Nakusalimu katika jina la Mkuu ya uzima, Mfalme wa wafalme, Bwana wetu Yesu Kristo. Sifa heshima na utukufu vina yeye milele na milele Amina.
Karibu tujifunze biblia. Leo tutatazama viashiria vikuu vitakavyomtambulisha huyo mpinga—kristo ambaye anatarajiwa kuja duniani. Kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na mikanganyiko mwingi, kuhusiana na ujio wake, na chapa yake ya 666, na hiyo imepelekea wengine kudhania kuwa mpinga-Kristo ni mkuu wa freemason atatokea kuzimu au ni ugonjwa wa Corona, kwamba mtu akichanjwa tayari ameshaipokea hiyo chapa ya 666. Lakini je! Biblia inatufundisha hivyo?
Ni kweli Bwana Yesu alisema wapinga-kristo wengi watatokea duniani, ambao kimsingi hadi sasa wapo wengi, lakini yupo mmoja ambaye atakuja. Ili kuleta uharibifu huku ulimwenguni (Soma 1Yohana 2:18). Ambaye ndio huyo tutakayekwenda kusoma tabia zake, na kwamba tukiona hizo zote zipo ndani yake, basi tujue ule mwisho umefika, tayari ameshafunuliwa, dunia imebadikiwa na kipindi kifupi sana zisichozidi miaka 7 (2Wathesalonike 2:1-6).
Zifuatazo ni tabia zitakazomtambulisha.
1) ATATOKEA KATIKA DINI KONGWE.
Mpinga-kristo tofauti na watu wanavyodhani kwamba atazuka tu ghafla kama mwanaharakati Fulani, pasipokuwa na chanzo, hapana, biblia inatuonyesha atatokea katika utawala utakaokuwa unaongoza ulimwengu wakati huo, ambao ulishawahi kuongoza pia hapo kabla, Na utawala wenyewe ni Rumi-ya-rohoni, na utakuja kupata nguvu tena kipindi cha kukaribia mwisho wa dunia, na utafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu tu, yaani kwa maelezo mafupi ni kuwa mpinga-Kristo hatotokea mahali pengine isipokuwa katika ofisi ya UPAPA.
Ufunuo 17:11 “Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu”
2) DUNIA NZIMA ITAMSTAAJABIA:
Tabia nyingine ni kuwa dunia nzima itamstaajabia, kustaajabia maana yake ni kushangazwa na matendo yake, na ukuu wake, ikiwa na maana atakubalika sana na makundi yote, biblia inasema mataifa yatakubaliana naye, na watu wa itikadi zote, na kabila zote, na jamii zote za watu ulimwenguni. Hakuna hata mmoja atakayemwona kuwa ni mtu mwovu, isipokuwa tu wale masalia machache yatakayokuwa yamebaki duniani wakati huo.
Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule….
8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”.
Lakini sio Corona, au mtu Fulani mbaya, mwenye mapembe ambaye, leo hii anaogopeka, hapana mpinga-Kristo ataonekana ni mkombozi wa ulimwengu wakati huo.
3) ATAITWA MTU WA AMANI:
Sio mtu wa vurugu, au mchinjaji, kwani mikakati atakayokuwa ameipanga na ulmwengu, italenga katika kuleta amani ya dunia, na hivyo jambo lolote atakalolianzisha, au mfumo wowote atakaouleta duniani utapokewa na mataifa yote kwa moyo mmoja, na huko huko atapatia nguvu ya kuileta chapa yake yenye 666 ndani yake, na kwamba hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kuuza au kununua asipokuwa nayo.
Danieli 11: 21 “Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.
22 Na wale wenye silaha mfano wa gharika watagharikishwa mbele yake, na kuvunjika, naam, mkuu wa maagano pia”.
4) ATAKUJA NA ISHARA NA MIUJIZA YA UONGO:
Mpinga-Kristo atakuwa na uwezo pia wa kufanya miujiza, Kwasababu roho ya shetani itakuwa nyuma yake, mfano wa Yane na Yambre kipindi kile walipokuwa wakishindana na Musa, ambao tunaona nao pia shetani aliwapa uwezo wa kufanya miujiza,. Ili tu kushindana na kuwapinga watakatifu wa Mungu. Hivyo mpinga-Kristo naye atakuwa na uwezo huo wa shetani,lengo likiwa ni kuwachukua wale ambao watadhani ni yeye ni mpinga Kristo.
2Wathesalonike 2:8 “ Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu”
5) ATATAKA KUABUDIWA KAMA MUNGU.
Kwasababu atakuwa ni mtu wa rohoni, na vilevile mtu wa mwilini, lengo lake litakuwa ni kufikia kilele cha kiti cha enzi cha Mungu duniani. Atataka watu wamwone yeye kama Mungu,.Hivyo atajiinua juu ya dini zote, na madhehebu na imani zote duniani, ili apewe sifa na utukufu kana kwamba ni yeye ni Kristo.
2Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu”.
6) ATATOA MANENO YA MAKUFURU.
Kutaka kuwa kama Mungu tu peke yake haitoshi, bado atakuwa anaitukana njia ya wokovu, Ataukandamiza ukristo wa kweli pia, atadiriki kumtakana Mungu anayeabudiwa na watakatifu. Ili tu aonekane yeye ndio kila kitu.
Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa”
7) HESABU YA JINA LAKE ITAKUWA NI 666.
Vilevile jina lake litakuwa ni hesabu ya 666. Yaani ukizihesabu tarakimu za jina lake, ni lazima ziishie na jumla ya 666
Ufunuo 13:16 “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Sasa haya yote kwa jumla ukiyaona kwa wakati mmoja ndani ya huyo mtu mmoja, basi ujue huyo ndiye mpinga-Kristo mwenyewe, ambaye ataipelekea duniani ifikie kiama chake. Wakati huo ukifika dunia haitakuwa na zaidi ya miaka 7 tu mpaka itakapoisha, Na kulingana na maandiko watakaokumbana na kazi zake ni wale wote ambao hawatakwenda katika unyakuo, ambao hivi karibuni unakwenda kutokea.
Huyu mpinga-Kristo ataleta dhiki kubwa sana kwa wale watakaoachwa katika unyakuo. Kwasababu hutaruhusiwa kuuza wala kununua kama huna chapa yake. Ni dhiki ambayo watu watatamani vifo lakini vifo vitawakimbia.
Dalili zote zimeshatimia, Na huyu mtu wakati huu pengine anaishi duniani, ndio, anaishi duniani, kwasababu atatokea katika dini kongwe duniani, ya kirumi, katika kiti cha UPAPA,.kinachongojewa tu ni unyakuo wa kanisa, na baada ya hapo, aanze kutenda kazi yake ya kuuharibu ulimwengu. Huyu ndio lile Chukizo lenyewe la uharibifu linalozungumziwa katika maandiko.
Ndugu Je! Hadi sasa upo upande gani, Yesu akirudi leo utakuwa mgeni wa nani huko uendako?. Jibu unalo.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze tena maandiko siku ya leo. Kwasababu Neno la Mungu ndio mwanga wa njia zetu na taa iongozayo miguu yetu. Maana yake tukiwa na Neno la Mungu vya kutosha ndani yetu basi njia ya maisha yetu itakuwa wazi, tutakuwa tunajua tulikotoka, tulipo sasa na tunapokokwenda…kwasababu ile Nuru inamulika nyuma yetu, mahali tulipo na mahali tunapoelekea.
Kama wengi wetu tunavyojua kuwa muunganiko wa madhehebu na dini ni mpango wa Yule Adui. Lakini unaweza kujiuliza ni kwanini uwe ni mpango wa Adui na ilihali tunajua kuungana ni jambo jema na zaidi ya yote Biblia imehimiza tuwe na umoja.(Yohana 17:11, Yohana 17:21, Waefeso 4:3 na Waefeso 4:13)..Mistari yote hiyo inazungumzia suala la umoja. Lakini kwanini huu muunganiko wa madhehebu na dini usiwe ni mpango wa Mungu?. Kama kweli ni mtu wa kutafakari hili swali ni lazima utajiuliza..Na kama hutachunguza kwa makini unaweza ukajikuta unakubaliana nalo na kusema hakuna ubaya wowote kuwepo umoja huo au unaweza kujikuta unakuwa tu mshabiki wa kuupinga lakini usijue ni kwanini unaupinga..
Hivyo leo kwa neema za Bwana tutaangalia kasoro moja iliyopo katika muungano huo kwa kutumia Biblia na mifano dhahiri katika maisha …ambayo hiyo ndio itakayotufanya tuhukumu wenyewe kama kweli ni mpango wa Mungu au sio mpango wa Mungu..
Kabla ya kwenda kwenye biblia hebu tafakari mfano huu kisha tutakwenda kwenye maandiko..
Wanandoa wawili ambao wamefunga ndoa halali mbele ya madhabahu ya Mungu…wamegombana na kuachana na kila mmoja akaenda kuoa na kuolewa na mwingine…na huko walikokwenda kila mmoja akapata watoto..na wakawa wamekaa katika hali hiyo muda mrefu sana miaka mingi sana ikapita pasipo kuonana wala kuwasiliana kwa ufupi kila mmoja akawa ameanza maisha yake mengine na ana mipango yake…
Siku moja katika shughuli zao wakakutana mahali pamoja pa kazi kila mmoja akiwa na mpenzi wake mpya na watoto wake…
Sasa kwasababu tayari kila mmoja ana mpenzi wake mpya na familia mpya, na walishaachana kitambo na wameshakuwa watu wazima sana hata ule upendo haupo tena…. ikabidi watambulishane tu kwamba huyu alikuwa ni mpenzi wangu wa zamani lakini tulishaachana kitambo sana..kila mmoja akamtambulisha mwenziwe na sasa hatuna mahusiano yoyote…lakini kwasababu wote tumekutana na shughuli yetu ni moja basi hebu tushirikiane tufanye kazi pamoja tujiendeleze kiuchumi na kutunza familia zetu..
