Jibu: Tusome,
Ayubu 22:12 “Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!
13 Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?
14 Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU.
15 Je! Utaiandama njia ya zamani Waliyoikanyaga watu waovu?”
Kuba ni mzunguko wa Anga, Ukitazama juu utaona ncha za mbingu ni kama duara, ndio maana jua wakati wa asuhuhi ni kama “linachomoza kutoka chini upande wa mashariki” na wakati wa mchana linaonekana lipo juu kabisa (utosini) lakini inapofika jioni “linazama tena chini upande wa magharibi”..
Sasa huo mduara wa anga ndio unaoitwa “KUBA” na maandiko yanasema Bwana anatembea juu ya mduara huo, kuonyesha utukufu wake.
Ayubu 22:14 “Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU”.
Hivyo andiko hili linaonyesha utukufu na ukuu wa Mungu, kuwa yuko juu sana na mwingi wa uweza.
Je umemrudia yeye aliyezifanya Nyota na Mwezi, na anga na viumbe vyote?..
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua”
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?
Biblia haijatoa ‘fomula’, ya idadi ya nyakati tunazopaswa kuomba kwa siku. Ila imesema ‘tuombe kila wakati’ na sehemu nyingine imesema ‘tuombe bila kukoma’. Hiyo ni kutupa uelewa kwamba maombi yanapaswa yawe ni endelevu lakini pia yawe ya wakati wote. Na hakuna mahali maandiko yanatoa nafasi ya mwaminio kutokuomba kabisa.
Waefeso 6:18 “kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;”
1Wathesalonike 5:17 “ombeni bila kukoma”
Hivyo ni sisi kutazama, watakatifu walikuwa na desturi gani, na nidhamu gani waliyojijengea katika kuomba. Je! Walitumia vipindi vingapi kwa siku? Vilevile tutaona Bwana Yesu anasemaje kuhusiana na hilo pia. Ili na sisi tuige vielelezo vyao katika utaratibu wetu wa kusali.
DAUDI
Daudi aliomba mara tatu(3) kwa siku . Asubuhi, adhuhuri na jioni.
Zaburi 55:17 Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.
DANIELI
Danieli pia aliomba mara tatu (3), kwa siku.
Danieli 6:10 Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Hivyo hii ni kutuonyesha kuwa ilikuwa ni desturi ya watakatifu wa kale, kwenda magotini walau mara 3 kwa siku. Na maombi waliyoyaomba hayakuwa ‘sala’ za dakika tano (kama zile za kuombea chakula). Bali ni maombi ambayo huwenda yalizidi saa moja, kwasababu maombi ya kulalama, na kuugua, (mfano wa hayo ya Daudi) sio ya dakika chache.
YESU KRISTO.
Bwana Yesu aliomba alfajiri na usiku, na majira mengi nyakati za adhuhuri aliahirisha huduma na kwenda mahali pa utulivu kusali.
Marko 1:35 “Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko”
Na usiku
Mathayo 26:40 “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”.
Adhuhuri
Luka 5:16 “Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba”
Hivyo tunaona pia Bwana aliomba nyakati zote. Alipopata nafasi.
Hivyo kiwango cha chini kabisa cha nyakati za kuomba kwa siku kwa sisi wakristo ni MARA MBILI. Yaani asubuhi na jioni. Unapoanza siku huna budi kuanza na Bwana kwa kumshukuru na kumwomba mwongozo wa siku hiyo, vilevile unapomaliza siku wapaswa ufanye hivyo hivyo.
Na ndio maana Bwana alisema maneno haya, kwa watu wake wanaoomba alisema;
Luka 18:7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
Kumbe usiku na mchana tunapaswa tuombe. Walau mara mbili kwa siku. Alisema, Yeye ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Kufunua kuwa yupo katika mwanzo wetu na mwisho wetu. Hakikisha uanzapo siku unatenga muda wa kutosha wa kuingia uweponi, na umalizapo siku unafanya hivyo hivyo. Utakuwa imara sana kiroho.
