SWALI: Naomba kufahamu kwanini mafuta yaliendelea kutumika wakati Yesu tayari alikuwa ameshakuja duniani?
Marko 6:12 “ Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. 13 Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza”
JIBU: Ndio, Bwana Yesu alikuwa na kanuni nyingi za kuwaponya watu, kuna wakati alitamka tu na mtu akapokea uponyaje wake, utakumbuka habari ya Yule mtu aliyepooza alimwambia jitwike kitanda chako uende nyumbani(Marko 2:1-9), vilevile kuna wakati alimgusa kwanza mgonjwa, kisha akaponywa, utamkumbuka Yule mkoma, aliyemfuata na kumpigia magoti kumwomba amponye, maandiko yanasema akamgusa na kusema nataka takasika,(Marko 1:40-42). Vilevile Kuna wakati alitoa tu agizo la kutekelezwa na katikati ya agizo hilo, mtu anapokea uponyaji wake, ile habari ya wale wakoma 10, inatuthibitishia hilo,(Luka 11:17-19) na kuna wakati alitumia visaidizi, kama udongo, mate, kama ishara ya nje, ya mtu Yule kupokea uponyaji wake. Ukisoma habari ya Yule mtu ambaye alikuwa kipofu tangu kuzaliwa utali hakiki hilo nalo (Yohana 9:6).
Na hapa ndivyo ilivyokuwa aliwapa maagizo wanafunzi wake, Pale alipowaita na kuwatuma kwenda kuhubiri injili Ukisoma kuanzia mstari wa 7, Utaona aliwapa maagizo hayo ya kutoa pepo, na bila shaka na ya kuwapaka mafuta wote waliokuwa wagonjwa kwa jina lake.
Lakini hiyo haikuwa staili, kwamba kila mahali watakapokwenda wawe na chupa za mafuta, au maji, au udongo au chochote.
Hata sasa, hatupaswi kudhani Bwana hawezi kutuagiza tutumie kitu chochote cha asili kama ishara ya nje ya kuachilia uponyaji wake. La! Tusifikiri hivyo, Lakini hilo halipaswi lifanyike mara zote, au kama staili, kama inavyofanywa sasa, watu hawahubiri tena Neno la Mungu, kinachopigiwa kampeni ni mafuta na maji ya upako. Lakini mitume hawakufanya hivyo, ukisoma mstari wa 12, hapo anasema “Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu”. Umeona, Walijua jukumu lao kubwa ni kuwahubiria kwanza watu habari za dhambi zao. Na katika huduma hayo mengine yanafuata tena kwa uongozo wa Roho Mtakatifu.
Ni jambo linalosikitisha sasa, Jina la Yesu halitumiwi tena, shetani ameingilia eneo hili na kulivuruga, watu wakidhani hiyo ndio kanuni ya Mungu iliyobora ya watu kupokea uponyaji, wamemgeuza kama mganga wa kienyeji ambaye yeye kazi yake ni kutoa tu miti-shamba lakini hajali hali ya mtu ya kiroho.
Wengine wanakimbilia lile andiko la Yakobo ambalo linasema,
Yakobo 5:14 “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa”
Wanasahau kuwa kilichotangulia ni kuombewa kwanza..kuungamanishwa dhambi zake, kupatanishwa na Mungu, kisha ndio mafuta yafuate, kwa jina(agizo) la Bwana.
Tukikariri kwamba wakati wote tunapaswa tutumie chumvi kisa Elisha aliagizwa atupe chumvi kwenye chemchemi ya maji ili aondoe mapooza(2Wafalme 2:19-22), basi tukariri pia kitendo cha kulala juu ya maiti, kila tunapowaombea wafu ili wafufuke, kwasababu Elisha naye alifanya kitendo kama hicho(2Wafalme 4:32-34). Unaona, tutaonekana ni wachawi.
