Jibu: Tusome kuanzia ule wa 2 ili tuweze kuelewa vizuri.
Ayubu 24:2 “Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.
3 Humfukuza punda wake asiye baba, Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.”.
Hapa Ayubu anazungumzia juu ya kundi la watu wabaya ambao wanawaonea Mayatima na kuwadhulumu wajane.
Ndio hapo anasema wapo (watu duniani) ambao.
1. Wanaondoa alama za Mipaka, na kuyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.
Maana yake wanawadhulumu watu mashamba/ardhi kwa kuondoa mipaka iliyokuwepo na kuweka mipaka ya uongo!,..na baada ya kumiliki ardhi kwa dhuluma namna hiyo bado wanalisha mifugo yao juu ya hizo ardhi za dhuluma.
2. Humfukuza punda wake asiye baba,
Maana yake humfukuza Punda wa Yatima, (mtoto asiye na Baba). Punda wake anapoingia mahali kula vichache vilivyosalia katika mashamba yao, wao humfukuza punda Yule, pasipo kuzingatia kuwa Yule ni yatima asiye na uwezo wa kujimudu mwenyewe, asiye na uwezo wa kununulia chakula punda wake, lakini wao hawajali hayo yote, bali wanazifukuza punda zake.
3. Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.
Hawa watu pia wanachukua Ng’ombe za wanawake wajane, ambao wamefiwa na waume zao, na hata nguvu za kufanya kazi tena hawana!.. wanachukua Ng’ombe zao na kuwaweka Rehani, kutokana na mikopo wanawake hao waliyoichukua.. Jambo ambalo ambalo si jema machoni pa Mungu..Wangepaswa wawahurumie na kuwapa mikopo bila kuwawekea rehani chochote kwasababu wao hawana tumaini msaada wowote wapo wao kama wao, na umri wao umeshakwenda..
Kumbukumbu 24:17 “Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;
18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili”
Hivyo watu wa namna hii ambao wanawatesa Wajane na Mayatima, Bwana Mungu alitaja hukumu yao katika kitabu cha Kutoka 22:22
Kutoka 22: 22 “Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.
23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima”.
Hivyo na sisi hatuna budi kuwatendea Mema watu hawa, na kuwapenda ili na Bwana atubariki
Shalom
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?
Kwanini wajane vijana hawakupaswa kuandikwa?
NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?
TENDA AGIZO LA YESU, HILO NDIO LITAKALOKULINDA.
Jina la Bwana na Mwokozi, Mkuu wa Uzima, Yesu Kristo lihimidiwe!..karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu.
Upo wakati ambao TAA ya Mungu itazima!.. Tuitikie wito wa Mungu, kabla ya huo wakati kufika..
1Samweli 3:2 “Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),
3 NA TAA YA MUNGU ILIKUWA HAIJAZIMIKA BADO, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu;
4 basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.”
Sasa ili kuelewa vizuri Taa ya Mungu ni kitu gani, na ilikuwa inazimika wakati gani..hebu turejee ile Hema ambayo Musa aliagizwa aitengeneze, tunasoma Ilikuwa imegawanyika katika Sehemu kuu tatu, Ua wa Ndani, Patakatifu na Patakatifu pa patakatifu.
Na ndani katika Patakatifu, palikuwa na madhabahu ya uvumba, Meza ya mikate ya wonyesho pamoja na KINARA CHA TAA, ambacho kilikuwa na Mirija saba. (Tazama picha juu).
Hiki kinara cha Taa kazi yake ilikuwa ni kutia Nuru ile hema wakati wa USIKU. Kwamba Nyakati zote za usiku ni sharti ndani ya Hema kuwe na Nuru, na amri hiyo ilikuwa ni ya Daima, maana yake ya kila siku!.. haikupaswa hata Usiku mmoja upite bila Kinara hicho kuwashwa ndani ya Hema.
Kutoka 27: 20 “Nawe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima.
21 Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza TANGU JIONI HATA ASUBUHI MBELE YA BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israel”
Tusome tena..
Walawi 24:1 “Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
2 Waagize wana wa Israeli kwamba wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima.
3 Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza TANGU JIONI HATA ASUBUHI MBELE ZA BWANA DAIMA; ni amri ya milele katika vizazi vyenu”
Hapo mstari wa 3, unasema ataitengeneza “tangu jioni hata asubuhi” maana yake wataiwasha tangu jioni mpaka asubuhi, na kukiisha pambazuka basi taa ile inazimwa, kwasababu kulikuwa na Nuru ya mwanga wa Nje wa jua iliyokuwa inaingia ndani ya Hema.