Hivyo familia hizo mbili zikaungana kufanya kazi pamoja…kwahiyo kukawa na kaumoja Fulani lakini si cha mahusiano bali cha maslahi fulani. Familia hizo zikawa zinakutana kuuziana bidhaa na kushirikishana fursa mpya za kazi, na kutekeleza mipango mengine ya kimaisha n.k..
Sasa hebu jiulize?..Huo muungano ni muungano wa ki-Mungu?…Ni kweli wameungana, wanasadiana kiuchumi, kimawazo na hata kifursa lakini mbele za Mungu wanaonekanaje?..Mbele za Mungu wanaonekana ni wazinzi na waliotengana…maandiko yanasema hivyo…
Luka 16:18 “Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini”.
Haijalishi watafanya vitu vingapi kwa umoja, mbele za Mungu wanaishi katika uzinzi, haijalishi wameachana kwa makubaliano mazuri kiasi gani, haijalishi watakwenda pamoja kusaidia mayatima na maskini kwenye makambi lakini mbele za Mungu bado ni wazinzi..Na hivyo huo umoja ni umoja wa shetani hata kama wanafanya mema elfu, wakifa wote wanakwenda motoni…Kwasababu Mungu hawezi kuunganisha wazinzi wawili wapatane..Badala yake Mungu angewarudisha kwanza warudiane ili wasiishi katika uzinzi..na ndipo hayo mambo mengine yafuate.
Ili uwe umoja wa KiMungu ilikuwa ni sharti kila mmoja amrudie mpenzi wake wa kwanza ambaye walifunga naye ndoa kanisani, na kuachana na huyu aliyenaye sasa….Endapo wangerudiana na kuungana kwa namna hiyo, hapo mbele za Mungu wangekuwa wameungana na hivyo ungekuwa tayari ni umoja upo katikati yao.
Ndicho kinachotokea kwenye madhehebu sasa…Shetani kawatenganisha wakristo na kuwaweka katika makundi makundi…dhehebu hili, na lile…kaondoa ule umoja wa Roho ambao ulianza pale Pentekoste ambapo hakukuwa na dhehebu lolote wote walikuwa wamoja…
Matendo 2: 44 “Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika”.
Mitume hawakuanzisha madhehebu…waamini wote walikuwa ni kitu kimoja…Sasa shetani kashatutenganisha..halafu anataka kutuunganisha katika hali ya matengano tuliyopo…tupo tumetengana na bado anataka tuungane tusaidiane kifursa, TAG na EAGT tuungane tusaidiane kutatua matatizo Fulani Fulani ya kijamii, Lutheran na katoliki tuungane, Anglikana na Morovian tuungane ili tushirikiane kutatua kwa pamoja matatizo Fulani Fulani. Wakati kila mmoja msingi wa Imani zetu zimepishana.
Je! unadhani huo ni mwunganiko wa kiMungu?…La! hata kidogo sio muunganiko wa kiMungu kabisa… Ili uwe muunganiko wa kiMungu ni sharti wakristo wote tungepaswa tuungane na kuwa kitu kimoja katiba yetu ikiwa biblia na si kuunganisha madhehebu…pasipowepo kusema mimi ni wa dhehebu hili au lile..wote jina letu linapaswa liwe moja (wakristo), huo ndio umoja wa Roho unaozungumziwa katika maandiko kwamba tunapaswa tuwe nao..
Ni sawa na kijana kapewa gunia la mchele la kila 50, na akaambiwa akifika nyumbani auchanganye vizuri na kuutoa uchafu na kisha ahamishie ule mchele kwenye gunia lingine lililosafi zaidi…na kijana alipofika nyumbani akalifungua akaanza kutenga ule mchele kuuweka kwenye vifungashio tofauti tofauti .. akatenga kilo 5 akazifungia kwenye mfuko, kilo nyingine kumi kwenye gazeti, kilo nyingine 2 kwenye kichupa kidogo, nyingine 4 kwenye kopo nyingine 8 kwenye kijimfuko cha rambo nyingine 10 kwenye kiroba na hicho kiroba akakipiga lebo..mpaka zilipotimia zote 50. Na akavichukua hivyo vifungashio vyote na viroba vyote akavitumbukiza kwenye gunia hilo jipya la kila 50.Na kusema tayari kauleta pamoja ule mchele…hapo kauleta mchele pamoja au viroba pamoja?..Atakuwa hajatumia akili kwasababu alipaswa aumimine mchele wote uliosafi kwenye lile gunia moja haikuhitajika tena kufungwa matita matita. Na madhehebu yote ni vifungashio…ndani ya Gunia kuu la ukristo.
Na vifungashio hivyo Mungu kavikataa..Ndio maana anasema katika Ufunuo 18: 4 “Tokeni kwake enyi watu wangu..msishiriki dhambi zake”..Maana yake tutoke kwenye kamba za udini na madhehebu…tuunganike wakristo na si madhehebu..
Ndio Mungu kaweka tofuati ya utendaji kazi katika kanisa, Lakini kumbuka ni utofauti wa utendaji kazi, na sio utofauti wa Imani,..Leo hii katika ukristo zipo Imani tofauti tofauti haiwezekani mmoja anaamini mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja tu Yesu Kristo, mwingine anasema pembeni ya Yesu kuna mwingine anayeitwa Mariamu n.k. Halafu hao wote bado wawe kitu kimoja. Na kibaya Zaidi umoja huu unalenga kufikia hadi kuunganika na dini nyingine zisizomtambua hata Kristo.
Sasa tukirudi katika maandiko madhara ya muunganiko huo ni nini?
Madhara ya muunganiko wa madhehebu ni kuitengenezea njia roho ya Mpinga kristo kufanya kazi…Kumbuka Mpinga-kristo atakuwa ni mtu wa kidini na atakuwa mshirika wa muungano huo..Roho ya kumpinga kristo haianzii freemason, kama wengi wanavyofikiri, wala kwa waislamu, wala kwa mabudha…roho ya mpingakristo inaanzia kwenye huu umoja wa dini na madhehebu…Waliompinga Kristo wa kwanza wakati akiwa hapa duniani hawakuwa wachawi, wala watu wa mataifa bali walikuwa ni mafarisayo na masadukayo (watu waliokuwa wameshika sana dini).
Sasa mafarisayo na masadukayo yalikuwa ni madhehebu ya kiyahudi…Kila moja lilikuwa linadai linamjua Mungu zaidi ya lingine…hivyo yakatengana kama madhebu yalivyotengana leo..na baada ya kutengana wakati Bwana Yesu anakuja na kuhubiri…yakainuka yote kumpinga Bwana Yesu na kufanya shauri pamoja ya kumuua…Na muunganiko wa madhehebu leo hii utakuja kusimama kuwapinga wakristo wakweli katika siku za mwisho, na kuwaletea dhiki.
Yohana 16:2 “Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada”.
Na yatamtengenezea njia pana Mpinga-Kristo ambaye atanyanyuka na kuutumia huo muungano kuiunda ile CHAPA YA MNYAMA. Ambapo itafikia kipindi watu hawataweza kununu wala kuuza bila kuwa mshirika wa umoja wa muungano huo.
Mathayo 22: 34 “Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja”.
Je upo chini ya kifungashio gani? Cha Neno la Mungu au cha dhehebu lako?..Je unajisifia dhehebu au Imani?..Hebu jifikirie tangu upo katika dhehebu lako umejifunza kuhusu kumjua Yesu kiasi gani?..unamjua Mungu kiasi gani,Neno unalifahamu na umelishika kiasi gani?..je umekuwa mtakatifu kiasi gani?..una uhakika kwa kiasi gani kwenda mbinguni?..Je umeshawahi kutenga muda mwenyewe pasipo kuambiwa kusoma maandiko?, au kusali au kwenda kuwahubiria wengine habari njema…
Kama hujawahi kufanya hayo na zaidi ya hayo na bado unajiisifia dhehebu…tenga muda ujitafakari tena ndugu yangu…Usijisifie dhehebu, wala usiufurahie kila muungano unaosimama mbele yako…Rudi katika Neno la Mungu ambalo ndio katiba yetu. Unyakuo umekaribia sana, Kristo anakaribia kuja na Mpinga-Kristo kashatengeneza mazingira yake yote ya kufanya kazi zake.
Bwana akubariki.
Tafadhali share na kwa wengine na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya kujifunza kwa njia ya inbox au whatsapp basi utatutumia ujumbe kwa namba hii 0789001312
Mada Nyinginezo:
MPINGA-KRISTO
MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.
Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?
ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
NENO LA MUNGU NI DAWA ILIYO TOFAUTI NA DAWA NYINGINE.