Lakini zaidi sana Bwana anataka tuwe watu wa kuomba siku zote kufikia hata kukesha. Hivyo ikizidi hapo ni vema sana, kwasababu utajiwekea akiba ya maombi kwa wakati ambao utakuwa na nguvu chache.
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
HIZI NI NYAKATI ZA KUFUNGA NA KUOMBA
NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?.
JIBU: Ipo mitazamo mingi, ihusuyo eneo halisi la makaburi ya wazazi wetu wa kwanza, Kwamfano kwa mujibu wa hadithi za kiyahudi, wao wanaamini kuwa Adamu na Hawa walizikwa pale Israeli, mahali palipoitwa Hebroni katika pango lijulikanalo kama pango la Makpela. Ambalo baadaye Ibrahimu na Sara walikuja kulinunua likawa ni eneo la maziko yao ya kifamilia, (Mwanzo 49:29-31) kwa urefu wa habari hiyo fungua hapa usome >>> Pango la Makpela ni lipi,
Wengine, wanaamini kuwa pale Kristo aliposulubiwa Golgota, ndipo palipokuwa kaburi la Adamu, wakiamini kuwa kama Kristo alivyoitwa Adamu wa pili, maana yake ni alikuja kurudisha kile kitu ambacho Adamu wa kwanza alikipoteza, yaani uzima. Hivyo kama Adamu alileta kifo, Kristo alileta uzima kwa msalaba wake, na aliyafanya hayo juu ya kaburi la Adamu.
Lakini je! kuna usahihi kwa mitazamo hiyo.
Kwasababu biblia haijaeleza chochote, kuhusiana na kaburi la Adamu na Hawa, hii yote ni mitazamo, ambayo yaweza kuwa ukweli au uongo, tusiweke imani yetu moja kwa moja katika mitazamo. Kwasababu gharika ilipokuja ilivuruga ramani yote ya ulimwengu, isingekuwa rahisi kupatambua mahali sahihi alipozikwa Adamu, isipokuwa kwa ufunuo.
Na habari hiyo kutoandikwa ni kutuonyesha kuwa hakuna umuhimu sana wa kujua Adamu alizikiwa wapi. Ushindi tulioupata kwa kifo cha Kristo, na kufufuka kwake, ni habari tosha tunayopaswa tuitafakari usiku na mchana, zaidi ya kaburi la Adamu.
Lakini swali ni Je! Yesu amefufuka ndani yako? Fahamu kuwa Ikiwa bado hujazaliwa mara ya pili, kifo kina nguvu juu yako, ukifa hakuna maisha kwako, ni mateso katika moto wa jehanamu. Lakini ukizaliwa mara ya pili uzima wa milele unao na hata ukifa, utakuwa unaendelea kuishi.
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
Unasubiri nini? Usiokoke leo.
Saa ya wokovu ni sasa, ni pale tu unapotubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kumwita Yesu ayatawale maisha yako, kisha kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. Hapo unakuwa tayari umezaliwa mara ya pili. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa, basi fungua hapa kwa mwongozo wa Sala hiyo ya toba.>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Maziara ni nini? Je! Na Tunaruhusiwa kuyajenga kwenye makaburi yetu?
Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Katika biblia mtu ambaye alipokea taarifa iliyofichwa kutoka Kwa Mungu na kuiwasilisha Kwa watu aliitwa mwonaji. Alipokea aidha kupitia, maono, ndoto, au kufunuliwa dhahiri, Mfano wa Hawa alikuwa ni Samweli…
1 Samweli 9:9-12
[9](Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.)
[10]Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu.
[11]Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko?
[12]Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu;
Lakini baadaye watu Hawa walikuja pia kuitwa Manabii kama tunavyosoma kwenye vifungu hivyo
Isipokuwa Maana ya Nabii ni Pana zaidi sio tu kupokea taarifa kutoka Kwa Mungu na kuiwasilisha Bali pia alisimama kufundisha na kuwarejesha watu, katika Sheria ya Mungu.ikiwemo kukaripia na kukemea, na kuonya. Mfano wa Hawa ni Isaya, Yeremia, Ezekieli, Yona, Hosea, Mika, Hagai, Malaki na wengine.
