Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Nakukaribisha tuyatafakari maneno ya uzima ya Bwana wetu.
Leo nataka tujifunze asili ya ushujaa wa rohoni, ambao wakati mwingine tunadhani mpaka tuwe na uzoefu ndio tuweze kufanya makuu kwa Mungu. Wakati Fulani Taifa la Israeli liliingia katika hali mbaya ya njaa isiyokuwa ya kawaida, mpaka kufikia hatua ya baadhi ya watu kuchinja watoto wao na kuwala (2Wafalme 6:28-29), Na hiyo ilikuwa ni kwasababu ya kuzungukwa na maadui zao wenye nguvu kwa muda mrefu walioitwa washami. Hivyo wakashindwa kuingiza au kutoa chochote ndani ya mji kwa muda usiokuwa mchache.
Hivyo hali ikiwa mbaya sana, mfalme akafunga mji, hawajui cha kufanya, watu wamepaniki, wanakula vitu visivyopaswa kulikwa, kiasi kwamba hata ‘mavi ya njiwa’ tu yalikuwa yanauzwa kama chakula. Tengeneza picha taifa kubwa kama hilo, linakumbwa na janga la njaa kali namna hiyo, hadi askari wake wazoefu wa vita, wanatetemeka na kujificha ndani ya mji, kwasababu walijua wakitoka tu ni kifo.
Na ndicho maadui zao walichokuwa wanakisubiria kwao, aidha watoke wawaue, au wafe na njaa ndani. Hivyo hali ilikuwa ni ya kutisha sana. Lakini tunaona siku moja Nabii Elisha, akapewa unabii na Mungu, na kuambiwa kuwa chakula kitapatikana na kuuzwa kwa bei ya chini kiasi ambacho hakijawahi kuuzwa hapo kabla siku ya kesho yake, ni sawa na uambiwe siku ya kesho, gunia la mahindi, linauzwa kwa Tsh1, wakati unatambua kuwa halipungui wastani wa bei ya Tsh,70,000. Ndivyo ilivyokuwa kwa Israeli, Mungu alipompa Elisha unabii huo akaambiwa siku ya kesho yake, chakula kitauzwa kwa bei ile.
Sasa kulikuwa na wakoma wanne(4), waliokuwa nje ya mji, wakoma hawa walitengwa na taifa, kwasababu ilikuwa ni kuwa watu walioathirika na ugonjwa huu watengwe mbali na makazi ya watu wao wasije kuleta maafa hayo ndani ya jamii, ni sawa na ugonjwa wa Ebola tunavyouona sasa, ndivyo ilivyokuwa ukoma kwa wakati ule.
Tengeneza picha watu hawa walikuwa ni wagonjwa, hawana wa kuwatazama, na zaidi sana wamekuwa dhaifu kwa njaa kali. Lakini tunaona walishauriana jambo kisha wakafanya maamuzi, ambao ndio ulikuwa ukombozi wa taifa la Israeli; Tusome hapo;
2Wafalme 7:1 Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.
2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula
3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?
4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu.
5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu.
6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.
7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao.
8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.
9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme.
10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
11 Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.
Ni nini kimejificha hapa?
Siri nayotaka uone ambayo imejificha nyuma ya hawa wakoma wanne, ni kwamba, pindi tu walipoamua kufanya uamuzi, wa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha yao, na kuanza mwendo, kuelekea kambi ya maadui, kumbe kule kwenye kambi ya washami, wanasikia kama JESHI kubwa sana la maaskari linawafuata. Hivyo wakakimbia kwa kasi sana, na kuacha kila kitu nyuma. Lakini wale maaskari wa kiisraeli waliokuwa wazoefu wakati huo wamejifungia ndani ya mji hawadhubutu kuchukua hatua..
Watu waliokuwa dhaifu na wagonjwa, ndio waliowafukuza washami na kuleta ukombozi Israeli. Watu wanne tu, waligeuka kuwa jeshi la maaskari elfu rohoni.
Hiyo ni kutufundisha nini?
Na sisi pia pale tunapoamua kufanya jambo kwa ajili ya Mungu, bila kujali hali zetu au udhaifu wetu, tufahamu kuwa jeshi la shetani linaogopa na kutetemeka kushinda hata sisi tunavyoweza kudhani. Daudi alijijua kuwa yeye si mtu wa vita, hajazoea vita, hawezi kutumia upanga wala mkuki, lakini yeye ndiye aliyesimama, kinyume na Goliathi, na kulifukuza jeshi lake lote.