Ndugu, kuwa makini na staili za kisasa za uponyaji, ni makundi machache sana yanayoongozwa na Bwana kutumia vitu hivi vya asili katika kufanya huduma, na utaona havitumiki mara kwa mara au kila siku bali kwa mwongozo Fulani. Lakini ukiona mahali hapo ndio imekuwa staili, kimbia hapo Mungu hayupo hiyo ni ibada ya sanamu. Wana wa Israeli walimkosea Mungu hivyo hivyo, baada ya kuona Mungu amewaponya kwa kuitazama ile nyoka ya shaba, Musa aliyoagizwa aiunde kule jangwani, wao wakadhani Mungu sikuzote yupo katika sanamu ile, matokeo yake ikawa walipofika katika nchi ya ahadi wengine waliendelea kuiunda, wakiitazama ili kutatuliwa matatizo yao, ikawa ni chukizo kubwa sana kwao. Mpaka baadaye sana mfalme Yosia alipokuja kuivunja vunja, ndipo hasira ya Mungu ikaisha.(2Wafalme 18:1-5)
Hivyo usigeuze kitu chochote kuwa sanamu yako, kukitegemea hicho angali maisha yako yapo mbali na dhambi utakumbana na laana badala ya baraka. Tumepewa jina la YESU hilo ndio mwanzo na mwisho. Vinginevyo vyote tusubiri kwanza uongozo wa Roho Mtakatifu, kama haupo, tuache.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)
NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?
MAOMBI YA KUFUNGULIWA KIUCHUMI.
Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?
SWALI: Katika Mithali 30:24, tunaona wanatajwa wanyama wanne, wenye akili sana, lakini naomba kufahamu juu ya Yule wanne ambaye ni mjusi, Anaposema “Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme” Maana yake ni nini?
JIBU: Tusome,
Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. 25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari. 26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba. 27 Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi. 28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme”
Mjusi ni kiumbe ambaye ameumbiwa wepesi wa kupanda na kupita karibia sehemu zote zenye upenyo hata ule mdogo sana, uwezo wa mikono yake unamfanya aweze kusimama katika pembe yoyote ile ya ukuta, iwe ni ukuta wa juu, au wa pembeni, au wa chini, kwake vyote ni sawasawa, tofauti na wanyama wengine, ambapo pengine hutegemea kucha zao, ambazo hizo zinawasidia kupanda baadhi ya maeneo tu kama miti.
Na ndio maana utawakuta katika kila nyumba, hawazuiliki, hadi katika majumba ya wafalme biblia inasema hivyo utawakuta, mahali ambapo pana ulinzi, pana uangalizi, lakini wao wanaingia huko bila shida yoyote na kufanya makazi.
Ni kutufundisha nini katika hekima yake?
Ni kwamba, na sisi tunapokuwa ndani ya Kristo tunapewa mikono kama ya mjusi katika roho. Uwezo wa hali ya juu kupanda kila kuta ngumu, Hatuzuiliki kwa kitu chochote, popote tutakapotaka kupafikia tutapafikia, hata katika malango mazito ya ibilisi tutayamiliki.
Mwanzo 22:17 “katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; NA UZAO WAKO UTAMILIKI MLANGO WA ADUI ZAO; 18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu”
Je! Unataka uupokee uwezo huo? Kanuni ni moja tu, nayo ni kumpa Kristo maisha yako, jikane nafsi yako, simama kikamilifu na Bwana, kisha utaona jinsi Mungu anavyokupigania kuangusha kuta na kumshinda ibilisi kiwepesi, ziwe za kimaisha au za kiroho. Kwako hakuna kikwazo kitakachokuwa kigumu kukishinda.
Bwana akubariki.
Je! Utapenda kufahamu hekima iliyo nyuma ya wale watatu waliosalia?
Fungua link hizi>>>
Wibara > Wibari ni nani?(Mithali 30:26)
Nzige >TUWATAFAKARI NZIGE WA JANGWANI.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
Nzige, Parare, madumadu na tunutu ni wadudu gani? (Yoeli 2:25)?
Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5
Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8)
Ayala, Paa na Kulungu ni wanyama gani?
Jibu: Turejee..
Waefeso 5:25 “……kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na KULISAFISHA KWA MAJI KATIKA NENO;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”..
