Title asiyefanya kazi

ASIYEFANYA KAZI NA ASILE

Biblia ina maanisha nini iliposema “Asiyefanya kazi na asile”?

Maandiko hayo yanapatikana kutoka katika kitabu cha 2 Wathesalonike 3:10 “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula”.

Mstari huo unatafsiriwa isivyopaswa na wengi wanaousoma..

Lakini mstari huo, unawahusu Wakristo! yaani watu wanaokusanyika  pamoja kanisani.

Katika Kanisa la Kwanza ulikuwepo utaratibu wa Waumini wote kufanya vitu kwa shirika,  ikiwemo kila mmoja kutoa sehemu ya mali zake na kuzileta kanisani ili zitumike katika kusaidiana pamoja na kunyanyuana..hususani kwa wale wenye mahitaji…. Hilo tunalisoma katika kitabu cha Matendo ya Mitume 2

Matendo 2:44 “Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika,

45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.

46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,

47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa”.

Sasa kilichokuwa kinatokea ni kwamba, kulikuwepo na watu wachache ambao, walikuwa na uwezo wa kwenda kufanya kazi, lakini kwasababu wanaona kuna ofa hiyo ya kugawiwa baadhi ya vitu bure ikiwemo chakula kanisani, wakawa hawaendi kufanya kazi, na kukaa kusubiria hilo fungu la kanisa lifike wapewe, hivyo hiyo ikawa inasababisha kanisa kulemewa, kwa kuongezeka kwa watu wasio na shughuli zao na huku bado wanataka kupewa fungu kutoka kanisani.

Sasa kulitatua tatizo hilo, Ndipo Mtume Paulo kwa Uwezo wa Roho akaagiza katika makanisa yote kwamba watu wakafanye kazi, wale chakula chao wenyewe ili kanisa lisilemewe…Wabakie tu wale wanaostahili kweli kweli kupata fungu kutoka kanisani…Na wengi wa hao wanaostahili walikuwa ni wajane wenye umri wa miaka 60 na kuendelea, tena wasio na ndugu wa kuwasaidia, wameachwa wenyewe, na pia wana rekodi nzuri ya kuifanya kazi ya Mungu kanisani…hao ndio waliostahili kupokea sehemu ya fungu… na watu wasio na uwezo kabisa..Lakini wengine waliosalia wasipewe kitu chochote hata chakula kutoka kanisani, wakafanye kazi ili kanisa lisilemewe.


Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?

TUNAPOSEMA TUISHI KWA NENO, INAMAANISHA TUISHI MAISHA YA NAMNA GANI?

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

JE! KUBET NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Biblia inasemaje kuhusu Kazi?

Jibu: Biblia imetuelekeza kufanya kazi za Mikono, ambayo kupitia hiyo Mungu atatupa riziki zetu za kila siku.

1Wathesalonike 4:11  “Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;

12  ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote”

Hivyo ni wajibu wa kila mmoja mwenye uwezo wa kufanya kazi, afanye kazi, aidha za Mikono au za kiutumishi.

Kazi za mikono ni zile zote zinazohusisha kuajiriwa au kujiajiri, na kazi za kiutumishi ni zile zote za Madhabahuni au za kiinjilisti. Mkristo yoyote ni lazima awepo katika kundi mojawapo ya hayo mawili, akikosekana katika yote (na ilihali ni mzima, au hana tatizo lolote lile) basi mtu huyo yupo kinyume na Neno la Mungu, aidha kwa kujua au kutokujua.

Mtume Paulo alisema kwa uongozo wa Roho, kuwa mtu yeyote asiye na shughuli yoyote katika Mwili wa Kristo, yaani asiyefanya kazi yoyote ya Madhabahuni  kama Uchungaji, Uinjilisti, au Shemasi, au Mzee wa kanisa au ya Uinjilisti, au mfanya kazi wa kanisani (inayomfanya muda wake mwingi atumie kuhubiri) mtu huyo basi asipewe fungu lolote kutoka kanisani..

1Wathesalonike 3:10 “ Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.

11  Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.

12  Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe”

Kumbuka pia unapoamua kufanya kazi za Mikono, basi huwezi kuwa Mchungaji kwa wakati huo huo, kwasababu huwezi kushikilia mambo mawili kwa wakati mmoja.. Ni aidha ushikilia moja uache lingine! Huwezi kuwa mchungaji na huku ni Mbunge, huwezi kuwa Mchungaji na huku ni Mfanya biashara mashuhuri.. jambo hilo haliwezekani!, haijalishi mtu atalilazimisha kiasi gani?.

Mathayo 6:24  “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali”

Tofauti na inavyodhaniwa na wengi kwamba Mtume Paulo alikuwa anafanya kazi muda wote!, kwamba alikuwa anashona Mahema kila wakati ili kujipatia riziki, nataka nikuambie kuwa haikuwa hivyo, ni sehemu chache sana ndizo alizokuwa anashona mahema, lakini sehemu kubwa ya maisha ya Paulo ilikuwa ni kuhubiri injili, na Mungu alikuwa anamfungulia milango ya riziki kupitia injili hiyo, na alikuwa haombi kwa watu fedha wala mali, (ili awe kielelezo) bali watu walikuwa wanampa kwa kadiri wanavyoguswa.

Tunalithibitisha hilo katika kitabu cha Wafilipi, 4:1-19, (Zingatia Mistari iliyoainishwa kwa herufi kubwa)

Wafilipi 4:14  “Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu.

15  Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika HABARI HII YA KUTOA NA KUPOKEA, ila ninyi peke yenu.

16  KWA KUWA HATA HUKO THESALONIKE MLINILETEA MSAADA KWA MAHITAJI YANGU, WALA SI MARA MOJA.

17  Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.

18  Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; NIMEPOKEA KWA MKONO WA EPAFRODITO VITU VILE VILIVYOTOKA KWENU, HARUFU YA MANUKATO, SADAKA YENYE KIBALI, IMPENDEZAYO MUNGU.

19  Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu”

Umeona hapo ? Sio wakati wote Paulo alikuwa anafanya kazi ya kushona, Soma pia 2Wakorintho 8:1-5..

Lakini biblia inatufundisha nini katika hali tulizopo (yaani ya kufanya kazi ya Mikono au ya Madhabahuni)?

Biblia imetufundisha kutumika kwa uaminifu popote pale tunapopatumikia, maana yake kama ni Mtumwa basi tumika ipasavyo kwa Bwana wako (maana yake Boss wako, au Mkubwa wako) kana kwamba unamtumikia Kristo.

Waefeso 6:5  “Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;

6  wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;

7  kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;

8  mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru”.

Vile vile kama tunatumika katika utumishi wowote ule.. Maandiko yanatufundisha  KURIDHIKA, Maana yake TUSIJISIKIE VIBAYA kutumika pale tulipopachagua sisi, kwasababu ni mapenzi ya Mungu. Kama ni Mfanyakazi wa kuajiriwa maana yake wewe ni Huru kwa kazi ya Bwana ya madhabahuni, hivyo usijisikie vibaya kuifanya kazi hiyo, kilicho kikubwa na cha muhimu ni wewe kuwa Mwaminifu katika kazi unayoifanya na pia katika kumtolea Bwana, na mwisho wa siku utapokea thawabu kutoka kwa Mungu, vile vile kama wewe ni mtumishi wa Madhabahuni au wa Injili, maana yake wewe ni Huru katika utumishi wa kazi za kidunia, hivyo basi usijisikie vibaya kutumika hivyo, maana ni Mungu kakuita katika hali hiyo, wala usiitamani kazi nyingine zaidi ya hiyo uliyopewa!.  