Hivyo, hupaswi kujidharau, ikiwa umeokoka leo, au jana, usiseme mimi sina uzoefu, au sijui biblia vizuri, kama kushuhudia watu wenye dhambi ambao wengine wameshindwa, wewe nenda, usisubiri mpaka mchungaji wako afanye hivyo, hujui kuwa wakati huo ndio Mungu kakuchagua kuwa sababu ya ukombozi kwa wengine.
Hivyo, popote unapojiona hukidhi vigezo, fahamu kuwa rohoni ndio unakidhi. Unajiona hustahili, jua tu kwa Mungu unastahili, kuwa na imani, chukua hatua, usingoje ngoje. Tumia karama uliyopewa ndani yako kuujenga ufalme wa Mungu. Popote pale unapojiona unafaa, basi tumia nafasi hiyo kumtangaza Kristo kwa wengine. Na hakika rohoni shetani atatoweka kama jeshi la washami.
Bwana akubariki.
Shalom.
Je, umeokoka? Kama bado basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo huo wa kumwalika Yesu maishani mwako.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Hazina za gizani ni zipi? (Isaya 45:3).
BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
Karibu tujifunze biblia.
Leo tutajifunza moja ya taratibu illiyokuwa inaendelea katika Hekalu la Mungu ambayo haikuwa inampendeza Mungu.
Tusome,
Marko 11:15 “Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa;
16 WALA HAKUACHA MTU ACHUKUE CHOMBO KATI YA HEKALU”.
Maandiko haya ni maarufu tunapoyasoma husuani mahali hapo Bwana alipowafukuza waliokuwa wanauza njiwa na waliokuwa wanabadili fedha.
Lakini tukizidi kujifunza, tutaona sio kundi hilo tu Bwana alilolifukuza na kuliadhibu. Bali kulikuwa na kundi lingine pia ambalo lilikuwa linapandisha harufu mbaya mbele za Mungu. Na kundi hilo ni lile la watu waliokuwa WANACHUKUA CHOMBO NDANI YA HEKALU.
Sasa kuchukua Chombo kunakozungumziwa hapo si “KUIBA VYOMBO VYA HEKALUNI au KUHAMISHA CHOMBO NDANI YA HEKALU” Hapana! Bali ni KUPITA au KUKATISHA na Chombo ndani ya Hekalu, Na chombo ni kitu chochote cha kubebea bidhaa au kurahisisha kazi kama makapu, au matenga au baiskeli.
Sasa mahali hekalu lilipojengwa lilikuwa linatengenisha sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni Bethsaida (mahali palipokuwa na soko kubwa la kondoo) na Sehemu ya juu ya “Mji wa juu”. Hivyo watu waliotoka Mjini kuelekea Bethsaida sokoni walianza tabia ya kukatiza katika ukumbi wa hekalu kama njia ya mkato (shortcut) ya wao kufika Bethsaida.
Kwahiyo kulikuwa na kundi kubwa la watu wanaokatiza pale wakiwa na vyombo vyao kila siku, Kwaufupi paligeuzwa kuwa njia, mtu yeyote alipita, wezi walikatiza, wahuni walipita, wasengenyaji walikatiza na stori zao za kuwasema wengine, waliotaka kwenda sokoni kuweka vimeza vya Kamari walikatiza kila siku na meza zao, matapeli ndio shortcut yao hiyo n.k
Tabia ambayo Bwana Yesu hakupendezwa nayo!. Hivyo akasimama pia katika maingilio na matokeo ya Hekalu akawazuia wote waliokuwa wanakatiza!.. Huenda pia nao walitandikwa na kile kikoto!!.
Sasa tabia kama hiyo pia inaendelea katika nyumba za Mungu leo (Makanisani), utakuta kuna miingiliano ya watu wanaokatiza katiza na wanaozunguka zunguka!, wasio na fikra habari na mambo ya kiMungu… Wengi wa hao hawapiti kwa lengo la kumsogelea Mungu bali kwasababu ya shughuli zao, na biashara zao na ajenda zao, wanaouza chakula wanaingia wanavyotaka, wanaouza viatu wanaingia wanavyotaka, watoto wanaotaka kucheza kutoka huko nje basi eneo la kanisa ndio ukumbi wao n.k.. ni muhimu kuwa makini sana!!
Ni lazima, kuifanya Nyumba ya Mungu kuwa nyumba ya Mungu… kama tu sisi hatupendi watu wakatize kwenye maeneo ya Nyumba zetu, tena tunawaza wakati mwingine tuzungushe uzio vipi kwa Mungu??. Kama tu sisi tunapenda watu waziheshimu nyumba zetu vipi kwa Mungu?..
Na pia nyumba ya Mungu si jengo tu bali pia miili yetu, maandiko yanasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu (1Wakorintho 3:16, na 1Wakorintho 6:19). Ikiwa na maana kuwa pia miili yetu sio NJIA YA KILA MTU KUKATIZA!!!!.. (Maana yake si chombo cha zinaa wala kuchezewa).