Cheo cha Mpinga-Kristo, kimeshafunuliwa Zaidi ya Karne moja iliyopita huko nyuma, nacho si kingine Zaidi ya cheo cha ki-PAPA, Wakati wa Mwisho utakapofika atanyanyuka mmoja atakayekikalia hicho kiti, ambaye atafanya mambo maovu na ya ajabu, yale yote yaliyotabiriwa katika maandiko matakatifu. Huyo bado hajafunuliwa kwasasa jina lake ni nani?… Lakini hatatoka pengine mbali na kiti hicho cha Kipapa..Lakini kwasababu tunajua majira na nyakati, kwamba hizi ni siku za mwisho, labda huyu aliyeko sasahivi ndiye!..au kama siye miongoni mwa wachache sana wanaokuja huko mbeleni atakuwa mmojawapo!…Huyo ndiye atakayeihimiza chapa! Huyo ndiye atakayeidanganya dunia kuwa ataleta amani! Lakini badala yake ataipeleka kwenye matatizo na kiama.. Na ndiye atakayetafuta kwenda Yerusalemu kwenye Hekalu litakalotengenezwa kule hivi karibuni kule Israeli aabudiwe pale kama Mungu (2Wathesalonike 2).
Vipo viishara vingi vinavyotuthibitishia utendaji kazi wake, katika kizazi chetu…lakini pia kipo kiashiria kimoja kikubwa sana! Cha kutufanya tuzidi kuwa macho na kufunguka fahamu zetu, kujua ni majira gani tunaishi.
Kiashiria hicho si kingine Zaidi ya Roho yake huyo Mpinga-Kristo kuwavaa watu(wanaojiita watumishi),
Leo hatutazungumzia, jinsi hii roho ilivyoyavaa makanisa pamoja na serikali..Bali tutaangalia ni jinsi gani imewavaa wanaojiita watumishi.
Zamani, kusikia Mtu anayejiita mtumishi wa Mungu, kuwa na walinzi wa pembeni (ma-bodyguards) ilikuwa ni jambo la kushangaza sana…Hata hivyo halikuwepo kabisa, kwasababu Bwana Yesu mwenyewe ambaye sisi tunamwita Bwana! Hakuwa na mabody-guards, wapo watu wanasema wale mitume walikuwa ma-bodyguards wake, huo sio ukweli, bodyguard huwa anatembea na silaha na kazi yake ni kumlinda Yule ili asidhuriwe anakuwa tayari hata kuua ili kwamba tu Yule anayelindwa akae salama, lakini Bwana hakuwaita mitume kwa kazi hiyo, ya kumlinda yeye, kinyume chake Petro alipojaribu kufanya hivyo kwa kumkata Yule mtu sikio alimkemea …Zaidi ya yote yeye mwenyewe alijitoa kwa hiyari yake kufa kwa ajili ya wengi, ingawa alikuwa na uwezo wa kuagiza malaika waje wampiganie lakini hakutumia uwezo huo, ili kwamba awe sadaka kwa wengine (soma Mathayo 26:51-54 )…
Na Neno lake linatuambia kama yeye alivyojitoa kwa ajili yetu na sisi pia tunapaswa tujitoe kwa ajili ya wengine. (1Yohana 3:16)
Lakini leo ni kinyume chake utaona Mhubiri anakwenda kuhubiri injili na Mabody-guards ambao wameandaliwa mahususi kumtetea yeye, na ndani ya kifuko yao wamebeba silaha..yote hiyo hataki kufa! au Anaogopa kufa!..Ukimgusia habari za kwenda kuhubiri bila bodygurds anapambana na wewe!..Leo malengo ya wahubiri wengi ni kununua Helikopta na ndege, ili hatimaye waziandike majina yao, na wajulikane dunia nzima, na hatimaye waonekane mbele ya vyombo vya habari ili wapate heshima duniani kote…
Sasa hiyo yote imetoka wapi? Na kwanini haikuwepo kipindi cha nyuma?
Jibu ni rahisi! Hiyo yote ni ile nguvu ya mpinga-Kristo mkuu imewavaa hawa watumishi!….Roho ya Mpinga kristo ndiye inayowafanya watafute fahari na ufalme katika dunia hii, sasa roho hiyo haijaanzia kwao, bali imeanzia kwenye kile cheo cha Mpinga Kristo mwenyewe, (yaani kiti cha upapa)…Papa ambaye anajulikana kama mhubiri maarufu, ndiye Mhubiri pekee aliye kinyume na Kristo, ambaye analindwa na JESHI! Linaloitwa “Swiss guards” linalomzunguka na kumlinda kila anakokwenda..Mabodyguard hao kabla ya kumlinda Papa, wanaapa kuwa tayari hata kuutoa uhai wao ili tu kumlinda Papa asife!…jambo ambalo Kristo aliye Bwana hakufanya, wala hakutamani kulindwa kwa namna hiyo…hivyo si ajabu leo kuwaona hawa wahubiri wengine wadogo wakifanya hayo hayo…wakiajiri mabodygurd kuwalinda hadi madhabahuni..ni roho ile ile ya mpinga-kristo ipo kazini.
Papa ana ndege yake maalumu inayoitwa “Alitalia Flight AZ4000” inayokaribiana sana kufanana na Ndege ya Raisi wa Marekani Airforce one… roho hiyohiyo imewavaa manabii wa uongo wanaozuka sasahivi, nao pia wanafanya juu chini kumiliki ndege kama ya Papa, lengo lao sio kutumia hizo kumuhubiri Kristo, bali kujihubiri wao wenyewe na ufahari wao.
Papa anaabudiwa na ana pete iliyopo mkononi mwake ambao maelfu ya waumini wa kikatoliki, wamkaribiapo ni lazima waibusu, mkononi mwake…roho hiyo hiyo imewavaa manabii wa uongo leo, wanatafuta kwa bidii kuangukiwa na kusujudiwa..na hata watu kuwapa heshima fulani kubwa ya kipekee…Na mambo mengine mengi Papa anayafanya yameshaanza kuonekana kwa wanaojiita wahubiri.
Ndugu tuonapo Mambo hayo yaliyo kinyume na Kristo, ambapo hapo kwanza yalikuwa yanafanyika na mtu mmoja tu Papa, lakini sasa yanafanyika na maelfu ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu, ni wakati wa kunyanyua vichwa vyetu juu, kwasababu ule mwisho umekaribia sana..Ile roho ya mpingakristo imeshateka ulimwengu mzima…kinachosubiriwa ni unyakuo tu! Dhiki kuu ianze..Ni kama ugonjwa! Ulioanzia kichwani kama upele lakini sasa umeenea mwili mzima…hiyo ni dalili mbaya!
Tabia hii, ikishamalizika kusambaa, itamsaidia baadaye mpingakristo kufanya kazi yake kirahisi. Atakapoanzisha chapa, afanye kazi kirahisi kwasababu watakuwepo watu wengi watakaosapoti mambo anayoyafanya…Kwasasa yataonekana si ajabu tena.
Je umeokolewa? Na kama umeokoka una uhakika na wokovu wako? Biblia inasema
2 Petro 1:10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe”
Ufunuo 3:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”.
Bwana akubariki.
Tafadhali share na wengine
Mada Nyinginezo:
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
SWALI: Nina swali kuhusu alama ya mnyama, kulingana na baadhi ya injili zinazohubiriwa ni kuwa ..alama ya mnyama itapimwa kwa siku ya kuabudu, yani wale watakaokubali kusali jumapili wote watakuwa wamepokea 666, ikimaanisha kuwa Papa atatangaza siku moja tu ya kuabudu iwe jumapili dunia nzima, lengo likiwa kuvunja amri ya nne itunze siku ya saba, kwahyo amri ya papa itakapopita itapiga 666 kwa wote watakaokubaliana nayo, wana refer maandiko ya Danieli 7:25 KUWA ATABADILI MAJIRA NA SHERIA.
JIBU: Shalom ndugu, Ni kweli kabisa wapo wanaoamini kuwa Papa atageuza MAJIRA NA SHERIA kulingana na Danieli 7:25….Lakini ukijifunza biblia utagundua kuwa majira yanayozungumziwa hapo sio siku moja maalum itabadilika…hapana! Kwasababu majira ni Neno pana na la wingi ambalo linaweza kuwa kipindi Fulani cha muda…labda cha siku kadhaa, wiki, miezi au miaka kadhaa…kinachoambatana na tukio Fulani. Ili tuelewe vizuri hebu tuchukue mifano kadhaa ya kwenye biblia..
Luka 21: 7 ‘’Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia? 8 Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, MAJIRA YAMEKARIBIA. Basi msiwafuate hao’’.
Katika mstari huo unaona neno MAJIRA lilivyotumika hapo, sio kipindi cha SIKU MOJA MAALUM ambacho kitafika watu watakuja kwa jina lake na kusema wao ndio…Utaona sio tafsiri yake hiyo, bali majira ilivyotumika hapo ni kwamba ‘itafika kipindi Fulani cha muda’ ambacho hakijulikani kitadumu kwa muda gani ambapo watatokea manabii wa uongo wakija kwa jina la Yesu…Na hicho kipindi ndio hichi tunachoishi sasa, Pia tunaweza kujifunza katika huu mfano mwingine Bwana alioutoa..
Luka 12:54 ‘’Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo. 55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua MAJIRA haya?’’
Unaona hapo tena?…Majira yanayozungumziwa hapo ni kipindi Bwana Yesu alichokuwepo duniani akihubiri na kufundisha njia za haki…ni majira ambayo makutano walishindwa kufahamu kuwa Masihi yupo ulimwenguni…Na majira hayo ni kipindi cha miaka mitatu na nusu Bwana aliyokuwa anahubiri..na sio siku Fulani moja maalum. Pia mfano mwingine ni huu..
Kutoka 21:18 ‘’Watu wakigombana, na mmoja akimpiga mwenziwe kwa jiwe, au kwa konde, asife, lakini yualazwa kitandani mwake;atakapoinuka tena na kuenenda nje kwa kutegemea fimbo, ndipo hapo yule aliyempiga ataachwa; ila atamlipa kwa ajili ya hayo majira yake yaliyompotea, naye atamwuguza hata apone kabisa..’’..
