MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.
Sehemu ya pili: Kaa Majangwani:
Luka 1:80 “Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli”.
Ni kawaida ya Mungu, kuwaandalia Watoto wake, mahali maalumu pa kukulia kiroho.. Ikiwa unatamani nguvu zako za rohoni ziongozeke kwa kasi wewe kama mwongofu mpya uliyezaliwa mara ya pili, huna budi kukaa majangwani.
Mungu alipowatoa wana wa Israeli Misri, hakuwavukisha moja kwa moja na kuwafikisha Kaanani ndani ya siku moja, bali aliwapitisha kwanza jangwani, kuwalisha huko na kuwakuza kiroho, kwa muda wa miaka 40, kwasababu walikuwa bado ni Watoto wachanga, na ndipo baadaye wakaingia Kaanani, wakiwa Hodari na nguvu nyingi rohoni.
Hosea 11:1 “Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri”.
Biblia pia inatuambia Yohana mbatizaji alipozaliwa, alikimbilia majangwani huko kuishi, na matokeo yake akakua na kuongozeka nguvu nyingi sana rohoni kwa kasi, na ndio maana hatushangai kwanini Bwana Yesu anamshuhudia na kusema katika wazao wa wanawake hakuwahi kutokea mtu aliyekuwa mkuu kama Yohana Mbatizaji.(Mathayo 11:11).. Hiyo yote ni kwasababu gani? Ni kwasababu alitumia Muda mwingi majagwani.
Haimaanishi kuwa ni sisi tukimbilie majangwani tukaishi huko, ili tukue kiroho hapana… Kama tunavyojua jangwani ni mahali ambapo hapana uwepo wa wanadamu, ni mahali pa ukiwa, pasipokuwa na huduma zozote za kijamii.. Ndivyo inavyompasa mkristo aende rohoni.
Unapaswa katika hatua zako za awali za wokovu: Kwa bidii zote uwe tayari, kuukana huu ulimwengu. Kukaa mbali na mambo yote yanayousonga wokovu wako, bila kujali unapoteza nini, au unakosa nini..
Ukiokoka, kubali kuachana na wale marafiki zako wa kale uliokuwa unakwenda nao disco, uliokuwa unakunywa nao pombe, uliokuwa unatukana nao, kubali kuwa mpweke, kwa kipindi Fulani, kwani hivyo ndivyo unavyoiponya roho yako.
Ukiokoka, kubali wakati mwingine, kupoteza hiyo kazi isiyo halali kwa Mungu, kama unafanya biashara ya pombe acha, ..wala usidhani kuwa utaangamia, kwamba Mungu atakuacha ufe, hilo wazo ondoa, uwezo wa kukulisha Mungu anao, Kama alivyofanya kwa wana wa Israeli kule jangwani, atafanya na kwako pia..
Biblia inasema..
Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, AENDE ZAKE NYIKANI HATA MAHALI PAKE, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo”.
Umeona, Mungu ameshaandaa mahali pako huko nyikani, pa kukulisha kwa wakati wako na majira yako. Hivyo usiogope wewe uliyemzaa Kristo maishani mwako.
Kama wewe ni binti kubali kukaa mbali na Fashion, kubali kujisitiri na kuchoma hivyo vimini na masuruali, kubali kuonekana umerukwa na akili kwa ajili ya Kristo, hata ulimwengu mzima ukikuona mjinga, kubali hiyo hali, weka kando kila mzigo wa dhambi, kwasababu ndivyo unavyoiponya roho yako.
Je! Faida yake ni ipi?
Faida yake ni kwamba Yesu anapata nafasi ya kukupitisha katika madarasa yake, na kwasababu husongwi na mambo mengine, hivyo kasi yako ya kukua kiroho itakuwa ni kubwa sana..
Maandiko yanasisitiza hilo katika;
Isaya 40:3 “Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu”.
Kuonyesha kwamba mahali pekee ambapo utamtengenezea Mungu njia, katika maisha yako ni jangwani.
Leo hii utaona watu wengi wamedumu katika wokovu kwa miaka mingi, lakini huoni mabadiliko makubwa yoyote ndani yao, bado ni wachanga kila siku wanataka wanyweshwe tu maziwa, ni kwasababu gani?
Ni kwasababu hawakumpa Kristo, nafasi ya kuwafundisha majangwani..Walilikimbia jangwa, wakakaa ulimwenguni, na hivyo Bwana akawaacha.
Ndugu/Dada uliyeokoka hivi karibuni usiipuzie hiyo sauti inayokuambia, acha hiki, acha kile, mwache Rafiki yule, acha jambo lile..usiipuuzie kabisa, fanya hivyo, ni sharti upoteze, ili upate baadaye, majira haya ni kujikana nafsi yako, kuichukia nafsi yako, na kujitwika msalaba wako kumfuata Yesu, hilo haliwezi kuepukika ikiwa unataka ukue kiroho kwa kasi anayoihitaji Kristo ndani yako.
Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake”.
Kabla ya kumzalia Mungu matunda ni lazima upitishwe jangwani, kutakaswa na Mungu, hivyo kuwa mwepesi kuacha udunia wako. Umfuate Yesu.
Bwana akubariki.
Shalom.
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA: Sehemu ya 1
EE MUNGU, MUNGU WANGU, NITAKUTAFUTA MAPEMA:
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 13 (Kitabu cha Hosea).
Unajua ni kwanini Bwana Yesu alisema “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo?” (Luka 8:18)
Alijua kuwa kuna hatari kubwa sana ya mtu aliyesimama kupotea kwa kile tu anachokisikia ikiwa hakitokani na yeye.. Hivyo si kila jambo ni la kulisikiliza na kuliweka moyoni, Zama hizi ni zama za uovu.
Mambo haya makuu matatu, kuwa nayo makini sana siku hizi za mwisho.
Ikiwa Maisha yako yote unayoishi ni kutegemea tu maono unayoonyeshwa, au ndoto, au mafunuo, na huku umeliweka Neno la Mungu nyuma basi ujue, hatari ya kupotea ni kubwa sana..tena sana. Haijalishi yatakuwa yanatoka kwa Mungu au kwa shetani, kama unaliweka Neno la Mungu nyuma..Bado hatari ya kupotea ni kubwa sana kuliko unavyodhani ndivyo ilivyo.. Najua inaweza ikawa ni ngumu kupokea lakini ukweli ndio huo.
Leo tupo wakati ambapo mtu atakuambia nimepelekwa kuzimu, nikaonyeshwa hiki, na kile, nimeonyeshwa watu wanaokula pipi za ivory, na soda za cocacola wapo kuzimu, nimeonyeshwa mabinti wote, walioingia katika ndoa bila ubikira, wanazini, waume zao ni wale wakwanza waliozini nao, kabla hawajaokoka hao ndio wanapaswa wakaolewe nao, hivyo wakiolewa na wengine wanazini..Nimeonyeshwa watu wote wanaosali siku ya jumapili wapo jehanamu, nimeambiwa na Yesu watu wote wanaoota ndoto wanapaa wajiandae na moto, nimeambiwa, kama umeokoka, unapaswa urudishe madeni yote uliyowahi kuwatapeli watu huko nyuma hata kama huna uwezo huo, usipofanya hivyo ni ziwa la moto, kama unakwenda beach kuogelea ni kuzimu, kama upo katika ndoa na unatumia uzazi wa mpango ujue ni motoni moja kwa moja…n.k n.k. Ni mengi mno..