1Wakorintho 6:15 “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”.
Itunze na kuiheshimu nyumba ya Mungu (Mwili wako mwenyewe pamoja na Jengo unalokusanyikia).
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NI NANI ALIYEKUPA MAMLAKA HII UYATENDE HAYA?
TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?
Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?
Ni nani aliyemshawishi Daudi akawahesabu Israeli? Ni Mungu au shetani?
Hii ni Orodha ya Mitume 12 wa Bwana YESU.
Orodha hii inapatika katika Kitabu cha Mathayo 10:2-4, na kitabu cha Marko 3:18, na Luka 6:13-16.
Katika Vitabu hivyo panaonekana Mitume kutajwa kwa jina Zaidi ya Moja katika injili nyingine, kwamfano Mtume aliyeitwa Thadayo (Mathayo 10:3), kitabu cha Luka 6:16 anaonekana akitajwa kama “Yuda wa Yakobo”, Hiyo ni kuonyesha kuwa Mtume huyo alikuwa anajulikana kwa jina Zaidi ya moja. Vile vile Mtume anayeonekana kuitwa Nathanaeli katika Yohana 1:45 ndio huyo huyo anayekuja kuoenakana akiitwa kwa jina la Bartholomeo katika Mathayo 10:3.
Lakini pia baada ya Yuda kumsaliti Bwana na kwenda kujinyonga, maandiko yanaonyesha kuwa Mtu aliyeitwa Mathiya alichukua nafasi yake na kuhesabiwa miongoni mwa mitume 11 wa Bwana Yesu.
Matendo 1:26 “Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja”.
Hiyo ndiyo Orodha ya Mitume 12 wa Bwana Yesu Kristo, ambao Bwana aliwaweka kuwa kama Mashahidi wa kufufuka kwake (Matendo 10:39-42 na Matendo 1:22), na baada ya hawa Bwana alinyanyua mitume wengine mfano wa hawa, ambao miongoni mwao alikuwa Mtume Paulo.
Na Mitume wanatajwa katika Agano jipya tu na wao ndio walioweka msingi wa Imani kwa kanisa, katika Agano la kale walioweka msingi wa kumjua Mungu kama Yehova ni Manabii, hivyo kwa muunganiko wa Mafunuo waliopewa Mitume wa agano jipya na Manabii wa agano la kale, kanisa la Kristo linajegwa juu ya Msingi wao.
Waefeso 2:20 “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”.
Je unajua jinsi Bwana alivyowachagua Mitume wake? na ni kigezo gani alikitumia?.. kufahamu zaidi fungua hapa >>JINSI BWANA ALIVYOWACHAGUA MITUME WAKE.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)
Orodha ya mistari ya biblia kuhusu watoto
ORODHA YA IMANI POTOFU- Sehemu ya 1
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu. (Zab. 119:105).
Kuna tofauti ya Msamaha wa dhambi na Ondoleo la dhambi.
Mtu anapokukosea labda amekutukana au kukuibia na akikuomba msamaha unaweza kumsamahe (ukamwachilia kabisa moyoni mwako) lakini kumsamehe kwako hakumfanyi yeye kuacha ile tabia.. Maana yake ni kwamba kama ile tabia haitaondoka ndani ya huyo mtu basi ni wazi kuwa atarudia lile kosa siku nyingine. Atapumzika siku mbili au tatu na baadaye atarudia lile kosa. Sasa mtu kama huyu kapata msahama lakini si ondoleo la ile tabia.
Vile vile kwa Mungu tunaweza kupata msamaha wa makosa yetu na dhambi zetu, lakini kama hatutapata Ondoloe la dhambi hizo (Maana yake kama ule mzizi wa dhambi ndani yetu hautang’olewa) basi tutabaki vile vile, kila mara tutarudia makosa yale yale. Na mzizi wa dhambi ni lazima uondoke maishani mwetu kwasababu ndicho kitu kilichomleta Bwana Yesu duniani.
Bwana Yesu hakuja tu kuleta msamaha wa dhambi bali pia ondoleo la dhambi..Kwasababu msamaha wa dhambi ulikuwepo hata kabla ya Bwana Yesu kuja duniani, watu waliomba msamaha mbele za Mungu na wakasamehewa makosa yao, lakini Ondoleo la dhambi halikuwepo, Dhambi hazikuondolewa katika kumbukumbu za Mungu (zilifunikwa tu) na vile vile hazikuondolewa ndani ya mtu, bado watu waliendelea kurudia makosa yale yale, baada ya Bwana Yesu kuja watu ndipo wakapata ondoleo la dhambi, ndani yao (utumwa wa dhambi ukakoma kwa wale wote waliompokea).