Hivyo nabii ni lazima pia awe mwonaji, kwamba apokee pia taaarifa za Moja Kwa Moja kutoka Kwa Mungu, na kufichua Siri zilizositirika lakini mwonaji haikuwa lazima afanye kazi ya kinabii, Bali ni kusema tu kile anachoelezwa, au kufichua Siri zilizojificha, au kuomba mwongozo wa Roho wa Mungu, Kwa ajili ya jambo/tatizo Fulani.
Hivyo kuhitimisha ni kwamba Kuna maandiko mengine yanawataja waonaji, lakini yalimaanisha pia ni manabii, na mengine yanabakia kumaanisha walewale tu waonaji.
Mfano wake ni Samweli, ambaye alikuwa ni mwonaji lakini pia ni Nabii.
1 Mambo ya Nyakati 29:29
[29]Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji;
Soma pia vifungu hivi, kufahamu zaidi.
(2Samweli 24:11, 2Nyakati 16:7, 29:30,)
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA.
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA
Maelezo ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.
Hekima inatufundisha tusiwe watu wa kujibu au kuzungumza kabla hatujasikia habari yote au taaarifa yote na kuitafakari kwanza..Kwamfano mwenzako anazungumza jambo Kisha wewe ukaingilia kati na kutaka kujibu, hoja ambayo haijakamilika..Matokeo yake hapo ni Nini kama sio kutoa majibu yasiyosahihi?. Au ambayo hayajakamilika?
Ndio hapo anasema ni upumbavu na aibu kwake.
Hii imeathiri hata kusambaa Kwa taaarifa za uongo. Mtu atasikia jambo, kwasababu Hana taaarifa nalo vizuri, atatoka muda huo huo na kwenda kumpasha mwingine, na yule mwingine atampasha mwingine..Hivyo taaarifa za uongo huzagaa Kwa upesi sana. Ndivyo ambavyo hata waandishi wa habari ambao hawawi makini wanavyosambaza habari ambazo bado hawajazifanyia uchambuzi yakinifu. Na matokeo yake husababisha matatizo makubwa katika jamii.
Mafarisayo na wayahudi walimpinga Yesu kwasababu walikuwa ni watu wa kupokea tu taaarifa ambazo hawazitafiti, walisikia Yesu anatokea Nazareti, wakahitimisha amezaliwa Nazareti, wengine wakamwita Msamaria. Lakini kama wangesubiri kutuatilia Kwa ukaribu mawazo Yao yangebadilika, na wasingekuwa wapumbavu kama tunavyowasoma kwenye biblia.
Hata wakati alipokuwa anazungumza nao, hawakutaka kusikiliza mpaka mwisho ni Nini Bwana anataka kuwaambia, kwamfano Kuna wakati aliwaambia, mtu akilishika Neno lake hataonja mauti milele. Lakini wao Hawakutaka ufafanuzi alimaanisha Nini.. hapo hapo wakarukia na kumwita ana Pepo;Kwa kauli Ile.
Yohana 8:52-53
[52]Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.
[53]Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
Wakati mwingine aliwaambia livunjeni hili hekalu,nami nitalisimamisha baada ya siku tatu. Wakairukia hiyo kauli bila kusubiria maelezo yake , ndio ikawa habari ya mji mzima Kuna mtu kasema anaweza kulijenga Kwa siku 3 hekalu lililojengwa Kwa miaka 46. Kumbe hawakujua Kristo anazungumzia habari ya mwili wake.(Yohana 2:20)
Biblia inatuasa tuwe wepesi wa kusikia, na si wa kusema; Ina faida nyingi.
Yakobo 1:19
[19]Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
HAUWEZI KURUKA MADARASA YA MUNGU!
FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Maana ya Mithali 19:15 ‘Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;
Fahamu Maana ya;
Mithali 18:18 Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.
