SWALI: Huyu “Yeye ashindaye” anayezungumziwa katika kila mwisho wa jumbe za makanisa saba. Ni mtu mmoja maalumu au wengi?
JIBU: Tunasoma Bwana Yesu alipotoa agizo au onyo kwa yale kanisa saba mwishoni alimalizia na kutoa thawabu. Lakini thawabu hiyo aliielekeza kwa yule ashindaye tu.
Kwa mfano ukisoma juu ya lile kanisa la Thiathira alisema..
Ufunuo wa Yohana 2:26
[26]Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
Sasa swali huulizwa je? kuna mtu mmoja maalumu ambaye anaonekana atashinda? na kupokea tuzo hiyo ya kuwa na mamlaka juu ya mataifa au ni mjumuiko wa watu.
Ni raisi kudhani tuzo hiyo imeelekezwa kwa mtu fulani mmoja lakini ukweli ni kwamba inamuhusu kila mtu…ni sawa na mwalimu awaambie wanafunzi wake atakayefaulu mtihani wangu..nitamlipia ada ya muhula mmoja.
Sasa yeye kutumia lugha ya umoja “atakaye” na sio “watakao”…hamaanishi kuwa amemlenga mtu fulani mmoja.
maana yake ni kuwa yeyote yule atakayefaulu, basi atalipiwa ada, iwe ni mmoja, au wawili au wote. watalipiwa. Kwasababu wamefaulu. Kigezo ni kufaulu sio atakayefaulu kuliko wote.
Vivyo hivyo na Bwana alichokimaanisha hapo kwenye hayo makanisa saba. Lengo lake ni wote washinde lakini inaonekana ni kama si wote watakaoshinda…bali wale watakaoshinda watazipokea hizo thawabu.
Hivyo ni kujitahidi…kwasababu kuna uwezekano wa wengi kukosa thawabu hizo.
Mtume Paulo alitumia mfano wa wachezaji ambao hushiriki katika mchezo, kwamba wachezao ni wengi lakini apokeaye tuzo ni mmoja..(1Wakor 9:24)
Lakini hakumaanishi kwetu sisi atakuwa mmoja, ni mfano tu alitumia kueleza uhalisia kwamba kuna kunga’ng’ana ,sio jambo rahisi rahisi…fahamu kuwa sisi wakristo hatuna mashindano ya ukubwa na nafasi mbinguni…tunashindana ili tuyatende yale tuliyoagizwa na Bwana kikamilifu na sio kuzidiana…
Ndio maana mahali pengine akasema watatoka wengi, kutoka mashariki, na magharibi kuja kuketi na Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote, (Luka 13:28-29) Umeona kumbe wazee wetu hao, ni kama vile wamewekwa sehemu moja na wengine watakuja kuungana nao. Na wote watakua kitu kimoja na wao, lakini pia angalizo ni kwamba watakaofikia hapo si wengi sana.
Mathayo 8:11
[11]Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
Kwahiyo ni kujitahidi hapo tusikose..Kwa kumaanisha kweli kweli kujitwika misalaba yetu na kumfuata Yesu. Na kujitenga na dhambi, na hakika thawabu hizo tutazifikia wote.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 4)
Rudi Nyumbani
Print this post
Danieli 2:2[2]Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme.
Wasihiri ni kundi la wachawi, lililojikita kwenye mazingaumbwe. Linatumia uchawi kubadili vitu kwa hila, mbele ya macho ya watu kuwafanya waone kama ni muujiza umetendeka, na wakati mwingine kutumia njia hiyo kuleta madhara kwa watu.
kwamfano wale yane na yambre kipindi cha Musa walikuwa ni wasihiri, walijaribu kubadili fimbo kuwa nyoka, na kuleta vyura.(Kutoka 8:7)
Mfano mwingine ni yule Simoni mchawi, tunayemsoma katika;
Matendo 8:9-11
[9]Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. [10]Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. [11]Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake.
[9]Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.
[10]Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.
[11]Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake.
Tofauti na waganga ambao, wenyewe wanajifanya kama matabibu, na wachawi na wale wakaldayo ambao ni wanajibu(wasoma nyota)…hawa wasihiri kazi yao hasaa ni ile ya kiini macho.
Lakini Mungu anathibitisha kwamba makundi yote haya, hakuna hata moja lenye uwezo wa kufikia hekima ya Mungu ipitayo vyote Hayana nguvu ya kupambanua mambo. au kufanya miujiza. Hakuna mganga wala wachawi, mwenye uwezo wa kufanya muujiza.
Sasa utauliza ni nini kile wanachokifanya kama sio miujiza?
Awezaye kutenda miujiza ni Mungu tu. wasihiri na waganga wanafanya kazi ya kulaghai fikra za watu kwa elimu ambayo ni ya siri (ya mashetani), ndio maana wanaofanya hizo kazi huenda kujifunza kufanya hivyo, namna ya kuchezea fikra za watu, na si kingine.