Hapo pia utaona ‘majira’ sio siku moja maalumu bali kipindi cha muda. Kadhalika pia tunaweza kujifunza mfano huu wa mwisho maana ya majira..
Luka 21: 29 ‘’Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote. 30 Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba MAJIRA YA MAVUNO yamekwisha kuwa karibu. 31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.’’
Unaona majira ya mavuno yanayozungumziwa katika maandiko sio siku moja MAALUMU, kama wasabato wanavyodhania, bali ni kipindi Fulani cha mavuno ambacho kinaweza kuwa ni siku kadhaa, au wiki kadhaa…Ipo mifano mingi unaweza ukapitia Pia (pitia Luka 21:54-55, Luka 21:23-25, Luka 19:41-44 utaelewa zaidi juu ya jambo hilo).
Kwahiyo tukirudi pale kwenye Danieli 7:25…Kwamba Mpinga kristo atabadili ‘’majira na sheria’’ biblia haikumaanisha kuwa mpinga kristo atakuja kubadilisha siku moja ya kuabudu Jumamosi na kuwa jumapili…Hapana bali MAJIRA yatakayobadilika hapo ni MAJIRA YA mfumo mzima wa maisha, kutoka kuwa ya amani na kuwa ya dhiki, huwezi kununua wala kuuza bila ile chapa…wakati huo Majira ya Neema yatakuwa yameisha na sasa ni majira ya dhiki kuu….yatakuwa ni majira ya mavuno..na hayo hayatakuwa siku moja hapana ni kipindi fulani cha muda ambacho kitadumu miaka mitatu na nusu…Kwahiyo mfumo wake mpya wa umoja wa dini na madhehebu yote ndio utakaobadili majira ya ulimwengu mzima..
Kama vile ujio wa Kristo ulivyobadili majira kutoka majira ya utumwa wa dhambi na sheria na kutuingiza katika majira ya Neema na uhuru wa roho, kadhalika baada ya unyakuo wa kanisa kupita Mpinga Kristo ataiingiza dunia katika majira mapya ya dhiki kuu na ghadhabu ya Mungu. Kumbuka sasahivi tunaishi kipindi cha majira ya Neema ya Kristo, ambacho kinajulikana kama kipindi cha MAJIRA YA MATAIFA.(ukisoma Luka 21:24 utaona jambo hilo) Na kipindi hichi kitaishia na unyakuo. Hivyo fundisho la wasabato linalosema kutotunza sabato, ndio kupokea alama ya mnyama, ni fundisho potofu na linapaswa liepukwe kwasababu halina msingi wowote wa kimaandiko.
Bwana akubariki sana.
Mada Nyinginezo:
SABATO HALISI NI LINI, JE! NI JUMAPILI AU JUMAMOSI?, NI SIKU GANI ITUPASAYO KUABUDU?
LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
KWANINI MUNGU ANAMPA NABII HOSEA MAAGIZO YA KUMUOA MWANAMKE KAHABA?
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, natumai u mzima, karibu tushiriki pamoja maneno ya uzima, leo tutazungumzia juu ya ujio wa mpinga-kristo.
Mpaka sasa dunia inatazamia ujio wa watu wawili huko mbeleni kabla ya mambo yote kuisha, wa kwanza ni KRISTO na wa pili ni MPINGA-KRISTO. Na kila mmoja amekuwa akitazamiwa na watu na bado anaendelea kutazamiwa. Lakini kuna mahali ambapo watu wengi wanakosa shabaha hususani katika namna ya kumtambua mpinga-kristo na utendaji kazi wake. Tambua kuwa njia pekee ya kumjua shetani ni kumfahamu Mungu tu, hakuna njia ya mkato, huwezi kusema unamjua vizuri shetani na huku hata mahusiano yako na Mungu ni mabovu, Neno la Mungu halipo ndani yako Roho wa Mungu yupo mbali na wewe, hapo ni sawa na unajidanganya tu hata kama utasema wewe unamjua shetani namna gani, na ndio hapo utamwona mtu anaishia kudhani shetani ni freemason aliyekaa kuzimu anawatajirisha watu na kuwaambia watoe kafara za watu ili awape utajiri, na kusababisha ajali, na mambo mabaya hilo tu,.na utakuta mtu huyo anapoteza muda wake mwingi kuchunguza ishara na alama kila mahali, na kwenye vibao, vya kichawi ili kujiepusha navyo, utakuta anafahamu alama zote wazitumiazo wachawi. Na kwa hilo anajisifu kuwa anamfahamu shetani, lakini hafahamu kuwa hivyo ndivyo shetani anavyotaka afikirie siku zote, apoteze muda mwingi kuwafahamu wachawi na vikundi vyao, lakini asidhubutu hata kidogo kumfahamu Kristo na Neno lake.
Ndugu usipoifahamu noti original utawezaje kuitambua noti feki, watu wengi wanafikiria kuwa Mpinga-kristo atakuja kuwa ni mtu wa ajabu na wa tofauti, mtu katili sana, mtu ambaye ulimwengu mzima utakwenda mbele yake na kumsujudia na mtu yeyote asipomsujudia atauawa kama kuku, mtu ambaye atawalazimisha watu kwa nguvu wapokee chapa na endapo mtu asipopokea atachinjwa hadharani bila huruma yoyote, atakuwa mtu mkali kupindukia, atakuwa anakunywa damu za watu hadharani n.k..Hivyo hiyo inawafanya watu wastarehe wadhani kuwa bado muda mrefu sana, mpaka atokee mtu wa namna hiyo, bado hajaanza kutenda kazi na siku atakapoanza tutajua…
Lakini turudi katika upande wa pili..watu vivyo hivyo wanadhani YESU yupo mbinguni ametulia , na yeye ipo siku moja atakuja, na siku atakayokuja makaburi yatafunguka na watu wote watawaona wafu wakifufuka, atasimama mawinguni, parapanda italia, malaika wataonekana kila pande, hivyo kwasasa bado unyakuo haujaanza siku utakapotekea siku ndiyo tutakapojua.
Kitu ambacho hatukifahamu mpaka sasa ni kwamba Kristo anakuja katika roho na anawanyakua watu wake mbali na watu waovu, Bwana Yesu hajakaa katika kiti fulani huko mbinguni mpaka sasa miaka elfu mbili imepita akisubiria tu siku moja ifike aje kuwachukua wateule wake, hapana badala yake tangu kuondoka kwake amekuwa na AGENDA, na bado anatenda kazi, na agenda hiyo imekuwa akifanyia kazi kizazi baada ya kizazi, amekuwa akizungumza na watu wake katika kipindi kimoja cha kanisa hadi kingine, vipindi hivyo tunaviona katika kitabu cha ufunuo 2&3. Kila nyakati amekuwa akilinyakua kanisa lake na kulihadhi mahali fulani, hata sasa bado anaendelea kuwanyakua watu wake na kuwahifadhi, na kama utakufa na ule mwisho bado haujakukuta unahifadhiwa mahali fulani ukingojea siku ya kujumuika na wengine watakao kuwa hai na kwenda nao mbinguni.
1Wathesalonike 4.13 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”.
Unaona hapo siku ile unyakuo haimuhusu tu yule atakayekutwa hai hapana bali inawahusu na wale wengine ambao walishakufa wakiwa wanatembea katika mstari wa Kristo kabla ya hapo.
Lakini vigezo vya kunyakuliwa vipo wazi, ni hicho si kingine zaidi ya alama utakayotiwa, au Chapa au Muhuri uliojuu yako..Na muhuri wenyewe si mwingine zaidi ya ROHO MTAKATIFU. Pasipo huo muhuri huwezi Kunyakuliwa ndugu..aidha iwe hai au uwe umekufa..
Waefeso 4.30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; AMBAYE KWA YEYE MLITIWA MUHURI HATA SIKU YA UKOMBOZI”.
Hali kadhalika na kwa mpinga-kristo, hangojewi eti mpaka kipindi fulani kitakapofika ndio adhihirishe kazi zake, ni kweli kwasasa hajatokea lakini biblia ipo wazi kabisa kuwa utendaji kazi wake upo tangu zamani na ile roho inazidi kuendelea kufanya kazi hata sasa,..na kama vile Bwana alivyokuwa na Muhuri au chapa yake, Halikadhalika ibilisi naye anayo chapa yake au Muhuri wake,.Na chapa hiyo ni KU-MPINGA-KRISTO, na mtu anampingaje Kristo? Ni kwa kumkataa Roho Mtakatifu ndani yake..Kuupinga wokovu ndani ya moyo wako..Kuzipinga-kazi za Mungu ndani ya moyo wako…Kwenda kinyume na njia za Bwana, kukaidi maagizo ya Mungu kama shetani mwenyewe alivyo. Kuutua msalaba, kulikosoa Neno la Mungu, kuipuuzia injili na kuona kama ni hadithi za kizee, kuwatukana watu wote wanaoutumainia msalaba. N.k. sasa mtu ukishajiona upo katika hali hiyo basi ujue tayari ulishapokea chapa ya mnyama..Hivyo mtu yeyote atakayekufa leo katika hali hiyo yeye naye atahifadhiwa mahali pa mateso panapoitwa, akisubiria siku ya kukamilishwa kwa wapinga-Kristo wenzake, na kwa pamoja wote wataungana na kwenda kuhukumiwa kwa kupokea chapa ya mnyama, na wote kwa pamoja watatupwa katika lile ziwa la moto.