Mambo kama haya embu tujaribu kudhania kuwa ni kweli yanatoka kwa Mungu..Lakini nikikuuliza swali ni nini kimekupa uhakika kuwa kinatoka kwa Mungu, utanipa jibu gani? Utasema ni kwasababu mpendwa yule kaonyeshwa au mimi nimeonyeshwa?? Au ninamwamini sana yule? Unadhani hilo tu linatosha?
Je! Ikitokea mwingine akakamwambia watu wote wenye Ngozi nyeusi, wanayo laana ya Hamu, hivyo wasipokombolewa kwa kupitishwa kwenye kemikali maalumu ya kuchubuliwa Ngozi zao, hawataingia mbinguni..Je! hilo nalo utalithibitisha vipi?
Ndugu ukiishi kwa Neno la Mungu, ni elimu tosha, ni ushuhuda tosha..hata kama mtu akikuambia nimeonyeshwa mashoga wote wapo motoni, wewe uliye na Neno, hutashangaa kana kwamba ni jambo jipya, kwasababu Neno linakuambia hivyo..Hata kama asingekuletea maono hayo.
1Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi”.
Hivyo hapo hujaishi kwa maono yako, bali kwa Neno la Mungu, basi upo salama.. Hatari inakuja ni pale mtu unapotegemea tu shuhuda, na kuziamini moja kwa moja bila hata ya kuzipima..ndugu utatoka nje ya mpango wa Mungu, utachanganywa, utaishi kwa hofu na wasiwasi, na presha kubwa, kwasababu huyu atakuambia hivi yule vile, yatachanganyikana ya ukweli na uongo..matokeo yake utashindwa kujua ni wapi umesimama..Na mtu wa namna hii ni rahisi sana kuanguka dhambini. Na ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana wa kuijua biblia.. SOMA BIBLIA.
Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.
Kuwa makini na shuhuda unazozisikiliza mitandaoni (youtube)..Kuwa makini na watu unaowafuatilia mitandaoni. Usipoijenga Imani yako katika Neno la Mungu, shetani atakusaidia kujenga Imani yako katika misingi yake mwenyewe.
Usiniamini mimi, wala usimuamini mtu yeyote, iamini biblia yako, hiyo inatosha..Utakuwa salama.
Mwingine atakuambia Bwana ameniambia leta nywele zako, na kucha zako, weka kwenye kitambaa chekundu, tuombe Pamoja, ukimuuliza misingi hiyo ameitolea wapi, atakuambia nimefunuliwa, na usipofanya hivyo huwezi kufunguliwa.. Hii ni Hatari kubwa sana! ..Kataa kusikiliza hayo mafunuo.
Mwingine atakuambia, pasipo kuniamini mimi, huwezi kwenda katika unyakuo, kataa
1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;”
Usiwe mwepesi wa kuamini Neno lolote usilolithibitisha katika maandiko,
Bwana atusaidie..
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
Kama unadhani mazingira ni sababu ya wewe kutokuwa Mwanafunzi wa Yesu, basi tafakari mara mbili!.
Unaweza kusema labda Nimezaliwa katika dini inayompinga Kristo, nawezaje kuwa Mkristo tena yule wa kujikana nafsi?..nimeolewa na mtu ambaye anampinga Bwana Yesu? Na familia yangu yote haimwamini Yesu wala haiamini Ukristo..je inawezekana mimi kuwa mkristo na kuanza kwenda kanisani na hata kumtumikia yeye?
Jibu ni Ndio! Yote yanawezekana endapo utaamua kujikana nafsi kwa kumaanisha kumfuata Yesu..
Inawezekana kabisa kuwa mwanafunzi wa Yesu, na hata kuifanya kazi yake. Wewe sio wa kwanza kukutana na mazingira kama hayo, hata katika biblia walikuwepo watu wa namna kama yako, ambao walikutana na mazingira magumu kuliko yako, lakini walishinda…lakini pia walikuwepo walioshindwa..
Hebu tujifunze katika makundi yote mawili, ya walioshindwa na walioshinda.
1 . WALIOSHINDWA.
Tusome,
Yohana 12:42 “Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi”.
Hawa ni Wayahudi, ambao walimwamini Kweli Yesu lakini, walihofia kutengwa na ndugu zao na zaidi sana masinagogi yao, yaani watu wa dini yao!. Hivyo wakaishia tu kumwamini Yesu lakini hakuna chochote walichozalisha.
2 . WALIOSHINDA.
Lilikuwepo ambalo lilikuwepo katika mazingira magumu, lakini lilishinda.
Mfano wa hao ni YOANA MKEWE KUZA, wakili wa Herode. Na MANIELI ndugu wa Herode.
YOANA, MKEWE KUZA.
Huyu Yoana, alikuwa ni mke wa mtu aliyeitwa Kuza, ambaye alikuwa ni wakili wa mfalme Herode. Sasa ili kujua vizuri familia ya Herode ilikuwa ni ya watu wa namna gani, tusome mistari ifuatayo..
Mathayo 2:16 “Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi”.
Herode alimtafuta kumwua Bwana Yesu katika uchanga wake, na hata kipindi amekuwa mkubwa mwanae alimkata kichwa Yohana mbatizaji.(Mathayo 14:1-10), na Zaidi sana baadaye alikuja kumwua Yakobo, mtume wa Bwana Yesu (Matendo 12:1-2) na alitafuta kumwua na Petro pia, lakini Bwana alimwepusha na mauti yake hiyo..
Kwahiyo kwa ufupi ni kwamba Herode alikuwa ni mpinga Kristo kwa wakati huo, na endapo angesikia yeyote katika watu wake kajishikamanisha na Bwana Yesu, wazo lake ni lile lile la kuua.. lakini tunaona huyu mke wa Wakili wake, aliyajua hayo yote, na Pamoja na hayo, akaamua kumfuata Yesu na kuwa mwanafunzi wake, pasipo kujali atapitia nini mbeleni.
Na tena sio yule mwanafunzi wa siri siri, bali yule wa wazi kabisa..ambaye anaambatana na Bwana Yesu kila mahali, na tena anamhudumia..
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,
2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
3 NA YOANA MKEWE KUZA, WAKILI WAKE HERODE, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao”.
Umeona?..Yoana alijua kuna kifo kinamgoja wakati wowote, lakini alijikana nafsi na akawa moja ya wanawake wa mbele kabisa walioheshimiwa na Bwana Yesu.
MANAENI
Sio huyo tu! Kulikuwepo na mwanaume mwingine anayeitwa Manaeni..Huyu maandiko yanasema alikuwa ni NDUGU WA KUNYONYA wa Mfalme Herode…maana yake wametoka katika familia moja na Herode, wanajuana ndani na nje!.. lakini pamoja na kwamba anajua ndugu yake ni mfalme tena Mpinga-Kristo, yeye hakumwogopa.. bali aliacha vyote akachukua msalaba wake, akamfuata Yesu, na hatimaye Bwana akamfanya kuwa NABII wake.