1Wakorintho 7:21  “Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.

22  Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.

23  Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

MAOMBI YA KUFUNGULIWA KIUCHUMI.

Orodha ya mistari ya biblia kuhusu watoto.

Kwanini iwe ni nchi ibubujikayo maziwa na asali?

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

Rudi nyumbani

Print this post

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Karibu tuongeze maarifa katika Neno la Mungu,

Tukisoma kwenye biblia kitabu cha warumi 4 tunaona mtume Paulo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kwa matendo yake bali kwa Imani, lakini tukisoma tena katika kitabu cha Yakobo 2, Yakobo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki kwa Imani tu, bali pia na kwa matendo. Tunaona sentensi hizi mbili zinaonekana kama kupingana, Lakini je! Biblia kweli inajipinga au ni sisi uelewa wetu ndio unaojipinga??..tuichambue mistari hii miwili kwa undani kidogo..

1) Warumi 4:1-6

“1 Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili?
2 KWA MAANA IKIWA IBRAHIMU ALIHESABIWA HAKI KWA AJILI YA MATENDO YAKE, ANALO LA KUJISIFIA, LAKINI SI MBELE ZA MUNGU.

3 Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.

4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.

5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

6 Kama vile Daudi anenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,.

Ni dhahiri kuwa hapa mtume Paulo alipokuwa anazungumzia MATENDO, alikuwa analenga matendo yatokanayo na sheria  ya kwamba hakuna mwanadamu yoyote anaweza akasimama mbele za Mungu kwa matendo yake kuwa ni mema au amestahili kumkaribia Mungu.

Kwa mfano mtu kusema nimestahili kwenda mbinguni kwa matendo yangu mazuri, mimi sio mwasherati, sio mwizi, sio mtukanaji, sio mlevi, sio mwongo, sio mwuuaji n.k. kwa kusimamia vigezo kama hivyo hakuonekana hata mmoja aliyeweza kumpendeza Mungu isipokuwa mmoja tu naye ni BWANA wetu YESU KRISTO! wengine wote kama biblia inavyotaja kuanzia Adamu mpaka mwanadamu wa mwisho atakayekuja duniani Mungu alishawaona wote tangu mwanzo kuwa wamepungukiwa na utukufu wake,

Warumi 3:23″ kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; “

 na ukisoma pia Zaburi 14:2-3 inasema

 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.” 

Hivyo hii inadhihirisha kabisa hakuna hata mmoja atapata kibali mbele za Mungu kwa matendo yake mazuri.

 Lakini swali ni je! kama sio kwa matendo, basi mtu atapata kibali mbele za Mungu kwa njia gani tena??..

Ukiendelea kusoma mbele tunasoma mtume Paulo anasema ni kwa njia moja tu tunaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu nayo ni njia ya kumwamini BWANA YESU KRISTO tu!. Ndio njia pekee inayotupa sisi kupata kibali mbele za Mungu, kwa namna hiyo basi tunayo haki ya kuwa na uzima wa milele, kwenda mbinguni, kubarikiwa kwasababu tumemwamini mwana wa Mungu YESU KRISTO na sio kwa matendo mema tuyatendayo.

Kumbuka zipo dini nyingi zenye watu ambao wanatenda matendo mema lakini je! wanao uzima wa milele ndani yao? utakuta ni wema kweli wanatoa zaka, wanasaidia maskini, sio waasherati, sio  walevi n.k. lakini bado Mungu hawatambui hao. Lakini sababu ni moja tu, hawajamwamini mwana wa Mungu ili aziondoe dhambi zao.

Kwahiyo tunaona hapo jambo kuu Mungu analolitazama ni wewe kumwamini mwana wa Mungu, na ukishamwamini (yaani kumpa maisha yako) ndipo ROHO wake MTAKATIFU anakutakasa na kukufanya uishi maisha matakatifu ya kumpendeza.

2). Lakini tukirudi kusoma kitabu cha Yakobo 2:21-26 

“21 JE! BABA YETU IBRAHIMU HAKUHESABIWA KUWA ANA HAKI KWA MATENDO, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?

22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.

23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.

24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.

25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?

26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Katika kifungu kile cha kwanza ukiangalia kwa undani utaona kuwa mtume Paulo alikuwa anazungumzia juu ya MATENDO YATOKANAYO NA SHERIA. Lakini hapa Yakobo hazungumzii habari ya matendo yatokanayo na sheria bali ni MATENDO YATOKANAYO NA IMANI.. hivyo ni vitu viwili tofauti. 

MFANO WA MATENDO YATOKANAYO NA IMANI:  

Kwamfano: Mtu amepimwa na daktari na kuambiwa kuwa anaugonjwa wa kisukari, na hatakiwi kula vyakula vyenye asili ya sukari na wanga. lakini mtu yule akilishikilia lile Neno kwenye biblia Mathayo 8:17 linalosema ” ….Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu. ”

Na kuliamini na kuamua kuchukua hatua na kusema mimi ni mzima na sio mgonjwa kwasababu yeye alishayatwaa madhaifu yetu, na kusimama na kutembea kama mtu mzima asiyeumwa na kula vyakula vyote hata vya sukari na wanga ingawa daktari alimkataza, akiamini kuwa amepona kwa NENO lile atapokea uponyaji wake. sasa  kitendo cha yeye kuchukua hatua ya kuishi kama mtu mzima ambaye haumwi japo ni mgonjwa na kula vile vyakula alivyoambiwa asile hicho ndicho kinachoitwa MATENDO YA IMANI Yakobo aliyoyazungumzia..

Unaona hapo haki ya huyo mtu kuponywa haikutokana na matendo ya sheria (yaani utakatifu, kutokuwa mwasherati, au mlevi au mwizi n.k.). bali ni matendo yaliyotakana na kumwamini YESU KRISTO katika NENO lake ndio yaliyomponya. Na ndio jambo hilo hilo lililomtokea Ibrahimu pale alipomwamini Mungu na kumtoa mwanae kuwa dhabihu, kwahiyo kile kitendo cha yeye kumtoa mwanawe hayo ndiyo MATENDO yanayozungumziwa na Yakobo YA IMANI kwasababu hiyo basi ikampelekea yeye kupata haki mbele za Mungu.

Unaona hapo haikuwa sababu ya yeye kutokuwa mwongo, au mlevi, au muuaji n.k. ndio kulimpa haki yeye ya kubarikiwa hapana bali ni kumwamini Mungu na kuiweka ile imani katika matendo. Kwasababu kama ingekuwa kwa usafi wake Mtume Paulo asingesema Ibrahimu hana la kujisifu mbele za Mungu.

Vivyo hivyo kwa mambo mengine yote kwamfano haki ya kuzungumza na Mungu, haki ya kuponywa magonjwa,  haki ya kubarikiwa, haki  ya kwenda mbinguni, haki ya karama za rohoni, haki ya kuwa mrithi, n.k. havitokani na MATENDO YA SHERIA bali MATENDO YA IMANI. Kwa sisi kumwamini YESU KRISTO katika Neno lake ndipo tunapopata vyote.

Kwahiyo matendo yote mema ya sheria yanakuja baada ya kuwa ndani ya Kristo na hayo ndiyo yanayokupa uhakika kama upo ndani ya Kristo, ni kweli huwezi ukawa ni mkristo halafu bado ni mlevi, mwasherati, mwongo, mwizi n.k.. lakini jua katika hayo mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kama tukitaka tuhesabiwe katika hayo hakuna mtu atakayesimama mbele za Mungu.