Kupiga kura ni Moja ya njia ambayo ilitumika kuleta suluhisho lenye utata, na wakati mwingine kuchagua viongozi/wamiliki. Pitia hapa ujue zaidi kuhusu kura zilivyopigwa zamani za biblia…>> Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo;
Na Mungu wakati mwingine aliingilia kati na kuleta majibu yake sahihi kwa kupitia njia hiyo. Kwamfano wakati ule Yona anamkimbia Mungu, Hali ilipochafuka kule baharini, utaona wale watu walipiga kura, ili kujua sababu ya mambo yale ni nani na Ile kura ikamwangukia Yona.
Mitume wa Bwana baada ya kuomba, kuhusu mrithi wa nafasi ya Yuda wakapiga kura katika ya wale wanafunzi wawili, nayo ikamwangukia Mathiya, na likawa kweli ni chaguo la Mungu.(Matendo 1:15-19),
Hata wakati wa nchi ya Israeli kugawanywa . Kura zilitumika kuamua nani akae wapi, na nani arithi wapi (Hesabu 26:55).
Hivyo kupiga kura ilikuwa ni mojawapo ya njia kuleta jibu lisilokuwa na upendeleo. Au lililoegemea upande Fulani mmoja. Na kwa kufanya hivyo malalamiko mengii yalikomeshwa kwasababu maamuzi hayakuamuliwa na upande wowote ule.
Ndio maana ya hili andiko
Mithali 18:18
[18]Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.
Hata kipindi Cha sasa njia ambayo hutumiwa kuchagua viongozi wengi ulimwenguni Huwa ni ya kura. Isipokuwa hii siyo ya kurusha SHILINGI, au kete angani inayomwangukia mmojawapo ndio anakuwa kiongozi..hapana Bali ni kuruhusu Kila mmoja kutia maoni yake..Kisha zinahesabiwa na yule mwenye nyingi hupewa. Na hivyo hakuna malalamiko.
Tofauti na Ile mtu atawadhwe tu Moja Kwa moja kuwa kiongozi, Hiyo huleta ukakasi mwingi.
Hivyo ni kutufundisha kua Bwana anaouwezo wa kuingilia kura zipigwazo na kuleta majibu yake sahihi..hususani pale anaposhirikwa Kwa maombi, na kama hakusema Kwa njia nyingine ya Moja Kwa moja.
Bwana akubariki
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?
Mzushi ni nani kibiblia? (Tito 3:10).
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?
Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo vya ndoa?
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake
Nini maana ya Mithali 27:21 inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”
Swali: Biblia inatufundisha katika Wagalatia 5:23 kuwa “tuwe wapole kiasi”, sasa napenda kujua mtu utakuwaje mpole kiasi.
Jibu: Tusome,
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 UPOLE, KIASI; juu ya mambo kama hayo hakuna sharia”.
Hapa biblia haisemi kuwa tunda la Roho Mtakitifu kuwa ni “Upole kiasi” kana kwamba “upole unapaswa uwe na kiasi”…. La! Bali inasema tunda la Roho ni “Upole”, halafu “Kiasi”… hayo ni maneno mawili yaliyotengenishwa na alama ya mkato.
Maana yake “Upole” ni kitu kingine na “Kiasi” ni kitu kingine. Ikiwa na maana kuwa Tunda la Roho “Upole ulio wote” na sio upole kiasi.
Biblia inatufundisha tuwe watu wapole kama Hua (Njiwa).
Mathayo 10:16 “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua”
Hua ni ndege mpole sana ndio maana Roho Mtakatifu alitumia umbile la Hua kushuka juu ya Bwana Yesu wakati ule alipobatizwa (Mathayo 3:16)... Na maandiko yanazidi kutufundisha kuwa Bwana Yesu ni Mpole..
Mathayo 21:5 “Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, MPOLE, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda”.
Soma pia, Mathayo 11:29, utaona sifa hiyo ya Bwana ya upole ikitajwa..
Na sisi pia ni lazima tuwe na sifa hiyo ya “Upole” kama ishara mojawapo ya kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu… shetani kaligeuze Neno hili la Upole na kuweka “Upole kiasi” ili kuchochea ubaya ndani ya watu.. Kwamba ni vizuri kuwa wapole lakini tusiwe wapole sana, tuwe wapole tu kiasi!. Huo ni uongo wa adui!.