Matendo 13:1” Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na MANABII NA WAALIMU, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na MANAENI ALIYEKUWA NDUGU WA KUNYONYA WA MFALME HERODE, na Sauli.
2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia”.
Kupitia watu hawa wawili YOANA Pamoja na MANAENI, itoshe kutupa kila sababu ya sisi kujikana nafsi!.
Watu hawa watasimama siku ya hukumu Pamoja na sisi, ambao tunasema tupo katika mazingira magumu ya kumfuata Yesu, watatuhukumu.
Hivyo ndugu kama wewe umeolewa na mtu asiye mkristo, na sasa umemwamini Yesu, usione aibu wala usiogope, mkiri Kristo hadharani…kama wewe unaishi na wapagani ambao hawamwamini Yesu au wanampinga!.. bali usiwaogope.. wewe mfuate Yesu, kuwa mwanafunzi wake, jikane nafsi kama Yoana na Manaeni. Na Bwana Yesu atakuheshimu kuliko kawaida, atakutukuza kama alivyowatukuza Yoana na Manaeni.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.
Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?
NI NANI ALIYEKUPA MAMLAKA HII UYATENDE HAYA?
Wanafunzi wa Yesu, walimaanisha nini kusema kama “Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa”?
Kwanini Herode aliwakasirikia watu wa Tiro na Sidoni? (Matendo 12:20)
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe karibu tujifunze biblia,
Luka 21:37 “Basi, kila mchana alikuwa akifundisha hekaluni, na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni
38 NA WATU WOTE WALIKUWA WAKIAMKA MAPEMA WAENDE HEKALUNI ILI KUMSIKILIZA”.
Je unaijua sababu ya Bwana Yesu kulala juu ya mlima wa mizeituni?
Si kwasababu hakuwa na watu wa kumkaribisha kwake awe analala kwao? La! alikuwa nao tele!!, na wengine wenye uwezo mkubwa tu!.. mfano wa hao ni Yule Yusufu mwanafunzi wake ambaye alikwenda kumwomba Pilato auondoe mwili wake pale msalabani, maandiko yanasema alikuwa ni mtu tajiri.
Mathayo 27:57 “Hata ilipokuwa jioni akafika MTU TAJIRI wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;
58 mtu huyu alimwendea Pilato akauomba mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe”.
Mwingine ni Yule aliyempa chumba Bwana Yesu wakati wa Pasaka, (maandiko yanasema mtu huyu alikuwa ni mtu anayemiliki ghorofa, na kuna chumba maalum, juu ya ghorofa ambacho alikuwa amempa Bwana Yesu na wanafunzi wake).
Marko 14:13 “Akatuma wawili katika wanafunzi wake, akawaambia, Nendeni zenu mjini; atakutana nanyi mwanamume amechukua mtungi wa maji; mfuateni;
14 na po pote atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu asema, Ki wapi chumba changu cha wageni, niile pasaka humo, pamoja na wanafunzi wangu?
15 Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieni”.
Umeona?..watu hawa wote walikuwa wanaishi pale pale Yerusalemu, ambao wangeweza kumhifadhi Bwana kipindi yupo Yerusalemu…na siyo hao tu, bali pia walikuwepo na wengine wengi,
Lakini jiulize kwanini Bwana kipindi anakaribia kuteswa hakuwa anakwenda kulala katika nyumba zao?.. Sababu zipo mbili. 1) KUOMBA. na 2) KUWAHI IBADANI.
KUOMBA.
Bwana Yesu alikuwa ni mtu wa kuomba sana..na alijua mazingira bora ya kuomba ni yapi?, si ghorofani wala nyumbani. Bali ni sehemu iliyo na utulivu. Alijua Nyumbani kunakuwa na usumbufu mwingi ambao ungeweza kumwondoa katika uwepo,(usumbufu wa watu na kimazingira), Ndiyo maana utaona mara kadhaa akipanda mlimani pamoja na wanafunzi wake kuomba.. Hiyo ikitufundisha na sisi tuwe watu wa kuchagua mazingira sahihi ya kuomba.
KUWAHI IBADANI.
Sababu ya pili ya Bwana Yesu kulala katika mlima wa Mizeituni, ni ili AWAHI IBADANI. Alijua mazingira ya nyumbani si mazingira ambayo si rafiki kwa yeye kuwahi hekaluni.. kwasababu ya maandalizi kuwa mengi..
Utaona kipindi tu yupo kwa akina Miriamu na Martha, ni jinsi gani, Martha alivyokuwa anamhangaikia kumwandalia vyakula, mara chai, mara maji ya kunawa na kadhalika…mahangaiko yale, yakachukua mpaka muda wa kuanza kujifunza, mwisho Bwana Yesu ikabidi aanze kufundisha kabla hata ya Martha kumaliza kupika.. na kilichofuata utaona Martha!, alikwazika!..
Sasa mambo kama hayo hayo Bwana Yesu aliyajua ndio maana akatafuta mlima ulio karibu na hekalu awe analala huko kipindi anaendesha semina ya Masomo pale Hekaluni.
Kwasababu kukisha pambazuka tu, kazi aliyo nayo ni yeye pengine ni kunawa tu uso na kuteremka hekaluni kufundisha, pengine ingemchukua tu robo saa, kufanya maandalizi, tofauti na angekuwa nyumbani kwa watu..kwasababu Mlima wa Mizeituni na hekaluni ni mita kadhaa tu, si mbali..!
Hivyo Bwana Yesu akawa anawahi hekaluni mapema sana, wa kwanza kabla ya wote!..na kuwafundisha wale waliowahi kama yeye (akawa kielelezo). Na wengine wote walipoona kuwa anawahi, na kumkuta akifundisha wachache waliowahi kama yeye, na wenyewe wakawa wanaamka asubuhi na mapema kwenda kumsikiliza, wasikose madarasa hayo ya asubuhi..
Luka 21:37 “Basi, kila mchana alikuwa akifundisha hekaluni, na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni. 38 NA WATU WOTE WALIKUWA WAKIAMKA MAPEMA WAENDE HEKALUNI ILI KUMSIKILIZA”.
Kristo hata leo anawahi asubuhi na mapema Nyumbani kwake!.. na wote walio wake kweli kweli, wanawahi nyumbani kwake kumsikiliza! Na wanapokea Baraka!.
Katika siku hizi za mwisho, shetani anawaharibu wengi katika eneo la USINGIZI, na KUTOKUJALI. Asilimia kubwa ya watu wanaochelewa ibadani, au wasiofika kabisa ibadani ni kwasababu ya Usingizi!, au Kutokujali.
Kama kweli unamjali Bwana Yesu na maneno yake, huna sababu yoyote ya KUCHELEWA IBADANI, hata kama unakaa mbali na kanisa!, Amka mapema wahi kanisani!, KATISHA USINGIZI!!..Tabia ya kupenda usingizi kimwili, inafunua tabia ya kupenda usingizi katika roho, ambayo ni mbaya sana.