Kumbuka Ibilisi anawinda IMANI yetu kwa Bwana pale tunapoiweka katika matendo na sio kingine, tunasamehewa dhambi kwa imani, tunaponywa kwa imani, maombi yetu yanajibiwa kwa imani, kila jambo tunapokea kwa Mungu kwa IMANI IPATIKANAYO KATIKA NENO LAKE.

Lakini shetani anaenda kinyume kukufanya udhani utasamehewa dhambi kwasababu unashika amri kumi, au  kwa kufunga na kuomba sana ndio utapata haki ya kuponywa, n.k. Bwana amesema Waebrania 10:38 ” Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. “

Wagalatia 2:16 ” hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki. “

Waefeso 2:8-9 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;  wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. “

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA

KUNA TOFAUTI GANI KATI YA SALA NA DUA?


Rudi Nyumbani

Print this post

Miungu wasio na kikao pamoja na wenye mwili.

SWALI: Wale wachawi walikuwa na maana gani waliposema..”Miungu wasio na kikao pamoja na wenye mwili”?.

Danieli 2:11

[11]Ni neno la ajabu, hili analolitaka mfalme, wala hapana mwingine awezaye kumwonyesha mfalme neno hilo, ila miungu, wasio na kikao pamoja na wenye mwili.


JIBU: Hiyo ni baada ya Mfalme Nebukadneza kutoa mtihani mzito wa kukumbushwa na kupewa tafsiri wa ndoto aliyoiota,..lakini tunaona wale wachawi wote walishindwa kupokea taarifa yoyote kutoka kwa miungu yao..ndipo wakakiri wazi kuwa fumbo hilo, si kila aina na mungu ilimradi mungu tu anaweza kulifichua, bali ni miungu wengine isiyofanya kikao na wanadamu.

Sasa hawa wachawi walitumia neno “miungu”..kwasababu waliamini katika miungu mingi, ndio màana utaona wanatumia neno miungu na sio Mungu asiyefanya kikao na wanadamu…lakini walimaanisha Mungu mmoja ( ambaye ni Yehova) yeye peke yake, ambaye huwa hafanyi vikao na wanadamu.

Sasa aliposema…asiyefanya vikao na wanadamu” maana yake ni kuwa asiyeishi pamoja na wanadamu..yaani Mungu ambaye makazi yake si duniani, bali ni mbinguni.

Miungu yote ya kipagani, makao yao ni hapa duniani, mizimu, mapepo, vibwengo, majini, n.k. vyote hivyo vinaishi katikati ya watu, na vinawategemea watu kutenda kazi zao..vinazurura zurura huku duniani kukusanya taarifa za matukio mbalimbali…havina kitu cha ziada zaidi ya kupeleleza peleleza, kama baba yao shetani (Ayubu 1:7)..

Haviwezi kujua mambo yajayo, haviwezi kutambua siri za ndani za mioyo ya watu..wakati mwingine hata vikitaka taarifa  fulani ya mtu vitakuambia niletee kwanza unyayo, au nywele, jinsi gani vilivyo vidhaifu, havijui, wala havipo kila mahali..na ndio maana wale wachawi walitaka kwanza wasimuliwe ile ndoto..ndio walau wakisie kisie tafsiri yake..

Lakini  Yehova peke yake ndiye ambaye hategemei, mwanadamu, au kiumbe chake chochote kufahamu au kutenda jambo alitakalo,  

Hii ni kutuonyesha kuwa Mungu pekee(Yehova) ndio tumaini la kweli, shetani au vipepo haviwezi kueleza hatma ya mtu. Unapotazama utabiri wa nyota, ujue kuwa umedanganyika, unapokwenda kwa waganga ujue kuwa ndio umekwenda kujitafutia matatizo, unapofanya mila na kuamsha mzimu, ujue unajifungulia milango mwenyewe wa kupelekwa kuzimu.

Zaburi 115:3-9

[3]Lakini Mungu wetu yuko mbinguni,  Alitakalo lote amelitenda.

[4]Sanamu zao ni fedha na dhahabu, 

Kazi ya mikono ya wanadamu.

[5]Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni,

[6]Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu,

[7]Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake.

[8]Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia.

[9]Enyi Israeli, mtumainini BWANA; Yeye ni msaada wao na ngao yao.

Amen.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Bwana aliposema kuwa yeye ni “Mungu wa miungu” alikuwa na maana gani?..je! yeye ni Mungu wa sanamu?

JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?

Kuwiwa maana yake nini katika biblia?

Wasamaria walikuwa ni watu gani?

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.

Rudi nyumbani

Print this post

UBATIZO NI NINI NA ULIO SAHIHI NI UPI?

Kabla ya kufahamu ubatizo ni nini…Hebu jiulize mtu katokea na akakuuliza “kuzamisha maana yake ni nini?”..utamjibuje?…Bila shaka utamwelezea kwa kina kwamba ni kitendo cha kukitosa kitu chote kwenye kimiminika Fulani au kitu Fulani, pasipo kubakisha sehemu ambayo ipo wazi. Meli iliyopata ajali na kushuka chini ya bahari, tunasema meli hiyo imezama baharini. Mtu anayechimba shimo la taka akachimba chini sana na kuzitupa humo na kuzifukia, hapo ni sawa na kusema kazizamisha/kazizika.

Sasa mpaka hapo tutakuwa tumeshajua maana ya neno “KUZAMA au KUZAMISHA”..Sasa ukilichukua neno hilo “kuzamamisha”  ukalitafsiriwa kwa lugha ya kigiriki linakuwa ni BAPTIZO…Ni sawa uchukue Neno la kiswahili “kanisa” na kulitafsiri kwa kiingereza na kuwa “CHURCH”…Vivyo hivyo Neno “kuzamishwa” likitafsiriwa kwa kigiriki linakuwa ni Baptizo..neno hilo hilo likipelekwa kwa lugha ya kiingereza linakuwa ni “IMMERSION”..na linaweza kutafsiriwa kwa lugha mbali mbali..

Kwahiyo mtu anayesema “leo naenda chachi”..ni sawasawa na mtu aliyesema “leo naenda kanisani”…neno “chachi” sio Kiswahili, na wala sio kiingereza fasaha lakini utakuwa umemwelewa amemaanisha nini kusema hivyo.

Vivyo hivyo mtu akikuambia “leo nime batizwa kwenye maji” utakuwa umemwelewa kwamba amemaanisha leo kazamishwa kwenye maji…kwa lengo Fulani.. (katumia tu msemo wa kigiriki lakini utakuwa umeshamwelewa).

Kwahiyo mpaka hapo utajua kuwa hakuna mtu atakayekuambia kwamba kabatizwa kwenye maji halafu awe “amenyunyuziwa”…Mtu aliyenyunyuziwa hajabatizwa!…kwasababu kubatizwa sio kunyunyuziwa bali kuzamishwa kabisa. (mpaka hapo tutakuwa tumeshaelewa ubatizo ni nini)

TUKIRUDI KATIKA IMANI YA KIKRISTO.

Katika imani ya kikristo, yapo mambo ambayo yanafanyika kama ishara lakini yanafunua kitu kikubwa sana katika roho. Kwamfano utaona Bwana Yesu alitoa maagizo ya kushiriki meza ya Bwana, ambapo wakristo wakutanikapo wanakula mkate pamoja na divai. Hivyo ni vyakula vya kimwili lakini vinapolika kwa maagizo hayo ya Bwana Yesu vinakuwa vinafunua vitu vingine katika roho. Kwamba ni sawa na tunainywa damu ya Yesu na Mwili wake katika ulimwengu wa roho. Na alisema mtu asiyefanya hivyo basi hana uzima ndani yake. (maana yake hana ushirika na Yesu).

Yohana 6:53 “Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu”.