Sasa tunapataje ondoleo la dhambi?.. kiasi kwamba dhambi haitupelekeshi tena wala kututawala?
Kwanza ni kwa kutubu mbele za Mungu, na kukiri kwamba sisi ni wakosaji, (hapa unatubia makosa yako yote ambayo umeyafanya kwa kujua, na kwa kutokujua mbele za Mungu, kwa tendo hilo Bwana atakusamehe ikiwa toba hiyo imetoka kweli ndani ya moyo na kwamba umekusudia kubadilika kabisa..)
Sasa hatua inayofuata ili Dhambi zako ziondolewe (ule mzizi wa dhambi ndani yako uondoke) baada ya kutubu ni wewe kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi… Hiki ni kipengele cha muhimu sana ambacho si cha kupuuzia hata kidogo..
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU”
Ubatizo sahihi unakamilisha toba na hivyo mtu anayefanya hayo Mungu anampa zawadi ya Roho Mtakatifu pamoja na Ondoleo la dhambi, jambo ambalo ni muhimu sana.
Mtu huyu kama toba yake imetoka ndani ya moyo kabisa basi ule uzinzi uliokuwa unamsumbua mara kwa mara unakufa, anajikuta anaushinda uasherati na haurudii tena, kwasababu dhambi imeondolewa ndani yake, zile tabia zilizokuwa zinamwendesha mara kwa mara zinaondoka ndani yake kwasababu ule mzizi wa dhambi umeondolewa ndani yake n.k n.K
Na kumbuka ni muhimu sana kubatizwa ubatizo ulio sahihi, kwasababu si kila batizo zinaondoa dhambi.. nyingine utabatizwa lakini utabaki vile vile. Na ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la Bwana Yesu Kristo (Matendo 19:10)!.
Je unataka usiendelee kuwa mtumwa wa dhambi?.. Tumia kanuni hiyo ya Matendo 2:27-37. Na Mungu ni mwaminifu atafanya sawasawa na Neno lake.
Maran atha.
Ikiwa hujabatizwa bado na unahitaji msaada wa kupata ubatizo sahihi, basi waweza kuwasiliana nasi kwa namba zetu na tutakusaidia kwa hilo.
Shalom
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.
Wagalatia 6:1 ‘Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’.
JIBU: Hapa biblia inatupa mwongozo sahihi wa jinsi ya kuwavuta upya ndugu ambao walianguka katika dhambi.
Tunafundishwa tuwarejeshe katika Roho ya upole, maana yake sio ya kulaumu au ya ukali. Kwamfano utakuta mtu karudi nyuma katika ulevi wake aliokuwa nao mwanzoni. hapo yakupasa utumie busara kumrejesha upya ili iwe rahisi tena mtu huyo kugeuka na kutubu, kuliko kutumia ukali mfano kumkaripia au vinginevyo. Ukitumia kauli za lawama au mashtumu, si rahisi kumvuta, kinyume chake zitamfanya achukie zaidi au akasirike.
Lakini pia sehemu ya pili anasema..ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
. Maana yake ni kwamba hata wewe mwenyewe Unaweza ukajaribiwa na shetani uwapo katika kazi hii ya kuwavuta wengine waliokengeuka katika wokovu. Kwamfano huyo mlevi anaweza akakutukana, halafu wewe ukakasirika, ukaanza kurejesha lugha za matusi kwake kwasababu ya hasira, hapo tayari umeshaanguka katika dhambi.
Baadhi ya watu wa Mungu wamejaribiwa na kuanguka katika uzinzi walipokuwa wanafanya huduma Kwa watu walio wa jinsia tofauti na wao. Wengine katika anasa waliposhirikiana na watu wa kidunia waliowashuhudia habari za Yesu.
Hivyo tunapaswa tujichunge nafsi zetu sana tuwapo katika kuipeleka habari njema kwa makundi ya watu tofauti tofauti. Kwasababu na sisi pia shetani anatuwinda. Lakini Tukiwa watu wa maombi na kuliishi Neno tutajilinda sana nafsi zetu na mitego hiyo ya shetani. Ndio maana ya hilo Neno ‘ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Wapelelezi wa uhuru wa wakristo ni watu gani (Wagalatia 2:4)?
Waliouawa Shitimu kwa pigo walikuwa ni watu Elfu 23 au elfu 24?.
Hizi ni dalili 9 za mtu mwenye pepo.
1.Hofu.
Ukiona kuna hofu ndani yako isiyoisha, kila wakati unaishi katika hali ya wasiwasi wa kitu usichokijua wala usichokiona, kila wakati unapata mshtuko na mkandamizo mkubwa wa mawazo, furaha inakuwa haidumu ndani yako, dakika yoyote unaona au unahisi kama utapoteza maisha..hizo ni roho chafu za mapepo zimekuingia, hivyo tafuta msaada wa maombezi haraka sana.
Warumi 8:15 “Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba”.
2. Ndoto zinazojirudia rudia.
Ukiona unaota Ndoto zinazojirudia rudia, ndani ya kipindi kifupi… na zote zina maudhui ya kishetani ikiwemo vifo, uzinzi, mauaji, au vitisho. Tafuta msaada wa maombezi.
3. Sauti.
Ikiwa unasikia sauti zinakuita jina lako au zinakupa taarifa Fulani au maagizo fulani na zinajirudia mara kwa mara, (tofauti na ukiwa katika mazingira ya kusali au katika nyumba ya ibada), Tafuta msaada wa maombezi.
4. Kiburi
Ukiona una kiburi kilichopitiliza kilichoshuhudiwa na watu wengi pamoja na chuki nyingi na vinyongo na hasira zilizopitiliza, hiyo sio hali ya kawaida…katafute msaada wa maombezi haraka sana.
5. Nguvu za Ajabu
Ukiona una nguvu za ajabu katika mwili wako, ambazo chanzo chake hukielewi katafute msaada wa maombezi.
6. Kufanya vitu pasipo kujitambua
Ukiona unafanya vitu pasipo kujitambua, (pasipo kuwa na habari)… baada ya muda kupita ndio unakuja kuambiwa kuwa ulifanya hiki au kile, au wewe mwenyewe ndio unakuja kugundua ulifanya hiko kitu pasipo kujitambua.. Katafute msaada wa maombezi.
7. Tabia chafu
Ukiona unaendeshwa na tabia chafu usiyoweza kujizuia, tafuta msaada wa maombezi.
8. Magonjwa yasiyoeleweka
Ukiona unapata ugonjwa au magonjwa yanayoonyesha tabia zisizo za kawaida, (maana yake yana badilika badilika), leo utaumwa hiki kesho kingine tofauti kabisa na cha jana, tafuta msaada wa maombezi..
9. Hamu ya kusoma Neno na kufanya Maombi
Ukiona Hamu ya kusoma Neno na kufanya maombi imepungua ndani yako kwa kiwango kikubwa, tafuta msaada wa maombezi.
Kumbuka!…Mtu mwenye pepo ndani yake kamwe hawezi kumtumikia Mungu, kwani roho hizo siku zote zinapingana na roho wa Mungu. Mtu anaweza kweli kutamani kumtumikia Mungu, lakini roho hizo zitamvunja moyo na kupingana naye na kumtesa na kumletea kukata tamaa na mateso. Hivyo ni lazima zitoke kwanza na kuwa huru ndipo aweze kumtumikia Mungu.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TABIA KUU TATU ZA WAHUBIRI WALIORUDI NYUMA NA KUMWACHA MUNGU.
KWANINI MITUME WAMUULIZE BWANA FARAGHANI?
KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.
BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
SWALI: Katika ule mlima mrefu, aliopanda Yesu na wanafunzi wake kuomba, kwanini atokewe na Musa na Eliya na sio manabii wengine? Mfano wa Isaya au Samweli?
JIBU: Awali ya yote yeye kutokewa na wale watu halikuwa Kwa lengo lake. Bali Kwa lengo la wale wanafunzi aliokuwa nao, Ili kutimizi mambo yafuatayo.
a) Unabii wa kwanza ni ule alioutoa Musa kuwa atakuja Nabii mwingine kama yeye na kwamba watu wamsikilize..
Kumbukumbu la Torati 18:15
[15]BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.
Soma pia Matendo 3:22-25,. Hivyo wayahudi walikuwa na matarajio ya kuona mtu anayefanana na Musa atakayeleta Sheria mpya akija duniani, lakini akiwa na nguvu na uweza mwingi mfano wa Musa..
Ndio sababu ya Musa kutokea mbele ya wanafunzi wake, ili Mungu awathibitishie huyu ndio yule Musa aliyemnenea habari zake.
b) Lakini pia unabii uliohusu kutangulia Kwa Eliya kabla ya Kuja kwake duniani.
Wanafunzi walikuwa na dukuduku kama huyu, ndiye Kristo aliyetabiriwa au sio, na kama ndio mbona Eliya hajatangulia mbele yake tukamwona? Kwasababu waliambiwa hivyo na waandishi. Lakini sasa walipomwona Eliya mwenyewe amesimama mbele ya Yesu wakaamini lakini bado hawakuelewa..Sasa walipokuwa wanashuka ndio wakapata nguvu ya kumuulizia hilo swali.. Na hili ndio likawa jibu lake.
Mathayo 17:9-13
[9]Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.
[10]Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
[11]Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote,
[12]ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
[13]Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.
Utakumbuka kabla ya kupanda mlimani aliwaliza watu kuwa wanamzungumzia kuwa yeye ni nani? Wanafunzi wakamjibu kuwa wanasema yeye ni Eliya, wengine mmojawapo wa manabii wa Kale.n.k. Hivyo kulikuwa na utata mwingi. Lakini siku hiyo alitoa utata huo Soma.Mathayo 16:13-18.
Mitume walipoona sura za manabii wao wa kale wamesimama mbele ya Yesu, mwenye utukufu mwingi sana kupitia wao. Wakaamini yeye ni zaidi ya manabii wote wakubwa Kwa wadogo waliowahi kutokea katika historia.
Musa alikufa, lakini Eliya alipaa.
Yesu ndio mtu pekee miongoni mwa wanadamu, aliyekufa, Kisha akazikwa, kisha akafufuka.na mwisho akapaa. Kwa hiyo Ile ilikuwa ni lugha ya kinabii, kueleza hatma yake na ndio maana hata manabii Hao walikuwa wakizungumza mambo yahusuyo kufa kwake na kufufuka.(Luka 9:31).
Hizo ndio zilikuwa sababu kuu za Bwana kutokewa na manabii wale wawili na sio wengine. Na walipokuwa wanashuka Akawaambia wanafunzi wake wasimwambie mtu mpaka atakapofufuka katika wafu.
Kufunua nini?
SI wote watamwona Yesu katika kilele Cha utukufu wake, isipokuwa wale tu walio na kiu na yeye. Ambao watakuwa tayari kuwa karibu naye wakati wote mfano wa Hawa wanafunzi watatu yaani Yohana, Petro na Yakobo.
Ukimpenda Yesu tumia muda mwingi kuwepo uweponi mwake. Utamjua sana Kwa mapana na marefu yake.
Je! Umeokoka? Je unatambua kuwa hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi? Dalili zote zimeshatimia, unasubiri nini usimpe Bwana maisha yako, embu fanya uamuzi leo. Tubu dhambi zako, mgeukie Yesu, Unyakuo usikupite. Ikiwa utapenda upate mwongozo huo, wasiliana nasi kwa namba zetu hizi bure +255693036618 /+255789001312
Shalom
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha;
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
Jina la Bwana Yesu litukuzwe Daima. Nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya Mungu.
Lipo andiko ambalo tunaweza kuona ni la kinyonge lakini linatiba kubwa sana kama tukilitumia. Embu tuone ni nini mwandishi huyu mwenye hekima aliomba Kwa Bwana
Mithali 30:7-9
[7]Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa. [8]Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. [9]Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
Nataka uone hapo aliposema..
“Usinipe umaskini wala utajiri;”
Katika maombi yetu ni rahisi sana kumwomba Mungu asitupe Umaskini, lakini ni ngumu sana kumwomba Mungu asitupe “UTAJIRI”.. Nadhani huo ndio ukweli..
Utajiri ni Ile Hali ya kuwa na uwezo wa kumiliki au kuwa na vitu vingi.
Lakini huyu mtu hapa anamwekea Mungu mipaka katika maeneo hayo mawili, yaani Utajiri na Umaskini, Kwa lugha nyingine anamwambia Mungu sitaki UTAJIRI.. na sababu anaitoa pale “Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, BWANA ni nani?”
Alijua Kuna madhara ya kuwa na tamaa ya kutaka vitu vingi, mfano kuwa na mabilioni ya pesa kwenye akaunti, kuwa na mahekari ya mashamba mengi, kuwa na nyumba nyingi za kuishi na za kupanga, kuwa na magari mengi n.k. Alijua hayo ni matamanio ya Kila mwanadamu lakini alikataa kuyaomba kabisa.
Lakini Watu wengi tunaposoma huu mstari tunaelekeza mawazo yetu kwenye mambo ya Mali tu. Lakini Bwana anamaanisha pia utajiri wa kiroho.
Uchu huu wa kupata Kila kitu, kuwa na Kila kitu, umewavaa watu wengi hata watumishi wa Mungu. Labda utaona anakwenda mbele za Mungu, maombi yake na matazamio yake ni kuwa na upako kuliko watu wote, anachotaka ni Mungu ampe karama zote za Roho. Yeye naye awe Nabii, awe Mchungaji, awe mwinjilisti, awe mwalimu, awe mtume, awe na karama zote 9 za Roho. Yaani atakaposimama mimbarani watu wamwone yeye ni kama Yesu. Awe mhubiri wa Dunia nzima wa kimataifa, mwenye mafunuo mengi kuliko wote duniani, mwenye kanisa kubwa kuliko yote duniani.