Na kama ukiona mahali ulipo ni mbali sana, basi siku moja kabla ya ibada, hamia karibu na maeneo ya kanisa, au kesha kanisani omba, asubuhi yake uamkie nyumbani kwa Bwana, utakuwa umejizolea Baraka nyingi zaidi.
Lakini kama utafika nyumbani kwa Bwana kwa kuchelewa kwasababu ya usingizi!.. basi ni heri usingefika kabisa kanisani hiyo siku, kwasababu hakuna chochote unachokwenda kupokea hiyo siku!!, ni heri urudi nyumbani ukamalizie usingizi wako tu!!. Tabia ya KUPENDA USINGIZI na ya KUTOKUJALI ni tabia zinazomchukiza Bwana kuliko zote (soma Luka 22:46, Marko 13:35-37).
Na kumbuka hakuna maombi ya kuondoa KUONDOA USINGIZI!!..Dawa ya kuushinda usingizi ni kuamua kubadilisha tabia tu!, na wala si kuombewa!!.. Bwana Yesu alipowakuta akina Petro wamelala muda wa kuomba, hakwenda kukemea mapepo ndani yao!.. alichofanya aliwaambia WAAMKE WAOMBE!.. Roho zao zi radhi, lakini miili ndio midhaifu, hivyo wajilazimishe waamke!.
Na wewe leo hii, Amka mapema nenda Ibadani, amka mapema nenda kwenye maombi, amka mapema nenda shambani kwa Bwana, Ukatae usingizi, na pia Acha kuwa mtu wa KUTOKUJALI.
Bwana atubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
:
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Sehemu ya kwanza: LIA NA NYONYA.
Nakusalimu katika jina kuu lenye uweza la mwokozi wetu Yesu Kristo, sifa na heshima vina yeye milele na milele.
Haya ni Makala maalumu kwa waongofu wapya, ikiwa wewe umeokoka hivi karibuni, au una ndugu/mpendwa ambaye amempokea Bwana Yesu siku za karibuni basi Makala hizi ni muhimu sana kwako au kwa yule mwingine.
Tunaposema kuokoka, tunamaanisha Kuzaliwa mara ya pili. Na mtu anazaliwa mara ya pili, kwa kutubu dhambi zake kwa kumaanisha kabisa kuuacha ulimwengu, na pia kwa kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi (Yohana 3:23), na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na kwa kupokea Roho Mtakatifu..Kwa kuzingatia hivyo vigezo, basi mtu huyo anakuwa ameshazaliwa mara ya pili.
Lakini sasa hilo peke yake halitoshi, wengi wanapotimiliza maagizo hayo wanajisahau na kudhani ndio tayari wameshatimilika, hakuna cha ziada.. Hawajui kuwa mtu unaweza ukawa kweli umezaliwa mara ya pili lakini ni kiumbe kilicho kufa.. Utajiuliza ni kwa namna gani inakuwa hivyo?
Mtu anayezaliwa mara ya pili katika roho anafananishwa na mtoto, anayezaliwa mara ya kwanza katika dunia. Kwa kawaida mtoto huyo, ni lazima aonyeshe tabia kuu mbili. Kabla hajaweza hata kuona, au kuzungumza, au kujitambua..Ni lazima
ALIE kwa sababu gani.. Mtoto anapotoka tumboni kwa mama yake, anakuwa kama kiumbe mfu, wanachofanya wakunga ni kumpiga kidogo, kumshutua ili atoe sauti, wakisikia analia basi wanatambua kuwa kiumbe kilichozaliwa ni hai, hivyo baada ya muda kidogo wanamsogeza katika hatua nyingine,
Ambayo ni kunyonyeshwa.
Cha kushangaza ni kwamba mtoto yule anaposogezwa katika nyonyo la mama yake, hakuna mtu yeyote anayemfundisha kunyonya, utaona ni yeye mwenyewe anajua wajibu wake, wa kula, ndio hapo utaona saa hiyo hiyo ataanza kufyonza maziwa kana kwamba alishawahi kufundishwa huko tumboni jukumu lake kabla hajafika duniani.
Sasa kiroho pia ndio ipo hivyo. Ikiwa wewe umezaliwa kweli mara ya pili, hizi ni hatua za awali kabisa ambazo utazionyesha. Na kupitia hizo sisi wengine tutathibitisha kweli wewe ni kiumbe kipya hai. Kwani ni lazima utoe kelele fulani rohoni.. Huwezi kutulia, ambao sisi tuliokomaa kiroho tutazitambua, japo wewe hutoweza kuzielewa katika hatua yako ya uchanga rohoni..
Sisi tutaona kuhangaika kwako kutaka msaada wa kumjua Mungu, Na sisi tukishalitambua hilo, basi tunakuwa na wajibu mkubwa sana wa kukusaidia, kukosegezea matiti (Neno la Mungu) unyonye..
Hebu tujifunze kisa cha Musa, pindi anazaliwa..Biblia inatuambia, alipozaliwa, mama yake alimficha ili Farao asimuue, lakini alipoona hali imekuwa mbaya, alimtengenezea kisafina kidogo, kisha, akamtupa mtoni.. Lakini mtoto yule alipokuwa katika kila kisafina, hakukaa kimya tu, bali alikuwa anapiga kilele, analia,sana na binti Farao aliposikia alikwenda kutazama na kufungua aone ni nini kipo ndani, akakaona katoto, wakakahurumia..Embu tusome kwa ufupi kisa hicho;
Kutoa 2:6 “Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, MTOTO YULE ANALIA. BASI AKAMHURUMIA, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania.
7 Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu?
8 Binti Farao akamwambia, Haya! Enenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto.
9 Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha.
10 Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa, akasema, Ni kwa sababu nalimtoa majini”.
Umeona? Mtoto yule angeangamia kama asingelia, lakini alipolia, akahurumiwa akatafutiwa msaada mapema wa kunyonyeshwa, na hatimaye akakua akaja kuwa Mkombozi wa Israeli, ndiye Musa tunayemsoma.
Ndugu/Dada uliyeokoka hivi karibuni, kutojishughulisha kwako na mambo ya Mungu, kunathibitisha kuwa wewe ni kiumbe mfu, kutoulizia kwako Habari ya ibada, kunatuambia kuwa wewe si kiumbe hai..Hupaswi kujificha, hupaswi kujiepusha na kiongozi wako wa kiimani..hupaswi kukaa mbali na wapendwa, hupaswi kupitisha siku nyingi hujulikani upo wapi, au maendeleo yako ya kiroho hayatambuliki.. kataa hiyo hali kwa nguvu zote..
Wewe tayari ni kiumbe kipya, yatamani sana maziwa ya roho.. Usisubiri kukumbushwa kumbushwa kuhudhuria mafundisho ya kuukulia wokovu, kama mtoto mchanga ambaye hafundishwi na mtu kunyonya ni wajibu wako kutafuta kufundishwa Neno la Mungu, kwa bidi zote..Sio wewe utafutwe.
1Petro 2:2 “Kama watoto wachanga wazaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili k hayo mpate kuukulia wokovu.
Hivyo anza sasa kubadilisha mwenendo wa Maisha yako.. Jifunze kuomba na wapendwa, jifunze, kusoma biblia mwenyewe kuanzia sasa, jifunze kuuliza maswali, jifunze kumshirikisha na kukuonyesha njia sahihi.