Umeona ni agizo dogo tu, la kula chakula cha kimwili, lakini lina maana kubwa sana katika roho, sio la kulipuuza wala la kulifanya isivyopaswa…Na hapo hajasema tuonje!..bali tuule..

Kadhalika Bwana Yesu alitoa maagizo mengine yanayofanana na hayo ya watu kuzamishwa katika maji kwa jina lake(au kirahisi kubatizwa), ambapo alisema kwa kufanya hivyo katika mwili..kunafunua jambo kubwa sana katika roho, ambalo jambo lenyewe ni “kufa na kufufuka pamoja naye”

Wakolosai 2:12 “Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu”.

Umeona na hapo?..maana yake usipobatizwa (yaani kuzamishwa katika maji)..basi katika roho bado hujafa wala kufufuka pamoja naye…wewe bado si wake!. Vile vile kama hujazamishwa na badala yake umenyunyuziwa hapo bado hujabatizwa, unapaswa ukabatizwe tena katika maji mengi.. kwasababu ndio tafsiri ya neno ubatizo.

Sasa yapo maswali machache machache ya kujiuliza?

Je ina maana kama mtu hajabatizwa katika maji mengi na badala yake katika kunyunyiziwa hawezi kwenda mbinguni?..Na kama hawezi vipi Yule mwizi aliyesulibiwa na Bwana pale msalabani..mbona yeye aliokolewa na wala hakubatizwa?..mbona wakina Musa hawakubatizwa?…mbona wakina Eliya hawakubatizwa?…Majibu ya maswali haya yote utayapata hapa >> Mtu akifa bila kubatizwa atakwenda mbinguni?

Hivyo ndugu mpendwa kamwe usiudharau “ubatizo”..kama bado hujaelewa kwa undani ubatizo ni nini, na umuhimu wa ubatizo tafadhali rudia kusoma tena taratibu na nakuomba chukua muda mwingi…katafute kuuliza huko na huko na pia piga magoti peke yako mwulize Roho Mtakatifu, halafu kasome biblia yako atakupa majibu.

Na ubatizo sahihi ni wa Jina la Yesu kulingana na mistari hii; Matendo 2:38, 8:16,10:48 na 19:5. Jina la Yesu ndio jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kufahamu haya zaidi fungua masomo mwisho kabisa mwa somo hili (sehemu ya chini)..yanaelezea kwa kina masuala ya ubatizo.

Bwana akubariki.

Kama hujampokea Yesu saa ya wokovu ni sasa. Kristo yupo mlangoni kurudi kuwachukua wateule wake..hivyo ingia leo ndani ya neema hii, kabla mlango wa neema haujafungwa. Yesu anakupanda na anataka kukupa raha nafsini mwako leo kama utamkubali…sawasawa na neno lake hili..

Mathayo 11: 28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.

Je, kama hauna ubatizo sahihi hauwezi kuwa na Roho Mtakatifu?

MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:

BIBLIA TAKATIFU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini tofauti kati ya Amri, sheria na Hukumu?

Nini tofauti kati ya Amri, sheria na Hukumu?


JIBU: Tukisoma kitabu cha Kumbukumbu 7:11 biblia inasema…

“Basi zishike AMRI, NA SHERIA, NA HUKUMU ninazokuamuru leo, uzitende.

12 Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako”

Ukisoma kwa makini utaona kweli kuna vitu vitatu hapo..Amri, Sheria na Hukumu..Hivi vi vitu vitatu tofauti lakini vinategemeana sana.

Tukianza na Amri:

Amri maana yake ni Agizo lililotolewa na mamlaka iliyo kuu ambalo linapaswa litekelezwe bila shuruti..Amri huwa haina uchaguzi kwamba mtu anapaswa aitekeleze au asiitekeleze..Amri ikitolewa ni sharti wote waitekeleze na asiyefanya hivyo atakuwa hatihani. Katika Agano la kale..Mungu alitoa Amri kuu kumi kama tunavyozisoma katika kitabu cha Kutoka Mlango wa 20, na Kumbukumbu 5:3-21. (Unaweza ukazisoma binafsi).

Sheria:

Lakini pamoja na hizo Amri 10 kuwepo…bado zilikuwa hazijakamilika…Kwamfano kuna Amri moja inayosema USIZINI…Hiyo ni amri kweli..Mtu hatazini na mke wa jirani yake…lakini je! Ikitokea kazini na mnyama itakuaje?..atachukuliwa hatua gani? Atahukumiwaje?, au ikatokea mtu kazini na mzazi wake je atahukumiwaje? Hukumu yake itakuwaje, ikitokea mtu hajazini na mke wa jirani yake lakini kalala na mtu wa jinsia moja na yeye itakuwaje? N.k…Sasa maswali kama hayo unaona kabisa amri peke yake haijajitosheleza inahitajika ziwepo sheria pamoja na hukumu juu ya hizo amri…

Ndio maana unaona kwenye biblia zimeongezeka sheria nyingi nyingi ambazo zote zinasapoti Amri ya USIZINI. Na baadhi ya sheria hizo ni kama zifuatazo.

Walawi 18: 23 “Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko”…Hii ni sheria inayosapoti amri ya USIZINI.

Nyingine ni hizi.

Walawi 18: 6 “Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana.

7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.

8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.

9 Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.

10 Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe.

11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake”. Kufunua Utupu wa mtu maana yake kulala na huyo mtu (hiyo ni lugha ya kibiblia).

Hukumu:

Sasa hizo ni sheria zinazogongelea msumari Amri ya USIZINI..Lakini pamoja na hizo sheria ikitokea mtu kazikiuka atahukumiwaje?..Ndio hapo zijahitajika pia HUKUMU juu ya sheria na Amri.

Mfano wa hukumu hizo ni kama ifuatavyo..

Kutoka 22: 19 “Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa”.

Walawi 20: 10 “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.

11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.

12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao.

13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao”.

Umeona na Amri nyingine zote 9 zilizosalia zina sheria zake na hukumu zake…Kwahiyo Amri hazijakamilika bila sheria na hukumu. Hiyo ndiyo tofauti ya Amri, sheria na Hukumu.

Hivyo Mungu alipowaambia wana wa Israeli wazishike hukumu zake, alikuwa anamaanisha pia wazitelekeze hukumu za amri zote bila kuacha hata moja, aliyestahili kutozwa kitu atozwe, aliyestahili kutengwa atengwe, aliyestahili kifo, afe n.k.

Je katika agano jipya, amri,sheria na hukumu zinatekelezwaje?

Lakini Katika Agano jipya tulilopo sasa Amri za Mungu zinaandikwa ndani ya mioyo yetu, na kadhalika sheria na hukumu (Soma Yeremia 31:31-34)...Roho Mtakatifu anapoingia ndani yetu, hatuhitaji sheria kuzishika amri za Mungu..Sisi hatuhitaji kuambiwa kuzini na mnyama ni dhambi..tayari Roho aliyeko ndani yetu anatushuhudia kwamba jambo hilo si sawa..

Sheria anakuwa zinakuwa zimeandikwa ndani kabisa ya mioyo yetu..hatuhitaji kuambiwa kulala na mtu wa jinsia moja nasi ni dhambi..tayari sheria hiyo imeandikwa ndani ya mioyo yetu ipo..Hatuhitaji kuambiwa kuvaa vimini au nguo za nusu uchi ni dhambi..tayari ndani ya moiyo yetu Roho Mtakatifu anashuhudia kuwa jambo hilo si sawa kabla hata ya kuambiwa…hatuhitaji kupewa sheria ya kwamba tuwaheshimu wazazi wetu..tayari sheria hiyo ipo ndani ya mioyo yetu tunaitimiza bila shuruti…Hiyo ndio maana biblia inasema hatuishi kwa sheria bali kwa Imani..