Sasa tukirudi katika habari hiyo ya Samweli, maandiko yanasema Samweli alikuwa analala katika Hema karibu na sanduku la BWANA, na wakati ambapo Taa ya Mungu bado haijazimika..Maana yake bado hakujapambazuka, (kwasababu kukisha pambazuka tu, tayari ile taa ilikuwa inazimwa).
Wakati huo ndipo Samweli aliisikia Sauti ya Mungu ikimwita mara 4, na Samweli akaitikia wito wa Mungu.
Lakini ni nini tunajifunza katika hiyo habari?
Upo wakati ambao sauti ya Mungu inaita juu ya Mtu..na wakati huo ni wakati wa giza Nene juu ya maisha ya mtu.. Huo ndio wakati ambapo Mungu anamwita mtu, na anamwita kwa sauti ambayo inakuwa inayofanana na ya watu wa Mungu.. kiasi kwamba mtu anaweza kudhani ni mtu anayemwita/kumshawishi kumbe ni Mungu, ndio maana Samweli alipoitwa alikimbilia kwa Eli akidhani ni Eli anayemwita kumbe ni MUNGU.
Vile vile Mungu anawaita leo watu kutoka katika dhambi, na uvuguvugu lakini watu wanadhani ni wachungaji wao ndio wanaowaita, wengine wanadhani ni wahubiri ndio wanaowatafuta wawe washirika wao, pasipo kujua kuwa ni sauti ya Mungu ndio inayowaita na si watu.
Sasa endapo Samweli asingeitikia ule wito wakati ule ambapo TAA BADO HAIJAZIMIKA, huenda ile sauti ya Mungu asingeisikia tena kwa wakati ule mpaka labda kipindi kingine ambapo Taa hiyo itakuwa inawaka.
Ndugu TAA ya Mungu leo ni NEEMA, Hii Neema kuna wakati itasimama!, na hakutakuwa tena na nafasi ya kumkaribia Mungu, wakati ambao unyakuo wa kanisa utapita, ndio wakati ambao TAA itakuwa imezima, vile vile wakati ambao utaondoka katika haya maisha huo ndio wakati ambao Taa ya Mungu itakuwa imezimika juu yako.
Je umemkabidhi Yesu maisha yako?.. Umebatizwa katika ubatizo sahihi? Umeokoka?.. Kama bado ni vyema ukafanya hivyo sasa kabla Taa haijazimika.
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
Maran atha!
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?
Kiango na Pishi ni nini (Mathayo 5:15)?
NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANA-KONDOO.
Thenashara ni neno la kiebrania linalomaanisha namba “kumi na mbili” (12). Kwahiyo badala ya kusema watu 12, ni sahihi kabisa kusema “watu Thenashara”, au badala ya kusema “miezi 12” ni sahihi kusema “miezi Thenashara”…badala ya kusema makabila 12 ni sawa na kusema “Makabila thenashara” n.k
Biblia imelitumia Neno hilo Thenashara kuwakilisha wale Wanafunzi 12 wa Bwana Yesu, ambao baadaye waliitwa Mitume.
Marko 3:16 “Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro;
17 na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo;
18 na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo,
19 na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti. Kisha akaingia nyumbani”
Na ni kwanini wanafunzi hawa 12, watenganishwe kwa kuitwa hivyo Thenashara?.. Ni kwasababu Bwana Yesu alikuwa anao wanafunzi wengine wengi zaidi ya 70,
Luka 10:1 “Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.”
hivyo ili kuwatofautisha hawa wanafunzi 70 na wale 12 aliowateua kwanza kndio likatumika hilo neno “Thenashara”
Unaweza kulisoma neno hilo pia katika Mathayo 26:14-16, Marko 4:10, Marko 9:35, na Yohana 20:24
Je umefanyika kuwa Mwanafunzi wa Yesu? kwa kutubu dhambi zako zote, na kumaanisha kuziacha na vile vile kuchukua msalaba wako na kumfuata yeye?
Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Wahuni ni watu gani katika biblia?
Hesabu 11:6 “lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu”
Nakusalimu katika jina lenye uweza la YESU KRISTO mwokozi wetu. Ni siku nyingine tena Bwana ametupa neema ya kuifikia hivyo, nakukaribisha tuyatafakari pamoja maneno yake.
Wana wa Israeli walipofika jangwani hawakujua kuwa watalishwa chakula cha aina moja tu, Mwanzoni waliifurahia ile mana, jinsi ilivyokuwa nzuri na tamu, lakini siku zilivyozidi kwenda, hamu ya mana ile ikaanza kupungua ndani yao, wakaanza kutamani na vyakula vingine..Walipoona asubuhi kifungua kinywa ni mana, mchana ni mana, chakula cha jioni ni mana.. wakasema haya mambo yataendelea mpaka lini?..wakaikinai, Wakaanza kufikiria ni wapi watapata chakula cha aina nyingine walau wabadili ladha. Ni wapi watapata nyama, watapata kuku, watapata pilau, na pizza, na Baga.
Hesabu 11:4 “Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule? 5 Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu; 6 lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu. 7 Na hiyo mana ilikuwa mfano wa chembe za mtama na kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake bedola”
Wana wa Israeli wakasau kuwa vyakula hivyo ndivyo vilivyokuwa vinawaletea magonjwa makali kule Misri, ndivyo vilivyokuwa vinafubaza miili yao. Tofauti na mana, ambayo walipoila hawakuumwa, wala kudhoofika maandiko yanasema hivyo (Kumbukumbu 8:3-4), japokuwa kilikuwa ni chakula cha aina moja tu, lakini ni salama.. Wao wakaidharau.
Ndugu yangu Mana inafananishwa na “Neno la Mungu”. Tunapookoka, tujue kuwa tutapewa chakula cha aina moja tu, nacho ni Neno la Mungu [Hilo usiliondoe akilini].. tutaamka nalo, tutatembea nalo, tutalala nalo. Ndio chakula cha Roho zetu pekee, kitufaacho kwa wakati wote hakuna kingine..Hatutalishushia na jbo lingine lolote…Hatujapewa biblia, pamoja na kitabu cha saikolojia, kitufariji Hatujapewa biblia na vilabu vya mipira (FIFA) vituburudishe , tunalimeza hivyo hivyo, bila kugoshiwa.
Lakini kwasababu ya tamaa ya mambo ya ulimwengu na mengineyo. Inasikitisha kuona wakristo wengi tunavyolikinai Neno la Mungu kwa haraka sana.. Utakuta mwanzoni mwa wokovu wetu, tulikuwa tunapenda sana kusikiliza Neno, tupo tayari kushinda muda wote kusikiliza mahubiri na mafundisho, tulikuwa tupo tayari kusoma mstari baada ya mstari, , kitabu baada ya kitabu, kudumu muda mrefu kwenye Neno la Mungu.Tukielezwa habari za mambo mengine, tuliona kama ni takataka..
Lakini ulipofika wakati tumekula tumeshiba, tunaona sasa kama hivyo vingine vya nje vinatupita.. Tunapoona biblia ni ile ile, haina matoleo mapya, maagizo ni yaleyale, yanayotutaka tuwe watakatifu na wenye imani, na tujiepushe na mambo ya ulimwengu huu.. Tunaona kama ni habari zile zile za kale za kujitesa.
Ndio hapo utamwona Mkristo anapoa anaanza, kufuatilia na miziki ya kidunia, anaanza kuwa mshabiki wa mipira na thamthilia za kidunia, tena anazichambua kwa undani kama vile tu anavyochambua Biblia, ili tu aipe nafsi yake ladha nyingine..mwingine anachanganyia na miziki ya kidunia humo humo..Mpaka Neno la Mungu linakuwa sio chakula kikuu kwake, bali sehemu ya vyakula vyake. Kama wana wa Israeli walivyoifanya mana, kuwa sehemu mojawapo ya vyakula vyao..
Lakini viliwatokea puani, wakaanza kufa, na kupata mapigo mengi sana, kutoka kwa Mungu. (Soma Hesabu 11:33).
Ndugu tunapoamua kumfuata Kristo tusitegemee tutapewa chakula kingine zaidi ya NENO LAKE. Na kama tukilikinai mapema sana, hatutamaliza mwendo wetu salama. Si ajabu tunakutwa na majaribu mengi, na mapigo mengi, kwasababu tu ya tamaa ya mambo mengine zaidi ya Neno la Mungu.
Tukijifunza kuishi sawasawa na biblia,tuitegemee hiyo tu, hata kama tutakosa vingi, hatutafaidi na vingi vya ulimwengu huu, lakini roho zetu na nafsi zetu zipo salama. Hivyo tujifunze, kukifurahia chakula hiki hiki kimoja, Mungu anatambua kuwa hatutadhoofika, kinyume chake ndio tutaimarika na kubarikiwa.
Tuache kutanga tanga na tamaa..Tii kile biblia inasema, vingine tuwaachie mataifa, Ili tuweze kufanikiwa na kuishi maisha mema katika hii dunia Mungu aliyotuweka, ndani yake.
Kumbuka shetani alilijua hilo, ndio maana alipomjaribu Bwana kule jangwani, kwa kumletea vyakula vyake vya vigeni, wakati ananjaa. Yesu alimwambia, imeandikwa mtu hataishi kwa mkate bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” (Mathayo 4:1-4).
Akamfukuza, na wewe usimvulie shetani na mambo yake maovu.
Bwana atusaidie.
Ubarikiwe daima.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?
FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Ni nani atakayeigeuza mioyo ya watoto iwaelekee mababa?
SWALI: Naomba kujua Mstari huu unamaana gani?
Mhubiri 6:3 ‘Mtu akizaa watoto mia, akaishi miaka mingi, nazo siku za maisha yake ni nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo;’
JIBU: Biblia inatuonyesha yapo makundi mawili ya watu “Ambao wakiwa hapa duniani hawatapenda maisha yao hata kufa”
Kundi la kwanza: Ni la watakatifu waliojikana nafsi, mfano wa hawa ni Ibrahimu ambaye ijapokuwa alikuwa ni tajiri, mwenye mali nyingi, lakini aliishi kama mpitaji hapa duniani, akaka katika mahema, akijua kuwa wenyewe wake ni kule mbinguni, hakufurahishwa na anasa zozote za ulimwengu huu kama Lutu.
Waebrania 11:9-10
[9]Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
[10]Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
Mfano wa hawa pia ni akina Musa, Yohana mbatizaji, pamoja na mitume na manabii wote tunaowasoma katika biblia..(Soma Waebrania 11:23-40 )
Hawa hawakuyafurahia maisha ya duniani, walijitesa nafsi zao, wasile raha yoyote ya duniani mpaka kufa kwao . Hivyo Wana heri kwasababu katika ulimwengu ujao walioungojea watatukuzwa sana na Kristo. Na sisi pia kama wana wa manabii na mitume tunapaswa tuwe kama hawa. Akili zetu na fikra zetu tuzielekeze katika ulimwengu ule na sio hapa.
Lakini kundi la Pili: Ndio kama hilo linalozungumziwa hapo..Ambalo pia linafanikishwa duniani, linapewa uzao mkubwa, watoto wengi, linajilimbikizia mali na heshima,…lakini halinufaiki na chochote katika vitu vyake, mpaka linakufa linakuwa bado halijaridhika. Huwenda linafanyakazi miaka yote usiku na mchana hadi uzeeni, na kufanikiwa kuhifadhi fedha nyingi kwenye akaunti. Halafu linakufa bila kuonja chochote..tena linakosa maziko.
Sasa Mhubiri anasema ni heri mimba iliyoharibika..kuliko hao..kwasababu halijafaidi hapa duniani wala kule mbinguni halitaonja chochote..
Afadhali yule atuamiaye/ alaye akiba yake, hata kama hatakwenda popote lakini jasho lake limemrudishia malipo kuliko hili, ambalo lilikuwa linasubiri siku moja lijifurahishe lakini hiyo siku haijafika.
Mstari huo unafanana na ule wa juu yake unaosema..
Mhubiri 6:2
[2]mtu aliyepewa na Mungu mali, ukwasi, na heshima, hata asipungukiwe na kitu cho chote kwa nafsi yake, katika yote anayoyatamani walakini Mungu hamwezeshi kula katika hizo; bali mgeni hula. Hayo ndiyo ubatili hasa, nayo ni ugonjwa mbaya.
Bwana atusaidie tuwe watu wa kujiwekea hazina mbinguni. Ikiwa umebarikiwa chochote ni vema ukiwekeze kwa Mungu, kubali kuwa kama mpitaji duniani, ili utajiri wako uwe ni kule na sio hapa. Bwana Yesu alisema hazina ya duniani hupotea, na haidumu lakini ile ya mbinguni hudumu milele.
Kumbuka hazina inayozungumziwa hapa si ile ya kujitunzia akiba yako ya miezi mwili/mwaka mmoja mbele, kwa matumizi ya msingi hapana..lakini ni ile ya kujihakikishia maisha kana kwamba utaishi milele duniani, hiyo ndio inayozaa uchoyo, ubinafsi, na kutoridhika, na kuwa mtumwa wa mali n.k. Hii, Ina hatari kubwa sana, sisi kama watakatifu kesho yetu yapaswa iwe mikononi mwa Mungu, sio katika akiba zetu, kama watu wa ulimwengu huu.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KAMA MHUBIRI USIWE MFANO WA DIOTREFE.
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.
KWA KUVUMILIA AKAIPATA ILE AHADI.
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Jibu: Kutoka 40:20 “Akautwaa ule ushuhuda, akautia ndani ya sanduku, akaiweka miti ya kuchukulia juu ya sanduku, akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku”.
