SWALI: Naomba kufahamu maana ya huu mstari;
Mithali 17:17 “Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu”.
JIBU: Huu mstari unaeleza rafiki wa kweli anapaswa aweje, pia rafiki ambaye atazidi kuwa kama ndugu anapaswa aweje?
Anasema ‘Rafiki hupenda sikuzote’, Ndio.. hii ni tabia ya rafiki wa kweli, hupenda nyakati zote, ziwe ni nzuri , au ni mbaya, kwamfano, rafiki ambaye siku umemfurahisha anakupenda, lakini siku pia umemuudhi anakupenda, siku umempa anakupenda, lakini siku umemnyima bado anakupenda zaidi. Rafiki ambaye wakati mnawasiliana anakupenda, lakini wakati mlipopotezana kimawasiliano kwa muda mrefu bado anakupenda.
Huyo ndio rafiki wa kweli..
Lakini hapo anaposema “Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu” ..Maana yake ni kuwa Yule ambaye anakuwa na wewe bega kwa bega, katika wakati wa shida zako, na taabu zako, na misiba yako huyo si rafiki tena bali ni ndugu..
Unamwona anakujali, wakati unaugonjwa wa hali ya juu, unamwona, anakushika mkono wakati umefilisika, unamwona unakufariji sana wakati wa msiba wako, unamwona anatafuta kila mbinu, kukusogeza mahali wakati upo katikati ya mateso. Huyo ni rafiki aliyefanyika ndugu.
Kwasababu kama hapo inavyosema ‘ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu’..Maana yake ili mtu aitwe ndugu, ni lazima awe amezaliwa mahususi kwa ajili ya siku za shida zako.
Je! Na sisi tunapoitana ‘ndugu’ na ‘rafiki’ tunatambua wito wetu katika hayo?
Lakini tunamwona mmoja ambaye, ni zaidi ya rafiki, ni pia ni zaidi ya ndugu, ambaye sio tu amekuwa karibu na sisi katika shida zetu, na mateso yetu na hukumu zetu.. Lakini pia aliyatoa maisha yake yote, pamoja na uhai wake, ili kufa kwa ajili yetu.
Yohana 15:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.”
Hivyo basi, hatuna budi na sisi kuuthamini upendo mkuu namna hii, kwa kukubali kukombolewa na yeye, ili tuoshwe dhambi zetu. Kumbuka hakuna ukombozi nje ya Yesu Kristo, vilevile hakuna uwezekano wowote wa sisi kumpendeza Mungu kwa matendo yetu wenyewe. Na ndio maana ilimpasa aje, ili atukomboe, kutoka dhambini.
Waebrania 2:3 “sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia”;
Ikiwa upo tayari kumkabidhi Bwana Yesu maisha yako, basi waweza wasiliana nasi kwa namba zetu hizi, +255693036618/ +255789001312 kwa ajili ya mwongozo huo, bure, na hakika Bwana atayaokoa maisha yako, na kukufanya kuwa mpya tena.
Bwana akubariki.
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KAMA VILE UMEME UTOKAVYO MASHARIKI UKAONEKANA HATA MAGHARIBI.
Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?
Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?
Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo. Nakukaribisha tena tuzidi kuyatafakari maandiko.
Moja ya mambo ambayo, yalimuhuzunisha sana Bwana Yesu ni pale alipowatazama watu wake na kuwaona wanafanana na kundi la kondoo wafugwao waliopoteza tumaini kabisa na kutawanyika, kila mmoja mahali pake anapopajua yeye..Ina huzunisha sana..
Embu Tusome; kwa utulivu habari hiyo;
Mathayo 9:35-36
[35]Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
[36]Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa WAMECHOKA na KUTAWANYIKA kama kondoo wasio na mchungaji.
Hapo biblia inasema walikuwa WAMECHOKA..na KUTAWANYIKA.
Kuchoka kunakozumgumziwa hapo, sio tu kule kwa kutembea umbali mrefu, katika kutafuta chakula / maji…hiyo ni sehemu ya kwanza..Bali kuchoka kunakolengwa hapo hasaa kunakuja kutokana na kukandamizwa, kujeruhiwa, na kufukuzwa, kutishwa..pamoja na hofu na wasiwasi wa mashaka ya kuraruliwa na mbwa mwitu wakali.
Hii ndio hali halisi yasasa.. Watu wa Mungu WAMECHOKA. Sio kidogo bali wamechoka kwelikweli, Kutokana na kudanyanywa, kuumizwa na watumishi wa uongo, wameharibiwa, wametawanywa.., manabii wa uongo wamechukuliwa fedha zao wakiwaahidia kubarikiwa na kufunguliwa, lakini mwisho wa siku wanajikuta wapo katika matatizo zaidi, wanahangaika huku na kule kutafuta msaada wa kumkaribia Mungu, lakini hawauoni,
badala wapewe tiba ya Neno la Mungu wanapewa maji ya upako, wanafika makanisani badala wahubiriwe Yesu, wanahubiriwa bikira Mariamu na watakatifu wa kale, na sala za wafu, badala wahubiriwe neema iliyo katika Kristo Yesu, wanahubiriwa siri zilizo ndani ya wachawi.