Watu wa agano la kale hawakuwa na upendeleo tuliopewa sisi wa kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye angewasaidia kuziishi sheria pasipo nyaraka…lakini sisi tumepewa zawadi hiyo ya Roho..Ni Neema ya ajabu sana..Ndio maana kuna umuhimu sana wa kuwa na Roho Mtakatifu. Ukiwa na Roho Mtakatifu hutakuwa kuwa ngumu kwako kuyatekeleza maagizo yote yaliyopo katika maandiko.

Je umepokea Roho Mtakatifu?..

kumbuka biblia inasema wote wasiokuwa na Roho Mtakatifu hao sio wake (Soma Warumi 8:9). Hivyo kama unaona bado ni ngumu wewe kuishi maisha matakatifu basi hauna Roho Mtakatifu, unamhitaji..Na huyo ataingia ndani yako ikiwa utaamua kabisa kwa moyo wako kuukana ulimwengu na kumgeukia yeye..kwa kutubu dhambi zako leo, na kujinyenyekeza mbele zake..Na baada ya kutubu kwa dhati kabisa..bila kuchelewa nenda katafute ubatizo sahihi ukabatizwe kama hujabatizwa…Kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi(Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38)..Na kisha Roho Mtakatifu atakutia muhuri uwe wake milele. Hapo na kuendelea sheria za Mungu kwako hazitakuwa ni utumwa..bali zitabubujika zenyewe moyoni mwako pasipo hata kusukumwa sukumwa wala kuhubiriwa hubiriwa…

Bwana akubariki sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Tofuati kati ya Myahudi, Mwisraeli na Muebrania ni ipi?

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

Je! hizi roho saba za Mungu ni zipi? na je zinatofautiana na Roho Mtakatifu?

ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.

Tunasoma katika Matendo 17 Mtume Paulo, alipofika Athene mji mkuu wa Ukigiriki, mji ambao ulikuwa umejaa wasomi wengi ambao hata sasa historia ya dunia inarekodi sehemu kubwa ya Elimu na Sayansi tuliyonayo leo hii chimbuko lake lilikuwa ni huko Ugiriki, Wanafalsafa maarufu ambao wanafahamika kwa akili zao na hekima zao nyingi walizowahi kuzionyesha duniani mfano Aristotle, Xenophon, Plato,Pythagoras,Socrates,Plotemy, n.k. wote hao Walitokea huko huko Ugiriki, hivyo tangu zamani hawa watu walijulikana kama ni watafiti wakubwa (Great thinkers), na wagunduzi wa vitu vingi, na hivyo hawakuwa watu wa kubabaishwa tu na habari zinazovuma au maneno ya kutungwa yasiyoweza kuthibitishwa uhalisia wake yanayokuja katika jamii zao…

Na ndio hapa tunaona Mtume Paulo anaingia Athene sasa baada ya kuzunguka mataifa mengi na nchi nyingi kuhubiri, nchi hii kwake ilikuwa ni ya tofauti kidogo Kama Biblia inavyotuleza watu hawa wa Athene walikuwa hawana muda wa kufanya mambo mengine yoyote isipokuwa kutoa habari tu na kusikiliza juu ya taarifa mpya zinazowafikia (Soma Matendo 17:21), hii inaonyesha ni jinsi gani walivyokuwa wamejikita katika masuala ya utafiti na usomi ili kujua nini maana ya mambo yote na uhalisia wake zaidi ya kuganda katika mambo yale yale wanayoyaona kila siku..

Hivyo mtume Paulo alipoingia katika mji ule alianza kuupeleleza ili aone ni mambo gani yanayoendelea kule, lakini alipokuwa akizunguka huko na kule alikutana na madhahabu kubwa sana, iliyoandikwa maneno haya KWA MUNGU ASIYEJULIKANA..Hilo likateka sana fikra zake kupelekea kutaka kufahamu ni kwanini waandike vile, ni kwanini watengeneze madhabahu kwa Mungu wasiyemjua,

Kumbuka kama tulivyoona hapo mwanzo Wagiriki hawakuwa kama watu wa mataifa mengine mfano wa warumi au wamedi, hapana hawa ni watu waliokuwa wanafikiria sana, na wadadisi na wachunguzi wa kina wa mambo yote, hivyo kuandika vile sio kwamba walijisikia tu kuandika au walibuni wazo hilo kisha watengeneze madhabahu ya Mungu asiyejulikana kisha waabudu juu yake, hapana badala yake, ni kweli walitazama mambo yote,na kutathimini kwa kina na kwa utaratibu wakagundua kuwa katikati ya vitu vyote vilivyopo duniani na vinavyoabudiwa hakuna hata kimoja kinachoweza kuleta ufasaha wa mambo yao yote, isipokuwa kwa Mungu asiyejulikana asifanya vikao na wanadamu. hii ikiwa na maana japo kulikuwa na miungu mingi ugiriki watu wanayoiabudu wakati ule, lakini hakuna hata mmoja aliyefikia viwango vya kustahili kupokea Ibada zote za kiungu kwa kazi zake zote zinazoonekana ulimwenguni kote..

Walijua kabisa kipo kitu kingine zaidi ya wao wanavyoweza kukifikiri au kikitafsiri kiitwacho Mungu au vinginevyo, kinachoendesha shughuli zote za ulimwenguni, na wanadamu na kitu hicho hawawezi kuwasiliana nacho kwa njia za kawaida kwasababu ni kikuu sana, zaidi ya upeo wa kufikiri wa wanadamu, ni cha elimu ya juu sana, hakijulikani kama kipo mbali na sisi au karibu na sisi, ni kwamba tu hakina ushirika na wanadamu, wala hakielezeki, wala hakifananishwi, njia zake hazieleweki hali kadhalika hazichunguziki na makao yake hayafahamiki, na hivyo wakaona ili kufanya habari zake kuwa fupi basi wakaweka madhabahu yake mahali pa juu sana kuliko madhabahu nyingine zote na kuanza kumwabudu hivyo hivyo tu pasipo maarifa yoyote kumuhusu yeye..Ila walichokuwa wanajua ni kwamba ni kwa Mungu huyo anayeishi na ni mkuu kuliko vitu vyote.

Matendo 17:22 “Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini.

23 Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.

24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;

25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.

26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;

27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.

28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

29 Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.

30 Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.

31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.

32 Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena katika habari hiyo.

33 Basi hivi Paulo akaondoka akawaacha.

34 Baadhi ya watu wakashikamana naye, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao”.

Kama tunavyosoma tunaona mtume Paulo alifika na kuanza moja kwa moja kuwafunulia kwa utaratibu habari za Mungu huyo ambaye wanamwabudu pasipo wao kumjua, Mungu asiyejulikana. Na hivyo waliposikia habari za jambo hilo jipya masikioni mwao wengi wao walikaa chini na kumsikiliza.

Ndugu, hao watu walikuwa wapo sahihi kabisa kuenenda katika hali hiyo ni kweli kumwelewa ni kazi sana,au tunaweza kusema haiwezekani kabisa kumwelewa yeye au kumjua yeye kama hatutajua njia fasaha ya kumwendea…

Mambo hayo hayo ya Athene yanajirudia hata leo hii, Wanasayansi sio kwamba hawaamini kuwa hakuna nguvu ya kimiujiza (Supreme being) inayouongoza huu ulimwengu hapana wanaamini kabisa isipokuwa wao wanamtambua kwa jina lingine (nature) na hiyo inawafanya wasiamwamini kabisa Mungu tunayemwamini sisi, hawaamini kama huyo (nature) ambaye sisi tunamwita Mungu anaweza akawa dhaifu namna hiyo etu ajishughulishe na wanadamu na kutazama dhambi zao ili awaadhibu, angali yeye tunamfahamu anayo mambo makubwa sana yasiyokuwa na mwisho huko angani na ulimwengui kote yasiyoweza kuelezeka kwa fikra za kibinadamu iweje leo, eti udhaifu wa mtu umuudhi, huyo sio Mungu…Unaona? Ndivyo wanavyowaza na kuamini.