Maombi ya namna hii ni maombi ya utajiri. Na mara nyingi tunapoomba hivi Bwana Huwa hatupi, kwasababu si mapenzi ya Mungu kuomba vitu vilivyo zaidi ya uwezo wetu alivyotukirimia. Kila mmoja kawekewa kipimo chake na Mungu. Na katika hicho ndio tunaomba Mungu akibariki. Lakini si kila huduma Kila karama itakuwa ni yako.
1 Wakorintho 12:28-30
[28]Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
[29]Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza?
[30]Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?
Hivyo pale tunapokuwa na Nia ya kiasi, ndipo Mungu anapotuongezea neema, na ndio tutakapomtumikia Mungu vizuri. Hekima inatufundisha tubadilishe matamanio. Yetu kutoka katika UCHU, mpaka “kutosheka na mishahara yetu”. Na hivyo tutafanya vizuri zaidi katika huduma, karama, na utumishi wetu Kwa ujumla. Watu watasaidika na kile ulichonacho sasa, kuliko kile usichokuwa nacho unakingoja.
Nabii Eliya ambaye alikuwa ni mkuu Kwa nguvu za Mungu, lakini pamoja na hayo hata katika maombi yake alisema “Mimi SI mwema kuliko Baba zangu (1Wafalme 19:4)”akataka Bwana asitishe huduma yake. Kwasababu aliona kama kipimo kile hakustahili kupimiwa.. Hakuwa na uchu wa kiroho. Si ajabu Kwanini Mungu akamtumia Kwa viwango vikubwa namna Ile.
Bwana atusaidie tuonyeshe sasa bidii katika nafasi zetu alizotukirimia leo, zaidi vile ambavyo tunavitazamia kesho. Tutumike Kwa kadiri ya alivyotujalia.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?
Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)
Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?
Je unajua kuwa kama utii wako haujatimia mbele za Mungu, kuna mambo utashindwa kuyafanya?? Kama utiifu wako kwake ni mdogo basi upo hatarini sana, Kama ulikuwa hulijui hili, basi ni vizuri ukalijua leo.
Hebu tusome maandiko yafuatayo..
2Wakorintho 10:3 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, KUTII KWENU KUTAKAPOTIMIA”
Hapo mwishoni anamalizia kwa kusema “KUTII KWENU KUTAKAPOTIMIA”. Ni wengi wanalisoma hili andiko lakini hawafiki hapo mwisho, au hata wakifika hapo mwisho basi hawatafakari vizuri maana ya maneno hayo “Kutii kwenu kutakapotimia”.
Maana yake ni kwamba kama kutii kwako mbele za Mungu hakujatimia basi HUTAWEZA KUANGUSHA NGOME, hutaweza KUANGUSHA MAWAZO YALIYOINUKA juu yako na juu ya maisha yako na familia yako na shughuli zako… kama kutii kwako hakujatimia mbele za Mungu vile vile HUTAWEZA KUTEKA NYARA, wala hutaweza KUPATILIZA MAASI yoyote yaliyoinuka kinyume chako… Kwaufupi hutaweza kabisa kushindana vita vya kiroho!!..utaishia kusumbuliwa tu na shetani na wanadamu.
Mungu anapenda UTII, Na Utii una nguvu nyingi.. Kwa jinsi tunavyoongeza viwango vyetu vya kumtii Mungu ndivyo NGUVU ZETU ZA KIROHO ZINAVYOONGEZEKA.. Na hivyo tunakuwa na uwezo mkubwa wa kumshinda Adui na hila zake na njama zake.
Lakini leo hii kama Mungu anakuambia uache dhambi hutaki kumtii unategemea vipi Uwe na Nguvu za kuangusha Ngome ndani yako?, kama Ukiambiwa ukabatizwe hutaki kutii unategemea vipi uweze kuangusha ngome za mizimu ya ukoo wenu na mababu?.
Kama unaambiwa tu uache kuvaa mavazi hayo yasiyokupasa hutaki kutii, unategemea vipi hayo maradhi ya muda mrefu na hizo shida zikuondoke????.. Kama tu kumtii Mungu ni shida utawezaje kutiisha fikra nyingine imtii Kristo? Sawasawa na hilo andiko??.
Mtii Mungu kwanza ndipo uwe na nguvu za kuwafanya wengine wamtii Kristo…Ukikosa utii kwa Mungu ndivyo unavyojimaliza mwenyewe…
Na si kumtii Mungu leo na kesho kuendelea na mambo mengine… Hapana! Bali biblia inatufundisha kuwa utii wetu unapaswa uwe endelevu ndipo tufikie kiwango cha “kutimia” kule biblia unakokusema, ndipo matokeo yatakapoonekana.