Imefikia hatua watu wamekata tamaa kabisa, kila mmoja anaona ni heri, asiamini kanisa lolote, ajisalie tu peke yake nyumbani..kuliko kwenda na kusikiliza madanganyo. Ni ni mbaya sana..
Ndio jambo ambalo Bwana Yesu analiona sasa hivi ulimwenguni..na kulihurumia kundi lake jinsi lilivyotawanyika…na kuonewa sana..
Ikiwa wewe ni mhubiri, halafu hutimizi wajibu wako wa kuwaongoza watu katika njia sahihi..ujue kuwa utawajibishwa siku ile mbele za Bwana.
Kama tunaigeuza kazi ya Mungu biashara, hatujali maisha ya kiroho ya watu wa Mungu, hata wakija watakavyo kanisani tunaona ni sawa, …tufahamu kuwa tutawajibishwa na Bwana siku ile.
Yeremia 23:1-4
[1]Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema BWANA.
[2]Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu, Mmetawanya kundi langu, na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama; angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema BWANA.
[3]Nami nitakusanya mabaki ya kundi langu, katika nchi zile zote nilizowafukuza, nami nitawaleta tena mazizini mwao; nao watazaa na kuongezeka.
[4]Nami nitaweka juu yao wachungaji watakaowalisha; wala hawataona hofu tena, wala kufadhaika, wala hatapotea hata mmoja wao, asema BWANA.
Tujiulize, sisi tunaosema tumeitwa kumtumikia Bwana.. Ni utumishi gani tunaoufanya? Tunadhani watu wa Mungu watapotezwa sikuzote?
Mungu anajua kuwakusanya watu wake. Na atawanyanyulia watumishi waaminifu. Sawasawa na Neno lake. Lakini sisi wengine tutawajibishwa.
Bwana atusaidie.
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Gongo na Fimbo ni nini? Na vinawezaje kumfariji mtu? (Zaburi 23:4).
“Nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika”,Maana yake nini?
NI LIPI KATI YA MAKUNDI HAYA, WEWE UPO?
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, Mkuu wa mbingu na nchi libarikiwe.
Kitabu pekee chenye mwongozo kamili wa maisha ni biblia takatifu, Mtu mmoja wa Mungu aliwahi kusema “endapo nikifungiwa katika chumba chenye giza, nikapewa mshumaa na biblia, basi ninaweza kueleza yote yanayoendelea nje katika ulimwengu”.
Hakika hiyo ni kweli kabisa..kwasababu biblia ndio kitabu pekee kinachoelezea uhalisia wa nyakati na majira tunayoishi, na mambo yajayo..
Leo napenda tujifunze kanuni moja rahisi ya kupokea baraka..Wengi wetu, tunategemea maombi tu, tunakuwa tunatumia nguvu nyingi katika kuomba ili kusudui tupokee baraka katika mwili, lakini ipo kanuni moja rahisi ya kupokea baraka.. Na kanuni hiyo Bwana Yesu aliisema katika Marko 4:24..
Marko 4:24 “Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho NDICHO MTAKACHOPIMIWA, na TENA MTAZIDISHIWA”.
Hapo nataka tuyatazame hayo maneno miwili. 1)Kipimo mpimacho ndicho mtakachopimiwa. na 2) tena mtazidishiwa
Maana yake ni kwamba Kama utampimia mwingine kwa kumpa “sh.elfu moja”..basi Bwana atahakikisha anakurudishia kwa njia nyingine hiyo “elfu moja” uliyoitoa. (Huenda ikawa siku hiyo hiyo, au wakati mwingine ambao haupo mbali sana).
Lakini haiishii hapo tu kukurudishia hiyo elfu moja..bali anaendelea kwa kusema “na tena mtazidishiwa”.
Ikiwa na maana kuwa Bwana akishakurudishia kile ulichokitoa, sasa kinachofuata ni yeye kukulipa wema ulioufanya kwa “kwa kukuzidishia”.
Maana yake atakupa na kingine kingi zaidi ya hiyo elfu moja uliyoitoa,
Sasa ili tuelewe vizuri ni kiasi gani tutazidishiwa, hebu tuyatazame tena maneno ya Bwana Yesu katika Luka 6:38.
Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa”.
Hapa nataka tuugawanye tena mstari huu katika sehemu mbili.
1) Wapeni watu vitu nanyi mtapewa na 2) Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa kifuani mwenu.
Maana yake tunapowapa watu, kipimo fulani labda elfu moja na sisi Bwana ataturudishia hichohicho kipimo cha sh elfu moja…lakini hataishia hapo, kwasababu akishaturudishia kipimo kile tulichokitoa, ndipo anaanza kutubariki kwa wema tulioufanya, sasa swali anatubariki vipi?..
Anatubariki kwa kutumia hao hao watu kutupa sisi vitu vifuani mwetu kwa kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika..Haleluyaa!!
Kwahiyo kama umetoa elfu moja kwa moyo mzuri na mwema Basi Bwana atakurudishia hiyo elfu moja yako, na atakuzidishia na nyingine nyingi kwa kiwango cha kujaa na hata kumwagika…(unaweza kutafakari jinsi zilizvyo nyingi fadhili zake)..huenda ikawa zaidi ya mamilioni..
Jifunze kuwa mtoaji, kama unataka kupata baraka maradufu.
Maran atha
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano.
Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?.
JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
Swali: Ule mretemu ambao Nabii Eliya alijilaza chini yake ulikuwa ni aina gani ya mti, na je una muujiza wowote kiroho? (1Wafalme 19:4).
Jibu: Mretemu ni aina ya mti ujulikanao sasa kama “MTARAKWA”. Zipo jamii nyingi za mitarakwa kulingana na mahali na mahali. Mtarakwa unaomea katika bara la Afrika ni tofauti kimwonekano na ule unaomea katika bara la Ulaya, (kutokana na hali ya hewa). Lakini yote inamatawi yanayofanana na tabia zinazofanana, kinachoitofautisha ni unene na urefu.
Mti wa Mtarakwa (au Mretemu) ni mti unaovumilia ukame sana, na kamwe matawi yake hayapotezi rangi yake ya ukijani, hata kama yatapitia ukame mkali.
Ndio maana utaona kipindi Eliya anamkimbia Yezebeli, tayari dunia nzima ilikuwa ni jangwa kwasababu mvua haikunyesha kwa miaka mitatu na nusu, na Eliya anauona mretemu na kukaa chini ya uvuli wake, sasa kikawaida mti uliokauka na ukame hauwezi kuwa na uvuli.
1 Wafalme 19:4 “Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi CHINI YA MRETEMU. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
5 Naye akajinyosha akalala chini ya MRETEMU; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule”
Kutokana na sifa hiyo, na jinsi malaika alivyomtembelea Eliya alipokuwa chini ya huo mretemu(au mtarakwa), basi inaaminika kuwa mti huo, una miujiza fulani kiroho.
Vile vile miti hii ya Miteremu/mitarakwa inatumika katika tamaduni nyingi kama miti ya Krismas (Chrismass tree).
Asili ya mti huo kutumika kama alama ya Krismasi ni hadithi ya inayoaminika na baadhi ya watu kuwa kipindi Herode anataka kumwua mtoto Yesu, pale alipotoa amri ya kuuawa kwa watoto wote walio chini ya umri wa miaka miwili, inaaminika kuwa askari wa Herode walipomkaribia Yusufu na Mariamu ili wamwue mtoto, walikuwa karibu na huu mti wa Mteremu, na ghafla ukawafungukia matawi yake yakawaficha, askari walipokuja hawakumwona Yusufu, Mariamu pamoja na mtoto.
Hiyo ndio maana mpaka leo, watu wanautumia mti huo kama alama au nembo ya Krismas.
Lakini swali ni je!. Ni kweli mtu huo umebeba miujiza yoyote kiroho?.
Jibu ni la!. Mti wa Mretemu/Mtarakwa hauna muujiza wowote kiroho, ni mti tu kama miti mingine, sifa yake ya kuvumilia ukame ndiyo inayowachanganya wengi, lakini kiuhalisia ni mti tu kama miti mingine.
Na zaidi sana, si kweli kwamba mti huo ulimsaidia Mariamu na Yusufu kuwalinda dhidi ya Mauaji ya Bwana Yesu.. Hizi ni hadithi za kutunga, ambazo zimetungwa kwa uerevu wa akili za watu, uliovuviwa na shetani mwenyewe.
Kwasababu Yusufu tayari alikuwa ameshaondoka Bethlehemu kabla ya Herode kuanza mauaji. Hivyo kusema kwamba mti uliwasaidia huo ni uongo wa shetani.
Na si tu mti huu ni wa kawaida, bali hata miti mingine yote haina miujiza yoyote kiroho, kitu pekee ambacho kinaweza kutuletea miujiza chanya katika maisha yetu ni KUISHI MAISHA MAKAMILIFU na kitu pekee kinachoweza kutuharibia maisha yetu ya hapa na yajayo ni MAISHA YA DHAMBI..Na si miti wala kitu kingine chochote.
Hivyo kwa hitimisho, ni kuwa Mretemu ni mti wa kawaida, na hauna muujiza wowote kiroho.
Kama hujaokoka, kumbuka hizi ni siku za mwisho, na Yesu yupo mlangoni kurudi. Mwamini leo, akuoshe dhambi zako, na kukupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?
Mti wa MLOZI alioonyeshwa nabii Yeremia 1:12 tafsiri yake ni nini?
Mti wa Mshita ni mti wa namna gani?
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?
Kwa tafsiri za kidunia mtu asiye na akili ni mtu ambaye hawezi kufiriki, kuelewa, kuwasiliana, kupanga au kutatua matatizo. Hivyo, mwanadamu mwenye mtindio wa ubongo, anajulikana kama hana akili, mtu anayefeli darasani, anajulikana kama hana akili, mtu anayeshindwa na wenzake katika maisha anajulikana pia kama asiye na akili.
Lakini je! Biblia nayo inasemaje kuhusiana na mtu asiye na akili. Sifa zake ni zipi.
Zifuatazo ndizo sifa za mtu asiye na akili mbele za Mungu, ikiwa wewe unayo mojawapo au zote, basi fahamu huna akili, haijalishi utakuwa ni wa kwanza, kimaisha, au kielimu, au kicheo. Mungu anakuona unao mtindio wa ubongo, hujakamilika. Na matokeo yake utashindwa kutumia akili zako zote kumpenda yeye kama alivyotupa maagizo katika ‘Mathayo 22:37’
Zaburi 14:2 “Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. 3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja”.