Sasa wewe kwasababu hujaijua hiyo elimu unaweza ukasema umeona muujuza kumbe ni uongo tu..wamekudanganya.
ni sawa na leo unapoona mtu akiwasiliana na mtu mwingine akiwa mbali na kuiona sura yake kwenye kioo, kama huijui elimu ya darasani, utasema ni muujiza lakini kumbe ni maarifa tu ya kibinadamu.
vivyo hivyo na hawa wachawi na wasihiri, hawana jipya kusema wanafanya muujiza fulani, ni elimu zao tu za kipepo
Hawawezi kuumba chochote. wale vyura waliofanya kutokea kipindi cha Farao, hawakuumba vyura wao wapya kimiujiza..Vinginevyo mpaka leo shetani angekuwa na uwezo wa kuumba na angeumba vyura wake wengi tu na viumbe vyake vimwabudu. Alichokifanya pale ni kuchukua vyura walioumbwa na Mungu, na kuwapumbaza watu macho, waone ni mawe yamegeuzwa vyura kumbe hakuna kitu. Ndio maana ujinga wao ulikuwa wazi baadaye…walipodhani kila eneo ni kiini macho, walipojaribu kwa chawa wakashindwa, kibao kikawageukia, wakakiri ni Mungu tu awezaye.
Kwahiyo wewe uliye na Yesu, shetani anakuona kama mungu duniani, mwenye nguvu nyingi sana, hekima mamlaka zaidi ya yeye. Wewe unaweza kutenda muujiza kabisa kwa jina la Yesu. yeye hawezi
mwamini Yesu mtegemee yeye tu, kwanini kutafuta msaada kwa vitu dhaifu, ukamtia Mungu wivu?. Kwenda kwa waganga ni kupungukiwa akili, ni kujitenga na fadhili zako, mwenyewe, ni kumdharau muumba wa mbingu na nchi, Yehova, atupaye vyote.
Okoka sasa, mpokee Yesu, upate uzima wa milele. Wachawi waliokutana na Yesu walisalimu amri na kuchoma mikoba yao. sasa wewe unaenda kufanya nini huko?
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).
JIHADHARI NA ROHO YA YEZEBELI.
Huu ni mwongozo maalumu ya njia bora ya kuiomba sala ya Bwana. Wengi wetu tunaiomba aidha kwa kukariri au kwa kukosa ufahamu wa jinsi ipasavyo kuombwa, kulingana na majira ya nyakati za agano jipya. Lakini kama tukijua namna ya kuiomba ipasavyo basi tutaweza fungua milango mingi sana rohoni, ukizingatia kuwa ni sala ambayo Bwana wetu mwenyewe alitufundisha kwasababu ndio hiyo hiyo hata yeye alikuwa anaiomba.
fungua chapisho hili lililo katika pdf kwa kubofya download uweze kusoma;
Kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.
Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?
https://wingulamashahidi.org/2023/04/01/jinsi-ya-kupigana-maombi-ya-vita/.
SWALI: Naomba kufahamu nini maana ya vifungu hivi;
Mathayo 6:29
[29]nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
JIBU: Katika habari hiyo Mungu anaeleza jinsi anavyoweza kutujali na kututunza sisi kipekee kwa uweza wake wa ki-Mungu, akifananisha na jinsi anavyoyatunza maua yake ya kondeni ambayo leo yapo kesho yananyauka na kutupa tanuruni.
ndio hapo anasema tusiwe na shaka ya leo tuvae nini, kama Mungu anayavika vizuri maua hayo ambayo ni kwa muda mfupi tu huchanua baadaye hunyauka, si zaidi sisi tulio na thamani nyingi zaidi ya hivyo vyote?
Tena anasisitizia hata Sulemani katika fahari yake yote, hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya maua hayo.
Kumbuka Sulemani alikuwa ni mtu tajiri sana, mavazi yake yalikuwa ni ya thamani sana, lakini yalitegemea kuchovywa na kurembwa kwa rangi mbalimbali, ambazo hizo baada ya kipindi fulani hupauka au kuchuja.
Lakini maua hayapakwi rangi bali uzuri ule ni rangi yao kwa asili itokayo ndani. hayafifi rangi. Sulemani hakuwahi kuwa na vazi la namna hiyo.
Isitoshe maua nayo licha ya kuwa na mwonekano mzuri lakini pia hutoa harufu yao nzuri ya asili, kitu ambacho hawezi kukiona kwenye vazi la aina yoyote zuri duniani kutoa harufu yake yenyewe, yanategemea kupuliziwa marashi.
Hivyo hiyo ni kutufundisha kuwa Mungu anaweza kutunawirisha na kutupendezesha zaidi ya matarajio yetu, lakini hiyo hutimia kwanza pale tunapojishughulisha na mambo ya ufalme wake, ndio hayo mengine sasa ya chakula na mavazi atuzidishie.
ONA FAHARI JUU YA BWANA.
Nyinyoro ni nini?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Tangu mwanzo mwanadamu alikuwa akijaribu kujiokoa kwa njia yake mwenyewe ikiwemo kuonyesha matendo yake mazuri, na mwenendo wake mkamilifu lakini hakuweza. Pengine aliweza kushinda wizi kikamilifu lakini uongo ukamshinda, aliweza kushinda uzinzi wote, lakini tamaa zikamtawala, aliweza kushinda ibada za sanamu na vinyago, lakini kusamehe kukamshinda. Alipoweza kushinda kimoja, nyuma yake kulikuwa na elfu vinavyo mhukumu.
Na hiyo ilimfanya asikidhi vigezo vya kuingia mbinguni, kwasababu watakaoiona mbingu na Mungu ni watakatifu asilimia mia wasio na doa lolote. Ndio maana maandiko yanasema wote wameoza,wamepotoka hakuna amtafutaye Mungu. Bali tunahesabiwa haki bure kwa neema ya Bwana Yesu Kristo.
Warumi 3:11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. 12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
Ndio sababu ya Yesu kuja duniani, ili kwa kupitia kumwamini yeye tuipokee hiyo neema ya kuitwa watakatifu, bila kuonyesha kwanza kipimo chochote kwa Mungu.
Maana yake ni kuwa mimi na wewe tunapomwamini Yesu Kristo, ni moja kwa moja tunaitwa watakatifu, tuliosamehewa dhambi zetu, na kuondolewa pia.
Ikiwa umemwamini leo Yesu Kristo, moja kwa moja Mungu hakuhesabii tena dhambi yoyote kama mkosaji. Ijapokuwa utakuwa hujakamilika bado. Hii ndio maana ya neema, yaani kukubaliwa kusikostahili. Ilikupasa kwanza uwe na matendo makamilifu asilimia 100 kama Bwana Yesu, ndio uitwe mtakatifu uliyestahili kumwona Mungu. Lakini sasa kwa kuupokea ukombozi wa Yesu Kristo, dhambi zako, zimefuta unaitwa mtakatifu, kabla hata ya ukamilifu wa utakatifu wenyewe kukufikia. Ndio maana sisi tulio ndani ya Kristo hatuna budi kuwa na amani, na furaha wakati wote. Kwasababu ule mzigo mzito wa kujitahidi sisi wenyewe kuingia mbinguni umeondolewa na Yesu Kristo Bwana wetu, kwa kifo chake pale msalabani.
Lakini sasa, katika nyakati hizi za mwisho suala hili la neema limetafsirika vibaya, kama tu nyakati zile za zamani, na hapo yatupasa tuwe makini sana. Ni sawa na taifa litangaze neema kwa nchi yake na kusema, sasa huduma zote za maji ni bure, hakuna kulipia bili,matumizi ni kama unavyotaka. halafu uone watu wanatumia fursa hiyo kwenda kufungulia mabomba yatiririshe maji kwenye mitaro na mabarabarani, kila mahali kuwe ni maji tu, Bila shaka utasema hawa watu wamerukwa na akili, hawana sifa ya kupewa huduma hiyo tena.
Ndivyo ilivyo kwa jambo linaloitwa neema, tusijipojua kanuni zake, tutajikuta badala ya kupokea wokovu, tunapokea maangamizi. Badala ya kukazana kumpendeza Mungu, tunastarehe katika dhambi, Na ndicho kinachoendelea sasa kwa sehemu kubwa miongoni watu na madhehebu.
Yafuatayo ni mambo ambayo ujiepushe nayo kwa nguvu zote, wewe uliyeipokea neema ya Mungu.
2 Wakorintho 6:1
[1]Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.
Ukisoma vifungu vichache vya nyuma anasema mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya.
Mtu ambaye hataki geuko, baada ya kusamehewa dhambi zake, huyo ni mtu ambaye ameipokea neema bure, haithamini, ameitwa mtakatifu, halafu hataki kuishi maisha matakatifu, anaendelea na maisha yake yale yale ya kale.. Mtu kama huyo asijidanganye neema hiyo ni batili. Mtu yeyote aliyeokoka wakati huo huo una wajibu wa kuanza kupiga hatua za mabadiliko, na unapaswa uithamini sana hiyo zaidi ya vyote, kwasababu ni Mungu ndiye akutakasaye baada ya hapo.
Lakini pia mtu ambaye amekaa muda mrefu hamzalii Mungu matunda, anahesabika kama aliyeipokea neema ya Mungu bure, na hivyo mwisho wake unakuwa ni kukatwa.
Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Je! Umeitii neema hii inayokufundisha kukataa machafu ya duniani?. Leo yapo madhehebu yanayosema, ukiokoka umekoka milele, kazi yako imeisha, hata usipoonyesha bidii nyingine yoyote kwa Mungu,huwezi potea. Ndugu yangu kuwa makini sana na imani hizi. Neema haipokelewi bure.
Epuke pia kuipungukia neema.
Waebrania 12:15-17
[15]mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. [16]Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja. [17]Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.
[15]mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
[16]Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.
[17]Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.
Kuipungukie neema Ni tabia ya kuishusha thamani neema, na kuilazimisha itende kazi hata katika kiwango ambacho si chake.
Hii hasa huja kwa watu ambao wanazoelea kufanya dhambi mara kwa mara wakiamini kuwa kwasababu Mungu hawahesabii makosa basi hata wakifanya kosa lolote hawawezi kupotea.
Ndugu, neema si kuhalalisha maisha ya dhambi.
Biblia inasema..
Warumi 6:1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? 3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Warumi 6:1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Usitende dhambi za mazoelea, ukadhani neema itakuwa sikuzote kukufunika. Ukiifanyia jeuri neema, itaondoka kwako.
Waebrania 6:4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
Waebrania 6:4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
Yuda 1:4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.
Neema ya Mungu inaweza badilishwa ikamaanishwa kivingine kabisa. Kwamfano utaona leo hata mashoga, wanavyama vyao wakisema sisi tupo chini ya neema. Walevi nao, wenye dhambi nao wanasema neema ya Yesu ipo duniani sasa, kumwokoa kila mtu.
Hivyo watakuambia maneno kama usihukumu usije ukahukumiwa. Na wana amani na ujasiri katika hayo wanayoyafanya na wengine wanajiita maaskofu na wachungaji, wakihalalisha kila kitu kiovu kufanyika kwa kivuli cha neema.
Hao ndio waibadilishao neema ya Bwana Yesu kuwa ufisadi, hilo Neno ufisadi ni zaidi ya uasherati, Ni pamoja na matendo yote maovu kupita kiasi. Lakini neema ya Yesu,.haikuja kufunuki dhambi, bali ilikuja kuondoa dhambi ndani ya mtu. Usiwe mmojawapo aibadilishaye neema ya Mungu.
Hivyo kwa vifungu hivyo itoshe kusema kuwa NEEMA tunaipokea bure, lakini ili iweze kufanya kazi lazima tujue sifa zake, kisha tuzikubali, vinginevyo tutajidanganya na kuangamia. Ni sawa na mtu akupe gari bure, lakini usipoliweka mafuta, na kujua kuliendesha linakuwa halina tofauti na mdoli wa gari.
Lakini ukiithamini neema, itakutunza, itakuhifadhi na kuyaficha makosa yako yote, Hivyo utaendelea kuonekana mkamilifu asilimia mia mbele za Mungu, na hata ukifa, ni moja kwa moja mbinguni.
Shalom.
JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.
MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?
JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.
Siuze ni ‘Sembuse’, kwa uandishi mwingine.
Kwamfano mtu anaposema kauli hii
“Kama Bwana Yesu alikuwa mwombaji siuze mimi, kuzidi hapo?
.Ni sawa tu na kusema “Kama Bwana Yesu alikuwa mwombaji sembuse mimi, kuzidi hapo?
Maana ya Neno hilo ni. “Si zaidi”
‘Kama Bwana alikuwa mwombaji si zaidi mimi kuzidi hapo’.
Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu ambavyo utalisoma neno hili kwenye biblia;
2 Mambo ya Nyakati 6:18
[18]Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga!
2 Wakorintho 3:9
[9]Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi.
Shalom
Neno vuruvuru linamaanisha nini katika biblia?
Nini maana ya mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe? (Mathayo 24:35).
Kuna Mbingu ngapi?
WhatsApp
Zipo kanuni za ki-Mungu tunaweza kuzifuata na zikaleta matokeo kabisa halisi, lakini zisiwe na manufaa kwetu katika suala la wokovu. Sasa kabla ya kuangalia ni kwa namna gani?
chukulia mfano wa kawaida.
Mwanamke yeyote anaweza kubeba ujauzito katika mazingira mbalimbali, kwamfano anaweza akatwezwa nguvu (akabakwa), na akapata ujauzito, lakini pia anaweza kwenda kujiuza kama kahaba na bado akapata ujauzito, vilevile anaweza akasubiri aolewe kwanza katika ndoa halali ndipo apokee ujauzito na likafanikiwa vilevile tu, kuleta kiumbe duniani, kama angefanya hayo kabla ya ndoa, au atokapo nje ya ndoa yake.
Sasa unaweza jiuliza, katika njia zote hizo ambazo angepata ujauzito ni ipi iliyo halali inayokubalika mbele za Mungu na wanadamu. Bila shaka ni hiyo njia ya mwisho ambayo ni ya kuolewa kwanza, ndipo apokee ujauzito kutoka kwa mume wake mmoja wa halali. Na ndio mtoto huyo hujulikana kama halali sio haramu.
Lakini cha ajabu ni kuwa ijapokuwa njia halali ipo lakini feki pia huleta matokeo yaleyale mfano wa halali. Kwasababu gani? Kwasababu kanuni ya kupata mtoto, si kanuni ya uhalali. Hivyo ni vitu viwili tofauti,
Hata Ibrahimu, alikuwa na watoto wengi, alitangulia Ishmaeli, kisha baadaye wakazaliwa na watoto wengine sita kwa suria mwingine, mbali na Isaka. Wote walikuwa wanadamu, viumbe wa Mungu, wenye akili na nguvu na baraka, wasio na hatia. Lakini lilipokuja suala la urithi, ndipo kubaguliwa kulipokuja, Watoto wote wa masuria walifukuzwa wakapewa zawadi tu bali Isaka alipewa vyote.
Mwanzo 25:5-6
[5]Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo. [6]Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
[5]Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo.
[6]Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
Zipo kanuni nyingi sana za kiroho ambazo mtu yeyote, hata ambaye hajamwamini Yesu anaweza zitumia na zikatoa matokeo yaleyale sawa tu na mtu ambaye ameokoka.
Kwamfano, kufanya miujuza na ishara kwa jina la Yesu. Watu hawajui kuwa jambo hili huhitaji imani tu, katika jina lake. Hivyo wale wafikiao kiwango hicho haijalishi ni mwizi, ni mpagani, anaweza pokea muujiza na akafanya pia muujiza sawa tu na yule aliyeokoka.
Kwasababu gani? kwasababu amefanikiwa kufuata kanuni ambayo ni Imani.
Akijua lile neno linalosema ‘yote yawezekana kwake yeye aaminiye’’ (Marko 9:23). Ndio maana walikuwepo watu wengi wasiokuwa wayahudi kipindi kile cha Yesu walipokea miujiza mikubwa, zaidi ya wayahudi kwasababu tu ya ukubwa wa imani zao. Na sio haki zao.
Vivyo hivyo hata katika kuomba. Mtu yeyote aombaye hupokea. Ni kanuni ya asili ya rohoni, haijalishi ni nani.
Mathayo 7:8
[8]kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Watu hawajui hata kufanikiwa kwa shetani hutegemea maombi, na yeye pia huenda mbele za Mungu kuomba na hupewa..hajiamulii tu mambo yake ovyo ovyo bila idhini ya Mungu, kwasababu hii dunia si yake… utauliza kwa namna gani, ? unamkumbuka shetani kipindi cha Ayubu, yeye naye alikwenda kujihudhurisha mbele za Mungu, ndipo akaleta uharibifu. Akapeka haja zake akasikiwa, dua zake na magoti yake.
Ayubu 1:6
[6]Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao.
Watu wengi wanapoona wanamwomba Mungu wanajibiwa wanadhani, ndio wamekubaliwa na Mungu. Kumbe unaweza kuomba kama mwana-haramu usiyekuwa na urithi wa uzima wa milele, bali haki ya kupokea tu unachokiomba.
Unaweza ukafanya miujiza kama mwana-haramu. Lakini usiende mbinguni.
Mathayo 7:22-23
[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? [23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
[23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Unaweza ukamwamini Yesu, na kumuhofu, lakini ukaamini kama mashetani.
Yakobo 2:19
[19]Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
unaweza ukawavuta watu kwa Kristo na wakaokoka, lakini ukawa mtu wa kukataliwa kama tu Paulo alivyosema katika;
1 Wakorintho 9:27
[27]bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
Kanuni Mungu anayoitazama kwetu ni Wokovu uliokamilishwa kwa matendo yake.
Angalia mwishoni pale kwenye Mathayo 7:23 Bwana Yesu alichokisema;
“ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Umeona je unaishi maisha gani?. hicho ndio kipimo cha ki-Mungu,
Alisema pia.
Yakobo 2:24
[24]Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
Hakikisha maisha yako yanaendana na ukiri wako, wa imani yako, usiishi tu kama mtu ambaye hajaamini ukijitumainisha, kuona maombi yako yanajibiwa, karama yako inafanya kazi, imani yako inatenda kazi..hizo ni kanuni za kupokea lakini sio kanuni za uhalali wa kuurithi uzima wa milele. Ishi kama mtu ampendezaye Bwana wake kimwenendo, ndipo hayo mengine yakifuata huna hasara.
Nyakati hizi za mwisho, adui anaweka uzito kwenye mioyo ya watu wasipende kutafuta maisha matakatifu, kinyume chake wabakie tu kwenye miujiza, uponyaji, utabiri…Siku ile hivyo vitu havitafuata na wewe ndugu, bali matendo yako.