Kiti cha Rehema kilichokuwa juu ya Sanduku la Agano hakikuwa “kiti” kama viti hivi tuvijuavyo, vyenye miguu minne, na vyenye nafasi ya Mtu kuketi.. Bali neno “kiti” kama lilivyotumika hapo limemaanisha “Nafasi ya wazi”.
Kwahiyo juu ya sanduku la Agano hakukuwa na Kitu Fulani mfano wa “Stuli” juu yake, hapana! bali palikuwa na nafasi wazi ambayo ndiyo iliyoitwa “kiti cha rehema”. Nafasi hiyo ilikuwa ipo katikati ya wale Makerubi wawili wa dhahabu ambao walikuwa wanatazamana, na mbawa zao kukutana kwa juu na kuifunika hiyo sehemu ya wazi (yaani kiti cha rehema).
Nafasi hiyo haikuwa kubwa sana, na pia ilikuwa ni sehemu ya mfuniko wa Sanduku zima (maana yake wale Makerubi wawili pamoja na kile kiti cha rehema vilikuwa vimeungana, na kwa pamoja kufanya mfuniko wa sanduku), na ndani ya sanduku kulikuwa na Mana, zile Mbao za mawe zenye amri kumi pamoja na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka. (Tazama picha juu).
Hivyo ulipofika muda wa Upatanisho, Kuhani Mkuu aliingia na damu Ng’ombe na kwenda kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema mara saba, na damu hiyo inakuwa ni upatanisho kwa wana wa Israeli, dhidi ya dhambi zao.
Walawi 16: 14 “Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba”.
Katika Agano la kale, Israeli walikitazama hicho kiti cha Rehema kama kitovu chao cha kwenda kupata msamaha, kupitia kuhani mkuu wao aliyeteuliwa kwa wakati huo.
Lakini kiti hicho cha rehema kilikuwa na mapungufu yake, kwasababu watu hawakuwa wanapata msamaha wa dhambi, bali dhambi zao zilikuwa zinafunikwa tu!, na kulikuwa na kumbukumbu la dhambi kila mwaka….kwamaana damu za Ng’ombe na Kondoo haziwezi kuondoa dhambi za mtu, vile vile Makuhani wa kibinadamu ambao nao pia wamejaa kasoro hawawezi kuwapatanisha wanadamu na Mungu, kwasababu wao pia ni wakosaji!.. Na pia kiti cha rehema ambacho kipo duniani, kilichotengenezwa na mikono ya wanadamu hakiwezi kufanya utakaso mkamilifu wa dhambi, kwasababu na chenyewe kimetengenezwa na mikono ya watu wenye dhambi..
Hivyo ni lazima kiihitajike kiti kingine cha Rehema kilicho kikamilifu ambacho hakijatengenezwa na mikono ya wanadamu, na vile vile ni lazima ipatikane damu kamilifu ya Mwanadamu asiye na kasoro, na hali kadhalika ni lazima apatikane kuhani Mkuu ambaye hana dhambi..Ndipo UTAKASO na UPATANISHO WA MWANADAMU UWE KAMILI.
Na kiti hicho cha Rehema kipo Mbinguni sasa, na kuhani Mkuu mkamilifu tayari tumepewa, ambaye si mwingine zaidi ya YESU, na damu kamilifu isiyo na kasoro imeshamwagwa kwaajili yetu, na damu hiyo si NYINGINE ZAIDI YA DAMU YA YESU. Hivyo Msamaha mkamilifu unapatikana sasa, na upatanisho mkamilifu unapatikana sasa kupitia Damu ya YESU, kwa kila aaminiye.
Waebrania 9:11 “Lakini Kristo akiisha kuja, ALIYE KUHANI MKUU wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa HEMA ILIYO KUBWA NA KAMILIFU ZAIDI, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu
12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali KWA DAMU YAKE MWENYEWE aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele”.
Je umemwamini Yesu na kuoshwa dhambi zako? Na kupata ukombozi mkamilifu?. Kama Bado unasubiri nini? Kiti cha Rehema kipo wazi sasa, lakini hakitakuwa hivyo siku zote, siku si nyingi baada ya unyakuo kupita mlango wa Neema utafungwa.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.
SWALI: Bumbuazi la moyo ni nini? Kama tunavyosoma katika
Kumbukumbu 28:28 “BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
JIBU: Pale mtu anapopatwa na mshangao, unaomfanya ashindwe kuongea neno hata moja, au anapopigwa na butwaa..hapo tunasema mtu huyo amepigwa na bumbuazi..
Kwamfano bumbuazi linaweza likaja pale unapopishana na ajali Fulani mbaya ambayo ingekusababishia kifo, mfano labda unanusurika kugongwa na Lori la mchanga,kwa kawaida hali kama hiyo inaweza ikakufanya uwe nusu mwendawazimu hujui la kutenda muda huo, hilo ndio linaloitwa bumbuazi..
Sasa linapokuja bumbuazi la moyo, maana yake unakuwa kama mtu asiyeweza kufikiri lolote, rohoni, mtu aliyeachwa njia panda, uliyechanganyikiwa, huna ueleweko, hujielewi ni wapi unapaswa usimame..
Hiyo ndio mojawapo ya laana ambayo Mungu aliitoa kwa watu wote ambao wanaicha sheria yake, na maagizo yake..Alisema..
Kumbukumbu la Torati 28:15, 27-29
[15]Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata….
[27]BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
[28]BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na KWA BUMBUAZI LA MOYONI;
[29]utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
Hali hii ni mbaya, kwasababu inakufanya usiwe na uwezo wowote wa kuchanganua mambo ya rohoni. Unakuwa upo upo tu, huoni mbele, wala huelewi kinachoendelea.
Watu waliopigwa na bumbuazi hili huwa hawajali injili inayohubiriwa kwao hata kama ni kali namna gani, hata kama ukiwaambia Bwana asema “kesho” utakufa..Wataishia kukucheka tu.
Mfano wa hawa ndio wale wakwe zake Lutu, ambao alipokwenda kuwaambia juu ya uharibifu ambao Mungu anauleta juu ya Sodoma na Gomora..alionekana kama anacheza tu machoni pao.
Mwanzo 19: 14 ‘Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze’.
Leo hii, usiwaangalie wanadamu wanaodhihaki injili, wanaosema huyo Yesu mnayemsubiria miaka 2000 sasa yuko wapi..usiwaangalie hao…wengine tayari Mungu kashawapiga bumbuazi hili la moyo..
Ikiwa wewe unashuhudiwa ndani kwamba wakati umefika wa kumwamini Yesu na kujitwika msalaba wako na kumfuata, ni heri ufanye hivyo, bila kujali umati wa watu…okoa nafsi yako kama Lutu. Kwasababu mapigo kama haya Mungu anaendelea kuyaachilia kwa kasi sana kwa watu wanaokaidi amri zake.
Ithamini neema ya Kristo inayougua ndani ya moyo wako leo hii…kwasababu hiyo haitadumu milele, na wengi wameshaipoteza, kwa kutoitii sauti ya Kristo.
Maran Atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “wazimu” katika biblia?
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?
Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)
Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)
SWALI: Mstari huu unamaana gani?
Mithali 18:9 “Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu”.
JIBU: Mharabu ni neno linalomaanisha “Mharibifu”.. Hivyo hapo anaposema yeye aliye mvivu katika kazi yake ni ndugu yake aliye mharabu. Anaonyesha ni jinsi gani uvivu katika kazi, unavyokwenda sambamba na uharibifu wa vitu/mambo. Kama mtu na ndugu yake.
Kwamfano, mtu anayefanyakazi chini ya ubora, labda tuseme mkandarasi wa daraja, .. Kwasababu, hawi makini na kazi yake, atajenga daraja bovu, sasa licha ya kwamba atapoteza pesa nyingi za watu waliompa hiyo kazi, lakini pia anaweka maisha ya wengi hatarini, siku likikorongoka wengi watapoteza maisha. Sasa huyu hana tofauti na mharibifu, au Yule muuaji.
Watu wengi wamesababishiwa matatizo ya kiafya, kwasababu wamekula vyakula vilivyotengenezwa chini ya ubora. Mtu mvivu hutafuta njia ya mkato, ili kufikia malengo yake, na hiyo ndiyo inayopelekea kusababisha madhara kwa wengine..
Hata katika kazi ya Mungu, watu wengi wakiona jambo walilolitarajia linakawia au linapatikana kwa ugumu, huanza kutafuta njia za mkato kwa kutunga mafundisho ya uongo, na kutumia njia ambazo Mungu hajaziruhusu, lengo ni ili wawapate watu wengi kiharaka. Hatuwezi kusubiri, kwa kuomba na kujifunza kwa kipindi kirefu, mpaka tutakapokomaa, badala yake tunaruka madarasa ya Mungu, tunaona njia ya jangwani itatuchosha, haina faida, hatupati chochote, wacha tuifuate njia ya kora .. Matokeo yake tunafanya kazi ya Mungu chini ya ubora, tunawapotosha wengine, kwa elimu na injili gheni.
Maandiko yametutahadharisha sana katika kuitenda kazi ya Mungu, yanasema.