Na kumbuka kuna tofauti ya “upole” na “unyonge”. Biblia haitufundishi kuwa wanyonge, bali kuwa wapole, Mtu mpole ni yule ambaye ana uwezo wote wa kutumia ukali lakini hautumii!, kama alivyokuwa Bwana Yesu… Lakini mnyonge ni yule anayekuwa analazimika kuwa hivyo mpole kutokana tu na mazingira..na akitoka katika hayo mazingira basi tabia yake ya ubaya na ukali usio na maana na vurugu inajidhihirisha.
Bwana atusaidie .
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.
Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).
Jibu: Tusome kuanzia mstari wa 5..
Zaburi 91:5 “Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri”.
“Uele” ni janga linaloleta mauti linaloweza kumpata mtu.. ajali ya gari ni mfano wa Uele, Ajali ya kuzama kwenye maji ni mfano wa “Uele”, janga la kuungua moto mpaka kufa ni mfano wa “Uele”.
Maandiko yanatufundisha kuwa wote wamtumainio Bwana, na kumkimbilia na kumfanya kuwa ngome na msaada, hawatakuwa na hofu na majanga hayo, kwani Mungu ni ngome ya wote wanaomcha, naye ndiye awaokoaye na majanga.
Zaburi 121:4 “Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.
6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
7 BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele”.
Je una hofu na UELE?..Mpokee Yesu kwa kutubu dhambi na kujazwa Roho Mtakatifu, naye atakupa furaha nawe utaishi maisha ya raha na ya utulivu.
Zaburi 127:2 “……Yeye humpa mpenzi wake usingizi”
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?
Je! Mungu anasababisha ajali au Majanga?
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).
Fahamu Maana ya Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”.
Mara nyingi Sulemani kwa hekima ya Roho aliongozwa kuona uhusiano uliopo kati ya uvivu na umaskini. Kama tu kinyume chake, sehemu nyingine alivyoweka uhusiano kati ya bidii na utajiri(Mithali 10:4). Vivyo hivyo uvivu na umaskini havipishani.
Na kama anavyosema hapo, uvivu humpeleka mtu katika usingizi, lakini sio usingizi tu bali ule mzito, Kwasababu gani? Ni kwasababu mwili haupo katika hali ya kujishughulisha, na hivyo utalala tu, na Bado utaendelea kulala siku baada ya siku.. Na matokeo yake kutokuzalisha chochote kinachoonekana, hatimaye, umaskini unaingia.
Hivyo mstari huo unalenga Nyanja mbili. Ya kwanza ni ule uvivu wa mwilini, na ya pili ni ule uvivu wa rohoni.
Mungu katuumbia kufanya kazi, watu wote (ikiwemo watakatifu). Maana yake ni kuwa ikiwa huna huduma yoyote ya madhabahuni Bwana amekuitia, ambayo inakufanya utumike muda wote hapo. Ni sharti ufanye kazi. Mtume Paulo alilionya kanisa juu ya watu ambao hawafanyi kazi kwamba ni sharti wajishughulishe ili wapate na kitu cha kuwagawia na wengine (2Wathesalonike 3:10)
Lakini pia Uvuvi wa rohoni. Mtakatifu anapokuwa mvivu, kusoma Neno, yaani muda wa Neno anakwenda kutazama filamu, anakwenda kijiweni kucheza drafti,.Anakuwa mvivu kuomba, Unapofika huo muda tu anaona usingizi ni bora kuliko kuomba,.Au Mtakatifu hataki kushuhudia habari za Kristo kwa wengine, anasema jua kali. Sasa mtu huyo anajiandaa kuwa maskini kiroho. Yaani atakuwa katika wokovu usiokuwa na matunda, ukuaji wake wa kiroho utakuwa hafifu, Neema ya Mungu haitatenda kazi kwa wingi juu yake, na hivyo atakosa mema mengi ya Mungu katika safari yake wa wokovu hapa duniani.