Siri ya kanisa kutakaswa kwa “Maji” inaanzia pale Msalabani, wakati Yule Askari anamchoma Bwana mkuki ubavuni, biblia inaonyesha kuwa palitoka “Maji na Damu”. Ikifunua kuwa Maji ni lazima yahusike katika hatua za utakaso wetu, ndipo damu ya Yesu iweze kututakasa kabisa. Utauliza tunazidi kulithibitisha vipi hilo? Tusome Matendo 2:37-38
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”
Umeona hapo?.. Anasema tubuni mkabatizwe, mpate ondoleo la dhambi.. kwahiyo kumbe ubatizo unahusika sana katika kusafika utu wa ndani.. maana yake utakaso wa Damu, unategemea ubatizo wa Maji, ili Roho Mtakatifu aweze kukaa ndani ya mtu.
Vitu hivi vitatu vinaenda pamoja (DAMU, MAJI na ROHO Mtakatifu). Huwezi kukichukua kimoja na kukiacha kingine!… Wala kusema kimoja kina umuhimu kuliko kingine… Vyote hivi vitatu vina umuhimu na maandiko yanasema vinapatana katika UMOJA!
1Yohana 5:9 “Kisha wako watatu washuhudiao duniani], ROHO, NA MAJI, NA DAMU; na watatu hawa hupatana kwa habari moja”.
Hiyo ndio sababu pia kwanini tunapaswa tubatizwe!.. Wengi leo wanaupuuzia ubatizo wa maji wanasema hauna umuhimu sana, ubatizo wa Roho Mtakatifu ndio wa muhimu.. Pasipo kujua kuwa Roho, na Maji na Damu vinapatana katika Umoja, ndio maana Bwana Yesu alimwambia Nikodemo kuwa kama hatazaliwa kwa MAJI (maana yake kwa ubatizo wa maji) na kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu, hatauona ufalme wa mbinguni, na huko ndiko kuzaliwa mara ya pili.
Maana ya kuzaliwa mara ya pili ni kubatizwa katika maji na katika Roho Mtakatifu.
Yohana 3:4 “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa MAJI NA KWA ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.
Na ubatizo ulio sahihi ni ule wa maji Tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Bwana Yesu (Matendo 2:38, Matendo 8:16, Matendo 10:48 na Matendo 19:5)
Bwana akubariki.
Ikiwa bado hujapata ubatizo sahihi, basi unaweza kuwasiliana nasi, tutakusaidia juu ya hilo, kwa Neema ya Bwana.
Shalom
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
SWALI: Naomba kufahamu maana ya huu mstari..Kwanini biblia imtaje Mungu kama mtu, angali maandiko yanasema yeye sio mtu.
Kutoka 15:3
[3]BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake.
JIBU: Neno hilo halimaanishi kuwa Mungu ni mtu, Bali biblia hutumia mifano halisi ya kibinadamu kuwasilisha picha Fulani Rohoni..
Kwamfano ukisoma andiko lingine linalopatikana katika Mithali 30:26, utaona mnyama anayeitwa Wibari anatajwa kama mtu..
Mithali 30:26
[26]Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.
Tunafahamu kabisa wanyama hawa wibari(Pimbi) sio watu, isipokuwa kwa wingi wa akili zao, mwandishi anawafananisha na watu, Ni kwasababu gani? Ni Kwasababu ijapokuwa ni waoga, wadhaifu, wanawindwa na kila mnyama mkali..lakini hawajengi nyumba zao katika sehemu dhaifu kama kwenye viota, au kwenye mashimo, au vichaka, ambapo ni rahisi kuvamiwa au kuharibiwa na majanga, Bali wanaweka makazi Yao katika miamba mikubwa iliyojificha sana Mahali ambapo ni ngumu adui kuwashambulia.. wanafananishwa na watu waliojenga maisha yao juu ya MWAMBA, pekee yaani Yesu Kristo
Mathayo 7:24 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba”
Hivyo tukirudi katika andiko hilo, anaposema “BWANA ni mtu wa vita”. Anajaribu kumfananisha Bwana na shujaa wa kivita, jemedari mwenye uzoefu mkubwa sana katika vita vikali, mfano wa Sauli, au Daudi, ambao walikuwa wanasimama mstari wa mbele katika vita, ili sisi tupate picha jinsi gani Mungu wetu alivyo mkuu sana, pale anapoitwa Bwana wa Majeshi, tumwelewe uweza wake wa kutupigania na kutusaidia kuangusha ngome za ibilisi jinsi ulivyomkubwa haijalishi zimekita mizizi kiasi gani.