Yeremia 48:10 “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu..”
Tukiitwa kumtumikia Mungu, katika nafasi yoyote, iwe ni uchungaji, uimbaji, utume, ushemaji n.k. tukubali na gharama zake. Kwamba “tumeaminiwa uwakili” kama alivyosema mtume Paulo, tukijua kuwa siku ya hukumu tutaona hesabu ya utumishi wetu (1Wakorintho 9:16-17). Hivyo tuwe makini katika hilo, tusije tukawa waharibifu, kwa uvivu wetu.
Bwana atusaidie.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mharabu ni nani katika biblia?
SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.
Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?
Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu?
Nini maana ya “Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea;?
Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?
Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?
Hii ni orodha ya Imani potofu, ambazo ndani yake zina uongo, unaotaka kukaribiana na ukweli.
1.IMANI YA MUNGU BABA.
Hii ni imani ya kwanza ambayo ni ya kujihadhari nayo kwasababu ni kutoka kwa Yule Adui asilimia mia moja. Imani hii inaelekeza kuwa Mamlaka ya Bwana Yesu duniani sasa hivi haipo!, imekwisha na sasa iliyopo ni mamlaka ya Mungu Baba!.
Imani hii inazidi kuelekeza kuwa unyakuo wa kanisa ulishapita, na hakuna chochote sasa tunachokisubiri, na hakuna haja ya utakatifu wa nje!
Imani hii haimtaji shetani kama shetani, bali inamtaja shetani kama “Kerubi”, jambo ambalo sio sahihi, kwasababu shetani alikuwa kerubi alipokuwa mbinguni lakini sifa hiyo aliipoteza baada ya kutaka kuabudiwa, na kutupwa chini akalaaniwa na kuwa shetani, kwahiyo sasahivi haitwi tena Kerubi, bali shetani na ibilisi, Yule joka!.. Makerubi wamebaki mbinguni, wakimtukuza Mungu na kumwabudu, ambao ni watakatifu na wasafi.
Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, AITWAYE IBILISI NA SHETANI, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye”
Imani hii imeanzia Afrika mashariki, katika nchi ya Tanzania, Mwaka 2003 na muasisi wa Imani hiyo, alijiita Eliya na Adamu wa pili, shetani anaipalilia kwa kasi imani hii na inalenga lile kundi ambalo halipendi kusoma Neno, bali linasubiria tu kupokea na kutazama uzuri wa nje!..
Tahadhari: Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya”.
2. IMANI YA IBADA ZA WAFU.
Hii ni imani inayoamini kuwa wafu wanaweza kutuombea, au tunaweza kuwaombea!..Imani hii inapatikana katika dini nyingi na madhehebu mengi, ikiwemo dini ya kikatoliki. Imani hii ni imani kutoka kwa shetani asilimia mia moja! Na haina ukweli wowote kimaandiko. Lengo la shetani kuizindua imani hii duniani ni ili kuwatumainisha watu kuwa kunayo nafasi nyingine ya kutengeneza mambo baada ya kifo!..
Hivyo kwa wanaoifuata inawafanya wastarehe katika dhambi zao!.. wakiamini kuwa hata wakifa watakatifu waliopo duniani watawaombea na Mungu atawapunguzia adhabu..
Neno la Mungu linasema kuwa mpatanishi wa sisi na Mungu ni YESU TU PEKE YAKE!...
1Timotheo 2:5-6 “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake”
Na anatupatanisha si kwa kusubiri tufe! Hapana! Bali angali tukiwa hai baada ya kumwamini!.. Tukifa katika dhambi zetu kazi yake yakutupatanisha na Mungu inakuwa haipo, tutakachokuwa tunangoja baada ya hapo ni hukumu!… yeye mwenyewe alisema hivyo katika Yohana 8:24
Yohana 8:24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”.
Na ndio maana kuna umuhimu wa kumpokea Yesu na kuoshwa dhambi hapa duniani!, lakini tukifa na dhambi zetu bila kutakaswa tumekwisha!
Vile vile hakuna mwanadamu yeyote mbinguni, au duniani au kuzimu anayeshughulika na habari zetu sisi tulio hai kutuombea au kutusikiliza.. anayetuombea sasahivi na kushughulika na mambo yetu sisi tulio hai ni mmoja tu ambaye ni YESU KRISTO, na hatuombei tukiwa tumeshakufa!.. anatuombea sasahivi angali tukiwa hai kwamba tusamehewe na baba pale tunapoungama dhambi zetu kwa kumaanisha kuacha dhambi!.. Baada ya kifo hakuna maombi yoyote ya upatanisho kwaajili yetu. (1Yohana 2:1).