1Yohana 2: 18 “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo YUAJA, HATA SASA WAPINGA KRISTO WENGI WAMEKWISHA KUWAPO. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.
2Wathesalonike 2:5 “Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 MAANA ILE SIRI YA KUASI HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa”.
Hivyo usidanganyike kuwa ukifa sasa bila kuufika wakati wa mpinga-kristo umeotea, kwamba umeikwepa chapa yake..fahamu kuwa chapa inapigwa hata sasa, na jua kuwa chapa ile ipo katika roho na si mwili kama vile biblia inavyosema wale watakaokutwa hai wakati wa Bwana hawatawatangulia wale waliokufa siku ile ya unyakuo..Hali kadhalika wale watakaopokea chapa ya mnyama wakati ule wa dhiki kuu, hawatawatangulia wale waliokwisha kuipokea zamani kabla ya dhiki kufika;..Watakaosalia katika ile siku ya dhiki kuu, kwa kupitia kitambulisho cha dini na udhehebu wataithibitisha chapa ya mnyama ambayo tayari imo katika roho zao.
Pia biblia inatueleza kuwa Bwana alikuja, akaondoka, na atarudi tena, halikadhalika na yule mnyama biblia inasema, alikuwako, naye hayuko naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu..Hii inatuweka wazi kuwa kazi zilishaanza zamani sambamba na za Bwana wetu Yesu Kristo.
Ufunuo 17:8 “Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako”.
Unaona?, Sasa ni vizuri kufahamu pia Mpinga-Kristo mwenyewe atatokea wapi..Biblia inatueleza atatokea RUMI, katika ule utawala wa mwisho kabisa wa chuma..VATICAN ndiyo yatakayokuwa makao yake makuu, katika kiti cha KI-PAPA…Mpinga-Kristo hatashika bunduki, wala visu, anashika biblia, na anahubiri..lakini injili yake ni ya uongo.
Kwanini usifanye uamuzi sasa wa kumgeukia muumba wako?, hatari uliyonayo ni kubwa kama hutageuka sasa, mambo yote yanakaribia kuisha, ukifa leo katika dhambi huko utaenda kuwa mgeni wa nani. Tafakari hilo, usiishi tu ilimradi siku zinapita, Neema inapatikana bure, uamuzi ni wako, Ni matumaini yangu utatubu leo na kumgeukia muumba wako angali muda upo, saa zaja utakazotamani huu wakati wa sasa lakini utaukosa.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
Papa kiongozi wa kanisa katoliki duniani alipokuwa akihutubia mbele ya maelfu ya watu juni 25, 2014 St. Peter’s Square vatican akisema:
Mafundisho haya yanapingana na biblia ni mafundisho ya mpinga kristo,kulingana na ufunuo 17:5..”katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa kwa siri, BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI” katika maandiko mwanamke anawakilisha kanisa,kwa hiyo mwanamke huyu aliyezungumziwa hapa ni kanisa-kahaba,inamaanisha ni kanisa lililochanganya mafundisho ya neno la Mungu na ibada za sanamu hivyo limemwacha Mungu na kumwabudu shetani ndio maana likafananishwa na mwanamke kahaba na kanisa hili sio lingine zaidi ya kanisa katoliki,
hivyo basi tunaona hapa sio tu kahaba bali pia ni mama wa makahaba,amezaa mabinti ambao ni makahaba kama yeye, nao ni madhehebu yote na mashirika yote ya dini yaliyoiacha kweli ya neno la Mungu na kugeukia mafundisho kama ya mama yao ya kipagani.Leo hii tunaona makanisa yote ulimwenguni yanaungana na kanisa mama yaani katoliki, na kuiunda ile CHAPA YA MNYAMA,ambayo pasipo hiyo huwezi kuuza wala kununua katika kile kipindi cha dhiki kuu,itafika wakati kila mkristo itampasa asajiliwe katika dhehebu lake kwa yeye kutambulika kama ni mkristo vinginevyo hautaweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa,wala kufanya kazi yeyote usipokuwa na hiyo chapa ya mnyama ambayo ni..(utambulisho wako wa kidini au dhehebu lako) pia hautaruhusiwa kuabudu kwa uhuru kama unavyoabudu leo,..kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ataingia katika ile dhiki kuu.
Na kwa jinsi tunavyoiona dunia ya leo vitendo vya ugaidi vimekithiri kutokana na itikadi kali za kidini, shetani ameunyanyua uislamu kuvuruga amani ya dunia kwa kigezo cha itikadi kali za dini,hivyo basi leo dunia inatafuta mtu wa kuleta amani naye ni lazima awe mtu wa dini ili amalize hili tatazo. na yupo mmoja tu duniani sasa anayekubalika na dini zote naye ni PAPA ambaye anajulikana kama mtu wa amani (man of peace) kiongozi wa kanisa katoliki, baadaye atapewa nguvu na dunia ili maandiko ya daniel 11:21 yatimie “Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza”, ataleta ustaarabu mpya wa dunia wa kuleta amani (NEW WORLD ORDER).
Hapo ndipo itakapompasa kila mtu asajiliwe kulingana na shirika lake la dini na dhehebu lake, kwa dhumuni la kuwatambua watu wote, na kukomesha ugaidi, wengi wataliona kuwa ni jambo zuri bila kujua kuwa ndio wanaipokea ile chapa ya mnyama, lakini baadhi ya wale wakristo waliobaki wasiokwenda katika unyakuo hawatakubali kusajiliwa katika madhehebu ya dini, kwasababu watajua kuwa hiyo ndio ile chapa ya mnyama 666 ndani yake, ni hao tu watakao pitia dhiki kuu wakisingiziwa kuwa wao ndio waondoa amani na magaidi, kwa kutokutaka kusajiliwa kwenye dini zao, watakataliwa na watu wote, hawataweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa mahali popote, na mwishoni yule mnyama atawauwa wote akiwa na roho ya mpingakristo
Mkristo leo hii anayedai kutafuta uhusiano binafsi na Mungu kulingana na papa alivyosema ni “hatari na yenye madhara” hii ni roho ya mpinga Kristo inatenda kazi ndani ya papa ikizungumza maneno haya ya makufuru…dhumuni kubwa ni kuizuia Roho ya Mungu ndani ya watu kutenda kazi kwa sababu Roho ya Mungu aliachiwa kwa dhumuni moja tu kutuongoza katika kuijua kweli yote.. na pia yeremia 31:34..” Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana;….
Mtu ataijua kweli tu akiwa na Roho Mtakatifu na wala sio kwa kuwa mshirika wa kanisa lolote…biblia inasema warumi 8:9 “..lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo sio wake.”….warumi 8:14..”kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu” …na wala sio wanaoongozwa na kanisa.
(yohana 14:6 inasema “mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.” hivyo basi hatumfikii Baba kwa njia ya kanisa lolote,wala kwa njia ya kiongozi yoyote wa dini, wala kwa njia ya papa,wala kwa ukatoliki,wala kwa uanglikana,ulutheri,upentekoste,usabato, u-endtime,ubranhamite n.k
Ukweli ni kwamba KUTOKUWA NA MAHUSIANO BINAFSI NA YESU KRISTO NI HATARI NA YENYE MADHARA MAKUBWA…..
MARAN ATHA!
Mada zinazoendana:
Mada Nyinginezo:
UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.
Mwinjilisti mmoja alisema kuwa kuipokea chapa ya mnyama/Alama ya Mnyama ni kuukataa muhuri wa Mungu ambao ni Roho Mtakatifu, alisema kuna pande mbili tu, upande wa Mungu na upande wa shetani, hivyo ukikosa kuwa na Roho wa Mungu, maana yake ni una roho ya shetani nayo ndiyo chapa ya mnyama. Na ndivyo ilivyo
Kwahiyo roho ya mpinga kristo ambayo ndani yake imebeba chapa ya mnyama iliyozungumziwa kwenye kitabu cha ufunuo 17:1-6 tusome..
” Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu”.
Habari hii inamwonyesha mwanamke aliyeketi juu ya mnyama mwekundu sana, na juu ya paji la uso wake, alikuwa na jina limeandikwa la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA, NA MACHUKIZO YA NCHI,
Sasa huyu mwanamke anayezungumziwa katika sura hii, ni KANISA fulani kwasababu mwanamke siku zote katika biblia anawakilisha kanisa, na pia mwanamke huyu tunaona anaitwa MAMA WA MAKAHABA, Hii ikiwa na maana kwamba ni kanisa-kahaba mama, na ikiwa ni “mama” basi ana “MABINTI”, na hao mabinti ni makahaba kama mama yao alivyo. Kwahiyo kahaba ni mwanamke anayezini na wanaume wengi mbali na mume wake. Na tunaona kuwa kanisa pekee lililofanya uasherati kwa kuchanganya mafundisho ya Mungu na mafundisho ya kipagani ni kanisa Katoliki,
Hivyo basi yule mama wa makahaba aliyezungumziwa pale ni kanisa Katoliki, Na wale mabinti ni madhehebu mengine yote ya dini yaliyobakia, yaliyoacha uongozi wa Roho Mtakatifu na kuiga desturi zile zile za kipagani kama za mama yao kahaba yaani kanisa katoliki. Na sasa hivi tunaona madhehebu yote ulimwenguni na dini zote ulimwenguni zinaungana, pamoja na mama yao mkuu kahaba katoliki (ecumenical council) na KUIUNDA ILE CHAPA YA MNYAMA.