Wagalatia 6:6 “Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake up
Hivyo zingatia mambo hayo makuu mawili. Na Bwana akutie nguvu.
Shalom.
Sehemu ya pili itafuata…
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
:
Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?
ILI TUONEKANE SAFI MBELE ZA MUNGU TUFANYE NINI?
Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?
Swali: Bwana alimaanisha nini kusema wokovu watoka kwa Wayahudi?, kwani si tunajua Wokovu unatoka kwa Mungu, iweje hapo aseme unatoka kwa Wayahudi?
Jibu: Tusome,
Yohana 4:22 “Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.”
Wokovu unaozungumziwa hapo, ni “Wokovu wa Roho”..na si wokovu wa vita au kitu kingine!, na aliposema kuwa “unatoka kwa Wayahudi” hakumaanisha kuwa Wayahudi ndio wanaoutoa wokovu na kuwapatia wengine la!, hakuna mtu wala Taifa linaloweza kuiokoa roho ya mtu!!, bali alimaanisha kuwa “wokovu unaanzia kwa wayahudi”, na ndipo unaenda kwa wengine…(yaani kwa watu wa mataifa ikiwemo na wasamaria ndani yake).
Ndio maana utaona ni kwanini Bwana wetu Yesu hakuzaliwa nje na jamii ya Israeli, wala hakuzaliwa katika Samaria, au katika Taifa lingine lolote tofauti na Israeli, badala yake alizaliwa Israeli, sawasawa na unabii Mungu alioutoa kupitia manabii wake wa zamani kama Musa, Daudi, na wengineo.
Na baada ya kuzaliwa katika jamii ya Wayahudi (yaani waisraeli), hakuanza kuhubiri injili yake kwa jamii ya watu watu wa mataifa, halafu ndio afuate kwa watu wa jamii ya Israeli(wayahudi) bali badala yake alianza kwanza kwa Wayahudi, na walipokataa ndipo akaruhusu injili ihubiriwe pia kwa watu wa mataifa ambao ndani yake pia wapo wasamaria.
Mathayo 10:5 “Hao Thenashara Yesu aliwatuma, AKAWAAGIZA, AKISEMA, KATIKA NJIA YA MATAIFA MSIENDE, WALA KATIKA MJI WO WOTE WA WASAMARIA MSIINGIE.
6 Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia”.
Umeona?..Wanafunzi walikatazwa na Bwana kuhubiri kwa watu wa Mataifa katika mwanzo wa Injili, lakini baadaye, baada ya Wayahudi kushiba, na kukinai….Bwana Yesu aliwaruhusu pia wanafunzi wake waende kwa watu wa mataifa duniani kote wakahubiri injili kwa kila kiumbe.
Marko 16:14 “Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.
15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Tunazidi kulithibitisha hili pia, kipindi Mtume Paulo anawahubiria wayahudi wa Antioko..
Matendo 13:45 “Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.
46 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa LAZIMA NENO LA MUNGU LINENWE KWENU KWANZA; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.
47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.
48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini”.
Umeona?.. Wokovu umeanzia kwa Wahayudi, na ukaenda kwa watu wa Mataifa. Hiyo ndio sababu ya Bwana Yesu kusema.. “Yohana 4: 22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.”
Je umeupokea Wokovu wa Bwana Yesu ambao tumeletewa sisi watu wa mataifa, ambao hapo kwanza hatukustahili?. Kama bado unasubiri nini?.. Pengine kweli umeupata Wokovu, lakini je! Unaujali kwa kuutunza?.. Au ni kama tu utambulisho katika Maisha yako, lakini hauna thamani nyingine yoyote ya ziada katika Maisha yako?.
Kumbuka kama unavaa nusu uchi, au nguo ambazo si za kujisitiri, kama vile suruali(kwako wewe mwanamke) au vimini tambua kuwa unaudharau wokovu wa Bwana, kama unalewa, au unacheza kamari, au unazini, au unafanya uchawi, au unaiba baada ya kuisikia injili mara nyingi, au baada ya kubatizwa..tambua kuwa unaudharau wokovu wa Bwana.
Hatari ya kutouthamini Wokovu wa Bwana ni hii tunayoisoma katika Waebrania 2:1.
Waebrania 2:1 “Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.
2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,
3 SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia”
Utapataje kupona, wewe ambaye huujali Msalaba?..siku ile utakuwa mgeni wan ani?..ni heri ukatengeneza mambo yako leo ili uwe na uhakika wa maisha yako ya umilele.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)
Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?
Nakusalimu tena katika jina la Bwana Yesu mwokozi wetu, karibu katika kutafakari Maneno ya uzima..huu ni mwendelezo wa Makala zinazohusu malezo ya Watoto kwa mzazi.
Ikiwa wewe ni mzazi au mlezi na unao Watoto wadogo chini yako wa kuwalea, au unatarajia kuwa na Watoto.. Basi Makala hii ni muhimu sana kwako,
Zipo Makala nyingine tulishazitazama huko nyuma ikiwa hukuzipitia, basi waweza waweza wasiliana nasi inbox kwa namba hizi +255693036618 tuweze kukutumia.
Leo tutaona umuhimu wa kuwafundisha, Watoto nyimbo za kumsifu Mungu au kumwimbia..Awali ya yote ni lazima ufahamu kuwa, kila mtoto amewekewa ibada ya sifa ndani yake, haijalishi utalipenda hilo au hautalipenda..Na ibada hiyo huwa inakamilika pale anapokutana na Watoto wenzake kwenye michezo sehemu za wazi..Hapo ndipo utajua hicho kitu kipo ndani yake.
Kaa chunguza kwa makini, mahali palipo na Watoto wengi wamekusanyika, utasikia wakiimba vi-nyimbo Fulani mbalimbali, kulingana na kile ambacho walifundishwa, au wanachokisikia watu wengine wakiimba..
Na ndio maana Bwana Yesu alitumia mfano wa Watoto wanaocheza, masokoni, kwa kuimba, kukifananisha kizazi hiki jinsi mienendo yao ilivyokuwa na mwitikio mdogo wa injili..
Luka 7:31 “Bwana akasema, Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini?
32 Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia”.
Sasa wewe ukiwaona wanaimba unaweza kuchukulia kirahisi rahisi sana ukasema wanacheza tu, wanajifurahisha..lakini rohoni wanaonekana wanasifu katika ukamilifu wote, na hivyo wanasababisha madhara makubwa sana, hata kwa upande wa pili.
Ili tuelewe vizuri embu tujifunze kisa kimoja, kilichotokea Yerusalemu kipindi kile Bwana Yesu, anaingia akiwa amepanda punda na mwanapunda..Biblia inasema, watu walimtandikia nguo zao chini, na wengine majani ya mitende, wakaanza kumsifu kwa nguvu, wakisema Hosana hosana, Mwana wa Daudi..