Na wala hakuna mahali popote katika biblia panapoonyesha mtakatifu yeyote aliyekufa akiwaombea walio hai, wala hakuna sehemu hata moja katika biblia nzima inayoonyesha au kurekodi mtakatifu mmoja aliye hai kamwombea marehemu..
Kwahiyo imani ya watakatifu waliokufa kutuombea haina msingi wa kimaandiko, bali ni uongo wa shetani, ambao una sumu kali, na si wa kuupokea wala kuuamini, bali kujiepusha nao.
Tahadhari: 1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe”
Usikose sehemu ya pili….
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Tukiijua nguvu Mungu aliyoiweka katika injili, basi tutakwenda kuihubiri kwa bidii zote.
Wengi wetu tunasubiri tufikie kimo Fulani cha maarifa ndipo tukahubiri, wengine tunasubiri tupate upako Fulani au uweza Fulani ushukao juu ndipo tukahubiri.. wengine tunangoja unabii na maono au sauti utuambie tukahubiri ndipo tukaianze kazi hiyo… Wengine tunasubiri tupitia kwanza madarasa fulani ya theolojia ndipo tukaitangaze habari njema.. Kuanzia leo anza kufikiri tofauti!..
Hebu tusome maandiko yafuatayo…
Warumi 1:15 “Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi.
16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni UWEZA WA MUNGU UULETAO WOKOVU, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.
Hapo mstari wa 16, maandiko yanasema “INJILI NI UWEZA WA MUNGU UULETAO WOKOVU”.. Kumbe injili ni “UWEZA” yaani nguvu au maajabu… na Zaidi sana si wa mwanadamu bali wa Mungu. Ikiwa na maana kuwa NGUVU ILIYOPO KATIKA INJILI, inatoka kwa Mungu..na wala si kwetu!.
Tukilijua hili tutapata ujasiri wa kwenda kuhubiri bila hofu, bila mashaka yoyote… bila woga wowote, kwasababu katika kuhubiri ndipo Mungu atashughulika katika kuuingiza wokovu katika watu, na wala si kazi yangu mimi kuwageuza watu!.. kwasababu Injili yake NI UWEZA WAKE, ambao unaleta wokovu ndani ya mtu.
Ndugu baada ya kumwamini Bwana Yesu kama Mwokozi wa maisha yako, na kutubu kwa kumaanisha kuziacha dhambi na kubatizwa fahamu kuwa tayari umekidhi vigezo vya kwenda kuwahubiria wengine habari njema… usingoje ufikie ukamilifu Fulani!.. usingoje uanze kunena kwa lugha, usingoje uanze kuona maono!.. wewe nenda kahubiri hayo ambayo tayari umeshayajua.. na utaona uweza wa Mungu kwa hicho utakachokwenda kukihubiri.. utaona Mungu akiwaokoa watu na kuwafungua katika hicho hicho kidogo ulichonacho, kwasababu Injili ni UWEZA WA MUNGU!, na si uweza wa mwanadamu!.
Utasema tunazidi kulithibitisha vipi hili kimaandiko.
Rejea wakati Bwana Yesu anawatuma wanafunzi wake wawili wawili kwenda kuhubiri, utagundua kuwa Bwana Yesu alianza kuwatuma wanafunzi wake hata kabla ya Pentekoste…na waliporudi walirudi kwa kushangilia jinsi watu walivyokuwa wakifunguliwa…
Petro alianza kuhubiri hata kabla ya kupokea Roho Mtakatifu, wewe leo unasubiri nini?.. Petro na mitume wote wa Bwana Yesu waalianza kuwaeleza watu habari toba na msamaha wa dhambi hata kabla ya kunena kwa lugha!, je wewe uliyemwamini Yesu leo unasubiri nini?.
Luka 10:17 “Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako”
Hicho kidogo ulichonacho kinaweza kuleta mabadiliko makubwa sana ndani ya watu, endapo ukiamua! Kwasababu injili NI UWEZA WA MUNGU wa kuwaokoa watu na si uweza wako wewe au mwanadamu mwingine yoyote.
Amka hapo ofisini kwako, anza kuhubiri habari za Yesu, usijiangalie kama unaweza kuongea au la!.. wewe hubiri Bwana atakuwa na wewe katika kuzungumza…kwasababu kuna UWEZA wa kiMungu katika maneno ya injili.. Wakati unahubiri watu hawataangalia kasoro zako bali watalisikiliza lile Neno la litawageuza.. na baada ya pale utashangaa jinsi Bwana anavyofanya kazi.
Bwana akubariki.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!
Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?