Ufunuo wa Yohana 14:13
[13]Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Tuanze sasa kujipima mienendo yetu. Kisha tutumie nguvu nyingi hapo kujirekebisha, sawasawa na imani tuliyoipokea, ili tuwe wana halali waliozaliwa kweli ndani ya Kristo, watakaorithi uzima wa milele.
Wokovu wa kweli hufunuliwa kwa mwenendo mzuri. Tuitazame sana kanuni hii.
KANUNI JUU YA KANUNI.
KANUNI YA KUOMBA NA KUPOKEA.
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?
SWALI: Naomba kufahamu ujumbe ulio katika Mithali 29:5
‘Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake’.
JIBU: Mithali hii inazungumzia madhara yanayoibuka katika tabia ya kujipendekeza.
Kujipendekeza ni kitendo cha mtu kumthaminisha mtu, hata kama alikuwa hastahili sifa hizo, ili tu upate kitu Fulani kutoka kwake. Kumthaminisha kunaweza kuwa kumsifia, au kumpongeza, au kumzungumzia mema yake kupita kiasi, au kueleza mabaya ya wengine kwa huyo mtu, n.k.
Na yote hayo hayawi kwa lengo la kuuthamini kweli uzuri wa Yule mtu, hapana bali ni aidha upate kupendwa wewe zaidi ya wengine, au usaidiwe, au upewe cheo, au kipaumbele Fulani. Hata kama utaona mabaya yake huwezi kumwambia kwasababu, huna lengo la kusaidia bali upate matakwa yako tu.
Sasa hilo ni kosa, matokeo ya hilo biblia inatuambia “unamtandikia wavu ili kuitega miguu yake”. Yaana unampeleka kwenye mtego au aungamivu wake kabisa. Hii ni kweli, tunaona hata viongozi wengi wa nchi wameponzwa na wasaidizi wao wa karibu,na matokeo yake wakaiharibu nchi, kwasababu tu ya kupokea sifa za uongo kutoka kwao, kwamba wanafanya vema, wanawajibiki vizuri n.k.. Kama ilivyokuwa kipindi kile cha Mfalme Sedekia na wale manabii wa uongo wajipendekezao, walimtabiria uongo, lakini Yeremia alimweleza mfalme ukweli hawakutaka kumsikiliza. Matokeo yake Mfalme Sedekia akaingia katika matatizo makubwa ya kutobolewa macho na kupelekwa utumwani, hiyo yote ni kwasababu alikaa na manabii wajipendekezao (Yeremia 34-41), kama tu ilivyokuwa Kwa Mfalme Ahabu naye na manabii wake mia nne wa uongo.
Hii ni kutufundisha nini?
Hasaa biblia hailengi, tuwe makini na watu wajipendekezao. Hapana, kwasababu wakati mwingine si rahisi kuwatambua, inahitaji neema ya Mungu. Lakini inalenga hasaa katika upande wetu , kwamba sisi tujiepushe na ‘tabia ya kujipendekeza”. Kwasababu tunaweza kudhani tunatafuta faidi yetu tu wenyewe, lakini kumbe tunamsababishia madhara Yule mtu ambaye tunajipendekeza kwake. Tunategea wavu mbaya sana, aanguke na kupotea kabisa, na huo si upendo.
Itakusaidia nini akutendee mema, halafu yeye aangamie?
Hivyo, pastahilipo kweli kusifia tusifie, lakini si kwa lengo la kujipendekeza, kwasababu tukienda huko, tunatenda dhambi kubwa zaidi. Hiyo ndio maana ya hivyo vifungu, tufikiriapo kujipendekeza, tuone kwamba ni watu wasio na hatia tunawategea wavu waangamie.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
TUZIJARIBU HIZI ROHO.
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
USIJISIFIE KARAMA KWA UONGO.
Nehemia 8:10
[10]Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; KWA KUWA FURAHA YA BWANA NI NGUVU ZENU.
Ni habari ya kutafakarisha, lakini zaidi sana ya kuwafariji watu wote wampendao Mungu. Tukisoma katika biblia ile habari ya Ezra na Nehemia, katika juhudi zao wa kuwarejesha Israeli katika ibada na njia za Mungu Yerusalemu.
Tunaona wakati ule ukuta wa Yerusalemu ulipomalizwa kujengwa baada ya kurudi kwao utumwani Babeli, Ezra hakuwaacha tu hivi hivi, wafurahie kukamilika kwa majengo, bali alitaka wakamilishwe na mioyo yao hivyo, alikichukua kitabu cha Torati na kuanza kuwasomea wayahudi wote tangu asubuhi mpaka adhuhiri, ili wajue ni nini Bwana anataka kwao (Nehemia 8).