Mwanasayansi mmoja maarufu wa kizazi chetu ajulikanaye kama ALBERT EINSTEIN,ambaye dunia sasa inamwona kama mtu wa karne kwa mapinduzi yake makubwa aliyoyaleta katika ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia, yeye anasema hivi …..

“Mimi naamini katika Mungu, lakini sio katika Mungu huyu watu wanaomwita wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambaye yeye msingi wake ni kujishughulisha na vitu vidhaifu vya wanadamu, kama dhambi, na kuadhibu watu, huyu hawezi akawa ni Mungu ninayemfahamu: anaendelea kusema: mimi anasema naamini katika Mungu ambaye ni mkuu zaidi ya upeo wa kibinadamu muumba wa UNIVERSE, ambaye akili za kibinadamu hazijitoshelezi kumwelezea tabia zake”.. Yaani kwa ufupi anaamini kwa Mungu asiyeweza kufikiwa.

Unaona? Hali kadhalika jambo kama hilo tunaliona kwa ndugu zetu waislamu, wanasema Mungu tunayemwabudu ni Mungu mkuu sana (Allah), hajazaa, wala hajazaliwa, wala hana mtoto, wala hana USHIRIKA na mwanadamu yeyote wala kiumbe chochote, si mwanaume, wala si mwanamke, na hivyo mtu yeyote anayemwita Mungu baba, au mfalme wake anatenda dhambi kubwa sana ya kumshusha Mungu hadhi ya kumfananisha na Mwanadamu ambayo ni sawa na dhambi ya kukufuru…

Sasa hawa wote sio kwamba wanakosea kuamini hivyo, hapana, walichokiona kuhusu Mungu ni kweli kabisa, na ndivyo Mungu alivyo katika uhalisia wake, lakini kumbuka jambo hilo ndio kama lile lile lililowakuta watu wa Athene wao walitengeneza madhahaba na kumwabudu Mungu ndani yake lakini madhahabahu hiyo ilikuwa na jina la “KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.”

Unaona? Walimwabudu Mungu asiyejulikana, walimwabudu Mungu wasiyemjua, Sasa madhara yanayokuja kujitokeza kwa watu wa namna hiyo ni kwamba maisha yao yote wataishia kutokumwelewa muumba wao kabisa mpaka kufa kwao, pia hawatakaa wanufaike na chochote kutoka kwa muumba wao, Na mwisho wa siku wanaishi akutokumwelewa hata pale Mungu atakapotaka kusema nao hawatamwelewa na hivyo kupotea kabisa katika dira ya Mungu. angalia kwa makini utaona, watu na namna hiyo wanaishia kumwogopa, na kuwa na wasiwasi, na kumwendea kwa hofu zisizokuwa na maana yoyote, kwasababu wametaka kumwona yeye katika uhalisia wa ukuu wake lakini sio katika njia ambayo amewapangia wanadamu wote wamwone yeye.

Ndugu yangu Mungu kumleta Yesu Kristo duniani kulikuwa na manufaa sana, kwangu mimi na kwako wewe, ni kutufanya sisi tumwelewe yeye vizuri katika utimilifu wote, biblia inasema “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.”(Wakolosai 2:9), Unaona pale ambapo tulikwama pasipo kumwelewa Mungu sasa tunamwelewa kwa kupitia mwana wake YESU KRISTO.

Na ndicho Paulo alichokifanya mara moja kwa wale watu wa Athene, Aliwahubiria Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye kwa huyo sisi tunahama moja kwa moja kutoka kuwa viumbe tu vya kawaida vya mwenyezi Mungu, na kufanyika kuwa WANA WA MUNGU aliye hai kama yeye alivyokuwa.. Na kwa kumwamini yeye basi tunakuwa na uwezo wa kumwelewa Mungu na mapenzi yake katika maisha yetu kwa urahisi kabisa, tunakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya madhabahu ya Mungu mbinguni na kuzungumza naye bila kutaabika kama wengine walivyo sasa hivi…

Na ndio maana alisema… (Yohana 14.6…”Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.)..Na pia alisema… Aliyeniona mimi amemwona Baba;….Hatuwezi kumjua Mungu kwa njia yoyote ile isipokuwa kwa kupitia mwana wake YESU KRISTO. Huo ni ukweli ndugu wala usihangaike pengine”

Waebrania 1:1”Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao wautukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;

4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao”.

Tuchulie Mfano ulio hai ni sawa na leo hii unataka kuwasiliana na mimi bila kutegemea hicho kioo kilichopachikwa mbele ya simu yako, ni kweli kabisa Simu sio hicho kioo ambacho unakipangusa,na kuandika namba juu yake, …Simu ni ni kitu kingine cha ndani kilichojawa na Commands tofauti tofauti ili kufanya kifaa hicho kiweze kutumika kwa mawasiliano, sasa ikiwa utaondoa hicho kioo cha juu na ukataka kuwasiliana nami, basi jiandae kukukutana huko nambo ambayo hujayazoea maneno huko kama Galllery, au Contacts, au SMS, usitazamie utayakuta huko wala kidole hakitahitajika huko kufanya mawasiliano yaende.., ni wazi kuwa utakutana na vitu kama chips, cards,modems,processors,circuit board, na vinginevyo ambavyo hata kwa lugha ya Kiswahili havina tafsiri, ambavyo wewe kwa akili yako ya kawaida hutaelewa chochote isipokuwa yule mtaalamu wa hivyo vitu, yeye pekee ndiye anayeweza kupiga simu pasipo kioo kile, kwa vifaa na ujuzi alionao ..

Lakini sasa kwanini kile kioo kimewekwa, ni kwa faida yako wewe usiyejua hayo mambo magumu yaliyopo ndani ya hiyo simu, ili kufanya simu ionekane kuwa na maana kwako ndio hapo ukawekewa hicho kioo kizuri kwa nje chenye mpangilio mzuri wa mafile, kazi yako wewe ni kubofya tu au kupangusa, na moja kwa moja taarifa zako zinapelekwa ndani ya simu, na hivyo simu inafahamu kuwa ulimaanisha nini, na saa hiyo hiyo simu inapigwa kwenye minara kuungwa na mimi mahali nilipo kuwasiliana na wewe, Unaona hapo? jambo ambalo lingepaswa lifanywe na wataalamu wa hali ya juu, kuamrisha hizo code za simu lakini sasa linafanywa na wewe kirahisi tu kupitia kidole chako juu ya kile kioo.