Chapa ya mnyama ipo rohoni na mwilini, (nje na ndani). kwa NDANI ni kama hauna Roho Mtakatifu, umeshaipokea ile chapa ya mnyama(Au Alama ya Mnyama), kwahiyo ndugu tafuta kuwa na Roho wa Mungu angali muda upo, maana biblia inasema huo ndio muhuri wa Mungu, (soma waefeso 4:30). Na pia kuipokea chapa ya mnyama(Alama ya Mnyama) kwa NJE ni kama upo au umejiunganisha au umejifunga na mifumo yote ya madhehebu ambayo yameuacha uongozi wa Roho Mtakatifu, na kuweka mifumo ya kipagani, pamoja na taratibu za kibinadamu na desturi zisizoendana na NENO la Mungu. hivyo kuipokea chapa ya mnyama ni kujishona na madhehebu na kuwa na utambulisho mwingine wowote nje ya UKRISTO mfano, kujitambulisha kama mlutheri, mwanglikana, msabato,mbaptisti, mkatoliki, mbranhamite n.k. badala ya kujitambulisha kama MKRISTO.
(kumbuka maana ya haya majina sio mbaya, lakini madhehebu ambayo yamebeba hayo majina yana ile chapa ya mnyama ndani yake kwasababu yameshafanya uasherati kama wa mama yao katoliki, na Mungu ameyakataa soma ufunuo 3:1 ” …Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. “) kwahiyo kwa kujiita tu hivyo tayari umeshakwisha kubaliana na ile alama ya mnyama bila ya wewe mwenyewe kujijua. Fikiria tu hili kama sisi sote ni WAKRISTO huo utambulisho mwingine unatoka wapi?. Ujue tu unatoka kwa mpinga kristo ambao mwisho wake unapelekea kuiunda ile alama ya mnyama. Na nguvu ya hii alama ya mnyama itakuja kujidhihirisha sana katika kipindi cha dhiki kuu, baada ya kanisa (bikira safi) kunyakuliwa.
Kwahiyo hii alama ya mnyama kwasasa ipo sana katika roho na watu wanaendelea kuipokea kwa kukosa Roho Mtakatifu, lakini kwa nje, ipo wanakubaliana nayo ila itakuja kutenda kazi kwa Nguvu katika kipindi cha dhiki kuu. pale mpingakristo atakaponyanyuka na kupewa mamlaka juu ya ulimwengu mzima, na huyu mpinga kristo atakuwa sio mwingine zaidi ya Papa kiongozi wa kanisa katoliki wa Roma. Sio kwamba wakatoliki ni watu wabaya, Hapana ni watu wazuri wote bali ni vizuri kujua roho inayoliendesha kanisa katoliki ni roho ya mpinga kristo na haitokani na Mungu, Hivyo watu wa Mungu lazima waujue ukweli watoke huko.
Tunaweza tukaona leo hii, mambo mengi ya ajabu, yakitokea ulimwenguni ikiwemo vitendo vya kigaidi vikizidi kukithiri, amani inazidi kutoweka duniani,watu wanaishi kwa hofu za machafuko na vita, siasa na umoja wa mataifa umeshindwa kuihifadhi amani ya dunia, dunia inatafuta suluhisho la mambo hayo na bado haijapata, hivyo anatafutwa kiongozi atakayeonekana ana uwezo wa kurejesha amani duniani naye atakuwa si mwingine zaidi ya PAPA ili maandiko yatimie. Kama tunavyomwona leo hii anajulikana ulimwenguni kote kama mtu wa amani (MAN OF PEACE).
Hivi karibuni tunaweza tukaona jinsi kiongozi huyu wa kanisa Katoliki (papa Francis), akirejesha mahusiano kati ya Marekani na Cuba, ambayo yalikuwa yamevunjika kwa muda mrefu. Leo analeta dini zote ulimwenguni pamoja, anakubalika na kuheshimika na watu wote, Ni kiongozi mwenye ufuasi mkubwa wa watu kushinda kiongozi yeyote ulimwenguni.
(papa akiwa na viongozi wa dini mbalimbali duniani)
Kwahiyo katika kipindi cha ile dhiki kuu, atakuja na wazo la kukomesha ugaidi na vitendo viovu duniani akitaka watu wote, wasajiliwe kulingana na madhehebu yao na mashirika yao ya dini, kwasababu vitendo vinavyosababisha amani kutoweka vinasababishwa na dini na ndivyo ilivyo. kwahiyo ni lazima tatizo litatuliwe kwa namna ya KIDINI na si vinginevyo. Hivyo itahitaji kiongozi wa kidini na hakuna mwingine anayekidhi hivi vigezo zaidi ya Papa kiongozi wa kanisa katoliki.
Leo hii duniani vita vya kidini vimeiweka dunia katika mtazamo mpya, mfano mabomu ya kujitoa muhanga, na vikundi vya kigaidi, kama ISIS, Alqaeeda, Alshabaab, Boko haram Anti-balaka, LRA n.k.vimekuwa ni tatizo sugu kwa dunia nzima, ni mada iliyopo mezani kila siku sio kwa mataifa maskini wala matajiri wote wamevamiwa na tatizo hili .Hivyo kiongozi huyu atapewa nguvu kwa kujipendekeza (danieli 11:21), Jambo hili litatimiza ule unabii wa Daniel 9:27 “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja;….. “ Agano hili la amani litafurahiwa na dunia nzima, kwani litadhaniwa kuwa litaleta amani duniani,
UJIO WA USTAARABU MPYA WA ULIMWENGU
Hapo ndipo utakapowekwa utaratibu mpya wa ulimwengu (NEW WORLD ORDER). chini ya uongozi wa papa (mpinga kristo) baada ya kupewa nguvu na mataifa yote duniani kumbuka hatajiita mpingakristo wala hatakuwa na uso wa shetani, wala usidanganyike kama atakuwa freemason au illuminati, au kikundi chochote cha kichawi hapana bali ATATOKEA NDANI YA KANISA ni mtu anayekubalika na watu, anaonekana mpenda amani, anapenda dini, anajali watu wote wa dini zote, anabusu watoto na zaidi ya yote ataonekana ni mnyenyekevu kuliko watu wote duniani, lakini ndani yake ni SHETANI katika utendaji kazi wake. Biblia inasema “Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ufunuo17:8″
Kumbuka shetani ananyanyua sasa hivi kwa kasi vikundi vya kuvunja amani na ugaidi duniani kama mbinu yake ya sasa ya kutafuta kuwaangamiza wakristo, kama alivyofanya kwa wakristo katika kanisa la kwanza kwenye utawala ule ule wa KIRUMI chini ya Nero (AD 64),ambapo wakristo wengi waliuawa baada ya kusingiziwa kuwa wameuchoma mji, na ANGALI sio wao waliofanya hivyo. Na kwa njia kama hiyo hiyo shetani anawatafuta wakristo leo hii awaangamize, kwa vitu vya KUSINGIZIWA, maana anajua hakuna namna yeyote mkristo anaweza akashitakiwa na kuuawa kwa makosa yeyote ya kihalifu kwasababu wakristo sikuzote wanaishi maisha ya haki. Hivyo sasa hivi ameunyanyua ugaidi katika uislamu na vikundi vingine kama anti-balaka, ISIS, alshabaab,Boko Haramu, Al-qaeda, Hizbolah,Ku klax klan, pamoja na vikundi vyote vya siri vinavyouchafua ulimwengu, ili baadaye aweze kuwasingizia wakristo kwa urahisi kuwa wao ndio magaidi na kuwaangamiza wote).
(wakristo wasingiziwa kuuchoma mji, kusababisha wapitie dhiki kubwa ya kuuawa kikatili dhidi yao chini ya utawala wa Nero AD 64)
Hivyo basi utaratibu huo mpya utakapokuja watu wote watapaswa wahakikiwe taarifa zao muhimu zinazohusiana na DINI ZAO, itahusisha pia na kazi mtu anayofanya, kwenye makampuni, na mashirika. Kila mmoja ni lazima atambuliwe yeye ni dhehebu gani au dini gani katika shughuli anayoifanya kwa dhumuni la kuwapata watu wachafuaji wa amani duniani, kwamfano waislamu wenye itikadi kali, wanaojihusisha na vikundi vya kigaidi, pamoja na vikundi vya kihalifu vinavyohusisha vita vya kidini na mauaji ya kikatili ya watu watambulike na kukamatwa. Lakini nia ya shetani itakuwa sio kuleta amani wala kuwalenga waislamu au makundi mengine BALI NI KUWALENGA WAKRISTO, (kama ilivyotokea kwenye utawala wa NERO,)
Lakini wale ambao hawatakubaliana kujiunga na huo mfumo wa yule mnyama ambao ni MUUNGANIKO WA MADHEHEBU NA DINI ZOTE. Mtu huyo hataweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa asipokuwa na huo utambulisho, Hataruhusiwa kuabudu kwenye kanisa ambalo halijasajiliwa na muungano wa madhehebu, ndugu Branham alitabiri akasema itafika wakati haya makanisa tuliyonayo sasa yatafungwa yote.kwahiyo huu usajili utaanza karibu duniani kote, katika kila nyanja na kila taasisi, kwa waajiriwa na wasio waajiriwa, katika vitambulisho vya taifa,kura na serikalini na taasisi binafsi kama mabenki, ATM cards, VISA n.k. na sehemu nyingine zitatumika MICRO-CHIPS sana sana kwa mataifa yaliyoendelea.