Lakini wakati huo huo kulikuwa na kundi la Watoto linaongozana nao pembeni likiwasikiliza.. linajifunza hizo nyimbo..ndipo tunaona mwishoni kabisa wale watu walipomaliza sifa zao, Bwana Yesu aliingia Hekaluni, Lakini kule hekaluni, Watoto, hawakukaa kimya, wakaanza kutoa walivyovisikia,..wakawa wanakiimba kile wachokisikia kule nje! Hosana hosana, mwana wa Daudi..
Tendo lile likawa bughza kwa maadui wa Kristo, walipokuwa wanawasikia Watoto wakipiga kelele kama nyuki hekaluni, wakiimba walichokuwa wanakisikia, ndipo wakamfuata Kristo, kumuonya.. Lakini tunaona, Bwana hakuwaambia sawa nitawanyamazisha kinyume chake akawapa siri nyingine ambayo walikuwa hawaijui..akawaambia maneno haya.. “HAMKUPATA KUSOMA, KWA VINYWA VYA WATOTO WACHANGA NA WANYONYAO UMEKAMILISHA SIFA”
Mathayo 21:9-10,15-16
“9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?
11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya…..
15 Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika,
16 wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?”
Umeona? Kumbe sifa za kweli zimekamilika katika vinywa vya Watoto wachanga, sio ajabu kuona mapepo yale yakilipuka ndani ya wale waandishi na wakuu wa makuhani, na kutaka kumshambulia Yesu kwasababu yao..
Mapepo yaliyokuwa yameigeuza nyumba ya Mungu kuwa pango la wanyang’anyi, sasa yanakutana na waaabuduo halisi wanaomwabudu Mungu katika Roho na kweli wamefika..(watoto)..Ni lazima yataabikie tu..
Kama sifa za kweli zimekamilika katika vinywa vya Watoto wachanga, basi tunapaswa tutumie nguvu nyingi sana kuwafundisha Watoto kumwimbia na kumsifu Mungu, Ni muhimu sana, kwasababu hizo tu zinatosha kumtikisa shetani na ufalme wake..
Lakini kinyume chake ni kweli, kama mtoto hatoimba nyimbo za Mungu, badala yake amekaririshwa, bongofleva, na manyimbo ya kidunia, tufahamu kuwa sifa hizo pia zinakuwa zimekamilika kwa shetani. Hivyo, shetani anatukuzwa, na ufalme wa Mungu unadidimia.
Inasikitisha leo hii, kuona makundi ya Watoto wengi barabarani wanaimba nyimbo za wasanii wa kidunia, ambazo hata wewe mtu mzima kusikiliza unaziba masikio, mpaka unajiuliza hivi wazazi au walezi wao wapo wapi?
Wazazi wapo buzy na kazi, wapo buzy na biashara, wanachozingatia kwao tu ni elimu za duniani basi..Hayo mengine hawahangahiki nayo, hawajui kuwa mapepo yanapata nafasi katika mahekalu yao( yaani Nyumba zao), kwasababu ya sifa za Watoto wao za kipepo, zinamtukuza Ibilisi mwenyewe..
Ndugu, ukitaka furaha katika nyumba yako, embu wafundishe Watoto wako kuimba mapambio, vichwa vyao vijae sifa na nyimbo, waimbe hizo wakati wote, wachezecheze wakiimba hizo sio bongofleva.. kataa mtoto wako kujifunza, hizo nyimbo, wala usimvumilie unapomwona anaziimba bali mkemee.. sio kila mahali umpeleke mtoto au uende naye, huko atajifunza manyimbo ya ibilisi..
Wakati huu ambao bado ni wachanga, vichwa vyao huwa vinakamata sana upesi, hivyo tumia fursa hiyo, kuwapeleka Watoto, Sunday school, na kwenye mafundisho yao, ili wafunze huko kuimba na kumtukuza Mungu..Amani ije nyumbani kwako.
Bwana atusaidie sana, kuliona hilo.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.
KAMA “MAMA” UMEBEBA HATIMA YA MTOTO WAKO WA KIUME.
Je! Siku ya unyakuo watoto wachanga watanyakuliwa?
Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
SWALI: Mstari huu una maana gani? Je, ni kweli waandishi waliweza kubadilisha baadhi ya maneno ya torati, Na hivyo inaifanya biblia isiamike hadi sasa?
Yeremia 8:8 “Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
JIBU: Hii ni hoja inayotumiwa sana na wapinga-biblia, au wapinga-ukristo. Wakisimamia mstari huu, na kusema, unaona? Biblia ilichakachuliwa, zamani na waandishi wa kiyahudi kwa kuongeza baadhi ya maneno katika torati iliyoandikwa na mwenyezi Mungu,.. Kwahiyo hiyo inathibitisha kuwa biblia ni kitabu chenye kasoro..
Lakini je tukisoma vifungu hivyo, vinatuambia waliibadilisha torati?
Kabla ya kuendelea kusoma zaidi, embu tuitafakari tena hiyo kauli hapo mwishoni, anasema “kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo”. Ahaa Kumbe waandishi ndio wameifanya kuwa uongo..Lakini yenyewe kama yenyewe sio uongo.. Mfano nikikuambia, unanifanya kuwa mwongo mbele za ndugu zangu, haimaanishi kuwa mimi ni mwongo..maana yake ni kuwa, pengine ni kwasababu uliyawakilisha maneno yangu isivyopaswa, aidha kwa kuongeza chumvi au kupunguza, na kwasababu hiyo basi, mimi nikaonekana nimeongopa, lakini sivyo, mimi nilisema ukweli mwanzo, isipokuwa wewe ndio umeniwakilisha vibaya.
Ndivyo ilivyokuwa hapo, waandishi, ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kufundisha na kuwaelezea watu, walianza, kutoa tafsiri zisizo sawa za torati, na kuwafundisha watu na kuwaandikia, mfano Bwana Yesu alisema, waliipindua amri ya tano; inayosema waheshimu baba yako na mama yako, na kuwaambia watu, ikiwa kuna chochote umekiweka wakfu hupaswi kumsaidia mzazi wako, hata kama akiangamia kwa njaa ni sawa tu..Jambo ambalo Mungu hakuliagiza hata kidogo, ilikuwa ni wajibu wa kila mtu kumsaidia mzazi wake, awapo katika uhitaji (Soma Marko 7:7-13)
Umeona, sasa tukirudi kwenye ile habari ya mwanzo ili kuthibitisha hilo vizuri, ukiendelea kusoma vifungu vinavyofuata utaona Yeremia, anaeleza kwa undani jinsi kalamu za hao waandishi zilivyoweza kuipa torati tafsiri zisizo sahihi..
Yeremia 8:8 “Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
9 Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la Bwana, wana akili gani ndani yao?
10 Basi, kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao na mashamba yao nitawapa wale watakaowamiliki; MAANA KILA MMOJA WAO, TANGU ALIYE MDOGO HATA ALIYE MKUBWA, NI MTAMANIFU; TANGU NABII HATA KUHANI, KILA MMOJA HUTENDA MAMBO YA UDANGANYIFU.
11 KWA MAANA WAMEIPONYA JERAHA YA BINTI YA WATU WANGU KWA JUU-JUU TU, WAKISEMA, AMANI, AMANI, WALA HAPANA AMANI.
12 Je! Walitahayarika, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakutahayarika, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema Bwana..