Hivyo hivyo YESU ndiye kioo chetu kwa Mungu, ili tuweze kunufaika na Muumba wetu aliye mkuu sana, asiyechunguzika njia zake, asiyeelezeka kwa namna ya kibinadamu, asiyekuwa na mwanzo, aliye mwanadamu hatuna budi kumtumia yeye kama kirahisi chetu vinginevyo hatutakaa tumjue Mungu kwa kumchunguza.. Kwa kumwamini yeye na maneno yake,na sasa yale mambo yote ambayo tunayaona ni magumu kwetu, kumfikia Mungu wetu basi yanafanyika kuwa marahisi kabisa, embu fikiria kwa kuiamini tu damu ya Yesu unakuwa na nafasi ya moja kwa moja kusimama mbele za Muumba wa mbingu na nchi na kupata rehema ya kujibiwa maombi yako mambo ambayo watu wa agano la kale waliyatafuta kwa kafara nyingi lakini wasiweze kabisa kufikia hatua ya kuondolewa dhambi zao, au kusimama mbele ya madhabahu ya Mungu mbinguni…Unadhani hilo ni jambo dogo au rahisi, ukiwa nje ya Kristo hilo haliwezekani kabisa ndugu na ndio maana utaona hao wengine wanateseka huko nje, ni haki yao,kuwa hivyo japo wanamuheshimu Mungu kwa hofu lakini upendeleo huo hawataweza kuupata mpaka watakapoingia ndani ya KRISTO..

Wanamwamini Mungu lakini sio katika maarifa, wanamfahamu kuwa ni muweza wa yote lakini uweza wake hauna matunda yoyote ndani ya maisha yao, magonjwa yao hayaponywi, hawawezi kufunguliwa katika vifungo vya giza, hawawezi kupata faraha ya kudumu na amani ambayo ni YESU KRISTO tu pekee ndio anayeitoa, hawana uzima wa milele ndani yao, hawawezi kumwomba chochote kwasababu yeye huwa hajishughulishi na mambo ya wanadamu…Hana mshirika, ..Kwasababu hanawa ushirika naye kama wanavyosema…kwao ni Mungu asiyejulikana! Na asiyefanya vikao na wanadamu,..Lakini kwetu tuliomwamini Kristo Yesu, Mungu anafanya vikao na sisi, na anakuwa ni Mungu tunayemfahamu, tunakuwa ni watu wa Milki ya Mungu, ukuhani wa kifalme, uzao mteule haleluya!!

Hivyo ndugu yangu, ikiwa bado upo nje ya Kristo, wakati ndio huu, wewe mkristo-jina, wewe ni mwislamu, wewe ni asiye-na-dini mkabidhi leo maisha yako, utubu dhambi zako kabisa kwa kumaanisha kuziacha, kisha fanya hima ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na uwe ni kwa jina la YESU KRISTO, hapo ndipo utakapopokea uwezo wa kuwa mwana wa Mungu, na kuhesabiwa kuwa mtu wa kimbunguni kwasababu Roho wa Mungu atashuka ndani yako kuanzia huo wakati , kukusaidia wewe kumkaribia Mungu..na kumwelewa Mungu, Kwasababu atayatwaa yaliyo ya Kristo na kukupasha wewe habari.

Wakolosai 1:15 “naye (KRISTO) ni mfano wa Mungu asiyeonekana , mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

Lakini ikiwa utaendelea kubakia nje ya wokovu ufahamu kuwa hutakaa umfikie Mungu, wala kumjua wala maombi yako hayatakaa yamfikie yeye kama mwana, utakufa katika dhambi, utakufa katika kukosa maarifa ya kumjua Mungu hiyo haijalishi unaonyesha heshima nyingi kwake kiasi gani, utafanana na wale watu wa ATHENE wanamwabudu Mungu wasiyemjua.. na mwisho wake utaishia katika lile ziwa la Moto.Wakati ndio huu, fanya bidii uje kwa Kristo. Na Bwana atakusaidia.

Tafadhali “shiriki ” neema hii kwa wengine, ili nao waponywe na Neno la Mungu, na Bwana atakubariki.

Maran Atha. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

MWANA WA MUNGU.


Rudi Nyumbani

Print this post

TWEKA MPAKA VILINDINI.

NoLuka 5: 1 “Ikawa makutano WALIPOMSONGA wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,

2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao.

3 Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.

4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.

5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.

6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;

7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama”.

Tukio hilo lililowapata wakina Petro linaweza likaonekana ni dogo lakini linabeba siri kubwa sana ya mafanikio hususani kwa wale watu ambao shughuli zao za kujipatia kipato haziendi sawa. Hivyo kama wewe ni mmoja wapo somo hili litakufaa sana. Soma hadi mwisho, lakini kama mambo yako yanaenda vizuri basi halitakuhusu sana., Zidi tu kuendelea kujifunza masomo mengine yahusuyo utakatifu na ufalme wa mbinguni.

Ukitafakari hiyo habari utaona Bwana Yesu, alikuwa akihangaika sana katika kuwafundisha makutano, yale mazingira yalikuwa ni magumu sana kutokana na kwamba watu wengi walimsonga na yeye alitaka kuwafundisha zaidi katika utulivu, hivyo hakuona kama akiendelea katika hali ile ile atatimiza kusudi lake, ndipo akaamua atafute madhabahu ya kuwakutanisha wale watu pamoja, mahali atakapotulia ili awafundishe wale watu katika ustaarabu na utaratibu ambao Mungu ameukusudia..

Na alipogeuka akaona vyombo viwili vimeegeshwa pwani na wenye navyo wametoka, ndipo akikichagua cha mmojawapo na kukigeuza kuwa madhabahu yake ya muda.

Sasa Chombo kinawakilisha nini katika mazingira tuliyopo leo?. Chombo kinawakilisha kitu chochote cha kujipatia kipato, kumbuka chombo hicho Bwana alichokitumia kilikuwa ni cha akina Petro cha kuvulia samaki, kwasasa hivi chombo kinaweza kikawa, elimu ya mtu, ujuzi wa mtu, biashara ya mtu, fremu ya mtu, shamba la mtu, kiwanja cha mtu,n.k.

Lakini tunasoma katika habari hiyo, tunaona Bwana alipotazama hakuchagua vyombo vilivyokuwa kando kando vyenye wavuvi au samaki, kumbuka vilikuwepo tu vingi vizuri zaidi ya hivyo vilivyokuwa vinazungukazunguka maeneo yale, lakini yeye hakuchagua chochote kati ya hivyo bali alivichagua vile visivyokuwa na kitu ndani yake…(Na ndio maana somo hili linawahusu sana wale ambao shughuli zao haziendi sawa),

Sasa kilichotokea ni kwamba wakina Petro walifanya kazi ya kuchosha usiku kucha wakihangaika kutafuta samaki ukanda mzima wa ziwa la Genesareti kwa shida, na kujitoa kweli kweli lakini wasipate kitu, mpaka kulipokucha wakakata tamaa ya kuendelea kuvua tena, wakaona kilichobakia tu ni kukipumzisha chombo na kuzitengeneza nyavu zao tena, kisha kuzihifadhi mpaka wakati mwingine,

Lakini baadaye kidogo ndio tunamwona Bwana Yesu akisumbuka na wale makutano, ndipo wao wakamruhusu Bwana kutumia vile vyombo ili kutimiza kusudi lake la kuhubiri,. Na baada ya Bwana kumaliza kuhubiri, sasa wakati makutano yote wameshaondoka ndipo akawageukia wale wamiliki wa vile vyombo, na kuwaambia NENDENI VILINDINI MKASHUSHE NYAVU ZENU, MVUE SAMAKI.

Lakini wao walimwambia, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha pasipo mafanikio, na walipokubali tu kwenda kuvua walipata matokeo makubwa ya kushangaza, mpaka nyavu zao kuanza kukatika, mpaka kufikia hatua ya kuomba msaada kwa wingi wa Baraka hizo, maana rizki imekuwa nyingi na kuwalemea mpaka hawawezi tena kuimaliza wao wenyewe ikawabidi wawaite na marafiki zao na maadui zao waokote na wao pia wapate kidogo..