Zaburi 24:8 “Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita”
Hivyo mstari huo hakumaanisha kuwa yeye ni mtu.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
Ufunuo 12 inaelezea vita vya wakati upi?
Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza
NIMEAZIMIA KUWAKUSANYA MATAIFA. NIPATE KUWAMWAGIA GHADHABU YANGU
Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?
Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?
NA WATU WOTE WALIKUWA WAKIAMKA MAPEMA, WAENDE HEKALUNI.
Jibu: Tusome,
Mwanzo 24:67 “Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake”.
Andiko hilo halimaanishi kuwa Isaya alipendezwa na kifo cha mamaye Sara, na hivyo akapata faraja kwa kufa kwake, bali linamaanisha kinyume chake.
Ikumbukwe kuwa Isaka alikuwa ni mwana pekee wa Sara, na Isaka alimpenda sana mama yake, na siku mama yake alipokufa ni wazi kuwa alihuzunika kwa kipindi kirefu, lakini sasa kipindi anampata Rebeka kama mke wake, ile huzuni ikapungua kwa kiasi kikubwa na akajihisi faraja kama tu ile aliyokuwa anaipata kutoka kwa mama yake.
Ni nini tunajifunza kutoka katika habari hiyo?.
Hapa tunajifunza jinsi mwanamke wa kiMungu anavyopaswa awe!..
Rebeka alikuwa ni mwanamke wa mfano wa kuigwa, kwani aliweza kuwa faraja kwa mume wake kiasi kwamba mume wake akasahau uchungu wote wa kufiwa na mamaye (Maana yake Rebeka alikuwa ni mke kwa Isaka na hapo hapo mama kwa Isaka, kumlea na kumtia moyo). Lakini leo hii wanawake wengi wanafanyika mishale kwa waume zao, na si faraja.
Mama, dada, binti, msichana kabla ya kwenda kujifunza kwa akina Musa, Eliya, na Danieli, hebu kwanza tenga muda wa kujifunza juu ya wanawake hawa.. Kwasababu tabia ya Musa haitakusaidia sana katika uanawake wako zaidi ya akina Rebeka, au Sara au Mariamu au Ruthu..
Ukitaka kuwa mke bora na mama bora kajifunze kwa akina Hana, Debora, na Tabitha..ukitaka kuwa binti bora nenda kajifunze kwa mashujaa wote wa kike katika biblia kabla ya kuwakimbilia wanaume.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
Tofuati kati ya kifo na mauti ni ipi?
CHUKI ULIZO NAZO KWA MAADUI ZAKO, SIZO ALIZONAZO MUNGU JUU YAO.
Nilikuwa naomba kujua utofauti kati ya DHAMBI, UOVU na KOSA kibiblia.asante!!
Kibiblia mapepo yanafananishwa na inzi.
Inzi siku zote huvutiwa na mazingira ya aina mbili. Ya kwanza ni uchafu. Mahali palipo na uchafu hapakosi inzi, Na ndio maana Bwana baada ya kuhakikisha taifa la Misri linanuka uvundo, kwa harufu na uchafu wa wale vyura waliokufa, akawaanda na inzi waje juu yao ili wayafurahie mazingira yao. Ndio hapo utaona akawaleta wengi sana juu ya wamisri wakawa kero kubwa sana kwao.
Kutoka 8:24 “Bwana akafanya; wakaja wingi wa mainzi kwa uzito sana, wakaingia nyumbani mwa Farao, na katika nyumba za watumishi wake, tena katika nchi yote ya Misri; nayo nchi iliharibiwa kwa ajili ya wale mainzi”
Lakini sio hilo tu, watu wengi wanapuuzia wakidhani kuweka mazingira tu safi ndio kutawafukuza. Lakini pia inzi wanavutiwa na mazingira ya vidonda. Palipo na vidonda, utaona inzi wengi wanakusanyika kwenye eneo hilo.