Umeona hapo? Anasema, hao waandishi na makuhani, wanawatabiria watu amani, amani, na kuwaambia mnaishi sawasawa na torati ya Mungu inavyosema, hivyo hamwezi kupatwa na madhara, ili hali ndani yao wanatamani, ni waovu, waabudu masanamu, wanakula rushwa n.k..
Wakati torati inakataza vikali vitu hivyo, wenyewe wanawatumainisha watu, Mungu anawapenda, ndio hapo anasema, wanawaponya jeraha zao kwa juu juu tu, mwisho wa siku wanaadhibiwa, halafu wanasema Mungu ni mwongo.. Mbona anatupiga bila sababu!.
Je! Waandishi wa namna hii wapo hadi sasa?
Jambo hili lipo hadi sasa katika kanisa la Mungu, Siku hizi za mwisho makristo na manabii wengi sana wa uongo wametokea, nao wanawaponya watu wa Mungu juu juu tu, hawawaelezi ukweli, mpaka inafikia hatua Mungu anaonekana mwongo, hasikii wala hajibu.
Wanawaambia, utafanikiwa, utabarikiwa, kesho yako ni ya kung’ara kama jua, wanawaambia watoe sadaka nyingi, watumie maji ya upako, mafuta na chumvi, wakati mwingine wafunge mwaka mzima, Mungu atawabariki.. Lakini wanasahau kuwa hao watu wana mizigo ya dhambi, ndiyo inayowafanya wasijibiwe maombi yao.. Kama vile maandiko yanavyosema..
Isaya 59:1 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya”.
Hivyo hao watu wanataabika, januari mpaka disemba, lakini hawaona nuru yoyote, hawaona uzima wowote, ndio kwanza hali inakuwa mbaya, mwishoni wanakataa tamaa wanasema Mungu hajibu maombi, wanawageukia waganga wa kienyeji.
Ndugu, Neno la Mungu ni kweli kabisa, akisema atakuponya, atakuponya kweli, akisema atakubariki atakubariki kweli, lakini ni sharti ujue, anataka nini kwanza kwako ili hivyo vyote vikujie.. Anachotaka ni wewe uache dhambi, uache, rushwa, uache uzinzi, uache uongo, uache vimini, uache fashion za kidunia, anasa, uache ulevi, uwe mtakatifu. Ndipo hayo yote yatakapokujia..
Epuka injili zizisogusia dhambi katika maisha yako, ziepuke kama ukoma, hizo huwa zinakuja na maneno mazuri sana ya kushawishi na kufariji, lakini hazitakusaidia chochote, Mungu ni mtakatifu, kamwe hajibu maombi ya mwenye dhambi.
Je! Umeokoka? Kweli kweli kwa kumaanisha kumfuata Kristo? Kama la! Basi huu ndio wakati wako sasa kuanza upya na Kristo. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo, basi, waweza tupigia kwa namba uzionaza hapo chini.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MAJIBU YA MASWALI YANAYOULIZWA NA WASIO WAKRISTO (Sehemu ya kwanza).
Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?
Yesu ni Mungu?, Na Kama ni Mungu kwanini alikufa?
Nini maana ya “Torati na manabii”?
Neno “Mashehe” tunaliona likitajwa katika biblia(Agano la kale); Hawa mashehe ni wakina nani?
Je! Karamu za ‘Idi’ ndio zipo hizo tunazozisoma katika Hosea (12:9)
Unawaza nini juu ya kuipeleka injili mbele?..Je unafikiri nini juu ya hali ya kiroho ya wanao miaka kadhaa mbele?, endapo parapanda itakuwa haijalia miaka 20 ijayo, je hali ya kiroho ya wanao itakuwaje, ukilinganisha na kasi ya maadili kuporomoka?.. Je umewahi kufikiri kufanya chochote leo hii, ili miaka ya mbeleni watoto wako au Watoto wa wengine, wasikose chakula cha uzima?…
Kizazi tulichopo ni kizazi kinachoharibika kila siku, umewahi kufikiri hali itakuwaje miaka 10 mbeleni?..kama umewahi kufikiri kwamba hali utakuwa mbaya Zaidi kuliko sasa, basi pia jiulize leo hii unafanya nini ili wakati huo utakapofika, shetani asipate nafasi inayoiona mbeleni.
Kumbuka wewe usipotumia muda wako leo, au akili zako leo, au nguvu zako leo, kufikiri na kufanya jambo lolote juu ya ufalme wa Mbinguni, Bwana atafanya kupitia wengine, (kwasababu kazi yake ni lazima iende mbele) lakini wewe wewe utakuwa umejipunguzia thawabu zako mbele zake.
Hebu Leo tujifunze juu ya watu wawili katika biblia, ambao kupitia hao, tutapata hamasa na hekima katika kufikiri kuujenga ufalme wa mbinguni.
Mtu wa kwanza ni DANIELI, na wa pili ni YUSUFU. Watu hawa wawili wote walijaliwa uwezo wa kutafsiri ndoto, lakini kila mmoja kwa namna yake.
DANIELI:
Kuna wakati Mfalme Nebkadneza, (Mfalme wa Babeli) aliota Ndoto, lakini akawa ameisahau ile ndoto, na Danieli alipomwomba Bwana, aliweza kufunuliwa ndoto ile Pamoja na Tafsiri yake..na akaenda kumwambia mfalme, na ndoto ile na tafsiri yake vikathibitika..Na Mfalme akamtukuza sana Danieli, lakini si kama Yusufu.
YUSUFU:
Farao Mfalme wa Misri, naye aliota ndoto kama Nebukadneza…na ndoto ile alipoamka aliikumbuka…lakini cha ajabu ni kwamba hakuwaficha watafsiri wake ndoto ile, bali aliwahadithia alichokiota..yeye alichokuwa anahitaji tu ni maana ya ile ndoto..
Na alikuwa anajua kuwa watatokea waongo wengi, ambao watamwambia uongo..na kweli walitokea wengi wakampa tafsiri ya ndoto yake..lakini tafsiri zote hizo alizikataa..
Sasa ni Siri gani iliyofanya Tafsiri ya Yusufu ikubalike Zaidi ya zile nyingine zote??
Siri yenyewe ni mikakati baada ya kuielezea ile tafsiri..
Yusufu baada ya kusema kuna miaka 7 ya neema inakuja na 7 ya Njaa.. hakuishia hapo tu!.. lakini alitoa mikakati ni NINI CHA KUFANYA KATIKA HIYO MIAKA 7 YA NEEMA NA MIAKA 7 YA NJAA. Ndio utaona akamshauri Farao atafute mtu mwenye akili amweke juu ya kazi zake zote akusanye chakula cha kutosha katika miaka ya neema, ili itakapokuja miaka ya njaa basi hazina iwepo kubwa. (Hilo ndio wazo lililompandisha hadhi Yusufu, na wala si tu tafsiri)!..
Farao aliona hata kama tafsiri itakuwa ni ya UONGO, lakini wazo alilotoa YUSUFU NI LA HEKIMA NA AKILI…, hata kama Njaa haitakuja kama alivyotafsiri, lakini wazo tu la kuweka chakula akiba ni wazo kubwa sana na la akili sana, ambalo pengine katika utawala wake wote Farao hajawahi kushauriwa hivyo…
Tusome..