Bwana Yesu hajabadilika, ni yeye Yule jana, na leo na hata milele, njia aliyotumia kumbarikia Petro ndiyo hiyo hiyo atakayoitumia sasahivi kukubariki na wewe uliyefanya kazi ya kuchosha miaka na miaka bila mafanikio yoyote. Umejaribu kufanya kwa bidii kazi lakini unachokipata hakijitoshelezi…

Leo hii hicho chombo chako kigeuze kuwa MADHABAHU YA KRISTO kwasababu anakitafuta hicho ili ilifanye kusudi lake, kumbuka pale Bwana hakutafuta sinagogi la kuwakusanya wale makutano waliokuwa wanamsonga, hakutafuta hekalu, wala hakutafuta mahali patakatifu bali alitafuta MAHALI PA KUJIPATIA KIPATO KWA MTU, mahali ambapo mtu anapopategemea kujipatia mkate wake wa kila siku, na pia fahamu tu, siku zote Bwana anapaangalia mahali ambapo palipo patupu kama kwako wewe, Mahali ambapo pamefanyika kazi ya kuchosha miaka mingi, miezi mingi pasipo mafanikio yoyote, hapo ndipo anapopataka kwa ajili ya kazi yake, na akishamalizana napo hapo, ndipo atakwambia nenda katupe nyavu zako kilindini uvue samaki, kwa wingi wa atakachokupa Bwana utaita mpaka na marafiki na zako na maadui zako waje nao kushiriki Baraka zako Mungu alizokuandalia.

Leo Kazi yako wewe ni ya ufundi, una ujuzi wa kutosha kuhusu masuala ya ujenzi, na unaona mahali unapokusanyikia pengine ni kanisani kuna kasoro Fulani ya ujenzi, na shughuli zako za kijenzi haziendi sawa, umekuwa ukipata mapato kidogo kupitia hiyo,wakati mwingine unakosa kabisa kazi, huo ndio wakati wa kwenda kumruhusu Bwana atumie hicho chombo chako (ujuzi),

nenda mahali unapokusanyika (kanisa), kazi ya Mungu inapofanywa, angalia kasoro zinazohusiana na taaluma yako, na utumie ujuzi wako kurekebisha tatizo hilo bila kutazamia malipo yoyote, pengine umeona ukuta wa kanisa umebomoka au una ufa, uzibe, umeona mfumo wa maji haujakaa sawa na una ujuzi wa kufanya hivyo, urekebishe hata kama hauna chochote, umeona kanisa halina choo kinachostahili, na wewe una ujuzi wa namna ya kutengeneza vizuri, nenda kafanye hivyo, kajenge kwa ustadi wote, na maarifa yako yote, umeona kuna kasoro ya umeme na mfumo wa nyaya, na una ujuzi huo nenda karekebishe usisubiri hata mtu akamwambie, mruhusu Bwana atumie hicho chombo, na mwisho wa siku utaona tofauti yako na mtu asiyefanya hivyo wakati Fulani ukifika.

Au wewe ni polisi au mlinzi, anza kutoa mchango katika sekta hiyo ndani ya kazi ya Mungu..Usiseme Mungu kweli ataweza kutumia taaluma hii/ujuzi huu kwenye kazi yake??..kumbuka Bwana Yesu alitumia mtumbwi wa wavuvi kuwapelekea maelfu ya watu katika ufalme wa mbinguni…Na wewe vivyo hivyo mpe Bwana chombo chako.

Au wewe unafanya kazi ya upishi, na unaona kazi zako haziendi sawa, faida ndogo, na unaona kuna uhitaji mkubwa wa wapishi ndani ya nyumba ya Mungu, labda kwa ajili ya wazee wasiojiweza (wakristo), au wageni, au wenye mahitaji na mayatima (walio wakristo), ndani ya kanisa n.k usingoje uambiwe au uwe na kitu kwanza ndio ufanye, wewe mwenyewe anza kuchukua hatua ya kujitolea kwenda kuifanya, tena pasipo hata kuombwa.

Wewe ni mtengeneza bustani, na ndiyo kazi yako umekuwa ukifanya kwa ajili ya kujipatia kipato..Lakini mazingira ya kanisani ni machafu au hayavutii, panaonekana ni mahali pasipo tofauti na sehemu nyingine yoyote, Tumia chombo chako (ujuzi) kurekebisha mazingira ya Mungu, pakavutia kama vile unavyopendezesha bustani za watu wengine,..unaweza ukaona ni jambo dogo lakini linamaana kubwa na Bwana akisharidhika atakuambia shuka vilindini..utaona milango Mungu anayokufungulia katika hiyo hiyo kazi yako ilivyo ya ajabu.

Wewe ambaye ulikuwa unatafuta kazi,na bado hujapata, angali unao ujuzi Fulani, usiuache ulale utumie huo ujuzi katika kazi ya ufalme wa mbinguni, kwamfano labda wewe ni “ IT ” (mjuzi wa katika teknolijia ya Kompyuta), unaweza uka unda wavuti na tovuti kwaajili ya kutangaza ufalme wa mbinguni, unaweza ukabuni programu za kutangaza kazi ya Mungu kirahisi katika mitandao fanya kiuaminifu kabisa..Na Bwana akishamaliza kutenda kazi kwa kutumia chombo chako, atakuambia shuka vilindini…Utaona nafasi ambayo ulikuwa unaitafuta kwa kuhangaika kwa muda mrefu pasipo mafanikio kama wakina Petro walivyokuwa..unaipata ndani ya kipindi kifupi tena chenye faida mara 100 zaidi ya kile cha mwanzo ulichokuwa unakihangaikia..

Lakini hizo zote zinakuja kwanza kwa kumtolea Bwana chombo chako akitumie, kwa ajili ya kazi yake, lakini kuna wengine hawapendi kumpa Bwana nafasi lakini wanataka Baraka za Bwana, utakuta mtu analo eneo kubwa limekaa pasipo matumizi yoyote, hataki hata kukaribisha watu wafanyie kazi za mikutano ya injili hapo, na bado anataka Mungu ambariki, ndipo hapo zile roho za udanganyifu zilizoachiliwa katika siku za mwisho zinaanza kumdanganya na kumshawishi, akanunue mafuta ya upako, anunue chumvi na maji ya Baraka akanyunyuzie kwenye kiwanja chake na kwenye biashara yake, aanze kukemea roho za laana katika kiwanja chake, au biashara zake, ili mambo yake yaanze kwenda vizuri.

Utamkuta mwingine anazo fremu za vyumba na zimekosa mpangaji wa kufanyia biashara au tution,..na wakati huo huo kuna wakristo wenzake wamekuja kumwomba awape angalau fremu moja wawe wanafanyia bible study au maombi wakati wa jioni kwa muda huku wanatafuta eneo lingine..lakini kwasababu hajui uweza wa Mungu, anawazuilia na kuona bora tu ziendelee kuwa zimefungwa.na wakati huo huo anazunguka kutafuta kuombewa na kununua maji na mafuta ya upako huku na kule hata wakati mwingine nchi na nchi..Mtu wa namna hii hawezi kutazamia miujiza kama waliofanyiwa wakina Petro.

Bwana anasema nikaribieni, nami nitawakaribia… Wakati mwingine hilo pigo unalolipata la kuvuna haba, ni kwasababu kazi ya Mungu inakaa katika hali ya kusongwa songwa na wewe hutaki kulitazama hilo kwa kumzuilia Bwana chombo chako..(Soma Hagai 1:1-12). Anza leo kufanya kama akina Petro walivyofanya na Mungu atakubariki. Mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.

Ubarikiwe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu.

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

Print this post