Maana yake nini? Rohoni ukiwa na majeraha ambayo hayajafunikwa au kutibiwa, kunaweza kukusababishia kuvuta uwepo wa mapepo juu ya maisha yako, Unaweza kweli ukawa umejitahidi kuwa mbali na uchafu wa rohoni na mwilini, huibi,huzini, unaishi maisha ya utakatifu, unatumika kanisani n.k.
Lakini kama una majeraha rohoni mwako,ambayo hayajatibiwa, bado mapepo yanaweza kupata nafasi ya kukusumbua. Una kinyongo cha muda mrefu na mwenzako, hujaachilia, hujasemehe, una uchungu, una wivu, una hasira zisizoachilika,. Fahamu kuwa hayo ni mazingira mazuri ya mapepo.
Ndio hapo utaona mkristo, ameokoka halafu analipuka mapepo, au anasumbuliwa na nguvu za uovu. Unajiuliza mbona huyu hana maisha machafu lakini yanamkuta haya? Sababu kubwa ni eneo hili. Ndio maana biblia inatuambia tulinde sana mioyo yetu kuliko vyote tuvilindavyo. Moyo hukaribisha roho za nje kiwepesi.
Tibu moyo wako, jiachie kwa Yesu, kubali kujikana nafsi, kubali kujishusha, kubali kusamehe, kubali hata kupoteza hicho ulichonacho, ili uiponye nafsi yako. Wivu, hasira, chuki, visitawale kabisa maisha yako. Viwe na adui wako.
Unaweza kusema hizi hali nitazishindaje? Jibu ni kuwa yote hayo yanawezekana endapo tu, utaishi maisha ya kumtazama Kristo, zaidi ya nafsi yako. Macho yako yakielekea kwa Yesu tu daima ukajifunza kwake, kidogo kidogo utaona tabia za mwilini zinaanza kukuachia, unajifunza tabia za Yesu. Na yeye mwenyewe atakusaidia kukuponya kabisa kabisa kwasababu aliahidi hivyo katika Neno lake.
Hosea 6:1 “Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. 2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake”.
Alisema pia..
Yeremia 30:17 Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.
Jeraha zetu za rohoni ameahidi kuziponya. Na Neno lake ni kweli halitanguki, limethibitishwa. Hivyo anza sasa kumkaribia Kristo na kujifunza kwake.(Mathayo 11:28-29)
Bwana akubariki.
Maombi yangu:
Ee, Baba tumejifunza jinsi adui yetu ibilisi anavyopata nafasi katika mioyo yetu pale tunaposhindwa kuzitibu jeraha zetu. Lakini leo tumetambua makosa yetu, nasi tunatubu mbele zako. Tunaomba utusamehe Baba yetu, Tumedhamiria kutoka katika mioyo yetu kukufuata wewe, na kujifunza kwako, Tunaomba ututibu majeraha yetu yote, yaliyodumu kwa muda mrefu na mfupi, ondoa hasira, ondoa vinyongo, kutokusamehe, wivu, ndani yetu. Nasi tunaamini tangu siku ya leo unatukamilisha. Asante Baba kwa kutusikia. Tunaomba tukishukuru katika jina la Yesu Kristo. Amen.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
Kwanini wakristo walipomuona Petro akigonga walisema “Ni malaika wake”?
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.(Opens in a new browser tab)
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.(Opens in a new browser tab)
KUOTA UNA MIMBA.(Opens in a new browser tab)
KATAA KUWA EUTIKO, WA KUSINZIA IBADANI.
Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)
Kama Kristo alizichukua dhambi zetu na kutusamehe kwanini kila siku tunatubu?
Rudi nyumbani
Jibu: Tusome,
Marko 14:27 “Yesu akawaambia, Mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo watatawanyika”.
Kukunguwazwa maana yake ni “kuchukizwa”.. Mtu anapokufanya ukasirike au uchukie maana yake amekukunguwaza, biblia imetoa tafsiri ya neno hilo vizuri katika Mathayo 26:30.
Mathayo 26:30 “Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.
31 Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote MTACHUKIZWA kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika”.
Unabii huo alioutoa Bwana ulitimia masaa machache tu mbeleni, pale ambapo kikosi cha Askari wa kirumi kilitokea na kumkamata Bwana Yesu.
Na tunasoma Mitume hawakukifurahia kile kitendo, “WALICHUKIZWA SANA”, hata Petro kufikia hatua ya kutoa upanga na kumkata sikio mtumwa wa kuhani mkuu. Hicho ni kiwango kikubwa sana cha hasira.
Yohana 18:7 “Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti.
8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.
9 Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao.
10 Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lake ni Malko”.
Vile vile na sisi tuliompokea Yesu ni lazima tutapitia tu vipindi vya kuchukizwa kwaajili ya Yesu.
Unapofika mahali na kukuta watu wanalikufuru jina la Yesu ni lazima utachukizwa tu!, unapofika mahali na kukuta watu kwa makusudi kabisa wanahubiri injili nyingine tofauti na ile ya kimaandiko ni lazima utachukizwa tu!.
Unapofika mahali na kukuta unatolewa unabii wa uongo, au kweli ya Mungu inapotoshwa kwa makusudi, ni lazima utachukizwa tu!, Unapofikia hatua ya kusumbuliwa kiimani na watu wengine kwasababu tu umeokoka, au umeamua kwenda katika njia sahihi ni lazima tu utakunguwazwa! hata wakati mwingine kufikia kiwango kama kile cha Petro cha kutamani kumdhuru mtu kabisa.
Lakini sisi hatujapewa ruhusa wala amri ya kumdhuru wengine, hata kama ni waovu au wanatutendea maovu, au hata kama wanamtukana Mungu mbele yetu, kazi tuliyopewa ni kuziokoa roho, na si kuziangamiza, kwasababu kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali juu ya majeshi ya mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Lakini siku zote fahamu kuwa, ni lazima tu tutapitia vipindi vya kuchukizwa kwaajili ya Yesu, hilo haliepukiki kwa kila aliyezaliwa mara ya pili.
Yohana 15:20 “Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa WALINIUDHI MIMI, WATAWAUDHI NINYI; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu”.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
Nini tofauti ya Mtumwa, Mjakazi na kijakazi?
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.
Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?
Bwana alisema “Usiue” (Kutoka 20:6) lakini tunaona anawapa wana wa Israeli maagizo ya kuua wale wote wanaoabudu miungu? Je Hii inakaaje? (Kumbukumbu 13:6).
Jibu: Tusome,
Kumbukumbu 13:6 “Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako; 7 katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia;8 usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;9 MWUE KWELI; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote.10 NAWE MTUPIE MAWE HATA AFE; kwa kuwa alitaka kukupotoa na Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.11 Na Israeli wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako”
Ni kweli Mungu alikataza “Kuua” lakini pia kuna mahali pengine aliruhusu “kuua”, sasa ni rahisi kuhisi kuwa biblia inajichanganya, lakini kiuhalisia haijichaganyi.
Katika biblia zilikuwepo sheria za mtu binafsi lakini pia zilikuwepo sheria za Nchi/Taifa. Ikumbukwe kuwa Israeli lilikuwa ni Taifa la kidini, hivyo baadhi ya Amri na sheria zilikuwa ni za kitaifa. Kwahiyo mtu akiivunja sheria Fulani iliyoandikwa kwenye torati basi alikuwa amevunja sheria ya kitaifa.
Ili tuelewe vizuri tuchukue mfano wa mataifa ya sasa, katika mataifa mengi, (karibia yote) kuna sheria ya “kutoua” yaani raia haruhusiwi kumuua mwenzake kwa kosa lolote lile!!, lakini katika Taifa hilo hilo tunaona kuna sheria ya “kunyongwa” endapo mtu akikutwa na hatia iliyo kubwa sana..
