwenye picha.

Wanyama hawa utawaona wakitajwa kwenye vifungu hivi katika biblia;

Walawi 11:4 “Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu”.

Zaburi 104:18 “Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio la wibari”.

Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.

25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.

26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba”.

Lakini ni kwanini wametajwa kama moja ya viumbe vinne vyenye akili nyingi duniani?

Ni kwasababu ya tabia yao, wanyama hawa ni waoga, hawali nyama, wala hawapo machachari sana ukilinganisha na wanyama wengine, hawawezi kukimbia sana, kwa ufupi ni viumbe dhaifu ambavyo ni rahisi kukamatwa na maadui zao, lakini katika udhaifu wao, wanajua ni wapi pa kujihifadhi nafsi zao, na si hapo pengine zaidi ya kwenye miamba.

Wibari wanatengeneza nyumba zao kwenye mapango ya miamba, mirefu, na migumu, kiasi kwamba adui zao ni ngumu kuwaona au kuwakamata, tofauti na wanyama wengine kama ngiri au sungura n.k ambao wao wanachimba mashimo ambayo hata adui zao wanaweza kuwafuatilia na kuyafukua na kuwakamata, au mvua ikija ikajaza mashimbo yao wakafa, au upepo mkubwa ukivuma unaweza kufukia mashimo yao kwa udongo utakaoporomoka au kuingia, hivyo hiyo inawafanya maisha yao kuwa hatarini sana japokuwa ni machachari au wana uwezo mkubwa wa kukimbia.

Lakini wibari kweli sio kama wanyama wengine, ni wadhaifu sana lakini wanafahamu ni wapi wanaweza kuwa salama.

Je na sisi, tutashindwa akili na wibari?

Usalama wetu upo wapi? Je tumeyajenga maisha yetu wetu wapi? Je, ni mashimoni au kwenye vichuguu, au kwenye miti au kwenye mwamba?. Tujue tu kuwa mwamba ni mmoja tu, naye ni YESU KRISTO peke yake. Ukiwa nje ya Kristo, fahamu kuwa maisha yako yapo katika hatari zote, haijalishi utajiona wewe ni mjanja kiasi gani, haijalishi utajiona ni hodari kiasi gani, haijalishi ni tajiri  kiasi gani, shetani atakumaliza tu..Huna safari ndefu..

Sikiliza maneno ya Yesu..

Mathayo 7:24 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa”.

Kweli itakuwa ni ajabu sana tukishindwa akili na mnyama pimbi.

Shalom.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=mJ0AkfAcM4I[/embedyt]

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mavu ni nini katika biblia?(Kutoka 23:28, Kumb 7:20)

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.

Nini maana ya “katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni”.

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Bustani ya Edeni ipo nchi gani?

Bustani ya Edeni ipo nchi gani kwa sasa duniani?


Mungu alipoiumba dunia, alichagua eneo moja, na kulifanya kuwa la kipekee na la kitofauti na maeneo mengine yote aliyoyaumba duniani. Eneo hilo akaliita Edeni. Edeni maana  yake ni eneo la furaha kuu, utulivu,paradiso ya Mungu.

Lakini hakuishia hapo tu bali ndani ya hiyo Edeni upande wa mashariki alitengeneza bustani nzuri sana,  ambayo inajulikana na wengi kama bustani ya Edeni. Bustani hii ndiyo  Mungu aliyomweka mwanadamu wa kwanza hapo aishi (yaani Adamu na uzao wake.)

Lakini kama tunavyosoma biblia, wazazi wetu wa kwanza walipoasi, walifukuzwa kutoka katika bustani ile, na kuanzia hapo, hakuna aliyejua makao halisi ya bustani ya Edeni yalikuwa wapi, vifunguu pekee vinavyotupa taswira ya eneo la bustani ya Edeni ni hivi;

Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.

9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne.

11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;

12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.

13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.

14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati”.

Kama tunavyoona hapo, kulikuwa na mto uliokuwa unatoa maji kutoka bustanini na baadaye ukagawanyika katika vichwa vinne, na viwili kati ya hivyo (yaani Hidekeli na Frati) vinajulikana  mpaka sasa na vipo maeneo ya nchi ya Iraq, ili kusoma na kufahamu zaidi historia yao fungua hapa >>>> Mto frati na Hidekeli Na hiyo imewafanya masomi wengi wa biblia kudhania kuwa Edeni ilikuwa maeneo ya nchi ya Iraq au kando kando yake.

Lakini vile vingine viwili (yaani Pishoni na Gihoni) havijajulikana bado. Na iyo imewafanya wengine kudhani bustani ya Edeni ilikuwa nchi ya Uturuki ya sasa n.k.

 Hivyo, hakuna uthibitisho wa moja kwa moja wa kudhania kuwa Edeni ilikuwa Iraq, au Uturuki au sehemu nyingine yoyote. Na hiyo ni kwasababu ya mabadiliko makubwa ya nchi yaliyokuwa yanatokea wakati wa gharika na  ule wakati wa kugawanyika kwa nchi (Mwanzo 10:25). Historia inaonyesha kuwa dunia ilibadilika mwonekano wake kwa sehemu kubwa sana.

Lakini ni wazi kuwa Edeni haikuwa pengine zaidi ya mashariki ya kati, na sio Afrika kama wanasayansi wanavyoamini, nami naamini ilikuwa katika nchi Kaanani (Yaani Israeli ya sasa).

Lakini ikiwa biblia haikutupa maelezo ya kutosha kuhusu jeografia ya bustani ya Edeni baada ya wazazi wetu wa kwanza kuasi, ni wazi kuwa hakuna umuhimu sana wa kujua bustani hiyo iko wapi kwasasa, kwasababu hayo yalishapita. Bali sasa Mungu ametutilia mkazo hasaa kutufahamisha juu ya Edeni yetu ya mbinguni inayokuja.

Yaani ile Yerusalemu mpya, mji mtakatifu ushukayo kutoka mbinguni kwa Mungu. Na Yerusalemu hiyo itashuka juu ya mbingu mpya na nchi mpya zitakazoumbwa kwa wakati huo baada ya utawala wa miaka elfu moja kuisha. Kama vile tu ilivyokuwa  Edeni ilivyoumbwa juu ya dunia ya wakati ule. Kufahamu zaidi juu ya utawala wa miaka 1000 fungua hapa >>>  UTAWALA WA MIAKA 1000.

Lakini kisichojulikana na wengi ni kuwa, si kila mtu atakayeruhusiwa kuingia ndani ya mji huo. Bali wale watakatifu tu watakaoshinda ulimwengu huu.

Tujiulize, Je! Mimi wewe tutakuwa miongoni mwa hao watakaouingia huo  mji mpya wa dhahabu yaani Yerusalemu ya Mbinguni, Edeni halisi ya Mungu? Je! Mambo ya ulimwengu huu bado yanatusonga, mpaka siku ile itukute ghafla tukaachwa?. Je! Unajua kuwa unyakuo upo karibu sana, na dalili zote za kurudi Kristo duniani zimeshatimia?

Ikiwa wewe bado hujaokoka na leo hii utapenda kumkabidhi Kristo maisha yako ayaokoe na akupe uweza wa kufanyika mtoto wake, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako ambao hautaujutia milele. Hivyo kama upo tayari, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>>  SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

   Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?

Israeli ipo bara gani?

ORODHA YA WAFALME WA ISRAELI.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

UFUNUO: Mlango wa 1

Rudi Nyumbani:

Print this post