Na waliposikia waliona makosa yao mengi sana, na hukumu nyingi za Mungu, alizowatamkia kufuatana na makosa yao, yaliyowapelekea mpaka wakachukuliwa mateka. Ikumbukwe kuwa kitabu hicho cha torati hakikuwahi kusomwa tangu zamani walipochukuliwa utumwani, ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kukisoma baada ya miaka mingi kupita.
Hivyo wayahudi kusikia vile wakaanza kulia sana na kujuta na kuomboleza. Lakini tunaona kuna jambo lilifanyika la kitofauti.
Nehemia, alitambua wazo la Mungu…Hivyo akawazuia watu kulia na kuomboleza kwa ajili ya makosa yao. Kinyume chake akawaambia leo ni siku takatifu kwa Bwana, hivyo mle ,.mnywe, mtoe sadaka, mfurahi mbele za Mungu wenu kwasababu “furaha ya BWANA ni nguvu zenu”
Hivyo watu wakasheherekea, badala ya kulia, Sio kwamba Nehemia alisheherekea makosa yao, hapana, bali alipewa kujua kwamba furaha ya mtu kwa Mungu wake, ndio chanzo cha nguvu ya kumtumikia yeye.
Ndio hapo baada ya wayahudi kujua makosa yaowakimfurahia Mungu, siku hiyo, na wakapokea nguvu nyingi za kuishika sheria ya Mungu.
Yaani kwa namna nyingine, Mungu kuwakemea makosa yao,lengo lake lilikuwa sio awahukumu, au wainamishe vichwa vyao wakidhani kuwa wao ni kichefu-chefu kwake. Hapana..Bali anawapenda na hivyo anatarajia wajue nia ya makemeo yake.
Nehemia 8:10 Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. 11 Hivyo Walawi wakawatuliza watu wote, wakasema, Nyamazeni, kwa maana siku hii ni takatifu; wala msihuzunike. 12 Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale waliyohubiriwa
Nehemia 8:10 Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.
11 Hivyo Walawi wakawatuliza watu wote, wakasema, Nyamazeni, kwa maana siku hii ni takatifu; wala msihuzunike.
12 Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale waliyohubiriwa
Ni hata sasa, unaposoma biblia na kuona inakushitaki, inakuambia usiibe, usisengenye, amchukiaye ndugu yake ni sawa na muuaji, wazinzi wote sehemu yao ni katika lile ziwa la moto, inapokukemea maovu yako ya siri.. Usiinamishe kichwa na kusema “mimi sifahi mbele za Mungu, mimi ni mkosefu sistahili kuitwa mwana wake”..Ukaacha kukisoma kabisa, ukawa unalia tu, umenyong’onyea, na kujihisi wewe ni wajehanamu tu, Mungu hakupendi, ameshakuacha, ona sasa unamkosea kosea kila siku… Fahamu kuwa hilo sio kusudi la Mungu.
Kusudi la Mungu sio usome biblia, ujawe na hisia za Mungu kukuhukumu, au kukulaumu, au kukushitaki, bali kusudi la Mungu ni ujue upendo wake uliozidi sana kwako, kiasi cha yeye kuonyesha hisia zake kwako namna ambavyo unapaswa uwe kama yeye.
Hivyo ukitoka kuonywa na kukemewa, unapaswa utoke kwa kufurahi moyoni na kuruka-ruka, na hapo ndipo utapokea nguvu ya kuishinda hiyo dhambi. Lakini ukitoka kinyonge na mashaka utashindwa kwasababu furaha ya Bwana ndio chanzo cha nguvu zetu. Ukilipenda hilo katazo, utalitenda, usipolipenda kamwe huwezi litenda.
Mtunga Zaburi alisema,
Zaburi 119:52
[52]Nimezikumbuka hukumu zako za kale, Ee BWANA, nikajifariji.
Bwana anataka tuone upendo wake kwetu katika makemeo yake, tufarijike tupokee nguvu ya kushinda. Pengine umetoka kufanya dhambi fulani ya makusudi na Roho Mtakatifu akakumbusha kuwa watu wa namna hii, huangukia katika mtego mbaya wa shetani bila kunasuka, Sasa hapo usianze kupoteza ladha na Mungu wako, au biblia, ukauchukia wokovu, kabisa, maanisha kutubu, jifunze kutokana na makosa, kisha furahia mwambie Bwana asante kwa kunipenda,
hata wachezaji wa mpira, wafungwao kipindi cha kwanza, wanapotulia na kujihamasisha tena, hupokea nguvu ya kucheza vema kipindi cha pili, lakini wajilaumupo, hufanya vibaya zaidi
Na sisi pia tuiamshe furaha ya Bwana daima.Kila tusomapo Neno lake, tufurahi kwasababu ni barua ya upendo wa Mungu kwetu Ili tuweze kuwa na nguvu.
Kwasababu furaha ya Bwana ndio nguvu yetu.
SHUKURU KWA KILA JAMBO.
Furaha ni nini?
Fahamu maana 1Wakorintho 14:20 “Ndugu zangu msiwe watoto katika akili zenu;
Kuna wakati Elisha alifika Gilgali na mahali pale palikuwa na njaa kali, na watu wengi (manabii) pia walikuwa wamekusanyika kusikiliza mashauri ya mtu wa Mungu.
Hivyo akawaambia waweke sufuria motoni waandae chakula.
Lakini mmojawao akatoka akaenda mashambani kutafuta mboga. Na huko akafanikiwa kweli kukusanya zilizo bora, lakini kwasababu hakuwa na maarifa ya kutosha jinsi ya kutambua mboga sahihi ziwafaazo wanadamu akaona huko matango mwitu, na bila kujua, akidhani ni matango halisi, akayachuma na kuyaleta sufuriani. Matango yale yalikuwa ni sumu.
Lakini walipoonja kwa neema za Mungu walijua kuna kitu ambacho sio sahihi kimewekwa sufuriani, hivyo waacha wote kula. Ndipo Elisha akataarifiwa, juu ya jambo hilo, kama kimwagwe lakini kile chakula hakikumwagwa, bali aliwaagiza watie unga mule (kwa Neno la Bwana), na chakula kitaponyeka. Wakafanya hivyo, kikawa sawa, wakala wakashiba.
2 Wafalme 4:38-41
[38]Elisha akafika Gilgali tena; na kulikuwa na njaa katika nchi; na hao wana wa manabii walikuwa wakikaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, Teleka sufuria kubwa, uwapikie wana wa manabii. [39]Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtango-mwitu, akayachuma matango-mwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasua-pasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua. [40]Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula. [41]Lakini yeye akasema, Leteni unga. Naye akautupa ndani ya sufuria; akasema, Wapakulie watu, ili wale. Wala hakikuwamo kitu kibaya sufuriani.
[38]Elisha akafika Gilgali tena; na kulikuwa na njaa katika nchi; na hao wana wa manabii walikuwa wakikaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, Teleka sufuria kubwa, uwapikie wana wa manabii.
[39]Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtango-mwitu, akayachuma matango-mwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasua-pasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua.
[40]Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula.
[41]Lakini yeye akasema, Leteni unga. Naye akautupa ndani ya sufuria; akasema, Wapakulie watu, ili wale. Wala hakikuwamo kitu kibaya sufuriani.
Inatueleza hali ya kiroho ya watu iliyopo sasa.
Palipo na njaa ni rahisi mtu kula kila kitu, ilimradi tu asife. si rahisi akae chini na kufikiria ubora wa kile anachokula. Leo hii njaa ya Neno la kweli la Mungu ni kubwa, hivyo kila mtu anaenda kondeni kuokota kitu kimfaacho, huko huko tunakutana na vizuri lakini pia tunakutana na vibaya..
shida ipo hapo, je tunaweza kupambanua?
Kwasababu ukila sumu, ile sumu haitakuambia ngoja nisikuletee madhara kwasababu hukukusudia kunila, au hukujua kuwa mimi ni sumu, utakufa tu sawasawa na yule anayejua anachokifanya.Kumbe ujinga una gharama kubwa.
Bwana Yesu alisema..
Mathayo 7:15
[15]Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mafundisho yasiyomhubiri Kristo na utakatifu, ni kuwa makini nayo, ni heri usiyasikilize kabisa kwa usalama wako wa kiroho. Yanayokuambia tunaokolewa kwa neema tu, hivyo matendo yako ni kazi bure mbele za Mungu, ukiokolewa umeokolewa milele, hata ukiwa unatenda dhambi vipi huwezi potea, yapime sana hayo mafundisho.
Mafundisho ya kuzimu-kuzimu tu na majini na wachawi epukana nayo, Mafundisho ya sanamu ibadani, ni mauti chunguni. Mafundisho yanayopinga habari za mwisho wa dunia, ambayo hayana habari na unyakuo au kumfanya mtu atazame kurudi kwa pili kwa Kristo, kinyume chake ni kukuweka kidunia, ufikirie mafanikio ya mwilini ni matango mwitu.
Manabii wa uongo ni wengi, wapo wanaotenda kazi kwa uwazi, lakini wapo wanaotenda kazi kwa siri.
Jifunze kusoma biblia, jinsi usomavyo Neno la Mungu utagundua kuwa mtu uliyeokoka kwa wakati uwapo hapa duniani Bwana anakutana Utembee katika utakatifu (Waebrania 12:14). Lakini pia uelekeze macho yako mbinguni kwa yale mambo yajayo, ya mbingu mpya na nchi mpya.
Luka 12:35-36
[35] Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; [36]nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
Jihadhari na matango mwitu.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>>> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kusanyiko la makini/ mkutano wa makini ni upi?
USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.