Yakobo 4:7 “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 4.8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili”.
Je umeitii Injili?, Je umeitii kazi ya Mungu na maagizo yake yote?
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Ngome ni nini? Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?
Utii ni nini? na ni nani tunayepaswa kumtii au kutokumtii?
Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.
Je! Moyo wako upo kweli kwake?
Kuna kauli Bwana Yesu alisema kuhusiana na watu kumwelewa Mungu na uweza wake kwetu, alisema..
Mathayo 13:14 “Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. 15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, WAKAELEWA KWA MIOYO YAO, WAKAONGOKA, NIKAWAPONYA”
Ametaja mambo makuu matatu,
Hatua ya mwisho ambayo Mungu anatarajia, pindi anapomfundisha mtu, au kusema naye ni KUELEWA. Hivyo ataanza kwanza kwa kumwonyesha mambo kadha wa kadha, yatapita mbele yake, ataanza kusema na yeye kwa njia nyingi, aidha kwa wahubiri wake, au ndoto, au maono, au vitu vya asili, au kwa Neno lake, au kwa maisha yake mwenyewe.. Lakini pamoja na njia zote hizo bado mtu huyo anaweza asimwelewe Mungu, kama Moyo wako haupo kwake.
Jambo ambalo watu wengi hatujui, ni kwamba Mungu anazungumza na kila mmoja, Na kila mmoja anaonyeshwa maono mengi na Mungu, kila mtu ameshakutana na Mungu, aidha uso kwa uso au katika roho, haijalishi ni mwema au mwenye dhambi, Lakini ni wachache sana walioweza kuielewa sauti yake iliposema nao.
Ni kwasababu gani hawaielewi? Ni kwasababu inahitaji MOYO ili kuielewa, Na sio macho au sikio. Kama moyo wako haupo kwake, sahau kumwelewa Mungu anaposema na wewe kwa njia yoyote ile. Hata kama itakuja kwa dhahiri, bado hutamwelewa. Sauti yake kwako itakuwa ni ngurumo tu, kama ilivyokuwa kipindi kile Bwana Yesu alipokuwa anazungumza na makutano kuhusiana na ufalme wa mbinguni.
Yohana 12:28 “Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. 29 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu”
Ni kwanini iwe hivyo kwao? Ni kwasababu kilichowapeleka kwa Yesu sio wokovu wa Roho zao, au upendo wao kwa Mungu, kilichowapeleka kwake, ni miujiza, uponyaji, uzuri, mwonekano, mazingira, basi, hakuna jipya. Wakishapata walichokuwa wanakitafuta hao wanaondoka zao kuendelea na mambo yao ya dhambi ya sikuzote.
Ndio maana hakukuwa na hata mmoja ambaye aliyeelewa mifano yote Yesu aliyokuwa anaisema mbele ya umati. Isipokuwa wanafunzi wake tu, pamoja na wachache waliomfuata baada ya pale kutaka kufafanuliwa.
Ndugu ikiwa leo unakwenda kanisani kutimiza tu ratiba, kutazama kwaya, kuangalia watu wamevaaje, hata ukiwepo humo unasinzia, unaangalia muda utatoka saa ngapi, ni kweli utakutana na Mungu, atasema na wewe, utamwona, utahisi uwepo wake, utanena hata kwa lugha, utasisimka moyo. Lakini kumwelewa, haitakaa iwezekane. Kwasababu Mungu hajifunui kwa watu ambao mioyo yao haipo kwake.Hana utaratibu huo.
Na sio tu kanisani, hata mahali popote pale, iwe ni shuleni, kazini, nyumbani, barabarani, Mungu huwa anazungumza, anasema kwa njia mbalimbali tena kirahisi sana, Lakini hutaelewa ikiwa huna moyo wa dhati kwa Mungu wako.
Alisema hivi;;
2Nyakati 16:9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, WALIOKAMILIKA MOYO KUELEKEA KWAKE…”
Alisema pia..
Mathayo 15:7 “Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, 8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami”.
Yatupasa sasa tuondoe unafiki wa ndani, kwa kumaanisha kweli kweli kumpenda Mungu kwa moyo, ili sasa aanze kutufunulia sauti yake na kazi zake. Tukimfuata Kristo tujue kinachotupeleka kule ni Utakatifu na haki, na sio kwasababu tunashida tutimiziwe mahitaji yetu, hapo ndipo atapendezwa na sisi, na hatimaye, tutamwona kila inapoitwa leo.
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?
NIFANYE NINI ILI NIKUBALIWE NA YESU?