Mwanzo 41:28 “ Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.
29 Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri.
30 Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi.
31 Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana.
32 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.
33 BASI, FARAO NA AJITAFUTIE MTU WA AKILI NA HEKIMA AMWEKE JUU YA NCHI YA MISRI.
34 FARAO NA AFANYE HIVI, TENA AKAWEKE WASIMAMIZI JUU YA NCHI, NA KUTWAA SEHEMU YA TANO KATIKA NCHI YA MISRI, KATIKA MIAKA HII SABA YA KUSHIBA.
35 NA WAKUSANYE CHAKULA CHOTE CHA MIAKA HII MYEMA IJAYO, WAKAWEKE AKIBA YA NAFAKA MKONONI MWA FARAO WAKAKILINDE KUWA CHAKULA KATIKA MIJI.
36 NA HICHO CHAKULA KITAKUWA AKIBA YA NCHI KWA AJILI YA MIAKA HIYO SABA YA NJAA, ITAKAYOKUWA KATIKA NCHI YA MISRI, NCHI ISIHARIBIKE KWA NJAA.
37 NENO HILO LIKAWA JEMA MACHONI PA FARAO, NA MACHONI PA WATUMWA WAKE WOTE.
38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?
39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.
40 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe”.
Umeona?.. watafsiri wengine walikuwa wanakuja na tafsiri zao lakini mwisho wa siku wanamshauri Farao mambo yasiyo na hekima, wala yasiyojenga, wala yasiyo na manufaa..ndio maana hata tafsiri zao Mfalme alizikataa.. Lakini Yusufu alipotoa tafsiri na mikakati bora baada ya ile tafsiri ndipo hata tafsiri yake ikathibitika.
Na utaona Yusufu alipokea kibali sana mbele ya Farao, Zaidi hata ya Danieli alivyotukuzwa na Nebukadreza.
Je na wewe unataka kibali leo mbele za Mungu? Kama Yusufu alivyopata mbele ya Farao??..kama ndio! basi anza kufikiri kuhusu Injili ya Kristo, katika siku za mbeleni, na anza kufanya kitu kuanzia sasa. Kama ni mhubiri basi weka hazina kwa vizazi vinavyokuja… Kama ni mtu wa kukirimu, basi changia injili kwa mali zako kwa kadiri uwezavyo, ili kusudi Watoto wanaochipukia wasikue na kukuta idadi ya disco na bar zimezidi makanisa, wasije wakakuta idada ya vikundi vya wahuni vimezidi vya watu wema, wasije wakakutana na ugumu wa kuitafuta injili ya kweli, Zaidi ya huu tulionao sisi katika kizazi chetu..
shetani anayo mikakati sasahivi ya kuharibu kizazi hata cha tano kijacho..na hata sasa kashaanza kufanya juhudi hizo, inatupasaje sisi, tunaosema tumeokoka sasa? Kama wewe umeipata injili ya kweli, kiurahisi, basi rahisisha pia kwa wanaokuja, ambao kwa ambao hawajasikia..ndivyo Mungu atakavyokupa kibali.
Mithali 13:22 “Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi”
Tujifunze kwa Yusufu, ili na sisi tupate kibali mbele za Mungu.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
UKIOKOKA, JIANDAE KUPITISHWA USIPOPATAZAMIA.
Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?
Kwanini vizazi vya ukoo wa Yesu vinajipinga katika Mathayo na Luka.
Swali: Deuterokanoni ni nini? na je vitabu vya Deutorokanoni ni vitabu vya kiMungu? (ambavyo vimevuviwa na Roho Mtakatifu) na vyenye kufaa kwa mafundisho.?
Jibu: Deuterokanoni ni vitabu vingine saba (7) ambavyo vimeongezwa na kanisa Katoliki juu ya vitabu 66 vya Biblia takatifu, na hivyo kufanya jumla ya vitabu 73 katika biblia ya kikatoliki. Maana ya neno “Deuterokanoni” ni “Orodha ya pili” ambayo imekuja baada ya orodha ya kwanza yenye vitabu 66
Na ordha hiyo ya vitabu vya Deuterokanoni ni..
1. Tobiti
2. Yudith
3. Wamakabayo I
4. Wamakabayo II
5. Hekima
6. Yoshua bin Sira
7. Kitabu cha Baruk.
Vitabu vya Deuterokanoni, viliandikwa baada ya nabii wa Mwisho (Nabii Malaki) kupita!.. Na vitabu hivi hapo kabla havikuhesabiwa kuwa vitabu vitakatifu na pia wakristo!!..na wala havikuwekwa katika orodha ya vitabu vitakatifu au vya mafundisho ya kiMungu.
Vilikuja kuongezwa katika orodha ya vitabu vitakatifu na Papa Damasus 1 katika karne ya 4.
Lakini swali ni je!.. Vitabu hivi ni vitabu vitakatifu? Na kama sio kwanini?
Jibu ni kwamba vitabu hivi si vitabu vitakatifu wala vilivyovuviwa na Roho Mtakatifu, kwasababu zifuatazo.
Vinakinzana na vitabu vingine vitakatifu.
Kamwe Mungu hajichanganyi, na wala Neno lake halijichanganyi..lakini vitabu hivi vina mafundisho ambayo yanakinzana na mafundisho ya kweli ya Roho mtakatifu yaliyopo ndani ya vitabu 66. (Vitabu 66 havipingani hata kimoja, bali vyote vinakubaliana katika jambo moja, kwasababu vimevuviwa na Roho huyo huyo mmoja), lakini vitabu vya Deuterokanoni vinapingana na vitabu hivi vingine 66.
Kwamfano kitabu cha 2 Wamakabayo 12:43-45 kinafundisha Maombi kwa Wafu, na mafundisho ya toharani, jambo ambalo halionekani katika vitabu vingine 66 vya biblia.
Hakuna mahali popote katika biblia, panaonyesha kuwa wafu waliombewa au wanaombewa.. Zaidi sana biblia inasema katika Waebrania 9:27 “ kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu”.
Kwahiyo kitabu hiki si cha kiMungu, kwasababu Mungu kamwe hawezi kujichanganya..huku aseme hivi, na kule aseme vingine..
Na pia vitabu hivi, kuna sura zinazofundisha “Ulevi”, “Uchawi” na “Mazungumzo ya uongo”. Kwahiyo kwa ufupi si vitabu vya kiMungu, bali ni vya adui, shetani..ambavyo lengo lake ni kuwapeleka watu mbali na Mungu.
Biblia yenye vitabu 66, ndio biblia pekee ambayo mwanzo wake hadi mwisho wake imevuviwa na Roho Mtakatifu, na Ndio Neno la Mungu pekee, lakini hiyo yenye vitabu vya Deuterokanoni na nyingine yoyote yenye vitabu Zaidi ya hivyo ni ya kishetani, na si ya kuisoma wala kusikiliza mahubiri yanayotumia vitabu hivyo.
1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”
Bwana Yesu akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?
Je! tunapaswa kukiamini Kitabu cha Henoko?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Maran atha!