Uvuvi wowote, una hasara, kwahiyo tuuweke katika orodha ya maadui zetu wa imani.
Bwana atusaidie.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?
Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni ipi?
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
SWALI: Nini maana ya Mithali 24:11 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe.
JIBU: Mstari huu una maana mbili,
Mana ya kwanza ni uhai kama ‘uhai’ alionao mwanadamu yoyote,
Maana yake ni kuwa uonapo, mtu asiyekuwa na hatia, amepangiwa njama za kuuliwa, au ndio anakaribia kufa, na wewe unaowezo wa kumsaidia huna budi kufanya hivyo wala usijifanye kama hiyo sio biashara yako.
Ni mfano wa Yule mtu aliyevamiwa na wanyang’anyi ambaye Bwana Yesu alimtolea mfano, akasema mlawi alimpomwona akapita kando, kuhani naye alipomwona akapita kando, lakini Yule msamaria akamuhurumia, akamtibu, akaokoa uhai wake. Na Yesu akasema huo ndio Upendo.(Luka 10:25-37)
Ni sawa na wakati ule Paulo amepangiwa njama na wayahudi wamvizie auawe, lakini mjomba wake alipogundua alikwenda kumjuza akida wa kikosi (Matendo 23:12-22). Huyo amemwopoa aliyekaribu na kuchinjwa.
Ni sawa na Mordekai alichofanya kwa Mfalme, Ahusuero, wale watu walipopanga njama ya kumuua akaenda kuwasemelea (Esta 6:1-12),. Ni sawa na Yonathani, alivyomtunza Daudi dhidi ya upanga wa baba yake Sauli ili asiuliwe. Hivyo hawa wote, walilitambua andiko hili, na wala hawakuogopa kutoa siri, za wale waliokusudia mabaya juu ya maisha ya wengine.
Hata leo, vifo vingi vya kikatili, vingeweza kuzuilika kwa sehemu kubwa, endapo baadhi ya wanaojua matukio hayo wangetoa taarifa mapema. Kwamfano utaona mtu anawekewa sumu kwenye chakula, wewe unayejua, ni wajibu wako kutoboa siri hiyo, ili uutunze uhai wa mtu. Utaona mwizi anapigwa, huna budi kuripoti polisi mapema maadamu jambo hilo lipo ndani ya uwezo wako, ili askari waje kumkamata wampe wao adhabu stahiki, lakini ukipita ukasema hainihusu, atachomwa moto. Lakini kumbuka uhai unathamani, hata wa mtu aliye mbaya, unathamani nyingi.
Lakini ukisema hainuhusu, Utakuwa unajipunguzia pia rehema nyingi kwa Mungu, ndio maana mstari unaofuata unasema;
Mithali 24:11 “Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. 12 Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?”
Hivyo penda uhai, pia tunza uhai wa watu, popote pale uonapo unahatarishwa. Usiwe mzito kusaidia.
Lakini maana ya pili ya mstari huu ni ule Uhai wa rohoni.
Wapo watu ambao ibilisi, anakaribia kuwameza, na ukiwaacha ndani ya kipindi kifupi hakika wataangamia kabisa kiroho. Wengine wanakaribia kufa kwasababu ya huzuni mioyoni mwao, kukata tamaa, kwasababu ya dhiki na magonjwa, wengine wanakaribia kuzama katika ushirikina, wengine kwenye imani potofu ambazo zinakwenda kuwaua roho zao n.k. Hivyo makundi kama haya, unapoyaona, mwelekeo wao wewe kama mkristo uliyesimama huna budi kuwasaidia ili waokoke, wasipotelee katika mauti ya roho zao, na kwenye minaso ya adui mfano wa Yuda. Wala usisime hiyo sio shughuli yangu.
Yuda 1:22 “Wahurumieni wengine walio na shaka, 23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.
Hivyo tutunze Uhai, wa mwili na Roho za watu wa Mungu, naye Bwana atatunza na wetu.
Bwana akubariki
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?
Biblia inamaanisha nini inaposema “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake”?
Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?
Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?