Sasa Yule askari aliyetumwa kumweka kitanzi Yule mtuhumiwa, tayari kashafanya tendo la mauaji, lakini kwa kumnyonga Yule mhalifu, bado anakuwa hajavunja sheria ya “kuua”.. Kwasababu yeye kapewa amri ya kuua na mamlaka, lakini haja ua kwa matakwa yake yeye. Lakini kama ingekuwa kajichukulia sheria mkononi ya kuua basi angehesabika ni muuaji, na angekuwa amevunja sheria ya nchi. Na pia Nchi kuweka sheria ya Kuwaua wale waalifu sugu, haijamaanisha kuwa imeruhusu sheria ya watu kuuana huko uraiani.
Vivyo hivyo katika Israeli, Mungu alikataza mtu kujichukulia sheria mkononi za kuua, lakini pia aliruhusu mauaji kwa watu ambao watathibitika kisheria (yaani kitaifa) kuwa wamestahili kifo!. Na mamlaka hayo aliwapa watu wote, tofauti na sasa ambapo wanapewa tu wale askari walioteuliwa kwa kazi hiyo.
Kwahiyo biblia haijichanganyi, lakini pia tunachoweza kujifunza ni kuwa Lile baya mtu analolifanya litamrudia hata kwa njia nyingine, mtu aliye muuaji naye pia atauawa, mtu anayefanya ubaya ule ubaya utampata na yeye siku za baadae.
Mathayo 26:51 “Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
52 Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga”.
Soma pia Ufunuo 13:10.
Kwahiyo tujihadhari na dhambi tuwafanyiazo watu au tuzifanyazo mbele za Mungu, kwasababu yale tunayoyafanya tutapata malipo yake hapa hapa, kama ni mema au kama ni mabaya.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)
Je! Watu ambao hawajawahi kusikia injili kabisa siku ya mwisho watahukumiwa?
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 27:8 “Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huko na huko mbali na mahali pake”
JIBU: Hapa Sulemani alikuwa anajaribu kueleza jinsi tabia ya ndege inavyoweza kufananishwa na tabia ya mkristo katika maisha yake hapa duniani. Kwa kawaida ndege anapotoka katika kiota chake, huwa na lengo la aidha kutafuta chakula, au kukiendeleza kiota chake, au kujipumzisha mahali Fulani kwa muda. Hivyo huwa anaenda na kurudi, anaenda na kurudi kwa siku hata mara 10 na zaidi, anaweza kufanya hivyo.
Lakini wakati huo huo, awapo katika mazingira ya kuzunguka huko na huko, hukutana na hatari nyingi sana. Aidha Maadui au mitego. Hivyo asipokuwa makini anaweza asirudi, kabisa nyumbani kwake.
Hivyo ndivyo alivyo mkristo, ambaye misingi yake ni “biblia na Kanisa”. Ukweli ni kwamba si kila wakati atakuwa katikati ya watakatifu, au atakuwa uweponi akimsifu Mungu na kumwimbia, au akilitafakari Neno la Mungu. Zipo nyakati atatoka kwa muda ataenda kazini, atatoka kwa muda ataenda shambani pengine kujitafutia riziki, ataenda shuleni masomoni na kama si hivyo basi kwa namna moja au nyingine atajihusisha na mambo ya kijamii, kama kutembelea jamaa, na ndugu, majirani n.k.
Sasa awapo katika mazingira haya anafananishwa na ndege atokaye katika kiota chake na kuzunguka huko na huko. Hivyo anapaswa awe na busara kwa sababu huko nje, zipo hatari nyingi sana za yeye kunaswa na adui asipokuwa makini.
Ni lazima ajiwekee mipaka, si kila biashara afanye, si kila jambo la kidunia analoletewa mbele yake ajihusishe nalo, si kila mazungumzo ayaongee. Bali muda wote awapo nje, atambue kuwa makao yake ni KANISANI awezapo kufanya ibada, na kujumuika na watakatifu wenzake. Muda wote atambue usalama wake ni katika Neno la Mungu basi. Alale katika hilo na aamke katika hilo.
Akitafutacho huko nje ajue ni kwa lengo la kuendeleza tu kiota chake (kazi ya Mungu), na sio vinginevyo. Mtu huyo akizingatia vigezo hivyo atakuwa salama. Lakini watu wengi wamenaswa na ulimwengu. Hata Kanisani hawaonekani tena baada ya kupata kazi, Upendo wao kwa Mungu umepoa pale walipokutana na marafiki Fulani wapya, muda wa maombi wanakosa kisa wapo buzy na mihangaiko ya maisha. Kauli zao zimebadilika, kwasababu muda mwingi wamekaa na watu wenye mizaha, na matusi, hadi na wao wakajifunza lugha zao.
Biblia inatuambia,
Waefeso 5:15 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. 17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
Anasema tena..
Wakolosai 4:5 “Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. 6 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu”.
Hivyo tuwapo nje ya uwepo wa Bwana, tujichunge, tujizuie, tuwe na kiasi, tutakuwa salama. Ili tusijikute tunanaswa katika mitego ya ibilisi.(Mithali 1:17, 7:22)
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana,
Dia ni nini katika biblia? (Mithali 13:8)
Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?
Nini maana ya “Atamwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”. (2Wathesalonike 2:8).
Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
Tusome,
Matendo 27:25 “Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.
26 Lakini hatuna budi kupwelewa katika kisiwa kimoja”.
Kupwelewa maana yake ni “kusafiri katika kina kifupi”. Meli au Mashua inaposafiri katika maji yenye kina kifupi, maana yake Meli hiyo au boti hiyo “inapwelewa”.
Katika safari ya Paulo kuelekea Rumi chini ya kikosi cha maaskari, maandiko yanatuonyesha safari ile ilikuwa ni ya misuko-suko mingi baharini, kwasababu wale mahabaria hawakulisikiliza shauri la Paulo ambalo aliwashauri wasing’oe nanga lakini wenyewe hawakusikia hivyo. Mwishowe wakakutana na misuko suko mikuu baharini, mpaka wakakata tamaa ya kuokoka.
Matendo 27:10 “akawaambia, Wanaume, naona kwamba safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia.
11 Lakini yule akida akawasikiliza nahodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paulo”.
Wakiwa katika hiyo misukosuko, Paulo alitokewa na Malaika na kuambiwa kuwa hakuna atakayekufa katika safari hiyo, kwani ni lazima Paulo afike salama Rumi ili akalishuhudie Neno la Mungu na kule nako. Na jambo lingine aliloambiwa na Malaika yule ni kwamba Merikebu itapwelewa (yaani itasafiri katika kina kifupi) kando kando ya kisiwa kimoja, mpaka watakapofika kwenye hicho kisiwa.
Na kweli ufunuo huo mahabaria waliuhakiki kwani muda mfupi tu walipoanza kupima kina cha maji waliona kinaanza kupungua kwa jinsi walivyokuwa anaendelea mbele.
Matendo 27:27 “Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu.
28 Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano”.
Ni nini tunachoweza kujifunza katika safari hiyo ya Paulo?
1.Mungu atakuwepo na sisi hata katikati ya majaribu
Paulo, alikuwa amefungwa lakini katika kufungwa kwake, bado Mungu alikuwa naye, akimwongoza katika mapito yake, utaona pia wakati akiwa gerezani bado Bwana alikuwa naye, na kila mahali Bwana alikuwa naye, vile vile na sisi tunapokuwa katika majaribu, ambayo tunajua kabisa ni Mungu kayaruhusu basi hatupaswi kuwa na woga wala kukata tamaa, kwasababu Mungu atakuwa Pamoja nasi, na zaidi sana yeye alisema “hawezi kutuacha tujaribiwe kupita tuwezavyo”
2. Wokovu wa Mungu ni hata kwa maadui zetu.
Tunapokuwa katikati ya majaribu ni muhimu kujua kuwa Mungu katuweka pale kwa wokovu wa wengine, Utaona Paulo kafungwa lakini Mungu anamwokoa yeye Pamoja na wale Mabaharia, na wafungwa na watesi wake, anawaokoa na Mauti vile vile na sisi Mungu anapotuweka mahali ni ili tuokoke na wale tulio nao, haijalishi ni maadui zetu au watesi wetu.
Matendo 27:22 “Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila merikebu tu.
23 Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami,
24 akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.
25 Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.
26 Lakini hatuna budi kupwelewa katika kisiwa kimoja”.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.