Itakuwa ni sheria kila raia lazima ahakiki taarifa zake za kidini, na huo mfumo mpya. watu wengi wataukubali na kuupenda na kuhakiki taarifa zao pasipo kujua kuwa ndio wanaipokea ile chapa ya mnyama (au alama ya mnyama), na mfumo huo utafanikiwa kukamata wahalifu wengi.Ni wazi kuwa itakuwa ni ngumu kwa mtu kufanya biashara yeyote ya kuuza wala kununua wala kuajiriwa usipokuwa na huo utambulisho wa kidini. kwahiyo ukishahakikiwa taarifa zako utakuwa huru kufanya shughuli yako yoyote unayotaka.lakini sio kujiita MKRISTO tu! haitafanya kazi tena kipindi hicho, huko kutakuwa ni kuonyesha tu ID au CHIP ambayo imebeba taarifa zako zilizohakikiwa na huo mfumo mpya wa mpingakristo,
Lakini wale wakristo watakaokuwepo watamtambua yule mpingakristo na chapa yake, watakataa kuupokea huo utambulisho na usajili wake (chapa ya mnyama/alama ya mnyama). Sasa hao ndio watakaotafutwa na kuitwa magaidi, na hao tu ndio watakaopitia dhiki kuu wakati dunia inaendelea kufurahi. Na hawa hawatauliwa ovyo ovyo tu, kama inavyodhaniwa. bali watachukuliwa na serikali,(maana serikali itawatambua kama wahalifu na sio raia wa kawaida kwa maana serikali itashirikiana na mpingakristo kufanya kazi). Maana hawatakuwa wengi, na watapelekwa kwenye magereza maalumu ya mateso ya siri (concentration camps), huko ndiko kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea wala haitakaa itokee kama Bwana YESU KRISTO alivyosema.
Wakristo wengi watateswa kama magaidi, watasingiziwa wao ndio wanaoharibu amani ya dunia kama sivyo kwanini wakatae kusajiliwa, lazima kuna mambo ya siri wanayo. watakataliwa na jamii nzima, hata ndugu za hao jamaa hawatawaelewa.Hapo ndipo ndugu atamsaliti ndugu ili auawe, Tunaona kama vile wayahudi walivyofanyiwa na Adolf Hitler katika vita ya pili ya dunia kwenye zile concentration camps. watu jinsi walivyokuwa wakiuliwa kikatili na mateso makali yasiyoelezeka ndivyo itakavyokuwa tena na zaidi ya hapo katika wakati wa dhiki kuu kwa wakristo , mpinga kristo atawaua wote, (Na dhiki hii kuu itawahusisha na wayahudi pia) na itadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu ya mwisho wa lile juma la 70 la Danieli.
Na kwa mataifa yote yaliyobaki ambayo yamepokea ile chapa (yaani kwa kuukubali mfumo na utambulisho wa yule mnyama katika vitambulisho vyao na ID, na CHIP zao na vyeti vyao). wataingia katika ile siku ya KUOGOFYA ya BWANA ambayo itaanza mara tu baada ya ile miaka mitatu na nusu kuisha (baada ya dhiki kuisha),hapo ndipo hukumu ya mataifa itakapoanza.
(wayahudi katika mateso kipindi cha utawala wa Hitler)
Kanisa Katoliki ndio linaloongoza kwa kuwaua na kutesa wakristo wengi, na inakadiriwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68 katika historia ya kanisa. Na ndivyo linavyofanya hata sasa kwa siri na litakavyokuja kufanya katika kile kipindi cha dhiki kuu ambacho kipo karibuni kuanza.
Na ndio maana yule mwanamke aliyeonekana kwenye ufunuo 17 alionekana amelewa kwa damu ya watakatifu. Kuna wakristo wengi wanaoteswa na kuawa kwa siri duniani kote, kwa ajili tu wao ni wakristo na sio jambo lingine.
Shetani hapendi kuona mtu anajiita MKRISTO, kama vile asivyopenda kuona watu wakibatizwa kwa jina la YESU KRISTO, na ndivyo asivyopenda kumwona mkristo anautambulisho wa asili wa KUMKIRI KRISTO, Hakuna mahali popote mkristo katika biblia alikuwa anajiita mpaulo au mpetro au m-yohana mbatizaji, au m-eliya au m-timotheo, biblia inasema wote walikuwa wanaitwa wakristo. Kwahiyo utambulisho mwingine zaidi ya huo unatoka kwa shetani, na hiyo ndiyo chapa ya mnyama yenyewe. amina.
Papa akiwa kama kiongozi wa kanisa katoliki ana nembo katika enzi yake inayojulikana na kusomeka kama VICARIUS FILII DEI. tafsiri yake kwa kiswahili ni “BADALA YA MWANA WA MUNGU.”
Kwahiyo papa kulingana na kanisa katoliki anasimama hapa duniani badala ya mwana wa Mungu, anauwezo kama vile, kusamehe dhambi, kubariki, na kusujudiwa n.k.
Haya ni machukizo mbele za Mungu,. Na hesabu ya hilo jina, kwa kirumi ni 666. unaweza ukaona hesabu yake hapa chini.
kwahiyo kutiwa chapa katika mkono wa kuume au kwenye kipaji cha uso, ni kukubaliana na ule mfumo kichwani kwako,(hiyo ni kwenye kipaji cha uso) na kukubali kuutumia huo mfumo kama kitu cha kujipatia riziki au chakula (hiyo ni kwenye mkono wa kuume) tunafahamu kama vile mkono tunautumia kwa kula, kukubaliana na kitu, kusaini mikataba n,k kwa wale watakaokubali kuuza na kununua ndio watapokea hiyo chapa (666). Kumbuka hii 666 ni namba inayomtambulisha mpingakristo na chapa yake, na sio chapa yenyewe.
ukiulizwa wewe ni dhehebu gani, sema mimi ni mkristo usione haya Bwana Yesu alisema katika marko 8:38″Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu”. Uvae ukristo umfuate Yesu usiuvae udhehebu utakupeleka jehanum.
Bwana Yesu anasema mathayo 16:24-26 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?.”
Tubu ndugu mgeukie Mungu haya mambo yote, yatatokea kizazi tunachoishi sisi, unaona jinsi gani MPINGAKRISTO kashaweka mambo yake yote tayari, ni kutekeleza tu! mambo yaishe. YESU KRISTO YUPO MLANGO KURUDI, MUDA UMEENDA SANA KUSHINDA UNAVYOFIKIRI.
MUNGU AKUBARIKI!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.
CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZIUSIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.
Mpinga-Kristo ni nani?
Vita kubwa inayoendelea duniani leo ni vita kati ya MUNGU na SHETANI. Mungu anatafuta roho za watu vile vile shetani naye anawinda roho za watu. Hizi roho mbili zimekuwa zikipingana siku zote tangu ulimwengu ulipoanza kukaliwa na wanadamu.
Lakini baada ya mwanadamu kuanguka Mungu alitumia njia zote kwa Roho wake kumvuta kwake tena, mwishoni akaona vema kumleta mwanawe mpendwa YESU KRISTO kwa dhumuni moja tu! kutupatanisha sisi na Mungu, ili katika yeye sisi sote tuokolewe.
Vivyo hivyo shetani naye, kwa kuona hivyo kwa roho yake ya uovu, alitumia njia zake zote za kuweza kumtoa mwanadamu katika kusudi la Mungu na kumvuta kwake, jambo hili lilianza tangu Edeni, tunaona shetani jinsi alivyomtumia Nyoka kumdanganya Hawa ili aipate roho yake. Hivyo basi ulipofika wakati alipoona Mungu amemleta mwokozi katika mwili yaani YESU KRISTO na kuwavuta wengi kwa BABA, yeye naye alianza mipango ya kumwandaa mtu mmoja ambaye atakuwa na kazi maalumu ya kuwavuta watu kwake na kwenda kinyume na huyo mmoja Mungu aliyemteua (yaani YESU KRISTO). Sasa mwana huyu wa shetani ndiye anayeitwa MPINGA-KRISTO.
Kumbuka vita vya kwanza kabla ya Kristo kuja vilikuwa ni roho kwa roho (yaani Roho wa Mungu dhidi ya roho ya shetani), lakini vita vya mwisho ni MTU dhidi ya MTU (yaani YESU KRISTO dhidi ya MPINGA-KRISTO).
Wakristo wengi wanapokosa shabaha ni pale wanaposhindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani na MPINGA-KRISTO ni nani?. Ukishindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani huwezi kumfahamu MPINGA-KRISTO ni nani.
Hawa wote wawili waliandikwa kwenye NENO la Mungu katika “SIRI”. Ikiwa na maana utendaji kazi wao ulihitaji “UFUNUO wa ROHO” Kuutambua. Embu kwa ufupi, tutazame siri iliyopo kwa YESU KRISTO ambayo ilikuwa imefichika kwa Muda mrefu na hata sasa baadhi ya watu bado imefichika machoni pao.
1 Timotheo 3:16 ” Na bila shaka SIRI YA UTAUWA NI KUU. Mungu alidhihirishwa katika MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.”
Ukisoma hapo utaona kuwa jambo hili Mungu aliliweka liwe SIRI,na sio kitu cha wazi ya kwamba Yesu Kristo alikuwa ni MUNGU KATIKA MWILI. Yaani ni Roho ya Mungu ikitenda kazi katika mwili, lakini wengi hawakulijua hilo walimkataa na kumsulubisha,na hata leo wengi hawalifahamu hilo. maana Bwana Yesu alisema “Yohana 5:43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. “ unaona huyo mwingine BWANA YESU aliyemzungumzia akija kwa jina lake mtampokea ni MPINGA-KRISTO mwenyewe..tusome tena mstari ufuatao
1 Wakoritho 2:6-8″ Walakini iko HEKIMA tusemayo KATI YA WAKAMILIFU; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
7 bali twanena HEKIMA YA MUNGU KATIKA SIRI, ILE HEKIMA ILIYOFICHWA, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, WASINGALIMSULIBISHA BWANA WA UTUKUFU; “.