Ukishaona Mungu hana umuhimu kwako, ni uthibitisho tosha,akili zako zimepunguka kwa kiasi kikubwa mno. Ni sawa, na mbwa asiyemjua bwana wake anayemfuga siku zote. Au mtoto asiyemtambua mama yake amnyonyeshaye kila siku. Fanya bidii kumtafuta Muumba wako, kwasababu hilo ndio jaribio la kwanza alilotuumbia Mungu, ili kuthibitisha kwamba kweli sisi ni wanadamu tuliokamilika, tunaweza kumtafuta aliyetubuni.?
Mithali 11:12 “Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza”.
Ukishajiona wewe ni bora kuliko mtu mwingine, au unamwona mwenzako hana lolote jipya la kukufaa wewe, tambua kuwa tayari akili yako imeathirika, fanya haraka sana, kujirekebisha katika eneo hilo, ili usipoteze upeo wako wa kufikiri vema, na wa kupambanua mambo. Kamwe usimdharau mtu yeyote duniani. Hata kama ni mpumbavu wa mwisho.. Kwasababu Mungu naye hamdharau mtu aliyemuumba japokuwa ni mnyonge (Ayubu 36:5)
Mithali 28:16 “Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake”.
Kumuonea mtu kwasababu ya unyonge wake, au udhaifu wake, ni jambo la hatari sana. Ukimdhulumu mwenzako, au kumnyima haki yake, au kutumia hila kumwibia kisa tu hana maarifa ya jambo hilo, kumpiga mkeo, au watoto bila sababu, basi fahamu kuwa wewe ni sawa ni mjinga mbele za Mungu.. Tukae mbali na uonevu wa aina yoyote.
Mithali 6:32 “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”.
Uzinzi, ni kipingamizi sio tu cha kiroho, bali pia cha kiakili. Watu wazinzi, wanajiharibia sana uwezo wao wa kupambanua mambo ya kiroho kwa sehemu kubwa sana. Kwasababu Roho Mtakatifu huwa anategemea miili yetu kutenda kazi, hivyo mwili wako unapochafuliwa, hawezi kupata nafasi ya kuwa mwalimu wako. Ndio hapo Unabaki tu kuwa wewe kama wewe, kama mnyama tu. Epuka uzinzi kwa gharama zote, ni hatari..
Mithali 15:24 “Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini”.
Hapo biblia inatueleza wazi, mtu mwenye akili, huwaza ni jinsi gani atakavyoepukana na kuzimu iliyo chini, huwaza kwenda mbinguni, huwaza kuepukana na ziwa la moto. Lakini kinyume chake ni kweli, mtu asiyewaza hatma ya maisha yake baada ya kufa itakuwaje, badala yake yupo tu, anachowaza ni ajengeje magorofa hapa duniani, ukimweleza habari za kuzimu hata hashtuki, huyo kwa Bwana hana akili.
Mithali 10:8 “Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka”
Ukiwa ni mtu wa kupinga maagizo mema, unayopewa, bali unajiona upo sawa machoni pako mwenyewe, ukielezwa, uvaaji vimini ni dhambi, unasema hatupo agano la kale, unapoelezwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo ni lazima, unasema sisi hatuamini hilo. Ujue kuwa unajiangamiza mwenyewe. Kila agizo lililo kwenye Neno la Mungu linapaswa lipokelewe na kukubaliwa kama lilivyo pasipo kuuliza uliza.
Mithali 10:14 “Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu”.
Ukiwa mtu wa kutozingatia, au kutotendea kazi kile unachoambiwa au kukisikia, kuhusiana na mafundisho ya adili, yaani unasahau sahau, amri au fadhili za Mungu, unakuwa mwepesi kuanguka ovyo katika dhambi, ni uthibitisho kuwa huna akili kwa mujibu wa kibiblia. Tunapaswa tuwe watu wa kuzitafakari sheria za Mungu wakati wote, kama vile mwanafunzi akaririvyo kila siku masomo yake, ili yamsaidie kufaulu mitihani yake ya mwisho.
Mithali 3:3 “Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu”.
Mithali 24:30 “Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
31 Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake”.
Ukiwa mvivu, wa kufanya kazi ya Mungu. Bwana anasema huna akili, yaani Ikiwa hujishughulishi na chochote, unajitafutia matitizo yako mwenyewe. Tumeumbwa, tujishughulishe, kama Mungu alivyojishughulisha..Kama huwezi mtumikia Bwana kwa kujitoa kwa asilimia zote kwenye kazi yake, ni lazima ufanye kazi ya mikono, ili ufanikiwe. Lakini tukishindwa kujishughulisha, ni kwa hasara yetu wenyewe.
Hivyo tukiwa tuna mojawapo ya tabia hizo ni busara tukazidhibiti ndani yetu. Ili tuweze kuishi kwa akili Bwana anazotaka tuwe nazo.
Zingatia: Mungu anazungumza na mtu mwenye akili timamu, rohoni. Ni lazima tufikie hapo ili Bwana aseme na sisi.
Bwana atusaidie.
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?
Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?
Nini maana ya ‘Hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma’?
Jina la Bwana na Mwokozi wetu YESU Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia (Neno la Mungu wetu) lililo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu (Zaburi 119:105).
Biblia inasema katika kitabu cha Yakobo…
Yakobo 4:17 “Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi”
Kumbe haihitaji kwenda kuua, au kuiba, au kuzini ndipo ihesabike kuwa ni dhambi, bali hata “kujua tu kitu kilicho sahihi na kutokukifanya hicho” tayari ni dhambi mbele za Mungu!!!. Hii inaogopesha sana!!.
Ukijua kuwa unapaswa umtumikie Mungu, halafu humtumikii hiyo tayari inahesabika kuwa ni dhambi.
Ukijua kuwa unapaswa Uwe mwombaji, halafu hauombi hiyo tayari kwako ni dhambi.. Na watenda dhambi wote hawataurithi uzima wa milele, kulingana na maandiko.
Ukijua kwamba unapaswa uwe unawaombea wengine, halafu hufanyi hivyo, aidha kwasababu ya chuki au vinyongo au hasira, fahamu kuwa unatenda dhambi..
1Samweli 12:23 “Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi..”
Ukijua kuwa unapaswa uhubirie wengine habari njema za wokovu, wawe kama wewe, na hufanyi hivyo, basi fahamu kuwa unafanya dhambi!. Na watenda dhambi wote ni wana wa ibilisi na hawataurithi uzima wa milele.
1Yohana 3: 8 “Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi”.
Ukijua kuwa unapaswa ukabatizwe na hautaki kubatizwa au unapuuzia ubatizo, basi fahamu kuwa unafanya dhambi kulingana na andiko hilo “yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi”.
Ukijua kabisa kwamba unapaswa “ulisome Neno (yaani biblia)”, lakini hufanyi hivyo, kwa visingizio Fulani fulani.. Fahamu kuwa unatenda dhambi, na wewe ni muasi kulingana na biblia.
1Yohana 3:4 “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi”.
Ukijua kuwa unapaswa ufanye ibada na kukusanyika na wengine kanisani, kumfanyia Mungu ibada kulingana Waebrania 10:25, lakini wewe hufanyi hivyo, badala yake unabaki nyumbani umelala, au unaenda kufanya shughuli zako nyingine, basi fahamu kuwa unafanya dhambi..
Waebrania 10:25 “wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia”
Kaka/Dada usilipuuzie kamwe Neno la Mungu,..Unaposikia maonyo ya Neno la Mungu, usiyasikilize tu kama taarifa ya habari, na kuyaacha yapite, au kuyaweza akiba moyoni, bali yafanyie kazi kuanzia wakati ule ule unapoyasikia.. Kwasababu usipoyafanyia kazi baada ya kuyasikiliza basi kwako inahesabika kuwa dhambi, na hivyo utahukumiwa sana siku ile, Bwana Yesu alisema maneno yafuatayo..
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana”
Jiepushe na hukumu ya Mungu!!, Litendee kazi Neno baada ya kulisikia.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
JE UNA MATUMAINI YA KUPATA TENA KILE ULICHOPOTEZA?
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
Mume: Kumpenda mke wake Kama mwili wake mwenyewe, ( Waefeso 5:25): Ikiwemo kumuhudumia kiafya, kimavazi, kimalazi, na kiroho.
Mke: Kumtii Mume wake: Kumsikiliza, kumuheshimu, kukubali kuongozwa. (Waefeso 5:22).
Wote: Haki ya ndoa. (1Wakorintho 7:5)
Lakini ikitokea mmoja, ameshindwa kusimama katika nafasi yake, labda tuseme, mume hamjali mkewe, anampiga, anatoka nje ya ndoa, anamtukana, hamtimizii majukumu yake ya kimwili na watoto wake. Afanyaje?
Au mke hamweshimu mume wake, anamdharau, anafanya ukahaba, anamzungumzia vibaya kwa watu wa nje, anajiamulia mambo yake mwenyewe pasipo kumshirikisha mumewe..afanyaje?
Je! na yeye aache kutimiza wajibu wake?
Jibu ni hapana: Embu wazia hili jambo; Ulishawahi kuishi katika nyumba ya kupanga, ambapo mnajikuta wapangaji mpo 10 mnashea umeme au maji, na kila mwisho wa mwezi bili inakuja, na mnapaswa muigawanye sawa sawa kwa kila mmoja wenu. Kwa kawaida hapo panakuwa na ukinzani mkubwa, kwasababu wapo wengine watasema, mimi sina matumizi mengi kama ya Yule.. Na hiyo inapelekea mwingine kujiongezea matumizi yake kwa makusudi ilimradi tu afanane na wale wengine, labda atufungulia bomba la maji ili yamwagike, ili mwisho wa mwezi utakapofika alipe sawasawa na matumizi ya wale wengine.
Lakini hajui kuwa anajiumiza yeye mwenyewe na wale wenzake, kwasababu anapoongeza matumizi ndipo gharama inapokuja juu zaidi, atalipa zaidi ya mwanzo. Ni heri angebakia vilevile akubali kuumia yeye, ili wote wapone.
Ndivyo ilivyo katika ndoa ikiwa mmoja hatimizi wajibu wake wa kindoa, suluhisho sio mwingine kujibu mapigo, bali ni kuendelea hivyo hivyo katika nafasi yake. Ili kuinusuru ndoa. Kama mwanaume hakupendi, wewe mtii, mweshimu, msikilize, kama mwanamke hakutii, wewe mpende, mpe haki yake, ..
Biblia inasema; .. 1Petro 3:1 “Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu”.
Inaendelea kusema;
1Wakorintho 7:16 “Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?
Haijalishi itachukua miaka mingapi. Kuwa mvumilivu, timizia wajibu kwao. Hayo mengine mwachie Mungu.
Mithali 25:21 “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; 22 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu.
Hili andiko linaingia pia kwa wanandoa. Wakati unaona kama wewe unaonewa, hujui kuwa Yule mwingine anateswa rohoni anapoona hurudishi mapigo, hilo jambo linakuwa ni moto mkubwa ndani yake, na sikumoja tu, atakuja kwa machozi, na kutubu mbele zako. Ni kitendo cha muda.
Unapoumizwa, usidhani kuwa Mungu haoni, lakini unapomwachia Mungu yote, basi yeye peke yake ndiye atakayeshughulika kutafuta njia ya kutatua hilo tatizo. Kiboko cha Mungu kitapita, kitamnyoosha. Hivyo unapaswa uwe mtulivu, simama katika nafasi yako. Bwana atamtengeneza yeye mweyewe.. au atatengeneza njia kwa namna nyingine. Hivyo dumu katika utakatifu.
Warumi 12:17 “Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
18 Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana”.
Zingatia hayo, usirejeshe ubaya kwa mwanandoa mwanzako.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WANA-NDOA; FAMILIA TAKATIFU: Marimu na Yusufu.
Karibu katika mwendelezo ya Masomo ya wanandoa . Ikiwa wewe ni mwanandoa au unajiandaa kuingia katika ndoa, basi masomo haya ni muhimu sana kwako kuyajua.
Tulishatazama, huko nyuma jinsi ndoa ya kwanza ya wazazi wetu Adamu na Hawa ilivyokuwa, na changamoto walizokutana nazo, na jinsi walivyoweza kukabiliana nazo. Ikiwa hukupata masomo hayo, basi utatumia ujumbe inbox tukutumie.
Leo tutatazama familia nyingine takatifu. Ambayo ni ya Yusufu na Mariamu. Yapo mambo mengi sana ya kujifunza, juu ya wanandoa hawa, Na ndio maana kwanini Mungu alikusudia mwokozi wa ulimwengu aje kwa kupitia watu hawa, Ni Kwasababu kuna mengi ya kujifunza kwao. Tutaona pia utaratibu Mungu aliowawekea katika kutimiza kusudi lake hapa duniani.
Alikuwa ni mtu aliyeepuka madhara kwa wengine: Yusufu hakuwa kama Samsoni, ambaye alipoona mwanamke aliyemchumbia amepewa rafiki yake, akakasirika, na kwenda kuchukua mbweha mia tatu, na kuwapeleka kwenye shamba la ngano la wafilisti, kuyateketeza ili ajilipizie kisasi (Waamuzi 15:1-20).
Lakini Yusufu hakuwa hivyo, yeye alipoona binti aliyemchumbua ana mimba, alitafuta njia ya kuepusha madhara kwa dada huyo, hivyo akakusudia ‘’kutomuabisha’’. Akapanga mipango yake ya kumuacha kwa siri,..huenda alipoulizwa vipi mbona humwoi msichana huyu, akawa anasema bado sijafikia muafaka, nitawapa majibu.
Mathayo 1:18 “Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri”.
Sasa Ikiwa alikuwa na hofu ya kumwaibisha asipigwe mawe, unatazamia vipi mtu kama huyu, angeweza kumpiga mke wake hata baada ya ndoa , au awe anatoa siri za madhaifu ya mke wake kwa watu wa nje?
Mwanamke anapoteleza, sio lazima wakati wote upeleke taarifa kwa jamii, aaibike au umpige, au umfukuze, bali ni kumvumilia, kwasababu mengine yanatokea kwa sababu ambazo utakuja kuzijua mbeleni. Tabia hii alikuwa nayo Baba-wa-Yesu (kimwili)
Alikuwa ni bikira: Ni binti ambaye alijitunza tangu anazaliwa mpaka anakuwa mwanamke, Na hiyo ikapelekea kupata neema ya kuchumbiwa na mzao wa Daudi (Yusufu). Kumbuka ahadi ya kuzaliwa Kristo haikuwa kwa Mariamu, bali ilikuwa kwa uzao wa Daudi. Hivyo Mungu alipomuona Mariamu, na ukamilifu wake katika mwili ndipo akasema huyu anafaa kupata neema ya kukutana na Yusufu atimize kusudi la Mungu.
Maana yake ni nini, upo umuhimu sana, wa msichana kujitunza sana mwili wake, kwani hiyo itakupelekea kupata mwanaume bora, na uzao bora. Ni kweli si wote wataingia katika ndoa wakiwa bikira, lakini ikiwa umetambua sasa, wajibu wako, na umeokoka, huna budi kujitunza sana, na hata baada ya ndoa, ili hicho kitakachotoka tumboni mwako kiwe kitakatifu.
SASA BAADA YA KUONA SIFA HIZI KUU (2), WALIZOKUWA NAZO HAWA WANANDOA, TUONE UTARATIBU WA KIMAJUKUMU JINSI MUNGU ALIVYOUGAWANYA KWAO.
Malaika Gabrieli alitumwa kwa Mariamu, ili kumpa taarifa ya kupata mimba kwa uweza wa Roho na kwamba mtoto huyo ataitwa Yesu.
Lakini baada ya hapo, Mungu hakuendelea tena kusema na Mariamu moja kwa moja. Bali alimgeukia mumewe Yusufu, na kumwagiza kuwa atakapozaliwa amwite jina lake YESU.
Mathayo 1:20 “Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao”.
Na utaona baada hapo, wakiwa kule Bethelehemu, bado Malaika anamtokea Yusufu tu, na kumwambia, mchukue mtoto na mama yake, wapeleke Misri, kwasababu Herode anataka kumuua mtoto.(Mathayo 2:13-14)
Tengeneza picha Mariamu angekuwa ni mwanamke kiburi, angesema, mbona Mungu hajasema na mimi kuhusiana na hilo?, Kwanza si wewe uliyembeba masihi, mateso huyajui, huko Misri ni nani unayemjua, nangojea Mungu anithibitishie kwanza mimi..lakini hakuwa hivyo alikubali kutii, bila kujadili jadili.
Bado utaona, akiwa kule Misri, malaika anamtokea tena Yusufu peke yake na kumwambia, mchukue mke na mtoto urudi nao Israeli kwasababu Herode amekufa. Safari tena ya mihangaiko ikaanza, huku Mariamu akisikiliza maagizo ya mumewe na kutii (Mathayo 2:19-20).. Lakini wakiwa pale Bethelehemu, wametulia ili sasa waanze maisha, saa hiyo hiyo, Yusufu anamwambia mke wake, tuondoke hapa tuende tena Nazareti, Mungu ameniagiza hivyo (Mathayo 2:22-23).
Mariamu hakuwa na kigugumizi kumsikiliza mume wake, hakuwa na kazi nyingine yoyote zaidi ya kupokea maagizo ya uongozi kuhusu familia au mtoto kutoka kwa mumewe.
Kwa mwanamke: Tambua kuwa mume ndio kichwa cha familia, Mungu atamtumia yeye, kuyalinda na kuyatamia maono yako, huwezi kufanikiwa bila yeye. Haijalishi Mungu kakuonyesha mambo makubwa kiasi gani hapo mwanzoni. Ikiwa humtii mume wako, ujue kuwa unajiharibia wewe mwenyewe. Utiifu ni muhimu sana, hata wakati ambapo unaona sehemu unapopelekwa sio pa kuvutia.
Ndio maana unawajibu sana wa kumwombea mume wako, ikiwa ni mwenye dhambi, Mungu ambadilishe. Kwasababu yeye ndio usalama wa maono yako.
Kwa mwanaume: Umewekwa kama kichwa, ni lazima utambue kulinda maono mema ya mkeo, Si kila taarifa nzuri itakufikia wewe wa kwanza, Wakati mwingine inaanzia kwa mwanamke, kama ilivyokuwa kwa Mariamu, kisha wewe baadaye, hivyo uonapo hivyo, usipige vita, bali, sikiliza, tafakari, pia tendea kazi, Hapo ndipo Mungu atakapokutumia, kuijenga familia bora. Wewe kama mlinzi huna budi, kutimiza wajibu wako,wa kumtunza mkeo na kumpenda kama maandiko yanavyosema. Jambo lolote linaloihatarisha familia yako, shughulika nalo kwelikweli usimwachie mwanamke alitende.
Hivyo kwa kuzingatia mambo hayo, Ndoa zetu zitakuwa bora, mfano wa ile ya Yusufu na Marimu. Na Bwana atatupa zawadi ya kuzaa vitakatifu kama Ilivyokuwa kwa Yesu na wadogo zake wote. Tambua wajibu wako, simama katika nafasi yako.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
WANA-NDOA: Baba Mkwe, Na mama Mkwe.
ONDOA TAKATAKA KATIKA FEDHA, NA CHOMBO KITATOKEA KWA MTAKASAJI.
Jibu: Kibiblia “Mhuni” ni mtu anayefanya mambo yaliyo kinyume na maadili. Kwamfano mtu anayetanga kuzaa nje na ndoa, huyo kibiblia ni mhuni.
Katika biblia neno Mhuni/wahuni limeonekana mara moja tu! Katika kitabu cha Ayubu 30:8.
Ayubu 30:8 “Wao ni wana wa wapumbavu, naam, WATOTO WA WAHUNI; Walifukuzwa kwa mijeledi watoke katika nchi”
Na mambo mengine yote ambayo mtu anaweza kuyafanya kinyume na maadili, mfano uvaaji mbaya, uongeaji mbaya, utafutaji mbaya n.k mambo hayo ni mambo ya kihuni, na hivyo anayeyafanya ni mhuni.
Na Wahuni wote hawatairithi Nchi, watafukuzwa watoke katika nchi..kulingana na hilo andiko.
Mathayo 5:5 “Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi”.
Jihadhari na uhuni, kama wewe ni binti uvaaji wa nguo fupi ni uhuni!, uvaaji wa vimini ni uhuni, uvaaji wa suruali ni uhuni (biblia inasema mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanaume na mwanaume asivae mavazi yampasayo mwanamke), kuvaa nguo unayoonyesha mapaja, au mgongo ni uhuni, kunyoa kijogoo kwa mwanaume ni uhuni, kuvaa nguo za mlegezo ni uhuni, kuvaa nguo za kubana ni uhuni n.k
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mshahara wa Mbwa ni upi? Kama tunavyousoma katika Kumbukumbu 23:18
Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.
MUNGU ATAKUUA UKIWA MBAYA MACHONI PAKE.
Je unajua ni kwanini watu watahukumiwa?
Hebu tusome maandiko yafuatayo..
Yohana 3:19 “Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa NURU IMEKUJA ULIMWENGUNI, NA WATU WAKAPENDA GIZA KULIKO NURU; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu”.
Umeona sababu ya hukumu ya Mungu juu ya watu siku ile?.. Ni kwasababu watu walipenda GIZA kuliko NURU.
Nataka tulitafakari hilo neno “wakapenda” na hilo neno “kuliko”. Unajua mtu akikipenda kitu kuliko kingine, maana yake amekichunguza, akakitafakari na mwisho akachukua uamuzi wa kukichagua hiko kitu.
Na ndivyo Neno la Mungu linavyosema, kuwa hukumu yake itakuja juu ya watu, kwasababu “WATU WALIPENDA GIZA KULIKO NURU”. Ni heri kama Nuru isingekuwepo, halafu watu walipende giza!… lakini hapa inamaanisha Nuru ilikuwepo halafu watu wakalipenda giza kuliko Nuru… hilo ni jambo baya sana..
Hebu tafakari mpo ndani ya chumba chenye giza, halafu taa inawashwa na kumulika nyumba nzima, halafu ghafla unaanza kuona watu wanatoka kwenye hicho chumba chenye nuru, wanaelekea gizani, na zaidi ya yote hawataki kuja kwenye nuru!.. bila shaka utashangaa sana…
Ndicho Bwana Yesu alichomaanisha hapa kuwa watu kwa mapenzi yao wenyewe, wamechagua giza kuliko Nuru, ijapokuwa Nuru wameiona!..
Watu walipenda anasa kuliko kumcha Mungu, watu walipenda uchafu kuliko usafi, ijapokuwa tayari Nuru ilikuwepo (Roho Mtakatifu wa kuwatakasa alikuwepo, lakini hawakumtaka)…Watu walipenda ulevi, uzinzi, uuaji, ulafi, ufiraji, utukanaji, tamaa mbaya kuliko UTAKATIFU. Kwasababu hiyo basi hawatakuwa na udhuru siku ile (kulingana na Neno hilo).
Na ni kwasababu gani watu wanalipenda giza kuliko Nuru?, ni kwasababu matendo ya giza siku zote ni ya aibu, na yasiyokubalika na huwa hayapatani na mwanga.. Wezi wanaiba usiku, wachawi wanafanya shughuli zao usiku, walevi wanalewa usiku, hali kadhalika wazinzi, na makahaba wanafanya kazi zao katika giza…
Ayubu 24:15 “Tena jicho lake mzinifu hungojea WAKATI WA GIZA-GIZA, Akisema, Hapana jicho litakaloniona; Naye huuficha uso wake.
16 Wao hutoboa nyumba gizani; Hujifungia ndani wakati wa mchana; Hawaujui mwanga”.
Umeona tabia za wazinifu na watu wafanyao mabaya?..huwa zinasubiria kagiza kaingie!!..hawawezi kufanya shughuli zao mbele za watu!.
Yohana 3:20 “Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.
21 Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.”
Je! Na wewe umependa nini?,, umechagua nini?, NURU AU GIZA!, kwa matendo yako utatambulika umechagua nini, kamwe usimsingizie shetani!, kwasababu hapo Bwana hajasema “shetani akawachagulia kupenda giza” bali anasema “watu wakachagua wenyewe kupenda giza kuliko Nuru”. Kwahiyo ni watu wenyewe ndio wamechagua matendo ya giza, baada ya kukubali mapendekezo ya shetani.
Je! Na wewe umechagua nini leo?..kumbuka kama unafanya matendo ya giza, na huku unamjua Yesu…fahamu kuwa upo gizani, na umechagua giza kwa hiari yako mwenyewe, na upo hatarini kuangukia katika hukumu ya Mungu siku ile,.. Kwasababu Nuru ipo ulimwenguni na hujataka kuifuata, na Nuru hiyo si nyingine zaidi ya Yesu Kristo.
Yohana 9:5 “Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu”.
Amua leo kutoka katika hilo giza la ulimwengu, na kuja Nuruni.. na Unaingia Nuruni kwa kumwamini Bwana Yesu, na kupokea Roho Mtakatifu ambaye atakutakasa na matendo yote ya giza, na kwa kufanya hivyo utakuwa umetoka gizani na kuingia uzimani, na hivyo utakuwa ni mwana wa Nuru.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Hazina za gizani ni zipi? (Isaya 45:3).
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
Je ni kweli imani ya mtu ndiyo itakayomuokoa, na si kitu kingine?
Nuru yetu inapaswa iangaze au isiangaze kulingana na Mathayo 5:16 na Mathayo 6:1?