Kwa maandiko hayo hapo juu, hata leo watu katika mioyo yao wanamchukulia YESU KRISTO kama ni mtu wa kawaida kama walivyofanya watu wa kipindi kile, wanayadharau maneno yake sio kwa mdomo bali kwa matendo, lakini hawajui kuwa wanamkataa na kumsulibisha Mungu mwenyewe ambaye ni BWANA WA UTUKUFU, kwa heshima aliitoa damu yake, imwagike kwa ajili ya dhambi zetu kutupatanisha sisi na yeye lakini bado leo hii unaichezea hii damu ya thamani, itafika wakati hii neema haitakuwepo tena.
2 Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; AKAFUNULIWA YULE MTU WA KUASI , MWANA WA UHARIBIFU;
4 YULE MPINGAMIZI, AJIINUAYE NAFSI YAKE JUU YA KILA KIITWACHO MUNGU AMA KUABUDIWA; hata yeye mwenyewe kuketi katika HEKALU LA MUNGU, AKIJIONYESHA NAFSI YAKE KANA KWAMBA YEYE NDIYE MUNGU.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 Maana “ILE SIRI YA KUASI” HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule ASI, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.”
Ukisoma habari hiyo mstari wa saba inazungumzia SIRI YA KUASI ambayo inatenda kazi duniani, na hii siri ya kuasi inatenda kazi ndani ya yule ASI (ambaye ndio mpinga-kristo mwenyewe) kama maandiko yanavyomtaja kwenye mstari wa 9, kuwa “kutenda kwake kazi ni mfano wa kutenda kwake shetani mwenyewe”. Kama tu vile SIRI YA UTAUWA ilivyokuwa inatenda kazi ndani ya YESU KRISTO, na kutenda kwake kazi Yesu kulikuwa ni mfano wa kutenda kwake Mungu mwenyewe vivyo hivyo na huyu (Mpinga-kristo) siri ya kuasi inatenda kazi ndani yake na kutenda kwake kazi kutakuwa ni mfano wa shetani.
Baada ya shetani kuona kuwa hawezi kuwapata wanadamu wengi kwa kutaka wamwabudu moja kwa moja kama wanadamu wamwabuduvyo Mungu, aliamua kujibadilisha na kujifanya kuwa kama malaika wa Nuru (2Wakoritho 11:14), ili awapate wale wanaoonyesha dalili ya kuipenda Nuru. Kumbuka shetani hafanyi vita na watu wa ulimwengu huu, kwasababu hao alishawapata na siku zote wapo gizani, kwahiyo ili awapate wale wa nuruni ni lazima ajigeuze kuwa mfano wa malaika wa Nuru, vivyo hivyo na watumishi wake nao ni lazima wajigeuze kuwa kama watumishi wa nuru. Hapo ndipo penye vita vikali pale mbwa-mwitu anapokuja kwa vazi la kondoo. Hivyo inahitaji hekima ya Roho Mtakatifu kumtambua mpinga-kristo vinginevyo hawatakaa ufahamu adui yako yupo wapi na anatendaje kazi.
Ndugu kuna vikundi vingi vya kishetani na kichawi, vinavyosifika kama freemason, rotary clubs, iluminati, ku klux klan, brotherhood, n.k. vimekuwa vikiogopeka kana kwamba hivyo ndio makao makuu ya shetani, usidanganyike vikundi hivyo shetani anavitumia kuwadaka watu wasiokuwa wakristo na wakristo wachache wenye imani isiyothabiti kwasababu mkristo wa kweli yoyote hawezi kwenda kwa mganga na shetani analijua hilo, wala hawezi kujiunga kwenye mojawapo ya hivyo vikundi wala kupiga ramli, au kupunga-pepo, shetani anajua kabisa kama angetegemea njia hiyo tu, basi angewakosa wakristo wengi sana duniani. Anafahamu kuwa mkristo mahali pake pekee anajihisi atakutana na Mungu ni kanisani na ndiko huko huko anapowafuata wakristo.
Kumbuka, shetani anatenda kazi katika SIRI, na ndiyo maana ikaitwa “SIRI YA UASI”. na inatenda kazi ndani ya Kanisa la Mungu pale shetani anapovaa mavazi ya kondoo lakini ndani ni MBWA-MWITU(Hii ni SIRI). kuharibu roho za watu(wakristo wa kweli) na kuwapeleka kuzimu. Anatumia hila zake kuwafanya watu waone kama wanamwabudu Mungu, kumbe wanamwabudu yeye.
Anaingia kanisani na kuwafanya watu wajione kuwa wapo katika njia sawa, lakini mwisho wake ni kuzimu,. Na anaowapeleka kuzimu kwa njia hii ni kubwa sana kuliko hata hizo njia nyingine ndogo ndogo kama uchawi, freemason n.k. HAPA NDIPO KRISTO ALIPOTUTILIA MSISITIZO KWAMBA “TUJIHADHARI NA MANABII WA UONGO, WANAOVAA MAVAZI YA KONDOO LAKINI NDANI NI MBWA-MWITU WAKALI”..Ndugu, Bwana hakutuonya tujihadhari na wachawi au wapiga-ramli, au freemason, au wapunga-pepo hilo ni jambo dogo sana ambalo kwa namna ya kawaida mkristo yoyote anaweza kujihadhari nayo.
Baada ya shetani kujiingiza kwa siri kwenye kanisa la Mungu na kukomaa kwa muda mrefu, tunaona alianza kwa kuharibu mafundisho ya Mungu ya kweli na kupachika mafundisho ya kipagani kama ibada za wafu, ibada za miungu mitatu, kuongeza vitabu katika NENO la Mungu, Ibada za sanamu kanisani, kubariki pombe kanisani, na kupindisha maandiko na utaratibu uliokuwepo wa kanisa kwa kupotosha ubatizo sahihi wa maji, na wa Roho Mtakatifu, kwa kuua karama za roho, kuingiza siasa na vyeo katika kanisa visivyotakana na Mungu,kuua mafundisho ya uponyaji wa kiungu, n.k.
Kwa kuendelea hivyo alifanikiwa kutengeneza kanisa lake moja “MFU” lenye jina linalofanana na lile kanisa la mwanzo la kweli lakini sio, watu wakidhani kuwa ndio lile kanisa la kwanza (la Mitume) kumbe wamepotea pasipo wao kujua ROHO MTAKATIFU ameshaondoka muda mrefu imebaki roho ya shetani ikitawala, Kwahiyo shetani akalipa jina hili kanisa lake akaliita UNIVERSAL CHURCH yaani KANISA LA ULIMWENGU (KANISA KATOLIKI).
Na yeye (shetani) akiwa kama mungu wa hilo kanisa aliweka watumishi wake, Na akaweka cheo cha juu zaidi kabisa katika hilo kanisa ambacho ndio cheo kile cha UPAPA (hichi ndicho cheo cha MPINGA-KRISTO mwenyewe) kisimame kwa niaba yake duniani kama Yesu Kristo alivyosimama kwa niaba ya Mungu duniani.
Tunafahamu katika historia chombo chake kiteule alichokitumia shetani kupambana na uzao wa Mungu ni KANISA KATOLIKI,na si kingine, lilifanikiwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68, waliojaribu kuenda kinyume na mifumo yake ya kipagani. Na hadi leo kanisa hili linaendelea kuuwa watu wengi kiroho, kwa kudhani wanamwabudu Mungu kumbe wanamwabudu shetani katika hilo kanisa. Na litakuja kuuwa wengi zaidi katika kipindi cha ile dhiki kuu. HAYA NDIYO MALANGO YA KUZIMU.
Hivyo basi roho ya mpinga-kristo inakaa katika cheo cha UPAPA, kwahiyo mtu yeyote atakayekikalia hicho cheo atakuwa amekidhi vigezo vyote kuwa MPINGA-KRISTO.
Injili iliyopo leo hii, kulingana na wakati tunaoishi sio injili tu ya kuwavuta watu kwa Kristo, kwasababu wengi wameshampokea Kristo lakini hawajui kuwa wanamwabudu shetani pasipo wao kujua katika madhehebu yao wakidhani kuwa wapo sawa kumbe hawapo sawa. Ndugu Mungu kashatoa laana juu ya kanisa Katoliki na madhehebu yote yasiyokaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, (maana haya kwa pamoja ndiyo yanayounda ile chapa ya mnyama). Kwa kufahamu zaidi kwa undani juu ya chapa ya mnyama unaweza kusoma soma tuliloliandika linaloitwa “CHAPA YA MNYAMA”.
Haya ndiyo maneno ya Bwana mwenyewe.
Ufunuo 18:4-5″ Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “
Bwana anatuonya tutoke (sio kutoka kwa miguu bali kwa roho. Yaani kujihadhari na mafundisho yote yasiotoka na Mungu, ukiri ukristo wa biblia usiukiri udhehebu) Toka katika kamba za madhehebu, umwabudu Mungu katika roho na kweli kwasababu hayo yamefanya uasherati wa kiroho kwa kuchanganya NENO la Mungu na mafundisho ya kipagani hivyo Bwana ameyahukumu na yoyote atakayeshirikiana nayo atashiriki katika mapigo yake yote yaliyoandaliwa kwasababu yameshiriki katika kumwaga damu nyingi za watakatifu wa Mungu.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo: